TUJADILIANE!

Bwana Yesu Asifiwe! hivi hawa watumishi wanatupeleka wapi? utakuta kuna matangazo mengi siku hizi yako dizaini mbalimbali JE UNAHITAJI MME/MKE, UNAHITAJI WATOTO, UNAHITAJI PESA, UNAHITAJI GARI, KWENDA ULAYA N.K. NJOO MAHALA FULANI MUNGU YUPO. Wapendwa matangazo ya namna hii mnayaonaje? na wale watumishi wanaofanya biashara madhabahuni na kuwatoza pesa waumini ili wawaombee, mnalionaje?


 

 

335 thoughts on “TUJADILIANE!

 1. mambo matatu hapa.
  1. hivi kwa nini watu washangae, wakati Yesu alisema wazi kuwa mambo haya yangetokea?
  2. wengine si watumishi hata kidogo, wako katika biashara zao. ni mbweha wako shughuli zao, hata dhamira haiwashitaki.
  3. wanaotapeliwa nao pia ni wa kushangaza. Biblia inatuambia kuwa, tuajaribu kila roho, na pia tuwe na uwezo wa kupambanua. upofu wetu ndo unaotuponza.

 2. Nawasalimu kwa jina kuu la Yesu Kristo, Watu wa Mungu mnaosoma hii habari , iko hivi…watumishi wa siku za mwisho wanaenda na watu hawaendi na Mungu wanaipindisha kweli ya Mungu nakuweka uongo na hawa watumishi wanahubiri mambo yanayoonekana ya nje ya mwili kwa ajili ya watu fulani na hawa wanaenda kwa wakati wanaangalia tatizo ambalo linasumbua muda huo lengo lao haswa si kuwaponya watu kama mtu unamuhubiria baraka kila siku na bado anatenda dhambi,hajui hata kuomba na hawa watumishi ukienda ktk makanisa yao hawafundishi kweli (NENO) ya Mungu hata mafundisho ya Roho Mtakatifu hawana wanjua wakikufundisha utaweza kuomba na kujisimamia mwenyewe KIROHO na hautawafuatafuata na kumwambia Mtumshi niombee wanachotaka kila siku upige simu au uende ukaombewe.. HITIMISHO.. Mwana wa Mungu siku hizi ni zama za mwisho usaimtegemee mtu muda wowote anakengeuka we muamini Mungu tu hakikisha umejezwa Roho Mtakatifu, unasoma neno la Mungu na Kuomba, Roho mtakatifu atakujulisha yote,kukumbusha na kukufundisha yote na atakupa uwezo wa kupambanua roho za watumishi Feki….,BARIKIWE NA BWANA YESU KRISTO.

 3. haleluja
  wapenzi nawasalim katika jina la bwana Yesu Kristo
  ndg kwa sasa limejitokeza wimbi kubwa la watu kujiita mitume na manabii je kanisa liko macho na haya yanayo jitokeza maana Biblia imeandika mambo mengi kuhusu siku za mwisho kuwa watatokea manabii wa uongo na watafundisha mafundisho ya uongo na kufanya miujiza mingi iko mifano mingi ya hao manabii ila haipaswi kusema lakini mwenye macho ya kutazama na masikio ya kusikia na ayaone haya
  sasa je kanisa tunaenda wapi???????????????? KILA MTU SAIZI ANAJIITA NABII MTUME NDO HUDUMA ZILIZO TAWALA NA MADANGANYO MENGI HUDUMA ZINGINE 3 HAZIVUMI SANA ILA KUKITAKA UMAALUFU JIETE NABII AU MTUME WAKATI KAZI ZA KITUME NA KINABII M2 HAZIJUI ALAFU ANA JIPAKIZA HUDUMA HIZO
  HEBU FIKILINI NDG NA CKU HIZI ZA MWISHO UNAFILIA NINI KUHUSU NENO LA
  MATHAYO 7:15
  MATHAYO 24: 11
  UNAELEWA NINI KUHUSU MANABII WA UONGO
  NB C KWAMBA HAKUNA MANABII WA KWELI WAPO
  ILA UNAELEWAJE KUHUSU KUJIOKEZA KWA MANABII WA UONGO

 4. Hata wale wanao sema na kuandika ratiba ya maombi wakisema ; maombezi ya KAZI,BIASHARA,KURUDISHA NYOTA,UKIMWI,KISUKARI na magojwa sugu mengine yote, je? ratiba yote hii ya nini? au wamekuwa waganga wa kienyeji?

 5. Niko dilema juu ya hii, hv hawa wanoitwa watumishi walaghai na kama wanatumia nguvu za giza na miujiza ikatendeka ina maaana nguvu za giza zina nguvu kuliko za Mungu? Na kama hazina nguvu kumshinda Mungu yatupasa sisi tunaomjua Mungu na tuombe ili hiyo miujiza ya nguvu za giza ikose nguvu kabisa na Mungu wetu aweze kujiinua. Pia kuna sehemu moja kwenye maandiko ya biblia yalieleza watu walivyojiuliza kua YESU anaponya kwa nguvu ya Mungu au Nelkableza? Inaonesha tunavyomuinua shetani kwa kuamini miujiza yatoka kwa shetani na si Mungu. NAWAOMBA WANA SG WENZANGU TUOMBE NA TUMUINUE MUNGU NA KUVUNJA NGUVU YA WANAOAMINI NGUVU ZA GIZA.

 6. Wakristo wengi wa siku za leo hufuata miujiza,na kuna watumish wengine huwalaghai kwa kuwashawish waende kwenye ministry zao watafanikiwa kipesa na kuwa na maisha mazuri,lakin si hivyo kwan baraka za Mungu huwa zinakuja kwa wakat muwafaka na huwa zinakuja kwa hatuwa na hatuwa na ili baraka hizo ziwe baraka ndan ya maisha yako ina bidi neno la bwana liwe ndan yakooo,ujumbe tuwe makin sana na hizi ni siku za mwisho

 7. vitendo vingine ni vya kulaaniwa na wakristo! hii tabia ya wakristo wenzangu kuzidi kusema eti “tuombe, mungu atasaidia” ni upumbavu wa kiroho. Wakristo wanastahili kusimama kidete na kulaani hizo injili za utapeli. Mapasta chipukizi wanataka utajiri wa mikato na ili watimize ulafi wao, wameenda kwa waganga kutafuta uchawi na shirikina kwa madhumuni ya kutenda miujiza za kuzimu. Hizo miujiza zinawanasa wasio wakristo walio vunjikia mungu.

 8. watumishi wa Mungu wako sahihi kabisa, kwanza wanatangaza makanisa yao ili watu wajue yalipo, pia wanawaambia watu kuwa kwa jina la yesu kila kitu kinapatikana, pia kuhusu pesa hakuna mtu aliyefanikiwa ktk nyakati za biblia ambaye hakutoa, kila nabii alianza na kujenga madhabahu bila kutoa hakuna baraka watumishi wako sahihi ebu tuwaombee

 9. 12 Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke.
  13 Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.
  DUNIA YA SASA IMEGEUKA NA KAMA NI HIVYO,TUNATAKIWA TUFUNGUKE MACHO-ROHO MTAKATIFU ATUSAIDIE ILI TUSICHUKULIWE NA UPEPO WOWOTE WA DUNIA HII
  TUSOME MAANDIKO,TUOMBE SANA-TUISHI MAISHA YA KIROHO KWA NJIA YA KRISTO BWANA WETU.NAYE ROHO WA KWELI KUTOKA KWA BWANA ATATUFAHAMISHA YALIYO KWELI,YAANI-IBADA YA KWELI KWANI IBADA IPO NDANI YA MTU MWENYEWE

  1John 4:1 Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sa
  babu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.
  MUNGU NA AKUBARIKI “AMEN”

 10. Kwa kweli, mtumishi wa Mungu hatarajiwi kuita watu kwa matanio ya kidunia!
  Na haipendezi inapofikia wahubiri wanafundiha kuheshimu majina yao badala ya jina lake Mungu mwenyewe…
  Wokovu hauna mtu bali una bwana Amen.

 11. Huo ni utapeli tu ndugu yangu. Wanajua kuna watu wanatafuta mafanikio kwa njia za mkato na wanawapata kweli.

 12. 1kor 10:12-13. Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke.
  13 Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.

 13. ok kwa upande wangu siwezi kuwa shangaa sana maana neno lilisha sema n a mimi ninacho jua hakuna neno ambalo MUNGU alisema halafu lisitimie Yuda alimsaliti Yesu ili neno lipate kutimia so hakuna kipya chini ya jua coz Yesu. alisha sema watakuja.na siku ya mwisho watakapo sema tulimua tukifanya ishara na maajabu BWANA atawaambia siwajui so waendelee kujichanganya sana na kuoenda fedha na kuacha injili ya YESU wahuiri injili zao na walio waaminifu wataendelea kua waaminifu na watavuna walicho kipanda

 14. KIZAZI HIKI KIMEPOTOKA,SIJUI NANI ATAKIOKOA TENA KAMA WANASHINDWA KUFUATA YALE TULIYOFUNDISHWA NA KRISTO YESU BWANA WETU!!!
  KIZAZI KIMELISHWA SUMU,KIMELEWA MVINYO,KINAWAYAWAYA,HAKISIKII,HAKIELEWI,HAKIELIMIKI N.K
  MIOYO YAO IMEJAA KUTU,KINA MIOYO YA CHUMA,ISIYOTAHIRIWA,ISIYOPENDA MAFUNDISHO,CHENYE KUPENDA MAMBO YA DUNIA HII.
  NAWAOMBA NDUGU ZANGU TULIOMBEE KANISA NA NCHI YETU YA TANZANIA.
  MUNGU NA AWABARIKI SANA.

 15. Bwana Yesu asifiwe,hivi Bwana Yesu alimaanisha nini aliposema waache wafu wazike wafu wao

 16. hayo hayana budi kutukia ili maandiko yatimie… kwa hiyo wakuwepo tu waongo na kusema kweli ya Kristo, cc tunapaswa kuongozwa na Roho kama biblia inavyosema … barikiwa sana.

 17. UJUMBE KWA KANISA LA TANZANIA
  TAREHE 20/ 03 /2012 SAA 9:11

  MCHUNGAJI ADAM JOSEPH
  Nikiwa nyumbani kwangu majira ya saa8 nikitafakari mwenendo wa Dunia ulivyo, ndipo Neno la Bwana likanijia kusema, “Adam mwanadamu nakutuma kwa Kanisa langu la Tanzania nzima mjini na vijijini, ukaseme maneno yote ninayokuambia. Usiogope wala usitetemeke mbele yao nisije nikakutetemesha, uwe na moyo mkuu na wa uhodari maana najua wengi watakupinga kwasababu mioyo yao imetiwa ganzi soma YEREMIE 1:17-19, jitie nguvu ukaseme usiogope mimi niko pamoja nawe nikuokoe usiogope wala usifadhaike simama imara usiogope.

  Liambie kanisa langu limeacha kweli yangu na kugeukia njia zake, litambue huu sio wakati wa kustarehe wakati watu wanaangamia na kupotea. Kanisa langu limeacha upendo wa kwanza, kila mmoja anajijari nafsi yake na watoto wake soma UFUNUO 2:4-5. Kanisa langu limekosesha watu wengi wasiniamini kwa sababu hakuna utofauti wa matendo yao. Kama ni kutembea nusu uchi, na watoto wangu wanatembea nusu uchi, na kama ni kuvaa mavazi ya kigeni na watoto wangu wanavaa mavazi ya kigeni SEFANIA 1:8. Ole kwa wachungaji wanaokula na kupuliza wanapoza maneno yangu. Nyumbani mwangu hamna chakula cha kutosha, imebeki ni kufarijiana amani wala hapana amani soma YEREMIA 6:14. Hawawaambii watu makosa yao wanaogopa kukimbiwa wanafurahi kujaa watu ndani ya majengo makubwa lakini siyo kuwaambia watu makosa yao soma MATENDO YA MITUME 5:1-4. Kanisa langu limeikaribisha Dunia nyumbani mwangu. Hofu haimo, watoto wangu hawalipi zaka kamili bali ni uongo mtupu. Wachungaji wameruhusu mitindo ya Dunia iingie nyumbani mwangu soma WARUMI 12:2. Wanawake wanavaa mavazi ya kubana wamejaa tamaa ya kidunia. Nimewaambia wanawake wavae mavazi ya kujistiri lakini wamekataa soma 1TIMOTHEO 2:9-10. Waimbaji nao sijui wanamsifu nani, nani anayekubaliana na uchafu maana kusifu kunawapasa wanyoofu wa moyo. Waimbaji wamejaa majivuno, masengenyo, wivu, hasira, chuki na hawana moyo wa rehema ndiyo maana utukufu wangu haushuki kama hapo mwanzo, soma 2 NYAKATI 5:12-14.

  Nimeliagiza Kanisa langu kupendana lakini upendo haupo. Watoto wangu wanabaguana na kuchukiana hata wachungaji hawawafundishi watoto habari ya upendo bali mafanikio na kuwafariji kuwa wanakwenda mbinguni, kwa nani? Huko wanakokwenda ni wapi? Maana mimi Bwana Mungu wao ni Upendo. Soma 1 YOHANA 4:19.

  Jinsi Dunia iendavyo ndivyo baadhi ya watoto wangu wanavyoenenda. Wengine wameacha matumizi ya asili. Soma WARUMI 1:26. Naja kama Mwizi, siku msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja kuchukua Kanisa lake lililosafi, takatifu.

  Watoto wangu wanaangalia picha za ngono wanajitia unajisi. Kanisa langu nalipa shauri, huu sio wakati wa kucheka na kustarehe bali liomboleze maana siku za kujiliwa kwake zinafanya haraka kuja. Soma YOELI 1:13-15. Omboleza Ee Kanisa langu, maana siku usiyodhani unakwenda kunyakuliwa asema Bwana wa majeshi.

  Wanawake hawawatii waume zao, wamejaa kiburi za dharau wakati nimewafananisha na Kanisa. Soma WAEFESO 5:22-24. Watoto wangu hawawatii viongozi wao kama nilivyoagiza. Soma WAEBRANIA 13:17. Nasema tendeni mema, acheni maovu ambayo mwisho wake ni mbaya. Omboleza wewe uliyependwa, tangaza wokovu kwa watu, matendo yako yawe nuru wapate kujifunza kwako. Epuka mapema ghadhabu yangu inayokwenda kuikumba Dunia na wote wakaao ndani yake. Kanisa linitafute. Soma AMOSI 5:5-9. Enyi mnaopuuza maneno yangu, siku zinakuja ambazo mtanitafuta wala hamtaniona, mtalia sitasikiliza vilio vyenu. Geukeni basi mkatende haki, nawapenda nitafuteni nami nitaonekana asema Bwana”.
  MCHUNGAJI ADAM JOSEPH,
  KANISA LA EVANGELISTIC ASSEMBLIES OF GOD,
  SIMU +2755 768 657482 / +255 688 856581.
  Ujumbe huu umeandikwa na David Carol na kutumwa kwenye mtandao
  Simu , +255 764 847847 / +255 782 847747
  Email: davidcarol04@gmail.com
  Blog: http://WWW.davidcarol719.wordpress.com
  Mungu akubariki sana kama utaona vema ku”share” au ku “like”

 18. hawa huwa wanafanya biashara na sio kuhubiri Neno la Mungu ipasavyo.wao ndo watakuwa wakwanza kuchomwa moto kwn wanaenda kinyume na maandiko.

 19. Bwana Yesu asifiwe!

  Ni vigumu sana kwa binaadamu kujua mapenzi halisi ya Mwenyezi Mungu. Nilichelewa kwa mada hii lakini subject ni hyo hiyo tu. Ya muhimu nafikiri, si kujua Mungu anapitia kwa mtumishi gani ili aokoe watu wake. Kuna hata wale watumishi watakaobaki bridge tu na wakombolewa wa Mungu wanapita. Tumuachie Mungu kazi yake ya kutenga mbuzi na kondoo.

  Jambo kama hili lilifikia mitume wa Yesu wakati walipokuta mtu mwengine akifukuza pepo wachafu kwa Jina la Yesu Kristo. Mitume wao hawakuvumilia na wakaenda kueelezea Yesu jambo hilo. Lakini Yesu aliwajibu akasema(soma):”Marko 9: 38 Yohana akamjibu, akamwambia, Mwalimu, tulimwona mtu akitoa pepo kwa jina lako, ambaye hafuatani nasi; tukamkataza, kwa sababu hafuatani nasi.
  39 Yesu akasema, Msimkataze, kwa kuwa hakuna mtu atakayefanya mwujiza kwa jina langu akaweza mara kuninenea mabaya;
  40 kwa sababu asiye kinyume chetu, yu upande wetu.”

  Nafikiri, wapendwa, tushike ya muhimu kwamba mtumishi awe wa kuomba pesa ao la, iwe anatukuza jina la Yesu Kristo. Sherti huyu mtumishi mshahara yake ni duniani. Lakini wale wenye kupokeya miujiza kuna vikundi vitatu:
  1. Wanaodhani kama pesa yao imewaponya. Hawa ni wa dunia kabisa.
  2. Wanaodhani kama mtumishi ndiye anaye na nguvu ya kuponyesha. Hawa wametimiza andiko “Anaetumainia mwanaadamu na alaaniwe”
  3. Walioshika kama waliponyeshwa kwa uweza wa jina la Yesu Kristo. Hawa wamepata rehema. Ina maana wamesamehewa zambi na pia wamepata uponyaji wa nafsi na mwili.

  Mubarikiwe sana.

 20. Bwana Yesu asifiwe!

  Ni vigumu sana kwa binaadamu kujua mapenzi halisi ya Mwenyezi Mungu. Nilichelewa kwa mada hii lakini subject ni hyo hiyo tu. Ya muhimu nafikiri, si kujua Mungu anapitia kwa mtumishi gani ili aokoe watu wake. Kuna hata wale watumishi watakaobaki bridge tu na wakombolewa wa Mungu wanapita. Tumuachie Mungu kazi yake ya kutenga mbuzi na kondoo.

  Jambo kama hili lilifikia mitume wa Yesu wakati walipokuta mtu mwengine akifukuza pepo wachafu kwa Jina la Yesu Kristo. Mitume wao hawakuvumilia na wakaenda kueelezea Yesu jambo hilo. Lakini Yesu aliwajibu akasema(soma):”Marko 9: 38 Yohana akamjibu, akamwambia, Mwalimu, tulimwona mtu akitoa pepo kwa jina lako, ambaye hafuatani nasi; tukamkataza, kwa sababu hafuatani nasi.
  39 Yesu akasema, Msimkataze, kwa kuwa hakuna mtu atakayefanya mwujiza kwa jina langu akaweza mara kuninenea mabaya;
  40 kwa sababu asiye kinyume chetu, yu upande wetu.”

  Nafikiri, wapendwa, tushike ya muhimu kwamba mtumishi awe wa kuomba pesa ao la, iwe anatukuza jina la Yesu Kristo. Sherti huyu mtumishi mshahara yake ni duniani. Lakini wale wenye kupokeya miujiza kuna vikundi vitatu:
  1. Wanaozani kama pesa yao imewaponya. Hawa ni wa dunia kabisa.
  2. Wnaozani kama mtumishi ndiye anaye na nguvu ya kuponyesha. Hawa wametimiza andiko “Anaetumainia mwanaadamu na alaaniwe”
  3. Walioshika kama waliponyeshwa kwa uweza wa jina la Yesu Kristo. Hawa wamepata rehema. Ina maana wamesamehewa zambi na pia wamepata uponyanyi wa nafsi na mwili.

  Mubarikiwe sana.

 21. Agizo la Bwana Yesu ni
  1. Kuihubiri injili kwa kila kiumbe kwa jina la Yesu (habari ya toba na ondoleo la dhambi) Lk 24:47, Mark 16:15
  2. kuwafanya mataifa kuwa wanafunzi, kwa kuwafundisha yote aliyotufundisha na kuwabatiza Math 28:19
  3. Aaminiye abatizwe ili aokoke Mark 16:16

  Mengine ni ya ziada maana Yesu alisema “na ishara hizi ZITAAMBATANA na hao waaminio, kwa jina langu watatoa pepo,watasema kwa lugha mpya, wataponya wagonjwa Mark 16:17-18

  Lengo kuu la injili ni toba. Asiyetubu hana nafasi katika ufalme wa Mungu. Lakini asiye na mali, asiyeponywa, asiye na gari (mali), asiyekwenda Ulaya au Marekani, maadamu ametubu, akamkiri Yesu na akaamini injili na kubatizwa anayo nafasi mbinguni.

  Shetani anatumia ufundi wa maneno kupoteza lengo la Injili kwa watumishi wa Mungu kuwaita watu waje kwa Yesu ili watajirike, waponywe magonjwa badala ya kuwaambia wazi lengo kuu ambalo ni kutubu na kuiamini injili.

  Mungu atufungue Macho.

 22. Neno la Mungu linasema hawa wanataja farasi wengine magari lakini sisi tunalitaja jina la Yesu Kristo na naamini kuwa Mungu achanganywi na chochote kile ipo siku Mungu atajidhihirisha kwa watumishi wauongo wanao danganya watu wa Mungu madhabahuni ….

  its me Ev

  Elibariki Zablon

 23. Wahusika wa mtandao huu, mnahitajika kuwapa watu uhuru wa kusema wanachokijua, sio mnachokipenda, kisha Neno la Mungu ndilo litakachokibainisha iwapo ni cha kweli au uongo. Pia wahamasisheni Wachungaji ambao ndio wana zuoni waweze na wao kuchangia.

 24. MUNGU atusaidie sana, asaidie kanisa la kizazi hiki na watumishi waelewe kuwa YESU anataka watu wajue neema ambayo MUNGU amewapa wanadamu ambayo ni neema wokovu, iliyopatikana kupitia kuteswa kwake yesu, kufa na kufufuka kwake. Maana yesu hakutumwa ulimwenguni aje kuleta mali kwa watu bali wokovu, kwasababu kama ni mali watu walikuwa nazo. Inatupasa tuwahubiri watu juu ya neema ya wokovu wao, msamaha wadhambi na ahadi zake yesu. Mali nimengineyo kwani hayo hutokana na baraka za MUNGU pekee.

 25. Mungu wa babu yetu Ibrahim hawabariki sana,awape moyo wa kumjua yeye peke yake na yule aliyemtuma Bwana wetu Yesu Kristu,mambo yote haya ni vile watu wanapenda miujiza wanasahau kuwa Bwana wetu Yesu kristu hakufa kwa ajili ya hao wahubiri tu,bali kwa ajil;i ya kila mmoja hasa wale wanaomwamini, jifunzeni kuomba wenyewe, cha msingi ujilinde matendo yako kwa kuangalia ni vp unaziishi amri zake,nawe utaiona miujiza yake, bila kujali unajiita mlokole au vp maana ,ulokole ni moyo wa mtu ukoje mbele zake yeye anayejua kusoma mioyo ya watu na si vinginevyo. Tuombeane katka kuziishi amri za Mungu tupate kuokolewa siku ya mwisho!
  Mbaki katika utimilifu mbele za Mungu.

 26. watu hao ni ma freemasons, watu hawahubiri kuhusu kuja kwa Yesu sijui nani kawambia tunataka kwenda ulaya, au tunataka magari tujaze folen barabaran, jamani Yesu anarudi tena amekaribia saana saana, watu wamefungwa masikio ya kiroho mpaka na ya kimwili mi naona, hawashituki kabisa nakuona kwa nini watu hawa hawasemi kuhusu kwenda Mbinguni kwamba yesu amekaribia?

  jamani kila mtu kwa kadili atakavyoweza aombe mungu saana ili aweze kufika mbinguni, tukumbuke kwamba mbinguni kila mtu ataenda ki vyake sio na mumeo/mkeo, baba/mama, dada/kaka au shosti wako…… so do the best if you wan see God in heaven…

  BE BLESSED ALL OF YOU

 27. mambo kama haya, yanatatanisha kwa kweli, hata kama wanatangaza kwa nia njema inaleta mashaka kwa watu hasa wachanga wa kiroho,maana matangazo yanafanana na ya Dunia, Biblia inasema wala msienende kama mataifa waenendavyo. mimi sioni kama wanakosea ila wale wenye kuwatoza Watu pesa ndipo wawaombee hawa ni ndio waliojiingiza kwa siri watu walioandikiwa hukumu tangu zamani.

 28. Manabii wengi wa uongo wameibuka na kuifanya dini kuwa biashara hvy 2natakiwa 2jihadhari

 29. Wapendwa, bwana asifiwe. Hivi kwanini tusiwe na misimamo yetu? Angalia moyo wako unataka nini ambacho unaona kinampendeza Mungu. Kuna baadhi ya wahubiri wanataka pesa. Kwetu kunammoja alishawahi kusema eti akitaka kukuombea mpaka utoe chochote. Kweli? Mungu anasema hivyo?. Enyi wahubiri acheni kumkasirisha Mungu. Watu wa Mungu tuweni na misimamo yetu.

 30. Jamani mimi naona hilo lisitupe shida kwa sababu manabii walikwisha kutabiri… Hivyo basi ili siku za mwisho zitimie mambo hayo lazima yatokee yatupasa tuzidi kuomba ili tusidanganyike lakini tusiombe ili hayo mambo yasitokee kwani yalikwisha tabiriwa!!!!!!!

 31. JAMANI TUANGALIE SANA TUSIJE KUTA TUNAMFANYA MUNGU KIBARUA NA SISI TUNAJIITA WAFALME TUJISHUSHE NAYE ATATUINUA.

 32. SHALOM WAPENDWA ,

  ALAMA ZA NYAKATI ZIKO UPANDE WANGU ,

  KUOMBEA MAISHA YA BAADAE LEO SOMO LINAENDELEA ,HATA SITAMAINI KUKOSE SEMINA LIPO DIRECT PROPOTIONAL TO MY LIFE THIS TIME

 33. unajua cku hz wasanii wamekuwa wengi hasa kwenye huduma y mungu ndo maana unakuta sehemu ambayo haifai kuwa kanisa unakuta kanisa sio kwmb wanataka kueneza injili hapana bali kupata wa2 ndo maana huduma y mungu imekuwa km matangazo y kibiashara ili kuweza kupata market ambao ni wa2,sasa kila m2 anaboresha huduma ya matangazo ya biashara yake.sasa ni kazi kwa mkristo kuwapima wa2mishi hawa na kuwatambua kwa matunda yao na wakristo wacpende sana kuombewa wajifunze kujisimamia wenyewe.

 34. Mungu awabariki sana kwa michango yenu yote mizuri zaidi na zaidi ushauri wangu katika hilo, Bibilia inasema uyaonayo hayo uje ulimwemwisho umekalibia shika saaaana ulicho nacho.

 35. Jina la Bwn lbarikiwe.

  MTUMISHI WA MUNGU NI MTU KAMA MIMI ANA KARAMA KAMA ZA MTU MWINGINE TOFAUTI YAKE NI KWAMBA YEYE AMEPAKWA MAFUTA KWA AJILI YA KUOKOA WENGINE. ANAYO MAMLAKA YA KUKANYAGA NYOKA NA NGE NA WALA HATAWAUMA, AMEPEWA MAMLAKA YOTE DUNIANI NA MBINGUNI KWA KUWA YESU KRISTO ALISEMA KAZI NIZIFANYAZO MIMI NANYI MTAZIFANYA. YER. 1;10.

  NAWAPENDA.

  MADAM LUCY

 36. Kwanza mimi binafsi kwenda kuabudu mahali kama hapo! pili naomba nichangie tu kidogo juu ya hili, ukisikia kanisa linajinadi kwa stahili hiyo basi hawana nia ya dhati ya kuokoa roho za watu ili waishi maisha matakatifu kisha waende mbinguni, wanatumia shida walizonazo watu ili wawavute waweze kuwanyonya vizuri, biblia inasema Yesu ni yeye yule jana , leo na hata milele, kwa hiyo kama aliweka kanuni za kufanikiwa hata aje nani hawezi kuzipindisha, kanuni za kufanikiwa zinapatikana katika kitabu cha kumbukumbu la torati 28:1…….. Mungu hajajificha juu ya hilo, na anachojali Mungu ni roho za watu kua salama kuliko hivyo wanavyovinadi, na ndio maana akasema “utafuteni kwanza ufalme wa mbinguni na mengine yote mtazidishiwa” inaonyesh ni jinsi gani Mungu anapenda sana watu wake wawe salama kwanza roho zao na ziwe tayari wakati wowote maana hatujui wakati atakao kuja mwana wa adamu, halafu pia biblia inasema, “mfanikiwe sana kama vile mfanikiwavyo rohoni” huu ni msisitizo kutuonyesha hayo yote wanayo yanadi ni ubatili na kujilisha upepo ila cha msingi hapa ni roho yangu kwanza!!!!!!!!!1

 37. Ni sawa hawa Wachungaji wanaweza wakawa na nia njema ya kumuonesha mtu kuwa kwa Yesu au kwa njia ya maombi yote hayo yanawezekana ila nafikiri hiyo siyo njia njema na sahihi ya kumtangazia mtu ambaye bado ufahamu wa Kimungu haujamfikia.

  swala la kuwatoza watu katika kuwafanyia maombi, jamani hii ni kutafuta laana tu,hata dhamira na nafsi zetu zitatusuta tu kuwa hili si jambo jemba mbele za Mungu na wanadamu pia/

  Hizi ni siku za Mwisho kwahiyo wanatokea watumishi wa kila aina, ni kazi kwetu kuomba Neema itokayo juu kuweza kupambanua lililo jema na lisilo jema, MUNGU ATUSAIDIE SANA KATIKA HILI!!

 38. Hakika hata mimi sipendezwi na mtu ama mtumishi unayejiita wa Mungu tena wa kuitwa kupeleka injili kwa wote wasiomjua YESU.Inafika sehemu unaanza kutumia karama uliyopewa kujitajirisha,je kweli haya ni mapenzi ya YESU ALIYOTUAGIZA?,KWELI INANIUMIZA SANA HATA KUSIKITIKA MNO KWA TENDO HILI.
  Injili imekuwa ya BIASHARA sasa na sio ya kumpendeza Mungu.Imekuwa sio ajabu kusikia watumishi wakijinadi kwenye RADIO,TELEVISION,MAGAZETI NA KWINGINEKO wakijitangaza juu ya HUDUMA ZAO.Kweli sio mbaya kutangaza juu ya huduma yako lakini juu ya hili la kusema NJOONI WOTE ……..KAMA HUNA MKE/MME UTAPATA HAPA NA MENGINE AMBAYO MIMI NINAYAITA VIVUTI VYA UTALII WA DHEHEBU NA DINI.NA KUJITAFUTIA UMAARUFU BADALA YA KUMTUKUZA MUNGU.Hebu soma ISAYA 42:8
  Mungu anasema ……….”utukufu ni wake wala hatampa mungu mwingine”.Sasa kwa nini ujitangazie kuwa unaweza badala ya kusema YESU?
  Watumishi wenzangu kweli sio vizuri hebu tutende kwa ajili ya YESU na sio kwa faida yetu.Sisi tutende mema tu kumwinua YESU hali ukijua kuwa utavuna kwa kiwango usiotarajia siku utakapoitwa na mwajiri wako aliyekuajiri kazini.
  UNAJUA KWANINI YESU ANASEMA …..”MAVUNO NI MENGI LAKINI WATENDA KAZI NI WACHACHE? NI KWASABABU WENGI WANATUMIA KARAMA WALIZOPEWA KUJITAJIRISHA JAPOKUWA MAVUNO YANAOENGEZEKA KWA BWANA,USISHANGAE WEWE USIHESABIWE KTK UFALME WA MBINGUNI

 39. John 7:24
  24Msitoe hukumu kwa kuangalia mambo juu juu. Hukumuni kwa haki.”

  John 7:24

  Amplified Bible (AMP)

  24Be honest in your judgment and do not decide at a glance (superficially and by appearances); but judge fairly and righteously.

