“Aliyeko Juu Mngoje Chini!”

wp-1478176412108.jpg

“Aliyeko juu mngoje chini”?  Hii ni methali ya kipepo kabisa. Ambaye anaitendea kazi mithali hii ataendelea kubaki chini akiwasubiria walioko juu kiuchumi, walioko juu kielimu, walioko juu kiroho, walioko juu kiufahamu, washuke chini. Na wasiposhuka chini atafanya kila njia awashushe ikibidi kuwaendea kwa waganga wa kienyeji na wengine wanakwenda mbali zaidi kwa kufunga na kuomba ili hao walio juu yake washuke chini. Badala ya kujifunza kutoka kwao mbinu zilizowazesha wao kufika juu ili ajue wamefikaje hapo walipo; yeye anatafuta mbinu za kumsaidia awashushe chini !!

 

Watu wa jinsi hii ndio wale ambao hufurahia wakiona jirani yake kafukuzwa kazi utasikia: “HALO HALOO… WALIKUWA WANAJIDAI KULA WALI NYAMA, SIJUI WALI MAINI, SIJUI MARA LEO KITIMOTO, TUWAONE SASA KAMA WATATULINGISHIA TENA HIVYO VYAKULA VYAO”.

YAANI WENZAO KULA VYAKULA VINONO WANAONA WANALINGISHIWA !!

 

Watu wa jinsi hii ndio wale ambao wakiona mfanyakazi mwenzake kapandishwa cheo wanamwendea kwa mganga wa kienyeji. Ni watu wasiopenda kuona wengine wanafanikiwa. BAHATI MBAYA ZAIDI WAPO WACHUNGAJI, MITUME, MANABII, NA WALIMU WA JINSI HII; AMBAO WAKIONA MWENZAO ANA KANISA KUBWA, MUNGU KAMFANIKISHA KIUCHUMI UTASIKIA OOOOH FREEMASON !! Yaani kila aliyefanikwa Freemason !! HIZI NI AKILI ZILIZOJAA FUNGUS KABISA AISEE !!

 

SIKIA USIWAOGOPE WATU WA JINSI HIYO, MUNGU NDIYE ALIYEKUWEKA JUU; WATASUBIRI SANA HADI YESU ARUDI. WATAENDA CHOLE WATARUDI, WATAKUKUTA BADO UKO JUU, WATAENDA UYOLE WATARUDI WATAKUTA UMEENDA JUU ZAIDI, WATAENDA NYANSHANA WATARUDI WATAKUTA UMEYAPITA MAWINGU KWA KWENDA JUU ZAIDI. WATAKUROGA NDIO, LAKINI HAUTAROGEKA, KWANI UKO NDANI YA YESU. WAMROGE KWANZA YESU NDIO WATAKUROGA  NA WEWE !! MAANA MAANDIKO YANASEMA; “HAKIKA HAPANA UCHAWI JUU YA YAKOBO, WALA HAPANA UGANGA JUU YA ISRAELI” (Hesabu 23:23). WATANGOJA SANA LAKINI HAWATAKUONA UKISHUKA ! Ni shauku yangu niweze kusema na japo mtu mmoja hapa. Haleluyah!!

 

AS LONG AS GOD IS WITH YOU EVEN THE SKY IS NOT THE LIMIT!!. FLAP YOUR WINGS LIKE AN EAGLE  AND LET THE STORMS TAKE YOU TO THE HIGHEST ALTITUDE !!

 

28 Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, Bwana, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki.

29 Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo.

30 Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka;

31 bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia. (IsaYA 40:28-31).

 

MUNGU WANGU AKUBARIKI !!

 

Mwalimu na Mchungaji Gibson Gondwe.

Ukishindwa, Ongeza Uwezo!


