“Nina tatizo na mpenzi wangu!”

 

Dear All,

Bwana Yesu Asifiwe,  Poleni kwa Huduma. Mie ni Mdada naitwa JJ, nimeokoka tangu 2004 nampenda Yesu,ila ninashinda yangu ambayo ninaomba niwashirikishe katika maombi yenu, mie ninatatizo na  mwenzi wangu ambaye tuliaidiana kuoana, ila mpaka sasa kila nikimwambia naona haeleweki na mie nampenda sana, ni nami kila siku namwomba Mungu huyo ndo awe mwenzi wangu. sasa ninaomba msaada wenu, make nimefunga na kuomba mara nyingi na kuwashirikisha wachungaji mbalimbali na wana maombi wengi, na huyu kaka ana onyesha interest kweli kuwa ananipenda lakini tatizo afanyi maamuzi yoyote yale,

Nawatakia huduma njema.

-J

Sitamani kuoa!!

mpweke

Bwana Yesu Asifiwe,
Kwanza namshukuru Mungu sana kwa kunijalia uhai na elimu hadi elimu ya juu na pia kunipa kazi. Naomba sana maombi yenu na ushauri kwani nina tatizo kubwa sana kwangu ambalo limenifanya nikate hata tamaa ya kuendelea kuishi. Nilipofikiria zaidi nikaona Mungu ana sababu ya mimi kuwa hai. Mimi ni kijana umri wa miaka 30! Sijawahi kufanya mapenzi au kuvutiwa na mwanamke yoyote maishani mwangu!!!

Ninapata msisimko wa mwili nikiwa mwenyewe tu ila nikiwa na msichana siwezi hata kuvutiwa kwa namna yoyote ya kutaka kufanya nae tendo la ndoa. Kwa uelewa wangu, nisipovutiwa na msichana na kusisimka hakuna maana ya kuwa na mchumba. Hivyo imenifanya nisitamani kuoa kabisa ila jamii itanionaje kama sitaoa kabisa? Najiuliza Married couples go old together!! As for me who will I go old with? Will I remain single forever?

Kuna wakati nikiwa na marafiki wakike, wanapoonyesha kunitaka kimapenzi huwa nawakimbia sana. Ukweli ni kuwa naogopa tendo la ndoa!! Wakati mwingine nikiona vijana wadogo zangu wakiwa wanaoa machozi yananitoka maana sijui mimi nitaanzia wapi ili niweze kuwa na mke. Sio tu mke niweze kumtimizia haja zake ikiwa ni pamoja na kufanya nae tendo la ndoa ambalo naamini ndilo la msingi zaidi kwenye ndoa. Kikristo kama waliooana hamkufanya tendo la ndoa maana yeke bado sio mke na mume, (marriage consummation)

Naomba sana niombewe niweze kujiona mwanaume halisi ili kukabiliana na ndoa au niweze kuishi maisha yenye amani moyoni kumtumikia Mungu maishani mwangu.

Ahsante sana na imani kuwa Mungu anasikia Maombi yetu ataniponya

–Brian

Kuna ugumba unasababishwa na majini mahaba – 1

pastor2

Biblia inatuambia:“Nami nimeona lililo na uchungu kupita mauti yaani,Mwanamke ambaye moyo wake ni mtego na tanzi na mikono yake ni kama vifungo; Yeye ampendezaye Mungu atamponyoka,bali mwenye dhambi atanaswa na yeyeMhubiri 7:26

Mpendwa mapepo dume na mapepo jike yapo na ni halisi. pepo mahaba dume kwa kiingereza linaitwa incubus. Pepo jike linaitwa sacubus. pepo dume linauwezo wa kulala na mwanamke kadhalika na pepo jike lina uwezo wa kulala na mwanaume katika ndoto. Mapepo mahaba yanatoka baharini au kwenye mito au kwenye maziwa.

wote ni watendakazi wa shetani asili yao kuzimu kuna wanaume ambao wameoa katika hali halisi na pia wameoa katika ulimwengu wa roho.hivyo kuna uwezekano wa mtu kuwa na mwanamke katika hali halisi na kuwa na mwanamke katika ulimwengu wa roho. Solomoni anasema “Nami nimeona lililo na uchungu kupita mauti,yaani mwanamke ambaye moyo wake ni mtego na tanzi,na mikono yake nikama vifungo; yeye ampendezaye Mungu atamponyoka,bali mwenye dhambi atanaswa na yeye” (Mhubiri 7:26).

