Huu ni ujumbe wako?

Utaishi kutimiza ndoto Mungu alizokupa, uta-shine kwenye dunia iliyojaa giza, usiogope aliyeinuliwa sana yuko ndani yako, adui anakuwinda sana na yeye anawindwa zaidi na jeshi la malaika walio hodari, adui akinguruma kama simba anamwamsha tu SIMBA WA YUDA wa ukweli ambaye ngurumo yake yamsambaratisha vibaya mbele zako. wewe ni wa THAMANI sana!

–“B” Family

Advertisements

Dondoo za kitabu cha HOSEA

Utangulizi:
Hosea ambaye maana ya jina lake ni ‘‘wokovu,’’alikuwa mwana wa Beeri (1:1) Hakuna mambo mengi yanayofahamika kuhusu nabii isipokuwa machache yaliyo katika wasifu wake kwenye kitabu hiki..

Nabii Hosea alikuwa mzaliwa wa ufalme wa kaskazini, yaani, Israeli, ambao yeye anauzungumzia pia kama Efraimu. (Majina mawili ya kwanza ya ufalme wa kaskazini) na kwa Samaria ambao ndio uliokuwa mji mkuu wa ufalme huo). Yawezekana kwamba alianza huduma yake kabla ya kifo cha mfalme Yeroboamu II ambaye alikufa mwaka 753 K.K. Huduma ya Hosea kwa ufalme wa kaskazini ilikaribiana sana na ile ya Amosi (nabii kutoka Yuda aliyetabiri kuhusu Israeli).

Amosi na Hosea ndio manabii wawli pekee wa Agano la Kale ambao vitabu vyao viliandika kuhusu ufalme wa kaskazini na uangamivu wake ujao. Hosea aliitwa na Mungu ili kutabiri juu ya matarajio yaliyoshindikana kabisa ya ufalme wa kaskazini (Israeli) katika kipindi chake cha mwisho cha zaidi ya miaka 30, kama Yeremia alivyokuwa akifanya kwa ufalme wa kusini (Yuda).Wakati Hosea alipoanza huduma yake katika miaka ya baadaye ya utawala wa Yeroboamu II, Isareli ilikuwa inafurahia ustawi wake wa kiuchumi na amani ya kisiasa iliyosababisha kuwepo kwa usalama pande zote. Mara baada ya kufa kwa Yeroboamu II mwaka 753 K.K., taifa lilianza kuharibika kwa haraka n a hatimaye kuangamia mnamo mwaka 722 K.K. Katika kipndi cha miaka 15 baada ya kifo chake, wafalme wane waliuawa, katika kipindi kingine cha miaka 15 Samaria iliteketezwa kwa moto, Waisraeli walipelekwa utumwani Ashuru na baadaye kutawanywa katika mataifa mbalimbali.

Wazo Kuu:
Kiini cha ujumbe wa Hosea ni kuonyesha upendo wa Mungu kwa wenye dhambi, yaani, upendo wa Mungu kwa Israeli aliyegeuka na kumwacha Mungu. Ujumbe huu wa Hosea ulionekana kwa dhahiri katika maisha ya ndoa ya huyu nabii. Yale majina aliyowaita watoto wake watatu kwa kufuatana kulionyesha kule kuvunjika kwa uhusiano wa upendo wa Israeli kwa Mungu.Jina la mzaliwa wake wa kwanza wa kiume ”Yezreeli,”linaonyesha hukumu ya mfalme anayetawala, yaani Yeroboamu , aliyekuwa wa ukoo wa kifalme wa Yehu (2Wafalme 10:1-14).Jina la binti yake “Lo-ruhama” ambalo maana yake ni “Asiyehurumiwa,” likitoa ujumbe wa Mungu kwamba alikuwa anakaribia kuondoa huruma Yake kwa Israeli. “Lo-ami,” jina la mtoto wake wa tatu, linamaanisha “Sio watu wangu”, likiashiria Mungu kuwakataa Israeli watu Wake.

Kukosa uaminifu kwa Gomeri, mkewe Hosea, kunaonyesha ile hali ya kukengeuka kwa Israeli kutoka kwenye uhusiano wao wa agano na Mungu. Badala ya kuupokea kwa shukrani neema ya Mungu waliyopewa kwa kuwapatia baraka za vitu, Waisraeli walitumia mazao yao kutolea sanamu kafara. Dhuluma, rushwa, kuwaonea wengine, haya yote yanaonyesha udhaifu wa upendo wao kwa Mungu na kati ya wao kwa wao.

Mambo Muhimu:
Hosea anaelezea hali ya taifa akitumia hali iliyojitokeza katika maisha ya kila siku: Mungu anafananishwa na mume, baba, simba, chui, dubu, umande, mvua, nondo, n.k. Israeli inafananishwa na mke aliyekosa uaminifu kwa mumewe, mtu mgonjwa, mzabibu, zabibu, mzeituni, mwanamke anayejifungua, jiko la kuokea, ukungu wa asubuhi, makapi, moshi n.k.

