MAOMBI

Je una hitaji lolote ungependa kushirikisha watu/mtu kwa ajili ya kumuomba Mungu? yaweza liwe lako binafsi, nchi, watumishi wa Mungu na mengineyo. Strictly Gospel Tuna Team ya Maombi ambapo tunaombea maombi haya. Pia Yeyote popote Ulipo unaweza kuguswa kumuombea mtu mahala hapa na akapokea Uponyaji kwa Jina la Yesu Kristo.

Ukipokea Uponyaji, Tutafurahi kupata ushuhuda wako. Karibuni

Kujiunga na Team ya maombi wasiliana nasi kwa

Email: strictlygospel@yahoo.co.uk

1,038 thoughts on “MAOMBI

 1. Shalom, jamani tuiombee nchi ya Kenya, matokeo uchaguzi yakawe ya amani. Kenya, kuwe na amani nchi nzima.

 2. Bwana Asifiwe Wapendwa! Napenda kuwashirikisha,naomba tushirikiane kwenye maombi ,mniombee niko kwenye kipindi kigumu sana cha mapito!Naomba kuwashirikisha mniombee ili Mungu atende kadri ya Mapenzi yake.

  Vilevile naomba mniombee nizidi kusimama kwenye imani maaana majaribu ni mengi sana,

  Asante na Mungu awabariki sana! Wapendwa hakika Mungu anaweza!

 3. Shalom, naomba mniombee wapendwa niko katika kipindi kigumu na vita kali inazidi juu yangu mniombee nizidi kukua katika imani, mniombee nipate amani, furaha na utulivu Mungu awabariki sana

 4. wapendwa mniombee niko kwenye mapito magumu kazini kwangu naomba maombi yenu

 5. Shalom wapendwa hasa wenye mzigo wa kuomba, tuombe kwa ajili ya Kenya, machafuko yanazidi watoto wanapoteza wazazi na watu wanahama katika nchi yao. Tumwambie Mungu akaiponye nchi ya Kenya

 6. Ndungu nawasihi tuombee kenya yetu.Naamini mungu anaweza fanya jambo kubwa kubwa. Hasa kwa wale wamebaki bila makao an chakula pia. Tuombee amani.

 7. Bwana Yesu Asifiwe sana wapendwa! Naomba mniombee niko kwenye vita kali na adui yangu, amedhamiria kuniangusha, lakini mimi nataka afahamu kuwa mungu yupo na zaidi ya yote anaweza!

  wapendwa nimekuwa silali usiku wala kula chakula nashindwa, kwa jinsi adui anavyonitesa! Nataka Mungu ajidhihirishe kuwa yu hai jana,leo na hata milele! na halali wala hasinzii!
  Mungu awabariki sana! TUSIMAME KATIKA IMANI NA HAKIKA TUTAYAONA MATENDO MAKUU YA BWANA.

 8. Mungu atufanikishe sisi sote tmchao hasa tulio okoka tuwe vichwa na si mikia kila tutakapo weka nyayo za miguu yeu

 9. Always in our troubles JESUS CHRIST step in to give us victory.What we suppose to do is to continue praying and we shall prove that we have a working miracle GOD.May our Lord be with us cause without him in this world we can`t survive.Let us be in prayers always and we shall see God.Be blessed in Jesus name

 10. MSIOGOPE WAPENDW A NI WAKATI WA KULETA YANAYOWASIBU KWA YESU.MIMI LANGU NAMUOMBA YESU ANIPE MAISHA MAREFU.NA ANIONDOLEE UMASIKINI NILIONAO.PIA ANIPE KUMPENDA YEYE SANA NA WATU WENGINE NA NAOMBA MNIOMBEE.

 11. Shalom wapendwa katika bwana,
  naomba mniombee maana napitia katika mateso na kipindi kigumu sana hasa kwa ndugu zangu, mchumba wangu, na marafiki zangu
  naomba mniombee ndugu zangu niko katika hali ngumu sana.

  Mungu awabariki wote mnaomtumikia kwa moyo wa ukunjufu

 12. Bwana Yesu asifiwe!

  Nakabiliwa na kipindi kigumu sana katika masomo yangu, ndugu zangu naomba mniombee nitapate kushinda. Ninaamini katika YEYE ALIYE HAI hakuna kinachoshindikana.

  Bwana awabariki sana.

 13. Bwana wetu Yesu asifiwe. Naomba watu wa Mungu tuombe kwa ajili ya amani Zanzibar. Tusipoomba tutajikuta tuko hatarini karibu nchi nzima. Tuombe pia kwa ajili ya Somalia, Darfur, DRC, Afghanistan, Zimbabwe na Iraq

 14. Bwana Yesu asifiwe!

  Namuomba Yesu aliye hai azinusuru ndoa zetu. Atufunike wanandoa wote ili tutambue kwamba tuliapa kanisani mbele ya Mungu na akili zetu timamu kuwa tutakuwa waaminifu katika ndoa zetu. Basi awafunike wote na damu ya Yesu wale wanaoenda kinyumbe na kiapo hicho wawe waaminifu. Afute tamaa zote zinazowaingia wale ambao wanaasi ndoa zao na hatimaye watulie katika ndoa zao. Ninaomba hayo kwa jila la bwana wetu Yesu Kristu aliye hai

 15. Naomba mniombee wapendwa, nipo kwenye ndoa miaka mitatu sasa sijapata mtoto. Mniombee Mungu anijalie haja za moyo wangu.

 16. bwana yesu asifiwe sana
  naomba mniombee, nilipomzaa mwanangu nilipata hedhi kama kawaida baadaye ikaapotea,baada ya muda ikaanza tena, na baadaye ikapotea kama miezi nane,
  nasasa imeanza kama miezi mitatu nipo kwenye hadhi nawasiwasi kama nina matatizo.
  ila madaktari wameniambia sina tatizo nasubili kuwaona madaktari wa wanawake .sasa
  najua kwa mungu hakuna lisilowezekana.
  nipo kwenye kipindi kigumu sana
  naitaji maombi yenu sana
  asanteni na mungu awabariki

 17. • Tembea katika Nguvu ya Mungu

  Neno la Mungu ndiyo mwisho wa matatizo yote. Unapoliamini na kulikiri linatenda. Neno la Mungu pekee ndilo linaweza kugeuza laana kuwa baraka, kushindwa kuwa ushindi, ugonjwa kuwa uzima, umasikini kuwa utele linaweza kuumba na kufanya kisichokuwepo kikawepo. Ni ajabu Mungu ametupa neno lake lenye nguvu. Tatizo ni pale wengine wetu hawalijui au hawaliamini kwa asilimia zote ndani yao. Watu wanapolijua neno la Mungu na kuliamini na kulikiri watatembea kama wafalme na siyo kama watumwa. Lakini kwa kutokuliamini neno wengi wanaishi chini ya kiwango kilichokusudiwa na Mungu juu yao. Wapendwa tushirikiane kwa pamoja kuomba kwa ajili ya ndugu zetu wenye matmbalimbali kwa kadri Roho Wa Mungu atakavyokuongoza. BARIKIWENI

 18. jamani kwa kumwambia yesu shida zetu tutashinda,lakini tuamini tatizo hatuamini kuomba tunaomba lakini tunamashaka ni lazima tuamini na tusubiri.NA UKIANDIKA HAPA KATIKA UKURASA HUU UJUE MAJESHI YAMEANZA KUOMBA JUU YAKO KAA TAYARI KUPOKEA KILE ULICHOSEMA TUOMBEE. USILALAMIKE TENA TUNAOMBA KWA NIABA YAKO NA HUYU YESU ATAJIBU PAPO HAPO AMINI TU.

 19. Shalom,
  Bwana Yesu Asifiwe,
  wapendwa niombee nahitaji mtoto,
  nimeolewa miaka zaidi ya kumi sasa sijapata mtoto naomba
  Mungu anayejibu maombi akutane na haja ya moyo wangu.

 20. Bwana asifiwe!!!!
  Wapendwa katika bwana,Naomba mniombee ili niweze kupata chuo huku Finland, maana kuna Interview kama 2 nimeshafanya.
  Mungu azidi kuwatia moyo,Nahitaji sana maombi yenu.

 21. Bwana Asifiwe,
  Wapendwa katika Bwana Yesu, naomba mniombee nina vita sana kazini, kama haiwezekani nipate mahali pengine. Hali ni mbaya sina amani kabisa na kila nikiingia kazini naona kizunguzungu sana.
  Mungu awatie moyo na nguvu, Maombi ndio silaha kuu ya kushinda vita zote.
  Maombi yenu ni muhimu sana kwangu

 22. shalom,
  wapendwa naomba mniombee vita kali juu ya nyumba ninayoishi kwani inajihusisha na ushirikina sana pia,kwani naami kwa mchango wa maombi mungu atawaibisha
  pia na mabaya wanitakiayo hayanipata bali yatageuka kuwa mafanikio makubwa kwangu.
  pia amani moyoni mwangu na afya pia kudumu katika kazi yangu na kuaminika zaidi naami
  mungu atanitendea miugiza mingi juu yangu.

  NAWAPENDA SANA.

 23. Bwana yesu asifiwe,
  wapedwa naombeni maombi juu ya mama yangu mzazi kwani anasumbuliwa na maradhi kila
  wakati pia mungu amjalie miaka mingi na mafanikio katika biashara zake pia hata kilimo
  zaidi ikiwepo dada zangu na mdogo wangu pia ndungu zangu wote nawaombea mafanikio
  pia familia yetu iwe ya upendo na amani kila tunalofanya tuzidi kufanikiwa .

  MUNGU AWAJALIE MOYO HUO HUO.

 24. Ndugu zangu..bwana asifiwe.

  Naomba mjumuike nami kwatika uniombea…ninakabiliwa na kesi kubwa sana ambayo inaweka maisha yangu katika hali isiyotabirika na itanifanya nipoteze watoto wangu. Mnisaidie kumuomba mungu anipe nguvu, uvumilivu na aweze kuniokoa katika matatizo haya…. Naomba haya yote kwa mungu aliye mwema na mwenye huruma.

 25. Bwana yesu apewe sifa ,
  Wapenda katika bwana naomba niwashirikishe katika maombi juu ya dada zangu wanahitaji watoto,Binafsi nilikuwa mmojawapo katika hilo ila namshukuru bwana ametenda juu yangu na sasa nina mtoto wa kike mwenye afya njema asante YESU,naamini kwa maombi na sala zetu nao watafanikiwa katika utatu,bwana awatangulie kwa yote ,Amina.

 26. Niko pamoja nao katika mapito wanayopitia.
  Binaadamu hatuwezi kutatuwa shida zote ila Baba yetu wa Mbinguni hutusaidia.

  Jambo la maana hapa wasiikane imani kwa sababu ya kukosa watoto. Maana Mbinguni kila mtu ataingia kwa nafsi yake. Na Mungu anawatambuwa wao kwa majina yao si kwa majina ya watoto wao. Huo ni Urithi bora zaidi ya watoto elfu.

  Naamini Mungu pamoja nao kwamba atawapa haja za mioyo yao. Kama kwako iliwezekana, kwao itawezekana pia!

  Barikiwa dada Doro!

 27. Pole dada Lilian. Lakini sijaelewa unaposema kwamba ‘unaweza ukapoteza watoto’. Ni kwamba watauawa au ni vipi?

  Lakini ukisimama vyema katika nafasi yako Mungu atatenda katika nafasi yake!

  Barikiwa!

 28. Bwana Yesu Asifiwe wapendwa,
  Naomba mtuombee mimi na mume wangu tuna vita kali sana na ndugu, wao niwakutambika na kuabudu mizimu, sisi hatukubaliani nao, tunaomba Mungu atupe uzima na ulinzi na azidi kuonekana katika maisha yetu ili wajue hakika Mungu wetu ndio jibu.
  Pia naomba maombi kwa ajili ya mama yangu Mungu amtie nguvu na kumponya na kumpa miaka mingi na mafanikio katika yote.
  Naamini Mungu atafanya haya yote.
  Mbarikiwe wapendwa.

 29. Ameni wapendwa wenye matatizo tofauti wote tuseme hivi:aliyedhaifu na aseme mimi ni hodari,sitashindwa bali nitashinda maana vita si yetu bali ni ya bwana cha muhimu ni kuona shida ndogo na mungu wetu ni mkubwa matokeo tutayaona.mungu atayaondoa hayo mateso yote .isaya49:15.

 30. Bwana Yesu Asifiwe!
  Mie ni mjane kwa muda wa miaka minne nina mtoto mmoja. Naomba mniweke kwenye maombi nipate moyo wa ujasiri niweze kumlea mwanangu pamoja na kuacha ULEVI ambao naona unanirudisha nyuma sana. Nina kazi nzuri lakini sina la maana, naomba mnisaidie niweze kuachana na hiyo hali. Vilevile niweze kupata mwenza wa kweli maana nahangaika sana kila ninayempata ananichezea na kuniacha. Nina affair na mume wa mtu hilo nalo linanitesa sana sipendi ila amekuwa ni mtu wangu wa karibu ktk kila jambo ingawa sipendi huu uhusiano, najua natenda dhambi kubwa sana naomba mnisaidie kwa maombi maana nimekuwa mvivu ata kwenda kanisani na muda wa kusoma biblia pia sina. Nahitaji msaada.

 31. Wapendwa Bwana yesu apewe Sifa,
  kwanza niwashukuruni kwa kazi nzuri mnayoifanya.
  nimemuona Mungu baadhi ya maombi ambayo nilimwomba Mungu kwani nimeona majibu yake baadhi pia naombeni mniombeoombee zaidi ili mungu aonekane katika vita juu nyumba ninayoishi kwani imekuwa na maneno kila wakati pia wanajihusha na nguvu za giza sana,pia mniombee juu ya waganga wanaowaleta hapo nyumbani kwa lolote walifanyalo
  wasifanikiwe bali waabike pia Mungu aonekane.

 32. Dada Vivian, kama uliyoyasema ni kweli yametoka ndani ya moyo wako, ushauri wangu ni huu:

  Ili uweze kufaidi uzuri wa Yesu unatakiwa umkaribishe moyoni mwako kwanza. Yesu akiingia moyoni mwako mambo yafuatayo (na kuzidi) yatatokea:

  1) – Utakuwa na uhakika ukifa unakwenda mbinguni. Uhakika huu
  utaleta amani ya ajabu moyoni mwako
  2) – Utaweza kuishi maisha matakatifu
  3) – Utapata ujasiri na hekima ya kumlea mtoto wako
  4) – Kiu ya ulevi wa aina yoyote itakwisha
  5) – Yesu atakupa nguvu (kwa msaada wa Roho mtakatifu) kushinda
  tamaa za mwili hadi utakapopata mwenzi wako
  6) – Na kwa kuwa sasa utaishi maisha ya heshima ni rahisi kupata
  ‘mwenza wa kweli’ kuliko maisha ya sasa ya ‘ulevi’ unayoishi.
  7) – Nawe utakuwa na mamlaka ya kulitumia JINA la Yesu kama
  silaha yako mwenyewe. Matatizo mengine utayaamuru wewe
  mwenyewe kwa JINA la Yesu nayo yatakwisha.

  Kwa ufupi ni kwamba Yesu ndiyo UFUNGUO wa maisha yenye FURAHA na AMANI.

 33. Dada Vivian,

  Asante kwamba umeupokea ushauri! Natumaini utaufanyia kazi.

  Tuonane Mbinguni

  Barikiwa!

 34. DADA DAINESS HIYO NYUMBA HAMA USIKAE NA WACHAWI.KAMA UMEPANGA HAMA NA KAMA NI YAKO WAHAMISHE WACHAWI KWA JINA LA YESU.USIFUNGIWE NIRA PAMOJA NA WASIOAMINI.PIA UCHAWI AU USHIRIKINA HAUNA KAZI KWA MWANA WA MUNGU.NGUVU ZA USHIRIKINA ZILIVUNJWA KWA WOTE WANAOMWAMINI MUNGU KATIKA YESU.HAWATUWEZI TENA WANATISHA TU.MITHALI 26:27 HUU MSTALI NI AMINI.

 35. Wapendwa, Bwana Yesu asifiwe.
  Namshukuru Mungu kunipa nafasi ya kukutana na website hii. Mbarikiwe wana maombi wote. Naomba tuungane sote kuliombea Taifa letu, Rais JK na Baraza lake lote la Mawaziri likafunguliwe ktk minyororo ya shetani likamjue Mungu nchi iwe na amani ya Mungu. Tuombe kwa ajili ya machafuko ya Zanzibar, na nchi zote ulimwenguni zenye machafuko ya kivita. Binasfi nahitahi mshirikiane nami ktk vita hii ya shetani inayoniandama kazini, ndoa, familia, marafiki na adui, ili niweze kusimama ktk Imani yangu ya Kumwamini Bwana Yesu kuwa yeye atosha ktk maisha yangu. Nguvu ya Roho Mtakatifu wa Mungu izidi kutenda kazi maishani mwangu.

  Wapendwa tusimame kwa moyo mmoja ktk imani ya kweli na yote yatajibiwa.
  Baraka ya Mungu wetu iwe nasi sote!..AMEN

 36. Wapendwa katika Bwana, Bwana Yesu asifiwe.
  namshukuru Mungu kukutana na ninyi katika website hii. Mungu awabariki sana watumishi wa Mungu mimi naitwa maria, nilikuwa na rafiki yangu tulianza urafiki yapata miaka saba hivi sasa. Kitu cha kusikitisha au kama ni mipango ya Mungu siwezi jua alikuwa na rafiki mwingine bahati mbaya alimpa mimba (jina litalihifadhi ) mimi nilikuwa sijuhi, muda kama wiki moja imepita yule msichana alijifungua na Mungu akambariki na akapewa mtoto wa kiume. Kitu alicho kifanya alisema hataki tena mawasiliano na mimi wala nisizoee namba yake ya simu tena maana anaishi na mke wake nyumbani ambaye ndiye huyo msichana. niliumia sana ila nikamwomba Mungu anitie nguvu Mungu akasikia kilio changu.

  wapendwa katika Bwana naomba mniombee Mungu anipatie Mume mwema kutoka kwake.

 37. Wapendwa katika Bwana Yesu, Bwana Yesu apewe sifa.
  Ninaitwa Bezaleli (LMKT), (tarehe 27 Juni mwaka huu ikimpendeza Mungu nitatimiza umri wa miaka thelathini na nane) kwa sasa ninasoma, cha kushangaza ni kuwa uwezo wangu wa kumbukumbu umepungua sana, ninakuwa kila wakati ninapofanya mitihani ni lazima nirudie tu maana sipiti baadhi ya mitihani yangu.

  Niombeeni ili Bwana Yesu aweze tena ‘kunikumbuka’ na kunirudishia kumbukumbu nilizokuwa nazo miaka ya ’80 na ’90.

  Mungu awabariki sana.

 38. Nashukuru sana wapendwa na Mungu awabariki sana naombeni mniombee Mungu anifanikishe katika masomo yangu ya chuo nifaulu vizuri ili jina la Yesu liinuliwe sana zaidi ya yote anipe mume mwema kutoka kwake naomba mniombee sana nisije nikakosea katika mtihani huu wa ndoa maana najua yote yanawezakana kwa Mungu na ni kwa maombi tuu,upako ule ule wa Bonny Mwaitege naomba anitumie na na mimi nipate mume mwema kutoka kwa bwana UNGU AWABARIKI SANAAAAAAAAA

 39. Asante sana dada LEVANA KATANA kwa ushauri wako ndugu yangu kwani nyumba ninayoishi nimepanga2 na ndio mwanzo wa kuanza maisha kwani sijawahi kupanga nyumba
  na hivi niko kwenye mtihani mgumu wa kutafuta nyumba nyingine pia kwa mchango wenu wa maombi naombeni mnisaidie kuniombea kabla ya mwezi huu niweze kupata nyumba nyingine kwani hali siyo nzuri katika nyumba hiyo kabisa pia kuna hata mtumishi mmoja aliwahi kuniambia kuwa nyumba hiyo ina vitu amabavyo vimezikwa hapo yeye alionyeshwa akiwa maombini nisaidieni wapendwa nipate room kabla ya mwisho wa mwezi.
  lingine tujumuike kuiombea SOUTH AFRICA kwani kule sasa hali sio nzuri kwani wamefikia hatua ya kuchoma watu ovyo pasipo hatia toumbe pia kwa ajili ya hilo wapedwa wangu wote mliopo katika web hii MUNGU AWATIE NGUVU MUWAPO MAOMBINI NA KATIKA SHUGHULI ZENU ZOTE.

 40. niko new york,nimepata faraja kwamba kuwa kunaopenda kuwaombea watu wenye shida na magonjwa mbalimbali kama mimi kwanza kabisa najiona mzima japo wamesema naumw ila mimi siumwi naamini hivyo kwani hata majibu yakija naona wataona miujiza imetandeka kwa kunisaidia kuomba,bwana yesu asifiwe sana,nataraji kupokea wokovu kuanzia mda huu nisafishwe kwa damu ya yesu initakese niwe mweupe kama firuji katika moyo wangu amin.wapendwa katika jina la yesu naamini hukuna mungu anishndwa kila ktu chawezekana kwa imani asnteni MUNGU AWABARIKA SANA.

 41. Ndugu wapendwa,
  Mungu ni baba yetu kabisa. Na yeye akiwa baba yetu hapendi kuona sisi watoto wake tukiteseka maana Yesu alimaliza yote pale msalabani. Damu ya Yesu na Jina la Yesu ni silaha za ajabu, katika ulimwengu wa roho, zikitumiwa na watakatifu. Nguvu zozote za giza haziwezi kamwe kuwadhuru wote wanaomwamini Yesu na kukaa ndani yake maana malaika wa Mungu huwazingira kwa ngome imara ya ulinzi wakati wote. Tunaomwamini Yesu huwa tunateseka kwa sababu ya kupungukiwa na maarifa na ufahamu juu ya uweza wa huyu Yesu tunayemwamini. Maisha yetu tunayoishi wakati mwingine yanatuweka mbali na msaada wa Mkono wenye Nguvu wa Mungu!

  Hebu tuombe Mungu ili tuweze kuishi maisha matakatifu. Maisha matakatifu ni ufumbuzi wa matatizo mengi yanayotuzunguka. Pia imetupasa kumtaka Bwana Mungu na nguvu zake (1Nyakati 16:11)

  Nawatakia baraka ya amani katika maisha ya kila siku.

 42. Ninahitaji maombi kwa ajili ya uponyaji wa Robinson Mchau:
  Huyu ndugu ni mpendwa ambaye hivi karibuni amepatwa na matatizo katika mfumo wake wa chakula. Alifanyiwa operesheni mara ya kwanza katika hospitali ya KCMC Moshi na wakakata sehemu ya utumbo mpana. Baada ya muda ikagundulika kuwa kifaa cha operesheni kilisahaulika tumboni, hivyo ikabidi wamfanyie operesheni nyingine kukitoa. Alipomaliza operesheni ya pili akarudi nyumbani, lakini baadaye akapata tatizo la usaha kwenye kidonda, hivyo akarudi tena hospitali kutolewa usaha na kuwa anapakwa dawa itakayokausha kidonda haraka. Hivi sasa wamepeleka India sample ya utumbo uliokatwa kwa ajili ya kuchunguza kiini cha tatizo na majibu yatarudi Jumatano ya tarehe 11/06/2008. Leo hii tarehe 09/06/2008 wamechukua kipimo kingine kwenye njia ya haja kubwa kwa uchunguzi zaidi na majibu watatoa saa 12 jioni ya leo hii (09/06/2008). Hivyo huyu kaka anahitaji maombi kwa ajili ya uponyaji upatikanao kwa Yesu Kristo. Matibabu yanagharimu pesa nyingi kiasi kwamba sasa upatikanaji wa pesa kwa ajili ya matibabu na chakula umekuwa mgumu. Jambo hili linahitaji msaada wa Yesu Kristo. Tumuombe Bwana Yesu atende muujiza wa uponyaji. AMEN.

 43. Ndugu yangu Prisca.

  Nakuombea ili uwe na ujasiri katika moyo wako na uweze kukata shauri na umpokee Yesu Kristo kama Bwana Na Mwokozi wa maisha yako.

  Sema sala hii

  Bwana Yesu, naamini kuwa wewe pekee ndiye mwokozi.
  Naomba unisamehe zambi zangu zote na uniponye na magonjwa yote.
  Njoo ndani ya moyo wangu na uniumbe upya kabisa.
  Ee Mungu na shukuru kwa zawadi ya msamaha wa zambi zangu zote.
  Nampokea Yesu Kristo sasa, kama Bwana Na Mwokozi wa Maisha Yangu.
  Ninaamini moyoni mwangu ya kwamba Yesu ndiye Kristo, na Mungu ulimfufuwa kutoka katika wafu.
  Ninaujasiri sasa wa kusema Nimeokoka.
  Mimi ni kiumbe kipya sasa. Mungu ni Baba Yangu, Yesu ni Mwokozi wangu na Roho mtakatifu ameingia ndani yangu kuwa msaidizi wangu, Amen.

  Niandike email kama umesema sala hii, ili nizidi kuomba pamoja na wewe.
  pastorfidelis@gmail.com

  From: Birmingham, Alabama USA.

 44. Vivian Dada Yangu.

  Katika watu wote hapa duniani, sijaona wala kusikia wenye ujasili na wakweli kama wewe.
  Naomba nikutie moyo kwanza kabisa. Maana watu wengi wasingeweza kueleza hayo yote. Ninaamini huu ni wakati wako wa kupokea rehema za Mungu.
  Ninasikia moyoni mwangu kuwa, moyo wako unamlilia Bwana Yesu ili akusamehe.
  Na yeye ameshasikia kilio chako. Kwamaana amesema katika:
  Isaiah 65:24:
  I will answer them before they even call to me.
  While they are still talking about their needs,
  I will go ahead and answer their prayers!

  Nakuomba dada vivian useme sala ambayo nimemtumia Prisca.
  Ni maombi ambayo ni rahisi kabisa lakini yana nguvu za Ki-Mungu ndani yake.
  Hayo mengine yote yatafuatia baada ya nguvu za Mungu kuingia ndani yako (Roho Mtakatifu).
  Mimi sifahamu wewe ulipo (TZA au USA…) Lakini Mungu yupo pamoja na wewe mahali ulipo. Pokea ujasiri ndani ya moyo wako na umkiri Yesu Kristo kama Bwana Na Mwokozi wa maisha yako sasa hivi. Hakuna nguvu zozote za giza zinazo weza kukuzuia kufanya uamuzi huu. Kama zitafanikiwa ni kwasababu utakuwa umezipatia nafasi hiyo.
  Kwa hiyo basi, Tamka maombi ambayo nimemtuma Prisca. Hakikisha yanatoka moyoni mwako na Mungu atakusamehe zambi zako zote; na atakufanya kiumbe kipya.
  Tafadhali tuwasiliane ili tuweze kuzidi kuombeana.

  Pastor Fidelis Irengo – USA.

 45. NAWAOMBEA WANARIADHA WEZANGU WAMPENDE BWANA YESU NDIYO NJIA PEKEE, NAJUA SANA WENGI WANAABUDU WAGANGA WA KIENYEJI ILI KUPATA MALI :OKOKENI????? HALELUYA

  MIMI PIA NI MWANARIADHA NIMEOKOKA MWAKA JANA NAMPENDA YESU SANA NAISHI ARUSHA MIANZINI

  SIMU-0784-36-41-20

 46. SHALOM WAPENDWA WOTE WA GLOB HII.

  NIMEONA NISHIRIKIANENI NA NYIE KWANI NAAMI YA KUWA MAOMBI YENU YATANIFARIJI KWANI MAMA YANGU MZAZI NI MGONJWA KWANI ANASUMBULIWA NA KIFUA ZAIDI VICHOMI NA MGONGO KUUMA NA HIVI HAPA NINAPOTUMA SMS HII YUPO KCMC AMELAZWA HIYO NAHITAJI MSAADA WENU WA MAOMBI ILI MUNGU AWEZE KUMPONYA TENA.
  PIA HATA WAGONJWA WENGINE WALIOPO PALE PIA MUNGU AWAPONYE.
  0782 897446.
  dainess Arusha.

 47. naomba mniombee katika mitihani ninayofanya hapa chuoni kwa sasa hivi kwani ni migumu kupita kiasi, nimejitahidi kusoma kwa bidii lakini bado mitihani inazingua sana. LAKINI NAAMINI KUPITA MAOMBI YENU NITAFANIKIWA NA SITAFELI SOMO hata MOJA . KWA YESU YOTE YAWEZEKANA (MARKO 9:23) . MUNGU AWABARIKI.

 48. Tuombee amani ya nchi yetu, Bwana Yesu atuepushe na hila za adui shetani Efeso 6. 10

 49. Mpendwa GILIAD Kwanza nakupa pongezi kwa kumalizia hitaji lako maneno ya ushindi kwamba KWA YESU YOTE YANAWEZEKANA ni Kweli kabisa YOTE YAWEZEKANA KWAKE AAMINIYE;
  KWA KUWA HAKUNA NENO LISILOWEZEKANA KWA MUNGU LUKA 1:37

 50. Tuombe kwa ajili ya uchumi wa watu waliookoka kwasababu mwovu shetani anakwamisha mipango ya kiuchumi ili watu wakate tamaa na kumkosea Mungu

 51. shalom,
  wapendwa nipende kuwashukuru kwa msaada wenu wa maombi kwani kama nilivyowaambia ya kuwa mama yangu kalazwa KCMC.hivi sasa ameruhusiwa kutokana na nafuu kidogo aliyopata kwani pia bado anasumbuliwa na tatizo la vichomi,mwili nao bado unamuuma na zaidi hana amani rohoni mwake kwani anasema kila wakati anakosa amani pia anakata tamaa ya maisha kutokana na maumivu apatayo hivyo ndugu yangu naombeni mumuombee baraka tele katika kazi zake pia awe na amani pia mawazo ya kukata tamaa yamuishe.kwani anapokosa amani mimi huwa najisikia vibaya zaidi yake.
  MUNGU AWAONGOZE.

 52. DADA DAINESS MNUNULIE MAMA KITABU KIMEANDIKWA HIVI USIKATE TAMAA MUUJIZA WAKO UPO NJIANI NA KILICHOANDIKWA SIRI YA KUTUNZA MUUJIZA WAKO KWA MCHUNGAJI NTEPA ATAPONA AKISOMA TU KUKATA TAMAA KUTAKWISHA ATAPATA IMANI NI VIZURI SANA NO.0755029602 NI MCHUNGAJI MPIGIE,NA MIMI NIMEKATAA KILA HALI YA VICHOMI NA KUKOSA AMANI NIMEZIKATAA KATIKA MAOMBI, NAAMINI KUWA YESU AMETENDA.AAMINI TU MAANA YEYE HUDUMU KWA KUAMINIWA.JE AMEOKOKA?

 53. Asante sana dada Levana kwa kumuombea mama yangu Mungu akupe miaka mingi na akuongezee moyo huo huo wa kuombea wengine kwa moyo. Ameokoka japo hajakomaa bado. Ubarikiwe sana nimechukua namba ya mchungaji ili nimtafute nipate hivyo vitabu naamini vitamjenga zaidi.

 54. DADA DAINESS KAMA AMEOKOKA USIWE NA SHAKA AMEPONYWA TAYARI HIZO HALI ZINGINE ZITAKWISHA,ILA MUNUNULIE HIVYO VITABU HAKIKA UTASHANGAA AKIANZA KUVISOMA ATABADILIKA MAWAZO KABISA.NA UWE KARIBU NAE SANA NA MUNGU WA ISRAEL ATATENDA KWA AJILI YAKE.

 55. Nina rafiki yangu tulisoma pamoja Advanced level na kuhitimu 2006 anaitwa Imani. matokeo yake hayakuwa mazuri lakini anaweza kupata nafasi ya private colleges kuendelea na masomo ya Chuo. ndugu zake wengi wana uwezo lakini hakuna hata mmoja mwenye nia ya kumsaidia. Baba yake mzazi ni mfugaji na pesa anayo ya kutosha lakini hayuko tayari kumsomesha. sisi rafiki zake tupo chuoni na tunasikia vibaya kwa rafiki yetu kushindwa kusoma wakati uwezo wake kitaaluma ni mzuri. naamini yote yanawezekana kwa Bwana…..tumuombee!

 56. Pastor Bwana Yesu Asifiwe,
  Napenda kukufahamisha kuwa tayari nimesema sala hii naomba uendelee kuniombea, natamani sana niweze kumtumikia Mungu kama atakavyo ni wezesha.
  Bwana akubariki.

 57. Naomba maombi yenu nipo katika mapito na majaribu makubwa nyumba yangu nayo ipo kwenye majaribu naomba maombi yenu nipone na jaribu hili ambalo ninalo Bwana awabariki

 58. YOHANA NI VIZURI TUJUE LILE LINALOKUSUMBUA ILI TULITAJE KWENYE MAOMBI,YESU AMEKUONA, ILA TUAMBIE NINI TATIZO LAKO MAANA HATUJUI TUOMBE NINI UPONYAJI AU PESA AU KITU CHOCHOTE, SEMA TATIZO LAKO MPENDWA.

 59. Shalom Wapendwa,
  Naomba mniombee niweze kupata kazi ya kudumu kwani ni mara nyingi sana na pata kazi lakini zinakuwa ni za muda mfupi mfupi tu. na leo ndio mwisho wa hapa nilipo. Naamini Mungu ataenda kunipa mahali pengine pazuri zaidi.

 60. Mimi niliguswa na kipindi cha TUTASHIDA kilichoendeshwa na Mzee wa upako channel 10 ya tarehe 25-06-008, nikatuma msg kuahidi kuwa ningechngia laki moja mara nirudipo Dsm kwani nilikuwa nje ya Dsm kwa wakati huo,

  Leo Mungu amenijalia nimechangia laki moja na kuweka Corporate bank makao makuu ya NBC yaani leo 08-07-008

  Ninatuma msg kwenye no tuliyopatiwa siku ya kipindi ina kwenda lakini nikipiga haiende sina uhakika kama maombi yangu niliyokusudia kumweleza Mchungaji wangu kama kweli utamfikia

  No Zangu ni 0714-900128 na 0764-021229, ninaomba kuapatiwa no sahihi ili nitume shida zangu kwa mchunagi kwani huaenda nilinukuu vibaya no ya simu siku ya kipindi

  Ahsante

  Dr Kingu Said Mtemi

 61. Bwana asifiwe wapendwa katika bwana. nahitaji mshiriki nami kuniombea kwani nimepita katika mapito makubwa sana nimeteseka, nimenyanyasika, nimeonewa, nimekata tamaa nahitaji kusahau hayo yote pia na kuwasamehe wote walionitesa kwani nahitaji amani kwenye maisha yangu naomba mniombee kwajili yakupata mme mwema ambaye ni ubavu wangu asiwe bali mme wakunitesa naomba kwajili ya kufunga na vifungo vyote pia nahitaji kukua ki imani zaidi pia kupata kazi mpya na hata kufaulu kwa interview ambazo nimefanya kwa ujumla nahitaji mabadiliko makubwa katika maisha yangu kwa sasa.

 62. Bwana asifiwe wapendwa naomba mniombee kwa jili ya mamake Dalila aliepata ajali jana ya basi iliyopelekea kuvunjika kwa mbavu 2 na mkono naomba Mungu atende muujiza wake kwa ajili yake na awape faraja watoto kuwaondolea majonzi yanayomkabili hivi sasa mimi ni rafiki yake dalila nimeandika kwa niabayake kwani yuko katika kipindi kigumu sana kinachohitaji msaada wa Mungu. Mungu awabariki sana

 63. Dada Cossy,

  Mimi ninaomba pamoja nawe. Nataka tushirikiane machache wakati tunaendelea kuomba toka kwa Mungu:
  Mungu ni baba yetu na kamwe hapendi kuona sisi tunateseka. Ukosefu wa amani katika maisha yetu ya kila siku tunaoupata sisi wanadamu ni kwa sababu ya kutaka kuishi kama tunavyotaka sisi na si kama Mungu anavyotaka. Na katika hali hii huwa tumekaa mbali na ulinzi wa Mungu na kumpa nafasi shetani kututesa kwa kadri apendavyo yeye. Wakati mwingine mapokeo ya dini na madhehebu yetu vinaweza kuturuhusu kufanya mambo fulani fulani ambayo kwa Mungu si sahihi. Katika hali kama hii Mungu hunyamaza na yanapotokea matatizo huwa hataki kutusaidia kwa lengo kwamba akitusaidia katika hali hiyo tutafikiri dini na/au madhehebu yetu ndiyo vimetusaidia. Kusudi kuu la Mungu ni kutaka tufahamu kwamba msaada wetu wote uko katika yeye. Na tukilijuwa hilo tutakimbilia kwake na kuwa salama rohoni na mwilini.

  Jambo la msingi kabla Mungu hajatusaidia ni kumkimbilia yeye kwanza. Hili hufanyika kwa kumwamini na kumpokea Yesu moyoni. Imani hii ni lazima iambatane na matendo kwa kuacha maisha ya zamani na kuishi maisha mapya kutokana na mafundisho ya Bwana Yesu. Tunapokuwa ndani ya ufalme wake hapo ndiyo tunakuwa katika nafasi nzuri na kuwa na haki zote za kudai ahadi zake kwetu. Na Mungu ni mwaminifu mno. Ni yeye aliyesema kwamba hakuna mtu ambaye mtoto wake akimuomba mkate atampa jiwe au akiomba samaki atampa n’ge. Na akasema kwamba kama sisi watu tunaweza kuwapa watoto wetu vitu vilivyo vema, si zaidi kwamba yeye atawapa mema wale wamwombao (Mat 7:9-11). Kwa hiyo tukiwa ndani ya Yesu kupokea majibu ya maombi yetu ni haki yetu na Mungu anatuhakikishia kabisa kwamba yuko tayari kutupatia mema yote tumwombayo.

  Nimeyaandika haya kwa sababu unataka Mungu pia akusaidie ukuwe ki imani. Jambo la kufanya hapa ni kwamba kama umeshampokea Yesu moyoni mwako anza kutambuwa kwamba ni haki yako kupata amani, kuwa mshindi, kutokuteswa, kutokunyanyaswa na uanze kumkumbusha ahadi zake kwako. Ukiomba haya kwa Jina la Yesu yeye atatenda.

  Lakini kama bado hujampokea Yesu moyoni fanya hivyo SASA na utaona mabadiliko ya ajabu maishani mwako. Utakuja kugunduwa kwamba kumbe chanzo cha matatizo mengine ni kwa sababu tu ya kutokuwa na uongozi wa Mungu. Yesu akiingia moyoni atakuja na suluhisho sahihi la kukufanya usiteseke tena,usinyanyasike tena, usionewe tena, usikate tamaa tena na kukupa neema ya kuwasamehe wote waliokusababishia hayo. Yeye ni Mfalme wa Amani kwa hiyo amani yake itaambatana na maisha yako. Amani hii si kama amani ya dunia. Dunia imekuwa ikiwafundisha watu kwamba ‘Pesa ni sabuni ya roho’. Hii si kweli maana pesa haiwezi kuleta amani moyoni. Watu wengi wana pesa lakini pesa hiyo hiyo ndiyo imekuwa chanzo cha matatizo. Amani ya Yesu ni amani ya Moyoni! Ni amani ya kweli. Yesu pia atakuwezesha kupata mume mwema. Mume mwema ni yule anayemcha Mungu; mwenye imani kama ya kwako ambaye kwa pamoja mtashirikiana katika kuhimizana kwenye safari ya kwenda mbinguni, ambalo ndilo tarajio letu wote sisi tunaomwamini Yesu Kristo.

  ….na Mungu akubariki unapoyafanyia kazi maneno haya!

 64. BWANA YESU ASIFIWE WAPENDWA,NAOMBA MAOMBI YENU NINA MTOTO ANAVUTA BANGI VIBAYA MNO NA PIA PEPO LA ZINAA ,WANAWAKE ANAPENDA SANA .NA NINA MTOTO MMOJA TU,WAPENDWA MIMI MAMA YAKE NIMEOKOKA NINAOMBA MSAADA WENU WA MAOMBI NIMEKUWA NIKIKWAZIKA SANA KIMEKUWA KITANZI KWANGU.JINA ANAITWA CORIN NI MWANAMME NA EMAIL YANGU KWA MSAADA NI. (josephine.unda@gmx.net )KAMA KUNA USHAURI WOWOTE NISAIDIENI.NAISHI ZURICH SUISS NINAE HUKU PIA HUYO MTOTO NA AMEOA.

 65. TUMSIFU YESU KRISTO WAPENDWA. NAKUOMBENI MTUSAIDIE KATIKA MAOMBI ILI MIMI NA MKE WANGU TUWEZE KUFANIKIWA KATIKA NIA ZETU, MKE WANGU ANATAFUTA KAZI MPYA, HIVYO TUNAOMBA MAOMBI YENU KWA MUNGU ILI AWEZE KUPATA KAZI MPYA, NA MIMI NAKUOMBENI MAOMBI YENU ILI NIFANIKIWE KATIKA MASOMO YANGU. NAAMINI KATIKA MUNGU KILA JAMBO LINAWEZEKANA.

 66. WAPENDWA,TUMSIFU YESU KRISTO! KWANZA NAMSHUKURU MUNGU KUPITIA WEBSITE HII,MUNGU AZIDI KUWAPA MAANA YA MAOMBI ILI WOTE WENYE SHIDA TUWEZE KUFUNGULIWA.NAOMBA MNIOMBEE, NIKUWE KIIMANI,UPENDO KATIKA FAMILIA YANGU NA MUNGU ATENGENEZE MAHUSIANO YALIYOHALIBIKA. ANIINUE KATIKA KAZI YANGU NA ANIPE MARAFIKI WALIO WEMA. MBARIKIWE!

 67. polen na kazi ya Bwana, naomba mniombee niweze kusimama imara katika Bwana,
  niweze kufanya vizuri ktk field yangu mimi ni mwalimu nafanya field katika shule ya secondary iliyopo Tukuyu mkoa Mbeya, nahitaji Bwana anipiganie katika masomo yangu ya ualimu.

 68. Dr. Kingu Said Mtemi,

  Unaendeleaje? Ulishapata namba sahihi ya mchungaji?

  Nakutakia baraka ya Amani ya Mungu.

 69. Ndugu Josephine,

  Pole kwa makwazo yanayosababishwa na tabia ya mwanao. Ni tatizo linalowasumbuwa watu wengi. Na shida inayokuwepo ni kwamba mwenye kufanya hivyo huona kama anafaidi sana kumbe anajiangamiza. Fikra huwa zimegeuzwa na kufikiri kinyume.

  Nakutia moyo tu kwamba usichoke kuongea naye maneno ya Mungu kwa upole na unyenyekevu na tuzidi kuomba rehema za Mungu juu yake ili aweze kuiona nuru ya wokovu.

  Tuko pamoja katika hili pia!

 70. Tumsifu Yesu Kristu wapendwa….
  Mimi ni mwanafunzi nipo canada masomoni. sasa niko katika muhula wangu wa mwisho. tangu nimekuja hapa nimekuwa nikitafuta kazi bila mafanikio yoyote. sasa hivi nimebakiza muhula mmoja ambao natakiwa nifanye field yangu ili niweze kuhitimu masomo yangu na kurudi nyumbani Tanzania. Nawaomba ndugu zangu wapendwa mniombee, ili niweze kupata kazi kwenye kampuni itakayonilipa, ili niweze kufanya field yangu na wakati huo huo niweze kutengeneza nauli itakayoniwezesha kurudi nyumbani pindi nitakapo maliza shule na kuhitimu. Kwani naamini maombi yananguvu na kila aombaye kwajina la Yesu Kristu mwokozi wetu, atafanikiwa……., pi ningependa Tuwakabidhi wakristu wote katika mikono ya bwana, kwani imani ya wengi wetu inazidi kuterereka kadri siku hata masaa yanapopita….Tumsifu Yesu Kristu wapendwa.

 71. Mimi ni dada wa miaka 26, naomba mniombee ili niondokane na tatizo la kutokuwa na ajira inayoeleweka, naomba nipate kazi nipate, mume ili niwe na familia yangu, kwa pamoja wapendwa wote naomba mniombee, amina

  Tumsifu Yesu Kristo!

 72. Bwana Yesu asifiwe wapendwa,
  Well, mimi nimeokoka japo bado sijaimarika hasa kwenye maombi lakini namwamini sana Mungu. Naomba mniombee sana ili nisimame katika maombi na imani yangu iimarike zaidi. Pia nina vita kazini kwangu kwa sasa mambo hayaendi sawa na ningependa sana kupata kazi ya profession yangu maana niko nje ya mstari sasa hivi. Pray for me wapendwa.

 73. Tuko Pamoja Judy, Mimi binafsi nimemwona mungu Akifanya Mambo ya ajabu. Simama naye Yeye ni mwaminifu. Atakupa unayohitaji kwa wakati wake maana anajua lini unahitaji nini. Songa Mbele Dada!
  Steve

 74. K.Mfula, Bwana Yesu asifiwe. mimi nakuombea wewe pamoja na wote wanaotaka kukua kiiamani, ila naomba niwashirikishe neno moja ambalo ni ufunguo wa kukua kiimani. ukiijua kweli hii, pamoja na maombi, utashinda tu.
  kwanza, kukua kiimani ni process, hivyo ni kitu kitakachokuwa kinaendelea katika maisha ya kila mkristo anayejiweka vizuri na Mungu katika kumruhusu atende hilo. Biblia inasema katika warumi 10:17 ‘ faith cometh by hearing, and hearing by the word of God’. the more you study the Word, the more your faith, and your knowledge of God, grows. kwa hiyo nakutakia mafanikio mema katika safari ya kukua kiimani kupitia neno la Mungu. barikiwa!

 75. Divine, amina,Asante sana kwa maombi natumaini mungu ataniongoza napenda kusimamia Mithali 3:5 – 6. Pia katika mausiano yangu napita ktk mapito magumu sana ila najua mungu atanijibu kwa wakati wake.asante na mungu akubariki.

 76. Shalom watumishi wa Mungu aliye hai.

  Naleta kwenu ombi hili kwa ajili ya mdogo wangu aliyeko msalato sec.school yupo form six anahitaji kufaulu mitihani yake ili afanikishe ndoto zake za kuendelea na elimu ya juu.Nahisi amevunjika moyo na mambo aliyopitia au anayopitia hivyo tumuombee Mungu ampe nguvu nyingine kwa ajili ya kumalizia shule.Anaitwa Diana Audax Mulokozi.

  Asanteni na Mungu awabariki.

 77. Dada Cathy,
  Mungu wa Mbinguni na ampe ujasiri wa kujua si kwa ujanja tunafaulu bali ni kwa Roho wa Mungu. Uoga ni silaha ya Ibilisi. Tunamwombea. Aaamini tu na Mungu atafanya
  S.

 78. Bwana Yesu asifiwe!
  Naomba mniombee ili niweze kupata kazi inayoeleweka na mshahara mzuri ili niweze kuwasomesha watoto wangu, pia naomba tuwaombee watoto wangu Peace na Pamela Erick ili waweze kufanya vizuri darasani wafaulu mitihani yao yote maana mi ni mjane nina watoto wawili

  Mungu awabariki

 79. Bwana YESU apewe sifa, Mimi Magdalene ni bint mwenye umri wa miaka 25 niko Masasi mijini, nafanya kazi ktk mission moja ya hapa mjini, tuna karibu miezi 6 sasa hatujapata mishahara hapa kazini kwetu hivyo naomba niwashirikishe mniombee ili Mungu aweze kufungua milango na tuweze kupata mishahara ukizingatia mimi ni bint na naishi mwenyewe tu kwa maana ya kuwa najitegemea na nategema mshahara bila huo nashindwa kujipatia mahitaji ya kila siku. Kwa hali jinsi ilivyo sasa ni rahisi shetani kunipeleka ktk vishawishi na kuipoteza Imani yangu kitu ambacho sitaki kije kunitokea maana nampenda sana YESU wangu na ameniokoa nikiwa Bint ili nitumike mbele zake.

  naamini Mungu atajibu, nanyi hatawaacha bure kwa kutumia muda wenu kuniombea.

  Mungu awabariki sana.

 80. Wapendwa, Bwana Yesu Asifiwe!
  Nashukuru kwa maombi yenu,kwani Mungu ameanza Kutenda Maajabu! Napenda kuwashukuru sana na Mungu awabariki na aendelee kuwapa Moyo huo huo wa kuhurumia wengine, Naomba muendelee kuniombea bado niko kwenye mapito magumu, ingawa Shetani ameanza kushindwa katika hayo! Nataka Mungu atende lile ninalolitaka na si wanalolitaka wengine!

  Vile vile wapendwa naomba mniombee kwaajili ya afya ya baba yangu,
  SIFA ZOTE NAMPA BWANA! HAKIKA MUNGU ANAWEZA!

 81. Dada maggie,
  Nikutie moyo kwa kweli Mungu ni mwaminifu. Pamoja na kwamba nakutia moyo, huu ndio ukweli: Mungu ni mwaminifu. Kumbuka Ayubu aliteseka kwa kuwa Mungu alijivunia. Nakuhakikishia kuwa mwishowe, shetani akiisha kuabuika, Mungu atakuinua. Ninasema hivyo sababu nimepita na nimemwona Mungu huyu atawalae Mbingu na Nchi

  Kaza Mwendo na Mungu yupo na wewe. Japo ni maji mengi, hayatakugharikisha wala moto hautakuchoma. Kaza Mwendo dada, ni jangwa tu na ukiendelea mbele kuna nchi ya kanaani

  Steve

 82. bwana yesu asifiwe mpendwa
  naomba mnijumuishe kwenye maombi yenu katika hiki kipindi kigumu nilichonacho maana ninamatatizo kazini sana yanahusu hasa chuki binafsi ninaumia na kukerekwa sana mpaka ninaanza kutafuta kazi mahali pengine,wapendwa katika jina la yesu naomba mniombee niweze kupata kazi mahali pengine kwenye fani yangu zaidi ili niweze kumudu maisha
  katika jina la Yesu ninashukuru sana kuweza kuleta maombi yangu hapa maana naamini nitafanikiwa

 83. BWANA ASIFIWE WAPENDWA!

  Natumai wazima! Naomba mniombee wapendwa wangu, nakaribia kufanya mitihani yangu, hivyo naomba mniombee niweze kufaulu na hatimaye niweze kusonga mbele!

  ASANTENI NA MUNGU AWABARIKI NA KUWATIA NGUVU!

 84. noelahusna, Bwana Yesu asifiwe!
  nimekuombea Mungu akushindie, lakini naomba pia nikupe ushauri. kama wakristo siku zote tuko uwanja wa vita, kama sio mahala pa kazi basi ni nyumbani n.k. na dawa ya vita ni kuipigana, sio kuiepuka. ngoja nikwambie jambo, wewe kama binti wa Mungu, aliyeko ndani yako ni Mkuu kuliko anayeweka chuki ndani ya adui zako, hivyo wanaotakiwa kuhama kazi ni wao, na si wewe, unless of course unataka kuhama kazi kwa sababu ingine zaidi ya kumpisha adui yako. GOD is not a waster, He has a reason for placing you at that particular place of work, please do not leave until He takes you out of there. Niliwahi kupitia uzoefu kama wako, lakini nilisimama na ahadi ya Mungu kwenye zaburi ya 18, hasa mstari wa 16-19,31-36,43-47. isome yote kwa uelewa mzuri, kisha utasimama na lile atakalouongoza Roho wa Bwana katika hiyo zaburi. lakini amini kuwa Mungu ndiye atakayekufundisha kupigana vita, Yeye ndiye atakayekutia nguvu, atakufunika kichwa chako siku ya vita na atakutiishia wanaokuondokea. alinifanyia mimi, atakufanyia na wewe. barikiwa!

 85. Mpingeni shetani naye atawakimbia, na tazama nimewapa mamlaka ya kukanyaga nyoka na n’ge. Yesu ametupatia kila kitu tukitumie tuvae silaha zote hakika hawatatuweza zaidi sana vyeo watatuachia sisi na ushindi tutaumiliki siku zote tukizitumia vizuri silaha zetu. maana kuna mahali Yesu anaahidi kuwa mali ya wakosaji ni akiba ya wenye haki. Ndugu Noelahusna usikimbie wewe neno linasema atakimbia yeye sio wewe leo vaa silaha zote uingie vitani na Mungu wa Yakobo atakustarehesha. usimlilie Yesu yeye anashangaa kulia kwetu na wakati anataka akiona tukivipiga vita kwa silaha alizotupa, usiweke silaha zako chini Yesu anakutegemea sana sana usimwaibishe soma hapa ujue unavyotegemewa:YEREMIA 51:20 _22

 86. SHALOM WAPENDWA WOTE.
  Dada levana habari ya siku nyingi kwani kila ninapofungua website hii mimi huwa nabarikiwa sana pia inanikuza imani yangu. Pia nikushukuruni sana kwa kunitia moyo wakati mama yangu ni mgonjwa pia hata maombi yamefanya kazi kwani kwa sasa mama ni mzima na anaendelea vizuri na shunguli zake. Mungu awabarikini sana pia nawapenda sana.

 87. bwana Yesu Asifiwe wapendwa katika bwana nimara nyingine tena naomba mshiriki pamoja nami katika mahitaji yangu ili Mungu akutane na mahitaji haya

  (1) kukua kiroho na kiimani
  (2) kuitwa kuanza kazi niliyokwishaipata
  (3) kwajili ya ndoa ninayotarajia kuifunga
  (4) kuwafunga wote wanaopanga kuaribu nakule vizuizi na makwazo
  (5) kwajili ya mchumba wangu kukua kiimani zaidi
  (6) upendo , amani, uaminifu na kuwa waaminifu katika kutoa zaka dhabihu.

  Mungu awabariki sana na azidi kuwatia nguvu daima .

 88. Bwana Yesu kristo asifiwe wapendwa!!
  naomba mniombee niko kwenye kutafuta kazi na pia nina maombi mengi ambayo naamini nikishirikiana kwenye kuomba pamoja na ninyi wapendwa naenda kufunguliwa kwasababu Mungu anasema wakusanyikapo wawili au wa tatu kwa jina langu nami nitakuwa pamoja nanyi. Wapendwa naomba mniombee Mungu akafanye kitu kwenye Maisha yangu. Naaamini Mungu anaweza na anaenda kunimiminia mibaraka.
  Mungu awabariki sana wapendwa

 89. PRAISE BE THE LORD AND BLESSED BE HIS NAME. I SUBMIT MY PRAYER REQUEST BEFORE THE ALTAR OF THE MOST HIGH JEHOVAH AND TO YOU SERVANTS OF THE LORD TO PRAYER FOR MY REQUEST AS FOLLOWS. WE ASK YOU IN THE NAME OF THE LORD TO PRAY FOR:-

  1. MY DAUGHTER THUREYA WHO IS GOING TO SIT FOR THE NATIONAL BOARD EXAMINATIONS FORM IV FROM 6TH OCTOBER, 2008 ONWARDS. WE PRAY FOR HER THAT OUR LORD BLESSES HER AND GIVES HER THE COURAGE TO DO WELL AND THROUGH YOUR BLESSINGS OF THE WORKS OF YOUR HANDS MAY GOD ENLIGHTEN HER AND STAND FOR HER.

  2. TO BLESS MY SON DAUDI WHO IS IN STANDARD ONE. MAY GOD BE HIS PROTECTOR AND SAVIOUR AND MAY THE LORD BLESS HIM IN HIS STUDIES FOR HIM TO CARRY ON DOING WELL THROUGHT HIS STUDIES.

  3. PLEASE PRAY FOR ME IRENE THEIR MOTHER FOR GOOD HEALTH AND FOR ME TO UNDERSTAND GOD MORE BETTER AND FOR HE WHO DWELLS IN ME TO OPEN UP TO ME THROUGH THE HOLY SPIRIT. HOLY FATHER IN HEAVEN PLEASE HELP ME TO GET BACK MY LIFE AFTER MY ILL FATED MARRIAGE AND TO BLESS ME!

 90. Shalom.
  Napenda niwaombe mfanye maombi maalumu kwa ajili ya huduma hii.
  Kama nilivyoeleza katika baadhi ya kurasa kwamba Moriel ni neno la kiebrania lenye maana ya Mungu ni jmwalimu wangu.
  Tumedhamiria kufundisha neno la Mungu kwa ufasaha na hii imetuwezesha kufikia nchi zote unazoziona kwenye tovuti yeu http://www.moriel.org ikiwemo vatcan city ( Roma )
  Sasa kwa hapa Tanzania tumejitahidi kushiriki shughuli mbali mbali za kijamii kama kuhudumia watoto maskini na yatima, kukopesha watu wenye uhitaji kwa kuwapa mitaji midogo, tumejitahidi kuwapatia mafunzo ya ufundi vijana na yatima ambapo computer, ushonaji na masomo ya neno la Mungu hutolewa bure.
  Jambo tunalohitaji sasa ni kujenga kituo ambacho wasichana waliozaa pasipo kuwa na waume watapewa mafunzo mbali mbali ya kijamii na kiroho bila malipo yoyote samba mba na kuwatunza watoto wao kituoni.
  Tunamshukuru Mungu tumeomba kila anayejisikia kuchangi juu ya ujenzi huu utakao fanyika Moshono Arusha atusaidie.
  Tumepata majibu mazuri kutoka nchi za uingereza, Australia na hata Afrika kusini wakionyesha kushiriki kwao katika kusaidia ujenzi huu. Tumpepata Mtanzania mmoja tu ambaye naye amesema tafadhili mradimmojawapo kati ya hii tunayofanya na hata katika kujenga pia.
  Tunaomba maombi yenu kwanza Mungu atupatie watenda kazi wazuri na pili tupate fedha za kutosha ili tunapoanza kujenga kituo hicho mwisho wa mwezi huu tuweze kuamliza mapema ili mwakani vijna hao waanze.
  Pia tutakuwa na SEMINA YA WATUMISHI itakayofadhiliwa na chama cha watumishi cha Nchni UINGEREZA kijulikana cho kwa jina maarufu kama CHRISTIAN MINISTERIAL FELLOWSHIP INTERNATIONAL ( http://www.cmf-international.org ).
  Hawa ndugu wana malengo ya kusaidia watumishi wa aina mbali mbali kama vile mitume, manabii, wainjilisti, maaskofu nk, pia watatoa leseni kwa watumishi na hati za uanachama kwa wale watakao penda kujiunga kuwa mmoja kati ya wana CMFI.Semina itafanyika tarehe 15 NOVEMBA 2008 hapo VICTORIUS CHURCH SEKEI mjini Arusha….
  Hivyo wapendwa wangu wote ninawakribisha kuombea semina hiyo na kama utakuwa na maswali wasiliana na mwezenu NORBERT kwa simu namabri 0755-29 66 74.
  MUNGU AWABARIKI SANA …

 91. Hellow Magdalena. Leo unapofanya maombi anza kwa kujitakasa, toba , jutia lolote unalolijua mbalo unadhani ni tatizo na limekutenga na upendo wa Mungu. Ukimaliza fanya maombi ya kumshukuru Mungu kwa kukupa mtoto…fanya hivyo kila siku kisha utanipatia majibu muda si mrefu. Unajua mama Magdalena , watu wengi wameshindwa kupokea miujiza yao kwa sababu ya mashaka. Tendo la kupokea muujiza lina hitaji kuthubutu na kufanya mazoezi ya kuukomaza muujiza huo.

  Mfano, Petro alipoambia apite juu ya maji amfuate Yesu alihofu, ingawa alijua kuwa anayemwita ni mkuu wa maji na vyote vilivyomo baharini. Hofu iliwafanya wanafunzi wa Yesu wapige kelele kwamba Bwana tuokoe twa angamia, licha ya kwamba walijua kuwa kule chomboni walikuwa mamesafiri na Kristo Yesu..Tafadhali Magdalena, pokea mtoto kwa jina la Yesu. Mtoto huyo umlee katika maadili yanayo mpendeza Mungu.

  Ni kweli kwamba wapo watu wamekosa watoto kwa sababu Mungu anaona lengo la wao kutaka watoto ni kinyume na lengo alilokusudia Mungu kwa watoto aliotaka kuwapa…Sina maana unakusudi baya kwa mtoto utakaye mpata, ila nina maana kwamba uliwahi kunena lolote ama kwa wazi ama moyoni juu ya malezi yasitofaa ya mwanao? kama lipo ndiyo maana nilikwambia wali unahitaji toba na uyakatae hayo maneno ya awali..

  KARIBU KWA SWALI LOLOTE.