Andiko hili linatuonyesha picha ya utendaji kazi wa mapepo mahaba. Na haya mapepo yapo katika jinsia zote.kwa hiyo ukipenda dhambi utanaswa na ukichagua kumpendeza Mungu utaponyoka. uamuzi ni wako kunaswa au kuponyoka (nimeshakupa maarifa). Mungu akusaidie uponyoke ndiyo sababu nimeleta kwako somo hili ili ujue dalili za mapepo mahaba na ufunguliwe kutoka katika kifungo cha ndoa za mapepo mahaba. Pepo mahaba ni pepo awezaye kumtawala mwanaume au mwanamke katika ulimwengu wa roho, pepo huyu mchafu ana madhara mengi sana mfano kuzuia kushika mimba au kuharibu mimba,au kuzuia kuoa au kuolewa (kuvunjika uchumba/ndoa) pepo mahaba hujidhihirisha katika ndoto,kwani mtu aliyenaswa na pepo mahaba huota ndoto akifanya ngono.

UTAJUAJE KAMA UNA VIFUNGO VYA KIPEPO MAHABA/JINI MAHABA?

Unaweza ukawa umeoa au hujaoa / umeolewa au hujaolewa katika hali halisi.Na wengi wanakuwa hawana watoto kwa sababu ya majini haya katika huduma niliyonayo nimepata kuwaombea wengi na wamepata watoto na kuwekwa huru

UNAJUAJE KWAMBA UNAHITAJI HUDUMA YA KUFUNGULIWA KUTOKA VIFUNGO VYA MAPEPO MAHABA?

Ilikujibu swali hili ngoja tuone dalili za mapepo mahaba katika maisha ya watu mbalimbali.Kwa ufahamu huu utajua kwamba unahitaji huduma ya kufunguliwa.

DALILI ZA MAPEPO MAHABA

1.Kuchoka katika ndoa – Kabla ya kuoa au kuolewa kila mtu alikuwa na shauku ya kufurahia ndoa.lakini baada ya muda mfupi wanandoa wamechokana na ndoa imekosa ladha.Wakati mwingine mwnandoa mmoja anamchoka mwenzi wake.Kama ungepewa nafasi ya kuamua kwaupya huenda usingekubali kuolewa na mwanaume huyo au kuoa mwanamke huyo. Mpendwa msomaji kama unajisikia kuchoka ndoa hiyoni dalili ya kuwepo kwa mapepo ya mahaba tafuta msaada wa huduma ya kufunguliwa

2.Kufanya tendo la ndoa au mapenzi kwenye ndoto na mtu unayemfahamu au usiyemfahamu.

3.Kuchukia kuoa au kuolewa (unajuta kama usingeolewa au usingeoa)

4.Kufanya maamuzi yasiyo sahihi wakati wa kuoa au kuolewa. Kuolewa au kuoa mtu asiye sahihi.

5.Kuachwa na mume au mke.Kila mwanamume akikuoa baada ya muda mfupi anakuacha.Ujue unamapepo mahaba yanayofukuza wanaume katika maisha yako.Unakuta mwanamke mzuri amesoma na ana (uwezo) kazinzuri lakini anaachwa na wanaume au anatelekezwa na wachumba hapo unahitaji huduma ya fufunguliwa.

6.Kuchukia mahusiano ya kindoa na mumeo au mkeo.Wakati usiku unatembelewa na mapepomahaba.

7.Kunyonyesha watoto kwenye ndoto wakati huna mume wala mchumba /au umeolewa na huna mtoto kabisa! Ni dalili ya kifungo cha pepo mahaba.

8.Kuogesha watoto kwenye ndoto wakati hujaolewa ni dalili mapepo mahaba.

9.Kuota una familia kwenye ndoto wakati hujaolewa / au kuoa na wala huna mchumba.

10.Kuota unafanya shopping na mwanaume au mwanamke wakati huna hata mchumba.

