JE! UNAHITAJI KITU CHEMA (MKE MWEMA)?

wp-1469595133132.jpg

Hili ni swali ambalo kila mwenye uhitaji wa mke ni lazima ajibu ndiyo, kwa sababu anajua akimpata mke mwema mambo yataenda vema:- maisha yao yatajaa.

Upendo

Furaha,

Amani

Uaminifu

Na pia kupitia mke huyo mwema mume huyo atakuwa amejipatia kibali kwa BWANA (MUNGU)

Mithali 18:22 Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa BWANA.

Kwa akili za kibinadamu tulizo nazo siyo rahisi kumtambua mke mwema maana kimo chake ni kikubwa ajabu.

Mithali 31:10 Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani.

11 Moyo wa mumewe humwamini, Wala hatakosa kupata mapato.

12 Humtendea mema wala si mabaya, Siku zote za maisha yake.

KUNA FAIDA KUBWA SANA UKIMPATA MKE MWEMA, maana huyo hatokufanyia matendo mabaya, sasa usihadaike na kuwekewa mikono uombewe ili MUNGU akupe mke mwema:-

Bali tengeneza njia zako uwe Mkamilifu mbele za MUNGU hakika hatokunyima kitu chema (mke mwema)

Zaburi 84:11 Kwa kuwa BWANA, Mungu, ni jua na ngao, BWANA atatoa neema na utukufu. Hatawanyima kitu chema Hao waendao kwa ukamilifu.

TENGENEZA NJIA ZAKO UENDE KWA UKAMILIFU ILI MUNGU AKUPE KITU CHEMA (MKE MWEMA), MUNGU HAWEZI KUKUPA MKE MWEMA WAKATI WEWE NI:-

Mkorofi

Mwasherati

Mtu wa tamaa

Fisadi

Mlevi

Mtu wa kisasi

Mtukanaji

Ngumi mkononi

Mtu wa hasira.

Tapeli

Mwizi

Muhuni

Akupe Mke huyo mwema ili umtese? umnyanyase?

Jua kwamba atakupa wa kufafana nawe mwenye tabia mbaya kama zako, kwa hivyo  hata uwekewe mikono mara milioni kama huendi katika UNYOFU kumpata mke mwema itakuwa ni ndoto isiyo na utimilizo,  maana mikono ya Wachungaji, Mitume na Manabii haimpi mtu mke mwema, bali ni MUNGU peke yake ndiye mpaji Mke mwema.

Mithali 19:14 Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na BWANA.

Fanya mambo safi yampendezayo yule atoae mke mwema, ili akupe kitu hicho chema.

Abel Suleiman Shiliwa

Advertisements

3 thoughts on “JE! UNAHITAJI KITU CHEMA (MKE MWEMA)?

 1. kwa kweli, mada ni nzuri,sasa kazi ya binti nikutulia tu au naye aombe apate mume mwema?

 2. yukwapi au wako wapi sasa? au wanapatikana wapi….mbona umenukuu tu maandiko!!!

 3. mzidi kutujenga na hasa ambao wameshaoa.
  kwa mfano;
  kabla hamjapata mtoto mapenzi ni motomoto
  kinachoshangaza mkipata mtoto zaidi ya mmoja mapenzi yanapungua
  mala utaambiwa nimechoka mala sijisikii hili linasababishwa na nini?
  Hebu nisaidieni (yamenikuta)

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s