Kuokoka vs Kutenda Dhambi

wp-1470656303150.jpg

 

Biblia katika 1Yohana 5:18 inasema hivi:

“Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hamgusi”

Swali lililopo hapa ni kwamba:

a). Hivii, Mtu AKIOKOKA huendelea tena KUJIZUIA kutenda dhambi au HUWA HAJISIKII kufanya dhambi kwa kuwa msukumo wa kutenda dhambi haumo ndani yake?? ( Yaani HAIHITAJI KUJITAHIDI asitende dhambi bali huwa HAWEZI kutenda dhambi kwa kuwa Nguvu ya dhambi haimo ndani yake??)

b) Kama anatakiwa aendelee KUJIZUIA ASITENDE DHAMBI hata baada ya kuwa amempokea Yesu, Je! Nini tofauti na mtu ambaye HUJITAHIDI KUTENDA MEMA hata kama hajampokea Yesu (Yaani anajitahidi kutimiza Sheria zile 10)?

 

19 thoughts on “Kuokoka vs Kutenda Dhambi

 1. Upo msaada mkubwa kwa mtu ambaye tayari amekwisha kuokoka juu ya kutokutenda Dhambi kwa maana kabla anakuwa hana Uungu ndani yake Roho mtakatifu hutusaidia kutenda matendo mema baada ya kuokoka.

 2. Ni kipi kinatangulia KUOKOKA AU KUOKOLEWA?
  Nikitazama manenno haya mawili ni pacha maana kwangu kuokoka kunatokana na kuokolewa. Maana yake ni kwamba mtu alikuwa hatarini na kisha akawepo mtu mwingine aliyemwona huyu aliyemo hatarini na kisha kumpa ofa ya kumwokoa katika janga lake. Mtu huyo aliyemo hatarini ana uamuzi wa kukubali ofa au kuikataa.
  Kwangu mimi kuokoka ni kuishi ndani ya TOBA kila siku.
  Daudi alimwuliza swali Mungu: Kama, ee mwenyezi Mungu ungekumbuka maovu yetu nani, ee Bwana ni nani angeweza kusalimika? Lakini kwako twapata msamaha, ili sisi tukuheshimu. Zaburi 130
  Wapendwa, mimi navipenda sana viatu vyangu. Kila siku na kila mara ninapotaka kuvaa viatu vyangu huchukua brashi na dawa ya viatu na kuvipiga tena kiukweli hadi vinang’ara. Nikianza kutoka nyumbani hujitahidi kutoingia katika mavumbi na hata matope, najaribu kutafuta mahali pazuri ili nisichafue viatu vyangu, lakini mwisho wa siku pamoja na jithada zangu zote viatu vyangu huwa vimechafuka. Hivyo yanilazimu tena kuvisafisha na kuvipiga brashi.
  Hapa nashuka na kuyalinganisha maisha yangu ya kikristo ndani ya wokovu niliopewa na BWANA. Najitahidi sana kuwa mwenye haki kwa matendo ya sheria ili nisimkosee Mungu na wanadamu, lakini siku ikmazikapo najikuta nimemkosea Mungu na hata wanadamu wenzangu. Ni nani basi apigaye brashi makosa na udhaufu wangu mbele zake Mungu na wanadamu. Jibu langu tena nina uhakika nalo ni moja tu: NI YESU TU anayesimama mbele za BABA yake na BABA yetu akiniombea ili niendelee kuishi kwa mwaka mmoja zaidi. Na ndio wokovu na kokolewa kwangu. Namwomba Mungu anikirimie roho wa toba.

 3. 👏👏👏 eliakim!
  Wokovu = moyo mpya + roho mpya + Roho Mt
  Yaani, ukiisha kupewa moyo mpya, katikati yake hupandwa roho mpya ili kuuongoza huo moyo mpya, ukidumu ktk Neno, sasa Mungu hukupa Roho wake ambaye hukaa katikati ya hiyo roho mpya na hivyo kuviongoza vyote ktk Njia yake!!!
  ““Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.””
  ‭‭EZE.‬ ‭36:26-27‬ ‭

