Usikate Tamaa!

wp-1468997924869.jpg

ELIYA ALIKATAA KUKATISHWA TAMAA

OMBI: Mwenyezi Mungu na Baba yetu mwema wa mbinguni, tunakushukuru sana kwa ajili ya ukuu na upendo Wako kwetu! Asante kwa kutupenda na kutusamehe dhambi zetu. Tunaalika uwepo Wako katika tafakari hii. Tusaidie kulifahamu Neno Lako, tubadilishe ili tufanane Nawe, na pia tupatie uwezo wa kuyatenda mapenzi Yako. Tunaomba na kuamini katika Jina la Yesu Kristo. Amina!

Tuendelee na kutafakari bahari za Eliya:

“Ikawa mara ya saba akasema, Tazama, wingu linatoka katika bahari, nalo ni dogo kama mkono wa mtu. Akanena, Enenda, umwambie Ahabu, Tandika, ushuke, mvua isikuzuie” (1 Wafalme 18:44 ).

Hapa tunapata mafundisho muhimu kutokana na uzoefu wa Eliya. Alipokuwa pale Mlimani Karmeli aliomba mvua inyeshe, imani yake ikajaribiwa, lakini “alidumu katika kufanya maombi yake yajulikane kwa Mungu.”

Aliomba kwa dhati mara sita na bado hapakuwa na ishara iliyoonesha kwamba ombi lake lilikuwa limekubalika, lakini huku imani yake ikiwa na nguvu, alisisitiza ombi lake kuelekea kwenye Kiti cha Enzi cha neema. “Kama angechoka na kukata tamaa mara ya sita ombi lake lisingejibiwa.”

Tunaye Mungu ambaye sikio Lake halijafungwa ili asisikie maombi yetu, na “ikiwa tutalijaribu Neno Lake, ataheshimu imani yetu”. Yeye anataka shauku zetu zote ziwe zinefungamanishwa pamoja na mapenzi Yake na hapo ndipo atatubariki kwa uhakika kabisa, kwani hapo ndipo hatutajitwalia utukufu wakati baraka zitakapokuwa zetu, bali “tutaelekeza sifa zote kwa Mungu.”

Siyo mara zote ambapo Mungu hujibu maombi yetu papo kwa papo tunapomwita kwa mara ya kwanza, kwani akifanya hivi, “tunaweza kukichukulia kirahisi tu kwamba tulikuwa na haki kupata baraka na fadhili zote ambazo alitupatia”.

Mtumishi wa Eliya alikuwa akimtazama Eliya alipokuwa akiomba. Alipokuwa akichunguza moyo wake, alionekana kupungua zaidi na zaidi, kulingana na alivyojitazama mwenyewe na jinsi alivyojiona machoni pa Mungu. llionekana kwake kwamba alikuwa sio kitu na kwamba Mungu ndiye aliyekuwa kila kitu, “na pale alipofikia hatua ya kuikana nafsi, huku akimng’ang’ania Mwokozi kama nguvu na haki yake pekee, jibu lilikuja.”

Hata mtu awe jasiri na mwenye mafanikio kiasi gani afanyapo kazi maalum, “asipodumu kumtazama Mungu” wakati mambo yanapotokea kujaribu imani yake, “atapoteza ujasiri wake”. Hata baada ya Mungu kumpatia vielelezo dhahiri vya uwezo Wake, hata baada ya kuimarishwa kufanya kazi ya Mungu, atashindwa asipomtegemea kikamilifu Yeye aliye na uwezo wote!

Unapokuwa umekwenda mbele za Mungu kwa ajili ya hitaji lako kamwe Usikate tamaa!!

Mchungaji Samuel Imori

Advertisements

5 thoughts on “Usikate Tamaa!

  1. amen be blessed pastor, you encourage us never to give up,but sometimes it needs God power to pass

  2. Barikiwa sana mtumishi wa Mungu Biblia inatuambia kuwa Furahini siku zote, “OMBENI BILA KUKOMA;”shukuruni kwa kila jambo , maana hayo ndiyo mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.” 1 Wathesalonike 5:16-18.

    2016-07-20 10:16 GMT+03:00 Strictly Gospel :

    > Strictly Gospel posted: ” ELIYA ALIKATAA KUKATISHWA TAMAA OMBI: Mwenyezi > Mungu na Baba yetu mwema wa mbinguni, tunakushukuru sana kwa ajili ya ukuu > na upendo Wako kwetu! Asante kwa kutupenda na kutusamehe dhambi zetu. > Tunaalika uwepo Wako katika tafakari hii. Tusaidie kulifaham” >

  3. Pastor Mi Na Mwamin Sana Mungu Ila Wakat Mwngine Nahisi Kama Hanisiki Ktk Mahitaji Yangu Mana Naomba Sana Zaid Ya Mara 7 Ila Bado.

  4. Bwana Yesu asifiwe,nimebarikiwa sana na nmejifunza .Mungu akubariki mtumishi

  5. Thank you for this good massage of encouragement. Kwa kweli nimebarikiwa saaana.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s