Sauda Mwilima aimba na kucheza nyimbo za Injili Landmark Hotel!!!

saudamwilima

Akiandika katika ukurasa wake wa Instagram Mtangazaji wa Startv alisema “……hawa hapa ni kati ya wasanii walioimba ndani ya Landmark hotel, dah nime-enjoy sana nimecheza na kuimba pia huyu dada mwenye kitenge ni Upendo Nkone wengi mnajua uwezo wake wa uimbaji na huyu kaka Ni Edson Mwasabwite dah jamaa kanyanyua ukumbi mzima hadi mgen Rasm Mh Mwigulu Nchemba, watu wote tumeimba “Ni kwa Neema tuuuu na Rehemaaa ainuliwe Mungu aliye juuu”Hapa nilipo mimi ni kwa neema zake tuuu’ Kiukwel huu wimbo mzuri sana kama unajua mistari mingine tiririka hapa chini.” – Sauda Mwilima wa Startv

Inapendeza sana, Muziki wa Injili una nguvu, Karibu sana dada Sauda kwa Bwana Yesu kuna raha na amani ya kweli.

Babu wa Loliondo atangaza watu kumiminika upya, Apata maono mengine.

millard

Millard Ayo wa Clouds FM Alipokua akifanya mahojiano na Mchungaji Ambilikile Masapila maarufu kama Babu wa Loliondo

Hivi karibuni mtangazaji maarufu Millard Ayo katika kipindi chake cha Ampifaya alifanya mahojiano na Mchungaji Ambilikile Masapila na kuelezea kwa urefu mwanzo wa huduma yake ya kikombe, changamoto, walioiga kutoa vikombe, vipingamizi pamoja na waliokufa, ambao hawakupona hawakufuata masharti ya dawa.

Mwishoni mwa mahojiano Babu wa Loliando akasema kuhusu mafuriko mapya yatakayotokea hivi karibuni huko Samunge, alizungumza hivi

Siwezi kusema moja kwa moja kwamba ni mwezi wa tatu, ingekuwa pengine mpaka sasa tungeanza kupata watu wengi, na inawezekana ikawa mwezi huo wa tatu, au kabla au baada, mimi siwezi kusema moja kwa moja kwasababu kuna vipingamizi vingi tu, ambavyo Mungu anasubiri vitimie ndipo kazi hiyo ianze, Kuna miujiza mingi imeandikwa ndani ya biblia kitabu cha Mwanzo, Zaburi, Ezekiel, Ufunuo yapo maajabu mengi ambayo Mungu ameyaandika hayakutimia katika nchi ya Israel yatatimia hapa, Samunge, kwahiyo mafuriko ya watu watakaokuja si kwa ajili ya kunywa dawa tu lakini ni kwa ajili ya mambo mbali mbali kuja kuona miujiza ya Mungu itakayofanyika

Alipoulizwa ni maajabu gani yatakayofanyika akasema

“Si vizuri, sijamwambia mtu yeyote ba hata hapa kwako sitasema, isipokuwa mimi nimeyaona mengi tu nimeyaona tayari lakini Mungu hajaniambia tangaza napewa (Maono) kila wakati linakuja hili, linakuja hili napewa kila wakati lakini si zaidi ya labda nusu mwaka sasa

Ili kulinganisha habari ndipo mtangazaji Millard Ayo alipomuuliza Mchungaji Onesmo Ndegi ni maajabu gani hayo ya kwenye biblia

Mchungaji akasema “Hakuna muujiza ambao haujatendeka zaidi ya ule muujiza wa unyakuo, miujiza mingine yote iliyotabiliwa ilishatendeka kwa mfano ukisoma muujiza mkubwa sana ambao Mungu aliuzungumza kutoka Mwanzo 3:15 biblia inasema hivi nami nitaweka uadui kati yako na huyu mwanamke na kati ya uzao wako na uzao wake huo utakuponda kichwa na wewe utauponda kisigino, sasa hapa alikuwa anazungumzia juu ya ujio wa Kristo na ushindi wa Kristo dhidi ya nguvu za giza au shetani na ilishatokea na tunaishi katika kipindi hicho, Yesu Kristo alishakuja akazaliwa, na uwezo wake ukadhibitika ushindi dhidi ya shetani ulionekana pale msalabani, kwa hiyo hakuna muujiza mwingine ambao utasema kuanzia mwanzo haujatimia sasa kuna mtu anataka kuutimiliza, hakuna muujiza wa namna hiyo

