NAMNA YA KUOMBA

Hatua na vipengele muhimu katika kuomba

 

MKARIBISHE ROHO MTAKATIFU. *Rum 8:26-27 *Yoh 14:16-17

Yesu alisema Roho Mtakatifu ni msaidizi wetu. Atatusaidia na kutufundisha yote, kwa maana pasipo yeye, sisi hatuwezi neno lolote. Na sisi peke yetu hatujui kuomba ipasavyo, bali yeye (Roho) ajua kutuombea kwa Mungu kama vile Mungu apendavyo. Hivyo kabla ya kuanza maombi au kusoma neno au ibada au safari au mitihani au kikao n.k. jifunze kujikabidhi kwa Roho Mtakatifu, uombe msaada wake, akupe ufanisi/ubora katika yote yakupasayo kufanya.

Tambua Utu wake, Uungu na Uweza wake.

Jikabidhi katika Nguvu ya Uongozi wake.

Tii kila Uongozi anaokupa.

FANYA TOBA NA UTAKASO. *Isa 59:1-2, Yoh 9:31, 1Yoh 1:8-9,7

Sikio la Bwana si zito kusikia wala mkono wake si mfupi kushindwa kututendea mambo tumwombayo, bali maovu yetu ndiyo yanatufarakanisha na Mungu wetu. Mungu hawasikii wenye dhambi. Hivyo chukua muda wa kutafakari na kuungama dhambi zako mbele za Mungu na kuzitubu kwa kumaanisha kuziacha. Mungu ni mwaminifu kutusamehe na kututakasa na uchafu wote. (Isa 1:18). Lakini, kabla hujafanya toba yako binfsi;

(i) – Kwanza, samehe wote waliokukosea, hata kama hawajaja

kukuomba msamaha. Usipowasamehe waliokukosea, na Mungu

hataweza kukusamehe wewe. (Math 6:12,14-15)

(ii) – Ndipo nawe ufanye toba yako binafsi. Na Mungu atakusamehe kabisa.

Hata kama ni nyekundu sana, zitakuwa nyeupe sana. (Isa 1:18, Isa 43:25)

3. MSIFU, MUABUDU NA KUMSHUKURU MUNGU. *Zab 147 na Zab 148

Msifu Bwana kwa Matendo yake makuu, mwabudu Bwana kwa uzuri wake na kwa sifa zake. Mwadhimishe Mungu kwa Tabia zake, wema wake, fadhili zake na baraka zake mbalimbali anazotutendea. Sifa yako ikifika vizuri mbele za Mungu, ndipo atakuwa tayari kukupa haja za moyo wako. Haja zetu zimefichwa nyuma ya mgomgo wa sifa. Ndio maana Neno linasema;

‘Nawe utajifurahisha kwa Bwana (kwa kumsifu, kumwabudu na kumshukuru), naye atakupa

haja za moyo wako’ (Zab37:4).

Yesu anatuonyesha mfano; angalia sentensi yake ya kwanza katika kuomba kwake imekuwa “Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe.” (Math 6:9). Anaanza maombi kwa kumsifu Mungu. Msifu Mungu kwa kuimba na kwa kunena/kusema/kuelezea. Mungu anataka kusifiwa na kutukuzwa. Ukifanya sifa nzuri, ya kuufurahisha moyo wake, atakupa hata na vile ambavyo hukutegemea/hukuomba.

4. MWELEZE MUNGU MAHITAJI NA HOJA ZAKO. *Wafilipi 4:6-7,19 Isa 43:26

Mweleze Mungu zile hoja zilizokusukumwa kwenda kumwomba. Nenda mbele za Mungu kama ‘kuhani’ (1Pet 2:9). Kwa unyenyekevu na heshima. Lakini kabla ya kumweleza mahitaji yako binafsi;

(i) Kwanza fanya ‘maombezi’ – ombea watu wengine; (1Tim 2:1-4)

Viongozi mbalimbali na wenye mamlaka, watumishi wa Mungu, marafiki zako, wenye shida, ndugu zako, nchi yako, shule yako, shirika lenu, ofisi yenu, chama chenu, n.k. Usianze kujiombea mwenyewe tuu, zoea kuwatanguliza wengine.

(ii) Kisha fanya ‘maombi yako’– ombea haja za moyo wako. (Math 7:7-11)

Mweleze Mungu haja zako. Ongea na Mungu kwa uwazi na ukweli. Japo anazijua haja zetu, lakini ameagiza kuwa tumwombe ndipo atafanya. ‘aombaye hupokea’ yaani; asiyeomba, hapati. Mungu anasema tumpelekee hoja zenye nguvu (Isa 41:21). Omba vitu vizuri na mambo makubwa ili upewe (pray for good things and big things)

5. FANYA MAOMBI YA VITA VYA ROHONI. *Efe 6:10-13 *2Kor 10:3-5

Baada ya kumwendea Mungu na kumweleza mahitaji yako, sasa simama kama ‘mfalme’, kwasababu wewe ni ‘mfalme’ (Ufu 5:8), tumia mamlaka yako ya kifalme, ongea na hali/hitaji ulilokuwa unaliombea, na kwa mamlaka, amuru iwe kama vile ulivyoomba/unavyotamani. Ndio maana Bwana Yesu alipokabidhiwa mamlaka yote na Mungu, naye akatukabidhi sisi (kanisa lake) “Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge na nguvu zote za yule adui. Wala hakuna kitakachowadhuru” (Luk 10:19, Yer 1:10, Yak 4:7). Tuma neno lenye mamlaka katika hali/jambo ulilokuwa unaliombea, Amuru iwe vile ulivyokuwa unamwomba Mungu iwe. Kemea kila roho ya shetani inayoweza kuwa inasababisha tatizo katika swala lako.

6. OMBEA ULINZI JUU YA ULIYOYAOMBEA. *Math 6:13a

Baada ya kupiga vita vya kiroho, weka ulinzi katika yale uliyoyaombea, ili shetani na mapepo yake wasiweze kuirudia hali/jambo/mtu yule uliyemkomboa kwa maombi ya vita. Yesu alisema shetani akifukuzwa mahali, haendi mbali, anasubiri kuona kama atapata upenyo wa kuparudia mahali pale alipokuwa kwanza. (Math 12:43-45). Kwahiyo, usipoweka ulinzi, kuna uwezekano wa adui kurudi na kuliharibu zaidi lile jambo uliloliombea na kulipata.

Kumbuka, unapoomba vizuri, unapokea papo hapo (katika ulimwengu wa roho), lakini udhihirisho wake katika ulimwengu wa mwili, unaweza kuchukua muda fulani. Hivyo katika muda huo wa kusubiri, shetani anaweza akapita na kuzuia au kuharibu kile unachokisubiri kidhihirike katika ulimwengu wa mwili. Ndio maana Yesu alitufundisha kuombea ulinzi, “tuokoe na yule mwovu” (Math 6:13a). Weka ulinzi juu ya mambo yako yote. Jengea wigo wa moto wa mbinguni (2Fal 6:16-17), Yafunike kwa damu ya Yesu na agiza malaika walinzi walinde mambo yako masaa yote. Omba hivyo kila siku. (Zab 34:7, Zab 91:9-11, Ebr 1:13-14)

MSIFU, MWABUDU NA KUMSHUKURU MUNGU. *Math 6:13b

Yesu alianza maombi kwa kumsifu Mungu na kumtukuza. Na akamaliza maombi yake kwa kumtukuza Mungu tena. Akasema “kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu ni zako, sasa na hata milele” akamaliza. Kwahiyo nawe kwa kumaliza maombi yako, msifu na kumshukuru Mungu tena, kwa ukuu wake, uaminifu wake, na ahadi zake juu yetu. Ndipo ufunge maombi yako.

MUHIMU: TUMIA MAANDIKO KATIKA KUOMBA *Kol 3:16

-Katika kuomba kwako, mara zote tumia maandiko kumkumbusha Mungu ahadi zake .(Isa 43:26). Mungu analiangalia neno lake ili alitimize. Sababu pekee itakayomfanya Mungu akupe alichoomba, ni ili kulitimiza neno lake. Hivyo, baada ya kumweleza unachohitaji (kwa ajili yako au kwa ajili ya mtu unayemwombea) mpe Mungu andiko/neno lake linalokupa wewe uhalali wa kuomba hicho kitu mbele zake na kupewa.

-Hata unapompinga na kumkemea shetani, baada ya kutoa amri yako dhidi yake, shetani atasubiri kusikia andiko/neno linalomnyima yeye uhalali wa kushika alichoshika. Ndio maana Yesu alimshinda shetani kwa neno la Mungu. Alisema “imeandikwa” na shetani akashindwa. “Nao wakmshinda (shetani) kwa damu ya Yesu na kwa Neno” (Ufu 12:11)

 MBINU ZA KUKUSAIDIA KUOMBA VIZURI  KWA MUDA MREFU

1. CHAGUA MAHALI PAZURI PA UTULIVU. *Mk 1:35

ili uweze kuomba kwa utulivu na kwa umakini, chagua au tafuta mahali pazuri

patakapokupa utulivu katika kuomba (concentration in prayer). Ndio maana Mungu

alipenda kuongea na Musa juu ya mlima. (Kut 24:12-18). Hata Yesu alizoea kwenda

kuombea mlimani, mahali palipo mbali na vurugu za watu, alipenda kwenda mlimani.

(Math 14:22-23). Tafuta mahali patulivu; chumbani, kanisani, mlimani (Math 6:5-6)

2. CHAGUA MUDA MZURI. *Mhu 3:1,7

Ili uweze kuomba kwa umakini mzuri, chagua muda mzuri ambao akili yako ma mwili

wako viko fresh. Usilazimishe kuomba hata kama akili yako au mwili wako umechoka sana. Kila jambo lina wakati wake. Kama umechoka sana, huo si muda wa kuomba, bali wa kupumzika. Usilazimishe ratiba. ni bora upumzike ili baadaye uweze kuomba vizuri baadaye. Usije ukajikuta unamkemea Yesu badala shetani. Penda kuomba wakati una nguvu ya akili na mwili, ili uwe makini kuongea na Mungu kwa akili timamu. Ndio maana Yesu alipenda kuamka alfajiri sana kwenda kuomba mlimani. (Mk 1:35, Luka 4:42)

3. OMBA KATIKA ROHO (NENA KWA LUGHA). *Efe 6:18, Rum 8:26-27

Mbinu nyingine nzuri ya kuomba kwa muda mrefu na kwa ufanisi, ni kuomba kwa Roho; yaani kuomba kwa kunena kwa lugha. Tunapoomba kwa akili za kibinadamu, Mungu anasikia pia, lakini maombi yako yanakuwa na mipaka / limited kwasababu akili ya mtu haijui kila kitu. Bali Roho wa Mungu anajua kila kitu. Naye hutupa kipawa cha kuomba kwa lugha ya mbinguni iliyo bora zaidi. (Yuda 1:20, Mk 16:17, 1Kor 14:1-4, 15-16,7)

4. OMBA KWA KUFUNGA WAKATI MWINGINE. *Math 6:16-18

Kufunga kula kunasaidia kudhoofisha mwili, ili roho iwe makini zaidi kuongea na Mungu kwa kina zaidi. Mwili huu siku zote haupendi kufanya mambo ya Mungu. Na mwili ukiwa umeshiba, unakuwa na uchovu na uzito wa kufanya mambo ya kiroho. Mbinu mojawapo ya kuudhibiti, ni kuunyima/kuupunguzia posho yake ya chakula. Mwili ukidhoofika kiasi, roho yako inapata nguvu na upenyo mzuri zaidi (Zab 35:13). Mashujaa wote wa imani walifunga na kuomba. Ndio maana Yesu anasema ‘mfungapo’ akimaanisha ratiba ya kufunga, ipo. Inasaidia.

5. OMBA NA RAFIKI (PRAYER PARTNER). *Mhu 4:9-10

Neno la Mungu linasema, ni heri wawili kuliko mmoja. Kuna faida ya kuomba pamoja na rafiki yako. Kwanza, mnapokuwa wawili au watatu, inaleta hamasa na ari ya kuomba zaidi. Si rahisi kujisikia mvivu unapokuwa na waombaji wenzako. Pili; nguvu ya kiroho inaongezeka. Neno linasema, mwombaji mmoja anafukuza adui elfu moja, bali wakiwa wawili, wanafukuza (sio elfu mbili) bali elfu kumi! Shangaa! (Kumb 32:20) Hiyo ni kanuni ya mbinguni/kanuni ya Ki-Mungu. Kadri mnavyoongezeka, nguvu ya Mungu huongezeka.

Kwahiyo, wakati mwingine, omba na rafiki yako, unayemwamini, unayeweza kumshirikisha mambo yako ya binafsi. Mashujaa wengi wa imani, walikuwa na marafiki wa kiroho. (Prayer Partners). Kwa Mfano:- Math 17:1-9

Musa – alikuwa na Joshua, Haruni na Huri

Eliya alikuwa na Elisha

Daniel alikuwa na Shadrack, Meshack na Abednego.

Yesu alikuwa na Petro, Yakobo na Yohana.

Paul alikuwa na Barnaba, Timotheo na Tito.

Wewe Je? Uko na nani katika urafiki wa kiroho?

 

Kama huna rafiki wa karibu wa kuomba naye, usikurupuke kujichaglia. Tulia umwombe Mungu akupe mtu atakayekuwa wa msaada kwako. Mtu mtakayefungamanishwa naye katika roho, hata kama mmetengana kijiografia, lakini katika roho, mko na umoja mzuri wa imani. (Math 18:18-19)

6. OMBA KATIKA MKAO UNAOKUPA UHURU NA NGUVU ZAIDI.

Katika kuomba kwa muda mrefu, mkao uliouzoea utakusaidia kwenda mwendo mrefu. Yakupasa kujua nguvu yako na udhaifu wako (strong point and weak point). Wakati wa kuomba, epuka mikao inayokuchosha haraka na tumia mikao inayokua nguvu zaidi. Kwa Mfano:- Ukiwa umechoka, usipende kuomba kwa kupiga magoti au kwa kuegemea kitandani. Ni bora uombe ukiwa umesimama au unatembea tembea, ili kuepuka usingizi na uchovu. Waombaji hodari wanaujua mikao inayowasaidia kuomba maombi marefu. Wengine hawana mikao maalum, bali wakiwa katika maombi, huwa wanabadilisha-badilisha mikao ili wasichoke. Hiyo ni mbinu nzuri pia.

Mifano ya Mashujaa wa imani;

Ibrahim – aliomba kwa kusimama (Mwa 18:22)

Daniel aliomba kwa kupiga magoti (Dan 6:10)

Paul aliomba kwa kupiga magoti (Efe 3:14)

Yesu aliomba kwa kulala chini (Math 26:38-39)

Eliya aliomba kwa kukaa chini na

kuweka kichwa kati ya miguu (1Fal 18:42)

Mimi huwa napenda kuomba kwa kutembea tembea

Naweza kumaliza kilomita nyingi chumbani kwangu

Nikitembea huku nikiomba.

Wewe Je? Unaujua mkao wa nguvu? Kama hujui, Tafuta kujua.

OMBA NA MUZIKI LAINI KWA KUMWABUDU MUNGU.

Muziki wa kiroho, na wataratibu, unaweza kukutengenezea mazingira mazuri sana ya kuomba kwa muda mrefu. Muziki wa kuabudu, unavuta uwepo wa Mungu kwa namna ya pekee. Neno linasema, waimbaji na wanamuziki walipoimba na muziki ukapigwa, nao wakawa kama mtu mmoja, utukufu wa Mungu ukashuka na kulijaza lile hekalu hata makuhani hawakuweza tena kuhudumu (2Nyak 5:12-14). Kule mbinguni, kila malaika wa sifa, ana kinubi (zeze/gitaa). Elisha hakutoa unabii, mpaka mpiga kinubi alipopiga kwa ustadi, ndipo mkono wa Bwana (Roho wa Mungu) alipokija juu yake, naye akatabiri.

