“Sisi wa Rohoni”

image

Kama kuna sentesi ambazo unaweza mara nyingi kuzisikia, kuziona kutoka kwa wapendwa/wakristo wanaomuamini Yesu ni hii ya  “Sisi wa rohoni”

Utasikia:
Sisi wa rohoni tumejua;
Ukiwa rohoni utajua tu;
Lazima ukae rohoni ndiyo uelewe;
Tuendelee kukaa rohoni;
Haya ni mambo ya rohoni;
Watu wa rohoni wanajua; nk.

Hivi huwa tunamaanisha nini hasa?
Sasa kama jambo limeulizwa na majibu yakawa hayo aliyeuliza yupo upande upi sasa?

Haya! Kama watu wa rohoni mnajua kwa nini muendelee kunyamaza wakati watu wa upande mwingine wanaendelea kupotoka?

Kuna faida gani sasa ninyi kufunuliwa mambo hayo?

Je hii haiwezi kuwa kama ni woga au kutaka kufumba fumba tu watu wengine?

Je hiki siyo kiashiria cha kukosa ujasiri wakati mwingine?

Hivi Mungu akikufunulia jambo ni kwa faida ipi na ya nani?

HATA sijajua ninapouliza haya maswali kama nipo rohoni au kwa nguvu ya sembe na dona tu hata sielewi!
Naomba kusaidiwa kwenye vipengere hivyo nilivyouliza.

Alphonce Kwende

Advertisements

6 thoughts on ““Sisi wa Rohoni”

 1. Kwende,
  Haya ni maswali mazuri sana. Kwa upande mwingine mtu anaweza kuyafasiri kama ni kejeli hivi, lakini ukiyaangalia vizuri ni maswali tu yenye lengo la kutaka kujuzwa zaidi.
  CHa ajabu zaidi hao wanaosema wako rohoni, hata Biblia yenyewe wanaikanyaga! Ukweli ulioandikwa ndani hawaujali, wanafuata tamaa na hisia zao wenyewe tu. Ukiwauliza, watakwambia wako rohoni! Ufedhuli mtupu!
  Siyi

 2. Ivi dada Magreth hujui Kiswahili au hii michango yako huitoa mahala fulani na kuitupia hapa kama ilivyo?
  Ni swali tu!

 3. YEREMIA 9:23
  “BWANA ASEMA HIVI, MWENYE HEKIMA ASIJISIFU KWA SABABU YA HEKIMA YAKE, WALA MWENYE NGUVU ASIJISIFU KWA SABABU YA NGUVU ZAKE,WALA TAJIRI ASIJISIFU KWA SABABU YA UTAJIRI WAKE.”

  MAJIVUNO SI MAZURI KATIKA SAFARI YA MBINGUNI,TUSIJIFANYE WA KIROHO BALI TUFANYWE NA BWANA,MAANA KAMA NI BWANA AKIFANYA KAZI NDANI YETU TUWE WAKIROHO HATUJISIFU KWA KUWA HATUKUJIFANYA HIVYO BALI TUMEFANYWA, MAANA REHEMA ZAKE ZATUFUNIKA UTUPU WETU.

  TUSIWADHARAU WAKRISTU WACHINI NDANI YA MAKANISA YETU TUKASEMA HAWANA ROHO,KWA KUWA WACHANGA KIIMANI.

  -ASIPOOMBA DAKIKA NYINGI TUNASEMA SIO WA KIROHO,AKIOMBA SANA HUYO NI MTUMISHI, MTUMISHI……..

  KILA MMOJA AUPONDE MOYO WAKE KWA IMANI KWA YESU,NA KIBURI CHA UZIMA KITAKOMA.

 4. The reason that God calls for us to covet the gifts, especially prophecy, is that these manifestations are not for our own benefit, but primarily for the benefit of others. It takes an unselfish, dedicated Christian to be raised in purity and maturity in their ministry.

  The Gifts of the Spirit are a manifestation of God’s love and grace. God continues to reveal Himself to individuals and groups of Christians in the Church today to mature them and to bring about His plan and His Kingdom in the Earth.

  He wants you to eagerly desire to be used in the gift of personal prophecy so that He can make Himself known to lost and hurting people through you. What a privilege it is to be His minister of reconciliation to his lost sheep (2 Cor. 5:18-20). We are His ambassadors in the earth today. He desires for believers to walk in the manifestation of the Holy Spirit to see the Great Commission fulfilled so that those who are lost in darkness can come to know Him as their Father.

 5. zaeni matunda mema,zaeni yenye baraka x2 bwana akiyapokea yatabarikiwa… wa rohon kwa ajili gani kama jamii haibadiliki?

 6. Kaka alphonce kwende. Joeli 28 inasema Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;
  29 tena juu ya watu. Roho yule yule anaeongea na hao wa rohoni iwapo utaamua kukaa kwa Mungu kwa uaminifu. Usisubiri watu wa rohoni wafunuliwe hata wewe Mungu anaweza kuongea na wewe

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s