Mapato na Matumizi ya Kanisa

image

Katika nchi mbali mbali Duniani, na Tanzania ikiwemo, pamekuwa panatokea misuguano ya hapa na pale; Vyombo husika vya serikali vikitaka kuonyeshwa MAPATO na MATUMIZI ya pesa zinazokusanywa (a.k.a SADAKA) na Wachungaji/Wainjisti/Maaskofu au msimamizi yeyote anayehusika!

Je, Ni sawa kwa Serikali KUTAKA KUJUA Mapato na Matumizi ya Makanisa/Huduma au Kikundi chochote kilichosajiliwa kwamba Kinafanya kazi ya Mungu kupitia kuhudumia watu Kiroho na/au Kimwili?

Advertisements

11 thoughts on “Mapato na Matumizi ya Kanisa

 1. Mimi naona ni sawa kabisa kwani kuna kunakitu gani tunaogopa jamani si makanisa yote waumini wanajua kitu gani kinaendele ndani ya makanisa yao haiwezekani tu mtu akaripuka na kutaka kujua lazima kuna kitu kimeoenekana kinaendelea ndani ya makanisa au waumini wetu jamaani,
  Mara nyingi tumekuwa watu wa kulaumu tu si watu wa kutafakri kabisa

 2. Inategemea kwa nini Serikali itake kujua mapato ya Kanisa au Taasisi ya Kidini……kwa mfano Marekani….taasisi za kidini mradi ni za kidini haziombi msamaha wa Kodi, tayari zimeisha samehewa kulipa kodi kwa mamboimengi, Hivyo inapotekea kwamba mapato ya kanisa/taasisi yanaponekana yanatumika au kumekuwa na tuhuma kufanya jambo kinyume kabisa na kile ambacho taasisi imesajiliwa kufanya……..Hapo Serikali ya Marekani huwa inaingilia kati kutaka kujua kulikoni.

  Lakini serikali ( hapa USA) Haiamki asubuhi na kusema leta taarifa zako za fedha….!! La hasa, lazima ujue liko jambo, kuna tuhuma fulani, hasa kutumika vibaya KINYUME NA MALENGO YA TAASISI…….kama…..Kanisa kujihusisha na siasa…….ugaidi……nk.

 3. Makoko,

  Unaposema mtu anamiliki magari ya thamani lakini mchungaji tu, picha ninayoipata kichwani mwako ni kwamba mchungaji hapaswi ama hawezi kumiliki hivyo vitu, kitu ambacho siyo kweli.

  Acha ishu ibaki kuwa je anamiliki hivyo vitu kihalali, hajavipata kutokana na matumizi mabaya ya fedha ya kanisa, hajavipata kutokana na biashara haramu?

  Kumbuka vitu hivyo mtu anaweza kuvimiliki kihalali pia, au kutokana na kufanya kazi kwa bidii, au anatoka familia tajiri, au Mungu kaamua kumbariki tu kiukweli.

  Tusihusishe maisha ya kumtumikia Mungu na ufukara, kwamba mtu akimtumikia Mungu huku akiwa masikini ndo mtumishi hasa wa Mungu, siyo kweli.

  Utajiri na umasikini hautokani na kumtumikia Mungu au kutomtumikia, wenye bidii na maarifa mara zote hufanikiwa.

  Amen

 4. Paulo anasema katika maisha yake

  “Sikutamani fedha wala dhahabu, wala mavazi ya mtu.”
  Matendo 20:33

  sikuhizi watu wanajiita mitume na manabii lakini wanaishi kwa tamaa ya fedha na mali

  Watu wanafundishwa na wachungaji kuabudu mali, badala ya Mungu
  japo wanasadaka nyingi wanatoa kana kwamba wanamkopesha Mungu si kumrudishia.