 92. Hellow dada PRISCA.
  Shalom.. Nimefurahishwa kwamba unataka maombi ya kukufanya uweze kuokoka.
  Tafadhali fuatana nami katika waraka huu kisha uokoke leo hii. Mimi niliamini sana kwamba wokovu ni mambo ya watu fulani wajinga tena maskini. Niliwaza hivi nikiwa ni maskini kama hao ninaowadhani ni maskini. Nilifikiri kwamba nikifa ni kama vile anavyokufa kuku au mnyama yeyote, hakika sikuamini kama kuna mbingu.. Zaidi ya yote nilijifurahisha kwa upuuzi mwingi, lakini mwisho wa yote nilichoona ni kwamba waliookoka wanapiga hatu kweli na zaidi ya yote hawana kesi za ajabu ajabu katikati ya jamii. Sasa jambo la muhimu kwako anza kukiri maneno ya toba kwa kusema hivi:-BWANA YESU, MIMI NI MWENYE DHAMBI, NIMEGUNDUA UDHAIFU WANGU, NAJUTA, NAKIRI KWAMBA NIMEKUTENDA DHAMBI WEWE, NA HATA JIRANI ZANGU, KWA MAWAZO NA MANENO, NA KUSHINDWA KUTIZA WAJIBU WANGU, NASIKITIKA SANA KWA AJILI YAKO YESU KRISTO, UNISAMEHE NA KUNISAFISHA KWA ROHO WAKO MTAKATIFU ILI NIWEZE KUKUTUMIKIA KATIKA UPYA WA MAISHA NA KWA UTUKUFU WA JINA LAKO AMEN.

  Mpendwa Prisca, ukimaliza nenda ukamtafute mtu akubatize baada ya kukufundisha zaidi juu ya wokovu.
  Nakusihi sana, usipoteze muda, wokovu ni muhimu sana, unadhani ukifa utakwenda wapi leo? Prisca kuna mambo makubwa mbele yanayokuja kama vile dhiki kuu n.k

  Nakuonea huruma, wewe utakuwa mgeni wa nani ? Prisca natamnai tuwe wote mbinguni…OKOKA LEO.

 93. Bwana yesu asifiwe

  napenda kuwashirikisha katika maombi kama ifuatavyo
  -tuwaombee wanafunzi wa form four
  -tuombee serikali yetu ya tanzania
  -mniombee Mungu akanifanye kichwa darasni kwa kuwa na mshukuru Mungu kwa kupata chuo. sasa nataka kufanya vizuri sana darasani ili kila mtu akakiri mwenyewe kuwa Mungu wangu ni wa kweli.
  -nikapate kazi nzuri na yenye malipo mazuri
  Mungu mwenyewe anatupa ahadi kama kwenye isaya 43;26 kuwa tukumbushane na tuhojiane eleza shida yako upate kupewa haki yako.
  -familia yangu yote pamoja na wazazi wangu
  Mungu wangu wa mbinguni awape amani ipitayo akili yote iwafunike nyote Mungu awabariki sana ndugu zangu.
  katika kristo Yesu mpatinishi na Mwokozi wetu.

 94. Bwana Yesu asifiwe wapendwa katika jina la Yesu kristo wa nazareth
  napenda kuwashukuru kwa maombi yenu napenda kuwaambia naomba mshirikiane nami katka maombi
  nimetuma maombi ya kazi UNDP naomba mniombee ili nipate hiyo nafasi kwasababu hakuna jambo linalomshinda Mungu
  mimi ninaamini kuwa hiyo nafasi Mingu ameniandalia mimi naomba tushirikiane katika maombi na hakika tutamuaibisha mwovu shetani. Mungu awabariki sana naamini kazi ile ni yangu na ipo kwa ajili yangu

  Mungu awafunike ninyi nyote
  Amen

 95. SHALOM,
  KWANZA NIWASHUKURUNI KWA MAOMBI YENU KWANI KAMA NILIVYOTUMA UJUMBE KUHUSU NYUMBA NILIYOKUWA NAKAA ILIKUWA SIO NZURI KWANI NILIHITAJI KUPATA NYINGINE ILI NIPATE NZURI KWANI
  NASHUKURUNI SANA KWA MSAADA WA BWANA NIMEPATA NYUMBA NA TAYARI NIMESHAHAMIA JAPO NAOMBENI MNIOMBEE NA HIYO ISIWE NA NGUVU ZA GIZA KAMA ILE KWANI NYUMBA NYINGI ZA KUPANGA HUWA ZINAHITAJI MAOMBI SANA.
  ZAIDI TENA WAPENDWA WANGU NAOMBENI MNIOMBEE NISISHINDWE KWA KUKOSA KODI YA NYUMBA BILI YA UMEME NA YA MAJI PIA PESA YA KULA NA MATUMIZI MANGINEYO KWANI NAAMINI PIA NA HILO LITAWEZEKANA.

  MUNGU AWABARIKINI SANAAA.

 96. BWANA ASIFIWE WAPENDWA KATIKA BWANA NAOMBA MAOMBI YENU MDOGO WANGU NDALIMA AMEPATA AJALI MBAYA SANA NA YUKO KATIKA HALI MBAYA NAOMBAMAOMBI YENU AWEZE KUPATA NAFUU MUNGU WEWE NDIO TEGEMEO LETU ASANTENI SANA

 97. MBARIKIWE NYOTE MNAOMTEGEMEA MUNGU.
  Naomba pia utambue kuwa tangu neno la Mungu lisemapo kuwa ufalme wa Mungu umo ndani yake pia ni kinyume chake kuwa ufalme wa giza upo ndani yenu endapo inaonekana kufanya kazi kati yetu hivyo tusiangalie nyumba kama eneo lenye nguvu za giza kwani nguvu za shetani ni roho iliyo na uwezo wa kuwa mahali popote [fananisha na kisa cha AYUBU WA BIBLIA NA KILE CHA NABII MIKAYA KATIKA KITABU CHA WAFALME].

  Tambua nafasi yako katika ufalme wa Mungu kuvunja nguvu za shetani[2kor10:1-3,5:7;efeso6]
  SILAHA ZA VITA VYETU ZINA NGUVU ZA KUANGUSHA NGOME NA KUANGUSHA KILA FIKRA IPATE KUMTII KRISTO NA KUPATILIZA MAASI YOTE.
  Mungu akubariki sana kwa kuwa muwazi.

 98. Bwana apewe sifa!
  Nawasalimu wapendwa wote katika jina lenye uweza na nguvu,hvi hapa naandika mail ni kwa msaada wa Mungu niko katika mapito makubwa sana ambayo kuyakabili kama mm siwezi basi wapendwa naomba mniombee ili na mimi nipate mwenza wangu toka kwa Mungu,maana nimekuwa nikiumizwa sana kuhusu swala zima la mahusiano hivi ninavoongea tayari uchumba wangu umevunjika tayari nimeshatolewa mahari na kuvishwa pete ya ndoa na harusi ilikuwa ifanyike december baada ya kugundua mchumba wangu alikuwa na kona nyingi ingawa alikuwa mwanakondoo aliyejivika ngozi ya kondoo ila namshukuru mungu maana amenitoa katika bonde la uvuli wa mauti,kwa sasa ni kwamba naumwa naomba Mungu aniponye kabisa!

  Naomba wapendwa mnisaidie katika maombi yenu na mimi nimpate yule niliyetoka katika ubavu wake!

  Asanteni sana na Mungu awabariki sana sana

  Amina

 99. Tafadhari mpendwa naomba Mungu kabla hajakupa mwenza upate mafundisho na mausia ya kutosha kuhusiana na hilo unalolihitaji kwani nashuhudiwa kuwa unafanya uchaguzi kwa kuangalia vigezo vya mwili na si vya roho ingawa ni vyema pia kuangalia hayo lakini yafuate baada ya uongozi wa Mungu ambaye ni Roho.
  Ni vyema ujue kuwa maisha yako ya ndoa hayawezi kuwa ya ushindi endapo utauangalia mwili ukuongoze.
  Mungu akubariki mpendwa dada yangu.

 100. Suala hili la mtu kupata mke au mume anayefaa kwa watu waliookoka limekuwa ni tatizo kubwa sana. Kuna maswali ambayo yamekuwa yakisumbuwa mioyoni mwa vijana wa kikristo. Swali kubwa ambalo hujirudia rudia ni NAMNA GANI KIJANA ANAWEZA KUFAHAMU KWAMBA MCHUMBA WAKE NDIYE ALIYE KATIKA MPANGO WA MUNGU? Wengi hujiuliza kwamba nitajuaje kama huyu ndiye chaguo la Mungu?….lakini mimi naamini Mungu huwa hamchagulii mtu mke au mume wake. Mtu (aliyeokoka) hubainisha vigezo vya mume au mke anayemtaka na kisha kwenda mbele za Mungu kwa maombi ili Mungu amfanikishe katika kupata mtu mwenye tabia hizo. Kwa kufafanuwa zaidi hapa ni kwamba Mungu anamfahamu kila mtu na anafahamu ni mwenzi wa namna gani anayefaa maishani mwake. Kwa hiyo Mungu akiona unampenda mtu ambaye hawezi march na wewe hapo ndipo Mungu huingilia kati kwamba mtu huyo si sahihi kwako, na ikifika hapa ndipo watu hufikiri Mungu anachagulia watu wenzi wao! Lakini kwa kweli ni kwamba Mungu huelekeza tu yule mnayeendana naye na uchaguzi ni hiari ya mtu mwenyewe. Mtu aliyeokoka na akawa anaishi maisha matakatifu mbele za Mungu huhitaji mke au mume anayeishi maisha matakatifu pia. Kwa hiyo aina ya Mke au Mume unayemuhitaji kwa Mungu lazima awe na tabia za namna waliyonayo watu walioko ndani ya Mungu. Hapa ndipo Yesu aliposema ‘Mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu ombeni lolote mtakalo nanyi mtatendewa’ (John15:7). Neno LOLOTE hapa inamaanisha LOLOTE LILILO KATIKA MAPENZI YA MUNGU maana mtu tayari yuko ndani ya Yesu kwa hiyo hawezi kuomba lolote kwa maana ya hata yale yaliyo nje ya Yesu, hapana!

  Sitaendelea sana ila WITO wangu ni kwamba kama kuna mtu mwenye MAFUNDISHO NAMNA YA KUPATA MKE AU MUME kikristo (kwa watu waliookoka) anaweza kuyaleta hapa maana naamini ni wengi ambao wanahitaji mwanga katika hatua hiyo muhimu ya Maisha.

  Mungu awe nasi sote!

 101. Wapendwa nawasalimu katika jina la Yesu nikitumaini kwa uweza mkuu nyie nyote mtakuwa wazima mkiendelea kusonga mbele,mimi kwa sasa nina tatizo nilienda hospital nikagundulika na Lowpressure,sasa imekuwa ikinisumbua kuna muda nakosa nguvu kabisa,sasa kuna ugonjwa umejitokeza kwa sasa kuna muda nasikia kuanzia kisogoni hadi mgongoni panakuwa panachemka kama panawaka moto vile hiyo hali inatokea kwa muda mchache mara inapotea, nawaomba wapendwa wangu mniombee maana hii hali sieelewi!

  Nina hakika Mungu atatenda maana nina imani maombi ya wengi yanasaidia!

  Nawapenda wote katika kristo!

 102. John Paul nakusalimu katika Jina la Yesu ni kweli naungana na wewe kuhusu swala hili jinsi ya kupata mke/mume naomba kama kuna mtu ana mafundisho atusaidie kutuandikia hapa maana hili naona limekuwa tatizo!

  Me mwenyewe binafsi linanichanganya naomba Mungu amguse mtu mwenye kujua hili atuelimishe na sisi tuelewe!

  Mungu awabariki sana

 103. Wapendwa nawasalimu katika jina la Bwana!! Naomba sana maombi yenu kwani natakiwa kwenda kwenye Interview ya shule tarehe 12.11.2008,naomba mniweke kwenye maombi ili niweze kufaulu.

  MUNGU AWABARIKI SANA.

 104. MPENDWA KARUNGI NENDA KWA WATUMISHI WA MUNGU WAKUOMBEE USIPOTEZE MUDA, YAWEZEKANA UMEVAMIWA NA ADUI.
  MUNGU AKUBARIKI

 105. mimi nina simamiya kikudi cyawatu na kinaitwa Bethisaida Ministriy of Rwanda kazi ku nikueneza injiri popote kwahiyo tunaitaji musaada wamaombi kusudi njiri ieneye popote .mutusaidi yekwama ombi

 106. Bwana asifiwe sana…Naomba mniombee niko kipindi kigumu sana chakutafuta mchumba,nahisi watu wote kama ni wema mbele ya Mungu
  naombeni sana muniombee sana na MUNGU atawajaza….Amina

 107. Wapendwa naomba mnisaidia kwa maombi yenu, kila mara ninatubu na kurudia makosa yaleyale!

 108. WAPENDWA NAWASALIMU SANA KATIKA JINA LA BWANA! WAPENDWA NAOMBA MNISAIDIE KWA MAOMBI YENU NIKO KTK KIPINDI KIGUMU SANA KWANI NINA TATIZO LA UZAZI HUU NI MWAKA WA TANO SIJAWEZA KUPATA MIMBA NA SASA NINA ZAIDI YA MIEZI 6 SIJAPATA SIKU ZANGU KABISA NA KILA NINAPOKWENDA KWENYE HOSPITAL WANASEMA UMESHAFIKA UKOMO WA KUPATA HEDHI NA VILEVILE MIRIJA YOTE MIWILI IMEZIBA KABISA KWAHIYO LABDA NIENDE NJE YA NCHI NDIO TATIZO WANAWEZA KUJARIBU WAKATI HATA MIAKA 40 SIJAFIKA. NAOMBA UNIWEKE KWENYE MAOMBI NDUGU ZANGU ILI NIWEZE KUPATA MTOTO.

 109. Shaloom, ndugu yangu nitgar, bila shaka Bwana Yesu anakupenda na anakujali sana, ndiyo maana anazidi kukupa neema ya kuliona kosa lako, na kukufanya uzidi kulitubia na kulijutia kila unapojigundua kuwa umelitenda.

  Cha kufanya mpendwa wangu nitgar, ni kwamba usijiruhusu kuwepo bila sababu katika mazingira yanayoweza kukuvuta hata ukatenda dhambi. Epukana na marafiki au makundi yanayoweza kusababishia hali hiyo. Usiruhusu mawazo kuanza kuwaza juu ya mabaya usiyoyapenda. Mawazo yakikujia, tenga muda anza kukemea kwa Jina la Yesu, bila shaka Mungu ni mwaminifu anasema hatatuacha tujaribiwe kupita tuwezavyo (1Wakorinto 10:13 Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu, atafanya mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili). Mpendwa wangu jipe moyo zidi kumwomba Mungu atakufungua kabisa katika halo.

  Lakini pia, ni muhimu kufahamu kuwa ufalme wa Mungu hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka (Mtathayo 11:12). Japo twaenenda kwa imani bado jitihada za mwili zinahitajika, tunatakiwa kuyakataa matakwa ya mwili kwa nguvu zetu zote ndipo tutashinda. Tukilegea na tukasema, kila jaribu lina mlango wake na kukaa kimya, Shetani atachukua nafasi hiyo na kutuangamiza. Hivyo, pamoja na maelekezo mazuri ya Mungu wetu, yanayosema hatatuacha tujaribiwe kupita tuwezavyo, anahitaji pia kutuona na sisi tunachukua hatua za makusudi za kukataa matakwa ya mwili, ndipo Mungu naye atatusaidia. Basi mtiini Mungu, Mpingeni shetani naye atawakimbia (Yakobo 4:7).

  Bwana akutie nguvu, mpendwa wangu nitgar katika Kristo, na tutazidi kuombeana, Amen!

 110. Wapendwa Shalom
  Napenda kuwashirikisha kunisaidia katika maombi, niko katika kipindi kigumu sana katika ndoa yangu, imekua ndoa ya misuko suko, mmuombee mume wangu ambaye shetani amemfunga na anamtesa sana mungu amfungue. Pia mtoto wangu anasumbuliwa na nguvu za giza usiku hawezi kulala kabisa nahitaji mnisaifie katika maombi haya.

  Asanteni na Mungu awabariki.

 111. Wapendwa katika bwana, bwana yesu asifiwe,

  naomba wapendwa wenzangu mnisiadie kuomba kwa Mungu mchumba wangu aliyeniacha kwa ajili ya majaribu anirudie na kufunga ndoa mimi na yeye.

  na pia naomba mnisaidie kuombea maisha yangu na hali yangu ya uchumi izidi kukua.

 112. Mungu awabariki sana ninawaomba mniombee Mungu ahusike kipekee kufanikisha mambo yangu yaliyonileta Marekani.
  Mambo yenyewe ni haya 1.kuwa Registered nurse hapa nikubalike 2.Nipasi mtihani wao 3.Nipate kibali cha kufanya kazi . ninaamini maombi hayana umbali Mungu akinijbu nitamshuhudia hili jambo limechukua muda mrefu sana ndugu zangu sijachoka kungoja ila na nyie niombeeni

 113. NATAMKA MANENEO YAKINABII JUU YA WOTE WALIOTUMA MAOMBI YAO KATIKA WEB HII ISIPITE MUDA MREFU KABLA MUNGU HAJAFANYA MUUJIZA WAKE NA KILA ASOMAE ASEME AMEN.

 114. Tukio la kweli lililotokea usiku wa tarehe 23, November, 2008:

  ”Nilikuwa chumbani nikasikia, kwa nje, watu wakibishana kuhusu jambo fulani. Nilipozingatia nilikuja kutambuwa kwamba wanabishana kuhusu ukristo na uislam. Muislam alikuwa anataka kufananuliwa inakuwaje Yesu awe ni Mungu. Yule aliyekuwa anaulizwa, huku akijibu kwa sauti ya mtu aliyelewa, alianza kwa kuelezea jinsi Mungu alivyoamuwa kujionyesha kwa wanadamu kwa sababu watu walikuwa wakitaka kumuona Mungu. Hivyo Mungu aliamuwa kuingia tumboni kwa Mariamu ili azaliwe kama wanadamu maana kwa macho ya nyama Mungu hawezi kuonekana. Ndipo akazaliwa kama Yesu. Hivyo Yesu ni Mungu Mwana na si Mungu Baba. Na akaongeza kwamba Mungu ana nafsi tatu yaani; Baba – Mungu, Mwana – Yesu na Roho Mtakatifu. Hivyo Yesu ni Mungu mwana na si Mungu Baba. Walipofika hapo yule aliyekuwa upande wa uislam alionyesha kuelewa na yale maelezo.. .

  Yule aliyekuwa upande wa uislamu akauliza inakuwaje wengine wanasema Yesu ni Mungu, yule jamaa akasema hayo ni mambo ya walokole, na wala yeye si mlokole kwa hiyo swali halimhusu. Mazungumzo yalipofika hapo wote wakawa upande mmoja wakiwashangaa walokole kudai wameokoka. Yule aliyekuwa akielezea Mungu (kumbuka alikuwa amelewa) akasema mtu huwezi kusema umeokoka wakati uko hai. Kuokoka ni baada ya kufa. Walikubaliana kwa pamoja na mazungumzo ya Mungu yakawa yameishia hapo kisha wakaendelea na story za kawaida. .

  Walipoendelea na mazungumzo nilitamani kuwaona kwa karibu, ili kama nitapata jinsi, niweze kuendelea kuongea nao kuhusu ajenda waliyokuwa wameshaiacha. Nilitoka, nikazunguka nje ya uzio, kuelekea upande zilipokuwa zikitokea sauti, lakini bahati mbaya sikuwakuta.”

  Kutokana na maelezo hapo juu, ndugu yangu unayemwamini na kumfuata Yesu utakuwa umeelewa jinsi tatizo lilivyo kubwa. Watu wengi wanajiita ni wakristo kwa sababu tu ana jina la kikristo, au huwa anakwenda kanisani jumapili nk. Tatizo lenyewe ni kwamba watu wasiomwamini Yesu hawajuwi tofauti iliyoko kati ya Mkristo anayemwamini na kumfuata Yesu na Mkristo wa jina tu. Kwao mkristo ni mtu yeyote ambaye kwa maana moja au nyingine hutumia Biblia. Nimeona ni vema niliweke jambo hili ili tutafakari kwa pamoja jinsi hali ilivyo na kisha tumuombe Mungu.

  Mambo ya kuombea:
  1. Tuombe Mungu awasaidie viongozi wa dini ili wawafundishe watu kuwa WAKRISTO ambao ni wafuasi wa Yesu na si wakristo wanaofuata madhehebu yao.
  2. Watu wengi wasiomwamini Yesu wanapotoshwa na wengi ambao wanajiita Wakristo huku wakiwa hawamfuati Kristo mwenyewe. Tuombe Mungu, tena, apeleke watendakazi wa kweli watakao wasaidia watu wasiomjuwa Yesu ili wamwamini na kumpokea.
  3. Pia omba kwa lolote kadri utakavyoongozwa kuhusu suala hili.

  Amina!

 115. +1 John!

  LDS ni dini nyingine iliyojificha nyuma ya Jina ukristo kama walivyo wajiitao mashahidi wa Yehova na wengineo. Ni muhimu mpendwa kama una uchungu na roho hizi zinazoangamia kila siku, Omba kwa Bidii! Na si uombe tu, bali uwe na upendo kiasi cha kuwashuhudia injili.

  Je umewahi kuwashuhudia watu wangapi kazini, nyumbani, shuleni n.k? Je unawapenda kweli? Mbona huwaonyi juu ya hukumu inayokuja wasipotubu?

  TUOMBE WAKRISTO TUWE NA UJASIRI WA KUSHUHUDIA WENGINE
  Mbarikiwe!

 116. BWANA YESU ASIFIWE WAPENDWA. ZAIDI NINAOMBENI MNIOMBEE NIWEZE KUPATA MUME MWEMA KWANI NIKO KATIKA KIPINDI CHA UHITAJI PIA NINAOMBA MUNGU AWEZE KUTIMIZA HAJA YA MOYO WANGU.

  MUNGU AWAZIDISHIE BARAKA TELE.

 117. Bwana Yesu asifiwe,
  Wapendwa naomba mniombee nilipokua bint niliamini kwamba Mungu atanipa mume mwema na saasa nimeshafikia umri wakuhitaji mume na nimesubiri sana nabado naendelea kusubiri kwa kufunganakuomba naomba msaada wenu kwani naamini kwa nguvu zangu mwenyewe sito weza.

  Jambo la pili naomba mnikumbuke kwa maombi ili nipate kazi nyingine kwani kazi ninayofanya sasa hailipi kwa kipato kwamaana nina familia yaniwazazi wangu nyumabani wananitegemea silalamiki najua huu ni mzigo wangu na Mungu naamini ananipigania sana hivyo sitochoka kumuomba nimejaribu kutuma maombi ya kazi kwenye maofisi mengine tofauti lakini sijafanikiwa huu ni mwaka wa 2 nahangaika kutafuta kazi nyingine sipati napata mawazo sana naumia moyoni kuona mzigo niliyonao na kiasi cvha mshahara ninaopata havilingani.

  MWENYEZI MUNGU AWABARIKI SANA NA AWAWEZESHE KTK KILA JAMBO.

 118. shalom
  wapendwa mimi naomba maombi yenu nimekua nikipitia wakati mgumu sana maishani mwangu,na sasa hivi nimekua nikitafuta kazi bila mafanikio
  naomba maombi yenu wapendwa ili Mungu aweze kufungua milango ya kazi

  MUNGU AWABARIKI SANA

 119. Bwana asifiwe wapendwa,Naomba mnikumbuke katika maombi yenu wakati nami naomba Mungu ,kwa ajili ya mchumba wangu amlinde na vishawishi na kutokueleweka na mwishowe tukafunge ile ndoa takatifu kama ipasavyo.Vile vile naomba mnikumbuke kwenye maombi kwa ajili ya mitihani yangu ambayo yaja wiki ijayo.ninapigana nahuzuni moyoni mwamngu tafadhali nisaidie mistari y kusoma kwenye biblia kwa ajili ya faraja .Mbarikiwe sana na bwana

 120. Wapendwa mnaoomba wake/waume
  Ningependa kuchangia jambo ambalo nimeliona kama kikwazo kwa watu wengi kupata wake/waume ambao Mungu anataka wapate (sijui kuhusu ninyi haya ni maono yaku kutokana na ninayoona kila siku).

  Kwanza mpendwa, fahamu Mungu anataka akupe mtu ambaye atakusaidia kufika mbinguni nawe pia viyo hivyo. Pia Mungu anataka akupe mtu ambaye utajenga nae familia bora ya kimungu kabisa. Sasa basi, watu wengi hasa akina dada wamesahau namna ya Mapambo ya wana wa Mungu. Wameacha kujipamba kwa tabia za kimungu bali wameng’ang’ania namna ya kutafuta wenza ya dunia hii. Wanataka watafute waume na pamba nyepesi, push pedal, gold chains, kubabua nywele,…..nk.

  Zamani watu hata wanne mtaani watagongana kwa mlokole mmoja, ambaye watu wa dunia hii walimwita mshamba, wakitaka kufunga uchumba! Sasa mliangalie sana hili. Kitabu cha esther, Ruthu, na wakina mama wengine watakatifu wa Biblia na wawe nembo yenu kama ilivyo kwa Yusufu, Isaka, na wababa wengine watakatifu. Sisi hao ndio watu tupaswao kujifunza toka kwao na si wakina Jayz, Bang magazine, Beyonce, Madonna , Levy’s, Rocawear na wengineo.

  Kwa nini hili ni muhimu? Ukijiweka katika hali hiyo, watakuja wanaume wapitaji, na wenye lengo la kupata Mke/Mme watakuweka pembeni (Hata ktk kundi la wapendwa kuna Mbwa mwitu eti! ). Hakikisha unajitunza mwili wako wa asili badala ya kujifanya mzungu ilhali ngozi yako ni mwafrika, au kuchoma nywele ili uwe kama Muhindi wa amerika ilhali ni mwafrika au kuficha nywele zako za asili ili wigi ionekane. Hiyo ni namna ya dunia hii. Badala yake tengeneza nywele zako za asili ziwe smart, na uipendezeshe ngozi hiyo hiyo, ilhali ukijipamba kwa utauwa. Kuwa smart hata katika rafiki ulio nao, weka misimamo yako wazi kabisa kila mtu ajue.

  Mwisho, kwako la muhimu ni Yesu! Kipimo cha mwanamume yeyote ajaye, ni lazima Baba yako (Yesu) apitishe. Mpime bila yeye kujua unampima, juu ya upendo wake kwa Yesu. Kama anampenda Yesu, atamtii kwa gharama yeyote, ikiwapo kumpenda mme/mke wake unconditionally!

  Mungu Baba yetu, awape haja za moyo wenu sawasawa na mipango yake juu ya maisha yenu!
  Amina

 121. BWANA ASIFIWE WAPENDWA,

  NI SAWA KAKA STEVE NA UNAYOYASEMA ILA SIDHANI KAMA KUNA MWANACHAMA AMBAYE ANATUMA MAOMBI YAKE HAPA PASIPO KUJIJUA ANAHITAJI NINI, MAANA KWENYE HILI SWALA LA MTU KUHITAJI MKE AU MUME NI WENGI WANAHITAJI ILA KUNA BAADHI YAO WANAHOFU FULANI KWANZA WANAONA KAMA WAKITUMA MAOMBI YA KUTAKA MUME/MKE WANAWEZA KUONEKANA TOFAUTI.

  ILA MIMI BINAFSI YANGU HILO SUALA LIMEKUWA LIKINISUMBUA NA NDIO MAANA NIKAONA KUPITIA WEB HII KWANI NIMESHATUMA MAOMBI MARA NYINGI KWANI SIKUACHA KUJIBIWA HATA MOJA NA HATA SASA NDIO NIMETUMA HILI LA KUHITAJI MUME MWEMA NA KWA KUAMINI KUWA NITAKAYEMPATA ATAKUWA KAKAMILIKA KWANI MUNGU NI MKAMILIFU NA ATAMKAMILISHA ZAIDI.

  UBARIKIWE STEVE KWA KUTUELEWESHA ZAIDI.

 122. Oooh Sorry dada kama nimekukwaza, lakini mimi nilichoongelea ni general observation na kama nilivyosema hapo juu, sikuwa nawalenga ninyi, bali angalizo.

  Naamini nimeeleweka, tuendelee kuombeana

 123. shalom steve,
  hujanikwaza kabisa mpendwa ila sisi sote tunapaswa kueleweshana ndugu yangu, mimi nimependa ulivyomaanisha, kuwa na amani kabisa na pia tuzidi kueleweshana bila woga.

  barikiwa

 124. Wapendwa tuombee kwa ajili ya wale wanaongàngània dini,ili waweze kuokolewa,maana wameshikilia mapokeo ya wazee wao,Tuombe ili waijue kweli waokolewe maana nimepambana na wengi ukijaribu kumugusa utasikia dini zote ni sawa lakini je umeokoka anasema sisi hatuamini wokovu ila yesu tunamuamini.Wapendwa tuwaweke katika maombi mahala popote pale walipo hawa kondoo waisikie sauti ya Mwana wa Adamu ikiongea nao kupitia maombi yetu tuombe waijue kweli .Asante YESU.

 125. Naungana nawe dada Levana katika kusisitiza ombi uliloliweka hapa. Dini ndiyo kikwazo kikubwa sana kitakachowakosesha watu wengi kuingia mbinguni. Yesu hakuleta dini bali alileta wokovu. Dini zilikuwepo hata kabla ya Yesu kuja. Kumwamini Yesu bila kuamini wokovu maana yake ni Kutokumwamini. Yesu ni wokovu!

  Ee Mungu, usikie kuomba kwetu na kilio chetu kikufikie!

 126. Ameeeeeeeeeeeeeeeeeni kaka John Poul ! mungu wetu waguse hao nao ni watu wako walioshikilia dini.

 127. BWANA YESU ASIFIWE ILE TAREHE NDUGU ZANGU IMEFIKA YA KUFANYA MTIHANI NI 29.12.08 NINAOMBA MNIINUE MBELE ZA BABA YETU ALIYE MBINGUNI AHUSIKE KIPEKEE NIWEZE KUFAULU NIWE KICHWA AMEN

 128. Hey Mary, here is you massage Joel 2:26-27
  hakika Mungu akiwa upande wako hakuna awezaye kusimama
  Mungu akutiye nguvu

 129. bwana yesu asifiwe naitwa charles naomba mniombee na mitihani natakiwa kufanya pia natafuta kazi kuna sehem nimeshaomba ndo nasubiri nahitaji sana sala zenu mbarikiwe sana.

 130. Bwana Yesu asifiwe!
  Wapendwa naomba mniombee sana kwa Mungu azidi kunishika kwa mkono wake hodari maana hiko katika jaribu kubwa sana ila nina hakika Mungu ataniwezesha!
  Asanteni sana na Mungu azidi kuwatumia kwa ajili ya utukufu wa Jina lake!

 131. wapendwa naomba mniombee kwa mungu kwani mwaka uliopita nilikuwa na matatizo makubwa sana

 132. Bwana Yesu asifiwe wapendwa katika Bwana,mimi ombi langu wapendwa naomba mnisaidie kwa maombi yenu,kwani nafanya kazi kwenye ofisi ambayo niliyeokoka ni mimi tu,hivyo nakumbana na upunzani mkubwa hapa ofsini ninapofanya kazi.Mimi nazidi kuomba Mungu ili watu wengi hapa ofisini wampokee Bwana Yesu,lakini Bwana Yesu alisema mkiomba lolote mkiwa mmepatana kwa jina langu hilo limekuwa lenu,ndio maana nawashirikisha wapendwa katika hili…Bwana Yesu asifiwe

 133. Bawa Yesu asifiwe,nakutia moyo ndugu Upendo Ombatia katika haja za moyo wako ulizoomba,Bwana Yesu ni mume wa wajane na tena ni Baba wa yatima …..hivyo hayo yote uliyoomba umekwisha pokea katika jina la Yesu,wewe amini tu,na katika maombi yako mkumbushe Yesu kwamba yeye ni mume wa wajane na tena ni baba wa yatima utaona majibu yake.Bwana Yesu asifiwe

 134. Bwana Yesu asifiwe wapendwa,nukushukuru sana ndugu yangu Bernard Mwenda katika Bwana,maana umenitia moyo na kuniombea na sasa hakika naona mabadiliko katika maisha yangu ya uokovu,sasa nimeweza kusimama kwelikweli katika safari yangu ya kwenda mbinguni.na ninahisi nguvu ya Mungu ndani yangu kadiri siku zinavyokwenda,nazidi kumuomba Bwana Yesu aniongezee nguvu ya kusimama, na wewe ndugu yangu usiniache katika maombi yako,maana umenitia moyo sana…..Bwana Yesu akuzidishie…maana naamini mimi ni tunda ulilozaa kwa maombi yako…..Amen……

 135. BWANA YESU ASIFIWE!
  WAPENDWA NINA WASALIMU KATIKA JIN LA BWAN WETU YESU KRISTO ALIYE HAI. NAWATAKIA HERI YA MWAKA MPYA WOTE.
  JAMANI TUWAOMBEENI MA ALBINO WANAPATA SHIDA, PIA WANAFUNZI WOTE KUANZIA PRIMARY MPAKA VYUONI! MIMI PIA NINA OMBI LANGU BINAFSI MWAKA HUU NATARAJIA KUFUNGA NDOA NAOMBA MAOMBI YENU WAPENDWA KUSIWE NA KIKWAZO CHOCHOTE, PIA NIMETUMA MAOMBI YA KAZI SERIKALINI NAOMBA MNIOMBEE NIKAPATE KIBALI MAANA HIZO KAZI NI ZANGU NINA IMANI HIYO. MUNGU AWABARIKI NA AWATIE NGUVU NAWAPENDA WOTE.

 136. wapendwa bwana yesu asifiwe,
  Mimi ni msichana wa 30yrs ,ninaomba mniombee kwa Mungu ili amponye Kaka yangu na mapepo wachafu ambao wamemuacha na ukichaa usiopona (kwakweli nimehangaika sana na niko pekee sina wazazi) Pili naomba mniombee kwa Mungu amponye Mdogo wangu mpendwa Yatima huyu Ukimwi na ili aendelee na shule.
  Bwana awabarikini wote,Amen
  Philo

 137. nitakuombea sana na mimi niombee sana ninatatizo la uzazi katika ndoa yangu namwomba Mungu anifungue tumbo langu kama alivyofungua kizazi cha mjakazi wake Hana akamzaa Samwel, niombee!

 138. tumsifu Yesu Kristu na Bwana asifiwe, wapendwa naomba mniombee juu ya ndoa yangu inayoelekea kuvunjika, yote yawe kwa mapenzi ya Mungu. ina miaka kumi na moja, watoto 2 , ila pamoja na kuokoka kasheshe na manung’uniko toka kwa mke hayaishi, kila ninalojitahidi kwake ni kero, asante na Mungu awabariki.

 139. bwana yesu asifiwe.wapendwa katika bwana naomba mniombee juu ya dada zangu waweze pata watoto .na pia mie niweze fanikiwa katika kupata kibali.

 140. Shalomu!

  Naomba kupata maelezo kidogo kutoka kwa ndugu Mark-Mirack kama ataweza kuyatoa ili tuone kama tunaweza kushauri pamoja na kumuombea.

  1: Naomba kujua kama mke wako naye ameokoka?

  2: Mmeokoka lini?

  3: Je mmefanikiwa kuwashirikisha viongozi wenu wa kiroho?

  4: Najua si vema sana kutoa maelezo mengi juu ya ndoa kwenye blogu, lakini kama inawezekana basi jaribu kufafanua chanzo cha tatizo ni nini na ni nani anayetaka kumuacha mwenzake, wewe au mkeo?

  Mungu awabariki

  Shalomu

 141. SHAAAALOOOOOOOM Watu wa JEHOVA.
  Mungu ni wakushukuriwa na kila ulimi,najua hili halina mjadala kwa mtu yeyote anaesoma ujumbe huu kwani ni wazi kuwa hata kuvuka mwaka ilikuwa ni kwa MAPENZI yake na ULINZI ulio mkuu.

  Pili: Ndugu zangu hongereni sana kwa maombi,mijadala na mengine mengi mnayofanya. nilipotea kwa muda kidogo kutokana na kwamba niko kijijini kwa hiyo ikawa ngumu kidogo kupata mawasiliano na wapendwa wa strict Gospel, ukweli niliwamisi saaaaaana sana. Na sasa namshukuru JEHOVA kwa nafasi hii ya kipekee kwakweli.

  Tatu: Ndugu MARK-MIRACK.Kwanza pole sana kwa tatizo kubwa lililokuwa linaisumbua ndoa yako. Nimeamua kutumia wakati uliopita kwani kwa sasa halipo tena najua waombaji wote watasema AMINA.
  Kaka MARK Ili uweze kuona namna ambavyo MUNGU anaipenda ndoa yako na ukitaka kuamini maneno ninayokuambia yakuwa ndoa yako haitavunjika fanya yafuatayo halafu baada ya siku 3 najua utatuletea ushuhuda ktk blog hii.

  KWANZA: KIRI KWA KINYWA CHAKO MBELE ZA MUNGU YA KUWA MUNGU AMEKUPA MKE MWEMA, NA YAKUWA NDOA YAKO HAITAVUNJIKA KAMWE.

  PILI: ELEWA KUWA HAUGOMBANI NA MKEO BALI UNAGOMBANA NA SHETANI ANAYEIWINDA NDOA YAKO, NAKUAMBIA HAKIKA MKEO HANA SHIDA TENA KATI YA WATU AMBAO MUNGU AMEWAPA WAKE WAZURI NA WENYE ADABU NI WEWE MARK. SHIDA KUBWA WEWE BADALA YA KUGOMBANA NA IBILISI UNAGOMBANA NA MKEO. ANZA LEO KUGOMBANA NA SHETANI KWAKUTUMIA UPANGA WA NENO HALAFU BAADA YA SIKU TATU UTANIAMBIA MAAJABU UTAKAYO YAONA

  TATU: KATIKA WARUMI 8:31 Anasema “tuseme nini basi kama Mungu akiwa upande wetu ni nani aliye juu yetu?” HATA SIKU MOJA MUNGU HAWEZI KUMUACHA MJA WAKE ILA MJA WAKE NDIYE AMUACHAE MUNGU kama anavyosema ktk Isaya 59:1-2 kuwa SIKIO LA MUNGU KUSIKIA KILIO CHA MARK SI ZITO WALA MKONO WA MUNGU KUIGUSA NDOA YA MARK SIO MFUPI HATA USHINDWE KUIPONYA ILA………………………………………………hapo nimeacha ili upite mwenyewe kwenye maandiko. Kaka Mark nakuhakikishia aishivyo MUNGU wa mbinguni NDOA YAKO HAITAVUNJIKA NA KILA ASOMAE ASEME AAAAAAAAMEN.

  NNE; Kaka mark yote hayo niliyokueleza yatafanikiwa ikiwa tuu utakuwa siriazi na kutafuta msaada kwa MUNGU.
  SASA MARK NIKUPE SIRI: TENGA MUDA KABISA WAKUMLILIA MUNGU KWAAJILI YA NDOA YAKO NAKUAMBIA HAKUNA NAMNA AMBAVYO MUNGU HATAKUHESHIMU. TENA ATAIPONYA NDOA YAKO NAKUKUAMBIENI KWAMBA ANAWAHITAJI MUMTUMIKIE YEYE. Amin amin nawaambieni Ndoa yenu haina shida ila MUNGU ana shida na huduma alizoweka ndani yenu

  MWISHO kaka mark SOMA WAEBRANIA 12:1-3 Tambua MUNGU ANAHITAJI HUDUMA ALIYOIWEKA NDANI YENU.

  MIMI SINA MENGI NAWATIKIA BARAKA ZA MWENYE ENZI MUNGU AMBAE JINA LAKE NI JEHOVA.

  I LOVE YOU ALL.

  SAYS BARAKA MORI
  (A LITTLE CHIEF)

 142. Wapendwa, Mungu ni mwema sana kwetu. Mimi nimeolewa tangu mwaka 2003, sijajaliwa kupata mtoto.Nilifanyiwa upasuaji mwaka 2007 kuondoa uvimbe tumboni, ndipo daktari wangu akaniambia kuwa sitakuwa na uwezo wa kupata watoto tena kwa kuwa uvimbe uliathiri kizazi…naomba sana maombi yenu wapedwa wangu. Asanteni sana!

 143. Dada yangu mpenzi hakuna la kumshinda Mungu, Sahau hiyo kauli ya doctor na uweke neno la mungu badala ya hiyo kauli ya daktari ya kukatisha tamaa ,kuna neno ambalo halikatishi tamaa ni neno litokalo kinywani mwa Mungu na ukumbuke neno la Mungu usikumbuke kauli ya doctor, kumbuka neno la Mungu lisemalo kuwa Hakuna lisilowezekana kwa Mungu.nakutakia matokeo mema baada ya kufuta mawazoni mwako kauli ya doctor na kuamini kuwa hakuna lisilowezekana kwa Mungu.kwa Yesu hakuna gumu wala lisilowezekana ,ninamuomba Yesu akutendee sawa sawa na ahadi yake.

 144. Dada Evelyn Mungu wetu anaweza yote yote yote kabisa ana uwezo wa kufinyanga kizazi kipya nakuomba ulielewe hilo ripoti yako ya mwisho anayo yeye wewe jinyenyekekeshe tu chini mkono wake hodari yeye ni mwema na mkweli na mwamifu anaangalia neno lake na kulitimiza wewe anakujua vema kuliko hata unavyojijua wewe Bwana Yesu akutie moyo Amen

 145. Bwana Yesu Asifiwe,
  Wapendwa ninaomba mniombee Mume wangu aweze kupatana na Baba yangu mzazi, hawaongei wana mwaka sasa. Ni maombi yangu wawe wanaishi kwa umoja na kupatana na kuongea kama wengine walio katika Bwana. Vile vile muwaombee waokoke hawajampokea Yesu bado. Neno la Mungu linasema kuomba kwa mwenye haki kwafaa sana hasa akiomba kwa bidii. Naamini maombi yenu ndio yatakayowafungua. Mungu awabariki sana.

  Amen.

 146. Bwana Yesu Asifiwe
  Naomba mniombee nipate mchumba mwema, maana umri wangu ni mkubwa , Natamani sana kuwa na familia kama wenzangu . Maombi yenu naamini Mungu atayapokea
  Amen

 147. Bwana yesu asifiwe, naomba maombi nipate mume niolewe nina umri mkubwa sasa napenda kuitwa mama siwezi kuzaa nje ya ndoa nimeokoka japo kuna watumishi wananiambia siwezi kuolewa kwani nina pepo dume na laana za ukoo saa nyingine naona nakuwa depressed na saa nyingine naona nayumba kiimani. Mungu awabariki!

 148. Dada dear,Witness na wengine wote wanaohitaji wachumba kwa MUNGU. nina neno kwa ajili yenu.

  -Nawasihi mwingie ktk maombi ya kuomba rehema na msamaha kwa MUNGU kabla ya kuomba mchumba kwani yeye anawajua fika kuliko mtu mwingine yeyote. Kwanini nasema hivyo ni kwasababu inawezekana umemlalamikia sana MUNGU kuhusu swala hilo na kumlalamikia MUNGU siyo jambo la baraka. Lakini pia inawezekana hukulalamika ila umewahi kushiriki ktk dhambi ya
  UZINZI,UASHERATI,UTOAJI MIMBA NA MAMBO MENGINE yafananayo na hayo. kwahiyo kama ikiwa ni hivyo n vigumu MUNGU kutusikiliza maombi yetu huku ibilisi akitushitaki mara kwa mara mbele zake.

  PILI: Kama umeomba swala hilo kwa muda mrefu na bado hujafanikiwa nakushauri onana na wapakwa mafuta wa MUNGU ufanyiwe maombi ya ukombozi.

  Hii ni kwasababu yawezekana wewe hauhusiki na mambo hayo matatu niliyoyataja hapo juu lakini ukawa unarithi kwa mtu mwingine mwenye shida ya namna hiyo ktk ukoo au familia yenu.
  Nakuhakikishia ukiyafanya hayo lazima MUNGU atafanya kitu kwako.
  Kama uko mkoa wa Kilimanjaro au Arusha na unahitaji huduma ya jinsi hii naomba tuwasiliane. SOMENI ISAYA 41:10

  MUNGU AWABARIKI WOTE, AMEN

 149. asante kaka baraka naomba tuwasiliane katika mail yangu ni [anuani ya email imepelekwa kwa ndugu Baraka na Strictly Gospel]. Tutaongea mengi kaka Baraka Mungu akubariki sana.
  kizuguto

 150. Bwana Yesu Asifiwe.

  Wapendwa wote na wasalimu katika Jina la Bwana Yesu!

  Naomba mniombe kwa Mungu anisaidie Matatizo yangu yote niliyonayo sasa hivi.
  Asimamie watoto wangu.
  Ulinzi katika Kazi yangu.
  Mwili wangu.
  Mapato yangu.
  Nipate Mwanaume Mwingine Mzuri Sanaaaaaaaa.
  Asanteni

 151. Mimi ni msichana nimefanya kazi kwa muda wa miaka mitatu lakini sijaona mafanikio ya aina yoyote na kwamba hata huyo mama ananilipa mshahara mdogo sana kiasi kwa hata nauli na chakula inazidi mshahara ninaopokea kila mara anasema ataniongezea lakini wala haniongezei sasa mimi niimeamua kutafuta kazi kwingine ili niepukane na hayo matatizo yote
  ndiyo naomba sasa mnisaidie katika maombi niweze kupata kazi ya kudumu na nzuri
  nahitaji sana ushirkiano wenu

 152. BWANA YESU ASIFIWE WAPENDWA,

  YAANI HILI SWALA LA KULIPWA MSHARA MDOGO HATA MIMI NINA HILO TATIZO WAPEDWA KWANI HATA UKIMWELEZA BOSS ANKUAMBIA TU TUTAPANGA .
  YAANI SASA HUU NI MWAKA WA TU NAINGIA BILA YA NYONGEZA YA MSHAHARA, NA HATA SASA NIKO KAZINI TANGIA DESEMBA SIJAPUMZIKA KWANI MWENZANGU ALISAFIRI KWA MDA MREFU NA KAZI YENYEWE NI YA KUINGIA ASUBUHI NA KUTOKA USIKU(3).

  WAPENDWA NISAIDIENI KWA MAOMBI KWANI NAKATA TAMAA YA KUFANYA KAZI KABISA KWANI HII INANIKWAZA MAANA JUZI NIMEMUOMBA ANIONGEZE MSHAHARA HATA HIZI SIKU NILIKUWA KAZINI MWENYEWE ANANIAMBIA TUTAPANGA NA MIMI NINA SHIDA YA PESA NA NINADAIWA KODI YA NYUMBA NASHINDWA NIFANYEJE KWANI PIA HATAKI HATA USIKILIZE NYIMBO ZA DINI KAZINI NA HATA SIMU IKIITA WIMBO WA DINI NI TAABU KWANI YEYE NI MWISLAMU NA NI MSOMALI.

  NAOMBENI MAOMBI YENU KWANI NAHITAJI AMANI,KUHESHIMIWA NIWAPO KAZINI NA HATA KUPATA HATUA NYINGINE ZAIDI,
  KWA KWELI NAAMINI KWA MAOMBI YENU MUNGU ATANIONEKANIA .

  MUNGU AWAINUE ZAIDI.

 153. Asifiwe Mfalme Yesu!
  Nimekuwa nikipitia maombi mengi ya wapendwa na ninona niwashirikishe japo sehemu public kama hii si mahali pake. Nimekuwa nikipima mienendo yetu wakristo, na nina ujasiri wa kusema tumeacha misingi yetu. Upendo wa udugu haupo tena. Ni kweli tunatiana moyo na kuombeana, lakini hatusaidiani! Hii imeniumiza kwa muda mrefu mno. Tunahitaji kuinuana, na kusaidiana. Waraka wa Yakobo uko wazi, na model ya Kanisa (Matendo ya Mitume) iko wazi.

  Mbarikiwe na Yesu

 154. Wapendwa naomba mniombee nimekosa amani moyoni mwangu nimekuwa na mawazo makali sana juu ya maisha yangu nakosa hata usingizi, Maana kuna baadhi ya vitu nimevikosa, naomba saLa zenu niweze kuvipata
  Amen

 155. Mungu ni Roho na wote wamwabuduo imewapasa kumwabudu katika roho na kweli. Pia napenda nieleweke kwamba katika maisha yangu ya wokovu nimegundua kuwa ndani ya wokovu, kuwa michanganyo hivyo kila mtu asimame kwa zamu yake na wala asimtegemee mtu, wachawi na wazinzi na aina mbalimbali za nguvu za giza zimelitawala kanisa.

  Kwa upande mwingine ajali mbalimbali zinazotokea mahali mahali si mpango wa MUNGU mbali ni kazi za shetani, hivyo kanisa linatakiwa kusimama na pia ninashauri maombi yafanyike maeneo yenye ajali kama vile daraja la mto nduruma na mengineyo.

 156. Bwana yesu apewe sifa. Mimi Ombi langu kuu ni hili naomba mungu anipatie kazi nzuri inayoendana na nilichosomea na iwe ya kudumu na iwe sehemu yenye amani. Asante Baba kwa maana unajibu maombi.

 157. Bwana Yesu apewe Sifa! Wapendwa naomba mniombee nipate Mume ambaye Mungu ameniandalia maana najiona niko mpweke sana. Mungu awabariki

 158. Katika yote na kwa sala zenu zote, ombeni ili mapenzi yake yatimizwe.
  Iwei watu wa subira naye kwa uweza wake, kwa mapenzi yake atatuwezesha.
  Kwani yote ni kwa neema. Mungu awatie Nguvu sana na mbarikiwe naye.

  Algeria.

 159. Bwana Yesu asifiwe sana,
  Mimi niko katika kipindi kigumu sana, nahitaji maombi yangu yalenge kwenye kumjua na kusimama imara na kiimani katika kumtegemea Mungu wangu pekee.
  Mbarikiwe sana na bwana kwa maombi yenu
  Milley

 160. Na yule umwaminiye ni mwenye nguvu fika. Historia yaonyesha kwamba ameweza an anazidi kutenda maajabu. Basi na tuamini yale asemayo Bwana. Nguzo zetu zisimikwe katika imani kwa Bwana, mapendo kwa viumbe wake na matumaini kuwa yeye huokoa. Na mapenzi yake ni ilituishi, tuwe watu wenye furaha tukimtumikia Mungu.

  Nami japo mbali nawe, nakuombea naye Bwana atakubariki. Nipo ndani ya kisiwa cha uislamlakini Bwana ananiwezesha.
  Mbarikiwe nyote katika Bwana.
  Bonaventura B. Mwenda (Algeria): mwendabm@yahoo.com

 161. NAWAOMBA SANA KWA JINA LA YESU KRISTU WA NAZARETH MNIOMBEE KWANI MWAKA HUU UCHUMI WANGU UMEPOROMOKA NINASOMESHA WATOTO WATATU NA NATUMIA FEDHA NYINGI KWA MAHITAJI YAO MUNGU AWABARIKI SANA

  GERALD MWANZA

 162. Naomba mnisaidie kumuombea mama yangu Angela ambaye kwa muda mrefu anakohoa sana. Pamoja na jitihanda zote za vipimo aina mbalimbali tumeshindwa kumsaidia. Na hivi karibuni ameanza kupata maumivu makali sana katika kiuno chake kiasi cha kushindwa kutembea. Inawezekana sababu ya uzito wake au umri wake, lakini Mungu Mwenye uwezo wote anaweza kumsaidia, kwani bado ana nguvu zake na angeweza kufanya kazi zake kama kawaida, ila anaanza kushindwa kutokana na maumivu aliyonayo. Naomba tuungane katika sala kumuombea mama huyu. Nawashukuru wote kwa kazi nzuri mnayoifanya kuwaleta watu wa Mungu pamoja katika kumsifu na kushuhudia uweza wake. Mungu awabariki sana

 163. MUNGU ASTAHILIE SIFA NA HESHIMA NA ASIMAME NA KILA MWENYE HITAJI LOLOTE HUSUSANI ALIYETUMA KTK BLOG HII.
  NINAWAOMBEA SAANA. NA MUNGU WANGU HAJAWAHI KUSEMA UWONGO LAZMA ATAFANYA KUBWA ANALOHITAJI KWETU NI UTAKATIFU.
  NAWAPENDA MBARIKIWE MNOO!

 164. Bwana Yesu asifiwe sana wapendwa,Naomba mnisaidie katika kumuombea rafiki yangu ambaye shetani amejiinua katika ndoa yake na kumusababishia maumivu makali sana na sasa anaumwa Sukari imepanda anakosa usingizi anawaza watoto wake ambao wamepata msuko suko kwa ajili ya matatizo haya ya familia,Mungu amupunguzie maumivu aliyonayo na aweze kusimama imara na kumutumaini yeye katika maisha yake na ainuke juu ya shughuli zzake zote ili asiende kinyume.

  Mungu awabariki sana wote mnaoungana nami katika maombi haya.

  Mungu ni wetu sote na mwema siku zote jana na leo ata milele,ainuliwe yeye awezaye na anitiaye nguvu katika yote.
  Milley

 165. Shalom Wapenda.. Yesu aliniokoa mikononi mwa maamuzi ya kuolewa na mchumba muislam,yaeni nilipokuwa sijampa Yesu maisha yangu nilikuwa naona sawa 2 kubadili dini ,Yesu ni Bwana! nilipata neema ya kufunguliwa na kujua nakoelekea siko, ndipo nikampa Yesu maisha ,baada ya hapo nilijitahidi sana kuishi maisha ya kumpendeza Mungu kwa muda mrefu kwani baada ya hapo nilifundishwa jinsi ya kujiombea na zaidi naweza kusema nilikuwa nina imani kubwa sana na Mungu wangu, kwani hakuna nilichomuomba akaninyima sasa ni muda sana nimekuwa nikiomba juu ya mwenzi mwema, ajabu ni kwamba wachumba woote wanaotaka kuniposa ni wa IMANI tofauti nadhani mmenipata , Wakristo wenzangu Nachoomba ni maombi yenu kwani walioko mbele yangu na tayari kwa ndoa ndiyo hao.nipo njia panda maombi yenu ni muhimu sana kuokoa imani yangu !
  Tudumu kt kristo Yesu !

 166. Praise GOD!,Ningependa kupata msaada wa maombi katika kutimiza yaliyo yake katika ujana wangu.na ningependa kupata msaada wa maombi MUNGU anifundishe vema habari ya uchumba kabla sijaingia kwenye uhusino.Pia akutane na haja ya moyo wangu.MUNGU NAKUSHUKURU AMEN…

 167. Dada Mercy,

  Jambo la kushukuru Mungu ni kwamba ulishaamuwa kumpa Yesu Kristo maisha yako.

  Ninaheshimu sana uamuzi wako wa kuleta hitaji hili hapa ili kwa pamoja tuombe kwa Mungu. Lakini naomba kujadili kidogo pamoja na wewe katika hitaji hili ulilolileta hapa. Nimepata dukuduku hili baada ya kusoma kwa makini maelezo yako. Na katika kupitia maelezo yako nimeibua maswali kadhaa ambayo naamini yatakupa sababu ya kutafakari. Sihitaji maswali haya uyajibu hapa lakini kama ITAKUPENDEZA waweza kuyajibu hapa ili na wengine, kwa kusoma majibu yako na mjadala utakavyokuwa unaendelea, waweze kujifunza kitu. Najuwa ni wengi tunahitaji msaada wa Mungu katika jambo hili.

  Katika maelezo yako kuna sehemu umeandika hivi: “nilikuwa nina imani kubwa sana na Mungu wangu, kwani hakuna nilichomuomba akaninyima”
  Kutokana na maneno haya mimi ninashawishika kwamba kuna tofauti kati ya imani uliyokuwa nayo wakati huo, ulipokuwa unajitahidi kuishi maisha ya kumpendeza Mungu na SASA ambapo unaendelea kuombea suala la kupata mwenzi mwema. Nasema hivi kwa sababu KAMA UNATAMBUWA KWAMBA HUKO NYUMA KILA ULICHOMUOMBA MUNGU ALIKUPATIA Inakuwaje sasa UMUOMBE MWENZI MWEMA ASIKUPATIE? Kama ulishawahi kumthibitisha Mungu kiasi hicho huko nyuma inakuwaje sasa UNASHINDWA KUELEWA KWAMBA MWENZI ANAYEMLETA YEYE NI YUPI?

  Mambo ambayo nataka tujadili kwa pamoja ni haya yafuatayo:

  1. Kutokana na jinsi ulivyoandika kwa kutumia WAKATI ULIOPITA kwamba “ulikuwa na imani”. Je, unafikiri sasa imani hiyo haipo tena?

  2. Kama imani hiyo bado ipo, ninaamini utakuwa unafahamu Mungu anapojibu maombi hujibu namna gani [kutokana na uzoefu wako wa wakati uliopita].

  3. Kama unafahamu Mungu anavyojibu [kwa sababu alishajibu maombi mengi ya kwako] inakuwaje sasa ushindwe kutambuwa kwamba kati ya hao “wachumba wanaotaka kukuposa” jibu la Mungu ni lipi? [ingawa hapa pia napata tabu, maana kama bado unamuomba Mungu lakini kumbe tayari una “wachumba”]

  4.Kama unamuomba Mungu juu ya jambo hili natumaini utakuwa umeshapeleka mbele za Mungu hitaji kwamba akupatie mume mcha Mungu, mwenye Imani kama ya kwako [mengi yameelezwa juu ya hili katika mada moja ya dada yetu mpendwa aliye(kuwa) na mchumba muislamu]. Sasa wanapokuja watu wenye IMANI TOFAUTI Je, unataka kusema hao ndio Mungu anawaleta? Au labda kwenye mombi yako hujaweka bayana unataka mume wa namna gani?

  5.Kinachokuweka njia panda ni kipi: Je, ni kwa sababu muda mwingi umekuwa unaomba na sasa unaona kama Mungu hajibu tena ndiyo maana unataka “kujichukulia sheria mkononi” kwamba inawezekana ukamkubalia mtu mwenye IMANI TOFAUTI na hilo likahatarisha Imani yako?
  Maana hapa nafikiri kama bado TUMAINI LAKO LIKO KWA MUNGU huna sababu ya “kuwa njia panda” kama si kwamba unataka kuchukuwa maamuzi yako mwenyewe kabla ya kusubiri jibu kutoka kwa Mungu.

  Dada yangu mpendwa Mercy, mimi naona [siyo lazima iwe hivyo] kama kuna badiliko kwenye Imani yako ya kwanza na ya sasa. Kama kweli ulishamuomba Mungu mambo mengi na yeye akakujibu ni wazi kwamba unaelewa fika ni jinsi gani Mungu anavyojibu. Lakini kwa sababu ya badiliko hilo katika Imani yako SASA huwezi tena kuelewa Mungu anakujibu vipi. Vie vile utakuwa unaelewa kwamba Mungu hawezi kumpa mtu kitu ambacho hajaomba. Sasa kama hao wanaokuja kwako si kati ya UNACHOKIOMBA KWA MUNGU kwa nini unataka kufupisha safari kwa kuweka ‘mbele yako’ watu wenye IMANI TOFAUTI? Je, unafikiri Mungu anaweza kukupa MUME MWENYE IMANI TOFAUTI ATAKAYEHATARISHA IMANI YAKO KATIKA KRISTO YESU?……Hivi ni kweli Mungu, aliyekuokoa, huyo huyo tena akusababishie HATARI kwenye Imani yako?
  Hapa naomba utafakari sana!

  Umesema maombi yetu ni muhimu sana katika kuokoa Imani yako. Mimi nakushauri kwamba kitu kitakachookoa imani yako, na zaidi sana, kitakachokuokoa wewe mwenyewe ni KUKAA KATIKA MAKUSUDI YA MUNGU. Mungu tayari AMESHAKUSUDIA KUOKOA IMANI YAKO. Lakini utendaji wa Mungu huonekana kwa mtu ambaye AMEKAA KATIKA MUNGU kwa KUISHIKILIA IMANI.

  Ninajuwa wengi wanahitaji kuoa na pia wengi wanahitaji kuolewa. Lakini KITU CHA MSINGI HAPA katika uhitaji huu ulioko mbele yetu TUSIJE TUKAIKANA IMANI kwa sababu ya kupata mke au mume! [au hitaji jingine lolote]. Mahitaji tunayo mengi lakini naomba Mungu atujalie KUFANYA UAMUZI MGUMU lakini SAHIHI KWAMBA HATA KAMA VINGINE VYOTE VITAKOSEKANA LAKINI YESU AKABAKIA MOYONI, INATOSHA! Maana mbinguni tutakwenda pasipo mwili huu!
  Amina!

  Mambo mengi yanayotusumbuwa sisi Binaadamu ni kwa sababu HATUJAKAA VIZURI katika IMANI. Kukaa katika Makusudi ya Mungu HULETA MAJIBU NA UFUMBUZI WA MATATIZO MENGI YANAYOTUSONGA. Tunapokuwa nje ya mpango wa Mungu msaada wa Mungu huwa mbali nasi. Na kwa sababu hiyo tunapokuwa tunatazamia AMANI huja UHARIBIFU na tunapotazamia UZIMA huja MATATIZO [Yeremia 8:14]. Lakini tukipata neema, tukipata neema ya KUKAA KIMAMILIFU KATIKA IMANI Mungu anasema Tukiwa katika maongezi yeye atasikia na kabla ya kuomba yeye Atajibu! Loh! Ni maneno mazuri sana haya ;lakini je, tunawezaje kufikia katika hatua hiyo ya IMANI?

