Waimbaji wa nyimbo za Injili ni wanafki – Stara Thomas

Mwimbaji wa zamani wa Bongo fleva ambae sasa ni mwimbaji wa nyimbo za Injili Stara Thomas hivi karibuni alitaja sababu za kushindwa kushirikiana na waimbaji wengine wa nyimbo za Injili kwenye album yake ya kwanza iliyo sokoni sasa.

Aliongea haya alipokuwa akihojiwa kupitia AMPLIFAYA na Millard Ayo  “kwenye upande wa Injili waimbaji wengi bado hawajawa na ufahamu wa kufanya kolabo japo lile ni neno la Mungu linalosimama peke yake haijalishi mnashirikiana au hamshirikiani lakini kushirikiana ni jambo jema, ugumu ambao nimeuona na nimejifunza ni kuhusu unafiki mkubwa sana, mtu anaweza kukuchekea machoni lakini moyoni ni muongo, kuna wengine wasanii wakubwa niliwaona nikafikiri lakini nilipowakaribia nikagundua sio, unafiki ni mwingi, kule kwenye bongofleva kulikua kuna upendo”

Na inasemekani hii sio mara ya kwanza Stara Thomas kutoa madai hayo, mwigizaji Dokii mwanzoni alipookoka, aliwahi kusema wazi waimbaji watano wakubwa wa Injili Tanzania,  ni wanafiki, wana ubinafsi, chuki, kujisikia na kujitenga na hawakukubali kumpa ushirikiano wowote.

Millard Ayo pia aliandika kwenye website yake kwamba waimbaji wa Gospel wenyewe wameshawahi kukiri kwamba hakuna upendo kati yao, watu wanachukiana, hawana umoja. Rose Muhando, Upendo Nkone na Miriam Mauki walishalisema hilo kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM.

Masanja Mkandamizaji atoa tahadhari!

Mchekeshaji maarufu Tanzania ambaye pia ni muimbaji wa nyimbo za Injili Masanja au kwa jina jingine Mchungaji mtarajiwa, ametoa tahadhari kwa wanaombeza kuigiza wakati yeye Mungu hajamwambia kuacha. 

Msanii huyo ameyasema hayo hivi karibuni alipokuwa akihojiwa na mtangazaji maarufu Millard Ayo kutoka radio moja ya kijamii. Hata hivyo hapo kabla Masanja aliwahi kunukuliwa kwamba ipo siku atakuwa mchungaji pia ataacha uigizaji Mungu atakaposema naye. 

Mbali na hayo amewatangazia wanaouza CD feki kwamba “nimemaliza kufanya album yangu ya Gospel najua wako watu mamasta wa kuburn kazi za waimbaji nimewakaribisha waburn hii yangu, yani hamna kesi hashikwi mtu atakaeburn kazi yangu kwa sababu hii ni huduma ukiburn wauzie watu hata mia mia usiziweke ndani”

Kwenye sentensi nyingine Mchekeshaji huyu wa Orijino Komedi ya TBC1 amesema “kuna watu wananiambia Masanja tumeona watu wanauza CD feki nasema kama na wewe unaweza nunua na  ukatengeneze zako kwa sababu hii ni huduma nataka watu wapate ujumbe huu wabadilike wamjue Yesu tunaemuhubiri mwanawane”

Sikiliza wimbo mzuri wa Masanja Mkandamizaji – Hakuna jipya ambao umebeba jina la Album, iko tayari!

Source: Millard Ayo

John Lisu kufanya huduma Ulaya

John Lisu wakati wa huduma

Mwimbaji wa nyimbo za Injili John Lisu yuko Norway kwa sasa, anaendelea na huduma ambapo mpaka sasa amefanya Oslo, Stavanger, Kopervik, baada ya Norway anatazamia kwenda Belgium na Denmark na sehemu nyingine atakazoalikwa.

Anategemea kurudi nyumbani mwezi August ambapo atafanya live recording na kumalizia album yake ya pili, zimebaki nyimbo chache iwe tayari.