  John 7:24

  New King James Version (NKJV)

  24 Do not judge according to appearance, but judge with righteous judgment.”

  Ndugu Faines saimon naomba niambie kifungu hapo juu kina maana gani kwa sababu nimeona sehemu mbali mbali mambo yakiwa yanakemewa! watu wanapenda kukimbilia andiko la usihukumu. Ili watu wasiweze sema.
  Naona maandiko niliyotoa hapo yanaruhusu kutoa HUKUMU ila iwe ya HAKI TU. Sijawahi kuona mtu akinakiri andiko la matayo kisha aseme na hilo la yohana…ili kufafanua kwamba mtu anahukumu.
  Nimeona watu wengi wakilikumbuka andiko la matayo kirahisi ila la yohana sijawahi kuona wakilizungumzia.
  Naomba ufafanuzi. Mtu yeyote mwenye uelewa mzuri wa andiko la Matayo na la yohana yaliyotajwa hapo juu naomba afafanue…
  Ili watu tuweze jua namna ya kuyatumia…ili isije tokea mtu anakemea maovu/upotofu sisi tukakimbilia nyamazisha kwa andiko eti anahukumu.

 40. Bwana Yesu asifiwe minaona watumishi kama hao tusiwahuhumusis wanadamu maana katika Mathayo mtakatifu sura ya 7:1-4 inasema tusihukumu tusije tukahukumiwa Mungu mwenyewe atawahukumu kama walitenda mema au mabaya na biblia imesema tusifurahi kwakuwa mapepo yanatutii bali tufurahi kwakuwa majina yetu yameandikwa mbinguni. Mwenyemasikio na asikie neno ambalo roho ayaambialo makanisa. mbarikiwe kwa mtandao huu AMINA

 41. Hebu tuwe na imani dhabiti juu ya mambo yakiroho tusiyumbishe maandiko hata kamwe yatadumu swala la Babu sisi kama wakristo wa kweli tusilishibikie maana nyakati siyo za mashindano ya kiima bali ndio wakati rehema dumu kwa Yesu maandiko yanasema siku za mwisho zitakuwa za kutisha lakini si hiyo tu na wengi wataikana imana ndugu kuwa na moyo mkuu

 42. Bwana yesu asifiwe sana, yani Mungu wa ajabu kweli nimefurahi kuona hii website kuliko kukalia eti facebook…???so wat hizi ni nyakati za mwisho wapendwa yote yanayotokea yametabiliwa jamani hawa wanabii wa uongo jamani si tunawaona….?sasa wakristo wapendwa tuweni makini na madhehebu yanayotokea sasa..at the end tutajikuta mmepotea njia…ninawasihi vijana wenzangu mkumbukeni Mungu siku za ujana wenu kabla azijaja siku mbaya.achananeni na mambo ya dunia yote yanapita,tafuteni ufalme wa Mungu mengne mtazidishiwa…nuru ya Bwana iliyo mbinguni imulike kwenu kila zito liwe jepesi..nawapenda sana.mubarikiwe..
  Sarah.

 43. Nawashukuru kwa masomo mazuri na hata shuhuda zenye kujenga Mungu awabariki sana

 44. Haleluya! sijasimama Upande wa Babu au Upande wa Mtu yeyote, napenda kusimama katika kweli ya Mungu! Ni watu wangapi wameombewa na wakapona lakini bado mpaka sasa wanakunywa dawa za Hospitali? Kipindi hiki ni kweli cha kuangalia! ila bado mkazo wangu uko palepale, kama mtu akienda Loliondo kwenye kikombe na akapona its OK, FINE! lakini naomba kikombe cha BABU tusikiweke kwenye masuala ya IMANI yetu ya KIKRISTO! Babu aponye au asiponye YESU Yuko pale pale, habadiliki hata kidogo! Lakini kumbukeni Mungu hana mfumo mmoja wa uponyaji, na ndiyo maana wakati mwingine tunaweza kuwaombea wagonjwa sana na wakapona baada ya kunywa dawa fulani za Hosptalini, lakini hata hapo tunamsifu Mungu, Je mbona hatumsifu Mungu katika kikombe cha Babu? mbona tunawaombea madaktari na manesi kwamba Mungu awasaidie na dawa wanazotoa kwa wagonjwa ziwe na nguvu ya kuwaponya wagonjwa wale, je kuna aliyewahi kuomba kwa ajili Ya Mch. Mwasapila? kama sio matatizo nini? mimi nasimama katika ukweli kwamba NENO la Mungu liko pale pale hata kama taifa la TANZANIA lijawe na vikombe! Mungu atusaidie sana!
  Daniel Seni
  Presbyterian Church T
  Dar es salaam

 45. Mungu nimwabuduye mimi hatendi kwa jinsi hiyo. Hafungwi na majira wala nyakati, wala jiografia. Tena Mungu wangu hajichanganyi kiasi cha kuja na masharti mapya kila uchao. Tena anapoponya hahitaji msaada wa dawa za hospitali kuendelea kutumika kwani Yeye ni yote katika yote. Kizazi chenye kutaka miujiza! Hakika shetani anajitwalia utukufu.

 46. ujue juu ya Tiba hii, kinachowasumbua akili watu wa Mungu ni je dawa hii ni kweli inatoka kwa Mungu au inatoka kwa Shetani? sasa katika utafiti wa Wizara ya Afya, tunaona haina tatizo! tatizo ni katika masuala ya Imani, je utaiweka katika kundi lipi? je huu mti ni mti tu wa kawaida ambao hauhitaji mashariti mengi kama ambayo Mchungaji anadai au ni mti wa Kimiujiza tu? Mimi naona kama kuna anayetaka kwenda kunywa aende akanywe tu, maana lengo la Mgonjwa ni kupona. hajui kitakachomponya, iwe amepona kwa nguvu za giza au amepona kwa nguvu za Mungu, lengo ni kupona tu. sasa kama watu wanakunywa na kupona, mimi kama mtumishi wa Mungu, ya nini niwazuie? hatuwezi kujua mambo ya Mungu, Pengine kaamua kufanya hivi ili kutuweka sawa sisi tunaojiita wachungaji wa vituo vya maombezi.

  Daniel J Seni
  Presbyterian Church T
  Dar es salaam

 47. Kumbe Suala la Loliondo ni kubwa hivyo! Hata serikali inafuatilia!! Soma taarifa hiyo ya Wizara ya Afya. Inapatikana katika website ya Wizara.

  Wednesday, April 06, 2011.

  Home > News in Detail

  28th March 2011
  Taarifa ziliifikia serikali kuwa, Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila, anatibu magonjwa sugu kwa kutumia dawa aliyooteshwa na Mwenyezi Mungu. Inasemekana kuwa, mchungaji alianza tiba hii tangu mwezi Agosti 2010, lakini watu wengi walianza kumiminika kwenda huko Samunge, kuanzia mwishoni mwa mwezi wa pili, mwaka huu wa 2011.

  Kufuatia taarifa hii, serikali iliielekeza Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuwa, ufanyike haraka uchunguzi kuhusu dawa hii na itoe ushauri Serikalini ipasavyo. Baada ya kupokea maagizo hayo, wizara iliteua wataalamu kutoka taasisi zake tukiwemo sisi, TFDA, NIMR, Muhimbili kwa maana ya MUHAS, Mkemia Mkuu na tulijumuisha wataalamu wa hapa wizarani, ili kuifanya kazi hiyo muhimu, akiwemo Msajili wa Tiba Asili na Mbadala.

  Hapo Machi 7 mwaka huu, sisi TFDA na wenzetu wanasayansi tulifanya safari kwenda Samunge kuonana na kufanya mazungumzo na Mchungaji mstaafu AmbilikileMasapila. Sisi TFDA na wataalam wenzangu wote, tunamshukuru sana mchungaji mstaafu, kwa ushirikiano na msaada mkubwa aliotupa sisi watafiti wote. kwa kuwa, tulifanya mazungumzo kwa masaa kadhaa kuhusu dawa hiyo jinsi alivyoanza, pia, alituonyesha mti unaotumika na alitupa sehemu mbali mbali za mti huo, kwa uchunguzi zaidi. Kadhalika, alituonyesha jinsi anavyotayarisha dawa hiyo na kutupatia sampuli yake iliyokwishategenezwa, tayari kwa matumizi. Sisi TFDA na wataalamu wenzetu tuliondoka nayo, kwa ajili ya uchunguzi zaidi, kwenye maabara zetu.

  Baada ya kurejea kituoni Dar es Salaam, kazi ya utafiti wa dawa hiyo ilianza:
  Jambo la kwanza kama watafiti, ilikuwa ni kuangalia na kuhakikisha usalama wa dawa ya Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila kwa watu. Uchunguzi uliofanyika, umetoa matokeo ambayo tumeridhika kuwa, dawa kwa kipimo anachotumia Mchungaji mstaafu AmbilikileMasapila, haina madhara yoyote yanayotambulika kwa sasa, kwa matumizi ya binaadamu.

  Kazi inayofuata kwetu sisi watafiti baada ya matokeo haya, ni kuchunguza na kubaini, kama kweli dawa hii inatibu magonjwa hayo matano (5), kama anavyoeielezea yeye Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila. Uchunguzi huu utakapo kamilika, matokeo yake yatatolewa mara moja kwa wananchi wote!.

  Hata hivyo, ninaomba kuwatahadharisha kuwa, hatua hii ya uchunguzi, si ya muda mfupi. Kwa mujibu wa kanuni na taratibu za kisayansi duniani, tafiti za namna hii zina mchakato unaohitaji muda wa kutosha kukamilisha hatua zake mbali mbali, na pia, kufikia viwango na vigezo vinavyokubalika Kitaifa na Kimataifa. Tunafanya hivyo kwa kuzingatia kuwa, dawa hii ni kwa ajili ya matumizi ya binadamu, na inafuatiliwa na wananchi wetu na mataifa mbalimbali.

  Sambamba na utafiti katika hatua hii, pia tunafanya uchambuzi wa kisayansi, katika maabara zetu, kwa sampuli tuliyoichukua kwa Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila, kwa kuangalia mambo mengine mawili muhimu kama ifuatavyo:

  (i) Kwa hatua tuliyofikia na taarifa tulizo nazo za dawa hii mpaka sasa, tumeandaa na tunakamilisha taratibu, ili tuweze kufuatilia maendeleo ya kiafya ya wagonjwa 200, ambao wamekubali kwa ridhaa yao wenyewe, kushiriki katika utafiti huu, ili kuona maendeleo yao kiafya, baada ya kunywa dawa ya Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila, kwa maradhi walionayo. Hatua hii, inafuata vigezo vyote vya Kitaifa na Kimataifa.

  (ii) Pia tumeweka utaratibu madhubuti, wa kufuatilia matumizi ya mti huu, kama “mmea tiba”, katika sehemu nyingine za nchi yetu, kwani tuna taarifa kuwa, makabila mbali mbali yamekuwa yakitumia mti huu kama tiba. Makabila hayo ni pamoja na; Wagogo, Wamasai, Wabarbaig na Wasonjo kule Samunge.

  Kwa niaba ya watafiti na wataalam wenzangu, ninaomba nimalize kwa kusema kwa muhtasari kuwa;:
  (i) Sisi sote tumeridhishwa kuwa, dawa anayotoa Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila, haina madhara yeyote yanayotambulika kwa sasa kwa matumizi ya binadamu. jambo hili mwazoni lilitia wasiwasi Serikali, Wataalam mbalimbali na wananchi kwa ujumla.
  (ii) Kazi hiyo ya utafiti inaendelea ili kubaini magonjwa inayotibu,
  (iii) Katika hatua hii, ninapenda kuwashukuru wataalamu wenzangu wote wa kikosi kazi cha wataalam wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Ofisi ya mkuu wa wilaya, Ngorongoro na ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha na wananchi wote kwa kufanikisha zoezi hili mpaka sasa.
  (iv) Pia sisi tunamshukuru sana Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila, kwa ushirikiano alioutoa, kwa timu ya watafiti waliofika kumuona, kuanzia siku ya kwanza mpaka leo hii..

  Mwisho ninachukua fursa hii, kuwaomba wananchi wawe na subira katika kipindi hiki ili watupe nafasi tuweze kufanya kazi hii ya utafiti na uchambuzi zaidi, kwa utulivu na umakini wa juu kwani duniani kote, tafiti za aina hii, hazina njia ya mkato, nasi tunaahidi kwamba, tutatoa taarifa ya kina mara utafiti utakapo kamilika.

  Asanteni na Ninawashukuru kwa kunisikiliza!

 48. TIBA YA UKIMWI YA MWASAPILE NAHISI HAIKUTOKA KWA MUNGU

  salam ndugu zangu katika jina la Yesu.

  Ikiwa watu wengi sana wamefungua vinywa kuzungumzia tiba ya magonjwa sugu yakiwemo UKIMWI, Kisukari nk. inayotolewa na mchungaji mwasapile huko Loliondo, nami leo nafungua kinywa kuzungumzia.

  mamilioni ya watu wakiwa wametibiwa na mchungaji huyo na kupata uponyaji,huku maelfu wakiamini kwamba mzee huyu kapewa dawa kutoka kwa Mungu.lakini mimi niko kinyume na mtazamo huo, sipingi kwamba ni dhambi kuwapa watu dawa wakanywa, hapana, yeye siye wa kwanza kufanya hivyo kwani hata bwana wetu Yesu alitengeneza matope akampaka kipofu usoni naye akapata kuona. hata Nabii Elisha watu walimwendea wakamwambia kwamba maji ya nchi hii ni machungu na kila anywaye maji haya huzaa mapooza! Ndipo Elisha akawaambia wamletee chomba kipya na chunvi kisha akaimwagia katika chanzo cha yale maji yakaponywa hata leo.

  kinachonifanya mimi nipinge huduma ya mzee huyo kwamba haijatoka kwa Mungu ni pale wachawi wanapopata nafasi ya kwenda kumchezea katika eneo lake la Huduma,kwa mujibu wa gazeti la Risasi la tarehe 16-18 march 2011, liliripoti kwamba kuna watu wanaonekana katika eneo la huduma ya mzee huyo kisha ghafla wanapotea, na watu walimuuliza mmoja wa wasaidizi wa mchungaji akasema hao ni wachawi.

  ikiwa kweli mwasapile ametumwa na Mungu wachawi wanapata wapi nafasi ya kumchezea vile, tunaona mifano mingi tu kwenye biblia Paulo alikutana na mtu mmoja mchawi akamlaani yule mchawi kwa muda huo huo aliharibikiwa, Musa naye alikutana na wachawi wa Farao wakatupa fimbo zao zikawa nyoka lakini nyoka wa Musa aliwameza wale nyoka wa wachawi wote.

  lakini ikumbukwe kwamba Biblia inasema siku za mwisho atainuka myama mwenye jeraha la mauti naye akapona jeraha la mauti watu watamstaajabu kumuona mnyama huyo kapona jeraha la mauti na watu wengi wakamwendea kwa sababu amepona jeraha la mauti. (ndugu yangu tafakari andiko hili.)

  Pia nawaomba ndugu zangu msiiamini kila roho bali ichunguzeni mjue kama imetokana na Mungu.

  mbarikiwe wote:

  Ev:moses mayila

 49. How to Discern if a Word is From the Lord

  This article will serve as a good followup to an an article we just released titled, “How to be Led by the Holy Spirit.” In that article, we gave you 9 basic ways in which the Lord will use to supernaturally communicate to us in this life.

  In this new article, I want to take you one step further and show you how to properly test any type of supernatural communication you may receive so you know for sure the word you are receiving is really coming from the Lord and not from your own imagination or from a demon. Many Christians
  do not properly test any type of supernatural communication they receive and as a result, they sometimes get duped by a demon who is trying to masquerade as the Lord with the message he is giving to them.

  Below I will give you 8 very basic tests that you can use to test any type of supernatural communication you think you are receiving. The word “test” means to carefully analyze, scrutinize – to prove and to try.

  Remember, if you are receiving any words or messages, it is either coming from one of three sources:

  1.From the Lord

  2.Your own mind and imagination, as the OT has told us how some prophets would prophesy out of their imagination

  3.Or it could be coming from a demonic spirit who is trying to knock you off course
  As we have said in our first article on how to be led by the Holy Spirit, do not be afraid if sometimes you miss this, as all of this is a learning process with the Lord. You will learn how to hear from God through a process of trial and error with Him. And just because demons can try and mess with us at times does not mean you want to totally shut God down with the different ways He will use to supernaturally communicate to us in this life.

  God was constantly communicating to His people back in both the OT and NT and He still wants to do it in this day and age since He is the same today as He was yesterday. We just have to learn how to do this with Him.

  Now I will break down these 8 different ways on how to test a word from the Lord so you will know for sure that the word you are receiving is really coming directly from Him and not from your own imagination or a demon.

  How To Test Any Type of Supernatural Communication You May Receive
  Before I get into the 8 different ways in which you can test any type of supernatural, divine communication you think you may be receiving, here are a few good verses from the Bible showing us that we have to test these kinds of supernatural things out when we do receive them.

  1.“Test all things; hold fast what is good.” (1 Thessalonians 5:21)

  2.“For Satan himself transforms himself into an ANGEL OF LIGHT. Therefore it is no great thing if his ministers also transform themselves into ministers of righteousness, whose end will be according to their works.” (2 Corinthians 11:14)

  3.“Beloved, do not believe every spirit, BUT TEST THE SPIRITS, whether they are of God; because many false prophets have gone out into the world. By this you know the Spirit of God: Every spirit that confesses that Jesus Christ has come in the flesh is of God, and every spirit that does not confess that Jesus Christ has come in the flesh is not of God. And this is the spirit of the antichrist, which you have heard was coming, and is now already in the world.” (1 John 4:1-4)
  The first verse hits the nail right on the head when it tells us to test all things. And all things means any kind of supernatural communication you think you are receiving, including those that are coming direct from the Lord. God will not be offended if you attempt to test what He is trying to tell you. He will want you to test it, otherwise He would have never put the above verses in His Word. Too many Christians have been seriously hurt over the years because they have never stopped to test the words they were receiving.

  Now here are some good, basic, common sense tests you can use to properly test any type of supernatural communication you think you may be receiving.

  1. Does the Word Line Up With Scripture?
  This is without a doubt the first test you must use to make sure that what you are receiving is truly coming from the Lord. If the word or message does not pass this first test, then you have to immediately throw it out, as it is no longer trustworthy.

  This first test is that the word and message that you are are receiving has to line up with the Word of God – the Bible. God will never go against His own Word. And if the message you are receiving is not lining up with Scripture or is blatantly going against Scripture, you have to immediately discard it – no questions asked!

  Here are some examples on where you can receive a false word that will not be lining up with Scripture:

  1. If you are dating a girl and all of a sudden you think you are receiving a word from the Lord that it would be alright for you to start having sex with her, that word will not be from the Lord. That would be the sin of fornication and that sin is specifically mentioned in the Bible numerous times. Thus the word you are receiving cannot be trusted as being a pure, true word from the Lord, as God would never go against one of His own basic commands in the Bible.

  Demons love to try and get people off track by committing these types of sins, so do not fall for it if you think that type of word is coming in on you. Immediately rebuke the demon and tell him to leave you in the name of Jesus if you ever feel that kind of false word is coming in on you.

  2. If you are married
  and you are starting to have some troubles in your marriage, and then all of a sudden you feel like you have received a word that it would be alright to start having an affair with someone else because you are no longer happy and fulfilled in your marriage – again, do not fall for for it. This would be adultery, and the Bible has the sin of adultery listed as one of the 10 commandments. Again, God would never, ever tell you to commit this sin, as this would be going against His own Word on this topic.

  Believe it or not, we have heard from numerous Christians over the years who felt they were receiving this kind of word and release from the Lord due to the bad state of their marriage. In each case, we told these people that God would in no way authorize this kind of sinful behavior and that they could not act on it, as this word was not coming in from the Lord. This word was either coming in from their own imagination and their own desires, since they were no longer happy in their marriages, or it was coming in from a demon.

  3. Another very interesting area where this test will come into play is when a Christian is dating an unbeliever. They then all of a sudden think they have received a release and a word from the Lord to marry this person, even though their partner still has not been saved and still has not shown any interests to get saved.

  Again, the Bible tells us not to be yoked together with unbelievers and if you marry this unbeliever, you are definitely going to be yoked together with them, thus violating this basic command from the Bible. Unless God is making a strong move to get your dating partner saved, I would never commit to marrying this person, as the Bible is very clear on this command. Once again, here is this verse if you were not aware that it was in the Bible:

  “Do not be unequally yoked together with unbelievers. For what fellowship has righteousness with lawlessness? And what communion has light with darkness? And what accord has Christ with Belial? Or what part has a believer with an unbeliever? And what agreement has the temple of God with idols? For you are the temple of the living God.” (2 Corinthians 6:14)

  I had a friend from work who married an unbeliever and within one year, the entire marriage blew up and she was divorced several months later. There was no anointing on this marriage because God never authorized it in the first place because she was violating this basic verse from Scripture on not being yoked together with an unbeliever.

  I could go on and on with more examples, but the point to get is to make sure the word you are receiving is lining up with the Bible. If you are a bit weak in the Bible, then talk to your pastor or to another Christian who does know their Bible and then run the word by them. They should be able to tell you if the word is lining up with Scripture or not.

  2. Does the Word Line Up With the Character of God?
  Another basic test that you have to use is to make sure the word you are receiving is lining up with the character and personality of God Himself. In other words, is this something that God would really ask you to do or tell you to do? Is this one of His ways?

  The closer you get to God in your own personal relationship with Him, and the more time you spend reading the Bible, the better you will get to know God. And the better you get to know God, the better you will be able to see and discern if a word is lining up with His character and personality.

  Many Christians get burned in this area because they are not walking close to God nor have they spent much time in the Bible. As a result, they really do not know God and they thus are easier pickings for demons to give them false words of guidance.

  Again, if you think you are receiving a word, but you may not be really close to God, ask several other Christians who do have close walks with the Lord and who do know their Bible and their God. They should be able to help you with the word you think you are receiving.

  Where this particular test will come in is when you receive a word, but there is really nothing in Scripture on it. If there is nothing in the Bible on it, then you will really need to apply this test to it to see if the word is lining up with the character and personality of God Himself.

  3. Does the Word Line Up With What God is Doing With Your Life?
  Sometimes the word you may receive has to be analyzed to see if it will fit into what God has already been doing with your life. The Bible tells us that God is one One who will build the “house” of our lives. As a result, any word that you receive that has to do with your big picture with the Lord has to be carefully analyzed and see if it fits into what God has already been doing with your life.

  If God is calling you to be an attorney and He is building you up in that area so you can enter into that calling when the time is right, God is not going to be throwing you a curve ball and all of a sudden ask you to go off into the far reaches of Africa to do missionary work for the next 20 years of your life.

  If God is going to put a call on your life, then He is going to carefully build you up in that call so you can enter into it when the time is right. Demons love to try and knock you off course by trying to give you a false word to try something else different so they can knock you out of your call with the Lord.

  There have been documented cases of Christians thinking they have received a word from the Lord to go off and be missionaries. Without seeking or getting any type of confirmation that this word was really from the Lord, they immediately pack up their bags and leave for the missionary fields. And then a year later, they are flat broke, all beat up, and they then return back home with absolutely no success on the missionary fields.

  The reason they were not successful was because God never called them to do this in the first place. And since God never called them to do this, there was no anointing on their efforts. And with there being no anointing to do this, they had no basic protection, provision, favor, money or supplies coming to them when they were needing it.

  In other words, there was no divine support for them because they were out of the will of God and they were either following their own imaginations and desires, or they got played and duped by a demon. That is why you have to carefully analyze and test any type of divine communication you think you are receiving – to make sure that it really is the Lord talking to you and not your own imagination and desires, or possibly a demon.

  Again, if you are receiving a word from the Lord that has to do with what He is calling you to do in this life, make sure that you carefully analyze this word to see if it fits into what He has already been doing with your life and with what He has already built up in your life.

  4. Does Your Spirit Bear Witness With the Word?
  As we explained to you in our article, “How to be Led by the Holy Spirit,” the number one way the Holy Spirit will communicate to you in this life is through the inner witness – the inner knowing. If you are receiving a true word from the Lord, the Holy Spirit should be bearing witness with that word out of your own human spirit.

  So the next test will be – does your own spirit bear good witness with the word, since the Holy Spirit lives in your human spirit and that is where He will be bearing witness at.

  If you are not getting a good witness from the Holy Spirit, or the witness feels really flat and dull, then stop and ask God the Father for confirmation to make sure this word is really coming from Him. Not getting a good witness from the Holy Spirit is always a major red flag, since the Holy Spirit is always in perfect unity and harmony with both God the Father and Jesus Christ.

  5. There is Safety in the Multitude of Counselors
  Another test you can use is to run the word by a few other seasoned Christians who really know their Bible and their God. The Bible tells us that there is safety in the multitude of counselors. Sometimes another seasoned Christian will be able to see something with the word that you are not seeing.

  Here are several good verses from the Bible telling us that we can do this with the Lord:

  1.“Where there is no counsel, the people fall; but in the multitude of counselors there is safety.” (Proverbs 11:14)

  2.“A wise man is strong, yes, a man of knowledge increases strength; for by wise counsel you will wage your own war, and in a multitude of counselors there is safety.” (Proverbs 24:5)

  3.“Every purpose is established by counsel; by wise counsel wage war.” (Proverbs 20:18)

  4.“Without counsel, plans go awry, but in the multitude of counselors they are established.” (Proverbs 15:22)

  5.“Listen to counsel and receive instruction, that you may be wise in your latter days.” (Proverbs 19:20)

  6.“Cease listening to instruction, my son, and you will stray from the words of knowledge.” (Proverbs 19:27)
  As you can see from the way these verses are being worded, God does want you to consult with other wise and seasoned Christians from time to time depending on exactly what it is that you are dealing with. And sometimes when you think you are receiving a word from the Lord, you may need to run this word by a few of these wise and seasoned Christians so you can make sure that you are reading the word correctly and that the word is really coming in from the Lord and not from a demon or your own mind and imagination.

  So if need be, do not be afraid to run your word by a few other wise Christians if you are not 100% sure the word is from the Lord. Sometimes a fresh pair of eyes are needed to see what the real truth is and whether or not the word is truly coming from the Lord. That is why the Lord has given us the above verses, to let us know that sometimes we will need help from other Christians due to our own imperfections and possible shortsightedness.

  6. Ask God to Confirm the Word For You
  Another big thing you can do if you are not quite sure the word is from the Lord is to just go back to God in prayer and ask Him to confirm His word for you.

  This is one area that gets many Christians into major trouble. They receive a quick word, but instead of properly testing it and/or asking God to help confirm the word for them, they immediately take off running with the word. And if that word was not from the Lord, they then end up taking a major wrong turn in their life and serious damage can be done as a result.

  Marrying the wrong person because you did not wait for more confirmation from God, or taking the wrong job at the wrong time could all lead to disastrous results. The bigger and more serious the word is, the more you have to properly test it and get God’s confirmation to make sure that it really is Him talking to you.

  Many Christians have ended up marrying the wrong people in this life because they did not wait for God’s confirmation to the original word. Again, demons love nothing more than to try and knock you off course by trying to get you to marry the wrong person or take the wrong jobs in this life. This is why you should never be afraid to ask God to confirm His own word for you.

  The way God can confirm His own word for you can be done in many different ways. The Bible says that out of the mouth of two or three witnesses every word will be established. What people have found out is that sometimes God will cause two or three witnesses to come up to you in close proximity and basically tell you the same thing that God told you in the original word. These two or three witnesses could be total strangers or people you already know, but in either case, they will know nothing about the original word that was given to you by the Lord.

  Another way God could confirm the word for you is through the gift of prophesy. All of sudden you will have someone prophesying over you telling you basically the same thing you were told with the original word. Many times prophecy is used by God to help confirm what was already given to you by Him. And the person prophesying over you will have no prior knowledge of the original word given to you by the Lord.

  When you get a person prophesying over you, or two or three witnesses coming up to you who have no prior knowledge of what God had told you – and they then tell you basically the same thing that God had originally told you – this will be so supernatural, that is how you will know that it really was God talking to you and not your own imagination or a demon.

  God can also use dreams, visions, or possibly a very strong witness from the Holy Spirit Himself to help confirm for you that the word was really from Him. Again, just ask God to confirm the word for you if you are not sure, and then watch and wait for that confirmation to come to you if the word was truly from the Lord. You will know the confirmation when it does come to you from the Lord. You will not be able to miss it, because many of these confirmations will be so supernatural and “so in your face.”

  7. Will the Word Glorify God?
  Another test you will want to use is to make sure any words, messages or guidance you are receiving from the Lord will always bring Him all of the glory. Always remember – we work, live and die for the Lord. We work for Him in this life, not for ourselves or for our own glory.

  Many secular men and woman in this world only work for their own self-interests and their own glory in this life. It is all about them, and anything they achieve and accomplish in this life is all for their own ego. They work for themselves, they do not work for God. As Christians, we always have to remember that these divine calls and assignments are all coming from the Lord, they are not coming from us or the world in general.

  As a result, we always have to remember that we work for the Lord in this life, not for ourselves, our parents, our friends, or the world in general. That is why you always have to make sure that anything you do in this life will always bring all of the glory to the Lord.

  Demons are all about their own glory and their own self-exaltation, as that is what got Satan thrown out of heaven. As a result, they will try to get people to think it is all about them rather than the Lord. Satan fell as a result of this kind of prideful, evil and wrong thinking, and he still wants to try and bring down as many people as he can through this same type of prideful and evil thinking.

  The devil’s tactics are always the same. Inflate the ego, get major pride worked into someone’s personality, and then it won’t be long until that person takes his eyes off of God and then places it all on his own self. And from there, it will only be a matter of time before they fall and lose it all, as the Bible tells us that pride and a haughty spirit will come before the fall.

  Here are 5 very good verses showing us that all of the glory always belongs to the Lord, not to us:

  1.“I am the Lord, that is My name; and My glory I will not give to another, nor My praise to graven images.” (Isaiah 42:8)

  2.“Therefore let no one glory in men. For all things all yours …” (1 Corinthians 3:21)

  3.“Therefore, whether you eat or drink, or whatever you do, do all to the glory of God.” (1 Corinthians 10:31)

  4.” … that no flesh should glory in His presence.” (1 Corinthians 1:29)

  5.“So on a set day Herod, arrayed in royal apparel, sat on his throne and gave an oration to them. And the people kept shouting, “The voice of a god and not of a man!” Then immediately an angel of the Lord struck him, because he did not give glory to God. And he was eaten by worms and died.” ( Acts 12:22-23)
  The very last verse is rather bone-chilling, as an angel of the Lord literally struck a man dead as a result of him trying to steal the glory that only belongs to the Lord.

  By always remembering to make sure that all of your activities for God always bring Him all of the glory, this will really help you in making sure that you never take your eyes and attention off of the Lord and then start to place too much of it on your own self.

  8. Will the Word Produce Liberty or Bondage?
  The last test you will want to use on any type of word you think you are receiving is to make sure the word will lead to liberty and not to any type of bondage and fear. The Bible says that where the Spirit of the Lord is at, there is liberty. Here is this most important verse, along with two others that will show you that the Lord is all about liberty and freedom – not fear, intimidation and bondage.

  1.“Now the Lord is the Spirit; and where the Spirit of the Lord is, there is liberty.” (2 Corinthians 3:17)

  2.“For you did not receive the spirit of bondage again to fear, but you received the Spirit of adoption by whom we cry out, “Abba, Father!” (Romans 8:15)

  3.“The Spirit of the Lord is upon Me, because the Lord has anointed Me … to proclaim liberty to the captives and the opening of the prison to those who are bound …” (Isaiah 61:1)
  If you are a Christian woman dating a Christian man, and this man has been severely verbally abusing you during most of your dating life, and then all of a sudden you think you are receiving a word from the Lord to marry this man, this word will have major red flags all over it.

  If you are in a verbally abusive relationship, you are in a certain amount of bondage. And if you marry this man, you will go into even more bondage as you will now have to put up with that verbal abuse 24/7 as compared to what you had to put up with in the dating relationship.