  Mitume na manabii wa kweli walilitaja jina la Bwana si magari na farasi

  “Hawa wanataja magari na hawa farasi,Bali sisi tutalitaja jina la BWANA, MUNGU wetu.” ZABURI 20:7

 5. Kabla ya kujibu swali hilo ni vizuri kujiuliza kwa nini serikali zinaamua kufanya hivyo? Imagine mtumishi mmoja hapa Tanzania anakiri wazi kuwa ana magari binafsi 6,tena kwenye TV.Gari zenyewe ni range,Mercedes Benz,hammer,…..Huyo ni mchungaji tu,je, serikali ziamini tu kuwa hiyo ni hela ya sadaka na siyo unga? Mi nadhani inapobidi ni vizuri vyanzo vya mapato vijulikane.Ni vizuri pia watumishi kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha za kanisa/huduma.Nawasilisha.MAKOKO

 6. Suala la kanisa kulipa kodi limetoka wapi hapa, mbona hata muuliza swali hajaliuliza?

  Ishu iliyoulizwa ni mapato ya kanisa kufanyiwa ukaguzi (Auditing ) na serikali, hilo ndo muuliza swali kauliza kama ni sawa.

  Mimi sioni ubaya mapato ya kanisa kufanyiwa ukaguzi ili kujua uwiano wa mapato na matumizi. Ni ukweli usiofichika kuwa kuna matumizi mabaya ya mapato kanisani, mapato yamekuwa ya mtu mmoja (mchungaji), ambaye anafanya anavyotaka bila hata kushirikisha kanisa ( viongozi).

  Hii si injili waliyotuachia mitume na manabii, hawakuwahi kujilimbikizia mali kwa ajili yao na familia zao, bali walijali sana kuwapa wahitaji.

  Ni sawa mapato na matumizi ya kanisa kukaguliwa na wataalamu wa serikali. Hii ni kutengeneza mazingira ya waumini kujua kama mali wanazotoa zinatumika kwa malengo husika.

  Na si mbaya kusomewa mapato na matumizi ya kanisa, mimi nadahni iko kimaandiko, na dio dhana nzima ya uwazi ilivyo, kanisa linatakiwa kuwa na kiwango cha juu sana cha uwazi (Transparency)

  After all, haiko kinyume na maandiko. Kama unajiamini uko safi kwa nini uogope polisi kukagua begi lako?

  NB: Si kila mchungaji tajiri katajirika kwa pesa ya kanisa, wengine wanafanya biashara zao, wengine ni waajiriwa wa makampuni, na wengine wameokoka na kuingia uchungaji wakiwa matajiri!

 7. Mimi naona ni sawa kuto a kodi kwani kila unachokusanya ninlazi utoe kodi hii ni sawa tunaibia serikali,ukizingatia sasa hivi tunaona kazi kubwa inayonfanywa hivyo kanisa nimlazima litoe kikumi kwa serikali

 8. Kwa kweli tuombe Mungu sana maana kila serekali sasa hivi wanafuatilia sana kuhusu mambo ya sadaka pia wanataka walipe kodi, kitu ambayo hiyo ni sadaka Mungu isitoshe sio kila kikundi ina pesa nyingi. Tuombeane katika hii dunia.
  Asante sana Mungu awabariki sana watumishi wa radio safina.

 9. Mapato yeyote yanazidi kiwango kadhaa ya kampuni, au shirika lolote duniani na ambayo yamesajiliwa na serikali ikiwa hata mtu binafsi afanyaye kuingiza mapato na kusajiliwa kwa kiwango Fulani, ni lazima Inland Revenue ijue na ikusanye kodi bila kujali nani na yupi? ndio maana tunashindwa kupanga matumizi na mapato ya nchi.

  Ikiwa serikali inafaidika kutoka makanisani na misikitini kuwa sadaka zinaisaidia sector ya social welfare- kama kuinua wajane na yatima basi, fine- na wasiguswe waachiwe huru hao makanisa na misikiti. lakini utakuta yatima na wajane pale kanisani wamesahaulika. uchoyo umeingia makanisani na misikitini.

