KAZI na FAMILIA

family

Haina maana yoyote kusifiwa kuwa wewe ni kiongozi mzuri, manager mzuri, Mchungaji mzuri, halafu wakati huo huo familia yako ikawa katika mapungufu makali kwa sababu baba au mama hana muda na familia yake kwa kisingizio cha majukumu mengi!! Kwa kisingizio cha kutafuta pesa, shame!

Eti kwa sababu baba ni mbunge, ni waziri, ni CEO wa kampuni, ni mfanyabiashara au vyovyote eti hana muda na familia yake! Hii ni uzembe wa hali ya juu tena juu sana! Kuwa na kazi nyingi haikuhalalishii wewe, baba au mama kuisahau familia yako!

Ni kweli umefanya vizuri sana, biashara yako imeendelea sana ni sawa, ni kweli unaongoza kampuni vizuri sana ni sawa, ni kweli ni Mchungaji mzuri sana Kanisa limesimama imara kwa sababu yako. Lakini familia yako umeisahau, sisi wanafamilia tunahitaji muda na wewe, tunahitaji malezi yako, tunahitaji upendo wako, tunahitaji uwepo wako nyumbani katika wakati sahihi, tunahitaji connection na wewe, tunahitaji uongozi wako!

Eti unawadanganya watoto kwa kuwapa kila kitu wanachohitaji na wasivyohitaji (physical things). Simu kali, usafiri kwenda shule wanapelekwa, I-pads, Computer games, vyakula vya kila aina, vingi vikiwa processed viwandani matokeo yake unawaharibu afya. Ni kweli umefanya vizuri, lakini hii ndo inaitwa being SUCCESSFUL IN A WRONG THING! Unadhani maisha ni vitu? Jamii inabaki kukushangaa tu, mbona yuko vizuri sana lakini watoto wake mmoja tu ndo amesoma, wengine wamekataa shule, wanavuta bangi, ni wezi, ni wakorofi, wamezalishwa zalishwa tu! Wakati mwingine unaiga mambo ya wazungu, sasa wewe ni mzungu? Acha kuigaiga, unapotea!

Nelson Mandela ni kiongozi aliyepita ambaye kwa Afrika nzima na hata dunia yote wengi au wote walimkubali kuwa HE WAS A GREAT MAN in leadership and humility. Lakini tunaweza kusema, he was SUCCESSFUL IN A WRONG THING! Maana Hakupata muda na familia yake, matokeo yake watoto wake 4 wamekufa na HIV/AIDS. Jambo la kusikitisha sana!

Wako wachungaji wanakuwa committed kweli kweli kwenye kulea Kanisa, familia inamkosa baba. Yupo nyumbani kila siku kumbe hayupo, kwa macho yupo na sisi kumbe hayupo! Matokeo yake watoto mpaka wanaichukia kazi ya uchungaji!

Ukweli ni kwamba, kama huna muda juu ya jambo fulani, fahamu kuwa jambo hilo si MUHIMU KWAKO, halina MAANA KWAKO. Je, familia yako (mke au mume, watoto) ni wa muhimu kwako?? Au ATM CARD yako ni muhimu kuliko mtoto wako wala mke au mume wako! Tatizo umeweka fedha mbele sana kuliko utu, tena uliingia kwenye ndoa kwa kufuata MAZOEA, hujui kulea familia, hujafundishwa wala hutaki kujifunza. Ndo maana unaacha familia Arusha wewe unaishi Dar, familia Mwanza wewe Morogoro! Hayo siyo maisha bali ni utumwa wa maisha. Jifunze nini maana ya familia, malezi yake, nini wanahitaji toka kwako ili uwe BABA au MAMA mzuri. Familia kwanza ndiyo utakuwa kiongozi mzuri, anayejitambua. Huwezi angalia kutafuta fedha tu halafu familia inaharibika, fedha hizo hazina maana kama familia yako imeparanganyika.

Jamii yetu ina watu wasiojitambua, wezi, hawajiamini, waongo, wachakachuaji, wasiojituma, wavivu, wazembe, wala rushwa na mafisadi wengi maana wazazi wao hawajafundishwa namna ya kulea familia, hakuna malezi kwa watoto maana wanazaliwa na kuachwa watafute wenyewe nini maana ya maisha, nini maana ya kuwa mtu katika jamii, matokeo wanajifunza kwa wezi, mafisadi, wavivu nk. Ee Mungu tusaidie kuifahamu kweli!

Connect na watoto tangu uchanga wao hadi unapowaozesha, ili uwaonyeshe nini maana ya maisha, nini maana ya kuwa mtu katika jamii. Wafundishe ili wajitambue, endelea kuwa-mentor katika ubaba au umama wao pia. Ukiwaacha wawe wakubwa ndiyo uwe karibu nao tayari watakuwa wamejitengenezea mifumo ya maisha yao, na wewe wanakuona STRANGER kwenye mifumo waliyotengeneza. Kuwa baba au mama acha kujifanya uko busy, kwa nini ulianzisha familia kama uko busy???

Mungu utusaidie kuiona kweli, tukafanye kama inavyopaswa kuwa ili kukuza familia zenye michango katika jamii. Amina.

NOTHING CHANGES UNTIL YOUR MIND CHANGES!

Theophil

7 thoughts on “KAZI na FAMILIA

  1. Theophil bwana!
    Unatuwakia badala ya ku sympathise nasi, wenzako tuko bize!

    Ila leo natimua mapema nikale chakula cha join pamoja na familia yangu, nakushukuru kea kutupiga shoti!

  2. Amen!!! Dunia ya sasa inachangamoto nyingi sana hususani familia na maisha,wakati mwingine mazingira ya kupatia mkate wa kila siku inakuwa ni mbali na sehemu ambapo familia inaishi,hii husababisha baba au mama kuwa mbali na familia,pia uhamisho makazini nacho ni kichocheo kikubwa cha utengano wa familia

  3. Ni kweli kuitunza familia na kuijali ni vyema na Mungu ndivyo alivyoagiza. Lakini pia mtoto kupatwa na ugonjwa kama sio kwa sababu hukumjali.
    Naomba uwaonee huruma na kuwaombea wagonjwa wa ukimwi sio kwamba walipenda.

  4. So true. A successful man is known by the family he raises. Not by his bank account.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s