Najaribu kukuonyesha, kuna connection kati ya muziki wa kiroho na utukufu wa Mungu. Kwahiyo, ukiweza kuomba huku umeweka kanda au CD ya nyimbo za kiroho za taratibu, utapata (experience) hamasa ya kiroho (motivation) na utasikia una nguvu ya kuomba kwa muda mrefu. Kama unaweza, tengeneza kanda au CD maalum yenye nyimbo nzuri unazozipenda wewe, ili uwe unaipiga wakati wa maombi. Utajikuta unaweza kuomba kwa muda mrefu na kwa bubujiko zuri zaidi

Mwl. Mgisa Mtebe,Bsc Economics

Mzumbe University,+255 713 497 654

mgisamtebe@yahoo.com

353 thoughts on “NAMNA YA KUOMBA

 1. Mbona hujaweka nukuu za vitabu vya roho ya unabii eg.Ellen White kama hayo unayoyasema ni ya kweli ni saws Bible inatosha ila bado rejea inahitajika ili kutudhibitishia hayo usemayo ni ya kweli na ni hakika

 2. Mungu akubariki, akuongezee na nguvu ya kumhubiri popote duniani mataifa wapate kumjua!

 3. Si kila kunena kwa lugha kunahitaji tafsiri. Kuna aina 3 za lugha ya Roho Mtakatifu.
  1. Lugha ya Maombi (intercessory tongue). Hii aliisema Yesu (Marko 16:16-18) na pia Mtume Paul (1Kor 14:1-5). Kila aaminiye, anaweza kunena kwa Lugha hii. Mtu hunena mambo yake ya siri za moyo wake kwa Mungu. Hivyo Kunena kwa lugha hii mtu HAHITAJI TAFSIRI mambo binafsi ya mtu. Mtume Paul aliita “lugha ya malaika” kwasababu binadamu anenaye na yule asikiaye, wote hawaelewi mambo ambayo Roho Mtakatifu ananena ndani ya mwombaji (Rum 8:26-27, 1Kor 14:2,14)

  2. Lugha ya Kinabii (Prophetic tongue ). Hii aliiongea Mtume Paul zaidi (1Kor 14:6-33). Swahili Bible wametumia neno “kuhutuhu” Lakini English Bible wametumia neno “prophecy” ikimaanisha “kutabiri” au kutumiwa na Mungu kuleta ujumbe kwa watu. Hivyo kuna kunena kwa ajili ya kulijenga kanisa, basi kunena kwa lugha hiyo ndo inahitaji tafsiri. tena wanenaji wa hii, wasiwe wengi. Tena wangojane. Lakini ile ya kwanza (intercessory tongue) , mtu hasemi na watu bali na Mungu. Hii HAITAKIWI TAFSIRI.

  3. Lugha za Wanadamu (Men tongue ). Hii imesemwa na Luka Mtakatifu alipoandika Matendo ya Mitume 2:1-22-nk. Mtu ananena kwa lugha ambayo ni ya wanadamu wa hapa hapa duniani. Japo yeye mnenaji anaweza asijue kuwa alipokuwa ananena kwa msaada wa Roho, alikuwa ananena kinyaturu au kiarabu au kichina. Ila wanadamu hao waliopo, walisikia ujumbe kwa lugha zao.

  MSIKATAZE KUNENA KWA LUGHA. NENO LA MUNGU NI PANA SANA.

 4. Naitwa Stephen Tungu 1/12/2016
  Kuhusu kunena kwa lugha katika maombi utakuwa unaongea na nani kama hakuna mtu wa kutafisri maana mitume waliponena kwa lugha watu waliokuwepo walisikia kwa lugha yao na wakamtukuza Mungu na si vinginevyo soma 1 Kor 14:1-40

 5. Mungu akubariki mtumishi wa Mungu. Je, mafundisho au masomo yako mbali mbali naweza kuyapa yote ukanitumia? NAHITAJI SANA

 6. MIMI NAITWA MWASHIBANDA WA KKKT KOLA MOROGORO NIOMBE MUNGU AKUPE ZAIDI MAANA KWA KWELI MIMI NIMEKUWA NATUMIA KAMA SOMO LILIVYONINAPOKUWA NA HUDUMA KATIKA MAENEO TOFAUTI

 7. Ubarikiwe na bwana Mtumishi kwa mafundisho haya mazuri. Nimepata pa kuanzia sasa . Mwenyezi Mungu akubaliki kwa kila ufanyalo.

 8. nashukuru sana kwa mafundisho nimeona nguvu za mungu kupitia mafundisho hayo.mungu awabariki sana.

 9. Asante mtumishi wa Mungu kwa Mafundisho mazuri nimebarikiwa sana na nimejifunza naomba ya kuomba na kuambatana na mtu mwingine kuwa kunatia nguuvu zaidi sawa na mafundisho ya watumishi wa Mungu waliopita,

 10. Asante sana mwalimu tena mtumishi kwa funzo zuri la kiroho. Nimejifunza mengi nashukuru

 11. AMIAMINA…barikiwa sana. Hakika nimefarijika sana na nimejifunza mambo mengi sana. MUNGU azidi kukuinua katika utukufu na kukubariki zaidi

 12. Amina, Bwana azidi kuwatia nguvu kwa mafundisho mazuri kwa kweli yananibariki sana na kuniimarisha kiroho

 13. Mungu akubariki sana mtumishi wa mungu, leo kupitia mafundisho yako nimejifunza jinsi ya kuomba

 14. Utukufu kwa BWANA Yesu Kristo. Mnanitia moyo kama mafunisho haya yanaeleweka na yanawasaidia kwa namna fulani. Tayari somo liko ktk kitabu chake na CD (mp3) yenye vipindi 7 ndani yake. kwa maelezo zaidi, tembelea website yetu kwa anuani http://www.mgisamtebe.org, WAPO Redio FM 98.1 kila Alhamisi, at 10pm-11pm and Upendo Redio FM 107.7 kila Jumanne at 9pm-10pm. Nawatakia kkua katika Neema juu ya Neema (Yoh 1:16), Imani juu ya Imani (Rum 1:17), Nguvu hata Nguvu (Zab 84:4-7) na Utukufu hadi Utukufu (2Kor 3:18)
  Mwl. Mgisa Mtebe (0713497654)

 15. hongera kwa kazi nzur ya kiroho unayotoa humu!kwangu nimeipata katika wakati mzur sana na naamin “wanadamu tumekua wagumu kumtumikia mungu kwakua mambo ya kidunia yametawala nafsi zetu”lkn ukimwamin na kumtanguliza MUNGU hakika yote yanawezekana!pasipo kuyatazama macho ya wanadamu!ubarikiwe MTUMISHI WA MUNGU!Kwa somo hili

 16. Ahsante kwa somo zuri mungu akubariki sana nimejifunza kitu kikubwa sana katika kuomba

 17. pole kwa kazi iliyo ngumu na nyepesi kwa kuwa wayafanya haya katika mungu ubarikiwe sana mtumishi nae mungu wa mbingu akufanyie wepesi katika hili naweza sema nashukuru kwa kuitengeneza imani yangu mara dufu

 18. Mungu akubariki katika kutufundisha jinsi ya kumuomba yeye aliye juu maana bila yeye tusingelikuwa hapa

 19. NASHUKURU SANA JAMAN KWA SOMO HILI LA MAOMBI, LIMENIJENGA SANA TENA SANA, NAHITAJI KUTENDEA KAZI SASA

 20. mbalikiwe,sabab naimani toka nianze kuingia mitandaon mara chach sana kukutana na neem hii na maarif nilipata leo.nimepat shida sana maan kila nikiomba siwezi kuzidisha nusu saa,yaan siku hata ikifik hiyo nusu saa nasema leo nimeomba kweli. kumbe nilikua bado mchanga nashukul nimetambua wap nilikua nakosea amina.

 21. MUNGU APEWE SIFA; MTUMISHI WA MUNGU MWL MGISA MTEBE SOMO LAKO LIMENIFUNGUA SANA HASA KUHUSU NAMNA YA KUOMBA HAKIKA NIMEVUTIWA SANA NA SOMO HILO HAPO JUU HASA KIPENGELE CHA KUFUNGA SOMO HILI LIMENIKUTA NIKIWA KWENYE MFUNGO HIVYO MUNGU AENDLEE KUKUTUMIA VEMA. UBARIKIWEA SANA,

 22. Napenda kumshukuru Mungu kwa ajili yako mtumishi kwani Roho wa Mungu anakuongoza na kukutumia hasa juu ya mafundisho yako. sifa na utukufu nikwa Mungu mwenyewe.

 23. Utukufu kwa mungu.
  Ahsante kwa mafundisho yaliyo mema, yaani kunifundisha KUKUMBUKA.
  Musa – alikuwa na Joshua, Haruni na Huri
  Eliya – alikuwa na Elisha
  Daniel – alikuwa na Shadrack, Meshack na Abednego.
  Yesu – alikuwa na Petro, Yakobo na Yohana.
  Paul – alikuwa na Barnaba, Timotheo na Tito.
  Wewe Je? Uko na nani katika urafiki wa kiroho?

  MIMI NIKO NA FRANCIS na YASINTA

  Hupenda kuomba nikiwa nimelala.

 24. Shalom.
  Naitwa Lucy,

  Mungu anataka kusifiwa na kutukuzwa. Kweli sifa na zivume kwa kuwa nifanyapo sifa nzuri, ya kuufurahisha moyo wake,atanipa hata na vile ambavyo sikutegemea wala kuomba. Anifundishe ipasavyo kuomba, kushukuru, kuheshimu na kuabudu yanipasayo.
  Yer.3:33

  Nsongo

 25. Utukufu kwa BWANA. Mnanitia moyo kama vinaeleweka na vinawasaidia kwa namna fulani. Tayari somo lina kitabu chake na CD (mp3) yenye vipindi 7 ndani yake. for more, visit http://www.mgisamtebe.org, WAPO Redio FM 98.1 kila Alhamisi, at 10pm-11pm and Upendo Redio FM 107.7 kila Jumanne at 9pm-10pm. Nawatakia kkua katika Neema juu ya Neema (Yoh 1:16), Imani juu ya Imani (Rum 1:17), Nguvu hata Nguvu (Zab 84:4-7) na Utukufu hadi Utukufu (2Kor 3:18)
  Mwl. Mgisa Mtebe (0713497654)

 26. Utukufu kwa BWANA. Mnanitia moyo kama vinaeleweka na vinawasaidia kwa namna fulani. Tayari somo lina kitabu chake na CD (mp3) yenye vipindi 7 ndani yake. for more, visit http://www.mgisamtebe.org, WAPO Redio FM 98.1 kila Alhamisi, at 10pm-11pm and Upendo Redio FM 107.7 kila Jumanne at 9pm-10pm. Nawatakia kkua katika Neema juu ya Neema (Yoh 1:16), Imani juu ya Imani (Rum 1:17), Nguvu hata Nguvu (Zab 84:4-7) na Utukufu hadi Utukufu (2Kor 3:18)
  Mwl. Mgisa Mtebe (0713497654)

 27. Mwalimu ubarikiwe kwa mafundisha mazuri. Nimehamasika sana katika maombi Jina la Bwana libarikiwe.

 28. Ubarikiwe sana Mtumishi wa Mungu. Mafundisho yako ni ufunuo wa kipekee kwa wengi. Mungu akubariki na kukujalia afya njema ili uweze kuendelea kutuelimisha.

 29. mtumishi ilisomo nimelipenda sana MUNGU akubariki zaidi na zaidi BARIKIWA sana

 30. Nimebarikiwa sana, na shuhuda na mafunzo na Mungu awazidishie, lakin Nina swali moja je katka kuomba ntajuaje kama hii n sauti au mpango Wa Mungu jambo Fulani kutokea

 31. Mungu wa rehema akuzidishie uweza wa kutufundisha mafundisho haya. Nimesikia furaha ya moyoni kweli kwa kupata mafundisho haya.

 32. Mwenyezi Mungu akupe nguvu na azidi kukuimarisha katika njia ya kueneza injili kwa wanadamu. Hakika nimepata faraja!

 33. Mungu azidi kukuinua katika utumishi huu na akufunulie yaliyo mazuri katika maisha yako pia Mungu akubariki sana kwa mafundisho yako yote.AMINA

 34. Mungu azidi kukuinua katika ujumishi huu na akufunulie yaliyo mazuri katika maisha yako pia Mungu akubariki sana kwa mafundisho yako yote.AMINA

 35. Asante mtumishi wa Mungu , umefanya kazi njema kutujenga kiroho, jina la Bwana Yesu akupaye nguvu, ufahamu na uwezo alihimidiwe. AMINA

 36. Asante, mtumishi wa Mungu. Mungu akubariki na akutie nguvu na maarifa katika kutenda kazi yake, kwa ajili ya utukufu wa jina lake. AMINA

 37. Mungu akubariki mtumishi umenipa kitu ambacho nilikuwa sikijui roho wa mungu aendelee kusema na maisha yako ya kiroho ili nasi tuziidi kushibishwa roho zetu kwa mafundisho yake.AMINA

 38. Kwaza napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniongoza katika kutafuta neno lake katika sehemu mbalimbali maana nimekutana na mbinu, ushauri na maombi mazuri ambayo nakiri toka nizaliwe sijawahi kufahamu namna nzuri ya kuomba. Pili napenda kukushukuru Mwalimu kwa mafundisho yako mazuri juu ya maombi yaliyo ya kweli. Nasema Ubarikiwe sana na Mungu akupe kila lililo hitaji lako hapa duniani na abariki hata kizazi chako pia. AMINA@

 39. Naamini ipo siku MUNGU aliye HAI atafanya alilolikusudia katika maisha ya kila mwenye mwili anayemtegemea, tuendelea kumwomba tusikate tamaa maana yeye ni mwaminifu kwa ahadi zake. AMIN!

 40. mimi nateswa na roho za kupoteza na kuibiwa nimeomba mpaka nimechoka ninalia na Mungu usiku na mchana sipati jibu matatizo ndio yanapamba moto kuibiwa kupoteza mashine zangu ofcn zinakufa nanunua spare mafundi waazidi kuziharibu haziponi copy computer magari matatu yameharibika miaka miwili hayaponi mafundi wanakula pesa tu nimefunga nimechoka kila j. mosi nafunga na ninakesha nikimuomba mungu. nisaidieni jamani hali hii imenitesa tangu 2008 nimechoka mwili akili na roho.

  matatizo haya yamenifanya nikawa komandoo wa kufunga ninaweza hata kufunga 3 kavu nimewahi kufunga siku 40 nikapata ufumbuzi fulani lakini bado matatizo hayajaisha

  naomba ushauri

 41. Haleluya Mungu azidi kukufunua katika kufundisha kwani shambani mwa Bwana mavuno ni mengi lakini watenda kazi ni wachache.

 42. Mungu akubariki sana, mafundisho yako yamenipa mwanga mpya wa kiroho na yamenibariki sana

 43. Thank you brother Mgisa. Ni neema ilioje kuwa na mtumishi kama wewe Tanzania. Hakika wewe ni zawadi ya Mungu kwa ajili ya Tanzania. Mungu akubariki! Amen.

 44. mungu akubariki san kupitia mafundisho na semina inayoendela pale boko lutharani, nimebarikiwa sana mungu nakubariki.

 45. Mungu mwenye rehema na neema nyingi akubariki na kukuzidishia hekima uendelee kutumika kutufundisha.ubarikiwe sana mwalimu.

 46. Kusema ukweli Mtume Paulo anasema “Usiuendekeze mwili kuupa matakwa yake” sasa ukisema umechoka usisali maana yake hutasali hata siku moja maana hakuna siku ya starehe au kinyume chake tusifanye kazi ili tusichoke tusali tu. ikiwa unaelewa maana ya sala na kwamba Mungu yupo popote huwezi kuchagua mahali pa kusalia. Ingawa kuna muda ambao unatakiwa utulie mahali ili kuongea na Mungu lakini hiyo haizuii wewe kusali wakati wowote na maali popote.

 47. Mungu akubariki sana kwa mafungisho haya, kwani nilikuwa naomba pasipo mpangilio, sasa nimejifunza namna nzuri yakuomba na kuyawekea maombi ulinzi wa malaika wa Mungu ili malaika wabaya wasiweze kuharibu Baraka na Neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

 48. Bwana yesu asifiwe…Nashukuru kwa andiko hili hakika nimejifunza mno maana nilikuwa nasali kijumla jumla na sasa nitazingatia hii flow ya kumwita roho mtakatifu, kuabudu then kusifu.Barikiwa Mtumishi..

 49. Roho wa bwana awe na we mtumishi wa mungu. Nimejifunza mengi kupitia ujumbe wa mungu wa MUNGU uliopewa utufikishie watumishi wake!!!!!!!!!!!! Bwana akubarik sana

 50. Nimepata kitu katia mafunzo haya,Bwana anitie nguvu nami niweze kuyafanyia kazi kwani hata nilipokuwa nasoma nilihisi kanakwamba naomba! Mungu akubariki!!

