Kumpigia Magoti Mtumishi wa Mungu

kneeling.jpg

Bwana Yesu asifiwe mpendwa!

Kumekuwa na tabia ya watu wanapokwenda kuonana au kuwa karibu na Mtumishi wa Mungu, ANAPIGA MAGOTI. Anaweza akapiga magoti ndiyo akaongea naye au kuonyesha uhitaji wa dharula wa kuhudumiwa, na pengine sababu nyingine aliyonayo yeye mwenyewe.

Jambo hili limekuwa likitafsiriwa kama ni jambo BAYA na wengine wanatafsiri kwamba SIYO JAMBO BAYA, kiroho!

Wewe una maoni gani?

Advertisements

6 thoughts on “Kumpigia Magoti Mtumishi wa Mungu

 1. Kuna mababa wa aina tatu, wa kimwili (waliokuzaa), waliokuzidi umri na wa kiroho. Wa kwanza Wawili hawana shida katika maoni haya yaani wa mwili na waliokuzidi umri. Viongozi wa kidini ni mababa wa kiroho. Ikiwa kama mababa wa kimwili tunawapa heshima iwe kwa kuwapigia magoti au kuinamisha vichwa vyetu tunapowasalimia je ni kwasababu tunawaabudu?, La! hasha. Je si zaidi sana mababa wa kiroho? hata hivyo heshima iko ndani ya moyo wa mtu. Mtu yeyote anayeshangaa watumishi wa Mungu kupigiwa magoti ana kasoro na moyo wake yaani hata Mungu hawezi kumpa heshima. Kwa nini? hutakuja kukutana na Mungu hapa duniani ila mtumishi wake. (hakuna mtu aliyewahi kumwuona Mungu wakati wowote1 Yohana 4:12), ukitaka kukutana na Mungu mtafute mtumishi wake. Lakini je Mungu anakaa wapi? utaniambia mbinguni kama ni hivyo tusingeyaona matendo makuu ambayo Mungu anafanya duniani kupitia watumishi wake eg. uponyanyaji, upatanishi, adhabu wanazopata wakosaji! kwa vipi? ni kwa sababui Mungu anakaa kwa mtu ndiyo maana akajiita”Mimi ni Mungu wa Ibrahim (anakaa kwa Ibrahuim), Mungu wa Isaka (anakaa kwa Isaka), Mungu wa Yakobo (anakaa kwa Yakobo) Mungu wa mama Rwakatare ( anakaa kwa mama Rwakatare), Mungu wa Josephat Mwingira (anakaa kwa J. mwingira) Mungu wa Fernandes (anamakaa kwa mt Fernandes). Kwa kila mtumishi iko namna anavyojifunua kivyake kutegemeana na kusudi alilopewa huyo mtumishi na Mungu. Kama Mungu anakaa kwa mtumishi maana yake ;
  (i) Ukimpigia magoti mtumishi ujue unampigia magoti Mungu
  (ii) Ukimdharau mtumishi wa Mungu ujue unamdharau Mungu
  (iii) Ukimnenea mabaya mtumishi wa Mungu ujue unamnenea mabaya Mungu na hivyo waweza kuleta hasira ya Mungu juu yako na uzao wako. Kumbuka Haruni mna Miriam walivyomnenea mabaya Musa Mungu alichowafanya. Soma hesabu 12: 1-15 Mungu mwenyewe anasema katika maandiko “msiwaguse masihi wangu”. Ndugu wengine wanasema “Kiongozi wa dini hana sehem ya Baraka ya mtu isipokuwa Mungu peke yake” Tusidanganyane baraka zako anazo mtumishi wa Mungu na sio Mungu soma 2Nyakati 20:20, Mwaminini Mungu ili awathibitishe tu, lakini mkitaka mafanikio (incl. baraka) waaminini manabii (watumishi wa Mungu). kama humwamini mtumishi wa Mungu sahau kubarikiwa labda ukachukue baraka zako kwa kumwamini mganga wa kienyeji (shetani). Viongozi wadini wachukue nafasi waliyopewa na Mungu na wamwakilishe Mungu duniani ipasavyo na wasikatishwe tamaa na waumini ambao wanawanena vibaya kwa sababu ya kutojua neno la mungu (sio maandiko kwa sababu andiko laweza kukuhuisha au kukuua soma Yohana 5:38 -39).

  Huyu anasema “kupiga magoti kwa mtumishi ni kwa lengo la kumwabudu,kumuinua kama Mungu wake yule mtu inakuwa ni ishara ya kumtumainia na kumtegemea yeye badala ya Mungu,hapo ni makosa makubwa sana,tena hata kwa mtumishi kuchukua utukufu wa Mungu kutoka kwa wanadamu ni dhambi mbaya sana iliyo mshusha kuzimu Ibilisi kwa kiburi cha utukufu na sifa”.