  Unless God is making a strong move to get your partner cleaned up, I would not commit to marrying this kind of man, as many of the times the abuse will only get worse once you marry him. Too many women marry abusive men thinking or hoping they will change once they get married. But most of the time they never do unless God Himself makes a strong move to convict them and get them cleaned up.

  Again, demons would love nothing more than to try and get you to marry into an abusive relationship so they can use this abusive person to try and control you and completely destroy your life. That is why you have to make sure that any words you are receiving from the Lord will lead to liberty and freedom, not to any type of bondage, fear or slavery.

  Conclusion
  If you use the above 8 tests to test any type of divine communication you think you are receiving, they should for the most part be able to tell you what is truly coming from the Lord and what may be coming from your own natural desires and imagination, or from a demonic spirit.

  Again, it is extremely important that you test all supernatural communication you think you are receiving, as believing and acting on a false word could either destroy your life, or cause major delays to occur with what God is doing with your life.

  If demons cannot kill you, they will either try and paralyze you or knock you off the path that God has set up for your life. That is why all supernatural communication has to be tested – to make sure that it really is coming in from the Lord and not from your own imagination or from a demon.

  Many Christians have been seriously burned and hurt because they did not properly test a word that was coming to them. They have either married the wrong people, took the wrong jobs, or hung out with the wrong people.

  As a result, they either lost their calls and their divine destinies with the Lord, or they lost valuable years in that call due to having to deal with the consequences and repercussions of making those wrong turns in the roadway. And this was all because they jumped the gun too quickly and did not properly test the word they were receiving – especially words of actual guidance like who they should be marrying and what jobs they should be taking in this life.

  We do not want to scare anyone away from learning how to hear from God and how to be led by Him in this life. Every Christian can learn how to do this, but you always have to remember that we still live in a fallen, cursed, and imperfect world with demons still being allowed to roam in the air.

  As a result, we have to always filter any type of supernatural communication we think we are receiving through some of the above tests so we can make sure that we are on safe ground and that the word we have received has truly come to us from the Lord. This topic is taken from Bible Knowledge.com

 50. Bwana Yesu Asifiwe wana wa Mungu! WATUMISHI wa Mungu walio wengi kwa sasa wameshindwa kutumika ipasavyo! wanapoanza huduma ni wanyenyekevu mno!!! lakini wakipata hela kidogo tu, utawaona wanaanza kutoa matangazo ya ajabu ajabu kama ya waganga wa kienyeji! na wengine wameenda sana siku hizi mpaka kwenye hizi redio zetu za kikristo wanatangaza utadhani ni wafanyabiashara fulani hivi. Utamkuta mtumishi akitoa pepo siku moja tu utamuona anatangaza “njoo ufunguliwe” badala ya kuwafungua watu wanawafunga. sasa mawazo yangu juu ya watumishi hawa ni kwamba; NI WATUMISHI wa uongo! wanahitaji KUTUBU ili wawe watumshi wa UKWELI

 51. Watumishi kama hawa hawafai kwani biblia haisemi hivyo ni vyema kama kweli wanataka kumtangazaYesu wasome maandiko. imeandikwa mmepewa bure, toeni bure.kwanini wanauza jina la Yesu?
  mfano:
  kuna mmoja wa huku kwetu alinunua maji ya chupa akayaombea kisha akaanza kuwauzia watu kwenye mkutano chupa
  sh.20,000/=ikaendelea kupigiwa mnada mpaka ikafika sh.2000/= kwa hiyo waliokuwa na pesa siku hiyo ndio waliopona magonjwa maana waliamini kuwa wakinywa maji hayo watapona. nauliza? ambao hawakuwa na pesa inakuwaje maana walirudi na magonjwa yao na vilio vyao. sasa maombi yanauzwa siku hizi? jamani watumishi tuangalie watu wataenda mbinguni sisi tuishie jehanamu. usihubiri kwa kuwa umekosa kazi ya kufanya hubiri kwa kuwa mungu amekuita. huo ni wizi mtupu.

 52. Watu wakitangaza kuwa wana Mungu wa Hivyo upo uwezekano huyo Mungu ndiyo tangazo hilo. Mimi nasema: KAMA MUNGU ANAKUTUMIA HIVYO, USIJAZE WATU UWANJA WA TAIFA ILI TUJUE; WEWE KAFANYE HOSPITALI ZIWE TUPU BILA WAGONJWA TUTAJUA TUU…!

 53. Mpendwa Joyce na yeyote mwenye hitaji hili;

  Ukitaka ku-post swali lako unaweza kututumia kwa email: strictlygospel@yahoo.co.uk au kuandika tu kwenye MASWALI/MAJIBU na kama tutaona linafaa tutaliweka kama post.

  Endelea kutembelea blog hii!

 54. TUSIHUKUMU,NASI TUSIJE TUKAHUKUMIWA.hilo ndo nalo weza kusema,tafadhali naomba unielekeze iwapo nataka kupost swali langu hapa ili niweze kusaidiwa kwa maoni nafanyaje,,endeleeni na moyo wenu,Mungu atawabariki,kwani mnakuza imani yangu na wengine wengi.

 55. Kwanza nikushukuru mtumishi wa Mungu kwa ufafanuzi mzuri juu ya mambo yanayotendeka kwenye makanisa siku hizi.

  Kitu kinachonishangaza siku hizi ni wachungaji kutofundisha utakatifu na kweli. Kitu wanachokisisitizia ni baraka pamoja na miujiza. Wakati neno la Mungu linasema hiyo kweli tukiijua itatuweka huru. Kweli inatuweka huru na mambo mengi yakiwemo magonjwa.

 56. Haya ni matangazo kama matangazo ya waganga wa kienyeji tu, kwa sababu sioni mantiki ya kutangaza kwamba Yesu anaponya baadhi ya magonjwa au anaondoa baadhi ya shida na zingine anaondoa nani? Unajua hizi ni nyakati za mwisho, Neno la Mungu alilishatuonya kwamba wengi watasema Yesu yuko huku na wengine watasema yuko kule, Neno la Mungu likasisitiza msiende huko na aliyeko darini asishuke maana sasa ni vita vya kugombea waumini ili kujipatia mahitaji/malengo ya mwilini zaidi kuliko ya rohoni. Ndio maana utakuta matangazo hayo yameangalia zaidi mambo ya mwili ambayo wana hakika mtu yeyote atakayeona atakimbilia kwenda huko kwani shetani naye alivyo mjanja kwa kuwa anajua hiki ni kizazi kinachohitaji ishara naye amewaletea wanadamu magonjwa ya kila namna ili watu wavutike na ishara wasahau habari za maisha ya utakatifu ambayo kama wangekuwa nayo hata hayo magonjwa yasingewapata, kwani maneno ya Mungu yanatudhihirishia kwamba hatatupiga tena kwa magonjwa yote ya Misri. Na tumeingia katika kifungo kigumu sana cha ishara maana mtumishi yeyote ili aonekane ametoa huduma sawasawa ni lazima awe amesababisha muujiza angalau mmoja kutendeka vinginevyo kama mkutano au semina hiyo ikiendelea kesho yake idadi ya wahudhuriaji itapungua. Wengi hawapo katika semina au mikutano ya Injili kujifunza Neno la Mungu, kuutafuta uso wa Mungu bali kutafuta miujiza, na kwa sababu ya miujiza wakati mwingine ninaogopa kusema watumishi wengine wameingia katika majaribu ya kuigiza huduma za watumishi wengine wakidhani upako uko katika namna ya mtu anavyotoa huduma, au wengine wameingia katika mtego hata wa kutumia manguvu ya giza ili tu muujiza utokee. Hii ni hatari watu wa Mungu!!!!!!!!!

  Mimi sipingi miujiza, ishara na maajabu yanayotokwa kwa Bwana, ninalopinga ni kuyafanya kuwa msingi wa kuutafuta uso wa Mungu. Najua wataalamu wa Biblia watanijia juu kwamba hata Yesu alifanya muujiza ndio akakubalika na Wayahudi kuwaambia Habari Njema, ni sawa, lakini kwa nini alifanya hivyo? Kwa sababu ya shingo zao ngumu kumkubali. Je na sisi ndio maana yake?

  Suala la watumishi kufanya biashara madhabahuni ili wawaombee watu, huu ni upofu wa wasiolifahamu Neno la Mungu. Yer 17:5 inasemaje? “Amelaaniwa mwanadamu amtegemeaye mwanadamu, amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake na moyoni amemwacha Bwana”. Anayetakiwa kupewa shukurani ni Mungu mwenyewe. Neno la Mungu linasema uponyaji ni chakula cha watoto, utawauziaje watoto chakula? Sio kwamba sielewi suala la fungu la kumi, dhabihu na matoleo ya shukurani, hapana! Ninalolikataa ni maombi yanayotolewa kwa viwango vya fedha. Je Mungu naye anagawa upako kulingana na viwango vya fadha? Kama ingekuwa hivyo si matajiri tu ambao wangefika mbinguni? Hawa wanachezea madhabahu na madhabahu hizi siku moja zitajibu!!!

  Sisi kama waakristo tunatakiwa tusimame katika kulijua Neno la Mungu ndio tutaweza kuchambua pumba na mchele. Kwani sasa hivi kuna watu ukipinga kidogo juu ya miujiza utashambuliwa kama nyuki na ndivyo hata wengi watapinga ukweli ya maono yangu haya. Tuache ulimbukeni wa kiroho, tutulie katika Neno la Mungu, Mungu atatufungua macho ya rohoni na tutayaona yote yanayotendeka kama ni ya nuruni au ya gizani na Mungu atakusaidia kuona ni wapi utapata msaada wa kweli wa matatizo yako lakini pa kuanzia ni wewe mwenyewe na Yesu wako. Mungu akubariki.

 57. WATU KAMA HAWA WANA TAMAA NAHAWAJAITWA MA MUNGU MAANA WATUNAMIA NENO LA MUNGU KUWADANGANYA WATU KWA SABABU WAKRISTO TULIO WENGI NI WAVIVU WA KUSOMA NENO LA MUNGU. MUNGU ALITUAGIZA TUFANYE KAZI NA TUKIFANYA KAZI TUTAKULA MEMA YA NCHI TUKIWA NA YESU, NA NENO LA MUNGU LINASEMA MMEPEWA BURE TOENI BURE.

  “AMEN”

 58. Shalom kwa kweli matangazo yanachanganya, yanainamia upande mmoja tu hasa kwa habari ya kubarikiwa, ufike wakati tuzungumzie
  utakatifu, kwa mahana vyote vinapita.
  BWANA atusaidie na wimbi ili.

 59. Bwana yesu asifiwe mimi nashangaa sana watumishi wengi wana sahau kuwalisha waamini neno, wana watangazia waamini kutoa sadaka kubwa.ndio sadaka ni muhimu lakini kikubwa zaidi ni je imepandwa mbegu kwenye mioyo ya waamini? maana watu kujawa na neno ni muhimu sana.maana neno huleta imani.wachungaji msitumie sadaka kwa manufaa yenu wenyewe, iwe ni kwa kuieneza injili ya Yesu.
  Mungu awabariki sana.

 60. JINSI WACHAWI WANAVYOWEZA KUKUFUNGA USIFANIKIWE KATIKA MAISHA YAKO

  Salam wapendwa katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo.

  Leo nipo hapa kuwaletea topic mpya kabisa ambayo wachungaji wengi hawaifundishi makanisani na yamkini baadhi yao hawaijui.kama kichawa cha habari kinavyosema, leo nataka kuzungumza juu ya wachawi.kunawatu wengi sana Duniani wanalia kila wanavyojaribu kuyakwamua maisha yao inashindikana, lakini hawajui ni kwa nini? nataka nikuambie leo, wapo watu ambao Mungu ameamua kuwanyima mali kwa makusudi anayoyajua yeye mwenyewe, na kuna watu ambao Mungu hakuwanyima mali mpango wa mungu ni kwamba watu hawa wapate mali lakini hawana! hapa ni kwamba shetani huamua kuwaonea na kuwadhulumu watu hawa. unajua kila mmoja wetu anakitu alichopewa na Mungu ili kuweza kuzikamilisha shughuli za ulimwengu huu. ngoja nikupe siri moja kuu sana, kila mwanadamu anapozaliwa huwa anakitu kinachoitwa nyota, kitu hiki ni ishara au ni kitambulisho cha mtu huyo katika ulimwengu wa roho ya kuwa yeye kapewa nini hapa duniani,soma mathayo 2:1-5.biblia inasema ‘Yesu alipozaliwa zamani za mfalme herode mamajusi wa mashariki walikwenda kumwona, na walipofika wakauliza yuko wapi aliyezaliwa mfalme maana tuliiona nyita yake nasi tumekuja kumsujudia. Ukisikia mamajusi ujue si watu wema.kasome biblia ya kiingereza imesema ‘Astroggers’ yaani wabashiri au wanaanga. pia biblia ya NIV imesema Maggi, yaani washirikina, biblia nyinge imesema the Meggicians yaani wachawi.kwa tafsri hizi moja kwamoja tunatambua kwamba hawa mamajusi kuwa ni wachawi. Sasa rejea katika kauli yao walipofika kwa Yesu walisema “Yuko wapi waliyezaliwa mfalme maana tuliiona nyota yake nasi tumekuja kumsujudia” mpendwa wangu sasa naomba ufungue akili yako ili Mungu akusaidie. watu hawa ni wachawi, lakini cha ajabu wanasema wameiona nyota ya Yesu wakajua ya kuwa aliyezaliwa ni mfalme. kwa hiyo tunajifunza kwamba kumbe wachawi wanauwezo wa kutazama katika ulimwengu wa roho na kutambua kwamba wewe unanyota gani katika maisha yako. si kwamba walikosea kwa yesu kusema kwamba Yesu ni mfalme< walisema kweli kabisa rejea kauli za Bwana wetu alipokuwa kwa pilato aliulizwa wewe ndiye mfalme wa wayahudi hakukataa bali alijibu wewe wasema.pia akaongeza kusema kwamba ufalme wangu si dunia hii. kwa hiyo ni mfalme. pia ukirejea katika Isaya 9:6 biblia inasema "na uweza wakifalme utakuwa mabegani mwake" Hivyo basi wachawi wakishatazama katikaulimwengu wa roho na kuona nyota yako kuwa ni ya kifalme kama ya Yesus au labda nyota yako ni Biashara, au Elimu, au Ajira,nak. wanachokifanya ni kwamba wanaiba ile nyota na kuiweka kwa mtu mwingine au wakaiacha tu.

  kuna dalili za kutambua nyota yako ni ipi hasa ni rahisi sana kutambua nyota ya mtoto mdogo. kwa mfano: mtoto akiwa na nyota ya uongozi,utambua hivi watafute wanapokuwa wanacheza watoto wengi kwa pamoja, kisha angalia vizuri kaa utulie usipige kelele kisha uangalie vizuri ni lazima atakuwepo mtot atakayewadhibiti wenzake na kuwalazimisha kufanya anavyotaka yeye na lazima watafanya, kwamfano anawezakusema nyamazeni na wote kweli wakanyamaza, au twendeni na wote kweli wakamfuata.

  Pia dalili za kutambua Nyota iliyoibiwa ni hizi, kwa mfano mtoto alikuwa anafanya vizuri kabisa darasani lakini sasa hivi anazidi kudidimia wala hapendi kusoma, ukiona hivyo ujue tayari wameshachukua wanjanja! pia kwa mtu mzima unaweza kukuta kwamba unaandaa mipango lakini haitimii mipango yako.unapanga mwaka huu lazima nitafungua Duka lakini utashangaa linazuka tatizo hutafungua hilo duka mpaka mwaka utaisha. au unaandaa mpango mzuri kabisa lakini utashangaa unamwona mwenzako tayari ameshaanzisha mpango uleule kama ulivyokuwa unapanga. au kama ni biashara utaona mwingine kaanzisha vilevile kama ulivyokuwa unafikilia hapo ujue Nyota yako inatumiwa na mwingine.
  unajua nyota hizi huambatana na mawazo yako. jinsi mawazo yako yalivyo ndivyo na nyota yako ilivyo hawezi mtu akaitumia nyota yako pasipo mawazo yako.utajikuta kwamba wakati mwingine unapoteza fahamu kama hujielewi vizuri vile. hapo ujue kuna kitu.

  SASA TUNAKWENDA KURUDISHA HIYO NYOTA YAKO KUTOKA KWA WACHAWI:
  sali sala hii kwa bidii:
  Baba katika Jina la Yesu kristo nimetambua kama kunawizi wa nyota uliyonipa katika maisha yangu sasa kwa Jina lako naiamuru Nyota yangu kokote iliko irudi.katika jina la Yesu ninakuja kinyume na kila nguvu za shetani nazikata kamba zashetani nilizofungwa katika jina la yesu.asante bwana kwa kurudisha nyota yangu.

  SASA SHIKA MKONO WAKO KATIKA SCREEN YAKO NIKUOMBEE:
  Baba katika Jina la Yesu asante Mungu kwa sababu wewe ni mkuu kuliko wote.kwa Jina lako Mungu ninaamuru Nyota iliyoibiwa ya mtoto huyu, mama huyu,kijana huyu, binti huyu irudi mara moja na taabu iwapate hao waliomwibia nyota yake mtu huyu katika jina la Yesu.

  na baada ya hapo ni lazima utajiona tofauti katika mawazo yako, umekuwa na mawazo tofauti hii ni ishara kwamba nyota yakko imerudi,kama hutaona hizo dalili hizi ni ishara kwamba nyota yako haijarudi tafadhali rudia tena sala hii usichoke mpka uzione dalili hizi.
  bwana akubariki.
  Ev.Moses mayila 0715961270
  mosesmayila@yahoo.com

 61. Katika ujenzi wa ufalme wa mbinguni hiki kitu ni hatari sana,kwa maana itafika wakati mtu kama hana pesa basi hatopata msaada wowote toka kwa watumishi.

 62. wasiliana na mimi kupata kitabu hiki bure.

  UTANGULIZI

  Kitabu hiki kimeandaliwa na Mwinjilisti Moses Mayila wa Sengerema Mwanza Tanzania, kwa msaada wa Mungu kupitia maandiko matakatifu (Biblia) na kuhaririwa nay eye mwenyewe. Kitabu hiki kimeandaliwa na kusambazwa bure kabisa bila kodi yoyote, na hii ni kutaka kulieneza neno la Mungu na kutoa Msaada zaidi hasa kwa watu wanaohitaji msaada wa maandiko, “Binafsi nimeona kuwa ni vizuri sana kama nikisambaza vitabu hivi bila kumtoza mtu yeyote yule ushuru au gharama yoyote ya uchapaji, pia ninaamini kuwa Mungu atanibariki zaidi na zaidi katika jambo hili, ni wahubiri wengi sana Duniani wanafanya jambo hili lakini wanalifanya kibiashara zaidi kwa kuwatoza watu gharama ya juu zaidi ya ile iliyotumika kuandaa kitabu kile, Mimi Moses watu hao ninawaita ni watu wafanyao kazi kwa hila wakijali mapato yao na si kazi yake aliye juu. Kupitia kitabu hiki ninaamini kuwa utapata msaada zaidi katika maisha yako ya kiroho na hata katika maisha yako ya kimwili pia. Naomba usome kwa makini sana aidha katika kitabu hiki nimejaribu kuyafafanua baadhi kya maandiko ya Biblia na kuyaeleza kwa mapana zaidi.

  SURA YA KWANZA

  MSAADA WA MUNGU KATIKA MAISHA YA MWANADAMU

  Biblia inasema katika kitabu cha Mathayo sura ya 11 mstari wa 28 hadi 31. Inasema kuwa “NJOONI KWANGU NINYI NYOTE MSUMBUKAO NA WENYE KUELEMEWA NA MIZIGO NAMI NITAWAPUMZISHA, JITIENI NIRA YANGU MKAJIFUNZE KWANGU MAANA MIMI NI MPOLE NA MNYENYEKEVU PIA WA MOYO NANYI MTAPATA RAHA NAFSINI MWENU. MAANA NIRA NIWAPAYO MIMI NI LAINI NA MZIGO WANGU NI MWEPESI”.

  Haya ni maneno ambayo Yesu aliyasema wakati akihutubia katika baadhi ya mikutano aliyowahi kuifanya. Lakini katika haya, swali lililopo mbele ni kwamba kwa nini Yesu aliyasema haya? Yesu aliyasema haya akimaanisha kuwa kila laiyendani yake yaani aliyemkubali Yesu kuwa Mwokozi wa maisha yake hataona tabu tena, ni kama vile Biblia inavyosema katika kitabu cha Nabii Isaya sura 65 kifungu cha 19 hadi 25 inasema hivi “nitaufurahia mji wangu Yerusalemu wala kilio na maombolezo havitasikika tena ndani yake, wala hapatakuwa na mzee asiye timiza siku zake tena, maana mtoto ataishi miaka mia bali mtenda dhambi akiishi miaka mia amelaaniwa, watajenga nyumba na kuishi ndani yake watapanda mizabibu na kuvuna mtunda yake, wala hawatajenga akaishi mtu mwingine tena kwenye nyumba hiyo wala hawatapanda akavuna mtu mwingine tena. Ni kama zilivyo nyingi siku za mti na watu wangu wataishi kama hivyo. Wateule wangu watafurahia kazi za mikono yao. Wala hawatazaa kwa uchungu watakuwa ni watu waliobarikiwa na Bwana.

  Hii inaonyesha vigezo vingi sana ambavyo Mungu huwapa wale wanaozishika amri zake. Hapo juu amesema kilio na maombolezo havitasikika mjini Yerusalemu. Hapa hana maana ya Yerusalemu pekee tu, bali ana maana ya watu wote wanaomcha yeye. Na aliposema kilio hakitasikika ndani yake ina maana kwamb atakomesha kila aina ya tabu, shida magonjwa, mateso na matatizo ya aina zote. Vile vile amesema hawatapanda akavuna mtu mwingine ana maana ya kwamba hawatajitaabisha bure maana shetani huharibu kile ambacho mwanadamu anakifanya ikiwa ni pamoja na mwanadamu mwenyewe. Biblia inasema mwivi kazi yake ni kuiba, kuchinja na kuharibu, ndipo Mungu akanena na Malaki akisema ‘NAMI NITAMKEMEA YEYE ALAYE MAZAO YAKO NA MIZABIBU YAKO HAITAPUKUTISHA MAJANI YAKE” hapa alikuwa na maana ya kwamba atamkemea shetani asiharibu kazi ya mikono yako, lakini hatamkemea kula matunda ya watenda dhambi bali ya wamchao yeye. Hii inamaanisha wazi kwamba Mungu humlinda amchaye, yeye na mali zake.

  Kwa sababu hii na ndiyo maana Yesu alisema njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kuelemewa na mizigo nami nitawapumzisha. Kuna sehemu kubwa sana katika jamii hasa katika nchi za Kiislamu hususan Iraq, Tajikistani, Iran na nyinginezo wanaamini kabisa kwamba Yesu alikuwa ni Nabii tu na wao wnamwita Nabii Issa. Lakini mimi Moses ninakataa hadharani usemi huo ni uongo na upotoshaji wa hali ya juu sana. Hizi mbinu tu za shetani kutaka kuutenda ulimwengu kwa maneno yanayoonekana kuwa na maana hali ni ya uongo, kila siku shetani katika kazi zake hutumia kitu inachoitwa hila, Hila ni nini? Hila ni mipango mibaya. Shetani antumia hizi hila kuuteka ulimwengu kwa maneno yasiyokuwa na ukweli wowote ndani yake ambayo kwa mtu asikye na upeo wa kutosha katika Biblia ni lazima atayaamini. Jamii hii inaamini kuwa Yesu alikuwa ni binadamu tu wa kawaida kabisa kama wewe na alizaliwa na mwanamke kama ilivyo kawaida kwa wanadamu wote. Lakini ukweli kamili ni kwamba, Yesu ni Mwana wa Mungu, na kwa habari ya kuzaliwa na mwanamke ni kwamba, Yesu alichukuliwa mimba kwa miujiza kwa uwezo wa Mungu aliye juu. Biblia inasema katika kitabu cha Mathayo sura ya 1 kifungu cha 18 inasema hivi “HIVI NDIVYO KUZALIWA KWA YESU KRISTO KULIVYOKUWA, MARIAMU ALIKUWA AMEPOSWA NA YUSUFU LAKINI KABLA (HAWAJAKARIBIANA) MARIAMU ALIONEKANA KUWA NA MIMBA AMBAYO ILIKUWA NI KWA UWEZO WA ROHO MTAKATIFU”. Biblia hiyo hiyo imeendelea kusema katika Yohana 3 kifungu cha 16 KWA MAANA MUNGU ALIUPENDA ULIMWENGU NA HATA AKAMTUMA MWANAYE WA PEKEE ILI KILA AMWAMINIYE ASIPOTEE BALI AWE NA UZIMA WA MILELE. Hii inaonyesha wazi kuwa Yesu ni Mwokozi wa Wanadamu. Pia kuna siku Yesu aliwachukua baadhi ya wanafunzi wake akaenda nao mlimani kusali, walipokuwa huko wingu zito likawafunika na sauti ilisikika kutoka kwa wingu hilo ikisema “HUYU NDIYE MWANANGU MPENDWA NILIYEPENDEZWA NAYE MSIKILIZENI ATAKAYOWAAMBIA” hii ilikuwa ni sauti ya Mungu MARKO 9 kifungu cha 7. Vile vile kuzaliwa kwake alitabiriwa na Nabii Isaya kwamba Bikra atachukua mimba na atamzaa mtoto wa kiume atakey wachunga mataifa kwa fimbo ya chuma ISAYA 7 kifungu cha 16-16. Katika historia nzima ya dunia hakuna record ya mwanamke bikra ambaye alishawahi kuzaa mbali na Mriamu kumzaa Yesu, (Bikra yaani Mwanamke ambaye hajawahi kufanya tendo la ndoa tangu kuzaliwa kwake) pia Isaya alizidi kumtabiri huyu Yesu akisema “Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa tumepewa mtoto tena wa kiume na uweza wa kifalme uko mabegani mwake (The Governmen of heaven) naye ataitwa mshauri wa ajabu Baba wa milele Mfalme wa amani jina lake. Maongeo ya enzi yake na amani haya mwisho kamwe. ISAYA 9 kifungu cha 6 – 7 inasemakana kwamba Isaya alimtabiri Yesu kabla ya miaka elfu moja (1,000) ya kuzaliwa kwake. Hivi vyote ni vielelezo vya kutosha kabisa vya kumtambulisha Yesu kuwa ni mwana wa Mungu na anauwezo wa kuratibu katika sector yoyote ile ya maisha yako. Nimeona kuwa kumbe kila wakati upatapo shida tatizo na mateso ya aina yoyote ile Yesu peke yake ndiye jibu. Na yeye ana mpango wa kukusaidia maadamu tu utakubali kufuata yale ambayo anataka uyafuate, wala hakuna kitu kisichowezekana kwake kila kitu kinawezekana LUKA 1kifungu cha 37. kwa maana moja, kila tatizo lako kwa Yesu lazima litatukuka tena kwa muda mfupi sana. Japo matatizo yamekukalia kwa muda mrefu sana siku ya leo naomba uamini kuwa yamefika mwisho, pamoja na kwamba umeombewa sana na watumishi wa Mungu mbali mbali leo utapokea muujiza wako.Hapatakuwa tena na kushindwa kufaulu kwako mwanafunzi, hapatakuwepo tena na utasa tumboni mwako mwanamke, hapatakuwa na ugomvi tena katika ndoa yako, maumivu yote ya ugonjwa wako yamefika mwisho leo, hautafukuzwa kazi tena na waliokufunza kwa muda mfupi kuanzia leo watakuletea barua ya kukutaka urejee kazini. Kila aina ya matatizo uliyo nay oleo yamefika mwisho.

  Nimefanya maombi mara nyingi sana na watu wenye matatizo mbali mbali lakini meomuona Yesu akiwapumzisha papo kwa papo, nimeombea wagonjwa wengi sana ambao hata siwezi kukumbuka idadi yao, nimetoa huduma kwa wenye mapepo waliosumbuliwa na majini ya ukoo kwa muda mrefu sana, pamoja na wenye matatizo mbali mbali, papo kwa papo Yesu aliwaponya. Na wewe naomba uamini kupitia hiki kitabu matatizo yako yote yamekwisha.

  MWISHO:

  Weka kitabu hiki kifuani kwako kwa muda wa dakika tano ukiwa umefumba macho na kasha fumbua macho yako, kasha kagua ugonjwa uliokuwa nao, na kuhakikishia kuwa hautauona tena.

  Baada ya hapo nenda zako ukiwa mzima ukasimulie ndugu, jamaa na rafiki zako mambo yote ambayo Mungu amekutendea.

  BWANA WANGU YESU KRISTO NAOMBA UYATIMIZE MAMBO HAYA KWA MTU HUYU SAWA SANA NA UWEZO WAKO. AMINA

  SURA YA PILI

  NYAKATI ZA MWISHO

  Inasemekana kuwa zamani Iraq ilikuwa ikiitwa Babeli,nchi hiyo ni miongoni mwa nchi maarufu sana duniani na ilishawahi kuitawala dunia nzima kisiasa na kiuchumi, nchi hiyo iliwahi kuongozwa na mtu mmoja jina lake Nebkadreza, ambaye alikuwa mfalme enzi hizo. Katika utawala wake yeye na jeshi lake waliondoka kwenda kuvamia huko Israel kipindi hicho Israel ilikuwa ikiongozwa na Mfalme Yeehoyakimu, katika vita hivyo mfalme Yehoyakimu alishindwa na watu wake wakachukuliwa mateka na mfalme Nebkadreza, miongoni mwa watu waliochukuliwa mateka alikuwemo kijana mmoja jina lake Daniel.

  Siku moja Mfalme Nebkadreza aliota ndoto ambayo ilimsononesha sana katika moyo wake, lakini ndoto hiyo aliisahau, mfalme akawaita wachawi, waganga, wanajimu na wafuga majini ili wamwambie na wamfasirie ndoto hiyo, wote walishindwa wakamjibu hakuna mtu ambaye anaweza kulijua jambo hili ambalo mfalme analiomba isipokuwa ni miungu isiyoishi na wanadamu. Kwa kauli hiyo mfalme alikasirika sana akaagiza waganga, wafuga majini, wanajimu na wachawi wote wauawe.

  Ndipo Daniel akamwomba mfalme asiwauwe hao watu, akamwambia yuko Mungu wa mbinguni ambaye atamwambia na kufasiria ndoto yake. Ndipo mfalme akamuuliza Daniel “Je unaweza kuniambia ndoto hiyo na ukaifasiri? Daniel akamjibu “Hakuna mwenye hekima, mchawi, wala mnajimu ambaye anaweza kuieleza siri ambayo mfalme anaiomba. Lakini yupo Mungu wa Mbinguni afunuaye siri, aliyemuonyesha mfalme Nebkadreza yale ambayo yatatokea siku zijazo.

  Ndoto yako ee mfalme ilikuwa hivi: uliona ee mfalme mbele yako sanamu kubwa imesimama, sanamu hiyo ilikuwa ni ya kutisha sana. Kichwa cha sanamu hiyo kilikuwa kimetengenezwa kwa dhahabu safi, kifua chake kilikuwa ni silver, kiuno chake na mapaja ni shaba, miguu yake ni chuma mchanganyiko na udongo. Wakati ulipokuwa unaendelea kuona haya likatokea jiwe kubwa ambalo halijatengenezwa kwa mikono ya wanadamu likaiponda miguu ya ile sanamu na kuisagasaga, ndipo chuma, udongo, dhahabu, na silver likazivunja vipande vipande kwa wakati ule ule na zikawa kama mapepe, upepo ukazipeperusha kwenda mbali. Lakini lile jiwe lililoiponda ile sanamu likakua na kuwa mlima mkubwa mpaka likaijaza dunia nzima”.