 51. Barikiweni wote wapendwa katika Bwana,,,,,
  Malaika walinzi waweke ulinzi wao Kwa vitanda vyenu…….
  Type amen

 52. Uonapo Kama hii website imekusaidia basi Hebu nawe okoa mmoja.kuna vijana wana hold conversation Facebook na kwingineko ambazo hazina manufaa Kwao….please Hebu tuwashauri vijana wenzetu ili wajiunge kwenye SG……

 53. Amina mtumishi wa Mungu,nimefarijika sana na mada,maudhui yaliyomo kwani Hakika wakati nikisoma nimehisi naongea na mungu moja Kwa moja…….
  NI upendo wa mamna gani ametupa mungu.?
  Nawaombeeni watumishi wote na mungu Waite nguvu katika kueneza injili yake…..
  Amina,,,

 54. Mushi Caroline
  mtumishi ubarikiwe sana kwa makala hii ubarikiwe na Bwana
  Nimeweza kupata mtiririko mzuri wa maombi

 55. aminaaa..cz maombi ndo kila kitu..na lazma uwe na neno ya kumwambia MUNGU huwez kuomba Kiwanisiwe sana
  mtupu huna maandiko..na huko ni kukosa shabahaa..utaomba sana bila kuwa na shabaha ni kaz buuree..ubar

 56. Asante mtumishi kiukwel nimefurahi sana kwa mafunzo haya,mungu akujalie afya njema ya mwili na roho ili uendelee kutufunza.

 57. Hakika mtu aongozaye wengine kutenda mema atang’aa siku ile. nimeongezewa hatua kubwa kiroho kupitia mafundisho haya. Bwana akuongezee zaidi na akufanye uwe kielelezo. nuru yako iangaze zaidi watu wengi waione na wamtukuze Mungu!!

 58. Hakika nimejifunza jambo bora sana katika mafundisho haya Mungu abariki kazi zako

 59. Bwana YESU apewe sifa,. mtumish wa Mungu ubarikiwe sana kwa kutupa chakula cha roho,. tumejifunza mengi katika kuomba, stay blessed

 60. TUNAKUOMBEA UZIDI KUFUNDISHA MUNGU AENDELEE KUKUZA KIPAWA CHAKO HICHO BARIKIWA SANA AMEN.

 61. Mungu akubariki mtumishi wa Bwana mwalimu Mgisa. tunabarikiwa sana tukisoma mafundisho yako na tunajikuta tunasonga mbele kiimani na kuomba. Mungu aendelee kukutumia kama chombo.

 62. Praise be to God,finally i’ve found wat ve bn lookin’ for all ths tym,bt God is gud i’ve got it now.b blssd man of God

 63. sifa na utukufu namrudishia Mungu wetu aliyekupa marifa na ufunuo Mwl.nimejifunza kuwa maombi zaidi ya mmoja yana faida.

 64. Jamani Mungu azidi kukubariki na kukufunulia zaidi,nimepata vitu muhimu sana ambavyo nilikuwa sivijui,kweli Mungu anapatikana tukimtafuta kwa bidii.

 65. Asante sana mwalimu, mimi nimeanza maombi kwa ajili ya mtoto wangu anayemaliza kidato cha nne lakini nilikuwa napata shida jinsi ya kuomba, ikabidi niingie katika mtandao ili kujifunza jinsi ya kuomba maombi maalum, na ndipo nikakutana na maelekezo haya. nakushukuru sana mwalimu nimepat upeo mkubwa sana ambao sikuutarajia, mungu akuongoze utupanue zaidi na zaidi. UBARIKIWE SANA.

 66. Asante sana mwalimu mgesa mtebe umenifanya na kuweza kunibadilisha kujua Mungu katika ulimwengu huu juu kuna mambo mingi ambazo mimi sikua nazijua na mpaka kupitia kwa masomo yako kwa kweli nimejua kweli Mungu yuko nasi Mungu akubariki na uweze kuishi miaka mingi hili uweze kufunza watu neno la mungu Asante sana ubarikiwe.

 67. Akii Mungu awabariki nimejengeka kiroho ju nimekua nikiomba na cd za Kuabudu na uomba sana lakini huona kueka cd uchangie nisinzungumze kwa lugha au Roho Mtakatifu..ki lugha au kutabiri..God blss everyone…

 68. Ubarikiwe mtumishi wa Mungu kwa mafundisho yako hasa somo la jinsi ya kuomba.\
  nimejifunza kitu kwa kweli. Mungu akubariki sana kwa huduma yako

 69. Thanx sana mwl binafsi nimebarikiwa na mwongozo wako jinsi ya kuomba na nitapractise sasa ili Mungu anionekanie maana nilikuwa nachanganya mambo na sikuwa napata majibu mazuri!

 70. Bwana Yesu Asifiwe
  nashukuru kwani nami nimejifunza pale nilipo kuwa nikikosea sasa ni wakati mzuri wa kujisahihisha asanteni

 71. nami naomba Mungu azidi kunisaidi sana sana kwa majaribu ambayo nimeyapata kutoka kwa mme wangu ivyo nahitaji kuomba sana ili niweze kuwa sawa kiakili

 72. Bwana Yesu Asifiwe, nashukuru sana kwa mafundisho juu ya kuomba maana unaweza kujikuta unaomba bila kujua unaanzaje, kuomba kumbe basi kuna vipengele vya kuanza kuomba nashukuru sana na Mungu akubariki amen

 73. Bwana asifiwe, nashukuru sana kwa mafundisho yako kwani nimejifunza vitu ving ambavyo sikuvijua. Mungu akubarik sana.

 74. Mungu akubariki mtumishi kwa masomo mazuri.Nimebarikiwa hasa katika somo la namna ya kuomba.

 75. Mungu akubariki sana kwan sasa nimepata kufunguliwa ktk kifungo nilichokuwa maana nilikuwa sijuw kuuomba lakin kwa hili somo nimepata kujuwa,Mungu akubariki sana Mtumishi wa Mungu

 76. Mungu azidi kukupa nguvu katika kutafsiri neno la Mungu ili lipate kujenga mioyo yetu katika kuabudu na kumsifu

 77. Mungu akubariki mafundisho yamenigusa sana nami sasa naweza kuomba mwenyewe

 78. Nimefurahia masomo haya maana watu wengi wanaomba bila utaratibu,ahsante mimi mwenyewe nimejifunza.Mungu akubariki Mchungaji.

 79. Napenda sana masomo yako, na malanyingi huwa naya print, au na copy kama yalivyo, bila ya kuongeza wala kupunguza neno, then natoa copy kwa gharama zangu na kugawa bure kwa wengine. MUNGU AKUBARIKI SANA KWA MASOMO MAZURI. Amen.

 80. Kwa kweli siwezi sema ila Mungu wa mbinguni ameona mwenyewe barikiwa na azidi kukupa maarifa zaidi katika kutupatia

 81. Mwalimu ahsante sana kwa darasa lakini nashukuru sana mara tu nilipo ingia kwenye brog hii nilikuwa na usingizi lakini ghafla usingizi ukaniishia jina la Bwana lisifiwe amen.

 82. Amen nimejifunza jambo kubwa sana ambalo linanifanya niendelee mbele kwenye maombi, ni kweli Mungu ana mpango na watu wake, kwangu mimi leo ni siku njema sana kwani Mungu Roho Mtakatifu amenifunulia jambo asubuhi ya leo nikiwa kazini na sasa ametaka nijue jinsi ya kuomba hasa maombi ya vita! Mungu akubariki sana Mtumishi wake, hakika Mungu amesema nami wazi wazi kupitia mafundisho yako. Barikiwa AMEN

 83. Mtumishi nimebarikiwa sana na somo hili la maombi limekuwa msaada kwangu kwa jinsi ya ajabu mnoo.Mungu akubariki sana

 84. Mtumishi wa Mungu ubarikiwe sana, kwa mbali na anza kuona mwanga ukiangaza fahamu zangu, ubarikiwe sana.

 85. Mwl.Mgisa Mungu akubariki sana ktk utumishi wako hakika nimejifunza mengi na nimeona wapi nakosea

 86. Mungu akubarikie sana kwa mafundisho yako mazuri akujaze nguvu na aman ya rohoni kwa maana silaha nzuri ya mwili ni upole, uvumilivu,heshima ,upendo nk

 87. Mungu akubariki sana mimi sijui namna ya kuomba kabisa sasa nimepata mwangaza nlikuwa naomba kama naongea na mtu thanks so much.

 88. Ubarikiwe sana sana. nilikuwa sifahamu hayo. asante sana umenisaidia sana maana napata shida sana niombapo. kiujumla najifunza kuomba.

 89. Mwl ubarikiwe sana kwa somo lako la maombi umenifungua kwa mambo mengi Mungu awabariki wote waliosoma somo lako la maombi wapate kuwafikishia waumini wengine Amen

 90. Mungu akubariki sana Mtumishi,nimejifunza mengi kupitia somo hili.kweli ni shauku ya moyo wangu kuomba kunako mpendeza Bwana.Mungu akubariki mnoooooooooo.

 91. Mnanitia moyo sana sana sana kwa namna mnavyoonyesha kwamba Neno/Somo hili linavywasaidia wengi. Mnaweza kupata masomo mengine mengi kwa kutembelea website yetu ya http://www.mgisamtebe.org, kisha gonga kitufe cha Bible Lessons; download na uwasambazie wengine wengi. wakaribishe uwapendao kutembelea site yetu. Utukufu apewe Bwana.

  Ninapenda pia kuwakaribisha katika vipindi vya mafundisho kwa njia ya redio, kila siku za Jumanne, kupitia Upendo FM redio 107.7 kuanzia saa 3:00 usiku mpaka saa 4:00 usiku; na kila siku ya Alhamisi, kupitia WAPO Redio FM 98.1, kuanzia saa 4:00 usiku mpaka saa 5:00 usiku. Kwa wale walio nje ya Dar, mnaweza kupata redio WAPO kwa njia ya mtandao http://www.gospelkitaa.blogspot.com

  Weka kengele kwenye simu yako, ili ikukumbushe muda wa vipindi ukifika. Endapo utapenda tuwe tunakukumbusha kwa njia ya simu, andika neno KIPINDI, na ulitume kama ujumbe mfupi (SMS) kwenda namba 0713497654. muda fulani kabla ya kipindi kuanza, utapokea kikumbusho kupitia simu yako ya mkononi.

  Endapo ungependa kuwa unapata mafundisho mbalimbali, kwa njia ya email yako, tuma email yako kama ujumbe mfupi (SMS) kwenda namba 0713497654.

  Mungu akubariki sana.

 92. Mungu akubariki sana mtumishi wa Mungu,akujalie mema na akupatie umri mrefu ili uzidi kuifanya kazi yake na kuuleta ufalme wake.Somo limenitoa sehemu moja kwenda nyingine juu ya ufahamu ktk kuomba.Asante sana mtumishi Utukufu, Sifa na Heshima ni kwa BWANA wa mabwana akuwezeshae kuyatenda haya.

 93. Barikiwa na Bwana.Ni maombi yangu BWANA awainue waombaji,hasa wakati kama huu.Na yale Bwana aliyoyaahidi ktk 2Ny 7:14 yatimie kwetu.( kusikia maombi yetu,kusamehe dhambi zetu,na kutuponya )AMEN.

 94. asante sana mtumishi Mungu azidi kukufunulia makuu yatokaye kwake nasi tupate kupokea asante sana kwa kutupa njia jinsi ya kuomba na kusimamia maandiko Mungu akubariki wewe na familia yako na awazidishie Amen.

 95. mwl ubalikiwe kwa msaada wako ulioutoa. umenipa mwongozo mkubwa kwasababu nimempokea yesu hivi karibuni kwahiyo umenipa mwanga katika maombi

 96. Asante Mwalinu Mungu akubariki nimejigunza mambo mengi kupitia kwako naimani Mungu atanipa nguvu.Amen

 97. Namshukuru Mungu kwa ajili ya kutambua namna ya kuomba sasa nitapata Baraka nyingi kwa Mungu aliye Hai na neno lake ni Hai.

 98. nimenyeshewa nvua ya baraka kwa somo hili, na pia naongezekewa kiu rohoni
  kwa hiyo Mungu wetu apewe sifa na akubariki wewe mtumishi wake
  mwalimu Mgisa Mtebe

 99. Asante kwa chakula kizuri mtumishi,siku zote ntataman kula chakula cha namna hii ili Roho yangu ishibe.

 100. Ubarikiwe sana kaka, nilikuwa sijui namna ya kuomba lakini kwa maelezo yako nimesoma, namwomba roho wa mungu anisaidie nisimamie maelezo yako katika kuomba

 101. Mwitikio wenu unanipa kujua kuna haja ya kusinga mbele katika kulipa gharama ya kufundisha watu, mbarikiwe sana. msiache kuniombea ili nizidi kupokea na kutoa. Nanyi pia anyieni kazi maneno ya Mungu, tuone mabadiliko mazuri. endlea kupata mafundisho kupitia http://www.mgisamtebe.org au WAPO Redio 98.1 kila Alhamisi usiku wa saa 4 mpaka 5. Sambaza taarifa hizi kwa wengine.

 102. Nimebarikiwa sana na Mafundisho mazuri, Roho mtakatifu azidi kukuongoza. Umenipa mwongozo mzuri sana wakati wakuomba nimefarijika sana. Mungu akupe nguvu na Uweza katika yote.

 103. Mungu ashukuriwe na Roho Mtakatifu aliyekuongoza kuandika page hii,nakuombea hekima na akili zaidi kwa msaada wako kwa umma na kizazi kiishicho.

 104. kwa kweli nakubaliana na wewe kabisa hasa katika kipengele cha kuweka muziki wa kuabudu na mkao wakati wa kuomba, mimi bila kuweka kamuziki kwa kweli naona huwa nakosa flow nzuri ya maombi na mikao mingine nikikaa kwa kweli hata uwepo wa Mungu siusikii, ila nikipiga magoti na kuimana chini weeeee naona kama Yesu kaingia mzima mzima ndani

 105. Nashukuru sana,mwalimu umenifungua kwa sehemu kubwa ktk kipengele hiki.Ubarikiwe na Yehova.

 106. Mungu mweza wa mambo yote hata yaloyojificha ameweza kuwajulisha wampendao siri iliyojificha ya namna ya kwenda kunako kubalia mbele zake.Ni maombi yangu kwa Mungu akutie nguvu, na Roho Mtakatifu aendelee kukufundisha zaidi na zaidi ili tupate kile alicho kusudia kwetu tuaminio katika Yeye Yesu Kristo.
  AMEN

 107. Nashukuru sana Mwl l jana nilikuwa kwenye semina wazo nikaona website yako nimefungua na kusoma jinsi ya kuomba nimepata vitu vingi sana ,Mungu azidi kukubariki na kukupa nguvu na uweza katika jina lake,

 108. MUNGU AKUBARIKI KWA MAANA NIMEPATA KITU ROHO YANGU IKAFURAHI, NAOMBA TUOMBE PAMOJA NIPO KWENYE WAKATI WA KUTAFUTA KAZI. MUNGU AKUBARIKI SANA.

 109. MOYO WANGU UNABARIKIWA SANA NIPATAPO MSAADA WA KIROHO. MUNGU YU MWEMA SANA JAMANI. TUMTAFUTENI KWA BIDII, KWA NJIA ZOTE, ATATUONEKANIA TU. AMINA

 110. Ninakushukuru Ingawa sikufahamu. Nimepata msukumo moyoni tu na ku-goggle “Namna ya Kuomba” post yako ikaja. Kwakweli umenishibisha. Niko katika wakati mgumu, ambao ninasikia sauti moyoni mwangu ikiniambia kila siku kuwa nifunge na niombe, kwakweli ninaamini ninachokihitaji nitakipata. Mungu akubariki kwa kunipatia mwangaza. Amen

 111. NIMEWEZA KUELEWA NA KUJIFUNZA MENGI KUHUSU MAOMBI NLIKUA SIJUI SIRI YA KUJUA KUOMBA NA KUA KARIBU NA MUNGU WANGU JAPO KUNA WAKATI NAKATA TAMAA SANA ASANTE KWA KUELEWESHA

 112. Mungu akubariki saana Mtumishi nimeyapenda mafundisho yako nimetiwa moyo nimeinuliwa nimehuishwa tena! niko na maombi ya siku 3 ya kufunga, ninamwitaji Yesu katika maisha yangu ayabadilishe na kunifanya wa tofauti, kunitoa hapa nilipo na kunipeleka anapotaka yeye. ninauhitaji wa kazi nimeomba kwa maombi haya naamini Bwana tayari amekwisha nipatia ni yangu kwa imani. nahitaji maombi yako zaidi.

  Ubarikiwe Mtumishi

 113. Ubarikiwe. Asante kwa somo na kwa kunikumbusha kuandaa nyimbo za kufanyia maombi.

 114. Kwanza kabisa namshukuru Mungu sana alie nikutanisha na haya mafundisho yako Mtumishi wa MUngu .kitu ambacho kilikuwa kinanisumbua ktk maisha yangu namna ya kufanya maombi muda mwingi huwa nimekaa kitandani huwa najikuta nachoka mapema na maombi yangu yanakuwa niyamuda mfupi mno.lakini ajabu kama nikiwa naimba nyimbo mapambio huwa nalalia mgongo hapo naweza imba mpaka asubuhi ,nawakati huo machozi yakimwagika.Nakushukuru sana Mwl Mgisa nathani nimepata ufumbuzi wa maombi yangu Mungu akubariki sana.

