Kutoka Dodoma na Mchungaji Peter Msigwa…

msigwa

“Samwel Sitta HUNA uelewa wala mamalaka ya kulikosoa kanisa. Mmezoe kuweka Viongozi wa DINI mifukoni safari hii ndio mnaona Upinzani na uelewa wa kweli . Kwa Bahati mbaya hamkujiaanda hamjui namna ya kukabiliana ,na Upinzani wa kweli . Viongozi wa DINI wanayo haki ya kukemea , kufundisha kuonya ,kuelekeza na kuombea, Mungu hasemi tuitii mamalaka za kihuni ,kifisadi, WEZI , WAONGO, mbinu hizo zilitumiwa na wakoloni, MAKABURU , walitumia bibilia ili wabaki madarakani ili Hali wanakiuka haki za binadamu. Utumwa ili kuwa ni HALALI kisheria,
Yeyote aliyekataa kuuzwa alivunja Sheria, Ubaguzi wa rangi ilikuwa ni sheria . Ukiingia choo cha mzungu ungeshitakiwa,
Mandela alipobisha aliambiwa atii mamalaka, ,hapa KWEtu kuna sheria za kipuuzi na kuna Viongozi wapuuzi Kama wakina Sitta hawapaswi kuheshimiwa hata kidogo, Sitta kamwe huwezi kulisemea kanisa,WHAT WE SEE IN DODOMA IS IGNORANCE IN ACTION …. remember ignorance is very dangerous when is active”

–Mchungaji Peter Msigwa

Kuna haja ya kuombea uchumi wa Nchi?

pastor

“Mwenyekiti, kuna Mbunge mmoja alishauri hapa tuombewe lakini sioni hata theory ya uchumi inayosema kama unataka kutatua matatizo ya uchumi eti ufanye maombi, ninashangaa huyu amepata wapi hilo? As a Theologians hata Paul anasema asiyefanya kazi na asile siyo aombewe, unamnyima chakula lakini yeye anasema watu waombewe. Mimi kama Mchungaji naombea wazinzi, wanaofumaniwa na wake za watu, ndiyo tunawaombea, mimi kama Mchungaji tunawaombea wenye mapepo na hii ni principle tuna apply, una-consumers wengi lakini producers wachache maana yake you have to produce more tafuta njia za ku-produce zaidi, we don’t pray for this, we don’t have to pray for this”

MCH PETER MSIGWA BUNGENI 19/6/12
Habari Kamili…..

“Matatizo hayawezi kutatuliwa kwa akili ile ile iliyotumika kuyasababisha”

Akichangia mjadala juu ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2011/2012 pamoja na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa mwaka 2012/2013 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2012/2023 siku ya tarehe 19 Juni mwaka 2012; Mhe Mchungaji Msigwa alijenga hoja zifuatazo;

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru sana kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuanza kwa nukuu ambayo naipenda sana inayosema:-

“Insanity is keeping doing the same thing in the same way and expecting different result” yaani uwendawazimu ni kufanya jambo lilelile kwa njia ileile huku ukitegemea matokeo tofauti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwanafalsafa Albert Einstein anasema:-

“Problems can not be solved by the same level of thinking that creates them”. Ndugu zangu, kabla sijawa Mbunge kama alivyosema kaka yangu Mheshimiwa Akunaay, nilikuwa nawa-admire (nawahusudu) sana Wabunge wanavyokuwa Bungeni, wakivaa suti, nilikuwa naona hapa ni mahali ambapo tuna reason (tuna -dadisi), mahali ambapo tuna question (tunahoji) na mahali ambapo tunatoka na solutions (ufumbuzi) ambazo zinalikabili taifa lakini kwa bahati mbaya nimeona is the opposite (ni kinyume kabisa), binafsi najisikia vibaya sana. Kama taifa tupo hapa, we are dealing na future ya taifa hili, tunashughulika na mamia ya maskini wa Tanzania, tunashughulika na barabara mbovu za Watanzania, tunashughulika na hospitali mbovu za Watanzania, halafu tunakuja hapa tunaongea mambo ya khanga!