Wakazi wa sehemu hizo mnaweza kuwasiliana na John Lisu kwa namba 474 095 3969

Sikiliza wimbo Mpya wa John Lisu – Yu Hai Jehova

John Shabani Alifanikisha Tamasha la Sifa na kuabudu, Kuombea Taifa

Watu wengi walijitokeza kwenye tamasha la John Shabani. Tamasha hilo lililokuwa maalum kwa ajili ya Kusifu na Kuabudu na Maombi kwa ajili ya Taifa Letu la Tanzania lilifanyika Katika Kanisa la TAG Magomeni. Mgeni Rasmi wa siku hiyo alikuwa ni Mhe. Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dr. Fenella Mukangara.

Mkongwe wa Muziki Mzee Makasy alihudhuria

   Cosmas Chidumule akiimba

                                              Chidumule na Stara Thomas pamoja walikuwa waimbaji maarufu hata kabla hawajaokoka

 Upendo Kilahiro hakukosekana

 John Shabani akimtambulisha Apostle John Komanya na Upendo Kilahiro ambapo waliimba wimbo wa KALE NILITEMBEA uliogusa watu wengi

 Mwimbaji na Mtangazani wa PPR Victor Haroun akiwa na Raisi wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Addo November

 Baadhi ya wahudhuriaji

 Bloggers wa Injili waliwakilisha, kuanzia kulia Tunu, Samsasali.blogspot na Victor hosannainc.blogspot
Mchungaji wa Kanisa la TAG Magomeni Pastor Kanemba akiwa na Mkewe siku ya Leo Kwenye Tamasha.
John Shabani alipoagana na Mgeni Rasmi,  Mhe. Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dr. Fenella Mukangara

Katika tamasha hili rangi iliyotawala ni Red kama ionekanavyo pichani na pia  limehudhuriwa na Rais wa waimbaji nchini Mtumishi Addo November. Waimbaji wengi pamoja na kwaya na vikundi mbalimbali wamehudhuria katika tamasha hilo. Pia waandishi mbalimbali wa habari na vyombo mbalimbali vya habari vikiongoza na Television ya taifa TBC vilikuwepo. Maombi maalumu kwa ajili ya Nchi yetu yameongozwa Na Mchungaji Danstan Kanemba pamoja na Bishop Rechael.

Pia John Shabaani ametaja nyimbo mpya zitakazotoka hivi karibuni kwenye album yake inasimamiwa na Kampuni ya Msama Promotion. Nyimbo zingine zilizomo katika album hiyo ni pamoja na

Kwa Yesu kuna raha – John Ft Cosmas Chidumule

Tunaye Baba – John Ft Jane Misso

Wewe ni Baba – John Ft Faraja Ntaboba (DRC Kongo)

Mungu yu mwema – John ft. Christina Matai

Nimemwona Bwana – John ft. Tina Marego

Akisema Ndio – John ft. Destiny Sisters (Kampala)

Wakati wangu – John ft. Bella Kombo

Sikiliza moja ya wimbo wa John Shabani NEEMA YAKO

—www.johnshabani.blogspot.com

Waimbaji ”KWETU PAZURI” Wawasili Dar Leo

Sarah Uwera mmoja wa waimbaji wa kundi hilo, walipotembelea nchini mwaka jana

Kwaya ya Ambassadors of Christ kutoka jijini Kigali nchini Rwanda imewasili leo Jijini Dar es salaam wakitokea nchini kwao Rwanda, tayari kwa ajili ya kutoa huduma ya uimbaji katika mkutano mkubwa wa kimataifa unaofanyika katika viwanja vya Biafra Kinondoni jijini Dar es salaam.

Kundi la kwanza la kwaya hiyo liliondoka jana kwa njia ya basi kuja jijini, huku kundi la pili ndio limewasili leo mchana.

Hii itakuwa mara ya nne kwa waimbaji hao kufika nchini ambako wamekuwa na mashabiki lukuki, kutokana na uimbaji wao, ambapo safari hii wanatarajia kuwepo kwa wiki nzima jijini Dar es salaam ikiwa maalumu kwa mkutano huo,Pia wanatarajia kuwasili na toleo lao jipya la kanda ambalo baadhi ya nyimbo zimeanza kusikika katika vituo vya radio za injili jijini Dar es salaam.