 115. Amen. Mbarikiwe sana atumishi wa Kisto Yesu aliye hai kwa kujitoa kwenu kuwaonesha wengine mapenzi yake.

 116. Ni somo zuri sana la kumsaidia mkristo kuukulia wokovu na kuwa na mbinu bora za maombi. .

  Nimebarikiwa vya kutosha.

  Mungu akubariki sana.

 117. Mungu akupe kuongezeka katika maarifa yake ili uishi maisha ya ushindi na mafanikio. Ni maombi yetu kwamba masomo haya yalete mabadiliko mazuri katika maisha ya watu wote wa Mungu. Nakutia moyo kusambaza ujumbe huu kwa watu wengi zaidi, ili dunia ijazwe maarifa ya Mungu kama maji yaifunikavyo bahari. Tembelea http://www.mgisamtebe.org kwa masomo mengi zaidi. sikiliza WAPO Radio kila alhamisi saa 4:30 usiku hadi sa 5:30 usiku kwa mafundisho mengi zaidi. Mary Damian, asante kwa kutuunganisha na ulimwengu kwa njia ya mtandao huu wa strictly gospel. Ubarikiwe zaidi na zaidi.

 118. Mtumishia Mungu Bwana Yesu Asifiwe sana!
  Kusoma hii article kwangu ni muujiza,kwani niko kwenye maombi ya mfungo na Roho Mtakatifu ameniongoza kufungua mtandao ili niweze kujifunza namna ya kuomba!!! yaani nimejifunza kitu kikubwa sana kwenye utumishi wangu dohh..

 119. Walokole watafundishana saaana kuhusu maombi yao ya kulialia, kanisani 24hrs, monday to sunday. jumapili mahubiri ya kutishia watu na jehanamu, bila kusahau, tena kwa msisitizo mkubwa na jasho kuhusu matoleo ya sadaka na fungu la kumi. watoe nini washirika masikini wanafundishwa tena kwa msisitizo hesabu ya kutoa tu bila kujumlisha na kuzidisha? kama ilivyo kanuni ya MAGAZIJUTO. Huo nao ni utapeli unaofanywa makanisani. watamwambia nani habari njema awasikilize wakati wao wenyewe wamechoka, wananjaa na wanapiga myayo? kanisani imeku ni mahali pa kukimbilia watu waliochoka, wasio na shughuli za kufanya, wasiowabunifu na waliokata tamaa. iliwakafarijiwe kwa maneno kama-matajiri wa rohoni. ndiyo maana hata maombi ni ya kulialia kutafuta huruma ya mungu. ndiyo maana hata ikiwekwa mikutano ya injili, wanaosikiliza na kujitokeza kuokoka ni walewale tu waliochoka. yesu pale msalabani hasa alishughulikia dhambi ambayo inaleta mauti, magojwa na maradhi pamoja na umaskini. nihubiriwe injili sawa ntaokoka, ngurumo ya upako itaniponya magojwa na maradhi yangu, then?

 120. Jesca, thank you. Ni neema ya Mungu tu inafanya kazi ndani yetu kwa ajili yenu. Mzidi kutubeba, kwani peke yetu hatuwezi. Sambazia wenzako wengi baraka hizi. pia unaweza pata mafundisho kwa http://www.mgisamtebe.org au Upendo FM Radio, J’nne 3-4 usiku na WAPO Radio, Alhamisi, 4:30-5:30 usiku. Barikiwa.

 121. Nashukuru sana kwa maandiko mazuri na ya kutuelimisha kiroho. Nataman sana cku moja nipate nafas ya kuwa mwombaji mahili.

 122. Mimi ni Mwl. Mgisa Mtebe, nimetiwa moyo sana na comments zenu. Namshukuru Mungu kunipa neema ya kuwafikishia mafundisho haya. Ni matumaini yetu mtayafanyia kazi na maarifa ya mambo ya Mungu yataongezeka na kubadili maisha yenu yawe ya ushindi na mafanikio kwa utukufu wa Mungu. mnaweza kuendelea kupata mafundisho kama haya na kuya-download katika http://www.mgisamtebe.org Pia tunarusha vipindi Upendo FM 107.7 saa 3:00-4:00 usiku na WAPO Radio 98.0 FM saa 4:15-5:15 usiku. Nawatakia baraka za Mungu.

 123. ubarikiwe sana Mtumishi wa Mungu na Mwl Mgisa nimebarikiwa na somo lako!!

 124. asante sana Mungu akubariki sana kwani nimejengeka upya katika uombaji kunavitu nimejifunza ambavyo nilikuwa sijuwi hivyo sina budi kuwashukuru asante mungu akubariki

 125. Kuwe na semina au maswali tofauti tofauti ambayo yatasaidia kumjua mungu na kazi zake kwa wanadamu hapa duniani na maisha ya baadaye

 126. Nimefarijika sana! mungu awabariki wote, nimekuwa nikitumia sana internet lakini hii page ni mara yangu ya kwanza kuiona! nimesiajabu sana! Namshukru mungu sana kwa kuniongoza kufika ktk page hii!! Nimejifunza mengi!!

 127. Kwa kweli nimejifunza mengi Naomba Mungu ambariki Mgisa mtebe na aendelee kumpa mafunuo zaidi. Mgisa mtebe ubarikiwe sana kw mafundisho yako mazuri.

 128. kwa kweli mtumishi mgisa ubarikiwe sana kwa masomo yako yaani yanajenga sana kiroho natamani kila mtu wa mungu angejifunza haya masomo angepata kitu cha kumsaidia katika maisha yake ya kila siku, Mungu aendelee kukutumia na kukulinda na kukupa uzima ili tuendelee kujifunza kile ambacho hatukijui

 129. Barikiwa mtumishi wangu. Nimebarikwa sana. Nataman huduma yako ila najua nigarama kufika kiwango cha juu hivi. Mungu azidi kukuinua siku adi siku ili tuzidi kumjua Mungu na yatupasayo kufanya ili tuishi km Mungu wetu atakavyo na si km tupendavyo. Barikiwa nasi tutazidi kukuinua ktk maombi. Nabarikiwa sana na huduma yako hasa ukiwa ktk mahubiri huboi wala sitamanig umalize kuubiri. Mungu ashukuriwe kwa kipawa alichokupa.

 130. umenena kweli kabisa mtumishi, mimi maombi yangu huwa naomba nikiwa natembea tembea chumbani, huwa naomba kwa staili hii hata mpaka kufikia masaa tisa none stop!

 131. Duh! Nzuri sana MUNGU akutie nguvu uendelee kutupa somo,, pia furaha katika kuomba ni nzuri kama Wafilipi 4:4 inavyotuambia’

 132. Nimebarikiwa sana mimi ni mvivu sana wa kuomba yaan umenifundisha kitu kikubwa . Niliingia hapa kiutani tuu wakati nataka kuilalA ila nimepata required dose. Barikiwa sana mtumishi utukumbuke kwenye maombi yako hasa sisi wa aina yangu kwn Yesu yuu mlangon.

 133. Bwana Yesu asifiwe sana.. kiukweli namshukuru mungu kwa kunifunulia kuhusu kuomba, nimeangaika sana kujua namna ya kuomba kiusahihi. Na mara nyingine nilihitajika kuwaelekeza rafiki na ndugu zangu namna ya kuomba maana wanajua kuwa nimeokoka, hivyo nilitumia utashi wangu kuwaelekeza namna ya kuomba sikuwa na uhakika saaana, lakini sasa nitakuwa na uhakika… Namshukuru Roho wa Bwana kunielekeza kufungua eneo hili naamini sasa nimepona juu ya hili. Mungu akubariki mtumishi Mlm Mgisa.

 134. Bwana Yesu asifiwe. kwa kweli nimebarikiwa sana na somo hili na kwa kweli nimebarikiwa sana. sasa ntakuwa naomba sawa sawa na mapenzi ya Mungu. Naomba Roho wa Mungu anisaidie. je ni vema kuomba ukiwa umelala kabisa kitandani au lazima uwe umepiga magoti au kusimama? asante na barikiweni sana

 135. Tumsifu YESU KRISTO, nimefurahi sana kwa mafundisho yako nakutufundisha jinsi ya kuzungumza na MUNGU, sasa mimi napenda kuomba sana lakini nikiwa naomba huwa nasinzia nifanyeje? iliniweze kuzama kwenye maombi asante na MUNGU akubariki sana kwa somo alilokupa ili utufundishe AMEN

 136. KWA KWELI NENO HILI LIMENIBARIKI SANA, SASA NAWEZA KUOMBA KAMA VILE IMPASAVYO MKRISTO

 137. Bwana Yesu asifiwe. Namshukuru MUNGU pamoja na Roho mtakatifu kwakuniongoza kwenye huu mtando wa maombi.pili Ndugu wote waliotayalisha utalatibu huu. MUNGU awabariki sana. Imenisaidia sana kujua jinsi ya kumwomba MUNGU. Naomba mniombe naumwa.

 138. Habari.Mungu akubariki kwa kunifundisha jinsi ya kuomba.Mungu akuwezeshe uendelee kufunza watu zaidi na zaidi amen.

 139. Asante mwl Magisa nimejifunza mengi naomba Roho Mtakatifu aniwezeshe katika eneo hili

 140. Bw Yesu asifiwe, nawapongeza sana strictly gospel kwa kutusaidia kupata masomo haya ya kutujenga kiroho. Niwasihi msichoke maana (isaya 40:31)

 141. Shalom,asante sana na ubarikiwe kwa mafundisho nimebarikiwa na nilitamani sana kujua jinsi ya kuomba na maombi ya kufunga sababu bado mchanga kwenywe wokovu. be blessed

 142. BWANA YESU APEWE SIFA NAMSHURU MUNGU KWA KUNIPA UWEZO WA KUTEMBELEA BLOG HII AMBAYO NINAHISI INANIJENGA KIIMANI HASA KUONGEA NA MUNGU NA KUIMARISHA UUSIANO WANGU NA MUUMBA. MUNGU AKUBARIKI

  ASANTE SANA
  IRENE -MOMBASA
  KENYA

 143. Mungu akubariki mtumishi kwa kazi nzuri.katika hatua zakuomba zilizoainishwa.toba imekuwa ya 2.Roho Mtakatifu aweza kushuka kumsaidia muombaji kabla ya toba? thanx.

 144. bwana apewe sifa nakushukuru sana mtumishi wa mungu kwa mwongozo uliotufundisha jinsi ya kuomba mungu aendelee kukutumia na kutufundisha ubarikiwe na bwana kweli wengi hatujui kuomba.

 145. NASHUKURU KWA MAFUNDISHO YENU MAZURI NA JITIHADA ZENU ZA KUTUELIMISHA KIROHO.MUNGU AWAINUE.

 146. MAY THE LORD BLESS YOU AND POUR MORE ANOINTING TO YOUR TEACHINGS….???

 147. Mungu akubariki sana mtumishi wa Mungu na akuongeze siku mingi duniani. Nimejifunza mambo mengi sana ambayo sikujua na nimeshangaa sana jinsi nimekua nikijiombea kila wakati. I’ll put this into practice. Mungu akubariki tena sana.

 148. shalom Mtumishi! Ubarikiwe sana kwa somo zuri la namna ya kuomba limenifungua sana.

 149. Namshukuru Mungu kwa kujifunza namna ya kuomba. asante saana mtumishi Mgisa kwa somo lako nzuli. Mungu akubaliki sana sababu nimejifunza mambo mengi ambayo yatanisogeza kalibu na Mungu zaidi. balikiwa mtumishi.

 150. Shalom mtumishi wa Mungu kweli nashukuru kwa kunifungua kwa njia ya pekee kuhusu (namna ya Kuomba) nimejifunza vitu vya pekee sana kwenye somo hili sasa naamini kupitia kanuni hii nitamwomba Mungu na nitapokea mahitaji yangu Mungu akubariki sana sana na uendelee kutufundisha maaana inaonekana unakipawa cha kufundisha Amina

 151. Mwl.mugisa ahsate kwa mafunzo yako umenipa mwangaza nimeyajua mengi na nitayafanyia kazi,nampenda Yesu nampenda saaana,yaan nimejisikia furaha na faraja moyoni, Mungu akubariki .Sekela

 152. ebwanaaa nimekubali njia hizi ni very strong.inatupasa tuzitumie ilitusonge mbele zaidi.mtumishi mungu akubaliki akupe mafunuo mengi juu ya njia zipasazo katika kuomba.coz my self i am blessed after learning it

 153. Mungu akubariki mtumishi kwa somo, kweli limenijenga na nitalifanyia kazi ktk Roho.

 154. may God bless you, nimejifunza mengi, na ninamuomba mungu anisaidie ili mbegu hii niliyoipata leo, ikazae matunda katika huduma yangu ya maombi. Asante sana Mungu kwa kumtumia mwalimu mtumishi wako.

 155. Ahsante, Nashukuru kwa mafundisho yako mazuri ya jinsi ya kumwomba Mungu, kwa kweli nimebarikiwa sana na mafundisho haya ni mazuri sana na Mungu akubariki na kukupa mafunuo mengi zaidi ili tupate kuimarika zaidi na zaidi. Kuna mambo ambayo nilikuwa sijayajua zaidi ila nimepata ufunuo watofauti katika kujifunza namna ya kuomba. Ubarikiwa sana na nimefurahi sana pia nimejifunza mambo mengi sana.

 156. Mungu awbariki sana wapendwa wote mliopata ujumbe huu wa neno la Mungu.Ndugu yangu Edna kuomba kifudifudi ni ishara ya kusujudu mbele za Mungu,ikiwa unakua huru sana kwa style hiyo basi usihofu,cha msingi uweze kuomba pasipo kuchoka,Jambo la msingi hasa ni Heshima yako kwa Mungu wetu aliye hai.Basi nawatakia heri na Baraka za Mungu katika kujua neno lake.Tuzidi kuwasiliana kwa jambo lolote.

 157. Bwana yesu asifiwe.nimebarikiwa sana na huduma ya namna ya kuomba nimejifunza mengi ambayo yalikuwa mapungufu kwangu.mungu awabariki sana.

 158. MUNGU AKUBARIKI SANA MTUMISHI WA MUNGU.
  NIMEJIFUNZA JINSI YA KUOMBA, NAMI NITAWAFUNDISHA WENGINE.

 159. mimi huwa naomba nikiwa nimelala kifudifudi. Je, mtumishi, hii ni sahihi?

 160. Sifa na utukufu ni kwa BWANA YESU KRISTO,watumishi mmbarikiwe sn kwa mafundisho yanayojenga na kuimarisha.

 161. kwa kweli nimepata mambo ya kujifunza juu ya namna ya kuomba, nakaza mwendo ili nifike, pia nahitaji kuombewa nisimame imara. Mungu akubariki sana wako Tumaini.

 162. Natamani sana nimpate rafiki wa kweli ambaye nitakuwa naye karibu katika maombi. Ninapokuwa peke yangu huwa nikitaka kusali tu usingizi unanijia kwa hiyo sina mtu wa kusali naye.

  Mtumishi wa Mungu uzidi kuongezewa nguvu ya kutufundisha juu ya Maombi.

 163. asante sana kwa kutupa kitu muhimu sana ktk maisha yetu na kutupa mwongozo.Mungu akubaliki

 164. Bwana yesu asifiwe, kwa kweli kwanza namshukuru Mungu, pili namshukuru mwalimu Mgisa, kwa msaada wake kupitia kitabu, majarida na hata CD, kwa kweli vimenitia nguvu ya kusimama, ila bado sijajua kuomba vizuri, il akwa sababu ninania najua nitafanikiwa tu, mwenyezi Mungu azidi kukupa afya njema wewe na familia yako na teamwork nzima. UBARIKIE MWALIMU MGISA

 165. Mungu azidi kuwabariki watu wa Mungu kwa kazi ya kuelimishana juu ya ukuu wake ‘mwalimu’ neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nawe.kiukweli nimefunguka ubongo najua kuomba sasa

 166. Nashukuru sana mwl kwa mafundisho yako mazuri niilikuwa sina namna nzuri ya kupangilia maombi yangu na sasa nimejua na Mungu akubariki sana pamoja na familia yako. Luka 14:14

 167. Lihimidiwe jina la Mfalme wa wafalme!. Ubarikiwe sana kwa kujitoa kwako kuwahubiria watu kama sisi. una wanafunzi wengi sana! ingawa hututambui tu. mie ulianza kunifundisha zamani sana na ninazo power points zako ambazo umekuwa ukizitoa. Sina cha kukupa kama vile ilivyotokea kwa akina Petro na yule mlemavu bali walimpa kile walichoweza kumpa. Nakuombea baraka kutoka kwa yeye aliyekufunulia hayo unayotufundisha!. Yesu alimwambia Petro kuwa hayo unayoyaongea hayajatoka kwako ila Baba wa Mbinguni ndiye aliyekufunulia, Sina mashaka kabisa haya nayo yametoka kwake. Katika hali isiyoyakawaida isingekuwa rahisi kutoa kitu kinachonigusa tokea mwanzo wa article mpaka mstari wa mwisho. Ubarikiwa sana rafiki wa Yesu.

