Kuenenda Kwa Imani (2Kor. 5:7)

 

images-3.jpeg

Kadri siku zinavyokwenda ndivyo mambo MAPYA yanaibuliwa ili kusindikiza imani!

Katika suala la maombezi, hasa nchini Tanzania, ilikuwa mtu anaombewa tuu kwa kuwekewa mikono na kwa IMANI anapokea uponyaji na anaondoka amepona.

Mambo yaliendelea hadi ikafikia mtu anapewa kitambaa, mafuta, bangiri au kitu chochote kinachobebeka kwa urahisi, kwamba UPONYAJI WAKE UKO NDANI YA HICHO KITU. Anapewa na kuelekezwa namna ya kukitumia!

Mambo yameendelea na sasa, kwa mfano, Watu inabidi Wapite, wakanyage mafuta au wapite kwenye beseni la maji, kwamba kwa kufanya hivyo watapokea UPONYAJI au Majibu ya mahitaji yao. Na mengine mengi!

Jee, Katika Hali ya namna hii bado kweli IMANI IPO au sasa TUNAENENDEA KWA KUONA?

Ni wapi ambako Ukristo Unaelekea?

Haya mambo yanayofanyika wakati wa maombi, mfano wa hayo yaliyotajwa hapo juu, LENGO LAKE NI ZURI au BAYA?

 

Advertisements

19 thoughts on “Kuenenda Kwa Imani (2Kor. 5:7)

 1. Wakati yesu hajaondoka aliwauliza wanafunzi wake hivi, mwana wa adamu atakaporudi je atapata IMANI ingalipo?, na jibu tanaliona Wakati huu, KWELI IMANI HAIPO,

 2. Ninawashukuru sana wote waliotoa mchango wao katika mjadala huu nami nimeipata kuchelewa, lakini naomba nami nitoe maoni yangu,
  Wanaotumia vitu hivi Kwanza hawana imani na neno la mungu halimo ndani yao, hawamjui mungu wala nguvu za utendaji wake. lakini mungu wetu ni mwema naye huturehumu ata katika ujinga wetu, ndo sababu wanaopewa vitu hivi kwa imani yao wanapata uponyaji, siyo kwamba hiyo njia ni nzuri lakini huwarehemu kwa kuwa ni wajinga katika imani, na hukumu inawangojea wote siku za mwisho wanaopewa na wanaopeana. maritime,

 3. Ndugu Kuna mchangiaji anasema nitapigwa kibao nisiinuke
  NAULIZA: kwani kuna wachungaji wa kweli ambao ni wauaji?

  Moja: matumizi ya vifaa huondosha akili za watu kutoka kwa yeye aliyesema
  “Njoni kwangu ninyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo nami ntawapumzisha” Mathayo 11:28

  Pili:Kuweka imani yako kwa mtu badala ya neno la Mungu ndio,kummweka kwako kama Mungu wako na ndio ibada yako kwake, Watu wengi kabla ya kuja Yesu mara ya kwanza waliweka imani yao kwa viongozi wa dini badala ya Mungu, mafarisayo,masadukayo, wote hawakujua hata masihi anazaliwaje wala hawakuhusishwa. Maana hawakuongoka mioyo bali mwonekano wa nje tu na imani ya kujionyesha.

  Katika zama za Giza matumizi ya misalaba,mapambo ya sanamu, ngazi ambazo watu walipanda kwa magoti na kuambiwa na viongozi wa dini kuwa watasamehewa dhambi kupitia hivyo, viongozi hao wasomi wa dini,madakatari,maprofessor waliishia kuamini, vitu wakimwacha Yesu aliyekuwa wazi akiinua mikono kuwapokea bila malipizi ya kubusu sanamu,nna kutumia vitu.