 4. wokovu ni mwitiko wa wito wa Mungu juu ya upatanisho baina yako na yeye kupitia mpatanishi wa ulimwengu na Mungu kristo yesu.
  mwitiko huu ni matokeo ya maamuzi uliyoyafanya ili kutengeneza agano baina yako na Mungu.
  agano hili lina haki na wajibu, haki yako ni kuhesabiwa haki mbele za mungu bule na kufanyika mtoto wake. haki hii inakupa kustailishwa kurithi yaliyo ya baba yako n haki ya kuwa kunasibishwa naye.
  kama baba alivyo ndivyo utakavyokua. wajibu ulionao ni kuwa mtiifu na kuangali jinsi utakavyo maintain uhusiano wako na mungu wako na wajibu wako si zaidi ya kuonyesha kuithamini zawadi hiyo ya kupatanishwa na mungu.
  basi kwa msingi huo, ukiokoka kipaumbele chako ni kutii na kumpenda Mungu, na kipa umbele hicho si zao la nguvu zako bali ni asili mpya unayopewa na Mungu ili kufanana na Baba yako.
  badiliko hili ndio zao la kuishinda nguvu ya zambi, na ikitokea umetenda zambi ni kama umejipaka tope na ndani yako hutatamani kubaki kwenye tope kwani asili yako sio uchafu tena. jambo hili ndo tofauti kubwa kati ya aliyeokoka na aliye bado kuokoka , kwani asiyeokoka zambi kwake siyo issue ya kuichukia, infact ndio lifestyle yake, wala hatokaa ajizuie kutenda zambi.

  ufanisi wa kuishi sin free life ni matokeo ya utakaso wa mwana wa mungu baada ya kuwa mtiifu wa neema ya wokovu na kugeuzwa nia kwa neno la kristo lililojaa kwa wingi ndani yao ambalo uleta nuru na maarifa ya kuzitambua na uzishinda hila za shetani amabazo uwaleta zambini watoto wa mungu.

  hitimisho; niseme hivi wokovu ni badiliko la kubadili vipaumbele vya mtu na kuamua kufuata vipaumbele vya Mungu ili uwe mwana kwelili kweli na siku moja uishi naye milele.( ndo maaana wokovu ni kujikana)
  bali kutookoka ni kuchagua kutii vipaumbele vya kidunia na baba wa dunia hiii ibilisi shetani ambaye ni baba wa uongo ambaye yeye na zambi ni kama ulimi n amate.

 5. WATOTO WA NURU WA KWELI : “Kwa Maana zamani niyi mlikuwa giza, Bali sasa mmekuwa “NURU katika BWANA, enendeni kama watoto wa NURU, kwa kuwa tunda la NURU ni katika WEMA WOTE NA HAKI NA KWELI, MKIHAKIKI NI NINI IMPENDEZAYO BWANA, (waefeso 5:8-10).

  KUJIHAKIKI: Sisi kama watoto na Makuhani wa KRISTO, MUNGU atusaidie sisi tulio wa nuruni tujue wajibu na majukumu yetu katika BWANA!, Maana mahali pengine NURU anatafsiriwa kama “KIONGOZI” au “MWONA MAONO”nk. Hivyo, ni lazima kuenenda kwetu kuwe katika HAKI na KWELI, ili tukaitende haki kwa kila MTU na kila NAFSI tuliyopewa, tena tukaiseme KWELI ya Kristo kwa kila eneo tulilopo na kwa kila kiumbe. Sisi hatutafuti HAKI kwa kuwa Kristo tuliyempokea, amekwishatupa haki yake, Sisi tunatakiwa tuithibitishe ile haki ya Kristo kwa njia ya imani mbele za watu wote….yaani tuhakiki yale yampendezayo Mungu. Maswali ya msingi ya kujiuliza, je, umejihakiki binafsi kujua lililo kusudi la Mungu kwako ?/ katika majira haya magumu tuliyonayo, je, unayatenda yaliyo makusudi ya kristo sawasawa na neno lake?/ Kule kanisani kwenu, wanalichambua na kulihubiri neno la Kristo sawasawa na injili yake, au wanatumia muda mwingi kufanya mambo yao mengine ya kikanisa na kimapokeo?. Hayo ndiyo ya kuyahakiki ktk ukristo wako.