 168. Mungu akubariki sana kwa mafundisho mazuri ya maombi ambayo ni silaha yetu ya kiroho.

 169. Mungu wetu apewe sifa!kwa niaba ya mwalimu mgisa mtebe,Tunawaombeni radhi kwa kukaa kimya kwa mda mrefu sana!kuna swali kuhusu mtu mmoja kufukuza adui elfu;hili kweli tulikosea kwenye kuandika katika somo hilo la maombi,usahihi ni kwamba hilo linatoka kumb32:30 na sio kama tulivyoandika.tunakaribisha maoni na maswali,mtuombee nasi tutafanya kazi yetu kwa kadri Roho wa Mungu anavyotupa uhuru.Mungu awape haja ya mioyo yenu,

 170. Mtumishi wa MUNGU Ubarikiwe sana kwa kunifundisha kuomba ntajitahid na nina mwomba MUNGU anisaidie kufuata mafundisho hayo kwa manufaa yangu na jamii kwa ujumla kwamaana ntaomba hata kwa jamii iliyonizunguka,Mbali na hayo ntajayatumia mafundisho haya kuwafundisha wale ambao hawana uwezo wa kukupata kuptia mtandao,MUNGGU AKUBARIKI SANA mtumishiAmen

 171. Hakika nimefurahia utaratibu huu wa maombi ya kufunga.
  Kila aombaye hupewa na tuzidi katika kuomba maana siku za mwisho zimekalibia.
  Mungu awabariki sana.

 172. Bwana asifiwe sana,

  Nashukuru Mungu sana kwa mafundisho kuhusu kuomba.

  Mimi ni myarwanda, ninajiswali je naweza kumona mzee Pastor kakobe, ili aweze kunisaidia kwa kucukuwa mzigo huu.
  Pastor nimemujua kupitia DVD @ Burundi. Nimeona Mungu akimutumikisha kimiujiza. Nami naomba msaada wa maombi
  Yesu kristo awabariki sana,

 173. Kwa kweli hili somo lina upako, nimelifanyia kazi this weekend, nimeinuliwa sana, halafu ajabu jana nimekutana na somo linaloendana na hili kanisani, kweli Mungu akubariki, naendelea kuomba sawa sawa na uongozi huu na ninaamini nitaona mafanikio kabisa zaidi na zaidi

 174. Nimeshukuru Mwalimu kwa mafundisho haya yanayojenga na kutuimarisha kiroho. Mungu akuzidishie na ubarikiwe sana.

  Joseph Mkala
  Mombasa, Kenya

 175. Thanks be to LORD GOD our father in JESUS NAME who give you the light to write this Good spiritual article, Thanks so much for your efforts. Its a very good article with Christian values and ethics. Born again Christian should pass their eyes upon this article.

  Thanks and cheers.

 176. KITABU CHA KWANZA CHA MOSES MAYILA KIITWACHO
  THE POWER OF GOD

  UTANGULIZI

  Kitabu hiki kimeandaliwa na Mwinjilisti Moses Mayila wa Sengerema Mwanza Tanzania, kwa msaada wa Mungu kupitia maandiko matakatifu (Biblia) na kuhaririwa nay eye mwenyewe. Kitabu hiki kimeandaliwa na kusambazwa bure kabisa bila kodi yoyote, na hii ni kutaka kulieneza neno la Mungu na kutoa Msaada zaidi hasa kwa watu wanaohitaji msaada wa maandiko, “Binafsi nimeona kuwa ni vizuri sana kama nikisambaza vitabu hivi bila kumtoza mtu yeyote yule ushuru au gharama yoyote ya uchapaji, pia ninaamini kuwa Mungu atanibariki zaidi na zaidi katika jambo hili, ni wahubiri wengi sana Duniani wanafanya jambo hili lakini wanalifanya kibiashara zaidi kwa kuwatoza watu gharama ya juu zaidi ya ile iliyotumika kuandaa kitabu kile, Mimi Moses watu hao ninawaita ni watu wafanyao kazi kwa hila wakijali mapato yao na si kazi yake aliye juu. Kupitia kitabu hiki ninaamini kuwa utapata msaada zaidi katika maisha yako ya kiroho na hata katika maisha yako ya kimwili pia. Naomba usome kwa makini sana aidha katika kitabu hiki nimejaribu kuyafafanua baadhi kya maandiko ya Biblia na kuyaeleza kwa mapana zaidi.

  SURA YA KWANZA

  MSAADA WA MUNGU KATIKA MAISHA YA MWANADAMU

  Biblia inasema katika kitabu cha Mathayo sura ya 11 mstari wa 28 hadi 31. Inasema kuwa “NJOONI KWANGU NINYI NYOTE MSUMBUKAO NA WENYE KUELEMEWA NA MIZIGO NAMI NITAWAPUMZISHA, JITIENI NIRA YANGU MKAJIFUNZE KWANGU MAANA MIMI NI MPOLE NA MNYENYEKEVU PIA WA MOYO NANYI MTAPATA RAHA NAFSINI MWENU. MAANA NIRA NIWAPAYO MIMI NI LAINI NA MZIGO WANGU NI MWEPESI”.

  Haya ni maneno ambayo Yesu aliyasema wakati akihutubia katika baadhi ya mikutano aliyowahi kuifanya. Lakini katika haya, swali lililopo mbele ni kwamba kwa nini Yesu aliyasema haya? Yesu aliyasema haya akimaanisha kuwa kila laiyendani yake yaani aliyemkubali Yesu kuwa Mwokozi wa maisha yake hataona tabu tena, ni kama vile Biblia inavyosema katika kitabu cha Nabii Isaya sura 65 kifungu cha 19 hadi 25 inasema hivi “nitaufurahia mji wangu Yerusalemu wala kilio na maombolezo havitasikika tena ndani yake, wala hapatakuwa na mzee asiye timiza siku zake tena, maana mtoto ataishi miaka mia bali mtenda dhambi akiishi miaka mia amelaaniwa, watajenga nyumba na kuishi ndani yake watapanda mizabibu na kuvuna mtunda yake, wala hawatajenga akaishi mtu mwingine tena kwenye nyumba hiyo wala hawatapanda akavuna mtu mwingine tena. Ni kama zilivyo nyingi siku za mti na watu wangu wataishi kama hivyo. Wateule wangu watafurahia kazi za mikono yao. Wala hawatazaa kwa uchungu watakuwa ni watu waliobarikiwa na Bwana.

  Hii inaonyesha vigezo vingi sana ambavyo Mungu huwapa wale wanaozishika amri zake. Hapo juu amesema kilio na maombolezo havitasikika mjini Yerusalemu. Hapa hana maana ya Yerusalemu pekee tu, bali ana maana ya watu wote wanaomcha yeye. Na aliposema kilio hakitasikika ndani yake ina maana kwamb atakomesha kila aina ya tabu, shida magonjwa, mateso na matatizo ya aina zote. Vile vile amesema hawatapanda akavuna mtu mwingine ana maana ya kwamba hawatajitaabisha bure maana shetani huharibu kile ambacho mwanadamu anakifanya ikiwa ni pamoja na mwanadamu mwenyewe. Biblia inasema mwivi kazi yake ni kuiba, kuchinja na kuharibu, ndipo Mungu akanena na Malaki akisema ‘NAMI NITAMKEMEA YEYE ALAYE MAZAO YAKO NA MIZABIBU YAKO HAITAPUKUTISHA MAJANI YAKE” hapa alikuwa na maana ya kwamba atamkemea shetani asiharibu kazi ya mikono yako, lakini hatamkemea kula matunda ya watenda dhambi bali ya wamchao yeye. Hii inamaanisha wazi kwamba Mungu humlinda amchaye, yeye na mali zake.

  Kwa sababu hii na ndiyo maana Yesu alisema njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kuelemewa na mizigo nami nitawapumzisha. Kuna sehemu kubwa sana katika jamii hasa katika nchi za Kiislamu hususan Iraq, Tajikistani, Iran na nyinginezo wanaamini kabisa kwamba Yesu alikuwa ni Nabii tu na wao wnamwita Nabii Issa. Lakini mimi Moses ninakataa hadharani usemi huo ni uongo na upotoshaji wa hali ya juu sana. Hizi mbinu tu za shetani kutaka kuutenda ulimwengu kwa maneno yanayoonekana kuwa na maana hali ni ya uongo, kila siku shetani katika kazi zake hutumia kitu inachoitwa hila, Hila ni nini? Hila ni mipango mibaya. Shetani antumia hizi hila kuuteka ulimwengu kwa maneno yasiyokuwa na ukweli wowote ndani yake ambayo kwa mtu asikye na upeo wa kutosha katika Biblia ni lazima atayaamini. Jamii hii inaamini kuwa Yesu alikuwa ni binadamu tu wa kawaida kabisa kama wewe na alizaliwa na mwanamke kama ilivyo kawaida kwa wanadamu wote. Lakini ukweli kamili ni kwamba, Yesu ni Mwana wa Mungu, na kwa habari ya kuzaliwa na mwanamke ni kwamba, Yesu alichukuliwa mimba kwa miujiza kwa uwezo wa Mungu aliye juu. Biblia inasema katika kitabu cha Mathayo sura ya 1 kifungu cha 18 inasema hivi “HIVI NDIVYO KUZALIWA KWA YESU KRISTO KULIVYOKUWA, MARIAMU ALIKUWA AMEPOSWA NA YUSUFU LAKINI KABLA (HAWAJAKARIBIANA) MARIAMU ALIONEKANA KUWA NA MIMBA AMBAYO ILIKUWA NI KWA UWEZO WA ROHO MTAKATIFU”. Biblia hiyo hiyo imeendelea kusema katika Yohana 3 kifungu cha 16 KWA MAANA MUNGU ALIUPENDA ULIMWENGU NA HATA AKAMTUMA MWANAYE WA PEKEE ILI KILA AMWAMINIYE ASIPOTEE BALI AWE NA UZIMA WA MILELE. Hii inaonyesha wazi kuwa Yesu ni Mwokozi wa Wanadamu. Pia kuna siku Yesu aliwachukua baadhi ya wanafunzi wake akaenda nao mlimani kusali, walipokuwa huko wingu zito likawafunika na sauti ilisikika kutoka kwa wingu hilo ikisema “HUYU NDIYE MWANANGU MPENDWA NILIYEPENDEZWA NAYE MSIKILIZENI ATAKAYOWAAMBIA” hii ilikuwa ni sauti ya Mungu MARKO 9 kifungu cha 7. Vile vile kuzaliwa kwake alitabiriwa na Nabii Isaya kwamba Bikra atachukua mimba na atamzaa mtoto wa kiume atakey wachunga mataifa kwa fimbo ya chuma ISAYA 7 kifungu cha 16-16. Katika historia nzima ya dunia hakuna record ya mwanamke bikra ambaye alishawahi kuzaa mbali na Mriamu kumzaa Yesu, (Bikra yaani Mwanamke ambaye hajawahi kufanya tendo la ndoa tangu kuzaliwa kwake) pia Isaya alizidi kumtabiri huyu Yesu akisema “Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa tumepewa mtoto tena wa kiume na uweza wa kifalme uko mabegani mwake (The Governmen of heaven) naye ataitwa mshauri wa ajabu Baba wa milele Mfalme wa amani jina lake. Maongeo ya enzi yake na amani haya mwisho kamwe. ISAYA 9 kifungu cha 6 – 7 inasemakana kwamba Isaya alimtabiri Yesu kabla ya miaka elfu moja (1,000) ya kuzaliwa kwake. Hivi vyote ni vielelezo vya kutosha kabisa vya kumtambulisha Yesu kuwa ni mwana wa Mungu na anauwezo wa kuratibu katika sector yoyote ile ya maisha yako. Nimeona kuwa kumbe kila wakati upatapo shida tatizo na mateso ya aina yoyote ile Yesu peke yake ndiye jibu. Na yeye ana mpango wa kukusaidia maadamu tu utakubali kufuata yale ambayo anataka uyafuate, wala hakuna kitu kisichowezekana kwake kila kitu kinawezekana LUKA 1kifungu cha 37. kwa maana moja, kila tatizo lako kwa Yesu lazima litatukuka tena kwa muda mfupi sana. Japo matatizo yamekukalia kwa muda mrefu sana siku ya leo naomba uamini kuwa yamefika mwisho, pamoja na kwamba umeombewa sana na watumishi wa Mungu mbali mbali leo utapokea muujiza wako.Hapatakuwa tena na kushindwa kufaulu kwako mwanafunzi, hapatakuwepo tena na utasa tumboni mwako mwanamke, hapatakuwa na ugomvi tena katika ndoa yako, maumivu yote ya ugonjwa wako yamefika mwisho leo, hautafukuzwa kazi tena na waliokufunza kwa muda mfupi kuanzia leo watakuletea barua ya kukutaka urejee kazini. Kila aina ya matatizo uliyo nay oleo yamefika mwisho.

  Nimefanya maombi mara nyingi sana na watu wenye matatizo mbali mbali lakini meomuona Yesu akiwapumzisha papo kwa papo, nimeombea wagonjwa wengi sana ambao hata siwezi kukumbuka idadi yao, nimetoa huduma kwa wenye mapepo waliosumbuliwa na majini ya ukoo kwa muda mrefu sana, pamoja na wenye matatizo mbali mbali, papo kwa papo Yesu aliwaponya. Na wewe naomba uamini kupitia hiki kitabu matatizo yako yote yamekwisha.

  MWISHO:

  Weka kitabu hiki kifuani kwako kwa muda wa dakika tano ukiwa umefumba macho na kasha fumbua macho yako, kasha kagua ugonjwa uliokuwa nao, na kuhakikishia kuwa hautauona tena.

  Baada ya hapo nenda zako ukiwa mzima ukasimulie ndugu, jamaa na rafiki zako mambo yote ambayo Mungu amekutendea.

  BWANA WANGU YESU KRISTO NAOMBA UYATIMIZE MAMBO HAYA KWA MTU HUYU SAWA SANA NA UWEZO WAKO. AMINA

  SURA YA PILI

  NYAKATI ZA MWISHO

  Inasemekana kuwa zamani Iraq ilikuwa ikiitwa Babeli,nchi hiyo ni miongoni mwa nchi maarufu sana duniani na ilishawahi kuitawala dunia nzima kisiasa na kiuchumi, nchi hiyo iliwahi kuongozwa na mtu mmoja jina lake Nebkadreza, ambaye alikuwa mfalme enzi hizo. Katika utawala wake yeye na jeshi lake waliondoka kwenda kuvamia huko Israel kipindi hicho Israel ilikuwa ikiongozwa na Mfalme Yeehoyakimu, katika vita hivyo mfalme Yehoyakimu alishindwa na watu wake wakachukuliwa mateka na mfalme Nebkadreza, miongoni mwa watu waliochukuliwa mateka alikuwemo kijana mmoja jina lake Daniel.

  Siku moja Mfalme Nebkadreza aliota ndoto ambayo ilimsononesha sana katika moyo wake, lakini ndoto hiyo aliisahau, mfalme akawaita wachawi, waganga, wanajimu na wafuga majini ili wamwambie na wamfasirie ndoto hiyo, wote walishindwa wakamjibu hakuna mtu ambaye anaweza kulijua jambo hili ambalo mfalme analiomba isipokuwa ni miungu isiyoishi na wanadamu. Kwa kauli hiyo mfalme alikasirika sana akaagiza waganga, wafuga majini, wanajimu na wachawi wote wauawe.

  Ndipo Daniel akamwomba mfalme asiwauwe hao watu, akamwambia yuko Mungu wa mbinguni ambaye atamwambia na kufasiria ndoto yake. Ndipo mfalme akamuuliza Daniel “Je unaweza kuniambia ndoto hiyo na ukaifasiri? Daniel akamjibu “Hakuna mwenye hekima, mchawi, wala mnajimu ambaye anaweza kuieleza siri ambayo mfalme anaiomba. Lakini yupo Mungu wa Mbinguni afunuaye siri, aliyemuonyesha mfalme Nebkadreza yale ambayo yatatokea siku zijazo.