  Daniel akasema Hii ndiyo ndoto yako ee mfalme ngoja nikufasirie, Mungu wa mbinguni amekupa uwezo, nguvu na mamlaka, na amewaweka watu, wanyama wa porini na ndege wa angani mikononi mwako wewe mfalme, popote wanapishi Mungu amekupa kuwa mtawala juu yao wote. Wewe ni kile kichwa cha dhahabu baada yako ufalme mwingine tena utainuka, baada ya huo, ufalme mwingine tena utainuka (shaba) utatawala juu ya Dunia yote, mwisho kutakuwa na tawala nne, ufalme wa chuma utakuwa na nguvu kuliko zingine hivyo utazipiga na kuziangusha zile zingine, kama ulivyoona miguu yake ilikuwa chuma mchanganyiko na udongo, huu utakuwa ni ufalme uliogawanyika upande mwingien utakuwa wenye nguvu na mwingine dhaifu. Kama ulivyoona chuma mchanganyiko na udongo watu watakuwa wamechanganyikana lakini hawana umoja kama chuma kisivyo shikamana na udogo. Katika wakati wa wafalme hao Mungu wa Mbinguni atapandisha ufalme ambao hautaharibiwa wala hautamwachia mtumwingine tena. Utaziharibu zile falme zote na kuziondosha lakini ufalme huo utadumu milele, hii ndio maana ya lile jiwe kuiponda ile sanamu. Hii ndiyo ndoto yako ee Mfalme. Daniel 2 kifungu cha 24-45.

  Kufuatia ndoto hiyo ya mfalme, inasemekana kuwa kuna falme ambazo ziliinuka baada ya utawala wa mfalme Nebkadreza, miongoni mwa falme hizo ni pamoja na utawala wa Rumi, utawala wa Mjerumani na utawala wa Mwingereza. Lakini pamoja nahayo upo utawala ambao uemsemwa kuwa ni utawala uliochanganyikana chuma na udongo ambao watu wake watakuwa pamoja lakini hawana umoja, na huu ndio utawala nne katika mlolongo wa tawala zilizotajwa hapo juu. Nimetazama hivi sasa nimeona kuna jumuiya ambazo nchi nyingizimefanya lakini jumuiya hizo hazina umoja hata kidogo ndani yake, kwa mfano Jumuiya ya nchi za Kusini mwa Afrika, Jumuiya hiyo bado ipo haijavunjika lakini cha kushangaza raia wake hawapatani kabisa, hebu chukulia mfano kule nchini Afrika kusini, jinsi wageni walivyopigwa na kuuawa na raia wa Afrika kusini, chukulia mfano mwingine mzuri kabisa hapa nchini kwetu Tanzania, kuna umoja ambao ulifanywa na Raisi wa kwanza wa Tanganyika Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuziunganisha nchi hizi mbili na kuwa nchi moja na wakabadili hata majina ya nchi hizo, badala ya Tanganyika na Zanzibar wakaziita kwa jina moja la Tanzania, umoja huu umedumu kwa muda mrefu, lakini cha kushangaza hivi sasa raia wa Tanganyika (Tanzania bara) hawaruhusiwi kuingia Zanzibar bila hati ya kusafiria, sheria hii imewekwa mwaka 2008 na serikali ya Zanzibar, hii inaonyesha wazi kwamba watu hawa hawana umoja wa kweli kutoka mioyoni mwao, wana umoja midomoni tu. Na huu ndio utawala wa chuma mchanganyiko na udongo.

  Mpendwa napenda kukujulisha kuwa, kama Daniel alivyosema kuwa baada ya utawala wa chuma mchanganyiko na udongo Mungu wa mbinguni atainua utawala wake ambao hautapita na hii ndiyo maana ya lile jiwe lililoiponda ile sanamu. Ninapenda kukujulisha kuwa jiwe hili ni Yesu Kristo ambaye Mungu wa mbinguni ammuweka kuwa kuhani milele. Waebrania 7 kifungu cha 24 pia anajulikana kama jiwe kuu la pembeni Zaburi 118 kifungu cha 12 na kama Daniel alivyosema kwamba jiwe hili (Yesu Kriso) litazivunja tawala hizo katika kipindi cha utawala wa chuma mchanganyiko na udongo ambao ndio utawala tulio nao sasa.

  Hii inaonyesha wazi kwamba wakati wowote kuanzia leo Yesu atarudi kuihukumu Dunia na kuharibu tawala zote za Duniani, wala hatakuja kwa kutoa taarifa, bali atakuja kama mwivi, Ufunuo 3 kifungu cha 3 (“Tubu usipotubu naja kama mwivi) pia hakuna mtu ambaye anaifahamu saa ya kuja kwake maana inasemekana hata yeye mwenyewe Yesu haijui sik wala saa ya hukumu ya Dunia. Yesu mwenyewe alisema katika kitabu cha Mathayo 24 kifungu cha 36 (wala hakuna aijuaye siku wala saa iwe ni malaika wa mbinguni au mwana wa Mungu bali aijuaye ni baba peke yake) jambo hili linatuasa kujiweka tayari kwa kila saaa na kwa kila wakati kwa maana hatujui ni lini na saa ngapi atarudi.

  SURA YA TATU

  MAJARIBU

  MAJARIBU NI NINI? – Majaribu ni kipimo ambacho hutumika kumpima mtu au kitu ili kutambua kuwa kinauwezo au anauwezo kiasi gani wa kufanya kazi katika sekta anayohitajika.

  Inasemekana palikuwa na mtu mmoja jina lake Ayubu, mtu huyu ni miongoni mwa watu hapa duniani waliopata majaribu kwa kiasi kikubwa sana. Siku moja malaika walikwenda kujihudhurisha mbele za Mungu shetani naye akaenda kujihudhurisha mbele za Mungu, Bwana kamuuliza shetani “umetoka wapi wewe?” shetani akamjibu Bwana “nimetoka duniani kuzunguka zunguka huku na hna humo” ndipo Bwana akamuuliza “Je umemuona mtumishi wangu Ayubu? Kwani hakuna hata mmoja duniani aliye mkamilifu, mwelekevu na mwenye kujitenga na uovu na mwenye kumuheshimu Mungu kama yeye. Shetani akamuuliza Bwana “Je huyo Ayubu yuamcha Bwana bure? Wewe hukumzingira yeye na nyumba yake, umezibariki kazi za mikono yake makundi yake ya mifugo na ya kondoo yamesambaa nchini kote. Hebu sasa nyoosha mkono wako uyaguse hayo uone kama hatakufuru mbele yako. Bwana akamjibu Shetani “hayo yote yako mikononi mwako lakini usimguse yeye mwenyewe.AYUBU 1:6-12.Shetani akaondoka, siku moja watoto wa Ayubu walikuwa wakisherehekea ndani ya nyumba ghafla ukavuma upepo ukaangusha ile nyumba na wote kwa pamoja wakafa, wala hakusalia hata mmoja. Wakati huo huo wachunga mifugo wake wakavamiwa na majambazi na wakauawa isipokuwa mmojatu ndiye aliyebakia kumpelekea Ayubu habari, na baada ya kuuawa kwa wachungaji hao mifugo yote ilichukuliwa na majambazi hao.

  Mtumishi wa Mungu Ayubu hakukufuru wala kumlalamikia Mungu, lakini mkewe alimshauri amkufuru Mungu ili afe, lakini Ayubu Mtumishi wa Mungu alimjibu mkewe kuwa wewe nawe u mmoja katika hao wanawake wajinga. Pamoja nahayo shetani aliona kuwa Ayubu bado amesimama na Imani yake shetani akaamua kumpiga Ayubu kwa Majipu mwili mzima ktoka uwayo hata kitosi cha kichwa chake, AYUBU 2 kifungu cha 7. Pamoja na kujaribiwa sana lakini Ayubu hakumkufuru Mungu wala hakufanya dhambi.

  Hapa nimeona kuwa kumbe mtu ambaye anamcha Mungu kwa kumaanisha toka moyoni mwake kwanza Mungu huimarisha ulinzi wa kutosha kwa mtu huyo yeye pamoja na familia yake pamoja na mali zake, hii ina maana moja mke au mume au mtoto anapotangaza kumfuata Yesu usimzuie maanaKupitia yeye utapata rehema na ulinzi wa Mungu kwa sababu Mungu atamlinda yeye na familia yake pamoja na mali zake. Kwa maana nyingine shetani hataweza kumzuru mtu huyo maana Mungu amemzunguka, na ndiyo maana shetani alipoulizwa na Mungu kuhusu Ayubu alisema wewe (yaani Mungu) umemzunguka yeye na familia yake, kumbe ukimfuata Mungu nguvu zozote zile za shetani hazitakudhuru wala hazikutishi kwa sababu Mungu amekuzunguka, wala mchawi hakutishi akikuona hata kama alikuwa anaenda kuloga ataanza kutetemeka na kukimbia mbali na wewe.

  Kitu kingine ukiumfuata Mungu kwa kumaanisha kabisa, kumbe Mungu atakubariki sana katika shughuli zako zote maana Ayubu alikuwa amembariki katika kazi za mikono yake na kuiongeza mifugo yake katika nchi. Lakini unapoamua kumfuata Mungu unatakiwa ufahamu kwamba kuna kitu kujaribiwa ndani ya hiyo safari, hivyo basi unatakiwa kujipanga kikamilifu ili kukabiliana na hayo majaribu yote utakayoyapata, mfano mzuri ni jamaa watatu vijana wa Kiebrania ambao ni Daniel Meshack na Abednego. Vijana hawa walilazimishwa kuabudu miungu ya mfalme wa Iraq, lakini vijana hawa walikataa kufanya hivyo mfalme huyo aliagiza wauawe. DANIEL 3:14-24 Mfalme akawaambia ni kweli kwamba ninyi mmkataa kuitumikia miungu yangu wala kuiabudu sanamu yangu? Sasa mtakaposikia sauti za filimbi na vinubi na kila aina ya muziki kama mtakuwa tayari kuanguka na kusujudia na kuiabudu sanamu yangunitawafanya vizuri sana, lakini msipofanya hiyo mtatupwa kwenye tanuru la moto, nitaona ni Mungu gani atakayekuja kuwaokoa mikononi mwangu.

  Vijana hao wakamjibu mfalme “Ee mfalme Nebkadreza hatutaki kujitetea sisi wenyewe mbele yako katika jambo hili. Kama tukitupwa katika tanuru la motoyupo Mungu ambaye atakuja kutuokoa, hata kama asipotuokoa elewa ee Mfalme kuwa hatutaitumikia hiyo miungu yako wala kuiabudu hiyo sanamu yako” ndipo mfalme akakasirika sana akaagiza ile tanuru itiwe moto mara saba kuliko kawaida yake askari wakawafunga na kuwatupa katika atanuru hilo, kwa sababu ya ukali wa ule moto kiasi kwamba hata ukilisogelea tu lile tanuru unakufa, askari hao walikufa hapo hapo lakini cha kushangaza moto huo ulizikata zile kamba ambazo vijana hao walikuwa wamefungwa nazo, lakini haukuwadhuru wao hata kidogo. Mfalme akasimama akasema “hivi hatukuwatupa watu watatu tu ndani ya tanuru? Lakini mbona ninaona kuna watu wane wanatemea tu ndani ya tanuru hawajafungwa na wala hawadhuriki na moto, na huyo wa nne anaonekana kuwa ni mwana wa Miungu, (Mtu wa nne alikuwa ni Yesu Kristo mwana wa Mungu aliye hai) ndipo mfalme akasimama akawaita vijana hao “Enyi Shadrack, Meshack na Abednego njoni nje ya tanuru, ndipo mfalme akasema “Na ahimidiwe Mungu wa Meshack, Shadrack na Abednego aliyemtuma malaika wake kuja kuwaokoa watumishi wake Meshack, Abednego na Shadrack ambao waliamua kuyapoteza maisha yao kwa ajili ya Mungu wao kuliko kujitia unajisi kwa kuabudu miungu mingine isipokuwa Mungu wao. Sasa ninaagiza mtu yoyote yule atakayesema neno kinyume na Mungu wa Vijana hawa atakatwa vipande vipande yeye na familia yake, maana hakuna Mungu mwingine anayeweza kuokoa namna hii.

  Mpendwa wangu hapa tunaona wazi kabisa kwamba kumbe wakati wa kujaribiwa hautakiwi kuogopa uzito wa jaribu ni ahueni uyapoteze maisha yako kuliko kuupoteza uzima wa milele, hili hata Bwana wangu Yesu Kristo alilisema “Mwanadamu atanufaika nini kama akiupata ulimwengu wote kasha aukose uzima wa milele? Hapa kuna faida zaidi ya tatu, ya kwanza ukimshika Mungu sawa sawa kama Shadrack, Abednego na Meshack, Mungu mwenyewe atakutukuza, faida ya pili utapata uzima wa milele, faida ya tatu utasababisha na watu wasiomcha Mungu waanze kumcha Mungu kwa kasi nzuri sana. Kwa nini ninasema hivi? Kwa sababu mfalme alikuwa anaitegemea miungu yake lakini siku hiyo akasema hakuna Mungu anayeweza kuokoa kama Mungu wa Vijana hawa isitoshe akaagiza kwamba yeyote atakayesema neno kinyume na Mungu wa vijana hawa atauawa yeye na familia yake. Hii inaonyesha wazi kabisa kwamba kupitia Imani ya hawa vijana na miujiza ambayo Mungu aliifanya, Mfalme alimwamini sana Mungu wa Mbinguni na kuona miungu mingine haifai.

  Kumbe katika imani yako unaweza kusababisha hata watu wengine waokolewe kupitia imani yako wewe hata unapokuwa katika kipindi cha majaribu, lakini unatakiwa ufahamu kwamba chanzo kikubwa cha majaribu ni shetani, yeye huenda mbele za Mungu na kuomba ruhusa ya kukujaribu, lakini kukujaribu anategemea kabisa kwamba atakuangusha. Lakini wakati ujaribiwapo Mungu naye yupo chonjo kukuangalia ni namna gani utamshinda shetani, na Mungu anapotoa ruhusa na wewe kujaribiwa huwa anataka wewe uyashinde hayo majaribu , pia ninamshukuru sana Mungu Baba Mwenyeezi kwa saababu huwa haruhusu kwetu yaje majaribumakubwa kuliko uwezo wa imani zetu soma 1WAKORINTHO 10 kifungu cha 13 biblia inasema hivi “Hakuna jaribu lililokubwa kuliko uwezo wako ambalo Mungu ataliruhusu likufikie ispokuwa ni lile lililo sawa na uwezo wako, pia Mungu ni mwaminifu hukuwekea mlango wa kutoke”.

  Hii inaonyesha wazi ni jinsi gani Mungu anakupenda mimi naona kama vile Mungu humzihaki shetani kwa maana anapomruhusu akujaribu hamruhusu akujaribu zaidi ya uwezo wako, ina maana moja kwamba hamruhusu akuangushe wala akusumbue kiasi kwamba ushindwe kuvumilia. Hii ni thabiti kabisa kwamba shetani ni mjinga kwa sababu haiwezekani mtu akuagize kumuua nyoka lakini akuagize usimpige kichwani ila mkiani tu kweli utampiga hata mkia, lakini cha kushangaza huyo huyo aliyekuagiza kumpiga alipoona umemkata mkia anampa mkia mwingine tena anamwongezea na wa pili mbele yako. Je huyo mtu ni kweli kwamba anataka umuue huyo nyoka au anataka kukusumbua tu? Hapa nimeona kwamba Mungu humsumbua kijanja shetani, kwa sababu shetani hana busara halioni hilo. Mpendwa wangu napenda ufahamu kwamba hakuna jaribu linaloweza kukuua, pia hakuna jaribu linaloweza kudumu miaka yote ya maisha yako Mungu asiliondoshe. Mfano Ayubu watoto na mali zake wakati wa kujaribiwa vyote kwa mpamoja vilikwisha, lakini baada ya jaribu kupita alipata mara mbili zaidi ya yale aliyokuwa nayo mwanzo. Soma AYUBU 1 kifungu cha 1-3, hapa ilikuwa ni kabla ya kujaribiwa. Kisha soma AYUBU 42 kifungu cha 12 – 15, hapa ni baada ya kujaribiwa. Hivyo hivyo tumeona hata kwa hawa vijana wa Kiebrania akina Meshack na jamaa zake, baada ya kutoka katika tanuru la moto mfalme aliwaweka kuwa watumishi wa ngazi za juu sana katika ikulu ya Iraq.

  Hapa moja kwa moja nimeelewa kuwa hata kama ulikuwa mtumwa kwa kumcha Mungu na kuvumilia katika majaribu Mungu atakufanya kuwa Mtawala. Hata kama ulikuwa maskini sana atakufanya kuwa Tajiri maana hata Ayubu aliishiwa kila kitu kwa maana moja alikuwa masikini lakini kwa kushinda majaribu alipata mara mbili ya yale ya kwanza. Lakini nimekuandalia mada hii ili kukujulisha kuwa unapoamua kumfuata Yesu elewa kuwa umetangaza vita, hata mambo ambayo ulikuwa huyapati utayapata hivyo basi kuwa mvumilivu katika hizo dhiki Mungu yupo pamoja na wewe wala hajakuacha. Jitahidi majaribu yako yasigeuke kuwa mateso kwako, nina maana moja kusema hivyo. Kuna tofauti kati ya majaribu na mateso mtu ambaye anapata mateso akiwa kwa Yesu huyo ndiye anajaribiwa ambapo asipotenda dhambi katika hayo mateso atapewa zawadi kutoka kwa Mungu mwenyewe. Lakini yule ambaye anapata mateso akiwa kwa shetani huyo yeye anateswa tu wala hatapata faida yoyote ile ya mateso yake.

  Ninakusihi katika jina la Bwana wangu Yesu Kristo usitende dhambi ndani ya majaribu hayo ukaikosa zawadi ambayo Mungu alikuwa amekuandalia.

  BWANA YESU AKUSAIDIE SANA UMSHINDE SHETANI

  SHUKRANI

  Ninamshukuru Mungu Baba Mwenyezi aliyezifanya mbingu na nchi kwa kuniwezesha kutengeneza kitabu hiki. Ni dhahiri kabisa kuwa kwa akili zangu tu mimi Moses nisingeweza kufanya kazi hii hasa kulingana na umri wangu kuwa ni mdogo sana. Vile vile ninamshukuru sana kwa kunifanya kuwa mtumishi wake katika umri mdogo sana.

  OMBI LANGU KWAKO

  Mpendwa wangu katika Bwana ninaamini Mungu wa mbinguni humpenda na humbariki sana yeye atangazaye habari zake duniani, hivyo basi ninakuomba mpendwa wangu kama ukiweza angalau uzalishe nakala moja tu ya kitabu hiki na umgawie mtu mwingine ili kuweza kusambaza msaada huu wa injili kwa watu wengi zaidi ulimwenguni mwote.

  MUNGU AKUBARIKI SANA KWA KUFANYA HIVYO

  MKAKATI NA LENGO LA KITABU HIKI

  Mkakati na lengo langu ni kukisambaza kitabu hiki katika nchi zote zinazotumia lugha ya Kiswahili hususani Afrika Mashariki, na katika nchi zisizotumia lugha ya Kiswahili tayari nimeshaanza kukiandaa kitabu hiki kwa lugha ya Kiingereza. Kitabu hicho kitatoka hivi karibuni na kitaanza kusambazwa huko nchini Nigeria, Swazilandi, Marekani, Tahailandi, India na hata Tanzania pia. Lengo hasa la kufanya hivyo ni kueneza msaada zaidi wa maandiko duniani pote.

  Hivyo basi ninakuomba uniombee sana kwa nguvu zako zote ili niweze kufanikisha suala hili, pia uniombee sana ili Mungu anitie nguvu zaidi niweze kumtumikia zaidi ya vile nilivyopanga kumtumikia.

  BWANA AKUTENDEE YALIYO MEMA MAISHANI MWAKO.

  AMINA

  HAKI YA KURUDUFU

  Kitabu hiki kinaruhusiwa kukizalisha na kukisambaza sehemu yoyote lakini kisambazwe bure kisiuzwe kwa gharama yoyote iwe ya juu au ya chini. Pia kitumika katika misingi ya Mungu na katika mashauri mema na si katika uhalifu. Hairuhusiwi kutumia neno lolote la kitabu hiki katika uovu wa aina yoyote ile.

  ENDAPO UTAHITAJI MSAADA ZAIDI:

  Wasiliana na mimi kupitia simu namba: 0755 961270 au +255 715961270

  Barua pepe: mosesmayila@yahoo.com

 63. BWANA YESU ASIFIWE! NDUGU ZANGU WAPENDWA KATIKA BWANA NASHUKURU KUPATA NAFASI HII KUTOA MAONI YANGU MACHACHE YA KUJENGA KANISA NAKUMBUKA 2008 WAKATI KULIPOKUWA NA MUSWADA WA TANZANIA KUSILIMISHWA NA KUINGIZWA KWENYE OIC YAANI UMOJA WA NCHI ZA KIISILAMU WAPENDWA TULIFUNGA NA KUOMBA KWA BWANA WETU YESU KRISTO PIA LILIPOKUJA SUALA LA MAHAKAMA ZA KADHI TUKAPIGA MAGOTI NA KUMWITA BWANA WETU SASA TUKUMBUKE KUWAKATAA VIONGOZI WOTE WENYE KULETA UDINI WAKATI HUU WA UCHAGUZI,MUNGU AWABARIKI WOTE

 64. Tuweni makini sana WATEULE wa Mungu hali ya ulimwengu ni tete sasa, Roho ya mpinga kristo i kazini, ukiona matangazo kama hayo yakimbie, tena mwombe Mungu wakati ukikimbia huduma kama hizo usianguke wala kugeuka nyuma! Ogopa matangazo ya upako juu ya mafanikio ya kimwili tu afu kiroho badae, KIMBIAAAAAAA……………….!!
  Tumwangalie Mungu tu! kama ni mali kwake zipo, wake wazuri wapo kwake!, utajiri msafi wa kila namna upo kwake!, tukikaa katika mpango wa Mungu siku zote kwa uaminifu, HAKIKA tutaifaidi dunia hii mpaka basi…..!
  Tuwaheshim na kuwatii viongozi wetu wa kiroho, naamin tukifanya hivo, kupitia wao kuna mafanikio yetu! LAKINI tusisahau kuwaombea ili wasonge mbele zaidi”
  ENDELEA KUWA MTAKATIFU SIKU ZOTE!

 65. haleluya!!
  ni kweli dada christina uliyoyasema. Ni muhimu kusoma vitabu vya unabii ili kupata ufahamu wa mambo yajayo sawasawa na daniel mlango wa tisa (DANIEL 9)

 66. wapendwa katika bwana mi nafikiri yale mambo ya mpinga kristo ndo yanaanza taratibu.inasikitisha kuona yale mambo yaliyo elezwa ndo hayo yanatokea tena kwa haohao watumish naomba someni sana DANIEL na UFUNUO na ufunuo muombe roho akuongoze uelewe ni mambo ya kutisha KWAN ni vitabu vya kinabii sasa watumishi weka akili kichwani kaza mwendo.MUNGU NI MUWEZA

 67. Ndugu zangu katika Kristo nimefurahishwa sana na mijadala hii yenye lengo jema na inayoonyesha mambo ya msingi katika ulimwengu huu. Ni mara ya kwanza na leo ndio nimejiunga na forum hii. nawapongeza sana washiriki na hasa wale wenye ufuhamu mkubwa ambao wanawalimisha wengine kwa lengo jema tu la kumuinua Kristo. Ni imani yangu kuwa forum hii itakuwa kubwa huko mbeleni. Mungu awape hekima na maarifa yake wale waoitangaza injili ya Yesu Kristo kwa ujasiri kwa njia mbali mbali ikiwemo na hii. Nawapongeza sana ndugu zangu waanzilishi waforum hii. Bado najifunza mambo mengi na nitakuwa mshiriki mzuri

  Pia nimefurhishwa na maandiko machahe yalioacha historia na thiolojia za kidini na mapokeo alizokuwa anatoa bwana DOMINIC MZIRAI na kujibiwa kiinjili na Bwana Bernard Mwenda
  nilikuwa na mtizamo huohuo na manaeno haya hayo. Mungu akubariki sana Bwana BERNARD

 68. Napenda kuwahukuru sana waliotangulia katika mada hii.
  Mimi pia napenda kuchangia kwamba sasa hivi kuna spirit of manipulation sana katika kanisa, yaani mtu anafanya kitu ili apate kitu. Sasa unakuta watu wengi wanaacha lengo la wokovu wanaanza kuangaika na vitu vingine. Wapendwa Yesu alisema “utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na HAKI yake na mengine yote mtazidishiwa”. So unakuta watu wako busy kuomba bwana naomba unipe utajiri,naomba uniponye,naomba unipe kazi na Mungu anapoangalia haoni njia kwanini haki hana maana laana za mababu na mabibi zinamfuatilia,kwa hiyo haki ya ufalme inakuwa bado haijatimizwa na kumbe angetafuta ufale]me lazima angetubu kwanza ufalme ushuke uondoe hizo laana na vifungo ili baraka zikujie.
  Wapendwa tusipotambua mambo haya tutakaa katika wokovu tutamkasikia Mungu na wengine watachoka njiani na kukimbia maana hawaoni mafanikio.
  So stop manipulating God let’s Worship him in Spirit and Truth. PIA NINGEPENDA KUWASHAURI WALE WOTE WANAOPENDA KUSOMA VITABU VYA KIROHO WATAFUTE KITABU KILICHOANDIKWA “EXPOSING DEMONIC DEVICES” kilichoandikwana ndugu kutoka Nigeria (ONYECHI DANIELI) Hii itakusaidia kujua vitu vinavyoblock baraka zako.
  Mbarikiwe na Bwana Yesu!!

 69. Kwa kweli matangazo kama haya si mageni kuyasikia especially kwenye vipindi vya j2 asubuh kabla ya mida ya makanisan…. kitu cha muhimu aLIYE SIMAMA NA AANGALIE ASIANGUKE! Kila kilichoijaza dunia ni mali ya bwana. Tuutafute kwanza ufalme wa mbinguni na haki yake na mengine yote tutazidishiwa! NB Nikinukuu kutoka kwa baba yangu wa kiroho(Pastor Mtelevu) huwa anasema kuwa original ya kila kitu iko kwa Mungu peke yake!! Shetani ana photocopy tu…

  NB Kwa nin tusiamue kumtafuta mungu Kwanza kwa kuwa Mungu wetu si dhalimu huwapa mema watakatifu wake wamwombao usiku na mchana.Tena Mungu anasema Je? Ni nani kwenu ambae mwanae akimwomba mkate atampa Jiwe au Samaki ampe Nyoka?
  Baraka za Mungu haziangalii unasali Kanisa gani…lenye watu wengi au wachache? Tajiri au Maskini… ASANTE

 70. My dia Maria,Yesu sifiwe sana nashukuru sana kwa upendo wako wa kunishaur jambo zur nimefurah sana ubarikiwe na Mungu wetu.MUNGU akutunze amen!

 71. Dada Hope,
  Bwana Yesu asifiwe sana. Kwakweli kila mtu anabarikiwa sana na mijadala hii mimi pia nikiwa mmoja wao.
  Kutokana na swali lako hapa dadaangu, pia ninakushauri ujiunge na kundi moja zuri sana ambalo linafafanua na kuelewesha vizuri sana yani ukiwapa tuu swali lako daah!! utafurahi mwenyewe. Watumie Email, strictlygospel@yahoo.co.uk wakuunganishe Kwenye Kundi. Dada Hope utafurahi na utaniambia.
  Haya dadaangu Mungu akutunze.

 72. Wapendwa Mungu awabariki sana mie ni mgeni katika majadiliano haya kiukwel nimefurahishwa sana na mada zenu.mie nilikuwa napenda kujua kwa habari ya wito(huduma)ninachojua mim kuwa kila binadamu ana wito wake je hii ni kwel?na kila m2 atajua vip wito alioitiwa?mbarikiwe wapendwa

 73. Imeandikwa;

  Tafuteni kwanza ufalme wake na haki yake, na menhine yote mtazidishiwa, mtume paulo ameutafsiri ufalme wa Mungu kama Haki, Amani na Furaha katika Roho mtakatifu. hivi ndio vitu tunavyopaswa kuvitafuta. haki ipatikanayo kwa njia ya Imani, Furaha ya bwana ambayo ndiyo nguvu zetu, na Amani ya Yesu ipitayo akili zote. Hivi vitu vitatu vinaumba Ufalme wa Mungu ambao yesu alisema umo ndani yenu. Tatizo la wakristo wa sasa wanatafuta Vitu badala ya Ufalme,wanataka kubarikiwa, lakini hawataki kuingia ndani ya kusudi la Mungu zilimo baraka. wanataka baraka za Mungu ziwafuatie huko waliko ili waendelee kufanya mambo yao ya anasa. Hii ni dhuluma kwa Mungu kwa kuwa Mungu anapokubariki ni kwa ajili ya kuliendeleza kusudi lake, yaani kuliimarisha agano lake.
  Ikumbukwe kwamba, Njia kuu atakayotumia shetani nyakati za mwisho ni udanganyifu, kuwafanya watu waamini zaidi katika mafunuo wanayopewa na wanadamu badala ya kuyashika maneno ya Mungu. Matangazo ya namna hii ni njia rahisi zaidi ya kuwadanganya watu ambao mioyo yao imeelemea katika kutafuta vitu badala ya ufalme wa Mungu (haki, Amani na Furaha katika Roho Mtakatifu.)
  baraka za Mungu zinapatikana ndani ya kusudi la Mungu. ukitaka kuuona utukufu wa Mungu maishani mwako, tafuta kujua vipaumbele vya Yesu nyakati hizi za mwisho na fuata hivyo. Yesu aliomba akisema “Baba hao ulionipa nataka wawe pamoja nami popote nilipo wapate kuutazama utukufu wangu ulionipa tangu kabla ya kuumbwa ulimwengu”
  Utukufu wa Mungu na Fahari yake vinapatikana Yesu alipo, ndani ya kusudi la Mungu.

 74. KWELI SASA NI ‘BIASHARA KWENDA MBELE’ WATU WAMEJIINGIZA KATIKA WOKOVU NDIYO SABABU WENGINE WANATAFUTA FEDHA KWA KUFUNDISHA UTOAJI LAKINI KWA NIA MBAYA WAJIPATIE FEDHA NA MALI,
  MTAKATIFU UNATAKIWA KUWA MACHO NYAKATI ZA MWISHO HIZI MAANDIKO YANATIMIA ‘WENGI WATAPENDA FEDHA’ NA HIVYO KUITAFUTA KWA NJIA YOYOTE HATA KWA KULITUMIA NENO ISIVYO HALALI.
  Mungu atusaidie!

 75. naomba nizungume kuhusu injili ya ishara na miujiza.watu wengi wamekumbwa na mashaka juu ishara na miujiza huku wakiwa na mashaka juu ya baadhi ya watumishi wa Mungu wakidhani kuwa wanatumia nguvu za giza! naomba unifuatilie kwa makini sana, nimefanya utafiti kwa muda wa takriban miaka miwili nimegundua kuwa watu wengi wanaamini kuwa shetani ana nguvu sana kuliko Mungu, hili ndilo tatizo kuwa sana lililowakumba watu wengi. biblia inasema wale waaminio ishara na miujiza zitafuatana nao.lakini pia kumbuka biblia inasema kulikuwa na mtu mmoja jina lake bar-yesu mchawi alikuwa akifanya miujiza na kuwavuta watu wengi sana. hivyo suala la miujiza ni la pande zote upande wa Mungu na upande wa shetani, lakini miujiza mikubwa ni ya Mungu na si ya shetani, kumbuka pale Musa alipokutana na wachawi wa Farao walitupa fimbo zao zikawa nyoka na Musa akatupa yake ikawa nyoka lakini nyoka wa Musa aliwameza wote nyoka wa wachawi wa farao. hivyo ili kutambua kuwa muujiza huu ni wa Mungu au ni wa shetani sio rahisi mpaka uwe na uzoefu na huduma hiyo. lakini mimi ninawashauri ndugu zangu epukana sana na watumishi kutoka Nigeria! sio kwamba nawakataza musiwafuate watumishi watokao Nigeria ila ninatoa tahadhali kwa sababu miujiza mingi yakishetani imekuwa ikitoka Nigeria.