 6. Bwana Yesu asifiwe, Mimi ngoja nichangie kidogo halafu niendelee kujifunza kutoka kwa wachangiaji wengine. Kwanza swali (a). Sisi hatuna nguvu za kushinda dhambi kwa njia ya kujizuia wenyewe, isipokua nguvu tunaipata kutoka katika neno la Mungu tukiongozwa na roho wa kristo, …ndiyo maana bwana Yesu akasema” ninyi bila Mimi hamuwezi”. Sisi wajibu wetu ni kuyaamini na kuyaishi maneno ya Yesu kristo sawasawa na injili yake, na baada ya kutimiza hayo, nikweli kabisa kwamba, ule msukumo wa kutenda dhambi, unaondoshwa na neno la Kristo, na hatimaye, Mtu anajikuta anapata ujasiri wa kushinda dhambi bila ya kutumia nguvu zake mwenyewe.

  Swala (b) ni kwamba, tafsiri au maana ya neno “Kujizuia” haitofautiani sana na tafsiri za maneno ya injili ya bwana Yesu, yanayotutaka: tujiepushe, tujilinde, tujihadhali, tuikimbie nk. Kiukweli hatimaye ni lazima tujikute tumekua hivyo, bila hata ya kutumia nguvu zetu. Mtu mwenye imani ya kweli ya bwana yesu, ni lazima ataidhihirisha imani yake kwa kutokubali kufanya dhambi, ndiyo maana injili inasema “MSITENDE DHAMBI”. Soma(waefeso 4:26) (warumi 6:15,16). Lakini ni kwanini tunajikuta wakati Fulani tumetenda dhambi, na wakati tayari Mungu amekwishatia nguvu ndani yetu?…..Jibu ni kwamba, wakati mwingine, roho zetu hudhoofika kwa kukosa chakula cha kutosha ambacho ni neno la kristo, hatimaye tunajikuta tumetenda dhambi…..kwahiyo, ni lazima neno la kristo liwe kwa wingi ndani yetu. Soma(wakolosai 3:16,17). Mwisho…….bila Yesu umepotea. Mwenye haki wa Mungu ataishi kwa imani, tazama,(warumi3:27)…..sio kwa matendo ya sheria. Ule uadilifu wetu, unazaliwa na imani, na hatimaye tunajikuta tunaenenda sawasawa na mapenzi ya Mungu . vile vitu vya msingi vyenye kutufanya tukubalike mbele za Mungu, kama utakatifu, ukombozi nk…tayari anavyo yesu kristo, soma(1wakorinho 1:30)….ndiyo maana bila yesu umepotea maana Mungu alikwisha kaza kazi yake kupitia uzao wa Daudi, soma(isaya 22:22-23).

 7. Yesu pia alisema ” si wote wasemao bwana bwana watakaourithi ufalme wa Mungu” hii inatupa tahadhari kuwa kuokoka tu na kufanya matendo ya miujiza si tiket ya kuingia Mbingun, bali kuzaa matunda yatokanayo na toba yetu, maana hata din znawatu wasemao wameokoka lakn dunia na tamaa zake znawashinda, Atakaye vumilia mpaka mwisho ndiye ataokoka, ishu sio tumeanzaje, bali tunamalizaje. Wokovu s ktu rahis kama wengne wanavyozan wapendwa, Mungu atutie nguvu tumalize vzuri.

 8. Sungura,
  Nimekuona! Ubarikiwe pia!

  Albert
  Jifunze zaidi maana ya “KUOKOKA” maana unadhani unaijua kumbe huijui rafiki yangu! Hata mimi sijaifahamu kiukamilifu. Ila wewe naakuona uko nyuma zaidi kiuelewa! Mungu akuti nguvu unapofanya jitihada za kujifunza Biblia
  SIyi

 9. UKWELI WA LEO NI “KUOKOKA NI HAPA HAPA DUNIANI”

  Fuatana Nami Katika Hili Ili Ujue Ukweli Wa NENO “KUOKOKA”
  Watu Wanadanganywa Eti Hakuna Kuokoka, Jambo Ambalo Wanapotosha.

  YEHOVA/BWANA aliwajulisha mapema Watumishi Wake Kuwa Watu WATAOKOKA.

  YOELI 2:32 Na Itakuwa Ya Kwamba Mtu Awaye Yote Atakayeliita Jina La BWANA ataponywa; kwa kuwa katika mlima Sayuni na Katika Mlima Yerusalemu Watakuwako Watu Watakaookoka, Kama BWANA alivyosema; na katika mabaki, hao awaitao BWANA.