Nakumbuka ilikuwa ni tar 29/9 mwaka huu, nilipoamka asubuhi, nikiwa ninawaza juu ya baadhi ya mambo ambayo niliyafanya lakini nikashindwa. Nikawa najiuliza ni kwanini nilishindwa ? Je ni kwa vile yale mambo hayawezekani ? Nikasikia sauti ndani yangu inaniambia sio kwamba hayawezekani, kuwezakana yanawezekana ila uwezo wako ni mdogo. Unachotakiwa kufanya ni kuongeza uwezo sawa na neno la Mungu linavyosema “Mtu mwenye hekima ana nguvu; Naam, mtu wa maarifa huongeza uwezo”. (Mithali 24:5) 
Ile sauti ikaendelea kunifundisha, ikaniambia kuwa kulikuwa na watoto wa 3 wa mfalme ambao walikuwa ni mapacha, na mfalme alikuwa anataka mmoja kati ya hao watoto wa 3 arithi kiti chake cha ufalme. Akawapa mtihani wa kubeba mzigo uliokuwa na kilo 300 na kuuweka juu ya ukuta ambao ulikuwa na urefu wa futi 4 kutoka ardhini. Na aliwapa muda wa mwaka mmoja na nusu wawe wamekamilisha hilo zoezi. 
Wale watoto wote walikuwa na urefu wa futi 6 kila mmoja na uzito unaolingana. Mtoto wa kwanza alipoungalia ule mzigo na kugundua kuwa unauzito wa kilo 300, alikata tamaa mapema na kusema kuwa hawezi kuubeba. Akaja wa pili, akajaribu kuunyanyua lakini akashindwa, akajaribu tena akashindwa, akajaribu hadi mara 5 lakini akashindwa kuunyanyua. Akajisemea moyoni huu mzigo ni mzito sana hauwezi kubebeka, hakuna mtu kati yetu anayeweza kuunyanyua. Akaamua kuuacha. Akaja mtoto wa tatu, yeye alijaribu kuunyanyua mara moja tuu, aliposhindwa akaamua kuuacha. Akaanza kuwaza nifanyeje ili huu mzigo niweze kuunyanyua. Akaamua kutafuta majarida yanayoelezea wanyua vitu vizito, kujua ni jinsi gani wanaweza kunyanyua vitu vizito. Katika utafiti wake na kusoma kwake akagundua kuwa wale watu wanaobeba vitu vizito hawakuzaliwa wakiwa na uwezo huo, bali huwa wanafanya mazoezi ya kubeba vitu vizito ili kuifanya misuli yao iwe na nguvu ya kubeba vitu vizito. Alipogundua hilo akasijisemea moyoni kwa kuwa baba ametupa mwaka mmoja na nusu nitaanza kufanya mazoezi ya kubeba vitu vizito. Najua baada ya mwaka mmoja nitakuwa nimeijenga misuli yangu vizuri kuwa na uwezo wa kubeba huu mzigo.
Yule kijana akaanza kufanya mazoezi ya kubeba vitu vizito kila siku jioni baada ya muda wa kazi. Wakati anafanya hayo mazoezi kila baada ya muda wa kazi jioni, wale wenzake wawili walikuwa wanamcheka na kumuona kama mjinga. Wao muda wa jioni baada ya kazi walikuwa wanautumia kustarehe na wanawake. Walishasahau habari ya kubeba ule mzigo wakijua kuwa hakuna hata mmoja kati yao mwenye uwezo wa kuubeba ule mzigo. Na kwa vile hakuna anayeweza, baba ataamua mwenyewe wa kumrithisha kiti chake cha kifalme. 
Yule kijana baada ya kufanya yale mazoezi kwa muda wa mwaka mmoja, mwili wake ulikuwa umejengeka vyema, misuli yake ilikuwa ni mikubwa. Akamfuata baba yake akamwambia nataka nifanye ile kazi uliyotupa ya kubeba ule mzigo wa kilo 300 na kuuweka juu ya ukuta. Basi basi baba yake pamoja na wasaidizi wake wakatoka kwenda kuangalia kama yule kijana ataweza kuubeba ule mzigo. Yule kijana akausogelea ule mzigo, akaunyanyua juu na kuuweka juu ya ukuta. Wenzake na wale watu waliokusanyika kuangalia lile tukio walishangaa sana!! Wakasema imekuwaje huyu aliyeshindwa kuubeba huu mzigo mwaka jana, leo hii ameweza; tena kirahisi tuu!! Baba yake alipoona kuwa ameweza kuubeba ule mzigo na kuuweka juu ya ukuta alifurahi sana. Akamrithisha yule mtoto kiti cha ufalme. Akawaambia watoto wake niliwapa hii kazi nikijua ya kuwa kwa wakati ule mlikuwa hamna uwezo wa kuifanya lakini nilijua kuwa ndani yenu mna uwezo wa kuifanya kazi ile. Mlichotakiwa kufanya ni KUONGEZA UWEZO WENU, na huyu mdogo wenu aligundua hili; ameongeza uwezo kwa kufanya mazoezi ya kunyanyua vitu vizito; na ndio maana ingawa mwanzoni alishindwa kunyanyua ule mzigo lakini sasa ameweza.
NI NINI NINACHOTAKA UJIFUNZE KWENYE HUU MFANO.
Ni kwamba katika maisha tunayoishi watu wengi sana wameacha kufanya vitu ambavyo walipenda kuvifanya na vingewapa faida baada ya kushindwa mara kadhaa. Kushindwa kwao kufanya yale waliyotaka kuyafanya kuliwafanya waamini kuwa hawana uwezo wa kufanya yale waliyotaka kufanya; na wengine kuamini kuwa yale waliyotaka kufanya hayawezekani. Lakini ukweli ni kwamba wameshindwa kufanya sio kwa sababu hawawezi kufanya, ila ni kwa sababu uwezo wao wa kufanya lile jambo kwa wakati ule, ulikuwa ni mdogo. Walichotakiwa kufanya ni kuongeza uwezo kama yule kijana alivyoongeza uwezo kwa kufanya mazoezi ya kunyanyua vitu vizito. Na pia wameshindwa kufanya sio kwa sababu lile jambo walilotaka kufanya haliwezekani, ila ni kwa sababu wao ndio walikuwa hawana uwezo wa kulifanya lile jambo.
Sikia; kuwezekana kwa jambo au kutokuwezakana kwa jambo lolote lile, hakuko kwenye lile jambo, bali katika uwezo wa yule anayetaka kulifanya lile jambo. Ukimpa mtoto wa miaka 5 abebe ndoo ya maji ya lita 20 hataweza kuibeba ile ndoo. Hataweza kuibeba sio kwa sababu ile ndoo haibebeki, ila ni kwa sababu uwezo wake ni mdogo. Kwa hiyo hatuwezi kusema hiyo ndoo haibebeki eti kwa sababu yule mtoto ameshindwa kuibeba. Lakini ndoo hiyo hiyo ukimpa kijana wa miaka 18 ataweza kuibeba. Hii inamaanisha kuwa kubebeka kwa hiyo ndoo au kutokubebeka kwake hakuko kwenye hiyo ndoo, bali katika uwezo wa yule anayetaka kuibeba. Tunaliona hili swala la kuwezekana au kutokuwezekana kwa jambo hata kwa Yesu na wanafunzi wake. Neno linasema:

