Adui King’ang’anizi

 

wpid-index.jpeg

 

Mhhh!

Maadui wengine kwenye maisha wako kama
Farao!

Unakutana na mtu kazini, kwenye biashara au
katika uwanja mwingine wowote wa maisha.
Inatokea tuu anakuwa adui yako pengine kwa
kusikiliza maneno ya uongo ya kuwachonganisha,
anayakazia kamba, anakuwa adui na kujiapia
kwamba atakula na wewe sahani moja! Au tuu
inatokea ulitaka kumshauri jambo, anageuza post,
inakuwa wewe ndiyo unajifanya unajua kila kitu,
anaanza kupambana na wewe ili udhaifu wako
auweke hadharani!

Kwa yule inayewezekana kujitenga naye
unajitenga, unahakikisha huingii katika “18” zake,
ukijua yatakwisha! Lakini wapi. Utashangaa
anaanza kupeleleza shughuli unayoifanya na
kutaka kukusanya data kwa kila mtu
anayekufahamu ili tuu apate pa kukutafutia
sababu akufuate huko huko uliko, pamoja na
kuwa ulishampisha kabisa katika uelekeo wake
wa maisha!

Anaanza kutafuta ulipopita ili na yeye akufuate!
Hapati raha kama hajapata nafasi
yakukukarahisha na anaweza akazua jambo
kubwa la kukusingizia ili tuu uadui uendelee
kuimarika na watu wakuone kumbe hufai!
Sasa unaanza kuwaza: Mbona huyu
nilishamuachia mambo ya maisha yake? Mbona
kama ni ofisi tulitengana kila mtu akabakia na ya
kwake?? Mbona nilishahama kabisa toka kwenye
kampuni anayofanyia yeye kazii?? Sasa kwa nini
bado ananifuatilia??

Ndipo linakuja jibu hiviiii: Kuna watu wana “roho”
ya Farao!
Wana wa Israel wameshakwenda zao lakini bado
jamaa aliwafuatilia hadi ndani ya baharii!!
Huyo mtu anayelazimisha vita na mtu asiye na
hatia mwisho wake ni lazima uwe kama jeshi la
Farao: Kumezwa na bahari!!

Solution: Ukiona mtu wa namna hii yuko nyuma
yako, kila ukibadilisha gia, na yeye anabadilisha.
Ukiingia garini na yeye anaingia; ukisema ngoja
nimuachie ntasafiri kwa trekta na yeye anashuka
anapanda trekta: Ukibadili namba ya simu
unashangaa kishaipata na anaendelea
kukuandikia sms za maudhi na vitisho-bubu….

Ukimuona mtu wa Hivyo Kaza Kumtazama
Mungu! Tafuta uso wa Mungu aliye Mtetezi wa
wenye haki! Kwa Hakika Mungu atakuelekeza
kwenye Bahari…siyo lazima iwe ya Shamu!
Itafika tuu mahali Mungu atamshughulikiaa na
atapotelea humo na ndiyo unakuwa mwisho wa
kumuona tena akisumbua sumbua maisha yako!

(Na ole wako wewe ambaye itamlazimu Mungu
akushughulikie ili mtu wake, mcha Mungu wake,
apate Amani maishani mwake!!!)

Wanadamu tupendaneni!

John Paul

8 thoughts on “Adui King’ang’anizi

 1. nzuri sana, kuna adui wanaonekana kimwili, kuna wengine unaweza usiwajue kama upo kimwili, which means wao huharibu rohon tu kama kwenda kwa waganga au kuloga kwa namna yeyote ile lkn kwa nje ni marafiki wazuri sana na wakt mwingine ndo wafariji wataabishaji. tusimame na Yesu ushindi ni wetu siku zote… watatawanyishwa, watapondwa kabisa

 2. Bwana asifiwe,
  asante ndugu Herman kwa mchango wako. Inasikitisha kusema kuwa kuna madudu zaidi tunayoyatenda kwa kutokupendana. Nakumbukiaa mpendwa mmoja alikuwa ananiambia jinsi anavyofunga na kuomba ili mtu ambaye anayemchukia (vile anapendelewa na boss, anapewa upendeleo wa Safari na marupurupu, na sie wengine kama hatupo.) Ili afutwe kazi au afe kabisa.
  Ni kama uliyosema Yesu hakuleta dhehebu, alikuja ili tuwe na uzima kamili, tupendane. Ukikutana wa dizaini ya boss na rafiki yangu wa kiroho, ni n kuomba tu upenyo, utoke uwe mbali nao, ndio nolichofanya.
  Greta