  Kuokoka Katika Sayuni Na Yerusalemu, Hapo Duniani.
  OBADIA 1:17 Bali Katika Mlima Sayuni Watakuwako Wenye Kuokoka, Nao Utakuwa Mtakatifu; Na Nyumba Ya Yakobo Watamiliki Milki Zao.

  Hapa Panataja Kuokoka, Hapa Hapa Duniani.
  YESU AKATAJA KUOKOKA TENA, MAANA ALIKUJA KUOKOA.

  MATHAYO 18:11 [Kwa maana Mwana Wa Adamu Alikuja Kukiokoa Kilichopotea]

  Kilichookoka Ni Mwanadamu Hapa Hapa Duniani.
  LUKA 19:10 Kwa Kuwa Mwana Wa Adamu Alikuja Kutafuta Na Kuokoa Kile Kilichopotea.

  Kilichookaka Ni MWANADAMU na si kingine.

  YOHANA 5:34 Lakini Mimi Siupokei Ushuhuda Kwa Wanadamu; Walakini Ninasema Haya Ili Ninyi Mpate Kuokoka.
  Yesu Anasema Watu Waokoke.

  MATENDO 2:21,47
  21 Na Itakuwa Kila Atakayeliitia Jina La Bwana Ataokolewa.
  47 Wakimsifu Mungu, Na Kuwapendeza Watu Wote. Bwana Akalizisha Kanisa Kila Siku Kwa Wale Waliokuwa Wakiokolewa.
  Hapa Watu Walikuwa Wanaokoka/wanaokolewa Hapa Hapa Duniani.

  Wewe Unaokoka Kisha Ukifariki Unapewa Ujira Wako Tu.
  NDUGU YANGU KWA HAYA MACHACHE Nadhani Umeelewa Kuwa KUOKOKA NI HAPA HAPA DUNIANI, na ukifa ni Hukumu

  Waebrania 9:27 Na Kama Vile Watu Wanavyowekewa Kufa Mara Moja, Na Baada Ya Kufa Hukumu.

  Baada Ya Kufa Ni Hukumu Na Si KUOKOKA.
  OKOKA SASA ili Hukumu Isikuangamize.
  KUOKOKA NI HAPA HAPA DUNIANI, MBINGUNI NI UJIRA au ZAWADI KWA MEMA ULIYOYATENDA
  MUNGU akubariki.

 10. Biblia inasema, “Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake”. Mtu asoiyemwamini Kristo huyo ni mbaya tu maana yuko upande ule wa ibilisi. Kamwe hawezi kuwaza/kutenda jema. Halikadhalika, mtu mwema, hawezi kutenda mabaya. Ikumbukwe kwamba, mtu mwema yuko kwenye mapambano makali zaidi dhidi ya dhambi kuliko mtu mbaya. Mtu mwema mara nyingine hujikuta ameanguka dhambini katika makuzi yake ya kiimani kwa sababu ya mitego ya ibilisi. Atakapofikia ukamilifu kiimani, ndipo atakuwa amekamilika kiuzaliwa –maana dhambi itakuwa imekoma maishani mwake. Tofauti na hapo, ukijiita umeokoka na hutaki dhambi itajwe kwako wakati huohuo wewe bado uko kwenye makuzi ya kiimani, kimsingi UNATUDANGANYA tu! Maana wewe hujafikia ukamilifu! Kanuni ya mbingu ni kwamba, “Kwa maana hakuna mti mzuri uzaao matunda mabaya, wala mti mbaya uzaao matunda mazuri; kwa kuwa kila mti hutambulikana kwa matunda yake; maana, katika miiba hawachumi tini, wala katika michongoma hawachumi zabibu”.

  Sisi wenyewe hatuwezi kitu/kujiokoa/kujizuia kutenda dhambi! “Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote”.

  Mungu awabariki.
  Siyi

 11. “Lakini Mungu ashukuriwe,kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mlitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini,
  na mlipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki” Warumi 6:17,18

  Kama ingekuwa ni wakristo wako barabarani wanaelekea mbinguni, Yesu angekuwa ametangulia. Nyuma ya Yesu wangefuata wakristo,wanaofuata nyayo za Yesu, Nyuma ya Wakristo kungekuwa na sheria, na nyuma ya sheria kungekuwa na mdhambi.