“14 Nao walipoufikia mkutano, mtu mmoja akamjia, akampigia magoti, akisema, 15 Bwana, umrehemu mwanangu, kwa kuwa ana kifafa, na kuteswa vibaya; maana mara nyingi huanguka motoni, na mara nyingi majini. 16 Nikamleta kwa wanafunzi wako, wasiweze kumponya. 17 Yesu akajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, kilichopotoka, nitakaa pamoja nanyi hata lini? Nitachukuliana nanyi hata lini? Mleteni huku kwangu. 18 Yesu akamkemea pepo, naye akamtoka; yule kijana akapona tangu saa ile. 19 Kisha wale wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha wakasema Mbona sisi hatukuweza kumtoa? 20 Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu. 21 [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.] (Mathayo 17:14-21). 

Wanafunzi wa Yesu walishindwa kutoa pepo. Tusingeweza kusema kuwa pepo lile haliwezi kutoka, eti kwa sababu wanafunzi wale wameshindwa kumtoa. Walishindwa kumtoa si kwa sababu ilikuwa haiwezekani kumtoa yule pepo, ila ni kwa sababu wale wanafunzi walikuwa hawana uwezo wa kumtoa kwa wakati ule. Pepo yule yule ambaye wanafunzi wa Yesu walishindwa kumtoa, pepo huyo huyo Yesu alimtoa. 
Baada ya kushindwa kumtoa yule pepo wanafunzi wa Yesu walimuuliza Yesu; ni kwanini sisi tumeshindwa kumtoa ? Yesu akawajibu ni kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Akawaambia namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga. Kwa maana nyingine alikuwa anawaambia kuwa wanatakiwa waongeze uwezo kwa kusali na kufunga ili waweze kutoa aina ile ya pepo. 
Wanafunzi wa Yesu baada ya kugundua ile siri ya kuwa wanatakiwa kuongeza uwezo waliitendea kazi, na tunaposoma maandiko hatuoni mahali popote tena ambapo wanafunzi wale wakishindwa kutoa tena pepo; ila tunaona wakifanya miujiza mikubwa zaidi ya kutoa pepo. Walifikia hatua ya kufufua maiti. Maandiko yanasema,