Babu wa Loliondo alipoulizwa tena ana ushauri gani kwa Serikali juu ya maajabu  hayo makubwa yatakayotokea hivi karibuni akajibu

Nilitaka kusema kwa upande wa Serikali, nitasema ya kwamba Serikali iwe makini kupokea watu watakaokuja maana ni wengi, ni mafuriko kwa hiyo wawe makini”

Hata hivyo babu amewasamehe watu wote waliomsema vibaya “Kisasi ni kwa Bwana” alisema

–Millard Ayo

Kesha na Praise Power Radio, kila siku! – Erick Brighton

Kama wewe ni mpenzi wa Praise Power Radio. Erick sio jina geni masikioni kwako hasa usiku, na kila Jumamosi kuanzia saa 7:00 mchana hadi saa 10:00 Jioni kwenye Gospel Annointing.

Erick amekuwa ni mtangazaji mwenye bidii na kazi yake huku akionesha upendo kwa wasikilizaji wake wanaompigia simu wakati wa mkesha na kuomba nao pamoja.

Mbali na utangazaji ni mchoraji mzuri sana, na ni fundi wa kutengeneza transmeter na street Airway. Mara nyingi amekuwa akiwakumbusha wasikilizaji wake kuwa wakati wa kuokoka ni sasa kwa kuwa hatujui siku wala saa na kwamba mtu asitegemee kumuona Mungu kwa kusihi maisha yasiyompendeza.

Kanisa likumbuke kuombea Taifa la Israel – Robin Ulikaye

Kwa wakazi wa Mbeya,Rukwa, Songea, Iringa, Malawi, Zambia, Tabora, Iramba na Singida Jina la Robin Ulikaye sio geni masikioni mwao hasa kwa wale wapenzi wa Radio za Injili, ambapo Ulikaye anasikika siku za juma katika vipindi vya asubuhi na jioni pia Jumamosi mchana.

Ni Mtumishi wa Mungu na mtangazaji wa vipindi vya redio masafa ya 98.6 Ushindi Fm Radio iliyopo Mbeya, Tanzania!

    • Katika kuitangaza Injili miji hiyo na kuboresha vipindi vyake vya redio amekuwa mwenye mapenzi makubwa na nchi ya Israel na katika kipindi chake anachotangaza kila Jumamosi saa 12:00 Jioni, Anaielezea Israel na habari zake pamoja na mgogoro mashariki ya kati lakini pia vinahusiana vipi na unabii wa Biblia. Katika maelezo yake hayo mara nyingi anasisitiza kanisa kuliombea Taifa la Israel ili mapenzi ya Mungu yatimizwe sawasawa na Neno lake.

      Pia kanisa lisisahau kuombea Neema ya Wokovu kwa jamii ya wayahudi kwani pamoja na Neema kuanzia Kule bado jamii haijaijua kweli ya Wokovu unaopatikana katika Yesu Kristo Bwana Wetu.

      Mbali na Ijue Israel pia kaka Robin anafanya Praise and Worship Experience Kila siku za Juma saa 11 Jioni pia na Kurunzi la Matukio na Habari kila siku za Juma saa 3:00 Usiku.

Hongera Joseph na Adella!

Joseph na Adella Msami, tarehe 4 Septemba 2011 imekua siku ya kumbukumbu kwao kwa kufunga ndoa. Joseph Msami aliwahi kuwa mtangazaji wa Radio ya kikristo WAPO radio 98.0 Fm, kwa sasa ni mtangazaji wa TBC 1 Taifa.

Pichani Martha Mwaipaja akiimba wimbo wake “Kwa msaada wa Mungu tutashinda ya dunia” ambapo Joseph Msami na mkewe Adella wakicheza!

………Tunawatakia kila la heri, kwa msaada wa Mungu, mkafanikiwe na kuzidishwa!…..