  Tatu: zama hizi badala ya viongozi wa dini wenye digrii za miaka saba,miaka mitatu,wamejifunza zaidi mafundisho ya binadamu na wamekuwa wa kwanza kutomwamini Mungu, ambaye anataka imani na utii,
  wakizifungamanisha dhamiri za watu wa Mungu na imani zao za ubunifu.Ziondoazo hisia za watu kwa Kristo na kuzielekeza kwao ,ili wafungwe matita kuwatumikisha kadiri wapendavyo. Huku wakiishika Biblia mkononi huku wakimkanyaga Yesu chini. wakimbusu Yesu huku wakimsaliti.

  Yeye anayesahau historia Daima atatenda makosa yaleyale.

  Mafundisho ya mashetani,yanayowekewa maiki kupitia watu wenye mapepo ni uaguzi wa kisasa. Kuwafanya waumini wayasikie mafundisho ya mapepo hayo,na mahitaji yao kwa waumuni. Ndio uganga uleule wa kienyeji ambao mapepo huruhusiwa kutoa mahitaji yao, na vitu wanavyohitaji ili kuponya wagonjwa.

  Jenga Imani juu ya Mwamba/Neno/Kristo si juu ya vitu,viongozi wa dini

 4. Ni kweli Sungura ulivyosema; Mungu ana njia nyingi za kiutendaji, lakini I’m worried na motive behind some of who self-call mitume na manabii. These people crave to perfom miracles so much! And they wear all the titles on themselves. Because they have got a business out of ministries. And their markrting strategy has been healing and healing, wonders and wonders, miracles and miracles, no different from the “waganga wa kienyeji”. The grand objective is to have a big congregation that can maximize earnings.
  And many Africans are still bewitched under fortune-telling and sort of. Easy to win them. The gospel is not about miracles & wonders; the gospel is about the “Kingdom of God.”

 5. Ni Kwel Kabisa Ukristo Wa Sasa Unaendea Kubaya Sana Kwani Vitendo Vinavyofanyika Sasa Ni Tofauti Kabisa Na Kipindi Kile Cha Bwana Wetu Yesu Kristo Alivyokuwa Akifanya Huduma Zake. Ila Mungu Wa Mbinguni Atusamehe Na Kutuokoa Katika Hayo.

 6. kwako mile, unadhani jambo hili la ku2mia vitambaa,maji,mafuta n.k limeanza leo? wakatoliki ku2mia misalaba na picha ya b.maria haijaanza leo, inazungumzwa sana, unadhan katoliki na sisi tunaopewa vitamba,mafuta n.k kuna tafauti? au kwa kuwa wao iko open kila siku? huenda tafsir ya matumiz ya misalaba au picha zao ikawa sawa na hii ya mzee wa upako,kakobe,gwajima n.k ila usimzungumzie gwajima akikusikia atakupiga kibao usiinuke tena,ana upako uliopitiliza yule ndio mchungaj wa kwel. mambo haya huendana na imani za waombewa na anayeomba,si ndio mambo ya imani hayo? tusishangae wakatoliki wakija na mengne. sandeni

 7. Maji hayaponyi, mafuta hayaponyi, kitambaa hakiponyi, chumvi haiponyi,hata mikono ya anayemwombea mgonjwa haiponyi!

  Kwa hiyo kama unaona watu wanapona kwa jina la Yesu ujue wanapona kwa imani.

  Elisha alimlalia mtoto mdomo kwa mdo na pua kwa pua, vipi kama dada yako leo angelaliwa na mhubiri mdomo kwa mdomo na pua kwa pua, kisha akapona/akafufuka si ungerusha kwenye mitandao kuwa hayo ni maombezi ya ajabu na ya kishetani!!!!

  Mama aliyetokwa na damu alisema moyoni ‘nikigusa tu upindo wa vazi lake’. Na alifanya hivyo akapona kweli. Je upindo wa vazi ndo ulimponya?

  Jifunzeni kujua viwango (Dimensions) vya imani, ili msienende kwa kukariri.

  U can’t limit God!

