Kuonyeshwa Mbinguni

heaven.jpg

Hebu Tujadili jambo hili.

Yawezekana umeshasikia ushuhuda wa mtu ambaye alisimulia jinsi ALIVYOPELEKWA MBINGUNI kisha akarudi tena hapa Duniani. Au pengine ni mmoja wao wa watu waliopata ujuzi wa namna hiyo.

Jambo linalosababisha mjadala huu ni kwamba katika Shuhuda hizi kila anayesimulia husimulia mambo tofauti na mwingine! Yaani mmoja akisimulia jinsi alivyoingia na Mambo aliyoyaona huko Mbinguni huwa TOFAUTI na asimuliavyo mwingine.

Mfano:  Mmoja anaweza kusema aliowaona kule Sura zao zinafanana, mwingine akasema sura hazifanani. Mmoja anaweza kusema walifika mahali wakala vitu fulani, Mwingine akasema kule hakuna wala kunywa; na mambo mengine mfano wa hayo!!

Mambo ya kujadili ni pamoja na yafuatayo:

Je, Suala hili la watu kuchukuliwa katika Roho kisha akapelekwa Mbinguni lipo kweli? Na usahihi wake ni upi? Twaweza kulipata katika Biblia?

Kama kweli Mbingu ni moja ni kwa nini kila anayeshuhudia kwamba alifikishwa Mbinguni masimulizi yake hutofautiana na mwingine, ambaye naye husimulia habari za huko huko Mbinguni?

Je, Inawezekana mtu kwenda akaonana na Mungu kisha akarudi tena hapa Duniani kuishi?

Kuna watu wamekuwa wakizinduka akielezea ushuhuda wake anasema Amepewa ujumbe aje awaambie watu, mfano, juu ya kutubu na kuacha dhambi au ujumbe mwingine. Je, Hii haipingani na maneno ambayo aliambiwa Tajiri kwamba Watu yawapasa kusikiliza maneno ya watumishi wa Mungu walioko Duniani, maana hata akitumwa mtu kutoka kwa wafu haiwezi kusaidia kitu? (Kisa cha Tajiri na Lazaro masikini)

Karibu katika mjadala kuhusiana na hayo, pamoja na mengine yatakayojitokeza!

 

Advertisements

10 thoughts on “Kuonyeshwa Mbinguni

 1. BIBLIA HUSEMAJE JUU YA ROHO KATIKA KUFA?

  “Kila kitu chenye pumzi ya roho ya uhai puani mwake kikafa,” Mwanzo 7:22

  “Kwa maana linalowatukia wanadamamu linawatukia wanyama; jambo moja lawatukia; anavyokufa huyu ndivyo anavyokufa huyu; naam, wote wanayo pumzi moja wala mwanadamu hana kitu cha kumpita mnyama; kwa maana yote ni ubatili. Wote huenda mahali pamoja; wote hutoka katika mavumbi; na hata mavumbini hurudi tena.” Mhubiri 3:19-20

  “Ni nani ajuaye kama roho ya binadamu huenda juu, na kama roho ya mnyama huenda chini?” Mhubiri 3:21

 2. Ndugu @Iqualiptus Malle, Nilichokimaanisha si kwamba roho za watu waliokufa zinakaa kabrini, la, nilichokimaanisha ni kuwa mtu anapokufa roho yake inamrudia Mungu. Roho inamaanisha “pumzi” au “upepo” ambao ndio uhai wa mtu alioupuliza Mungu ndani yake.

  Muhubiri 12:7 inasema, “Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa.”

  Neno la kiebrania lililotumika hapo kwenye neno “roho” ni “ruach”(“ר֫וּחַ” [roo’-akh]) linalomaanisha “pumzi” au “upepo”. Hivyo Muhubiri 12:7 inasema mtu akifa mwili wake unarudi mavumbini, lakini pumuzi ya uhai inamrudia Mungu aliyeiweka ndani yake tangu mwanzo. Ayubu 27:3 inathibitisha kwa kusema, “(Kwa kuwa uhai wangu ukali mzima ndani yangu, Na roho ya Mungu i katika pua yangu;)” Hapa anaonyesha uhai na roho kuwa kitu kimoja katika pua ya mtu. Kuthibitisha ukweli huu zaidi katika Mwanzo 7:22 inasema, “kila kitu chenye pumzi ya roho ya uhai puani mwake kikafa, kila kilichokuwako katika nchi kavu.”

  Roho ya mtu kumrudia Mungu haimaanishi kwamba roho hiyo inaenda kuishi na kuwa hai mbinguni.

  Ufunuo 20:4 inasema, “Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu…nao wakawa hai,wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu.”

