Injili Ruksa kuhubiriwa vilabu vya pombe

3137de4f-218b-4125-8a76-506085aaa093

Mkuu wa Mkoa Wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda tarehe 8 mwezi Wa tisa ametoa kibali kwa Watumishi wa Mungu wa Dini zote kuhubiri na kutangaza neno la Mungu kwenye Sehemu za Club, Disko na Kumbi za Starehe ili neno la Mungu lizidi kuenea na kuwafikia watu wote jambo litakalosaidia kujenga jamii inayomjua Mungu.
_
RC Makonda amesema Mtumishi wa Mungu atakapohitaji kuhubiri mziki utazimwa kwa muda wa Nusu saa na baada ya hapo watu wataendelea na starehe zao wakiwa tayari wamepokea Neno la Mungu na kuahidi kuwa Mmiliki wa Club atakaemkatalia Mtumishi Kuhubiri RC Makonda atamwombea Mtumishi huyo na ikibidi atamsindikiza.
_
Hatua hiyo ya RC Makonda imekuja baada ya kubaini uwepo wa Idadi kubwa ya watu kwenye sehemu za starehe na pindi watu hao wakienda Makanisani na Misikitini wanaishia kusinzia na wengine wanakuwa wamechoka kiasi cha kushindwa kulisikiliza kwa ufasaha neno la Mungu.
_
Hayo yote yalijiri wakati akizungumza na Waumini wa Kanisa la Arise and Shine linaloongozwa na Mtumishi wa Mungu Apostle Boniface Mwamposa.

3 thoughts on “Injili Ruksa kuhubiriwa vilabu vya pombe

  1. Linahitaji umakini kidogo , lazima mtu asikilize kama Roho Mtakatifu anamwongoza kuhubiri maeneo hayo , wasije waka ” act” kwasababu mkuu wa mkoa ameruhusu na anataka wahubiri huko.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s