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma historia, nchi za Ulaya karne ya 14, Marekani na Ulaya na nchi zilizoendelea, zilikuwa na fikra na mawazo kama tunavyofanya sasa hivi lakini ilipofika karne ya 18, inaitwa age of enlightenment, reasoning age, walianza kufikiri, kuhoji na kudadisi. Tunapofika katika karne hii katika Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania, tunapojadili bajeti maana yake tunazo changamoto zinazotukabili kama taifa. Badala ya kukaa na kujiuliza kwa nini tupo hapa, tunatokaje hapa tulipo, tunaanza kuongea ngonjera na maneno ya uswahiliuswahili yaani unafiki, woga, kujipendekeza na kutokujadili mambo ya msingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, najisikia uchungu sana mamia ya wananchi wametuamini tuje tujadili vitu vya maana hapa lakini tunakubaliana akili ndogo itawale akili kubwa. James Madison mwaka 1822 alisema, “knowledge forever will govern ignorance”. Tumekubali Bunge hili knowledge ndogo i-govern knowledge kubwa, tumekubali ignorance i-govern knowledge, tunalipeleka wapi taifa? Akichangia professor hapa hana tofauti na mtu wa darasa la pili. Huwezi kutofautisha mtu mwenye masters na mtu wa darasa la pili, where are we taking this nation? Watu wametupa kura, tunapoteza fedha za Watanzania, tumekaa hapa tunaacha kujadili mambo ya msingi kwamba tunawezaje kutoka kwenye matope haya? karne hiyo ya 18 ninayoisema walipoanza kuhoji, walipoanza kudadisi ndipo mapinduzi ya viwanda yalivyojitokeza, no wonder watu wanaosema ni wataalamu wa uchumi
wametufikisha hapa tulipo, if that is the case, haya ndiyo masuala ambayo tunapaswa tuyajadili kama taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti inaonyesha hapa, kitabu cha uchumi cha Mheshimiwa Wassira kwamba deni limekuwa shilingi trilioni 20. Ukigawanya ni kama karibu kila Mtanzania anadaiwa shilingi laki nne na themanini na zaidi, hata mimba inadaiwa, ndiyo taifa tulipofika hapa sasa hivi. Pia ninashangaa katika mapango wake wa bajeti taifa hili kama tunafuatilia na tunakwenda na takwimu, mdogo wangu amezungumza hapa kwamba tunatumia takwimu za nyuma, unawezaje kupanga mambo na takwimu za nyuma? Leo hii katika taifa hili 44.2% ni watoto walio chini ya miaka 15 maana yake hawa ni consumers, wanakula zaidi hawa-produce, wako shuleni na wanao-produce katika nchi hii ni wachache sana kuliko wanaokula ukijumlisha na wazee tuna mzigo mkubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa utaratibu wa bajeti tulio nao hapa, there is no way kama tunaweza tukafanya maendeleo, it will take ages kubadilisha taifa hili kama tunaendelea na ngonjera za namna hii na kuruhusu akili ndogo itawale akili kubwa. Watu wenye akili kubwawanaweka akili zao mfukoni kwa sababu ya ushabiki wa kivyama badala ya kukaa tuka-discuss namna ya kutatua matatizo yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kama wanao-consume ni wengi na wanao-produce ni wachache maana yake nini? Tutaendelea kuomba fedha nje na kukopa fedha nje ili tuwalishe kwa sababu ni wajibu wa Serikali kusomesha watoto, ni wajibu wa Taifa kuhakikisha watoto wanavaa na kusoma shule nzuri lakini mpango mzima wa uchumi uko kimya, hauzungumzi. Hapa watu wasomi ambao tupo 350 taifa limetuamini tukae hapa tunatakiwa tujihoji, ndiyo maana nimesema problems can not be solved by the same level of thinking that created them, you guys you are tired! Kwa sababu hamuwezi kutetea matatizo haya, mmetuweka kwenye mess ninyi wenyewe, ni lazima akili ya juu zaidi iweze kutatua, ni principle hii yaani huwezi kubadilisha that is the principle, iwe ni mwanamahesabu na nikiunganisha na insanity is keeping doing the same thing in the same way and expecting different results and this is what we are doing.

Tunafanya hayo hayo kila mwaka bajeti ya namna hiyohiyo. Ukienda kwenye elimu ni matatizo, ukienda kwenye kilimo ni matatizo, ukienda kwenye afya ni matatizo mwaka baada ya mwaka ni matatizo yaleyale, why can’t we think a little bit more? We can’t stretch our brain a little bit more kama taifa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeongea na watu wengine ambao ni ma-professor wanasema mara nyingi wakitoa ushauri wa kitaalamu, Serikali hamsikilizi na inawezekana wanakaa watu wachache, wanajifungia halafu wanatoa maamuzi kwa sababu wanajua mambo ni yaleyale, business as usual. Ndugu zangu, where are we going? Where are we heading?

Mheshimiwa Mwenyekiti, takwimu zinaonyesha tena karibu 42% ya watoto wanaozaliwa wanadumaa, they can not think properly, they can not question, they can not ask. Ubongo aliotupa Mungu ni lazima uwe stretched ili uweze kuchambua kwani tumeumbwa ili tutatue matatizo hapa duniani na siyo tu-create matatizo. Tulipokuja hapa Bungeni tunatakiwa tu-solve problems, Bunge hili naliomba liwe Bunge la kimapinduzi, tu-change namna ya kufikiri na tu-change namna ya kufanya vitu na wengine wanapata taabu hapa kwa sababu tumezoea Bunge la chama kimoja. Tuna mfumo na traditional ya chama kimoja cha zamani, ulimwengu umechange halafu tumesimama mahali pamoja hatuendi na ulimwengu unavyokwenda. Maendeleo duniani yamekuja kwa kuwa na mawazo tofauti yanayopingana, badala ya kutuzomea mtusikilize, huu ndiyo wajibu wetu. Mimi kama opposition siwezi kusifia bali nakukosoa ili ufanye kazi yako vizuri ili na wewe utimize wajibu wako.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa deni kama hili kila mwaka linaongezeka halafu tunakaa hapa tunasema Serikali ya CCM itaendelea kutawala, so what? Ili iweje? Kwa sababu lengo la Serikali kuwepo ni kutatua matatizo ili tuhakikishe tuna-improve maisha ya watu lakini watu kwa sababu wanalinda vyeo, kuna mmoja amesema Mchungaji, lakini nitasema tu hata kama mtasema au kunitoa nje ya Bunge lakini kama ukweli unakosewa I will speak out kwa sababu hiyo ndiyo kazi ya
Wachungaji vilevile.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna Mbunge mmoja alishauri hapa tuombewe lakini sioni hata theory ya uchumi inayosema kama unataka kutatua matatizo ya uchumi eti ufanye maombi, ninashangaa huyu amepata wapi hilo? As a Theologians hata Paul anasema asiyefanya kazi na asile siyo aombewe, unamnyima chakula lakini yeye anasema watu waombewe. Mimi kama Mchungaji naombea wazinzi, wanaofumaniwa na wake za watu, ndiyo tunawaombea, mimi kama Mchungaji tunawaombea wenye mapepo na hii ni principle tuna apply, una-consumers wengi lakini producers wachache maana yake you have to produce more tafuta njia za ku-produce zaidi, we don’t pray for this, we don’t have to pray for this.