  Napenda kumalizia kwa kuweka maswali mawili ya changamoto kwa wote wenye mahitaji mbali mbali, hasa hili la kupata mwenzi:

  1. Je, ni kweli tunaishi maisha ya kumpendeza Mungu YANAYOTUPATIA HAKI ya Mungu kututatulia mahitaji yetu? Au tunahitaji tu msaada wake huku Maisha yetu yanatushuhudia wazi kwamba HAYANA MSINGI KATIKA MUNGU WA YESU KRISTO?

  2. Kama maisha yetu yako SAFI mbele za Mungu, Je tunapomuomba juu ya jambo fulani TUNAWEZA KUTAMBUWA SASA KWAMBA JIBU LA MAOMBI YETU NDILO HILI?

  Mungu wa mbiguni na atusaidie!

 168. Ninalo jambo ambalo ningependa mnisaidie nielewe. Maana neno linatuambia kuwa watu wangu waangamia kwa sababu ya kukosa maarifa.
  Mimi nikijana nimeokoka na ninamtumikia Mungu kwa huduma mbalimbali kanisani na kwenye mikutano ya injili, inje na nchini. Basi kwa mizunguko yangu ya kihuduma nikakutana na binti kwenye huduma, nikampenda, bila kumuambia maana nilikuwa sijajuwa hari yake ni ipi. Kwa kuwa nilikuwa na mda maeneo hayo, na yeye akaniamini na kuanza kunisimulia hali alio nayo, akanielezea njisi alivyo kuja jijini Dar kijana mwengine akamdanganya na kumbebesha mimba, ikawa swali kubwa maana hakukuwa na mtu yeyote jijini amabaye angekimbilia, basi akarazimika kwenda kukaa na kijana huyo ambaye amembebesha mimba. Akiwa na matumaini kwamba kijana yule atakubari afunge naye ndoa, ila kijana akakataa. Maisha yakawa mabaya kwake. Huku binti akaendelea kukuwa kiroho, hata kanisani wakamuamini na kumfanya shemasi mkuu, .. sasa ikifika kwenda kutembelea wenye ndoa, akawa analia saana maana alikuwa akikumbuka kwamba naye bado hajafunga ndoa…
  Mimi nikamfariji na kumonyesha kwamba yale yasiowezekana kwa mwanadamu kwa Mungu yanawezekana, na nia ya kumpenda ndani yangu ikaisha ikabidi sasa nimsaidie kiroho maana niliona hitaji hilo ni kubwa. Ila nikajiuliza pia kwa nini amenijia mimi kuniambia hayo???? Kwa nini hajaenda kuambia mchungaji ama watumishi wengine! Basi baada yangu kuondoka na kurudi nyumbani, nikapata habari kwamba binti yule amefukuzwa nyumbani, nikajitahidi kumuonya ili arudi kwa kijana huyo, ila akakataa, na kusema kwamba hawezi kurudi kwake, bora akae nyumbani akamtumikie Mungu.
  Baada ya miezi kadhaa, nikampigia simu ili nijuwe hari yake nikakuta bado yupo peke yake.
  Sasa mimi nikajisikia kumpenda sana japo amepitia yote hayo maana nimeona ananifaa ili niendelee kumtumikia Mungu kwa ukamilifu. sasa naomba msaada ili ni juwe niamue nini maana tayari moyo wangu umeshampenda ila sijamuambia. ndoa. Barikiwa.

 169. Bwana Yesu apewe sifa watumishi wa Mungu.

  Nami ninahitaji maombi yenu kwa tatizo gumu la kiafya ambalo nimedumu nalo muda wa miaka 14, naomba msaada wenu wa maombi ili Mungu afanye kitu cha tofauti kwangu maana kwake hakuna jambo gumu la kumshinda. Nisaidieni wapendwa katika Bwana mnibebe katika maombi yenu ya kila siku.

  Mbarikiwe wote kwa huduma njema

 170. Mimi naomba kukushauri ndugu Gregory Edy kama ifuatavyo:

  Kwa kuwa umeshaamuwa kumpenda wewe mwenyewe pasipo kushawishiwa na mtu, nafikiri ni vigumu sana mtu mwingine kuuondoa upendo huo kwa dada huyo. Kuna mambo kadhaa ambayo unatakiwa uyahakikishe kama siyo hayo ndiyo yamekusababisha ujisikie unampenda:

  Kuna suala la KUMHURUMIA. Kwa kuwa ulimuona alivyokuwa anapitia mambo maisha magumu nawe ukawa umeingiwa hali ya kumhurumia na kutaka kumsaidia japo kwa mawazo. Huruma hiyo, kama huwezi kuwa makini, waweza kufikiri ndio upendo wenyewe. Lakini kwa upande mwingine hiyo ndiyo yaweza kuwa sababu ya kuwafanya mfahamiane.

  Pia lipo suala la KUMTUMIKIA MUNGU. Kwa kuwa huyo dada alikuambia bora aende nyumbani ‘akamtumikie Mungu’, hiyo inaweza kuwa imeongeza chachu, kwa kuwa wewe mwenyewe unasema uko katika utumishi, tena kwa muda kadhaa sasa.

  Kitu muhimu sana kwako, kama mtumishi, hakikisha mtu unayetaka kumuoa awe ameokoka. Kama dada huyo ameokoka, na ushuhuda wake ni mzuri huko aliko, basi hapawezi kuwa na sababu yoyote ya nje [external] ambayo mtu mwingine anaweza kukushauri tofauti na unavyojisikia juu yake. Wakati unaendelea kuombe jambo hilo, amani ya kristo itakupa majibu moyoni mwako.

  Mungu akutangulie!

 171. Barikiwa sana Mtumishi John Paul kwa ushauri wako. Nimeelewa 100% ulivyoeleza. Niliposoma kwa mala yakwanza nimesimamisha kwanza nikafikilia kwa suala hilo la KUMHURUMIA: Nikaona sio, maana aliponielezea kuwa ana mtu anakaa naye, basi nilibadirisha mawazo nikaanza kumusaidia kama mwenye ndoa. Hata nilipopata habari kwamba ameachana na kijana huyo, nimemuudhi kwa kumbembereza ili arudishane na kijana huyo, hata akawa anakataa kupokea simu yangu. Nilipoona sasa kwamba hana nia ya kurudi ndipo ni kaachana naye, huku nikiperereza kwa mbali mienendo yake.
  Kuhusu suala hilo : LAKUMTUMIKIA MUNGU: Hilo nimeliweka mbele za Mungu tangu zamani kwamba mke ninaye mhitaji, awe mtumishi wa Mungu maana ajuwaye kutunza huduma ya Mungu, na huduma za nyumbani pia ataziweza.
  Barikiwa sana ndugu mpendwa, kweli wewe Mungu amekuweka kwenye blog hii ili uwe baraka kwa wengi. Mungu aendelee kukukuza zaidi.

 172. Brother Edy,
  naungana na John Paul juu ya suala hilo.
  Kumpenda mtu ni jambo la kawaida lakini pia ni vema kufuata maelekezo ya Mungu wetu. Hivi ni vigezo mama katika uchaguzi wako:
  1. Lazima huyo dada awe ameokoka
  2. Lazima ukiri wake uendane na matendo yake
  3. Lazima uwe umempenda na si kumtamani au kumhurumia au namna nyingine tofauti na upendo

  Pia kuna mambo fulani ambayo si ya msingi sana (kwa maana kuwa hayakuzuii kumuoa na yanaweza kuwa negelected), lakini ni vizuri kuyafikiria kama uko makini na huduma:

  Je atakuwa msaada kwa huduma ambayo Mungu amekuamini nayo? Mfano Mungu amekupa huduma ya uinjilisti na unakuta yeye asingependa mizunguko. Hii inaweza kuleta matatizo baadaye

  Kuhakikisha kama kweli ummependa, au tu ni misisimko ya mwili ni jambo la muhimu mno! Kumbuka moyo ni mdanganyifu sana na una ugonjwa wa kufisha. Kama una hakika na mambo haya yote, na mengine ambayo Roho wa Mungu anaweza kukuongoza kuyaangalia, unaweza kumweleza.

  Mungu akupe neema ya kuvuka hapo pia ndugu!

 173. Asante sana ndugu Gregory Edy kwa kunitakia baraka za Mungu. Nashukuru Mungu zaidi kwa kuwa umeelewa na umeweza kupata machache ya kukusaidia katika hilo lililoko mbele yako.
  Tuendelee kuombeana katika safari hii ya mbinguni.

  Mungu akutunze na kukufanikisha katika huduma yako.

 174. Amina wapendwa kwa maneno ya faraja. Mbarikiwe na Bwana Yesu milele na milele.

 175. Bwana Yesu asifiwe,
  Neno linatuambia kwamba tutakuwa mashahidi wa Yesu, sio nchini mwetu tuu, bali dunia nzima na kwa watu wote. Leo hii kuna nchi zingine zinagoma kutoa entry visa. Ninaona ni mpango wa shetani ili injili isihubiliwe, nakushuhudia matendo makuu ya Yesu kila mahali. Mimi na wenzangu ninaohudumu nao nchini canada, tumejaribu kuwaarika wahubiri kutoka afrika, ila wengi wamenyimwa Entry Visa, na wengine kuzipata kwa tabu. Inauma saana kutegemea mhudumu, harafu asifike kwa sababu ya kukosa visa,, jamani. kwa hiyo tuombe ili Mungu abomowe nia hizo za shetani na mipango yake yote ili visa zipatikane kirahisi. Kinacho nishangaza ni kwamba wao, mtu wao akinyimwa visa, wanalalamika. kwa kweli ni mbinu shetani ametumia ili Canada kusiwe uamusho na mabadiriko katika imani zao haswa za kikatoliki.
  Tuunganeni kwa maombi.

  JOSE N. EDWARD

 176. Mpendwa Gregory Edy!!

  Shalomu!

  Kwanza nikupe hongera kwa kumtumikia Mungu na moyo ulio nao katika kuwasaidia wapendwa, Mungu akubariki.

  Nimejaribu kupitia maelezo yako kuhusiana na suala hili, pamoja na ushauri wa wapendwa wenzetu hapo juu, nikaona nami nijaribu kutoa maoni yangu niliyo nayo.

  Ni kweli kuwa wewe ulianza kumpenda huyo binti hata kabla hujajua maisha yake, lakini baadae akakupatia maelezo kuhusu maisha yake. Katika maelezo yako kuna swali moja ulijiuliza “Kwa nini hajaenda kumwambia Mchungaji au watumishi wengine” swali ambalo sijajua kama ulipata jibu lake.

  Majibu ya swali hilo ni muhimu sana kabla hujachukua hatua yoyote. Nafahamu kuwa wewe uliliangalia kwa upande mmoja(postive), lakini nadhani ni vema uliangalie kwa upande mwingine (negative).

  Maswala ya ndoa ni nyeti sana kwa ajili ya maisha ya wokovu na utumishi. Wewe kama mtumishi, sehemu moja ambayo adui anaweza akakupata ni kwenye ndoa hivyo unapaswa kuwa makini sana na kumuomba Mungu.

  Sijafahamu huyo dada aliokoka lini, baada ya kupata mimba au kabla, je ilikuwaje kanisa limuamini kiasi kikubwa hivyo bila kujua undani wa maiSha yake (yaani kuwa anaishi na mwanaume) au kanisa lilikuwa linafahamu? Kama kanisa lilikuwa linafahamu, kwa nini wakati wa kwenda kutembelea wenye ndoa alikuwa analia?

  Kuna mambo mawili hapa, kama kanisa lilikuwa linafahamu kuwa anaishi na mwanaume akiwa ameokoka, je lilimhesabia huyo mwanaume kuwa ni mume wake au nani wake? Kama kanisa lilikuwa halijui kuwa anaishi na mwanaume, basi hapo kuna tatizo kubwa sana, kwanini aishi na mwanaume bila kanisa (mchungaji) kujua?

  Naomba ujiulize swali hili, Je huyo mwanaume aliyekuwa akiishi naye alikuwa kama mume wake au kimada? Kama ni mume je hiyo ndoa imevunjika? na kama imevunjika, je unaweza kumuoa mke wa mtu? Kama kimada, je ilikuwaje aishi kimada huku akiwa mtumishi ndani ya kanisa na kanisa lisijue?

  Ninapozungumzia mtu kuwa mke, si lazima awe amefunga ndoa kanisani ndipo useme huyu mke wa fulani, hapana, yako mambo mengi sana ya kuangalia.

  Mwisho nikutakie mema, naomba uyafanyie kazi haya niliyokuuliza kabla ya kuanza kuingia kwenye mahusiano, unaweza ukajikuta unaoa mke wa mtu au mtu ambaye si mkweli na muwazi!! Naomba ufahamu kuwa mimi simjui huyo dada na hivyo nimetoa maoni yangu kulingana na maelezo yako, hivyo ikiwa kuna jambo ambalo limelizungumza tofauti na hali ilivyo basi ni kutokana na ufinyu wa ufahamu wangu juu ya huyo dada.

  Shalomu.

 177. Mpendwa Gregory Edy.Bwana wetu Yesu Kristo akubaliki katika huduma yako.Baada ya kusoma maelezo ya hali yako katika utumishi. Nimeona nikufariji kwanza, nakukupatia msaada ambao utakupatia angalau mwangaza katika maisha ya utumishi na ya ndoa .Kigezo cha ndoa si kwa binti tu hata kwa kijana wakiume lazima na yeye ashuhudiwe vema,na ningependa kukufahamisha kuwa kama mke alibebeshwa mimba si wakwanza kanisaniniwaimbaji wengi wanao beba mimba kisha wanaamuwa kujipeleka kabla havija fahamika kanisani.Ila nilishukulu kwa huyo Mama alikuwa amekiriri dhambi zake ndio sababu alikuja kukuelezea hayo matatizo na alichokiona kwako ni utumishi wako,pia inawekana hata neno ulihubiri lilikutana na matatizo aliyo kuwa nayo.jambo lingine kama we ni mtumishi nafikiri sijambo geni kuona watu wenye makamu kukuzidi wakikujia ili kukutaka maelezo ju ya shida zinazo wasumbuwa.kuwa nahuluma kwa mtumishi wa Mungu nilazima ila ukiwa kwenye huduma nikujihadhari sana kama kijana pia kama mtumishi wa Mungu.mtu akisha kuangukia dhambini ni mtumwa wa dhambi na akisha tubu amekuwa kiumbe kipya hata usipo mpeleleza kwa ushuda wake na wawatu wa inje utamtambulisha yu nani NB.sehemu nyeti ambayo ni tatizo kwa mtumishi ni pale mtu anapo kwenda kwenye huduma akiwa na malengo mawili:Uchumba na Injili.kwanjia mmoja ni vibaya ukiwa hauko kwenye huduma maalumu na kwanjia nyingine si vizuli kwa mtumishi,hilo swala uchumba linakiwa mda wake malumu kwa nafikili kwa msemo huwo Mungu atakupatia ufahamu.

  Kama mwana mke yule alikuwa hajatolewa mahari au hakuna mapatano kati ya wazazi wa binti na wa kijana na kama kijana haja hiali kuishi na mke yule bado anao uhululu wa kukaa kwao. baada ya kutubu mbele ya kanisa anaweza kuendelea na kazi ya Mungu kanisani.mtume paulo alisema ju ya watu wawili :mke aliye okoka na mme ambaye haja okoka wakikubaliana kuishi waishi pamoja ila yule asiye amini akiamuwa kutoishi nayule anaye amini basi aaminie yuko huru ,kwasabu wakristo wengi hujindanganya pale wasemapo kuwa wataweza kugeuza wenzi wao myume paulo auliza je unauhakika gani kama wewe mke au mme kama mtaweza kugeuzana? nahuku wakiisha kuishi pamoja hulaumiana na kuwaabia kuwa walipo waoana hawa kuuliza mungu? Ndugu Gregory ninalo kushauli kwannza ,usiwe na msukumo wowote utokanao na mwili,au moyoni ,angalia kuwa wakati wako wakutafuta mchumba umewadia, kisha yule unaye mtaka angalia kama anahuduma zile uzipendazo na ushuduma kanisani na wa innje ni muhimu ,usithubutu kutaja neno uchumba kwa binti yeyote na huja kuwa na uamuzi wa kutaka kukamilisha tendola ndoa utakapo muacha au kudanganya mmoja tu utumishi wako utakuwa umeingiwa na dosali.usimfikiliye aliko toka angalia anako elekea na mwenendo alionao sasa sote hatungestahili kuwa watumishi ukiangalia tukotaka.Sasa ndugu Gregory, zaidi ya yote achia mapenzi yake Mungu yatimizwe na umkabidhi Mungu njia zako zote naye atatengeneza.1kor7:14-16.laki kwa yuke aliyefunga ndoa imeandikwa kuwa wasiachane ila kwa sababu ya uzinzi,kuhusu hali yake ya zamamani usisahau kuwa Hosea aliambiwa na Mungu kuowa mke mzinzi ,picha ya mke nzuli ni yule aliye kiumbe kipya kwa kumalizia na kutakia ufanisi na Mungu wa amani azidi kukupa muongozo na uamuzi sahihi na Mungu akubaliki

  Past Ev. Nkorikori Johnson
  Quebec Canada
  1(418)6631837

 178. Kwa ndugu Gregory
  kwa nyongeza nataka kukupati ushuhuda wa dada yangu ambaye ni mtumishi wa Mungu sasa.Yeye ana miaka kumi hana mme na an watoto wawili watu wengi walijifanya watumishi wa Mungu na maombi ya kufunga waliweza kuyakamilisha bila wasiwasi.Ilifika kipindi fulani wakaja kumtolea mahali ,wakatangaza hata siku ya halusi, na alitaka kuolewa nakijana msomi aliye maliza chuo kikuu mhublili mzuli sana .Lakushangaza dada yangu akamwambia hivi kabla ya kufunga ndoa twende tukapimwe kijana akasema je hatuaminiane kama tumkwisha okoka kuna haja gani ya kujipimisha ? dada akmwambia chukuwenu mali yenu kama hamkubali kijana akang’amua kuvunja uchumba hayo yametokea kwa vijana zaidi ya watatu tena wote ni watumishi wa Mungu.kwa nini nimese vivyo?nikukutahadhalisha na kukuambia kuwa shetani anatafuta watu wenye afya kiroho na kimwili.na shetani amejiingiza kwa sili makanisani na ameiba hata huduma au anaigiza utumishi ni kukaa chonjo.hata kama dada au kijana wameokoka lazima hata kwa muganga wapitie kisha ndugu kama kweli umkwisha kusudia kuoa na uko tayali chukuwa hatuwa ya kwanza uende mlimani ,muulize Mungu akupatie kibali kisha onana na watumishi wa kanisa lake ili kupata ushuhuda. mfahamisha Mungu kwanza kabla ya mutu yeyote nasi tuko tayali kukusaidia kwa maombi na hata kwa sherehe ya harusi yako.Mungu akubaliki
  Past EV. Nkorikori Johnson

 179. BWANA Yesu apewe sifa sana watumishi wa Mungu! najua mko wazima wa afya njema! na kwa neema ya Mungu mnaendelea na shughuli za kukuza ufalme wa Mungu! NAOMBA MSAADA WENU KWAMBA NIFANYAJE………mimi ni mtumishi wa Mungu katika kanisa la SHEKINA MISSION CENTER-MIKOCHENI A PLOT 1004. Tarehe 14-01-2009 hapa kanisani tuliibiwa vyombo vya muziki; kinanda, mixer, na fedha za sadaka! nilienda polisi katika kituo kidogo cha hapa mikocheni A wakasema kwamba watakuja kuangalia walivyobomoa milango ya nyumba!..cha kushangaza kabisa hawakuja hawa mapolisi. Tulienda Ostabey na huko ni hivyo hivyo wakatuambia kwamba watatuma upelelezi wafanye hiyo kazi..lakini mpaka sasa hatujawaona…NINACHOSIKITIKA SANA ni kwamba hao walioiba mali hizo tunawafahamu mpaka kwa majina na wanazidi kutudhihaki kwamba “mbona siku hizi hamna mziki?” yaani ndugu zangu tunaumia sana moyoni! nashangaa kwamba mamlaka serikali yetu haiko tayari kusaidia raia hapa nchini! sasa swali langu ni kwamba; je nifanyeje? maana kama ni kuwasamehe hawa vijana tayari nilishawasamehe, lakini nataka serikali itimize wajibu wake wa kuwakamata ili wasiendelee kuwaibia hata watu wengine!! Jamani kwa mtu yeyote ambaye anaweza kunipa msaada ya kwamba niende wapi, naomba anisaidie. Mchango wako ni wa maana sana. unaweza kunitumia hata sms kwa namba hizi 0786 684 062 au 0712 135 100 au email: senishekinah@gmail.com. Mchango wako ni wa maana sana nami nitautumia. Lengo ni kwamba tushirikiane kujenga jamii safi mbele za Mungu. Na pia watu wamwogope Mungu wetu wasifikiri kuiba kanisani watapata “msamaha” tu! hapana! kuna nafasi yetu ya kusamehe…tayari tumesamehe…lakini nafasi ya serikali pia! maana wananikwepa kila nikienda, nafikiri wameshiriki wizi. nisaidieni kwa hilo.

 180. Ev. Daniel John.

  Shalomu!

  Kwanza nikupe pole wewe pamoja na kanisa kwa tukio lililowapata, ni jambo la kusikitisha sana kuwa watu wanaiba hata kanisani.

  Mimi ninakushauri kuwa uende kwa Mkuu wa Kituo hapo Oysterbay upeleke malalamiko yako. Nasema hivyo kwasababu Mkuu wa Kituo anao wajibu wa kupokea malalamiko yote. Aidha, unaweza kuonana na OCD wa eneo la huko uliko au hata RPC wa eneo lenu. Ikishindikana kabisa basi unaweza kumuona hata Kamanda wa Kanda Maalum ingawa nadhani si lazima sana kufika huko.

  Najua pengine sijakusaidia sana, lakini kwa ajili ya haki kutendeka ni vizuri kufuata ngazi zilizopo katika kupeleka malalamiko yako.

  Jambo lingine, ni muhimu tukumbuke kuliombea taifa letu na vyombo vyake ili viweze kutenda haki. Kama wanashindwa kushughulikia suala la kanisa, je masikini wako katika hali gani? Wakati mwingine huwa nadhani Mungu anaruhusu baadhi ya mambo yatupate ili tuweze kukumbuka kutekeleza wajibu wetu kwa taifa.

  Shalomu!

 181. Bwana asifiwe!
  Pole sana Mtumishi, naomba uende kwa IGP Mwema. Mpe jina langu na uombe appointment nae. kama kuna shida wasiliana nami.

  Ubarikwe.

 182. eemungu nisaidie katika matatizo makubwa yanayo nikabili kiafya. bwana ahimidiwe amen;

 183. Asanteni watumishi wa Mungu kwa msaada wenu mzuri! Ni lazima kweli tunahitaji kukumbuka wajibu wetu kwa taifa la Tanzania na pia nashukuru sana Mch dkt Malisa-ila tu kinachonisumbua sasa ni kwamba kila ofisi ninayoenda naambia niende kwa mkuu wa KITUO OSTABEY mkuu naye anasema kwamba yeye hakuwa zamu wakati wa Tukio hilo! hiyo ni ajabu—-tuombee taifa la Tanzania kwa makini sana mbele za Mungu! tulie kama Nabii Daniel kwa ajiliya Yerusalem–Tanzania! amina!

 184. Thanks to the Almighty for this blog.wapendwa mimi niko kenya. naomba muniombee dadangu kama aliyepangawa.Akili za nikama hashiki kitu chochote tangu alipokua shule ya msingi.Hivi karibuni alitushangaza kwani alipiga nduru nyumbani akidai eti watu wlimwambia eti mama kajiua.watu walishangaa sana ka yaliyotukian kwani haijawahi fanyika hivyo.Alipoteza fahamu kabisa kiasi cha kuaga lakini mama mzazi alimuombea akapata nafuu.cha maajabu mzee nae wakati mwingine hupagawa a kisema kuna watu wana muendea kinyume.naomba maombi ili familia yetu iwe huru namapepo hayo kwa jina la yesu Kristu.Nimeoa na bibi yangu pia ana brochitis inayo msumbua kila mara.Nahitaji maombi yenu pia. Mungu awabariki nyote.

 185. BWANA ASIFIWE MIMI NIMEOKOKA NAMPENDA YESU NAOMBA KUWASHILIKISHA WATUMISHI WA MUNGU,KUENDELEA KUNIOMBEA MAANA MWAKA JANA MWEZI WA NNE MKE WANGU ALIKWENDA KUPIMA NA KUKUTWA ANAMAAMBUKIZI YA UGONJWA WA UKIMWI HIVYO NAOMBA SANA WATUMISHI WA KUNIOMBEA PAMOJA NA FAMILIA YANGU TUWEZE KUISHI NA KUPONA,MAANA MAANDIKO YANASEMA HAKUNA LISILOWEZEKANA KWA MUNGU ILIMRADI AMIMINI.HATA MIMI NA FAMILIA YANGU TUNAAMINI KUWA YESU NI MWOKOZI WA MAISHA YETU.TUNAABUDU KANISA LA ASSEMBLIES OF GOD MAGOMENI,MUNGU AWATIE NGUVU AMEN

 186. Pole bwana Ngaya! naamini kwamba YOTE yawezekana kwake yeye aaminiye–amini kwamba kama bado Mungu ana mpango na maisha yako hutakufa leo wala kesho! utakaposoma ujumbe huu, tafadhali chukua biblia yako na Soma (ZABURI 118:17)bwana Ngaya “unaamini maandiko hayo? kweli? kaa pamoja na mke wako na tamkeni kwa viywa vyenu maneno hayo kwa sauti! maana yake ni kwamba mnatangaza ushindi katika maisha yetu! Wote njoni mshuhudie matendo ya Mungu kanisani matendo ya Mungu! maana hilo ndilo kusudi la uponyaji! Naamini utakapotamka tu….utapona! na nenda kapime na mkeo!—-AMEN!………NIOMBE SASA..” Baba Mungu wetu, tunakushukuru kwa sababu unatupa uzima tele, neno lako linasema kwamba Yesu ulikuja ili tuwe na uzima kisha tuwe nao tele Yoh 10:10b..sasa BWANA rejesha uzima tele kwa Ngaya na mkewe…kwa jina la YESU AMEN.

 187. Tumsifu Yesu Kristo.
  Ndugu zangu katika kristo naombe mniweke kwenye maombi yenu kwani familia yetu inaandamwa na nguvu za giza. Sisi ni familia tuliyobahatika kwenda shule na tuna kazi nzuri lakini swala la ndoa kwa watoto wa kike limekuwa na ugumu katika familia yetu. Tuko kwenye vita dhidi ya Ibilisi. Baadhi ya waliotangulia wamekuwa wakiolewa wake wa pili, lakini sisi ambao bado kuolewa hiyo hali tuinakataa kwa jina la Yesu. Naomba mniombee hasa mimi niweze kufunga ndoa ya kikristo pamoja na kijana ambaye amejitokeza na kuishi maisha ya ukristo. Umri wangu ni miaka 35. Namuomba sana Mungu anipiganie katika hili na naomba nanyi nyote mniweke katika maombi yenu.

  Mungu awabariki sana.

 188. Dada Leah,

  NI hatua nzuri uliyochukuwa ya kutambuwa kwamba KWA YESU KUNAPATIKANA MSAADA. Ingawa hujaeleza sana kuhusu nguvu za giza zinavyoandama familia yenu. Lakini Mungu analijuwa hilo. Ila sitarajii maelezo yako kuhusu tatizo la suala la ndoa kwa ‘watoto wa kike’ katika familia yenu kuwa ndiyo linalohusiana na hizo nguvu za giza. Ingawa hili linaweza kuwa hivyo kwa upande mmoja lakini mimi naomba kushirikiana nawe kwa upande mwingine ambapo tatizo la kuolewa HUWEZA KUSABABISHWA NA SISI WENYEWE BINAADAMU. [Kwa sasa sitaongelea sababu zisababishwazo na nguvu za giza katika suala la ndoa, ninaweza kufanya hivyo kama itahitajika].

  Naendelea na ushauri wangu kama ifuatavyo:

  MWENENDO WA MAISHA YETU HUWA NI SABABU YA MAOMBI YETU KUJIBIWA

  Ni rahisi sana kwa binaadamu kuhitaji msaada toka kwa Mungu lakini si kila mtu anayehitaji msaada toka kwa Mungu/Yesu ambaye huweza kutathmini mwenendo wa maisha yake kama SI NDIYO sababu ya tatizo alilonalo.

  Kwa kuwa sasa tunaongelea ‘watoto wa kike’ nitajikita hapo, hapa haina maana kwamba ‘watoto wa kiume’ hawana matatizo. Kwa sasa ninaongelea watoto wa kike:

  Wako akina dada wengi sana ambao ni wazuri kwa sura, wanaelimu nzuri, wana pesa na pengine wameokoka vizuri tu lakini kuolewa kwao limekuwa ni tatizo. [Wale ambao hawajaokoka tatizo ni kubwa zaidi maana wako gizani]. Sababu KUBWA ambayo napenda tushirikiane hapa ni KIBURI. Wanawake wengi, akisoma, akawa na kazi nzuri na pesa nyingi huingia kiburi. Kiburi hiki kusababisha mdada wa namna hii kusema “..mwanaume hawezi kunibabaisha”. Mdada akishakuwa katika hali hii huwa ni vigumu kukubali ushauri wowote. Pesa na mafanikio kwake huwa ndiyo kila kitu. Hasikii la mchungaji, mzee wa kanisa wala mshirika mwenzake. Hata akionywa kuachana na mwenendo mbaya ambao hauleti USHUHUDA MZURI kwa mdada aliyeokoka bado dada huyu hushikilia kwa kusema kwamba “KAMA NINGEKUWA NAFANYA VIBAYA NISINGEKUWA NA MAFANIKIO HAYA”. Katika hali hii mdada huyu HUJICOMPLICATE kiasi cha kuwafanya wakaka wakristo kumuogopa kwa kuhofu kwamba ‘inaweza kuwa ngumu sana kum-handle dada wa jinsi hiyo kwenye ndoa’. Ndiyo unakuta kila mkaka anayemu-approach huwa ni mtu ambaye si Mkristo na hata kama ni mkristo si Mkristo mwenda mbinguni bali mkristo wa dini, kwa ujumla huwa ni WAPITA NJIA!

  Wadada wengi wamekumbwa na tatizo hili na akisha kata tamaa ndiyo utakuta anaamuwa kujiachilia na kuolewa hata kama ni kuwa mke wa pili. Kwa nini? Kwa sababu vijana ambao hawajaowa wanamuongopa. Wana hofu kwamba mtu unaweza ukaoa ukifikiri umeoa mwanamke kumbe umeoa ‘jike dume’, Hakuna UTII wowote kwa mume kwa sabau ya PESA, ELIMU na CHEO kizuri.

  Mfano hai unaoweza kufaa hapa ni kuangalia wengi wa wanawake MAARUFU kwa namna moja au nyingine WENGI HAWAKO KWENYE NDOA na kama zipo HUWA ZINA MIGOGORO MINGI, MINGI SANA! Sababu ya jambo hili ni kwamba UTII kwa mume unakuwa haupo. Pesa, Kazi, na Elimu husababisha mgongano moyoni mwa mwanamke.

  Mungu aliumba mwanamke awe MTIIFU kwa mumewe [lakini si mtumwa, hapa naomba nieleweke vizuri]. Sasa ukichangaya KIBURI cha elimu, pesa, na cheo kizuri pamoja na MAMBO YA USAWA WA JINSIA tabia za wadada wengi hazivutii mkaka yeyote kwamba amuowe mdada huyo. Cha kusikitisha utakuta dada wa namna hii haachi kutuma maombi kwamba anahitaji mume wakati hajuwi KIMLACHO KINGUONI MWAKE!….yaani tabia yake haifai.

  Maisha matakatifu pamoja na mwenendo WENYE USHUHUDA mbele za watu wema na KUJIWEKA MAZINGIRA YA KUHESHIMIKA, ambayo hayawezi fanya wakaka wakufikirie VIBAYA ni mtaji mzuri sana kwa MDADA aliye katika hitaji la kuolewa!

  Mdada akiishi maisha yenye MUONEKANO MZURI, SAHIHI kwa watu wema huwa ni sababu moja wapo ya akina kaka kumuona kama anaweza kuwa MKE MZURI.

  Kwa hiyo dada Leah, pamoja na maombi yanayoendelea pia inabidi kujichunguza maisha ambayo Unaishi. Unaweza kukuta UMEWAFUKUZA WENGI kutokana na mwenendo wako [si lazima iwe hivyo na wala sikuhukumu kwamba una mwenendo mbaya bali natoa ushauri tu].

  Mungu wa mbinguni atusaidie!

 189. Nashukuru sana kaka Paul kwa maoni na ushauri wako. Pengine ilikuwa vigumu sana kwetu sisi kujielewa kuwa maisha tunayoishi yanaweza kuwa kikwazo kwetu kuolewa. Lakini kutokana na maelezo yako nashukuru sana umenifungua akili. Sikujua kuwa vijana huwa wanatabia ya kuogopa kwa kuangalia maisha ya mdada. Sisi tumekuwa tukiangalia historia ya familia na kuona kuwa mashangazi wetu wote waliolewa wake wa pili. Harafu swala la nguvu za giza lipo tunaliona katika matukio maana tunasali na kuomba na tunazidi kufunguliwa. Hivyo basi namuomba sana Mungu azidi kutusaidia. Mungu awabariki wote

 190. Dada Leah,

  Nashukuru Mungu kwamba umeweza kufunguka akili kutokana na maelezo yangu. Sifa na Utukufu ni kwa Mungu aliye Hai.

  Endelea katika kulitumainia Jina la Yesu na kuamini kwamba Kuna nguvu Damuni mwa Yesu Kristo. Nguvu za giza SI KITU mbele ya Uweza wa Jina la Yesu Kristo!

  Naamini Mungu atafanya Njia kwa ajili yako!

  Tuko pamoja!

 191. Ahsante sana kwa kunitia moyo. Naamini siku zinazokuja nitakuwa natoa ushuhuda kwa wengine.
  AMEN

 192. Wapendwa katika kristo. Mimi ni mgeni katika blog hii lakini si mgeni katika kuisoma. Ni mojawapo ya blog ambayo naisoma kila siku iendayo kwa mungu. kabla sijapeleka maombi yangu ninayo machache kwa wale wote ambao wametuma maombi mbalimbali. Mungu awatie nguvu akawape uvumilivu na mzidi kumtegemea yeye siku zote kwani hakuna asiloliweza. Maisha siku zote ni safari ndefu yenye majaribu mengi lakini ukimtegemea yeye katika sala na maombi anaweza. Nimepita katika majaribu na mitihani mingi ya maisha lakini siku zote bado namshukuru mungu kwa kunitia moyo na kuniwezesha kufika hapa nilipo. mungu amenibariki katika mengi sina maana ya utajiri ila katika kuyashinda majaribu mengi na vikwazo vingi katika maisha. Naungana na dada Leah katika maombi ya kumpata mume mwema nami nipo katika hali hiyo naomba mungu akaifunge milango ya shetani akanijalie kunipa mume mwema aliye mkristo na anayemjua mungu. Naomba maombi yenu. Mungu awabariki wote na awatangulie katika shughuli zenu za kila siku. Tuzidi kuwaombea wenzetu wanaoishi na virusi vya ukimwi kwani wengi wao wamekata tamaa ya maisha lakini ninayo imani, kwa maombi yetu mungu atawatia nguvu na kuwajalia uzima.

 193. Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu. Mimi ninamshukuru Mungu amekuwa anajiinua sana katika maisha yangu. ameniongoza na kunifanikishia mambo kazini na ametenda miujiza sana na mshukuru sana kwa hayo. Ninaomba maombi yenu nipate mwenza wa maisha kwani kwa sasa sina boy friend wala mchumba na umri wangu ni miaka thelathini.

  Ninaona umri unasonga sijapata hata wakuniambia aje kwetu.Ninakutana na vishawishi vya wakina dada wanaoniambia tuende kwa mganga. Nimekuwa nikifunga sana na kusali naomba mnisaidie jamani kwani sipendi kumkosea Mungu kwa kuzini nahitaji mume wangu.

 194. Shalom !!!
  Nawapenda sana naomba mniombee sana ili nikuwe nikimjua Mungu na nguvu za Mungu ziwe juu yangu na niweze kusimama kwenye nafasi yangu Mungu aliyenipa AMIN

 195. Jamani asanteni sana Mungu awabariki sana, nami naomba Mungu awatie nguvu wote mliotuma maombezi yenu ila ni vizuri kutaja shida yako ili tumweleze Mungu kwa wazi……………AMINA

 196. wapendwa nawasalimu katika jina la Yesu. Mimi nimekuwa nikitaka sana kujiunga na wapendwa wenye kumjua Mungu kama nyinyi. Kwa kweli mubarikiwe sana natuendelee kuombeana na kuinuana kiroho. Hakika Yesu ni mwenye huruma naye anaenda kutenda.

 197. Bwana Yesu asifiwe wapendwa katika bwana naomba mniombee swala la ndoa yangu linapata kikwazo juu ya mahari pia nahitaji la kupata msamaha wa kodi ombi kutoka wizarani nimetuma maombi naomba mniombe lipate kibali. Mungu awabiriki sana

 198. Dada CAROCHAO karibu sana na ubarikiwe sana na bwana tupo kwa ajili ya safari ya kwenda mbinguni tuombe kwa bidii sana ni wakati wa mwisho.

 199. wapendwa nawashukuru nyote na Mungu awabariki .Injili ya bwana ieendelee .Nilikuwa na mahitaji ya maombi hapo mbeleni ya bibi yangu akiwa na bronchitis.Kweli naendelea kuuona mkono wa bwana kwani maombi yanaendelea kufanya kazi.Dadangu aliyepagawa pia anaendelea vizuri.Nimeamini kweli kuwa na imani ni kitu muhimu sana.Bado naamini shetani atashindwa kabisa. ahsanteni.

 200. Shalom wapendwa, naomba maombi yenu tumepunguzwa kazi mimi na mume wangu kutokana na mambo ya uchumi duniani naomba tuombeeni Mungu atupe kazi nyingine ili tuweze kulipa bills na madeni mengine
  mbarikiwe na Bwana.

 201. Shalom,
  My prayer request is to get a well paying job that i will be able to cater for my family well.
  for God to fill me with the holy spirit.
  For God to bless my marriage and to bless my husband with a well paying job.

 202. Mimi naitwa Evarest ninahitaji maombi yenu ninampango wa kufunga ndoa mwezi sept 2009,lakini nimekumbana ni vipingamizi vingi tata ndani ya familia,nimewashirikisha baadhi ya watumishi ili Mungu adhibitishe kuwa je nimpango wa Mungu kumuoa huy mchumba wangu,wakachukua muda wa maombi na Mungu akadhibitisha hilo,ila sasa kuna ndgu yangu ananiambia kuwa Mungu amekataa,sasa ninashindwa kuelewa Mungu huwa anajichanganya? na ananiambia siyo mpangowa Mungu na nimemuomba kama Mungu amesema hivyo je mke wangu atakuwa yupi,hanijibu,sasa ninachowaomba ni kunisaidia katiak Mamombi ili Mung afanye njia katika hilokwani nimemwambia Mungu nahitaji kuoa kwanninaenda kutimiza miaka 40 mwezi april mwaka huu sihitaji kukaa hivi nisije nikaangukia kwenye majaribu.
  Mungu awabariki sana,na kama siyo Mpango wa Mungu afanye njia nyingine ila nimemwambia Mungu nahitaji kuoa mwaka huu.

 203. Shalom wana wa Mungu, naomba maombi yenu mimi ni muimbaji nategemea kutoa kanda yangu, nahitaji upako na kibali kwa bwana. Mbarikiwe na Bwana Yesu.

 204. Ndugu Evarest,

  Suala la kuoa/kuolewa, kwa mtu ambaye anahitaji uthibitisho toka kwa Mungu, muhusika ndiye huthibitisha. Kutegemea watu wengine wakuulizie kwa Mungu kama ndivyo au sivyo ni rahisi kudanganywa kwa kuwa si kila mtu anayesema ni ‘Mungu kasema’ huwa anasema ukweli. Wengi wamedanganywa sana na kujikuta wameingia kwenye matatizo makubwa!

  Wewe umeona msichana, ukampenda na kujisikia kwamba anaweza kuwa mke wako, jambo la kufanya ni kupiga magoti mwenyewe na kumuomba Mungu. Suala gumu katika sehemu hii ni mtu kufahamu Mungu anapojibu maombi hayo. Uthibitisho usio na utata ni AMANI YA KRISTO. Ni kipimo mioyoni kwa watu wa Mungu!

  Kuwategemea watu watakuchanganya sana ndugu yangu!

  Kama umemuomba Mungu kwamba afanye njia katika hilo ni heri ukamuomba Mungu akuthibitishie wewe mwenyewe juu ya huyo mchumba.

  Jambo jingine ninaloshauri ni kwamba ni vema zaidi kuomba Mungu kabla ya kuingia katika uchumba ili mchumba anapotokea iwe ni matokeo ya maombi. Kuomba Mungu kabla ya kupata mchumba kutafanya mtu upate mchumba ambaye ndiye atakuwa mke wako. Kuingia uchumba na mtu kichwa kichwa unaweza jikuta umekuwa ni mtu wa kuchumbia na kuacha na hiyo siyo sifa njema.

  Omba Mungu akuthibitishie wewe mwenyewe. Mungu akikuthibitisha wewe mwenyewe kutakupa ujasiri wa kwenda mbele zake tena kumuuliza imekuwaje. Watu wengine wakikuthibitishia kila likitokea tatizo itabidi uwaambie wakuulizie tena kwa Mungu na huo utakuwa ni utumwa.

  Kama una mawasiliano na Mungu piga magoti, Mungu Baba yetu, atakujibu nawe utakuwa huru!

 205. Ninaomba sana mniombee kwa Mungu ili niweze kushinda vishawishi vya mwovu shetani. Nifuate imani thabiti ya wokovu ili niijue kweli nini, niondokane na taabu za dunia hii. Niache pombe na tamaa za kiduniani. Nipate kibanda changu niondokane na maisha ya kupanga, Nibariki ndoa yangu. Nawaombeni sana sala zenu ili nimshinde adui shetani na mitego yake yote.

 206. Ndugu Ishengoma,

  Hongera kwa uamuzi wako uliouchukuwa. Lakini ninapenda kukushauri kama ifuatavyo:

  Jambo la kufanya ili kuvishinda vishawishi vya Shetani ni kumkaribisha Yesu Moyoni mwako. Yesu akiingia moyoni tamaa za mwili zitakufa. Vitu ambavyo unaviona kama ni starehe kwa sasa utaviona kama taka taka.

  Neno la Mungu linasema hivi katika Tito 2:11-13 “Maana Neema ya Mungu iwaokowayo wanadamu wote imefunuliwa, nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia, tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu.

  Kwa hiyo hapa tunafundishwa wazi kwamba tamaa za dunia ni za KUKATAA. Ni uamuzi wa mtu kukataa. Na ukisha mpokea Yesu moyoni yeye atakuwezesha kushinda kama utakuwa mtiifu katika mafundisho yake Yesu.

  Katika kitabu cha Waefeso 6:13 tunasoma kwamba hivi: Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.

  Hapa pia tunafundiswa kwamba ili tuweze kumshinda adui shetani tunatakiwa kuvaa silaza za Mungu. Silaha hizi zi mabunduki na mabomu bali silaha za mambo ya rohoni kwa kuwa vita vya rohoni ni juu ya ulimwengu wa mapepo na wakuu wa ufalme wa giza.
  Silaha hizi za rohoni ni katika Waefeso 6:14 ambazo ni pamoja na Kweli kama mkanda, Haki kama dirii kifuani, Injili ya amani kama viatu miguuni, Imani kwa Yesu kama Ngao kwa ajili ya kuzima mishale ya adui shetani, Wokovu kama chepeo kichwani na Neno la Mungu kama Upanga. Silaha zote hizi zinapatikana baada ya mtu KUMWAMINI YESU na KUMKARIBISHA MOYONI.

  Kwa hiyo ndugu Ishengoma kufanikiwa kwako katika Mambo ya Mungu na kuushinda ulimwengu kunategemea sana uamuzi wako wewe mwenyewe maana suala la mtu kuokoka ni suala la uamuzi kutoka moyoni. Lakini kwa kuwa umeshaliona hitaji hilo nadhani hakuna kipingamizi tena zha kukufanya UAMUWE MOYONI mwako kumkaribisha Bwana Yesu.

  Baraka za mwilini ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba yako mwenyewe zitafuata bila shaka kwa sababu ukishaokoka utaweza kulinda hata pesa zako zisipotee kwa mambo yasiyo na faida kwako bali yamejaa hasara. Kubariki ndoa yako pia itakuwa ni matokeo ya AMANI utakayokuwa umeipata baada ya KUSIMAMA katika Wokovu. Bila Amani huwezi kubariki ndoa yako.

  Mungu wa Mbinguni na akusaidie unapofanya UAMUZI HUU SAHIHI!

  Amina.

 207. Ndugu ishengoma,
  kama ndugu John alivyosema, unamwitaji Yesu. Si tu kwa ajili ya kushinda dhambi, bali, kwanza kwa ajili ya kwenda mbinguni. Sote tumemkosea Mungu na twastahili Jehanamu ya Moto. Mungu kwa neema yake alikuwa mtu ktk utu wa Kristo, akalipa deni Yetu na hivyo hatudaiwi, dhambi zetu zimesamehewa na tunaelekea mbinguni.

  Yesu alipoondoka alituachi Roho Mtakatifu. Yeye ndiye anyetusaidia kushinda dhambi na kuishi maisha ya ukiri wa neema ya Kristo! Huyu Roho ni kwa ajili ya wanafunzi wa Yesu tu. Kwa hiyo unahitaji Msaada wa Roho wa Mungu. Pia unahitaji fellowship yenye kumpenda Mungu, ili ukue kiroho.

  Kaa utafakari maana huu ni uamuzi utakaoathiri maisha yako, marafiki, n.k. Mungu akusaidie ufanye maamuzi sahihi.

 208. SHALOM WAPENDWA,
  nina washukuruni sana kwani maombi yenu yamekuwa
  ngao kwenye familia yetu zaidi ni kupitia mama yangu ambaye alikuwa mgonjwa kwani alikuwa hana hamu ya kula,vichomi sehemu za mbavu,miguu kufa ganzi,kifua na kusikia kizunguzungu pia kukata tamaa, lakini tangia nilipotuma ujumbe wa msaada wa maombi nimemuona Mungu akifanya mabadiliko pia ninaamini kupitia pasaka hii ataondokana na magonjwa yote.

  kwani kwa muendelezo wa maombi ninaamini kwakupigwa kwa yesu msalabani mama yangu atapona kabisa.

  pia ninaomba tuombee pia mvua ziweze kunyesha kwani kwa mwaka huu imekuwa tabu haswa maeneo kama ya wakulima ni tabu kwa msimu huu haswa wanaotegemea mvua na sote kwa ujumla kwani kwa sasa kumekuwa na shida ya mvua hadi hali inayoashiria kuwepo kwa njaa nchini mwetu.

  MWENYENZI MUNGU AWASHINDIE YOTE.
  AMINA.

 209. MUNGU WANGU NAKUOMBA UNIJALIE MIMI NA MUME WANGU NA FAMILIA YANGU TUWEZE KUJENGA NYUMBA YETU PIA NISAIDIE NIWE NA HEKIMA, UJASIRI, UVUMILIVU KATIKA NDOA YANGU. NIJALIE NIPATE KAZI NZURI YENYE KIPATO CHA KUTOSHA.NDUGU ZANGU NIOMBEENI NAMI NIWE NA MAFANIKIO.

 210. Praise the Lord watu wa Mungu,
  mi naomba kuwashirikisha mniombee nitulie katika kazi,hasira ipate kukoma katika maisha yangu maana nakua na hasira mara nyingi, na Neno la BWANA linasema hasira hukaa kifuani pa mpumbavu, pia naomba mniombee Mungu mwenye NGUVU anipatie Mume.

 211. I greet you all in the Name of Christ Jesus of Nazareth, naomba tena wapendwa katika Christo tuombe ili mambo ya uchumi wa dunia ikue normal, usiyumbe hii yote ni uongo wa ibilisi, sababu anajua we like money so much, basi katukamatia hapo lakini tuombeni jamani Mungu hajatuweka duniani tupate wakati mgumu, anatupenda sana ivyo atafutilia mbali ayo mambo ya uongo wa shetani ati WORLD ECONOMIC CRISIS, mi naenda kinyume kwanza na hiyo statement maana ata Fedha na Dhahabu ni mali za Bwana ivyo atatupatia vile tunataka. mbarikiwe sana

 212. Naomba mniombee niweze kurudi kumtumikia bwana kwani kwa sasa hata kanisani mahudhuri yangu yapo chini sana, watu wa mungu naomba mniombee sijui ni nini kinachonifunga hivyo mungu awabariki.

 213. Ndg. Maisha Mvungi,
  Chukua hatua ya kurudi bila kuchelewa, maadam umeona haja ya kufanya hivyo! Mkaribie sana Bwana naye atakukaribia, na hakuna kitakachokufunga!

  Ndg Regina maganga,
  Kwa kukaa sawasawa ktk Neno la Mungu pamoja na maombi, utaifanikisha njia yako, ikiwa ni pamoja na utulivu ktk kazi na kupata mume wako. Pia hasira haitapata nguvu kwani tunda la roho ambalo ni upendo,furaha,amani,uvumilivu n.k litachukuwa nafasi zaidi ndani yako.

 214. Tuombeeni ajili ya kazi za Mungu tunazo zifanya zikiwa ngumu, Bila msaada wa maombi kutoka wachaguliwa na watakatifu wa Mungu sisi atuwezi lolote. Tuko na mikutano ya Injili: Bujumbura, Kongo, Uganda, Tanzania Kigoma, Dar, Arusha. Tunamalizia Nairobi.
  Wote watakaye soma hayo, basi mtuhombeeni. http://www.afrikahjelpen.com, mahandishi yako kwa luga la Ki norvigien. NASHUKURU…
  Mchaguliwa:
  Pastor Ev. Missionary;
  Nundu K. S. Josue
  + 47 9888 2390.
  DOVREVEGEN 7340 OPPDAL/
  KING DOM OF NORWAY
  Norway

 215. Bwana yesu asifiwe,mungu azidi kuwatia nguvu katika kazi yake.
  Mi naombeni tusaidiane kuniombea naitaji kupata kiu ya maombi na kusoma neno la mungu,nina imani nikiweza hivi nitaweza kusimama kwa miguu yangu.
  Mungu azidi kutupa rehema yake tushinde majaribu.

 216. Wapendwa katika Kristo, minefurahi kusoma hii website na kuona jinsi watu wanavyomtukuza Mungu kwa Njia ya barua pepe na kuchota baraka tele. Ninawaombea na kuwapongeza wale wote wanaochulua mida yao kutoa huduma hii.Bwana Yesu apewe sifa. Nina mengi moyoni mwangu yanayonitenga na Mungu. Ninaomba sana sala zenu niweze kupata amani ya rohoni. Ni katika kuwa na amani nitasamehe, vumilia na kubeba msalaba wangu na kumfuata Yesu.Ninaomba roho wa Mungu awafunulie shida zangu ili katika kuomba mkapate kugusa mahitaji yangu.
  Ahimidiwe Bwana wa Majeshi.

 217. Ndugu wapendwa Bwana Asifiwe. Siku za karibuni nimebadilishwa kazi niliyokuwa naifanya bila ya kuambiwa rasmi nahamia kwenye kazi ipi nyingine. Ninaamini hili limefanyika kwa sababu nimekuwa namuomba Mungu kwa muda watakribani miaka miwili anipe baraka, anipandishe daraja ya kazi na aniepushe na maovu yote. Baada ya muda nikapata fununu kuwa huenda nikapewa kazi kubwa zaidi. Kwa hiyo nilipobadilishwa nikajua maombi yangu yamejibiwa. Imepita mwezi tangu nibadilishwe lakini bado sijaambiwa rasmi juu ya kazi hiyo mpya japokuwa upo uvumi hapa na pale. Nimeendelea na maombi ya kumuomba Mungu nifanikiwe kuipata hii kazi mpya.Ninaamini kuwa Mungu ni mwaminifu nitaipata hiyo kazi. Pamoja na hayo Ndugu zangu ninawaomba tuungane katika maombi tumuombe Mungu mafanikio katika hilo na ulinzi wa malaika wake na zindiko la damu ya Yesu ili shetani asiibe wala kuchelewesha hiyo kazi ambayo tayari kiimani katika ulimwengu waroho Mungu amenikubalia nikisubiri manifestation yake katika ulimwengu wa mwili wa uhalisia.Mbarikiwe sana. Amen.

 218. Mi naomba mniombee ili nikisoma neno nielewe. Na pia nipate mchumba aliyeokoka na mwenye kazi. Na Mungu aokoe ndugu zangu na kuibadilisha familia yetu. Na Mungu awaongezee wazazi wangu miaka ya kuishi.

 219. Bwana Yesu asifiwe wapendwa,

  Mi naomba tuiombee nchi yetu ya Tanzania amani na viongozi wetu hekima katika uongozi na maamuzi wanayoyafanya; Pia viongozi walio katika ngazi za juu kuongoza kwa kusudi la Mungu (yaani wawe na ofu ya Mungu) siyo kuifanya nchi mali yao na kufanya lile wanalojisikia na kujijazia mali wakati wengi wa watanzania wakiaangamia . Kwani tunakoelekea ni kubaya sana. Mungu awabariki wapendwa

 220. Bwana Yesu Asifiwe Patrick,

  Hongera kwa kupandishwa daraja kazini, katika ulimwengu wa roho wewe umeisha pata kazi hiyo, wala huitaji kuomba ila ni kushukuru kila wakati kwani tayari kazi ni yako, ila kuendelea kuomba kitu ambacho Mungu ameisha kupa shetani atajipenyeza na kukwambia wala hujapandishwa bali ulikuwa uvumi. tangu sasa aanza kushukuru kwa kupandishwa cheo. Mungu akupe imani katika kuamini kwako. Amen

 221. Bwana Yesu asifiwe. Mi ni msichana niliyeokoka naomba mniombee nasumbuliwa na tamaa mbaya. Mi tangu sijawahi kupenda kuwa karibu na wanaume lakini sa hivi hiyo roho inanisumbua na pia nimekuwa nikiwaza mapenzi tu kwa muda mwingi japo tangu kukua kwangu sijawahi kufanya mambo kama hayo. Naomba mniombee na pia mnishauri jinsi ya kufanya ili nishinde. Na pia mniombee ili nipate mchumba aliyeokoka na mwenye kazi. Asante kwa maombi yenu.

 222. MAOMBI YENU KWANGU NI MUHIMU SANA ILI NIWEZE KUSIMAMA KUSUDI LA MUNGU NDANI YANGU LIWEZE KULINDWA PIA MIPANGO YANGU YA CHUO INAYOENDELEA IWEZE KUFANIKIWA ASANTENI, MUNGU AWABARIKI SANA

 223. Kaka John Paul Mungu akubariki sana kwa msaada ambao Roho Mtakatifu kakutumia kumsaidia ndugu Evarest,mimi pia nimesaidika sana!mimi nilimpenda dada mmoja,ameokoka vizuri sana(japo wakati tunakutana sikua nafahamu hayo).nilimweleza na tukakubaliana.nilimwomba Mungu na kutaka uthibitisho katika mambo flani na namshukuru Mungu kwamba nilithibitishiwa hilo lakini nikataka tena uthibitisho kwa Baba yangu wa kiroho(mchungaji wangu) na baada ya muda nilionana nae na akasema anasikia amani tu na swala langu.nina amani sana na uhakika asilimia 100 kua niko na mtu sahihi kua mke wangu.nimekusudia kua na uchumba safi,hatutachafua malazi na tunaomba Mungu atufanikishe katika mipango yetu.mbali na njia nyingine nilipata uhakika kwa kua na amani moyoni.miezi miwili au mitatu ijayo tutatoa mahari naomba maombi yenu katika hili pia! Jambo la pili nisaidieni ndugu zangu.nasemwa sana kwa tabia mbaya(hasa uzinzi)lakini mi siko hivo.mwanzoni sikujali nikidhani kwa vile mimi naujua ukweli basi hamna shida ila tatizo linakua hata sijui nafanyaje.nilikua na marafiki wengi wasichana nikawa mbali nao nikidhani itasaidia lakini wapi.nina uhakika na kile Mungu kanambia kuhusu relationship nilonayo lakini kama binadamu mara nyingine hupata mashaka.nisaidieni nifanyeje!Mbarikiwe

 224. Bwana Yesu asifiwe,mimi ni msichana niliyeokoka na ninampenda YESU sana, naomba mniombee familia yangu iondokane na majaribu ya shetani, shetani ameiandama sana familia yangu. Pia naomba mniombee kazi yangu iendelee salama na nione mafanikio katika kazi ya mikono yangu na naomba Mungu aibariki. Pia namshukuru Mungu kwa kunipatia mchumba niliyemuomba kwa muda mrefu, anayemjua Mungu na kaokoka kama nilivyo muomba Mungu naomba muniweke kwenye maombi mimi na mchumba wangu; shetani asipate nafasi kabisa katika uchumba wetu najua palipo wana wa Mungu shetani anapenda kujiinua ila naomba akashindwe katika jina la Yesu aliye hai. Asante kwa maombi yenu Mungu azidi kuwa bariki

 225. Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 24, nilizaliwa tabora na hivi sasa naishi Marekani. Napenda kuomba kwa watu wa Mungu waniombee kwasababu nina majaribu mengi sana yanayo nisonga. Vile vile ningeomba mniombee maitaji haya : napenda Mungu abariki maisha yangu, anipe miaka mingi ya kuishi, aniepushe na majaribu, na vile vile nina wazo la kuwa na mke, naomba Mungu anipe mke mwema.

  Asanteni sana.

 226. Haleluya!
  Watu wa mungu Bwana apewe sifa. Baada ya kupotea kwa muda sasa nim erejea na ninamshukuru JEHOVA kuwa mimi ni mzima tena wa afya kabisa. Nimekuwa kimya kwa mda kutokana na kuwa eneo ambalo huduma hii ya i-net ni ngumu kidogo.

  Dada DORA! Nafurahi kusikia kuwa Mungu kafanya muujiza huo kwako kwa kukupa mchumba. najua kama BWANA amekupa atawalinda wala usiwe na hofu. Tatizo siku zote linakuwa kwa mwanadamu, hivyo wewe uwe tuu na utayari wa kujitunza kwani MUNGU anafanya kazi na watakatifu wake.
  Hivyo utakatifu ndicho kitu kitakachokufanya wewe undelee kuwa na mahusiano na MUNGU na wala si kitu kingine.

  Pili swala la familia kuondokana na majaribu,………
  Na hii ningependa pia nikukumbusshe wewe na ndugu Elias Mariste kuwa usitegemee hata siku moja kuwa mtu aliyeokoka majaribu yataisha kwake hii ni kwasababu tuu kuwa MAJARIBU NI MBOLEA YA MKRISTO KUKUA KIROHO.
  Jambo la maana ni kujitambua kama mteule na uwe mtu mwenye Neno kwani ni vema pia tukumbuke kuwa Kristo mwenyewe aliyashinda majaribu kwa kutumia neno.
  Kwa hiyo MUHIMU: Jukumu letu sisi ni kuwaombea muwe na kiu ya NENO la MUNGU ili liwawezeshe kushinda majaribu na si vinhginevyo kwani majaribu ni un-kwepabo kwa wanafunzi wa YESU kama ELIAS NA DORA.
  Basi MUNGU wangu awalinde mnooooooooooo. someni yohana 14:25-29.
  Salamu za upendeleo kwa Dada DEAR na MERY KILEO.
  MUNGU WANGU AWAPAKATE

 227. Wapendwa ktk bwana,naomba mniombee niweze kumtolea Mungu fungu la kumi na sadaka za shukrani, pia mniombee kupata msamaha wa madeni makubwa yanayonisonga kwa Mungu na wanadamu, wapendwa hebu pia msisahau kumshukuru kwa ajili yangu, ni mengi mema ametenda na anaendelea kutenda ktk maisha yangu, mwisho nahitaji gari; afya njema kwa familia na kuimudu vema kazi yangu ya ubenk aliyonipa na kupitia hiyo nimtolee na kusaidia watumishi. Mungu awabariki!

 228. Naomba sana mnisaidie kuomba kwani nina magonjwa yanayonisumbua sana na ninahitaji kuponywa katika jina la Yesu na ninahitaji kupata mtoto, najua msaada wenu wa maombi utanibairiki na Mungu atajibu maombi maana hakuna linashindikana kwake.