Kanda mpya ya Ambassadors of Christ Rwanda.

—GospelKitaa blog

Tanzania yapata mwakilishi tuzo za Africa Gospel Music Awards

Christina Shusho

Mwimbaji wa muziki wa gospel nchini Christina Shusho ameingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo za Africa gospel music awards zinazotarajiwa kutolewa tarehe 7 mwezi July mwaka huu huko jijini London nchini Uingereza.

Mwimbaji huyo amepata nafasi hiyo baada ya kupigiwa kura za kupendekezwa na watu mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi kutokana na huduma yake njema katika tasnia ya muziki wa injili kwa ujumla. Ambapo mwimbaji huyo amependekezwa kuwania kwenye vipengele viwili ambavyo ni mwimbaji bora wa kike wa mwaka tuzo ambayo anawania pamoja na

1.Emmy Kosgei-Kenya
2.Dena Mwana – Congo
3.Ntokozo Mbambo- South Africa
4.Rebecca- UK
5.Gifty Osei- Ghana
6.Kefee -Nigeria
7.Onos Ariyo- Nigeria
8.Diana Hamilton-UK
9.Christina Shusho -Tanzania
10.Lara George- Nigeria

Katika kipengele cha pili anachowania tuzo mwimbaji huyo ni mwimbaji wa mwaka anayowania pamoja na waimbaji wengine 9 ambao ni

1.Eko Dydda- Kenya
2.Emmy Kosgei – Kenya
3.Exodus- Uganda
4.Christina Shusho- Tanzania
5.Lam Lungwar- South Sudan
6. Sarah K- Kenya
7.Dawit Getachew-Ethiopia
8.Kambua-Kenya
9.Willie Paul- Kenya
10.Ann Marie Mutesi – Burundi


Christina Shusho akiwa kwenye huduma na muimbaji wa Kenya Geraldine Hephzibah Oduor

Katika waimbaji wanaowania tuzo hizo nchi ya Kenya inaongoza kwa kutoa waimbaji watano katika nchi za Afrika mashariki, huku Tanzania tukitoka kimasomaso na mwimbaji mmoja ambaye tukijipanga vyema kwakumpigia kura nyingi ataibuka na tuzo zote mbili kwakuwa waimbaji wengine mfano kama kutoka Kenya kwakuwa wanawakilishwa na waimbaji wengi watakuwa wakigawana kura jambo ambalo litakuwa faida kwa watanzania kwa pamoja kumwezesha Shusho kuibuka na tuzo mwaka huu baada ya kukosa mwaka jana.

Lakini pia katika tuzo hizo mwaka huu kutakuwa na mchuano mkali kwa waimbaji wa nchi nyingine kama Afrika ya kusini ambako waimbaji nyota kama Ntokozo Mbambo, Solly Mahlangu, Keke, Uche,S’fiso,Hlengiwe na wengineo wanaowania tuzo mbali mbali huku kundi la Joyous Celebration likiingizwa kwenye kipengele cha tukio kubwa la mwaka kupitia recording yao ya 16.

Kumekucha sasa Mtanzania tuna mwimbaji mmoja tu ni wakati wa kuunganisha nguvu kwa pamoja ili tuzo hizo zije nchini kwa utukufu wa Mungu, na kupanua muziki wa injili wa Tanzania katika nchi nyingi zaidi.Utaratibu unafanywa kuhakikisha kura ambazo zimeanza kupigwa hii leo mpaka tarehe 29 mwezi huu.
Ili kupiga kura yako fuata maelekezo yafuatayo baada ya kuingia kwenye tovuti hiihttp://www.africagospelawards.com/nominate.html

VOTE NOW
AGMA 2012 VOTING GUIDELINES
1. Click on the ‘VOTE NOW’ button.
2. Register your email address, confirm and submit.
3. Check your email (inbox) and you will find the link to vote.
4. If you do not find the link in your email inbox, please check your junk mail folder.
5. Once you have connected to the voting page please make your selections and submit (you can only vote for one nominee from each category).
6. You do not have to vote in every category.