“Na mwanafunzi mmoja alikuwako Yafa, jina lake Tabitha, tafsiri yake ni Dorkasi (yaani paa); mwanamke huyu alikuwa amejaa matendo mema na sadaka alizozitoa. 37 Ikawa siku zile akaugua, akafa; hata walipokwisha kumwosha, wakamweka orofani. 38 Na kwa kuwa mji wa Lida ulikuwa karibu na Yafa, nao wanafunzi wamesikia ya kwamba Petro yuko huko, wakatuma watu wawili kwake, kumsihi na kusema, Usikawie kuja kwetu. 39 Petro akaondoka akafuatana nao. Alipofika, wakampeleka juu orofani wajane wote wakasimama karibu naye, wakilia na kumwonyesha zile kanzu na nguo alizozishona Dorkasi wakati ule alipokuwa pamoja nao. 40 Petro akawatoa nje wote, akapiga magoti, akaomba, kisha akaelekea yule maiti, akanena, Tabitha, ondoka. Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua, akaketi. 41 Akampa mkono, akamwinua; hata akiisha kuwaita wale watakatifu na wajane akamweka mbele yao, hali yu hai.” (Matendo 9:36-40).

Kama ambavyo wanafunzi wa Yesu walitakiwa kuongeza uwezo kwa kusali na kufunga ili waweze kutoa aina ile ya pepo; vivyo hivyo na wewe unatakiwa uongeze uwezo ili uweze kufanya yale ambayo yalikushinda huko nyuma. Yalikushinda si kwa sababu hauwezi ila ni kwa sababu uwezo wako ulikuwa mdogo.

Inawezekana wewe ni tabibu(daktari) na umewahi kufanya operesheni kadhaa huko nyuma, na mafanikio ni madogo, umekata tamaa na kujiona kuwa hauko competence, nataka kukuambia kwamba you’re very competence; unachotakiwa kufanya ni kuongeza uwezo kwa kusoma medical journals na kujifunza kwa waliokutangulia waliofanikiwa kwenye field yako. Neurosurgeon Benjamin Carson maarufu kama Ben Carson, ndiye daktari wa kwanza kuwafanyia upasuaji watoto mapacha waliungana vichwa na operation hiyo ikafanikiwa. Kilichomfanya Ben Carson afanikiwe ni kuongeza uwezo kwa kusoma medical journals na kutaka kujua kilichowafanya madaktari wa mwanzo washindwe kuwatenganisha watoto walioungana vichwa ni nini. Alifanikiwa kungundua kuwa kilichokuwa kinasababisha watoto wafe ni kwa sababu ya upoteaji mwingi wa damu wakati wa upasuaji. Alipogundua hilo aliongeza uwezo kwa kujifunza kutoka kwa daktari wa moyo ni jinsi gani ambavyo anaweza kuzuia upoteaji mwingi wa damu wakati wa upasuaji. Matokeo yake ni kuwa alifanikiwa kuwatenganisha wale watoto waliokuwa wameungana vichwa.
Kama wewe ni mwanafunzi na kuna hesabu zimekuwa zikikushinda, usidhani ya kwamba hauwezi hizo hesabu, unachotakiwa ni kuongeza uwezo kwa kufanya mazoezi mengi zaidi kuhusiana na hiyo topic. Si unakumbuka kuhusu kukariri table, mwanzoni ulihisi kama hautaweza kukariri table zote kuanzia ya 1 hadi ya 12; lakini ulipoongeza uwezo kwa kuongeza bidii ya kujifunza hizo table, leo hii ziko kichwani. Hata ukiamshwa usingizini unazitaja bila kigugumizi. 
Kama wewe ni mkulima; ongeza uwezo kwa kujifunza njia za kisasa za ukulima ili uweze kuongeza kipato chako. Tembelea mashamba ya wakulima wengine ambao wako juu yako kiutaalamu na kujifunza kutoka kwao. 
Kama wewe ni mwalimu, ongeza uwezo kwa kusoma sana vitabu mbalimbali vya masomo unayofundisha. Kwa wale ambao A level wamesoma chemistry shule za Dar, au ambao walikuwa wanasoma tuition Dar, miaka ya 2000 kurudi nyuma, naamini jina la Mwalimu Mkandawile, na Mama Shija sio mageni kwao. Hawa ni moja kati ya walimu the best katika somo la chemistry kwa wakati ule. Ni kwanini walikuwa the best ? Ni kwa sababu waliongeza uwezo.
Kama wewe ni mpishi, ongeza uwezo kwa kujifunza aina tofauti tofauti za mapishi. Kama ulikuwa hujui kutengeneza Italian pizza, tafuta mpishi mwenzako mwenye ujuzi huo.