  Pia kila mtu asiyetumia jila yesu katika kufanya miujiza yake huyo sio wa Mungu kabisa, achana naye atakuumiza huyo. Kumbuka Petro alipotaka kumponya yule kiwete alisema “kwa jina la Yesu simama” hata Paulo alipomtoa yule pepo wa utambuzi alisema “kwa jina Yesu wa nazareti fumba kinywa na umtoke” pia Yesu mwenyewe alisema na ishara hizi zitauatana nao waaminio kwa jina langu watatoa pepo, wataweka mikono juu ya wagonjwa nao watapata afya, watasema kwa lugha mpya na………..hivyo kuweni waangalifu sana ndugu zangu.pia mwombeni sana Roho mtakatifu awafunulie haya.

 76. Mbarikiwe mliotangulia kuchangia. Ni kweli kuwa makanisa mengi sasa yanatangaza miujiza ili kuvutia watu haswa wale wenye uelewa mdogo wa neno la MUNGU. Utakuta mtu anashuhudia anasema mimi niliugua muda mrefu nimeenda kwenye mikutano mbali mbali nimekwenda kwenye makanisa mbalimbali lakini sikupokea uponyaji ila leo nimekuja hapa kwa fulani nimepokea, jamani MUNGU wa fulani anaweza!..ok, sio vibaya ila nikuulize wewe uliyeokoka miaka mingi iliyopita umekua na kazi ya kuhama makanisa, je huko kote toka ulipo okokea mpaka leo hii huko ulipokuwa hapakua na nguvu ya MUNGU? au tatizo ni nini? jiangalie sana imani yako acha kuamini makanisa kutokana na miujiza ebu anza kumwamini MUNGU asilimia zote uone baraka alizoahidi kwenye kumbukumbu 28.

  JACOB ISSACK(INNOCENT) WA MABIBO DAR.

 77. Nashukuru kwa kupata nafasi hii sassivi tunapaswa kumwabudu MUNGU.hili swala kweli linaumiza sana roho na limeua nafsi za watu wengi kwa sababu imefikia hatua utakuta watu wanaanza kusema”aisee kanisa fulani mimi siwezi kwenda”Ukimuuliza kwa nini anakwambia Mtumishi hanibariki hii ni kutokana na BaadhiyaWatumishi kukosa uaminifu na kufuata nafsi zao kinachohitajika ni kukaa chini na kuomba.TUNAMWITAJI SANA MUNGU ILI WANADAMU TUBADILIKE.Amen PENDO AYO-From INSTITUTE OF ACCOUNTANCY ARUSHA

 78. nashukuru kapata fursa hii. ok maoni yangu kuhusu mada hiyo hapo juu, nikwamba sasa hivi dini imekuwa kitega uchumi cha walio wengi. nasema hivi kwa sababu utakuta makanisa mengi sana tena mengi yakiwa haya ya uhamsho maubiri mengi yanaelezea kupata fedha,magari,nyumba,mke,mme na mengine mengi yanayo husu mambo ya kimwili tu,jamani tukumbuke kwamba dunia hii mambo mengi ya meharibika ikiwa nipamoja na kukosa hivyo vinavyo hubiriwa kwa sasa kutokana na dhambi mimi naamini kwamba tukiomba Mungu atusamehe dhambi na pia waumini wafundishwe namna ya kuacha dhambi pamoja na kuikimbia dhambi na kukwepa dhambi sio lazima uombewe hata ukiomba mwenyewe Mungu atajibu tuu hitaji lako.nashauri kwamba watumishi mwe mnaubiri mafundisho yanayo jenga sio kila ibada ni maombi yakupata tu hata jinsi ya kupata ufundishwi jamani tuwe makini sana shetani ni mjanja sana tena sana anatumia hizo hizo opportunity za mahitaji yetu ya kimwili.mungu awajalie watumishi muwe makini sana. napatikana kwa no.0755 462 420/0712 600 674 dar es salaam.

 79. Nimesoma mijadala ya hapa ndani kwa kiasi fulani nimebarikiwa sana na watumishi wa MUNGU walioandika na hata wale wengine waliochangia kwa uzoefu wao wa kimaisha. Lakini mimi nilikuwa na angalizo kuwa ushauri mwingine husiposomwa kwa makini zaidi unaweza kumtupa mtu mahala pabaya zaidi kuliko alipokuwa mara ya kwanza.

 80. Mungu asifiwe.Namshukuru Mungu, heshima, utukufu na adhama vina yeye. Hili somo la mwalimu Mwakasege linaloendelea katika semina inayofanyika pale biafra, kwa kweli limenifungua. Sikuwahi kufikiri namna Mungu anavyoweza kuzungumza mambo ambayo ndani yake yana siri ya ajabu sijapata kuona. Roho Mtakatifu anaendelea kunifundisha kwa habari ya Toba kwa wazaliwa wa kwanza kama malango.Sasa ninafanya toba hiyo kwa msaada wa roho mtakatifu. Mungu aendelea kumbariki na kumpa anoiting mtumishi wake Christopher Mwakasege. Kwa kweli tunapona kabisa na neno lile Mungu analozungumza nasi kupitia mtumishi wake.

 81. Wanakwiba tu wachungaji wa namna hii,siku hizi wizi uko mwingi madhabahuni,mke/mme/mcumba,pesa,magari havitafutwi madhabahuni,bali ni bidii na kazi.wapenzi wa mungu tisidanganyike na michango isiyorasimi makanisani haipendezi na wala haifai kabisa.

 82. bwana yesu asifiwe wapendwa ,haya ni mambo ya ajabu wanayofanya hawa wachungaji kikubwa zaidi tujikite katika maombi tutapata kujua roho hizi zingine zinazotokea za uongo .maana wachungaji wengi siku hizi ni waongo hizi ni siku za mwisho tusome sana neno kwani ndiyo tutakuwa tuanaimarisha mizizi ya imani zetu hata kikitokea kitu si cha kweli tunapata kutambua kiurahisi.

  mbarikiwe sana

 83. NDUGU KASULE UBARIKIWE ILA NA MIMI NILIKUA NAHITAJI
  KUJUA TOFAUTI KATI YA MALIMBUKO ZAKA SADAKA NA FUNGU LA KUMI.NAOMBA UNIJIBU ILI TUWEZE KUJADILI SUALA LAKO.

 84. Wapendwa Bwana Asifiwe,

  Nimesoma na kuona mambo hayo ambayo yanafanywa na baadhi ya watumishi ya kufanya biashara na hata uponyaji kwa njia ya kuigiza,na matangazo mengi kama yalivyotajwa hapo juu.

  Lakini ndugu zako haya yote Yesu aliyaweka wazi kwamba tutawajuaje wale watu ambao wameokoka kweli,ni kwa njia ya matendo yao na siku ya mwisho neno limetuambia wengi watakataliwa na bwana Yesu mwenyewe na wengine watajitetea kwa wao walitoa pepo na kuponya magonjwa lakini Yesu atawakataa kwa sababu walikuwa hawafanyi kwa ajili ya Yesu bali kwa ajili yao wenyewe.

  Tusimame katka kweli na kweli itatuweka huru.

  Elisante Yona

 85. Nini ukweli juu ya ZAKA:
  Wengine wanasema kuw ZAKA ilikuwa inatumika enzi za torati kwa ajili ya makuhani ambao walikuwa ni wa kabila la Lawi. Na wao walikuwa hawatakiwi kufanya kazi yoyote zaidi ya madhabahuni na wao ndio walikuwa walikuwa wanalibeba kanisa katika maobi mbele za Mungu. Walikuwa wanatubu dhambi la kusanyiko mara moja kwa mwaka kwa kuingia patakatifupa patakatifu.Kwa kuwa kipindi hiki hatuishi chini ya torati Mkristo habanwi tena na sheria hiyo.Hivyo Mkristo anaweza kutoa zaka mara mojakwa Mwaka ila kwa kiwango kikubwana inakuwa siku maalum. Mkristo aendelee kutoa sadaka na matoleo mengine kwa uaminifu na kaziya Bwana itaendelea vizuri.

  Wengine wanasema kuja kwa Bwana YESU hakujabadilisha utoaji wa ZAKA.Iendelee kutolewa kama zamani.
  Nimeuliza hivyo kwanin sikuhiziZAKA imekuwa ada ya Uanachama wa Kanisa pasipo hata kujali msingi mkuu wa Mkristo ambao ni UTAKATIFU.
  Naomba ushauriwenu wapendwa

  9

 86. Halelujah
  long time no see guys nilikuwa na kiu yakutembelea hapa mahala namshukuru Mungu kani wezasha leo.ama kweli mijadala hii inajenga,kiukweli katika haya makanisa na hizi huduma something is wrong somewhere some how, nawatumishi wakati mwingine tunaona kabisa lakini twaijfanya hautoni. kuna vitu vingine mbavyo ni rahisi kutafsirika navyo tuna vi complicate na vile vilivyo complicated nadhani tutakua tuna simplify

  A NEW COMMANDMENT matthwe22,37-39 AND A GREAT COMISSION matthew 28;8,19,20 tuki viishi hivi tutakua tumeishi bible nzima na tutasalimika hakika

  Mungu awatunze
  LOVE AND PRAYER

 87. ASANTENI WOTE MLIOCHANGIA.

  MIMI NINA HILI TU LA KUSEMA: WATU WANAABUDU NA KUYATUMIKIA MALUPULUPU NA KUACHA KUMWABUDU NA KUMTUMIKIA MUNGU,WATU WANAHUBIRI VITU VILIVYOWEKWA KUWA MATOKEO YA KUMWABUDU MUNGU,KWA MFANO MAFANIKIO KWA MTU ANAETEMBEA NA BWANA NI KITU KISICHOKWEPEKA,MITHALI 10:6.IMANI ZIMESHIKIZWA KWENYE MALI NA VITU NA NDO MAANA KAKA JOHN PAUL AMESEMA MTU HUYOHUYO ALIYESHUHUDIA UTAJIRI WAKE HAWEZI KUKEMEA HATA PEPO.UVIVU UNALIGHARIMU KANISA…

 88. Asanteni sana wapendwa wote mlioonyesha moyo wa kujifunza kitu katika majibu niliyoandika hapa. Zaidi sana ni kwa ndugu Shoo GAP mbaye ndiye alileta mada na kuuliza maswali haya, ambaye naye ameridhika na majibu ya maswali yake. Sifa na utukufu ni kwa Mungu! Asanteni sana pia kwa maombi yenu, nimeyapokea. Amina!

  Hitaji kuu lililoko sasa hivi kwa watu wa Mungu, nionavyo mimi, ni kuomba sana ili Mungu Afufue kazi yake, katika miaka hii atangaze habari na katika ghadhabu akumbuke rehema! [Hab 3:2]. Mimi naona kama tunaishi nyakati ambazo kweli ya Neno la Mungu imepotoshwa sana! Mafundisho mengi sana yanafundisha watu kupata maslahi binafsi [mali, uzima wa mwili – japo si vibaya] katika mwili badala ya kuwafundisha kuutafuta uwepo wa Mungu ambao una uwezo wa kubadilisha hadi mazingira anayoishi mtu,ya kiroho na ya kimwili! Na kwa sababu hii mambo ambayo alisema Yesu kwamba yangefanyika kwa wamwaminio yamekuwa adimu sana. Why? Kwa sababu uwepo wa Mungu katika maisha ya waamini ni mdogo sana!

  Fikiria mtu anaweza kusimama kanisani akashuhudia kwamba Mungu amemsaidia ameweza kupata biashara kubwa na sasa anamiliki kambuni kubwa mjini. Lakini utashangaa inapotokea kuna jirani amepatwa na mapepo, mtu huyo huyo aliyemshukuru Mungu kumpatia kampuni kubwa, hawezi hata kukemea hayo mapepo. Kwa hiyo cha kwanza kwake ni kumpigia simu mchungaji/mtumishi aje kukemea pepo. Inashangaza kwa maana kama huyo mtu anatambuwa kwamba ni Mungu ndiye alimfanikisha kupata biashara kubwa inakuwaje ashindwe kutambua kwamba nguvu za kutoa pepo zinapatikana kwa Mungu huyo huyo? Tunaugeuza ukristo ndani-nje!

  Tuzidi kuombeana ili Mungu atusaidie na kutufanikisha katika kuujenga mwili wa Kristo.

  Tuendelee kujifunza!

 89. Shalom,

  Kaka John Paul kuna kitu kizuri sana umefundisha, glory to Lord.

  Ni kweli hata mimi nimeshuhudia hayo, kuna tatizo kubwa sana kwa watu waliookoka siku hizi, namaanisha nimeyaona hayo kwa wengi. Wengi tumekuwa tukijihesabia haki, kwa kuona kuwa tabia na mienendo yetu haihusiki katika kusababisha kuumizwa na kuzidiwa na nguvu za giza katika kumshinda ibilisi na matokeo yake wengi wanasingizia kuwa wanayopitia hutokana na laana, uchawi wa ndugu zao, majirani n.k

  Yakobo 4;7

  ‘Basi mtiini Mungu mpingeni shetani naye atakayewakimbia’

  Kwa jinsi nilivyojifunza kupitia mchango wako na neno la Mungu, ni kwamba, uovu na kazi za ibilisi zitaendelea duniani na hatuwezi kuziondoa kabisa bali haziwezi kuwa na madhara kwetu kama tutamtii Mungu, kulitumainia jina la Yesu na kujua nguvu na ulinzi uliopo katika damu ya Yesu. Ndiyo maana Yesu hakuwaombea wanafunzi wake watoke katika ulimwengu (akimaanisha maovu, masumbufu yasiwepo kabisa duniani ndipo waweze kuishi kwa raha) bali aliomba nguvu ya Mungu iwalinde.

  Yohana 17;15

  ‘Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu bali
  uwalinde na yule mwovu’

  Alijua kwa nguvu ya Mungu wataweza kushinda yote ya dunia na hayatakuwa kikwazo kwao.

  Pale ambapo mwovu atakapotaka kutujaribu ndipo atakapokutana na ile nguvu ya Yesu ndani yetu na atashindwa, ataaibika, atasurrender na kujua kuwa kuna nguvu zaidi ya ile anayoitumainia (ya ibilisi) na atajigundua hayupo salama na akiwa mtii ataokoka.

  Kuna baadhi ya watu wakipata shida / mapito, anaanza kutafutaa historia ya ukoo au mazingira ili kujua huenda kuna mtu / mazingira ayaliyomsababishia badala ya kuchunguza njia zake mwenyewe huenda hajakaa vizuri na Mungu au kaboronga mahala fulani, au kutokana na kutojua jukumu lake na kukosa nguvu ya kumshinda adui.

  Ni kweli kabisa tunatakiwa kutembea vizuri na Mungu, ili kushinda nguvu za giza na uovu na kuwasaidia waovu wapate kujua / kuziamini nguvu za Yesu kupitia. sisi.

  Tuzidi kushirikiana katika kuujenga mwili wa Kristo,

  Nawapenda sana

  Faith

 90. Bwana Yesu asifiwe sana,
  kipekee namshukuru sana Mungu kwa ajili ya blog hii inatusaidia sana hasa kulingana na maswali mengi ambayo yanakuwa yanajibiwa naamini watu wengi wanabarikiwa sana kupitia blog hii.Asante sana John Paul kwa ajili ya majibu ambayo umeweza kuyatoa kulingana na swali alilokuuliza ndugu Shoo Gap umejibu vizuri sana swali hili naamini kwa wale ambao walikuwa wanakwenda kinyume Mungu atawabadilisha ubarikiwe sana na Mungu aendelee kukupigania.Amen.

 91. Wow! GREAT!
  GLORY TO GOD FOR WONDERFUL ADVICES THROUGH BRO JOHN PAUL.
  I’VE GAIN SOMETHING VERY SPECIAL IN THIS MSG. MAY GOD ADD MORE ANNOINT ONTO YOU MY BROTHER.

 92. Ndugu Shoo GAP,

  Mimi ninaomba kushiriki kujadili katika mada uliyoileta ya kama ni sahihi au si sahihi kwa mkristo kumuombea mchawi afe. Nitakachoandika hapa ni jinsi ninavyofahamu mimi. Kama nitakuwa nimepotoka katika baadhi ya maelezo yangu nitafurahi sana kusahihishwa. Na ikiwa maelezo yangu yatasababisha maswali mengine, maswali hayo nayakaribisha pia, ili tuendelee kujadiliana kwa kujifunza.

  Ninakubaliana na wewe katika sehemu kubwa, kama si yote, kwa yale uliyoyaandika kuhusiana na mwongozo wa maisha ya mkristo, ulioletwa kwetu na Bwana wetu Yesu Kristo. Kuja kwa Yesu kuliondoa baadhi ya mambo yaliyokuwa ni halali wakati wa Agano la Kale, [ kipindi cha sheria], na kuongeza mengine ambayo hayakuwa katika katika Agano la Kale. Mengine yaliyokuwa katika hali ya mwilini wakati wa Agano la Kale, Bwana Yesu aliyaingiza katika ulimwengu wa roho. Mfano mengine yaliyokuwa yakihitajika kukamilishwa kwa matendo, Bwana Yesu aliyaweka katika ulimwengu wa roho, ili kwa kuwaza tu jambo hilo litakuwa limekamilika. Mfano ni katika Mathayo 5:21-22 ambapo kumchukia tu mtu ni hatia sawa na kuua! katika ulimwengu wa roho.

  Mimi ninalichukulia suala la kumuombea mchawi afe ni kumhukumu. Sijafahamu kwa upana (na sina uhakika kama huwa inatolewa) sababu inayofanya mchawi aombewe kufa. [Habari njema ni kwamba si kila maombi Mungu hujibu, bali tu yaliyo katika mapenzi yake]. Kama mchawi anatakiwa aombewe kufa kwa sababu tu ni mchawi, hiyo si sahihi kwa sababu wachawi wengi tu wanaacha uchawi na kuokoka. Sasa hivi suala hili limeenea kila mahali ambapo watu waliokuwa wachawi wanaokoka. Hata nyakati za mapambazuko ya ukristo, kuna mchawi jina lake Simon, alikutana na Injili na akaacha uchawi na kuokoka. [Matendo 8:9-11]. Na ikiwa mchawi anaombewa kufa kwa sababu ni mwenye dhambi, hilo nalo siyo sahihi kwa sababu Yesu mwenyewe alisema hakuja kuuhukumu ulimwengu bali kuuokoa! [Yohana 12:47]. Alikuja kwa wenye dhambi ili waokoke.

  Lakini pia tukisoma maandiko ya Neno la Mungu tunaweza kuona kwamba dhambi ya uchawi ni sawa na dhambi nyingine yoyote mbele za Mungu. Kuna wakati dhambi ya uchawi inalinganishwa na dhambi ya kutokutii….kutokumtii tu Mungu ni sawa na uchawi! [1Sam 15:23]. Kwa hiyo japo kibinadamu tunaweza kuona uchawi ni dhambi mbaya au kubwa zaidi, lakini kumbe Mungu anaona ni sawa tu a dhambi nyingine yoyote. Na kwa kuwa uchawi ni sawa na dhambi nyingine, kumuombea mchawi afe ni sawa na kumuombea mwizi afe, au muongo afe. Na kwa mtindo huu badala ya kuuombea ulimwengu uokolewe, itakuwa ni kuuombea ulimwengu uhukumiwe. Na hili ni tofauti ni kusudi la Yesu kuja ulimwenguni.

  Ninafahamu wachawi wanavyosumbua na kutesa watu, usiku na mchana, masika na kiangazi, come sun – come rain! [Kinachosikitisha ni kwamba mchawi hana faida yoyote na uchawi wake bali ni hasara tupu. Uchawi ni utumishi wa shetani moja kwa moja]. Kutokana na usumbufu huu wa wachawi, labda ndiyo maana watu hufikiria kuwaombea wachawi wafe. Lakini mimi nafikiria INA FAIDA ZAIDI KUMUOMBEA MCHAWI AOKOKE kuliko kumuombea afe! Mchawi akifa kabla hajaokoka huyo atakuwa kapotea milele. Lakini ukimuombea aokoke, na akaokoka, atakuwa amepona roho yake na ataongeza nguvu-kazi shambani mwa Mungu. Wachawi wengi wakiokoka huwa ni watumishi wazuri kwa sababu wanaufahamu vema upande wa pili. Lakini zaidi pia wachawi wakiokoka, yale mateso na usumbufu wanaoufanya kwa watu hautakuwepo pia. Kwa kuwa ninaamini kwamba kinachohitajika ni amani na utulivu. Kwa hiyo kama amani na utulivu vinaweza kupatikana kwa mchawi kuokoka basi haina haja hadi wafe!

  Suala la msingi kwa wana wa Mungu ni kuutafuta kwa bidii uwepo wa Mungu. Mahali palipo na uwepo wa Mungu hapawezi kuwa na mchawi, na hata akiwepo nguvu zake lazima zitatiishwa! Kumuombea mchawi kufa ni kutafuta short cut ya kuleta amani na utulivu maishani. Lakini njia kamili ya kuepuka uchawi ni kujikabidhi mbele za Mungu kwa kuliitia jina la Yesu na kujifunika kwa damu ya Yesu Kristo. [Maneno haya yamekuwa yakidhaniwa kuwa ni ya kejeli kwa baadhi ya watu lakini ajabu ni kwamba wanaokejeli maneno haya ndiyo wahanga wakuu wa uchawi na wachawi]. Hakuna mchawi anayeweza kugusu damu ya Yesu. Wanaifahamu na wanafahamu Moto wake! Mtu ambaye hayuko katika milki ya Yesu, hata kama atawekwa mahali ambapo hapana uchawi, bado hatakuwa na amani na utulivu kwa sababu amani ya kweli huanzia moyoni; na Yesu Kristo ndiye Mfalme wa Amani.

  Jambo ambalo linaweza kumuua mchawi ni kama atakutana na nguvu za Mungu, lakini bado akakaidi na kulazimisha kuendelea katika uchawi wake, ingawa ameshatambua fika kwamba Nguvu ya Yesu aliyokutana nayo ni kubwa kuliko ya uchawi wake. Ushuhuda ufuatao ni mfano hai:

  Mchawi fulani alikwenda nyumbani kwa mwinjilisti mmoja aitwaye Longan Rein, nchini Tanzania. Wakati mwinjilist huyo akiwa amelala usiku alisikia kama amepigwa na teke usoni. Moja kwa moja alitambua kwamba hizo ni nguvu za giza. Alichofanya alikemea, “Upooze kwa jina la Yesu!’ kisha akalala. Kesho yake jioni wazee fulani majirani walikwenda kwake na kumwambia alikuwa anaitwa na mzee fulani, ambaye ni balozi katika eneo hilo. Pasipo kufahamu kinachoendelea alikwenda na kumkuta yule mzee aliyekuwa anamuita [ambaye ni balozi] hawezi kutembea, yuko kitandani amelala. Alipoingia chumbani mwinjilisti Longan alipata ufahamu kwamba ni kwa sababu ya lile tukio la usiku wa juzi yake, kwa kuwa alikumbuka kwamba alikuwa amekemea mchawi huyo apooze. Na huyo mzee, balozi, alikuwa amepooza kweli kweli!

  Yule mchawi alichofanya ni kumuomba msamaha mwinjilisti kwa kitendo chake cha kuwanga usiku na kuwasumbua watu wakati wamelala. Alisihi sana kwamba hakutambua ya kuwa mwinjilisti ana nguvu zaidi kuliko ya yeye mchawi. Bila kuwa na maneno mengi mwinjilisti alimwambia yule mchawi kwamba nguvu ya Yesu ndiyo aliyopambana nayo na usalama wake ni kumwamini na kumpokea Yesu kama mwokozi. Yule mchawi alisema yeye pia anamuamini Yesu kama nabii kwa hiyo hajuwi ni kwa nini anaambiwa amuamini tena. Mwinjilisti alimfafanulia kwamba Yesu ni Mwokozi si nabii tu na Jina lake ndilo linatawala katika ulimwengu wa roho. Yule mchawi hakutaka kukubali. Mwinjilisti alipoona hivyo alimwambia kwamba yeye ameshamsamehe lakini aliyemlaza hapo kitandani ni Yesu. Usalama wake amkubali Yesu ndipo angeinuka pale kitandani. Mwinjilisti alimpa siku saba kufikiria kisha afanye maamuzi na baada ya siku hizo kama hajaamua kukubali anaweza kufa.

  Mwinjilisti Longan alisafiri na aliporudi, baada ya siku 7, siku ile anarudi alikuta ndiyo ilikuwa siku ya mazishi ya yule mchawi ambaye kumbe hakukubali kumpokea Yesu, siku saba zikapita, akafa kweli!

  Mfano huu unaonyesha jinsi mchawi anavyoweza kufa akikaidi neema ambayo Mungu anaweza kuwa kamfunulia. Si wachawi wengi wanakutana na nafasi kama hizi na hata wanaokutana nazo si wengi wanazitambua na kuzifanyia kazi chanya.

  Wana wa Mungu tukikubali kujiweka kikamilifu chini ya damu ya Yesu, nguvu za Mungu ndani yetu na katika maisha yetu zitawakamata wachawi, automatically! Mchawi akishakamatwa na nguvu ya Mungu uamuzi unabaki kwake na kati yake na Mungu. Kwa hiyo mimi nafikiri kwamba jambo la kuombea ni WATU WALIOOKOKA WAWE NA NGUVU ZA MUNGU ZA KUTOSHA ambazo zitafanyika ushuhuda kwa wachawi, na kwa njia hiyo wale wataokubali wataokoka. Lakini kama wakikataa wataangamia wote, si kwa sababu wameombewa wafe, bali kwa sababu wanashindana na Mungu, Yehova!

  Tutakapokuwa wakamilifu mbele za Mungu, upendo wa Mungu utatuongoza kuwaombea hata wachawi waokoke, na si wafe. Halafu Mungu atafanya kwa sehemu yake. Mungu ana njia nyingi za kuifunua neema yake kwa hata wachawi. Kama alivyomkutanisha mchawi yule na mwinjilisti, hiyo ndiyo ilikuwa siku ya mchawi huyo kuokoka. Lakini hakuwa ametambua. Tukiombea wachawi waokoke Mungu atatengeneza mazingira ya wao kuokoka. Na wasipookoka Mungu atashughulika nao. Ikimpendeza mchawi afe ili kuwe na amani mtaani Mungu atafanya hivyo. Lakini ninajua hakika ni kusudi kamili la Mungu kila mtu, atakayekubali, aokoke! Haijalishi yuko katika vifungo vya namna gani vya dhambi.

  Namalizia kwa kusema kwamba si sahihi kwa mkristo kumuombea mchawi afe, bali sahihi ni kumuombea aokoke. Mchawi akishaokoka hapawezi kuwa na uchawi tena na yeye atakuwa ameingia kwenye ufalme wa Mungu.

  Ninashauri waalimu hao wasiwafundishe watu kuwaombea kifo wachawi bali wawafundishe hao wakristo kujitakasa na kumtafuta Mungu ili uwepo wa Mungu uwafunike. Uwepo wa Mungu unatosha kuumaliza uchawi kwa kuwavuta na kuwakutanisha na nguvu za Mungu. Wakishakutana na Mungu uso kwa uso, Mungu atajua la kuwafanya, kutokana na uamuzi wa mchawi atakapokuwa amekutanishwa na nguvu ya Damu ya Yesu Kristo!

  Ninaomba damu ya Yesu kristo imfunike kila mtu anayependezwa na Wokovu wa Yesu, ili asiteswe tena na wachawi [kwa yule ambaye anasumbuliwa] bali awe njia ya wachawi hao kumfahamu Yesu ili nao waurithi uzima wa milele. Amina!

 93. Shalom mimi ninachojua ni kwamba tumeumbwa kwa sura na mfano wa MUNGU na pia tuliumbwa ili tuvitawale vitu vyote.pointi hatujui tutawale vipi kwenye mithali anatuambia “NAWAPENDA WOTE WANIPENDAO NA WANITAFUTAO KWA BIDII WATANIONA UTAJIRI NA HESHIMA VIKO KWANGU NAAM UTAJIRI UDUMUO NA HAKI PIA”Tatizo tunakwenda kwa Yesu kutaka pesa na ndio maana tunazidi kuwa masikini hatumtafuti MUNGU tuna tafuta pesa..

 94. Dada Mary Nyukoi,

  Nashukuru kwa maombi yako ya kunitakia baraka za Mungu. Nimeyapokea! Tuzidi kuombeana katika safari hii ya mbinguni.

  Nilipoandika kwamba kwa kuwa umefanikiwa unaweza kutumia kufanikiwa huko kumuwezesha, niliandika kutokana na wewe kuandika kwamba sasa ‘umeshafanikiwa’. Na kwa kuwa hukuweka wazi kwamba umefanikiwa katika lipi, mimi nikaona nitafsiri kwamba una baraka zote za rohoni na za mwilini, pamoja na kufanikiwa ki uchumi. Na kwa kuwa wewe uliandika kwamba umshafanikiwa, mimi nilitafsiri kwamba kwa kuwa hapa wanazungumziwa watu wawili, basi yule mwenzako atakuwa ‘hayajafanikiwa’. [kwa tafsiri niliyoitoa]. Sikuwa na maana nyingine yoyote ya kwangu, ila nilichoandika ni kutokana na ulivyoandika wewe. Kwa kuwa ki uchumi anajiweza, basi, waweza kumuwezesha kiimani, ambapo tayari unaendelea kumuombea na kumshauri. Endelea na utumishi huo mwema!

  Umeongea neno zito na muhimu sana kwamba kuna wakati pesa huwa haina msaada. Na hili limekuwa mbali na akili ya watu wengi, ambao hukimbia usiku kucha, mcha kutwa wakitafuta pesa, kwa kuamini kwamba akishapata pesa, mambo yote yatakuwa shwari. Kumbe si kweli! Ndiyo maana Yesu anatuambia tuufatute kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake, na mengine tutazidishiwa. Amina!

  Mambo ambayo pesa haina msaada kwayo ni pamoja na magonjwa yasiyotibika mahospitalini pamoja na mashambulizi kutoka katika nguvu za giza. Msaada pekee kwa mambo kama haya ni kukimbilia kwa Yesu na kumlilia Mungu. Kwa kuwa suala hili la kumlilia Mungu tayari unaendelea nalo, mimi sioni kama kuna jambo jingine unaloweza kufanya.

  [Kama mapito magumu anayoyapitia ni mambo yaliyo nje ya uwezo wa kibinaadamu sidhani kama kuna jingine la kufanya. Lakini kama anachopitia unaona kuna namna wewe kama wewe unaweza kufanya, labda ingekuwa vizuri kama ungeandika hapa (ukijisikia amani kufanya hivyo) ni magumu gani anayopitia ili tuone kama kuna nini ambacho wewe unaweza kufanya zaidi ya kumuombea kwa Mungu.]

  Asante.

 95. Kutokana na swali la dada Maria Nyukoi na majibu mazuri aliyoyatoa Kaka John Paul, ninapenda kuuliza swali ambalo waalimu wengi wa Neno la Mungu nimewasikia wakifundisha. Waalimu hawa wamekuwa waki-quote Kutoka.22:18 “Usimwache mwanamke mchawi aishi” kwa hiyo wamekuwa wakiwaombea mabaya wachawi na mambo yanayofanana na haya, au kwa lugha nyingine wanatamani wachawi wote wafe. Huwezi kumwombea mtu mabaya isipokuwa umemchukia na ni lazima ukumbuke kuwa amchukiae ndugu yake ni muuaji.

