MASWALI/MAJIBU

Bwana Yesu Asifiwe! ikiwa una swali lolote linalohusu huduma mbalimbali, wahusika wa huduma hizo, swali lolote unalopenda kuuliza, waweza uliza na ukapata majibu hapa. Na yeyote mwenye majibu asisite kutusaidia. Karibu na Mungu awabariki!

251 thoughts on “MASWALI/MAJIBU

 1. Habari ya uzima watu wa MUNGU
  Swali langu ni kutaka kujua ni kwa namna gan unaweza kufahamu kuwa una mzigo wa kumuombea mtu mwingine
  Au ntaelewaje ninauhitaji wa kumuombea mtu mwingine?

 2. Bwana Yesu asifiwe wapendwa.
  naomba kuuliza miaka ya kijana inaanzia wapi na kuishia wapi kulingana na bibilia

 3. Bwana Yesu asifiwe
  je ubatizo upi ni sahihi ambayo unahisha maji mengi? je ni kwa jina la baba na mwana na roho mtakatifu? au kama walivyofanya mitume(PETRO) Ubatizo kwa jina la Yesu kama ilivyo Matendo 2:37-38 na nyinginezo??????? ahsante na Mungu awabariki

 4. Swali langu ni kuwa katika biblia kuna mafungu yanayozungumzia kuhusu sabato na limekuwa likinisumbua kichwa sana! Je siku ya sabato ni ipi ijumaa, jumamosi,au jumapili? Asanteni sana by Justine kutoka Daresalaam

 5. shalooom watumishi wa mungu kwa jina naitwa Namnyaki Millya naishi Arusha NAPENDA KUTOA SHUKRANI ZANG KWA WATUMISHI WOTE WA SAFINA REDIO KWA UKUU NA WEMAWAOO WANAYO TOA KWAAJILI YA KUSAIDIA WATU MBALIMBALI …………ASANTENI SANA………. MBARIKIWE NA BWANA SIKUZOTE ZAIDI NA ZAIDI ””””””””””””””””””””AMEN//////////////////////////////

 6. Mbarikiwe wapendwa ningependa kupewa tafsiri ya jina ayoub,kenedy na namgoli

 7. Bwana Yesu asifiwe. Nimeona swali la mwisho kuuliza lilikuwa tarehe 18.10.2015. Je Blog hii bado inafanya kazi? Na mbona kuna maswali macheche tangu mwaka jana hadi sasa kuna nini hasa?

 8. Bwana Yesu apewe sifa,,wapendwa,huu ni wakati Wa kushukuru kwa kila hambo linalotokea Tanzania sasa,kwakua tuliomba sana kwa muda mrefu,sasa Mungu yupo kazini,tusinung’unike tuendelee kuomba.

 9. Wapendwa katika Bwana, Bwana Yesu asifiwe!

  Naomba kujua majina ya binadamu watatu wa kwanza kufa katika mafundisho ya Biblia.
  Mungu awabaliki wote.

 10. Halloo everyone,
  I am writing this from Nairobi Kenya.
  I am looking for the album ”Kwaya Ya Uinjilisti Ya Vijana Arusha Mjini” and precisely Nyota ya Baraka. The songs/album has already been pulled down from youtube. Where can i get several/selected songs in MP3 format at a reasonable price? I am willing to pay for the songs even if someone sends me the song files via gmail. My email ad is amutua17@gmail.com and am also available through +254723779627
  May God bless you all

 11. Nimeipenda sana hii web sit.Mi ni mpya kwenye hii web site ningependa kujua jina langu John maana ni nini

 12. kaka kila mmoja anayekufa alikuwa freemason?
  mastaa wakifa utasikia “alikuwa freemason”
  watanzania acheni ushamba wa kiroho.

  Mi nadhani ni bora kujichunguza kwanza wewe unatoka wapi, uko wapi na unaenda wapi, nasio kuanza kuwajadili wengine!

 13. Kizinga wa kizinga,

  Bwana Yesu asifiwe, napenda kufahamu utumiaji wa maji au mafuta, wengine wanamini kwa kujipaka, wengine kunywa wakimshirikisha Yesu, hii inakaaje kibiblia.

 14. Bwana Yesu Asifiwe.
  Biblia inasema kwamba ili kutambua nabii wa kweli ni lazima unabii wake uweze kutimia. hii ina maanisha kwamba kama unabii haujatimia basi nabii yule atakuwa ni nabii wa uongo. juzi tumeshuhudia kifo cha aliyesema yeye ni nabii wa kizazi kipya, Eliya AD2,.
  Kama mnavyojua kuna mada iliwahi kuwekwa mezani kwa SG kuhusu mafundisho ya nabii huyu, watu walijaribu kujieleza, wengine kwa jazba, wengine kwa kutetea nk nk, sasa kitu ambacho kinaumiza akili yangu ni kwamba je ni kweli Munuo alikuwa nabii wa ukweli? ni kweli kwa jinsi alivyowaaga waumini wake kwamba Mungu amemwandalia gari la moto liweze kumbeba? ni kweli kama alivyodai kwamba Mungu amemwita kwa sababu hapa duniani amezungukwa na maadui wengi sana? hebu wa SG tutumieni muda kidogo kujaribu kujibu haya ambayo yamezagaa mitaani.
  kwa taarifa kutoka ndani ya kanisa hilo zinasema kwamba Munuo alikuwa amefunga mkataba na lucifa, kwa kawaida lucifa huwa anatoa vibali vyake ambavyo yeye anaona kwamba vinafaa kwako kama ukivihitaji. kumbukeni wakati wa majaribu ya Yesu Kristo, shetani alitaka kumhonga Yesu ili amwabudu. sasa inasemekana kwamba jamaa aliingia kingi, at the end of the day, mkataba wake umeisha, alipokuwa ameenda kurenew, jamaa alikataa kata kata akamwambia kwamba ‘sasa nataka sadaka yako wewe mwenyewe’ hakuwa na ujanja kabisa. na ndiyo maana inasemekana alijua atakufa tarehe ngapi.
  Niliwahi kusoma gazeti lake la NEEMA KUBWA alikuwa akielezea kwamba yeye hatakufa, bali ataenda tu sehemu Fulani na kukaa huko maisha yake yote kwa sababu yeye ndiye Adamu wa pili. alidai Adamu aliyetarajiwa kuwa wa pili ni Yesu, lakini hakufanya yale aliyopaswa kuyafanya, na hivyo alilalamika sana na kudai kwamba si vizuri katika kipindi hiki kutumia jina la Yesu kwa sababu alishindwa kutimiza makusudi ya Mungu.
  hebu watumishi naomba tujadili kidogo juu ya jambo hili ili tuweze kufufua mioyo ya watu. pengine labda sisi ndiyo tuna matatizo. siku moja nilisikiliza CD ya Munuo alidai kuwa ‘watu wengi hawaelewi mafundisho yangu kwa sababu wapo gizani’ labdda pengine tuko gizani. hebu naomba udadavuzi na uchanganuzi yakinifu. kama kuna member wa hapo ajaribu kutusadia kama anajua ukweli wa jambo hili

 15. Wapendwa naomba kuuliza jina la JIMMY lina maana gani? Namba yang ni 0714614488

 16. Naomba kuulizia juu ya Ndugu Fanuel Sedekia, juu ya kifo chake, alikuwa mgonjwa, au alikufa kupitia ajali? Na kama aliugua aliugua na nini?

 17. Bwana Yesu asifiwe Mtumishi, mimi nataka kujua Manabii wa kweli kwenye Biblia na majina yao na kazi zao walizozifanya katika kumtii Mungu na maagizo yake.

 18. naweza pata hili wimbo kwa Kiswahili? Because he lives, i can face tomorrow, Because he lives, all fear is gone, because i know, he holds my future, and life is worth a living just because he lives

 19. Ni kwanini Yesu hakuchagua mitume wanawake na wala Dina hatajwi katika orodha ya watoto wa Israeli?

 20. kaka ivan samahani ndugu yangu swali lako halieleweki vizuri naomba uliweke vizuri hasa kwenye mseto una maanisha nini? ila kwa kifupi nilivyoelewa kuwa kama ni ndoa ya wawili hawa isipokuwa wakiwa ndugu wa damu hairuhusiwi kabisa tena kabisa. lakini kama ni wote wakatoliki wa roma wanaweza kuoana bila shaka.
  pia kanisa katoliki la roma linaweza kuruhusu ndoa za wafuatao wakristu wa LUTHERAN, ANGLIKAN BASI KWA KUWA UBATIZO WAO UNAKUBALIKA.lakini baada ya kibali kutoka kwa baba askofu wa kanisa la roma baada ya kuona na kuchunguza undani wa ndoa hizo.

  Kaka Ivan pia kama Mseto wa kuwa MME MOJA WAKE ZAIDI YA MOJA KANISA KATOLIKI LA ROMA HALIWEZI KURUHUSU NDOA HIZO KABISA KABISA. HATA KAMA MKE ATAWEZA KUOLEWA NA WAUME ZAIDI YA MOJA HAIWEZEKANI NI KATAZO KWA BWANA.
  Ndugu yangu Ivan pia kanisa la Katoliki la Roma haliwezi kuhalalisha ndoa za jinsia/jinsi mmoja yaani mwa mwanaume kwa mwanaume ama mke kwa mke ni dhambi na sheria au biblia inakataza kabisa katika maandiko matakatifu ya BIBLIA.
  Haliwezi wala halitajadili suala hilo kwa kuweka vikao vyake kama baadhi ya makanisa mengine yalivyoamua kuzihalalisha ndoa za mseto. ama kwa kufuata mashinikizo ya serikali zao au zenyewe kwa kudai ETI ni HAKI ZA KIBINADAMU. Kwa kifupi maelezo hayo nadhani yanaweza kujibu suala lako ulilo uliza.TUMSIFU YESU KRISTU.

  Kuhusu suala la watoto watakuwa upande gani kama ndugu kaka na dada wameoana hapo jibu ni la kushangaza sana. Tumesema kanisa katoliki haliruhusu ndoa za kaka na dada wa ukoo moja . jE WATOTO WATAPATIKANA VIPI WAKATI HATA KABLA YA KUFUNGA NDOA KUNA MUDA WA MATAYARISHO AMBAPO KANISA NI LAZIMA LIJIRIZISHE MAHUSIANO YA WAWILI HAO KWA MUDA MREFU KUSHIRIKISHA NDUGU WA PANDE MBILI WA KAKA NA KWA DADA SASA LIKIONA KUNA KITU CHA UKOO MOJA NI WAZI KANISA LITAKATAZA KABISA. KWA HIYO WATOTO HAWATAZALIWA. LABDA WAO WAAMUE KUVUNJA SHERIA NA KUFANYA DHAMBI BILA YA KUSHIRIKISHA NDUGU ZAO.hapo kanisa halina hoja.NA PADRE WALA HAWEZI KUFUNGISHA NDOA HIYO KAMWE

 21. kama kupenda nyimbo za mch abiud dhambi ,bas mi nihukumiwe maana huyu Bwana ninapo sikiliza nyimbo zake .Yesu anafanya mabadiriko ndani yangu.nimeokoka nipo t a g so najisikia vizuri sana mtu anapo tumika kwa Mungu kama Mungu atakavyo.AMINA

 22. SAMAHANI NAPENDA KULIZA .DHEHEBU YA ROMANA CATHOLIC INARUHUSU KUFUNGISHA NDOA YA MSETO KATI YA MKA MKAKA MROMAN NA MDADA MROMAN!?? NA WATOTO WATAKUA UPANDE GANI!? SAMAHAN MWENYE JIB ANAWEZA NI ANDIKIA HATA SMS.0765652108

 23. Shalom.Madhehebu yameanzishwa na nani?Je, Bwana Yesu pamoja na wanafunzi wake walikuwa na dhehebu?

 24. Asifiwe Yesu kristo!Ntapataje nyimbo za Catherine Kakundi Kituo kwenye mtandao?

 25. Ailers ushauri wangu kuhusu tabia ya Mpenzi wako kwanza mkanye kua hupendi mawasilino anayoyafanya na huyo mpenzi wake wa zamani, wakati ukilifanya hilo piga tena goti umuulize Mungu kama yeye ndiye aliye wako hasa kama uliomba kabla hujampata. Mungu wetu ni mwaminifu kama ulimwomba Mungu na alikujibu kua huyo ndio mwenzi wako basi atakupa njia ya kulishinda hilo jaribu. Neema ya Mungu ikutangulie kwenye kulishinda hilo.

 26. kwan uchumba wenu ulikushafika hatuwa ya kujikana kwa ndugu na jaamaaa na kama tayar basi tafuta ndugu ama jamaa na marafiki wenye hekima wasuluishe na kama bado usiano wenu haujatambulika basi mkanye na akizid kuonesha moyo mgumu achana naye kwan lazima waludiana tu……

 27. mpenzi wangu nahisi ananisaliti katika mapenzi yetu na mpenzi wake wa zamani kwani imekuwa busy kuwasiliana nae kiasi nimemkataza kuawasiliana nae hataki yuko radhi tuachane ila asiache kuwasiliana nae nifanyeje?nahisi ananipotezea muda ili baadae warudiane na mpenzi wake kwani ananiona mimi si muelewa kumkataza asiwasiliane nae,naomba msaada wenu

 28. Tendo la kutoa sadaka lilikiwepo toka enzi na enzi.sadaka ina kazi kubwa katika ulimwengu wa kiroho.kama ilivyo roho hai ndivyo na sadaka ina pumzi ndani yake.kama itatolewa kwa utaratibu unaotakiwa ile pumzi ya uzima huachiliwa ndani ya mtu na huleta matokeo kulingana na ulivyoinenea.kama utaitoa kwa toba,shukrani,pia kufungua mtu kutoka katika magereza ya kichawi/kigiza.

 29. Shalom naomba watumishi wa Mungu mnisaidie, je sadaka inaweza kumuokoa mtu? maana mara nyingi nimekuwa nikisikia watumishi mbalimbali wa Mungu wakisema toeni sadaka ili tatizo lako liishe sasa ina maana bila sadaka tatizo la mtu haliwezi kumalizika?

 30. Naomba ufafanuzi kuhusu LUKA 5:36-39, Yesu alikuwa na maana gani aliposema hakuna mtu atiaye kiraka kikukuu ktk vazi jipya? na ni nini maana ya viriba vikukukuu na viriba vipya? na divai inayotajwa hapo ni iipi? naomba msaada wenu

 31. Ubarikiwe sana dada Angel kwa swali lako zuri. Mungu alipomuumba mwanamke na mwanaume aliwapa majukumu wote sawasawa na uwezo wao.Hapo mwanzo MUngu aliweka utalatibu wa mavazi soma KUMBUKUMBU LA TORATI 22 Mstari wa 5.pia soma,WAKORINTHO WA KWANZA 14 mstari wa 40. Dada Angel kumbuka tunaishi ktk ulimwengu uliooza mambo hayaenendi kwa utaratibU mwisho soma UFUNUO 22 mstari wa 18 na 19

 32. shaloom mimini msichana nimemaliza chuo kikuu, nimeokoka na nampenda sn Yesu ila napendda kuuliza je ni dhambi kwa msichana kuvaa suruali na andiko lipi linazuia kuvaa suruali mtoto wa kike kwani napenda sana suruali.

 33. Shalom, ubarikiwe mama k, usiache kuwaeleza watu njia ya kweli ili kuujenga mwili wa Kristo,lazima watu tujue kuwa utajiri msingi wake ni kumcha Mungu.

