Nini maana ya Ndoto hii?

wp-1449637914393.jpeg

Shalom wana Blog!

Naombeni kuambiwa maana ya ndoto hii kwani sio mara moja nimeota.

Kuota unapanda sehemu yenye mteremko sana(kilima) tukiwa na wenzetu lakini mimi hufanikiwa kupita, kisha kufanyiwa uchawi na watu nisowajua, na kuzungukwa na mapepo lakini huwa nayakemea sana kisha kutoweka.

Maana yake ni nini?

Mimi Sia

Shalom!

13 thoughts on “Nini maana ya Ndoto hii?

 1. Shalom Sia! Ndoto yako ni ujumbe tosha kuhusu mapambo yanayoendelea na ushindi wa kuwashinda hao maadui. Kumbuka ndoto ni ujumbe kamili Mungu anaoufikisha kwetu kwa kusudi maalum ikiwemo taarifa, kujiandaa, tahadhari au majibu ya mapito unayopitia. Endelea kuomba mpaka hiyo ndoto itapoacha kujirudia. Barikiwe!

 2. Kemea nguvu ya uchawi, vunja mitego iliyowekwa na shetani na wachawi mbele yako. simama vizuri kwa Yesu, ialike Damu yake inanayo mema inene kwa ajili yako…….

 3. bwana asifiwe wapendwa nami nimefurahi namna mmetoa maoni katika ndoto hii naomba nami pia kama kuna mtu anaweza nisaidia mara mbili nimeota mtoto analia sana moyo wangu unahangaika sana hata nikishituka bado moyo huuma ingawa sauti hukatika

 4. Sia nakushauri ufuate ushauri wa Gladys Simtitu Mungu ana tumia njia nyingi kuwasiliana na sisi kumbukeni jamani mnaochukulia simple hilo swala kuwa mtu ni roho anaishi ndani ya mwili na roho ina asili ya uungu hivyo inaweza kuona au kuoneshwa vitu vilivyoko sirini lkn kila inapo jaribu kuviweka wazi kwa mwili kupitia Nafsi inakumbana na vipingamizi hivyo roho hukaa kimya na hapo mabaya humtokea mtu lkn utaskia anakwambia hiki kitu kama vile nilisha wahi kukiota so hicho alichokwambia Gladys ni chamuhimu kwa kuwa roho ya mwnadamu inahitaji kusaidiwa na Roho wa Mungu kushinda na zaidi na zaidi so Mungu anasubiri utayari wako.
  Shalom.

 5. Mpendwa bwana Yesu asifiwe, Inaonekana unafanya kazi nyingi sana mchana, Mara nyingi ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi Jaribu kupumzika macha kipindi kirefu kidogo] Barikiwa

 6. Sia,
  Kwa neema ya Kristo naweza kukwambia hivi hiyo ni taarifa umepewa na mbingu kuwa mbeleni yako kuna jaribu gumu au kubwa ambalo limefananshwa na kilima chenye mteremko mkali. Kumbuka mteremko ukiwa mkali sana ni ngumu kushuka vvyo hivyo ni mgumu kuupanda.

  Umeahidiwa USHINDI sbb umeona unavuka lkn baada ya kulivuka jaribu hilo kuna vikwazo tena mbele yako.
  Nakushauri fanya Maombi makali sasa kutafuta nguvu ya kukuvusha wkt na baada ya jaribu hilo. Funga omba kiri USHINDI ndiyo salama yako. Barikiwa!

 7. pole sana mpendwa lakin kwa uwelewa wangu nafikiri unapewa picha fulani ya upepo wako,kuwa ktk safari yako kuna mafanikio ktk jumuia ulionao, ktk hayo yapo mafanikio makubwa unayoyapata kwa shda kubwa lakn unafanikiwa na kukutana na magumu yaliyotokana kufanikiwa kwako kama ujuavyo ktk jamii yetu 60% ya watu hupenda udumae aidha kiroho au kimmwili,mara ufanikiwapo kundi baya huenda mbele kukusukasuka urudi nyuma,ukomavu wako hukufanya ujitoe ktk misuko hyo(kemea) na kuwa huru/kufanikiwa zaidi. MUNGU hupenda kutuonesha safar zetu japo kwa ufupi. na hyo ndiyo safari yako. MUNGU wa mbinguni akujalie kuyashinda ufika salama chini ya kilima hicho.

 8. Dada Juliana,

  Namna ya kutuma mahitaji ni kama ulivyoandika hili ombi.
  Yakifika kwetu tutajua mahali pa kuyaelekeza. Kama siyo ya kuweka hadharani, tutafanya hivyo, kwa kadri utakavyoelekeza wewe!

  Mungu akubariki unapoendelea kutembelea blog hii.

  SG

 9. shalom nionavyo mimi unayafikia mafanikio yako lakini bado wapo wakupingao, mwenye kujua maana zaid atuambie ili tufahamu jamani.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s