Kiu yangu ni kuongezeka zaidi katika kumjua Mungu – Angel Bernard

Huu wimbo niliupata palepale studio. I heard the beat and hapohapo maneno yakaflow… Yes, ilikuwa ni desire yangu sana kujazwa zaidi Na zaidi, nilikuwa na kiu sana ya kukutana na Mungu katika hicho kipindi.

Mungu alifanyika halisia zaidi kwangu after that song, ikawa ni Maombi yangu na raha yangu zaidi na zaidi.

My message: Kiu yangu ni kuongezeka zaidi katika kumjua Mungu. I believe kama tusipoishi Kwa mazoea kuna mambo zaidi tutayajua na kuyapata kupitia Mungu.

Namshukuru Mungu sana Kwa kuwahudumia. Get ready for DVD launching tarehe 10 may.

–Angel Bernard

Munishi atoa ushuhuda aliyoyaona kanisani kwa Gwajima!!

munisi

“TANZANIA NILIWASILI SALAMA .

Mapokezi ya kufana Tamasha tukafanya, Maelfu walihudhuria wala MISUKULE sikuwaona nilichokiona ni Umati mkubwa wa watu kwenye Viwanja vya nje jijini Dar wanavyoviita ni KANISA LA UFUFUO NA UZIMA chini ya Mchungaji Bishop Gwajima mwanzilishi wa huduma hiyo.

Pamoja nami alikuwepo Rose Mhando, Bonny Mwaitege, Christine Shusho, Upendo Nkone na wengine wengi.

Bishop Gwajima aliingia na gari yake aina ya HAMMER chini ya ulinzi mkali na akatukaribisha tuimbe kisha yeye akahubiri na sikusikia akitaja MSUKULE ila alimwita Binti aliyedai alikufa siku tatu na alipoletwa kanisani akaombewa akafufuka.

Nliona ni Busara niende Nijionee mwenyewe.

Kwa sasa Nimerejea Nairobi”

–Faustine Munishi

Malaika Wamuokoa John Komanya kutoka kwenye Ajali!!

john

Mwimbaji anayetamba na wimbo wa “Zawadi gani nitamtolea BWANA” ambaye pia ni mtume akichunga kanisa jijini Dar es Salaam John Komanya amepata ajali mbaya juzi mchana maeneo karibu na daraja la Mto Wami akiwa njiani kuelekea mkoani Arusha kukutana na viongozi wanaohudumu na mwalimu Christopher Mwakasege, kwa ajili ya mkutano wa injili ambao utakuwa na lengo la kuombea taifa kwa siku nne mwezi Disemba.

Akizungumza na GK mtume Komanya amesema lengo lilikuwa ni kupeleka barua kwa viongozi hao ili wamfikishie mwalimu Mwakasege kwaajili ya mkutano huo. Amesema akiwa njiani katikati ya Msata na Wami na wakati huo hakuwa amefunga mkanda wa gari, ndipo akasikia sauti ya Roho Mtakatifu ikimwambia kwa upole afunge mkanda lakini akawa anapuuzia na kuanza kujiuliza kwanini, sauti ikarudia tena kwa upole ikimwambia afunge mkanda akiwa bado anajiuliza ndipo anasema akasikia sauti ya Mungu ikizungumza kwa haraka na ukali “John funga mkanda” ndipo akafunga mkanda.

Mtume Komanya amesema akiwa anateremka kuelekea wami akiwa katika mwendo wa 180 wakati akipita katika kona kulikuwa na malori matatu mbele yake kukawa na lori lingine likifuatiwa na mabasi matatu yakipandisha kutoka Arusha kuja Dar, kwa wakati huo aliona malaika saba ambapo walishuka mithili ya makomandoo washukavyo kutoka kwenye kamba ya helikopta, mmoja akiwa amekaa kwenye boneti mbele, mwingine kulia, kushoto na mwingine nyuma yake ambaye alimwambia Komanya afuate maelekezo yake, anasema akiwa anamwangalia malaika aliyekaa karibu naye katika kiti cha dereva aliambiwa afuate maelekezo anayopewa na malaika wa nyuma yake.