 34. Kwa
  PENUEL mimi niko tayari nipe namba yako nitakupigia. Mi
  Namba yangu ni +97474027216

 35. Kwa kaka Musa Kisomo, namshukru sana Mungu kwa kukupa majibu mema uliyompatia ndugu aliyeuliza habari za utajiri ktk wokovu, 2 wakolintho 8:9 inasema Yesu alikuwa tajiri lakini kwa ajiri yetu alijifanya masikini hili sisi tuwe matajiri, pia 1 nyakati 29:12 Daudi anasema kuwa utajiri na heshima vyatoka kwako , nawe unatawala juu ya vyote, mkononi mwako mna uweza na nguvu , tena mkononi mwako mna kuwatukuza na kuwawezesha wote, haya na maandiko mengi sana ya mafanikio ni sababu tosha za kusimama na Mungu kama umeokoka hili shetani aondoe mikono yake michafu ktk baraka zetu, lakini pia tukumbuke kuwa cha kwanza ni kuutafuta ufalme wa Mungu na mengine yote tutazidishiwa, siyo tutapunguziwa tutazidishiwa, Matayo 6;33. Yesu alisema utaifaamu kweli na hiyo kweli itakuweka huru, nilipojua ukweli kuusu utajiri wa Kimungu , nilianza kukiri maandiko ya mafanikio kama ninavyokiri manandiko ya uponyaji,nilianza kutembea ktk kanuni za Mungu , mfano 2 wakolintho 9;6-12. Luka 6:38 nk, Mungu akaanza kufanya, nilikuwa ninauza nyanya kijijini kwetu, nazipeleka sokoni, ninatembea na ndoo mbili na nusu kichwani tangu hasubuhi saa kumi na mbili hadi saa tano na nusu, nilikuwa nikifika sokoni kichwa kinawaka moto , Ushuuda wangu zaidi unaweza kuusoma ktk blog hii , ktk sehemu inayosema Muhimbaji wa nyimbo za injiri awataja wazi wahubiri wa uongo. anaitwa Shai .. . nimeandika habari zangu na mambo ambayo Mungu amenitendea. Mungu awe nanyi wasomaji na azidi kututia nguvu , tumtangaze kwa ujasiri. Mama K

 36. Amina. Alphaxad hilo tatizo lako linahitaji kuombewa lakini kama ukitaka kuomba wewe mwenyewe lazima uwe na toba ya ndani iliyo nia ya maombi na zaidi hili ndio muhimu MPAKWA MAFUTA WA BWANA ijapokuwa tu warithi kwa haki ya mkombozi wetu YESU KRISTO lakini neema ya kufunguliwa katika vifungo vya dhambi ipo kwa wote na inakibali kwa wachache kama upo tayari nitakupa namba za simu tushirikiane kujenga hekalu la Roho Mtakatifu yaani mwili wako.Uzidi kubarikiwa.

 37. Bwana yesu asifiwe
  mi naisi ninamapepo yananisumbu na mahali nilipo hakuna uwezekano wa kupata mchungaji wa kuniombea. je ni sala gani ambayo naweza kujiombea mwenyewe yakuweza kuyaondoa?

 38. Mimi natafuta sana matoleo ya kwaya ya KKKT Arusha Uinjilisti yenye Album ya MKO TAYARI?na USIYUMBISHWE Kama kuna anayezifahamu album hizi na mahali naweza kupata

  MBARIKIWE WOTE

 39. mimi ni Jacob mathew, naomba kuuliza katika Biblia, YESU alifukuza watu waliotumia hekalu kwa kufanya biashara, je makanisa ya leo hayatapata adhabu hiyo kwa mahubiri nusu saa ila fedha haina muda mpaka ipatikane?

 40. Shalom!! Dada Grace
  Nashukuru Mungu anayenipa nafasi kupitia blog hii na kujiongeza kwa maarifa, nimeona ujumbe wako kuhusu matatizo hapo kazini kwako, kuna mambo mawii unahiotaji kumuuliza Mungu, moja ni kwamba aidha Mungu anataka utatue hayo matatizo ili akuinue au c mpango wa Mungu kuwepo hapo ndo mana vita inakuwa ngumu kwa kuwa Mungu hayupo ktk hiyo kazi, tulia kwa maombi umuulize mungu!

 41. Dada Gile shalom! Unapogundua kuwa unapendwa ni jambo la kumshukuru Mungu kwa sababu yapo mapepo ambayo huwatenga watu na kuwafanya wasipendwe wala kuthaminiwa. Kwa tamaduni nyingi duniani ni wazi kwamba mwanamke huambiwa (huchumbiwa) na mwanaume kwa kuwa wewe umeokoka hebu mwambie Mungu akupe mume maadam kama unaona ni wakati wako sasa, kumwambia kwamba unamuhitaji kunaweza kumfanya asikuzingatie sana wakati wa mahusiano hai akihisi wewe ndo mwenye wajibu wa kumea eti tu kwa sababu uitanguia kumwambia. Nakuhakikishia kwa jina la Yesu kama huyo ni mumeo mtarajiwa kwa maombi yako hata afanye ujanja gani kwako atakuja tu. Endapo kuna vitu kwako vinamfanya asiwe huru plz viondoe (sina maana uruhusu mzaha na dhambi) lakini kwa mtazamo wangu na uzoefu niionao bia shaka kijana bado anakusoma tabia namitazamo yako, omba Mungu shetani asipande pando baya ndani yako!

 42. Ndugu mima shalom! Bila shaka una roho wa Mungu ndio maana umehisi kama hilo jambo haliko sawa, mtazamo wangu wa rohoni ni kwamba studio unazozizungumzia zina upako wa giza na tukiendekeza tabia hiyo bila maombi na mwongozo wa roho wa Mungu tunaweza kuwa na nyimbo za biashara na sio za upako, kwa hiyo hata bidhaa nyingine ambazo zatoka tusikozijua tunatakiwa kuziombea ili kuzikabidhi kwa Yesu ndipo tutumie, lakini haina maana moja kwa moja kutotumia, tumsikilize sana roho mtakatifu kuliko chance au promo ambazo hata shetani aweza kupitisha hila zake! barikiwa msomaji!

 43. Ukisikia ndoa zinasumbua eti baba na mama hawaelewani muda mwingine si kwamba shetani anaharibu, hapana ni kukosa tu maarifa ambako kwaweza hata kuangamiza ndoa yako, nakupa ushauri huu mfanye mwenzi wako awe rafiki yako hapo utajikuta mnapendana na kuelewana sana kwa sababu mawasiiano yenu yanakuwa hayana vikwazo vingi. Kumbuka kwwamba Mungu alimuumba mwanamke ampe company mwanaume ambaye alikuwa peke yake(mpweke) na Mungu akaona si vema. so utashangaza kama umepewa mtu wa kupiga naye story halafu we huishikukasirika na kununa, huyo si shetani hebu badilisha mambo!!! Barikiwa!

 44. Shalom ndugu Regan,
  Nafurahi kuona unamfurahia mke wa ujana wako, Kubarikiwa kiuchumi ni haki yako na ahadi za Mungu katika uchumi ni nyingi hebu soma ISAYA 45:2-3, na uanze kuomba kwa kusimamia neno hilo, tambua kuwa mkono wa bidii utatawala na tunarithi baraka za Ibrahimu kwa njia ya kristo Yesu, kiri mafanikio muda wote kwa sababu Yesu amezichukua taabu na umaskini wako ili uwe na raha na utajiri rohoni na mwilini.ukihitajimaandiko zaidi endelea kufunguka hapa SG ili tuhakikishe tunamgaragaza shetani na umaskini wake.

 45. Shalom! ndugu mwalusamba upo sahihi kabisa kutaka watu wautanguliza kwanza ufalme wa Mungu hata katika mahubiri yao, lakini kuhubiri mafanikio pia ni sehemu ya ufalme wa Mungu kwa sababu huo utajiri wa fedha,mali na dhahabu ni wa Mungu hivyo ni sawa na kuwatamanisha watu waje kwa yesu ili wawe warithi wa baraka hizo baada ya kumpokea Yesu. pia kwa watu waliookoka ni vizuri pamoja na kufundishwa kuenenda katika kweli pia wakaambiwa habari za kumiliki mafanikio na nguvu na upako na uponyaji na kila karama njema kutoka kwa Mungu kwa jina la Yesu. Ubarikiwe!

 46. Shalom.

  Nimeshukuru sana juu ya kujibu swali langu juu ya DADA BAHATI BUKUKU kweli ndugu ninaendelea kusikiya na kununuwa manyimbo zake kwa IMANI niko nayo kwa DAMU ya YESU ata sasa nikifata nyimbo yake DUNIA HAINA HURUMA inanipa tena moyo wa upendo na kusamehe na ya kusonga karibu na YESU .

 47. Kwanini watumishi wengi wameacha kumuhubiri Yesu wamejikita na mahubiri ya mafanikio na baraka badala ya wokovu? nukuhu “TAFUTENI KWANZA UFALME WA MUNGU NA HAKI YAKE NA HAYO YOTE MTAZIDISHIWA”

 48. @Lusajo uko wapi? kama Uko dar vitabu viko sehemu nyingi kutaja sehemu chache CLC Posta, Mwenge, The Winners church na Efatha shop mwenge.

  @E&Mashiba, Ukiwa na Yesu hatakuacha uangamize, Yeye anawainua maskini na kuwafanya matajari, humwinua mtu mavumbini na kumweka jaani, huwaketisha watu pamoja na wafalme, Biblia imeandikwa utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake yote. Mengine Utazidishiwa. Mathayo 6:33

  @Salome Jeniffer Mgendi ana filamu nyingine inayoitwa “Chai ya Moto”

  @MUSA KISOMA ubarikiwe sana kwa kazi njema ya kujibu maswali

  @Felix Salingwa Uvumi huo unatufundisha kusimama kwenye nafasi zetu na kuwaombea. Pia na kusimama Imara kumtegemea Bwana Yesu sio watumishi wa Mungu. Kumbuka Neno la Mungu limeandikwa alaaniwe amtegemeaye mwanadamu.

  @Rova Olombi, tutamuuliza dada Bahati swali hilo, Endelea kubarikiwa usikiapo nyimbo zake zenye ujumbe mzuri.

  @Tegemea J, Utukufu kwa Mungu kwa kuipenda blog hii, wajulishe wengine pia. Endelea kutembelea – SHALOM MARANATHA!

 49. YESU ATUKUZWE, nimependa sana hii blog tangu nimegundua siku chache zilizopita, japa kua nimeona kuna watu wameuliza maswali yanayowatatiza hawajajibiwa. JEHOVA SHALOM!!!!!

 50. Bwana asifiwe naomba mbele masamaha juu ya swali yangu juu ya DADA mwimbaji BAHATI BUKUKU eti ameachana na mume wake ? ama nimesoma vibaya munisaidiye.

 51. je uvumi wa watumishi wa mungu juu ya freemason unatufundishan nini kwamaana watoa ushuhuda ni wengi nao huja baada ya matukio makuu mfano kifo cha kanumba?

 52. Kaka samweli Shalom!! Tatizo lako ni dogo sana,hayo ni matendo ya mwili, badilisha mtazamo wako na soma neno mara nying kwa sababu neno la Mungu likijaa ndani ya moyo wako hakika maneno mazuri ya kutia moyo, ya furaha na ushindi yatatoka kwako kwa sababu utakuwa na hazina njema. Usiache pia kuomba kama unavyoendelea, ubarikiwe

 53. Ama kwa hakika vijana tuna nguvu tena za kumshinda shetani, lakini kwa mwelekeo wa vijana tulio nao sasa kwa kweli maombi ni muhimu sana, lakini pia tupatapo nafasi kuwafundisha ili vijana tuwe na akili tusije tupwa huku na huko kwa mafundisho ya kishetani kama Paulo anavyomuambia Timotheo kwa habari za siku hizi za mwisho.Vijana tukimcha Mungu hata taifa litakuwa na mwelekeo mzuri katika kila jambo!!

 54. Bwana asifiwe, vipi Jenifer Mgendi hajatoa mchezo mwingine baada ya teke la mama? kama ametoa inaitwaje? Kama bado basi akitoa asisahau kucheza na bibi kigaloni muhimu sana hiyo

 55. nitapata wapi sehemu wanayo uza cd za mahubir kama ya benny hinn kenneth hagin moses kulola.mwakasege paster chris

 56. shalom wana wa S.G!!
  vijana ndio tegemezi katika kusukuma gurudumu au kwa lugha nyingine iliyopo katika bible tumeandikiwa sisi vijana maana tuna nguvu ya kumshinda yule adui shetani lakini kwa dunia hii ya sasa shetani amewavuta vijana wengi sana kwake naomba sana wana wa S.G tuungane tuwe kitu kimoja kama baba wa mbinguni alivyo pamoja nasi tuwaombee vijana kwani akipotea hata mmoja tutaulizwa.
  thanks,
  Regards,
  Regina.

 57. Shalom Dada Regina!! Ni kweli kabisa unajua kwa maombi ya mtakatifu mmoja ambaye biblia inasema akiomba kwa bidii yafaa sana naamini tunaweza kuibadili dunia tukianza kanisani kwetu na hatimaye ulimwengu mzima, tukumbuke sisi ni nuru ya ulimwengu, dunia ikiwa gizani tujiulize tunafanya nini?

 58. shaloom kaka Musa,
  Ahsante sana kwa jbu lako ila kwa sababu Mungu wetu ni wa upendo na umoja tuungane sote kuombea wenzetu waliotawaliwa na ibilisi.na Mungu wetu wa milele mwenye nguvu atusaidie ili tudumu katika uweza wake.

 59. Neema ya Mungu ipo kutuhesabia haki lakini si kutupa kibali cha kufanya dhambi kwa sababu waliozalia wa mara ya pili hawatendi dhambi kwa sababu roho wa Mungu huwaongoza ktk kweli yote yaani pamoja na kuishi maisha yanayompendeza Mungu.Ni muhimu kuwaombea wanaoshindwa na si kuwalaumu au kuwashangaa,ubarikiwe sana!

 60. shaloom,
  mm nina swali moja ambalo linanikera sana kwamba mtu anazifuata njia mbaya ambazo hazimpendezi MUNGU na bado analitaja jina la YESU ovyo akidai kwamba ameokoka je huo ni wokovu au ni nini kwa sababu mtu aliyeokoka unaweza kumtambua kwa matendo.

 61. Bwana Asifiwe watu wa Mungu! Naomba kama kuna mtu anajua mashairi ya wimbo wa MUNGU ANAKUPENDA na IKAWA MABINTI WAWILI (Iyaa iyaaa eeeh noah) za Upendo group, Kijitonyama.
  Asanteni

 62. BWANA YESU ASIFIWE ndugu KIBII kwaya iliyo imba wimbo uombao ni kwaya KUU ARUSHA MJINI ubarikiwe sana mpendwa

 63. ndugu kwaya iliyo imba wimbo uombao ni moja kati ya kwaya hizi kwaya kuu ARUSHA mjini ubarikiwe sana

 64. BWANA YESU asifiwe
  Nahitaji kujua albamu ya kwanza ya J Sisters (Bado Kickb) ilikuwa na nyimbo ngapi? na majina yake ni yapi?
  Na BWANA Awabariki

 65. kwako mina

  upande wangu sioni tatizo lolote kwa waimbaji wa injili kupata hizo promo. mfano tunapoenda kufanya shopping kununua bidhaa zetu je tunaangalia kuwa hizo bidhaa zimetoka kiwanda gani?.. na hata ukifahamu kiwanda, je unajua waliotengeneza kama wameokoka au hapana? bidhaa kubwa kubwa mfano magari yametengenezwa na watu wasiomjua Mungu lakini tunavitumia kwa utukufu wa Mungu hivyo hata wao wakiproduce bado wanafanya kwa utukufu wa Mungu….hata vifaa vinavyotumiwa kwaajiri ya mziki je aliyetengeneza alikuwa mwamini? au alitengeneza kwa makusudi gani? yote hatujui lakini imempendeza BWANA vitumike.
  natumaini nimekujibu

  ubarikiwe

 66. Bwana Yesu Kristo apewe sifa. ndugu wapendwa katika kristo mnaonaje hii hali ya watumishi wa Mungu hasa waimbaji kupata promo ya kuimba na lebo kubwa za duniani, tena lebo ambazo mara nyingi zinakuwa zinapromote muziki wa dunia. Naomba kupata ufafanuzi maana ni jambo ambalo linanikereketa sana hasa ukiangalia shetani ananjia nyingi za kupotosha wanadamu.

