Je, Ni sawa Kupiga picha ukiwa katika Maombi kisha unaituma kwenye mtandao?

wp-1476940721194.jpg

Bwana Yesu alisema:

“Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. (Mathayo 6 : 6).

Siku hizi mtu anakuwa kwenye maombi, anapigwa picha kisha anairusha kwenye mtandao na kutangaza kwamba alikuwa mbele za Mungu, au anaandika alikuwa anabubujika!!

Mwingine anaamua kufanya maombi ya Kufunga, anakwenda Mlimani, halafu anakuwa anapiga picha kila siku, akiwa huko mlimani na kuzituma katika mtandao.

Nini maoni yako kuhusu suala hili??

 

11 thoughts on “Je, Ni sawa Kupiga picha ukiwa katika Maombi kisha unaituma kwenye mtandao?

 1. Sungura za siku ndugu, majibu yako nakubaliana nayo asilimia zote, tatizo kubwa naloliona kwa wengi ni kutomjua Mungu kitu ambacho hupelekea kufanya mambo ya kufurahisha nafsi zao, Sasa jambo hilo hupelekea kufanya mambo ya machukizo. Lakini kupiga picha pasipo nia ya kukuonyesha hilo halina tatizo.

 2. haipendez kwa mtu wa mung imani unayo wwe mwenyewe

  2016-10-20 8:39 GMT+03:00 Strictly Gospel :

  > Strictly Gospel posted: ” Bwana Yesu alisema: “Bali wewe usalipo, ingia > katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele > za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. (Mathayo 6 > : 6). Siku hizi mtu anakuwa kwenye maombi, anapigwa pi” >

 3. Hayo maneno walikuwa wanaambiwa akina nani hasa, kwa nini waliambiwa, na yanatuhusuje sisis kanisa leo?

  Chumba cha ndani ni kipi, na je tunavyo hivyo vyumba?

  Tuna shida kubwa kabnisa la leo kutokujua lini hasa Agano jipya lilianza., wengi wanadhani Yesu aliishi kwenye Agano jipya pia..

  Kwa kifupi Yesu alikuwa anawaambia hawa watu kwamba wasifanye wema mbele za watu kwa lengo la kujionesha kwa watu hao ili wawasifu. Hakuwa anasema wasifanye wema mbele za watu. Alikuwa anaonya kufanya wema ili watu wakusifu. Kwa hiyo alikuwa anashughulika na NIA zaidi. Yako mambo mema huwezi kuepuka kuyafanya mbele za watu.

  Kinachokatazwa ni kuomba ili kujionesha kwa watu kuwa unaomba, kwa hiyo unkuwa unajionesha kuwa wewe ni mwenye haki. Lakini hakusema kuwa tusiombe hekaluni au mahala ambapo watu wapo.

  Kumbukeni alipokamatwa Petro kanisa walikuwa pamoja wanaomba kwa pamoja, hawakujificha kila mmoja kwenye chumba chake. Nia yao haikuwa kujionesha kwa watu.

  Kupigwa picha ukiwa unaomba kwangu sioni tatizo, tatizo ninaloliona ni nia yako ya kupigwa hizo picha, nia yako ya kurusha hizo picha kwenye mtandao,nia yako ya kufanya mambi radioni ni nini, ndo kina kina maana zaidi.

  Mafarisayo walikuwa wamefika mahali pa kufanya kila kitu ili kusudi watazamwe na watu.

  Sisi tufanye mambo ili kusudi tutazamwe na Mungu, bila kujali tunayafanya mbele za watu au vyumbani mwetu.

 4. Sio sawa Mungu ajasema tushikirie vitu viwili,kuomba ni njia ya kuongea na Mungu nakumueleze haja zako.

 5. The habitual difficulty in prayer is distractions.
  we live in a world where the average attention span is less than a goldfish and that greatly impacts our ability to pray. We need to struggle and combat the various distractions and discover what it is that helps us stay focused. Above all things, we should take our weaknesses to God and ask Him for help.
  In order to stop checking our watch during prayer we need to prepare beforehand, set a timer (when possible) and remember that prayer is not all about us and our devotions. God wants to speak to us and so we should try our best to not let time dictate our prayer.