Alipokuwa akiangalia mbele akaona gari linayapita mengine kwa spidi hali iliyomfanya Komanya kutaka kuingia katikati ya magari mengine lakini malaika akamwambia afuate maelekezo yake na kuambiwa aachie uskani jambo ambalo alilipinga kwakuwa aliona kifo mbele yake na kutaka kuingia katikati ili kukwepa, lakini malaika akamwambia ukiingia katikati utakufa, wewe achia usukani kama ninavyokwambia kwakuwa wametumwa kumlinda, akawa bado anatafakari kutokana na kuliona korongo kubwa upande wake huku malaika wakimwambia asiguse kitu chochote ikiwemo kutokanyaga breki lakini bila kusikia akakanyaga na kusababisha gari kuyumba sana, malaika akamwambia tena aachie breki na kuweka mikono yake kifuani. Anasema alipoweka mikono kifuani aliona wakiligonga lori huku malaika akiwa ameshika usukani na kuonyonga sana huku yeye akisema alijikuta akiwekwa kwenye kitu kama chupa ya maji, na yeye kwa wakati huo kuona kama vile yupo ndani ya glasi ya maji, ila anaona kinachoendelea.

Kisha baada ya hapo, upande wake wa usukani ndio uliogongwa, mara baada ya malaika kuchezesha usukani kidogo ili kuepusha madhara zaidi, na kisha ile semi-trailler ikamtupia kwenye korongo na kubinuka mara tatu hewani kabla ya kutua chini kwa mara ya nne, ambapo gari ilikuwa juu chini, yaani matairi yakiwa yanatazama juu.

Baada ya hapo kilichofuata ni kuendelea kusikiliza malaika wasemacho, ambapo hapo alisikia sauti ikisema fungua mkanda utoke, na kwa wakati huo kulikuwa na moshi ullioanza kutoka kwenye gari – na hapo akapewa dakika 12 kuchukua baadhi ya vitu alivyokuwa navyo kwenye gari. Maajabu ya Mungu, hakuna kitu chochote kilichogusa mwili wake, na wala hakuna damu iliyovuja kutokana na gari hilo kupindukia kwenye korongo.

Hakika utukufu ulimrudia Mungu kwa wakati huo kwani baadhi ya mashuhuda walikiri hapohapo ya kwamba hakuna mtu anayeweza kusalimika kwenye ajali hiyo, bali ni lazima tu mkono wa Mungu umehusika hapo kuokoa.

Baadhi ya mashuhuda ambao walikuwapo kwenye mabasi ya mkoa (hadi mkoa) walimtambua mtumishi wa Mungu ya kwamba ni John Komanya na hatumaye kumshukuru Mungu hapohapo, ambapo baadae Polisi walifika kwa ajili ya kazi yao – lakini hilo halikumzuia Mchungaji Komanya kupiga magoti na kumshukuru Mungu licha ya umati wa watu – na tukio hilo liliambatana na yeye kuisikia sauti ya Mungu ikimwambia “Nimekupa kazi ya kutengeneza kanisa langu,… usiogope nitakulinda, ila kuwa mwaminifu na nitakuweka kwenye uaminifu

Sauti hiyo ilitoka kwa kiumbe ambacho kilikuwa na muonekano wa malaika, Pastor Komanya anaieleza GK na kusema kuwa sauti yake ilikuwa ya tofauti, na mavazi yake yalikuwa ni meupe na kwamba alielezwa dhahiri kuwa hiyo semi trailer ilikuwa imetumwa kummaliza, lakini ndio maana malaika walitumwa kumlinda.

“Zawadi Gani” kama ambavyo alikuwa akiitwa akiwa hospitali ya Muhimbili, alifanyiwa vipimo na kuonekana ya kwamba hana shida yoyote. Na hili linadhihirika hata pale alipotoka kwenye gari lililopiinduka, kwa kuwa alitoa vifaa vyake na kuanza pia kupiga picha, picha ambazo kama mtu akiziona zote, hakika hawezi kuamini kama kuna kusalimika hapo.

Mwisho wa yote Mchungaji Komanya anakiri kuwa amepona kwa rehema ya Mungu, na baada ya hapo amemuahidi kumtumikia kwa kazi aliyompa licha ya kwamba ni ngumu na ina vikwazo vingi. Jumapili hii, Mchungaji Komanya ataimba wimbo mpya kumshukuru Mungu kutokana na kumuepusha na kifo. Kwa wasafiri wote, hapa kuna funzo la kujikabidhi mikononi mwa BWANA kila mara safari inapotokea, katu tusienende kwa mazoea.