  Je umeona hapo? Hapa Yohana akionyeshwa tukio la mwisho kabisa wakati wa hukumu, aliona roho za waliochinjwa lakini hawakuwa hai, ila ndio wakapewa uhai kisha wakatawala na Kristo miaka 1000 mbinguni.

  Kwa ushahidi zaidi kuhusu roho angalia…

  *. Je roho zinazomlilia Mungu katika Ufunuo 6:9 hazithibitishi kuwa mtu anapokufa tu, moja kwa moja huenda mbinguni?

  KUHUSU SWALA LA Luka 23:43.

  Siku ya Ijumaa Yesu alimwambia yule mwivi kwamba “leo hivi utakuwa nami peponi”, lakini siku tatu baadaye Yesu Mwenyewe katika Yohana 20:17 akasema, “hajaenda mbinguni kwa Baba”. Sasa Je kama walienda ijumaa hiyo peponi, kwanini Ijumapili Yesu akasema kwamba hajaenda kwa Baba?

  Mfano wetu wa kuigwa ni Yesu, alikufa ijumaa, akafufuka jumapili na akasema hajaenda mbinguni. Je Yeye roho yake ilikuwa wapi, kama mtu akifa roho inaenda kuishi mbinguni?

  Na kama ni kweli kwamba watu wanapokufa roho zao zinaenda kuishi na kuwa hai mbinguni, au jehanum. Je siku ya ufufuo Mungu atawafufua kutoka mbinguni na jehanum, au kutoka kabrini?

  Ndugu zangu: Ukweli ni Ukweli, mtu akifa roho(pumzi) yake inamrudia Mungu, harafu mwili wake unayarudia mavumbi aridhini. Lakini haimaanishi kwamba roho yake inaenda kushi au kuwa hai mbinguni au jehanam. Ayubu anahitimisha mjadala huu kwa kusema,

  Ayubu 14:12 inasema, “Ni vivyo mwanadamu hulala chini, asiinuke; Hata wakati wa mbingu kutokuwawako tena, hawataamka, Wala kuamshwa usingizini.”

  “Hata wakati wa mbingu kutokuwako tena”; yaan, siku ya mwisho ndipo watakapofufuliwa. Lakini kabla ya hapo “hawataamka, wala kuamshwa usingizini; yaan, kifoni”

  *. Je tunapokufa tunaenda wapi?

  BWANA ATUBARIKI SOTE. AMINA.

 3. Shalom Aleichem!
  Ni kweli kwamba Mungu huweza kuwaonyesha watoto wake yale yaliyofichika katika ulimwengu wa roho na ule wa damu na nyama. Si yote yasemwayo kuwa yemeonwa au kufunuliwa kwa watu huwa yametoka kwa Yehova na si yote huwa si maono kutoka kwake Muumba. Ingekuwa zama hizi ni zile ambazo Yohana anapata ufunuo (kama ilivyo katika kitabu cha Ufunuo), ni wachache sana kati ya binadamu wanaoishi leo wangekubali kwamba ni Mungu amenena naye. Tunaihitaji neema ya Mungu kupitia Roho mtakatifu ili kuyang’amua yake Mungu walau kwa sehemu.

  Ndugu JackofSLM, Link ulizoweka hapo zinamambo ya kujifunza lakini si yote ni sahihi. Kuna upotoshaji wa Neno, Kusema kwamba mifano ya Yesu haikuwa inamaanisha kile alichotolea mifano, watu wanapokufa roho zao hukaa makaburini palepale, “…leo hii utakuwa nami peponi” eti maana yake “siku ya mwisho itakapofika”>>Kulithibitisha hilo ukasema Yesu alipofufuka alikataa kuguswa kwakuwa alikuwa hajakwenda mbinguni (peponi). Je unakumbuka kuwa Yesu alikaa siku ngapi kabla hajapaa? Aliguswa na watu?….Samahani mpendwa ila ninapenda kujifunza ila hizo link zina Neno lililoghoshiwa.

 4. Kama mwana ni Mungu pia huyo huwezi kumwona. Maana Mungu alijifunua kwetu kwa mfano wa wanadamu. Na hakuwa mwingine bali ni yuleyule katika utatu wake @ edjost.

  Ndiposa twajua Mungu ni Mmoja tusilazimishe fahamu zetu tukaziweka kama vile mbinguni kuna YESU MUNGU NA ROHO . kiufaham wangu hakuna Mungu watatu. Yupo mmoja tu.

 5. ni vema kuangalia maneno ya Mungu yenye kweli yote na si shuhuda za watu. ni vigumu kufikiri kuwa yanayosimuliwa kama ni kweli yaweza kuwa tabu. Nashauri kuangalia anayosema Mungu katika maandiko matakatifu kuliko shuhuda za kwenda mbinguni na kurudi.