 8. Yaani mimi kwa kweli bado naona kuponywa kwa maji, mafuta, vitambaa na kadhalika ni upotofu hasa kwa nyakati hizi ambazo wahubiri wengi si wa kweli. Tumwombe Mungu atusaidie kujua lipi ni sahihi

 9. Mungu anajisimamia yeye mwenyewe ila leo watu wanafika mahara wanageuza kanisa kama nyumba ya mganga wa kienyeji hayo mambo tulikuwa tukifanyiwa kwa mganga kipindi ambacho hatujaokoka sasa hii leo yamefika hadio kanisani huwezi kusema hao wameokoka hapana hao ni manabii wa uongo tena ni kufunga na kuomba ili washindwe wasiendelee kupotosha watu kwa uongo na kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu ni bora waweke biblia chini wachukue matunguli wawe waganga wa kienyeji tu, na MUNGU AWABARIKI SANA.

  Ni mbaya sana na hakika ningepewa uwezo wa kuwahukumu nisingewaachia kabisa maana wanapotosha Biblia kifupi hao ni MATAPELI WA NENO LA MUNGU NA NI WAHUNI TU

 10. ni baya sana na hakika ninge[pewa uwezo wa kuwahukumu nisingewaachia kabisa maana wanapotosha Biblia kifupi hao ni MATAPELI WA NENO LA MUNGU NA NI WAHUNI TU

 11. BWANA YESU ASIFIWE WAPENDWA, MI NAONA KINACHOMPONYA MTU NI IMANI KUPITIA KITENDO KINACHOFANYWA IWE NI FRUTO CHUMVI NK
  DAYANA

 12. Hizo ni hirizi tusidanganyike

  Ezekiel 13:21

  18 useme, Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao wanawake wale, washonao hirizi katika viungo vyote vya mikono, wawekao leso juu ya vichwa vya kila kimo, ili wawinde roho za watu; je! Mtaziwinda roho za watu wangu, na kuzihifadhi hai roho zenu wenyewe?

 13. wengine ni waganga wa kienyeji waliovaa suti wanaiba roho za watu

  Ezekiel 13:21
  21 Na leso zenu nazo nitazirarua, na kuwaokoa watu wangu katika mikono yenu, wala hawatakuwa katika mikono yenu tena kuwindwa; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.

 14. Hiyo sio mbaya kabisa ni imani ya mtu tu,na nafikiri kila mwenye pumnzi anatakiwa waheshimu jina la bwana yesu kwa kumpa shukukurani kila sekunde,dakika,saa,week mwazi na mwaka,kila utokapo na utakaporudi ndani

  Sent from my Samsung GALAXY S5

 15. Sasa hivi imani imekuwa haba watu wanaamini kuliko kusikia na nafikiri tunasoma sana Agano la kale na kusahau Agano jipya

 16. Maandiko yanaonyesha uponyaji uliopatikana kwa Maji, nguo na hata mafuta .
  Hapa ndo tatizo linapokuja, neno linasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.
  Waumini hawana maarifa ambayo ni neno la Mungu, umeokoka.. hutaki kusoma neno , hutaki kusali. Unataka kuwekewa mikono tu, unataka miujiza na unabii, vipi kuhusu kusudi la wokovu ambalo Kulishika neno kulitenda ili na wewe ubebe miujiza badala ya kuitafuta? Ndio maana wakristo tunaishia kugeuza vitambaa na mafuta kuwa Mungu badala ya kumwamini Mungu, very soon watu wataanza kuogeshwa makanisani.

 17. Kama hiyo mambo wanafanya yanatokana na Nguvu za Mungu,kwangu mi naona kama wanafanya poa,but kama ni mambo ya Mtu Mwenyewe hapo si poa.. Shukurani ni Brother Symon

 18. Kiukweli iman ipo bado, na ndio maana hata kwa hayo maji na wengine fruto na wengine culture za kuvaa mikonon na wanaamin ktk hayo. Ila tukirud kwenye biblia ndio tutawajaji kwamba wapo Sawa au hawapo Sawa.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s