 229. Naamini maandiko haya,
  Luka 1;37 kwa Mungu yote yawezekana
  Rum 8;37 Sisi ni washindi na zaidi ya kushinda kwa yeye aliyetupenda.
  Math 7;7 ombeni nanyi mtapewa,tafuteni nanyi mtaona, bisheni nayi mtafunguliwa

  Ila, ili upate kukiri maandiko haya na kupokea msaada toka kwa Bwana ni lazima kwanza umkiri Bwana kuwa mwokozi wako.Biblia inasema watu ‘wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa’, [Hosea 4:6]. Maarifa biblia inayosema ni ufunuo mtu anaopewa akishaokoka. Ukiokoka kila kifungo kinaondoka: magonjwa,madeni,mikosi na mabalaa yote yanafagiliwa na uwepo wa Mungu.Sijawahi kuona panya wanaishi na paka nyumba moja bila mmoja [hasa panya-shetani]kufunga virago na kumuachia mbabe paka, Yesu, atawale nyumba.Mwili wako ni hekalu la roho mtakatifu na haiwezekani ukaandamwa na mizigo maana bosi wako Yesu amesema, njoo nikupumzishe math 1;28.

 230. NINGEPENDA TUOMBE MUNGU ATUTIE NGUVU TUZIDI KUKAA NA KUDUMU KATIKA MAOMBI

 231. Dora sisi tutakuombea kuhusu kazi na hata kuhusu nguvu za shetani, lakini nataka kukwambia jambo moja,(waefeso 6;11-18) yakwamba wokovu ni vita, hivyo vaa silaha, huyo shetani anayeiandama familia yako, kwanza ana njia aliyoingilia, pili dawa, nikufanya yafuatayo kwanza jitakase, pili zivunje hizo nguvu kwa maombi, ikibidi ufunge dadayangu huo ndio wokovu, hebu simama kwa zamu yako umwone YESU anavyotenda, yote yataisha.
  adam mpunga

 232. Bwana yesu asifiwe sana wependwa
  around for quiet sometimes

  ninaamini Mungu anaweza yote na yeye ayajua mahitaji yetu na hakuna linalo mshinda kwahio wa pendwa naomba mnisaidie katika maombi kwa sababu maombi ya mtu mmoja yana fukuza mapepo elfu lakini yawawili sio elfu mbili bali elfu kumi kwahiyo naomba mnisaidie naomba Mungu anisimamishe Kiukamilifu PLEASE. katika njia zake kwani njia zangu truly speaking hazimpendezi Yeye alie niumba. Thank you kwa umoja

 233. Mpendwa Isaac,

  Ni kweli kwamba Mungu anaweza yote lakini kwa suala la wokovu kinachohitajika ni mtu mwenyewe kuchukuwa hatua na kugeuka.

  Kwa kuwa umeshafahamu kwamba njia zako hazimpendezi Mungu hiyo tayari ni neema ya Mungu na yawezekana ni kwa sababu ya maombi ya watu kwamba Mungu akufungue macho ya rohoni uone jinsi njia zako hazimpendezi Mungu. Si kila mtu ambaye hajaokoka huona hivyo. Wengine husema Mungu ni wa rehema kwa hiyo atasamehe tu! Wengine husema watu wote watakwenda mbinguni kwa sababu shetani hatajaumba chochote! Wengine husema Mungu atapima mizani kuona kinachozidi kati ya wema na uovu! Mawazo ya namna hii yote ni kinyume na neno la Mungu na watu wenye kuamini mawazo haya binafsi hujikuta wakiendelea kutenda maovu kwa sababu macho ya mioyo yao yametiwa giza na mioyo yao imetiwa ganzi ili wasiweze kuuona wema wa Mungu na kuutammbuwa ubaya wa matendo na njia zao.

  Mungu amekupa neema hiyo ambayo ni hatua muhimu sana katika kuupokea wokovu. Biblia inasema tukisema hatuna dhambi twajidanganya wenyewe na wala kweli haimo ndani yetu na tukisema hatukutenda dhambi twamfanya yeye (Yesu) kuwa muongo wala neno lake halimo ndani yetu BALI Tukiziungama dhambi zetu yeye (Yesu) ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote. 1Yohana 1:8-10.

  Kuungama kunakosemwa hapa si kule kutaja dhambi zako kwa kiongozi wa dini halafu mnaagana kwamba mtaonana jumapili inayofuata wakati ukija kuungama tena BALI ni kutubu dhambi na kumkaribisha Yesu ili yeye ndiye awe kiongozi wa Maisha. Ni kutubu dhambi na kugeuza uelekeo kwa kumkabidhi maisha Yesu na kuchukuwa uamuzi wa KUTO-kutenda tena mambo maovu ambayo sasa huwa ni kama kwa MAKUSUDI. Yesu alipokuwa anawaaga watu aliowasamehe dhambi alikuwa anawaambia “WASITENDE DHAMBI TENA” Yohana 8:11; Yohana 5:14 nk.

  Jambo unalotakiwa kufanya sasa ni kutubu dhambi zako kwa Mungu kupitia Yesu kristo na kisha kumkaribisha moyoni mwako akuongoze. Ni jambo la kujikana. Ni uamuzi. Hakuna malaika atayekuja kukushika mkono kukuzuia usiende kwenye maovu lakini hiyo SAUTI unayosikia ndani yako ikikuambia kwamba NJIA ZAKO HAZIMPENDEZI ALIYEKUUMBA ndiyo sauti yenyewe ya ROHO. ITII SAUTI HIYO KWA KUTUBU DHAMBI ZAKO NA KWA HIYO UTAKUWA UMEUPOKEA WOKOVU.

  Soma somo la MAANA YA WOKOVU kwa utulivu (linapatikana kwa kuingia pale juu kabisa kulia kwa “Home” palipoandikwa MAANA YA WOKOVU) na utafute kanisa lililokaribu nawe wanaoamini na wanafundisha WOKOVU.

  Mungu akutangulie katika uamuzi huo ulio MGUMU lakini SAHIHI.

 234. wapenda shalom,

  napenda kushilikiana nanyi kuomba ili nifanikiwe kupata kazi mahali pengine na niweze kumalizia kujenga nyumba yetu,niweze kuendelea na masters.na pia niwe na busara na hekima zaidi

 235. Bwana Asifiwe! wapendwa hakika kazi yenu ni njema sana Bwana awabariki. naomba tushirikiane katika maombi tumwombee mme wangu aokolewe,akae na kudumu kwenye mafundisho,awe na hofu ya Mungu.naamini tutaomba pamoja.Amen.

 236. Bwana Yesu apewe sifa na utukufu
  wapendwa katika jina la Yesu nawapeni sifa kwa kazi nzito ya kumtumikia Mungu natamani hata ningekuwa mimi
  Yesu alisema kabla hamjaomba ninajua hitaji lenu na hakuna lisilowezekana kwa Mungu
  nina hitaji langu nalileta mbele yenu kwa kusaidiana na Roho mtakatifu nina mchumba na tumeishi naye miaka karibu sita lakini shetani ameingilia uchumba wetu naomba kwa Mungu kwa kusaidiwa na roho mtakatifu mapenzi yake yatimie kama mwanzo. Amina
  Mbarikiwe sana watumishi wa redio Safina na Mungu awatie nguvu

 237. Bwana Asifiwe!! nipo katika wakati mgumu sana naitaji maombi yenu,ofisini kwetu wanataka kupunguza watu kazini,pili mme wangu haeleweki amekuwa mtu wa ahadi zisizo za kweli nafikia hatua najuta kuolewa nae kanisani amekuwa mvivu kwenda,hana hofu ya Mungu.Mchungaji na wapendwa wote nahitaji maombi yenu nimekata tamaa sina amani tena naomba bwana anipe amani na uvumilivu nizidi kumuishia yeye amgeuze mme wangu kama alivyomgeuza Sauli.
  AMEN.

 238. Pole dada Cathy,
  Mungu akutie nguvu katika magumu unayopitia. Mwamini tu yeye na tuko pamoja.

  Kuhusu kupunguza kazi, mtegemee yeye (Phil 4:17). Ni rahisi kwa sisi wanadamu kuomba mambo magumu yatuepuke, lakini tusisahau “mapenzi yako yatimizwe”. Kwa hiyo tuombe pamoja alichopanga Mungu pekee ndicho kisimame. Kama yeye anataka ubaki hapo, basi hilo ndilo lisimame, na kama amekuandalia mahali pengine, basi hilo lisimame. Tunamwomba Baba akupe nguvu kusimama, bila kujali kilicho mbele yako.

  Pili kuhusu mume, pole sana! Kuna maswali ambayo ningependa kuuliza:
  1. Umemwuliza kwa nini amekuwa mvivu kwenda kanisani?
  2. Je ameokoka au la?

  Mwisho, usikate tamaa dada yangu. Mungu aliyesimamisha Jua, aliyegawa bahari na mengine mengi anaweza kabisa kumbadili mumeo.

  Mungu akutie nguvu!

 239. Ndugu Regina,

  Pole kwa hilo pito unalopitia. Lakini pamoja na pole hiyo mimi naomba kukushauri namna hii:

  Umeandika umeishi na mchumba huyo kwa miaka karibu sita lakini hujafafanua ‘uliishi naye’ kwa namna gani. Kama mliishi kama mke na mume huku mkifikiri kwamba ni wachumba tu hapo pana tatizo. Lakini kama mlikuwa ni wachumba tu na hamkuwa na mahusiano mengine zaidi ya kuomba Mungu awafanikishe mfikie hatua ya kuoana hapo inabidi ushukuru Mungu. Mchumba si mume. Kama wewe umekuwa ukimuomba Mungu kwamba mapenzi yake yatimizwe inawezekana yametimizwa kwa namna ili kuepusha matatizo ambayo yangetokea kama mgefikia hatua ya kufunga ndoa.

  Ninalosisitiza hapa ni kwamba inabidi kwanza kujichunguza mtu uko upande gani kabla ya kuanza kumuomba Mungu. Kuna wakati mwingine tunahitaji kutubu mbele za Mungu kutokana na mambo ambayo yawezekana tuliyaingia ki-makosa. Hapo ni mahali pa kuomba rehema za Mungu kwanza na kisha kuanza upya kwa kusikiliza uongozi wa Mungu.

  Kuharibika kwa uchumba si lazima shetani. Mungu pia anaweza kuingilia kati ili kumlinda mtu wake. Pia binaadamu mwenyewe anaweza akaharibu. Kwa hiyo nakuanchia changamoto kwamba inabidi ujichunguze mwenyewe kwa kuangalia vigezo hivi:

  1. Je, uchumba huo ulikuwa katika misingi ya utakatifu?
  2. Je, kuharibika huko ni Mungu, Shetani, au mmoja kati yenu aliyeharibu?

  Ukishafahamu kuhusu mambo hayo ndipo unaweza kuchukuwa hatua sahihi kama ni kuombea uchumba huo huo au nikutubu kwanza.

  Unaweza kusoma zaidi kuhusu kuishi na mchumba katika mada ya ‘Je,kuishi na mchumba ni dhambi?” inayopatikana katika ukurasa wa Maswali ambapo wasomaji wengi walichangia kuhusu hili.

  Mungu akuongoze.

 240. JOHN PAUL
  Mungu Akubariki sana kwa Ushauri wako or mwelekezo
  kweli Mungu apewe sifa kwani I was empty but his love does not run out. I was weary but His touch has restored my life

  It’s not that i wasn’t a christian
  ofcourse I am. a born again.
  lakini na hali hii ya ujana shetani anapenda kujiingiza sana katikati yangu na Mungu mara kwa mara kupitia njia hii aidha ile lakini mara tena Mungu akubariki kwa mwelekezo wako and thanks be to God I’ve the light again!!!

 241. Bwana Yesu asifiwe sana. Nina mwanangu anayeitwa Ronald aliugua sana vidonda vya tumbo na akafanyiwa operesheni mara mbili. kwa sasa hivi anaendelea vizuri ila tatizo amepoteza kumbukumbu (memory). naomba watumishi wa Mungu mumuombee ili kumbukumbu zake zirudi haraka aweze kuendelea na masomo yake ya kidato cha Tano mchepuo wa sayansi (PCB)

 242. Bwana Yesu asife,wapendwa watumishi wa wa MUNGU.Dada yangu (Furahini) pekee na wa mwisho ktk watoto 7 wa baba na mama yangu(wote 2 wameitwa mbinguni)anahali ya kuchanganyikiwa kwa muda mrefu.Pia kijana wangu Joseph alipata shida ya kutosikia vizuri,baada ya kumaliza masomo ya kidato cha 4 mwaka 2002 mpaka sasa hajapata usikivu mzuri,japo yupo chuo Kikuu.Nisaidieni kuwaombee,kupata kiini kama zipo laana za Ukoo ili wafunguliwe na kupokee uponyaji.Mbarikiwe.

 243. Bwana asifiwe!
  Asante kwa ushirikiano na kunitia moyo, nakujibu kaka yangu Steve:

  1.mume wangu ameokoka na tumefunga ndoa tukiwa wote tumeokoka tuko moto.
  2.nimemuuliza sababu ya kuwa mvivu kwenda kanisani anasema amebanwa na kazi, maisha magumu.
  ila sijachoka nazidi kumwombea Bwana ambadilishe.
  Mungu awabariki!

 244. Bwana asifiwe;
  Mimi ni Mwajiriwa wa VETA Dodoma, Nimeomba uhamisho wa kumfuata mume wangu ambaye alihamishiwa Dar es salaam, lakini bahati mbaya hadi leo sijajibiwa barua yangu. Naomba tushirikiane kwa maombi kwa ajili ya kujibiwa barua yangu. Pia nimeandika maombi ya kazi Ministry of Constitutional Affairs and Justice naomba mnisaidie kwa maombi niweze kupata kazi. mbarikiwe sana na Mungu awatangulie katika shughuli zenu za kila siku.

 245. Bwana Yesu Apewe sifa na utukufu,

  Poleni kwa kazi za Mungu
  nina ombi langu mimi ninaomba kwa kushirikiana na radio safina naomba kwa maombezi ya aliye juu, kwa maana imeandikwa kwamba utamwacha baba yako na mama yako na utaambatana na mume wako
  kupitia kwenu naomba Mungu anipe mume bora kutoka kwake aliye juu.
  Mungu awabariki na kuwatia nguvu Amine

 246. Bwana yesu apewe sifa!
  nina maombi mengi,lakini kubwa zaidi ni kwamba bibi yangu mzaa mama ni mgonjwa sana alipelekwa hospitalini kufanyiwa uchunguzi wa kidaktari na akakutikana ana ugonjwa wa kansa ya ini na ilijulikana baada ya kuwa imeshasambaa mwilini hivyo haina tena tiba na badala yake arudi nyumbani tu apewechakula ale na dawa za kutuliza maumivu kwa hiyo maana yake yeye asubiri kufa tu.yani amevimba miguu sana na sasa hivi mikono nayo imeanza kuvimba jamani naombeni maombi kwa ajili yake na familia yake pia.yeye binafsi ni muislam na anaishi mwanga kilimanjaro,huko upareni.
  Mungu awabariki,
  Amen.

 247. Bwana asifiwe sana. Namwomba Mungu.
  1. niweze kumaliza masomo yangu na kufauli vizuri katika mchepuo wa CIMA.
  2. Mungu anijalie mwanamme niliye naye awe mume wangu wa NDOA, tupendane na tuwe na familia.
  3. Mungu awajalie wote waombao kwa imani.

 248. Bwana Yesu asifiwe.Naomba maombi yenu nipate viza ya italy mwezi wa 8 ili nikaungane na mme wangu Italy na nikapate kazi.Mungu wetu ni Mungu mwema kwetu na ndiye anayetuwazia mema kila wakati.Mungu awajalie kila mliombalo.Amen.

 249. Dada Lulu,

  Ni kweli kabisa Mungu husikia maombi kwa wale wamuombao. Lakini kumuomba huko lazima kuendane na mapenzi yake kwa kuwa Mungu ni Mungu wa utaratibu na ili kuweza kupokea kutoka kwake ni lazima kufuata taratibu zake.

  Pamoja na mahitaji yako mengine uliyotaja hapa mimi nimeguswa na hitaji la “mwanamme uliyenaye awe Mume wako wa ndoa”!

  Yawezekana nikawa nimekuelewa vibaya, lakini mimi nilichoelewa hapo ni kwamba tayari unaishi na mwanamme. Lakini mwanamme huyo unayeishi naye hamkufunga ndoa na sasa unahitaji kwamba muweze kufunga ndoa. Kama nilivyokuelewa ni sawa, basi wewe unachohitaji si maombi bali ushauri kwanza.[Ninasema hivyo kwa sababu ili maombi kwa Mungu yaweze kuleta matokeo ni lazima kufuata taratibu za Mungu wa Yesu Kristo ambaye wewe pia unapeleka mahitaji yako haya kwake!]

  Kama hali iko hivyo sitakushauri kwanza hadi tukubaliane kwamba nilivyokuelewa ndivyo ilivyo. Na kama nimekuelewa tofauti na hali ilivyo ninaomba unisamehe!!

  Ningefurahi sana kama utarudi tena ili kukubaliana au kutokukubaliana na nilivyokuelewa ili niandike kile nilicho nacho ambacho kinaweza kuwa ni ushauri kwako na kwa mwingine mwenye hitaji lenye mazingira kama ya hitaji lako.

 250. Bwana Yesu Asifiwe. Wapendwa katika Kristo, naomba mnisaidie kwa maombi ili niweze kununua nyumba ninayoishi. Mwenye nyumba yuko tayari kuniuzia lakini uwezo wangu ni mdogo. Najua, kwa Bwana yote yawezekana. Kwa maombi yenu na yangu, Bwana atajibu. Amani ya Bwana ipitiyo fahamu zote ikae nanyi daima.

 251. Nahitaji maombi wapendwa napitia hali ngumu sana kifedha na mimi nasoma najilipia ada mwenyewe sasa naona mambo magumu Mungu awabarik.
  Dear

 252. Wapendwa , nahitaji maombi kwa mambo yafuatayo;
  1. Mimi ninaishi Lindi mume wangu alihamishiwa Tanga mwaka miaka 3 ilyopita, nilikosa nafasi Tanga , nayeye pia yuko tayari kurudi Lindi , kuna ugumu wa kibinadamu unaendelea , wameahidi kumrudisha , na mara wanageuka. Naomba ahamishwe na kurudishwa Lindi.
  2.Mtoto wangu wa kiume (kulwa) ana alegy , mafua hayaishi na hayatoki nje huwa yanatulia tu. na najua Mungu wetu hashindwi jambo
  MUNGU AWABARIKI.

 253. Shalom wapendwa,
  Mi naomba kuuliza kama kuna mtu/watu ambao wanaoombea haya mahitaji huku kwenye thread ya maombi? Maana mimi leo ndo nafungua na ninakutana na mahitaji ambayo mengi yahahitaji urgent prayers.

 254. Mpendwa Noela,

  Strictly Gospel ina mtandao wa wanamaombi ambao huombea mahitaji haya ambao pia hufanya maombi kwa kufunga.

  Vile vile mtu ye yote mwenye mzigo wa maombi anapoona hitaji la mtu hapa na kuliombea kwa mzigo tayari huwa ameshafanya utumishi. Tunaamini wako wengi pia ambao hufanya maombi haya kwa mzigo. Na hii ndiyo sababu ya kuyaruhusu maombi haya hadharani ili kila mtu atakayeguswa na hitaji la mtu alipeleke mbele za Mungu kwa kuwa sisi sote ni viungo katika mwili mmoja – Kristo!

  Pia kuna utaratibu ambao SG huwasiliana na wenye mahitaji mbali mbali ambao walituma maombi yao ili kuweza kufahamu wanavyoendelea. Mawasiliano haya hufanyika kwa email. Inawezekana pia mtu akawa aliweka maombi hapa lakini hajaweza kuandikiwa email yoyote kutoka SG hii ni kutokana na wingi wa majukumu. Lakini kama mtu hajapata ujumbe wowote kutoka SG hiyo haina maana kwamba hitaji lake halijashughulikiwa. Kwa hiyo hata kama wewe, uliyeleta mahitaji yako hapa, hutapata email yoyote kutoka SG jambo la kuzingatia ni kwamba MAOMBI YAKO YANAFANYIWA KAZI, tena kwa mzigo.

  Strictly Gospel ni familia kubwa na kila anayetutembelea tayari huwa ameshakuwa mwanafamilia!

 255. Mungu awabariki kwa kuifanya kazi ya Mungu kwa bidii. Ni vizuri sana kuwa na wana maombi ambao specifically wanahusika na hii thread ya maombi. Maana mtu kama mimi ni jana tu ndo nimeiona.

 256. Mpendwa Dear,
  Umesema tukuombee upate fedha ya kujilipia masomo.Tunakuombea.
  Naomba unipe namba yako ya simu kwa msaada zaidi.

  Jehova Jire ndiye mpaji wetu!

  Ubarikiwe!

  Martin.

 257. Bwana yesu asifiwe wapendwa,mimi ndio leo nimekutana na hii website,namshukuru Mungu kunikutanisha nayo,Naomba mniombee naumwa tumbo na Mgongo,nimekwenda hospital mara nyingi tatizo halionekani,pia nina tatizo la kuota ndoto mbaya,naomba mniombee nipate mtoto nina miaka miwili kwenye ndoa sasa.nimeoka

 258. Let us not be “weary in well-doing,” or discouraged in the pursuit of holiness. Let us, like Moses, go to the Rock of Horeb–and God says to us what He said to him, “You will find me waiting for you there” (Ex 17:6 NEB).surely is waiting for you to pray for me to have the good leaders in our place for his Glory.(Church and Government)
  Celestina.

 259. Dada Adelina,
  Umechukua hatua gani baada ya kuona hospitali hawaoni chochote? Kuna watumishi wa Mungu umewaona ili kumlilia Mungu na kutafuta solution ya tatizo hilo?

 260. Asante kaka Steve kwa swali lako,nimeshirikisha watumishi kuniombea,napia wakati mwingine naombewa kanisani,nikiwa naombewa wakati mwingine tumbo linatetemeka sana na wakati mwingine nguvu za giza zinajidhihirisha kwani huwa nadondoka chini na kupiga kelele nahisi nasumbuliwa na nguvu za giza,nimeanza kuumwa toka mwaka jana mwezi wa kwanza.naendelea na Maombi na kushirikisha watumishi kuniombea.Naamini Mungu atanifungua.Amen

 261. Vema,
  Ni vizuri kabla ya kukemea nguvu za giza kuangalia kama kuna kitu chochote au kifungo fulani ambacho kinatoa uhalali kwazo kukutesa. Kama kitu hicho hakijaondoka, kuna uwezekano mkubwa wa tatizo kujirudia/kutopona kabisa. Kwa hiyo kabla ya kufanya maombi ni vema kumwomba Mungu akuongoze ujue nini tatizo na/au suluhisho.

  Mungu ni mwaminifu kabisa na hakika atakuonesha. Chukua hatua ya kufunga na kumlilia Mungu ukimwuliza tatizo nini na kumwuliza ufanye nini. Tatizo lako ni dogo sana kulinganisha na ukuu wa Mungu wetu. Mimi (naamini na wengine wengi tu hapa SG) tunakuombea!

 262. Asante,kaka Steve kwa ushauri wako,umenitia moyo,asante pia kwa Maombi,pia na wana SG wote ninawashukuru kwa kuniombea.naomba muendelee kuniombea naamini maombi yenu yatanifikia huku niliko na kunifungua.nitaendelea kuwasiliana nanyi.Mungu awape baraka zote.

 263. Bwana Yesu asifiwe,
  Mimi ni dada ninaomba uniombee nipo katika wakati wa kujifungua, Mungu aniwezeshe nijifungue salama na mimi niweze kubeba mtoto kama wanawake wenzangu.

  Na pia Mungu anilinde katika ndoa yangu.

  Mungu akubariki. Amen.

 264. Mungu akupe mtoto mwema na mwenye afya tele.
  Kumbuka kupata mtoto ni hatua ya kwanza, kumweka wakfu na kumlea ni hatua nyingine kubwa zaidi na muhimu sana. Mungu akusaidie uwe mwaminifu ktk malezi ya mtumishi huyo anayekuja

  Amina!

 265. Bwana wetu Yesu apewe sifa, kwanza napenda kumshukuru Mungu kwa web hii nzuri inayokutanisha wana maombi.
  1. Naomba mshirikiane nami kuniombea nina mtihani mwenzi wa kumi, Mungu aniwezeshe niweze kufaulu
  2. Tuombee nchi yetu kwa uchanguzi mwakani, amani ya nchi yetu izidi na watanzania wamjue Yesu zaidi.

 266. shalom,
  naomba maombi yenu wapendwa, niko kwenye majaribu na mapito makubwa sana,akili yangu imefika ukomo wa kufikiri,Mungu anasema yu karibu na mi naamini lakini katika haya naona Mungu ameniacha na yuko mbali sana nami,nahitaji maombi yenu kwani bado naamini Mungu anajibu maombi.

 267. Bwana yesu asifiwe!
  Jamani niko kwenye jaribu kwa miezi miwili sasa, mume wangu nimefunga nae ndoa ameondoka nyumbani ameenda kwa kahaba, na wazazi wake wanam support hivyo anavyofanya,niko na mtoto ambaye aliugua degedege akiwa na siku 2 kwa sasa anakaribia miaka 2 hajaweza kukaa, kutembea wala kuongea naombeni sana maombi yenu kwa ajili ya mtoto wangu na mume arudi nyumbani kwani tulikuwa tukipendana sana na kwa muda mfupi akabadilika hivyo.
  Pia nawashauri wanandoa wenzangu kuwa shetani ameelekeza nguvu sana kwenye ndoa hasa zile ambazo uchumi umeanza kuwa mzuri wamama kaeni sana kwa Yesu ili ndoa zenu zilindwe na Bwana,ziko ndoa nyingi zinapita ninakopita sasa ambazo nazishuhudia.
  Naombeni maombi yenu jamani kweli naumia moyo mno haswa nikimwangalia mtoto wangu.
  Asanteni sana

 268. DADA VERONICA HILO JARIBU NI LEPESI SANA HAKUNA LA KUMSHINDA YESU MAADAMU TU UKAE KATIKA UWEPO WAKE. WOTE WANAOMFANYA AWE KICHWA NGUMU WATAACHA NA MMEO ATARUDI NYUMBANI MLEE MTOTO.SASA BASI WEWE USIWATAZAME WATU NA WALA USIMTAZAME MMEO MTAZAME YESU TU NA WALA USIJISUMBUE KUPAMBANA NAO WEWE KAA KIMYA KAMA JINSI MWOKOZI WETU ALIVYOKAA NA AKAWA MSHINDI.UKISHAWEZA KUWA MTULIVU SASA DAWA YAKO NI NENO NA AHADI ZILIZOPO KWENYE NENO NA MAOMBI NA KUFURAHI PIA ISAYA 43:1_4 NA MINGINE MINGI KULA NENO NA UANZE KULIISHI HAKIKA UTAONA MABADILIKO MARA MOJA. YESU NI MUNGU NA BIBLIA YOTE HAKUNA MAHALI YESU ALIPOHUDUMIA WENYE SHIDA WALIOBAKI NA SHIDA ZAO. DADA YANGU YESU WA WAKATI ULE NI YULE YULE MPAKA SAA HII. NYAMAZA KIMYA KWA WANADAMU ILA KWA YESU ONGEA KILA WAKATI. HUWA HASHINDWI NA LOLOTE . YOTE ANAWEZA. HUYU YESU HUWA ANAONA YOTE UWE MWAMINIFU TU UTAUONA MKONO WAKE. NAMUOMBA MFALME WETU YESU MWENYE KUFUFUA WAFU NA MIUJIZA KIBAO AMRUDISHE MMEO KWA JINA LA YESU.

 269. Asifiwe Yesu sana. mimi ninachoomba jambo kubwa kwamba tuungane wapendwa kwa pamoja ambao tunasoma mtandao huu kuombea vyanzo vya mafanikio kama huu mtandao ili Mungu afungue milango zaidi na watu wa Mungu waenee katika nyanja zote ndipo maasi na vitendo vibaya ambavyo watoto wetu au vijana wamekuwa wakiangalia na kujifunza kufanya na matokeo yake wamekuwa wakipotea alafu tunatumia nguvu ya ziada kung’oa ambavyo tayari vimepandwa ni afadhali kuvizuia kabla ya kung’oa ,jambo jingine ambalo ningependa wapendwa tushirikiane kuomba ni kuhusiana na suala zima la watu kutokupata shida wakati wa kupata wenzi wao Mungu awasaidie wampate aliye sahihi kwake siyo mwisho wa siku aseme hakuwa Bwana ,pia kwa kuwa kila mwanamke ameumbwa kutoka kwa mwanaume basi hili suala lisiwe gumu kwa wapendwa manake limekuwa likiwasumbua sana vijana wengi makanisani wanachanganyikiwa na hasa yale ya kiroho tatizo kwanini?na bibilia inasema tumekilimiwa mambo yote ya mwilini na rohoni tatizo liko wapi haswaaaaaaaaaaaa liko wapi?

 270. Shalom wapendwa habari za uzima!
  Naombeni maombi yenu ni dada wa miaka 29 nimeolewa na nina watoto wawili, Ombi langu ni juu ya afya yangu jamani nateswa sana na huyu mwovu shetani kwani haipiti week bila kuniangushia maradhi kila leo naugua mara maralia utasikia tumbo sasa hivi upande mmoja wa mwili unaniuma kuanzia kichwa hadi mguu vyote vya kushoto jamani naombeni mniweke mikononi mwa bwana hata mie naomba Bwana Yesu aniponye,AMINA

 271. Dada Getrude,Pole kwa hali unayopitia. Pamoja na kuleta hitaji lako hapa kwa ajili ya kusaidiana kuomba mimi ninaushuri ufuatao kwako:

  Kama umeokoka nenda kamshirikishe kiongozi wako wa kiroho katika kanisa unaloabudia. Kwa sababu hali uliyoitaja inaonyesha uko kwenye wakati mbaya na kama wewe ni mtu unayemkiri Yesu halafu uwe na matatizo namna hiyo basi yawezekana kuna sababu na hivyo unahitaji kushirikiana na watu kwa maongezi na ushauri ili kuona kama nini kinaweza kuwa sababu ya hali hiyo na ufumbuzi wake ni nini. Natumaini katika kushirikiana huko kwa maongezi unaweza kupata na ushauri unaofaa kwamba yawezekana kuna mambo ambayo unatakiwa utengeneze na Mungu ili Nguvu ya Damu ya Yesu iweze kufanya kazi ndani yako.

  Halafu kwa magonjwa kama malaria na tumbo yawezekana kuna sababu za kibinaadamu zinazoyasababisha. Sababu hizi inaweza kuwa ni pamoja na kuishi sehemu yenye mbu wengi pasipo kuchukuwa tahadhari ya kujikinga, hasa wakati wa usiku ukiwa umelala kama vile kutumia chandarua. Au kama kuna tatizo fulani kwenye chakula unachokula mfano namna chakula hivyo kinavyoandaliwa yaweza kusababisha matatizo ya tumbo. Nimeona niandike maneno haya kwa sababu si kila Ugonjwa unatokana na nguvu za giza! Yapo magonjwa yanayosababishwa na shughuli za kibinaadamu. Na binadamu amepewa akili ya kuweza kutatua yale yaliyochini ya uwezo wake.

  Natumaini ukimshirikisha kiongozi wa kiroho utaweza kuongea naye mengi ambayo mengine si rahisi kwako kuyaandika hapa. Na hiyo italeta mwanga wa namna gani upate msaada.

  Nami naomba pamoja nawe ili Mungu aonyeshe njia ya kutokea katika hali hiyo mbaya!

  Lakini kama hujaokoka fanya haraka ili huyu Yesu, mtenda miujiza, akae ndani yako mwenyewe kwa ajili ya kusalimisha roho kwanza halafu ndipo mambo ya mwili yafuate!

 272. shalom!! Naomba mniweke mikononi mwa Mungu Naripoti shule mwezi Septemba, 2009 kwa ajili ya kumalizia mtihani wangu mmoja. Nawatakia kazi njema shambani mwa Bwana Songeni mbele pasipo kuchoka wala kukata tamaa.
  Mungu awabariki sana!!!!!!

  Nawatakia safari njema katika Kazi ya Bwana.

  Atu.

 273. shalom!naombeni maombi yenu wapendwa maana gafla kumetokeo mtafaruko kati yangu na dadangu hadi nimeamua kuhama kutoka kwake kwenda kupanga.nimeokoka ila naona njia salama pia ni kwenda mbali nao km waswahili wasemavyo heri kinga kuliko tiba

 274. Dada Agnes,

  Yawezekana kabisa uamuzi wa kuhama ukawa umeufanya kwa busara kwa kutegemea kwamba hapakuwa na njia nyingine ya kumaliza mtafaruku huo na pia chanzo cha mtafaruku huo sio wewe. Maana kama chanzo cha mtafaruku huo ni wewe basi suluhisho lake lingetoka kwako pia, hata pasipo kuhama mahali hapo.

  Nimeandika maneno haya kwa sababu kuna watu wengi wanajiita wameokoka lakini tabia zao huwezi kuitofautisha na ya mtu mabaye hajaokoka. Ni wagomvi tu kama akawaida, maneno mengi mdomoni ambayo si ya hekima wala busara, hawapendi suluhu bali ni watu wa visasi, hawataki kutubu na kuomba msamaha na tabia nyingine ambazo huzaa mitafaruku. [Sina maana wewe Agnes ndiwe mwenye tabia hii, please!]. Watu wa namna hii ndio wengi wanaosababisha ionekane wokovu ni kama staili tu nyingine ya maisha kwa ajili ya maslahi fulani binafsi. Na hili ni tatizo!

  Kwa maneno hayo ninakushauri Agnes kwamba hakikisha chanzo cha mtafaruku sio wewe. Hakikisha kwamba ushuhuda wako ni mzuri. Yaani pamoja na kuwa umehama lakini mwisho wa siku dada yako aje aseme kweli kumbe mdodo wangu alikuwa sahihi. Safisha mapito yako ili ushuhuda wako uwe mwema siku zote. Na kwa hiyo jina la Bwana Yesu litatukuzwa.

  Nikija upande wa hitaji lako la maombi hujaeleza unahitaji maombi ili nini kiwe nini. Maana tayari umeshahama baada ya mtafaruku. Kama unahitaji maombi ili amani irudi ungeeleza hivyo; au unahitaji maombi ili Mungu akutangulie huko ulikohamia ungesema pia…

  Mimi nafahamu kwamba tunapohitaji maombi ni lazima kuwa na lengo kamili kwamba maombi ni kwa ajili ya nini. Hii pia huonyesha kwamba tunatazamia kupokea badiliko baada ya maombi kutoka na hitaji lililowekwa. Lakini kusema tu mtu unahitaji maombi pasipo kueleza ni kwa ajili ya nini mimi nadhani siyo rahisi hata kufahamu kwamba maombi yamefanya kazi kwa sababu hujuwi ni nini kilichokuwa kinaombewa.

  Mimi nashauri kwa kila mtu anayehitaji maombi ni lazima kuweka wazi unahitaji maombi kwa ajili ya nini hasa ili watu wanapoombea hapa wataje mbele za Mungu kwamba wanaomba jambo fulani liwe hivi au vile! Na hii itaonyesha ni jinsi gani tunaheshimu na kuthamini sehemu hii ambayo ni kwa ajili ya kuwashirikisha wapendwa katika mwili wa kristo kuchukuliana mizigo na kuinuana mbele za Mungu.

 275. Agnes nakumbuka wakati fulani nikiwa ninaishi na mzazi wangu (baba)kulitokea mtafaruku wa maneno maneno kutoka kwa baba maana alikuwa anakunywa pombe kwa hiyo akirudi alikuwa anasema maneno ambayo yalikuwa yananiumiza sana na hata niliwahi kuwaza kuhama nyumbani na wakati mwingine nilikuwa ninawaza kwa nini Mungu asimuadhibu baba lakini katika kuomba kwangu Mungu alinipa maneno haya “kautakieni amani mji ule ambao nimewafanya mchukuliwe mateka mkauombee kwa BWANA maana katika AMANI yake MJI huo ninyi mtapata amani” (yeremia 29:7).

  Unajua unapokaa kwa mtu hata kama ni ndugu yako au wazazi wako unakuwa kama mateka,yaani unakuwa huna uhuru wa kufanya mambo mengine hata kama ni mazuri kwa sababu tu hapo si kwako.wakati mwingine unataka kwenda kanisani lakini utaona vikwazo kwa hiyo unakuwa kama mateka tu.na ukitaka kufanya mambo kwa uhuru wewe tafuta tu mji wako utaona uhuru wa kweli maana hakuna atakayekuuliza.nachotaka uone hapo ni kwamba Mungu alinipa hiyo mistari akiwa na maana hii kwamba kama ninataka kuwa na amani ni lazima niombee amani ya pale nyumbani maana katika amani ya pale nyumbani ndipo na mimi nitapata amani,na ndiyo maana aliwaambia Israel japokuwa amewapeleka uhamishoni Babeli lakini waiombee Babeli amani maana katika amani ya Babeli ndipo na wao watapata amani na siyo kwa kuhama au kwa kukimbia.unakumbuka Hajiri mtumwa wa Ibrahimu alipokimbia baada ya kuona ananyanyaswa na Sara? malaika alimwambia hivi, “……wewe mjakazi wa Sarai unatoka wapi nawe unakwenda?Akanena Nakimbia mimi kutoka mbele ya bibi yangu Sarai.Malaika wa BWANA akamwambia,rudi kwa bibi yako UKANYENYEKEE chini ya mikono yake.(mwa 15:7-9) sasa kama ni msomaji mzuri wa Bible utaelewa vizuri nini namaanisha.kwa ushauri wangu mimi nakushauri kama malaika alivyomwambia Hajiri rudi kwa dada yako ukanyenyekee,na hata ikitokea kuondoka kwa dada yako hakikisha unaondoka kwa amani ili hata siku nyingine uwe na uhuru wa kwenda kumsalimia au yeye kuja kwako kukusalimia.siku zote sisi ndo watu wa kunyenyekea hata kama tumekosewa.ubarikiwe!!!!!!

 276. Bwana Asifiwe sana,

  Wandugu katika Kristo, kwanza naomba nitoe shukrani zangu kwa Mungu kwa kunionyesha website hii yenye mambo mazuri ya kumsifu Yeye na kuonyesha njia ya kweli. Pili nawaomba mniombee kwa Mungu niwe na amani moyoni na akilini mwangu na pia afya njema. Miezi ya karibuni baada ya kuchukuwa uamuzi wa kumrudia Mungu kwa kubadili tabia, nimekuwa nikipatwa na mawazo na ndoto za kutisha kila mara zinazolenga kunikatisha tamaa. Kwa kweli niliishi maisha yasiyomfurahisha Mungu hata kidogo. Nimetenda dhambi kwa miaka mingi, nilishiriki katika uzinzi,uhuni,ulevi,uongo,majungu na mambo mengine mengi ambayo kwa sasa nikiyafikiria kwa kweli yananikosesha amani kabisa ndani yangu.

  Huwa inafikia wakati nashindwa hata kulala au nikilala naamka usiku wa manane nikiwa nabubujikwa na jasho baada ya kuota ndoto za kutisha sana. Ni kama kuna sauti au nguvu ya aina fulani inayonikumbusha mabaya yote na uchafu wote niliotenda. Jinsi imani yangu inavyoimarika ndivyo naona ile nguvu inazidi kufanya jitihada kunizamisha.

  Tatu nawaomba mniombee kwa Mungu niweze kufanikisha azma yangu ya kuoa baada ya kumuomba Mungu anipe mchumba atakayenifaa ambaye naamini amenipa kwa sasa. Mniombee ili mimi na mchumba wangu tuache kuishi katika dhambi na hatimaye kuoana katika Kristo. Mbarikiwe wote.

 277. Bwana Yesu asifiwe,
  namshukuru MUNGU kwa kukutana na website hii ya kuombeana na kupeana maneno ya faraja, mimi ni mwanamke niliolewa na niko ndani ya ndoa ni mwaka wa tatu sasa, ila kuna majaribu mengi sana kwenye ndoa yaliyotokea hivi karibuni nilikua na msichana wa kazi na nimeishi naye kwa muda wa karibu mwaka na nusu hivi juzi alisema mume wangu alishamtaka kimapenzi na alienda kusema kwa wazazi wangu maana mama yangu ndiye aliyemleta yule msichana jambo hilo lilinishtua sana ila nashangaa nilipata moyo wa ujasiri nikamuuliza mume wangu kwa upole akajibu ni kweli na akatubu kwa hilo mimi nilimwambia nimekusamehe ila nilimpa masharti mawili akapime virusi vya ukimwi na aende kwa mchungaji wa kanisa letu akamweleze ili roho hizo chafu zimtoke na alifanya hivyo alipima akakutwa negative na baadae tulienda kwa mchungaji tukiwa wawili kwa ajili ya maombi, baada ya hapo moyo wangu ulikua na amani mno. cha kushangaza ni yule msichana maana alibaki kwa mama juzi alipandisha mapepo makali sana akaombewa akanyamaza. hivyo moyoni mwangu nikatambua ilikua roho chafu za mapepo alizokua nazo yule msichana ndo maana mume wangu alipatwa na jambo kama lile. maombi yangu kwenu MNIOMBEE FAMILIA YANGU IWEZE KUSIMAMA KATIKA IMANI NA MUME WANGU AWEZE KUMJUA MUNGU ZAIDI MAANA ANAMJUA ILA BADO ANAHITAJI MAOMBI ZAIDI AWEZE KUSIMAMA IMARA.

  NASHUKURU SANA NA MUNGU AWABARIKI AMINA

 278. Wapendwa naomba maombi yenu mniombee niachane na ulevi na laana, matambiko ya mizimu,yapate kunitoka nimejaribu mara nyingi kuachana na ulevi imeshindikana.

 279. isaya 41:1-10.
  WAPENDWA KRISTO APEWE SIFA!

  NAWAKUMBUKA SANA WOTE WENYE MAHITAJI.
  NAAMINI MUNGU WETU AMEWATEMBELEA WENGI TOKA TUANZE
  KUOMBA.

  BINAFSI NASIKITIKA KUTOKUONA SHUHUDA ZA WALIOKUTANA NA MAJIBU YA MAOMBI TUNAYOFANYA KTK BLOG HII.

  PLZ NAOMBA KUKUMBUSHA KUWA MKITOA SHUHUDA MNAWATIA MOYO WAOMBAJI NA SI HIVYO TUU LAKINI PIA MNAWAFUNGUA WENYE MATATIZO MBALIMBALI YAFANANAYO NA HIILO ALILOFANYA MUNGU KWAKO. ZAIDI YA YOTE KUPITIA SHUHUDA MUNGU ANATUKUZWA NA NDIPO BARAKA NYINGI ZITAAMBATANA NAWE.

  UKAMILIFU WA MUUJIZA WAKO NI KUTANGAZA KWA KILA MWENYE SIKIO. MUNGU WANGU AWAPAKATE.
  TUKO PAMOJA NA MUNGU AWABARIKI

 280. My name is Samson ndeti from Kenya; I was usually positively moved by the genuine request of prayers from most of you. It is also my wish and prayers that our Mighty father will meet us in the diversified points of needs. My brothers and sisters in Christ I wish the same spirit of communication and praying for one another be highly continued knowing God is ever listening to grant us richly.
  Thank you in advance and be blessed.

 281. Shalom wapendwa! Sifa na Utukufu kwake Mungu kupitia Jina la Yesu, nimeona nijitokeze kushukuru Mungu kwa kunipatia course mwezi uliopita. Nilipost hapa kuwa ninaomba nianze shule mwezi July, lakini rohoni nilikuwa sina amani na chuo nilichotaka kuomba. Msukumo ulikuwa nipate tu ufahamu kwa kazi mpya ninayofanya, basi Mungu kanipa ghafla course fupi ambayo nimerudi wiki hii kutoka nchi ya jirani. wiki hii pia nimepokea kutoka kwa wapendwa wangu SA, na mie pia nimepata chuo hapa hapa Tz, hivyo namuona Mungu kwa haraka baada ya maombi yenu, Mbarikiwe na Mungu azidi kuiinua SG. Amen.

 282. Nashukuru sana kusikia mambo mema wapendwa tunatoshirikishana kupitia mtandao huu,BW.YESU asifiwe sana.
  Naomba nisisitize alichokisema ngudu BARAKA kwamba USHUDA ni kitu kikubwa sana.Kwa mfano tuangalie katika ktabu cha ufunuo 12:11,kwamba “WAKAMSHINDA KWA DAMU YA MWANAKONDOO NA KWA NENO LA USHUHUDA WAO,…kwa hiyo ushuhuda ni NGUVU ya ushindi.Amen?
  Mshuhudie YESU,Mpe sifa mfalme mkuu,tumpe dhabihu za vinywa vyetu ili ungamayo jina lake naye atapigana kila upande kwa ajii yetu.

  OMBI langu kubwa:Tuwaombee vijana sana sana hasa wa Kitanzania wapate MAONO yale aliyosema MUNGU katika kitabu cha Hosea 2,na Isaya 11:1-4.
  AMEN.

 283. pray for me Murage to be free from familiar spirits attacks in dreams.THERE IS WITCHCRAFT IN MY FAMILY.PRAY THAT MY MUM AND BROTHERS ARE ALL SAVED AND DELIVERED FROM THE CULT OF JEHOVAH WITNESSES AND JEALOUSY AND ENVY AND DRUNKENNESS.SHETANI ALIIBA KAZI YANGU YA UALIMU 1992..TUOMBE AIRUDISHE MWEZI HUU KWANGU HAPA KU DEPT YA ENVIRONMENTAL EDUCATION

 284. Wapendwa Bwana Yesu Asifiwe, Mimi naitwa Upendo napenda kuwashirikisha hitaji langu ili ndugu wapendwa tuweze kuomba kwapamoja kwani hili limekuwa ni tatizo kwangu na limekuwa ni lamuda mrefu sasa, mimi ni mtumishi wa Serikali na nimekuwa nikifanya kazi kama Katibu Muhutasi kwa zaidi ya miaka kumi sasa lakini cha ajabu nimekuwa nikilipwa mshahara kama Mhudumu na kila ninapojaribu kufuatilia naambiwa subiri tunalifanyia kazi, na wakati mwingine nimekuwa nikipewa majibi ya kutia moyo kiasi kwamba najikuta nimeingia kwenye madeni nikijua kuwa mbona nitalipwa pesa ambayo ni stahili yangu.

  Hivyo wapenda naomba mshiriki kuomba pamoja nami ili Bwana mwenyewe aingilia kati maana yeye ndiye kimbilio letu.

 285. Wapendwa naomba maombi yenu kwa ajili ya shangazi yangu.amepagawa na mapepo namimi nipo mbali japo haijalishi umbali Yesu kila kona yupo ila naomba tumsaidie kimaombi kwanza Aokoke,haambiliki wala hasikii ndoa yake imeharibika kwa kuwa shetani ndie dereva wa maisha yake tumuombee kwa pamoja apate kuupokea Yesu akiwa ndani ya Yesu atafunguka tu.jina lake ni TUMAINI MWASHIVYALA

 286. Shalom wapendwa,nawapenda sana.
  Kaka Paul Bwana atukuzwe kwa ajili yako, nafurahia sana changamoto na msaada wako kwangu kijana wa kike ambaye napitia mambo mengi katika kipindi hiki cha miaka 27.
  Nina miaka 2 ktk wokovu na nimejionea ushindi mkubwa ambao sikuweza kudhania Hakika Yesu ni Bwana.
  Kwa ajili ya Yesu nimeweza kuyashinda mazoea na vitu vilivyokuwa nkivipenda sana vya kidunia

  1.Kuachwa na mpenzi tuliyekuwa na mahusiano ya miaka minne,baada ya kukataa kuacha wokovu na kurudia dini pamoja na tabia za uzinzi tuliokuwa tukiona ndiyo mapenzi na hatua za kuelekea ndoa. Bwana ameniokoa na ndoa yenye misingi mibovu.

  2.Natumia muda wangu katika mambo ya maana.Katika kazi yangu ambayo Mungu aliyonipa as a Researcher ktk Government Institute, najibiidisha kusaka elimu zaidi, kujifunza neno la Mungu kila siku, na kuangalia vipindi vinavyoleta changamoto za maendeleo nchini.

  3.Nina amani kubwa sana na wala sina hofu, nimeamini kuwa Bwana ameshanipa mume since January nilipopokea ktk ulimwengu wa roho na kila siku namshukuru Mungu na kumuombea huyo mume nikiwa na hakika kabisa kuwa atamdhibitisha katika mwili na nyama mwaka huu.Na sijakata tamaa licha ya majaribu na wachumba feki ambao ibilisi anawainua kutaka kunipoteza, najua Bwana hawezi nijaribu zaidi ya uwezo wangu.

  4.Nawaomba tuwaombee sana vijana wa kike kwa kweli tunapitia majaribu mengi katika kila kona ya maisha, uvumilivu na subira vimekuwa ni vikwazo kwa akina dada wengi. Dunia imekuwa ikikatisha tamaa sana kuwacheka kuwa wanachelewa,na hasa watu wa dunia wanapoolewa kwa urahisi. Jamani vita yetu ni kubwa sababu ya vizazi vitakatifu tulivyobeba, tung’ang’ane na Yesu kwa imani katika maombi.

  BWANA AWABARIKI SANA!!!

 287. 1Peter 5:9-10
  9 Whom resist stedfast in the faith, knowing that the same afflictions are accomplished in your brethren that are in the world.

  10 But the God of all grace, who hath called us unto his eternal glory by Christ Jesus, after that ye have suffered a while, make you perfect, stablish, strengthen, settle [you].

  Mpendwa Faith, MAISHA YA WOKOVU NI MAPAMBANO HADI MWISHO! YESU KRISTO YU KARIBU SANA KUJA HIVYO INUA MACHO YAKO JUU!
  USITAFUTE VITU VYA DUNIA HII.TAFUTA UFALME WA MUNGU; TAFUTA VILIVYO JUU KRISTO ALIKO! USIVIANGALIE VINAVYOONEKANA(pesa, mme, watoto, kazi, nyumba,…) MAANA NI VYA MUDA.ANGALIA VITU VISIVYOONEKANA VYA MILELE! LOOK UNTO JESUS CHRIST THE AUTHOR AND THE FINISHER OF OUR FAITH!

  Romans 13:11-14
  11And that, knowing the time, that now [it is] high time to awake out of sleep: for now [is] our salvation nearer than when we believed.

  12The night is far spent, the day is at hand: let us therefore cast off the works of darkness, and let us put on the armour of light.

  13Let us walk honestly, as in the day; not in rioting and drunkenness, not in chambering and wantonness, not in strife and envying.

  14But put ye on the Lord Jesus Christ, and make not provision for the flesh, to [fulfil] the lusts [thereof].

  1.THE NIGHT IS FAR SPENT, THE DAY IS AT HAND!
  2.JESUS CHRIST IS SOON COMING TO CATCH HIS CHURCH!
  3.PUT YE ON THE LORD JESUS CHRIST, AND MAKE NOT
  PROVISION FOR THE FLESH!
  4.WATCH AND PRAY AND BE READY!

  PUT YE ON THE LORD JESUS CHRIST, AND MAKE NOT
  PROVISION FOR THE FLESH!

  Mungu awabariki!

 288. Thanx brother Martin,for such courage giving words.
  Iam sure with this shield of faith in JESUS,we can quench down all the fiery sparks of the devil.

  Jesus is alive,Greatest he is inside me!!
  STAY BLESSED!!

 289. please pray for me.Am tormented by satan through dreams,people,sicknesses,diseases,drunkeness,immorality,curses,losses,rejection,anger,violence,lies,stealing,conning,….am a total mess.rotten to the core.I have sinned against God and man…..i need total deliverance of body,soul,and spirit…. there is witchcraft in my family……. have mercy and intercede

  pray for Gods favour TO REST UPON ME FROM NOW

 290. praise GOD with me for the EXACT place and how I am right now. I NEED DELIVERANCE FROM FAMILIAR SPIRITS THAT OPPRESS AND TORMENT THROUGH DREAMS AND PEOPLE AT HOME,PLACE OF WORK,KIANYAGA,KAGONGO……..SATAN HAS ROBBED ME SO MUCH. HE HAS TO PAY ME BACK 7 TIMES

  OMBEA MAMA YANGU NA ESTHER WANGU ELIUD NA NDUGU ZANGU BENSON MURITHI SHEKIH,PAUL WAWERU SHEKIH,EJIDIUS KARIUKI SHEKIH…WAOKOKE NA KUKOMBOLEWA KUTOKANA NA KUABUDU SHETANI,ULEVI,WIVU,UCHAWI NA MATUSI

 291. Bwana Yesu asifiwe! Mbarikiwe kwa kazi nzuri ya maombi, nina hoja moja naomba kuileta ktk jukwaa hili: naona maombi ni mengi na inamuwia vigumu mtu kusoma na kisha akifunga computer kukumbuka yote ktk kuomba. je haiwezekani tukayagawa ktk makundi tofauti mfano 1. Magonjwa 2. Nguvu za giza au vifungo 3. Baraka au upenyo (kazi,biashara, shule) 4. Ndoa au uchumba / wenza 5. Huduma / karama mbalimbali 6. Wokovu etc naona hii itasaidia hata mtu kukumbuka majina ya wahitaji ktk kundi fulani bila kuwa kila siku unaangalia hapa. Pili shuhuda zao zitawabariki wenye shida zinazofanana na kuwaongezea imani kwani watazikuta ktk sehemu wanapoweka ombi lao. Najua ni kazi kubwa kwa SG lakini itasaidia sana ktk kupelekana mbele za Mungu. Mbarikiwe

 292. watu wa MUNGU BWANA YESU APEWE SIFA. NINAOMBA MAOMBI YENU BABANGU KALAZWA HOSPITALI YA KCMC anatatizo la INI Asanteni kwakuwa mtamwombea. MORI B

 293. Mr. MURAGE SHEKIH
  In the name of JESUS CHRIST I command every kind of demonic spirity concerned about dreams,people,sicknesses,diseases,drunkeness,immorality,curses,losses,rejection,anger,violence,lies,stealing,conning TO MOVE OUT OF YOUR LIFE NOW, IN JESUS NAME. SAY AMEN.

 294. Mr.Murage Shekih,
  Mungu anaweza kukuweka huru.Kama unahitaji kuwa huru fanya yafuatayo:
  1.Mpokee Yesu, uzaliwe mara ya pili.-Yohana 1:12 na Yohana 3.
  2.Jazwa Roho Mtakatifu.-Efeso 5:18,Matendo 1:8,Yohana 14:16-17,Yohana 16:13-15.
  3.TAFUTA WATU WALIOOKOKA NA WANAOFUNDISHA BIBLIA KWA USAHIHI ILI UFUNDISHWE NJIA YA MUNGU KWA USAHIHI.

 295. i say hi to all of you in Jesus name!!! i’m a boy living i usa,
  i’m 23,i would like to ask an assistance of prayers:
  -I’m christian,i love God but sometimes i fail and sin!! so i want God to help me so i can stay straight in faith.
  -i need help so i can get my truly fiance.
  God bless y’all.

 296. Wapendwa naomba maombi yenu kwani ninasongwa sana na ndoto mbaya “mara niko chini ya kaburi” mara kunanyoka mkubwa sana chini ya meza yangu” hizi zote naona ni nguvu za giza naomba maombi yenu ili damu ya Yesu inifunike nisipatwe na mabaya

 297. pray for me,my mum,my wife,kids and my promotion.the devil is attacking me thru family members,coallegues,dreams,addictions,familiar spirits,witchcraft,immorality,anger,wastage,violence,pride,premature deaths,losses,rejections etc…..pray for my entire family salvation and deliverance….

 298. Dear Lilian,
  Natumaini UMEOKOKA.Kama haujaokoka basi UOKOKE.

  KUOKOKA/KUZALIWA MARA YA PILI:
  A.MKARIBISHE BWANA YESU MOYONI MWAKO
  John(Yohana) 1:12
  But as many as received him, to them gave he power to become the sons of God, [even] to them that believe on his name:

  John(Yohana) 3:5-6
  5Jesus answered, Verily, verily, I say unto thee, Except a man be born of water and [of] the Spirit, he cannot enter into the kingdom of God.
  6That which is born of the flesh is flesh; and that which is born of the Spirit is spirit.

  Romans(Warumi) 10:9-10.
  9That if thou shalt confess with thy mouth the Lord Jesus, and shalt believe in thine heart that God hath raised him from the dead, thou shalt be saved.
  10For with the heart man believeth unto righteousness; and with the mouth confession is made unto salvation.

  B.TAFUTA KANISA LENYE KUKUBALI WOKOVU ULIOLETWA NA YESU KRISTO na wanaoishi sawa na Neno kisha jiunge nao ILI UUKULIE WOKOVU

  1Peter 2:2-3
  2As newborn babes, desire the sincere milk of the word, that ye may grow thereby:
  3If so be ye have tasted that the Lord [is] gracious.

  KAMA UMESHAOKOKA BASI:
  TAFUTA KANISA LENYE KUKUBALI WOKOVU ULIOLETWA NA YESU KRISTO na wanaoishi sawa na Neno kisha jiunge nao ILI UUKULIE WOKOVU(1Petro 2:1).

  UNAHITAJI UKAE PAMOJA NA WATAKATIFU UFUNDISHWE NENO la MUNGU KWA USAHIHI ILI UJUE NAFASI YAKO KATIKA UFALME WA MUNGU NA HAKI ZAKO KAMA MWANA WA MUNGU.

  Tukikuombea tu bila ya wewe kulijua Neno(KWELI) HAUTAWEZA KUPATA UFUMBUZI WA KUDUMU.
  John 8:31-32
  31Then said Jesus to those Jews which believed on him, If ye continue in my word, [then] are ye my disciples indeed;
  32And ye shall know the truth, and the truth shall make you free.

  MUNGU ANATAKA WATOTO WAKE WAMJUE YEYE:
  Job 22:21
  Acquaint now thyself with him, and be at peace: thereby good shall come unto thee.

  Philippians 3:10
  That I may know him, and the power of his resurrection, and the fellowship of his sufferings, being made conformable unto his death;

  Tukikuombea tu bila ya wewe kulijua Neno(KWELI) HAUTAWEZA KUPATA UFUMBUZI WA KUDUMU.

  All my love and prayers,

  Martin.

 299. Dear MR.G,
  You asked prayers so as God may help you to stay sraight in the Faith of JESUS CHRIST.
  I HAVE A GOOD NEWS FOR YOU!
  GOD HAS ALREADY PROVIDED A HELP FOR YOU TO LIVE VICTORIOUS LIFE IN CHRIST JESUS!
  GOD GAVE JESUS FOR OUR SALVATION.
  HAVE YOU RECEIVED JESUS CHRIST IN YOUR HEART AND BE A NEW CREATURE?
  IF YOU WANT TO RECEIVE JESUS CHRIST IN YOUR HEART,
  JUST CALL HIM RIGHT NOW, WELCOME HIM INTO YOUR LIFE AND ACCEPT HIM IN YOUR HEART.

  John 3:5-6
  5Jesus answered, Verily, verily, I say unto thee, Except a man be born of water and [of] the Spirit, he cannot enter into the kingdom of God.
  6That which is born of the flesh is flesh; and that which is born of the Spirit is spirit.

  Romans 10:9-10
  9That if thou shalt confess with thy mouth the Lord Jesus, and shalt believe in thine heart that God hath raised him from the dead, thou shalt be saved.
  10For with the heart man believeth unto righteousness; and with the mouth confession is made unto salvation.

  John 1:12
  But as many as received him, to them gave he power to become the sons of God, [even] to them that believe on his name:

  2 Corinthians 5:17
  Therefore if any man [be] in Christ, [he is] a new creature: old things are passed away; behold, all things are become new.

  IF YOU WELCOMED JESUS INTO YOUR HEART, THEN FIND A BIBLE BELIEVING CHURCH WHICH TEACHES ABOUT SALVATION AND LIVE AS WORD INSTRUCTS AND JOIN THEM SO THAT YOU BE TAUGHT THE WORD AND YOU BE VICTORIOUS IN EVERY AREA OF YOUR LIFE

  1Peter 2:2-3
  2As newborn babes, desire the sincere milk of the word, that ye may grow thereby:
  3If so be ye have tasted that the Lord [is] gracious.

  HOW TO OVERCOME LUSTS OF THE FLESH:
  Romans 13:14
  But put ye on the Lord Jesus Christ, and make not provision for the flesh, to [fulfil] the lusts [thereof].

  1Peter 2:11
  Abstain from fleshly lusts that wage war against your soul.

  Job 31:1
  I Have made a covenant with my eyes; How then could I gaze at a virgin?

  2Timothy 2:22
  Now flee from youthful lusts, and pursue righteousness, faith, love and peace, with those who call on the Lord from a pure heart.

  MEMORIZE MANY SCRIPTURES.
  1 John 2:14
  I have written to you, young men, because you are strong, and the word of God abides in you, and you have overcome the evil one.

  Psalm 1:2
  But his delight is in the law of the Lord, And in His law he meditates day and night.

  Psalm 119:11
  Thy word I have treasured in my heart, That I may not sin against Thee.

