HAKI Iinuayo Taifa ni Ipi?

 

wp-1448628784201.png

Haki huinua taifa; Bali dhambi ni aibu ya watu  wote. (Mithali 14 :34)

Ni haki Ipi iinuayo taifa! Je, ni HAKI ya Kumcha Mungu au Ni Haki ya Kutenda mambo kama yalivyopangiliwa kuwa katika taifa husika??

Ziko nchi nyingi Duniani ambazo viongozi wake hawamchi Mungu lakini nchi hizo ziko juu kiuchumi. Hali za maisha ya watu wake ni bora kabisa!

Karibu kwa maoni yako!

 

Advertisements

3 thoughts on “HAKI Iinuayo Taifa ni Ipi?

 1. naungana na wapendwa/watumishi wa Mungu waliochangia hoja hii,haki inayozunguzwa ktk mith 14:34 ni ile ya kumhofu Mungu (kumcha Mungu),ukisoma ktk kitabu cha k/torati 28:1–14 utaona Mungu anavyo agiza kwamba tutakapoisikiliza sauti yake kwa bidii na kufanya sawa na alivyo tuagiza ndipo atakapo toa baraka.Pia kumbuka kuwa Mungu ndie aliyeumba vitu vyote hivyo ili taifa au hata mtu binafsi afanikiwe nilazma amskilize Mungu anacho Muagiza kufanya.

 2. Bwana asifiwe.
  Nakubaliana kabisa maneno yaliyosemwa na Mille hapo juu.
  Na nimeguswa kusemea hilo la kuwa kuna mataifa ambayp viongozi wake hawamchi Mungu lakini wana maendeleo kiuchumi. Nashukuru umeishia hapo kiuchumi maana ndio maendeleo waliyonayo.
  Nimebahatika kuishi hizo nchi wana matatizo mengi. Kuna mahonjwa ambayo hujawahi kuyasikia. Umeshawahi kusikia dementia wazee wao wengi wao wakizeeka wanapata huo ugonjwa ni kama wazimu fulani wanawasahau hata watoto wao., hawakumbuki tena wao ni nani tena. Na Watu wazima nao wameshikwa na kazi hadi hawana muda wa kuwaangalia wazee wao, ukizeeka unapelekwa kwenye nyumba za kulea wazee watakuja kukusalimia wakati wa xmas basi. Watoto wao wamelewa na madawa ya kulevya na ushoga. Umesikia vyombo vya habari jinsi wanawake wanavyotaka kujibadili wawe wanaume na wanawake na vs., hayo yote ni magonjwa ya akili na kutokujitambua. Wati hawawawajui hata majirani zao, mtu anaweza afe ndani kwake kwa wiki na hamna mtu anayejua kama kuna mtu kafa.
  Hivyo ni hatari kupima maendeleo ya nchi kwa uchumi wake. Wapo nyuma katika ngazi zote kimaisham hivyo hawajaendelea kama unavyodhani

 3. UMEULIZA Ni haki Ipi iinuayo taifa! Je, ni HAKI ya Kumcha Mungu au Ni Haki ya Kutenda mambo kama yalivyopangiliwa kuwa katika taifa husika??

  Haki inayozungumziwa hapa ni haki ya Kumcha Mungu,

  “Kumcha BWANA ni kuchukia uovu;” Mithali 8:13

  Fungu ulilolitoa la haki,huisema dhambi kwa upande wa pili

  “Haki huinua taifa; Bali dhambi ni aibu ya watu wote.” Mithali 14 :34
  “Kila lisilo la haki ni dhambi,……” 1 Yohana 5:17

  Huwezijiita wewe ni mtu wa haki kama huchukii na kuiacha dhambi,hata kama utaonyesha watu kuwa unajali watu kwa nje sharti haki hii iwe haki ya Kristo si haki ya maonyesho. Upendo wa ndani kuwapenda binadamu wenzako kama nafsi yako,wapate raha kama wewe hutowaibia,kutamani mali zao na hata kupora, kutompendelea mtu bali ukimpenda kila mmoja kwa usawa,huku ukimcha Mungu yaani kuchukia uovu…ndipo taifa linapoinuliwa.

  Nebukaneza:
  Danieli 4 : 27
  Kwa sababu hiyo, Ee mfalme, shauri langu lipate kibali kwako; ukaache dhambi zako kwa kutenda haki, ukaache maovu yako kwa kuwahurumia maskini; huenda ukapata kuzidishiwa siku zako za kukaa raha.”

  Huwezi tenda haki ya Kristo kwa watu hata kama wewe ni mtawala, bila kuacha dhambi, utakuwa una tatenda ile haki ipatikanayo kwa sheria ambayo hauwezi kuifikia haki halisi yaani haki ya Kristo.

  Haki ya wajibu ni haki ambayo hata dikteta hitler alimfanyia mkewe na watoto,kuwalisha,kuwavisha, na kusukuma taifa mbele kimaendeleo lakini hakuchukia,uovu akawaonea na kuwaua wayahudi akaangusha taifa badala ya kuliinua.
  Yesu anaitwa
  “Kristo Haki yetu”
  “Mfalme wa wafalme”

  Kwa kuwa Yesu, ufalme wake unachukia dhambi, wala hauna upendeleo
  Mfalme akiiga tabia ya utawala wa Yesu atainua taifa.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s