“Aliyeko Juu Mngoje Chini!”

wp-1478176412108.jpg

“Aliyeko juu mngoje chini”?  Hii ni methali ya kipepo kabisa. Ambaye anaitendea kazi mithali hii ataendelea kubaki chini akiwasubiria walioko juu kiuchumi, walioko juu kielimu, walioko juu kiroho, walioko juu kiufahamu, washuke chini. Na wasiposhuka chini atafanya kila njia awashushe ikibidi kuwaendea kwa waganga wa kienyeji na wengine wanakwenda mbali zaidi kwa kufunga na kuomba ili hao walio juu yake washuke chini. Badala ya kujifunza kutoka kwao mbinu zilizowazesha wao kufika juu ili ajue wamefikaje hapo walipo; yeye anatafuta mbinu za kumsaidia awashushe chini !!

 

Watu wa jinsi hii ndio wale ambao hufurahia wakiona jirani yake kafukuzwa kazi utasikia: “HALO HALOO… WALIKUWA WANAJIDAI KULA WALI NYAMA, SIJUI WALI MAINI, SIJUI MARA LEO KITIMOTO, TUWAONE SASA KAMA WATATULINGISHIA TENA HIVYO VYAKULA VYAO”.

YAANI WENZAO KULA VYAKULA VINONO WANAONA WANALINGISHIWA !!

 

Watu wa jinsi hii ndio wale ambao wakiona mfanyakazi mwenzake kapandishwa cheo wanamwendea kwa mganga wa kienyeji. Ni watu wasiopenda kuona wengine wanafanikiwa. BAHATI MBAYA ZAIDI WAPO WACHUNGAJI, MITUME, MANABII, NA WALIMU WA JINSI HII; AMBAO WAKIONA MWENZAO ANA KANISA KUBWA, MUNGU KAMFANIKISHA KIUCHUMI UTASIKIA OOOOH FREEMASON !! Yaani kila aliyefanikwa Freemason !! HIZI NI AKILI ZILIZOJAA FUNGUS KABISA AISEE !!

 

SIKIA USIWAOGOPE WATU WA JINSI HIYO, MUNGU NDIYE ALIYEKUWEKA JUU; WATASUBIRI SANA HADI YESU ARUDI. WATAENDA CHOLE WATARUDI, WATAKUKUTA BADO UKO JUU, WATAENDA UYOLE WATARUDI WATAKUTA UMEENDA JUU ZAIDI, WATAENDA NYANSHANA WATARUDI WATAKUTA UMEYAPITA MAWINGU KWA KWENDA JUU ZAIDI. WATAKUROGA NDIO, LAKINI HAUTAROGEKA, KWANI UKO NDANI YA YESU. WAMROGE KWANZA YESU NDIO WATAKUROGA  NA WEWE !! MAANA MAANDIKO YANASEMA; “HAKIKA HAPANA UCHAWI JUU YA YAKOBO, WALA HAPANA UGANGA JUU YA ISRAELI” (Hesabu 23:23). WATANGOJA SANA LAKINI HAWATAKUONA UKISHUKA ! Ni shauku yangu niweze kusema na japo mtu mmoja hapa. Haleluyah!!

 

AS LONG AS GOD IS WITH YOU EVEN THE SKY IS NOT THE LIMIT!!. FLAP YOUR WINGS LIKE AN EAGLE  AND LET THE STORMS TAKE YOU TO THE HIGHEST ALTITUDE !!

 

28 Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, Bwana, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki.

29 Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo.

30 Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka;

31 bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia. (IsaYA 40:28-31).

 

MUNGU WANGU AKUBARIKI !!

 

Mwalimu na Mchungaji Gibson Gondwe.

3 thoughts on ““Aliyeko Juu Mngoje Chini!”

  1. Hapana hiyo siyo tafsiri ya hiyo methali. Haifai kupotosha maana halisi ya methali zetu za kale. Juu inyozungumziwa hapo, siyo ile itokanayo na mafanikio baada ya mtu kufanya kazi kwa juhudi na maarifa. Juu inayozungumziwa hapo ni ile ya kiujanja ujanja kwa mfano kupiga hela kwa udanganyifu na hila. methali hiyo ilikuwa inawaasa watu wabaki na shughuli zao halali kuliko kuwaiga watu wenye mapato ya aibu . Maisha ya binadamu yapo ardhini, ijapokuwa kwa muda atapanda juu ya mti huyo lazima atashuka tu chini. Kupanda juu huko ni kule kusivyokuwa halali. Kunalinganishwa na kupanda juu ya mti huko hakuna mwendelezo wa maisha kwa mtu. Atashuka tu chini.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s