USIKIMBIE

mpweke

*Naye Abramu akamwambia Sarai, Tazama, mjakazi wako yu mkononi mwako, mtendee lililo jema machoni pako. Sarai akamtesa, naye akakimbia kutoka mbele yake. Malaika wa BWANA akamwona kwenye chemchemi ya maji katika jangwa, chemchemi iliyoko katika njia ya kuendea Shuri. Akamwambia, Hajiri, wewe mjakazi wa Sarai, unatoka wapi, nawe unakwenda wapi? Akanena, Nakimbia mimi kutoka mbele ya bibi yangu Sarai. Malaika wa BWANA akamwambia, Rudi kwa bibi yako, ukanyenyekee chini ya mikono yake. (MWA. 16:6‭-‬9 SUV)*

Kuna wengine wetu ambao tukiteswa tu kidogo tunaamua kukimbia.

Tukiteswa kazini tunaacha kazi.

Tukipata mapito kanisani tunakimbia kanisa.

Tukipata tu mapito kidogo kwenye urafiki, ushirika, mahusiano tunakimbia.

Hatupendi shida lakini tunasahau shida na mateso huwa mara nyingi vinatumika na Mungu kushape tabia zetu.

Moto ulipowaka kazini kwake, Hajiri aliamua kukimbia lakini malaika wa Mungu akakutana naye akamwambia rudi ukanyenyekee chini ya bibi yako Sarai.

Mara nyingi sana kinachotufanyaga tukimbie ni kiburi.

Mungu kuna wakati ataruhusu mateso ili kushughulika na kiburi, ujeuri na ukaidi wetu.

Daudi anasema, “Kabla sijateswa nalipotea, lakini sasa nimelitii neno Lako.”

Kuna wakati mateso yanakuja kukusaidia kuona ni eneo gani umepotea na kinachotakiwa sio kukimbia bali ni kutii neno la Mungu.

Mara nyingi tunachodai kuwa ni kuumizwa kwa kweli ni kiburi chetu tu ndo kimeumizwa na mimi nasema kisiumizwe tu, kiuawe kabisa.

Daudi anaendelea kusema, “Ilikuwa vema kwangu kuwa naliteswa, nipate kujifunza amri zako.”

Katikati ya mateso yako jifunze amri za Mungu, sio unakimbia.

Isaya akasema, “Nimekuchagua katika tanuru ya mateso.”

Acha kukimbia tanuru ya mateso, tulia maana Bwana atakuchagulia humo.

Sulemani anasema kwenye mhubiri, Roho ya mtawala ikiinuka kinyume chako usiondoke mara mahali pako ulipo kwa maana roho ya upole hutuliza machukizo mengi.

Ukiinukiwa acha kukimbia.

Tuliaaaaaaaaaaa.

Kuwa mpole laa sivyo kuondoka kwako nje ya wakati na utaratibu wa Mungu utainua machukizo mengi sana.

Isaya anasema Maana hamtatoka kwa haraka, wala hamtakwenda kwa kukimbia.

Acha kufanya haraka kusepa.

Acha kukimbia.

Mwangalie Yusufu mateso aliyoyapata Misri.

Je angekimbia angekuwa Waziri Mkuu?

Wakati wa kuinuliwa kwake ungefika lakini angekuwa hayupo ili kuinuliwa.

Isaka alitaka kukimbia nchi ya ahadi kwa sababu ya ukame.

Alitaka kushuka kwenda Misri.

Mungu akamwambia usishuke kwenda Misri.

Kaa katika nchi niliyokuonyesha nami nitakubariki.

Wengi hatujui kuwa tunapokimbia mahali ambapo Mungu ametuweka tunazikimbia baraka za Mungu maana ameahidi kukubariki katika nchi aliyokupa sio uliyojipa.

Natumaini nimezungumza na mtu mahali hapa.

Nyenyekea.

Acha kukimbia.

Mchungaji Imori

Advertisements

4 thoughts on “USIKIMBIE

  1. Amina!!..Nimebarikiwa Na Nita Share Na Wengine ili Wabarikiwe pia…
    ASANTE,NA UBARIKIWE PIA..

  2. bwana asiwe mchunga neno lako limenipa faraja sana mwaka jana nilifiwa na mume wangu nimekuwa na mjaribu sana wakati mwingine naona mungu ameniacha nilipo soma neno hili limekuwa faraja kubwa sana kwangu

  3. Nashukuru mtumishi kwa NENO Hili,hakika limekuwa msaada sana kwangu asubuhi ya leo,nimeumizwa kazini,nikapata hasira,lakini Mungu mwema kwa neno hili nimepona,naendelea na kazi.Bwana Yesu Apewe Sifa!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s