11.Kumchukia mwenzi wako kiasi cha kutamani afe ili uoe au uolewe na mtu mwingine.

12.Kuota wanawake au wanaume wako uchi,au wewe mwenyewe kujiota ukouchi.

13.Wanandoa kuota mwanaume au mwanamke yuko katikati yenu au pembenimwa kitanda chenu wakati mmelala.Kujikuta umeanguka kutoka kitandani na uko chini mara kwa mara

14.Mwanaume kukosa nguvu na kushindwa katika tendo la ndoa.

15.Mwanamke kupata maumivu makali sana wakati wa hedhi (maumivu makali ya tumbo)

16.Matatizo ya mfululizo ya magojwa ya kike mfano ya tumbo la uzazi,kuziba mirija ya uzazi.

17Kuota unabakwa ndotoni.Kuharibu mimba baada ya kuota unafanya tendo la ndoa.

18.Kujutia kuoa / kuolewa bila sababu ya msingi

19.Kukosa hamu / moyo wa kuambatana na mwezi wako.Hujisikii tena kuongea na mwenzi wako wa ndoa unapenda kucheka na wanawake / wanaume wengine kuliko mwenzi wako hizi nidalili za kifungo cha pepo mahaba tafuta msaada wa kufunguliwa haraka upone!.

20.Kila wakati kuwaza kwamba ndoa itavunjika unapotazama miaka miaka mitano ,kumi huoni kudumu kwa ndoa yako hata hapo ulipo unaonakama muujiza.

21.Kukosa utoshelevu wa moyo katika ndoa uliyonayo.

22.kama ni msichana huoni kijana yeyote aliyewahi kukusemesha kwamba atakuoa ujue mara nyingine hata wachawi wanaweza wakawa wamekufunga.

24.Kupewa ahadi za kuolewa bila kutimiwza / kama hakuna anayemaanisha unahitaji huduma ya kufunguliwa.

25.Kuachwa baada ya wanaume kuujua mwili wako au kuchukiwa baada ya mwanaume kulala na wewe.

26.Kucheza na nyoka ndotoni wala hung’ati hili si jambojema ni hatari.

27.kubakwa mara kwa mara katika hali halisi.

28Kumpa mimba msichana mwingine halafu unaoa mwanamke mwingine.

29.Mchumba kufariki kabla ya ndoa (kufa ghafla mipango ya harusi imeandaliwa)

30.Kuachiswa kazi au biashara kufa mara baada ya kuoa au kuolewa.

31.Kupata ajali mbaya baada tu ya kuoa au kuolewa.

32.Mwenzi wako hakubaliani na wewe katika jambo lolote mnalopanga (anakuwa mpinzani tu!)

33.Kila mwenzi anaye kuoa au unaye muoa anakufa

34.Kuwa na uamuzi wa kutoolewa au kuoa kwa kuogopa matatizo ya ndoa (hofu ya ndoa).

35.Mwenzi kutokukujali wakati unaumwa unajihudumia mwenyewe hadi unapona na yeye yupo hata ulalamike maumivu anaendelea na shughulizake bila kujali.

36.kupigwa mara kwa mara bila huruma na mume wako.

37.kutishiwa kufukuzwa mara kwa mara na mumewako. Au kutamani kurudi kwenu

38.Kupotelewa na pete ya ndoa au cheti cha ndoa ktk mazingira ya kutatanisha.

39.Kupewa pete za mapenzi na waganga wa kienyeji au wanajimu.Vua hiyo pete katika jina la yesu ni antena / agano la kuvutia mapepo katika maisha yako.

40.Kujuta kuolewa au kuoa mwenzi huyo.

41.Kupanga kwamba niki rudi nyumbani tu nitapokeana na mwenzi wangu kwa furaha ghafla unawasili unaingiwa na chuki moyoni juu yake.

42.Kuchelewa kurudi nyumbani bila sababu ya msingi (Baada ya ndoa mwenzi wako anabadili tabia ghafla).Sura yako kuonekana mzee kuliko umri wako.

43.Kutokwa damu sana au kwa muda mrefu wakati wa hedhi kukiambatana na maumivu makali (maranyingine siku zinakuwa za mvurugiko mvurugiko).