Kama wewe ni mjasiriamali ongeza uwezo kwa kujifunza kutoka kwa waliokutangulia na kusoma majarida yanayohusiana na aina ya bidhaa unazozalisha .
KWA VILE KIMEKUSHINDA, HAIMANISHI KUWA HAUWEZI !! INAMANISHA KUWA UWEZO WAKO NI MDOGO. HIVYO ONGEZA UWEZO KWA KUJIFUNZA ZAIDI NA HATIMAYE UTAWEZA.  
Mungu wangu akubariki.
Mwalimu na Mchungaji Gibson Gondwe.

KABLA HUJAMWOMBA MUNGU AKUPE KIATU, MSHUKURU KWANZA KWA KUKUPA MGUU WA KUVALIA HICHO KIATU.

wp-1469994595672.jpg

Kuna baadhi ya maombi hauwezi kumwomba Mungu kama huna kitu fulani. Kwani kuna baadhi ya vitu ukiwa navyo ndivyo vinavyokuwezesha kuomba maombi hayo unayaomba. Kwani bila hicho kingine kuwepo, hata ukipata hicho unachoomba hauwezi kukitumia.

Inawezekana umemwomba Mungu akupe kiatu cha kuvaa lakini hadi leo hajakupa, lakini mshukuru Mungu kwa kukupa mguu wa kuvalia kiatu, kwani kama usingekuwa na huo mguu hilo ombi la kiatu lisingekuwepo. Kwani wapo watu wenye uwezo wa kununua viatu, lakini hawana miguu ya kuvalia viatu. Inawezekana unamwomba Mungu akumpe mtoto; lakini mshukuru kwanza Mungu kwa kukupa mume; au mke. Kwani ombi hilo la mtoto lisingekuwepo kwako kama usingekuwa na mume au mke. Kwani wapo wenye uwezo wa kutunga mimba na kutungisha mwanamke mimba lakini hawana waume au wake. Inawezekana uko kazini muda mrefu na haujapandishwa cheo; na umekuwa ukimwomba Mungu upandishwe cheo kazini kwako, lakini mshukuru Mungu kwa kazi uliyonayo. Kwani ombi la kupandishwa cheo lisingekuwepo kama Mungu asingekupa kazi. Inawezekana umemwomba Mungu akupe saa ya mkononi lakini hadi sasa hajakupa; badala ya kumlalamikia kwanini hajakupa saa mshukuru kwa kukupa mkono wa kuvalia saa, kwa sababu kama usingekuwa na huo mkono ombi la saa lisingekuwepo.

Ni kweli tunapitia changamoto, lakini wapo wenye changamoto kubwa zaidi yetu. Ukiona huna sababu ya kumshukuru Mungu, nenda hospitali ya rufaa iliyopo mkoa uliopo halafu zungukia wodi za majeruhi wa ajali, wodi za wagonjwa wa kansa, na wodi za wagojwa wa T.B utapata sababu ya kumshukuru Mungu.

Katika yote tunayopitia kama binadamu bado tunasababu lukuki za kumshuru Mungu. Mungu anajua changamoto unazopitia lakini anayo sababu nzuri ya kuiruhusu. Kwani chochote Mungu anachoruhusu kwenye maisha yetu huwa anasukumwa na upendo.