  Ndoto yako ee mfalme ilikuwa hivi: uliona ee mfalme mbele yako sanamu kubwa imesimama, sanamu hiyo ilikuwa ni ya kutisha sana. Kichwa cha sanamu hiyo kilikuwa kimetengenezwa kwa dhahabu safi, kifua chake kilikuwa ni silver, kiuno chake na mapaja ni shaba, miguu yake ni chuma mchanganyiko na udongo. Wakati ulipokuwa unaendelea kuona haya likatokea jiwe kubwa ambalo halijatengenezwa kwa mikono ya wanadamu likaiponda miguu ya ile sanamu na kuisagasaga, ndipo chuma, udongo, dhahabu, na silver likazivunja vipande vipande kwa wakati ule ule na zikawa kama mapepe, upepo ukazipeperusha kwenda mbali. Lakini lile jiwe lililoiponda ile sanamu likakua na kuwa mlima mkubwa mpaka likaijaza dunia nzima”.

  Daniel akasema Hii ndiyo ndoto yako ee mfalme ngoja nikufasirie, Mungu wa mbinguni amekupa uwezo, nguvu na mamlaka, na amewaweka watu, wanyama wa porini na ndege wa angani mikononi mwako wewe mfalme, popote wanapishi Mungu amekupa kuwa mtawala juu yao wote. Wewe ni kile kichwa cha dhahabu baada yako ufalme mwingine tena utainuka, baada ya huo, ufalme mwingine tena utainuka (shaba) utatawala juu ya Dunia yote, mwisho kutakuwa na tawala nne, ufalme wa chuma utakuwa na nguvu kuliko zingine hivyo utazipiga na kuziangusha zile zingine, kama ulivyoona miguu yake ilikuwa chuma mchanganyiko na udongo, huu utakuwa ni ufalme uliogawanyika upande mwingien utakuwa wenye nguvu na mwingine dhaifu. Kama ulivyoona chuma mchanganyiko na udongo watu watakuwa wamechanganyikana lakini hawana umoja kama chuma kisivyo shikamana na udogo. Katika wakati wa wafalme hao Mungu wa Mbinguni atapandisha ufalme ambao hautaharibiwa wala hautamwachia mtumwingine tena. Utaziharibu zile falme zote na kuziondosha lakini ufalme huo utadumu milele, hii ndio maana ya lile jiwe kuiponda ile sanamu. Hii ndiyo ndoto yako ee Mfalme. Daniel 2 kifungu cha 24-45.

  Kufuatia ndoto hiyo ya mfalme, inasemekana kuwa kuna falme ambazo ziliinuka baada ya utawala wa mfalme Nebkadreza, miongoni mwa falme hizo ni pamoja na utawala wa Rumi, utawala wa Mjerumani na utawala wa Mwingereza. Lakini pamoja nahayo upo utawala ambao uemsemwa kuwa ni utawala uliochanganyikana chuma na udongo ambao watu wake watakuwa pamoja lakini hawana umoja, na huu ndio utawala nne katika mlolongo wa tawala zilizotajwa hapo juu. Nimetazama hivi sasa nimeona kuna jumuiya ambazo nchi nyingizimefanya lakini jumuiya hizo hazina umoja hata kidogo ndani yake, kwa mfano Jumuiya ya nchi za Kusini mwa Afrika, Jumuiya hiyo bado ipo haijavunjika lakini cha kushangaza raia wake hawapatani kabisa, hebu chukulia mfano kule nchini Afrika kusini, jinsi wageni walivyopigwa na kuuawa na raia wa Afrika kusini, chukulia mfano mwingine mzuri kabisa hapa nchini kwetu Tanzania, kuna umoja ambao ulifanywa na Raisi wa kwanza wa Tanganyika Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuziunganisha nchi hizi mbili na kuwa nchi moja na wakabadili hata majina ya nchi hizo, badala ya Tanganyika na Zanzibar wakaziita kwa jina moja la Tanzania, umoja huu umedumu kwa muda mrefu, lakini cha kushangaza hivi sasa raia wa Tanganyika (Tanzania bara) hawaruhusiwi kuingia Zanzibar bila hati ya kusafiria, sheria hii imewekwa mwaka 2008 na serikali ya Zanzibar, hii inaonyesha wazi kwamba watu hawa hawana umoja wa kweli kutoka mioyoni mwao, wana umoja midomoni tu. Na huu ndio utawala wa chuma mchanganyiko na udongo.

  Mpendwa napenda kukujulisha kuwa, kama Daniel alivyosema kuwa baada ya utawala wa chuma mchanganyiko na udongo Mungu wa mbinguni atainua utawala wake ambao hautapita na hii ndiyo maana ya lile jiwe lililoiponda ile sanamu. Ninapenda kukujulisha kuwa jiwe hili ni Yesu Kristo ambaye Mungu wa mbinguni ammuweka kuwa kuhani milele. Waebrania 7 kifungu cha 24 pia anajulikana kama jiwe kuu la pembeni Zaburi 118 kifungu cha 12 na kama Daniel alivyosema kwamba jiwe hili (Yesu Kriso) litazivunja tawala hizo katika kipindi cha utawala wa chuma mchanganyiko na udongo ambao ndio utawala tulio nao sasa.

  Hii inaonyesha wazi kwamba wakati wowote kuanzia leo Yesu atarudi kuihukumu Dunia na kuharibu tawala zote za Duniani, wala hatakuja kwa kutoa taarifa, bali atakuja kama mwivi, Ufunuo 3 kifungu cha 3 (“Tubu usipotubu naja kama mwivi) pia hakuna mtu ambaye anaifahamu saa ya kuja kwake maana inasemekana hata yeye mwenyewe Yesu haijui sik wala saa ya hukumu ya Dunia. Yesu mwenyewe alisema katika kitabu cha Mathayo 24 kifungu cha 36 (wala hakuna aijuaye siku wala saa iwe ni malaika wa mbinguni au mwana wa Mungu bali aijuaye ni baba peke yake) jambo hili linatuasa kujiweka tayari kwa kila saaa na kwa kila wakati kwa maana hatujui ni lini na saa ngapi atarudi.

  SURA YA TATU

  MAJARIBU

  MAJARIBU NI NINI? – Majaribu ni kipimo ambacho hutumika kumpima mtu au kitu ili kutambua kuwa kinauwezo au anauwezo kiasi gani wa kufanya kazi katika sekta anayohitajika.

  Inasemekana palikuwa na mtu mmoja jina lake Ayubu, mtu huyu ni miongoni mwa watu hapa duniani waliopata majaribu kwa kiasi kikubwa sana. Siku moja malaika walikwenda kujihudhurisha mbele za Mungu shetani naye akaenda kujihudhurisha mbele za Mungu, Bwana kamuuliza shetani “umetoka wapi wewe?” shetani akamjibu Bwana “nimetoka duniani kuzunguka zunguka huku na hna humo” ndipo Bwana akamuuliza “Je umemuona mtumishi wangu Ayubu? Kwani hakuna hata mmoja duniani aliye mkamilifu, mwelekevu na mwenye kujitenga na uovu na mwenye kumuheshimu Mungu kama yeye. Shetani akamuuliza Bwana “Je huyo Ayubu yuamcha Bwana bure? Wewe hukumzingira yeye na nyumba yake, umezibariki kazi za mikono yake makundi yake ya mifugo na ya kondoo yamesambaa nchini kote. Hebu sasa nyoosha mkono wako uyaguse hayo uone kama hatakufuru mbele yako. Bwana akamjibu Shetani “hayo yote yako mikononi mwako lakini usimguse yeye mwenyewe.AYUBU 1:6-12.Shetani akaondoka, siku moja watoto wa Ayubu walikuwa wakisherehekea ndani ya nyumba ghafla ukavuma upepo ukaangusha ile nyumba na wote kwa pamoja wakafa, wala hakusalia hata mmoja. Wakati huo huo wachunga mifugo wake wakavamiwa na majambazi na wakauawa isipokuwa mmojatu ndiye aliyebakia kumpelekea Ayubu habari, na baada ya kuuawa kwa wachungaji hao mifugo yote ilichukuliwa na majambazi hao.

  Mtumishi wa Mungu Ayubu hakukufuru wala kumlalamikia Mungu, lakini mkewe alimshauri amkufuru Mungu ili afe, lakini Ayubu Mtumishi wa Mungu alimjibu mkewe kuwa wewe nawe u mmoja katika hao wanawake wajinga. Pamoja nahayo shetani aliona kuwa Ayubu bado amesimama na Imani yake shetani akaamua kumpiga Ayubu kwa Majipu mwili mzima ktoka uwayo hata kitosi cha kichwa chake, AYUBU 2 kifungu cha 7. Pamoja na kujaribiwa sana lakini Ayubu hakumkufuru Mungu wala hakufanya dhambi.

  Hapa nimeona kuwa kumbe mtu ambaye anamcha Mungu kwa kumaanisha toka moyoni mwake kwanza Mungu huimarisha ulinzi wa kutosha kwa mtu huyo yeye pamoja na familia yake pamoja na mali zake, hii ina maana moja mke au mume au mtoto anapotangaza kumfuata Yesu usimzuie maanaKupitia yeye utapata rehema na ulinzi wa Mungu kwa sababu Mungu atamlinda yeye na familia yake pamoja na mali zake. Kwa maana nyingine shetani hataweza kumzuru mtu huyo maana Mungu amemzunguka, na ndiyo maana shetani alipoulizwa na Mungu kuhusu Ayubu alisema wewe (yaani Mungu) umemzunguka yeye na familia yake, kumbe ukimfuata Mungu nguvu zozote zile za shetani hazitakudhuru wala hazikutishi kwa sababu Mungu amekuzunguka, wala mchawi hakutishi akikuona hata kama alikuwa anaenda kuloga ataanza kutetemeka na kukimbia mbali na wewe.

  Kitu kingine ukiumfuata Mungu kwa kumaanisha kabisa, kumbe Mungu atakubariki sana katika shughuli zako zote maana Ayubu alikuwa amembariki katika kazi za mikono yake na kuiongeza mifugo yake katika nchi. Lakini unapoamua kumfuata Mungu unatakiwa ufahamu kwamba kuna kitu kujaribiwa ndani ya hiyo safari, hivyo basi unatakiwa kujipanga kikamilifu ili kukabiliana na hayo majaribu yote utakayoyapata, mfano mzuri ni jamaa watatu vijana wa Kiebrania ambao ni Daniel Meshack na Abednego. Vijana hawa walilazimishwa kuabudu miungu ya mfalme wa Iraq, lakini vijana hawa walikataa kufanya hivyo mfalme huyo aliagiza wauawe. DANIEL 3:14-24 Mfalme akawaambia ni kweli kwamba ninyi mmkataa kuitumikia miungu yangu wala kuiabudu sanamu yangu? Sasa mtakaposikia sauti za filimbi na vinubi na kila aina ya muziki kama mtakuwa tayari kuanguka na kusujudia na kuiabudu sanamu yangunitawafanya vizuri sana, lakini msipofanya hiyo mtatupwa kwenye tanuru la moto, nitaona ni Mungu gani atakayekuja kuwaokoa mikononi mwangu.

  Vijana hao wakamjibu mfalme “Ee mfalme Nebkadreza hatutaki kujitetea sisi wenyewe mbele yako katika jambo hili. Kama tukitupwa katika tanuru la motoyupo Mungu ambaye atakuja kutuokoa, hata kama asipotuokoa elewa ee Mfalme kuwa hatutaitumikia hiyo miungu yako wala kuiabudu hiyo sanamu yako” ndipo mfalme akakasirika sana akaagiza ile tanuru itiwe moto mara saba kuliko kawaida yake askari wakawafunga na kuwatupa katika atanuru hilo, kwa sababu ya ukali wa ule moto kiasi kwamba hata ukilisogelea tu lile tanuru unakufa, askari hao walikufa hapo hapo lakini cha kushangaza moto huo ulizikata zile kamba ambazo vijana hao walikuwa wamefungwa nazo, lakini haukuwadhuru wao hata kidogo. Mfalme akasimama akasema “hivi hatukuwatupa watu watatu tu ndani ya tanuru? Lakini mbona ninaona kuna watu wane wanatemea tu ndani ya tanuru hawajafungwa na wala hawadhuriki na moto, na huyo wa nne anaonekana kuwa ni mwana wa Miungu, (Mtu wa nne alikuwa ni Yesu Kristo mwana wa Mungu aliye hai) ndipo mfalme akasimama akawaita vijana hao “Enyi Shadrack, Meshack na Abednego njoni nje ya tanuru, ndipo mfalme akasema “Na ahimidiwe Mungu wa Meshack, Shadrack na Abednego aliyemtuma malaika wake kuja kuwaokoa watumishi wake Meshack, Abednego na Shadrack ambao waliamua kuyapoteza maisha yao kwa ajili ya Mungu wao kuliko kujitia unajisi kwa kuabudu miungu mingine isipokuwa Mungu wao. Sasa ninaagiza mtu yoyote yule atakayesema neno kinyume na Mungu wa Vijana hawa atakatwa vipande vipande yeye na familia yake, maana hakuna Mungu mwingine anayeweza kuokoa namna hii.

  Mpendwa wangu hapa tunaona wazi kabisa kwamba kumbe wakati wa kujaribiwa hautakiwi kuogopa uzito wa jaribu ni ahueni uyapoteze maisha yako kuliko kuupoteza uzima wa milele, hili hata Bwana wangu Yesu Kristo alilisema “Mwanadamu atanufaika nini kama akiupata ulimwengu wote kasha aukose uzima wa milele? Hapa kuna faida zaidi ya tatu, ya kwanza ukimshika Mungu sawa sawa kama Shadrack, Abednego na Meshack, Mungu mwenyewe atakutukuza, faida ya pili utapata uzima wa milele, faida ya tatu utasababisha na watu wasiomcha Mungu waanze kumcha Mungu kwa kasi nzuri sana. Kwa nini ninasema hivi? Kwa sababu mfalme alikuwa anaitegemea miungu yake lakini siku hiyo akasema hakuna Mungu anayeweza kuokoa kama Mungu wa Vijana hawa isitoshe akaagiza kwamba yeyote atakayesema neno kinyume na Mungu wa vijana hawa atauawa yeye na familia yake. Hii inaonyesha wazi kabisa kwamba kupitia Imani ya hawa vijana na miujiza ambayo Mungu aliifanya, Mfalme alimwamini sana Mungu wa Mbinguni na kuona miungu mingine haifai.

  Kumbe katika imani yako unaweza kusababisha hata watu wengine waokolewe kupitia imani yako wewe hata unapokuwa katika kipindi cha majaribu, lakini unatakiwa ufahamu kwamba chanzo kikubwa cha majaribu ni shetani, yeye huenda mbele za Mungu na kuomba ruhusa ya kukujaribu, lakini kukujaribu anategemea kabisa kwamba atakuangusha. Lakini wakati ujaribiwapo Mungu naye yupo chonjo kukuangalia ni namna gani utamshinda shetani, na Mungu anapotoa ruhusa na wewe kujaribiwa huwa anataka wewe uyashinde hayo majaribu , pia ninamshukuru sana Mungu Baba Mwenyeezi kwa saababu huwa haruhusu kwetu yaje majaribumakubwa kuliko uwezo wa imani zetu soma 1WAKORINTHO 10 kifungu cha 13 biblia inasema hivi “Hakuna jaribu lililokubwa kuliko uwezo wako ambalo Mungu ataliruhusu likufikie ispokuwa ni lile lililo sawa na uwezo wako, pia Mungu ni mwaminifu hukuwekea mlango wa kutoke”.

  Hii inaonyesha wazi ni jinsi gani Mungu anakupenda mimi naona kama vile Mungu humzihaki shetani kwa maana anapomruhusu akujaribu hamruhusu akujaribu zaidi ya uwezo wako, ina maana moja kwamba hamruhusu akuangushe wala akusumbue kiasi kwamba ushindwe kuvumilia. Hii ni thabiti kabisa kwamba shetani ni mjinga kwa sababu haiwezekani mtu akuagize kumuua nyoka lakini akuagize usimpige kichwani ila mkiani tu kweli utampiga hata mkia, lakini cha kushangaza huyo huyo aliyekuagiza kumpiga alipoona umemkata mkia anampa mkia mwingine tena anamwongezea na wa pili mbele yako. Je huyo mtu ni kweli kwamba anataka umuue huyo nyoka au anataka kukusumbua tu? Hapa nimeona kwamba Mungu humsumbua kijanja shetani, kwa sababu shetani hana busara halioni hilo. Mpendwa wangu napenda ufahamu kwamba hakuna jaribu linaloweza kukuua, pia hakuna jaribu linaloweza kudumu miaka yote ya maisha yako Mungu asiliondoshe. Mfano Ayubu watoto na mali zake wakati wa kujaribiwa vyote kwa mpamoja vilikwisha, lakini baada ya jaribu kupita alipata mara mbili zaidi ya yale aliyokuwa nayo mwanzo. Soma AYUBU 1 kifungu cha 1-3, hapa ilikuwa ni kabla ya kujaribiwa. Kisha soma AYUBU 42 kifungu cha 12 – 15, hapa ni baada ya kujaribiwa. Hivyo hivyo tumeona hata kwa hawa vijana wa Kiebrania akina Meshack na jamaa zake, baada ya kutoka katika tanuru la moto mfalme aliwaweka kuwa watumishi wa ngazi za juu sana katika ikulu ya Iraq.