 67. jamani hii blog ina pendeza sana tunapo jadiliana kuhusu habari za kristo.

 68. Dada Agnes Martin, ukitaka kujua khs masomo ya mzaliwa wa Kwanza tembelea tovuti ya Mwalimu Christopher Mwakasege uulize na utapata ushirikiano http://www.mwakasege.org/

  Ndugu Megan, mafundisho yake hayako kwenye youtube, naamini kuna utaratibu unaowekwa kwa mama Rwakatare zitaanza kupatikana. Tutakujulisha. Kwa Mchungaji Lusekelo hatuna taarifa

  Marystella, ubarikiwe kwa kazi njema kwa kumjibu Reggan. Naamini amejifunza kitu

  Yusuph, unaweza kupata majibu ya maswali yako kutoka kwa wachangiaji wengine tembelea
  https://strictlygospel.wordpress.com/2008/09/18/swali-14/ Kuvaa Suruali
  https://strictlygospel.wordpress.com/2011/06/27/mungu-anajali-unavyovaa/
  https://strictlygospel.wordpress.com/2011/05/18/uvaaji-kwa-kina-dada/
  https://strictlygospel.wordpress.com/2010/11/30/wadada-muonekano-wa-nje/

  Mungu awabariki!

 69. Kaka Reggan,

  naomba nichangie kwa kukushauri kuwa kama umemwona Mungu akitenda katika ndoa yako, afya yako, ni Mungu huyohuyo anayeweza kukuinua katika uchumi! Endelea kutulia ukimuomba na ukisubiri muujiza wako.

  Inawezekana Mungu anakuchelewesha kukubariki kiuchumi maana anajua unaweza ukaanguka kwa maana hiyo ataendelea kukupa mitihani kadha wa kadha kabla hajainua uchumi wako ili apate uhakika kuwa hata kama akikubariki uchumi wako hutaweza kumuacha Angalia Kumbukumbu la Torati 8: 12-18. Kwa hiyo katika hali hiyo uliyonayo ya uchumi Mungu anataka aangalie uaminifu wako kwake uko kwa kiwango gani
  .
  Endelea kunyenyekea kwa Mungu ukifuata zile kanuni za utoaji za Mungu, zinalipa sana zile, yaani jinsi unavyojitolea kwa Mungu mali zako, haswa zile sadaka zinazouma kutoa huwa zina baraka mara dufu ya unachotoa. Kwa hiyo katika hali hiyohiyo uliyonayo ya uchumi mjaribu Mungu kwa kumtolea sana uone kama hatakubariki mpaka ukashindwa mahali pa kuweka!

  Mungu akusaidie!

 70. Bwana Yesu Asifiwe. Kwa nini Mungu ni rahisi sana kuponya kuliko kubariki? Nifuate vipengele gani, au maombi gani ili ni barikiwe? Zaka natoa, sadaka natoa, naishi maisha matakatifu. Mungu kanibariki kwenye ndoa na afya, bado uchumi tu!

 71. Bwana Yesu asifiwe.
  niko nje ya Tanzania nataka niwe naangalia mahubiri ya mama Rwakatare au Lusekelo vile vipindi wanavyorusha kwenye TV ntapata wapi hizo video. Nimeangalia sana you tube ila sijaona.. kama unajua website yeyote au kama huwa wanaweka you tube wanatumia jina gani asante.

 72. bwana Yesu asifiwe ni mtumishi natamani kupata cd ya maombi ya mzaliwa wakwanza akiwa tanga Mungu awabariki

 73. Bwana yesu sifiwe wapendwa” Biblia inasema dhambi zote zaweza kusamehewa bali dhambi ya kumkufuru ROHO MTAKATIFU hautasamehewa.
  ¡/Je, dhambiya kumkufuru Roho mtakatifu ni ipi?
  ¡¡/je,mtu kama amefanya dhambi ya kumkufuru Roho mtakatifu pasipo kufahamu kama amemkufuru ROHO.Je atasamehewa dhambi? Maana watuwengi hawafahamu ni kwanamna gani wanakufuru ROHO.bwana awatie nguvu.

 74. Ndugu Loy, Ni hakika Yesu alimshinda Shetani, Shetania anawasumbua wanadamu kwakuwa hawana Yesu ambaye alimshinda Shetani.
  Ili uwe mshindi dhidi ya Shetani ni lazima uwe unaye Yesu ndani yako. Yesu akiwa ndani yako na wewe unakuwa ndani yake, ndipo nguvu yake inakutetea dhidi ya shetani. Watu wanaosumbuliwa na shetani hawako ndani ya Yesu. Jambo lingine la kufahamu kusumbuliwa au kuteswa na Shetani si sawa na kujaribiwa au kushindana, majaribu hayana budi kuja kwani haya humfanya mwenye Kristo Yesu kuwa imara na thabiti kwakuwa nguvu ya Yesu iliyo ndani yake humshindia. Haya ndio mashindano na changamoto za hapa duniani ambayo yanaisha punde unapoiacha dunia.

  Ndugu Emmanuel MchaMungu,
  Si sahihi kabisa kwa mtu yeyote, awe mchungaji, ama kiongozi wako wa kiroho au ndugu au mwenza kukupangia kiasi cha sadaka za kutoa. Sadaka hutolewa kutoka moyoni, mawasiliano yako na Mungu ndio yanasababishaa wewe utoe kiasi unachoshuhudiwa kutoa na si vinginevyo. Ni vyema kuwa na nidhamu kwa Roho wa Mungu anavyokuongoza na si vyema kuongozwa na nidhamu ya woga kufanya jambo hasa la kiMungu.

  Mbarikiwe!

 75. Duh, bwana Mchamungu, kwanza imekuwaje mpaka mchungaji akajua mshahara wa mwumini wake? Nikipata majibu ya hapo ndo nitatoa mchango wangu.

 76. BWANA YESU ASIFIWE JE WAPENDWA NI SAHIHI KWA BAADHI YA WACHUNGAJI WETU KUTUPANGIA KIASI CHA SADAKA ZA KUTOA KWA VILE TU ANAJUA WEWE NI MFANYAKAZI AU UMEBARIKIWA KUA NA PESA NA MAANDIKO YAPI? NI SAIDIENI e_mail mchamungu@rocketmail.com SMS 0715840000

 77. Bwana Yesu asifiwe watumishi wa Mungu! Nina swali naomba nisaidiwe. Tunavyosema Yesu kamshinda shetani, ndiyo ni kweli kabisa Yesu kamshinda shetani sasa kwanini bado shetani anasumbua wanadamu?

 78. wazima jamani za jumapili naomba mwenye ni ya jackson mmbando yulle afisa masoko airtel ninashida nae nisaidieni no yangu 0712526362

 79. bwana yesu acfiwe. naomba mnisaidie no ya silas mbise wa radio wapo 98.0 fm. ya jijini dar es salaam

 80. nina swali. je kwa mwanamke kusimama na kuhudumu katika kanisa ni sahihi na kwa andiko gani linalompa fursa hiyo.

 81. Bwana Yesu Asifiwe unajua nini, Yesu Kristo alipo kuwa hapa duniani alisema ya kwamba inabidi tusimamie kweli nayo itatuweka huru kwa hiyo inatupasa kusimamia neno la Mungu nini linataka tufanye kwakuwa ndio chakula cha roho bila kufanya hivyo hatuwezi kukua kiroho ata siku moja kwa hiyo kwa mwezangu unayekaa na kudhani kuwa upo salama bila kusoma Neno la Mungu ambalo ni biblia kiroho inakuwa haupo salama natumaini ushauri wangu utakusaidia kwa kuwa imeandikwa simamia kweli nayo ita kuweka huru.

 82. hei nashukuru kwa hiyo link ya \Vitabu vya nabii Rick Joyner Mungu akubariki uliyeitoa.
  Regards, d’e….

 83. Line, nyimbo nyingi za zamani hazipatikani online kwa yeyote mwenye kufahamu anaweza kutusaidia. Patric Balisidya aliimba nyimbo nzuri natumai tutazipata hata kwa audio.

  Elinazo Kabialo, kwenye kibox unachokiona wakati wa kuandika Jina na email yako, ukiandika na kutuma swali tutaliona.

  Eric Esron, unaweza kununua Tenzi za Rohoni Amazon fuata link hii http://www.amazon.com/s?ie=UTF8&rh=n%3A283155%2Ck%3ATenzi%20za%20rohoni&page=1

  Shinji, Mungu akubariki kwa kazi njema ya kujibu swali alilouliza Samuel Golanga

  Shadrack Lazaro ni Mungu peke yake yeye ndiye yupo tangu misingi ya ulimwengu, na atakuwepo hakuna mwingine zaidi yake. Katika Waebrania 1:10 -12″Na tena, Wewe Bwana, hapo Mwanzo uliita misingi ya nchi, Na mbingu ni kazi za mikono yako. Hizo zitaharibika, bali wewe unadumu. Nazo zitachakaa kama nguo. Na mavazi utazizinga, nazo zitabadilika; Lakini wewe u yeye yule, Na miaka yako haitakoma”

  Amina …anwani ya Harris Kapiga
  P.O.BOX 383
  DAR ES SALAAM
  TANZANIA
  E-mail: alamazanyakati@gmail.com
  Mob:+255 715 484 737,+255 764 484 737
  Physical Address: Shekilango Rd, Sinza Kamanyola near King Palace Hotel.

  Roy Robert, Mungu anajibu maombi. Hatumlazimishi Mungu atujibu kama tunavyopenda sisi, Wengi tunapenda kujibiwa sawasawa na tamaa zetu zilivyo. Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia….2 Petro 3:9a. Endelea kuomba mpaka uone majibu yako yanatokea wala usikate tamaa. Warumi 8:26-27 “Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya roho ilivyo kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.” Muhimu zaidi ni kuwa mtakatifu, Mungu hasikii maombi ya wenye dhambi. Soma Isaya 59:2 “Lakini maovu yenu yamewafarakisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia”

  Lakini pia fuata links kuhus maombi mahali hapa
  https://strictlygospel.wordpress.com/2009/09/30/maana-ya-kufunga/

  https://strictlygospel.wordpress.com/2010/12/30/majibu-ya-maombi-yakichelewa-ni-nini-cha-kufanya/

  https://strictlygospel.wordpress.com/namna-ya-kuomba/

  @d’emmanuel, Vitabu hivyo unaweza kuagiza online http://www.amazon.com/s/?ie=UTF8&keywords=rick+joyner+the+final+quest&tag=googhydr-20&index=stripbooks&hvadid=3188557199&hvpos=1t1&hvexid=&hvnetw=g&hvrand=564500424397408142&hvpone=&hvptwo=&hvqmt=b&ref=pd_sl_4v1eh5hwbp_b lkn pia kama kuna anayefahamu maduka ya vitabu anaweza kuelekeza.

  ….MUNGU AWATENDEE MEMA NYOTE…. AMEN

 84. Shalom, naitwa D’e natafuta mahali ambapo naweza kupata VITABU VYA NABII RICK JOYNER 1.THE FINAL QUEST NA
  2.THE CALL

 85. Bwana Yesu acfiwe wapendwa, mimi nataka kujua kwa nini maombi hayajibiwi? cyo yangu tu kuna watu wengi ninawafahamu wana matatizo na wanaomba kweli mpaka na kufunga lakini kinachonishangaza ni kwamba majibu hakuna, je tatizo ni nini?

 86. bwana acfiwe wapendwa, naitwa dada naomba email ya haris kapiga. mungu awabariki

 87. Bwana asifiwe! ,pole na majukumu ya kuitangaza na kuineza injili. Swali. Waebrania sura ya kwanza inazungumzia habari ya mtu mmoja merkzedeck,mtu huyu inasemekana hana mwanzo wala mwisho wa siku zake, je mtu huyo ni nani? Naomba ufafanuzi wako mtumishi.aksante na kazi njema!.

 88. Nimefurahi sana kupata web site ya wapendwa,ningependa kumshauri ndugu yangu samwel golanga anayeuliza kuwa mawazo machafu yanapokuja na kukemea anakuwa ametenda dhambi? jibu si kweli anakuwa ametenda dhambi,dhambi unatenda unapokubaliana na hayo mawazo au maneno unayoambiwa na mtu yaliyokinyume na neno.mfano shetani alimwambia Yesu ukinisujudia nitakupa milki zote za dunia,lakini Yesu alimpinga kwa neno.

  Ndugu samwel wakati mwingi ukidumu na ktk maombi na neno mawazo machafu hukosa nafasi kabisa moyoni mwako,ni jaribu tu kemea litaisha.na mara nyingi shetani huleta mawazo kwa kile ulikuwa unakipenda ikiwezekana urudi nyuma.
  Maombi yanaudhibiti mwili.endelea mbele wewe umeokoka na hakuna dahambi ila ukikubaliana na hayo mawazo machafu kuanza kuyatafakari dhambi ndipo inaanzia.

  kwa mfano kumuona mtu furani ni mzuri si dhambi ila unapowaza mambo machafu mfano ukimpata ungeweza zini naye ndo dhambi.

 89. Hello WanaSG, Shalom!
  Ni wapi nawezanunua kitabu cha Nyimbo za Wokovu au Tenzi za Rohoni online?
  Natanguliza Shukurani

  E. Esron

 90. Napenda kujua kama kuna yoyote anayeweza kunisaidia kupata nyimbo za injili zilizoimbwa na Patrick Balisidya, sikumbuki title ya album lakini baadhi ya nyimbo ni kama Mwanamke mwema ni taji ya mumewe, halafu nyingine ina maneno kama “lakini mimi najua mteteaji wangu yu hai, na siku moja atasimama juu ya nchi..”

  Pia naitafuta sana kanda ya Uraia wetu haswa ni mbinguni, waimbaji ni kwaya ya kolandoto shinyanga, ni ya miaka ya tisini hivi kama sikosei. Natanguliza shukrani!

 91. Mpendwa Nickson, wimbo huo uliimbwa na Rose Jeffa, unaweza kuusikiliza Youtube kwa kutumia hii link. Ubarikiwe!

 92. YAKOBO ALIOA BINAMU YAKE, IBRAHIMU ALIOA BINAMU YAKE – INFACT KWA UTAMADUNI WA AFRICA YA KATI HICHO NI KITU CHA KAWAIDA SANA. KWA HAPA TANZANIA WAISLAM WAMERITHI UTAMADUNI HUO. WAZANZIBAR, WARANGI NI BAADHI YA MAKABILA AMBAYO NI KAWAIDA KUOANA. KITAALAM SIO VIZURI SANA KWA SABABU YA KUZUIA MAGONJWA YA KURITHI MFANO KAMA UKOO WENU UNA PUMU AU WAGUMBA FIKIRIA MADHARA YATAKAYOTOKEA. UKIULIZA KIBIBLIA NI MPAKA UWE NA UWEZO WA KUTENGANISHA KATI YA NENO LA MUNGU NA UTAMADUNI WA NENO LA MUNGU LILIKOPITIA.