44.Unakuwa na roho ya liwalo na liwe hujali ndoa yako hata ukishauriwa hushauriki.

45.Kutokupata mimba katika ndoa yako hata vipimo vya kidaktari vikionyesha huna tatizo au kuharibika mimba mara kwa mara.

46.kutengana kwa wana ndoa hata ingawa mnakaa nyumba mmoja (mzungu wa nne) kila mtu ana chumba chake.

47.Tumbo lako kuonekana una mimba hata watu wana kuona hivyo wakati hauna.

48.Matiti kutoa maziwa wakati huna mimba wala mtoto.

49.Kujisikia mjeuri,hasira,ukaidi kutokuelewana katika ndoa.

50.Kuonywa na mtu katika ndoto kwamba hutaolewa.

51.udhihirisho wa wazi wa mapepo mahaba wakati wa usiku.

52.kukumbuka mahusiano ya mapenzi na rafiki zako wa zamani wakati una mkeo / mumeo kitandani.

53.Kujichua au kujiridhisha mwenyewe bila mwenzi usiku au bafuni.Na kuwaona wasichana wazuri kwa kila unayekutana nae yaani huwezi kumpita bila kuona mvuto kwake

Mpendwa msomaji hizi ni dalili kadhaa ktk nyingi kama unaona hapo iko sehemu inakugusa tafuta mahala penye huduma ya kufunguliwa upone, haya mapepo machafu yanaleta hata kukufanya uwe unaishiwa kila mara hata ungekuwa na pesa ya kutosha wewe mda mchache huna kitu, amani katika ndoa ni ndogo sana ni hekaheka tu!na kama kuoa au kuolewa kuna zuiwa na haya niliyo kupa mbinu jinasue kwa  jina la Yesu ! 

Tutaendelea sehemu ya pili….

Pastor Massawe

Maombi juu ya ndoa yangu!

ndoa

Shalom.

Mimi naitwa Caroline ni mama wa watoto wawili niko kwenye ndoa namshukuru Mungu kwa hizo baraka, nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa blog hii na maneno mazuri nabarikiwa sana jamani. Nahitaji mniweke kwenye maombi sana juu ya ndoa yangu na familia yangu kwa ujumla!

Asanteni na Mungu aendelee kuwabariki.

Caroline.

Masuala ya mahusiano sipati picha kamili!

Bwana Yesu asifiwe wapendwa.

Mimi ni mgeni kwenye blog hii ila naamini nimekutana nayo kwa makusudi muhimu.. kwenye pita pita nimekutana na maoni na shauri nyingi kutoka sehemu mbali mbali hivyo na mimi ningependa msaada toka kwenu..

Nina jambo ambalo kiufupi linanitatiza na bado sina majibu yake hivyo kwa michango yenu tofauti labda mwaweza nisaidia, kipindi cha nyuma naweza sema nilisumbuka sana katika maswala ya mahusiano yaani kila kijana alie nifuata alikua muisilamu au mkristo jina maana hata mlango wa kanisa haujui.

Nilimlilia Mungu juu ya hili akawa mwaminifu na kuniletea mtu.. kuna kaka nilimwona mara moja nikiwa na rafiki zangu kiukweli moyo ukagongana nae sikujua ni nani wala anaishu gani.. ikapita miezi miwili nakumbuka ndio siku nimetoka lia sana na Mungu kunipa kijana kwa imani, next day nakuta missed call hamuwezi amini sijui how ila ndani yangu nilihisi ni yule kijana nilomwona miezi miwili iliyopita.. basi akaomba tuonane nae akaonesha interest kwangu kiukweli tulikua na chemistry sijui niwaelezeje kama nilimjua maisha yangu yote.

Kabla sijajikita kwenye urafiki nilimwomba kwanza Mungu aniambie kama ni yeye au sie yeye.. katika ishara nilizo omba ZOTE zilitimia kama nilivyo omba Mungu.. Si mtu wa kanisani sana ila ana hofu ya Mungu na wazazi wake ni watumishi wa dhehebu fulani.. alionesha dalili zote za mtu anaetaka kuoa.. ila ni kama alikua anapatwa na wasiwasi leo anataka kesho ni mtu mwingine kabisa na baadae kesi za kujamiiana zikawa nyingi japokuwa alikua muelewa ukisha mtajia dhambi anatulia hasumbui… lakini nikachoka nikamwambia tuachane.

