KUUA MAPEPO

hendriksen_sensing_the_presence_of_the_demons_he_released.png

Kuna maneno ambayo wahubiri au wainjilisti na viongozi wengine wa kiroho wakiwemo Manabii na Mitume ambayo huwa wanayasema na kisha yanaleta mijadala kuhusu UHALALI au USAHIHI wake kutokana na Biblia.

Moja ya maneno hayo ni hili la KUUA MAPEPO! Wapo ambao hufanya hata “maombi’ ya KUUA mapepo. Na wengine hutoa shuhuda jinsi Upako wake una Nguvu ya kuua mapepo, hata kufikia kusimulia kwamba AMESHAUA MAPEPO MENGI kwenye Huduma yake!

Je, Ni kwa kiasi hani jambo hili ni Sahihi au Si sahihi, kutokana na Ufahamu wako Neno la Mungu??

Je, Mapepo huuawa??

 

 

 

Advertisements

14 thoughts on “KUUA MAPEPO

 1. Binafsi sijaona andiko linaloonyesha kuuawa kwa pepo ila kutoa pepo. Mfano Mathayo 10 :8 (Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure toeni Burr. )

 2. mapepo huuliwa na moto wa MUNGU ambao huharibu kabisa na kuyateketeza

  MUNGU pekee ndo anayaamiza wala si muhubiri

 3. Wapendwa, hamjambo wote?
  Labda kabla ya kusema mengi, naomba ndg Herman unieleleweshe kinachomaanishwa na hilo andiko ulilolinukuu kuwa “roho itendayo dhambi itakufa”. Je, kufa huko nikufa kwa namna gani? Swali la kwanza, lakini la pili ni kwamba, Mapepo ni “roho” inayotenda dhambi?
  (Ufahamu ni chembe ya Uhai!)

 4. kwa kweli nataka kusema kwamba kama kuna mtumishi ambae anaweza kuua pepo mimi sijui ikiwa ni katika roho mimi sijui ila najua Mungu ndie anayeweza kuuwa na kuangamiza sisi watumishi tumepewa mamlaka tu ya kuyatoa na kuyakemea angalia katika nchi ya wagerasi kulikuwa na mtu aliyekuwa na mapepo lakini yeshu aliyaamuru ya waingie nguruwe wakazama baharini narudia tena kwamba shala la kuuwa pepo nasema hakuna mtumishi anayeza kuuwa mapepo

 5. Kwakuongezea naweza kusema kuwa hakuna nafsi bila roho, roho ndiyo inabeba nafsi.

 6. Kwanza, siamini kama kuna mtumishi mwenye akili timamu anaweza kusema kuwa ana uwezo wa kuua mapepo.

  Pili wanaojaribu kutumia andiko la tafsiri ya Kiswahili kuwa roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa’ nao hata hawajui wanachokisema zaidi ya kusema tu bila kudadisi ukweli wa hilo andiko.

  ” Ezekiel 18:20 The soul that sinneth, it shall die.[KJV]
  ”eZEKIEL 18:20 The one who sins is the one who will die.[NIV]

  Kwa hiyo kama una akili ya kusoma maandiko kwa usahihi utagundua kuwa kinachosemwa ni nafsi siyo roho-itendayo dhambi!

  Kwa hiyo ukiuwa pepo linaenda wapi baada ya kufa?

  Kama kuna mtu husema hivyo, basi husema kwa ujinga wake mwenyewe,japo siamini kama kuna mtumishi mwenye akili timamu anaweza kusema hivyo.

 7. JINA LA BWANA LIPEWE SIFA, samahani niwaombe mnifowadie ujumbe uhusuo kuomba kimya uliotumwa kwa wadau siku chache zilizopita kwani naamini utanisaidia saana, be blesed by SG member.

 8. Hakuna uhalisia wowote!! Na ni vigumu saana kuua mapepo. Na kwa namna moja au nyingine naweza kusema ni uongo. Kwamaana kama mapepo yangekuwa Yana uawa basi Mungu ndio angekuwa wa Kwanza kuua mapepo, kwamaana kipind shetani anakosea ukisona ufunuo 12:11-12 utaona jinsi Mungu alivyoamuru mikaeli wapambane nae nao wakamshinda. Unaona hapo!! Kwahiyo kama mapepo yanauliwa basi Mungu angeyaua. Na kama ndio hivyo kulingana na Hao manabii na mitume, mbona wanayaua na bado yanaendelea kuwatesa watu??? Kikubwa hapa naona watu wasome neno la Mungu na kulielewa wasiendeshwe na watu kwamaana kila kitu kiko well explained in the Bible.

 9. Bwana yesu apewe sifa

  leo watumishi wengi wanaongeza zaidi ya maagizo tuliyo pewa

  ukisoma katika injili ya marko biblia inasema 16:17 na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio;kwa jina la Yesu watatoa pepo; sio wataua kazi yetu ni kukemea au kuamuru kuyatoa kwa jina la yesu sio kuua kwani mapepo na malaika walio asi mwenye kuyaangamiza ni Mungu pekee

  Balikiwa nyote

 10. kabla ya kujibu swali,pata kujua mapepo ni nini? hukaa wapi na kula nini, kisha tambua asili yake na kazi zake, sasa hakuna kisichokuda duniani na biblia(MUNGU) inasema “roho itendayo dhambi itakufa. unaebisha tena mwinjilisti una injili yako pekee?

 11. Ukweli ni kuwa mapepo ni roho,nayo ukimbia tu kutoka sehemu moja na kuingia sehemu nyingi,anayeweza kuua pepo ni Mungu peke yake,sisi kama watumishi tumepewa uwezo wa kutoa pepo kwa jina la anayetoa hao pepo yaani Yesu.
  Mengine uwa ni mbwembwe za kitumishi tu kama wanadamu tu,na wakati mwingine ni kutojua vizuri sana siri za mafumbo mengi ya Mungu,hivyo watu kufanya mambo haya kwa kudhania akili zao zina matunda juu ya mambo haya

 12. Mapepo ni roho na kila roho inaweza kufa. Ezekiel 18:20″ roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa” Ieleweke kwamba sisi tunayo mamlaka ya kukanyaga ng’e na nyoka na nguvu zote za yule adui wala hatudhuriki.
  Kuna uwezekano kabisa wa pepo kufa.

 13. No.. Haiwezekani kuua mapepo kwa sababu mapepo ni roho. Na roho huwa haifi. Hayo ni maneno tu ya mtu àjikwezaye.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s