 93. JAMANI MIMI NAOMBA MNISAIDIE KUJIBU HILI SWALI “JE KWA WAKRISTO MTU NA BINAMU YAKE WAWEZA KUOANA? NAOMBA UTUMIE REFERENCES YA BIBLIA KUNIJIBU”

 94. Bwana YESU asifiwe.. Nawashukuru kwaajili ya web hii make ntaweza kupata msaada sana mm niliye bado mchanga ktk wokovu. Naomba msaidie jinsi ya kupata wimbo unaosema “NILIANZA SAFARI KUTAFUTA AMANI” ni zamani kidogo make nlikuwa mdogo sana ila mwimbaji simkumbuki. BARIKIWA SANA.

 95. nini maana ya kutamani na ni wakati gani kutamani kunahesabika kuwa ni dhambi na siyo dhambi?

 96. Bwana Yesu asifiwe naomba kuuliza ratiba ya mwalimu Christopher Mwakasege kwa mwaka huu mkoa wa dar es salaam ikoje.Barikiwa

 97. Bwana Yesu asifiwe ningependa kujua je fungu la kumi la kila upatacho ni wapi hasa linalenga kupelekwa? na je kwenye mbegu fungu la kumi linafaaa kutoa? na jee malimbuko ni mahali gani hasa yapaswa mtu apeleke? ninaomba kujua zaidi.

  Mungu atusaidi tuzidi kumjua yesu

 98. Mimi ninashida na kitabu cha mafundisho kuhusu mzaliwa wa kwanza cha mwl Mwakasege.

 99. Ndugu Daniel unataka uombewe ili upate mchumba mzuri,je uzuri wa aina gani wa sura au tabia,kumbuka neno lasema UTAPEWA WA KUFANANA NAE siyo sura, na kama ulivyo ujijuavyo ndivyo utakavyopata wa hivyohivyo,jitunze upate mzuri kama wewe ni ovyo usitaraji kupata mwema ng’o, sikuombei ila nakutakia Mungu akupe wa kufanana nawe, amen.

 100. Nataka Album ya John Lissu,ananibariki sana na nyimbo zake za kuabudu,nikipata na namba yake nitashukuru

  napatikana katika namba 0717 450 300

  Nicholaus NNJONGE

 101. Bwana Yesu asifiwe

  Mimi ni kijana ambaye nimeokoka na namtafuta Yesu kwa nguvu sana kwani nimeachana na matendo mabaya nahisi ni machukizo kwake, ila kuna kitu kimoja ambacho huwa kinanijia yaani mawazo machafu lakini huwa najaribu kukemea sana kila yakija ila huwa sitelezi kwa kuhofia kumtenda Bwana wangu dhambi, Sasa nlitaka kujua hayo mawazo yakiniingia huwa natenda dhambi au ndio jaribu natakiwa nilishinde

  Nitashukuru sana kwa mchango wenu.

 102. Bwana asifiwe, mi naomba kufahamu hivi mke wa sedekia alijifungua mtoto gani?

 103. Ndugu Kemi,
  Kuhusu TALAKA na UASHERATI.
  Maelezo ya ndugu Bernard ni ya kina kama alivyoyarejea Maandiko. Katika kuyaweka sawa napenda kuongezea hili: Kwamba mke anapochumbiwa hupaswa kuweka wazi kwa mchumba wake mahusiano yote aliyokuwa nayo na wanaume wengine kabla ya kuchumbiwa. Juu ya ufahamu huo mwanaume anayemchumbia hufanya uamuzi wa kuendelea naye au kumuacha. Mwanamke anapomficha mchumba wake na kisha kuolewa, nao wakaishi vizuri kwa miaka labda 20, halafu yule mume akaja kujua kuwa kabla ya yeye kumuoa, yule binti kumbe alikuwa nyumba ndogo ya baba yake, basi huo ndio uasherati unaozungumziwa katika Biblia. Yaani ‘unconfessed sin’. Lakini kama alimueleza jambo hilo naye akaamua aendelee naye, basi nguvu ya kosa hilo hukoma katika ile confession hata likiibuka huko mbele hukosa nguvu lisiwe na madhara yoyote. Tena unapoyarejea yale Maandiko utaona kwamba Kristo anatoa ruhusa ya kumuacha mwanamke muasherati na si mzinzi hata wengi wetu tumeyachanganya mambo hayo mawili na kuyafanya ni moja kinyume na Maandiko. Kristo amesema wazi kuwa hakuja kuitangua TORATI. Torati inatoa adhabu ya kifo kwa mzinzi. Kwa hiyo mwanamke mzinzi haachwi bali huuliwa! Mwanamke anayeachwa ni MUASHERATI tu,ndio maana Kristo katika talaka hakumzungumzia mzinzi. Nayo adhabu hiyo haijawahi kuondolewa ila wigo wake Kristo ameupanua. Kwamba kuanzia siku alipoyatamka maneno hayo, wengi tunao acha wake zetu nje sababu ya uasherati, tunajitumbukiza na watu wengi katika kesi ya uzinzi bila kujua. Kwa vile leo hii hakuna aliye safi wa kuweza kuitimiza adhabu ya kuwapiga mawe wazinzi hadi wafe, ndio maana tunawaona wakizurura mitaani hata wametuaminisha kuwa hakuna adhabu! Leo kuolewa na kuachana ni fashion. Bali ukweli ni kwamba adhabu ipo, haijawahi kuondolewa, nasi wazinzi wa leo tumekwisha uawa kiroho licha ya kuyaona makasha yetu mitaani, kiroho Mungu amekwisha tutenga Naye. Jamani jihadharini!!!

  Ck Lwembe

 104. Kwa mychoir,

  Yawezekana kukawa na kanda zaidi ya moja zenye title “SIKU YA KUFA KWANGU”. Lakini mojawapo, ambayo pengine nawe ndiyo unayoihitaji ni ile yenye nyimbo zilizoimbwa na ndugu EDWIN NGOSO. Inaweza ikawa rahisi kuipata kanda hii katika maduka ya kanda jijini Nairobi kwa sababu nyimbo hizo zilirekodiwa Nairobi na album ikasambazwa kutokea hapo hapo Nairobi.

 105. Wapendwa huwa inaniuma sana nionapo waislam katika kona mbalimbali za jiji la dar wakiukashifu ukristo,kwa jinsi tulivyofanywa kondoo huwa ni wapole tunavumilia maana tunajua tunamwabudu nani ,ajabu kuna ndugu zangu wapendwa CHRISTIAN POWER IN JESUS. hao huuchambua uislam na kuifundisha iman ya kikristo kwa undan,week iliyopita walikuwa Ubungo mataa pale wanatupa gospel na kutujuza jinsi waislam walivyopotea, Mbuzi hao wameandamana na kuwaleta police wamebeba spika za CPJ ili muhadhara huo usiendelee, tunahitaj mihadhara hiyo iendelee ili kwamba tuwe na majibu waislam wanapotutusi na iman yetu ,tunafanyaje ili wapendwa hawa wawe free kujibu kashfa za waislam wanazotoa dhidi ya Ukristo?

 106. shalom..naomba mniombee nipate mchumba mzuri..kwa ushauri no.0718689848..god bless u

 107. free mason kwa nini inaonekana inachukua nafasi kwa kasi alafu hakuna hatua zinazochukuliwa kwenye vitabu vya dini?..inatakiwa vichapishwe vitabu kupambana na free mason..hiyo itasaidia

 108. Bwana apewe sifa Dada Betty Kipala neno unapouliza pia na mimi na jiulizaka kuhuzu ile wapime pia kutufafanuwa ile tendo ya MAJI ama MAFUTA na sisi pia tulize Roho yetu.

 109. Wapendwa katika Yesu Kristo Shalom, naomba kupata majibu kwenu kwamba nimesoma habari za kuenea kwa injili hapa Tanzania na kwingineko.Mfn hapa Tanzania hatuna miaka mingi sana ya kuenea kwa injili ni kama miaka mia hivi na ushee.Swali,je wale wote waliokufa kabla ya kuipata hii nuru ya Injili watahukumiwaje wao kama hawakusikia kabisa habari za Yesu na matendo yake?Vipi kuhusu maandiko juu ya hili?Mbarikiwe

 110. Ndugu Exaud Gadiel Minja Bwana asifiwe kwa swali yako kuhusu pombe ama kila kitu ya ulevi. ndungu Mungu anakupenda sana tena sana ujuwe wakati neno ya Mungu ilipoanza mimi na wewe atukuwa bado kuzaliwa . tunafata sheria ya Mungu kwa mandiko na kwa IMANI ujuwe kaka kuko fasi mingi inasema sana juu ya pombe ndani yake ni makelele.na usome ku WALAWI 10:8-10 na ikisoma unijibu nikupe ingine enye itakusaidiya

 111. Naomba kupata maandiko kutoka Biblia Takatifu kuhusu kunywa pombe, kuwa muhudumu wa pombe (ajira), kufanya biashara ya pombe na kumpangishia mtu nyumba kwa ajili ya kufanya biashara ya pombe kama ni dhambi au chukizo mbele za Mungu.

 112. mimi nimeota naongea na mungu huku akiwa amelala usingizi maana yake nini?

 113. Bwana Awabariki! Tafadhali mnisaidie kunielekeza kwa shirika lolote la Waaminio wanaoamini ujumbe wa Nyakati za Mwisho Uliohubiriwa na Ndugu wetu William Marion Branham lililo karibu na Usa River, Arusha. Ningependa kushiriki nao hapo kesho na niko MS-TCDC, Arusha (USA River)

 114. Kibii, wimbo wa nitume mimi bwana,

  3rd verse,
  ulinambia nisiogope,
  nitapata ujasiri mwingi kutoka kwako

  nitume mimi Bwana,
  nitume mimi Bwana
  nitume mimi Bwana
  Nitume mimi Bwana

 115. Bwana Asifiwe
  Niliweza kutizama filamu Joto la Roho na nikabarikiwa.
  Bwana Yesu awabariki ili muendelee kutubariki.

  Nitawezaje kupata kanda ya video Joto la Roho?

  Inshalla

 116. Bwana YESU asifiwe sana Jee ndugu naweza kupata jee adress Email ya Mwimbaji BONY MWAITEGE nataka kushirikiana naye katika Email.

  Aksanti
  KISS KISULA

 117. naomba nielekezwe kwa chuo cha watume na manabii cha wakristo(kenya) ambaye mwanzilishi wake ni bwana mmoja toka australia.

 118. wapendwa bwana asifiwe,
  nimeipenda hii blog,inafundisha mema na mazuri,tulizoea kuona blog za kidunia tu,wabarikiwe walioanzisha hii,nimeikuta kibahati bahati tu nikiwa kwenye internet.

 119. bwana yesu asifiwe naomba mnitumie mwimbo wa manukato wa mtumishi marehemu Fanuel Sedekia

 120. Napenda sana video za mahubili na mafundisho ya Mzee Moses Clula na Daniel Clola ila nashindwa jinsi ya kuzipata, naomba msaada wenu. Mbarikiwe!

 121. Bwana yesu asifiwe wana wa kristo mimi nauliza kitabu cha mitimingi cha nguvu iliyopo katika jina lako nitakipataje nakihitaji sana.

 122. Bwana Yesu apewe sifa.
  Naomba kuuliza, mme wangu ananisaliti yaani anazini na mwanamke mwingine. Je naweza kutumia andiko gani la kuteketeza roho chafu ya uzinzi na lipi kwa mwanamke anayezini na mme wangu? Maana kwenye biblia hamna sehemu inayoruhusu kuachana mme na mke? Naomba msaada wenu tafadhari.

 123. NI KWELI KAMA ALIVYOSEMA PRECIOUS, FUNGU LA KUMI NI KATIKA BASIC SALARY NA SIO NET SALARY NINA USHUHUDA MZURI SANA KUHUSU SEHEMU HII. NILIWAHI KUACHISHWA KAZI KUTOKANA NA KUTOA FUNGU LA KUMI KUTOKA NET SALARY KWANI MUNGU HAKUWA MLINZI WA KAZI YANGU.
  PIA IELEWEKE KWAMBA UTOAJI WA FUNGU LA KUMI NI AMRI TOKA KWA MUNGU NA SI OMBI!

  KWA USHUHUDA ZAIDI WASILIANA NAMI KWA 0754/0658 558 058.

  Kutoka SG: Ndugu Japhet, Ingekuwa vizuri zaidi kama ungetafuta muda ukauandika ushuhuda wako hapa ili uweze kuwafikia wengi badala ya mtu mmoja mmoja kukupigia simu. Lakini amani ya Mungu iamue moyoni mwako.
  Mungu akubariki!

 124. MIMI NINA SWALI JE WAKATI ULE JK KAPELEKA MUSWADA BUNGENI TANZANIA KUJIUNGA NA OIC NA KUANZISHA MAHAKAMA ZA KADHI ILIKUWA INA MAANA GANI?KWA WAUMINI WA DINI ZINGINE?

 125. Watumishi wa Mungu aliye hai nawasalimu kwa jina la Yesu,
  Nesi napenda nikujibu kuhusu swali lako kuhusu fungu la kumi. Fungu la kumi unatoa 1/10 ya mshahara wako kabla haujafanyiwa makato yoyote.
  Ubarikiwe.

 126. Ndugu uliyetumia jina la Nesi,

  Ili kupata kanda za miaka ya 80 na 90 unachotakiwa kufanya ni kutufahamisha, kupitia email yetu ya strictlygospel@yahoo.co.uk, majina ya kanda unazohitaji nasi tutazitafuta na kisha tutawasiliana nawe namna ya kukutumia kanda hizo.

  Huu ndio utaratibu unaotakiwa kuufanya.

  Mungu akubariki na tunakusubiri ili tukuhudumie.

 127. Je fungu la kumi kwa mfanyakazi MFN,serikalini au tasisi nyingine yoyote ni katika TAKE HOME au ni mshahara wote kabla ya makato?MFN MALAKI 3:10

 128. Je ni vyema kwa watumishi wa MUNGU kujiingiza katika siasa,hapa nalenga wachungaji,manabii n.k

 129. Bwana Yesu asifiwe wapendwa. Mungu awabariki sana kwa kazi njema mnayoifanya, ama kwa hakika hii ni injili kamili. Shida yangu ni kwamba naomba contacts za pastor Steve Wambura kwa yeyote anayemfahamu.
  Mungu awabariki.

 130. Yesu apewe sifa! nilikuwa naomba kupata contact ya John paul f pocble.
  MUNGU WA ISRAEL awalinde

 131. Bwana apewe sifa. mimi niko wilayani sengerema napenda kuuliza kuwa kwa nini mikutano ya Maboya haifiki wilayani?

 132. Shaloom Wapendwa.
  Mimi ni muimbaji mchanga wa nyimbo za injili.
  Niko na kazi ya audio ambayo iko tayari na ni nzuri.
  Ninaomba kupata sponsor/Promoter wa kunisaidia ili na mimi niweze kufikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa watu wengi zaidi. Kusema kweli Financially siko vizuri ndo maana nahitaji supporter at least nyimbo zangu zisikiwe na Wengi ikibidi nifanye hata video, Naamini zitakuwa msaada na faraja kwa wengi.
  Mungu awabariki!