  SOCKPILE YOUR THOUGHTS WITH GOOD THINGS

  Philippians 4:8
  Finally, brethren, whatever is true, whatever is honorable, whatever is right, whatever is pure, whatever is lovely, whatever is of good repute, if there is any excellence and if anything worthy of praise, let your mind dwell on these things.

  ALSO,
  Never assume that you are above suffering or that you deserve relief through sin. The pitfall of powerful self-pity.

  Acts 14:22
  [Paul went to his churches] strengthening the souls of the disciples, encouraging them to continue in the faith, and saying, “Through many tribulations we must enter the kingdom of God.”

  Luke 9:58
  And Jesus said to him, “The foxes have holes, and the birds of the air have nests, but the Son of Man has nowhere to lay His head.”

  2 Timothy 2:3
  Suffer hardship with me, as a good soldier of Christ Jesus.

  1 Timothy 4:16-17
  At my first defense no one supported me, but all deserted me; may it not be counted against them. But the Lord stood with me, and strengthened me, in order that through me the proclamation might be fully accomplished, and that all the Gentiles might hear; and I was delivered out of the lion’s mouth.

  Get busy with some task.

  Pray at all times in the Spirit for God’s deliverance.

  All my love and prayers,

  Martin.

 300. Dear MR.G
  PLease visit the below website:

  http://www.twft.com/?page=C2000

  You will get Bible Teachings, THEN IF YOU ACT/ (BE A DOER OF THE WORD) THEN you will experience VICTORY IN YOUR LIFE!

  JESUS SAID, you shall KNOW the TRUTH AND THE TRUTH THAT YOU KNOW AND ACT ON IT WILL CHANGE YOU(SET YOU FREE).

  IT IS THE TRUTH WHICH YOU ACT ON IT WILL SET YOU FREE!
  NOT PRAYERS! PRAYERS WILL ENABLE YOU TO GET SOMEONE TO TEACH YOU THE TRUTH THEN, IF YOU ACT ON THE TRUTH THEN YOUR VICTORY COMES!

  YOU MAY START WITH THE GOSPEL OF JOHN.
  THEN GO ON THE NEW TESTAMENT AND OTHER BOOKS.

  http://www.twft.com/?page=C2000

  All my love and prayers,

  Martin.

 301. Bwana Yesu Asifiwe, Mimi nimeokoka mwezi wa kwanza ila kabla sijaokoka nilikuwa na uhusiano na mtu ambae nahisi ameadhirika, natamani kwenda kupima lakini naogopa naomba mniombee nipate amani na niweze pima, niombeeni majibu yawe mazuri. Amina wapendwa Mungu awabariki

 302. Mpendwa Bahati, kwanza hongera kwa kuokoka, ni uamuzi mzuri sana na amini kuwa ukiwa ndani ya Yesu yote yanawezekana. Ninamwomba Mungu aliyekupa neema hii ya wokovu akujalie Roho wake Mtakatifu akuongoze katika safari yako hii ya wokovu katika Jina la Yesu. Ondoa hofu, amini hata UKIMWI Mungu anaponya! Ukiisha amini hivyo mwombe Mungu akujalie ujasiri wa kupokea matokeo yoyote kwani Yeye anajua yote hata yaliyo mbele yetu, na siku zote anatuwazia mema tu. Tunakuombea na ubarikiwe sana.

 303. Asante sana Mr. Kileo kwa majibu yako mazuri namimi nimeokoka ila nitazidi kuwa karibu na kanisa la walio okoka ili niweze kuukulia wokovu. Nampenda Yesu sana na nina sali sana na mara nyingi naziona nguvu za Mungu kwenye maombi yangu ila wakati huu naona kuzidiwa kila ninapoomba mambo yangu yanazidi kuwa magumu.

 304. Dear Brothers and sisters in Christ Jesus out Lord and Savior,

  I would like you to pray over my family because we are facing a number of hardships.One thing we need to get children and also spiritual power to overcome attacks from the devil.

 305. Wapendwa
  Bwana Yesu asifiwe!
  Mungu awabariki kwa moyo wenu hasa kushiriki katika maombi. Tuombee Wanandoa wawe waaminifu katika ndoa kwani shetani ametawala kwenye ndoa. Mungu atupe uaminifu na awafunike Waume zetu kwa damu takatifu.

 306. Bwana Asifiwe!
  jamani mimi nina shida ya kuombewa. nimekua nikiona kila ninachojaribu kufanya hakina mafanikio. Nimejaribu kujipa moyo na kujiombea mwenyewe mara kadhaa lakini naona tu muda unaenda na mambo mengi hayatekelezeki ni kama yanazidi vurugika na mengine mengi kusimama kabisa. Nina shida sana ya kufanyiwa nadhani maombi ya deliverance au?? nipeni msaada, na sadaka hua ninatoa.

 307. Amani ya Bwana wetu iwe nanyi!
  Wapendwa naomba mniombee ili nifanye
  vizuri kwenye mtihani wa tarehe 20 mwezi huu!!
  Asanteni sana.

 308. Bwana Yesu asifiwe, mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 31 naomba mniombee ili nipate mwenzi au mume pia ninasumbuliwa na ndoto mbaya,nimeokoka ningefurahi kama ningempata mwenzi aliyeokoka ninaishi dar

 309. Ndugu Jema,

  Pamoja na maombi, mimi nina ushauri ufuatao kwako:

  Tatizo la kukwama kwa kila unachojaribu kufanya laweza kusababishwa na sababu katika ulimwengu wa roho lakini pia kutokana na namna mipango yako unavyoipanga. Katika Biblia tunashauriwa kuto-kunia makuu kupita kiasi! Yawezekana unapochagua mambo ya kufanya huwa unapanga mambo makubwa ambayo mengine muda wake bado au labda uwezo wa kuyafanya unakuwa hujaufikia. Katika hali ya namna hii inawezekana kabisa yasifanikiwe. Kutokufanikiwa huku mtu anaweza akafikiria kabisa ni kwa sababu ya nguvu za giza. Kwa hiyo ninakushauri unapopanga mambo jitahidi kupanga yaliyo ndani ya uwezo wako wa kuyafanya. Huu ni ushauri tu na haimaanishi wewe hupanga mambo makubwa kupita kiasi!

  Kukwama kwa mambo mengine kufanikiwa kwaweza kusababishwa pia na Mungu mwenyewe. Kama uko karibu na Mungu kwa kiwango kizuri yawezekana akazuwia baadhi ya mambo yasifanikiwe kutokana na sababu anazozijua mwenyewe lakini kwa faida yako. Kwa hiyo unachotakiwa kufanya ni pamoja na kumuomba Mungu akusaidie kutambua ni nini ambacho ni mapenzi yake kukifanya! Mungu akishakupatia kibali kuhusu jambo fulani hakuna kinachoweza kukwamisha tena!

  Kuhusu suala la deliverance, wewe mwenyewe unaweza kuwa shahidi wa nafsi yako. Lakini kwa hali ya kawaida mtu ukishaokoka na ukajazwa na nguvu za Mungu uwezo wa kudeliver mambo unakuwa katika maneno ya kinywa chako. Katika hili nakushauri ujichunguze mwenyewe namna ulivyookoka. Kuna hatari nyingine iliyopo kwa watu ambapo mtu anaweza kusema kaokoka na anaaamini hivyo na kweli anaishi vizuri lakini kushuhudia nguvu za Mungu ndani yake inakuwa hakuna. Hili ni tatizo. Ndiyo maana unaweza kuta mtu kaokoka lakini kumbe kuna mambo mengi ambayo bado hayajaharibiwa kwa ujio wa nguvu za Mungu. Mtu wa namna hii huendelea kuishi pasipo kuwa na furaha ya wokovu na kinachofauatia hapa ni kutafuta deliverance. Wengi wamefanyiwa deliverance lakini mmambo yao bado magumu kwa sababu tu hawajaamua kujiunganisha na nguvu za Mungu. Lakini kwa mtu aliyeokoka, ukijimimina vema mbele za Mungu, Nguvu ya damu ya Yesu inatosha kabisa kukuweka huru! Ushauri mwingine hapa ni kwamba unaweza tafuta mtumishi unayemuona kuwa ana nguvu za Mungu umshirikishe ili akushauri katika hili; yaweza kuwa kanisani kwako [ambapo ni bora zaidi] au kwa mtumishi mwingine unayemfahamu kwamba ni mtumishi wa Mungu kweli.

  Suala la kutoa sadaka si kigezo kwamba ndiyo mambo yako yafanikiwe kwa namna unavyopenda wewe. Sema tu siki hizi suala la utoaji limeharibiwa na kufanywa kama ni malipo kwa Mungu ili mambo yaende vizuri. Ni kweli Mungu hubariki kutokana na matoleo lakini si kwa kumlazimisha na kumfanya kama SACCOS! Mungu huangalia moyo, haangalii kiwango cha pesa kinachotolewa. Mungu tayari ameshafanya makubwa kwenye maisha yetu si kwa sababu tulitoa sadaka au tulipanda mbegu. Kwa hiyo wakati mwingine mtu unapotoa sadaka inabidi kuichukulia kama shukurani tu kwa Mungu. Hata hivyo hakuna tunachoweza kununua kwa Mungu kutokana na sadaka zetu. Zaidi sana hatuna cha kumpa Mungu maana vyote ni mali yake bali yeye ndiye huturuzuku kila siku kwa kutugawia wema wake. Endelea kutoa sadaka kwa moyo wa shukurani na si kwa kukania kwamba lazima Mungu afanye jambo unalolitaka kwa sababu umemtolea. Tukipata mada inayohusika na mambo ya utoaji tunaweza jadili suala hili kwa kirefu.

  Ninaomba pamoja na wewe ili Mungu afanye njia ya kutokea!

 310. Dada Pamela,

  Mungu ni mwema, na ana mpango mzuri kwako pia!

  Nina ushauri hufuatao kwako:

  Ndoto mbaya kwa mtu anayesema ameokoka si dalili nzuri. Kuokoka ni pamoja na kuwekwa huru mbali na kila nguvu iliyo kinyume na wema wa Mungu katika maisha yetu. Ndoto mbaya si mpango wa Mungu kwetu. Ni hila za kutoka upande wa pili. Ashukuriwe Mungu kwa sababu kwa nguvu ya Damu ya Yesu na jia la Yesu tanapata kufunguliwa!

  Nimeanza na suala la ndoto kwa sababu yawezekana likawa na uhusiano na hitaji lako la kutaka mwenzi. Wakati mwingine ndoto huwa ni kivuli cha hali inayomzunguka mtu. Wewe ndiwe unafahamu aina ya ndoto ambazo huwa unaota.[najua inaweza isiwe rahisi kwako kuandika mambo yote hapa].Nakushauri ukipata mtu aliyeokoka unayemwamini mshirikishe ili muone kama nyuma ya ndoto hizo kuna roho inayoweza kuwa imefunga mlango wa wewe kupata mwenzi.

 311. Kwako Pamela, anavyosema ndg John Paul ni sawa kabisa, ukiokoka unawekwa huru. Kama hizo ndoto ulikuwa unaziona hata kabla ya wokovu basi ulihitaji kufunguliwa lakini hujafanyiwa hivyo, kama ndio zinaanza baada ya kuokoka pia utahitaji kufunguliwa.
  Nguvu ya Mungu kudhihirika kwa mtu inategemea na uwepo wa nguvu hiyo ndani yake pia (Efeso 1:3 na Efeso 6:10 – 18), utaombewa na hizo ndoto zitaacha lakini nawe uwe mtu wa maombi pia usimame ktk Neno ili zisikurudie. Maombi yatakayokufaa ni pamoja na wanayoita maombi ya hatari au vita hasa wakati wa usiku. Ukiishapokea nguvu ya Roho Mt ndani yako na kuitumia basi utashangaa zinaisha zote. Kabla ya wokovu nilikuwa nawaota sana marehemu hasa kama misiba itatokea (mizimu), pia ndoto nyingi tu za ajabu (majini) nadhani kwasababu nilitibiwa kwa waganga na hadi mashehe nikiwa mdogo,lakini mwezi mmoja tu wa wokovu zikaisha zote na wala sijaona tena, Yesu anaponya. Ubarikiwe

 312. Wapendwa, Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nanyi.
  Nashukuru sana kwa maombi yenu, najua mnaendelea kuniombea. Niliomba mnisaidie kuomba ili niweze kununua nyumba. Sasa nimepewa barua ya kuachishwa kazi. Najua huyo ni shetani anataka kunikatisha tamaa. Mungu wetu ni mwaminifu, hakuna atakayekwenda kwake akatahayarika.
  Tuendelee kuomba kwa bidii na mwishowe shetani ataaibika.
  Bwana Yesu Asifiwe!

 313. Shalom dada Thecla, pole, Bwana akutie nguvu, usikate tamaa kwani tunaposema sasa ndio mwisho wa nguvu zetu ndipo Mungu anapodhihirika na nguvu zake kuonekana 2Korintho 12: 9-10. Jipe moyo pia usimwekee Mungu mipaka bali mwache afanye atakavyo, kununua nyumba ni vigumu kama huna mkopo na mkopo ni lazima mwajiri akubali. hivyo ondoa wazo kuwa lazima nyumba iwe hiyo tu, angalia upenyo wowote unaotokea wa wewe kumiliki nyumba hata kwa kununua kiwanja na kujenga, mwache Mungu mwenyewe ndiye anaejua ipi ni nyumba itayokufaa wewe na wakati gani wa kukumilikisha. Ubarikiwe.

 314. Bwana Yesu asifiwe sana.Namshukuru Mungu kwa wokovu wake juu yangu na familia yangu, naomba maombi maana uzinzi umekithiri katika kanisa la Mungu na watumishi wake. Wamwogope Mungu,wawe waaminifu mbele za Mungu na wanadamu pia.Ubarikiwe

 315. Yesu Anisaidie!
  Wapendwa watumishi wa Mungu, mimi naomba msaada wa maombi kwani nina dhambi nyingi lakini dhambi inayonizinga na imenilemea ni ya uzinzi na uasherati.

  Jamamani nasumbuka sana moyoni sina amani kiasi kwamba nashindwa hata kuomba.

  Ntashukuru kwa msaada wa maombi yenu.

 316. shallom! wapendwa naombeni mniombee niko katika kipindi kikumu sana naombeni maombi yenu ndugu zangu mimi nampenda sana Mungu na pia nahitaji kumtumikia Mungu sana katika maisha yanu ila maadui ni wengi sana

 317. BWANA YESU APEWE SIFA WAPENDWA PIA NAWAPONGEZA KWA KUJITOLEA KUWAOMBEA HATA WENGINE.

  MIMI NINAMSHUKURU MUNGU KWA KUNIPA MUME KWANI NILISHALETA MAOMBI YANGU HAPA. NA NINAMSHUKURU MUNGU KWANI HATA HAIKUCHUKUWA MUDA KWANI NAMWAMINI MUNGU UKIMUOMBA KWA NIA NA KWELI ANAJIBU MAOMBI YA KILA MTU NA BILA UBAGUZI.

  NA HIVI NINAPOONGEA TAYARI AMESHAKWENDA KWETU JUZI JUMA PILI KWA AJILI YA KUNIVISHA PETE NA KUJITAMBULISHA KWA WAZAZI WANGU.

  ILA ANASAFIRI NJE YA NCHI KWA MDA WA MIEZI SITA AKIRUDI NDIO TUFUNGE NDOA,PIA BADO NAHITAJI MAOMBI YENU KWANI MUNGU AMLINDE AWEZE KWENDA SALAMA NA ARUDI SALAMA PIA AKIENDA ASIENDE AKABADILIKA ILA MUNGU ATUJALIE KWANI SAFARI BADO NI NDEFU SANA NAHITAJI MSAADA WENU ZAIDI.

  MUNGU AWALINDE.

 318. Dada Rose, asante kwa ujumbe wako wa tarehe 13/10/2009. Nashukuru sana kwa maneno yako ya faraja. Kwakweli yamenitia nguvu na kuimarisha imani yangu kwa Bwana. Tuendelee kuomba, najua Bwana atanipa mahitaji yangu. Ubarikiwe daima Dada Rose.

 319. Bwana Asifiwe dada Thecla, asante kwakuuona mchango wangu ubarikiwe na sifa kwa Yesu. Tunakuombea na kazana kuomba hakuna jaribu ambalo linamshinda Mungu.
  Tunakuombea na naomba soma Jeremiah 32 yote hasa ukikazia mistari ya 26 hadi 27. Mkumbushe Mungu kuwa anaweza, mkumbushe bila kuchoka, Ubarikiwe.

 320. Bwana Yesu asifiwe, nilikuwa naomba mniombee niko katika wakati mgumu na ndoa yangu, mume wangu ianafanya biashara hafanikiwa amefikia hata hatua ya kukata tamaa. nahitaji sala zenu pia mimi naendelea kuomba sana nampenda Mungu najua atatufungulia kama yeye alivyosema ombeni nanyi mtapewa bisheni nanyi mtafunguliwa basi nazidi kumuamini.

 321. Dada Theresia, jipe moyo utashinda. Unaweza pia kutumia ushauri wa Dada Rose hapo juu – hakuna asiloliweza Mungu wetu. Nasi tuko pamoja nawe katika maombi. Tuombe kwa bidii tutafanikiwa.
  Dada Rose, asante sana kwa ushauri mzuri. Ninaufanyia kazi na nitaendelea kuwapa ujumbe huu watu wengine. Naamini ni Bwana amekutuma ulieneze neno lake.
  Bwana na atubariki wote.

 322. Bwana Yesu Kristo Asifiwe!
  Dada Theresia,
  Mungu anakupenda na anakuwazia yaliyo mema!
  YEREMIA 29:11
  “For I know the thoughts that I think toward you, saith the LORD, thoughts of peace, and not of evil, to give you an expected end.”

  PIA ELEWA KUWA MUNGU ANA KANUNI ZAKE KATIKA MAENEO YOTE YA MAISHA YETU!

  KATIKA ENEO LA KUPATA MAFANIKIO YA KIPESA ANA KANUNI HII:

  TOA SAKADA ZAKO NAYE BWANA ATAKUJAZA BARAKA
  LUKA 6:38
  “Give, and it shall be given unto you; good measure, pressed down, and shaken together, and running over, shall men give into your bosom. For with the same measure that ye mete withal it shall be measured to you again.”

  MALAKI 3:10 – 11
  10Bring ye all the tithes into the storehouse, that there may be meat in mine house, and prove me now herewith, saith the LORD of hosts, if I will not open you the windows of heaven, and pour you out a blessing, that [there shall] not [be room] enough [to receive it].
  11And I will rebuke the devourer for your sakes, and he shall not destroy the fruits of your ground; neither shall your vine cast her fruit before the time in the field, saith the LORD of hosts.

  2WAKORINTHO 9:6-8
  6But this [I say], He which soweth sparingly shall reap also sparingly; and he which soweth bountifully shall reap also bountifully.
  7Every man according as he purposeth in his heart, [so let him give]; not grudgingly, or of necessity: for God loveth a cheerful giver.
  8And God [is] able to make all grace abound toward you; that ye, always having all sufficiency in all [things], may abound to every good work:

  MPENDWA, INABIDI KUJIZOEZA KUFANYA JINSI NENO LISEMAVYO MAANA BILA HIVYO HAMTAWEZA KUONA MABADILIKO.

  1.JE, MNAMTOLEA MUNGU Zaka na SADAKA?
  2.JE, MNATOA PESA ZENU KUASIDIA WAJANE NA YATIMA?Yakobo 1:26-27.(Hata kama unaona una peasa kidogo, wewe toa hicho hicho kidogo maana Mnugu ndiye aonaye).

  HEBU ELEWA KUWA UKIANZA KUMTOLEA MUNGU SADAKA, MUNGU ATAINGILIA KATI MAMBO YA FEDHA ZENU NA ATAMKEMEA YEYE ALAYE NA ATAFUNGU MILANGO MINGI ZAIDI YA KIPESA!Malaki 3:10-11

  BILA KUTOA SADAKA KWA MUNGU NA WATU Shetani ataendelea kufunga milango ya fedha zenu!

  KUMBUKA NENO LA MUNGU LITADUMU MILELE NA MILELE,
  HIVYO KUWA MTENDAJI WA NENO NA UTAYAONA MABADILIKO!

  All my love and prayers,

  Martin.

 323. Bwana Yesu apewe sifa waumini…
  Nashukuru kupata fursa hii ya kuja mbele zenu na kuwashirikisha katika maombi yangu. Mimi ni mwanamke ambaye nahitaji mume. namuamini mungu na atatenda kwa wakati wake na ndo maana naomba na kusema mapenzi yake yatimilike.

  Sasa ndugu zangu naomba mniweke katika maombi na mungu anifungulie nipate mume ambae anamjua mungu na kumwamini pia.

  Asante na mungu awabariki.

  Koku

 324. Nawasalim katika jina la Yesu kristo!
  Wapendwa naomba mnisaidie maombi nina dada yangu baada
  ya kumaliza A-level alipatwa na matatizo ya akili,(mental desorders)
  huwa sometimes anaonekana anaelekea kupona, baada ya mda vinarudi tena!Nashukuru kwa msaada wenu!

 325. Ndugu Gabriel,

  Pole sana kwa tatizo hilo. Ni kweli kabisa mambo kama hili huwa yanasumbua sana.

  Pamoja na maombi mimi ninashauri kwamba ingekuwa vizuri dada huyo akaelezwa habari za Yesu. Ninaamini kama atampokea Yesu moyoni mwake Moto wa Yesu utaanza kuwaka ndani yake na yumkini tatizo hilo likaisha. Lakini kama ameshampokea Yesu naona ni vizuri pia kukaa na kiongozi wa kiroho au kukaa na wapendwa wengine na kuwashirikisha jambo hilo, yawezekana mkapata mambo fulani yanayotakiwa yawekwe sawa, kwa mfano yawezekana kukawa na maagano fulani yaliyofanyika juu yake na hivyo ili kuyaondoa hayo inatakiwa jitihada ya makusudi ya kumkaribia Mungu ili nguvu zake [Mungu] ziweze kuharibu maagano hayo. [Huu ni mfano tu. sina maana kwamba kuna maagano].

  Katika namna yoyote, jambo moja najua ni kwamba Yesu anaweza hata sasa!

 326. Ndugu John Paul, nashukuru kwa ushauri wako!
  Ila dada yangu huyo ni mkristo!Nina Imani Kwa Maombi Mungu atatenda miujiza.Asante.

 327. Shalom,

  Kaka Gabriel,

  Nafikiri ingekuwa ni vizuri kufahamu kama ameokoka au ni mkristo wa dini tu. Licha ya kuwa mkristo wa dini kuna nguvu ya pekee na tofauti katika wokovu, inayopatikana kwa kukubali kumpokea Yesu Kristo Kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake.

  Tuna hakika atapona,katika Jina la Yesu, pia jaribu kushirikisha viongozi katika makanisa ya kiroho yanayohubiri wokovu kama alivyokushauri kaka John Paul
  Mungu akubariki!!

 328. Wapendwa,naombeni mniombee kwani niko katika kipindi kigumu sana katika maisha yangu.Nina matatizo ya kifedha ambayo yananifanya nishindwe kabisa kupata usingizi,nahitaji maombi yenu watumishi wa Mungu.Wote tunafahamu God Is Great kuliko kila kitu na kila kitu ni mali yake.Tafadhalini niombeeni mungu afanye miujiza yake mapema,napata shida sana.
  Mbarikiwe.

 329. Asante sana kaka john paul nimekuwa nimesoma ushauri wako kwa watu wengine unatia moyo Bwana apewe sifa

 330. Mpendwa Neisa Martin,

  Nashukuru Mungu kwa kuwa umeweza kuona hilo katika michango yangu. Utukufu wote ni kwa Mungu!

  Tuzidi kuombeana katika safari hii ya mbinguni!

 331. Namshukuru Mungu kwani anazidi kupigania familia yangu nawashukuru sana kwa maombi yenu.kwa kweli MUNGU NI MKUU kwani nimemwona na ninazidi kumwona. tuzidi kuombeana

 332. Ndugu Tino,

  Pole kwa matatizo ya kifedha yaliyofikia kiasi cha kukufanya ukose usingizi.

  Mimi nina changamoto kwako. Ni kweli Mungu hufanya miujiza. Lakini anapofanya miujiza hiyo haifanyi kama ‘miujiza yake’ kama ambavyo wewe umeiita. Mungu anataka nasi tuwe sehemu ya miujiza maana yeye hahitaji miujiza hiyo bali sisi ndio wahitaji. Kwa sababu hii basi inabidi wewe, pamoja na kuhitaji maombi na huku ukiendelea kuomba, uwe sehemu ya kufanikisha miujiza hiyo ya Mungu kwako.

  Jambo la msingi la kukufanya uwe sehemu ya kufanikiwa kwa miujiza hiyo ni kuhakikisha Uko katika uhusiano mzuri na Mungu. Mara nyingi huwa tunadai mambo toka kwa Mungu hata ambapo hatuna uhusiano mzuri naye. Kuwa katika uhusiano mzuri na Mungu kutafanya Mungu asikie na kujibu maombi yako.

  Jambo jingine unalotakiwa kufanya ni kubainisha ni nini hasa unahitaji toka kwa Mungu. Mfano wa kubainisha kile unachohitaji watu waombe kwa ajili yako inaweza ikawa ni unahitaji kupata kazi. Na kama ni ndivyo wewe pia unatakiwa kuchukuwa hatua kama vile kutuma maombi kwenye makampuni mbali mbali kutokana na elimu na ujuzi wako. Katika kutuma maombi hayo ndipo Mungu anaweza kufungua mlango wa majibu mazuri kwako. Ingawa hii inaweza ku-sound kama kumsaidia Mungu kazi lakini ni ukweli usiopingika kwamba Mungu hafanyi kazi na/kwa watu wasio na malengo! Hata kama umeshafanya mara nyingi fanya tena na tena, pasipo kukata tamaa!

  Hiyo ndiyo changamoto na ushauri wangu kwako kwa sasa.

  Ukiwa mwaminifu kwa Mungu, hakika atafanya njia!

 333. Bwana Yesu Asifiwe!

  Naomba tuwaombee wanafunzi wa darasa la nne wanaofanya mitihani

 334. Shaloom wapendwa
  maombi yangu ninayotaka mshiriki nami ni kuniombea niweze kupata msaidizi wangu wa nyumbani mzuri wa tabia na anayemjua Mungu aweze kumlea mtoto wangu vizuri na awe na hofu ya Mungu na mwaminifu na pia mzidi kuombea ndoa yangu izidi kusimama na tuzidi kumjua Mungu zaidi maana Mungu ndiyo kiongozi wa ndoa. MUNGU AWABARIKI

 335. Maombi yangu ni Mungu wafuraha na neehema na rehema anisamehe yote na apate ROOM kubwa ndani ya ya roho yangu na anipe upendo zaidi na kuniponya na ugonjwa ninayo iko kama miba ndani ya maisha yangu
  na munipe moyo ya kusonga mbele kwa safari yetu ya mbinguni na muniombeye watumishi wote na nita mushuhudiya popote duniani fasi ninapotembeya
  amen

 336. Wapendwa Shalom! leo nimejitokeza tena baada ya kupotea kwa takriban miezi minne, papenda kuwaarifu ninyi mlio katika vita dhidi ya wakuu wa giza hili, yakuwa msife moyo vita ni vya BWANA yeye atapigana ninyi mtanyamaza kimya, ila vaeni silaha Waefeso 6;11-18. Msiogope kuomba tena ikiwezekana kwa kufunga, kwani vita ni vikali, simameni kwa ajili ya roho mbalimbali zinazolitafuna kanisa la BWANA, kuna roho za hatari yaani uzinzi, uchawi,ushirikina na hata ibada za sanamu zinazolivuruga kanisa la BWANA, tena tazameni malango ya makanisa yenu yakuwa ni malango ya MUNGU au ya shetani. Kwa maana YESU ndiye lango la mbinguni lakini yapo malango ambayo hayana mahusiano na MUNGU yamelitawala kanisa. Hakuna njia ya kuyavunja malango hayo ila ni kwa maombi tu. Kwa leo naomba niishie hapo tu.Ndimi mtumwa katika BWANA

 337. Bwana yesu asifiwe,

  Mimi naomba msaada wa maombi kutoka kwenu nina magumu mengi yanayonisumbua kwanza kabisa ninaomba Mungu anisaidie ili nifanikiwe kupata riziki ya kutosha ili niliweze kujikimu mimi na familia yangu

  pili naomba msaada wa maombezi kutoka kwenu ili mume wangu afanikiwe kupata kazi

  Mungu wabariki

 338. Wapendwa naomba msaada wa maombi niweze kukubalika ofisini kwani naonekana kama sina ufanisi katika kazi, Ndoa yangu ambayo ni changa pia Mungu alinde pia ampe Mume wangu Hekima ya kukubali usauri wangu, na kunishirikisha katika mambo yake. pia naiombe ofisi yangu Mungu anyooshe mkono wake kwani kuna imani nyingi za kishirikina zimetawala,pia naomba Muniombee niwe na Hekima katika maisha yangu.Mtoto wang Gabriel pia na muweka kwenye Maombi akukuwe kwenye mafundisho mema.

 339. Wandugu katika Bwana na mimi pia nashukuru Mungu sana kunipa wakati kama huu na kuomba msahada wa MAOMBI juu ya maisha yangu ya kimwili na kiroho na jamaa yangu na ndoa yangu imefika kiwango ya kuvunjika au kuachana nawaomba sana wandugu katika YESU munisaidiye na maombi turudishe upendo wetu wa kwanza na mke wangu hata pia usingizi sipata.MUNGU awabariki

 340. wapendwa ktk bwana,naomba mniombee.ninafanya ktk taasisi moja.tatizo langu,kuna bosi wangu mmoja ananichukia sana eti kisa na sababu anahisi natumiwa na watu kumloga yeye{kwamba huwa napewa dawa halafu nakuja kumuwekea} wakati sijawahi kufanya kitu kama hicho hata siku moja na nna muomba mungu anisaidie nisije kufanya kitu kama hicho. Nategemea kwenda kusoma naomba mniombee niweze kupata ruhusa kwani chuki iliyopo ni balaa.na pia mungu amsamehe kwa kua hajui atendalo.mimi nimemsamehe.

 341. Ninaomba maombi kwaajili ya Kupata kazi niliyoiomba mwenzi huu wa kumi na moja. Ni naomba pia mniombee niweze kupata ada na admission kwa ajili ya masomo niliyoomba kwenda kusoma. Pia Mungu anipatie kibali cha kuweza kufanya kazi na kusoma. Ninaomba Mnisaidie kumwombea Mume wangu mungu amrejeze kama alivyokuwa wakati alipokuwa akikutana nami. Na amani ya kweli na upendo wa kweli udhihirike maishani mwetu. Mungu awasaidie watoto wetu waweze kusoma kwa bidii na wapate ada. Asante

 342. Bwana asifiwe wandugu katika Yesu . Na mimi naomba pia maombi ya nguvu sana juu ya familia yangu iko katika vita sana mimi na bibi tuko na kipindi ya nguvu sana karibu ya kuachana an mimi na juwa pamoja na imani niko naye Mungu anisaidiye tusamehane na turudishe UPENDO yetu ya kwanza . na zaidi katika YESU

  Mungu atusaidiye

 343. Bwana Yesu Asifiwe,

  Naomba kuombewa familia yangu Baba yangu, Mama Yangu, Mimi Mwenyewe, Mke wangu, Mtoto wangu, Mdogo wangu wa kiume na wa kike tupone mangonjwa yote tuliyonayo, tufanikiwe katika maisha yetu na pia tumche Mungu.

  Mimi Tatizo langu ni usahaulifu, Tumbo, Sina nguvu, Mke wangu anauvimbe kama ziwa la tatu, baba yangu anaumwa sijajua ni nini ila ni mgonjwa, mama yangu ni mgonjwa wa kisukari na BP, Mdogo wangu wa kiume anakohoa sana, mtoto wangu analia hovyo wakati wa kula, kulala na kuamka na pia wakati wa kuoga.

  na pia tunapanga maendeleo katika familia zetu hatufanikiwi.

  kwajina la Yesu Tunaomba Msaada wako Mwalimu.

 344. Wapendwa katika kristo!mimi ni binti ni miaka 26! ninahitaji sana ushauri wenu wa kiroho,kwanza namuomba Mungu anisamehe maana nimemtenda Mungu dhambi, ila ninajua ni mwingi wa rehema naomba anisamehe nilijikuta ktk mahusiano ya kimapenzi na kijana mmoja ambaye tulikutana huko mkoani,ila kwa upendo alokuwa nae me nikaondoka huko mkoani baada ya muda akanifuata huku ila alikaa kwa kipindi kifupi sana akarudi kwao mara nikasikia amefungwa yuko jela kwa kesi ambayo haina nguvu anadai ni fitina za watu hadi sasa ninavyoongea mimi ni mjamzito nina mimba yake na hali yangu ya uchumi kwa sasa sio nzuri wapendwa naomba ushauri wenu wa kiroho nifanye nini katika hilo na mimi sina uwezo wa kwenda kumtoa huyo mtu ndani?

  Kwa ufupi niko ktk hali ngumu sana ,nashindwa la kufanya naogopa kuwaeleza kwetu!

  Asanteni sana !

  Naomba tuombeane!

 345. Kweli Dada FURAHA pole sana tayari Mungu wambingu anasikiya maombi yako . na kukusameheya kitu inabaki kufanya tu mapenzi yake na zile vingine tutaipokeya kwa imani . ata mume wako mahali anapokuwa Mungu iko na muona . Mungu aikumbuke zambi yetu ya zamani kupitiya Damu ya Bwana Yesu yote imesamehewa
  tuko pamoja kwa maombi
  ata maitanji yako anaijuwa yote.

  tuko pamoja kwa na Yesu

 346. Dada Furaha,

  Pole kwa yanayokupata. Lakini mimi kabla sijaandika mawili/matatu niliyonayo kama ushauri kwako ninahitaji na ninaomba, uthibitisho toka kwako kwamba ulichoandika ni habari ya kweli na si ya kutunga. Ninasema hivi kwa sababu kuna watu huwa wanatunga hadithi ili aone wasomaji wata-react namna gani! Na kwa kuwa umesema unaomba ushauri,ni wazi kwamba upo na unafuatilia ili usome ushauri unaopewa. Kwa hiyo natumaini utathibitisha!

  Asante!

 347. Wapendwa tuombeane, mniombee nina mimba naomba Yesu wa Nazareth aniwezeshe ili nifikie kujifungua salama na la muhumu sana tena sana nijaliwe mtoto wa kiume maana sina mtoto wa kiume, Tuombe ili Mungu afanye muujiza wake pia niwe na afya njema katika kujifungua maana huwa napata shida kujifungua mpaka mtoto avutwe na vyuma naomba hilo lisinitokee tena kwa jina la Yesu kutokana na Maombi yenu.

 348. DADA KEMILEMBE

  Ujuwe bado haujaanza kuomba msaada ya maombi Mungu wambingu anajuwa hitaji yako mwenye HAKI anaisha kwa IMANI uwe tu na IMANI MUngu atafanya vile unataka….

  Lakini ujuwe kama vile Mungu alisema ya kama mwanamuke utazala kwa ujungu kama vile inapoandikiya mu biblia atuwezi kugeunza ile lakini utazala salama

  Mungu akubariki

 349. naomba maombi yenu Mungu anisaidie nipate hela ili niweze kulipa madeni yanayoninyima amani.

 350. Nawasalim katika jina la bwana! kaka yangu John unafikiri mtu anaweza kutunga uongo ili imfaidie nn?
  Ni kwamba hilo tatizo liko kweli ndo maana nikaomba ushauri wenu!
  Naomba mnisaidie ni kitu kimetokea kweli!
  Sina thibitisho juu ya hilo zaidi ya nyie kuniamini tu!
  Asanteni!

 351. Nawasalimu katika jina la Bwana Yesu Kristo! nashukuru sana kwa sala zenu na maneno mazuri mliyonipa tuendelee kuombeana na nina IMANI MUNGU ATATENDA KAMA NILIVYOMUOMBA MAANA YEYE NI MWAMINIFU

  MUNGU ABARIKI HUDUMA HII!

 352. Dada Furaha S,

  Nashukuru kwa kuwa umeshanijibu kile nilichokuwa nataka. Nilipokuuliza uthibitishe nilikuwa na maana kwamba useme tu kama ulichoandika ni cha kweli, ndiyo hicho nilichokiita ‘uthibitisho’. Nisamehe kwa usumbufu unaoweza kuwa umetokea!

  Nitaandika ushauri wangu haraka iwezekanavyo.

 353. watumishi wa Mungu naomba msaada wa maombi juu yangu nimekuwa na matatizo ya kazi kila mahali nikipangwa kufanya kazi nahamishwa kutoka na utendaji wangu kuwa mbovu. nimejitahidi vya kutosha kubadilika lakini imeshindikana, nikifanya kazi za watu zina mapungufu makubwa sana hata nikifanya kwa uangalifu kiasi gani, Naomba msaada wenu Ndugu zangu kwani hali hii inahatarisha maisha yangu katika kazi.Niombeeni hilo jaribu liniache kwani nimejitahidi sana. wakati mwingine napata usingizi mzito kazini hata kama niko busy na kazi lakini najikuta nimechoka sana.Naombeni msaada wa maombi na Mungu awabariki

 354. Bwana Asiwe,
  Dada Kimelembi napenda kukupongeza kwa kuchua hatua nzuri ya kumkumbuka Mungu katika Shida zako,nami nitakuombea na Mungu ninae mwamini mimi atakupa Mtoto wa Kiume km utakavyo,kwani alisema:tangu lini mtu akiomba samaki ampe nyoka?na pia kila mtu atamtizia haja yake kwa kadili aombavyo.Amen

 355. SHALLOM,
  NAOMBA NIWASHIRIKISHE MAOMBI YANGU KWENU WAPENDWA KATIKA KRISTO NAOBA MNIOMBEE WATUMISHI WA MUNGU MIMI KILA NIKITAKA KUFIKIA MAFANIKIO YANGU VITA VINAINUKA VINAKUWA VIKALI SANA WAPENDWA KATIKA KRISTO NAOMBA MNIOMBEE MAANA NIMECHOKA SANA HALI YA VITA KILA LEO NISAIDIENI WATUMISHI WA MUNGU NAOMBA MAOMBI YENU NAJUA KWA MAOMBI YANU NITAVUKA

 356. nirahisi sana mbingu na dunia kupita lakini Neno la Mungu halitapita.

 357. Bwana Asifiwe, Wapendwa

  Naitwa lilian

  Mimi naomba tushirikiane maombi mimi nafanya kazi na nimesimamishwa kwa mda wa wiki mbili yaani leave but ilikuwa sio rahisi itokee leave hiyo lakini kutokana na maneno ya kazini tupo wasichana wengi ikabidi itokee naombeni maombi yenu Mungu akasimame katika kazi yangu, Na mungu akasimame mwaka ujao nataka nikafanye biashara ya kwenda nje, na hapo hapo asimame kwenye masomo yangu ambayo nakwenda kusoma,na Pia mungu aniepushe na majaribu napata kweli majaribu najua majaribu ni mtaji wa maisha lakini kwangu yamezidi.

  Mbarikiwe sana

 358. da lilian usiogope mungu ameshajua haja za moyo wako amini tu katika yote,

 359. SHALOM!!SHALOM!WAPENDWA KTK JINA LA YESU NAOMBA MAOMBI YENU MUNGU AKAPATE KUNISKIA YALE NIMEYAOMBA ILI MWAKA UJAO NIWE NA AFYA NJEMA NA MAISHA MZURI ZAIDI,NAOMBA WATU WA MUNGU WOTE MUWE PAMOJA MANI TAF NAOMBA SANA,I WILL CHANGE MY LIFE COPLETELY IN THE NAME OF THE LORD, AMEN HALELUYAA !AAAMEN HALELUYAAAA!!

 360. Bwana Yesu asifiwe wapendwa,dada Lilian Mungu atakusaidia.Mungu ndiye atakaye jidhihirisha katika kazi yako.

 361. bwana yesu asifiwe,napenda kumshukuru Mungu naomba watumishi wa bwana mniombee mimi niponywe magonjwa yangu yoote na bwana anisaidie katika kazi ninazofanya.na kaka yangu anaumwa HIV najua yesu kwetu ni rafiki tukiomba kwa babaye maombi asikia.pia kaka yangu bado ibilisi amemfunga mwombeeni ili yesu kumwonyesha njia ipasayo ili aingie shambani mwa bwana amfanyie kazi.mama yangu pia biashara si nzuri bwana awaongoze na kuwabariki Mungu mkono wake si mfupi hata ushindwe kuokoa.

 362. Naomba mniombee,niweze kusimama ktk maombi kwani nilikuwa nasali sana lakini sasa ivi nimerudi nyuma mno naomba maombi yenu watumishi

 363. Herini ya chrismas pia na hata mwaka mpya wapendwa.

  Kwanza namshukuru Mungu Kwa kuimaliza sikukuu hii nikiwa salama,pia hitaji langu ni kuomba ushirikiano wenu zaidi katika kuingia mwaka 2010 ili Neema ya Mungu iwe juu yetu sote,zaidi mniommbee amani kazini kangu kuaminika na hata kuheshimika,pia mchumba wangu Mungu Amlinde kwa yote apate hatua nyingine zaidi katika kazi yake, pia na mimi Mungu anilinde na aniepushe na mabaya yote anipe amani na kunijalia mema katika maisha yangu.pia hata ndungu zangu wote zaidi mama yangu mungu amuepushe na maradhi amjalie katika biashara yake pia hata shambani Mungu amtangulie kwa yote.ninaomba hayo nikiamini Mungu atatusimamia yote zaidi katika mwaka ujao wa 2010 uwe mwaka wa Bwana wenye mafanikio tele.
  Amina.

 364. BWANA YESU ASIFIWE SANA.
  NAMSHUKURU MUNGU AMENIBARIKI KWA MENGI SANA.
  NINAHITAJI; NAOMBA KUSHIRIKIANA MAOMBI NANYI WATUMISHI ILI NIPATE KAZI NYINGINE YENYE KIPATO KIZURI. PIA MUME WANGU EMMANUEL AOKOKE ILI TUJENGE FAMILIA INAYOMCHA MUNGU.

  MBARIKIWE SANA

 365. Bwana Yesu asifiwe mm naomba tuiombee Tanzania iwe Nchi ya amani na upendo bila kusahau kuwaombea watumishi wa Mungu ili Bwana awa kumutumikiape nguvu na kusimama imara ktk

 366. Bwana Yesu asifiwe mm naomba tuiombee Tanzania iwe Nchi ya amani na upendo na pia tuombee uchaguzi ujao ili Bwana mwenyewe atupe kiongozi anayefaa

 367. Glory to God, namshukuru Mungu kwa kuniwezesha/kunipa neema ya kuiipata Website hii. Ombi langu ni kuiombea website hii izidi kujulikana kwa watu wengine na izidi kusimama imara, shetani asiweze kuigusa. Mungu wetu anaweza, Amen!

 368. Bwana Yesu asifiwe watumishi wa Mungu, ninawapenda sana.

  Watumishi nina ombi naomba mnisaidie kulisogeza mbele za baba yetu, mimi ni binti wa miaka 31 naomba Mungu anipe mume atokaye kwake, na kwa sasa niko kwenye maombi makali kwamba mpaka mwezi wa tatu mwishoni Mungu awe ameyasikia maombi yangu na kunijibu, naamini anaweza na tena ahadi zake si za uogno, yeye huliangalia neno lake na kulitimiza, sasa akaliangalie neno lake katia Isaya kidogo nimesahau ni sura gani ila anasema “hapatakuwa na mtu wa kukosa mwenzi wake”

  Mbarikiwe sana sana sana

 369. Ndugu Wapendwa katika Bwana,

  Tuiombee nchi yetu ya Tanzania na viongozi wake ili pepo la ufisadi lisiitafune nchi yetu na pia tuombee amani ya nchi yetu

  Elisante Yona

 370. Dada Naeju mimi nakubaliana nawe kabisa kwamba ahadi za Mungu si za uongo, naye huliangalia neno lake ili apate kulitimiza. Na andiko ulilosema umesahau kidogo, ninatumaini ni hili katika Isaya 34:16 lisemalo,

  “Tafuteni katika kitabu cha BWANA, mkasome; hapana katika hao wote atakayekosa kuwapo, hapana mmoja atakayemkosa mwenzake, kwa maana kinywa changu kimeamuru, na roho yake imewakusanya”

  na katika kiingereza (NKJ) imeandikwa hivi,

  “Seek ye out of the book of the LORD, and read: no one of these shall fail, none shall want her mate: for my mouth it hath commanded, and his spirit it hath gathered them”

  Lakini pamoja na kukubalina na wewe kuhusu maneno niliyoandika hapo mwanzo ninaushauri fulani ambao ninaona ni vizuri nikuandikie ili kuongeza kiwango cha imani yako, na kukufanya uwe upande salama kwa kuchukua tahadhari.

  Ni kweli kwamba Mungu huliangalia neno lake alitimize na kwamba ahadi zake si za uongo. Nimesoma umepanga kwamba hadi mwezi wa tatu mwishoni Mungu awe amesikia maombi yako na kukujibu. Hii nayo ni ahadi. Lakini ninachotaka uchukuwe tahadhari hapa ni kwamba HADI MWEZI WA TATU MWISHONI ni ahadi yako na si ahadi ya Mungu, kwa kuwa ni wewe unapanga hivyo. Kama ungekuwa umeandika kwamba Mungu amekuambia hadi mwisho wa mwezi wa tatu atakuwa amekujibu, hilo lingekuwa ni suala jingine, na wala nisingendika haya ninayoandika! Sasa kwa kuwa umepanga wewe muda huo KUNA UWEZEKANO HADI MUDA HUO UKAFIKA NA MAJIBU HUJAPATA kwa sababu ni wewe umempangia Mungu na si Mungu amekupangia wewe. Suala la kujiuliza ni hili kwamba JE, UTACHUKUA HATUA GANI IKIWA HADI MUDA HUO MUNGU ATAKUWA HAJAKUJIBU? Je, utapanga muda mwingine tena uendelee na maombi? au utafanya nini? Je, hautavunjika moyo na kuona kama Mungu sasa hakusikii tena?

  Nimependa sana kuhusianisha maombi yako hayo na maneno waliyoyasema Meshaki, Shadrak na Abedinego walipoambiwa kwamba wasiposujudia ile sanamu ambayo mfalme Nebukadreza aliyokuwa ameitengeneza watatupwa kwenye tanuru la moto [uliochochewa mara saba kuliko kawaida yake!]. Pamoja na kutishiwa hivyo hawa jamaa kwa kauli moja walisema maneno haya, katika Daniel 3:17-18 wakisema,

  “Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa katika tanuru ile iwakayo moto; naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme. Bali kama si hivyo, ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha”

  …yaani hawa wapendwa hawakuwa tayari kuisujudia ile sanamu HATA KAMA MUNGU WANAYEMTUMIKIA ASINGEWAOKOA NA MOTO ULE WA TANURU! Maneno yaliyojaa imani kwa Mungu…Come what may!

  Nia yangu si kukukatisha tamaa bali kukupa mbinu mbadala ya kufanya imani yako IWE KATIKA MUNGU peke yake bila kujali, muda, hali na wakati. Yaani hata kama mwezi wa tatu utapita bado wewe weka imani yote kwa Mungu. Na imani iliyozamishwa katika Mungu peke yake ndiyo ambayo Mungu huiangalia. Baada ya kuweka imani yote kwa Mungu, unaweza ukashangaa Mungu anajibu hitaji lako mapema zaidi kuliko ulivyofikiria.

  [Hata hivyo miaka 31 si kwamba umechelewa ki hivyo! Umri wako bado ni mzuri tu! Kuna watu walimngoja Mungu hadi Mungu alipoleta mume katika umri ambao nikitaja hapa wewe unaweza kujiona bado ni mtoto!]

  Ninachoamini ni kwamba hii si mara yako ya kwanza kuombea suala hilo la kupata mwenzi. Lakini ninachoona ni kuwa hatua hii ya kuanza kumpangia Mungu muda wa mwisho awe amejibu ni ya hatari sana, maana ni kama kumuamrisha Mungu na si kumuomba tena! Ni kweli tunaambiwa na Yesu kwamba tuombe lolote tutakalo, kwa jina la Yesu na Mungu atalitenda lakini tunaambiwa pia tutatendewa tuliombalo tukiomba sawa na mapenzi yake. Kwa hiyo ili tupokee tunayoyaomba ni LAZIMA tuombe sawa sawa na mapenzi yake. Kwa hiyo lililo muhimu hapa si kuomba peke yake bali kuomba sawa na mapenzi yake. Na ni lazima kufahamu mapenzi ya Mungu kwetu! Ndiyo maana ni vizuri kuangalia kama ni kweli ni mapenzi ya Mungu kwamba hadi mwishoni mwa mwezi wa tatu uwe umepokea jibu la hitaji lako? Ni lazima kumfunga Mungu katika miezi hii mitatu 3 tu? Nani anaweza kujua kwamba Mungu mapenzi ya Mungu ni kukujibu labda, kwa mfano,mwezi wa 5? au wa 7?

  Ndiyo maana nikasema nimependa kuhusianisha maombi yako na maneno ya akina Meshaki na wenzake. Na kwa wewe, hapa, unaweza kuimarisha imani yako kwa kujisemea mwenyewe maneno haya, kama ifuatavyo:

  “Ninaamini Mungu anaweza kunijibu kabla ya mwisho wa mwezi wa tatu lakini hata kama hadi muda huo atakuwa hajajibu bado nitaendelea kumuamini kwamba anaweza kunipatia mume atokaye kwake, kwa muda muafaka. Sitayumbisha imani yangu kwa Mungu kwa sababu ya kuchelewa kuolewa, kwa sababu ni heri niingie mbinguni pasipo kuwa nimeolewa kuliko kuolewa lakini niikose mbingu. Ee Mungu Baba naomba unisaidie niiweze kuishikilia imani yangu hadi mwisho”

  Ninakuhamasisha dada yangu kwamba imani yenye kutoa maneno hayo ni imani ambayo Mungu huingalia ili aweze kuitimizia matakwa yake. Kama umesema maneno haya kutoka moyoni, NINAAMINI, KWA JINA LA YESU KRISTO, TAYARI JIBU LA HITAJI LAKO LIKO KARIBU SANA KUKUFIKIA!

  …Baba Mungu, ninaomba pamoja na dada Naeju kwamba utampa haja ya moyo wake, sawa na mapenzi yako. Amina!

  Dada Naeju, Neno la Mungu katika Isaya 40:31 linasema hivi:

  “Bali wamngojeao BWANA, watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia”

  Hebu ruhusu nguvu yako iwe katika kumngoja Bwana, hadi hapo atakapofanya kwa wakati wake! Endelea kuufurahia wokovu kwa kuwa furaha ya Bwana ndiyo nguvu zako![Nehemia 8:10].

  Yeye ni mwaminifu na wa kweli, hakika atatenda usipozimia moyo.

  Amina!

 371. Amen kaka John, nashukuru kwa ujumbe wako wenye angalizo na pia wenye kutia nguvu sana, hakika umenihuisha kwa upya.

  sikufikiria kumuacha Mungu wala kulegeza imani yangu kwake, hata kama asingenijibu kwa muda huo niliokuwa nimejiwekea, lakini sikuwanimefikiria nitafanya nini kama hatanijibu kwa muda huo,kitu ambacho nimegundua kingekuja kunisumbua sana na pengine kingeyumbisha imani yangu, Mungu akubariki sana kwa kunitoa katika hilo.

  Naomba Mungu anisamehe kwa kumfungia katika miezi mitatu, ninabadilisha maombi yangu na kusema “Ninaamini Mungu anaweza kunijibu kabla ya mwisho wa mwezi wa tatu lakini hata kama hadi muda huo atakuwa hajajibu bado nitaendelea kumuamini kwamba anaweza kunipatia mume atokaye kwake, kwa muda muafaka. Sitayumbisha imani yangu kwa Mungu kwa sababu ya kuchelewa kuolewa, kwa sababu ni heri niingie mbinguni pasipo kuwa nimeolewa kuliko kuolewa lakini niikose mbingu. Ee Mungu Baba naomba unisaidie niiweze kuishikilia imani yangu hadi mwisho”

  Amen,

  hv a blessed day

 372. Thank God for using you brother John to minister to me too. May God continue to use you in this area of teaching.

 373. Nami namshukuru Mungu sana kwa kuwa Naeju na Noela mmepata kitu cha kujifunza katika mchango wangu! Utukufu wote ni kwa Mungu!

  Tuendelee kuombeana katika safari hii ya mbinguni!

 374. Nakubaliana na ndugu John kwa yale uliyoandika hapo juu, ila ninapenda kujua kama kuomba kwa kumpa Mungu muda au masharti hakuruhusiwi. Nimemtafakari mtumishi Gedion na kuona kuwa alimuomba Mungu kwa habari ya ile ngozi iwe na maji wakati sehemu zingine zikibakia kavu na vice versa. Au vile mtumishi Musa alivyomwambia Mungu uwepo wako usipoenda pamoja nasi usituchukue kutoka mahali hapa Exodus 33:12-17

  Binafsi nakumbuka niliwahi kuomba isipite miaka 25 kabla ya kuolewa ila ilikuja na kupita lakini muda mfupi baada ya hapo Bwana akajibu ombi langu. Na pia nimewahi kuomba maombi kadhaa ambayo kwa kweli niliweka muda na Mungu akanijibu kama nilivyoomba na mengine hakujibu/hajajibu bado.Mungu ni baba yetu, na kwa kila jambo kuna majira/wakati wake hivyo naamini kama ni wakati wa Bwana basi umpe muda au usimpe muda yeye atajibu kama tu upo katika mapenzi yake.Na wakati mwingine Mungu anataka tuchukue hatua ya imani mfano unaoomba kisha unaanza kuchukua hatua kama vile mtume Petro alivyomuomba Bwana Yesu amuamuru atembee juu ya maji na Bwana Yesu alipomwambia njoo basi mtume Petro alitembea juu ya maji. Namjua dada aliyenunua gauni la harusi kwa imani akiwa bado hana mchumba na baadaye mchumba akatokea.

  Shalom

 375. Mpendwa Abigail,

  Ninaona kama ninawajibika zaidi kujibu hoja yako kwa kuwa ni mimi niliyeandika kuhusu hatari ya kumpangia Mungu muda awe amejibu ombi fulani.

  Kama nilivyoandika kumshauri dada Naeju, kumpangia Mungu muda kuna madhara zaidi kwa aliyepanga muda huo ikitokea hadi muda huo utafika bila majibu kutokea. Na madhara yenyewe ni kuyumbishwa katika imani. Na nimeandika hayo kutokana na hali halisi inayotokea hivi sasa. Wadada na hata wakaka wengi wamekuwa wakinaswa katika mtego huo baada ya muda waliopanga kupita pasipo jibu la mwenza. Kinachofuata huwa ni maneno kama “nimechoka kusubiri”, “labda Mungu hanisikii”, sitaomba tena bali nitachukua hatua mwenyewe” nk. Baada ya kufikia hatua hiyo wengi huwa wanaamua kuoa/kuolewa na yeyote bila kujali suala la imani na kwa sababu hiyo wengi wamejikuta wakiuacha wokovu! Ndiyo maana wewe umeshauri kwamba kama ni wakati wa Bwana haijalishi kama utampa muda au hautampa muda bali yeye atajibu tu…

  Na hapa ndipo inakuja hatari ya kumpa Mungu muda afanye jambo ambalo huo si wakati wake. Inapotokea halijafanyika mtu ataanza kuyumba katika imani yake. Kumbe kuwa katika upande salama ni kumuomba Mungu afanye jambo unalohitaji, na kwa sababu yeye ni Baba yetu anafahamu zaidi kuliko sisi wakati muafaka kwa kila jambo!

  Mfano ulioutoa wa Gideon ni mzuri lakini inatakiwa tukumbuke kwamba Gideon hakuanza tu kuomba na kumpangia Mungu kwamba ile ngozi tu ndiyo iwe na umande ifikapo asubuhi na kwingine kuwa kukavu. Kulikuwa na mzungumzo, live, ana kwa ana, kabla ya hapo. Ndiyo maana nilimwabia Naeju kwamba kama ni Mungu angekuwa amemwambia hadi mwezi wa tatu mwishoni atakuwa amejibiwa, hilo lingekuwa ni suala jingine. Mungu alishamwambia Gideon kwamba yeye atawaokoa Israel kutoka katika mikono ya Wamidiani. Kutokana na kuambiwa hivyo ndipo Gideon akamuomba Mungu amwonyeshe ishara hizo. [Waamuzi 6:36-40].

  Alichoomba Gideon ni kumwambia Mungu aonyeshe ishara kuthibitisha yale aliyoyasema bali haikuwa kumwomba Mungu athibitishe yale aliyoyasema Gideon!

  Mfano wa Musa katika Kutoka 33:15-17 nao unafanana kwa kiasi fulani na huu wa Gideon, tofauti iliyopo ni kwamba kwenye maombi ya Musa hapakuwa na ombi la muda, kwamba muda fulani ukifika kitu fulani kitokee. Musa alichomwambia Mungu ilikuwa ni kwamba Mungu atende kama alivyosema, aende pamoja nao! Na wala haikuwa Mungu atende kama Musa alivyosema.

  Inapotokea Mungu ameahidi jambo fulani, yeye ni mwaminifu hata alitimize! [Kama nilivyomwambia Naeju kwamba kama ni Mungu alimwambia hadi mwezi wa 3 atapata jibu hilo lingekuwa jambo jingine]. Mungu huliangalia Neno lake apate kulitimiza. Alimwambia Gideon atawaokoa Israel kutoka kwa Wamidiani naye akathibitisha kwamba ni yeye alisema [kwa kuweka umande katika ngozi tu na kisha ngozi tu ndiyo ikawa kavu]. Alipomwambia Musa atakwenda naye, alitimiza kwa kwenda nao wakati wote wa safari yao jangwani!

  Mungu akikuambia muda fulani ukifika jambo fulani litatokea, ni lazima litatokea. Hakuna haja ya kuwa na wasi wasi. Lakini unapomuomba Mungu kwamba muda fulani ukifika awe amefanya jambo fulani kuna uwezekano lisitokee kwa sababu pengine si wakati wa jambo hilo kutokea! Sasa linapokuwa halijatokea kama ulivyoomba kwa Mungu ni rahisi kujaribiwa, kama moyo wote ulikuwa umeuweka kwenye hitaji hilo!

  Wewe ulipoomba miaka 25 [naamini ni umri, siyo muda wa maombi]isipite, miaka hiyo ilipita lakini baada ya muda kidogo Mungu akajibu. Umri wa miaka 25 ni mdogo sana kwa mtu kuanza kuwa na wasi wasi ndiyo maana hili halikukusumbua. Ulikuwa bado hujafikia hali ya kuanza kupanga kwamba baada ya maombi ya muda fulani inabidi Mungu ajibu! Hata maombi mengine ambayo bado hayajibiwa ninaamini ni ya mambo ya kila siku kwenye maisha na si mambo ambayo yanahitajika ili ku-determine [au kuweka mustakabali wa maisha yako]. Mambo hayo huwa hayasumbui, yakijibiwa au yasipojibiwa maisha huendelea kawaida.

  Suala la ndoa/mwenzi wa maisha ni tofauti na hitaji lolote la maisha ya kila siku kwa binaadamu. Haliwezi kulinganishwa na kazi, pesa, nyumba, shamba, gari nk. Ni suala zito. Ni suala ambalo huchukua moyo wote wa mtu. Ninaamini ni suala namba moja linalotusumbua sana watu tunapokuwa tumefikia hatua ya kuhitaji kupata mwenzi wa maisha. Kwa hiyo ili kupanga kwenye maombi kwamba baada ya muda fulani Mungu awe amejibu, kunahitajika uthibitisho kwamba muda huo unaotajwa kwenye maombi Mungu haye anahusika katika kuupanga. Kwa sababu muda unaotajwa kwenye maombi ukipita imani inaweza kuingia kwenye jaribu, na jaribu hili ni la kujitengenezea mwenyewe!

  Nilichomshauri dada Naeju na ambacho naona wewe umekiandika pia ni kwamba hakuna sababu ya kupanga muda bali muda muafaka ukifika Mungu atatenda tu!

  Kwa hiyo kuomba Mungu kwa kumpa muda au masharti, ninavyofahamu mimi, kunaruhusiwa lakini lazima kuwe na ukweli kwamba unapompa Mungu masharti iwe ni yeye ndiye alianza kuahidi kwamba atatenda jambo fulani. [Hata hivyo ninafikiria kuna tofauti kati ya kumuomba Mungu ishara na kumpa masharti]. Kuomba kwa kumpangia Mungu muda madhara yake kwa mwombaji ni pale inapotokea muda aliompangia Mungu kujibu utapita pasipo majibu…na hiki ndicho niliandika kumshauri Naeju!

  Natumaini nitakuwa nimejibu hoja yako, japo kwa sehemu. Lakini kama majibu yangu yatakuwa yamesababisha maswali mengine ninayakaribisha ili tuendelee kujifunza.