 3. Bwana asifiwe,
  asante ndugu Herman kwa mchango wako. Inasikitisha kusema kuwa kuna madudu zaidi tunayoyatenda kwa kutokupendana. Nakumbukiaa mpendwa mmoja alikuwa ananiambia jinsi anavyofunga na kuomba ili mtu ambaye anayemchukia (vile anapendelewa na boss, anapewa upendeleo wa Safari na marupurupu, na sie wengine kama hatupo.) Ili afutwe kazi au afe kabisa.

  Ni kama uliyosema Yesu hakuleta dhehebu, alikuja ili tuwe na uzima kamili, tupendane. Ukikutana wa dizaini ya boss na rafiki yangu wa kiroho, ni kuomba tu upenyo, utoke uwe mbali nao, ndio nilichofanya.
  Greta

 4. Amen to that, binafsi nilishawai kumwamini mwanamke mwenzangu saaaana kiasi ambacho tulishare mambo ya ndani mana ndoa zetu zilikuwa na maumivu kwetu tulikutana katika mitandao ya jamii wote tukiwa katika grp moja la wanawake na tulikuwa tunashauriana mambo meeeeengi sana ndipo siku moja nikaona ya huyo mwanamke niliemwanini ninkama yangu tukaanza chart inbox kupeana moyo mana ndoa zetu zilikuwa zimevunjika ila mwenzangu alihakikisha amamtafuta mume wangu na kumweleza mambo siyo nimekuja kujua too late mpk leo sijaweza kujua sababu ya yeye kuwa nyoka, ndoa yangu badala ya kupona imekufa kabisaa, huyo mwanamke sijawai
  Kumwona kwa sura zaidi katika mitandao ila yooote namwachia MUNGU IPO SIKU NAYOAMINI MUNGU ATAMGUSA NA MWANAMKE HUYO ATAKUJA KWA MAGOTI, wanawake tupendane ndoa ni ngumu tupeane moyo na si kuchomeana utambi, namshukuru MUNGU kwa yote.

 5. salaaam wote, sasa ndg greta,na john paul mnashangaa nini hapo? hasa ndg greta,hao si ndio wa rohoni wa leo hii, wanafunzi na jamaa makutano wa YESU walipomwita mtakatifu alikemea na kusema ni mmoja tu mtakatifu baba wa mbinguni japo MUNGU anasema ni wazuri kama nini watakatifu walioko duniani lakn sio wa kujiita. greta na mtoa mada ninyi pia ni miongon mwa wa rohoni na mnashudia dunia inavyoigiza. ndg greta hyo ni ndogo sana yapo makubwa madudu zaidi. kilichobaki kila mmoja na ajitafakar mwenyewe na MUNGU wake, wapi alipo na aenda wapi! tuache makundi kimadhehebu hatufiki popote. ndg john paul ni kweli mambo hayo yapo tena sana na ndio mfumo wa sasa ulivyo. niombeeni kwa MUNGU niache kutenda dhambi

 6. shetani ndiyo adui yetu

  YAKOBO 4:7
  “Basi mtiini Mungu, Mpingeni shetani naye atawakimbia.”

 7. Bwana asifiwe!
  inasikitisha kusema kuwa watu wa aina hiyo wapo tena wengine ni watu wanaojiita wao ni wa rohoni, kuna mmoja nilikuwa nafanya nae kazi ofisi moja, chuki aliyokuwa nayo juu ya mtu fulani, ilinishangaza, ni kama ulivyofafanua, inatisha na kusikitisha.
  Nadhani unaweza kumfananisha na Sauli, aliyekuwa anamrushia Daudi mkuki ili amuue, Daudi alikuwa anakimbia mbali na uso wake, na ingekuwa rahisi kwake kuudaka na kumrushia mwenyewe, ukumbuke alikuwa shujaa wa vita, alimuua Goliat kwa kumlenga, angeweza kumlenga na kumuua, lakini hakutaka kumgusa mtiwa mafuta wa Bwana,
  na wewe hali kadhalika., usisumbuke kugombana na watu wa namna hiyo ni personality issues. Huwezi kuhangaika nayo. Utajiumiza, kaa mbali naye, muombe Mungu akupe wewe mpenyo
  Greta

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s