Ajabu wiki kabla sijamwacha niliota ndoto ya kwao wakiniambia niachane na mtoto wao kwani hawanitaki na mimi nikapatwa na kitu ghafla nikamwambia tuachane bila kujielewa na wala sikuomba juu ya ile ndoto..

Basi nikawa naumwa sana.. siku nikiomba na kikundi kanisani kuwa kama ni yeye tunampa siku kadhaa awasiliane na mimi kweli kabla ya zile siku kwisha akanitafuta kuwa ananijulia hali… nikiacha kuomba anapotea hanitafuti siku nyingine tena nikamwomba Mungu na kuna dada wa kanisani alidai ameona maono kua ni mume wangu ila anahitaji kuombewa sana maana kwao wana nguvu za giza.

Siku nyingine ndoto ikaja nasafisha nyumbani kwao na kupaweka safi, ndoto nyingine kua amekuja kanisani kujitambulisha.. basi kuachana kwetu kukawa miezi kadhaa anapotea baadae anaibuka hili ni jambo linalonisumbua sana. Na alisha jitambulisha kwa wazazi  wangu japo kwao hakunitambulisha.

Kila tulicho omba juu yake kinatookea ila yeye moyo wake bado mgumu, nakumbuka mwezi uliopita nilimtafuta na kumwambia achague either awe nami au aache kunichosha mara anaibuka mara anapotea.. akasema yeye mwenyewe anapitia wakati mgumu na haelewi kwanini maana anajaribu kweli kweli kutonitafuta au kuwasiliana ila anajikuta kuna kitu kina msukuma na haelewi kwanini na ana feel kama tutarudiana… nikamwambia uamuzi ni kwake mimi sitaki kupoteza nguvu akajibu si vyema tuwasiliane kwa simu vyema tuonane kuliongelea ila ajabu hadi leo hii kakaa kimyaa..

Sasa mimi naelewaje juu ya hili wana wa Mungu hili swala la mwenza limekua mzigo kwangu na la kuusumbua moyo wangu..mengi sijayasema ila kiufupi ni hayo.. ishara nilipewa ndoto zimeonwa na mimi mwenyewe nimeota pia japo sio ndio ndie au ndie sie ila yale nilomwomba Mungu afungue kwa wakati huo Alijibu ila kwa sasa naona amechoshwa na mimi maana kakaa kimyaaaa juu ya ombi hili yaani kila niombapo Mungu yuko kimyaaa.. japo kuna mama wa maombi kanisani anadai yeye bado ana msukumo wakuombea yule kijana na bado anaona uso wake mara kwa mara..

Kuna siku nilifanyiwa delivarance mtu tena wa kwao alidai tumuache na hawanitaki maana nimempeleka kwa Yesu..naombeni ushauri.. mnapata nini juu ya hili.. maana me nahisi niko too emotional hata kusikia Mungu atapo sema na mimi juu ya hili..

–YJ

————————-

Bwana Yesu asifiwe wana SG, tumejaribu ku edit baadhi ya maneno na kupangilia naamini itasomeka vyema, karibu yule mwenye msaada kiroho anaweza kumpa ushauri japo nasi tunawasiliana naye kwa mwongozo zaidi. Mbarikiwe

–SG

Je ni ulimwengu wa Sasa?

mahusiano

“Habari za uzima wana SG wenzangu, mwenzenu nina linalonitatiza, nimeangalia ulimwengu wa sasa naona wakaka wengi wanaoa wadada wanaopenda mambo ya kidunia tena hawana hofu ya Mungu na kutuposa sisi ambao tumemtolea Mungu maisha yetu kwa kuomba kila jambo, natamani kujua ni wapi tunakosea hadi hawa wa kidunia wanakidhi haja zao na wenye kumpendeza Mungu kuachiwa maumivu, imenitokea mara tatu japo hao wanaofanya hivyo huangukia pabaya na kuniletea usumbufu tena. Huwa nasimama na kutorudi nyuma naishia kutishiwa na kulaaniwa nao, naomba kusikia mitazamo yenu nimejeruhiwa sana”

–TH