 133. Shalom wapendwa katika BWANA.Ninaomba kuuliza jambo hapa,KIBIBLIA KUNA UMRI MAALUM WA KUOA AMA KUOLEWA?Mimi nina miaka 26 nina elimu ya chuo kikuu na ninafanya kazi.Nimekuwa katika wakati mgumu sana wakati ninapojiuliza kama nitakuwa nimewahi kuwaza suala la kuoa ama lah.je kuna faida ama hasara za kuwahi ama kuchelewa kuoa au kuolewa?KWENU WANDUDU.

 134. Bwana asifiwe wote wanaosoma kipindi iyi. kweli nimesoma juu ya ndugu lipoandika juu ya UNAFIKI zaidi mimi ndio ya kwanza mbele ya Mungu juu ya UNAFIKI kwa sasa nimechanganika juu ya neno fulani Mungu anisamehe ginsi mwili inaponisumbuwa sasa tumeachana na bibi baada ya miaka 26 sasa nitafanya nini sasa juu ya tamaa ya mwili watumishi mupime kunisaidia sasa niko apa Ulaya na maisha ni ngumu bila bibi

  ile ndio swali yangu

  Mungu wa mbingu awabariki sana kwa kazi nunapofanya kutafuta kondoo ya Mungu

  Amen

 135. Kwako Laizer,

  Napenda nielezee maana ya neno “Unafiki” kama ninavyolielewa katika biblia.

  “Unafiki” ninavyolielewa mimi kama linavyotumika katika biblia, ni hali ya mtu kujifanya kuwa ni wa namna fulani inayofaa wakati katika hali halisi hayupo hivyo kama anavyojionesha. Katika mambo ya rohoni unafiki ni hali ya mtu kujifanya kuwa ni wa kiroho kwa viwango vinavyokubalika au vinavyotakiwa na Mungu, wakati katika hali halisi hayupo hivyo. Mfano, mtu kwa nje anaweza akajionesha kuwa hanywi pombe, havuti sigara, hafanyi uasherati au uzinzi, hasengenyi, hasemi uwongo, haibi, n.k.,lakini mtu huyo huyo kwa ndani anayatamani na kuyafanya yote. Kujionesha kwa nje kuwa ni mwema tofauti na alivyo ndani inakuwa ndiyo unafiki wenyewe. Nafsi ya mtu inapokuwa haipo katika uhalisia wa kile anachoonekana nacho kwa nje anakuwa na unafiki.

  Pia wakati mwingine, “unafiki” inaweza kuwa ni tabia ya mtu kujifanya kuwa anaamini sana juu ya jambo fulani na analifuata, anaweza akawa anasema kuwa anaamini sana juu ya Kristo, wakati katika nafsi yake haamini chochote, amekuwa ni mtenda dhambi tu wa kawaida, anawaaminisha wengine wamwanini hivyo wakati yeye mwenyewe hayupo hivyo, huo nao ni “unafiki”.

  Kwa kingereza neno hili “unafiki”,
  linaitwa “Hypocrisy”. Katika kitabu cha Cambridge Advanced Learner’s Dictionary, neno “Hypocrisy” limetafsiriwa hivi; when someone pretends to believe something that they do not really believe or that is the opposite of what they do or say at another time, [Hypocrisy].

  Katika biblia, neno “unafiki” tunaliona maeneo mengi tu, maeneo yote tunayoweza kuliona neno hili, yanaashiria kuwa unafiki si jambo jema kwa binadamu anayelifanya. Miongoni mwa maeneo machache ambayo tunaweza kuliona neno hili ni katika, Zaburi 12:2, ambapo tunasoma, “Husemezana yasiyofaa kila mtu na mwenziwe, Wenye midomo ya kujipendekeza; Husemezana kwa MIOYO YA UNAFIKI”, Pia katika, Luka 20:47, inasomeka, “Wanakula nyumba za wajane, KWA UNAFIKI husali sala ndefu. Hao watapata hukumu iliyo kuu”. Warumi 12:9, imeindikwa, “Pendo na lisiwe na UNAFIKI lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema”. 2Timotheo 1:5, “nikiikumbuka imani uliyo nayo ISIYO NA UNAFIKI, ambayo ilikaa kwanza katika bibi yako Loisi, na katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo. Pia, Marko 12:40, Mathayo 23:28, 2Wakorinto 6:6, Wagalatia 2:13, 1Petro 1:22,n.k. tunakutana na neno “unafiki”.

  Tukisoma kwa makini maandiko hayo, tutagundua kuwa UNAFIKI ni namna ya kuigiza jambo, kulifanya jambo lionekane kuwa ndivyo lilivyo, wakati katika hali halisi halipo hivyo. Mfano, katika Warumi 12:9 andiko tulilolisoma hapo juu ambalo linasema “Pendo na lisiwe na UNAFIKI lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema”. Hapa tunajifunza kuwa kumbe tunaweza kuwa na pendo la “unafiki”, mtu anaweza kujifanya kuwa anampenda mwenziwe na kumjali, akimfanyia hiki au kile kilicho chema, kumbe ni unafiki tu, yale yanayofanywa na muhusika hayatoki moyoni. Pembeni anaweza kuwa anasema kuwa ah, fulani mimi simpendi kabisa namwonea aibu tu ndiyo maana namfanyia hivi na vile, namfanyia hivyo ili tu asinielewe vibaya; maana amenihitaji sana nimfanyie hivyo, unaona! Mtu kama huyo anakuwa anafanya unafiki tu katika kumpenda mwenziwe na kumsaidia analomsaidia; anakuwa kama anafanya mchezo wa kuigiza.

  Kumbe katika u-Kristo mtu anayefanya unafiki ni kama mtu afanyaye mchezo wa kuigiza. Katika mchezo wa kuigiza, mwanamke anaweza kujifanya mwanamume kwa kuweka ndevu za bandia kidevuni na akaigiza kama mwanaume akawa anamwamrisha mwingine kama mkewe katika mchezo, huo ndiyo unafiki
  wenyewe, “Hypocrisy”. Kumbe hata katika michezo ya kuigiza kama wa-kristo hatupaswi kuishiriki au kuifanya, tukiifanya tunakuwa tunafanya unafiki, maana hatufanyi kilicho kweli, tunadanganya nasi tunakuwa tu miongoni mwa waongo.

  “Unafiki” kwa mtu yeyote anayejidhania kuwa ameokolewa hapaswi kuwa nao kabisa, mtu mnafiki mahali pake ni katika ziwa la moto na kiberiti. Kama wa-Kristo hatupaswi kuwa watu wachukizao kwa kuwa wanafiki. Kuna watu nyakati hizi wanaweza kujifanya kuwa ni watu wa Mungu, lakini wanafanya kila namna ya machukizo kama watu wasiomjua Mungu, watu wa namna hiyo maandiko yanasema watatupwa katika ziwa la moto, [Ufunuo 21:8], “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ZIWA LIWAKALO MOTO NA KIBERITI ……”

  Kwa kuhitimisha naweza kusema tu kwa kifupi kuwa, UNAFIKI ni hali ya kufanya jambo fulani kinyume na hali halisi ilivyo, au inavyotakiwa kuwa. Hivyo ndivyo nilivyoweza kueleza maana ya unafiki kwa sasa.

  Amani ya Ktristo itufunike!

 136. bwana asifiwe!nampenda sana BAHATI BUKUKU hakika nyimbo zake zinanibariki naomba namaba yake ya simu kama inawezekana naishi usa

 137. BWANA ASIFIWE!NIMEFURAHI SANA KUIPATA BLOG HII KUTOKA KWA MICHUZI BLOG MIMI NI MTANZANIA NINAISHI MARYLAND USA NIMEGUSWA NA SWALI LA MPENDWA MMOJA ALIYETAKA KUJUA JUU YA BAHATI NASIBU YA WORK AND LIVE IN USA KWANI MIMI PIA NI MMOJAWAPO WA WASHINDI WA HIYO DV LOTTERY UKWELI NI KWAMBA BAHATI NASIBU HII INACHEZWA KILA MWAKA KUANZIA MWEZI WA OCTOBER HADI DISEMBA NA INAECHEZESHWA NA SERIKALI YA MAREKANI NA SIYO VINGINEVYO NA UKISHINDA UNATATUMIWA BARUA MOJA KWA MOJA KWENYE SANDUKU LAKO LA POSTA UNATAKIWA KWENDA UBALOZI WA MAREKANI PALE MSASANI KWA KILA KITU WATAKUAPA MAELEKEZO JINSI YA KUCHEZA NAKUOMBA TUWASILIANE rmwakapalila@yahoo.com

 138. Hi Strictly Gosper.I pray to God so that you can be there forever for the Groly of God. Because you have been bless to us.May God keeps you longer and longer.Amen

 139. Shalom! Kwa muda sasa nimekuwa nikitafuta kanda moja ya zamani sikumbuki ilitoka mwaka gani, lakini nahisi itakuwa mwishoni mwa miaka ya themanini au mwanzoni mwa miaka ya tisini inaitwa URAIA WETU HASWA NI MBINGUNI wameimba kwaya ya Kolandoto Shinyanga, nafikiri ni kwaya ya Tumaini ambao pia wametoa kanda yao ya video inaitwa SIKU ILE. Nilijaribu kuulizia Radio Habari Maalum wakasema hawana, hivyo yoyote aliye nayo au anayeweza kuniambia jinsi ya kuipata atakuwa amenisaidia sana.

  Natanguliza shukrani,

  Abigail

 140. Bwana Asifiwe,napenda kusaidiwa majibu ya utata wa mambo niliyonayo
  1.hakuna mpango wowote wa kuunganisha ukristo hapa duniani maana sisi tusiokaa mahali pamoja tunakosa huduma za kichungaji,kinabii na utume tunaingia katika huduma nyingi hazina historia katika kumhubiri Yesu.

 141. Ndugu Boniface,

  Mimi naamini kabisa swali lako ni la muhimu sana na ambalo jibu lake linaweza kusaidia watu wengi. Lakini naogopa namna ulivyoliuliza kwa kulituma kwa mch. Lusekelo ili yeye mwenyewe ajibu inawezekana lisijibiwe kabisa. Watumishi wengi, ikiwa ni pamoja na mch. Lusekelo wana ratiba ngumu ambazo wakati mwingine inaweza isiwe rahisi kutembelea mitandaoni ili kufanyia kazi mambo kama swali lako. Kwa wale ambao wanahudumu pia kwa kutumia mitandao/blog wao huwa wanajibu maswali kama hili la kwako.

  Kutokana na sababu hiyo mimi ninakushauri ungelileta swali lako kwa wasomaji wa blog ili tulijadili kwa pamoja, ukiwemo wewe mwenyewe, ambapo ungeshiriki kutoa duku duku lako kwamba kwa nini unafikiri kanisa la Lusekelo si la kweli [kwa mujibu wa swali lako]. Ninaamini kati ya wanaotembelea mtandao huu anaweza kuwepo hata mtu mmoja ambaye anaifahamu vizuri huduma ya Lusekelo na pengine ni mshiriki wa pale. Lakini pia Neno la Mungu, ambalo ndicho kioo cha mambo yote ya rohoni, lipo; na kwa pamoja tulipitia na kujifunza tungeweza kupata mwanga. Natumani kwa kufanya hivi tungeweza kupata mambo mengi ambayo yangekuwa ni vigezo vya kutumia ili kufahamu kanisa/huduma yoyote kama ni ya kweli au si ya kweli,zaidi ya kuelekeza kwa kanisa moja tu, ambalo kama ni la kweli yako mengi na kama si la kweli yanaweza yakaweko mengi pia; na hivyo tukawa tumepiga ndege wengi kwa jiwe moja!

  Jambo jingine ambalo ninashauri ni kwamba katika mambo ya mbinguni ni vizuri sana kujiweka wewe mwenyewe. Kama ni wewe unachanganywa na wingi wa makanisa ni vizuri kusema kuwa ni ‘mimi’ badala ya kutumia ‘sisi’. Kama umetumwa na kundi fulani la watu kuwawakilisha unaweza ukasema hivyo ili kuweza kupata msaada zaidi ikitokea kundi hilo liko katika hali fulani inayosababisha wawe katika tatizo hilo, kwa mfano kama ulivyotumia wewe, kuchanganywa na wingi wa makanisa. Lakini kama hujatumwa na watu kuandika ujumbe huo, naona ni vema sana kujiweka wewe mwenyewe ili jibu likija uweze kusaidika wewe! na mwingine anayesoma kama yeye mwenyewe binafsi, maana ‘kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe’.

  Unajua haya mambo ya mbinguni jambo fulani linaweza kuwa tatizo kwako, au kwangu na hivyo kufikiri hilo ni tatizo kwa watu wote, kumbe si lazima iwe hivyo. Inawezekana kabisa wingi wa makanisa kwa mtu mwingine si tatizo na wala hakumfanyi kuchanganyikiwa kwa lolote.

  Kwa maneno hayo ninakushauri, kama itakupendeza, ulipange swali hilo vizuri kisha uliweke uwanjani kwa ajili ya watu kulichangia ili pengine, kwa pamoja, tunaweza kufahamu kama kanisa la Mch. Lusekelo ni la kweli au la uongo, pamoja na makanisa/huduma mengi sana ambayo tayari yameshaibuka na mengine yanayoendelea kuibuka kila kukicha!

  Natanguliza kuomba samahani kama kwa namna moja au nyingine nitakuwa nimekukwaza! Lakini kama umenielewa ninachomaanisha natumaini utalifikiria hili na kisha kulifanyia kazi ili tuweze kujifunza kwa pamoja!

  Amani kwako.

 142. mchungaji Lusekelo miaka ya hivi karibuni kumekuwa na utaratibu wa kuanzishwa makanisa mengi ambayo yamekuwa yakidai kuwa yanatoa mafundisho ya kweli lakini wakati huohuo biblia inasema nyakati za mwisho wataibuka manabii wa uongo ambao wataacha kweli ya Mungu watafundisha mafundisho yao. je wewe kama mmoja wa wachungaji walioibuka hivi karibuni unatuthibitishiaje kwamba kanisa lako ni la kweli na si makanisa mengine, maana sisi kama waumini mnatuchanganya hatujui wapi tutapata mafunzo ya kweli,kumbuka miluzi mingi humpoteza mbwa.ahsante sana

 143. Ndugu Emmanuel,

  Mimi nakushauri uende kituo chochote cha polisi kilicho karibu nawe, na kama uko nje ya Tanzania unaweza kwenda ofisi ya ubalozi wa Tanzania katika nchi uliyoko. Kutoka katika sehemu hizo, naamini, unaweza kupata namba hiyo ya simu kwa haraka na kwa usahihi!

 144. Mpendwa Light, naomba nikujibu japokuwa wengi wamekuelewesha vizuri kabisa. Kabla ya wokovu nilikulia katika dhehebu moja ambalo kwakweli mambo mengi ni mapokeo na si watendaji wa Neno kabisa. Kwahiyo hakuna semina za vijana, wala wachumba au wanandoa, ukichangia na kuwa Biblia ilikuwa ni taboo ya kusoma kasisi tu na kuwafundisha jumapili basi watu mnachakarika kutafuta maarifa kila pembe. Hivyo nami nikawa ni msomi wa gazeti za udaku na mengine, hayasaidii chochote ktk ndoa, lakini katika kumtafuta Mungu nikajibidiisha sana kusoma Biblia, nikaokoka. Automatically nilipookoka vile vigazeti sina interest navyo kabisa! nilishangaa sana! Lakini sio kwamba hukutani navyo unaviona au hata baadhi ya vipindi vya TV vinahayo mambo sana, viepuke na kuvipuuza tu. Kwa mtu ambaye huna ndoa hayo mawazo yakikujia kemea kwa Jina la Yesu: ondoka! Ukiwa na shaka jiulize je hili linampa Mungu utukufu au nani? huna jibu na kinakutia shaka acha ni Roho Mtakatifu anakusemesha, ukiendelea kupinga atakuacha kama alivyomuacha Sauli na utakuja juta. Mkristo usiye na ndoa ni muda mzuri kumtumikia Mungu na kutafuta kwa bidii kusudi lake ktk maisha yako, mume/mke mwema hutoka kwa Bwana hutakuwa na haja ya kum”handle” maana wote mtaenenda ktk roho na si mwili. Ubarikiwe.