  Hilo hawezi kulithibitisha, wa kuthibitisha ni yule anayepiga magoti kwamba moyoni mwake anamwabudu mtumishi, hiyo siyo kweli nayo ni dhambi kushuhudia kitu ambacho huna uhakika nacho, hayo ni mawazo yake tu.

  Huyu anasema “Njoni, tuabudu,tusujudu,Tupige magoti mbele za BWANA aliyetuumba” Zaburi 95:6″ “Kwa hiyo nampigia Baba magoti, ambaye kwa jina la ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa,” Waefeso 3:14

  Mbona unapiga magoti mbele za padre, mchungaji au mtumishi ndiye Mungu? Hapana! Kwa hakika ni kwa sababu Mungu anakaa kwa mtumishi wake. Ushauri wangu kwa watu wa Mungu ni hivi, kwa hayo unayosema na uijihadhari usije ukawa unapigana na Mungu bila kujua ukapata hukumu iliyo kubwa. Soma Matendo ya Mitume 5:39 Na kwa watumishi wa Mungu;
  (i) Fanyeni kazi ya utume wenu kama Mungu alivyowatuma bila kuogopa maneno ya watu wasiomjua Mungu, wakidhani wanampigania Mungu kumbe wanapigana naye
  (ii) Dhambi ni ya kukemewa sana ili watu wapone
  (iii) Waombeeni wanaowaudhi ndipo Mungu atakapowainua zaidi na zaidi.
  (iv) Isikilizeni sana sauti ya Mungu maana Mungu anashughulika sana na watumishi wake na sio waumini kwa sababu waumini wanatakiwa wawasikilize na kuwatii watumishi wa Mungu.
  Naomba niishie hapo na mwenye masikio na asikie maneno hayo ili mwenye kupona na apone.
  Mbarikiwe nyote.

 2. Tumpigie mungu magoti wapendwa, ndiye mmiliki wa uhai wetu

  “Njoni, tuabudu,tusujudu,Tupige magoti mbele za BWANA aliyetuumba” Zaburi 95:6

  “Kwa hiyo nampigia Baba magoti, ambaye kwaa jina la ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa,” Waefeso 3:14

 3. Kikawaida Hata Kibiblia Kupiga Magoti Ni Ishara Ya Utii Mbele Za Mungu Au Kumwabudu Mungu Ivo “Na Alaaniwe Mtu Yule Amwabuduye Kitu Tofauti Na Mungu Wa Mbinguni” Basi Ikiwa Ni Mtumishi Wa Mungu Ingependeza Mtu Aongee Naye Kiheshima Hata Bila Kupigiwa Magoti Ili Mradi Itifaki Ya Maongezi Ya Kikristo Izingatiwe. Amen

 4. Sioni ulazima wakupiga magoti kwa ajili ya kupewa huduma, na ikiwa ni kazi yake.

  2016-07-16 1:07 GMT+03:00 Strictly Gospel :

  > Strictly Gospel posted: ” Bwana Yesu asifiwe mpendwa! Kumekuwa na tabia ya > watu wanapokwenda kuonana au kuwa karibu na Mtumishi wa Mungu, ANAPIGA > MAGOTI. Anaweza akapiga magoti ndiyo akaongea naye au kuonyesha uhitaji wa > dharula wa kuhudumiwa, na pengine sababu nyingine aliyona” >

 5. kuna ubaya au uzuri wa kupiga magoti kwa mtumishi,uzuri uko hivi,kama ni kwa lengo la kuonyesha heshima au nidhamu au adabu kama ambavyo makabila mengine yamefanya hivyo kuonyesha heshima ni vizuri sana.
  Kwa upande wa pili kama kule kupiga magoti kwa mtumishi ni kwa lengo la kumwabudu,kumuinua kama Mungu wake yule mtu inakuwa ni ishara ya kumtumainia na kumtegemea yeye badala ya Mungu,hapo ni makosa makubwa sana,tena hata kwa mtumishi kuchukua utukufu wa Mungu kutoka kwa wanadamu ni dhambi mbaya sana iliyo mshuka kuzimu Ibilisi kwa kiburi cha utukufu na sifa

 6. YESU asifiwe Sana? Ndugu yangu, tunae Mungu mmoja tuu anaishi MBINGUNI. Na kristo yesu peke yake. Sasa huyo anaeenda kumpigia magot kiongoz wa dini eti kwa kuwa anayo shida ndio ajieleze anakosea Sana. Kupiga magot ni sehem ya ibada. Sasa huyo mtu au huyo kiongoz wa dini ni Mungu?

  Kiongoz wa dini hanasehem ya Baraka ya mtu Isipokuwa Mungu peke yake. Huyo mtu waaina hiyo namshauri aache kabisa Mara moja hiyo tabia, hiyo ndio ibada ya Sanam. Viongoz wadini wasichukie nafas ya Mungu. Mungu akubariki Sana.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s