WAKRISTO WA JUMAPILI

mfungwa

Wakristo Wa jumapili: Hawa ni wale wanaomkumbuka Mungu siku ya Jumapili na kwenye nyumba ya ibada tu. Akitoka kanisani anamuacha Mungu anamuacha mlangoni. Anakuwa mpagani Wa kawaida mpaka Jumapili nyingine.

Hapa katikati ya wiki michanganyo kama kawaida; akifanya mambo yasiyompendeza Mungu na kutarajia kuungama ibadani Jumapili.

Ushauri:: Mpokee Kristo na umruhusu afanye makazi ndani yako,awe Bwana na mokozi wako,hapo Mungu atafanyika kuwa Wa kila siku maana atakuwa anaishi ndani yako,hautamuacha Tena pale kwenye geti la jengo la Kanisa.

Acha kuwa mkristo wa Jumapili,Bwana anakuita uende kwake. Mkabidhi maisha yako leo. Na Mungu akubariki!

Samson Chitalika

Advertisements

10 thoughts on “WAKRISTO WA JUMAPILI

 1. Jamani nafikiri watu tumeelewa mada ,ukristo wa jumapili tu, alikuwa anamaanisha , watu siku zote za katikati ya week huwa mara nying tunaishi maisha yasiyo mpendeza Mungu, mpaka siku ya Jumapili ,na ndipo tunafikiria kuwa tutaenda kutubu, lakini tunatakiwa kuishi maisha ya kumpendez Mungu siku zote za maisha yetu, na hao watu wapo, wengi hawapendi hata kuitwa wakristo siku za katikati ya jUma, kwa uelewa wangu mtu anae itwa mkristo anamipaka, hawezi kwenda kila mahali, hawezi,kula kila kitu, lazima awe na mipaka,
  sasa baadhi ya wakristo hiyo mipaka hawaitaki,
  wanataka wawe na uhuru wa kupindukia,
  asnteni sana,

 2. Jako SFLM,

  Unajaribu kuleta topic nyingine kinyamela.
  Hatuongelei kutunza siku hapa. Na wala huwa hatutunzi siku ya Ijumaa, Jumamos, Jumatatu wala Jumapili, ibada ni siku zote, masaa yote, dakika na sekunde zote popote ulipo, hata kama uko bafuni. Hizi ndo siku alizosema Yesu kuwa waabuduo halisi watamwabudu Baba ktk roho na kweli, si ktk sehemu fulani.

  Wewe kama hukusanyika Jumamosi, topic ingeweza kusema ‘mkristo wa Jumamosi’, ikimaanisha mtu anayejaribu kuigiza ukristo Jumamosi anapokuwa amekuja kwenye kusanyiko.

  Sasas kama wewe unataka tuongee juu ya sabato nenda kwenye topic ya sabato maana ipo hapa SG, au lete hilo suala kama topic.

 3. Huyu mtu anayemwacha Mungu mlangoni,alimpata lini huyo Mungu?

  Yaani Mungu wetu Yehova ni wa kubebwa na kisha kuachwa mlangoni,halafu tena anakuja anapitiwa wiki inayofuatia na huyo mwenda kanisani.

  Wapendwa tuna picha gani ya huyu Mungu jamani, ivi tunamjua kweli vizuri?

 4. amee

  ” Wakristo Wa jumapili: Hawa ni wale wanaomkumbuka; Mungu siku ya Jumapili na kwenye nyumba ya ibada tu. Akitoka kanisani anamuacha Mungu anamuacha mlangoni. Anakuwa mpagani Wa kawaida mpaka, Jumapili nyingine. Hapa katikati ya wiki michanganyo kama kawaida…”

 5. Hawezi mtu akawa mkristo halafu hapohapo bado anatakiwa kumpokea Yesu kristo. Maana kama hajampokea Yesu aliwezaje kuwa mkristo mpaka aitwe mkristo wa Jumapili?

  Maana ya neno ‘mkristo’ ni kuwa wa -kristo, yaani kumilikiwa na kristo. Na huwezi kuwa mali yake kwa njia nyingine ile ispokuwa ya kumpokea.

  Ndo hivyo!

 6. Nafikiri hakuna wakristo wa jumapili tu mungu hayuko jumapili tu mungu yupo kila siku na kila mtu anajinsi yake ya kumuabudu maana mara nyingi tunafikiri wale watu ambao tunawaona kila siku ndiyo tunawaona si wa jumapili kumbe ndani yao bora hata wale wa jumapili

 7. Nani alisema kuwa juma pili tuu ndio watu wanamuomba Mungu alafu wanamuacha Mungu?? Na pia hakuna wa krsto wa juma pili, kwamaana hakuna sehemu hata moja kwenye biblia pameandikwa wa krsto wa juma pili au juma Mos. Kristo mwenyew hakufundisha kwamba kwamba wanaomwamin waabudu juma pili au juma Mos Bali alisema kila siku “kesheni mkiomba..” siyo juma pili au juma mos.

  Na pia kwa yeyote aliyemuamin Bwana Yesu hajafungwa kumuabudu Mungu juma pili au juma mos. Ila ni tabia yake kuabudu na kumuomba Mungu kila siku. Tatizo dini zimeijaa mioyoni mwetu kuliko Kristo mwenyew.

  Hizi siku zilikuwepo tangu uumbaji. Suala hapa ni kila mtu ajue nafas yake kama muamin Kristo Ila siyo juma pili au juma mos au siku yeyote ktk wiki. Mungu atubariki Sana.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s