Mwandishi:
Hosea mwana wa Beeri (“Hosea maana yake ni wokovu”).

Mahali:
Ufalme wa kaskazini (Israeli), ambao nabii anautaja kama Efraimu. Mji wake mkuu ulikuwa.Samaria.

Tarehe:
715-710 K.K.

Wahusika Wakuu:
Hosea, Gomeri, watoto wao.

Mgawanyo :
• Maisha ya Hosea katika familia. (1:1-3:5)
• Hali ya dhambi ya Israeli. (4:1-6:3)
• Adhabu kwa ajili ya Israeli. (6:4-10:15)
• Hukumu ya Mungu na rehema Zake. (11:1-14:9)

Bwana wa Majeshi ya Mbinguni ndiye Bwana wetu leo!!

Bwana wa Majeshi ya Mbinguni ndiye Bwana wetu leo, Bwana wa Majeshi ya Israeli ndiye Bwana wetu leo, ni yeye yule jana leo na hata milele “Yehovah Sabaoth”! Kamanda na Komandoo…Amiri Jeshi mkuu na Bwana wa Vita …anasimama kwa ajili yetu, upande wetu, katikati yetu Shujaa aokoae kishujaa…Tunasonga mbele! tunakaza buti, Tunapasua mawimbi, tunamtazama aliyeianzisha kazi njema mioyoni mwetu yuko pamoja nasi hadi tumalize kazi.. tunatiwa nguvu mpya, kama Tai tunapaa, ujana wetu unarejeshwa, tu majasiri kama Simba. Pamoja kwa umoja katika Roho mtakatifu tuna kazi Kubwa mbele, kuhakikisha wanyonge wanainuliwa, dhaifu wanapata nguvu, maskini wanafanikiwa, walio mbali wanafikiwa, wenye dhambi wanatubu, wagonjwa wanapona, mepepo yanatoka, hofu ya Mungu inatawala, na Bwana wetu – Nyota ya alfajiri, Simba wa kabila la Yuda, Mfalme wa wafalme, Bwana wa mabwana, Alfa na Omega ANATUKUZWA kuanzia mioyoni, makazini, kwenye biashara, makanisani, mashambani, angani na ardhini …Ulimwengu ujue nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, na kwamba hakuna jina lingine juu ya JINA LA YESU.  Kila goti lijiandae kwenda chini, kila ulimi ujiandae kukiri ya kuwa YESU NI BWANA! utukufu heshima na adhama vina MUNGU wetu BABA YETU! katika JINA LA YESU

