KIBURI CHA UZIMA

way-of-the-world-pride-of-life-450x450.png

Ukitaka kujua sisi binadamu ni waajabu kuliko maajabu yote duniani…kuna watu tumelewa na KIBURI CHA UZIMA.

Wakati unasaka kazi huku na kule, ulikuwa mtiifu na mnyenyekevu mbele za Bwana, huku ukimwomba na kuhudhuria kila ibada za kanisani na maombi.

Kipindi unamwomba Mungu akupe mke/mume, ulikuwa mtiifu sana mbele za Mungu. Kwa kujitoa kwake kwa kila kazi itakayojitokeza kanisani ama kwenye vikundi vya vijana/wamama.

Ukiwa unasaka mtoto huku na kule, umetembea hospitali nyingi ukitafuta suluhisho, lakini ilishindikana mpaka ukapata ushauri wa kumwomba Mungu. Kufanya hivyo ukapata mtoto kweli.

Ulipokuwa maisha yamekuvuruga, ulikuwa mwema na mwaminifu mbele za Mungu. Na uliheshimu kweli watumishi wa Mungu, na kuwaomba wakuombee kwa Mungu maana ulishaomba sana na ukaona mambo bado hayaendi. Baada ya kukusaidia kubeba mzigo huo wa kukuombea ulifanikiwa.

Ulipokuwa unanyanyaswa na maisha ya ndoa, ulikuwa mnyenyekevu na mcha Mungu mzuri sana. Na uliheshimu sana kumpa Mungu muda wako, na ilipofika siku, Mungu akasikia kilio chako.

Ulipokuwa na cheo cha chini kazini kwako, na kuishia kutukanwa ovyo na wafanyakazi wenzako. Ulikuwa mpole na mwenye huzuni nyingi, huku ukimwona Mungu amekusahau…ila uliponyenyekea mbele zake uliona mafanikio makubwa ya kuwa kiongozi kwa wale waliokuonea na kukucheka.

Ulipokuwa shule, ulikosa tumaini kweli la kuendelea na masomo yako, na kuona ndoto zako ndio zimezimika kama watoto wengine walioishia darasa la Nne C kwa kukosa pesa ya kununulia hata pencil.

Lakini wewe Mungu alikuinulia mtu wa kukusaidia kutimiza ndoto zako.

Ulipokuwa kwenye nyumba za kupanga, na kutolewa vyombo kila siku. Kwa kukosa kodi ya nyumba, ulikuwa mnyenyekevu na mtu mwenye kutia huruma sana sana. Lakini Mungu alikupa maarifa ya namna ya kuondokana na hiyo hali, na sasa upo ndani ya nyumba yako.

Cha kushangaza na kusikitisha, leo hii umeachana na mambo ya Mungu. Na kuona ni ushamba na kupoteza muda kusali sali, na kuomba omba.

Umefika kipindi umeanza kuwakejeli wengine kuwa wanaomba omba, kwa sababu wana shida sana.

Binafsi hukumbuki mara ya mwisho ulimpa lini Mungu muda wako wa kukaa naye katika maombi na kusoma na kusikiliza neno lake. Umebaki na maombi ya kwenye Radio na Tv.

Nyakati zile ulikuwa unafunga tatu kavu, ila sasa hivi hata maombi ya masaa 12 yanakushinda. Ukiulizwa unasema huna muda, na huwezi kujitesa bure na njaa.

Baada ya mafanikio, familia yako huikumbuki tena..wala mke/mume wako huna habari naye. Mwanaume hujui mke wako anakula nini na watoto wenu, kazi yako imebaki kuruka viwanja vya starehe.

Neno la Mungu, linatusihi sasa usimsahau Mungu wako wakati wa mafanikio yako. Usiinue mabenga na kusema ulifanikiwa kwa akili zako, na nguvu zako.

Geuka umrudie Mungu wako, kabla nyakati mbaya hazijaja.

Omba msamaha kwa familia yako, na Mungu wako. Acha mafanikio yako yamtukuze Mungu, kwa kuwabariki wengine.

Mungu atusaidie kuelewa haya.

Ndg. Samson Ernest

Advertisements

5 thoughts on “KIBURI CHA UZIMA

  1. Tunashukuru mtumishi kwa maneno haya,ni kweli watu wakifanikiwa hujisahau kabisa.Tuombe Roho Mtakatifu atukumbushe kumtegemea Mungu kwa kila hali.

  2. Aisee,mtumishi umenena kweli,kama hii Gospel ingekuwa inashuka hivi hata unapokuwa madhabahuni kwa Bwana,hakika moto ungewaka kama wa Eliya.
    Yote uliyosema ni kweli kabisa mtumishi wa Mungu,kiburi cha uzima kimemaliza wengi hadi watumishi kamili wa Mungu,hapo napo unaweza kusema nini,maana naona kiu au njaa ya haki au ya kutenda mema imepungua hata kupotea kabisa.
    Ebu funua siri hiyo pia,tupate kuona na kujua hali ilivyo kwenye nyakati hizi za mwisho

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s