  Whatever it is, I have found that most distractions during prayer fall into four categories:

  Place (i.e. not being able to pray at a specific location)
  Time (i.e. continually looking at the clock) OR paying attention to camera
  The “To-Do List” (i.e. constantly thinking of all the things that need to get done)
  Wandering Thoughts (i.e. finding yourself thinking about that movie you watched last night).
  Thanks for your time.
  Magreth

 6. Mi nadhani si sahihi kupiga picha ukiwa kwenye maombi, hivi unapata muda upi wa kupiga picha kama umezama kweli kwenye maombi.Tusipojiangalia utandawazi unaweza kuondoa uwepo wa Mungu wakati wa maombi,ili tu mtu mwingine akuone. Roho Mtakatifu atusaidie ili tujue jinsi gani inatupasa kuenenda tukiwa ktk maombi.

 7. Mimi wakati mwingine ufika mbali sana pale Mungu anaposema mawazo yangu sio sawa na yenu,maana lengo kubwa la maombi ya kufunga ni kutafuta kumlingana Mungu kwanza kabla ya kuomba,na wala zoezi ili halianzi wakati tu ule wa kufunga ili kuomba,ila kufanya maandalio ya moyo,kutenda vema kwanza ili kupata kibali,kisha kuwa nayo nia ya dhati kwa ajili ya Bwana,ndipo yale maombi uweza kuwa na matokeo,hapa ni dhahili kama mtu anaingia kwenye maombi kwa staili hiyo basi anaweza kuvuna alichopanda mwishoni,yaani kufunga na kuomba kwa hasara tu,maana iko Saumu ambayo Bwana ameichagua-soma Isaya 58:1-14.

 8. Salaam wapendwa, Natafuta mchungaji au askofu anayezungumza kiswahili Detroit…Naomba mwenye contacts anisaidie Shukran Zawadi.

  Zawadi Machibya BBC World Service-Africa, 5th Floor, New Broadcasting House, Portland Place, W1A 1AA London, UK Tel: +44 (0) 203 6140503 Email: zawadi.machibya@bbc.co.uk Twitter: @zaipermena

 9. Nakusalimieni kwa Jina la kwake kristo Yesu mwokozi wetu? Naomba kuchangia hivi. Kwanza hicho kifungu cha hapo math 6 hakina mahusiano yoyote na hili swali na wala hakiwez kutetea chochote kwenye hili swali. Lakin pia Hakuna kifungu kwenye biblia kinachokataza mtu asipige picha akiomba au akiwa kwenye Hali yoyote ya kumtukuza mungu. Hebu tusilazimishe biblia kutangaza kila kitu kuwa ni dhambi, na tujue hivi “KUNA VITU VINGINE SIYO DHAMBI LAKIN SIYO LAZIMA” Kama wew unaona kwako kwamba haifai Basi waachie wanaopenda waendelee. Paulo alishauri vzur Kama kwako wew unaona kwamba siyo sahihi usiwakwaze wengine alipokuwa akishauri suala Zima la vyakula na vinywaji. Bado aman ya Kristo na iamue moyoni mwenu.

  Ushauri wangu ni kwamba “Naomba tujue, bible is not an academic book” siyo kitabu cha history au biology au chemistry. Let the Bible defend by its own. Thank you for your updates.

 10. Mungu anashughulika na NIA ya moyo wa mtu na siyo mbwembwe zake ama njia zake. Shetani anaweza kupenya akayaharibu maombi ya mtu kama hukuwa makini na nia ya hizo picha ni kutaka nini, kama anataka kuwahamasisha na wengine waingie magotini nakubaliana naye!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s