King’s Choir Kufanya Live recording, Morogoro

Ni tarehe 03 June 2012, Praise Team ya King’s kutoka mkoa wa Morogoro watafanya Live recording. Itakuwa ni Ibada ya kusifu na kuabudu kanisa la Canaan Calvary Assemblies of God, wakishirikiana na kwaya hiyo.

Tamasha hilo la uimbaji litarekodiwa kwa moja katika Audio na Video. Wakazi wote wa Morogoro na vitongoji vyake, Karibuni tumuabudu Mungu pamoja, tuone nguvu ya Mungu katika utendaji wakati tukimsifu na Kumuabudu yeye Aliye Hai.

Baadhi ya Wanakwaya kwenye picha

Tumsifu Mungu kwa wimbo huu ulioimbwa na King’s katika moja ya Ibada ya Jumapili, SIFA ZAKO ZIVUME

BUBELE&DIANA MINISTRIES Kuleta Uamsho wa Kusifu na kuabudu Afrika


Diana Kihayile akiongea kuhusu Afrika

Inapendeza kuona watumishi wanaoenda nje ya Nchi yao kuendelea na huduma na kuzidi kuwa na kiu katika kumtumikia Bwana. Pichani ni dada anayefahamika kama Diana Madida, alisikika sana na album ya MIMI NAJUA KWAMBA YESU ANANIPENDA. Ilikuwa ni baraka kwa wakazi wa kanda ya ziwa kumsikia na kuona nyimbo zake zikisambazwa sokoni mwaka 2003! Strictly Gospel ilipata nafasi ya kuzungumza naye na akaeleza safari yake kwa ufupi na maono aliyonayo kwa sasa. Utaweza kusikiliza na kuona video ya wimbo mpya AFRIKA alioufanya na mumewe Bubele E Kiyaile. Fuatilia chini habari kamili

Diana na Mume wake Bubele Kihayile

VIDEO YA WIMBO AFRIKA YETU

Diana Madida au Diana M Kihayile,ni jina jipya baada ya kuolewa mwaka 2006 na Mr.Bubele E Kihayile. kabla ya hapo au kwa watu wengi nimekuwa nikijulikana kwa jina la Diana Madida. Nimezaliwa na kukulia Mwanza Tanzania,kwasasa naishi Birmigham uk,mimi,Mr.Bubele na tuna watoto wawili wa kike,Rina Jodiah(2.4yrs) na Jaina Sasha(5.3mths)

Niliokoka june 1997, kupitia mikutano ya Moses Kulola na nikaamua kujiunga na kanisa la E.AG.T Imani kwa mchungaji Juliana Nyanda, hapo ndipo safari yangu ya huduma ilianza rasmi,1998 nilijiunga kwaya ya kanisa FAITH AMBASSADORS CHOIR, na baada ya muda Mungu alinisaidia nikaanza kuimbisha baadhi ya nyimbo,1999 niliendelea kukua kiroho na kihuduma nikaanza kuongoza ibada za kusifu na kuabudu ndani ya kanisa hilo na 2000 nilijiunga Kihayile band huduma hii Mungu alizidi kuizidisha na kuipaka mafuta na kupata nafasi ya kuhudumu ndani na nje ya kanisa.

2003 nilitoa solo album(MIMI NAJUA KWAMBA YESU ANANIPENDA)iliingia sokoni Tanzania kupitia Mamus distributors, ila hawakuweza kuendelea kuisambaza kwani niliondoka nchini mara baada ya kutoa album hiyo, 2004 Mungu alinifungulia njia nikaja masomoni Birmingham UK. ambapo niliendelea na huduma ya kusifu na kuabudu katika kanisa la Lighthouse chapel, 2008 kwa msaada wa Mr. Bubele niliweza tena kutoa album ingine ya pili (MILELE)ambayo niliingiza sokoni hapa UK na niliweza kuituma nyumbani kwenye baadhi za redio, nyimbo ambazo zilipendwa na waliosikia ni Uwe karibu nami, Tumeahidiwa ufalme mwema na milele. Baada ya hapo kwasababu siko peke yangu, nimeweza kuunganisha plan zangu kihuduma na mume wangu ambapo ni jambo la kumshukuru Mungu kwani naamini mmoja anaweza ua elfu ila wawili makumi elfu. Mr Bubele Kihayile is the perfect match from heaven to me, ni mentor wangu, mwalimu wangu, mtunzi wa nyimbo na muziki wote wa nyimbo zetu na mtumishi mwenzangu katika huduma. kwahiyo kwasasa tuna project mpya kama BUBELE & DIANA MINISTRIES ambapo tunatengeza album mpya au ya kwanza kama ministry, katika abum hii tunatajia kurekodi nyimbo 12 (kumi na mbili) ambapo zitakuwa out hivi karibuni(kufikia wakati wa summer) kwa msaada wa Mungu mpaka sasa tumesharekodi nyimbo nne na tumefanya video moja ya wimbo unaitwa Africa yetu.

Maono katika huduma.

Matarajio yetu ni kuona ufalme wa Mungu umetukuka duniani,we are created to worship and to usher his people into his presence. Ni matarajio yetu kuongeza uamsho wa kusifu na kuabubu kwanza nyumbani kwetu/Tanzania, Africa na duniani kote kwa ujumla, pia kwa kutumia muziki wa Africa kuleta uamsho ndani na nje ya afrika yetu. Tunaamini Mungu ametupa maono katika kuwafikia wengi kwanjia ya uimbaji kwahiyo in future tunategemea kuwa na Music organisation ambayo itakuwa ni kamili nikimaanisha kujumlisha mambo na nyenzo zote ambazo zinaweza kuinua, kupromote na kutangaza habari za Yesu kupitia muziki wa injili.

