Ufafanuzi wa MUUJIZA wa KIWETE katika Yohana 5:1-5

wpid-images-2.jpeg

 

Wapendwa katika Bwana, Nina swali linanitatiza na nina hitaji watu wasomaji wa Biblia wanifafanulie:

Namfuatilia mhubiri mmoja wa kimataifa na ninamuelewa sana na anibariki mno ila kuna wakati alihubiri kuhusu kiwete wa John 5; 1 -9, habari ya yule mgonjwa aliyekaa  pale kwenye kisima miaka 38, akisubiri malaika ambaye anakuja  mara moja kwa mwaka kutibua maji  na yeye atakeyewahi kutumbukia  mara malaika anayapoyatibua maji huponywa ugonjwa wake.

Mhubiri  wangu alisema kuwa Yesu hakupendezwa naye, ndiyo maana anamuuliza moja kwa moja kama anataka kuponywa, mgonjwa yule anashindwa kujibu moja kwa moja NDIYO au HAPANA badala yake anajieleza kwa nini hapati uponyaji, na Yesu anamwambia achukue godoro lake na aondoke. Mhubiri wangu alisisitiza kuwa kukosa miujiza ni uvivu wa watu, eti mtu utakaaje sehemu miaka 38? Kwamba hakuweza hata kusota au kuwaambia watu wanaomtembelea na kumletea huduma kuwa wamsogeze, na kwamba baada ya kufikiria mbinu za kuwahi yeye Analalamika tu.

Nakwazika na mahubiri haya kwa vile, kuna watu wanaofanya jitihada zao zote ili wapate mijuza yao ila wanakwama kwa sababu nyingi, haswa kama huo si mpango wa Mungu!

Nawaomba watu wa Mungu mnifafanulie hili hubiri: Ni mimi sijamuelewa mhubiri, au mhubiri alitakiwa asemeje?

Greta

Advertisements

12 thoughts on “Ufafanuzi wa MUUJIZA wa KIWETE katika Yohana 5:1-5

 1. Mmh ndugu Sungura.
  Biblia imesema wenye nguvu ndio watakauteka ufalme wa mbingu. Ni kweli na amini. Nguvu ya mwili, ya akili, ya kiroho nk. Kama Mungu amekupa ongeza jitihada uuteke ufalme wa mbingu ukiwa duniani. Maana Yesu alikuja ili tuwe na uzima tena tuwe nao tele hapa duniano na kesho mbinguni. Tumia kipawa chako kuendeleza ufalme wa.Mungu duniani. Kwa wapendwa watakaonufaoka na kwa kipTo chako. Tafuta phblishing companies kama kitabu kikiwa cha nguvu utazikamata tu baraka zako hapa duniani. Kuna waliobarikiwa kuimba, kufundisha, kuhubiri wewe una kipaji cha kuandika. Usilalie hiyo talanta. Kesho aliyekupa atakuuliza umeifanyia nini.Frederick

 2. Hahahaa, Fredrick,
  Asante sana ndugu yangu, nitafanyia kazi ushauri wako.

  Ubarikiwe!

 3. Sungura uko sahihi kabisa. Na nimefurahia ufafanuzi wako. Nimefuatilia majibu yako katika blogu hii. Naona una karama ya ualimu yaani kufundisha na kueleweka. Umeshafikiria kuandika kitabu cha maswali na majibu ya wapendwa wa Mungu katika safari yetu. Bila shaka kitauzika na kitatubariki wengi.
  Fredric

 4. John Pau ameuliza maana ya muujiza ni nini, mimi namjibu hivi:
  Muujiza ni ilie asili ya uungu au asili ya Mungu kujidhihirisha katika aslili ya ubinadamu.

  Au niiweke hivi: God’s nature is human being’s supernatural. Yaani kitu ambacho kwa Mungu ndio asili yake kikitokea kwa mwanadamu kinakuwa ni asili ya uungu(supernatural). Kuponya mtu bila dawa ndio asili ya Mungu, lakini kwa mwanadamu anayeponywa kwa njia hiyo huo ndo kwake unaitwa muujiza.

  Hivyo basi, mahubiri ya huyo mhubiri japo sikuyasikia mwenyewe, yalikuwa sahihi. Huyo jamaa sidhani kama alikuwa na tumaini la kuweza kuingia kwenye hayo maji siku moja. Maana kama angekuwa na tumaini angeweza kuona kuwa angalao Yesu ndo mtu aliyepatikana kwa ajili ya kumwingiza kisimani.

