USIOMBE KWA KUPIGA YOWE

maombi-

Kwa nini UOMBE KWA MUNGU mpaka majirani wasikie? au wapita njia wasimame na kutazama?? Tena siku hizi watu wanajenga hema ya kukutania karibu na barabara na wakianza maombi huku milango imefunguliwa kuelekea barabarani ndipo wanapaaaaza sauti humo, na vipaza sauti vinapaaaza sauti ya maombi hata mtaa wote wasikie kuwa kuna maombi yanaungurumishwa hapo. Fire for Fire ee!!

Mahubiri hufanyika kwenye hadhara, hemani ni sehemu ya faragha kwa walioamini. Sasa ikiwa wapita njia watasimama na kusikiliza maombi yenu, au watu wa mtaani watasikia maombi yenu mpazapo sauti na huko kuflow kwenu; je wao ndio watakuja wawajibu maombi hayo?? Au mwataka kusifiwa na watu wakisema >> hao jamaa ni hatari kwa maombi, yameombwa maombi ya hatari sana pale!!” Na kunena kwa lugha nako mtu ananena kwa sauti ya juu ili wengine wasikie, na kumbe hakuna mwenye kufasiri ujumbe ule!!

Na tena wakati wa sadaka na chagizo mbalimbali utasikia:- Wenye milioni kumi wanyoshe mikono/wapite mbele, wenye milioni tano, wenye milioni mbili, wenye milioni moja, wenye laki tano, wenye laki tatu, wenye laki moja!!

Sasa hizi sadaka/matoleo ya kutangaziana viwango yanatoka wapi katika fundisho la Kristo?? Au utasikia kwenye redio/TV mtu anapiga cimu “Naitwa Kanjongole nimeshatuma mchango/sadaka yangu efu 50<<

Kiongozi wa ibada anakaribisha watu kutoa sadaka kwa kuuonesha mnoti wake wa msimbazi juu kuashiria ni wakati wa kutoa sadaka!! Mwingine yupo hapo kazi yake kuchungulia huyu kaweka shilingi ngapi! Wewe fundisha neno la Kristo Yesu kuhusu matoleoa/chagizo/sadaka afu acha watu wafanye wao kwa mioyo ya upendo na hiari. Mtu akimdhihaki Mungu kwa matoleo/chagizo/sadaka, Mungu aonaye mpaka sirini ajuaye hali na ukomavu wa kiroho na kiuchumi wa watu wake, sambamba na ustahimilivu na neema ya Mungu, kwamba katika yote hayo Mungu ndiye atahukumu, kwamba mtu amemweshimu Mungu au amemdhihaki. Maana Mungu humsamehe na kumrehemu yeye amtakaye. Na tena Mungu awafahamu wakoseao kwa sababu ya ujinga na kutokuwa na imani, na wale wafanyao hivyo kwa kuikanyaga kweli ya Mungu. Basi uonapo kasoro, usiwe mwepesi wa kuhukumu, kwa maana dhamiri yako itaihukumu vipi dhamiri ya mwingine?? Na tena hukumu yako ni sababu ya hila zako za kutaka mapato kwa hila, au kumtumikia Mungu sawasawa na hekima za kibinadamu tu!

Mathayo 6 : 1-34

6.1 Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni.

6.2 Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu.

6.3 Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume;

6.4 sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.

6.5 Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao.

6.6 Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.

6.7 Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi.

6.8 Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba.

6.9 Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,

6.10 Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.

6.11 Utupe leo riziki yetu.

6.12 Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.

6.13 Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]

6.14 Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.

6.15 Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.

6.16 Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao.

6.17 Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso;

6.18 ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.

6.19 Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba;

6.20 bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi;

6.21 kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.

6.22 Taa ya mwili ni jicho; basi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote utakuwa na nuru.

6.23 Lakini jicho lako likiwa bovu, mwili wako wote utakuwa na giza. Basi ile nuru iliyomo ndani yako ikiwa giza; si giza hilo!

6.24 Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.

6.25 Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?

6.26 Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao?

6.27 Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?

6.28 Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti

6.29 nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.

6.30 Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?

6.31 Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?

6.32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.

6.33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.

6.34 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.

Emanuel Mwinamila

Advertisements

6 thoughts on “USIOMBE KWA KUPIGA YOWE

 1. somo zuri mtumishi tunashukuru,watu wengi kwakujua au kutokujua wameomba kwa sauti kubwa ili watu wajue wao ni waombaji wazuri,wamesahau kuwa Mungu pekee ndio anastahili kusikia maombi yetu.nakuhusu sadaka,wenye vipato vya chini wameshindwa kutoa sadaka kwa kuwa watumishi wengine hutangaza hadharani wanapotoa sadaka. Mungu atusaidie, tusome maandiko kwa usahihi,ili yatuongoze kila wakati.

 2. Amina kwa somo na ufafanuzi mzuri, mm nazan siku hizi zmefka mwisho maana n wachache mno wanaohubri injili ya kweli, wengne n kutaka pesa na umaarufu tu.