Unapookoka unakuwa juu ya mamlaka yote ya adui

https://strictlygospel.files.wordpress.com/2012/07/pst-abel.jpg

Kwa kuwa imeandikwa -Vaeni silaha anazowapeni Mungu mpate kuzipinga mbinu mbaya za Ibilisi (Waefeso 6:11) . na kwa kuwa – Tunajua kwamba kila aliye mtoto wa Mungu hatendi dhambi, kwa sababu Mwana wa Mungu humlinda salama, na yule Mwovu hawezi kumdhuru (1Yohana 5:18) .vilevile – Tunajua kwamba sisi ni wake Mungu ingawa ulimwengu wote unatawaliwa na yule Mwovu (1Yohana 5:19) Na kwamba twajifunza – ili tusimpe nafasi Shetani atudanganye; maana twaijua mipango yake ilivyo(2Wakorintho 2:11) . Na kwa kuwa tumeambiwa – Msiwaogope adui zenu, bali mwe hodari daima, na hiyo itawathibitishia kwamba wao watashindwa, nanyi mtashinda kwani Mungu mwenyewe ndiye anayewapeni ushindi. Wafilipi 1:28
Na kwa kuwa hatuko tayari kupoteza uhodari wetu kwani utatupa tuzo kubwa (Waebrania 10:35)
Kama familia ya Mungu ILIYO‘B’ARIKIWA na ambayo inatambua sehemu ya ‘B’araka ni pamoja na ushindi dhidi ya adui zetu, tunaendelea na mfululizo wa kujifunza Mbinu za adui kwa msaada wa Roho Mtakatifu.
Kama sehemu ya utangulizi ningependa kutaja majina ya adui yetu, kama yanavyojulikana katika maandiko :
1. Anaitwa Nyoka II Wakoritho 11:3 Lakini naogopa kwamba, kama vile yule nyoka kwa hila zake za uongo alimdanganya Hawa, fikira zenu zaweza kupotoshwa, mkauacha uaminifu wenu wa kweli kwa Kristo
2. Anaitwa Abaddon (Kiebrania) Apollyon (Kigiriki) ikimaanisha mharibifu (Destroyer), ufunuo 9:11.
3. Anaitwa Mshitaki wa ndugu zetu (Accuser of the brethren), Ufunuo 12:10.
4. Anaitwa Malaika wa kuzimu (Angel of the bottomless pit) = Ufunuo 9:11
5. Anaitwa Mpinga Kristo – aliye kinyume cha Kristo – (Antichrist )= I Yohana 4:3.
6. Anaitwa Beelzebuli Mkuu wa pepo Matthayo12:24, Marko 3:22, Luka 11:15
7. Anaitwa Beliari – II Wakorintho 6:15 Kristo anawezaje kupatana na Shetani? Muumini ana uhusiano gani na asiyeamini?
8. Anaitwa Ibilisi (false accuser, devil, slanderer) Matthayo 4:1, Luka 4:2, 6, Ufunuo 20:2 .
9. Anaitwa Adui(Enemy) Matthew 13:39
10. Anaitwa roho mbaya/ovu Evil spirit – I Samueli 16:14
11. Anaitwa ni Mwongo na Baba wa uongo Father of all liars (a liar) – Yohana 8:44
12. Anaitwa Mungu wa dunia hii God (god) of this world = II Wakorintho 4:4 ; Hao hawaamini kwa sababu yule mungu wa ulimwengu huu amezitia giza akili zao wasipate kuuona wazi mwanga wa Habari Njema ya utukufu wa Kristo, ambaye ni mfano kamili wa Mungu.
13. Anaitwa Joka Kubwa Jekundu (Great red dragon) = Ufunuo 12:3
14. anaitwa Lusiferi Lucifer (Roman rendering of morning star) = Isaya 14:12
15. Anaitwa Mwuaji tangu mwanzo Murderer = – Yohana 8:44
16. Nyoka wa zamani, Old serpent = ufunuo, 12:9, Ufunuo 20:2
17. Mwenye Nguvu za giza; Power of darkness = Wakolosai 1:13
18. Mkuu wa Ulimwengu huu (wa kutupwa nje) Prince of this world = Yohana 12:31, Yohana 14:30, Yohana16:11
19. Anaitwa mfalme wa uwezo wa anga (roho atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi Princ) of the power of the air = Waefeso 2:2
20. Mkuu wa giza (Ruler of darkness) = Waefeso 6:12 ;Maana vita vyenu si vita kati yetu na binadamu, bali ni vita dhidi ya jeshi ovu la ulimwengu wa roho; tunapigana na watawala, wakuu na wenye nguvu wanaomiliki ulimwengu huu wa giza.
21. Anaitwa Shetani (satan) Matendo ya Mitume 26:18; Utayafumbua macho yao na kuwawezesha watoke gizani na kuingia katika mwanga; watoke katika utawala wa Shetani, wamgeukie Mungu; ili kwa kuamini, wapate kusamehewa dhambi na kuchukua nafasi yao kati ya wale ambao wamepata kuwa watu wa Mungu. Warumi 16:20- Naye Mungu aliye chanzo cha amani hatakawia kumponda Shetani chini ya miguu yenu. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi.
22. Anaitwa Mjaribu/Mshawishi -Mathayo 4:3, I Wathesalonike 3:5 Ndio maana nilimtuma Timotheo kwenu. Sikuweza kungoja zaidi, na hivyo nilimtuma nipate habari za imani yenu. Isije ikawa labda Mshawishi aliwajaribuni na kazi yote tuliyofanya miongoni mwenu imepotea bure!
23. Anaitwa Mwizi – Yohana 10:10 Mwizi huja kwa shabaha ya kuiba, kuua na kuharibu. Mimi nimekuja mpate kuwa na uzima—uzima kamili.
24. Anaitwa Mwovu (Wicked one) = Mathayo 13:19, 38 .
Hayo ni baadhi ya majina yake na yanawakilisha kazi anazofanya Unapookoka unakuwa juu yake, Unapojazwa Roho Mtakatifu na kumjua Mungu na namna ya kutumia uwezo na Mamlaka ya Yesu, na kujua mbinu na hila zake unafanyika mshindi na zaidi ya mshindi…!

–B Family

Kwa Imani tunayaweza yote!!

Ni kwa Huruma za Bwana Hatuangamii, ni kwa Neema ya Bwana tunaokolewa na uharibifu ulioko duniani na kufundishwa kukataa mabaya, ni kwa Upako wa Bwana tunatumika, ni kwa Baraka za Bwana tunafanikiwa kiroho, kinafsi na kimwili; ni kwa Upendo wa Mungu tunatunzwa na kulindwa na kuwa nae karibu, ni kwa Nguvu za Mungu tunashinda, ni kwa Uwezo wa Mungu tunasonga mbele, ni kwa Mamlaka ya Bwana wa Majeshi Nguvu za giza zinatetemeka mbele yetu na kusambaratika, ni kwa Neno la Bwana tunaishi na Kuimarika, ni kwa Roho wa Bwana tuna karama na vipawa na matendo makuu ya Mungu yanafanyika, ni kwa Imani tunayaweza yote!

–“B” Family