  Lakini pia najiuliza, ni nani alikuwa anampa chakula, na kumsaidia atakapo kujisaidia? Lazima kulikuwa angalao na mtu wa kumfanyia hizo huduma, hivyo angeamua angawababna hao wamwingize kwenye maji.

  Si kila muujiza unaweza ukaja wenyewe bila bidii zako, nina mifano ya kutosha:

  Ahadi ya Mungu ilikuwa wana wa Israel wakae utumwani Misri miaka mia 4 tu, lakini walikaa miaka 430 – why?

  -Ahadi ya Mungu ilikuwa Israel wakae utumwani Babeli miaka 70, lakini ilimbidi Daniel amkumbushe Mungu kuwa muda umefika – why?

  -Bar Timayo yule kipofu asingesisitiza kuita Yesu Yesu unirehemu mnadhani siku hiyo angepata kuona? Yesu mwenyewe alikuwa ameshapita akienda zake, lakini bidii ya jamaa ilimrudisha.

  – Yule aliyetokwa na damu miaka 12, bila kufanya bidii ya kupenye makutano mnadhani angeweza kuugusa upindo wa vazi la Yesu? Alifanya kwa bidii kujipenyeza.
  N.k.

  Kwa hiyo kuna miujiza ambayo iko ndani ya mapenzi ya Mungu yanayohitaji ushiriki wa mtu (Tharema), na mingine iko ndani ya mapenzi ya Mungu yasiyohitaji ushiriki wa mtu ( Burumai), ambapo utake usitake Mungu atafanya!

  Kufufuliwa kwa Lazaro hakukuhitaji eti mpaka mtu fulani aamini!
  Kufufuka kwa Yesu ni muujiza ambao haukuhitaji mtu aamini au afanye chochote!

  Kwa hiyo ni kweli kuna mambo fulani yanaweza kukutesa na Mungu nae akakuangalia tu kama hakuoni, kama yanahitaji wewe uchukue hatua!

 5. Kuna jambo kubwa la kujifunza kwa huyo Kiwete, 38 years lkn still alikuwa na matumain ya kupona. uvumilivu ni Muhimu. kuna wakati wa Mungu ata ukimbie kiasi gan kama hujafika hutakiona kile unachokitafuta……. au tuseme Ibrahim nae alikuwa mzembe ndo maana alikuja kupata mtoto akiwa Mzee? no, sa nyingine tukubali kila jambo na majira….. kama una ahadi ya Mungu endelea kushukuru ktk wakati wake utaiona ikitokea, umeomba mda mrefu hujaona majibu nataka nikwambie mtu wa Mungu kuna wakati katika Jina la Yesu.

 6. Biblia inasema mnapotea kwa sababu hamyajuwi maanidiko. biblia imesema wazi kabisa kwamba “Yesu alipomwona huyo alimwonea huruma, akamwuliza wataka kupona?” cha kwanza kabisa angalia sehemu inayosema Yesu akamwonea huruma, Biblia haijasema Yesu “Hakupendezwa naye” na wala yule Mtu hakufukuzwa pale birikani isipokuwa aliponywa na mara baada ya kuponywa akaamriwa kwenda zake akaendelee na shughuli zake.
  hayo ni mafundisho ya walimu dhaifu

 7. Bwana asifiwe,
  Nakubaliana na wewe kabisa na maoni ya
  ndugu Zabloni, ndivyo mhubiri alivyosema, ange crawl, na kuwa abgekaaje miaka 38, kusubiri uponyaji la hasha, na kama alivyoweza kujieleza kwa Yesu, vile vile angejieleza kwa wanadamu ambao wangemsaidia. Na kuwa Yesu hakufurahishwa ndio maana aliposema hana msaada, hakumjibu kitu, akasema chukua godoro lako uondoke hapa. Na kwa msisitizo wa mhubiri. Ni kuwa aondoe uchafu wa maqazo ya kujidekeza, na uvivu wa kutafuta uponyaji. Na Yesuhakumgusa wala kuomba wala kumwambia umesamehewa Dhambi zako. Ni mahubiri magumu kuelewa au kukubaliana nayo ila anasisitiza kutokata tamaa unapoona muujiza unachelewa na kukazana kusoma neno la Mungu kuona muujiza wako unakwamia wapi, na ufanye nini kuhakikisha unapatikana chini ya miaka 38. Na tusidhanie kuwa hatuna uwezo wa kubadili hali zetu, yaani ukiwa katika Yesu. Hakuna lisilowezekana.
  asante
  greta

 8. Na hapa palikuwa na mtu, ambaye amekuwa HAWEZI muda wa miaka thelathini na minane. (msisitizo wangu)
  ( Yohana 5 :5)

  Hivii nini maana ya mtu ambaye HAWEZI??