–Gospel Kitaa

Kutoka kwenye Uislamu mpaka Mwimbaji wa Injili kimataifa- Fay Destiny

faydestiny

Amekutana na Bwana Yesu tangu akiwa na umri wa miaka 12 alipokuwa akiteswa na vifungo vya shetani katika utoto wake lakini mkono wa Bwana Yesu ukamuokoa na kumuita amtumikie kwenye kazi yake.

Japokuwa familia yake iliweka vizuizi mbali mbali, kukataliwa na kutengwa lakini Bwana Yesu alimtetea na kumpigania na hata sasa anasema Yeye ni ushuhuda halisi, Amepokea uponyaji na uzima kwa jina la Yesu.

Fay Destiny amezindua album ya nyimbo za kumwabudu Mungu na kulitukuza jina lake, album yenye shuhuda halisi na nguvu za Mungu katika nyimbo hizo.

Jipatie nakala yako na ubarikiwe zaidi,

Wasiliana naye moja kwa moja kwa number 614-772-6058

Au wasiliana na Strictly Gospel 484-751-7038 upate nakala yako

Kusikiliza Ushuhuda wake kwa kirefu sikiliza Interview aliyofanya na dada Pricilla Mushi kutoka Gospel Around the World

Baada ya Pennsylvania Askofu Maboya kuelekea Texas na Alabama….

Ilikuwa ni Ibada ya Uamsho na nguvu za Mungu iliyofanyika Norristown, Pennsylvania tarehe 11 – 13 October, 2013. Pamoja na watu kumpa Yesu Maisha yao pia matendo ya miujiza yalidhihirika wazi na watu kupokea baraka zao pale pale. Utukufu ni Kwa Mungu kwa yote yaliyofanyika kwenye mkutano huo, Baada ya kumaliza Pennsylvania sasa Askofu Maboya yuko Texas. Wakazi wa Texas waleteni wagonjwa na wenye kulemewa na mizigo ya dhambi nao watawekwa huru kwa jina la Yesu Kristo. Kwa Mawasiliano zaidi khs Texas wasiliana na Pastor Emmy simu 214-868-5151

Kuhusu Alabama wasiliana na Pastor Yohana Maginga 205-296-7126

Zifuatazo Ni baadhi ya picha za tukio zenye shuhuda ..

bish1

Askofu Maboya akimuombea mama aliyeponywa kansa, na aliyemshika nyuma aliponywa sikio lake pale pale

bish2

Mzee aliyekuwa akisumbuliwa na figo hakuweza kutembea vema kabla lkn aliombewa na kuruka kwa furaha

bish3

Mama pichani akifanyiwa operation ya titi lililokua likimsumbua kwa muda mrefu na kusema hasikii maumivu tena

mamamwesy

Mama aliombewa na kupona pale pale tatizo la mngongo lililomtesa zaidi ya miaka 35

kristabella

Dada Akitolewa unabii juu ya maisha yake

bishopdm

Mtumishi wa Mungu Clement Mboya akitafsiri kingereza kwa wageni

waimbaji

Praise and Worship Team

sifa

Baada ya Matendo Makuu ya Mungu na shuhuda watu wakimsifu Mungu

janeth

Dada Janeth Mganyizi akimshukuru Mungu

pstmelczedeck

Pastor Melchzedek Matulu naye alikuwepo

igogo

Pastor Igogo na Ency Mwalukasa pia walihudumu

psteric

Pastor Eric na Sharon

maria

Vaileth, Moulin na Mary

 

Tunamshukuru Mungu Strictly Gospel kuweza kuandaa Mkutano huu, tunatarajia makubwa zaidi kwa Utukufu wa Mungu. Kuhudhuria maombi yetu Na Neno la Maarifa kila Ijumaa  9E/8C pm Piga 626-677-3000 na Access code 8740052

Au kwa maelekezo Piga simu 484-751-7038

Ushuhuda na Shukrani kwa Mungu kunijalia mtoto

mtoto

Wapendwa jina la Bwana libarikiwe! Ninaitwa Faith, ni takribani miaka 2 imepita sasa tangu nilipotuma maombi yangu juu ya Mtoto,

Kabla ya hapo niliharibikiwa na ujauzito mara 2, ndipo september 2011 mimi na Mume wangu tulimuomba Mungu atuonyeshe tatizo. Mungu ni mwaminifu, mmoja wa marafiki akatuelekeza kwa Dactari mmoja katika hospitali fulani hapa Arusha, tukaanza kuhudhuria kwa kufanya vipimo vingi, ambavyo vingine vilionyesha kuwa ningeweza kuwa na Saratani ya kizazi.