 6. Biblia inasema,
  “Na Roho za manabii huwatii manabii.” 1 Wakorintho 14 :32

  kama nabii mmoja akasema maneno yanayompinga mwingine,mmoja lazima ana tatizo, Yesu angempinga Musa tungehoji kulikoni Musa.

  Roho ipi ni ya kweli? ipimwe kwa maandiko walimo manabii ambao Roho wao ni mmoja.

  Hivyo hatusikilizi maneno ya watumishi ila maneno ya Mungu waliyopewa wakristo wote kupeleka ulimwenguni, ambayo kamwe hayatakiwi yaseme tofauti na biblia ambayo ndani yake kuna manabii walioandika kwa karne tofauti bila kupingana.

  “Na Roho za manabii huwatii manabii.” 1 Wakorintho 14 :32

 7. Mungu wetu sio kwamba halishaacha kufanya kazi,kwamba yuko kimya tu,bali anafanya kazi zake hata sasa,ndio maana anasema mawazo yangu sio yenu.
  Tena ukisoma kitabu cha Isaya,anasema juu ya kufanya neno na hasa jambo jipya,lakini pia sio ajabu wale waliojaliwa kwenda mbinguni kuona tofauti kati ya mtu mmoja na mwingine maana hawaendi wote kwa wakati mmoja.
  Angalia yako makao yanaandaliwa na Bwana Yesu kila siku na kila wakati,bado pia Mungu anasema njia zake hazichunguziki,ni ukomo wa kuona na mawazo yetu tu uishia pale ambapo mmoja amekoma katika ufahamu wake wa kiroho

 8. Cha Msingi ni kulinganisha maelezo ya mtu na ukweli wa biblia, kama maelezo yake yanahitilafiana na ukweli wa Maandiko, tunaweza kujua kwa hakika kuwa ushuhuda wa mtu huyo ni wa uongo; kwa maana Mungu hawezi kujichanganya katika maneno yake Mwenyewe, Biblia inasema “Mungu habadiliki” na kwamba “Yesu Kristo ni yuleyule jana, na leo, na siku zote”. Hivyo, Maneno ya Mungu menyewe yameeleza mbinguni pakoje na patakuwaje watakatifu watakapofufuliwa siku ya mwisho. Hayo tu ndiyo kipimo cha waongo wote.

  Angalia kiungo kifuatacho kwa ajili ya ukweli kuhusu hali ya wafu…

  *. Je tunapokufa tunaenda wapi?

  Harafu baada ya kama wiki 2 (siku 14), leo ni 20-07-2016 hadi 04-08-2016 angalia Je mbinguni pakoje na patakuwaje?. Biblia inaeleza ukweli wote hivyo hatupaswi kuwaami washuhudiaji ambao wanasema kinyume na Maandiko.

 9. YESU akubariki Sana ndugu? Nimemsoma hii post yako vzur na nimeielewa. Sasa ntakuwa na swali kwako. (1) Tunawezaje kujadili kitu tusichokijua? “nkiwa na maana kwamba, nan anaweza kutuelezea MBINGUNI palivyo ili tufanye kupafananisha!”.

  Kristo mwenyewe alishindwa kupaelezea MBINGUNI palivyo au uhalisia wake. Sikumbuki ni fungu gani, ila kristo alisema “Mbinguni panafanana na……” yani yey mwenyewe alishindwa kutuambia pakoje.

  Ukisoma “Kumbukumbu 29:29” hapo utakuta biblia inaweka wazi kabisa mambo tusiyo yajua hayo ni ya Mungu.

  Sasa mim sisemi kuwa ni vbaya au ni sahih au siyo sahih ni Dhambi, HAPANA. Kwasababu hakuna sehem hata moja kwenye biblia ambayo imeweka wazi. IKIWA KRISTO MWENYEWE ALISHINDWA KUTUAMBIA KUHUSU MBINGUNI NA YEYE MWENYEWE NI MWENYEJI WA MBINGUNI, SASA SISI NI AKINA NANI?????

 10. Suala lakuoneshwa mambo ya mbinguni linawezekana na ninaweza kuliita MAONO.
  Jambo hili linaweza kutokea kwa msaada wa Roho Mtakatifu pale mtu anapikuwa KATIKA ROHO.
  Mifano ifuatayo inaweza kuthibitisha hili:
  a). Yohana; Ufunuo4:1
  b). Stefano; Matendo ya mitume 7:55-56
  Ni kweli Mungu anao uwezo wa kuonesha mambo magumu ambayo hata macho yetu hayajawahi ona au hata masikio hayajawahi sikia.
  Kuhusu kumwona Mungu naweza kusema kuwa HAKUNA AWEZAYE KUMWONA MUNGU AKAISHI isipokuwa hawa watu humwona MWANA na si BABA.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s