Maadamu bado tupo duniani, changamoto za maisha ni sehemu ya maisha yetu. Ndio maana Yesu akasema, “ULIMWENGUNI MNAYO DHIKI; LAKINI JIPENI MOYO; MIMI NIMEUSHINDA ULIMWENGU” (Yohana 16:33).  Ni mbinguni tuu ndio tutapumzika milele. Ninapomsoma mtume Paulo huwa ninatiwa moyo. Paulo alipitia changamoto nyingi sana lakini hakukata tamaa. Katika 1Wakorintho 11:16-33 anaelezea changamoto alizopitia wakati anahubiri injili. Anasema kuwa amepitia magumu mengi katika kuihubiri injili anasema “KATIKA TAABU KUZIDI SANA; KATIKA VIFUNGO KUZIDI SANA; KATIKA MAPIGO KUPITA KIASI. Anasema kwa Wahayudi mara tano alipata mapigo arobaini kasoro moja. Mara tatu alipigwa kwa bakora; mara moja alipigwa kwa mawe(hapa alipigwa kwa mawe hadi watu wakadhani amekufa. Lakini waliompiga mawe walipoondoka aliinuka na majeraha yake na kwenda kuhubiri injili sehemu nyingine. Soma Matendo ya Mitume 14:19-20 ). Halafu magumu haya yote aliyopitia Paulo anayaita kuwa ni dhiki nyepesi anasema “MAANA DHIKI YETU NYEPESI, ILIYO YA MUDA WA KITAMBO TU, YATUFANYIA UTUKUFU WA MILELE UZIDIO KUWA MWINGI SANA (2Wakorintho 4:17) Kuvunjikiwa mtumbwi baharini, anaita dhiki nyepesi, kupigwa bakora, anaita ni dhiki nyepesi, kupigwa kwa mawe hadi karibu ya kufa anaita ni dhiki nyepesi. Daaah this MOG (Man of God) was so amazing !!

Unajua kinachotofautisha kati ya washindi na walioshindwa, sio changamoto wanazopitia, bali kile wanachofanya wanapopitia changamoto. Paulo alipopigwa mawe hakumlalamikia Mungu, bali alimshukuru Mungu na kuendelea kupiga kazi ya Mungu,  kuna mwingine akianguka analala hapo hapo, kuna mwingine akianguka anakung’uta vumbi na kuendelea na safari. Kuna mwingine akipata hasara kwenye biashara anaamua kuacha biashara, kuna mwingine anatafuta mtaji tena na kuendelea na biashara. Kuna mwingine majibu ya maombi yanapochelewa anakimbilia kwa waganga wa kienyeji; kuna mwingine anasema nitang’ang’ana na Mungu kwenye maombi hadi kieleweke. Kuna mwingine anapopatwa na changamoto anamlilia na kumnung’ukia Mungu, kuna mwingine akipatwa na changamoto analia, akimaliza kulia anafuta machozi na kuingia kwenye maombi. FAILURE IS NOT FALLING DOWN BUT STAYING DOWN !! WHEN YOU FALL WAKE UP AND WALK AGAIN !!

Sikia nikuambie THE CHALLENGE YOU ARE  GOING THROUGH CAN STOP YOU TEMPORARILY; BUT YOU CAN STOP YOURSELF PERMANENTLY!! Changamoto unazopitia zinaweza kukuzuia kwa muda, ila wewe unaweza kujizuia mwenyewe daima !! Kilichowazuia wana wa Israel wasiingie Kanaani sio shetani wala sio changamoto walizopitia bali ni wao wenyewe !! Kufeli kidato cha nne sio kufeli maisha, usikate tamaa eti kwa sababu umefeli kidato cha nne, simama na uanze upya; kama mumeo amekutelekeza na amekuachia  watoto futa machozi na usonge mbele. Hauwezi jua hao watoto watakuja kiwa wakina nani baadae. Kamuulize mama yake Magufuli uone kama alijua kuwa mwanae atakuja kuwa Rais. Songa mbele no matter what !! Kuna mtu mmoja aliwahi kusema “KAMA HAUWEZI KWENDA MBELE KWA KUPAA BASI KIMBIA, KAMA HAUWEZI KUKIMBIA BASI TEMBEA, KAMA HAUWEZI KUTEMBEA BASI TAMBAA; FANYA KILA UWEZALO LILILO HALALI KUHAKIKISHA KUWA UNASONGA MBELE.

MAADAMU MUNGU YUKO UPANDE WAKO HAKUNA KITACHOKUSHINDA, SI SHETANI, SI MIZIMU YA KWENU, SI MALAIKA. Neno linasema Mungu akiwa upande wetu ni nani aliye juu yetu. Katika MAMBO YOTE TUNASHINDA NA ZAIDI YA KUSHINDA, KWA YEYE ALIYETUPENDA (Warumi 8:31,37).

NDIO MAANA NINASEMA; SISI NI ZAIDI YA WASHINDI !!

Mchungaji na Mwalimu Gibson Gondwe