Kiu yangu ni kuongezeka zaidi katika kumjua Mungu – Angel Bernard

Huu wimbo niliupata palepale studio. I heard the beat and hapohapo maneno yakaflow… Yes, ilikuwa ni desire yangu sana kujazwa zaidi Na zaidi, nilikuwa na kiu sana ya kukutana na Mungu katika hicho kipindi.

Mungu alifanyika halisia zaidi kwangu after that song, ikawa ni Maombi yangu na raha yangu zaidi na zaidi.

My message: Kiu yangu ni kuongezeka zaidi katika kumjua Mungu. I believe kama tusipoishi Kwa mazoea kuna mambo zaidi tutayajua na kuyapata kupitia Mungu.

Namshukuru Mungu sana Kwa kuwahudumia. Get ready for DVD launching tarehe 10 may.

–Angel Bernard

Uzinduzi wa KAMATA PINDO LA YESU kufanyika Dar es salaam!!

Sikiliza wimbo wa Kamata Pindo….

Uzinduzi wa album mpya ya Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Rose Muhando inayoitwa “KAMATA PINDO LA YESU”unatarajiwa kufanyika  August 03 2014 katika ukumbi wa DIAMOND JUBILEE, kuanzia saa 7 kamili mchana jijini Dar es salaam Tanzania, ambapo waimbaji  wote waalikwa wataimba  LIVE, ikiwa ni pamoja na yeye mwenyewe Mwimbaji anayelitukuza jina la Mungu Tanzania ROSE MUHANDO.

Album hiyo yenye mpya kama FACEBOOK, NA KAMATA PINDO LA YESU, na nyinginezo zitakuwa katika video na audio.

Video imetengenezwa na kampuni ya MSAMA VIDEO PRODUCTION, ambayo ni kampuni mpya dada ya MSAMA PROMOTIONS.

Mkurugenzi wa kampuni ya MSAMA PROMOTION ndugu ALEX MSAMA ambaye ndiyo waandaji wa tamasha hilo, amesema kuwa maadalizi  ya uzinduzi huo mpaka sasa yapo tayari na wadau wa muziki wa injili wakae tayari kumtukuza Bwana kwa siku hiyo.

Hongereni John Lisu kwa baraka ya watoto watatu!

lisus

Muimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania John Lisu na mkewe Nelly Kaisi, wamepata mapacha watatu siku ya tarehe 7 January 2014. Akiongea na blogs mbali mbali anasema “Mungu amenibariki kwa watoto watatu mapacha wawili wa kiume na mmoja wa kike”

Mama na watoto wanaendelea vema.

Hongereni sana familia ya John Lisu, Utukufu ni kwa Bwana.

Kutoka kwenye Uislamu mpaka Mwimbaji wa Injili kimataifa- Fay Destiny

faydestiny

Amekutana na Bwana Yesu tangu akiwa na umri wa miaka 12 alipokuwa akiteswa na vifungo vya shetani katika utoto wake lakini mkono wa Bwana Yesu ukamuokoa na kumuita amtumikie kwenye kazi yake.

Japokuwa familia yake iliweka vizuizi mbali mbali, kukataliwa na kutengwa lakini Bwana Yesu alimtetea na kumpigania na hata sasa anasema Yeye ni ushuhuda halisi, Amepokea uponyaji na uzima kwa jina la Yesu.

Fay Destiny amezindua album ya nyimbo za kumwabudu Mungu na kulitukuza jina lake, album yenye shuhuda halisi na nguvu za Mungu katika nyimbo hizo.

Jipatie nakala yako na ubarikiwe zaidi,

Wasiliana naye moja kwa moja kwa number 614-772-6058

Au wasiliana na Strictly Gospel 484-751-7038 upate nakala yako

Kusikiliza Ushuhuda wake kwa kirefu sikiliza Interview aliyofanya na dada Pricilla Mushi kutoka Gospel Around the World

Siku ya Emmy Kosgei

emmy

Kiongozi wa kanisa la Revival Assembly Mtume Anselm Madubuko wa Nigeria amefunga ndoa na mwimbaji wa Injili nchini Kenya Emmy Kosgei tarehe 31 Agosti 2013 nchini Kenya na tarehe 14 Septemba 2013 itakuwa ni siku ya shukrani katika kanisa la Revival Assemblies nchini Nigeria.

Kila la heri kuelekea mapya

Emmy Kosgei Kuolewa Nigeria!!

emmy

Mwimbaji maarufu nchini Kenya na Afrika Emmy Kosegei (33) anatarajia kufunga ndoa na mchungaji Anselm Madubuko wa kanisa la Revival Assembly Cathedral lililoko Nigeria.

Akiongea na gazeti la Daily Nation la nchini Kenya anasema “Jina lake ni Mtume Anselm Madubuko tunapendana na tunatarajia kufunga ndoa mwanzoni mwezi September”

Hata hivyo aliendelea kuweka sawa baada ya watu wengi kusema anaolewa na Mtume Madubuko kwa sababu ni tajiri, Emmy alijibu anahitaji mume anayemuelewa na si vibaya kuolewa na mtu ambaye ni tajiri.

“Mimi ni mwanamuziki wa injili na nimekuwa nikitafuta mwanaume ambaye atanielewa”

Naye Mtume Madubuko alipohojiwa na vyombo vya habari Nchini Nigeria alisema “Ukweli ni kwamba Mungu kamleta kwa ajili yangu, nilijua ndani ya roho yangu na nikaanza kuomba. Mungu alinionesha, mwanzoni alikataa ombi langu, lakini baada ya unabii mbali mbali akakubali”

pastor_anselm_madubuko.jpg

Apostle Anselm Madubuko

apostle

Akiwa na Juanita Bynum alipotembelea Nigeria