 10. Ni jambo linalohatarisha uhuru wa dini,na maandiko matakatifu,
  Mpango huo kwa kawaida unaipa nguvu serikali juu ya shughuli za kidini,

  Na maamuzi juu ya kile wanachozungumza au kuhubiri wachungaji.

  1.Kutoa mamlaka kwa serikali za dunia juu kile kinachoweza kufanyika na kutofanyika na dini.

  Dhumuni la mipango ya namna hiyo duniani ni kwa kuwa baadhi ya viongozi wa dini wanaipa serikali mamlaka yote, Viongozi hao wa dini pia watapewa mamlaka juu ya makanisa fulani/na mafundisho yao kukubaliwa.

  2.Mpango wa Social Justice/Haki ya jamii
  Mpango wa haki ya jamii ni mpango ambao unasema;
  kua Haki inawezekana pasipo Kristo”

  Mfumo huu unasema pia kuwe na mgawo wa rasilimali za dunia,kati ya walichonacho na wasichonacho ili maskini wasiichukie dunia, wajione wako sawa na matajiri pale matajiri wanaponyang’anywa mali na kuzigawanywa

  Baadhi Wachungaji matajiri wamewekwa katika kundi la vigogo ili wawe mfano tu wa kutekeleza mpango huu. wakichunguzwa mali zao na sadaka wanazopata kwa waumini.

  Lengo ni kuonyesha kuwa mtoaji sadaka/akiwa maskini na mchungaji tajiri
  hapo hakuna haki ya jamii.

  Hivyo kuzipa serikali za dunia kuingilia mipango yote ya kidini na mpango mzima wa upelekaji habari njema.

  mpango wa social Justice unahusisha kushughulikia pia viongozi wa serikali na matajiri ili kuleta mfumo wa Dunia usio wa kibepari au kisocialist.
  bali unapochuma usiwazidi sana wenzako

  Yaani watu wajifunze kutoa kwa wengine.

  MPANGO WA MATENDO YA HAKI, BILA YESU NA MGAWANYO UPYA WA MALI.

  KUMBUKA BIBLIA INASEMA KRISTO HAKI YETU,
  INASEMA PIA AKUNYANG’ANYAYE USITAKE AKURUDISHIE

  JE WACHUNGAJI WATAAMBIWA WAMEWAIBIA WAUMINI?

  MPANGO WA SOCIAL JUSTICE.unaukebehi Ukristo kushindwa kuleta haki ya Kristo kwa kuwa wachungaji wanajitajirisha, Lakini kuna wachungaji (mapandikizi wa propaganda) waliojilimbikizia mali ili kwa makusudi serikali za dunia zipate kuingiza mfumo huo kwa makanisa yote kwa kuwatolea wao kama mfano,Tanzania tunayo mapandikizi hayo. na makanisa kuwa chini ya serikali za dunia badala ya kuwa huru chini ya Yesu.

 11. Mim naona siyo muhim na Tena haifai kabisa kwa serikali au sector yoyote isiyokuwa ya tawi au ministry husika kutaka kujua mapato na matumiz au uingizwaji wa sadaka. Unajua serikali ikianza kuja kwenye sadaka tutaikosa maana ya sadaka na badala yake tutakuta tunafanya Kaz ya serekali na siyo ya mungu. Mathalan kwa Tanzania waende TRA kujua mapato Ila siyo kanisan. Lakin pia hili suala ni mshukuru mungu kupata kibali kwako coordinator kwamaana nimekuwa nkiliwaza hata Jana kwanin hata sis waamin ni kwanin tunataka kujua mapato na matumiz?? Mathalan kwa kanisa ambalo mim naabudu huwaga kila mwisho wa mwaka wanasoma mapato na matumiz kwa mwaka. Sasa hii itakuwa ni Kaz ya mungu au ni nin maana ya sadaka?? Tunatakiwa kweli kufatilia kwamba kimefanywa nin na Sadaka yenye ambayo tumetoa???? Nashukuru saaaana kwa ushirikiano. Lakin pia ntafurah kupata mtazamo wa watu wengine. Juma pili njema.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s