 145. Hellow watakatifu,
  Nina swali ambalo linanisumbua sana,

  Ni sahihi kwa mwanamke aliyeokoka kuzaa kwa uchungu?
  Kama ni laana ya kukosa kwa Adam na Eva,Yesu si ndiyo alikuja haswa kutuokoa nayo,
  Je ni kwa kukosa ufahamu tunaendelea kuteseka au?
  Naomba mnisaidie

 146. Ndugu Patrick,

  Kuna maswali kadha ambayo uliuliza kutokana na mkanganyiko wa mafundisho ya semina uliyohudhuria katika kanisa fulani hapo Dar.

  Mimi ninachotaka kuchangia, kujibu, kutokana na hali hiyo ni kwamba kwa kuwa tayari moyoni mwako ulishashuhudiwa kuwepo kwa lengo la kumjenga mchungaji yule na kisha vikaendelea viapo kwamba watu waape kuwa punda wa mchungaji hali hiyo inaonyesha kusudi la semina hiyo lilivyokuwa. Katika semina ya namna hii usitegemee kuwe na kipindi cha maswali. Kuna wakati viongozi wa makanisa huingiwa na roho mbaya kiasi cha kuitisha semina ili kuwaadabisha washirika inapotokea kwamba mchungaji huona kama washirika hawamtii inavyopasa. Suala la utii limekuwa likitumika vibaya sehemu nyingi kwa kuwafundisha watu wamtii kiongozi wa kanisa hata kwa mambo ambayo yako kinyume na kweli ya Neno la Mungu.

  Hali iliyotokea katika semina hiyo ni kielelezo cha semina nyingi ambazo zinaendelea katika pembe tofauti za Tanzania. Kama nilivyoandika kwenye mchango wangu fulani uliopita kwamba kadri siku zinavyokwenda mafundisho kuhusu utakatifu yanakuwa ni mada adimu kwenye makanisa mengi. Ni nyakati ambazo viongozi wengi wa makanisa wanapendwa kuinuliwa sana, waheshimike sana, huku wakiwa wanasahau yale maneno ya Bwana Yesu kwamba ‘anayetaka kuwa mkubwa na awe mdogo’.[Luka 22:26]

  Suala la kuhama na kwenda kanisa jingine linalohubiri wokovu hilo nakuachia mwenyewe kutokana na jinsi utakavyopata amani moyoni mwako.

 147. Dada light Mungu akubariki sana kwa kuwa wazi na kuwa na nia ya kutafuta njia sahihi.

  Nawapongeza wote waliochangia ili kukusaidia Light.

  Naongeza mchango kidogo katika kujibu swali moja kati ya maswali mawili uliyouliza.

  Swali linasema hivi “…… tutajifunzaje jinsi ya kuwahandle waume wetu pindi tutakapokuwa katika ndoa?” Mungu akikupa mume anao uwezo wa kuwafundisha namna ya kila mmoja kumhandle mwenzake. NINAKUSHAURI HAYA KWA UZOEFU WANGU BINAFSI. Hili ni tatizo kubwa kwa wanandoa na hata vijana wengi ambao wanatamani kujua namna ya kufanya hilo tendo takatifu kwa kutumia experience za watu wengine. Ni vyema kuingia katika ndoa mkiwa wajinga wawili kwenye hilo tendo, you will enjoy learning together. Mmoja akafahamu mambo mengi sana na mwenzake akawa hafahamu, ni tatizo kubwa sana Mungu asipoingilia kati. Hata kama kabla ya kuokoka ulitumikishwa katika dhambi ya zinaa unahitajika kumsihi sana Mungu akuvue ile experience ili uanze upya kwa upako wa Roho mtakatifu. Ninaamini kuwa Yesu aliumba vyote kwa utukufu wake, alipoweka suala hili aliweka neema pia ya kujifunza hata kwa mtu ambaye alijiheshimu pasipo kupata experience yeyote. NINAANDIKA HAYA KWANI HATA ENZI ZA UJANA WANGU LILIKUWA SWALI NILILOJIULIZA SANA, ILA LEO HII NAGUNDUA ULIKUWA WASIWASI TU.

  Badala ya kuangalia hizo picha huo muda fanya maombi ukimsihi Mungu akuandalie mume mwema(THE ONE CAN BE HANDLED), akuandae kwa ajili ya kumhandle mume wako huyo atakayekupa na awaandalie washauri wanaofaa mtakapokaribia kuingia katika ndoa takatifu. Hiyo siku ya siku kama Kristo atakuwa hajarudi utajatoa ushuhuda hapa SG jinsi Mungu alivyokuvusha hapo.

  Mungu akubariki sana.

 148. Mpendwa Light pornography kama walivyosema wapendwa wengine ni kazi ya Shetani. Wazo la ngono au tamaa ikikujia ifukuzilie mbali kwa Jina la Yesu halafu elekeza akili yako na moyo wako kwenye yale yanayompendeza Kristo. Huo ndiyo utii. Kwa mfano moyo wako unakutuma na unakuambia “ukiwa umejipumzikia chumbani kwako mwenyewe hebu chukua ule mkanda wa X uangalie upate ya kujifunza kabla ya kuolewa.” Wewe jibu kwa kuukemea moyo wako na useme tena kwa sauti, “hayo siyo mapenzi wala maagizo ya Bwana Yesu wewe Shetani nakukemea kwa Jina la Yesu toka hapa”. Halafu elekeza moyo wako kwa kulikumbuka Neno la Mungu ambalo ni Uzima, Nuru na Kweli. Na utubu na kumuomba Mungu msamaha. Pale pale Shetani atakimbia na vinyago vyake vya ngono. Kupenda mambo ya ngono ni ibada ya sanamu. Achana nayo. Na uingize ndani ya moyo mambo ambayo yanampendeza Mungu badala ya yale ya ngono.
  Kama ilivyoelekezwa ndani ya Wafilipi 4:8, tunatakiwa kuyatafakari mambo yenye sifa zifuatazo; Yawe ya kweli; Ya staha; ya haki; yaliyo safi; yenye kupendeza; yenye sifa njema;yaliyo mema ya;sifa nzuri yoyote. We are not to be controlled by our minds rather we should control our minds if we choose to do so.

  Inasemekana, na ni kweli kuwa:

  Ukipanda wazo unavuna tendo;
  Ukipanda tendo unavuna tabia;
  Ukipanda tabia unavuna mwenendo wa kimaisha!

  Kwa hiyo wazo la ngono ukilipanda ndani ya akili na moyo wako Inachofuata ni tendo ya kufanana na ngono. Kuna siku baada ya kuangallia angalia kwenye video utatamani kujaribu kimatendo. Kwa sababu kanaufurahisha mwili basi unaanza kuzoea kidogo kidogo kanakuwa katabia halafu inafikia siku ukiikosa unaanza kuhaha kuitafuta. Muombe Mungu usifikie huko si jambo zuri kwa Roho hata kidogo. Ni mauti.

  Kwa hiyo ukishinda kishawishi hakiwezi kuwa katika matendo, tabia wala mwenendo wa kimaisha.
  Ubarikiwe sana.

 149. Ndugu zangu nina swali na wala sitanii. Jambo hili limenipa tabu sana ndani ya moyo wangu. Jana (3/8/09) nilihudhuria semina kanisa moja hapa mjini DSM. Kanisa hilo ni maarufu sana. Tulitangaziwa kuwa kuna semina ambayo itaendeshwa na mchungaji mgeni kutoka nchi ya Kenya na ilikuwa inahusu ufufuko wa mtu na jinsi ya kufanikiwa kutoka lindi la kukandamizwa.

  Pamoja na kuwa mchungaji yule alikuwa anahubiri lakini niligundua (ninaamini Roho wa Mungu alikuwa ananionyesha) kuwa yale mahubiri yalikuwa yanalenga kumjenga Mchungaji Kiongozi wa Kanisa lile na tukawa tunaambiwa kwa kutumia maandiko ambayo mimi niliona yalikuwa hayaendani, kuwa ni lazima kila mmoja awe tayari kuwa ‘punda’ wa yule mchungaji kiongozi. Kama hiyo haikutosha aliwataka waumini wote waape kwa kutamka kuwa ‘kuanzia sasa mimi niko tayari kuwa punda wa mchungaji kiongozi’. Hilo mimi sikushiriki ila nilikuwa namwambia Bw Yesu ‘mimi niko tayari kuwa punda wako’. Swali, jamani hii ni sahihi kweli? Hii siyo cultism kweli?

  Baada ya hapo akawaagiza kila mmoja mwenye shs laki moja aende mbele achangie kulipa gharama zake za hoteli na kama hana basi aahidi. Halafu wakafuatia wa 50 elfu na elfu kumi. Mimi yakanishinda nikaondoka.

  Swali la pili. Hivi jamani semina siyo maana yake kunakuwa na kipindi cha maswali na majibu? Mbona semina zote kwenye kanisa hili huwa ni wale wahubiri kumnyanyua huyo mchungaji kiongozi kama vile waumini wake hawamsaidii? Na kumbe wazee wa lile kanisa wako tayari lakini yeye hataki kuwasikiliza. Kuna siku wazee walikutana wakatayarisha mapendekezo yao ya kulinyanyua kanisa. Lo alikasirika na kuwaita ni waasi. Jamani hili ni kanisa au ni shamba la Mgiriki. Au ni social club? Roho yangu kwa kweli inakwazika. Nimeamua kulihama na kwenda kanisa ambalo linahubiri wokovu. Au ndugu zangu nini maoni yenu kwenye suala hili? Nisaidieni.

 150. Dada Light,
  Kifupi ni kuwa, ukiokoka picha hizo ni marufuku, kwa nini?
  1. Wanaofanya hivyo huwa si mke na Mume – Hivyo kuangalia ni kinyume na Neno Efeso 5:11

  2. Hata kama ni Mke na mume, lazima ukiangalia utawaka tamaa na kumtamani mke/mume wa mtu mwingine ni kuvunja Amri ya Mungu (Kut 20)

  3. Si kuwa hupendi kuziangalia bure! Roho wa Mungu hukuonya kwa kuwa Yeye anajua hatari zote za kiroho kuliko sisi. Kumbuka, Roho anajua maandiko ambayo hata mengine hujawahi kusoma. Kwa hiyo kumtii bila swali ni njia njema ya kukwepa matatizo yanayoweza kukutokea baadae.

  Ushauri wangu ni kuwa tubu na uache haraka. Ni hatari!

 151. Dada Light zingatia sana alichokufundisha kaka John. Pia kwa kuongezea, jua kwamba miili yetu ni hekalu la roho mtakatifu. Hivyo usimhuzunishe Roho wa Bwana. Hakuna ibada yoyote takatifu katika “ponography” Unapoangalia hizo picha, ziko roho chafu kama tamaa, uasherati nk zitakuingia na ndipo utashangaa utakapoingia katika ndoa,mapepo hayo yanaweza kujidhihirisha na kuharibu ndoa yako. Nimeona shuhuda nyingi sana za watu wanaosumbuliwa na “spirit husbands or spirit wives”. Matokeo yake utajikuta unafanya uasherati na hayo mapepo wakati ukiwa umelala na ni mpaka ufanyiwe deliverance ndipo yanatoka.

  Hebu kubali kuacha huo uovu kwa USALAMA WA WOKOVU WAKO.

 152. Dada yangu mpenzi LIGHT tunae mwalimu wetu ambaye ni mwalimu wa walimu yeye atatufundisha yote yafuatanayo na utakatifu wala hakuna elimu nyingine zaidi inayomzidi Yesu.usiangalie picha za ngono kabisa hazifundishi lolote ila zitakusababishia mawazo ya zinaa na pia ni dhambi kuangalia hizo picha kwa mwana wa mungu,yesu atakufundisha, ndie aliyekuita naye atahakikisha unaweza kuishi bila mapungufu kwenye ndoa.Ubarikiwe maana naamini kuwa utajitenga na picha za ngono.

 153. Dada Light,

  Mimi ninajibu kwa ufupi kwa sasa.

  Ni vizuri kwamba umeokoka na kwamba umekuwa ‘mwaminifu’ sana katika wokovu ISIPOKUWA jambo hilo linalokusumbua. Kwa ninavyoelewa mimi kuwa mwamininfu katika wokovu ni pamoja na kujilinda na kujiepusha na mambo ambayo yanaweza kukuingiza katika dhambi. Kama si ya matendo iko dhambi ya mawazo pia. Kwa hiyo ili uamifu wako ukamilike ni HERI ukajiepusha na majaribu ya kutengeneza wewe mwenyewe!

  Picha hizo chafu ambazo huwa unaziangalia na wakati mwingine pasipokupenda hiyo ni ishara tosha kwamba unalazimisha kitu ambacho hatari katika maisha yako ya wokovu, huku dhamiri yako ikiwa inakusuta! Kama huwa hupendi lazima ujiulize kwa nini uangalie kitu usichokipenda? Ni lazima kuwe na nguvu inayokulazimisha kufanya hivyo.

  Watengeneza picha za ngono ni watu wanaoendeshwa na roho chafu. Roho zilizosababisha Sodoma na Gomora ziangamizwe. Roho ya zinaa! Roho za tamaa mbaya. Roho ambazo zimesambaratisha na zinaendelea kusambaratisha ndoa nyingi duniani. Kinachoenezwa na picha hizo ni tabia ya zinaa. Kila mtu mwenye kuangalia na kufurahishwa na picha hizo yuko katika hatari kubwa ya kutekwa na roho ya zinaa!

  Kinachofundishwa na katika picha hizo ni zinaa na wala si namna ya ku-handle mume kama ulivyosema wewe. Kama kuna mtu alikuambia kwamba humo wanafundisha namna ya ku-handle mume alikudanyanga. Anataka kukuingiza katika shimo ambalo ukiingia humo kutoka ni vigumu sana. Watu ambao hawana ndoa, wanaotengeneza mikanda hiyo, hawawezi kufundisha mtu namna ya ku-handle mume. Sana sana unachoweza kujifunza ni namna ya ku-handle buzi! Lakini kwa kuwa wewe umeokoka hayo mambo yako mbali nawe.

  Hakuna maadili yoyote wala namna njema utakayopata kutoka katika picha hizo kwa sababu humo huwa hawafundishi namna ya kuishi na mume. Ili kuweza kujifunza namna ya kuhudumia waume/wake ni lazima kujifunza katika Neno la Mungu na kusikiliza mafundisho yanayotolewa kanisani kuhusu namna ya kuishi katika na nyumba. Yako mafundisho mengi kwa vijana ambao hawajawa na wenzi na kwa watu ambao wako kwenye ndoa tayari. Mafundisho haya yenye msingi wa Neno la Mungu huwa na material sahihi kwa ajili ya wana wa Mungu. Hudhuria semina mbali mbali kanisani ambazo huwa zina mafundisho kwa ajili ya ndoa na unyumba!

  Kuendelea kuangalia picha hizo ni kujichimbia shimo ambalo ukijitumbukiza mwenyewe ni wewe mwenyewe utatakiwa kujitoa maana hukutambuwa yakupasayo USALAMA WA WOKOVU WAKO.