 376. Asante kaka John kwa majibu yako. Nimekulewa japo ninaomba wewe au yoyote anisaidie katika hili kwamba Mungu akikupa ahadi kuwa atafanya kitu fulani hapo ndipo unayo haki ya kumpa muda?nauliza hivi kwa sababu mwingine anaweza sema kwamba mtu haitaji kusikia live kuwa Mungu amesema mfano nitakupa mume/mke ila anaweza kusema kuwa neno la Mungu tayari lipo yaani Biblia na imejaa maneno mengi sana ya Mungu ambayo mtu anaweza kusimamia katika hitaji/ombi lake, sasa hapo je utasemaje? Mfano unaweza kusema neno lasema Bwana akasema sio vema mtu huyo awe peke yake, au apateye mke hupata kitu chema nk. Pia niongeze kwa kusema kuwa hata kama ni Mungu ndie aliyetupa muda au ahadi kuwa atafanya kitu fulani bado ni wajibu wetu kuendelea kuomba na kumkumbusha pasipo kuchoka (Luka 18:1)

  Pia ningependa tu labda kwa kuendelea kujifunza namna ya kuomba, tuangalie huko kumpa Mungu ishara ulikokusema ndugu John kuna tofauti gani na kumpa masharti. Mfano kama dada Naeju atabadilisha maombi yake kwa kuomba apate mume ifikapo mwezi wa tatu ili iwe ishara kuwa Mungu anaheshimu alichoahidi, mfano Yer 33:3 inasema niite nami nitakuitikia.. basi naomba unipe mwenzi na mwezi wa tatu usipite kwa kuwa Mungu unaliangalia neno lako ili ulitimize na umesema ombeni nanyi mtapewa!

  Ninasubiri kujifunza zaidi.

 377. Mpendwa Abigail,

  Ninaomba nikujibu na kama kuna mwingine mwenye kuwa na majibu ajisikie huru kuandika alicho nacho, ili tuendelee kujifunza.

  Ninavyofahamu ni kwamba Mungu akiahidi atatenda jambo fulani [la kipekee siyo la kiujumla kwenye Biblia], hapo unakuwa katika nafasi nzuri ya kumuomba Mungu athibitishe kama ni kweli jambo hilo litatokea. Hapa ndipo mtu unaweza kuomba kwamba ‘kama kweli ni wewe Mungu umesema utafanya hivyo, ninaomba wakati fulani utimize ishara hii ili nijuwe ni kweli wewe umesema’. Hiki ndicho alichofanya Gideon. Kama ni Mungu ndiye atakuwa amesema ni lazima atatimiza ishara hiyo inayotakiwa kufanyika katika muda unaoombwa ili isije ikaonekana si yeye aliyekuwa amesema.

  Niliandika kuhusu mazungumzo live kati ya Gideon na Mungu kwa ajili ya kufafanua mfano huo. Lakini hadi leo Mungu anasema na watu live, ukiacha Neno la Mungu lililo katika Biblia. Lakini bado inafaa kabisa kusimania Neno la kwenye Biblia, ili mradi tu uko katika mapenzi ya Mungu. Tatizo ni pale mtu anapotaka kusimamia mstari wa Biblia kwa ajili ya kujitafutia mahitaji yake pasipo kuzingatia hali ya uhusiano wake na Mungu. Hata hivyo Neno la kwenye Biblia ni neno la kiujumla. Kwa mfano hakuna mahali palipoandikwa ‘mtu anatakiwa aombe kwa miezi miwili ndipo apate jibu’ bali liko andiko linalosema ‘ombeni bila kukoma’ na ‘kila aombaye hupewa’ na maandiko mengine yanayofananana hayo. Kwa hiyo pamoja na kutumia Neno la kwenye Biblia kuna umuhimu wa mtu kuwa na uwezo wa kuisikiliza sauti ya Mungu, ambayo si lazima iwe audible/ya kusikika masikioni bali yaweza kuwa ya kusikika moyoni. Masikio ya nyama ni kwa ajili ya kusikizisha sauti mwilini inayosikika angani lakini pia kuna masikio ya rohoni ambayo husikia sauti ambayo masikio ya nyama hayawezi kuisikia. Na ana heri mtu ambaye anaweza kuisikia sauti ya Mungu!

  Ni kweli kwamba tunakiwa kuomba pasipo kuchoka. Lakini mimi nilipoandika Mungu akiahidi hatuna haja ya kuwa na wasi wasi ni kama vile alivyomuahidi Sara kwamba angepata mtoto. Hatusomi popote Sara akimuomba Mungu baada ya hapo,ili kweli ampate mtoto. Hata pale Mariamu,mama wa Yesu, alipoambiwa atapata mtoto kwa uwezo wa Roho mtakatifu, sidhani kama ni sahihi kusema aliendelea kumuomba Mungu ili ampe mtoto kama malaika alivyomwambia. Watu hawa, ambayo ni mifano, waliendelea kumsubiri Mungu huku wakidumu katika mapenzi yake. Hiki ndicho nilikuwa namaanisha nilipoandika kwamba Mungu akiahidi ni lazima atafanya, hakuna haja ya kuwa na wasiwasi. Lakini kwa habari ya kuomba, kwa ajili ya mambo ya kijumla, ni lazima tuendelee kuomba bila kukoma kwa sababu hatimaye Mungu husikia maombi na kuyajibu, kama ilivyokuwa kwa yule mjane katika Luka 18:1-5.

  Kumuomba Mungu atimize ishara, ninakokuandika mimi, ni kule kumuambia Mungu afanye jambo kuonyesha kwamba ni kweli ni yeye ndiye alisema. Hii hutokea ambapo mtu amesikia sauti moyoni/masikioni mwake lakini akawa hana uhakika kama kweli ni Mungu ndiye aliyesema. Hivyo ili kupata uthibitisho kwamba aliyesema ni Mungu ndipo mtu huyo huomba kwamba ‘kama kweli ni Mungu ndiwe umesema, ninaomba ufanya jambo fulani ili nifahamu ni wewe’. Huku ndiko kumuomba Mungu ishara!

  Wote tunajua kwamba Biblia ni Neno la Mungu. Hatuna wasi wasi kwamba pengine baadhi ya maandiko hayakusemwa na Mungu. Kama kuna maandiko tuna mashaka nayo kwamba hayakusemwa na Mungu, hapo tuna haki ya kumuomba Mungu afanye ishara ili tuamini kwamba ni kweli neno fulani la kwenye Biblia kumbe ni kweli linatoka kwa Mungu. Lakini kama tuna uhakika kwamba kila Neno la kwenye Biblia lina pumzi ya Mungu, na linafaa kwa mafundisho hatuna sababu ya kuomba ishara. Bali tunatakiwa kuomba Mungu alitimize kama alivyosema.

  Kumpa masharti Mungu ni kule kuomba kwa kudai kwamba ‘Mungu ninaomba hadi wakati fulani uwe umefanya jambo fulani’. Huku ni kumpa Mungu sharti la muda. Maana yake ni kwamba muda huo ukipita pasipo kujibiwa Mungu atakuwa ameshindwa. Kama tunakubaliana kwamba kila jambo lina wakati wake na kwamba Mungu anafahamu vizuri zaidi wakati muafaka wa kila jambo kuliko sisi, basi hatuna sababu ya kumfunga Mungu katika muda bali tunatakiwa kuomba mapenzi yake yatimizwe katika tunayoyaomba.

  Ahadi za Mungu ni za kweli naye huliangalia Neno lake apate kulitimiza. Lakini je, kuna ahadi yoyote ya Mungu kwamba ‘mtu akiomba kwa miezi mitatu ndipo atapata jibu?’ naamini jibu la swali hili ni ‘hapana’. Ahadi ya Mungu ni kwamba kila aombaye hupewa, lakini hakuna ahadi ya muda kwamba kila aombaye ‘kwa muda fulani’ atapewa. Kwa hiyo kama dada Naeju ataamua kubadilisha maombi na kuomba hivi; ‘basi naomba unipe mwenzi na mwezi wa tatu usipite kwa kuwa Mungu unaliangalia neno lako ili ulitimize na umesema ombeni nanyi mtapewa’ ninavyofahamu mimi ni kwamba Neno ambalo Mungu ataliangalia ili alitimize ni lile la kusema ‘ombeni nanyi mtapewa’ na si la ‘mwezi wa tatu usipite’ maana hilo la muda hajaliahidi yeye. Akiomba atapewa lakini si lazima iwe ndani ya miezi 3 kwa kuwa Mungu anafahamu muda muafaka kwa jambo hilo kwa mtu anayeomba. Inaweza kuwa kabla, ndani ya muda au baada ya muda ulioombwa jambo hilo lifanyike!

  Inawezekana kabisa kuomba Mungu atende jambo fulani ndani ya muda fulani. Kama jambo hilo lina kibali kwa Mungu atalitenda kwa muda huo. Lakini ikitokea haliko katika kibali cha Mungu haliwezi kutokea. Na linapokuwa halijatokea si lazima kwamba Mungu hataki kulitenda bali yaweza kuwa Mungu atalitenda lakini si kwa muda huo unaoombwa maana si muda muafaka. Na linapokuwa halijatokea, kama yule mwombaji hana msingi sahihi wa imani yake, kuna uwezekano mkubwa wa imani yake kuyumbishwa, kama ambavyo nimeshaandika kwenye michango yangu miwili iliyotangulia. Hili ndilo lengo langu la mwanzo kabisa na la msingi la kumshauri dada Naeju!

  Yeremia 33:inasomeka hivi;

  Niite nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu, usiyoyajua.

  Mtu anapokuwa amemwita Mungu na Mungu akamuitikia, yeye Mungu humuonyesha mtu mambo asiyoyajua. Mambo haya yasiyojulikana na mtu ni pamoja na mapenzi ya Mungu kwake. Na mtu akishayajua mapenzi ya Mungu kuomba kwake kutakuwa na mafanikio sana maana kila analoliomba ataliomba kulingana na mapenzi ya Mungu na wala si kulingana na matakwa yake mwenyewe. Kuomba kwa matakwa wakati mwingine kunaweza kusijibiwe, lakini kuomba sawa sawa na mapenzi ya Mungu ni lazima hujibiwa!

  Namalizia kwa kunukuu Warumi 12:2,

  Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.

 378. Shalom wapendwa,

  Nashukuru kaka JP kwa ufafanuzi wako mzuri, mimi nafikiri huenda hofu na kuangalia mazingira, maneno ya watu ndiko kunakotupa mahangaiko kina dada wengi

  Kutafuta na kujua mapenzi ya Mungu huleta amani kubwa ambayo hata kama watu wakikucheka au kuona umechelewa inakuwa si tatizo kwako. Nafikiri tukikaa ndani yake kwa uaminifu na kwa imani basi tutajua mipango yake kwetu

  Zab 25;14
  ‘siri ya Bwana iko kwao wamchao, Naye atawajulisha agano lake’

  Mimi nafikiri Mungu haangalii ndoa kwa kigezo cha umri. Ndoa inathamani kubwa kwa Mungu ndiyo sababu inahitaji maandalizi pia, anamuandaa kila mtu kwa muda tofauti tofauti, kwa sababu kila mmoja yupo tofauti. Kwa mfano hata watumishi wa Mungu nao waliandaliwa tofauti kwa kazi ambazo Mungu aliwakusudia, Musa aliandaliwa kwa muda tofauti ukilinganisha na Daudi na wengine tofauti.

  Nashauri tutafute kujua mapenzi ya Mungu kwetu, na kuisikia na kuitambua sauti yake ktk njia anazoweza kutumia, ndoto, moyo n.k.

  Roho Mtakatifu anahitajika mno katika hilo, maana hufumbua hata mafumbo magumu kuhusu maisha yetu na mipango ya Mungu kwetu ya sasa na yajayo.

  1Wakorintho
  ‘Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho, maana Roho huchunguza yote hata mafumbo ya Mungu”

  Mungu awabariki

 379. shalom.wapendwa naomba mnisaidie maombi.ninataraji kufunga ndoa mwezi huu.nimekuwa na wakati mzuri na mchumba wangu,kufhamiana na pia kuhakikisha uhalali wa kuwa kwetu pamoja.kwakweli namshukuru Mungu tumekua na uchumba safi,hatujaharibu!lakini tangu mwezi wa tisa mwaka jana we went through a very rough road but by God’s GRACE tukapita kwa ushindi.but now it’s even worse,vita imehama toka kua yetu(mimi na yeye)na wazazi wangu na sasa ni wazazi wake na kwa ufupi tu ishu ni mahala pa kuabudu.binti ameokoka na alihama hata kabla hatujakutana,wazazi wanasema hata wao wamokoka hata kama wanaabudu palepale.sisi hatuna tatizo na hilo ila sasa ni kama wanalazimisha hata taratibu za suala zima zifuatwe zile za kanisani kwao!

  Mchungaji wangu ameakasirika na anasema hawawezi kumpangia utaratibu since sisi ndio waoaji.kwa neema ya Mungu tulioneshwa hili suala disemba mwaka juzi na tukashughulikia lakini kwakweli sasa hata mara nyingine nawaza(Mungu anisamehe)mbona wasiofuata utaratibu huwa na unafuu kidogo (maana huishia kutengwa tu).natamani ndoa ya utukufu,sitaki kukosea.niombeeni Bwana anisaidie kutoka hapa na anitie nguvu.

 380. Bwana Yesu asifiwe wapendwa.Naomba mniombee nina vita kali sana kazini,lakini najua ni majaribu,napenda kumuonyesha boss wangu kuwa nguvu za giza anazozimini haziwezi kupambana na damu ya Yesu iliyomwagika msalabani.atashindwa tu,maana kazini hakuna amani kabisa.naomba mnisaidie kuniombea ili tumwangushe ibilisi.amina

 381. Bwana Yesu apewe sifa.Naomba mniombewe nifunguliwe katika vifugo vya shetani vingi nilivyofugwa navyo ili Mungu aweze kunifugua katika mahitaji yangu kama, elimu, mume mwema afya njema na mafanikio kiuchumi, hekima na maarifa.Kwakuwa Mungu nimwema na mwaminifu na amini yakwamba yote atanitendea na shetani hatapata tena nafasi ya kunijaribu Amen.

 382. Bwana yesu asifiwe. nawapenda sana na Mungu awabariki.naomba mniombee Mama yangu mkumbwa nasumbuliwa na mguu apate kupona pia mama yangu mzazi alipata tatizo la akili hadi sasa anatumia dawa hivyo hajapona kabisa. pili naomba mniombee katika kazi yangu niweze kufanikiwa na Mungu apate kunifungulia nipate mume bora katika maisha yangu. mbarikiwe wote

 383. Bwana Yesu apewe sifa! Nawapenda sana.Naomba niombee kwa Mungu hitaji langu likamilike la kupata mume mwema na mwenye upendo wa kweli.Nimekuwa nikiishi peke yangu na watoto 2,kwa miaka sita sasa, toka Mungu amchukue mume aliyenipa 1990.sasa nina hitaji hilo tena.
  pili,muwaombee watoto wangu waweze kushinda katika mitihani yao ya kidato cha nne mwaka huu 2010. pia Mungu awape ulinzi wake na afya njema na ufahamu katika masomo yao.pia awajalie kuenenda katika njia zinazompendeza Mungu,na kudumu katika imani ya mwana wake YESU KRISTO.
  Tatu, namshukuru Mungu kwa kunipa afya njema na ulinzi wake, pamoja na baraka zake kwa kipindi chote hiki nilichoishi bila mwenza.namuomba azidi kuwa pamoja nami katika kila jambo.

 384. bwana Yesu asifiwe wapendwa katika kristu wapendwa naomba niwashirikishe hitaji langu mniombee maana nahitaji msaada wa Mungu katika hiki kipindi kigumu mimi nimeolewa lakini toka niingie kwenye hii ndoa mambo si mazuri kama nilivofikiri maana mwenza anafanya mambo bila kunishirikisha ananidharau pamoja na ndugu zangu nikimweleza hanielewi hataki kujirekebisha anakua mkali na vijitabia vingine vingi tu vinanikwaza naomba mtuombee ndoa yetu ipone maana mahali tumefika si pazuri. Mungu awabariki sana

 385. Dada Kaijuko je Umeokoka? na mmeo je ameokoka? Yesu anaweza hilo sio gumu ni laini mno kwake.naomba ujibu swali langu ukiweza.

 386. Bwana asifiwe sana, naomba maombi yenu kwa kumuombea mke wangu Anita ambaye anaumwa sana na kusumbuliwa na mapepo,ameamua kumjua bwana tangu decemba 2009,tangu hapo anaumwa sana,anatetemaka sana,homa hazipungui na bado tunaendelea na maombi.kama kuna mtu mwenye ushauri anisaidie.Bado tunaamini kwa njia ya maombi na kwa jina la yesu atapona.bwana awabaliki sana amen.

 387. Kaka Elisha kama ameokoka matatizo yameisha matokeo ya mwilini yatadhihirika muda si mrefu,kwa sababu mtu anaanza kuponywa roho kwanza alafu mwilini kunafuatia hata kama unamuona anaumwa huo ni ujanja wa shetani tu ukweli ni kwamba ameponywa.baada ya mtu kuombewa na ukamuona amezidiwa juwa wazi kuwa tayari muujiza kaupokea ila sasa shetani anapinga na nikawaida ya shetani kupinga anataka kutengeneza hofu akiri kuwa hakuponywa alafu arudi kuombewa,hapo ajichunge unaweza ukakuta unaomba kitu ambacho tayari umepokea. wewe sasa mwambie mgonjwa aweke imani yake yote kwa yesu na pia usitazame hali ya mkeo inayokatisha tamaa wewe tazama neno la yesu tu simama kwenye kweli ya neno.na pia tutaungana na wewe kuombea hali hiyo ikome mala moja awe huru kwa jina la yesu.Ushauri mwaminini yesu tu.

 388. Shalom,

  Bwana Yesu Asifiwe,
  wapendwa niombee nahitaji mtoto,
  nimeolewa miaka zaidi ya mitatu sasa sijapata mtoto naomba maombi yenu.

  Mungu anayejibu maombi akutane na haja ya moyo wangu.

 389. Bwana Yesu Apewe sifa wapendwa

  wapendwa naomba mniombee mimi na familia yetu baba mama dada na wadogo zangu kwa sababu ni familia yenye matatizo tangu wazazi walipotengana.mimi nimeokoka kasoro wazazi wangu na wadogo zangu imekuwa kila jambo ninalotaka kufanya haliendi kama nitakavyo iwe ilikuwa kuanzia masomo yangu mpaka katika familia ninazopita na kuishi nao kwa sababu sijawahi kukaa na baba wala mama tangu nikiwa na miaka mitano mpaka sasa na miaka 22.dada yangu alipata ujauzito akiwa darasa na saba kwa sababu hakuwa na matunzo mazuri kwa baba wala kwa mama hilo pia likaja tokea kwa mdogo wangu ambae alitakiwa aende secondary baada ya kufaulu nae hakupata mtu wa kumpa support akapata ujauzito nae. Nahitaji niendelee na kusoma na hakuna nimtegemeae zaidi ya Mungu, nahitaji maombi yenu, ahsanteni kwa ushauri ntakaoupata na maombi

  BWANA YESU AWABARIKI

 390. PRAISE THE LORA.APOSTLE MABOYA PRAY TO GOD TO GIVE ME WISDOM,LOVE,PEACE,FAVOR,PROSPERITY IN JESUS NAME.PRAY FOR MY FINANCIAL BREAKTHROUGH.NOWADAYS I STRUGGLE A LOT TO GET MONEY FOR SCHOOL FEES,HOUSE RENT,FOOD,EVEN MONEY TO GO TO CHURCH ON SUNDAY WITH MY FAMILY.I AM MARRIED BLESSED WITH TWO BOYS.I WAS A MUSLIM I CONVERTED TO CHRISTIANITY.MY BUSINESS OF WRITTING AND SELLING CD’S IS COLAPSING.PRAY TO GOD TO GIVE ME MONEY TO TITHE,PAY ALL MY DEBTS,BUY MY OWN HOUSE,CAR,AND EXPAND MY BUSINESS.GOD BLESS YOU.

 391. Mungu awabariki sana nawapenda.
  Naomba mfanye maombi kwa ajili ya watoto wangu watatu ili Mungu azidi kuwapigania katika maisha yao hasa katika masomo yao wawe na uwezo mzuri katika msomo na hasa mkubwa anatarajia kufanya mtihani wa kidato cha nne mwaka huu aweze kufanya vizuri katika mtihani wake. Mungu awaepushe na magonjwa maana hayo ndo yanakwamisha watoto kimasomo. wamjue Mungu kwamba ndiye muweza wa yote na waepushwe na mabalaa yote

 392. wapendwa mbarikiwe,
  naomba mshirikiane nami katika maombi kwa ajili ya familia yangu na mimi mwenyewe kwan ninapita katika kipindi kigumu sana, adui yangu mwovu shetan amejiinua anawinda roho yangu, kwan magonjwa na mitihan imeniandama,machozi yangu ndo yamekuwa chakula changu, lakini sitokata tamaa, ninamtazama yesu wangu, tuwe pamoja

 393. Bwana yesu asifiwe, nilikuwanaomba mniombee niko katika wakati mgumu na ndoa yangu, mume wangu anafanya biashara hafanikiwa amefikia hata hatua ya kukata tamaa na hitaji sala zenu pia mimi naendelea kuomba sana nampenda mungu najua atatufungulia kama yeye alivyosema ombeni nanyi mtepewa bisheni nanyi mtafunguliwa basi nazidi kuamilini.

 394. nawasihi wote katika jina la Bwana kweli ombeni bila kukoma. kuhusu ndoa yangu namshukuru Mungu tangu nimeanza kumlilia Mungu juu ya suala hili ameonekana, mume wangu tuzidi kumuombea Mungu amrudishe speed zaidi ya YONA. YEYE MUNGU ANAWEZA SANA.hatimaye baada ya miaka mitatu ndio Mungu kaanza kuleta mawasiliano kati yangu na shemeji yangu. NAMSHUKURU KWA HILO, NAMSHUKURU ROHO MTAKATIFU KWA KAZI HIYO NZURI, LILIBAKI NIOMBEENI NAHITAJI KUWAONA WATOTO WANGU.

 395. HERI AOMBAYE KWA AJILI YA WENGINE NAYE BWANA ATAHUSIKA NA YEYE MAHITAJI YAKE YOTE. ILE LAANA YA KIZAZI CHA TATU NA NNE WAMCHUKIZAE ITABADILISHWA NA KUWA BARAKA VIZAZI VYAKE VYOTE.

  NAMPENDA YESU NA AHADI ZAKE. NAKUALIKA KUMWAMINI.
  imani ni kuwa na hakika na mambo yatarajiwayo ni bayana na mambo yasiyoonekana. imani akuongoze yote roho mtakatifu.

 396. kama maandiko yasemavyo kuwa OMBENI BILA KUKOMA – Nami bado namlilia Mungu aweze kunitimizia haja za moyo wangu.1- Namwomba awape watoto wangu mafanikio katika masomo yao, na awape kushinda katika mitihani yao.
  2. – Namwomba Mungu anipe mume mwema, mwenye upendo wa kweli, kwangu na kwa watoto wangu.
  3. – Namwomba Mungu afya iliyo njema na ulinzi wake maishani mwangu, mimi na familia yangu.
  4. – Anijalie baraka na neema zake zilizo nyingi.
  5. – Anisamehe dhambi zangu zote.- NAOMBA MSHIRIKIANE NAMI KATIKA KUOMBA HAYA.

 397. Bwana wetu Yesu asifiwe, wapendwa naomba mnikumbuke katika maombi. Naomba Mungu anifungulie milango nipate kazi nzuri na dada yangu mary apate mtoto.

 398. Bwana Yesu asifiwe. Wapendwa dada na kaka zangu ambao mpo katika maombi ya kumwomba Mungu mwenza, naomba mara unapompata urudi mbele za Mungu kuuliza kama ndiye kabla ya kufunga ndoa. Nipo katika hilo hitaji na ninapenda kushirikiana na vijana wenzangu katika hili. Miaka michache iliyopita tulikuwa na hitaji kama hili kwa ajili ya dada yangu mmoja, mwanzoni tulifikiri itachukua muda mchache Mungu kutujibu, lakini ilichukua zaidi ya miaka 5 Mungu kutujibu, kwa kweli mimi nilikata tamaa na dada yangu alikata tamaa zaidi yangu. why? sio kwamba katika kipindi hicho wachumba hawakujitokeza? hapana, walijitokeza wengi kwa nyakati tofauti, wengine wasomi, wafanyabiashara, wafanyakazi, watanashati na kila aliyekuja tulirudi mbele za Mungu kumuliza Mungu kama ndiye ila wote hao Mungu alisema hapana, kila pale Mungu aliposema hapana tulirudi tena kwake kuuliza hapana kwa nini? Wapendwa Mungu alinifundisha sana katika hili kuna mwingine alikuwa anasema ameokoka lakini kumbe ni mlevi, mwingine kahaba,mwingine hana pendo la dhati na Mungu alidhihirisha haya pale tulipokuwa tunarudi kwake kuuliza kwa nini hapana. Ilituchukua muda katika maombi lakini mwisho Mungu alimpa kilicho chema (mume wa kufanana nae) hii inanipa changamoto sana ya kuendelea kumngoja Bwana. Nimeshuhudia binti wengi wanapomwomba Mungu Mume na kijana akitokea huwa wepesi kuingia kwenye ndoa kabla ya kurudi tena mbele za Mungu kuuliza kama ndiye. Wapendwa tunapomuomba Mungu mweza shetani nae hutafuta mtu wake yeye hapendi ndoa yenye utukufu wa Mungu kwani ni pigo kwa ufalme wake, ila unaporudi tena mbele za Mungu atamweka wazi kama si wake. Mungu awasaidie wote mlio katika hitaji la kupata mwenza, tufunguke macho ya rohoni tuweze kujua mbinu za shetani na kuzishinda. Tuingie katika ndoa itakayomtukuza Yesu wetu na kumwaibisha shetani na ufalme wake. Amen

 399. Bwana asifiwe!

  Mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu,niko katika wakati mgumu sana siyo siri! Kuna assignment tulichelewa kusubmitt mimi na group ya watu watano na ikifika hadi mwisho maana yake ni incomplete na mwishowe ni disco,sasa ombi langu kwa Mungu ni kuiondoa hilo Incomplete iwekwe marks hata sifuri na kuendelea,naamini Mungu atafanya jambo katika hili na sitakata tamaa nitaendelea kupigania vita ya kuiondoa na kuwekewa marks kuanzia sifuri na kendelea. vile vile na kulegeza moyo wa mwalimu ili aweke marks maana alikataa kweli kupokea kazi yetu na kutusaidia,ombi langu ni kwamba Mungu achukue nafasi yake na aifanye kazi hiyo badala ya huyo Mwalimu.

  mambo yatakuwa mazuri katika jina la Yesu Kristo.

  Mungu awabariki!

 400. kwajina naitwa chonya essau mwnafunzi wa chuo kikuu cha DODOMA Mwaka wa tatu naomba mniombee nipate kazi pindi tu ntakapo maliza chuo mwezi Julay,Pia naomba muiombee familia yangu kaka angu naye apate kazi,Pia namshukuru MUNGU Dada yangu anepata kazi,Naomba pia mumuombee mama yangu MUNGU amtie nguvu na ampe ujasiri katika shughuli zake za kila siku BWANA YESU AWABARIKI.

 401. Praise the lord,
  kwa majina ni Edwin Nyamagwa kutoka wilaya ya Nyamache,kwanza kabisa namshukuru Mungu wetu kwa Amani na hutulifu tangu ‘2007′magombano na vita katika Nchi yetu ya Kenya.Na sasa wapendwa nawasii kwa jina safi la Yesu Kristo muiombee nchi,viongozi wetu wakisiasa na wa Dini Mungu awape ufunuo na maono,wanapopigana vita dhidi ya ufisadi.wapendwa naona nikama shetani ana mipango ya kuharibu nchi na kufuruga amani, twahitaji maombi ya dharura.Nami mniombee Mungu anisaidie katika maisha ya ukristo.Asanteni sana.

 402. Wapendwa,

  Ninampa pole kila mtu mwenye hitaji ambaye bado anasubiri jibu. Najua mahitaji yetu ni mengi lakini ninaamini pia si lazima yote yatakamilishwa. Kwa kuwa kuna wengine wetu hawatayaona majibu ya maombi yao, kwa kuwa wakati wa kuondoka duniani utafika kabla ya majibu ya mahitaji yao. Siandiki haya kwa ajili ya kutisha wala kukatisha tamaa bali ni kwa ajili ya kutia moyo na kuhimiza katika safari ya mbinguni.

  Mtume Paul aliandika hivi katika Wafilipi 1:20-21,

  “Kama vile nilivyotazamia sana na kutumaini, kwamba sitaaibika kamwe, bali kwa uthabiti wote, kama siku zote na sasa vivyo hivyo Kristo ataadhimishwa katika mwili wangu; ikiwa kwa maisha yangu au ikiwa kwa mauti yangu. Kwa maana kwangu mimi kuishi ni Kristo na kufa ni faida”

  Nimeona niandike haya ili kukumbushana kwamba kwa mtu ambaye ni mkristo kweli kweli kuishi au kufa yote ni faida tu; hakuna hasara. Kwa hiyo pamoja na kuwa tuna mahitaji mengi, na mengine ni mazito sana, yatupasa kujiangalia mioyo yetu isije ikalemewa na mawazo na maombi kwa ajili ya mahitaji yetu ya kimwili huku tukisahau roho zetu. Lakini hii haina maana tuache kuomba, hapana!….Tuendelee kumuomba Mungu tena tukiwa na imani na shauku ya kupokea majibu ya maombi yetu!

  Lakini kwa mtu ambaye hajajisalimisha kwa Yesu, kulitumia jina la Yesu kwa ajili ya kujipatia mambo ya mwilini peke yake ni kuli-under-utilize. Na wala hakuna faida yoyote kwa kupata vitu vyote unavyovihitaji wakati roho yako inaelekea upotevuni. Ndiyo maana Yesu alisema haitamfaa mtu chochote hata kama ataupata ulimwengu wote lakini akapata hasara ya nafsi yake [Math 16:26]. Kwa hiyo ili mambo yaende sawa sawa, utaratibu ni Yesu kwanza moyoni halafu ndipo mahitaji ya mwilini yafuatie!

  Yafuatayo ni maneno ya wimbo wangu wa maombi, ambayo kwayo ninaomba na kila mmoja kwa hitaji lake alilo nalo:

  Tumekuja mbele zako wenye shida mbali mbali
  Tukitazamia kupokea kutoka kwako Mungu
  Hakuna Mungu mwingine mwenye kutusaidia
  Wewe ndiwe kimbilio letu, tunakimbilia kwako.

  Hakuna mwingine, hakuna mwingine, hakuna mwingine tena.
  Hakuna mwingine, hakuna mwingine, wa kutusaidia.

  Wengine wetu ni wagonjwa, na wengine ni mahututi
  Kwa jitihada za kibinaadamu tumeshindwa kupata uponyaji, tunakimbilia kwako.

  Wengine twasaka amani, mioyo yetu yahangaika
  Amani ya dunia haitufai, yanyauka upesi kama maua, tunakimbilia kwako.

  Mahitaji yetu ni mengi, kila mmoja na la kwake
  Kwa kuwa uweza wote una wewe, hakuna linalokushinda Yehova, tunakimbilia kwako.

  Hakuna mwingine, wa kutusaidia
  Ni wewe Yehova, wa kutusaidia
  Ni wewe Mesiah, wa kutusaidia
  Hauna mbadala,wa kutusaidia
  Hakuna mwingine, wa kutusaidia.

 403. Wapendwa, nawasalimu katika jina lipitalo majina yote Bwana wetu Yesu Kristo. Nina kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa mambo mema na mengi anayonitendea toka kuzaliwa kwangu hadi wakati huu.

  Naomba mniombee na zaidi tuombeane kuondokana na umaskini, maana si mpango wa Mungu Binadamu aishi au afe akiwa maskini, nimejaliwa kupata Mume na tumebarikiwa kupata watoto 3. La zaidi naomba mniweke katika sala zenu tuweze kujenga ili tuishi vyema na familia yangu, naamini katika kushirikiana kwa maombi yote yanawezekana.

 404. Bwana asifiwe.
  Namuomba mungu aweze kuimarisha maisha ya ndoa yetu na mipango yetu iweze kufanikiwa ili tuweze kuwa na maisha marefu zaid.

 405. Bwana Yesu asifiwe wapendwa,namshukuru Mungu ni mwema kwangu maana amenitendea mambo mengi ambayo sikustahili ila ni kwa upendo wake.
  Naombeni mniombee niweze kupata kazi nategemea kumaliza chuo may, pia nina dada zangu wamemaliza chuo hawana kazi Mungu akafungue mlango wa kazi kwa ajili yao. EE BWANA YESU TENGENEZA NJIA KWENYE FAMILIA YANGU
  Asanteni Mungu awabariki

 406. Bwana Yesu asifiwe. Naomba mumuombee mwanangu Blandina Leah, anayesumbuliwa na vichomi vya ajabu, na maumivu ya kifuani na sehemu ya moyo. Naomba Mungu ampe ulinzi muda wote awapo shuleni. Amrudishie ufahamu wake na uelewa katika masomo yake.Pia mumuombee na dada yake Theresia Grace MUNGU aweze kumpa ulinzi wake, na ufahamu pia na uelewa katika masomo yake. AMIN

 407. Wapendwa mubarikiwe sana naomba samahani kwa usumbufu wa izi lines mana computer ninayo tumia ni ya kifaransa. Mimi naishi uku Canada nataka maombi yenu yatende miujiza nipata kazi nzuri nimemaliza masomo. Alafu mzidi kuombeya inchi ziko Uraya na Marekani shetani amekuwa na wa fuasi wengi kupita bwana Yesu.

 408. WAPENDWA, KOTE NAOMBA MAOMBI JUU YA MIMI KUWAONA WANANGU. YANI MUNGU HUYU ASIYESHINDWA NA JAMBO AFUNGUE NJIA YA MIMI KUKUTANA NA WANANGU AU KUMALIZA TATIZO.

  NINAKAZI, NINASHIBA ILA NAHITAJI kuwaona wanangu HOPENICE NA HOPELILY. SIWEZI KISASI KWA MUME WANGU BALI NAMUOMBA MUNGU AFUNGUE NJIA KWA HILI SUALA. ANIHURUMIE SANA SANA.KWANI NAWALILIA USIKU NA MCHANA.

  MUME WANGU ALIBADILIKA TABIA BAADA YA KUTOKA ULAYA. KWELI ALININYANYASA HADI KUNIFUKUZA, YEYE KWA SASA HAJUI MAENDELEO YANGU YOYOTE ANAJUA LABDA AKILI ZIMENIRUKA AU NIPO JALALANI. KUMBE MUNGU ALIYEKAUSHA BAHARI YA SHAMU YUKO NAMI PIA. KANIPA KAZI, KANIVIKA, NATARAJIA UJENZI WA NYUMBA. HIVYO YOTE SAWA WANANGU.

  NAOMBA MAOMBI YENU MUNGU ATASIKIA, NAMUAMINI SANA ALIKONITOA NI MBALI.

  NILIKUWA MWEMBAMBA LEO MNENESANA NGUO ZINABANA, HATA MUME WANGU HUYO ALIYENIFUKUZA TUKIONANA HATA AMINI NAE ATAKIRI KUWA MUNGU YUPO. ASIYEANGALIA UMBO, ELIMU.

  MBARIKIWE NAWAPENDA, NIWEKENI KWENYE MAOMBI JUU YA WANANGU HAO. PLEASE.

  ESTER. DAR.

 409. Naomba kuelekezwa jinsi ya kufanya maombi ya toba mana mwaka 2001 mwezi wa saba nilitoa mimba ya mwezi mmoja au miwili sikumbuki vizuri ilikuwa kubwa kiasi gani.Nilikuwa mwanafunzi wa chuo kipindi hicho.Naomba wapendwa mniombee Mungu anisamehe hiyo dhambi pia nilikuwa naomba kusaidiwa niombeje ili nipate kusamehewa na Mungu dhambi ya uuaji na dhambi zote nilizokwisha fanya

 410. Tafadhali naomba maombi yenu, mimi nimjamzito ninapata kizunguzungu na ninaota ndoto mbaya.Wapendwa naombeni muungane nami katika maombi katika JINA LA YESU AMEN. MT 18:18

 411. MIMI PAUL MEELA NAOMBENI MNIOMBEE MAANA SASA NIKO KWENYE WAKATI MGUMU NASOMA CHUO CHA UALIMU LAKINI ADA SIJAMALIZI NAOMBENI MNIOMBE

 412. nawaombeni mniombee niko katika jaribu zito kwanza nimezungukwa na maguu(ibilisi)kila kona ninayofanya kazi.nafanya kazi kwa ugumu sana.niombeeni nishinde wadhalim hawa ili nimtangaze yesu kwa kishindo cha hali ya juu.

 413. Wapendwa katika bwana nawaomba mniombee,kwani tangu mwaka huu ulipoingia nimekuwa sina amani nyumbani pamoja na kazini kila mtu ananichukia bila sababu,kila ninalolipanga haliende kama ninavyo lihitaji,hata nikiwa na pesa inapotea kiajabu ajabu.

 414. Naomba niombewe ili nipone tumbo linalonisumbua na naamini kwa jina la Yesu ninaenda kufunguliwa katika vifungo hivi

 415. nawasalimu ktk jina la yesu kristo.
  naomba mniombee nipate kazi nzuri yenye kunilipa vizuri na yenye mda mzuri wa kutoka. Pia naomba mnisaidie kwa maombi ili mume wangu aokoke. amen

 416. Bwana Yesu asifiwe!
  Wapendwa naomba mniombee sana kwa Mungu azidi kunishika kwa mkono wake hodari maana hiko katika majaribu makubwa familia na marafiki na adui, ili niweze kusimama ktk Imani yangu ya Kumwamini Bwana Yesu kuwa yeye atosha ktk maisha yangu. Nguvu ya Roho Mtakatifu wa Mungu izidi kutenda kazi maishani mwangu.sana ila nina hakika Mungu ataniwezesha!
  Asanteni sana na Mungu azidi kuwatumia kwa ajili ya utukufu wa Jina lake!

 417. Ninawapenda sana katika yesu kristo aliye bwana na mwokozi wa maisha yetu.
  Ninaomba mniombee mungu aonekane kwenye ndoa yangu kwani mume wangu anatumikishwa sana na shetani.
  Mimi nimeokoka naninampenda sana yesu wangu pia najua iko siku atomkomboa mume wangu.Pia naomba mungu aonekane kwa watoto wangu wakue ktk maadili yake,n kwenye masomo yao wawe vichwa na sio miguu.mungu mwenye huruma awabariki wote. Amen

 418. Mbarikiwe,
  wapendwa naomba mniombee juu ya ndoa yangu mume wangu ameacha wokovu zaidi sana amekimbia familia na hapigi cm wala hela ya matumizi kwa kweli niko katika kipindi kigumu sana naomba Mungu amrejeshe ampe uchungu,amfunulie,hofu ya Mungu imfunike ghafla huko aliko,naamini hakuna gumu la kumshinda.

  MUNGU AWABARIKI

 419. Jambo Rafiki

  Naomba mniombee! nimekaa muda mrefu bila kupata kazi, nimekatishwa tamaa na nachoka kuvumilia nahitaji Mungu anisaidie

  Mimi sijaokoka watu wamekua wakinishauri nifanye mapenzi na mpenzi wangu wakati mimi siko tayari kuoa, nifanyeje?

  Naishi Kenya naomba maombi na ushauri. Amen

 420. Bwana Yesu apewe sifa. Mungu awabariki wote wanaochangia katika kutoa mafundisho na kuwajenga watu kiroho.Namshukuru Mungu kwa kunionyesha website hii. Nina jambo la kuwatia moyo wale wote mnaomuomba Mungu maana ni kweli Mungu anajibu maombi…Nilikaa kwenye ndoa miaka sita bila kupata mtoto. Mume wangu alichukua mwanamke nje ya Ndoa akazaa naye.Nilipogundua iliniumiza sana..Hasa pale mume wangu aliposisitiza kuwa hawezi kuachana na huyo mwanamke kwa sababu ameshazaa naye.Nikazidi kumlilia Mungu kwa ajili ya jambo hili…LISILOWEZEKANA KWA MWANADAMU KWA MUNGU LINAWEZEKANA..mwaka jana nikapata ujauzito na nikajifungua mtoto wa kiume sasa ana miezi minne.PIA MUNGU AMEMWEZESHA MUME WANGU KUACHANA NA YULE MWANAMKE…Wapendwa naomba tumwombee huyu mwanamke apate Mume wa kumuoa ili asiendelee kuingilia ndoa za wengine ..na pia mume wangu asirudi kumtafuta tena.Ndoa iheshimiwe na watu wote….MBARIKIWE WATUMISHI WA MUNGU.

 421. Wakristo wenzangu, ninajua Mungu hutenda kwa wakati wake lakini kwa ubinadamu wangu naona kama amenitupa kwenye jambo moja, Upendo. Ni mpweke mno, nimemwomba mchumba, mume, marafiki lakini bado sijapata. Mnikumbuke katika maombi yenu.

 422. Ndg Derryl,

  -Binafsi ninamshukuru sana Mungu aliyekupa ufunuo kuwa mahali hapa [SG]kuna Mungu.

  -Pia, ninamshukuru sana Mungu wetu kwako Ngd. Derryl kwa kujijua kuwa hujaokoka, hii inaonesha wazi kuwa Yesu Kristo umekupa ufunuo wa kujua kuwa wokovu una thamani.

  -Pia ninamshukuru sana Mungu aliyekupa ufunuo kuwa kufanya ngono au uasherati si sizuri.

  Ni kweli kuna Mungu mahali hapa, (SG) ndiyo maana hata wewe umepata ufunuo kutoka kwake na ukahitaji uombewe na watu wa Mungu.

  Mimi mwenyewe kwa kushiriki katika web hii, (SG) nimejifunza mengi sana, hivyo nakupa tumaini kuwa hujakosea, mahali hapa pana Mungu aliye hai, ambaye atakuwezesha kupata mahitaji yako ya mwili na Roho.

  Baraka za Mungu huwaendea wale wanaomtambua na kumkubali kwa kujikabidhi kwake ili awatawale. Kumkubali Yesu ni kuokoka kwa tutubu dhambi zote kwa kumaanisha kuziacha kabisa na kumfanya Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yetu. Ukifanya hivyo yaani ukiokoka unakuwa na ujasiri hata wa kumwomba kwa sababu, tayari Yesu mtoa baraka anakuwa yuko ndani ya moyo wako.

  Pamoja na hayo yote, pia ni muhimu kufahamu kuwa, hakuna hata mmoja atakayemwona Mungu au atakayekuwa na Mungu milele iwapo atakuwa hajaokoka! Wote wanaokufa pasipo wokovu mahali pao ni Jehanamu ya moto na hatimaye ziwa la Moto! Hakuna hata mmoja aliyepata kwenda aliko Mungu pasipo wokovu kwanza hapa duniani. Hata kama mtu ataishika dini yake kwa viwango vyote, lakini kama hajaokoka yaani kuwa na Yesu, atakuwa anapoteza muda wake bure na hiyo dini yake!

  Maandiko yanatuambia kuwa Yesu ndiyo njia pekee ya kutufikisha mbinguni, [Yohana 14:6]. Hii ni kwa sababu mwanadamu wa kwanza, Adamu alitenda dhambi na wanadamu wote walioendelea kuzaliwa wameendelea kuwa na dhambi, [Warumi 5:12], (sikunukuu kama ilivyo). Yesu Kristo alikuja ulimwenguni ili kutulipia kosa alilolifanya Adamu wa kwanza. Alilipa kwa kutolewa sadaka ambayo ilikuwa ni kifo cha kumwaga damu msalabani. Hivyo kwa kumkubali na kumpokea tunakuwa tumeshika njia iliyo bora ya kutufikisha mbinguni.

  Tunapoamini kuwa damu ya Yesu ilimwagika kwa ajili ya dhambi zetu, nasi tukachukua hatua kwa kutubu dhambi zetu kwa kumaanisha kuziacha na kumwomba Yesu Kristo kwa imani kuwa atusamehe, tayari tunapokea wokovu. Tunasafishwa dhambi zetu kwa damu ya Yesu Kristo iliyomwagika akiwa msalabani kwa njia ya imani. Baada ya kufanya hivyo, dhambi tunakuwa tunaziona kama zilivyo, si kwa kuhizi tu au kutokufanya dhambi kwa sababu zetu binafsi, mfano; kama ulivyosema Ndg. Derryl hapo juu kuwa huwezi kufanya ngono kwa sababu hutaki kuoa! Hapa si swala la kutokutaka kuoa ambalo ni suala la ubinafsi, bali ni dhambi kabisa za kutupeleka motoni kwa kufanya uasherati huo, unaona!

  MTU BILA KUOKOKA HUWEZI KUZITAMBUA DHAMBI KATIKA ROHO!
  Ninakuomba ndugu yangu Derryl, na wengine kama wewe, kwa imani fuatisha maneno haya niliyoyaandika hapa chini, ambayo bila shaka baada ya kuyafuatisha kwa imani mtapata wokovu ambao utakuwa ni baraka sana.

  MUNGU BABA,
  HAKIKA MIMI NI MWENYE DHAMBI,
  NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE,
  KWA KUMAANISHA KUZIACHA,
  BWANA YESU,
  ULIYEISHI HAPA DUNIANI,
  BILA KUTENDA DHAMBI,
  NIPE UWEZO WA KUSHINDA DHAMBI,
  KATIKA JINA LA YESU,
  NAKUSHUKURU BWANA YESU,
  KWA SABABU UMENISAMEHE KATIKA JINA LA YESU, AMEN!

  Mungu ni mwaminifu sana, baada ya kutubu dhambi hizo kutoka moyoni kwa kumaanisha kuziacha kabisa, umeshapata wokovu. Maandiko yanasema kuwa, yeye anayekwenda kwake au anayejisalimisha kwake, yaani Yesu Kristo, hawezi kumtupa nje kabisa, [Yohana 6:37], (sijanukuu kama yalivyo).

  MPENDWA DERRYL na wengine waliofuatisha maneno hayo kwa imani, mpaka hapo umepata wokovu, tafuta kanisa linalohubiri wokovu, ili ukazidi kujifunza zaidi jinsi ya kuukulia wokovu ulioupokea.

  MPENDWA DERRYL na wengine kama Derryl wanaonifuatilia, maandiko yanatufundisha kuwa, tuutafute kwanza ufalme wa Mungu na haki yake, tukifanya hivyo Mungu atatuzidishia na baraka nyingine tunazozihitaji, [Luka 12:31].

  MPENDWA DERRYL, kuhusu kazi uliyokuwa unaitafuta kwa muda mrefu, kwa vile tayari umekabidhi maisha yako kwa Bwana Yesu, kuanzia sasa, kwa imani, anza kutuma maombi ya kazi kutokana na sifa zako au anza kutembelea sehemu ambazo utashuhudiwa kuwa unaweza kupata kazi eleza nia yako ya kutaka kazi hapo. Fanya hivyo kwa bidii, huku ukimtanguliza Mungu katika kila jambo, Bwana ni mwaminifu utaona matokeo yake.

  Hata hivyo, imani yako isilenge tu katika kupata kazi au baraka za dunia, bali katika moyo wako jiwekee malengo kuwa, maisha yako ni wewe na Yesu Kristo, katika kupata kazi , katika kukopsa kazi, katika shida katika raha, amani na machafuko, kufanikiwa na kutokufanikiwa, milima na mabonde; koke wewe na Yesu tu. Mungu akiuona moyo wako uko hivyo, hakika kwa wakati wake atakubariki.

  Amani ya Kristo ikufunike Amen!

 423. Bwana Asifiwe Wapendwa! Napenda kuwashirikisha,naomba tushirikiane kwenye maombi ,mniombee niko kwenye kipindi kigumu sana cha mapito!Naomba kuwashirikisha mniombee ili Mungu atende kadri ya Mapenzi yake.

  Vilevile naomba mniombee nizidi kusimama kwenye imani maaana majaribu ni mengi sana,

  Asante na Mungu awabariki sana! Wapendwa hakika Mungu anaweza!

 424. naomba mungu amsaidie mwanangu aweze kuendelea vizuri, amuepushe na magojwa, amuepushie nimonia pamoja na macho yanayobadilikaga kuwa njano

 425. Bwana Yesu asifiwe wapendwa, wapendwa mie nashukuru kwa huduma yenu Mungu azidi kuwatia nguvu. Mimi naomba mniombee kwani nimekutana na majaribu mengi baada ya kuolewa tu ndugu zangu wameinuka juu yangu hadi mama mzazi kumekuwa hakuna maelewano katika familia yetu pia naomba mniombee mungu aniwezeshe kupata mtoto kwani kila ikitokea inakuwa bahati mbaya naomba maombi yenu Mungu aweze kutenda muujiza wake kwani nimenenewa maneno mengi mno na ndugu zangu. asanteni sana.

 426. bwana yesu asifiwe, jamani wapendwa ninaomba maombi yenu kwa ajili ya ndoa jamani kumekuwa na pepo wa wanaume kutoka nje ya ndoa tuzidi kumwomba mungu kwa ajili ya ndoa zetu jamani, pia ninaomba tuombe kwa ajili ya wanawake wanaotumia nguvu za giza mungu aweze kuziteketeza na warudi kwa mungu ambae ana huruma ya ajabu, pia naomba tuwaombee watoto wetu jamanimungu aweze kuwalinda na kuwaepusha na mabaya yote ,, mbarikiwe sana nahitaji maombi yenu sana, mungu awatie nguvu

 427. Bwana Yesu apewe sifa naomba mniombee Bwana Yesu azidi kumbadilisha mume wangu na amani ipatikane ndani ya nyumba yetu, akatufungulie milango yote iliyofungwa uponyaji wa roho zetu na miili yetu tunaitakasa kwa damu ya Yesu Kristo

 428. Nashukuru lkwa maombi yenu,Mungu anijalie nipate watoto na wawe wema na waje kuwa watumishi wa Bwana Yesu Amina

 429. Bwana Yesu apewe sifa naomba mniombee Bwana Yesu azidi kumbadilisha mume wangu na amani ipatikane ndani ya nyumba yetu, ukatufungulie milango yote iliyofungwa uponyaji wa roho zetu na miili yetu tunaitakasa kwa damu ya Yesu Kristo na kupata watoto wema

 430. Tuombe kwaajili ya wale wote wasiojiweza na walioko katika mazingira magumu. Kuna watoto, wanawake, vijana, wazee, wanavijiji na watu wengi zaidi wanaoishi katika mikandamizo ya maisha, tuwaombee. BWANA WETU YESU KRISTO ASIFIWE

 431. Wapendwa Bwana Yesu apewe sifa.Napenda kutoa shukurani zangu kwani mwanagu Blandina Leah anaendelea vizuri sasa,vile vichomi vya sehemu ya moyo, vimetoweka.Bwana Yesu apewe sifa!
  Nami nimeokoka sasa,nimeyatoa maisha yangu kwa Bwana Yesu. Hivyo naomba mniombee nizidi kukua katika neno.Na kusimama kwa ukamilifu katika neno la Mungu.pia bado nomba tuendelee kuwaombea watoto wangu ulinzi wa damu ya bwana yesu katika maisha yao. na mafanikio katika masomo yao. magonjwa yasipate nafasi kwenye miili yao. Bwana Yesu awape baraka zake.Nami anipe ulinzi wake katika kazi yangu na nyumba yangu, na afya yangu. Amen.

 432. Shallom

  Wapendwa niombeeni kama mie navyaombea, natafuta mchumba niolewe, nina miaka 26, nina fanya kazi kampuni moja hivi Arusha, NIMEOKOKA,
  Niombeeni nipata mume mcha MUNGU.
  AMEN

 433. SHALOM WAPENDWA WA MUNGU.
  Ninamshukuru Mungu kwa uwezo wake mkuu kwani nimekuwa nikiandika maombi mengi mara kwa mara hapa SG na Mungu amekuwa akinipigania maombi hayo,

  Hivyo ninapenda kuwakujulisha ya kuwa Mungu kwa neema yake kuu kanipa ofisi kama nilivyo muomba nilikuwa ninaomba nipate sehemu yangu ili nifungue biashara kwani nimepata na tayari nimeshafungua sasa nina wiki mbili na bado ninaendelea nayo hivyo ninaomba mzidi kuniombea ili iwe ni biashara ya kuleta faida na maendeleo pia niweze kulijaza duka langu nipate wateja wengi pia nisipungukiwe na kodi ya kulilipia na hata gharama zozote zitakazohitajika pia mtaji ukue zaidi ya hapo kwani ninamwamini Mungu kwani sikutegemeaga kwamba na mimi ningepata shughuli yangu binafsi ila kwa kweli Mungu kumuelewa ni kazi.

  Basi wapedwa naombeni mzidi kuniombea hata mama yangu awe na afya njema, dada zangu wadogo zangu na hata familia yangu zaidi mchumba wangu ambaye yuko sudan kikazi Mungu amlinde sana ili arudi salama kwani nchi ile ni nchi yenye vita.

  pia hata mimi Mungu anilinde na Maradhi pia hata kazini nilipoajiriwa anilinde kwa yote pia nahitaji ulinzi wa maisha yangu kwa ujumla.

  MZIDI KUBARIKIWA WAPENDWA,

  AMEN.

 434. Nawasalimu nyote katika jina la Yesu Kristo.
  Ningependa kuwasilisha ombi la kufunguliwa maishani maana shida zinaniandama moja baada ya nyingine tangu mwaka wa 2001.
  Naamini Mungu yu nami pamoja na jamii yangu katika mapito haya magumu.
  Amen.

 435. nakusalimu kwa jina la yesu. mimi nahitaji maombi kwa ajili ya kupata kazi. pia nahitaji maombi niweze kutumika vizuri katika kusudi la Mungu kwa mafanikio na Mungu pekee anitumie kama apendavyo.

 436. Bwana Yesu apewe sifa wapendwa naomba mumuombee dada yangu anaitwa Angel Kidulile anaenda school of law apate kufanya vizuri katika masomo yake

 437. Nashukuru kwa wote ambao mtajumuika katika maombezi na Mungu awape neema na baraka. Naomba mniombee nipate kazi na pia rafiki yangu hajafanikiwa kupata mtoto kwenye ndoa kwa muda wa miaka saba.
  Asanteni kwa upendo wenu na Mungu awape nguvu.
  Aunty Nyamizi

 438. Naomba mniombee niweze kupata kazi nyingine kwani hii niliyonayo pato lake nashindwa hata kusomesha na kujikimu kimaisha

 439. Wapendwa ninaomba maombi yenu pamoja na msaada wenu kwani hivi sasa ninakabiliwa na madeni makubwa kiasi kwamba mawazo yangu hayakai sawa kila ninapokumbuka mzigo huu.

 440. Bwana Yesu Asifiwe sana!
  kweli Mungu ni mwema, na ni jukumu la kila mmoja katika ulimwengu huu mwenye pumzi kumshikuru Mungu na Kumtukuza.
  Kwa kweli kuwa karibu na Mungu na kumuomba Mungu kwa bidii inasaidia sana
  Mimi binafsi nimemuona Mungukupitia Maombi na bado anazidi kunipigania
  naomba mniombee niweze kusimama katika imani yang kwa sababu majaribu ni mengi, na zaidi pia naomba
  mniombee nifanikiwe katika maisha yangu na shughuli zangu hasa za kimasomo na wakati huo huo nikiwa natafuta kazi, na pia niwe na imani kuwa Mungu anaweza yote.
  Nawtakia kazi njema mnayoifanya, nasi tuzidi kuombeana
  Mungu awabariki sana na Roho wa Mungu awaongoze
  Ahsanten

 441. Bwana Yesu asifiwe!

  Naomba kuomba pamoja nanyi ili Yesu ambadilishe mke wangu katika mawazo ya kutaka talaka.

  Mungu awape pia awape hekima na busara wote wanaomshauri na kumpa nguvu katika jitihada za kuvunja ndoa. Mungu ameshawadhihirisha kwangu tayari.

 442. Damas,
  Mungu akutane haja ya moyo wako.
  Pia sababu za mke wako kutaka talaka zikijulikana kwa washauri wako, utaweza kushauriwa vizuri zaidi.
  Damu ya Yesu iwape upatanisho.

 443. ndugu naomba mniombe natafuta kazi.hasa naleta shirika la mwedo na mount meru flowers na nmb ambapo nilipeleka applicationzangu

 444. Shalom? naomba mniombee wana SG nime jaza maombi ya nyumba huku ninakoishi nimekubaliwa kesho ndio siku ya kuchukua funguo naomba muombe kwaajili yangu nitakapoenda kusiwe na pingamizi namimi pia naomba. Pia da mary naomba tuwasiliane ni mimi helen wa finland tuwasiliane kwa email na mungu awabariki team ya SG

 445. Bwana asifiwe!
  Kwanza nashukuru Mungu sana kwa hiyi website, waga nabarikiwa kila ninapo yitembeleya. Na Mungu azidi kuwabariki sana kwa kazi yake munayo yifanya.

  Mi naomba muniombeye nipate furaha na amani ndani ya moyo wangu na maishani mwangu. Pia naomba muniombeye nipone, iyo ugonjwa nimekuwa na karibia myezi5.

  Asante sana kwa musada wenu, Mungu abariki sana.
  Aimee

 446. Bwana Yesu asifiwe. Mimi ni dada, naomba maombi kwa atakayekuwa na mzigo wa kuniombea,hata ushauri pia nitashukuru. nimeokoka lakini bado nasumbuliwa na jini mahaba. Naota ndoto chafu, na siku nyingine naota nikiwa nanyonyesha watoto wakati sijawahi kuzaa. Naomba sana msaada wenu, maana naona kwa maombi yangu tu hali inajirudia.Nachukia sana jambo hili, naumia sana kufanya mapenzi ndotoni wakati binafsi nimeokoka na mambo hayo sina. Nisaidieni jamani nifanyeje mimi?

 447. Bwana Yesu asifiwe wapendwa!
  1.naomba mniombee wapendwa,shetani mbaya sn,nimepata mchumba,ila shetani anakuja kwa kasi kubwa sn sasa,ameingilia kipato cha mchumba wangu amesimamishwa kazi,na alipanga aende kutoa mahari ila inakuwa ngumu naona kwani hana kazi na alipanga aende kutoa mahari huu mwezi wa 5,sasa kazi shetani amempokonya je atawezaje kutoa mahari?
  2.kumekuwa kama pepo hivi au sijui ni nini,huyo mchumba wangu amekuwa mkali sn sana siku hizi yaani ukifanya kitu kidogo tu ambacho labda kitamuudhi jamani inakuwa ni ugomvi mkubwa kweli,ila zamamni hakuwa hivyo sasa nashindwa kuelewahuyu shetani anaingilia uchumba wangu au?
  NAOMBA MAOMBI JAMANI.

 448. Dada Agnes, tatizo lililokukuta ni sawa na la kwangu. Mimi nitakuweka kwenye maombi, na pia wanamaombi wa SG pia watatuombea. Ila Mungu ni muaminifu na hakuna kisicho wezekanana kwake. Nguvu za shetani zitashindwa kwa Jina la Yesu Kristo daima milele amina.
  Aunty Kay.

 449. Bwana Yesu asifiwe wapendwa.Mimi nahitaji maombi yenu. Bwana Yesu anipiganie katika maisha yangu ya kimwili,kiroho na kiakili pia. Aiponye mwili,nafsi na moyo.Amen.
  neema zephania

 450. Shalom Wapendwa,ninahitaji maombi kuhusu hali yangu ya kiuchumi.Ninaomba muujiza na rehema za Mungu ziniwezeshe kulipa madeni yote niliyonayo ili niweze kuishi kwa Amani na Kumtumikia Mungu vizuri.Ninakosa amani kutokana na madeni niliyonayo.Naomba maombi yenu.

 451. Shalom,
  mimi naomba maombi yenu niko katika matatizo makubwa.
  Nipo hapa Marekani, nimekutana na mtanzania online
  ambae yuko Malayshia tukafahamiana kwa njia ya email.
  baada ya mda aka niomba nimsaidie anunue vitu online
  huku Marekeni harafu vije kwangu nivipakie kwanye box moja alafu ni mu agizie sababu vilikuwa kwenye mabox mbalimbali akadai ni kuepuga galama ya ku post!!mi sikudhania lolote sababu alinambia ni mkristo,
  nikamuagizia hiyo ilikuwa mwaka jana. Undugu uliendelea sasa wiki jana akaniomba tena akidai hari ni ngumu anaomba anunue vitu vije kwangu nimuwekee kwenye box moja alafu nimuagizie kama awali ili auze angalau apate ka faida, nikasema wote tunatafta maisha haina shida nitakusaidia, alhamisi mzigo ukaletwa na POLISI wakadai yule kijana ananunua vitu
  kutumia CREDIT CARD ya wizi, ndo maana alinidanganya mzigo ipite kwangu!!!ni kafunguliwa kesi na sasa nangojea kujibu mashtaka naombeni msaada wenu wamaombi ili Mungu anitendee haki.