  1.hivyo wakristo wangekuwa wanaongozwa na Yesu
  2.Walio dhambini wangekuwa chini ya sheria wakitazama mbele ya msafara wanaona sheria tu ikitaja dhambi zao.
  3.Walio katika msafara nyuma ya sheria wangekuwa na kazi ya kutubu/kumwamini Yesu kuamini maneno yake ili waongozwe naye.
  watakaposoma neno na kuona jinsi Yesu alivyojitoa hawakumbuki tena dhambi ila wanaona kutii ni kuwa huru mbali na sheria.

  wakimtazama Yesu wanajifunza mema tu maana yeye hakuvunja sheria akawa chini ya sheria ni mtii daima. hivyo kwa kuwa nao wanakuwa ndani ya Yesu kamwe sheria haisimami mbele yao kuwahukumu.

 12. Aliyeokoka huwa ajisikii kutenda DHAMBI NA ANAOGOPA KUTENDA DHAMBI lakin si yule anayejizuia kutenda DHAMBI.

 13. Wote tumekosa nakupungukiwa na utukufu wa Mungu, ni lazima kutubu kila wakati kwani waweza kukosea bila kujua. Pia tambua kuwa Aaminiye na kubatizwa ataokoka.
  Ahsanteni

 14. Kuokoka ndiyo mwanzo wa kujua jukumu ulilo nalo la kukataa kutenda dhambi. Tamaa za mwili na mengine yanayofanana na hayo twajua kuwa kwa hayo hautaurithi ufalme wa Mungu (Galatia 5: 16-20). Nawewe umekwisha tangaza juu ya azima yako ya kurithi ufalme wa mbingu. Lazima ufanye juhudi kuishi kulingana na matarajio ya Baba yetu wa Mbinguni na jamii ya waaminio.
  Na katika kitabu cha Yakobo 4:7 tumeagizwa kumpinga shetani naye atatukimbia. Ni wazi kabisa kumpinga shetani inahitaji kutumia nguvu, uamuzi thabiti wa kukataa kutenda mambo ya tamaa za mwili. Mtu aliyeokoka ndiye mwenye jukumu la kukataa kufanya dhambi kwa sababu anajua ni kumkosea Mungu.Lakini ambaye hajaokoka anapojizuia kutenda dhambi au mambo kama hayo anachoangalia ni asimuudhi mwenzake au asionekane na mtu.
  Tambua pia kuwa bila juhudi binafsi Biblia imesema vyote ni halali lakini si vyote vifaavyo na pia Warumi 1:18-26 ghadhabu ya Mungu iliachiliwa kwa kutenda udhalimu na hata kuwapa wanadamu roho ya kutenda maovu. Kwa ufupi uliyeokoka utajizuia kutunza ushuhuda wako na Mungu Atakuwezesha kutokana na juhudi yako na kwa asiyeokoka yeye anaangalia mazingira.
  Mungu Atusaidie sana, na aksante kwa kuleta hoja ya kusisimua.

 15. ALIYEOKOKA ANASHIKA AMRI NA ANAKUWA AMEUSHINDA ULIMWENGU

  1 Yohana 5:2-4
  2. Katika hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake.
  3. Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito.
  4. Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.

  Katika agano la kale amri kumi (Katiba) iliandikwa katika mawe.
  katika agano jipya sheria inaandikwa moyoni mwa mtu anayempokea Yesu.

  Yesu aliye ndani ya kiumbe kipya Mtu/ aliyeamini ndiye anayeongoza huu mwili uliotolewa kwake.

  Kuitwa si Kuchaguliwa,
  Mvuvi akishavua huanza kuchambua kile katika nyavu kinachofaa, na kutupa kisichofaa. Ndivyo afanyavyo Yesu.

  Katika agano jipya tunamtazama Yesu,tukianguka sheria inatuhukumu.

  Sio wote walio makanisani watachaguliwa, kwa sababu tu walisema tumempokea Yesu, wakaingia majini,wakaimba,wakahubiri, wakatoa sadaka bali mbio wamezipigaje kutoka misri kupita jangwani hadi kaanani n.K

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s