  Get Outlook for Android

 3. Emmanuel,
  Shalom.
  Hakika umefanya utafiti wa kina ukagundua UPOTOFU uliomo kwenye madhehebu.
  Umegusa vitega uchumi vya wahubiri wa uongo.Utashambuliwa sana na wenye miradi yao ila usijali kwa sababu ndo gharama ya kuongea UKWELI.
  Kuomba kwa sauti si hoja bali hoja ni maombi yanayoombwa.
  Niliwahi kusema na ninaendelea kusema MADHEHEBU si ya Mungu bali ni Miradi ya wanadamu ya kutafuta Pesa,wanawake na Umaarufu.
  Ibada inatawaliwa na Matoleo ya mali badala watu kujitolea mwili , roho na nafsi kwa Mungu(Warumi 12:1 ) Wanawake wanawa hubiria wanaume na wengine wamefanywa wazee wa Kanisa na mashemasi.Aibu!
  Wanavaa nguo zenye mipasuo, vimini, suruali na nguo zingine zinazoonesha sehemu za miili yao.
  Utakuta madhehebu yanajenga Shule,hospitali, vyuo vya Biblia na vyuo vya fani mbalimbali.
  Mambo haya ni mazuri Lakini Je,ndio mambo Bwana Yesu aliagiza wanafunzi wake?
  Pepo anakemewa na huyo mwenye ‘pepo’ anawekewa Kipaza sauti kwa ajili ya kutafuta umaarufu.
  Hizo dalili ulizotaja ni ishara kuwa huko tayari ni pango la Wezi na Wanyang’anyi,
  Pia Maandiko yanasema ni pango la kila ndege mchafu. Ondokeni kwenye hizo kuta za Babeli.
  Wanafunzi wa Bwana Yesu hawakuwahi kuunda Dhehebu.
  Hii ndiyo njia ya kuwa Mkristo: MATENDO 2:38 ” Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu”.
  MATENDO

 4. UBALIKIWE KWA SOMO ZURI

  Nami naanza kwa kutoa mchango kama ifuatavyo:-

  1.kuhusu maombi wengi wanafikili Biblia inaposema kuomba kwa kupayuka ni kuomba kwa sauti na kudhani kumba kimya kimya ndio Mungu anapendezwa na maombi ya njinsi hiyo
  kuomba kwa sauti ya juu au kuomba kimya kimya hakuna shida kinacho takiwa kuomba ukiwa mtakatifu hilo ndilo la maana mbele za Mungu
  unaweza kuomba kimya kimya huku ukiwa na dhambi mbele za Mungu hayo maombi yanakuwa ni kelele tu soma isaya 1:-15 NANYI MKUNJUAPO MIKONO YENU,NITAFICHA MACHO YANGU NISIWAONE;NAAM,MWOMBAPO MAOMBI MENGI,SITASIKIA;MIKONOYENU IMEJAA DAMU (16) JIOSHENI,JITAKASENI;ONDOENI UOVU WA MATENDO YENU USIWE MBELE ZA MACHO YANGU;ACHENI KUTENDA MABAYA

  Nafikili mmeona neno linavyo sema wengi tumakalia,kulaumu watu wanaomba kwa sauti na kujidanganya kufikili wanao omba kwa sauti wanakosea huko ni kutokujua neno la Mungu wangapi bado wajaamini,wajaokoka,wajampa Yesu Maisha yao ,waasi,wezi,wazinzi nk kama ndugu zetu wa sara tano unafikili komba kwao kimya ndio Mungu anapendezwa nao MBELE ZA MUNGU MAOMBI YA WENYE DHAMBI WOTE WANAPO OMBA YANAKUWA NI KELELE
  2.OMBA KWA SAUTI WATU WANASIKIA HAKUNA SHIDA MAADAMU UWE MTAKATIFU SOMA DANIEL 6:10 HAPO UNA ONA DANIEL HAKUJIFICHA ALIOMBA KWA UWAZI KWA KUWA ALIKUWA MTAKATIFU MUNGU WA MBINGUZI ALIMSIKIA
  3.SOMA NJINSI DANIEL ALIVYO OMBA KWA SAUTI ALIVYO ONYESHA UKUU WA MUNGU WA ISRAEL HADHALANI ALIVYO OMBA KWA SAUTI NA MUNGU AKAJIBU MAOMBI YAKE 1WAFALME 18:21..39

  KUHUSU SADAKA KUTOA HADHALANO

  Kuna aina nyingi za sadaka
  1.zaka
  2.dhabihu
  3 .shukrani
  4 .nadhili
  5 .changizo nk
  katika sadaka hizo sadaka ambayo Mungu amesema unapotoa hata mkono wa kushoto usijue ni sadaka ya dhabiu lakini machangizo hakuna shida ndio maana kama msomaji wa biblia unaona mitume walitoa mashamba,viwanja nk maana yake hizo sadaka zilijulikana kwa mitume

  leo nikomee hapo balikiwa nyote

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s