 452. Bwana Asifiwe !
  Ndugu zangu napenda kuwashirikisha yafuatayo;
  >naomba tushirikiane kwenye maombi ,mniombee niko kwenye kipindi kigumu sana cha mapito! Hasa katika swala la mahusiano Maana kwa muda mrefu nimekuwa nikimwomba Mungu katika hili Kiasi nilihisi kukata tamaa. Mwaka ulipoanza Nimepata rafiki yamkini nazani atakuwa ndo niliyepangiwa na Mungu hivyo naomba sala zenu.
  > Zaidi ya hilo. bado siishi kulingana na mafanikio yangu kielimu. Bado naishi maisha duni. Yaani kipato kidogo. Naomba maombi yenu.
  > Tatu nimekuwa naishi kwa hofu sana, hofu ya majini, wachawi n.k.
  Hii ni kutokana na sababu za kihistoria na mazingira nayoishi. Kwa mfano mahali napoishi huwa nasikia vitu vya ajabu napambana navyo kwa jina la Yesu ila hujirudia rudia mpaka hofu imeniingia. Kazini vile vile.
  Natanguliza Shukrani
  Mungu atende kadri ya Mapenzi yake.
  Amina!
  Vilevile naomba mniombee nizidi kusimama kwenye imani maaana majaribu ni mengi sana,

  Asante na Mungu awabariki sana! Wapendwa hakika Mungu anaweza!

 453. bwana yesu kristo asifiwe.Naomba maombi Mungu anisaidie nisimame kiroho, nisiwe na hofu popote linapotokea jaribu nguvu za roho mtakatifu ziwe juu yangu kunishindia.Pia naomba mniombee nipate kazi,nimemaliza chuo tangu 2008 sijapata kazi ya kudumu.Mwisho ninaomba Mungu anisaidie niweze kushinda kesi ya nyumba ambayo hukumu imepangwa tarehe 14 mwezi wa sita.

 454. Bwana Yesu kristo asifiwe sana wapendwa. mimi mi mwanamke wa miaka 28 ninampenda yesu na Mungu amekuwa akinipigania kila iitwapo leo.Mimi ni mama wa watoto wawili wote ni wakiume.
  kwanza nimesikitika sana na kumuonea huruma sana kaka GABRIEL wa marekani, najua jinsi anavyojisikia maana na mimi niko marekani pia, kesi hii ya wizi Marekani ni ngumu sana lakini Kaka nakuhakikishia na uamini, HAKUNA HAKIMU ZAIDI YA MUNGU,Na bwana wetu Yesu alimaliza yote pale msalabani,wala usiogope kakangu mungu yupo pamoja na wewe na mungu ni mwaminifu siku zote jana,leo na hata nilele, Wewe omba na mimi ninakuombea pia minawaomba wanamaombi wote kote ulimwenguni tumuombee Kaka Gabriel Mungu akaonekane mahali pale alipo kaka huyu Amen.
  pia mimi ninawaomba mniombee ninatamani kuwa na amani kilawakati kwasababu nimekuwa nikikosa amani bila sababu kitu kidogo tuu kinanifanya nichukie. Nawaomba mniombee ili hali hii isinitokee tena. pia naomba muwaombee watoto wangu Mungu awape akili na uwezo mkubwa ktk kumjua mungu na ktk masomo yao pio.
  Pia tusisahau kuliombea Taifa la ISRAELI.
  MUNGU AWABARIKI NA AKUTANE NA HITAJI LA KILA MMOJA ALIE ANDIKA OMBI LAKE NA NINAAMINI MUNGU ATAJIBU KATIKA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETI AMEN.

 455. KAKA GABRIELL
  USIJALI MUNGU YUPO PAMOJA NA WEWE NA ALITUAHIDI KUTUSAIDIA NA ALISEMA HATAUACHA MGUU WA MTUMISHI WAKE USOGEZWE NA ADUI.
  PIA HAYO NI MAJARIBU TUU YA SHETANI YATAPITA KTK JINA LA YESU. MUNGU AKUTIE NGUVU NA TUNAKUOMBEA KWA MZIGO KAKA.
  AMINI YESU ANAWEZA.
  YESU NI MAMBO YOTE.
  ATAFANYA KATIKA JINA LA YESU.

 456. Shalom!!
  wapendwa kazi yeni ni njema Bwana azidi kuwatia nguvu.
  naomba mumkubuke mdogo wangu kwenye maombi anaumwa sana, ana maralia kali amepungukiwa damu, hivyo na amini maombi ya wengi yana nguvu naomba Bwana amponye amwezeshe kumalizia masomo yake salama.Na zaidi sana amwokoe. vile vile Bwana akuze kiroho changu anipe roho wa neema na kuomba.
  Hakika hakuna gumu la kumshinda.

 457. BWANA YESU ASIFIWE,MIMI NAOMBA MAOMBI YENU NIPO KATIKA KIPINDI KIGUMU UCHUMI, KIFAMILIA KIKAZI NAHIVYO NAOMBA TUSHIRIKIANE KATIKA MAPITO HAYA MAKALI KWANI NINA IMANI NITAYASHINDA KATIKA JINA LA YESU KWANI YEYE NDIYE MWEZA WA YOTE.ASANTENI KWA UPENDO WENU MUNGU AWABARIKI.

 458. Bwana Yesu asifiwe. Naomba maombi mungu anisidie katika masomo yangu na pia anijalie nipate mume mwema kwani swala la mume limekuwa ni jaribu kwangu, mungu anisaidie niwe mvumilivu. Pia mungu anisaidie katika kazi yangu niwe na mafanikio. Amen

 459. Bwana Yesu Asifiwe!!
  Naomba maombi yenu, kwani mi, na familiya yangu tunatatizo la kila tunapo panga tufanye kitu fulani kwa anjili ya familiya hatufikii malengo kunatokea matatizo/au mtafaruku tu (mzozo)usiokuwa na sababu juu ya lengo mliloweka na hitaji maombi yenu, kwani hii hali inapo tokea huleta ugovi na kuanza kulaumiana ndani ya familiya

 460. tumsifu yesu kristo,
  naomba maombi yenu, nipo njia panda
  nahitaji roho mtakatifu anifunulie yupi mume mwema kwangu.
  amen

 461. Bwana Yesu asifiwe naomba uniombee kijana wangu James aache pombe aokoke pia amalize masomo yake ya chuo na kupata shahada

 462. Bwana Yesu asifiwe
  Ninaomba tumwombee dada yangu, si wa mama mmoja, aache kuamini waganga na amtegemee Mungu aliye hai na apate Mume wa kumuoa.

  Pia naomba tumwombee kaka yangu, si wa mama mmoja, aache ulevi.

 463. Bwana Yesu asifiwe wapendwa,
  Naomba mniombee kwa kuwa nahitaji mtoto.
  Miaka miwili inakaribia kupita tangu tufunge ndoa yetu ila bado hatujajaliwa.
  Mungu awabariki.
  Amen.

 464. Bwana asifiwe!
  Dada Maria nashukuru sana kwa kunitia moyo, naamini Mungu atanipigania!

 465. Bwana Yesu asifiwe wapendwa! Nina rafiki yangu anamiaka minne kwenye ndoa yake haja bahatika kupata mtoto naomba mmuombee apate mtoto!

 466. Bwana Yesu Asfiwe wapendwa naomba mniombee nifanikwe
  katika mambo yangu. Mungu awabariki kwa huduma

 467. NAOMBA MNIOMBEE TANGU MWAKA HUU UANZE NAONA NAPUNGUKIWA NA NGUVU YA MAOMBI SIOMBI KAMA ILIVYOKUWA NYUMA.PIA USIKU NAOTA NALISHWA VITU NDOTONI,NAOMBA MUNGU ANIPIGANIE NITOKE KATIKA HALI IYO NA KUKOMBOLEWA KUTOKA KATIKA VIFUNGO MBALIMBALI.
  MUNGU AWABARIKI NA KUWATIA NGUVU.AMEN

 468. Nawasalimu katika Jina la Yesu.
  Naomba maombi yenu,Mimi na familia yangu tupate kukulia Uokovu ili Bwana Mfalme mwema, Yesu Kristo ajidhirihishe katika maisha yetu.Amen

 469. BWANA YESU ASIFIWE!
  NAOMBA MUMUOMBEE RAFIKI YANGU MPENDWA AOKOKE NA PIA MUNGU AMPE MUME MWEMA ALIYEOKOKA.
  MUNGU AWABARIKI.AMEN

 470. Mpendwa kaka John Paul

  Bwana Yesu Asifiwe!
  Nimependa jinsi unavyojibu na kuchambua hoja. Nina issue binafsi ya kiroho ambayo kwa jinsi ilivyo haitapendeza kama nitaiandika hapa. Naomba email address yako nikuandikie, pia unaweza kunitumia kwenye namba 0713 664341. Kwa kweli ninahitaji msaada wa haraka, hivyo nitashukuru kama utanijibu mapema.

 471. BWANA YESU ASIFIWE JAMANI.
  NAOMBA MUNIOMBEE WAPENDWA ILI NIFANIKIWE KTK MAHITAJI YANGU YOTE NINAYOHITAJI.
  PIA MUMEWANGU HAELEWANI NA MAMAYANGU MKUBWA. NATAMANI SANA TUISHI KAMA FAMILIA MOJA YENYE UPENDO NA AMANI. MAOMBA MUWAOMBEE JAMANI ILI WAPATANE.
  ASANTENI NA MUNGU AWABARIKI SANA

 472. Ndg Sesi,

  Namshukuru Mungu kwa kuwa unapata kitu cha kujifunza kutokana na ninavyochambua hoja, kama ulivyosema. Utukutu wote ni kwa Mungu na tuendelee kuombeana.

  Email yangu ni jopamark@hotmail.com.

  Mungu wa mbinguni azidi kututunza.

 473. Mpendwa Kaka John Paul

  Bwana Yesu asifiwe sana.
  Mimi ni mpenzi mzuri sana wa mchezo wa mpira na ninapatwa na huzuni sana kila ninapoona team zetu za Africa zikifungwa hasa na wazungu…. nina mshukuru Mungu kwa kuniumba Mwafrica pia..

  Ninaomba tuungane pamoja kuiombea Ghana Mungu awe pamoja nao waweze kuonesha kuwa Black We Can win the world cup….
  I believe everything is possible in Jesus Name.

 474. Naomba maombi wapendwa nimenyan’ganywa shamba langu jamani bila sababu na mkuu wa wilaya na mkoa na mratibu sina kimbilio zaidi ya maombi

 475. dear
  AMINI MUNGU ANAWEZA.
  NA MUNGU ALITUAHIDI KUTUSAIDIA KATIKA KILA HALI.
  NINAKWENDA KINYUME NA KUKATAA MIPANGO YOTE YA IBILISI SHETANI KTK JINA LA YESU. HIYO DHULUMA NA UNYAN’GANYI NINAVI KEMEA NA KUVISETA KUZIMU KTK JINA LA YESU KRIST WA NAZARETH.

  BWANA YESU NA ASIMAME AKUTEE DEAR KATIKA JINA LA YESU. TUKO PAMOJA MPENDWA TUNAKUOMBEA NA MUNGU ATAONEKANA WAKURUDISHIE SHAMBA LAKO KTK JINA LA YESU AMEN.
  AMINI DADA MUNGU ANAWEZA NA ATATENDA KTK JINA LA YESU.

 476. Bwana Yesu asifiwe sana ndugu!
  Nilikuwa nataka kuwa shukuru sana kwa maombi yenu. Mungu alinijibu, sasa nimesha pona.
  Lakini naomba mzidi kuniombea ili Mungu anisaidie na azidi kunijaza nguvu zake, furaha na amani.
  Asanteni sana. Mungu awabariki

 477. Bwana Yesu asifiwe watumishi wa Mungu nini waomba mtuombee kwani kazinituko katika wakati mgumu sana masengenyo,kati ya wafanyakazi nahatuna mda wa kumtumikia Mungu kwani hata jumapili tunaingia kazini Tunaomba maombi yenu watumishi

 478. Ndg. yangu Dear,

  Namshukuru Mungu kuona unatambua kuwa huna kimbilio jingine zaidi ya yeye! nami pia namuomba Mungu asimamie mwenyewe suala la shamba lako na kulimaliza.

  Bwana akutie nguvu

 479. Nawasalimu wote katika Jina la Bwana Yesu.Naamini kuwa maombi yetu yanapata kibali mbele za MUNGU.
  Ningeomba Kaka Gabriel wa Marekani utujulishe maendeleo ya ile kesi iliyokuwa inakukabili.Mungu si mwanadamu hata aseme uongo…akiahidi lolote anatenda.
  WAPENDWA TUSICHOKE KUCHUKULIANA MIZIGO. AMEN

 480. Eunice,Bwana Yesu akutie Nguvu. Tatizo lako hata mimi nimelipitia na Bwana ameniwezesha kushinda.Nausikia uchungu unaopata na jinsi unavyotamani.REJEA USHUHUDA WANGU PALE JUU WA TAREHE 16 March 2010.
  Usiangalie ukubwa wa tatizo lako ila Angalia Ukuu na Uweza wa Mungu.

 481. Bwana Yesu asifiwe wapendwa.
  mimi naomba mzidi kuniombea jamani maana bado shetani azidi kuniandama, nyumbayangu siku mbili tunaelewana siku mbili ugomvi. yani amani inakuja siku mbili siku mbili masikitiko. Jamani nateseka sana moyoni ila najua Mungu ajaniacha na hata niacha kamwe.
  NAWAOMBA MNIBEBE JAMANI MSINICHOKE.

 482. watumishi naomba mniombee kwani nina natatizo makubwa sana na shetani ananiandama kwa kasi ya ajabu naomba maombi yenu

 483. MUNGU AWABARIKI WAPENDWA NA AJIBU MAOMBI YA WOTE MWEZI HUU WA 08/2010 UWE MWEZI WA USHUHUDA KTK JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETH.

  TUOMBEANE JAMANI TUSICHOKE KWANI MUNGU WETU NI MWAMINIFU.PIA TUNAHITAJI KUWA WAVUMILIVU.

  KAKA JOHN PAUL
  NINATAMANI SANA KUWASILIANA NA WEWE KWANI NINAHITAJI USHAURI WAKO JE NIKIKIANDIKIA EMAIL KWA KUTUMIA EMAIL ADRESS YAKO HAPO JUU UTAJALI?

  AU NIKUPE EMAILL ADRESS YANGU MIMI?
  NA MUNGU MWENYE NGUVU AWABARIKI WOTE NA KUKUTANA NA MAHITAJI YENU YOYE.

  AMEN.

 484. Dada Maria,

  Unaweza tu kuniandikia kwa email hiyo iliyoko hapo juu. Hakuna tatizo lolote!

  Mungu akutunze

 485. Bwana Yesu asifiwe naomba tushirikiane katika maombi kwani nipo katika vita kali sana ya kikazi naomba mniombee niweze kushinda na nikapata kazi permanet kwani kuna vikwazo vingi naomba maombi yenu

 486. mpendwa Dinam !

  Mungu wetu ni mwaminifu na anaweza.
  Nakutia moyo nduguyangu,tuko pamoja ktk Maombi na Mungu wetu ni mwaminifu atafanya.

  Amen.

 487. Bwana Yesu asifiwe mimi ninaomba wanamaombi wenzangu mniombee kwani nina vita kali sana hapa ofisini kuhusu nafasi yangu ya kazi kwani bado ninahitajiwa kufanya kazi na niajiriwe lakini kuna vikwazo baadhi ambavyo naona vipo mbele yangu naomba maombi yenu najua nitashinda tu kwani hakuna kinachoshindikana kwa mwenyezi mungu

 488. Yesu asifiwe watumishi wa Mungu. Nimeokoka na ninampenda Yesu. Ninawaomba watumishi tubebane kuhusu Nyumba yangu juu ya watoto katika masomo waweze kufaulu vizuri na kumzalia Mungu matunda Mema. Aidha maombi kwa ajili ya mke wangu, tunahitaji mtoto wa kiume na kwa sasa imekuwa mimba ikitunga miezi miwili inaachia. Ninamwamimini Mungu sana na najua inawezekana kutunga sasa na isitoke maana anaysema hakuna aliyetasa katika Israel.

 489. Shalom, wapendwa naomba tushirikiane kwenye maombi niko kwenye mapito makubwa sana kazini na maisha yangu kwa ujumla. mungu awabariki

 490. Ndugu wapendwa sikuwa nimefahamu njia hii ya kuombeana kabla ya leo ambapo niko katika hitaji kubwa la faraja baada kupata msiba wa ndugu na rafiki yangu ambaye nilimpenda sana. Ninaomba maombi yenu ili mimi na familia yangu tupate kuimarika.

 491. Please pray for my dad at MPshah HOSPITAL with prostate cancer. I am believing GOD FOR A MIGHTY HEALING. PLEASE JOIN ME

 492. naomba tumuombee wazazi wangu. Baba amerazwa mpsha hospital nairobi, na ugojwa wa prostate cancer naye mama ako na ugojwa wa kisukari. Hakuna kingumu kwa Mungu kwa wale wanamumini. Anaweza kausha hizo cancerous cells na hiyo kisukari. na simama na saiah 65 vs. 20. Mungu amubariki

 493. Ndugu yangu Damaris,

  Nakutia moyo na ninajua hakuna Daktari wa kumshinda Mungu wetu wa Mbinguni alie hai.
  Tuko pamoja ndugu katika maombi na Mungu wa wote wenye mwili awaguse wazazi wako katika jina la Yesu kristo wa nazareth AMEN.

  TUKO PAMOJA NDUGU, MUNGU WETU NI MWAMINIFU, ATAWAPONYA.

 494. Brothers and Sisters in the Lord,

  I am disposing my property, I kindly need your prayer for genuine buyer with money worthy my property. I will prefer a buyer to be committed Christian.

 495. mungu akubariki dada maria na akutendee mema kwa kusimama na mimi. Nimepokea uponyanji wao on their behalf katika JINA KUU LA YESU WA NAZARETH. AMEN. GOD BLESS YOU.

 496. Bwana Yesu asifiwe sana. Wapendwa tusimame na neno la Bwana Isaiah 49:18 juu ya Watoto wetu na Mungu atasimama nyuma ya Neno Lake ili alitimiza.

  Nao wazazi wetu tusimame na Isaiah. 65 vs. 20. Mbarakikwe sana.

 497. Ameeen,
  Asante sana ndugu yangu Damaris.
  Pia asante kwa mstari wa biblia ulio tupatia tusimame nao na Mungu akubariki na Awazungushie ukuta wa Moto watoto wetu sawasawa na Zekaria 2:5(Zephania 2:5) Ili adui asiwaone wala kuwagusa katika jina la Yesu kristo alie hai.

  Pia naomba niomgeze mstari mmoja tusimame nao kwaajili ya wazazi Mwanzo 6:3 (genesis 6:3) Tuzidi kuwaombea wazai wetu, ndugu zetu na sisi wenyewe kwani Mungu wetu ametuandikia miaka 120. sasa shetani hana nafasi ya kutugusa wala Magonjwa hayana nafasi kabisa katika miili yetu.

  MUNGU WETU ANATUPENDA NA ANAWEZA YOTE.

 498. Shaloom Mtumishi! Hongera kwa huduma ya Mungu. Mimi naomba mliombee kanisa letu lisimame katika neno. Maana kuna machafuko yametokea baadhi ya wazee wa kanisa wamepasua kanisa sasa washirika wanaangaika hawajui waende wapi. Mtuombee Mungu atupe kutulia na kumuangalia yeye kwani haya yote yanamwisho. Mungu awabariki sana kwa kazi yake.

 499. Wapendwa Bwana Yesu asifiwe,
  Naitwa Anna Japhet. Napenda kuwasalimu katika jina la Yesu kristo wa Nazareti. Kwanza kabisa napenda kuwapa pole kwa kazi nzuri ya Mungu mnayoifanya kwa moyo. Mungu azidi kuwatia nguvu. Watumishi nina hitaji langu naomba mniombee Mungu anijalie nijifungue salama, nategemea kujifungua mwezi huu wa nane. Mungu awabariki sana na kuwalinda.

  Amen.

 500. Dada Anna

  Amini Mungu wetu ni muweza wa yote. Ukiomba kwa Imani utapokea. Tuko pamoja dada na Utajifungua salama ktk Jina la Yesu.Pia usiache kufanya mazoezi kama unaweza, hii itakusaidia kujifungua kiurahisi jikaze tembea fanya kazi ndogondogo unazo ziweza usikae au kulala tuu.
  Mungu akubariki na Utajifungua salama kwa Msaada wa Mungu.
  AMEN

 501. Dada Anna, Kama Mungu aliweza kukupa mtoto tumboni mwako amini atamtoa mtoto salama salimini tumboni na kutimilizaq mpango wake wa uumbaji. Kwa maombi Mungu ameshakup mtoto tena salama

 502. Bwana yesu asifiwe,
  Nawasalimu wote wamchao mwenyezi mungu kwa salam zooote za rohoni,naamini mungu yu pamoja nanyi nyote mlioitwa kwa jina lake.Nahtaji umoja ktk maombi kumwombea mtoto wangu shedrack kwani mtoto amekua hali chakula nikulia tu pia jirani yangu hapa kuna vita sana kwani kuna majirani ambao hawapendi kuona nikifanikiwa ktk kristo yesu,ila mie huwa naliitia jina layesu naowakishindwa.Kwani maandiko yananiambia kuwa wote waliitialo jina la bwana wataokolewa wala hamna watesi watakaoinuka juu yetu.Bwana yesu awzuidishie amani ndani yenu ili kazi ya bwana isonge mbele….Ameeeeeen.

 503. Wapendwa Katika jina la Bwana mimi nina mzigo wa maombi msululu wa ndugu zangu ni wagonjwa sana sasa hivi ninavyoongea nahitaji msaada wa maombi toka kwenu.Baba ana vidonda vya tumbo,mama na mdogo wake wana kisukari,anko yangu Mr Akile ana kansa ameshafanyiwa operation mara mbili bado hali yake si nzuri,dada Grace ana sukari na miguu imekataa kutembea inawaka moto anamiliki shule na yeye ni mgonjwa Naomba Tuwaombee,Mbarikiwe sana na Bwana amen

 504. Wapendwa ktk jina la Bwana wetu Yesu Kristo namshukuru sana Mungu kunionyesha web hii ya maombi Bwana Yesu asifiwe,Baadaya kusoma maoni ya waombaji wa nyuma mmoja wao amenipa neno la mwanga sana kwamba usiseme tu niombeeni ila useme umbewe juu yanini Kweli mimi nawaombea hao ndugu zangu wapone na waendelee na shughuli zao kama kawaida wakimshukuru na kumshangilia Mungu kwa kazi zake Amen
  Mbarikiwe

 505. Wependwa, Bwana yesu apewe sifa,Ninapenda kuchukua mafasi hii kumshukuru mungu kwa mema yote anayotujalia kila siku.Nilipigiwa majungu na wenzangu kazini ili nifukuzwe kazi,Niliomba na kumlilia mungu juu ya hilo,Ninamshukuru mungu Nimeongezewa mkataba wa kazi,Kinyume na matarajio ya watesi wangu,Bwana yesu apewe sifa.Nimepangiwa kituo kingine cha kazi kusini mwa sudan Wapendwa ninaomba mniombee sehemu nitakayokwenda kukawe na amani kuu,na kazi ninayokwenda kufanya ikapate kibali mbele za bwana wetu mungu wa majeshi.
  Neema ya bwana wetu yesu kisto na upendo wa mungu baba na ushirika wa Roho mtakatifu ukakae nasi sote sasa na hata milele.
  Amina

 506. shaloom wapendwa, ninahitaji sana MUNGU anipe mke mwema,awali sikuwahi kuwaza kama hili suala linamuhitaji MUNGU kwa namna hii.Ninahitaji rehema kuu za MUNGU ili nivuke hapa.Najua nikitumia akili zangu nitashindwa mahali fulani.Ninaogopa sana ninapoona vijana waliookoka hapo kwanza mara baada ya kuoa au kuolewa wamerudi nyuma kabisa.Binafsi ninaamini kuwa ndoa ni baraka toka kwa Mungu,na kama ni hivyo basi iweje mtu aoe au kuolewa na arudi nyuma KIROHO?Mimi ni mwalimu,na mahali nilikopangwa nilikuta kuna ROHO mbalimbali chafu mahali hapo.Mojawapo zilikuwa ni zile za KUWAHARIBIA MDA SAHIH WA AMA KUOLEWA AU KUOA kwa walimu vijana.Kama BALOZI wa YESU nimeanza kushughulikia moja baada ya nyingne ili KRISTO AINULIWE tu.Naomba mchukuliane nami hili jambo wandugu katika YESU.Mbarikiwe kupita maelezo.

 507. amen kindly pray for me i am financial unstable and wants to praise my God happily and to do his work without difficulty

 508. Ndugu watumishi mlishiriki nami katika maombi kwa ajili ya baba yangu mlezi, kipekee ninawashukuru sana japo hakuweza kupona alifariki septemba mwaka jana. Bwana alitoa na ametwaa jina lake lihimidiwe.

  DADA mery kileo barikiwa kwa juhudi zako za dhati za kutaka kujua maendeleo ya baba wakati akiwa mgonjwa. Mungu wangu na akulipe kwa upendo wako. soma rum 8: 31.GOD BLESS YOU.
  MORI MWANAHARAKATI.
  wapendwa namshukuru MUNGU kwa afya niliyonayo. Ninaamini ni kwa neema tuu. kwa muda mrefu nimekuwa kijijini ambako huduma hii ya intanet haipatikani. ila nikipata japo nafasi kama ya leo ninamshukuru Mungu.
  Kubwa na la msingi ninamshukuru Jehova kwani niliporejea nimekuta bado mpo na huduma inasonga mbele.

  Ninaomba maombi yenu kwani niko naandika kitabu na sasa niko hatua za mwisho kitabu hiki kina kichwa kisemacho “UPAKO WA KUFANYA MAAMUZI”

  Naomba mumsihi Mungu afungue milango ya fedha kwani inahitajika zaidi ya shilingi 700,000. kwajili ya publishing.
  Asanteni

  Niwaache na neno toka MATAYO 18.

 509. Bwana yesu asifiwe wapendwa naomba watumishi wa mungu pia na waombaji wote kwa ujumla wake waniombee kwani nimeanguka katika wokovu mniombee ili nisimame tena imara pia na familia yangu iokoke pia naomba niweze kuomba kwani kwenye maombi nashindwa kabisa, na maombi ndiyo ushindi kwa waliookoka ni silaha imara ninaamini kwa mungu yanawezekana, najisikia vibaya sana kwa maisha ninayoishi kwani hayampendezi mungu najua mungu ananipenda na ndiyo maana sina amani kabisa. Mungu awabariki kwa kazi njema na yakupandeza jina la bwana liinuliwe popote Amen.

 510. Watumishi wa Mungu Bwana Yesu asifiwe sana!!

  Ninaomba tushirikiane kuombea watu wote
  wamkiri Yesu ili wasiende jehanamu,pia naomba tumuombee rafiki yangu anaitwa Cecilia anauvimbe tumboni na madaktari wameshindwa kuutoa baada ya kumpasua

 511. Kwa mamlaka ambayo Mungu umetupa katika matayo 18:18 natangaza kuyeyusha uvimbe ulio tumboni mwa huyu binti Secilia kwa j ina na kwa Damu ya YESU Kristo. Nakataa roho za mauti, mateso na madhaifu ya jinsi zote Amen.Dada Janeth hongera kwa huduma nzuri mwambie Secilia hatokufa bali ataishi, mtie moyo lakini kubwa mwambie asjiulize kwanini anayapitia hayo ni kwakuwa KRISTO ANAMHITAJI. Barikiwa mno.

 512. Bwana Yesu asifiwe!
  Naomba mniombee ili nione God’s will ndani maisha yangu. Mimi nilikuwa na mchumba lakini kulitokea mambo magumu hadi ikafika hatua ya kuachana. Sasa mimi nilikua naomba Mungu aniongoze ili niweze kuchukua hatua njema hata na yeye pia aongozwe na Mungu achukuwe hatua njema.
  Ahsanteni, mbarikiwe.
  Uwineza

 513. Bwana mungu wetu aliye juu apewe sifa.
  Naomba tushirikiane katika sala kwa ajili yangu ,nimepewa marafiki na katika hao marafiki kuna wenye ombi la kuwa mchumba.Kwa nguvu zangu mwenyewe siwezi kujua nani amepangiwa kwa ajili yangu.Nakuombeni mniombee niweze kutegua mtego huu mkali kwenye maisha yangu

  haleluya
  Rahel

 514. Dada RAHEL, Shaloom.

  Nikuulize wewe si mtakatifu? na unayajua maisha unayoishi kama ni matakatifu? kama ni matakatifu usijali mwambie MUNGU kuwa unahitaji Mume kwani ni halali yako kupewa mume.

  Ninapozungumzia utakatifu ninalenga mambo kadhaa na mojawapo ni namna ulivyo/unavyotunza usichana wako.
  Kama hujafanikiwa ktk hilo niseme kweli usjaribu kuanza maombi kienyeji maana shetani atakuwa na kibali cha kukupa Mume ambae siye. Nini chakufanya?

  1. KAMA UNA UHALALI(Mtakatifu)katika maisha yako

  Ninamaanisha hujawafanya uzinzi na mtu yeyote basi uko nje ya laana na una haki ya kudai mume wako moj kwa moja mbele za Mungu nasisitiza “NI HAKI YAKO” Wewe ni MWANAMWALI.

  2. Biblia inasema aungwae na kahaba wamekuwa mwili mmoja. Kama wewe si msafi ktk hilo yaani umewahi kumruhusu mwanamme kufanya uzinzi na wewe kibiblia tayari UNAMUME, so ukienda mbele za Mungu kuomba mume shetani anashangaa mbona huyu ameolewa tayari? na hapo ndipo atakuwa na uhalali. Kwahiyo kama ndivyo ingia ktk toba ya kweli kwani utakuwa uliingia ktk agano la DAMU na mtu mwingine. BAADA YA TOBA YA KUMAANISHA SASA Mweleze Mungu juu ya hao watu na toka hapo utaona ATAKACHOFANYA KTK MAISHA YAKO.
  Usijali DAMU ya YESU ipo kwaajili ya Upatanisho.
  BARIKIWA.
  Mwanaharakati wa injili ya Kristo

 515. dada janeth nipe fdback ya binti aliyekuwa mgonjwa DADA CES maana MUNGU ameshafanya jambo la kumshangaza FARAO na JESHI LAKE

 516. wapendwa Shalom. Mimi ningependa tujumuike kwa pamoja Kuliombea taifa letu la Tanzania hasa kwa kipindi hichi cha Uchaguzi mwezi October ili Mungu akaonekane katika ratiba nzima. Pili watumishi tuwaombee vijana kwani shetani amewateka vijana na wasipomrudia huyu MUNGU MWEZA, YOTE HAWANA UJANJA. Zaidi kabisa ni mimi binafsi kuhusu maisha yangu ili Mungu azidi kunitumia ipasavyo pamoja na kunipa mahitaji ambayo nimezungumza na BABA YANGU AONAYE SIRINI. Mbarikiwe sana!!!

 517. Nawasalimu nyote katika Jina la Bwana Wetu Yesu Kristo. Wapendwa Mungu azidi kuwatia nguvu katika maombi na katika safari ya kwenda mbinguni.
  Naomba tushirikiane katika maombi kwaajili yangu, nimekuwa nikisumbuliwa na kifua kwa mda mrefu sasa na kuwa na maumivu katika ziwa langu la kushoto, naomba Mungu aniponye na hayo yote.
  Mbarikiwe sana.

 518. shalomu watu wa Mungu nawakumbusha tufuatilie kampeni za wagombea wa uongozi Tanzania ili tujue tunapaswa kuombea nini. NIMUHIMU SANA. MBARIKIWE SANA

 519. Nawasalimu nyote katika Jina la Bwana Wetu Yesu Kristo. Wapendwa Mungu azidi kuwatia nguvu katika maombi na katika safari ya kwenda mbinguni.
  Naomba tushirikiane katika maombi kwaajili yangu, mimi ni mjamzito naomba mniombee nijifungue salama
  Mbarikiwe sana.

 520. Ndg Simon,

  Uliandika mahitaji yako tarehe 5/8/2010. Na moja wapo wa matatizo ambayo unahitaji maombi ili liondoke ni kuharibika kwa ujauzito kwa mkeo kila baada ya miezi miwili. Ingawa hujaandika ni mara ngapi sasa ujauzito huo unaharibika, lakini nafikiri itakuwa ni zaidi ya mara mbili.

  Niliyonayo kwa ajili yako ni haya:

  Kama hali hiyo imeshatokea zaidi ya mara mbili ni wazi mtakuwa mlishachukua hatua kutafuta nini sababu ya tatizo hilo. Na kuna uwezekano mkubwa mkawa mlishakwenda hadi hospitalini na kuelezwa sababu. Sasa kama mlishaelezwa sababu ya tatizo hilo ni lazima pia mlielezwa hatu za kuchukua, kitabibu, ili kuondoa tatizo hilo. Ndipo sasa, hata baada ya kufuata taratibu za kitabibu bado tatizo hilo halijaisha, pengine ndiyo umeona ukate rufaa kwa Mungu, kupitia Yesu Kristo.

  Lakini kuna uwezekano mkawa mlikwenda hospitalini na madaktari wakasema hawaoni sababu ya tatizo hilo. Hali ikishakuwa hivyo ni rahisi kutambua kwamba hizo ni nguvu za giza moja kwa moja. Na maombi, kwa Jina la Yesu, ndiyo dawa pekee kumaliza matatizo ya namna hiyo.

  Vile vile inawezekana hamjachukua hatua yoyote. Mara ya kwanza ilitokea, mara ya pili ikatokea,pengine na mara nyingine ikatokea. Na kuleta mahitaji yako hapa inaweza kuwa ndiyo hatua ya kwanza kuchukua.

  Nimeandika hayo ili kuonyesha jinsi ambavyo maombi yanaweza kutumika kama rufaa, baada ya kushindwa kwa jitihada fulani, au kwenda moja kwa moja kwenye maombi pasipo kutafuta ufumbuzi mwingine ulio katika uwezo wa kibinaadamu. Kwa sababu yoyote ile maombi hufanya kazi, haijalishi ni kwa kukata rufaa au ni kwa kwenda moja kwa moja kwenye maombi. Yesu alikuja ili azivunje kazi za Ibilisi.

  Jambo ambalo linaweza kufanya maombi yasifanikiwe ni kama chanzo cha tatizo lililopo ni mtu mwenyewe anayehitaji maombi. Kwa hali ya namna hii maana yake chanzo kikiondolewa na tatizo litakuwa limekwisha! Ukikata mzizi wa mmea nilazima mmeo huo ufe!

  Katika kuandika umesema kwamba wewe umeokoka. Na kwamba mnahitaji mtoto wa kiume. Mimi nimeelewa kama tayari mna mtoto wa kike,[mawazo yangu] na sasa mnahitaji mtoto mwingine na kwa mapenzi yenu awe wa kiume! [Kwa sababu sidhani kama ni sahihi sana kung’ang’ania mtoto wa kiume wakati hata wa kike hajapatikana au kung’ang’ania mtoto wa kike wakati hata wa yule kiume hajapatikana]. Sasa kama tayari mna mtoto, maana yake ni kwamba tatizo hilo ni geni. Na kama ni geni ni lazima liwe limeingia kupitia mahali fulani. Si lazima tatizo hili liwe na uhusiano na nguvu za giza. Inawezekana ni tatizo tu la kiafya, labda upungufu wa aina fulani ya virutubisho mwilini, na ambavyo upatikanaji wake ni kula tu aina fulani ya chakula. Kwa hali ya namna hii kufuata maelekezo ya kitabibu kutaondoa tatizo.

  Lakini kama ninyi mmeokoka [mke na mume] na tatizo hilo ni geni, na sababu yake haionekani kwa madaktari, basi ni lazima kukaa chini kuangalia ni mlango gani adui ameingilia ili kuleta teso hilo. Kuna uwezekano kuna mlango alikuta uko wazi [mtu aliyeokoka anafahamu lugha hii] ndipo akaingia. Kwa hiyo mtakapotafakari na kuomba pamoja, neema ya Mungu itadhirisha mlango huo. Mlango huo ukishagundulika ni kuomba toba kwa Mungu na kisha kumfukuza adui huyo, na kisha kuufunga mlango huo ili kuhakikisha mnaishi katika boma lenye uzio imara wa damu ya Yesu.

  Watu wengi tuna mahitaji. Lakini si wengi ambao hukaa chini kwanza na kutathimini inawezekana imekuwaje hadi tatizo hili likatokea. Kufahamu chanzo cha tatizo ndiko husababisha HATUA SAHIHI ICHUKUKULIWE. Ni kweli Biblia imesema tusisumbuke kwa jambo lolote bali kwa kusali na kuomba, lakini pia Yesu Kristo, baada ya kumponya mtu fulani, [Yohana 5:14] alimwambia asitende dhambi tena lisije likampata jambo baya kuliko alilokuwa nalo. Kwa hiyo dhambi, kutokuwepo kwa uwepo wa Mungu maishani mwa watu, ni chanzo kikubwa cha matatizo yanayoletwa na nguvu za giza. [Kwa maneno hayo sina maana kila tatizo linatokana na nguvu za giza. Tulishajadili mengi kuhusu point hii katika mada ya Kwa nini mtu anakuwa bado kwenye vifungo hata baada ya kuokoka]

  Halafu jambo jingine la kutambua ni kwamba, mke wako hadi kufikia hatua ya kubeba mimba, YEYE SIYO TASA! Kwa hiyo ni vema ukabadilisha maandiko ya kutumia, ambayo yatasaidia kuijenga imani ndani yako. Neno huleta matokeo likitumika mahali pake sahihi.

  Hayo ndiyo nimekuwa nayo leo kwa ajili yako ndgu Simon. Lengo ni kukufanya uchukuwe hatua zaidi kuliko kusema tu unamwamini Mungu kumbe kuna jambo [kama lipo]ambalo unatakiwa kulifanya kwanza. Ninaamini watu wa Mungu wanaomba kwa ajili yenu. Mimi pia ninaomba pamoja nanyi.

  Mungu wa mbinguni atusaidie.

 521. Mh,mimi natoa ushari baada ya kuona watu wengi wanahitaji kuombewa kwa MUNGU juu ya haja zao.Kwanza niseme si vibaya kuombeana !ILA ninapendekeza kwa kuwa sisi ni wamoja tuchague walau siku moja na kwa saa moja kila mtu mahalialipo afanye sala maalum kwa hao wenye uhitaji wamaombi ili isije ikawatunasoma uhitaji wawatu na hatuweki katika matendo au wanaomba wachache,Lakini pia tukumbuke kupata nafasi ya kushukuru kwake tumwombaye!tukiamini tumepokea sawa na mapenzi yake pasipo kulaumu kuwa ametucheleweshea tulichoomba.

 522. wapendwa niombeeni nipo kwenye mapito magumu sana na nina mitihani mikubwa so pray for me nisirudi nyuma kiroho

 523. Bwana Yesu asifiwe nawaslimia katika jina la Yesu mimi naomba maombi yenu nina hitaji la mtoto ni mwaka wa 8 kwenye ndoa. pia muombee mume wangu make siwezi kujua mwenye tatizo nina. pia nasumbuliwa na ndoto mbaya
  Mungu wangu awabaliki

 524. Watumishi wa Mungu
  Bwana Yesu Kristo apewe sifa

  Ninawashukuru kwa maombi yenu kwa ajili ya ujumbe nilioutuma kwenu tarehe 26 August ya kwamba ninawaombe ndugu zangu katika Kristo tumuombee ndugu yetu Cecilia ni bado nipo hapo hapo ya kwamba tumuombeeni Cecilia jamani kwani uvimbe unazidi kuwa mkubwa na unambana mapafu lakini ninajua neno moja ya kwamba Mungu wetu hashindwi na kitu hata huo uvimbe anaweza tukimwomba katika ukamilifu

  Asanteni wapendwa mbarikiwe na Mungu aliye juu ya vyote

 525. BWANA YESU ASIFIWE WATUMISHI WA MUNGU MIMI NILIKUWA NAOMBA MLIOMBE BOMA LA KWETU KUNA MGAWANYIKO WA AJABU NDUGU WENYEWE KWA WENYEWE WANAPIGANA HAKUNA MAELEWANO YEYOTE NAJUA HAKUNA LISILOWEZEKANA KWA MUNGU

 526. Dada yangu Dorosela,

  Mimi nitaomba pamoja nawe, bila kujali tatizo lipo kwa nani, maana suala ni kwamba Mungu awapatie watoto!
  Lkn naomba ufanye kitu kimoja pia. Tunapomwendea Mungu juu ya suala lako, kwanza angalia ushirika wako na Mungu umekaaje, Mpe Mungu nafasi ya kukupeleleza ndani yako ili kama ipo njia iletayo majuto kwako, akuponye nayo. Pia, kama Mume wako pia anamuamini Mungu naamini mnashirikiana ktk kumuomba Mungu juu ya hili.
  Umegusia kuhusu kuota ndoto mbaya kitu ambacho si dalili nzuri kwa Mkristo! Hivyo muhimu sana kuangalia maisha yako ya kiroho yamekaaje, kisha chukua hatua sahihi bila kuchelewa.

  Mungu akubariki, tupo pamoja

 527. Shalom wapendwa! Namshukuru Mungu kwa kazi njema anayoifanya kwenu kwa kushirikiana kwenye maombi, kwa kuwa alisema wakutanapo wawili au zaidi kwa jina langu mi ni pamoja nao, hivyo basi naamini UWEPO WA BWANA UKO MAHALI HAPA, haijalishi mtu yuko mbali kiasi gani. Ninaomba tuombe kwa ajili ya yafuatayo:
  – Uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani mwezi Oktoba uwe wa amani na Mungu atupe viongozi kutoka kwake ili waweze kutuongoza katika kweli yake. MAFISADI hawana nafasi ktk Jina la Yesu.

  – Pili tuombe kwa ajili ya watoto wetu, Mungu aweze kuumba vitu vilivyo vyema maishani mwao, wakuwe ktk kumuamini yeye.

  – Naomba muuombee familia yetu (nilipozaliwa) Mungu akutane nao waache ibada za matambiko, waokolewe na waishi ktk KUMTUKUZA ALIYEWAUMBA SIKU ZOTE ZA MAISHA YAO.

  – Naomba muombe kwa ajili ya uchumi wetu (mimi na mume wangu) uweze kuimarika kwani tulimuomba Mungu kujenga nyumba kwa zaidi ya miaka miwili, sasa tumeanza msingi na naamini kazi aliyoianzisha yeye ataikamilisha bila kukwama mahali popote.

  Mungu awabariki sana wapendwa!!!

 528. Shalom bwana Yesu asifiwe,ninaomba kuwashirikisha na mniombee nipo katika hali ngumu kuna jirani yangu ameuza kiwanja changu bila idhini yangu naomba mniweke kwenye maombi kwani hakuna linaloshindikana kwa mungu, pia kazini kwangu sijapata ajira ya kudumu yote nimemwambia mungu na mungu alisema asiyefanya kazi na asile na ninamtegemea kuwa yeye ndo mwenza wa yote naomba mnisaidie katika maombi yenu. Asanteni na mungu awabariki na tuzidi kushirikiana

 529. tumsifu yesu kristu! ukweli nimeguswa na msg hizi na nimefurahishwa pia kwani nimegundua kua tunapata faraja na amani ipitayo yote kwa kupita bwana wetu yesu kristu! ni mara yangu ya kwanza kushiriki katika web hii lakini ninaimani itanijenga kiroho! ni kweli nimepitia magum mengi mengi jamani lakini nimedumu katika kumtegemea yesu kama bwana na mwokozi wa maisha yangu nikiamini kuwa hakuan lisilowezekana katka yeye,Naomba tuzidi kuombeana na kukumbukana katika sala watu wote kwa ujumla bila kulisahau taifa letu kwani hivi sasa tunakwenda katika kipindi kigum mambo mengi yanatendeka na nafikiiri tunamuhitaji mwenyezi mungu sana sana this time!tusali jamani Mungu ni mwema najua atatenda.

 530. Mungu asifiwe Wapendwa,naombeni tushirikiana na mimi katika maombi ya kupata mume na kazi.naamini vyote hivi ni haki yangu na ni mpango wa Mungu nivipate kwa wakati muhafaka.Kwa kweli napitia maumivu makali sana ya kuvunjika kwa uhusiano wangu na niliyetarajia kuwa angekuja kuwa mume wangu.

 531. Bwana yesu asifiwe wapendwa. Naomba mniombee niko katika kipindi kigumu kazini bosi wangu hanipendi pia kuna tetesi za watu kupunguzwa kazi hivo napata hofu. mniombee hilo jambo lisitokee kwangu na nina imani Mungu yuko upande wangu maana yeye ndiye mtetezi wangu.Pia nahitaji kuolewa lakini bado sijapata mwenzi nakosa furaha make najua kuolewa ni haki yangu.

 532. Bwana Yesu asifiwe, ninaomba kuwashirikisha katika maombi ya kuombea eneo langu ambalo nilinunua mwenyewe kwa hela yangu ya kipato changu halafu jirani yangu akauza kwa vile nilikuwa sijaenda kwenye eneo langu muda mrefu kwa sababu ya matatizo. Naomba mniombee ili jumapili mashahidi wangu watakapotoa ushahidi kuwa pale ni kwangu tuweze kumpa mungu baba yetu sifa kwa ushindi kwani hakuna linaloshindikana kwa mwenyezi mungu. Ninamuomba mungu sana asimamie haki yangu ili niweze kurudishiwa eneo langu kwani hati zote ninazo na ninaziombea kila siku ili mungu aweze kutenda. Mungu atusaidie katika maombi haya.

 533. Kwa ndugu Deo,

  Uliandika tarehe 15/9/2010 ukihitaji uombewe amani. Baada ya kusoma na kutafakari hitaji lako hilo nikapata machache ya kukushauri kuhusu hitaji lako hilo. Kwa hiyo pamoja na kuwa unahitaji kuombewa amani mimi nina haya yafuatayo:

  Kuhitaji kuombewa amani maana yake ni kwamba umegundua amani imetoweka au imepungua katika maisha yako. Na haiwezekani amani ikatoweka au kupungua hivi hivi tu, ni lazima kuna sababu zake. Na mwenye kuzifahamu sababu hizo kwa ukamilifu wake ni wewe mwenyewe muhusika. Kuzifahamu sababu zilizopelekea uhitaji huo wa amani ni hatua moja wapo muhimu sana katika kuchukua hatua zinazotakiwa ili kuirejesha amani.

  Amani, kama ilivyo kwamba lazima kuwe na sababu zinazoifanya ipungue au iondoke vivyo hivyo kuna sababu zinazoifanya irejee na idumu. Amani ni kitu kinachotakiwa kitafutwe na kikipatikana kitunzwe na kuhifadhiwa. Maana yangu ya kuandika haya ni kwamba pamoja na kuombewa amani lakini imani haishuki hivi hivi tu pasipo anayeombewa amani hiyo kuwa katika mazingira ya kuweza kuipata amani hiyo. Amani haimvamii mtu pasipo yeye kuanda mazingira ya amani. Kuna jambo ambalo binadamu anatakiwa kufanya ili aweze kupata amani. Ndiyo maana katika Biblia tumeagizwa ‘kuitafuta’ amani, tena si kuitafuta tu, bali KWA BIDII. [1Pet 3:10-11, Ebr 12:14].

  Amani ya Mungu inaendana na utakatifu. Ndiyo maana imeandikwa “Hakuna amani kwa Wabaya”. Isaya 57:21. Hii ndiyo kanuni ya AMANI kutoka kwa Mungu. Sasa hapa ninaomba nieleweke vizuri kwamba siandiki haya kukuhukumu kwamba ‘wewe ni mbaya’. Hapana. Nimeona tupitie haya ili kuangalia sababu zinazoweza kufanya amani iondoke na zile zinazoweza kufanya amani irudi.

  Tatizo linaloweza kuwepo hapa ni kama mtu hatakuwa na ufahamu juu ya sababu gani zimefanya amani yake iondoke au ipungue. Hapo ndipo panahitajika maombi ili ufahamu ufunguke kisha afahamu sababu zilizofanya amani ipungue au iondoke. Sababu hizo zikishafahamika basi kinachotakiwa ni mtu kufanya kinyume cha sababu hizo ili amani iweze kurejea. Kwa maneno mengine ni kwamba mtu ana sehemu katika kutengeneza amani yake mwenyewe. Suala linalotakiwa ni kufahamu namna gani mtu anaweza kufanya ili apate amani.

  Kwa hiyo pamoja na kuweka hitaji hili hapa, usikae kimya, idle, ukidhani amani itashuka tu hivi hivi. Tafakari nafasi uliyopo sasa. Tafakari nini kinaweza kuwa kimeondoa amani hiyo. Ninaamini kwa msaada wa Mungu, kupitia maombi haya, utapata jibu na hatimaye kuchukua nafasi yako katika mchakato huo wa kuitafuta amani na ikipatikana uitunze.

  Huo ndiyo mchango wangu kwa hitaji lako hilo.

  Mungu wa mbinguni na atusaidie.

 534. Bwana Yesu asifiwe,
  John Paul, Mungu akubariki kwa ushauri wako mzuri naona kuna ualimu ndani yako. Naomba Mungu akutumie zaidi na zaidi kwa ajili ya kuujenga ufalme wake.
  Ubarikiwe sana.

 535. Ndugu Precious,

  Nashukuru sana kwa kunitakia baraka za Mungu kutokana na ushauri wangu kwa ndugu Deo. Utukufu wote ni kwa Mungu ambaye Neema yake ndiyo ituwezeshayo.
  Basi, endelea kuniombea katika hilo unaloliona kuwemo ndani yangu.

  Mungu wa mbinguni akutunze!

 536. Shalom wapendwa,
  nawasalimu ktk Jina la Bwana wetu Yesu Kristo.
  Wapendwa naomba kuelekea uchaguzi mkuu Tanzania tuwe na maombi kila wiki ili Bwana akaitimize ahadi yake ktk Isaya 54:10 maana milima itaondoka na vilima vitaondolewa bali wema wangu hautaondoka kwako wala agano langu la amani halitaondolewa asema BWANA akurehemuye
  1. Tumshukuru Mungu kwa amani tulikaa nayo miaka hii yote na chaguzi zote zilizotangulia kwa amani
  2. Tumshukuru Mungu kwa muafaka wa visiwani ulioleta amani
  3. Tumwamini na tumuombe Mungu asiondoe amani Tanzania ambayo ameweka ktk mioyo yetu sote, Ombea Mungu adumishe amani hii yeye mwenyewe kwa kuiongoza serikali zote zitakazokuwepo Tanzania.
  Mungu akubariki unapoombea hili.

 537. Shalom Dinam,
  pole kwa majaribu makubwa, mradi ni ardhi unaimiliki kihalali, Mungu atakupigania. Je unatoa zaka na dhabihu? Kumbuka kumiliki kitu ni dhawabu unapswa kumtolea Mungu shukrani naye kwa wakati wake atamkemea yule alaye ktk hazina yako. Hujachelewa basi umshukuru Mungu kuwa una hati na mashahidi pia, rudi kuitakasa na kuikomboa hiyo ardhi mikononi mwa huyo jirani. Ujikagua na ujitakase ktk maeneo yote ya kumiliki kwa upande wako, vunja maagano yoyote jirani aliyoweka juu ya ardhi na weka agano lako tena kuwa ndiye mmiliki wake. Mlilie Mungu na umwahidi utamfanyia nini (sadaka, huduma kwa ushuhuda) akikurudishia. Isaya 43:11-13. Nitakuwa kwenye maombi kama haya wiki hii waweza jiunganisha nami kiroho ukiweza. Dada Rose

 538. NAWASALIMU KTK JINA LA YESU JINA LIPITALO MAJINA YOTE
  WAPENDWA NIPO KWENYE SAFU HII YA MAOMBI NIKILETA OMBI HITAJI HILI LA KITAIFA KWAMBA TANZANIA TUPO KATIKA KIPINDI CHA UCHAGUZI NINAWAOMBA WAPENDWA WOTE TUOMBEE UCHAGUZI NA SIO KUOMBA TU NI PAMOJA NA KUWAKUMBUSHA KUWA TUPIGE KURA KWANI IMANI BILA MATENDO IMEKUFA, HIVYO WATU WOTE TUKAPIGE KURA NA IJULIKANE KWAMBA TUNAPIGIA KURA MTU NA SIO CHAMA MWENYE KUSOMA NA AFAHAMU

 539. Nawasalimi Katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo!
  Naleta hitaji langu binafsi kwenu nikiomba msaada wa maombi yangu kwa Mungu kwamba. Nimeokoka, na ni mjane nimepita katika kipindi kigumu sana hasa pale nilipokutana na Adui kupitia wajakazi na watu wanaonizunguka. Nashindwa kuomba muda mrefu, kusoma neno na pia ninakuwa na vita vidogo vidogo ila ninamuona Mungu akinishindia. Naombeni maombi yenu niione furaha ya wokovu na Mungu anitie nguvu najua Yeye ni mume wa wajane nazidi kupata tumaini kwa Mungu. Naomba mniombee nipate Kiu ya Neno, Kiu ya maombi na karama za Roho Mtakatifu zitende kazi kwa kadri apendavyo yeye Roho. Mungu wangu awabariki sana.

 540. Bwana Yesu Asifiwe.
  Naomba mniombee mwanaume niliyezaa naye amenitelekeza na pamoja na mtoto. huu ni mwezi wa nne sasa unaisha hajui mtoto anakula nini, anavaa au havai, kodi ya nyumba. na sasa navyotuma haya maombi amekata mawasiliano nikipiga simu hapokei nikiandika massage hajibu.
  Naomba mniombee niko kwenye kipindi kigumu sana.

  MUNGU AWABARIKI

 541. Nawasalimu katika Jina la Bwana Yesu, Asifiwe, Watumishi naomba maombi yenu kwani kumeinuka ugomvi katika ndoa yangu na kwa kaka yangu na shemeji yangu kutokana na tatizo la uaminifu kwa wanandoa hao. naomba mungu ashushe mkono wake akaziponye kwani yeye aliyeianza safari ataimaliza. AMENI

 542. shaloom wapendwa

  namshukuru mungu kwa mambo mengi makubwa aliyonitendea,amenijalia afya njema,nimejifungua salama na amenipa mtoto mzuri sana,kanipa kazi nzuri.yot namshukuru mungu maana bila yeye mimi siwezi,naomben mniombee pia swala la ndoa limekuwa jaribu kubwa sana kwangu.mungu afungue moyo wa mzazi mwenzangu na aweke utayari maana kila tukipanga naona mwenzangu hayuko tayari.

 543. bwana yesu asifiwe naomba msaada wamaombi nipo kwenye kipindi kigumu sana familia yetu ipo kwenye matatizo makubwa na pia nijue kuomba kwa muda mrefu na kusoma neno

 544. Bwana wetu Yesu kristo asifiwe,
  Strictly gospel naomba maombi kwa ajili ya dada yangu ambaye ni muda mrefu sasa tangu aolewe hajapata mtoto, kila anapo pata mimba mimba zinatoka na zinafika mpaka miezi 6. tunaomba maombi yenu sana jamani.
  dada yangu baada ya kupata matatizo hayo yote aliamua kuokoka lakini baada yakuona hapati majibu kutoka kwa mungu shetani amemteka tena na ametumbukia kwenye dhambi ya ulevi.
  asanteni na Mungu awabariki wapendwa!

 545. Shalom wapendwa!mimi naomba mnisaidie katika maombi yenu kila siku kwani ninamchumba wangu ananipenda lakini
  kwenda kutoa mahali nyumbani haendi halafu kazi yake yupo geregi lakini hapati pesa. kwa mwezi anapata elfu 30 tu.Mungu awabariki wote.

 546. Amina, Bwana akuonekaniye kama umemthibitisha katika huo uchumba.
  Katika Jina la Yesu Kristo wa Nazareth aliye hai.
  Amen!!

 547. Bwana Yesu Asifiwe ,
  naomba msaada wa maombi kwa Mungu; naumwa kifua pamoja na vidonda vya tumbo.Pia naomba mniombee amani pamoja na kupata uwezo wa kusimama imara ndani kristo yesu (wokovu),vilevile niweze kupata uwezo wa kusoma neno la mungu (biblia).Mungu awabariki wote

 548. shaloom wapendwa,
  jina la yesu liinuliwe juu,namshukuru mungu kwa mambo mengi makubwa aliyonitendea,amenijalia afya njema,naomba msaada wa maombi kwa Mungu anijalie nipate mume ambaye mimi ni ubavu wake, napia anifungue macho na masikio katika yale yaliyo yake. nimefurahi sana kukutana na website hii,mungu awabariki wote.Elizabeth.

 549. Shalom wapendwa! Ahimidimiwe Bwana kwa kutuwezesha kuiona siku ya leo tena tukiwa wenye afya njema, tuzidi katika kutegemea yeye kwani ni kimbilio letu. Mimi naomba tuombe kwa ajili ya Tanzania jamani, uchaguzi huu Mungu asimame tupate viongozi bora toka kwake na si mafisadi pia atuepushe na vita kwani ushindani ni mkubwa sana kuliko miaka iliyopita.

  Mbarikiwe na Bwana

 550. sisi tunamuomba mungu awabriki watoto wote wanaofanya mtihani wa form four na form two tumekataa kushindwa hesabu na mungu awainue kupata marks nzuri pia tunaombea uchaguzi wa nchi yetu tanzania uwe wa amani na mungu atupe kiongozi mwenye hekima ya mungu.jina la bwana libarikiwe.

 551. Wapendwa Bw.Yesu asifiwe! naomba kuombewa:-
  1. Nipate mume ambaye anamjua Mungu na kumcha mungu
  2. Nipate kazi na nipate fedha
  3. Ninaomba ulinzi wa mungu katika maisha yangu na familia yangu.
  4. Mungu aniepushe na tamaa, magonjwa na niendelee kumjua yeye kwamba ni bwana na mwokozi wa maisha yangu.
  5. Amsaidia dada yangu ambaye yupo Arusha ambaye ana majaribu makubwa katika familia yake ambapo anatokewa na mambo ya ajabu.
  6.

 552. Bwana Yesu asifiwe,Poleni na kazi za kila siku.
  Naomba maombi yenu jamani,Nahitaji Mungu anisaidie nipate ada ya chuo.2-Pia nahitaji amani na mfanya kazi mwenzangu hapa kazini.3-Niishi sawasawa na mapenzi ya Mungu katika maisha yangu na nguvu za Mungu ziwe nami.Mungu awabairiki.

 553. Bwana yesu asifiwe poleni na kazi za kila siku
  Naomba maombi yenu jamani naomba mniombee ni pate mtoto na pia na mume wangu aweze kuacha pombe
  mungu awabariki sana naomba maombi yenu jamani

 554. Bwana Yesu apewe sifa, Poleni na kazi za kila siku.
  Naomba maombi yetu, naomba mniombee nipate mtoto na pia mume wangu aweze kuacha pombe, anakunywa sana pombe.
  Mungu awabariki sana katika huduma hii.Naomba maombi yenu jamani

 555. Shalom, wapendwa watu mungu na washukuru kwa kuiweka blog hii hewani. Ila napia namshukuru mungu kwa kuwa nimeona mungu amezidi kunipigania maisha yangu tangu nikiwa mdogo japo na hisi kwa sasa na pitia mapito fulani. Kwan nimekuwa nikimwomba mungu anipe kazi nzuri ili pia niweze kuisaidia familia yetu na jamii kwa ujumla japo sijafanikiwa kuipata.
  Basi naomba watu wa mungu tuzidi kuombeana katika hilo ili niweze kumshinda ibilisi shetani katika hilo.
  Muzidi pia kubarikiwa watu wa mungu kupitia huduma yenu.

 556. Za leo ndugu wapendwa, nashukuru sn kupata hii website. Nimefurahi na kufajirika kwa kweli. Jamani wapendwa niombeeni niko katika ndoa ya miaka 3 hivi, ndoa imeingia shetani hii nashindwa hata kuelewa. Mwanamme amekuwa haeleweki, mara nasikia anavimada huko nje. Yani imenipelekea kusitisha tendo la ndoa naye. Nilishaongea naye, akaomba msamaha lakini sioni tofauti yeyote. Kwa sasa nimeamua kumuacha afanye atakalo. Sina kazi na niko nchi za nje huku. Ambapo inapelekea nivumilie tuu haya mateso kwa ajili ya wanangu. Nimeshafanya mambo mengi, ikiwemo kutumia uganga ili japo atulie tuu, sikuwahi kuwa mshirikina usichana wangu imenitokea hivi kwa ajili ya haya matatizo tuu na kupewa ushauri wa hapa na pale. Yote naona yamegonga mwamba. Nimekata tamaa sijui hata nifanye nini tena. Namuamini Mungu sana tuu. Sijui nifanye nini. Naomba mzidi kuniombea jamani.