  Kama kweli umeokoka kaa na ishi maisha ya mtu aliyeokoka ambayo yanaelekezwa katika BIBLIA.

 154. Wapendwa Bwana Yesu Asifiwe.
  Mimi ni msichana niliyeokoka na nimekuwa mwaminifu sana katika maisha yangu ya wokovu ila kuna jambo linanisumbua sana na ningependa kupata msaada wenu watu wa Mungu,Hivi kuangalia picha za ngono ni dhambi? kwa maana wakati mwingine nimejikuta nikiangalia japo mimi mwenyewe huwa sipendi. Sasa kama ni dhambi tutajifunzaje jinsi ya kuwahandle waume zetu pindi tutakapokuwa katika ndoa?

  Naomba msaada wenu niko njia panda
  Bwana Yesu awariki ninyi nyote mnaotembelea hii Web hakika muda wenu si bure katika Bwana

 155. Noel Lameck Says:
  Sunday, March 1, 2009 at 8:44 pm

  Jamani wapendwa nawasalimu kwa jina la Yesu, mimi niko Tanzania na katika kupitia sehemu hii ya maswali nimeona kuna wenzangu wako USA nilitaka niulize wanajua lolote kuhusu bahati nasibu ya free lotto maana karibu kila siku napokea ujumbe toka USA kuwa nimeshinda kiasi fulani cha pesa sasa nashindwa kuelewa kama ni kweli au ni kundi la matapeli asante.

  ***************************************************

  Kama linavyoonekana swali hili liliulizwa miezi mingi iliyopita. Kwa sababu nadhani ninaweza kusaidia naomba nilijibu kama ifuatavyo.

  Bahati nasibu yoyote ni lazima uwe umenunua tiketi, kama tiketi yako ikishinda, ndipo unapewa zawadi. Sasa kama unaona mtu anakutumia tu ujumbe kuwa umeshinda wakati hukununua tiketi yoyote basi ujue huo ni utapeli.

  Wizi mwingi wa namna hiyo uko Nigeria au unatumwa toka Nigeria (ingawa unaweza kuonekana kama umetoka USA) na watu wengi wamepoteza fedha zao.

  Jambo la kufanya ni kuachana nao, usije ukajaribu kufuata maelekezo watakayokuletea ili upate zawadi yako. Lazima utaishia kupoteza hela zako kama utajaribu kufuatilia.

  Mwisho nikushauri kuwa; kama mkristo, unatakiwa uachane na bahati nasibu, nadhani hazistahili kwa mtu anayekwenda mbinguni. Ubarikiwe

 156. Haleluya wapendwa!
  Nikijana nimeokoka nampenda sana YESU,natatizo ambalo kwangu ni jaribu ama teso kwangu la kumpata mwenzi wa maisha,nina umri wa miaka 28 sasa nimeachwa na wachumba mara 3 baada ya wao kufanikiwa kimaisha,
  Nimemuomba MUNGU muda mrefu ktk hili lakini naona kimya.nahitaji msaada ktk hili,mbarikiwe wapendwa.

 157. Shaloom mama msofe,

  Nimefanikiwa kuipata namba ya Matilda Jojo ;;;;0714 988858, nami nampongeza saana kwanza kwakumwimbia Mungu vizuri, na pia nampongeza kwa kuendesha vipindi vya ndoa na maombi vizuri na kwakweli Mungu alikuwa anaonekana hivyo nawashauri Radio Safina wamrudishe huyu dada na pia dada Matilda nakusihi urudi redioni kipindi cha Twende kanisani kina pengo kubwa.

  Mungu awatunze.

 158. SHALOM, SHALOOM.
  Nimefuhi kuambiwa Matilda Mlay ameolewa na jojo jose kwakweli nimefurahi sana, pia nilikuwa nataka kuwaalika kwenye mkutano wa neno la Mungu ila sifahamu namba zakee za cm tafadhali naomba mnisaidie…… na pia video ya maserafi nimeipenda na ruhusiwakuwatumia ndugu zangu wako Marekani

 159. Bwana asifiwe sana,mimi ni kijana aliekoka siku nyingi,Mungu amenijalia kipawa cha uamifi,uchapa kazi kwa bidii,natafuta kazi ya udereva.Namba yangu ya simu ni 0713 846599,email ni lweikiza@gmail.com,naishi Dar es salaam

 160. HALELUYA
  Naomba ratiba ya vipindi kwa wiki nzima katika redio za WAPO, Praise Power na Upemdo FM.
  Mungu awabariki

 161. Elohim=Creator(Plural of El) – Genesis1:1
  El-Shaddai-Almight God/ Source of confort and provisuion – Genesis 17:1
  Jehovah Jireh= God will provide – Genesis 22:13
  Jehovah Rapha=The Lord tha health Exodus 15:24-26
  Jehovah Nissi=God our banner just after victory
  Jehovah Sabaoth= Lord of hosts or armies
  Jehovah Shalom=God our peace-Judge 6:22-24
  Jehovah Tsidkenu=The Lord our rightenouss – Jeremiah23:6
  jehovah M’kaddesh-The Lord that sanctfy you[God save us from eternal penalty of sin and influence of sin]
  Jehovah Shammah=The Lord is therem or god is ever present – Ezekiel 48:35 & Hebrew 13:5
  Ebenezer=Thus far has the LORD helped us-Samuel7:12

  Binafsi sijui ni Kiebrania au Kimrahic ila nimeyakusanya toka source mbalimbali. MUNGU AKUBARIKI

 162. B.Y.A. Kuna baadhi ya maneno yanayomsifia Mungu kwa lugha ya Kiebrania(?) au Kamrahic(?) kama vile Yehova, Shalom n.k. Naomba mnisaidie kunipa maneno mengine kwa lugha hiyo na tafsiri yake. Kuna El Shadai au Ebenezer sijui yanamaanisha nini? Kuna mwenzetu anaeyajua basi anisaidia na mimi nijenge glossary tafadhali.

 163. Watumishi wa Mungu. Bwana Yesu Asifiwe. Kama kuna website yenye biblia nzima ya kiswahili, tafadhali ninaiomba. Nimeona za English kama KJV na NIV ziko nyingi. Ya kiswahili sijafanikiwa kuipata. Mbarikiwe sana.

 164. Naomba kuuliza kama goodlucky sandy ameshatoa shuting yake ya wimbo wa milima na mabonde kwa sababu wimbo huu ni naupenda sana. kama hajatoa mimi ningependa kumshauri atoe shuting hiyo kwa kuwa nyimbo zake zinanigusa sana ili tuone live

 165. Bwana asifiwe wapendwa.

  Kwako Mpendwa Kemi, Shalom!
  Kuhusu swali lako fupi kabisa, lakini linalohitaji ufafanuzi mkubwa, uliloliuliza iwapo Mkristo anaruhusiwa kumwacha mke/mume kwa uasherati, mimi najibu kama ifuatavyo:-

  Katika ufahamu wangu, na pia kutokana na nilivyojifunza kutoka kwa watumishi mbalimbali, ni kwamba kuna tofauti kati ya UZINZI na UASHERATI kimatumizi.

  UZINZI ni dhambi inayofanywa na watu waliooana tayari na wanaishi pamoja. Moja anapotoka nje ya ndoa yake na kufanya ngono na mtu asiye mke/mume wake huyo anafanya UZUNZI.

  UASHERATI ni dhambi inayofanywa na watu ambao hawajaoa au kuolewa bado. Hawa ni pamoja na WACHUMBA wanaotarajia kuoana. Moja kati ya hawa wote anapokuwa anafanya ngono na mtu yeyote, anakuwa anafanya UASHERATI.

  Maandiko yanasema katika Mathayo 19:9….”Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya UASHERATI, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini. Kutokana na maelezo niliyoyaeleza hapo juu, maandiko haya aliyoyasema Yesu, yanaonesha kuwa wanaozungumziwa kufanya uasherati ni watu ambao ni wachumba kama tulivyozoea kuwaita.

  Yesu hapa alikuwa akizungumza na jamii mchanganyiko, wengine bila shaka walikuwa na wachumba wao na wengine walikuwa tayari wanaishi pamoja kama mume na mke n.k. Yesu alipokuwa akitaja neno UASHERATI kwa wenzetu wa nyakati hizo, tayari walikuwa wanaelewa kuwa sentensi hiyo ilikuwa inamhusu nani, na kama nilivyokwisha kusema sasa, sentensi hiyo ilikuwa inawahusu wale ambao hawajaanza kuishi pamoja kama mke na mume.

  Ni kwamba, katika biblia hakuna mahali tunapoweza kupaona pakiwa na neno “mchumba”. Nyakati za biblia watu waliofikia hatua zote za kuoana hata kabla ya kuanza kuishi pamoja, waliitana mke na mume. Ukweli huu tunauona kwa Yusufu aliyemposa Mariamu. Kabla hawajakaribiana Yusufu aligundua kuwa Mariamu alikuwa na mimba. Lakini hapa tunaambiwa kuwa Yusufu alikuwa MUMEWE kama tunavyoweza kuona katika maandiko, [Mathayo 1:18-20 Kuzaliwa kwake Yesu kulikuwa hivi, Mariam mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Naye Yusufu, MUMEWE, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu KUMWACHA kwa siri. …..malaika wa Bwana alimtokea katika ndondo, akisema Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariam MKEO…..] Hata hivyo inawezekana tatizo hili lilitokana na watafsiri wa maandiko, hawakuweza kuyachukua kama ilivyokusudiwa. Wataalam zaidi wanaweza kutusaidia. Lakini tunachotakiwa hapa kukijua ni kwamba Yesu alikuwa anazungumzia wachumba kwamba wanaweza kuachana.

  Mariam alikuwa mchumba wa Yusufu lakini maandiko yanataja kuwa mariamu MKE wa Yusufu. Tunajifunza kuwa, kumbe mchumba tunaweza kumwacha iwapo atakuwa amefanya UASHERATI kama tulivyoangalia huko nyuma.

  Ili kujua kuwa Uasherati na Uzinzi katika maandiko ya biblia zetu za kiswahili ni vitu viwili kiutendaji, tunaweza kuona katika Mathayo 15:19 tunasoma hivi, “Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, UZINZI, UASHERATI; wivu ushuhuda wa uwongo….” andiko hili na mengineyo ya aina hii, yanatuonesha wazi kuwa uzinzi na uasherati ni vitu viwili tofauti katika utekelezaji wake, ndiyo maana yameandikwa yote mawili.

  Ili kuzidi kufahamu zaidi tofauti ya maneno haya mawili, tunaweza pia kuona yule mwana mpotevu katika kitabu cha Luka, ambaye mali yake aliimalizia kwa uasherati wala si kwa UZINZI kwa sababu alikuwa hajaoa. [Luka 15:13….akasafiri kwenda nchi za mbali; akatapanya mali zake huko kwa maisha ya UASHERATI].

  Kimsingi watu waliokwisha kuoana na wanaishi pamoja, maandiko yanakataza kabisa kuwa wasiachane, ndiyo maana maandiko yanasema kuwa tangu mwanzo Mungu hakuruhusu jambo hilo. Musa aliruhusu kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao [Mathayo 19:8…..Musa kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi].

  Mungu anasema anachukia kuachana, na kama anachukia kuachana basi hawezi kuliruhusu jambo la kuachana kwa sababu yoyote ile, [Malaki 2:16 Maana mimi nachukia kuachana, asema Bwana Mungu wa Israel; ….basi jihadharini roho zenu, msije mkatenda kwa hiyana]. Maandiko yanazidi kusema wazi juu ya jambo hili katika Luka 16: 18 kuwa “KILA AMWACHAYE MKEWE NA KUMWOA MKE MWINGINE AZINI; NAYE AMWOAYE YEYE ALIYEACHWA NA MUMEWE AZINI” Maagizo haya ya Yesu, Paulo naye kwa kuuona umuhimu wake aliyakumbushia kwa Wakorinto waliokuwa wanaelekea uasi mkubwa ambayo tunayaona katika 1Wakorinto 7:10-11 nayo yanasema “Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi ila Bwana; mke asiachane na mumewe lakini ikiwa ameachana naye, na akae ASIOLEWE, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe”

  Kuhusu Mathayo 19:9, kwa kifupi tunajifunza kuwa, mke ambaye bado hatujaanza kukaa naye, ambaye sisi wa nyakati hizi tumezoea kumwita “MCHUMBA” pale tutakapogundua kuwa amefanya UASHERATI wakatu wa uchumba tunayo ruhusa ya kumwacha!

  Ndivyo nijuavyo mimi, hata hivyo sijaweza kuelezea vizuri sana kutokana na kushindwa kupangilia mawazo niliyo nayo juu ya jambo hili. Iwapo kuna mwenye maelezo mazuri zaidi anaweza akafafanua zaidi ili tuzidi kujifunza.

  Amani ya Bwana itufunike!

 166. BWANA YESU ASIFIWE!
  NINGEPENDA KUJUA KAMA MKRISTO ANARUHUSIWA KUMUACHA MKEWE AU MUMEWE KWA UASHERATI.NIMESOMA mathayo 19:1-9
  lakini ninependa kujua zaidi, kwa wanaoijua biblia vyema naomba msaada wenu.
  MUNGU AWABARIKI SANA.

 167. BWANA ASIFIWE WATUMISHI WA MUNGU,NAPENDA KUFAHAMU WEBSITE AMBAYO REDIO SAFINA WANATUMIA KUCHUKUA NYIMBO ZA INJILI ZA KIINGEREZA NA KIMAREKANI WANAZOTUMIA KWENYE KIPINDI CHA JUMAPILI JIONI KWANI HUWA ZINANIBARIKI SANA.NINGEPENDA KUWA NA NAKALA AU NI DOWNLOAD KWA AJILI YA KUSIKILIZA WAKATI WOWOTE NIKITAKA
  ASANTENI SANA.

 168. Ushauri wangu kwako dada Gile,

  Kama huyo amaeokoka na kama ana nia ya kukuchumbia kweli atakuambia ukweli. Watu waliookoka ni wajasiri. Atakueleza kusudi lake. Lakini kama hajaokoka jihadhari sana na mtego huo.

  Kumuota sana ndotoni yaweza kuwa ni kwa sababu unamfikiria sana. Mara nyingi ndoto huja kwa sababu ya mawazo mengi. Hivyo kumuota sana ni uthibitisho kwamba unamuwazia sana.

  Kitu cha kufanya endelea kumuomba Mungu ili jambo hilo lijidhihirishe wazi. Pia wakati huu angalia usije jirahisi sana kwake. Shikilia msimamo wako wa wokovu. Pia waweza kumueleza wazi pia kwamba kukutembelea ofisini kwako kunaweza kusababisha uambiwe kwamba wewe ni mzembe kwa sababu mara nyingi unakuwa unaongea na wageni na hufanyi kazi. Hata kama ni ofisi yako mwenyewe kuja kwake hapo kunaweza kukuharibia sifa na kuwafanya watu waanze kukusema vibaya. Utaharibu ushuhuda wako. Akija mtu ambaye anayetaka kukuchumbia kweli kweli anaweza ambiwa kwamba wewe hujatulia kwa sababu wanaume wanapishana hapo ofisini kwako. Si unajuwa tena watu wanavyotumika vibaya!

  Kwa ufupi: Chukuwa tahadhari zote za kiroho kwa kuvaa silaha zote za Mungu. Efeso 6:11-12.

  Yesu Kristo akutunze!