  Hapa moja kwa moja nimeelewa kuwa hata kama ulikuwa mtumwa kwa kumcha Mungu na kuvumilia katika majaribu Mungu atakufanya kuwa Mtawala. Hata kama ulikuwa maskini sana atakufanya kuwa Tajiri maana hata Ayubu aliishiwa kila kitu kwa maana moja alikuwa masikini lakini kwa kushinda majaribu alipata mara mbili ya yale ya kwanza. Lakini nimekuandalia mada hii ili kukujulisha kuwa unapoamua kumfuata Yesu elewa kuwa umetangaza vita, hata mambo ambayo ulikuwa huyapati utayapata hivyo basi kuwa mvumilivu katika hizo dhiki Mungu yupo pamoja na wewe wala hajakuacha. Jitahidi majaribu yako yasigeuke kuwa mateso kwako, nina maana moja kusema hivyo. Kuna tofauti kati ya majaribu na mateso mtu ambaye anapata mateso akiwa kwa Yesu huyo ndiye anajaribiwa ambapo asipotenda dhambi katika hayo mateso atapewa zawadi kutoka kwa Mungu mwenyewe. Lakini yule ambaye anapata mateso akiwa kwa shetani huyo yeye anateswa tu wala hatapata faida yoyote ile ya mateso yake.

  Ninakusihi katika jina la Bwana wangu Yesu Kristo usitende dhambi ndani ya majaribu hayo ukaikosa zawadi ambayo Mungu alikuwa amekuandalia.

  BWANA YESU AKUSAIDIE SANA UMSHINDE SHETANI

  SHUKRANI

  Ninamshukuru Mungu Baba Mwenyezi aliyezifanya mbingu na nchi kwa kuniwezesha kutengeneza kitabu hiki. Ni dhahiri kabisa kuwa kwa akili zangu tu mimi Moses nisingeweza kufanya kazi hii hasa kulingana na umri wangu kuwa ni mdogo sana. Vile vile ninamshukuru sana kwa kunifanya kuwa mtumishi wake katika umri mdogo sana.

  OMBI LANGU KWAKO

  Mpendwa wangu katika Bwana ninaamini Mungu wa mbinguni humpenda na humbariki sana yeye atangazaye habari zake duniani, hivyo basi ninakuomba mpendwa wangu kama ukiweza angalau uzalishe nakala moja tu ya kitabu hiki na umgawie mtu mwingine ili kuweza kusambaza msaada huu wa injili kwa watu wengi zaidi ulimwenguni mwote.

  MUNGU AKUBARIKI SANA KWA KUFANYA HIVYO

  MKAKATI NA LENGO LA KITABU HIKI

  Mkakati na lengo langu ni kukisambaza kitabu hiki katika nchi zote zinazotumia lugha ya Kiswahili hususani Afrika Mashariki, na katika nchi zisizotumia lugha ya Kiswahili tayari nimeshaanza kukiandaa kitabu hiki kwa lugha ya Kiingereza. Kitabu hicho kitatoka hivi karibuni na kitaanza kusambazwa huko nchini Nigeria, Swazilandi, Marekani, Tahailandi, India na hata Tanzania pia. Lengo hasa la kufanya hivyo ni kueneza msaada zaidi wa maandiko duniani pote.

  Hivyo basi ninakuomba uniombee sana kwa nguvu zako zote ili niweze kufanikisha suala hili, pia uniombee sana ili Mungu anitie nguvu zaidi niweze kumtumikia zaidi ya vile nilivyopanga kumtumikia.

  BWANA AKUTENDEE YALIYO MEMA MAISHANI MWAKO.

  AMINA

  HAKI YA KURUDUFU

  Kitabu hiki kinaruhusiwa kukizalisha na kukisambaza sehemu yoyote lakini kisambazwe bure kisiuzwe kwa gharama yoyote iwe ya juu au ya chini. Pia kitumika katika misingi ya Mungu na katika mashauri mema na si katika uhalifu. Hairuhusiwi kutumia neno lolote la kitabu hiki katika uovu wa aina yoyote ile.

  ENDAPO UTAHITAJI MSAADA ZAIDI:

  Wasiliana na mimi kupitia simu namba: 0755 961270 au +255 715961270

  Barua pepe: mosesmayila@yahoo.com

 177. Asante sana mtumishi jina la Yesu lipewe sifa mimi nimepata njia na alama ya ushindi kupitia kwako maana nimekuwa mvivu wa maombi na wakati mwingine siombi kabisa na wala kanisani siendi. kweli kwa kutumia formula hizi nimepata njia.

  Ubarikiwe sana ila natamani kukushirikisha mambo ya kuombea kwenye familia yangu ila ningetamani uniruhusu nitumie email yako personal, yangu ni misssecretary1978@yahoo.ca. nitashukuru kama utaniruhusu.

  BARIKIWA BABA

 178. shalom!kaz yako ni njema!kwa mafunzo haya satani atapata kipigo cha hali ya juu!coz wapiganaji wamepata kufahamu nn cha kufanya!songa mbele kaka!

  Lakini napenda kufahamu andiko la ‘mwombaji mmoja anafukuza adui elfu moja’ linatoka ktbu gan coz ulichotaja naona havihusiani!mungu akubariki!

 179. Hongera sana Mtumishi kwa kutoa shule yenye msaada mkubwa kwa mwili wa Kristo.Mungu akubariki.

 180. Nashukuru kwa mafundisho yako mtumishi wa Mungu yamenifundisha na nimebarikiwa. Mungu akuzidishie na akupe uwezo zaidi. Amen

 181. Mungu akubariki sana,umenipa moyo na msaada katika somo hili hakika ni bwana amekutumia,pia ninaombi naomba maandiko juu ya kupata mtoto, ubarikiwe

 182. Mpendwa mtuumishi, niliandika kuomba kuniombea, naomba uniombee baba, naendelea kupata majaribu mengi ukiacha kuambiwa mimi ni mchawi nimepata jaribu jingine la kufukuzwa katika nyumba.

  Na imani mtaniombea.

 183. Mtumishi wa Mungu GODBLESS YOU, nashukuru san kwa msaada wako na mafundisho yako mazuri ya kuweza kwenda mbele za MUNGU. Nami nitatumia elimu hii kuwaelimisha na wengine kwa msaada wa MUNGU ilituweze kumshinda huyu muovu ibilisi.

 184. Mungu akubariki, na nimebarikiwa na nimejinfunza jinsi ya kuomba kutokana na masomo haya

 185. nashukuru sana mtumishi kwa kunisaidia jinsi ya kuomba natumai nitakua nimepiga hatua kubwa. Mimi ni muislam nina matatizo naambiwa mimi ni mchawi. Mimi mwenyewe sijawahi kuzaa kama ni mchawi nafikiri ningejitahidi kutatua matatizo yangu mwenyewe. Na imani mtaniombea wapendwa katika bwana najaribu kutafuta web site itakayoweza kunisaidia kutatua matatizo yangu. Mungu ni mkubwa naendelea kupata karama nyingi kwani na hii web site sikuwa najua nina imani Mungu yu pamoja nami. namba yangu ya simu ni hii 0786 882976

 186. nashukuru sana mtumishi kwa kunisaidia jinsi ya kuomba natumai nitakua nimepiga hatua kubwa. Mungu akubariki!

 187. Ashura wa MUCE
  nakushukuru sana mwl Mungu akubariki endelea kutufundisha. nimepata kitu kikubwa sana kitanisaidia sana katika maisha yangu.

 188. Mwl Mgisa Mungu akubariki sana sana na zaidi ya yote akuzidishie hekima na maarifa zaidi

  Nimefurahi kusoma na labda niseme nimepata neema ya pekee kwangu mimi kusoma na kuelewa namna ya kuomba.

  Mungu akubariki sana sana Mwl
  Je naweza kukuuliza swali jingine la ufahamu zaidi au

 189. Mtumishi wa Bwana Mungu akubariki kwa ujumbe wako wa kulijenga kanisa pia katika mtiririko huu huu nivema wakristo wakajifunza kutulia na kumsikiliza Mungu na kusikia sauti yake…maana katika mtiriko huu mzuri wa maombi Mungu huwa anasema na watu wake nina maana ni two way communication, sisi tunasema naye naye anasema nasi….ni muhimu wakristo wakaijua sauti ya Mungu…Mungu anajibu…if Yes or No or Wait yote ni majibu, ni muhimu sana kumsikia na Mkristo ni muhimu aka experience kusikia pia na sikuongea tu kama redio then basi. Mungu awabariki sana watu wa Mungu kwa michango yenu

 190. Praise the lord Mwal,am so grateful for your teachings concernig how to pray have learned alot from you teachings.I never knew how to pray in deep.May almighty GOD grant you good health spiritually to stand firm for him work for him in your life let the glory of GOD being seen in you.AMEN
  irene
  Kenya-Mombasa
  Ubarikiwe sana

 191. Bwana Yesu asifiwe nimefarijika sana na mafundisho yako mtumishi wa mungu, kwani kabla sijasoma namna gani ya kuomba nilikuwa naomba kwa jinsi ninavyo jua mimi lakini sasa nimeelewa, namwomba Mungu akuzidishie katika huduma ya kumtumikia Mungu.

 192. Mungu akubariki Mwl. Mgisa kwa mafundisho yako ya namna ya kuomba, nimepata mwanga na kujua namna ya kusogea mbele za Mungu kwA njia ya maombi. Mungu akutangulie katika huduma.

  AMEN.

 193. Mungu akubariki kwa kutusaidia kupata neno la Mungu tuombee tuweze kuufikia ufalme wa Mungu nawe ubarikiwe na uzidi kufungua wengi

 194. Amina,Mungu akubariki kwa somo zuri lenye kuleta mafanikio kiroho. Maana shetani wengi ametushinda kwa kutokujua kuomba haki zetu kwa Mungu ,Baba yetu Mpenzi.Naamini kupitia ndondo hizi ulizozitoa shetani hataona mlango kwa kila atakaye soma na kuzitumia katika maombi.Mungu Wa Mbinguni Akubariki Sana.

 195. Amina,Mungu akubariki kwa somo zuri lenye kuleta mafanikio kiroho. Maana shetani wengi ametushinda kwa kutokujua kuomba haki zetu kwa Mungu, Baba yetu Mpenzi. Naamini kupitia ndondo hizi ulizozitoa shetani hataona mlango kwa kila atakaye soma na kuzitumia katika maombi. Mungu Wa Mbinguni Akubariki Sana.

 196. mtumishi mungu wa mbinguni akubariki sana kwa somo hili.wewe ni mtumishi wa mungu aliye juu.ubarikiwe sana.

 197. Mtumishi nakushukuru sana, roho wa Rwana amenigusa kwani hapa ndio mwanzo wa kujua na kupata ufahamu wa jinsi ya kuurithi ufalme wa mbinguni. Roho wa Rwana akuonyeshe maono zaidi ili tushirikishane baraka za Bwana.

 198. Aksante Mtumishi wa Mungu kwa article yako hii,kwani imenipa maarifa zaidi ktk kuomba.Mungu azidi kukupa maono na mafunuo ili utoe article zaidi ziweze kutujenga kiroho.Mungu wangu akubariki

 199. Asante sana Mwl.Mgisa, MUNGU akubariki saana kwa mafundisho uliyotoa kwani nimejifunza mengi na nimeona faida ya kusoma vifungu vya BIBLIA ulivyotoa.
  Ubarikiwe sana,MUNGU akutie nguvu!

 200. Mtumishi kwanza MUNGU akubariki sana kwa huduma unayotoa kwa jamii. Mimi binafsi nimehudhuria semina zako kwkweli nimefarijika sana na mefundisho yako. Lakini kikubwa ambacho nilikuwa sijui lakini kwenye semina zako nimejifunza ni umuhimu wa IBADA kwenye maisha yako. Kwakweli ni ajabu sana kuwa kwa miaka yote hii nilikuwa sijui umuhimu na muda wa kutumia kwenye IBADA. Lakini kwa sasa nimeanza kuona faida yake kubwa tu kwenye maisha yangu na familia, kazi na mahusiano na jamii kwa ujumla lakini zaidi mahusiano yangu na MUNGU.
  Ubarikiwe sana Mtumishi wa BWANA

 201. Ikiwezekana iwepo pia mafundisho ya ubatizo wa Roho mtakatifu na Ubatizo wa maji maan yapo makasnisa tayari yameshaanza kuona kwamba Ubatizo sio muhimu sna.

 202. Mungu akubariki sana, na aendelee kukufunulia zaidi mbinu za maombi na vita, maana bila kujua mbinu(techniques) ni rahisi sana adui kutushinda.

  Amen.

 203. Shalom!neno la mwombaji mmoja anafukuza adui elfu linatoka kitabu gani!maelezo yako kwny article yanasema kumb 32.20 lakn haiendani!naomba msaada

 204. WENGI TULIOMBA SALA YA BABA YETU WA MBINGUNI KAMA JINSI ILIVYO HATUKUJUA KAMA ULE ULIKUWA NI MFANO TU.MUNGU AKUBARIKI SANA MTUMWA WA BWANA,AMEN.

 205. asante mtumishi wa Mungu kwa mafundisho mazuuuri, mambo kama haya yana gharama fulani mf. kufunga, kusoma na kutulia mbele za Mungu na kumsikiliza Roho mtakatifu, endelea kuchochea karama aliyo kujalia Mungu,usije ukajisifu kila siku maishani MPE SIFA MUNGU,ili akutumie zaidi na zaidi katika masomo mengineyo, Ubarikiwe na Bwana!!!

 206. Mwalimu mgisa nakushukuru sana kwa sababu kila ninapoingia kwenye mwongozo wako wa maombi najikuta nikiomba machozi yananitoka kitu ambacho kilikuwa hakipo. mungu akubariki sana asante

 207. ASANTE SANA MTUMISHI WA MUNGU MAANA NIMEPOKEA KITU KUTOKA KWAKO NILIKUWA SIJUI JINSI YA KUOMBA, KILA MARA NASEMA MBONA NAOMBA MUNGU HANITENDEI KUMBE NILIKUWA SIJUI SASA HIVI NAAMINI MUNGU AMESHASIKIA MAOMBI YANGU

 208. Bwana Yesu asifiwe!.
  Mungu akubariki mtumishi kwa somo zuri kuhusu maombi,ni jambo la muhimu sana wapendwa kuendelea kukumbushana kuhusu maombi kwani ni silaha muhimu katika vita vya kiroho-Efeso 6:10-18.Ni jambo la muhimu pia kwa kanisa kuzingatia maandiko kuhusu kuendelea kukutanika kwa ibada kila inapoitwa leo kwani ni katika makusanyiko kama haya ya watu wa Mungu ndipo Mungu huwatumia watumishi wake kusema nasi,Ebrania 10:25 na Efeso 4:11-13.
  Zipo changamoto nyingi katika jamii kwa sasa hasa suala la kazi ambazo wakati mwingine zaweza kumfanya mtu asipate muda wa kuwa na ushirika na Mungu na hivyo kuwa vigumu kuzaa matunda,Mathayo 13-mfano wa mpanzi aliyeenda kupanda mbegu.
  Mungu atubariki mwaka huu 2010 na siku zote.
  MIAKA KUMI YA MAVUNO,TANZANIA KWA YESU!.

 209. Bwana yesu apewe sifa nami nimejifunza namna bora ya kuomba .Nimebarikiwa sana na mafundisho haya Mungu akubariki .

 210. Ubarikiwe sana mtumishi wewe na familia yako.Bwana akupiganie kila upande,upendeleo wa Bwana juu ya kizazi chako uwe dhahiri,mwisho mwema ufike.

 211. Nimebarikiwa sana na mafundisho haya juu ya maombi.Mungu azidi kukubariki Mtumushi wa Mungu.

 212. Nashukuru sana kwa ujumbe wako mtumishi wa Mungu,niko kwenye maombi ya kufunga kabla sijaanza nikaona niiingie kwenye internet nijifunze maneno ya Mungu hasa jinsi ya kuomba kwa kufunga,ndipo nikakuta msg hii imenijenga sana.
  Mungu akubariki.

 213. Mtumishi wa Bwana, Mungu akubariki sana kwa kututia moyo, nguvu mpya katika safari hii ya Mbinguni, hasa katika mbinu za kumwabudu Mungu wetu kwa style mbali mbali ili kuepuka kuchoka. Tukiwa safarini kwenda kwetu kaanani.Wengine huficha mambo kama haya wakitaka wenzao wawe wanapiga marktime. Chochea karama yako hii hakuna ubishi UBARIKIWE!!!