 557. niombeeni wapendwa nami nina miaka miwili ndani ya ndoa yangu,pia nafanya kazi mbali na mke wangu niombeeni nipate kazi karibu na mke wangu,naamini hakuna lililogumu mbele ya uso wa mungu, yesu hashindwi kamwe

 558. Bwana Yesu asifiwe, Namshukuru Mungu kwa ajili ya kazi nzuri kwenye tovuti hii. Mungu azidi kuwabariki sana. Siku za nyuma nilichukia sana kuolewa na hata kukiri kwa kinywa changu kwamba nitazaa tu mtoto bila kuolewa. Kweli midomo uumba nilipata mtoto nje ya ndoa na niliona ni jambo la kawaida kwa wakati ule. Kweli maisha yalisonga ila mara baada ya kupata shida nilianza kuhisi kwamba nilikosea na muda ulikuwa umesonga. Hivi sasa ninasikia sauti ndani yangu ikinihimiza kuishi maisha ya kumpendeza Mungu. Ninaomba watumishi wa Mungu mniombee ili Mungu aliye faraja,tumaini na muweza wa yote ayabadilishe maisha yangu na kunirudishia baraka zake alizoniandalia tangu kuumbwa kwangu. Niko kwenye kipindi kigumu naomba mniombee ili Mungu anijaze faraja, amani na furaha yake siku zote za maisha yangu, na mtoto (zawadi ya pekee) aliyonipa Mungu akulie katika kumjua, kumpenda , kumwamini, na kumtegemea Mungu tu siku zote za maisha yake. Upendo wa Mungu hauna mipaka, naomba mniombee ili Mungu azidi kurudisha pendo lake kwangu niishi maisha ya kumpendeza yeye, japo umri umekwenda ninaamini Mungu atanikutanisha na mume mwema na tutaishi maisha yaliyojaa amani, furaha,na nguvu za Mungu roho Mtakatifu ambaye ni mfariji katika hali zote. Mzidi kubarikiwa.

 559. Mamaa Emmy,

  Pole kwa yanayokusibu. Katika maneno yako nimezingatia sana haya uliyoandika hivi:

  “Nimeshafanya mambo mengi, ikiwemo kutumia uganga ili japo atulie tuu, sikuwahi kuwa mshirikina usichana wangu imenitokea hivi kwa ajili ya haya matatizo tuu na kupewa ushauri wa hapa na pale. Yote naona yamegonga mwamba. Nimekata tamaa sijui hata nifanye nini tena. Namuamini Mungu sana tuu. Sijui nifanye nini. Naomba mzidi kuniombea jamani.”

  Nilichoelewa mimi ni kwamba pamoja na ‘kumuamini Mungu sana tuu’ lakini bado ulishawishika kwenda kwa waganga wa kienyeji, kutokana na ushauri wa ‘hapa na pale’. Hii inonyesha jinsi ushauri huu haukutoka kwa wacha Mungu. Ni jambo lisilopingika kwamba uganga wa kinyeji, hata inapotokea umetatua tatizo fulani, side effects zake huwa ni KUBWA KULIKO TATIZO ULILOKUWA NALO. Unaweza ukamaliza tatizo lakini ukazalisha tatizo kubwa kuliko ulilokuwa nalo mwanzoni. Ni sawa na kuuza ng’ombe kwa kesi ya kuku!

  Ushirikina umegonga mwamba, na ndiko kunakufanya ukate tamaa! Ni jambo zuri sana KUYAKATIA TAMAA mambo ya ushirikina na TAMAA hiyo sasa uielekeze katika KUTAMANI MUNGU AKUSAIDIE kwa msaada wake. Lakini kinachotakiwa kwako sasa ni kuhakikisha UNAMWENDEA MUNGU kwa njia inayostahili. Unatakiwa utubu makosa hayo, ya kumchanganya Mungu na ushirikina, halafu useme bado unamuamini. Maana kwa hali ya kawaida mtu huwezi kumuamini Mungu halafu ukaenda tena kwa sangoma. Hiyo siyo njia ya kumfikia Mungu bali ni njia ya kumfikia shetani, maana mungu wa washirikina na shetani!

  Baada ya kutubu makosa hayo, badili mwelekeo wa fikra zako. [Na Yesu atakusaidia]. Anza kumwamini Mungu KUPITIA YESU KRISTO. Kwa maneno mengine SASA UMWAMINI YESU. Ni vizuri zaidi hasa utakapojikubali kutubu dhambi UENDE MAHALI WANAPOHUBIRI HABARI ZA YESU, hapo ndipo utapata namna sahihi ya kutubu dhambi na kupewa mambo ya msingi kwa ajili ya kumuwezesha mtu aliyetubu dhambi kwa jina la Yesu ili AENDELEE katika ushindi wa TOBA HIYO.

  Utakapotubu dhambi zako na kuendelea katika kumwamini Yesu, hapo ndipo Mungu atatenda kwako, kupitia Jina la Yesu. Mlango wa kutokea katika tatizo hilo utapatikana.

  Ninaamini hapo ulipo kuna watu waliookoka na wana Mungu kwa nji ainayostahili. Inabidi sasa utafute rafiki mmoja wao katika hao ili akusaidie kwa ushauri na mwenendo wa kila siku. Humu kwenye mtandao utapata ushauri sawa, lakini kukiwa na mtu wa karibu, phsyically, itakuwa bora zaidi kwako.

  Inabidi uchukuwe uamuzi huu SASA, kwa kuwa pasipo kufanya uamuzi sahihi mapema, unaweza ukajikuta wewe unafanya vituko zaidi kuliko huyo mume wako ambaye umesema umemuacha. Ukimpokea Yesu sasa utapata pia hakima na busara kwa ajili ya kukabiliana na tatizo hilo. Ingawa lengo kuu la kumpokea Yesu ni KUSALIMISHA ROHO, lakini ndani ya KUOKOKA kuna UFAHAMU na HEKIMA na akili njema kwa ajili ya kupambana na maisha ya kila siku.

  Huu ndio ushauri wangu na Mungu akusaidie!

 560. Ndugu ninapenda kuwasalimu wote ambao kwa namna moja ama nyingine mlishiriki kuifungua hii web site. nimefarijika sana sana. ninapenda kuwa mmoja wenu katika kushirikishwa na kushiriki namna mbali mbali ya maombi. lengo langu kubwa nina uchu wa kujua biblia kwa undani na namna ya kujazwa ROHO MTAKATIFU. ninajua lazima kuna vipengele mbali mbali vinavyoweza kuniongaza kujazwa roho mt. naomba msaada wenu.

 561. Bwana apewe sifa mimi nawaomba muiombee familia yetu ya Mzee lewis tulikuwa tunaishi ndugu kwa kupendana ila kwasasa ndugu hatupendani kila kukicha matatizo pia nawaomba watoto wetu.Nawaomba mniombee ili niweze kupata kazi nzuri zaidi niweze kunasidia famila yangu. Naamini Mungu atasikiliza maombi yenu. Nawatakia kila la heri na Mungu awajaze nguvu.

 562. Bwana Yesu Apewe Sifa, Nina furaha na amani tele hasa baada ya kufahamu hii website (nikiwa natafuta maana ya majina ndipo nilipogongana na website hii). kwa kweli web hii ni nzur sana Mungu azidi kuwabariki na kuwaongezea maarifa zaidi kwaajili ya kuwasaidia kondoo wa bwana, kwa sisi wote wenye mahitaji na matatizo mbali mbali, kwa imani na maombi naamini hakuna kisichowezekana kwa Mungu.

  Watumishi wa mungu naomba mnikumbuke katika maombi yenu ya kila siku katika mahitaji yangu haya
  Ninaomba ulinzi wa mungu katika maisha yangu na familia yangu.

  Kwanza Namshukuru Mungu kwa kunipigani na kunilinda kila siku toka nilipozaliwa mapaka sasa na hata milele.

  * Namuomba Mungu aniepushe na tamaa, vishawishi, magonjwa na niendelee kumjua yeye kwamba ni bwana na mwokozi wa maisha yangu.

  *Naomba mungu anionyeshe na kunipa Mume yule aliyeniandalia toka aliponileta hapa dunian, Mume mwema Mcha mungu, mwenye hofu ya mungu na mwenye upendo.

  * Naomba Mungu anifungulie milango ya mafanikio zaidi katika kazi zagu na azidi kubariki kazi zangu

  * Naomba Mungu anisaidie nizidi kumjua yeye nisitetereke wala kushawishika nizidi kusimama katika njia ya kweli impendezayo Mungu.

  *Mungu anisaidie na kunikinga nguvu zote za giza zinazoniandama

  Naamini kuwa kwa Mungu hakuna linaloshindikana kila kitu kinawezekana.

  Mungu Awabariki Sana

 563. C.I.M,

  Pole kwa yote unayopitia. Pamoja na kuendelea kukuombea lakini kutokana na maelezo yako mimi nimeona kuna mambo ambayo inabidi yawekwe wazi ili nawe ungalie ni nini unachotakiwa kufanya. Maana pamoja na kukuombea hapa pia inategemea wewe uko katika nafasi gani! Ninatanguliza kuomba msamaha kama kuna mahali utaona kama nimeandika maneno magumu/makali. Lengo langu ni kusaidia na si kukuhukumu!

  1. Umeandika kwamba umefika njia panda maana hujuwi la Mungu ni lipi.

  Hayo maelezo mimi nayaona ni sawa kabisa kwa sababu katika maelezo yako inaonyesha jinsi ambavyo HUKUWAHI KUKUTANA NA JAMBO LA MUNGU ili uwe na ujuzi nalo. Kama ungekutana na jambo la Mungu mahali fulani katika mapito yako NI LAZIMA ungekuwa unajua LA MUNGU likoje.

  Maelezo yanayoonyesha kwamba HUJAKUTANA NA JAMBO la Mungu ili uwe na uzoefu [experience] nalo ni pale ulipoandika hivi:

  i). Kabla ya kuolewa ulifunga mara nyingi tu kumwomba Mungu. [huku ukiwa hujaokoka]

  ii). Baada ya kufunga mara nyingi hizo ‘ukadhani’ umejibiwa. Hapa hukuwa na ‘uhakika’ kama umejibiwa.

  iii). Kisha mkafunga ‘ndoa takatifu’ katika kanisa katoliki.

  Hakuna ndoa takatifu kwa watu ambao hawajaokoka, kwa kuwa kilicho kitakatifu ni watu wanaofunga ndoa hiyo. Maelezo yako yanaonyesha kwamba mlifunga ndoa hiyo mkiwa hamjaokoka, na hadi sasa mume wako hajaokoka.

  iv). Umeomba muda mrefu kadri ya uwezo wako toka mwaka 2004 novemba, lakini wewe umeokoka januari 2010! Sasa kama umekuwa ukiomba kwa kadri ya uwezo wako na bado ulikuwa hujaokoka, sasa sijuwi ulikuwa unaombaje? Maana Biblia inasema Mungu hawasikii wenye dhambi. Mtu ambaye hajaokoka, hafahamu njia sahihi ya kuomba, maana uhai wa maombi hutokana na uhusiano wa kati ya anayeomba na Mungu, na SI uzito tu wa maombi.

  Kutokana na maelezo hayo ni wazi kwamba HAIWEZEKANI ukafamu ni LIPI LILILO LA MUNGU maana hakuna popote kwenye maelezo yako panapoonyesha ulikutana na LA MUNGU ili uweze kulifahamu. Na kwa hali hiyo ni lazima mtu atajikuta njia panda, kwa kuwa hajawahi kuvuka hapo:

  Kuomba Mungu wakati mtu hujaokoka ni kuzunguka njia panda. Kufunga ndoa halafu ikaitwa ni ‘takatifu’ wakati wanaofunga ‘si watakatifu/hawajaokoka’ ni kuzunguka njia panda. Kuomba halafu mtu ‘akadhani’ Mungu pasipo kuwa na ‘uhakika’ ni kuzunguka njia panda.

  USHAURI WANGU KWAKO

  1. Badili mwelekeo wa mawazo yako ili uache kumhusisha Mungu kwa jambo ambalo hakuhusishwa toka mwanzo. Usiwe na mashaka na Mungu na Mungu akusaidie usije waza lolote baya kuhusiana Naye.

  2. Kama sasa umeokoka inabidi ufahamu mpaka kati ya maisha ya dhambi/KABLA YA KUOKOKA na maisha matakatifu/BAADA YA KUOKOKA. Ukishafahamu mpaka huo utatambua kwamba tangu 2004 hadi januari 2010 maombi yote uliyokuwa unaomba yalikuwa ni ZERO. Kuanza kuhusisha maombi ya wakati ulipokuwa hujaokoka ili yatende kazi hata baada ya kuokoka ni sababu tosha ya wewe kuanza kujichunguza ULIVYOOKOKA ULIOKOKAJE pasipo kuyaacha ya KALE na kuanza maisha mapya!

  3. Kabla hujawaza kama yeye alikupendea kazi au mali yako NI HERI ukianza na kujihoji wewe mwenyewe kuwa NI NINI ULICHOMPENDEA hata ukakubali kuolewa naye! Ni kitu gani kilichokufanya ‘ukadhani’ ni Mungu amejibu hadi ukakubali kuolewa naye. [Mara nyingi watu tunakwama sehemu hii: linapotokea tatizo tunakuwa wepesi wa kunyoshea mikono upande wa pili pasipo kuanza kwanza na sisi wenyewe.] Sasa ukishaanza kujihoji wewe kwanza kabla ya kutupia lawama kwake UNAWEZA UKASHANGAA kwamba pengine chanzo cha hali yote hiyo ni wewe na hivyo ufumbuzi wa tatizo hilo unaweza kutoka kwako mwenyewe pia! [hili ni wazo tu na si lazima iwe hivyo]

  4. Usiwaze kabisa kwamba “SIJUWI NI MUNGU AMERUHUSU?” kwa kuwa HAUNA HATA UHAKIKA KWAMBA ni Mungu aliyehusika hadi ninyi mkaoana. Kuwaza hivyo kunaweza kukakufanya ujihesabie haki na ukaanza kumdai Mungu kitu ambacho hata ukidai vipi, jibu lake haliwezi kupatikana ki hivyo kwa kuwa madai hayafanyiki katika utaratibu unaotakiwa. Ni Heri kama utaanza kuwaza kama hivi, “SIJUWI NI MIMI NILIYEKOSEA?” Mawazo kama hayo yatakufanya ujisikie wewe ni mkosaji [kama utagundua kuwa ulikosea mahali] mbele za Mungu na hivyo kubadili namna yako ya kuomba ili kabla ya kumuombea Mume wako kwanza uanze na KUOMBA TOBA mbele za Mungu. Toba ya kweli hufungua milango kwa ajili ya kupokea toka kwa Mungu!

  5. Ondoa mawazo ya jumla kwamba kila ndoa inayofungwa katika dhehebu lolote la kikristo ni ndoa takatifu! Mawazo yakishaondoka hapo utapiga hatua na kutambua kwamba ndoa yako haikuwa takatifu, kwa kuwa kufungiwa RC si sababu ya utakatifu wa ndoa. Ndoa ingekuwa takatifu kama mngefunga mkiwa mmeokoka. Kutambua hilo kutabadili mtazamo wa ndoa yako na kukufanya uhitaji rehema za Mungu na kumuomba Mungu sasa AISAFISHE ndoa hiyo!

  6.Kumbuka njia ulizotumia ili na yeye apate kazi serikalini. Inawezakana kama hazikuwa njia nzuri zikawa pia ni sehemu ambayo inaweza kufanyika kifungo kilichomfikisha hapo alipofikia. Ukishagundua kama hazikuwa njia nzuri omba Mungu akusamehe kwa hilo.

  7. Tafakari kuhusu kuokoka kwako ili uone kama baada ya kuokoka kuna badiliko lolote lilitokea moyoni mwako. Nimeandika hivi kwa sababu ya maelezo kwenye pointi ya 2 katika USHAURI. Ukigundua kama kuna upungufu wowote ufanye uamuzi mpya na sahihi. Kufanya uamuzi mpya [kama utaona kuna haja hiyo] kutafungua ufahamu wako ambao utakusaidia katika kupata hekima za kuishi katika kipindi hiki cha mpito, ikiwa ni pamoja na kufahamu ni NI WAPI HASA penye tatizo.

  8. La mwisho; Kwa kuwa mlifunga ndoa kanisani nina imani ilikuwa na wasimamizi ambao naona ni vizuri ukawashirikisha [kama hujafanya hivyo]ili kuwaomba ushauri nao usikie watasemaje. Lakini pia unaweza kuwashirikisha viongozi wako wa kiroho wanaokuongoza sasa baada ya kuokoka.

  Mwisho niandike kwamba nami ninakuombea ili Mungu alete ufumbuzi sahihi wa tatizo hili unalokabiliana nalo.

 564. Bwana Yesu asifiwe sana! nakushukuru sana mtumishi wa Mungu kwa kunifungua masikio hasa sehemu ya maombi kabla ya kuokoka na baada ya kuokoka pia ndoa niliyonayo ya kikatoliki umenipa mwanga sana kakangu. kuhusu mengine yote nilishafanya imeshindikana, wamemshauri watu mbalimbali lakini wapi. mahusiano na mawasiliano yetu ni magumu sana.yeye shida yake ni mali tu. juzi alitaka kuuza gari yangu kwa nguvu misina taarifa akawa amepokea milioni 7 alipokuja kuchukua mi nikaizuia. jana akaja saa 10pm akasema anatoka na gari nikamwachia saa 12.30 ananipigia simu kuwa gari imeungua engine na vitu vingine na kweli imekufa imebakia bodi tu. nilishawahi kumwomba msamaha mara nyingi tena bila kuona kosa lolote lakini akasema hujanikosea chochote ndipo nika hisi anatamaa ya mali na utajiri wa haraka maana mi mbaya lakini malizangu anataka amiliki kila kitu hati za nyumba zote 3 na kadi za gari anataka akatunze anapojua yeye nilikataa. chuki na uhasama hana huruma kabisa anafanya matendo ya ukatili mkubwa ikawa moja moja mpaka leo.

  Ukweli katika hali hii sijui namna ya kuomba kwanza bado mchanga ktk wokovu. tangu nimeokoka januari nimepata angalau amani kidogo siyo kama kabla ya kuokoka maana nilikuwa nakimbia nalala nje ya nyumba kwenye maua. lakini sasa hivi nilikuwa siwezi hata kupata usingizi nilikuwa nalia kila wakati. namshukuru sana mungu baada ya kuokoka nina nguvu ya kuvumilia. hili ni mungu pekee ndio anaweza kulimaliza lakini wazee, marafiki zake wameshindwa ile roho ya utajiri imemshika hasa muda wote anafikiria akaibe wapi fedha hata kazini kwake anaiba vitu mbali mbali analeta nyumbani nimemshauri wapi. kazi yake alimtafutia kaka yangu mimi kabisa baada ya kumlilia sana kakangu amsaidie mume wangu basi akamsaidia akapata kazi nzuri hivi sasa ana pikipiki 3 na gari moja na anajenga nyumba yake lakini haridhiki anataka anyang’anye na za kwangu. gari yake anayo lakini anang’ang’ania ya kwangu, huyu ana roho gani sijui inayotenda kazi ndani yake. nisaidie unifundishe katika hali hii niombeje sasa ni badilishe maombi. hapo utakuwa umeshapata picha kamili na umeshajua huyu anaweza akawa na roho gani zinazotenda kazi ndani. pia nifundishe na kuniombea namna ya kumwomba mungu AITAKASE NDOA YANGU. MUNGU AKUBARIKI SANA JP. umesema nikuandike kuwa unaniombea naomba unieleweshe namna ya kukuandika! usinichoke mtumishi. mungu ameshanielekeza kwako ili kupitia wewe mungu ajitukuze

 565. Mpendwa C.I.M

  Namshukuru Mungu kwa kuwa umepata jambo lililokusaidia katika yale niliyoandika.

  Pale nilipoandika kwamba “Mwisho niandike kwamba nami nakuombea” nilikuwa naamanisha kuwa: Kwa kumalizia, yaani mwisho wa maoni yangu, nimalizie kwa kuandika kwamba na mimi ninakuombea. Sikuwa nakuambia wewe kwamba ‘uniandike’.

  Natumaini umenielewa sasa. Samahani sana kwa kuwa sikuandika kwa kiswahili fasaha.

  Nimesoma vizuri maoni yako, na nimepata picha kamili kama ulivyoandika. Lakini jambo moja ninalofahamu ni kwamba kuna watumishi mbali mbali wa Mungu wanaosoma hapa. Na kwa kusoma maelezo yako hayo kuna mtu anaweza kuwa ana jambo la kukushauri au kukuelekeza. Ninaomba tuuache mlango wazi ili kila mtu mwenye neno linaloweza kukusaidia afanye hivyo pasipo kusita.

  Mimi nitaandika kwa sehemu yangu yale nitakayoyapata kukushauri au kukuelekeza. Lakini wakati sijafanya hivyo, mazungumzo haya yako wazi,hivyo ye yote mwenye neno la kujenga anakaribishwa ili tumsaidie dada yetu huyu.

  Mungu atusaidie.

 566. Bwana Yesu asifiwe!!!!
  Namshukuru Mungu kwa kujibu maombi yangu ya kupata kazi, sasa nimeajiriwa na naanza kuyaona maisha si magumu sana.
  Namuomba Mungu kwa mara nyingine tena aweze kunisaidia nipate mchumba mwema ninaeendana nae na niishi naye vizuri pale atakapokuwa mke wangu.
  Najua Mungu anajua zaidi ya mimi nijuavyo naomba Mungu Uniongoze katika kupata mchumba mwema
  AMEEN!!!!

 567. Naomba wapendwa tuowaombee vijana waliookoka mungu awainue na awape nguvu waweze kuwa chachu kwa vijana wenginewaliopo katika hii dunia

 568. BWANA YESU ASIFIWE,
  WAPENDWA NAOMBA MAOMBI KWANI NIMEKUWA NA HALI NGUMU KIUCHUMI KIASI KWAMBA NASHINDWA KILIPA MADENI PAMOJA NA KUWA NA NIA SANA YA KULIPA. PIA NINAO WADAI HAWALIPI

 569. Bwana Yesu asifiwe wapendwa,
  nahitahi mnisaidie katika maombi shetani ananitesa sana nimekuwa mtu wa madeni kila siku kila nikipata pesa sioni cha maana ninachokifanya kifupi mimi ni mjane na nina watoto wa watatu ambao bado ni wadogo na sina msaada wowote niaopata toka kwa mtu yeyote zaidi ya kuhangaika mimi mwenyewe.Kwa kweli niko katika vita kali naomba maombi yenu. kwa taaluma mimi ni secretary na ni mwalimu wa computer nahitaji kufungua Center ili niweze kujiajiri mwenyewe naomba muwe pamoja nami katika maombi ili mungu aweze kutenda muujiza ndani yangu, napitia magumu mengi wapendwa ukizingatia umri wangu bado mdogo, asanteni naomba Mungu awabariki

 570. Naomba mniweke kwenye maombi ili niweze kupata kibali cha kukaa huku Finland, Nasoma ila kwa sasa kibali(Visa ) changu kina matatizo,Naomba saana mniombee ili nifanikiwe kupata maana nataka sana kumaliza shule yangu salama.

  Asante Mungu azidi kuwabariki woote.

 571. naombeni mniombee niweze kufanikiwa katika maisha yangu na mungu anifungulie milango ya mafanikio na niendelee vizuri katika masomo yangu na nifanikiwe nipate mke mzuri ambaye ninampenda na naamin mungu katenda amin.

 572. Dada C.I.M

  Natumaini unaendelea vema katika mapambano ya imani juu ya hayo unayopitia.

  Ninauliza kuwa wewe unaonaje kama ningewasiliana nawe kwa email yako kwa kuwa mambo mengine pengine yanaweza kuwa too personal kuyaandika hapa?. Ninahitaji tuendelee kuzungumza!

  Kama wazo hili ni sawa ninaomba unifahamishe, kisha anuani yako ya email nitaipata kwa wahusika wa mtandao ili nikuandikie. Au kama unaona hapa panafaa tu pia unaweza kunijulisha tu.

  Mungu azidi kukupigania!

 573. Kaka John Paul Bwana Yesu asifiwe sana! ukweli kama ulikuwa moyoni mwangu, namitoka siku ile nilipenda nikuombe kama inawezekana utumie email yangu. sawa nitumie

 574. Wapendwa bwana asifiwe!!!!

  Niko katika kipindi kigumu cha kutafuta mwenza wa kuishi naye, ni muda ambao nahitaji kumwomba Mungu aniongoze na ninyi wapendwa mnisaidie kuomba. Namshukuru Mungu amenipa kazi ambayo nilikua naiota tangu naanza masomo yangu ya digrii ya kwanza.
  Naomba wadau mnisaidie kuomba nipate mchumba Mwema ninayeendana nae.
  Kwa ushauri namba yangu ya simu ni 0714118949 karibuni sana na Mbarikiwe na bwana…..

 575. Bwana Yesu asifiwe! naitwa C.I.M kaka John Paul naomba basi tuwasiliane kupitia email yangu mhagamaclementina@yahoo. mambo magumu lakini Bwana Yesu ananipigania

 576. Bwana apewe sifa ndugu zangu. Napenda niwashirikishe katika kuniombea yafuatayo:
  1. maumivu niliyonayo ya tumbo.
  2. watoto wangu Theresa na Blandina. ili Mungu azidi kuwasimamia katika maisha yao na masomo yao.
  3. Naomba Mungu azidi kunisimamia katika kazi yangu na kunipa baraka zake.
  4. Mungu anijalie mume mwema na wa kumpendeza yeye.

 577. Bwana Yesu asifiwe!

  Kaka Ben, nataka kwanza kufahamu kama unamwomba Mungu mchumba ama mke? Mungu hatoi mchumba anatoa mke mwema. Kama ni mke nipo pamoja nawe katika maombi, nitakutumia mistari ya kusimamia hilo hitaji, ubarikiwe

 578. Bwana Yesu Asifiwe.
  Namshukuru Mungu kwa kunionyesha website hii nilikuwa nikisearch jinsi ya kuomba nikakutana na hii website, Jina la Bwana liimidiwe.
  Tatizo langu ni Mume wangu, nilikuta sms kwenye simu yake ya mwanamke mwingine baada ya kumuuliza akasema ni kweli anauhusiano nae na anataka kumuoa kuwa mke wa pili na ameishajitambulisha anataka kupeleka mahali. Nimesikitika sana kuzingatia ndio kwanza tuna mtoto wa miaka 2 na bado hatujafunga ndoa. Naomba mniweke kwenye maombi yenu niweze kufunga ndoa na nguvu ya kuoa mwanamke wa pili zishindwe.Mungu awatie nguvu katika uduma ya kiroho.

 579. Shalom wapendwa,
  Hakika Mungu ni Mwema kabisa, mimi ni mara ya kwanza kuingia ktk blog hii nimefurahishwa na ushuhuda na maombi yenu yanatia moyo na kusema Hakika MUNGU WETU NI MWEMA KTK MAISHA YETU. Mimi dada ambae nina tatizo la kutosikia vizuri namshukuru Mungu kwa kunitunza maana wazazi wangu wametangulia mbele ya haki zaidi miaka kumi, Wapendwa nawaomba mniombee kwanza nampenda Yesu,nahitaji nisimame imara ktk wokovu maana siku hizi najikuta nashindwa kusali usiku nalala sana, pili namshukuru Mungu nimepata kazi shirika la umma nina miezi mitatu bado sijathibishwa kazini,nahitaji mwenzi wa ndoa,kunifungulia milango ya baraka/ fedha, pia wapendwa nimekuwa ninadhulumiwa sana fedha kwa marafiki Na afya kwa ujumla.NAAMINI BWANA ATAFANYA MAANA YEYE ANAWEZA.
  MUNGU AWATIE NGUVU KTK KUTANGAZA UTUKUFU WAKE. MBARIKIWE SAAANA WAPENDWA.

 580. Bwana Asifiwe wapendwa,
  Mimi nimekuwa nikifanya maombi ya kupata mchumba kwa muda mrefu sasa, nina miaka 32 na ninaishi nchi moja ya kiarabu ambayo ni waislamu watupu, hakuna kanisa wala njia ya kukutana na wapendwa. Tafadhali mnisaidie katika maombi.
  Namba zangu ni +971508534354.
  eattinda@gmail.com.

 581. Bwana Yesu asifiwe naomba mniombee ndoa yangu inashida pia ktk kila biashara ninayofanya haifanikiwi,nadaiwa benki

 582. Naomba tushirikiane katika maombi juu ya haya, tumuombe MUNGU anijalie kazi anayotaka yeye, nina degree ya Cooperative Management and Accounts (Management Option) na sasa namalizia research yangu kukamilisha masters degree on Public Administration.
  Nina experience ya miaka miwili kabla sijaenda tena masomoni kama project coordinator at APT/KWIECOO Solar Drying Project dealing with supporting and capacity building for widows, disables, olds and HIV/AIDS.
  Naomba mniombee sana.

 583. Naomba mniombee kazini kwangu bosi kasema nisihubiri neno la MUNGU kwa sababu wengi hawataki, lakini nitashida kwa maana bosi wangu YESU won the game.pia nataka promotion kazini.

  Florence kutoka kenya

 584. Shalom watumishi wa Mungu!

  Naombeni mniombee nipate amani na nizidi kukua kiroho, pia naomba sana Mungu wa mbinguni anipe Mume tufunge ndoa takatifu maana yeye ndo mweza wa yote.

  Naamini Mungu atatenda sawa na nimwombapo

 585. BWANA YESU ASIFIWE!NIMEOKOKA,NALETA HITAJI LA KUPATA KAZI NZURI YA KUDUMU.NAAMINI MUNGU NI MWAMINIFU ATANIPATIA KAZI NZURI KWA WAKATI WAKE.MUNGU AWABARIKI WOTE MTAKAONIKUMBUKA KWENYE MAOMBI.

 586. Nawasalimu katika jina la Bwana Yesu!

  Ninawaomba pamoja mniombee kwa Mungu nifaulu masomo yangu. Matokeo yanayoka tare 31/12/2010. Ninamwamini Mungu. Ahsante.

 587. have faith in God. With God all things are possible.
  Mungu wetu tunamwaemwamini asikie kuomba kwenu, katika jina la Yesu Kristo na hali zotezilizo kikwazo katika njia yenu zisafike. Amen

 588. Wapendwa poleni na kazi ngumu ya kulitukuza jina na bwana wetu yesu kristo

  Ninaomba muombe nami mambo yafuatayo
  1. Kwanza namshukuru Mungu kwa kunipa kazi pia naomba muendelee kuniombea ili damu ya yesu kristo inifunike na kuibariki kazi yangu shetani asipate nafasi.

  2. Naomba muwe nami ili mume wangu aweze kupata kazi.

  3. Namwombea mtoto wangu mungu aendelee kumpa ufahamu wa elimu na hekima ya kuishi na watu.

  4. Namwomba mungu afungue milango ya baraka na neema.

  5. Kuwabariki wadogo zangu kutambua walikotokea na wanakokwenda.
  6. Kuwaombea wagonjwa wote walioko majumbani na mahospitalin.

  Ubarikiwe sana mpendwa.

 589. Bwana Yesu asifiwe, nawasalimu katika jina la Bwana, kwa pamoja ninaomba mniombee niweze kujifungua salama hapo mwakani January. pia nipate amani na nizidi kukua kiroho, pia naomba sana Mungu wa mbinguni aniwezeshe kufunga ndoa maana yeye ndo mweza wa yote.

  Naamini Mungu atatenda sawa na nimwombapo. Mbarikiwe sana

 590. shalom annaloyce! Mwamini Mungu aliyekusaidia ukapata ujauzito ambao wengine wanauomba kwa kushindwa kupata kwa juhudi zao pia atakusaidia ujifungue salama. Usiogope amini uweza wa Mungu kuliko matisho ya ibilisi. Nitakuombea na utajifungua salama na suala la kufunga ndoa nalo tutamwomba Mungu atende ili umtukuze yeye Amina!!!

 591. Dada Annaloyce na kwa ye yote ambaye maneno haya yatamhusu,

  NI kweli kabisa tunahitaji msaada toka kwa Mungu. Hakuna mwingine wa kutusaidia. Lakini pamoja na kuwa ndiye pake yake wa kutusaidia ziko kanuni za kupokea kutoka kwake. Ndiyo! Ni kweli yeye huwanyeshea mvua wema na wabaya; huwaangazia jua watu wote. Hata wale wanaomtukana na kumkufuru. Kwa hiyo yako mambo mengi ambayo tunaweza kuyapata tu hata kama hatumuombi yeye. Ni kwa sababu ya wingi wa wema wake kwetu. Lakini pamoja na hayo, linapokuja suala la mahitaji binafsi, hasa baada ya mtu kuutambua uwepo wa Mungu, hapo ndipo lazima mtu akae katika kanuni ambazo ndizo maagizo ya Mungu!

  Mimi niliposoma hitaji lako la maombi niliogopa! Kwanza hapo ulipo unatarajia kujifungua januari hii halafu unataka Mungu akuwezeshe kufunga ndoa!

  Kwangu mm ninaona kuwa mambo haya yako mbali mbali sana. Labda, narudia tena, Labda kama unayetarajia kufunga naye ndoa ni huyo baba wa mtoto mtarajiwa: Ili maana ya ndoa yenu iwe ni kule kupata makaratasi yanayotambulika kisheria za nchi.

  Lakini kama huna mtu ambaye unahitaji kufunga naye ndoa, ninafikiri kuwa suala la kuwekea kipaumbele kwa sasa ni kujifungua kwanza, umlee mtoto hadi afikie umri ambao angalau unaweza kuwa huru kidogo [kazi ya kulea na kunyonyesha ikipungua]. Mtoto akishakua ndipo lifuate suala la kuhitaji mwenza kwa ajili ya kuishi pamoja! Kikristo, kuishi pamoja maana yake ni kufunga ndoa!

  Na kama unayetarajia kufunga naye ndoa ni huyo anayehusika katika mtoto mtarajiwa hapo ni jambo jingine. Itategemea sasa, kama wewe umeokoka na yeye je? Au utaamua tu kufunga ndoa naye? Kama ameokoka mambo yalifikaje huko? Pengine mlipata nafasi yakutengeneza na Mungu? [kama mlitengeneza ni ninyi na Mungu ndio mnajua]. Na kama mlitengeneza labda sasa mnaishi pamoja ila bado tu uhalalisho wa ndoa?…nk, nk.

  Hayo ni baadhi tu ya maswali ambayo yamenisumbua katia suala lako hilo! Mimi sikuhukumu wala si hakimu lakini ninashauri tu.

  Mungu huwa hafanyi mambo kwa vile tu tunamuomba, bali hufanya mambo kutokana na kanuni zake. Sasa kama umeokoka [maana umehitaji kuombewa ukue kiroho] ninakuomba tulia mbele za Mungu. Tafakari sana na umuombe Mungu akupe neema ya kupambanua ili uweze kufahamu NINI cha kufanya kwanza na USAHIHI wake wa kukifanya katika Mungu.

  Pasipo kupambanua mambo tunaweza kujifariji hapa kwamba tunaombeana kumbe tunadanganyana!

  Mungu atusaidie!

 592. Dear my beloved brothers and sisters,

  Prayers are a primary thing in every believers life. I choose to use believers because we also have christians who profess Jesus Christ to be their Lord and Saviour, yet they have not accepted Him in their lives.

  Let us pray that we all who are doing God’s work will be strengthened by faithful intercessors. For they are those who say they will pray but are very weak in praying and are not at the level which I call the ‘Prayer Eagle’ stage whereby if they command the enemy is destroyed and I am not discouraging those who are praying for to get to this stage you have to go through a lot of preparations. The Lord bless you all and even if you are struggling continue for the race is won when you are 5 foot under and we are praising you at your funeral for your good works and the Christ we saw in you when you lived. Glory be to God.

 593. Bwana Yesu asifiwe! Wapendwa naomba maombi yenu ili niweze kupata mume wa kuishi naye. nina miaka 32 sasa nina kazi nzuri ila napata wakati mgumu sana kwani hadi sasa bado hitaji langu la kumpata mweza halijajibiwa. wapendwa naomba mnipatie mistari ya kusimamia katika hili hitaji langu.

 594. Bwana wetu Yesu apewe sifa sana wapenzi, naomba maombi yetu kwa watoto wangu ili waweze kuwa na mwenendo wa kumpndeza Mungu. Mungu awawezeshe kuacha yafuatayo:-
  1. KUNYWA POMBE
  2. WAACHE UZINZI
  Mimi naamini wkiacha kunywa pombe watakuwa wanafanya yale yampendezayo Mungu maana pombe ni kiatu cha shetani shetani namkataa na kumtupa kuzimu katika Jina la YESU.

 595. Bwana Yesu asifiwe Wapendwa naomba mniombee milango ifunguliwe kwa kila ninachofanya ili niweze kupata mafanikio.
  Mungu awabariki.

 596. Bwana Yesu asifiwe,Mimi nilikuwa naomba sana mniombee niweze kupata mtoto sababu nimehangaika lakini imeshindikana nina imani YESU ANAWEZA YOTE.

 597. Bwana Yesu asifiwe ndugu zangu ktk Kristo Yesu naomba sana mniombee,Nimeandamwa na roho ya madeni na kutokufanikiwa, kila ninachofanya hakiendi madeni yanaongezeka sina amani,lakini Yesu mwenyewe alisema tukiomba lolote kwa jina lake atafanya

 598. Bw Yesu apewe sifa. Mimi shida yangu kubwa naomba mniweke kwenye maombi yenu nipate mtoto, kwani ni muda mrefu sana nimehangaika. Nimefunga period sasa ni miezi mitatu nimecheck nimekuta negative. Niombeeni Mungu afanye miujiza yake. Jina la Bw libarikiwe AMINA.

 599. Shalom!watu wa Mungu, napenda kuwakumbusha juu ya jukumu la kuombea watoto wetu wa kiroho na kimwili pia maana adui yetu ibilisi na Shetani anatafuta kuwaharibu na kisha kuwaua, usilegee hata utakapoona wamekua na wameimarishwa. mbarikiwe! Shalomu.

 600. shaloom

  naombeni maombi yenu wapendwa nina vita kali sana ofisini kwangu,ibilisi anataka nifukuzwe kazi kwa ajili ya maneno yasiyokua yakweli.Mungu nitetee
  sina raha nina madeni pia niombeeni uchumi wangu unayumba .

  mama ivan

 601. Wapendwa ktk Bwana wetu yesu kristo naomba mniombee sifanikiwi ktk kila ninachokifanya wakati imeandikwa ktk 3 Yoh 1:2 mpenzi naomba ufanikiwe ktk mambo yote na afya yako kama vile roho yako ifanikiwavyo.pia nina madeni mengi,hadi benki wananidai niko ktk wakati mgumu.

 602. bwana yesu asifiwe wapendwa,poleni na kazi ya bwana,naomba mnisaidie katika maombi hali yangu ya uchumi ni mbaya sana.shetani amefunga milango yote ya kufanikiwa kwangu.NAJUA BWANA ANAKWENDA KUTENDA MAKUBWA.AMINA

 603. bwana yesu asifiwe wapedwa,polen na kazi ya bwana,naomba mnisaidie kutoka katika kifungo hiki mimi huwa naugua kila mwaka kuanzia mwez wa pil mpaka wa saba kwa hiyo naomba wapendwa nisaidieni kwa hilo kwani ninapoandika masage hii mdogo wangu wa mwisho wa damu moja anaumwa ugonjwa kama ambao naugua mimi ugonjwa tumeenda kila hospitari tunaambiwa ugojwa haueleweki mpaka ilifikia sehemu kwenda kwa waganga naomba nisaidiwe kwa hilo mungu awatie nguvu.amina

 604. Ndugu Peter,

  Pamoja na maombi yanayoendelea hapa, mimi nina haya yafuatayo:

  Natumaini unaposoma 3Yohana 1:2 huwa unasoma pia Zaburi 1:1-3 ambapo mstari wa 3 unasema hivi,
  “Naye atakuwa kama mti uliopandwa kando kando ya vijito vya maji, Uzaao mtunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki, Na kila alitendalo litafanikiwa”

  Nasisitizia ‘NA KILA ALITENDALO LITAFANIKIWA’.

  Katika hitaji lako umeandika kwamba “kila utendalo halifanikiwi” ambacho ni kinyume kabisa cha maandiko haya katika Zaburi. Katika Zaburi sharti la kufanikiwa katika kila alitendalo mtu ni yale maneno yaliyoandikwa kuanzia Zaburi 1:1-2. Lakini katika 3Yohana kigezo cha kufanikiwa katika mambo yote ni KWA KUWA ROHO INAFANIKIWA. Mzee Yohana aliona kuwa Gayo alikuwa amefanikiwa katika mambo ya rohoni kutokana na ushuhuda aliopelekewa na wapendwa [3Yhn 1:3].

  Sasa tukiyaunganisha maandiko haya mawili, yaani 3Yohana 1:2 na Zaburi 1:1-3 tunaona kwamba kufanikiwa kwa mcha Mungu, au kufanikiwa kwa kanuni ya Mungu ni matokeo ya mafanikio katika roho. Kutokwenda katika shauri la wasio haki, kutokusimama katika njia ya wakosaji, na kutokuketi barazani kwa wenye mzaha; kupendezwa na sheria ya Bwana na kuitafakati usiku na mchana ni moja ya sifa za mtu ambaye kwake yeye kila alitendalo litafanikiwa. Mambo mengine ni upendo, uaminifu, kufadhili kazi ya Injili nk. Kutokana na maneno hayo ni kwamba yeye asiyetenda hayo kwake “Kila alitendalo halifanikiwi”!

  Mara nyingi imekuwa rahisi kwetu, pamoja na mimi, kusoma tu sehemu moja ya maandiko inayoelezea matokea ya jambo pasipo kuangaliza sana maandiko yanayoeleza mambo yanayoweza kusababisha jambo hilo litokee. Watu wengi husoma kwa matumaini makubwa Nyakati 28 msatri wa 3 na kuendelea, maneno yasemayo, “Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani. utabarikiwa uzao wa tumbo lako……! Lakini si wengi huzingatia umuhimu wa ule mstari wa 1 usemao, “Itakuwa utakapoisikia sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake…..!

  Kubarikiwa kwa kanuzi za Mungu hakuji tu hivi hivi. Kuna jambo ambalo tunatakiwa kuwafanya. [Sasa hapa naomba nieleweke kuwa sikuhukumu wewe bali ninaandika maneno ambayo hata mimi mwenyewe yatanisaidia, na huu ni ushauri tu ili kama unaweza kupata la kukusaidia utachukuwa]. Kuna mambo ambayo ni lazima tufanye ili tuwe katika nafasi za kupokea toka kwa Mungu. Hivyo maandiko ni MUHIMU kuyatumia lakini ni MUHIMU ZAIDI kuhakikisha tunayatumia kikamilifu.

  Kwa kuwa umeamua kutumia andiko hilo,basi ninakushauri hakikisha pia kama roho yako imefanikiwa ndipo uweze kutumia andiko hilo la 3Yohana 1:2 kwa ujasiri. Maana hilo halifanyi kazi peke yake pasipo yale kwenye mstari ule wa 3 na 5.

  Nikiacha upande huo wa maandiko, kufanikiwa au kutokufanikiwa kwa mambo ya maisha si mara zote kunatokana na sababu za kiroho. Mzee Yohana alipomwandikia Gayo, ingawa haikuandikwa, lakini mimi naona kuwa, aliona kuna uwezekano Gayo akafanikiwa rohoni lakini mambo ya mwilini asifanikiwe. Yaani mtu anaweza akawa ameokoka vizuri lakini asifanikiwe maisha ya kimwili. Na hili linaweza kutokea kwa sababu ya kutokufuata kanuni za kufanikiwa maisha ya mwilini.

  Inawezekana kabisa mtu akawa ameokoka lakini asitumie akili yake vizuri. Kutokutumia akili vizuri ni pamoja na kuwa mvivu; kutokuwa na vipaumbele kwenye maisha; kutokuwa na mipangilio mizuri; kuishi kwa kuiga watu wengine; nk. Wako waliookoka lakini hawajishughulishi kabisa na mambo ya maisha au kama wanajishughulisha si katika bidii na ustadi unaotakiwa.

  Pesa ina kanuni zake pia. Na nyingi ya kanuzi hizi kufundishwa katika mafundisho mbali mbali ya biashara na ujasiriamali. Mambo ya kudaiwa benki, kama ulivyogusia, kunatokana na watu wengi kutokutafakari kwanza kabla ya kuchukua mkopo. [simaanishi wewe]. Wengi wanajikuta katika wakati mgumu, hata nyumba/mali zao kuuzwa kwa sababu tu hawakuwa wametafakari kwanza kabla ya kuchukua mkopo. Mikopo kwa ajili ya biashara ina kanuni zake. Ndiyo! Najua kuwa kuna matatizo yanaweza kutokea kutokana na sababu mbali mbali yakiwemo yaliyo nje ya uwezo, yanayoweza kukwamisha malengo fulani yasifikiwe. Lakini kwa takwimu zisizo ramsi,wanaokwama kwenye biashara baada kuchukua mikopo wengi zaidi wanakwama kwa sababu ya kutokufuata kanuzi za pesa kuliko wale wanaokwama kutokana na kuharibika kwa kile walichokuwa wanafanya.

  Kwa maneno hayo machache nasema kuwa , si kila mkwamo wa mtu wa Mungu unahitaji maombi ili kuutatua. Mikwamo mingine inahitaji kukaa chini tu na kutafakari tatizo lilipotokea kisha kuchukua hatua. Maombi yakitumika mahali pasipo pake hayawezi kabisa kuleta ufumbuzi unaotarajiwa.

  La msingi sasa ni kuangalia kama hayo unayopitia ufumbuzi wake ni maombi tu au kuna kitu unatakiwa kufanya. Mtu aliyeokoka anategemewa afanikiwe zaidi katika anayoyafanya hata yale ya kimwili. Lakini pia ni lazima awe anafuata kanuni zake. Akili njema na roho njema ndivyo vigezo vinavyoweza kumfanya mtu afanikiwe katika kila alitendalo. Kufanikiwa katika maisha ya kimwili ya mtu hakuji kwa miujiza, bali kunakuwa na mambo anayotakiwa ayafanye, ambayo yakifanyika hayo ndipo husababisha matokeo ya kufanikiwa katika mwili kama roho ifanikiwavyo na hatimaye kufanikiwa katika kila alitendelo!

  Mungu akutunze, nami pia ninaomba pamoja nawe!

 605. nakuwa mipango napata pesa ikifika kufanya niliopanga matatizo yantokea pesa inaisha mengi mara hili pesa inaisha niombeani jamani naushauri munipe roho madeni initoke

 606. Bwana asifiwe, naitwa Joy, nina miaka 32. Nina elimu ya chuo kikuu lakini nina tatizo la kupata kazi. Naomba sana mniombee niweze kupata kazi na pia niweze kupata mume mwema. Naamini kabisa Mungu atatenda. Pia naomba sana mniombee ili niweze kufunguliwa vifungo vyote vinavyonirudisha nyuma mafanikio yangu kila kukicha.

 607. Bwana wetu yesu kristo ainuliwe, mimi binafsi natoa maombi kwenu kikundi cha maombi tuliweke mikononi mwa Bwana bunge letu la jamhuri ya muungano ili katika kipindi hiki cha bunge la 10, waweze kujadiri mambo ya msingi kwa ajili ya maslahi ya nchi, badala ya kuanza kuongelea mambo ya kushabikia vyama kwani sisi wananchi ambao hatuna nafasi ya kuingia bungeni tumetuma wawakilishi wakatuwakilishe mambo yetu ya msingi, baadala ya kuzungumzia hayo wameanza kujadili mambo yasiyokuwa natija kwetu. wabunge wetu waweze kuwa na hofu ya mungu kuangalia ni nini kinatakiwa kipatiwe ufumbuzi na kama kuna kiongozi amekiuka apewe mwongozo na kama amekiuka sheria akubari kosa tofauti na sasa mwenye nacho hata kama amekiuka sheria hakuna wa kumsema. tuombee nchi watu wawe na hofu ya mungu. Naomba kutoa hoja na mungu awabariki

 608. wapendwa katika kristu,
  hitaji langu la kupata mke bado halijajibiwa na bwana
  naomba mniombee niweze kupata mke mcha Mungu, niweze kuishi naye ktk maisha yetu yote…
  mbarikiwe sana

 609. libarikiwe jina la bwana, Ndilo jina pekee liwezalo yote.wapendwa naomba mniombee ili niweze kushinda mitihani yangu. pia ntakapo malizam chuo mwezi wa tatu/2011 nipate kazi, ili niweze kumsaidia mama yangu, na familia yangu kwa ujumla.mungu awalinde na kutimiza ahadi zake.asante mungu kwa kunifikisha hapa nilipo.

 610. shaloom wapendwa.
  naomba tushirikiane mniombee kwa ajili ya hitaji langu la kupata chuo mwaka huu.lakini pia nifanikiwe kupata kiasi cha milioni mbili ambazo natakiwa kuzikabidhi kwa mwenye kiwanja ambacho nimepata. najua mali na vyote ni mali ya Bwana na mkiniombea nitapewa ili kiwanja kisiuzwe… Mungu awabariki mno

 611. Bwana Yesu asifiwe,ndugu John Paul nashukuru kwa kunitia moyo pia na ufafanuzi wa neno na kushiriki ktk kuniombea,namshukuru sana Mungu maana ameanza kujibu maombi yangu,naomba mzidi kuniombea,

 612. Bwana Yesu asifiwe naomba jamani mniombee niokoke? nimeanguka, kiroho na kimwili.
  MUNGU AWABARIKI SANA

 613. wapendwa katika Kristu,tumsifu Yesu Kristu,naomba mniombee ili niweze kupata ajira,ni mhitimu lakin kazi zimekuwa ngumu kupata,zinakatisha tamaa,watu wanasema mpaka ujuane na watu,lakin naimani Yesu anaweza kunipatia kazi nzuri bila kutoa rushwa.amen mbarikiwe

 614. Bwana Yesu asifiwe!Wapendwa naomba mniombee niweze kupata mume aliye mwema, nimekua nikisali kwa ajili ya hili lakini bado sijapata jibu,naomba pia mnipe mistari ya kusimamia ili niweze kufanikiwa.
  Mungu wetu ni mwaminifu na ninaamini kua atatenda sawa sawa na mapenzi yake. Kwa sasa nina umri wa miaka 28.
  Mungu wetu awabariki.

 615. Grace wala usipate shida sana dada yangu,maombi uliyoomba mwenyewe yanatosha.
  Mume wala mke hapatikani kwenye maombi ki hivyo. Cha kufanya wewe kaa mkao wa mtu aliyetayari kuolewa. Pia weka picha yako kwenye huu mtandao kisha utatupa ushuhuda siku si nyingi..
  Thanks.

 616. Tumsifu Yesu Kristu!
  Nadhan si vibaya kutoa maoni yangu hapa
  jamani mm nadhan nna shida sawa na grace , na pia nadhan Grace naye anawazo kama la kwangu ila anashindwa kulitoa kutokana na NATURE yetu binadamu
  mm niko serious natafta mke so kama tunaweza wasiliana itakua si mbaya email adress yangu ni veransebon@yahoo.com
  Ahsante Yesu najua utatenda muujiza nipate mke mwema
  Ameeeen!

 617. Shalom!
  Asante sana kaka Steve kwa mawazo na mchango wako,actually nilisahau kua specific katika email yangu,niko na urafiki na kaka mmoja kwa miezi 5 sasa,ni urafiki wa kawaida kabisa,huyu kaka wakati ananifuata alisema ya kwamba yuko serious anataka kuoa,Kwa muda huo mfupi tuliofahamiana nami nimetokea kumpenda.

  Sasa mimi ninachohitaji ni udhihirisho kama kweli huyu ndie yeye,katika vigezo ambavyo ninahitaji mume wangu awe navyo vingi anavyo, bado naendelea kufunga na kusali kwa ajili ya hili.

  Bado nahitaji nanyi watumishi wa Mungu mnisaidie katika kuomba ili nipate udhihirisho.Pia kama kuna mistari ya kusimamia juu ya udhihirisho naomba. Am very sorry for not being specific in first place.

  Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu:-Wafilipi 4:13

  Barikiwa.

 618. Bwana Asifiwe Wapendwa! Napenda kuwashirikisha,naomba tushirikiane kwenye maombi ,mniombee niko kwenye kipindi kigumu sana cha mapito!,khs kazi,mke,na yote kadri ya mapenzi ya BABA .Naomba kuwashirikisha mniombee ili Mungu atende kadri ya Mapenzi yake.

  Vilevile naomba mniombee nizidi kusimama kwenye imani maaana majaribu ni mengi sana,
  JINA LA BWANA LIHIDIMIWE

 619. Bwana Yesu asifiwe dada Grace! nimefurahi kuona jinsi ambavyo unaendelea kuomba kwa ajili ya mume unayemtaka. labda nikukumbushe kitu kimoja; katika maombi kuna pande mbili; 1. upande wa mwombaji(kuomba tu) 2. upande wa kupokea(receiving side) tatizo letu haliko upande wa kwanza; tunaweza kufunga mpaka kupata na vidonda vya tumbo! tunaweza kukesha katika maombi kwa ajili ya mahitaji yetu! kwa upande wa maombi hamna shida kabisa! tatizo liko katika upande wa kupokea kile tulichoomba! sasa hivi wewe tayari umeshaomba….tatizo lako ni KUPOKEA kile kile ambacho Mungu umemuomba! ili upokee kile kile ulichoomba ni lazima uwe na IMANI! EBR 11:6! Mfano wa imani ni sawa na jinsi unavyoamini kwamba kesho utaamka mzima na mwenye afya njema! yes, najua unamtegemea Mungu lakini pia unaamini kwamba utakuwa hai kesho! hata imani iko hivyo! amini kile ulichoomba kwamba ni cha kwako! sisi watu wa nuruni hatuendi kwa kuona bali kwa imani1 tukitarajia kisichoonekana kana kwamba kimeonekana! hivyo angalia imani yako! je KRISTO ameweka amani moyoni mwako kwa ajili ya huyo kijana? au ni kwa sababu ya mawazo yako tu? haya ni maswali ya kawaida kabisa! usijaribu kupunguza sifa ulizojiwekea wakati wa maombi kama hana hata sifa moja huyo sio wako! ninao mfano wangu mwenyewe1 mimi ni mtumishi wa Mungu, ninachunga kanisa, bado niko single(sijaoa), nimeweka sifa za mke nitakayemuoa awe ameokoka na anayeongozwa na Roho Mtakatifu tu! sifa zingine ndogo ndogo hazina maana! nimemwomba Mungu juu ya jambo hili, kwa hiyo nasubiri jibu la BABA tu1 lakini naamini kwamba mke wangu yupo! sijamwona kwa macho ya nyama lakini kwa IMANI ninamwona! kwa hiyo IMANI kwanza ni muhimu sana! Mungu akutie nguvu dada.

 620. Bwana Yesu asifiwe kaka Seni!
  Nashukuru sana kwa mchango wako na kunitia moyo,ninaamini kabisa Mungu anakwenda kujidhihiridha kwangu, Mungu amenipigania katika mambo mengi sana hataweza kuniacha katika hili.
  Pengine naomba unipe ushauri, nifanye nini ili niweze kusikia sauti ndani yangu ikiongea nami? Na nitaijuje?
  Hua natamani sana kusikia sauti ndani yangu.

  Tuendelee kuombeana.

 621. Bwana Yesu asifiwe, nawashukuru na kuniweka katika maombi mwaka jana nilipotuma maombi ya kuombewa mitihani yangu, namshukuru Mungu nilifaulu, naomba mnikumbuka katika maombi, nitakuwa na mitihani mingine kuanzine jumatano ya wiki hii, naamini Mungu atanifanya kicha na si mkia kwa jina la Yesu.

 622. Shaloom, Naomba mniombee Mungu anipe MUME MWEMA mwema aliyeokoka. nina miaka 26 sasa. Mungu ni mwaminifu naamini kwa uweza wake atatengeneze Njia.

 623. Bwana Yesu asifiwe,
  Ninaomba mnisaidie maombi kwani kuna jamaa namdai hela mpaka hivi sasa hajanirudishia na kwa muda huu nipo mbali naye(masomoni).Nimejaribu kutumia mtu aliye huko nyumbani ili afuatilie lakini mpaka sasa cja pata hata centi.E-mail yangu ni sephas2010@yahoo.com and phone no.0756797229

 624. Nawapongeza hasa kwa kazi ya Mungu mnayoifanya.
  Ushauri wangu niwaombe mtengeneze hata vipeperushi
  ili hata na wale ambao wako mitaani na hawana uwezo wa kutembelea mtandao wakaelimike kuptia njia hiyo.

  Mungu awabariki.

 625. Naomba mniombee nipate mtoto. Nimekuwa katika ndoa kwa muda wa miaka mitatu na sijafanikiwa.

 626. je remercie Dieu de notre seigneur Jésus Christ pour m’avoir orienté à tomber sur votre cite et je vous encourage pour le travail combien louable que vous êtes entrain de faire. je vous prie de prier pour moi afon que le travail que je fais m’apporte la paix et me permette d’avoir le temps de prier le Vrai Dieu

 627. Bwana YESU Asifiwe watumishi wa Mungu, naomba mnioombee nipate mwenza wa maisha nimehangaika sana na umri nao unaenda na pia ninatamani sana kuwa na mwenza wa maisha nimesemwa sana na ndugu na jamaa maana nina miaka 31 sasa wameshaanza niita bibi kwa sababu sijaolewa wala kuzaa, kweli ninateseka na kuumia sana moyoni, nafunga na kusali Mungu asikie kilio changu

 628. Bwana yesu asifiwe wapendwa naomba mniombee niko kwenye vifungo yaani kila nikipata mchumba tukikaa kidogo uchumba unakufa nilipoulizia historia ya maisha yangu ndo wakaniambia eti ni kwenye familia yetu ndo kuna vikwazo eti kuna mizimu ndo inanikataza nisiolewe naomba mniombee sana maana niliuliza watumishi wa Mungu kuhusu kuomba nikasema nikiomba mwenyewe siwezi kujifungua kwenye vifungo? wakasema na kushirikisha wengine ni vzr naomba jamani niko kwenye wakati mgumu nikiangalia wadogo zangu wote wameolewa but mimi bado roho inaniuma mpaka nikilala kitandani nakaa najiuliza peke yangu kwamba kweli ipo siku na mimi nitalala na mwenzangu jamani naomba Mungu anisaidie kwa hilo yaani nateseka mpaka nalia kwa wakati mwingine kuzaliwa katika familia hiyo but wakati mwingine namshukuru Mungu nasema labda ana makusudi na mm

 629. Bwana yesu apewe sifa,Naomaba muiombee kazi yangu ipo wakati mgumu sana,na Mungu wambinguni awabariki sana.

 630. Shaloom!!
  Najua hata baba yetu Ibrahim aliomba apate mtoto lkn alipata akiwa mzee,Basi kwa Imani moja,nia moja,Hata mimi naomba mke kwa kwa mrefu sasa lakini bado sijapata.Na mambo mengine niliomba nimepata lkn mke bado kitendawili hadi huvi sasa,Wapendwa mniombee nipate mke.Email kwa ushauri leonsaron@yahoo.com

 631. Shalom shalom!
  Ndugu ktk Bwana, naomba mnisaidie kuomba nipate mume mwema kutoka kwa Mungu.Naamini kama hakuna kitu chenye hakiwezekani kwa Baba yetu. Asante sana na mbarikiwe.
  Uwineza

 632. shalom shalom;
  wapendwa ktk Bwana,namshukuru Mungu kwa maombi yenu. Bwana amejibu maombiamefungua milango nimepata kazi, hakuna lisilo wezekana kwa Yesu.

 633. shaloom wapendwa.
  naomba mshirikiana nami kuomba. Mume wangu alipata kazikatika institution moja na kwa hivo alitakiwa apate nyumba pia. ila kutokana na urasimu ulioko hapo huchukua muda na wakati mwengine rushwa huombwa. mimi naamini MUNGU ndie mwenye mali na hata wakiweka ugumu sana atakalo hutendeka. naomba mniombee ili watawala waipokee ile barua na kutupa nyumba maana kweeeeli kabisa ninapata shida kwenye eneo niliko.
  Mungu awabariki.

 634. Bwana asifiwe wapendwa. namshukuru Mungu kuipata hii website, ni bahati ilioje. naombeni mniombee jamani, mabo kwa upande wangu ni magumu,imefikia mahali naona mbele ni giza,sioni kama ninaweza kupita.

 635. BWANA YESU ASIFIWE,naomba wapendwa mniombee nipate mume mwema kwani nimeomba na kufunga sajafanikiwa na watu wamekuwa wakinisema sanana umri unazidi kwenda nina miaka 31 sasa. kwa MUNGU yote yanawezekana naomba maombi yenu