  MTIZAMO WANGU
  Hii ni torati, na Yesu Kristo anasema katika Mathayo 5:38-48 Mmesikia kuwa watu zamani walikuwa wakisema, `Jicho kwa jicho na jino kwa jino.’……Lakini mimi ninawaambia, wapendeni maadui zenu na waombeeni wanaowatesa, ili mpate kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni…..
  Mahali pengine akasema Yohana 8:7 “Asiyekuwa na dhambi kati yenu awe wa kwanza kumtupia jiwe.”
  Hapa ni baada ya kuletewa mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, kulingana na torati alipaswa kupigwa mawe mpaka afe.

  Warumi 12:17 Msimlipe mtu uovu kwa uovu. Jitahidini kutenda yaliyo mema machoni pa watu wote. Kama ikiwezekana, kaeni kwa amani na watu wote. Wapendwa, msijilipizie kisasi, bali mtoe nafasi kwa ghadhabu ya Mungu, maana imeandikwa:“Kisasi ni juu yangu; Mimi nitalipa, asema Bwana. Badala yake, adui yakoakiwa na njaa, mpe chakula; akiwa na kiu, mpe kitu anywe. Maana ukifanya hivyo, utampalia mkaa wa moto kichwani pake. Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.(KUMBE 1.KISASI NI JUU YA MUNGU 2.ILI KUMPALIA MKAA MTENDA MABAYA MTENDEE MEMA or UBAYA HUSHINDWA KWA WEMA)

  YESU ANAPENDA WATU WOTE WOTE KABISA, ILA ANAICHUKIA DHAMBI SANA.

  SWALI
  Mkristo kuomba mchawi afe ni sahihi? Wachawi hawawezi kuokoka na kumgeukia Yesu?

  NOTE: Ninaichukia dhambi yeyote including uchawi, lakini nawapenda watu wote.

  NINAWAZA VIBAYA?

 96. Asante sana Kaka Paul you seems to have wisdom ya hali ya juu Mungu akubariki, Naomba nikujibu hivi
  KUhusu kumueleza alivyochangia kuniumiza tayari hilo nilishamweleza kitambo kabla hata hajaanza kuwa katika hali hii. na tumesameheana ila truly speaking sikumweleza kwamba niliwahi kuomba kwa jinsi ile.

  Unajua wakati mtu anapokuwa kwenye shida kila mtu ataongea lake kukutia moyo au kukusema vibaya. So i was confused na wengine wakanitia moyo tu kwamba nisimchukie nizidi kumpenda na nimuombee kkwa sababu ni ibilisi ndiye anayemtumia:Thanks again kwa kunielewesha hili.nimejifunza kitu.NI kweli nilimuomba MUngu ampitishe ili ajue maumivu alonisababishia na liwe fundisho asifanye kwa mwingine SIKUOMBA KUMDIDIMIZA. UMENIKUMBUSHA NA NIMEONA KWA MACHO KUWA APANDACHO MTU NDICHO ATAKACHOVUNA. Hujakosea kuhusu delivarence, ni kweli nikiwa kwenye mapito sikuacha kumwomba Mungu na nilifunguliwa kwenye semina moja ya maombi.nikapona magonjwa na milango ya baraka kufunguka nikamwomba Mungu Roho ya msamaha, nikamsamehe na nikampenda zaid yule ndugu hadi nikamshangaa Mungu. Ndipo baadaye nikamweleza alivyonikwaza, akaniomba radhi pia. from that time imepita takribani miaka miwili ndipo yakamsibu haya.
  KUhusu kumuwezesha sijui unamaanisha kivipi manake kama kiuchumi anajiweza kabisa i can say ni tajiri, ni matatizo ambayo pesa haina msaada. Unajua kuna wakati pesa unayo lakini haikufaidii kitu, hapo ndio mahali unafika na kusema kweli dunia na vyote viujazavyo ni mali ya Mungu, coz psa, magari, majumba, kazi, vyote vipo but still mtu yupo kwenye shida kulio yule maskini asiye na mbele wala nyuma ila tu nazidi kumtia moyo na kumuombea afunguliwe pia.

 97. Mpendwa Maria Nyukoi,

  Mimi naomba kushiriki katika mchango wako ulioutoa hapa, ukiuliza ufanye nini, hasa baada ya kuona kama kuna jambo linalotokea ambalo unaamini ni wewe umelisababisha.

  Mimi nafikiri kwamba wakati unamuomba Mungu ampitishe huyo mtu wako wa karibu kwenye hali uliyokuwa unaipitia, ulikuwa na maana akishaipitia ataona uchungu wake na hivyo ajifunze ili asisababishe tena hali hiyo kwa mtu mwingine. Kama hili ndilo lilikuwa kusudi lako, mimi sioni kama kuna tatizo, maana somo analolipitia likikamilika, Mungu atamuinua kutoka huko. Kama kuomba kwako ulikuwa na maana akishapitia kwenye hali hiyo ngumu uliyoipitia abaki huko huko hadi mwisho wa maisha yake, hapo yawezekana uliomba vibaya kwa sababu Bwana Yesu anatufundisha kuwabariki wanaotulaani na kutolipa baya kwa baya na mengine mengi kuhusu kuwa sababu ya baraka kwa wengine.

  Jambo moja ambalo linanisikitisha hapa ni vile ulivyosema kwamba ibilisi alimtumia huyo mtu wako wa karibu ili kukuingiza katika magumu WAKATI WEWE UMEOKOKA NAYE [mtu wa karibu] AMEOKOKA. Hapa ninapata tabu sana kwamba iweje mtu aliyeokoka atumiwe tena na ibilisi? Mtu kutumiwa na Ibilisi maana yake ni chombo cha ibilisi. Sasa mtu akiokoka, halafu bado awe ni chombo cha ibilisi, hapo kuna walakini katika wokovu wa mtu huyo. Ninafahamu kwamba wapo watu wanaojiita wameokoka lakini ni makwazo makubwa kwa ndugu, jamaa na marafiki zao. Wokovu huu mimi nauwekea question mark! Sielewi ni kwa jinsi gani mtu ambaye Kristo yuko ndani yake naye yu ndani ya Kristo kisha tena awe chombo cha ibilisi…

  Maana yangu nyingine ya kuandika namna hii ni kwamba ikitokea mtu aliyeokoka akawa sababu ya kumpatia mpendwa mwingine wakati mgumu, tusimtupie ibilisi mzigo, bali tatizo ni la huyo huyo mtu, kushindwa kuishi maisha makamilifu ili asiwe kwazo la namna yoyote kwa mwingine. Kufikiri kila tabia mbaya iliyo ndani ya mtu ni ibilisi kunawafanya watu wakwepe wajibu wao wa kujitahidi kwadri wanavyoweza, kwa kumuomba Mungu, ili wawe ni watu wanaofanyika baraka kwa mwingine. Siamini kama mtu aliyeokoka na anaishi maisha makamilifu, anaweza kutumiwa na ibilisi pasipo yeye mwenyewe kukengeuka kwa kuiacha njia ya kweli!

  Yule mtu wako kuwa katika mapito makali zaidi ya yale uliyopitia wewe si lazima iwe ni kwa sababu ya maombi yako. Yawezekana anavuna alichokipanda… Na hii ni kanuni ya Mungu. Lakini kama nafsi inakushitaki kuwa pengine uliomba vibaya, unachotakiwa kufanya ni hicho ambacho tayari umeshaanza kufanya, yaani kumuomba Mungu amfungue.

  Lakini jambo jingine ni kwamba inabidi suala hilo liwe wazi kati yenu wawili. Sina uhakika kama yeye anafahamu kwamba alikuwa sababu ya wewe kupitia katika magumu uliyopitia. Kama hafahamu inabidi uliweke wazi ili akishaelewa akuombe msamaha, nawe umsamehe [kama bado hamjafanya hivyo]. Na mlango wa hili uko wazi maana yeye anakushirikisha kwa kila jambo.

  Suala jingine ni pale uliposema kwamba ulipitia katika magumu hayo ukiwa ndani ya wokovu lakini before deliverance. Kwa kuandika hivi inaonyesha kwamba kuna deliverance fulani uliyoipitia ndipo ukawa katika hali uliyo nayo sasa. Kwa hiyo kama unafahamu ni some kind of deliverance ndiyo iliyokufungua, kwa nini usimueleze na huyo mtu wako wa karibu kupitia deliverance hiyo ili na yeye atoke huko aliko? [Sijaelewa unaposema ‘deliverance’ unamaanisha nini. Ni kwa sababu ya kutokuelewa huko ndiyo maana nami nimeona niitumie hivyo hivyo, ili nisijepoteza maana uliyokusudia].

  Jambo jingine ninaloshauri kwamba unaweza kufanya ni kumuwezesha. Kwa sababu wewe unasema umeshafanikiwa, basi unaweza kutumia kufanikiwa kwako ili umfanikishe na yeye. Wakati mwingine mtu anaweza kupitia katika magumu kwa sababu ya kukosa mtu wa kumuwezesha kuvuka hapo!

  Huu ndio ushauri wangu kwa sasa na ninakupa hongera kwa kufanikiwa!

 98. JE NILIOMBA VIBAYA?
  Bwana Yesu Asifiwe,Mie nina swali tofauti na mjadala hapo juu.
  kuna kipindi niliwahi kupitia magumu sana katika maisha ambayo ibilisi alimtumia mtu wangu wa karibu sana. niliteseka mno hadi nikapata magonjwa ya stress. wakati nikipitia mateso hayo nilikuwa nikimlilia Mungu sana, na wakati nikimlilia Mungu niliwahi kuomba kwamba MUngu ampitishe yule mtu kwenye hiki ninachopitia ili aone uchungu ninao upata. Ni miaka imepita Namshukuru Mungu niko safi na nimerudia hali ya kawaida tena nimefanikiwa. Ajabu ni kwamba yule mtu ana mapito makali zaidi yangu lakini yanafanana sana na yale nliyopitia. Naumia na kuteseka sana kwa hali aliyonao bcoz naelewa kwa sababu nilikuwa huko before deliverance(kumbuka yote yalinitokea nikiwa ndani ya wokovu na bado nimo na huyo mtu ni mpendwa). Sasa imeniathiri sana nahisi nafsi inanishtaki kuwa pengine niliomba vibaya kile kipindi nikiwa kwenye mapito yangu. nimekuwa nikiomba sana kwamba Mungu amfungue na amekuwa akinishirikisha kila jambo bila ya yeye kujua nawaza nini. NIfanyeje? Mungu awabariki

 99. shaloom watu wa MUNGU mbarikiwe sana.nawaomba wenye maswali watoe tuendelee kujifunza,amen mbarikiwe sana

 100. Mi leo sina mengi ya kusema ndugu zangu ili “MSINGI ULIYO IMARA NDIO HUU KILA ALITAJAE JINA LA BWANA NA AUCHE UOVU” Simama hapo ulipo kwenye kweli ya MUNGU.

 101. WATU WANGU WANAANGAMIZWA KWA KUKOSA MAARIFA…hili neno linafaa sana kizazi chetu kwa yote yanayotokea.Niseme kidogo tu kuwa nyakati tulizo nazo watu watakaoshinda ni wale ambao NENO LA MUNGU KWAO NI MKATE WA UZIMA NA HEWA YA KUVUTA(H20)

 102. Mi nadhani tusienende ktka mwili,tusimame hapo tulipo maana kila kukicha utasikia jipya.Tumuombe mungu sana.

 103. Mungu ametutuma tueleze kweli yake kwa watu wote na kila aliyeitwa na Mungu,lazima ataelezwa jinsi ya kuenenda ile kuwaleta watu kwa Yesu kwani.Siwezi kusema chochote ila Roho wa Mungu ndie mwamuzi ayajuaye yote na ndie mwamuzi wa kweli.Jinsi Mungu alivyo waita mimi sijui ila,
  Yesu yupo wazi kwetu amesema msitafute umaarufu ulimwenguni Roho wa Mungu akiwa ndani ya mtu ndiye mwamuzi wa kweli huyo atatupa amani na maamuzi ya kufanya.Amani ya Mungu iwatawale rafiki zangu wote basi Yesu na atutawale nafsini mwetu.

 104. Tunaishi ktk wakati wa hatari sana. Mpinga Kristo amekuja juu ya farasi wa kijivujivu (rangi ya udanganyifu sana, ni kuchanganya NYEUSI KABISA NA NYEUPE KABISA = KIJIVUJIVU). Kama maandiko yalivyosema, hizi roho (Roho wa Kweli na roho ya mpinga kristo) mbili zingefanana sana hata zingempoteza aliye mteule kama YAMKINI. Shetani anaweza kuigiza Neno asilimia 99.99, kama tu alivyofanya kwa Hawa. HAYA BASI, WOKOVU BANDIA UMEJAA MIMBARANI.

 105. Bwana Yesu asifiwe wapendwa katika blog hii.
  Nimekuwa mchangiaji kwa karibu miezi kadhaa sasa na kwa kweli nimebarikiwa sana na mijadala ya kujenga inayoendeshwa humu. Niwashukuru sana wapendwa John Paul,Charles Mapunda,Bandio,dada Noela na wengine wengi wenye michango ya moto mno ambayo kama ingekuwa ni ya wazi kama kwenye TV ama Radio nadhani ingejenga sana ufalme wa Mungu na kuubomoa ufalme mwovu wa shetani na malaika zake.
  Kabla sijauliza swali leo niguswe kutoa pendekezo kuwa pengine muda sasa umefika nasi wa blogu hii tukaamua kupanua wigo kwa kuendesha kama si mijadala basi tathmini ya mwenendo wa kanisa hapa Tanzania ili kuleta radha tofauti katika kuieneza injili ya Yesu Kristo. Watu wengi sasa wanaangalia televisheni na kusikiliza radio hata vijijini. Ninadhani sasa ni muda muafaka kwa kombania hii ya blogu hii tukaamua kwenda huko nako ili tusaidie kulijenga kanisa. Ninasema hivyo kwa kuzingatia kuwa kwa miaka kadhaa ambayo waendesha madhehebu na huduma mbali mbali wamesaidia kuleta uamsho mkubwa wa kiroho katika nchi yetu na ulimwenguni kwa ujumla lakini kwa sehemu wamekuwa na mapungufu ambayo sisi tumeyaona na tukayajadili kwa kina sana, mambo haya yangekuwa yanajadiliwa kwenye radio na televisheni kanisa lingepona ama kupata nafuu sana kwa baadhi ya mafundisho manyonge wanayopata wenzetu makanisani na kwenye vipindi mbali mbali.

  Sasa niulize swali ambalo ninadhani litafungua tena fahamu na maarifa makubwa ambayo Mungu ameweka ndani yenu enyi watumishi wa Mungu Baba wa Bwana na Mwokozi wetu Yesu kristo.
  Ninaye rafiki yangu mmoja wa kanisa fulani la kipentekoste hapa Korogwe siku moja alinieleza jambo la ajabu kweli hata ingawa hakusema kwa msisitizo. Yeye aliniambia kuwa wanatheolojia wengi wanaamini kuwa Adamu si mtu wa kwanza kuumbwa duniani bali ni mwanzo wa historia ya wokovu.
  Siku kadhaa zilizopita nimepata mafundisho kutoka Church of God in America yanayolingana na mtazamo huu wa mchungaji huyo. Katika kitabu kiitwacho THE TRUTH OF THE BIBLE(IS THE BIBLE TRUE?) kuna maneno haya;
  The age of the universe
  Man’s misguided theory of the structure of the universe was the first
  major astronomical controversy that pitted science against religion. Many
  more controversies followed. One of the most hotly debated concerned
  the age of the universe.

  Astronomers see evidence that the universe is many billions of years
  old and generally believe that it came into existence between 10 and 20
  billion years ago through an event commonly called the Big Bang. On
  the other hand, some Bible believers, embracing a particular interpretation
  of Genesis 1 and other passages, dogmatically maintain that the
  universe is only about 6,000 years old. This figure is calculated from
  the chronological benchmarks in Genesis and other books of the Bible.
  Astronomers respond that this view is insupportable. They offer evidence,
  gathered from viewing the heavens by powerful telescopes, that
  support their position. Asks one, “How is it that there are astronomical
  objects more than 6,000 light-years away?” (Sagan, p. 28). A light-year
  is the distance that light, moving at 186,000 miles per second, travels
  in one year.

  It is obvious there are light-years between some religious people
  and science on this issue. Some advocates of the biblical record reason
  around such evidence by stating that the seeming age of the universe
  (and of the fossil and geological evidence of the earth itself) is attributable
  to an “appearance of age” that God built into His creation. Many
  people, including some theologians, properly respond that, if this is the
  case, God would be engaged in a form of deception.
  Yet such arguments are unnecessary. The truth is that the Bible does
  not contradict scientific evidence, and science does not disprove the biblical
  record. The point most people on both sides of the argument miss
  is that the Bible does not say when the universe was created.
  According to the Bible, Adam was the first man (1 Corinthians 15:45;
  1 Chronicles 1:1), and adding the figures in the biblical genealogies does
  yield a date of about 6,000 years ago for Adam’s creation.
  However, the Bible does not state that the creation of mankind and
  the creation of the universe occurred at the same time. The age of the
  universe is simply not stated in the Bible. It may well have been 10 or 20
  billion years ago.

  The “Big Bang” is the most popular current idea advanced to explain
  the creation of an enormous and majestic universe. Yet the theory
  acknowledges that the universe came into being at a specific moment,
  even though those who support the theory but don’t believe in God
  cannot explain the origin of the material from which the Big Bang
  supposedly proceeded or how the universe came about.
  So scientists’ conclusions actually agree with the Bible’s statements
  that there was a specific moment of creation.

  In the beginning
  Let’s look at Genesis 1 and see what the often-misunderstood creation
  account really says.
  “In the beginning God created the heavens and the earth. Now the
  earth was formless and empty, darkness was over the surface of the
  deep, and the Spirit of God was hovering over the waters” (Genesis
  1:1-2, New International Version).
  The first statement in this account refers to God’s initial creative act.
  No exact time is given as to when this took place. What is evident, from
  comparing this passage with other scriptures, is that between verses 1
  and 2 something happened to render the earth “formless and empty”
  [in Hebrew, tohu and bohu].

  Isaiah 45:18 tells us that God “did not create [the earth] a chaos
  [tohu], he formed it to be inhabited” (New Revised Standard Version).
  The initial creation was followed by destruction and chaos.
  The New International Version’s footnoted alternate reading for verse
  2 is, “Now the earth became formless and empty . . .” This indicates
  a time difference between the original creation described in verse 1
  and the time leading to the creation of man beginning in verse 2 (see
  “Earth’s Age: Does the Bible Indicate a Time Interval Between the First
  and Second Verses of Genesis?” beginning on page 16).
  We are not told exactly when the initial creation took place. But
  the Bible hints that the original creation was followed by widespread
  destruction brought about by the rebellion of the powerful angel Lucifer,
  who became Satan (Isaiah 14:12-15). Thus the account of Genesis
  1:3-31 is apparently a description of a restoration of the earth as a habitable
  planet just before the creation of man (see Psalm 104:30). Biblical
  genealogies indicate that this occurred approximately 6,000 years ago,
  though nowhere does the Bible tell us when God first created the heavens
  and the earth.

  God’s Word does reveal that initially there was no physical creation—
  no earth, no solar system, no galaxies. The apostle Paul describes this as
  “before time began” (Titus 1:2). Then, by divine command, God created
  the universe.
  Science tells us something similar. “These days most cosmologists and
  astronomers back the theory that there was indeed a creation . . . when
  the physical universe burst into existence in an awesome explosion popularly
  known as the ‘big bang’ … The universe did not always exist” (Paul
  Davies, God and the New Physics, 1983, pp. 10-11, emphasis added).
  Both of these accounts, one from science and one from the Bible,
  speak of an instantaneous origin of the physical creation. (To learn
  more, download or request our free booklets Life’s Ultimate Question:
  Does God Exist? and Creation or Evolution: Does It Really Matter
  What You Believe?)

  Why was the universe created?
  Science cannot of itself tell us why the earth and the physical creation
  exist. Wrote Carl Sagan: “Why it happened is the greatest mystery we
  know. That it happened is reasonably clear” (Cosmos, 1980, p. 246).
  But the Bible tells us why! “You are worthy, O Lord, to receive glory
  and honor and power; for You created all things, and by Your will they
  exist and were created” (Revelation 4:11). Psalm 115:16 adds, “The
  heaven, even the heavens, are the Lord’s; but the earth He has given
  to the children of men.”

  God created all things. He set aside the earth as a place of habitation
  for man, for the working out of His purpose. His plan is ultimately
  to bring “many sons to glory” (Hebrews 2:10), to offer sonship to all
  people through His Son Jesus Christ. This is the reason God brought the
  creation into existence by His command. The Bible explains God’s plan
  in considerable detail—as well as that plan’s implications for us. (For a
  more complete explanation, request or download our free booklet What
  Is Your Destiny?)

  The Bible holds true in its description of the origin of all things. In
  response to the statement that God in the beginning created the heavens
  and the earth, one skeptical scientist stated, “But no one was there to see
  it” (Davies, p. 9). Not true—God and His angels were there. No human
  being there was to refute it, and there is no one who can refute it today.
  No man or woman has disproved the Bible. But there is a mountain of
  evidence to show it is true.
  Wapendwa mnasemaje kwa hili?

 106. Bwana Yesu asifiwe;

  Wapendwa katika Bwana kuhusu watumishi wanaowaita watu kwa kuwaahidi vitu kama MUME,MKE,UTAJIRI,KWENDA ULAYA,NA KUWATOZA FEDHA WATU ILI WAWAOMBEE NK. Mimi nina mashaka nao kwasababu biblia inasema mtawatambua kwa matunda yao,

  Yesu alisema mmepewa bure toeni bure sasa hawa ninasema si watumishi wa Mungu,bali ni watumishi wa hivyo vitu watu wa Mungu tuwe macho,Injili ya kweli inawafundisha watu kuhusu Dhambi,haki,hukumu sio vitu.

 107. Shalom!!
  Dada Rose, Ukimpokea Bwana Yesu unafanyika kuwa kiumbe kipya, ya kale yanapita, amani ya kweli inapatikana kwake, hasa tunapokuwa tukimfurahisha Yesu kwa kutenda mambo matakatifu, masafi kwa kuwa tunaongozwa na Roho Mtakatifu ambaye ni kiongozi, mshauri wetu wa kweli.

  Ukiitegemeza amani yako kwa mtu tena pengine kwa kushirikiana naye dhambi ni hatari sana dada na matunda yake ni machungu mno.

  Mwombe Roho Mtakatifu akusaidie kukupa mwongozo hasa pale unapokuwa huna hakika,atakusaidia kujua yaliyo mapenzi ya Mungu na yasiyo.

  Mdo 16:13
  ‘Lakini yeye atakapokuja huyo Roho wa kweli atawaongoza awatie kwenye kweli yote’

  Galatia 5:16
  ‘Basi nasema enendeni katika roho hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili’

  Bwana Yesu pekee aweza kutupa utoshelevu usio na hasara. Kuna wakati lazima tukubali kuusulubisha mwili na tamaa zake na ndipo Yesu anapoinuka na kutupigania, ni lazima tutambue kuwa muda wa kumtumikia shetani na udanganyifu wake umekwisha.

  Usitafute boy friend, bora usubiri mume toka kwa Bwana ambaye atapita katika taraibu za kiMungu na usafi akiheshimu mwili wako mpaka siku ya ndoa.

  Kwa sasa ni vema kama utakubali Bwana Yesu awe mume wako, ni mwminifu, mtoshelevu wa ajabu
  ‘ATOAVYO YEYE SI KAMA DUNIA ITOAVYO’
  Bwana Yesu Awabaiki sana

 108. Kwako Rose,

  Kama ulikuwa umeshakiri habari ya wakovu halafu bado ukawa na boyfriend natumaini alichoandika ndugu Bernard Mwenda kinaweza kabisa kukupa msaada na mlango wa kuondoka katika njia panda ambapo umenasa ili uendelee na safari. Lakini kama ulikuwa na boyfriend kabla ya kuokoka ushauri wangu ni huu ufuatao:

  Kama ulikuwa na boyfriend kabla ya kuokoka na labda ukalazimika kuachana naye baada ya kuokoka [hata hivyo sifahamu kama kuna sababu yoyote ya kumfanya mtu aliyeokoka aendelee na matendo yake ya giza]suala lako lina maswali mengi ambayo baadhi ya majibu yake unayo wewe mwenyewe. Na katika kutafakari maswali haya natumaini unaweza kujitambuwa kwamba katika njia panda uliyopo unachotakiwa ni kurudi nyuma [kugeuka]; au ni kuendelea mbele au ni kukata kushoto au kulia. La kuchunga ni isije tu ikawa hapo njia panda ndiyo uwe mwisho wa safari yako!

  1. Unapomuomba Mungu akusahaulishe, unamuomba Mungu akusahaulishe nini?
  Wakati mwingi huwa haiwezekani kusahau kitu kizuri. Inabidi kitu ukiweke katika mazigira ya ubaya ndipo itakuwa rahisi kukisahau. Wana wa Israel walipokumbuka Misri walikumbuka samaki, matango, matikiti, mboga na vitunguu na vitunguu saumu [Hes 11:5]. Wakiwa katika jangwa halafu chakula cha kikiwa ni mana peke yake ilikuwa ni lazima kukumbuka chakula kile cha Misri.

  Mtume Paul anasema katika Waraka wake kwa Wafilipi 3:7-8 kwamba , “Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo. Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kimjua Kristo Yesu, Bwana wangu, ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo”

  Hivi ndivyo mtu akiokoka anatakiwa kuyataza mambo yote ya nyuma. Uzuri wote ambao wakati huo ulikuwa unaonekana, anatakiwa augeuze kuwa takataka ukilinganishwa na uzuri wa Kristo. Mtu akishafikia hali hii nguvu ya kusahau hujengwa ndani yake na hivyo hakuna haja ya kumuomba Mungu tena kwamba alete usahaulifu. Hata ikitokea kumbukumbu haitakuwa na mdhara yoyote bali itaongeza nguvu zaidi ya kusonga mbele katika Bwana kwa sababu ya hasara iliyo katika mambo hayo ambayo yalionekana kuwa ni mazuri wakati huo wa maisha katika dhambi.

  Kwa hiyo badala ya kuomba Mungu akusahaulishe, nakushauri omba Mungu awashe tambi zake zimulike moyoni mwako ili uweze kujua jinsi ambavyo dhambi ni kitu cha kuchukiza. [maneno haya yako katika kitabu cha nyimbo; Tenzi za Rohoni wimbo namba 59 kifungu cha 3]. Ukishaona jinsi ambavyo maisha ya dhambi [pamoja na girlfriend na boyfriend] ni ya kuchukiza hutaweza kukumbuka tena!

  2.Hiyo hamu ya kuwa na mtu mwingine unapoikosa ni hamu ya kuwa na mtu mwingine kama mume au kama boyfriend tena?

  Kama jibu lako ni hamu ya kuwa na mtu mwingine kama mume inabidi utulie mbele za Mungu. Moto wa kuolewa ukiwa mkubwa sana ndani yako unaweza kuingia mahali kichwa kichwa halafu ndoa yote ikawa ni balaa tupu. Lakini kama jibu lako ni hamu ya kuwa na mtu mwingine kama boyfriend basi ujuwe ndani yako kuna tatizo bado. Na hapo nakurudisha tena kwa aliyoandika ndugu Bernard Mwenda.

  3.Unapomuomba Mungu amalize tofauti halafu unakuwa na amani,i). ni tofauti gani hizo? ii). je, amani huja kabla au baada ya tofauti kumalizwa? ii).ni hatua gani huwa unachukuwa baada ya kuwa na amani kutokana na wewe kumuomba Mungu amalize tofauti?

  i).Kama wewe umeokoka tofauti moja kubwa sana na ambayo inaweza kuleta mustakabali wa maisha yako ya kiroho ni kama huyo ndugu hajaokoka bado. Tofauti zingine zilizopo kati ya watu baadhi zaweza kuwepo hata kwa watu waliookoka. Kama bado hajaokoa sijuwi ni kwa namna gani huwa unapata amani pasipo huyo mtu kuokoka. Maana haiwezekani kwamba huwa ukiomba ndugu huyo huwa anaokoka halafu anarudi dhambini tena. Jibu hapa unalo wewe.

  ii).Kama nilivyosema tofauti kubwa na ya kujihadhari nayo ni kama huyo ndugu hajaokoka. Ni kwa namna gani tofauti hizo humalizwa kisha nawe ukapata amani? Jibu hapa pia unalo wewe.

  iii).Baada ya wewekupata amani kutokana na maombi yako kuhusu tofauti zilizopo, ni hatua gani wewe huchukua? Isije kuwa unapoona kama tofauti zimemalizwa [kwa vigezo ulivyonavyo wewe] huamua kurudisha tena mahusiano na mtu huyo. Kama ndivyo huwa unafanya, rejea aliyoandka ndugu Bernard Mwenda. Lakini kama amani huja baada ya tofauti kumalizwa na kama hata pasipo kurudiana naye huwa una amani tayari ni kwa nini tena uendelee kumkumbuka? Halii inaoyesha huwa kuna kitu unafanya ambacho dhamiri yako inakushuhudia kwamba si chema.

  Namaliza kwa kusema kuwa huwezi kujuwa ukweli kuhusu suala hili hadi umejiweka kikamilifu kwa Mungu. Ukiwa kwa Mungu ndipo utafahamu kwamba amani ambayo huwa inakuja moyoni mwako ni amani feki au ni ya kweli. Ukishathibitika katika Mungu utaifahamu kweli na kweli itakuweka huru ili uwe na uwezo wa kuchangua lililo jema!

 109. Rose,

  Unachotakiwa kufanya ni kutubu dhambi zako kwa kumaanisha kuziacha kabisa.

  Watu tunaotarajia kwenda mbinguni, hatupaswi kuwa na dhambi ya aina yoyote kabisa, hii ni pamoja na kutokuwa na boy friend au girl friend. Tunaruhusiwa kuolewa au kuoa! Kama ulikuwa na boy friend, ulikuwa katika dhambi, na iwapo unakosa amani baada ya kuachana na huyo boy friend, anayekukosesha amani si Mungu bali ni adui ibilisi; anataka uendelee kuwa katika dhambi. Ukiwa katika njia za Mungu, yeye ni wa amani.

  Cha kufanya; tubu dhambi zako zote mbele za Mungu kwa kumaanisha kuziacha kuanzia sasa , na umwombe Yesu Kristo kwa bidii kuwa akupe ushindi dhidi ya dhambi zote, kwa sababu yeye aliishi hapa hapa duniani bila kutenda dhambi akiwa katika mwili huu. Kisha tafuta kanisa linalohubiri kweli yote, na uwaeleze nia yako ya kukaa katika njia ya utakatifu, watakusaidia.

  Kuna makanisa mengi siku hizi, viongozi wake wamekuwa ni wachanga kiroho; hawajapata Neno kwa wingi na wanaanzisha makanisa, matokeo yake washirika wao wanakuwa katika hali ya kutokujua lipi la haki na lipi lisilo la haki. Mahali kama hapo baada ya kupata msingi wa wokovu, tusikubali kuendelea kukaa, tukikubali hatimaye tutakufa kiroho.

  Nakupa changamoto Dada Rose; usiogope, tafuta mahali palipo na kweli yote utabarikiwa sana.

  Shalom!

 110. Shalom!
  Nimewahi kuwa na boyfriend. Tatizo langu baada ya kuachana naye sina amani ya kuwa na mtu mwingine. Na ni muda mrefu umepita. Na kila nikimsihi Mungu anisahaulishe nakosa amani, ila nikimwomba Mungu amalize tofauti zetu napata amani. Je, nifanyeje ili kujua ukweli kuhusu hili?Naomba ushauri wenu kwa sababu niko njia panda. Nifanyeje?

 111. Ni kweli mpendwa John Paul, ili mada hii iwe na changamoto nzuri, anachotakiwa kufanya ndugu yetu David Moses, ni kutufundisha kile anachokiamini yeye katika imani ya usabato, kisha maswali yatapatikana kutokana na kile atakachokuwa ametufundisha au kutuelewesha. Nadhani tukianzia hapo tutakuwa na mwanzo mzuri,hata miongoni mwetu tusioijua misingi ya imani ya usabato, tutaweza kuwa na nafasi nzuri ya kuielewa na pia maswali yatakuwa rahisi kupatikana.