  Kwani ilikuwaje wale jamaa wakatoboa paa la nyumba ili kumfikisha mgonjwa kweny uponyaji??

  Ni rahisi kuanza kufanya mfano tukio fulani baya lililompata mtu mwingine lakini kama limekupata hilo unabakia kuwashangaa wanaokufanya mfano!

  Yule mtu alikuwa HAWEZI! Kama angeweza kutambaa na kufika yeye siyo mjinga akae pale miaka yoooooote wakati watu wanawahi, wanapona na kuondoka. Ndiyo maana akajibu HAKUWA NA MTU WA KUMTIA BIRIKANI: Alihitaji msaada wa mtu mwingine!! Peke yake alikuwa HAWEZI!!

  Sasa mimi sioni kama ni sahihi kumlaumu mtu ambaye ALIKUWA HAWEZI utafikiri tunafahamu alikuwa na uwezo wa ku-craw!!!

  Kwani muujiza maana yake nini?? Hivi kwani muujiza huwa unawekwa mahali kisha unaambiwa ukauchukue?? Au labda mi ndiyo sielewi maana ya muujiza!!

  @ Zabron Hibwa

 9. Bwana Yesu Asifiwe, mimi niliyaona hayo mahubiri, na niliyapenda sana! Alimaanisha Kuna watu wengine miujiza yao iko tayari ila wanafanya uzembe kuifikia.Akasisitiza kwa miaka 38 hata kwa “crawl” angefikia birikani. Wengine badala ya kupokea miujiza yao wamebaki kuwalaumu wachungaji wao.

 10. KUNA WAGONJWA WENGINE WALIKUWEPO KWA AJILI YA KUDHIHIRISHA UTUKUFU WA MUNGU WAKATI ULE WA YESU.

  MFANO UPONYAJI WA LAZARO AMEUCHELEWESHA MAKUSUDI,ILI WAJUE YEYE NI ZAIDI YA KUMPONYA LAZARO,YAANI ATAMFUFUA.

  YOHANA 11:1-4
  BASI MTU MMOJA ALIKUWA HAWEZI, LAZARO WA BETHANIA, MWENYEJI WA MJI WA MARIAMU NA MARTHA, DADA YAKE. 2 NDIYE MARIAMU YULE ALIYEMPAKA BWANA MARHAMU, AKAMFUTA MIGUU KWA NYWELE ZAKE, AMBAYE LAZARO NDUGUYE ALIKUWA HAWEZI. 3 BASI WALE MAUMBU WAKATUMA UJUMBE KWAKE WAKISEMA, BWANA, YEYE UMPENDAYE HAWEZI. 4 NAYE YESU ALIPOSIKIA, ALISEMA, UGONJWA HUU SI WA MAUTI, BALI NI KWA AJILI YA UTUKUFU WA MUNGU, ILI MWANA WA MUNGU ATUKUZWE KWA HUO.

  MGONJWA WA PALE KISIMANI:

  MGONJWA YULE ANGEPONYWA MIAKA 34 NYUMA YAKE YAANI AKIWA NA MIAKA MINNE YA UGONJWA WALA ASINGEKUWA CHANZO CHA UTUKUFU KWA MUNGU MAANA MIAKA 34 NYUMA YESU HAKUWA AMEKUJA DUNIANI.

  TENA ASINGEPONJWA PALE KISIMANI ILI ABEBE GODORO KICHWANI SIKU ILE WATU WASINGEJUA KUNA MTU AMEPONYWA, KWANINI MLEMAVU ALIYEKUWA ANALALA TU JUU YA GODORO LEO AMELIBEBA KICHWANI BADALA YA GODORO LIMBEBE.

  KWA HIYO WOKOVU WAKE HAUKUCHELEWA ILA ULIKUA KWA WAKTI ULIOKUSUDIWA, HIVYO LIWE SOMO YAANI SIKU YA KUTANGAZA, KUHUBIRI KUPITIA KUBEBA GODORO ALILOLIBEBA KICHWANI, ALILOKUWA AKILALIA ALITANGAZA INJILI.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s