Mengineyo

Mungu ni mwaminifu siku zote hawezi kumwacha mtu wala kumsahau, hivyo tuendelee kuamini ya kuwa ni baba na rafiki wa ajabu, kama mtu ni mkristo/amezaliwa mara ya pili, asikate tamaa anapopita katika hali ngumu na asimwache Mungu anapopitia furaha tele. Pia kama mtu si mwamini ni vizuri aje kwa Mungu kwa kumwamini Yesu kwasababu Yesu ndiye njia kweli na uzima, pia asijione kuwa hastaili kuitwa mwana wa Mungu kwani Mungu mwenyewe amesema hapendi mtu hata mmoja apotee na hafurahii kifo cha mwenye dhambi hata mmoja!

Pia kama wakristo tuna wajibu wa kutubu na kuiombea ardhi(nchi) ambayo Mungu anakuwa ametuweka tuwe resident wa hapo,tutamke mema na tutabiri mema kwa nchi tukijua ya kuwa haki uinua taifa,na Mungu anatuangalia sisi kama gates/milango ya kuleta Baraka na neema juu ya nchi tunayoishi, hivyo tutamke mema siku zote na tusilalamike na kulaani na walaanio,pia tukumbuke kuwa vinywa vyetu vinaumba kwa hiyo kila tusemayo katika ulimwengu wa roho yanakuwa na hatimaye hudhiirika katika halisi/ulimwengu wa mwili.

Africa Praise Night – Ottawa

Upendo Kilahiro amealikwa nchini Canada kwa ziara ya mwezi mmoja ambapo jumamosi wiki hii atafanya huduma kwenye kanisa la Christ Chapel Bible Church jiji la Ottawa. Huduma atakayoifanya ina lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya Watoto Yatima wa Morogoro.

Amechaguliwa kuwa muimbaji kutoka Tanzania ambapo siku zote atakuwa Canada atafanya huduma ya uimbaji sehemu mbali mbali alizoalikwa na atakazoalikwa.

SIFA EBENEZER FOUNDATION kuzinduliwa Biafra!

Mwimbaji wa Injili kutoka Tanzania Sifa John anatarajia kufanya Tamasha kubwa la uimbaji ambapo atazindua album yake USILILIE MOYONI na huduma yake SIFA EBENEZER FOUNDATION siku ya tarehe 29/4/2012 viwanja vya Biafra.

Akiongea na Strictly Gospel dada Sifa anaielezea SIFA EBENEZER FOUNDATION “nina mzigo wa kusaidia watoto, vijana na mabinti wasiojiweza, kuwasaidia waondoke kwenye mazingira magumu, kutoshawishika kufanya vitendo viovu, kufundishwa ujuzi mbalimbali, kuinua vipaji vyao pia na kupatiwa semina mbali mbali za kiroho”.

“Mgeni rasmi atakuwa Emmanuel Nchimbi, pia ninawakaribisha wadau wote kuhudhuria siku hiyo waimbaji wengi wataimba na kumtukuza Bwana” alimalizia kusema dada Sifa.

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na dada Sifa kwa email, sifajohn@ymail.com

Hongera dada Kambua

Jumamosi iliyopita tarehe 7/4/2012 ilikuwa siku ya furaha kwa dada Kambua Manundu. Ambapo alifunga harusi yake na mfanyabiashara na mchungaji Jackson Mathu kwenye bustani Windsor Golf Hotel.

Walihudhuria waalikwa kadhaa na baadhi yao ni pamoja na Esther Wahome, Mercy Masika, Marsha Mapenzi, Alice Kamande. Ambapo Esther Wahome alimshauri “Najua inawezekana kuolewa na kuwa mwenye furaha, Nina ndoa yenye furaha kwa miaka 16 na nina watoto watatu”

Watanzania tunakutakia heri dada Kambua!

Nani Mshamba – Stara Thomas

Muimbaji wa Injili nchini Tanzania, Stara Thomas. Ameachia wimbo wake wa Nani mshamba unaopigwa kwenye vituo vya redio za injili nchini. Wimbo huo una maneno yafuatayo

“Aliye kwa Yesu ni mjanja,

Aliye kwa Yesu si mshamba,

Yuko kwenye mwanga, mwanga wa milele”

Stara akiongea na moja ya redio ya Injili amesema baada ya yeye kumpa Yesu maisha yake “wengi walinitenga na wengine kunidharau lakini mimi sijali maana mtu anayekuwa kwa shetani ni mshamba”

Album ya dada Stara NANI NI MSHAMBA iko tayari na itasambazwa mwezi wa nne.

Habari nyingine zinazosikika ni kuhusu Beatrice William aliyepata umaarufu kupitia Bongo Star Search naye ameokoka tarehe 7/3/2012 kwenye kanisa la Mikocheni B Assemblies of God (Mlima wa moto)

Alipoongea akiwa madhabahuni tarehe 9 Machi kwenye mkesha kuhusu uamuzi wake wa kumpokea Bwana Yesu alisema “Ni uamuzi wangu wa dhati kuokoka na akili zangu timamu. Mara nyingi nilipenda sana kuokoka lakini niliogopa kumbipu Mungu kama wengine wanavyofanya”

Kufahamu mengine kuhusu Stara Thomas fuatilia link hii

https://strictlygospel.wordpress.com/2011/02/21/stara-thomas-ameokoka/