Mheshimiwa Mwenyekiti, halafu tumekaa hapa tumezalisha taifa la watu waoga, wanafiki na wanajipendekezapendekeza, mimi sijaja hapa kwa kupewa fedha bali wananchi wa Iringa wamenichangua, wananiamini na ninajua wananiunga mkono, wananisikiliza. Sasa sihitaji kujipendekeza nitaeleza ukweli as a nation tupo kwenye matatizo. We have to address this problems lakini siyo tunakuja hapa tunaweka ngonjera maneno ya khanga halafu watu mnawapigia makofi, tunalipeleka wapi taifa hili?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninajisikia uchungu, naomba niachie hapo. Ahsante sana.

MCH. MSIGWA

Ushauri wa bure kwa waimbaji

bish

Kuna watu wamejiingiza kuimba muziki wa Injili, sio kufanya huduma. Bali kwa sababu eti “Rose Muhando anaendesha Prado, Bahati Bukuku kajenga ghorofa”. Kwa hiyo wanaimba kwa sababu muziki ndio biashara inayolipa fasta. Wanachafua kanisa kwa kuimba vituko na wameteka vituo vya redio kwa kuhonga watangazaji ili nyimbo zao zipigwe kwa fujo na wapate mialiko makanisani. Saa ya anguko la watu kama hao imekaribia. Mtazunguka na CD bila kupata ndululu. 2013 Mungu anakumbuka watumishi wake kweli kweli kwa jina la Yesu”

Bishop Nickodemus Shaboka Jr.

“Usimuongelee mabaya Mchungaji wako kwenye Facebook au Twitter Utalaaniwa” – Pastor Creflo Dollar

Pastor Creflo Dollar akielezea jinsi ya kuheshimu mamlaka za kiroho

You teamed up with the world and the devil, and became an accuser of the brethren… and what it could have accomplished won’t be accomplished anymore because you joined the Twitter and Facebook crowd to dishonor spiritual authority ~ Pastor Creflo Dollar.

Swali; kutokana na maneno hayo, Je ni sahihi wakristo kunyamaza kuhusu watumishi wa Mungu?

Msikilize hapa

Pastor asema mafuriko na matetemeko ya ardhi bado!

Mtume Brain Carn amesema kwenye moja ya kusanyiko lake kwamba, Matukio ya kutikisha dunia bado hayajaja yanakuja makubwa zaidi kama watu hawataziacha njia zao mbaya na kumrudia Mungu.

Ameongea hivyo baada ya kimbunga Isaac kilichofika New Orleans. Katika maongezi yake hayo, watu wengi wamejitokeza kupinga kwamba Mungu hawezi kuhukumu nchi na kuacha wanadamu wapate shida. Akauliza swali, kama Mungu aliweza kufanya kipindi cha Sodoma na Gomora atashindwaje kwa kipindi hiki kiovu?

Tukio hilo limetafsiriwa na watu tofauti wengine wakisema ni Baraka kwa sehemu zilizokuwa na ukame na wengine akiwepo Buster Wilson kusema ni adhabu kwa wakazi wa New Orleans kwa sherehe za mashoga na wasagaji zinazotarajiwa kufanyika mwezi huu.

 

Kuna watoto wa wachungaji wenye ushuhuda mzuri!

“Watoto wengi wa wahubiri hawana sifa nzuri kwa jamii” haya ni maneno yaliyo mitaani kwetu na hata kwenye makusanyiko tunapokutana. Lakini huu sio ukweli, kuna watoto wa wachungaji wanaoendelea vyema kiroho na kuwa ushuhuda mzuri kwa jamii iliyowazunguka. Napenda kuchukua nafasi hii kuwaomba watumishi wa Mungu, tuendelee kuombea na kuwakanya watoto wetu, watoto wa wachungaji. Tusihukumu wanaoonekana wanapotea. Hawatapotea, watarudi kwa baba yao.