Mume wangu ni Daktari, kwa kuwa mimi sikutaka kuelewa maelezo ya majibu ya daktari basi mimi na Mume wangu tulitoka hospitali tukiwa hatuongei kwa kutofautiana imani kidogo (ukimya haukua na ugomvi). Siku iliyofuata mume wangu aliniita chumbani akajaribu kunichorea kabisa kwa maelezo ya kutosha ili nielewe hatari iliyokua inanikabili kutokana na majibu ya Daktari. Basi baada ya hapo nilimlilia Mungu kwa uchungu na kukataa kabisa yale majibu. Mwezi wa 10 mwaka 2011ule uvimbe uliokua kwenye kizazi ukatoka katika mfumo wa damu. Tukamtukuza Mungu kwa uponyaji, mwishoni mwa mwezi wa Decemba nikafanya vipimo vingine ambavyo vilionyesha kuwa nilikuwa na wingi wa sukari ktk mwili ambayo ingenipelekea kuugua kisukari na ndiyo iliyokua sababu ya kuharibika kwa mimba. Na pia vipimo vikaonyesha kuwa nisingeweza kuwa mjamzito kwa wakati ule na kwamba ningelitakiwa kuanza kumeza dawa za ugonjwa wa kisukari tarehe 17 mwezi February.

Moyo wangu uliinama kwa kiasi, nikakutana na mtumishi wa Mungu na bila kumwambia chochote aliniambia nipokee mtoto kwa jina la Yesu, nikaitika amina, wiki iliyofuata Nikakutana na mama mmoja mtumishi wa Mungu na nikamweleza mambo niliyokua nikipitia, Imani yake ilikua kuu sana, akaniambia, “Faith labda umebeba mapacha” kilikua kitu cha ajabu sana kwangu, wiki iliyofuata January 14 nikakutana na Mama mwingine wa imani, naye akaniambia Faith hauna tatizo la kubeba mimba, tatizo lako ni kutunza mtoto, naye akafanya maombi makali ya kumwombea mtoto katika tumbo, Siku iliyofuata nikaenda kumsalimu mama yangu mzazi (naye ni mtu wa imani) Akaniuliza kama nina habari njema, nikamweleza matatizo yote sawasawa na majibu ya Daktari, mama akaniambia hapana, wewe si mgonjwa una ujauzito wa mtoto wa kiume. Tarehe 17 Januari nikafanya vipimo na kugundua nilikua na ujauzito wa wiki 3.

Kutokana na hali ilivyokua, nilielekea hospitali ambapo vipimo vilionyesha kuwa mwili wangu haukuweza kuzalisha hormony za kumkuza mtoto, kwahiyo wakanipatia dawa mbadala ambazo nilikua nikizitumia. Ilipofika wiki zaidi ya 6, hormony zilikua zikishuka badala ya kupanda, ndipo Daktari akaniambia mtoto hataweza kukua ktk hali hiyo, nilirudi nyumbani nikiwa na huzuni sana. Nikajifungia chumbani kwangu nikimlilia MUNGU. Mungu akasema nami kwa lugha ambayo niliweza kuielewa akaniambia “MY MIRACLES ARE NOT THIRP PART but MY MIRACLES ARE COMPREHENSIVE” Ikiwa na maana kwamba muujiza wangu sio kama bima iliyo nusunusu ila umekamilika (bima kubwa). Ndipo nikajua kuwa Mtoto wangu ni Muujiza kutoka kwa Mungu na nikapata amani ya ajabu. Baada ya hapo mambo mengine mengi yalitokea lakini Mungu alitimiza Muujiza wake kwangu. Sasa nina mtoto wa kiume anayeitwa FarrellMiracle.

Jina la Bwana Libarikiwe.

Mungu awabariki kwa maombi yenu ktk hili.

Faith