 169. BWANA YESU ASIFIWE.
  NAPENDA KUULIZA, JE TELEVISION YA TRENET IPO AU IMEKATISHA MATANGAZO YAKE MAANA NI MUDA SASA IMEPOTEA HEWANI NA KILA NIKIJARIBU KUITAFUTA SIIPATI

 170. Bwana Yesu asifiwe!naomba kuwasiliana na mtumishi wa Mungu.Josephat Mwingira

 171. Bwana Yesu asifiwe sana wapendwa!naamini nyote ni wazima kabisa! naomba ushauri ktk hili!
  Mimi ni binti,nimeokoka nampenda Yesu,Nimetokea kuwa na mazoea na kijana mmoja tumekuwa marafiki wa kawaida tukiwasiliana kwa simu wakati mwingine akija kunitembelea ofisini kwangu! Huyo kaka nimemsoma baadhi ya vitu anaonyesha kuwa anataka kunichumbia ila anaogopa kunambia nilivyomuona, ila na mimi ninampenda kusema ukweli!tatizo yeye hajanitamkia kama ananipenda! Wapendwa naomba ushauri wenu nifanye nini ktk hali kama hii! ni kwamba namuota sana ndotoni!

  Naomba ushauri wenu!

 172. BWANA YESU APEWE SIFA!!!!Nawapenda katika jina la Bwana YESU! Namshukuru Mungu kwa nafasi hii. Wapendwa naomba mnisaidie namba za simu za IGP MWEMA au Mkuu yeyote wa polisi wa kanda ya huku Dar ess alaam….nataka namba hizo kwa nia nzuri tu na ya kutaka kufichuo uovu nchini sambamba na utekelezaji wa agizo la Rais la kufichua waovu na wauaji wa maalbino Tanzania

  IGP MWEMA anao wajibu wa kuwawajibisha watumishi walio chini yake kama wasipotenda ipasavyo…na ana uwezo wa kuadhibu watenda maovu (WARUMI 13:1-7) Ukisoma hapo utagundua umuhimu wa huyu MTUMISHI kushughulikia maovu. Msaada wenu ni wa muhimu sana nikizipata hizo namba!

 173. Ndugu Seni, nimekutafuta kwenye hizo namba hapo juu sijakupata naomba uniambie kama umefanikiwa kuipata hiyo kanda. Ubarikiwe.

 174. Jamani wapendwa nawasalimu kwa jina la Yesu,mimi niko Tanzania na katika kupitia sehemu hii ya maswali nimeona kuna wenzangu wako USA nilitaka niulize wanajua lolote kuhusu bahati nasibu ya free lotto maana karibu kila siku napokea ujumbe toka USA kuwa nimeshinda kiasi fulani cha pesa sasa nashindwa kuelewa kama ni kweli au ni kundi la matapeli asante

 175. Dada Abigail, kama unataka hiyo kanda njoo hapa Shekinah-Mikocheni, kuna vijana wengi wanatoka Kolandoto wanaweza kukusaidia zaidi na naamini utaipata tu. ni karibu na TSJ (CHUO KIKUU CHA UANDISHI WA HABARI) na ukifika nipigie kwa 0786684062 au 0715684062. asante

 176. Shalom! Kwa muda sasa nimekuwa nikitafuta kanda moja ya zamani sikumbuki ilitoka mwaka gani, lakini nahisi itakuwa mwishoni mwa miaka ya themanini au mwanzoni mwa miaka ya tisini inaitwa URAIA WETU HASWA NI MBINGUNI wameimba kwaya ya Kolandoto Shinyanga, nafikiri ni kwaya ya Tumaini ambao pia wametoa kanda yao ya video inaitwa SIKU ILE. Nilijaribu kuulizia Radio Habari Maalum wakasema hawana, hivyo yoyote aliye nayo au anayeweza kuniambia jinsi ya kuipata atakuwa amenisaidia sana.

  Natanguliza shukrani,

  Abigail

 177. Niliwahi kusoma gazeti la nyakati, kichwa chake kinasema “MZEE WA UPAKO ASEMA MVUA ZINAZONYESHA NI ZAKE” kwa ndani niliona mtumishi huyu anasema kwamba namnukuu “mvua zinazonyesha ni zangu kama nilivyowaahidi watanzania kama zawadi ya mwaka huu……hakutakuwa na upungufu wa mvua mwaka huu” jamani nataka kuuliza sasa kwamba je Tanzania hapa kunanyesha mvua kila mahali? mbona mikoa kama Shinyanga mvua ni za rasharasha tu? je huu nao tuuite unabii au ni mchezo madhabahuni?. Pia Mzee wa upako aliwahi kutoa ahadi alipokuwa anahubiri huko Shinyanga katika moja ya mikutano yake kwamba….mwakani(yaani mwaka huu)waendesha baiskeli wote wa hapa shinyanga watanunua kila mmoja pikipiki…alidai kwamba Bwana amemwambia hivyo…na pia kwamba hakutakuwa na vyumba vya kutosha kwa wanafunzi kidato cha tano maana wanafunzi wote watafaulu kwenda kidato cha tano! jamani huu nao ni unabii? je matokeo ya mwaka huu kwa shule za sekondari yamepanda au yameshuka? jamani kama nikisema kwamba huyu ni nabii wa UONGO nipo katika makosa? watu wa namna hii wananichanganya kabisa kabisa katika utumishi! au ndio kutimiza unabii wa kurudi kwa YESU? Nisaidieni. Ameni…Mungu awabariki wote.

 178. Bwana Daniel manabii wapo kwa sababu hizi ni siku za mwisho ili maandiko yatimie manabii lazima watokee sababu biblia inasema zitakuwa siku za mwisho ambazo wazee wetu wataota ndoto na wana wao watatabiri
  NABII ninani NABII ni mtu yule anayetumiwa na Mungu kutoa mafunuo ya wakati ujao……….

  Lakini naifurahia sana biblia kwa sababu haikuishia hapo Mungu pia alitutahadharisha kwa kutuambia tujihadhari maana siku za mwisho hizi watatokea manabii wengine wengi wa uongo nao watatumia jina la YESU hili hili tunalotumia cha msingi usibabaishwe na haya majina ya manabii na mitume jitahidi kujikabidhi kwa Mungu kuomba akupe mafunuo katika mafundisho yake ukiongozwa na roho mtakatifu kuweza kutambua mafundisho yake,ni huo mchango wangu mdogo maana mimi ni mchanga sana katika wokovu

 179. Danny,
  Mtu hapaswi kujibandika JINA la mtume/nabii/mchungaji nk. Kama ukisoma Waefeso 4 ina majibu ya maswali yako.

  Kifupi hivi sio vyeo, kama ambavyo vimefanywa siku za leo. Ni huduma, kama huduma nyingine. Utume ni huduma kama ulivyo uchungaji au uinjilisti, na vyote vina lengo moja, kuujenga mwili wa Kristo. Hakuna huduma muhimu kuliko nyingine, japo zinatofautiana ktk utendaji wake.

  Kristo pekee ndiye anatoa huduma hizo kwa Roho wake. Ni vema kila mtu kufahamu ameitiwa huduma gani ili aifanye kwa ukamilifu. Biblia inaonya kuna wachungaji wa mishahara, mitume wa shetani, manabii wa uongo na wainjilisti ambao Mungu wao ni matumbo yao; hilo hatutakiwi kulibeza.

  Kifupi ni kuwa, kuwa na huduma fulani, haikufanyi uwe superman. Utabaki kuwa mtu, tena unakuwa mtumishi, yaani unawatumikia watu.

  Yote juu ya yote, Yesu aliweka msingi, Mitume wa mwanzo wakajenga na mitume wa sasa hawana jipya la kuongeza, bali wanapokea ufunuo wa neno lile lile kwa ajili ya kulisimamisha kanisa katika msingi sahihi. Mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji na waalimu mpaka leo wapo. Lakini shetani naye anaowatu wake, hivyo piam kila kitu. Kipimo rahisi ni hiki: Mtu akisema ameitwa awe Mtume, pima kazi ya utume wake, kama yanenavyo maandiko. Akisema ameitwa kuwa Nabii, pima unabii wake, Mwalimu? anagalia anafundisha nini…n.k

 180. ndugu katika Bwana! BWANA Yesu apewe sifa sana! tafadhali naomba namba za simu na majina yao waandishi wa habari wa GAZETI LA UTATU, GAZETI LA MSEMAKWELI, GAZETI LA NYAKATI NA GAZETI LA KIONGOZI..yote ni magazeti ya kikristo! asanteni sana!

 181. je hivi kweli kwa sasa kuna mtu anayeweza kujiita yeye ni nabii au mtume? mbona sijawasikia wanaoitwa labda nabii Daniel au Ezekiel au Eliya? je haya majina ya kujibambikizia hawajui ya kwamba ni hatari? naomba jibu kutoka kwenu jamani mimi watu hawa wananichanganya sana! utakuta wanajiita majina makubwa tu kama vile MTUME NA NABII….yaani anashika ofisi mbili kwa pamoja, je kwa sasa kuna mitume?

 182. BWANA YESU ASIFIWE’…
  ningependa kupata somo la uchumba ‘KABLA NA WAKATI HUSIKA’Kijana wa kikristo aenende vipi?

 183. Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayofanya, naamini Mungu ataendelea kuwabariki. Ninatamani sana kupata nyimbo za Pastor Wambura. Nilikuwapo Tanzania kwa muda mfupi ila sikuweza kuzipata, kwa sasa niko nchini Estonia. Nitafurahi sana kama nitasaidiwa katika hili.

 184. Wapendwa bwana YESU asifiwe
  Mimi naomba kuombewa kazini kwangu sina amani kabisa, nina matatizo mazito ya migongano na wakuu wangu wa kazi, hivyo naomba mniombee hiyo roho iondoke kwa jina la YESU! Naamini hakuna lisilowezekana kwa MUNGU yote yanawezekana!

 185. Bwana Yesu asifiwe, nashukuru sana kwa kutufungulia hii website, naomba unisaidie namba ya Jackson Benty,pamoja na group la watu ambao huwa anaimba nao niliwahi kuwaona pia kwenye mkutano mkuu wa kinabii wa nabii GeoDavie.

  Pia kuna waimbaji wazuri wa nyimbo za kuabudu siwajui majina yao ila wanaimba mtindo wa R and B,wameimba wimbo wao mmoja unaimbwa,sema nami,sema nami,sema na roho yangu,sema na sema na roho yangu!
  wimbo mwengine ni,niguse tena,niguse tena,ninaomba Bwana,uniguse tena niguseee!!

  naomba mnisaidie majina yao pamoja na namba zao za simu,Pia naomba namba ya John Lisu,na ya Bahati Bukuku

 186. Help me to locate Dr Daniel Lema a former colleague at Corat Africva in Nairobi who is an Auditor and minister in Arusha. Could anyone give him my contacts and ask him to contact me? Thank you

  Dr Bishop Pepe Mutiri,Cleveland, Tennessee USA

 187. Asante sana Stictly Gospel! nimepata email ya John asante sana kwa ushirikiano wenu!
  Mungu awabariki!Dada Mary yupo????????????

 188. Kibii ,nakukumbuka verse 3 .inasema
  ” Waniambia usiogope ,utapata ujasiri mwingi kutoka kwangu”

 189. Dada Karungi,

  Email address ya John Paul imetumwa kwako kwa njia ya email.

  Asante

 190. Mpendwa Neema na watu ambao hawakuwa na taarifa:

  Mwili wa marehemu Fanuel Sedekia unaagwa leo Ijumaa, 9/1/2009, kuanzia saa Nane mchana katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
  Mazishi yatafanyika Jumamosi, 10/1/1009 katika eneo la makaburi ya Manispaa ya Arusha lililoko Njiro.

  Pole kwa msiba

 191. bwana yesu asifiwe wapendwa,poleni kwa msiba wa kaka yetu mpendwa fanuel sedekia
  ,naomba kuuliza mwili wa marehem utaagwa lini na saa ngapi na wapi,mazishi yatafanyika wapi.mungu awabariki na awatie nguvu

 192. Bwana YESU asifiwe! Namshukuru sana Mungu kwa ajili yenu wote mnaotumia hii blog kutuelimisha kwa ukweli inatia moyo sana,nimekuwa nikifuatilia sana hii blog kuna huyu John Paul for sure nimebarikiwa nae sana kwa namna anavyojibu kama inawezekana naomba nipate email yake binafsi!

  Nawapenda ktk Kristo Yesu!

 193. Bwana asifiwe

  Nduguzangu kama kuna yeyote anazo au anajua site ambayo naweza kuzi pata nyimbo za Rev. Charles Jangalson

  Thanks
  Godbless

 194. Hata mimi nahitaji contact za Zakayo Diigula. bado tunahitaji ushauri na mawazo yake. kwa sisi wasanii wa injili
  tafadhali wapendwa mtufahamishe.

 195. Heri za mwaka mpya wapendwa watengenezaji wa blog hii, na watumiaji wote wa blog hii. Kwa kweli blog hii imekuwa ya maana sana kwetu, ingawa nimegunduwa kwamba ipo si mda mrefu. Na mimi vilevile kama mwenzangu hapo juu, nahitaji contact za Diigula Zakayo kama inawezekana. Barikiwa.

 196. Ndugu Sosthenes Kamwila na ndugu Bonnie;

  Tutawatumia njia za mawasiliano ambazo mnaweza kuwapata watu mlioulizia katika anuani zenu za barua pepe mara baada ya sikukuu za mwaka mpya!

 197. Bwana Yesu asifiwe, nawea kupata contact ya Goodlucky Sandy kutoka Arusha, ambaye ni mtangazaji wa redio safina na mwimbaji wa nyimbo za injili. Ninavutiwa sana na njimbo zake.

 198. Wapendwa nauliza kuhusu, Zakayo Diigula! alipokuwa hapa alikuwa ni promota wa muziki wa injili vilevile alikuwa producer mzuri sana wa video’s, nasikia siku hizi anaishi marekani. Naombeni mnipe contact zake. Amen

 199. Naomba kuuliza kuhusu Beatrice Muhone yuko wapi, sijamskia kwenye gospel siku nyingi

 200. Bwana Yesu Asifiwe ndugu Kibii, Wimbo huo hatujaupata! kama yeyote anafahamu anaweza kusaidia!

 201. Bwana Asifiwe wapendwa.

  Mimi naishi ulaya. Kuna wimbo wa swahili natafuta verse ya mwisho. Niliimba zamani na inanifariji sana. Inasema:
  1. ‘Bwana asema, nimtume nani, naye ni nani atayekwenda badala yangu’.
  Chorus:
  ‘Nitume mimi bwana, nitume mimi bwana, nitume mimi bwana, nitume mimi bwaana’.
  2. Midomo yangu, ni chafu sana unichome kwa kaa la moto unitakaze.
  3. …………

  Nitashukuru sana.

  Baraza na heri za krismasi.

 202. Bwana Yesu Asifiwe ndugu Napendael, Christina Shusho ameolewa na ana watoto watatu!

 203. Bwana Yesu Asifiwe Neema, unaweza kuwasiliana na Ambele Chapanyota kwa simu hii +255 784 327 178.

  –Ndugu Samson Chambuso, kuhusu kupata nyimbo za Abiud Mishori, unaweza kuwasiliana nasi (Strictly Gospel) tunafanya huduma ya kutumanyimbo za waimbaji mbalimbali. Kwenye home page, TUWASILIANE utaona anwani zetu. Karibu

 204. Napenda mno nyimbo za kuabudu zilizoimbwa na Abiud Mishori lakini nasikitika kwamba kwa huku niliko kuzipata sio rahisi. Nipo kikazi nchini Lebanon. Can anybody tell me how I can get them?

 205. jamani naweza kuwapata contact za ambele chapanyota? mara ya mwisho nilionana naye mzumbe

  Neema from Boston

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s