 214. Mwalimu Mgisa ubarikiwa na Mungu wa upendo azidi ukupa kipawa cha kufundisha watu na kuelewa lilo kusudi la Mungu.

 215. Mwl. Mgisa, ubarikiwe na Bwana wetu aliye hai. Najisikia nimejengeka upya baada ya kusoma mafundisho yako. Namshukuru Mungu pia kwa kukutumia ili utuletee ujumbe huu. Ubarikiwe daima.

 216. Sunday, November 15, 2009 at 8:25 am

  Na Shukuru Mungu sana tena sana kwa yote ana vyo tenda juu yangu na wandugu katika YESU na soma ginsi mwana wa Mungu anaweza kuomba na wakati na kupata nguvu ya Mungu kweli imenijenga sana zaidi katika ukristu wangu leo ilikuwa tarehe 15-11-2009 apa Danmark usiku na saa 4:45 nikahamuka roho ikanituma nisome neno ndani ya computer juu ya UPONYAJI ya UKIMWI na nikahandika tu UPONYAJI ya UKIMWI tayari nikakuta USHUHUDA kubwa ya Pastor DEUS PAUL nikalisoma ikanijenga sana na nikafika mahali inaposema NAMNA ya KUOMBA .ikani saidia na juu na mimi nilikuwa mugonjwa ya iyo iyo nalishukuru Mungu sana . na tarehe iyo tuko na bibi mambo kuserekali juu ya kuachana juu niko na UKIMWI kweli mbele yake nali muomba masamaha na mbele ya watumishi wengi nalienda inje ya NDOA na pia kwenu munisamehe na Mungu anisamehe na kuniponya Roho yake ipate na fasi ndani ya maisha yangu sio UKIMWI lakini mwili wangu ni hekalu ya Roho ya Mungu.kweli yote mumehandika ni ya kutujenga katika neno ya Mungu na upendo kubwa enye munafanya juu ya watu ya Mungu muzidi pia kubarikiwa na mutuombeye sisi tuko uko ULAYA

  poleni sana swahili yangu ya kikongomani DRC
  Mungu wambingu awabariki sana

 217. Shalom servant of the living GOD.Nimelisoma somo hili na kwa kweli limenitoa mahali na. Kunipandisha kiwango cha maombi kwa upande wangu.Ila Mwalimu naomba unisaidie katika Biblia hamna mahali ambapo MUNGU mwenyewe ameagiza watu wamsifu?

 218. somo lako mwalimu ni zuri sana linafaa sana, mimi naomba Mungu akusaidie kukupatia mafunuo zaidi kwani hakuna jambo la kukatisha tamaa kama unaomba alafu hakuna majibu sasa kulingana na maelezo yako nimegundua watu wengi wamekuwa wakiomba bila utaratibu maalumu, Mungu akubariki sana

 219. Bwana Yesu asifiwe,Naomba niwashirikishe maombi yangu ili tuombe pamoja.Niko katika kipindi kigumu sana katika familia na kazini. Naomba Mungu aniwezeshe kushinda nanivuke salama.Pili niombee niweze kupata msichana wa kazi atakayekuwa na upendo na mtoto wangu awe na roho wa Mungu ndani yake.Ee Mungu pokea maombi na sala zetu.Amina

 220. Ahsante sana Mtumishi, kila leo kuna tunalojifunza SG, hii imeniinua sana sana. nami ninapenda kutembea katika maombi, iwe ni mkesha na wengine au nyumbani nitatembea nikiomba muda mrefu sana, nikipiga magoti muda kidogo tu nasinzia. Na ni kweli kuingia Rohoni kwa nyimbo za kuabudu ni rahisi zaidi sijui kwa vile tunakuwa tunasifu kuliko kuanza kuomba tu. Na pia ninapoomba kwa ajili ya wengine kunakuwa na nguvu ya ajabu kuliko ukikazania kuombea shida zako, Mungu ni wa ajabu!
  Ubarikiwe sana na tuzidi kujuzana ndani ya Kristo.

 221. Mtumishi wa Mungu mgesa,shukurani sana kwa kazi nzuri unayoifanya ya kutuwezesha kuutafuta ufalme wa Mungu.Mimi binafsi nimefunguka na nimejifunza mengi hasa kuhusu namna ya kuomba.Ubarikiwe sana.

 222. Be blessed Mtumishi wa Mungu Mgesa.Namshukuru Mungu kwa ajili yako.Kila siku yatupasa kujifunza na kila siku neno la Mungu ni jipya na Mungu anamfunulia kila mtu kwa apendavyo yeye Roho. nilikuwa naonyeshwa kila siku jinsi ya kuomba ingawa najitunza namna tofauti na nazitumia imepita mwezi nilionyeshwa jinsi ya kuomba kwenye njozi na Mungu na aliyekuwa ananifundisha ni Mtume na Nabii Josephat Mwingira, sikujua kuwa yanipasa niende Efatha kujifunza au vipi. nikawa najaribu kufuatilia vile nilivyoonyeshwa lakini narudi tena kwenye mazoea yangu ya siku zote. hivi sasa nipo Uingereza kwa mapumziko huku sasa wengi hawapendi kusali na hata wakisali hakuna hamasa kama za kwetu huko na hawaujui uokovu ni nini, na kwa nini wasali kwa jinsi hivi tunavyosali. nikawa najiuliza itakuwaje. mwenyeji wangu anasali na nikaanzisha tusali wote kabla ya kulala na maombi ya siku 7 Yeriko nimemaliza juzi. leo nafungua web site nipate maombi ya Tanzania nikapata hapa kweli Mungu anajibu. naomba na anipe mtu hapa uingereza atakayekuwa msaada kwangu na Mungu atuunganishe nae katika roho hata kama nikiwa mji wowote imani yetu iwe moja na tuanzishe prayer group hapa london, na Bristol ili watanzania waliopo huku wamjue MUNGU na kumkubali Yesu kwamba ndiye mwokozi wao. Mungu akubaliki sana Mtumishi uzidi kutuombea na sisi tuweze kusimama wenyewe ili tuweze kuwafundisha wengine kila nchi tuendayo. Amen

 223. Kwa kadri nijuanyo mimi kuna namna tatu za kuomba yaani kuomba kwa kawaida, kuomba kwa mikesha na kuomba kwa kufunga. Uchaguzi wa namna ipi inafaa kwa kuomba itategemea na uzito wa jambo unaloombea, yapo mambo ambayo yanahitaji maombi ya kawaida, ambapo mtu huomba au kuombewa kwa kawaida, pia yapo mambo ambayo watu hufanya maombi ya mikesha mara nyingi maombi haya hufanywa na watu zaidi ya mmoja japo hata mtu binafsi anaweza kufanya mkesha wake mwenyewe.

  Namna ya mwisho ya maombi ni ile ya kufunga, maombi haya yanawasumbua wengi sana, wengi wanaogopa kufunga, wanapiga gharama, lakini nataka kukuambia kwamba maombi haya yana nguvu sana kuliko aina nyingine yeyote ile ya naombi, kumbuka YESU alipoanza kazi alipandishwa nyikani akafunga muda wa siku arobaini, pia Paulo alipokutana na YESU akiwa safarini kwenda Dameski alifunga siku tatu, hivyo kufunga hakuepukiki hasa kwa mtu aliyeokoka, kuna manufaa kubwa sana. Mtu afungapo hushukiwa na nguvu kubwa sana za kiroho, tena tukumbuke kuwa vita vyetu si juu ya damu na nyama, bali ni juu ya falme za wakuu wa giza, wafalme hawa wananguvu kubwa sana hivyo bila kufunga hatuwezi kuwashinda, wameandaa mikosi,ajali na mabalaa mbele ya kila mmoja wetu ili wa muangamize hivyo bila kuomba na kufunga tutaendelea kuangamia, hebu anza na siku moja, kisha endelea na siku mbili, tatu na kuendelea.

  Mbona waislamu wanafunga mwezi mzima sasa kuna nini kwa ninyi watumishi wa Mungu wenzangu, hebu tufanye kazi ya BWANA, tena mkumbuke sisi ni wapitaji katika dunia hii, na kama hatutaifanya kazi ya BWANA basi yeye anaweza kuinua hata mawe yafanye kazi yake MUNGU hadhihakiwi, WOKOVU NI VITA.

 224. Asante sana Mtumishi na MUNGU Akubariki kwani tumepokea kitu kutoka kwako.
  Barikiwa.

 225. BWANA YESU ASIFIWE!
  Namshukuru MUNGU kwa namna ya pekee kwa kufungua mtandao na kukutana na maneno ambayo yameenda kuufungua na kunifariji kwani nilikuwa katika wimbi la mawazo. Zaidi sana nikushukuru mwalimu kwa mafundisho yako MUNGU azidi sana kukutia nguvu ili uihubiri neno lake. asante kwa neno uliloenda kutulisha naomba maombi yako na tuweze kuombeana kwa ujumla.

  amen

 226. Kuomba ni kupeleka mahitaji kwa BWANA, katika maombi mtu hupeleka mahitaji yake kwa BWANA, hii inaweza kuwa maombi ya toba,mahitaji binafsi, au hata kumwombea mtu mwingine jambo fulani au hata shukrani kwa BWANA. Kwa mtazamo wangu, kuna aina tatu za maombi yaani maombi ya kawaida, haya ni maombi ambayo mtu huyafanya kikawaida pasipo hatua yoyote. Aina ya pili ni ile ya maombi ya mkesha, hapa watu huweza kuomba kwa namna mbalimbali za mikesha ya makanisani na hata majumbani.Aina ya tatu ni ile ya kufunga,haya ni maombi mazito na yenye nguvu sana, hasa kama unatatizo linalokusumbua kwa muda mrefu, ni vema kwa mtu aliyeokoka kuwa na maombi ya kufunga, kati ya siku moja hadi tatu, ikiwezekana hata zaidi, lakini usifanye kwa kulazimishwa haitakusaidia. Pia kuna namna mbili za kuomba yaani kuomba kwa nadhiri na kusiko wa ndhiri, umbapo maombi ya nadhiri ni vizuri kuitimiza hiyo nadhiri yako kwani hiyo ni ahadi yako kwa BWANA,kwa wewe uliyeokoka hakikisha kila siku unapata muda wa maombi uongee na MUNGU WAKO. MUNGU AWABARIKI NYOTE,
  adam mpunga

 227. Mi binafsi nashukuru sana mwalimu kwa mafundisho yako na nina imani yamenifanya kuwa mtu mwingine katika uombaji!
  Mungu akubariki sana,na uendelee kutufundisha na mengine ambayo Mungu anakufunulia!

 228. Mwalimu Mgisa Mtebe mungu akubariki sana.
  Kweli ndugu zangu ni mara ya kwanza leo kuangalia hii website nadhani pia ni Mungu ndio ameniongoza hapa siku ya leo nitaprint haya mafundisho na kuwapa rafiki zangu wote pamoja na wadogo zangu.
  Imenifundisha mno na nitayafanyia kazi kwani kweli nilisoma mafundisho ila sikuwahi fundishwa hivi.
  Mungu akuzidishie na akupe mengine ya kutufundisha.
  AMEN

 229. Nashukuru mchungaji nimepata kitu hapa nilichokuwa naitaji kwa muda mrefu. Mungu azidi kukutia nguvu na afya njeme na ajaze pale palipopungua.amen

 230. wapendwa ktk kristo. mimi nilikuwa naomba maombi yenu watumishi hasa ktk kumshika Yesu na kushinda vishawishi. Mungu awatangulie katka kutenda kazi ya Bwana. amen

 231. Mimi kama judge binafsi nimejifunza kitu ambacho kuomba pamoja na mziki wa taratibu inaleta hamasa fulani pamoja na hisia zinazo weza kukufanya utokwe na machozi ubarikiwe sana mtumishi wa mungu.nimejifunza kitu

 232. ashukuriwe Mungu aliyekuongoza na kutupa wengi mafundisho haya maana tuliomba na wengine kukata tamaa ya kutojibiwa maombi sasa leo nimejua na kupata kitu kikubwa
  Mungu akubariki sana.

 233. Bwana yesu asifiwe,
  Mwalimu nakushukuru sana kwa mafundisho yako nimejifunza kitu chema na umenipa mbinu yakuweza kuomba kwa muda mrefu,mungu akubariki sana.
  Milley

 234. Mwalimu. Namuomba Mungu akubariki sana. Article yako hii nimeiweka kwenye favourites. Imenifundisha na kunifungua macho. Wemgi twapenda kuomba au kusali lakini hatujui hasa. Wewe umenipatia somo. Ninaamini ni mkono wa Mungu uliniongoza kwenye makala yako. Kabla ya hapo nilikuwa siijui. I was searching on Danstan Maboya only to come to your article. On each topic of yours kwa kila reference ndani ya biblia mimi nimekuwa nikinukuu ili nitajirike zaidi. You are indeed a blessing.Kumbe ili sala ijibiwe hatupaswi kuwa wachoyo.

 235. KWA KWELI MWL MGISA SINA LA KUSEMA MUNGU MWENYEWE ANAJUA JINSI NILIVYOBARIKIWA KWA NAMNA YA PEKEE MUNGU AZIDI KUKUTUMIA KWA KAZI YAKE.MUNGU WA MBINGU NA NCHI AZIDI KUKUPA MAFUNUO ZAIDI UBARIKIWE.TUTAZIDI KUWASILIANA UBARIKIWE

 236. Mungu akubariki mwalimu zaidi akupe hekima na ufahamu wakufundisha nimejifunza mengi na tena mengi zaidi
  kweli Strictly Gospel ROCKS in spiritual world

 237. NammHH!!! ubarikiwe mtumishi, maana yameniingia sawasawa. Kumbe kuna kipindi nilikua nacheza na maombi, vitu vingi nilikua nakiuka kabla ya kusoma huu msaada wako wa maombi.

  Nashukuru sana nadhani sasa shetani atakoma ubishi, maana naahidi kutupa mawe ya aina yake kuanzia huu mwaka mpya.

  Bwana awe nawe milele uzidi kutupa msaada zaidi wa kiroho.

 238. Ubarikiwe sana Mtumishi wa Mungu kwa huduma ya Mungu kuhusu maombi. mimi binafsi nimebarikiwa sana na nimejifunza kitu cha maana sana kupitia article hii. Namshuru sana Mungu kwa kunipa nafasi ya kusoma article hii. MUNGU AKUZIDISHIE NA AZIDI KUKULINDA NA KUKUZIDISHIA AFYA NJEMA SIKU ZOETE ili uweze kuendelea na huduma yake. AMEN

 239. BWANA YESU ASIFIWE KAZI YAKO NINJEMA SANA MUNGU AKUBARIKI NA KUKUHESHIMU KWA SABABU UMEKUBALI KUMTUMIKIA .UKWELI KUNA KITU NIMEFUNULIWA NACHO NI KUHUSU KUWEKA ULINZI KATIKA MAOMBI YANGU NIWASIANA NA WEWE KWA MASWALI UBARIKIWE . AMEN

 240. Bwana Yesu asifiwe!!
  Mungu akubariki Mwl Mtebe, Pokea baraka nyingi kutoka kwa Mungu. Nasema asante sana na nimefurahi leo kukutana na somo hili,Limenijenga nakunipa nguzu zaidi katika Maombi. Amani na iwe kwako. Amen

 241. MUNGU AKUBARIKI MTUMISHI WAKE KWA DOZE HII YA FAIDA KWA ROHO NA MIILI YETU PIA.
  ENDELEA KUUJENGA MWILI WA KRISTO KWA DOZI NYINGINE.

 242. Mwl,Mtebe
  Bwana Yesu asifiwe
  Naomba nichukue nafasi hii kukupongeza kwa article hii bora sana na kila mtu wa Mungu anapaswa kuisoma ili tuweze kwa pamoja kusimama imara katika maombi ya muda.Hakika nimefaidika sana na article hii,na nadhani kuanzia leo kwa msaada wa Roho Mtakatifu uombaji wangu utaboreka zaidi na zaidi.
  MUNGU AKUBARIKI KATKA UTUMISHI HUU.

 243. Mwl. Mgisa namshukuru Mungu kwa wewe! sababu umetupa kitu ambacho

  tulikuwa tunakosea thanks a lot Mungu akubariki SANA

 244. Mwl. Mgisa ubarikiwe sana, kwa article hii. Mi nikiomba nimepiga magoti uchoka lkn kwa kutembea nachukua muda mwingi, au nikisujudu mbele za Mungu naweza kuchukua muda mwingi

 245. Mwl Mgisa, asante kwa mafundisho yako juu ya Namna ya Kuomba. Nimejifunza vitu vingi. Ubarikiwa sana na uwendelee kutufundisha mambo mengi ya kiroho.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s