  Naamini atatumia zaidi maandiko ya biblia kama alivyosema, ambayo hata sisi wengine tutakuwa na nafasi ya kuuliza au kuunga mkono kutokana na maandiko hayo.

  Kama alivyotoa dondoo za maswali hapo juu, mimi binafsi ningefurahi iwapo angeanzia somo lake hapo, ili tujifunze na kujua Wasabato wanaamini nini katika maeneo hayo, na kisha tuendelee maeneo mengine.
  Shalom!

 112. Mpendwa David,

  Nashukuru sana kwa kunitakia baraka za Mungu.

  Samahani kama kwa namna moja au nyingine ninaweza kuleta usumbufu kwa sababu ya haya ninayoandika kama ifuatavyo:

  Mimi nilichokuwa nategemea ni kupata mambo [facts] ambayo hayo ndiyo yaaminika kuwa hivyo kutokana na imani ya Kisababto. Nilitegemea kupata mfano wa haya hiki kifuatacho nilichoorodhesha:

  1. Wasabato huamini mtu akifa anakwenda peponi
  2. Wasabato hunaamini Sabato ya agano la kale ndiyo sabato ya agano jipya.
  3. Wasabato tunaamini kazi ya Roho mtakatifu ni fulani na fulani,…

  …na kuendelea kutokana na hayo ambayo mtu akiyaona ndipo anaweza kuona tofauti iliyopo kati ya imani Usabato na imani nyinginezo.

  Mimi, kwa uzoefu nilionao, mtiririko huu husaidia sana katika kujifunza. Baada ya kuwa umeandika hivyo ndivyo msomaji fulani angependa labda kufahamu zaidi kwamba ni kwa nini Wasabato mnaamini mtu akifa huenda peponi wakati kwenye imani yake au kwenye Biblia imeandikwa mtu akifa anakwenda mbinguni (huu ni mfano tu). Na hapo ndipo ungekuwa na jukumu la kuelewesha na kama naye ana maswali zaidi anaweza akaendelea.

  Kwa mawazo yangu naona utaratibu kama huo unaweza kutusaidia kujifunza kwa utaratibu mzuri wenye manufaa ya kujenga. Maswali uliyoyaweka, mimi naona ni mazuri tu, lakini nafikiri kwamba yanatakiwa kujadiliwa na watu ambao tayari wanafahamu utofauti wao na/au kufanana kwao katika masuala ya imani. Kwa sababu mtu anaweza kujibu tu kumbe jibu lake ni kutokana na imani yake na hivyo linaweza kuwa ni tofauti na la mwingine ambaye naye katika imani yake anauelewa na msingi tofauti juu ya jambo hilo hilo. Hali kama hii ya kujibizana pasipo kufahamiana kama mna msingi unaolingana au unaotoautiana kiimani inaweza kuleta malumbano tu ambayo jumla yake si kujifunza bali ni kuonyeshana tu ni nani zaidi!

  Natumaini tukifanya kwa utaratibu mzuri mada inaweza kuwa na manufaa sana.

  Mbingu ni moja, Mungu ni mmoja na Yesu ni mmoja; Kwa sababu hiyo basi sisi ambao wote husema tunaamini katika Mungu Yeshova, Mungu wa Israel, Mungu aliyewatoa wana wa Israel utumwani Misri kwa mkono wa nguvu, Mungu aliyemtuma Yesu Kristo kuja duniani kwa ajili ya kuleta wokovu [kitu ambacho natarajia hata wasabato huamini hivyo] tunatakiwa kutafakari kwa pamoja ili kuona kama ni kweli tuko katika njia moja au kila mtu ana njia yake tofauti na ya mwingine huku tukijifariji kwamba njia hizi tofauti kule mbele zinaungana na kuwa njia moja! Kwa sababu pengine yawezekana njia [imani] hizi zote zinaelekea sehemu moja lakini yawezekana pia njia hizi zisiwe zinaelekea sehemu moja. Na kama ndiyo hivyo basi ni lazima kila mtu kuzingatia kwamba anatakiwa kuhakikisha yuko katika njia sahihi ili asije kupotea wakati siku yake itakapofika.

  Namalizia kwa kusema kwamba kwa kuandika maneno haya sina maana kwamba ni mimi tu ndiye ninayetakiwa kuwa ninajadiliana na wewe bali ninapenda kuchangia katika kuweka mwanzo mzuri ili na mwisho uwe mzuri pia. Yawezekana nisiwe na swali lolote kwako na yawezekana pia nikawa na maswali kwako lakini kama nitakuwa na au sitakuwa na swali lolote ninaamini yuko mtu mwingine anayesoma hapa ambaye naye angependa kufahamu zaidi Kuhusu Usabato au Msabato ambaye anapenda kufahamu kuhusu imani zingine zilizotofauti na Usabato.

  Tukishirikiana kwa pamoja tunaweza kufanya jambo zuri ambalo mwisho wake litakuwa ni la baraka kwa kila mtu.

  Narudia tena kuomba msamaha kama kwa namna moja au nyingine maneno yangu haya yanaweza wa yameleta usumbufu.

 113. Ndugu John Paul, ahsante sana kwa ujumbe wako ambao umesisitiza mimi kuwepo hewani kwa kujibu na kuuliza maswali. Pia umeomba angalau nikutajie mambo ya msingi ambayo usabato unaamini na unafundisha na ambayo ndiyo yanaitofautisha na imani zingine.
  1. mtu anapokufa anakwenda wapi? 2. sabato ya agano la kale ndiyo sabato ya agano jipya? 3. Kazi za Roho mtakatifu na kunena kwa lugha. 4.Kuja kwa Yesu mara ya pili duniani atakujaje?5. Namba 666 katika ufunuo 13:18 ina maana gani na nani mhusika, inafanya kazi au bado ama ilishapita. Mpinga kristo ni nani.

  Napenda kukuhakikishia kuwa sitatoweka katika mjadala na kama nitapata dharura yoyote nitatoa taarifa.

  Pia nasisitiza kutumia Biblia na vitabu rejea visivyopingana na Biblia vya waandishi wengine katika kujibu ama kuuliza swali.

  Naanza na swali hili, namba 666 katika ufunuo 13:18 ina maana gani na nani mhusika?Kumbuka kuwa, neno linasema unabii haufasiriwi kama apendavyo mtu fulani tu IPetro 1:20-21.

  Mungu akubariki John.

 114. Ndugu David Moses,

  Mimi naona ili kupata mahali pa kuanzia kwa ajili ya kuulizana maswali na kujadiliana kuhusiana na Imani ya Kisabato ingekuwa ni vizuri sana kama ungeweka, japo kwa uchache, mambo ya msingi ambayo Usabato unaamini na unafundisha na ambayo ndiyo yanaitofautisha na imani zingine.

  Natumaini kuanzia hapo wasomaji tunaweza, kama ikiwezekana, kupata mahali pa kuanzia kuuliza maswali.

  Nasubiri kwa hamu kujifunza kuhusu imani hii ya Kisabato.

 115. Bwana apewe sifa,

  Ndugu yangu John Bwana akubariki na kukutia nguvu kwa ajili ya kazi yake. Msafiri

 116. Mpendwa MT,

  Kwangu mimi hakuna tatizo lolote, ni amani tu!pu Lakini niliogopa kidogo maana ulivyoandika mchango wako wa tarehe 8 nilijisikia kama nimekuumiza kiasi fulani. Ninashukuru kwamba amani ipo! Basi tuendelee kujifunza na kujadili Neno la Mungu kwa moyo huu huu wa upendo na unyenyekevu.

  Nimeona umeandika kwamba si muda mrefu tangu umeingia kwenye ulokole [natumaini hapa unamaanisha kuokoka] na hivyo una kiu sana ya kujifunza. Ni jambo jema sana.

  Ushauri nilionao ni kwamba Biblia imekuwa ikitumika pia hata kwa walae wanaompinga Kristo. Kwa mfano utakuta waislamu nao wanasoma mistari fulani fulani kwa madai eti inatetea uislam, halafu maandiko mengine yanayoeleza ukweli wanasema Biblia imechafuliwa! Kwa hiyo Biblia kama Biblia ina maandiko mengi yanayojitosheleza lakini pia kuna maandiko mengine inabidi kuangalia sehemu nyingine ili kupata maana kamili ya andiko husika.

  Jambo jingine la kutambuwa katika kujifunza ni kufahamu aina ya ujumbe ulioko kwenye Biblia. Biblia ina jumbe nyingi zinazotofautiana. Ni mkusanyiko wa mambo mengi. Kwa ufupi kuna Historia, Unabii [uliotimia na ambao haujatimia] na Mafundisho ambayo yalikuwa, yana na yatafaa kufuatwa hadi siku Yesu atakaporudi mara ya pili. Ndani ya Biblia kuna Ujumbe toka kwa Mungu [pamoja na mafundisho ya Yesu], kuna maneno ya watakatifu mbali mbali binafsi, kuna mawazo yao binafsi na mitazamo yao kuhusiana na jambo fulani na mambo mengine mengi ambayo ni muhumu kufahamu wakati mtu anasoma Biblia. Yote haya yamewekwa kwenye Biblia ili kuujumuisha mfumo wote wa maisha ya Binaadamu na hivyo kuifanya Biblia kuwa ni kitabu kilichokusanya mambo yote kuhusiana na mwenendo wa binadamu, kwa kuwa kila andiko lina sehemu yake na umuhimu wake kwa watu. Kinachoweza kukosewa ni kule kufikiri kila andiko kwenye Biblia ni ujumbe toka kwa Mungu. Kwa mfano mtu anaweza kusoma maneno yanayohusu mtazamo binafsi wa mtu fulani kama vile Ayubu na kuyachukuwa hayo kuwa kama ndiyo kweli yote kuhusiana na jambo fulani husika. Lakini utakuta mahali fulani kuna maandiko mengine ambayo yako tofauti na neno hilo na utakuta yanaelezea kwa ukamilifu kuhusu suala hilo. Ndiyo maana utakuta watu kama mtume Paulo kuna mahali kabisa alikuwa anaandika kwamba maneno hayo yanatoka kwake kama Paulo na si kutoka kwa Bwana!

  Kwa hiyo unapondelea kujifunza Biblia ni vizuri kufahamu migawanyo ya jumbe kutokana na maneno yaliyoandikwa kwenye Biblia.

  Tatizo jingine ambalo huwa linasumbuwa watu wengi wanapokuwa wameokoka ni kule kuendelea kuwa na element za elimu ya kule alikotokea. Hali huwafanya wengi wajiwekee mipaka kwa kuwa yale mapokeo ambayo mtu alikuwa nayo kenye dini huwa yameweka kitu kama threshold ambayo kila anapojitahidi kuelewa zaidi hujikuta anazunguka pale pale alipokua. Kwa hiyo ndg yangu kwa kuwa umeshakubali kufungua moyo wako kwa Yesu inatakiwa kumuomba Mungu sana ili ule ufahamu wote wa kale uliokuwa nao kuhusu neno la Mungu uondoke na huu ufahamu mpya uingie!

  Naishia hapa kwa sasa, tuendelee kujadiliana na kujifunza

 117. Shalom John,

  Umejibu vema na Mungu akubariki sana. Mimi hapa najifunza tu ndio maana napekua na kuangalia Biblia inasema nini kwani nimeingia katika ulokole muda si mrefu na napenda sana kujifunza ndio maana nikiona somo fulani linatofautiana majibu na lingine napenda kujua undani wake, labda namna nilivyo kuwa nimerepresent haikuwa sahihi. Sorry again kama nitakuwa nimekukwaza. Ubarikiwe sana na Bwana. Msafiri

 118. Ndugu David Moses,

  Karibu sana kwenye ukumbi huu ambao mimi binafsi naufurahia sana. Na inapendeza kwamba upo tayari kwa maswali na kujadiliana.

  Jambo ambalo ninaomba kukufamisha ni kwamba wameshatokea watu wengi, kama hivi wewe, wenye imani tofauti tofauti, wakisema wamekuja kwa ajili ya kujadiliana. Lakini akiulizwa maswali mawili-matatu anakimbia. Sasa sifahamu wewe umejiandaa kwa kiasi gani na utayari ulio nao ni wa kiasi gani iwapo kutatokea maswali mengi hapa.

  Kwa hiyo nakushauri kabla hujauliza au hujaulizwa swali lolote uzingatie hilo kwa sababu kama utaulizwa swali halafu ukaacha kulijibu na ukatokomea haitaleta maana yoyote na lengo zima la kujadiliana, kama ulivyoandika, litakuwa limevurugika. Ninaamini maswali yako yote yatajibiwa hapa maana ni wengi wanaosoma, wenye ufahamu mbali mbali na viwango tofauti tofauti vya ufahamu wa neno la Mungu.

  Linaweza lisiwe swali ambalo ni lazima lijibiwe lakini ninapenda kukuuliza kama uko tayari kuwepo hadi mwisho wa maswali. Na mwisho wa maswali maana yake muafaka umepatikana.

 119. Ndugu Msafiri,

  Ni kweli kabisa ulivyoandika kwamba hapa ni mahali pa kujifunza. Na katika watu wanaotamani kujifunza mengi ni pamoja na mimi kwa sababu huwa natamani kuchangia kwenye kila mada ili kuona kama ninavyoelewa ni sahihi na kama si sahihi basi nisahihishwe.

  Ni kweli pia kwamba inapoonekana mtu ameandika ndivyo sivyo watu hujitokeza hapa kwa kumshauri au kumuelekeza. Na ndivyo nilivyofanya mimi baada ya wewe kuleta yale maeleo kuhusu Mauti. Ni mimi peke yangu nilichangia kwa kuuliza maswali. Kilichonifanya niulize kwanza ni ili kuelewa kama uliyoyaandika una uhakina nayo? Sikuona ni busara kuanza kumsahihisha mtu au kumshauri kabla sijafahamu kama alivyoandika ndiyo msimamo wake au ni vinginevyo!

  Nadhani unakumbuka kwamba kwanza nilipata wasi wasi kama hayo maelezo kuhusu MAUTI ni wewe umeyaandika. Unafikiri ni kwa nini nilipatwa na wasi wasi hadi nikauliza? Hii ni kwa sababu kwa muda ambao umeingia hapa SG nimekuelewa kwa namna fulani. Lakini maelezo kuhusu MAUTI yakawa ni tofauti na ninavyokuelewa. Maana yalionekana kama yameandikwa na mmoja wa watu wenye kutumia Biblia ili kuhalalisha IMANI ISEMAYO MTU ANAPOKUFA NDIYO UNAKUWA MWISHO WAKE.

  Sasa ili niweze kutoa mchango wangu kuhusiana na imani ya namna hiyo ndipo niliamua kuuliza kwanza maswali ili kupata uthibitisho wa yale yaliyoandikwa kwamba ndivyo ilivyo. Nilipouliza swali nilitegemea nipate majibu yenye kusisitiza kulichoandikwa kwenye maelezo ya MAUTI. Katika mchango wako fulani ulisema kwamba hayo hayakuwa maneno kutoka kwako bali yalikuwa ni mafunzo kutoka kwa mtu mwingine! Na hata kabla hujasema hivyo mimi tayari nilishaandika kwamba kama muhusika si wewe basi yaforward kwa mhusika ili nipate majibu hapa! [Mimi niliyaona kama ni maneno ambayo umekopi na kupaste].

  Sasa kilichonichanganya ni vile ulivyojibu swali langu moja ambalo hata hivyo majibu hayakuwa kwa maswali niliyouliza; ilikuwa ni kama muendelezo fulani wa yale maelezo ya MAUTI. [Hapa nikashangaa maana ulisema kwamba yale yalikuwa ni mafundisho kutoka kwa mtu halafu wewe tena ndiye ukajibu]. Kilichonichanganya zaidi nipale majibu uliyoleta yanapingana na maelezo yaliyokuwa mwenye ufafanuzi wa MAUTI. Ni maelezo yanayokinzana [opposite ideas].

  Baada ya kuwa umejibu kwa kupingana na maelezo yako ya mwanzo mimi nikabaki hewani! Maana nilitegemea ujibu kwa kusisitiza mchango wa mwanzo ndipo mimi nipate namna ya kuweka mchango wangu. Lakini baada ya kujibu kwa kupingana na maelezo ya mwanzo ikawa kama vile umeshajijibu. Na hapo mimi nikashindwa niseme nini! Ndiyo maana ilipofikia hapo nikasema labda una kusudi fulani ulilokusudia kwa kuleta maelezo yanayopingana na huenda kwa kutaka kuchangia kwangu au kuuliza maswali ningevuruga kusudi lako.

  Niliyasema hayo kwa nia njema kabisa na moyo wa upendo maana ilishatokea mtu mmoja alikuwa anauliza maswali kwa kujiweka katika nafasi ya muislam ili mada iendelee kuchangiwa. Lakini baada ya kuwa nimeandika maneno fulani, pasipo kutambuwa kusudi lake [maana mimi nilifikiri najadiliana na muislamu], yeye akajidhihirisha kwamba ni mkristo aliyeokoka lakini alijiweka upande huo ili kuwasaidia waislamu na akasema kwamba kwa sababu hiyo, ya maneno niliyoandika, hataweza tena kuendelea maana ni kama amekatishwa kwa kuwa nilichoandika mimi ilikuwa ni kutokukubaliana na masuala fulani aliyokuwa ametaka tuendelee kujadili!…Uko hapo?

  Ndiyo maana niliposoma mchango wako wenye maelezo ya MAUTI nilisita kwanza kama ni wewe umeandika hayo. Lakini hata hivyo nikaona niulize maswali ili nipate pa kuanzia. Kule kutojibiwa kwa maswali yangu halafu kukawa na mwendelezo wenye kutofautina na maelezo yaliyotangulia kukanikumbusha hicho kisa nilichoandika hapo huu na ndipo nikaona nikae pembeni nisijeharibu ulichokikusudia.

  Zaidi ya hayo sina tatizo lolote. Ninatamani sana tuendelee kujifunza. Na ninaamini pia tuko pamoja!

 120. Hamjambo wachangiaji wote? Mie mzima pia. Kwa mara ya kwanza ndiyo najiunga katika website hii. Naitwa David Moses toka Arusha. Ni MKRISTO WA MADHEHEBU YA KISABATO. Karibuni kwa maswali na tujadili pamoja. Mungu awe nasi daima kama ahadi yake.
  dmosesrev@yahoo.com.
  13292 ACC

 121. Bwana Yesu apewe sifa,

  Shalom ndugu yangu John,

  Naomba roho mtakatifu atuongoze sote kwa jambo hili. Mimi na wewe tunajifunza ili kuelewa jambo hili ndio maana tunasoma Biblia na kuelewa tofauti tofauti. Ndio maana hapa ni mjadala kama unaona mwenzio kaandika sivyo ndivyo uko na haki ya kumuelimisha na si kumuuliza tena maswali kwani hapa tunajifunza na inapotokea mtu anauliza maswali yamkini yuko na ufahamu tofauti sasa huo ufahamu tofauti ndio unapaswa kuutoa kwani hapa ni darasani. Mbarikiwe na Bwana. Tuendelee kujifunza, Msafiri

 122. Dada Rose,

  Asante kwa kunitakia baraka za Mungu. Tuzidi kuombeana katika safari hii ya mbinguni na tuendelee kumngoja Bwana!

 123. Mpendwa Msafiri,

  Binafsi sijaelewa lengo lako kutokana na kuleta mchango unaopingana. Na kwa kuwa sielewi naona nisijevuruga kile ulichokikusudia….

  Mimi katika kuuliza maswali nilisema kama muhusika siyo wewe basi yapeleke kwa mhusika ili ajibu. Katika maelezo yako ukasema yale maoni kuhusu ‘Mauti’ ni mafunzo tu kutoka kwa mtu. Lakini baadaye ukasema unajibu moja ya maswali. Sasa nashindwa kuelewa kama yale yalikuwa ni mafunzo toka kwa mtu lakini swali ukajibu wewe. Pamoja na kujibu tofauti na swali lilivyouliza pia Sijaelewa ni kwa nini wewe umjibie maswali huyo ‘mtu’.

  Swali ulilojibu lilikuwa ni la pili (2) katika maswali yangu, lenye vipengere viwili na lilikuwa hivi:

  “Kutokana na kuandika hivi, “Watu wanakufa kama wanyama (Mhu. 3:8); ikiwa mtu anakuwa na fahamu akiwa amepona kifo na kuishi mahali fulani, lakini yote mawili, maandiko na sayansi vipo kimya kuhusu hili.”
  Je, i).una maana kwamba mtu akifa ndio unakuwa mwisho wa maisha yake, yaani hakuna roho ndani yake ambayo huendelea kuishi katika ulimwengu wa roho?
  ii). Ni kweli hujaona andiko LOLOTE kweye Biblia Takatifu yenye vitabu 66 linaloonyesha kuwa kuna maisha baada ya kufa?”

  Nilitegemea jibu lake lieleze maana yake nini kuandika maneno niliyonukuu kwenye swali na pia kusema kama ni kweli kwenye Biblia hakuna andiko lolole linaloonyesha kama kuna maisha baada ya kufa. Lakini katika kujibu wewe umetengeneza maswali yako yanayofanana na niliyouliza na ukatolea majibu marefu ambayo naona yanapingana na maneno ya kwanza yaliyo katika mafunzo uliyoyaweka hapa tarehe 4/9/09 ambayo ndani yake kuna maneno haya hapa chini:

  “Jitihada za binadamu kurahisisha kilele cha mauti imepelekea aamini ya kwamba ana’nafsi /roho isiyokufa’ Mara ikikubalika kuwa kitu hiki kisichokufa kimo ndani ya binadamu, inakuwa ni lazima kudhani kwamba inabidi kiende mahali fulani baada ya kufa. hii imepelekea ya kwamba mautini inabidi ziwepo ajali fulani tofauti kati ya wenye haki na wabaya.”

  Lakini ni kama nilivyoandika mwanzoni kuwa yawezekana sijafahamu kusudi lako la kuleta maoni yanayopingana na ndiyo maana sielewi ni nini unataka kufundisha kwa kuleta maoni yanayopingana.

  Endelea na ulichokikusudia….

 124. Tuendelee kujifunza
  Swali: “Ni nini hufanyika baada ya kufa?”

  Jibu: Swali hili laweza kuwa na utata mwingi. Biblia haifafanui wazi wazi juu ya lini mtu atafika katika hatima yake ya milele. Biblia inatuambia ya kuwa baada ya mtu kufa, hupelekwa mbinguni au jehanamu kulengana na hoja ya kuwa alikuwa amemkubali ama kumkataa Kristo kama mwokozi. Kwa walioamini, kufa ni kuondoka katika mwili na kuenda kukaa na Bwana (wakorintho wa pili 5:6-8; wafilipi 1:23). Kwa wasioamini, kufa ina maana ya hukumu ya milele jehanamu (Luka 16:22-23).

  Hapa ndipo kwenye utata juu ya ni nini hufanyika baada ya kifo. Ufunuo wa Yohana 20:11-15 inaeleza juu ya wale walio kuzimu wakitupwa katika ziwa la moto. Ufunuo wa Yohana 21 na 22 inazungumzia juu ya mbingu mpya na dunia mpya. Kwa hivyo ina maana ya kuwa mpaka wakati wa ufufuo wa mwisho, baada ya kufa mtu hubaki katika mahali Fulani kwenye mfano wa mbinguni na kuzimu. Mahali pa mtu anapofaa kukaa milele hapatabadilika ila makazi ya muda yatabadilika. Muda Fulani baada ya kufa, waumini watapelekwa katika mbingu mpya na nchi mpya (ufunuo wa Yohana 21:1) na wasioamini katika ziwa la moto (ufunuo wa Yohana 20:11-15). Haya ndiyo makao ya milele ya watu yanayotegemea kama mtu alimwamini Yesu Kristo pekee kwa wokovu kutokana na dhambi zake.
  Msafiri

 125. Bwana apewe sifa, huu ni muendelezo wa kujifunza pia Mpendwa John napenda kujibu moja ya swali lako:Tuendelee kujifunza

  Swali: “Je kunayo maisha baada ya kifo?”

  Jibu: Je, kunayo maisha baada ya kifo? Bibilia inatuambia, “Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu. Yeye huchanua kama vile ua, kasha hukatwa; Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe… Mtu akifa, je! Atakuwa hai tena” (Ayubu 14:1-2,14)?

  Kama vile Ayubu, karibu sisi sote tumekabiliwa na swala kama hili. Ni jambo gani hasa hutukia kwetu baada ya kufa? Je, ni kukosa kuwepo duniani tu? Je, maisha ni kufa na kufufuka tu ili tujipatie umaarufu tena duniani? Je, watu wote huenda mahali pamoja, au huenda mahali tofauti? Je, kunayo kweli Mbingu na Jehanamu, au ni maneno tu ya kujitungia?

  Bibilia inatuambia yakwamba sio maisha pekee tu baada ya kifo, bali kuna uzima wa milele wenye utukufu mwingi “Hakuna jicho limeshaona, wala sikio kuyasikia,wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao’’ (1Wakorintho 2:9) Yesu Kristo, Mungu katika mwili, alikuja duniani kutupa karama ya uzima wa milele. “Alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona’’ (Isaya 53:5).

  Yesu alichukua adhabu aliyostahili kila mmoja wetu na akajitoa maisha yake. Siku tatu baadaye, akathibitisha ushindi wake juu ya mauti kwa kufufuka kutoka kaburini, katika roho na katika mwili. Alibaki katika dunia kwa mda wa siku arubaini na kushuhudiwa na maelfu ya watu kabla ya kupaa nyumbani kwake Mbiguni kwenye uzima wa milele. Warumi 4:25 yasema, “Alitolewa kwa ajili ya makosa yetu,na kufufuliwa ili tupate kuhesabiwa haki.’’

  Ufufuo wa Kristo lilikuwa ni jambo lililodhihirika Mtume Paulo aliwapatia watu changamoto kwamba wawaulize wale waliokuwapo wakati jambo hilo likitendeka wahakikishe kama jambo hilo si kweli. Hakuna aliyeweza kushindana juu ya ukweli huo. Ufufuo ndio msingi imara (jiwe la pembeni la) wa imani ya Mkristo; kwasababu Kristo alifufuka katika wafu, sisi pia tunaweza kuwa na imani ya kwamba tutafufuliwa.

  Paulo aliwaonya wakristo wa kwanza ambao hawakuyaamini haya: “Basi, ikiwa Kristo anahubiriwa ya kwamba amefufuka katika wafu mbona baadhi yenu husema kwamba hakuna kiyama ya wafu? Lakini kama hakuna kiyama ya wafu, Kristo naye hakufufuka” (Wakorintho 15:12-13).

  Kristo alikuwa pekee wa kwanza kati ya mavuno makuu ya wale watakao inuliwa kutoka kwa wafu. kifo kiliingia duniani kuputia mtu mmoja, Adamu ambaye sisi sote ni wa ukoo wake. lakini wale ambao wamefanywa wana wa Mungu kupitia imani juu ya Yesu Kristo watapewa maisha mapya (Wakorintho wa kwanza 15:20-22). Kama vile Mungu alivyofufua mwili wa Yesu, vivyo hivyo ndivyo miili yetu itakavyofufuliwa Yesu atakaporudi (Wakorintho wa kwanza 6:14).

  Ijapokuwa sote tutakuwa tumefufuliwa, hatutaenda sote mbinguni mahali pamoja. Mtu sharti afanye uamuzi wa kuchagua sasa juu ya mahali anapotaka kuenda kwa umilele wake. Bibilia inasema ya kwamba imetupasa kufa mara moja na baada ya kifo hukumu (Waebrania 9:27). Wale waliotakaswa wataenda kwa uzima wa milele mbinguni, lakini wasioamini watapelekwa kwa hukumu ya milele ama jehanamu (Mathayo 25:46).

  Jehanamu, kama vile mbinguni, si mahali patajwapo kwa utisho tu bali ni mahali dhahiri. Hapa ni mahali ambapo wasiohaki watakutana na ghadhabu isiyokoma ya Mungu. Watavumilia mateso ya kihisia, kiakili, na kimwili wakiwa katika akili zao timamu huku wakijihisi kuaibika na kujuta kwa matendo yao maovu.

  Jehanamu inaelezewa kama shimo la giza (Luka 8:31, Ufunuo wa Yohana 9:1), na ziwa la moto, liwakalo na kiberiti amabpo watakao kuwemo watateswa usiku na mchana milele na milele (Ufunuo 20:10). Huko kutakuwa na kulia na kusaga meno, ikiashiria machungu makali na hasira (mathayo 13:42). Hapa ni mahali ambapo mdudu hatakufa wala makaa kuzimika (Marko 9:48). Mungu hafurahishwi na kufa kwa mtu muovu, lakini hutaka wazighairi njia zao mbaya ili waishi (Ezekiel 33:11). Lakini hatatulazimisha kumkubali; tukiamua kumkataa yeye. Hana budi kutupatia tulilolichagua – kuishi mbali naye.

  Maisha ya duniani ya sasa ni mtihani tu; ni matayarisho ya yale yajayo. Kwa waaminio, huu ni uzima wa milele kuweko mbele za uwepo wa Mungu. Basi ni kwa jinsi gani tunafanyinyika wenye haki na kustahili kupokea uzima huu wa milele? Kuna njia moja pekee – kupitia imani na tumaini ndani ya mwana wa Mungu, Yesu kristo. Yesu alisema, “mimi ndimi huo ufufuo na uzima. Waniaminio mimi wajapokufa wataishi. Wanapawa uzima wa milele kwa kuniamini mimi na hawatapotea…” (Yohana 11:25-26).

  Kipawa hiki cha uzima wa milele kinapatikana na ni bure kwa wote lakini kinagharimu kujikana wenyewe raha Fulani za dunia na kutoa sadaka kwa Mungu. “na wote wamwaminio mwana wa Mungu wana uzima wa milele. Wasiomtii mwana hawatapata uzima wa milele bali ghadhabu ya Mungu inadumu juu yao” (Yohana 3:36). Hatutapatiwa nafasi ya kutubu dhambi zetu baada ya kufa kwa kuwa tukimuona Mungu uso kwa uso hatutakuwa na lengine ila kumwamini. Anatutaka tumjilie sasa kwa imani na upendo. Tunapokubali kwamba kifo cha Yesu msalabani ni malipo kamili ya dhambi zetu dhidi ya Mungu, tumeahidiwa si tu maisha mema duniani bali pia uzima wa milele mbele ya kristo.

  Mbarikiwe na Bwana, Msafiri

 126. Bwana apewe sifa,

  Ndugu yangu John hayo yalikuwa mafunzo tu kutoka kwa mtu ndio maana nikasema tuangalie hapa na mwisho nikasema tuendelee kujifunza. Nikipata muda wa kuchangia zaidi nitaweka mawazo yangu. Mbarikiwe na Bwana. Msafiri

 127. Ubarikiwe sana John Paul,
  Ni kweli swali lilikuwa nusu, nadhani ilikuwa kama mtu ameokoka na ameachwa je ni halali kwake kutafuta test tube babies. Lakini mie nilikuwa sijakaa nikaangalie procedures za jinsi ya kupata hao watoto, jumapili nimemuuliza mpendwa mmoja amenipa maelezo mengi yanayopingana na Biblia ikiwemo uuaji, uzinzi na mengineyo na mistari husika katika Biblia.
  Asante sana kweli vitu vingine kwa nje vinaonekana vizuri lakini kumbe vinajumuisha mambo mengi yasiyofaa sikuwa nayafahamu ndo maana niliona niulize. Kwani otion nyingine kama adoption kwa mzazi mmoja hawazikubali. lakini katika yote naona bora kumngoja Bwana kama Zaburi 27 inavyosema, tutauona wema na wokovu wake. Ubarikiwe

 128. Ndugu MT,

  Mimi nimesoma mchango wako wa mwisho nimepata tabu sana kufahamu kinachozungumziwa humo nini hasa. Lakini nafikiri umeandika kwa ajili ya kujibu maswali kadhaa kwenye mjadala uliokuwa unahusu MAUTI na KUZIMU. Hata hivyo sina uhakika kama maneno haya umeyaandika mwenyewe au umekopi kutoka mahali fulani. Kama umekopi na kuleta hapa ili tuyaangalie kwa pamoja basi, mimi nina maswali ambayo nimeya-address kwako kwa kuwa wewe ndiye umeleta mchango huu. Lakini kama kuna muhusika zaidi ya wewe basi unaweza kuya-forward ili ajibu maswali hayo na kisha ulete majibu yake hapa ili niyapate ikiwa ni pamoja na msomaji mwingine anayefuatilia.

  Nitajifunza vizuri zaidi kama yatajibiwa kutokana na mpangilio niliotumia kuyauliza:

  1. Je, una maana Mauti tafsiri yake ni Kutokuwa na
  Fahamu kabisa? [Yaani MAUTI = KUTOKUWA NA FAHAMU KABISA]

  2. Kutokana na kuandika hivi, “Watu wanakufa kama wanyama (Mhu. 3:8); ikiwa mtu anakuwa na fahamu akiwa amepona kifo na kuishi mahali fulani, lakini yote mawili, maandiko na sayansi vipo kimya kuhusu hili.”
  Je, i).una maana kwamba mtu akifa ndio unakuwa mwisho wa maisha yake, yaani hakuna roho ndani yake ambayo huendelea kuishi katika ulimwengu wa roho?
  ii). Ni kweli hujaona andiko LOLOTE kweye Biblia Takatifu yenye vitabu 66 linaloonyesha kuwa kuna maisha baada ya kufa?

  3. Kutokana na kuandika hivi, “Ushahidi wa kutosha umetolewa kwa ajili yetu unaosema wazi ya kwamba wazo la watu wengi kuwa wenye haki wanakwenda kwenye hali ya furaha na kupewa thawabu mbinguni moja kwa moja mara baada ya kufa, peke yake haupatikani katika Biblia.”
  Je, una maana wenye haki wakifa huwa wanakaa mahali fulani kwanza kabla ya kwenda kupewa thawabu mbinguni?

  4.Kwa maneno haya, “Baada ya hali yote ya magonjwa na maumivu ya maisha ya binadamu, Kaburini ni mahala pa usahaulifu kabisa. kwa wale ambao hawajui matakwa ya Mungu, usahaulifu huu utadumu milele.”
  Je, i). Unamaamisha kwamba mtu anapokufa mwili, nafsi na roho vyote hufukiwa na kubaki kwenye kaburi la kifusi cha udongo?
  ii).Unaweza kuelezea kidogo ni watu gani wanaojua na wale wasiojua matakwa ya Mungu na matakwa hayo ni matakwa gani?
  iii). Kwa watu wanaojua matalwa ya Mungu usahaulifu huu hudumu kwa muda gani?

  5. Kwa kuandika hivi, “Jitihada za binadamu kurahisisha kilele cha mauti imepelekea aamini ya kwamba ana’nafsi /roho isiyokufa’ Mara ikikubalika kuwa kitu hiki kisichokufa kimo ndani ya binadamu, inakuwa ni lazima kudhani kwamba inabidi kiende mahali fulani baada ya kufa”
  Je, una maana ndani ya binadamu hakuna roho itakayoishi milele?

  6.Umeandika pia hivi, “kutengeneza wazo hili, imesemwa kuwa inabidi kuwepo sehemu ya’roho nzuri zisizokufa’ huenda toharani – mbinguni…”
  Je, tafsiri ya kwamba toharani ni mbinguni umeipata wapi?

  7.Kwa kuandika hivi, “Awali tumeonyesha kuwa’nafsi au roho’ isiyokufa kwa Biblia haiwezekani.”
  Je, una maanisha hakuna maandiko katika Biblia yanayoonyesha kwamba roho ya binaadamu itaishi milele?

  8.Ikiwa mawazo matano(5) uliyoorodhesha mwishoni mwa mchango wako umeyaita ni mawazo POTOVU Ninaomba uandike masahihisho ya mawazo hayo kwa mpangilio ule ule kuanzia 1 hadi 5.

 129. Dada Rose,

  Mimi ninafikiri swali hilo halijakamilika kwa sababu haionyeshi ni nini kinasababisha hadi mtu afikie hatua hiyo. Ninasema hivyo kwa sababu swali hili linafanana na swali ambalo mtu anaweza kuuliza kama ni dhambi kwa mtu kuoa/kuolewa mara ya pili. Kwa haraka haraka ni rahisi kujibu kwamba kuoa mara ya pili ni dhambi. Lakini ukiuliza ni nini kilichopelekea mtu aowe au aolewe mara ya pili na ukaambiwa mke/mume wake wa mara ya kwanza alifariki. Ni dhahiri kwamba jibu la kwanza litakuwa si sawa kwa sababu mwenzi akifa aliye bakia hana hatia kama ataamua kuoa au kuolewa.

  Swali lako hili vile vile mimi naona lina utata kama huo. Ni sababu gani inafanya hadi mtu afikie hatua hiyo? Labda yawezekana kuna sababu genuine, ingawa sina uhakika ni sababu gani ambayo ulishaisikia ambayo hupelekea mtu kuchukuwa hatua hiyo.

  Kwa mtu aliyeokoka mimi naona kama jambo hilo liko mbali naye, labda kama kuna mtu ana kinyume chake anaweza kueleza. Lakini kwa mtu ambaye hajaokoka maisha yake yamezingirwa na matendo mengi ambayo ni dhambi kwa hiyo haiwezekani kuhesabu dhambi moja moja na kuanza ku-eliminate. Kwa hiyo kwa jinsi ulivyouliza mimi nimeliweka upande wa mtu aliyeokoka.

  Kama swali lako lingekuwa kwenye form hii: “Je, ni dhambi kwa mtu kufanya hivi au vile. . . . ikiwa hiki au kile. . . . kimekuwa hivi au vile . . . .” nadhani lingekuwa limeondoka katika hali ya utata.!

  Natumaini ukiweka wazi sababu za kitendo hicho inaweza kusaidia kwa mtu ambaye atakuwa anajibu la swali lako.

  Asante.

 130. Shalom wapendwa,
  Nina swali linanikwaza, je ni dhambi mtu akipata mtoto kwa njia ya chupa, yaani test tube baby au kwa artifial insemination?
  Bwana awabariki sana

 131. YESU Asifiwe!
  Napenda tu usema kwamba kama wapendwa walivyojibu ni sawa kabisa kwamba,kwenda makaburini inategemea mambo 2 either una ibada huko or una nia ya kufanya mazingira hayo yasipotee.
  Hivyo habari za kuombea wafu HAKUNAAAAA!!!! unless utakuwa mchawi na KUTOKA 22=18 itakuhusu kwamba,USIMWACHE MWANAMKE/ME MCHAWI AISHI.
  AMEN!!!

 132. Shalom wapendwa,

  Natumaini Bwana amewaweka salama toka jana,
  Tuangalie hapa:

  Mauti ni Kutokuwa na Fahamu Kabisa:

  Kutoka kile tulichojifunza mpaka hapo kuhusu nafsi na roho, kinachofuata ni kwamba muda mtu anapokuwa amekufa hawi na fahamu kabisa. Wakati matendo ya wale wanaopashwa kwa Mungu yatakumbukwa naye (Malaki 3:16; Uf. 20:12; Ebra. 6:10), Katika Biblia hakuna kinachodokezwa kuwa tunazo fahamu zozote mautini. Ni vigumu kubishana na shuhuda wazi zifuatazo kuhusu hili:-
  • “Pumzi ya (mtu) humtoka, naye hurudi katika udongo wake; siku hiyo mawazo yake yapotea” (Zaburi 146: 4).
  • “Wafu hawajui neno lolote, …. Mapenzi yao, na machukio yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja” (Mhubiri 9:5,6). Hakuna “hekima huko kuzimu” (Mhu. 9:10) – hakuna kufikiri na kwa hiyo hakuna fahamu.
  • Ayubu anasema kwamba mautini, atakuwa’Kana kwamba hakuwahi kuwepo’ (Ayu. 10:18); aliona mauti kuwa ni usahaulifu, kutokuwa na fahamu na kukosa kuwepo kabisa tuliokuwa nao kabla ya sisi kuzaliwa.
  • Watu wanakufa kama wanyama (Mhu. 3:8); ikiwa mtu anakuwa na fahamu akiwa amepona kifo na kuishi mahali fulani, lakini yote mawili, maandiko na sayansi vipo kimya kuhusu hili.
  • Mungu “anatukumbuka kuwa ni mavumbi. Mwanadamu siku zote si kama majani; kama ua la kondeni ndivyo asitawivyo …. Haliko; na mahala pekee hapatalijua tena” (Zab. 103:14 -16).
  Mautini hakika ni kutokuwa na fahamu, hata kwa wenye haki, yameonyeshwa maombi yaliyorudiwa ya watumishi wa Mungu waruhusiwe maisha yao yaweze kurefushwa, kwa sababu walijua kwamba baada ya kufa hawataweza kumsifu na kumtukuza Mungu, kwa kuwa mautini ni kutokuwa na fahamu. Hezekia (Isaya 38:17 -19) na Daudi (Zaburi 6:4,5; 30:9; 39:13; 115:17) wao ni mfano huu mzuri. mauti yamerudiwa kwa kutaja kuwa ni kulala au kupumzika, wote wawili kwa wenye haki na waovu (Ayu. 3:11, 13:17; Dan 1.12:13). Ushahidi wa kutosha umetolewa kwa ajili yetu unaosema wazi ya kwamba wazo la watu wengi kuwa wenye haki wanakwenda kwenye hali ya furaha na kupewa thawabu mbinguni moja kwa moja mara baada ya kufa, peke yake haupatikanai katika Biblia. Funzo la mauti na umbo la binadamu kweli linatoa amani kubwa ya maana. Baada ya hali yote ya magonjwa na maumivu ya maisha ya binadamu, Kaburini ni mahala pa usahaulifu kabisa. kwa wale ambao hawajui matakwa ya Mungu, usahaulifu huu utadumu milele. Sababu kuu ya huzuni hii na uhai wa kwanza hautarudi tena; matumaini yasiyofaa na hofu ya asili ya nia ya mwanadamu havitatambulika au kuogofya.
  Kwa kusoma Biblia, kuna utaratibu kweli wa kuivumbua; lakini, kwa bahati mbaya, pia upo utaratibu wenye kosa katika dini aliyojitungia mtu, kutokana na kutoiangalia Biblia. Jitihada za binadamu kurahisisha kilele cha mauti imepelekea aamini ya kwamba ana’nafsi /roho isiyokufa’ Mara ikikubalika kuwa kitu hiki kisichokufa kimo ndani ya binadamu, inakuwa ni lazima kudhani kwamba inabidi kiende mahali fulani baada ya kufa. hii imepelekea ya kwamba mautini inabidi ziwepo ajali fulani tofauti kati ya wenye haki na wabaya. kutengeneza wazo hili, imesemwa kuwa inabidi kuwepo sehemu ya’roho nzuri zisizokufa’ huenda toharani – mbinguni na sehemu nyingine kwa ajili ya’roho mbaya zisizokufa’ kwenda sehemu hiyo imeitwa kuzimu. Awali tumeonyesha kuwa’nafsi au roho’ isiyokufa kwa Biblia haiwezekani. Mawazo mengine potovu yaliyo ndani ya watu wengi jinsi wanavyofikiri sasa yatachambuliwa: –
  1. Kama thawabu ya maisha yetu inatolewa mautini kwa namna ya’roho yetu isiyokufa’ kugawiwa mahala fulani.
  2. Kama mtengano kati ya wenye haki na wabaya hutokea wakati wa kufa.
  3. Kama thawabu ya wenye haki ni kwenda mbinguni (Toharani) sehemu ya amani.
  4. Kama ikiwa kila mmoja ana’roho isiyokufa’, basi kila mtu inambidi kwenda aidha mbinguni au kuzimu.
  5. Kama’roho’ za waovu zitakwenda mahala pa kuadhibiwa panapoitwa kuzimu. (sehemu ya mateso).
  Tuendelee kujifunza.
  Bwana awabariki sana.
  Msafiri Thabit

 133. Wapendwa, kuhusu kufanya ibada kwenye makaburi, tusome hapa pia

  Isaya 8:19Wakati watu wanapowaambia kutafuta ushauri kwa waaguzi na wenye kuongea na mizimu, ambao hunong’ona na kunung’unika, je watu wasingeuliza kwa Mungu wao? Kwa nini watake shauri kwa wafu kwa ajili ya walio hai? 20Kwa sheria na kwa ushuhuda! Kama hawatasema sawasawa na neno hili, hawana mwanga wa mapambazuko.

  Bwana awabariki.

  Msafiri

 134. Bwana Yesu apewe sifa,

  Napenda kusema kuwa siko mbali sana ndugu yetu John, ni kuwa kama nilivyosema awali kuwa ni makosa kufanya yale uliyouliza ila kwa upande wingine kama makaburi hayo yapo maeneo ya nyumbani si mbaya kuyafanyia usafi au kuyatengeneza kwa maana kuyajengea ili yaonekane vizuri ila cha msingi hapo unafanya hivyo ili iwe nini? Dhamira moyoni mwako ni ipi? Mbaya mimi naweza sema ni kuabudu kile unafanya katikati ya makaburi hayo. Hapa???????(kutembelea makaburi kuna utata kwani utakuwa unayatembelea ili iwe nini? Kuna nini cha msingi ambacho kitakuwa kinakukumbusha kwenda kupatembelea hapo kwani hapo kuna makazi ya mtu yeyote??? ( kuwaombea marehemu) (kufanya ibada) Ipi zaidi ya ile uliyoifanya wakati ule wa safari yake ya mwisho????

  Ila napenda kusema kuwa cha msingi hapo ni moyo wako na dhamira ya kufanya yale unayotaka kufanya juu ya makaburi hayo yasiwe ya kumchukiza Mungu wetu. Rejea maandishi ya John hapo juu.

  Soma Isaya 65: 2Mchana kutwa nimeinyoshea mikono yangu kwa watu wakaidi, wanaokwenda katika njia ambazo si nzuri, wafuatao mawazo yao wenyewe. 3taifa ambalo daima hunikasirisha machoni pangu, wakitoa dhabihu katika bustani na kufukiza uvumba juu ya madhabahu za matofali, 4watu waketio katikati ya makaburi na kukesha mahali pa siri, ili kuabudu mizimu, walao nyama za nguruwe, nazo sufuria zao zina mchuzi wa nyama na mboga zilizonajisi.

  Samahanini sijapata muda wa kuchambua mafungu vya kutosha ni ubize tu wa maisha nikasema nipitie hapa kidogo na nikawa nasubiriwa kutoa chochote nikaona nisifunge web hii bila kusema chochote.

  Tuendelee kujifunza na Bwana awabariki sana .

  Msafiri Thabit

 135. Mpendwa Patrick,

  Mimi nilikuwa nasubiri ndugu Msafiri Thabit aandike kama ambavyo lisema angeandika kwa kutoa reference katika Biblia. Lakini nami nimeona niweke machache wakati tukiendelea kumsubiri ndugu MT afanye hivyo.

  Ninvyofahamu mimi kutembelea kaburi la ndugu na kulisafisha kama vile kufyeka nyasi na kuondoa vichaka kwa nia ya kufanya hivyo tu siyo tatizo. Tatizo ni pale mtu anapoheshimu kaburi kama kituo kingine cha ibada. Suala la kufanya ibada mwenye makaburi si suala sahihi kwa wanaomwamini Yesu kwa sababu kumwombea marehemu ni ibada hewa. Anayemuombea marehemu ni lazima atambuwe anaomba ili nini kiwe nini. Neno la Mungu linatuambia baada ya kufa ni hukumu. Kwa hiyo hakuna sababu ya kufanya maombi ambayo unajua hayana faida yoyote na hayawezi kubadilisha chochote.

  Katika Ebrania 9:27-28 kuna maneno haya, “Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu; Kadhalika Kristo naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi; atatokea mara ya pili, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu”

  Baada ya mtu kufa hakuna kinachoweza kubadilisha hali ya kiroho aliyokufa nayo bali kinachofuatia huwa ni hukumu. Kinachotakiwa ni mtu kumtazamia Yesu, akiwa ndani ya wokovu, wakati yu hai. Mtu wa namna hii akifa atakufa katika wokovu; atakufa katika matumaini. Huyi ndiye ambaye siku ya mwisho atafufuka kwa ajili ya kutawala pamoja na Yesu.

  Pia katika Warumi 14:8 kuna maneno haya, “Kwa maana kama tukiishi, twaishi kwa Bwana, au kama tukifa, twafa kwa Bwana. Basi kama tukiishi au kama tukifa, tu mali ya Bwana”

  Maneno haya yanaeleza jinsi mtu aliye katika Bwana anapokuwa hai, huyo akifa yu katika Bwana. Kinyume chake ni kwamba mtu ambaye hayuko katika Bwana wakati yu hai hata akifa hayuko katika Bwana. Kwa hiyo kama mtu alikufa katika Bwana hakuna sababu ya kumuombea maana yu katika Bwana tayari. Vile vile kama mtu hakuwa katika Bwana wakati wa uhai wake hakuna sababu ya kumuombea kwa sababu hakuwa katika Bwana, bali kinachofuatia ni hukumu kutegemeana na hali aliyokuwa wakati akifa.

  Pia katika Yohana 11:25-26 tunapata maneno haya, “Yesu akamwambia mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniamimiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi.Naye kila aishie na kuniamini hatakufa kabisa hata milele…..”

  Hapa tunapata msisitizo mwingine kwamba suala muhimu ni kumuamini Yesu ukiwa hai. Kwa sababu amwaminiye Yesu wakati akiwa hai, hata akifa atakuwa anaishi. Na anayemwamini Yesu wakati akiwa hai hatakufa hata milele. [Hapa Yesu alikuwa anazungumzia kifo cha kiroho kwa sababu kifo cha kimwili kwamcha Mungu ni njia tu ya kuingia uzimani]. Kwa hiyo mtu anayemwamini Yesu wakati yu ana uhakika wa kuishi milele. Hahitaji maombi ya walio tena.

  Nimeandika hayo kwa sababu sifahamu na sidhani kama kuna maombi mengine ambayo marehemu anaweza kuombewa zaidi ya kumuomba Mungu ‘amweke mahali pema peponi’, sala ambayo ni ya kujidanganya kwa sababu hakuna fundisho lolote toka kwa Yesu au hata mitume wengine kwamba mtu anaweza kuwekwa mahali pema peponi kwa sababu ya kuombewa.

  Hivi ndiyo nilivyoweza kujibu kwa sasa. Yawezekana una kuna sababu unazozifahamu ambazo ni kwa ajili ya kumuombea marehemu. Kama zipo ni vizuri ukaziandika ili tuzipime kutokana na Neno la Mungu.

 136. Shalom,

  Mjadala mzuri sana, mambo ya msingi ya mtu akimpokea Yesu ni kukaa katika Neno la Mungu,kumwomba Mungu ili atupe ufahamu wa kiroho, na hekima katika mapenzi ya Mungu (Kol 1: 9-11). Tujue kuwa kuna elimu ambayo Paul aliliandikia barua kanisa la Kolosai, na kila mtu kusimama na miguu yake. Hawa wanaofanya biashara kwa kutumia Neno la Mungu kuna siku watakutana na Mungu. Uchunguzi wangu ni kuwa watu hawafundishwi maisha matakatifu, unyenyekevu, utii na uaminifu kuanzia katika nyumba zao, familia, jirani na katika jamii, hili ndilo chimbuko la ufisadi. Pia tukumbuke Biblia kuwa miujiza itatufuata na siyo sisi kuifuata; ni kinyume na Neno la Mungu.

 137. mpendwa Alfred katuma. Mungu akubariki kwa jinsi ulivyojitahidi kumuelewesha mpendwa aliyetaka kufahamu kuhusiana na utoaji,lakini nafikiri unahitaji msaada zaidi ya unavyofahamu.
  tafadhari naomba unitumie e mail adress yako nikupe siri ya tatizo linalosumbua kanisa kuhusiana na utoaji ili iwe sehemu ya wajibu wangu mbele za Mungu.
  Mungu akubariki sana
  Email adress yangu ni aminnguluma@yahoo.com ama nguluma@accamail.com

 138. Ndugu zangu napenda kufahamu. Hivi ukiwa umeokoka mwenendo wako mkabala na makaburi ya wazazi au mkeo au mtoto wako au ndugu zako unatakiwa uweje? Hivi ni dhambi kwa mimi kutembelea makaburi hayo na kufanya ibada au kuwaombea marehemu? Ni dhambi kama siyatunzi kwa kuyasafisha kuyajengea kwa nia ya kuyapendezesha? Naomba mnielimishe tafadhali.

 139. Shalom Mtumishi Alfred,

  Ubarikiwe sana kwa majibu yako mazuri na Mungu akubariki sana na akutie nguvu. Kuna msemo nausikia kadri unavyotoa ndivyo utakavyo vuna na kuwa kama nina 40,000 katika pochi yangu naweza toa 20,000 kama sadaka na nitegemee kuvuna kama niko na imani sijui hapo ni sahihi?Mfano mshahara wangu baada ya kutoa fungu la kumi/matoleo mbalimbali na kutoa matumizi yangu ya mwezi na nikabakiwa na kiasi fulani na nikapanga kuwa kila nitakapo enda kanisani katikati ya week na jumapili nitakuwa namtolea Mungu kiasi fulani ili mradi tu nisiache kumtolea Mungu kanisani je ni sawa kwa upandee huu? au si vizuri kupanga kuwa utatoaje kwani kadri nitakavyotoa zaidi ndivyo nitakavyovuna?

  Ubarikiwe na Bwana,

  Msafiri Thabit

 140. Bw.asifiwe!Kwa mujibu wa neno la Mungu naomba nikujibu ndugu yangu MT kama ifuatavyo:
  1:FUNGU LA KUMI:-hii ni sadaka ya lazima kwa mtu yoyote awe ameokoka au hajaokoka na ni sehemu ya kumi ya pato lako.mf.kama wewe ni mfanyakazi na unapata mshahara wa sh.100,000 ni lazima utoe sehemu ya kumi ya huo mshahara wako ambayo ni sh.10,000 na kama ni mkulima labda umevuna magunia 100 magunia 10 ni ya Mungu. sasa utaelewa kwa nini Mungu anasema katika malaki 3:8-10 kwamba wanadamu wanamuibia,na anasema wamuibia kwasababu fungu la kumi ni la Mungu na utaona ametumia neno ZAKA ambalo ndo fungu la kumi.(soma pia Mwa.14:20)

  2:SADAKA:-hii ni sadaka ambayo mtu anatoa kwa moyo wa kupenda (kut.25:1-3,mdo.10:1-2)na kila kanisa lina utaratibu na mipangilio ya sadaka mf.sadaka ya jengo,ahadi n.k.

  3:MALIMBUKO:-hii ni sadaka ya kwanza katika vitu vyako (first fruit)soma kut.23;19a,kut.34:26) unamtolea Mungu mazao yako ya kwanza ktk ardhi au wazaliwa wa kwanza wa wanyama wako.soma tena mwa.4:4 na nehemia 10:35-38).sifa au heshima ya sadaka hii ni kitu hicho kutolewa cha kwanza!

  4:DHABIHU:- ni sadaka ya kuteketezwa hakuna dhabihu bila kumwaga damu na kwa sasa hatuna sadaka kama hii.
  (kut.23:18)

  Mwisho hakuna sadaka ya kupanda mbegu ila unapotoa sadaka kwa moyo wako na ikampendeza Mungu tarajia kuvuna baraka na mara nyingi watumishi wanatumia neno kupanda mbegu kwasababu tu kuna baraka katika kutoa sadaka,maana sadaka ina nafasi kubwa sana katika majibu ya maombi tunayoomba,sina muda wa kuandika mambo yote lakini kama ni msomaji wa bible utakuwa una elewa.

  Mungu awabariki woooooote!!!!

 141. Bwana Yesu apewe sifa,

  Naomba kama kuna mtu anajua somo la utoaji anisaidie kama ifuatavyo

  Fungu la kumi

  Zaka

  Sadaka

  Malimbuko

  Zabihu

  Kupanda Mbegu

  Nimekuwa sielewi namna ya utoji kwa namna zote zilizopo hapo juu.

  Mbarikiwe kwa kunisaidia

  Msafiri Thabit

 142. Mbarikiwe nyote na Bwana,

  Mtumishi Alfred Katuma Mungu akubariki kwa ushauri wako najua Mungu anafanya kitu kupitia maandiko uliyonipa na ushauri. Bwana awe naye na akutie nguvu.

  Mbarikiwe sana na kinachonitia nguvu ni kuwa imetupasa kumuabudu Mungu katika Roho na kweli na Roho mtakatifu ndie msaidizi wetu kwani hutusaidia kuomba ipasavyo kwani sisi hatujui kuomba na kila kitu kinachofanyika si kwa nguvu wala kwa uweza ila kwa Roho Mtakatifu.

  Amen na Bwana awape Amani na hekima katika kumtumikia.

  Msafiri Thabit

 143. Ndugu Alfred Katuma,

  Jisikie huru kabisa kutuma somo lolote ulilo nalo ambalo kwa hilo msomaji atapata kitu cha kumjenga katika imani ya wokovu. Kama ungekuwa na uwezekano wa kuyaandika halafu ukayatuma kama ‘MS Word’ ingekuwa vizuri zaidi. Lakini kama ku-scan na kutuma kama PDF ndiyo njia rahisi kwako unaweza kufanya hivyo halafu sisi tutafanya linalowezekana ili yaweze kusomeka kwa urahisi na mtembeleaji wa blog hii.

  Pia tunakaribisha mtu yeye yote mwenye somo ambalo anapenda awashirikishe na wengine. Kama una somo lolote unaweza kutuma kwenye email iliyoandikwa kwenye anuani yetu.

  Mungu akubariki unapotembelea blog hii na kushiriki kutoa michango zenye kujenga katika mada mbali mbali.

 144. Shalom John,

  Mpaka hapo sina swali, ila kwa kweli nilipata shida sana kuelewa ukweli as kila niliyekuwa namuuliza nilikuwa sipati majibu mazuri kama hayo mlionipatia. Bwana awabariki sana na kuwatia nguvu.

  Msafiri Thabit

 145. MT ubarikiwe pamoja na wote wanaotembelea Blog hii inayotusaidia katika kutiana moyo na kujengana katika imani! nashukuru na nishawishika sana kuandika tena hasa baada ya kusoma pale uliposema kwamba umeokoka hivi karibuni na unaomba watu wakuinue kiimani. tuko pamoja tutasaidiana na tutajengana maana usifikiri kwamba wewe hauna cha kutusaidia sisi, unacho sana na wewe ni mtu wa muhimu katika ufalme wa mbinguni ndo maana siku ulipookoka malaika walishangilia sana kama isemavyo Biblia.ushauri wangu kwako ni huu:

  1: jitahidi sana kusoma neno la Mungu maana hili ndilo kiongozi wako wa kukusaidia katika kitu chochote, kama kuna kitu unatakiwa kutamani ni NENO! sisi watumishi ni wanadamu tu wa kawaida japokuwa kuna wengine wanataka waonekane wanajua kila kitu lakini si kweli kuna kitu ninaweza nisifunuliwe mimi ukafunuliwa wewe. Nilipookoka Mungu alinipa kiu ya kusoma neno ambayo naweza kusema haikuwa ya kawaida, sijisifu lakini naweza kukwambia nimeshasoma Bible kuanzia kitabu cha mwanzo mpaka ufunuo kwa mpangilio wa kutoka kitabu hadi kitabu zaidi ya mara tatu tena kwa kumaanisha na kutafakari kwa kina kiasi kwamba ninaweza nikaa nikafundishwa na katika kufundishwa kwa sababu nimesoma neno limejaa kwa wingi ndani yangu kama mtu anayenifundisha atasema kinyume na neno nitajua tu amekosea!!! (kwa sababu ya NENO) nataka nini hapa? Nataka nikujengee hamu ya kuwa msomaji wa Neno litakalokusaidia kupambanua kati ya mchele na mawe. niishie hapo nina mengi ya kukuandikia kuhusu neno lakini kama Strictly gospel wanaweza kuruhusu niwatumie mafundisho ya neno la Mungu ili yarushwe watu wajifunze na tujengane mimi niko tayari kufanya hivyo na kama wako tayari maana najua ujumbe huu wanausoma kabla hawajauruhusu kuwa hewani naomba waseme kama inawezekana kuyatuma kwa kuscan kama PDF na kuwatumia kwa njia ya E-mail. kifupi Mungu amenipa kipawa cha kufundisha na sitaki kujisifu au naomba nieleweke kwamba sijipigii debe ila ninapenda kushirikiana na wapendwa katika kueneza ujumbe wa neno la Mungu.

  2: jambo la pili ni hili, tafuta Baba wa kiroho namaanisha mlezi atakayekulea kiroho. Fahamu kitu hiki: kila aliyeokoka ana mlezi wa kiroho ambaye humlea na kumfuatilia na kumtunza ili akue na kuzidi katika imani. soma kwenye Biblia utaona YOSHUA baba yake wa kiroho alikuwa MUSA, SAMWELI baba yake wa kiroho alikuwa kuhani ELI, ELISHA baba yake wa kiroho alikuwa ELIYA, TIMOTHEO baba yake wa kiroho alikuwa PAULO. sizungumzii mababa wa ubatizo!! nimetumia neno baba lakini mlezi wako wa kiroho anaweza akawa ni mwanamke (inategemea). Hawa watakusaidia kumjua Mungu na kujua mambo ya Mungu, mf. Samweli alipopelekwa na mama yake hekaluni kwa ajili ya kumtumikia Mungu ilifika wakati fulani Mungu akaanza kujidhihirisha kwake lakini kwa sababu alikuwa bado ni mtoto (kwa lugha ya kibiblia tunaweza kusema alikuwa ameokoka hivi karibuni) hakuelewa MUngu alipomwita badala yake alikimbilia kwa Eli na kusema,”mimi hapa kwa kuwa uliniita”. Bwana alifanya hivi mara tatu na Samweli alikwenda kwa Eli, biblia inasema “wakati ule neno la Bwana lilikuwa adimu na hapakuwa na mafunuo dhahiri”. Sasa utafahamu kwa nini point yangu ya kwanza nimekusisitiza kuhusu NENO, maana neno la Mungu likiwa adimu moyoni mwa mtu hata na mafunuo yanakuwa si dhahiri, kitu kikiwa si dhahiri maana yake ni kama kimefichwa, hakiko wazi. utaelewa pia kwa nini Samweli alipokuwa akiitwa na Mungu alikwenda kwa Eli. Ukiendelea utaona Eli kama Baba wa kiroho anayejua kulea aligundua kwamba anayemwita yule mtoto ni Mungu hivyo akamfundisha na jinsi ya kujibu (soma 1Sam. kuanzia mlango wa tatu utaona hiyo habari na itakusaidia kupiga hatua).

  naomba niishie hapa kwa muda nitakuandikia tena ukishatafakari haya lakini fuatilia maisha ya hawa watu niliokutajia na baba zao wa kiroho utaona jinsi ambavyo walikuwa ni watu wenye nguvu za Mungu. hata baba zao wa kiroho walipomaliza muda wao (walipokufa) waliendeleza huduma kwa nguvu ileile. zingatia malezi bora kutoka kwa walezi bora wa kiroho.

  Mungu akubariki pamoja na wasomaji wooooooote!!!!

 146. Mpendwa MT,

  Natumaini majibu mazuri waliyojibu wapendwa ndugu Asher na ndugu Alfred yamejibu swalo lako kikamilifu.

  Mimi nina nyongeza kidogo kwamba Ukristo/Wokovu siyo kama dini zingine ambazo watu hujitahidi kutafuta hadi viongozi wa dini hizo walikuwa wanavaa nini, kula nini, kuacha ndevu zao kwa urefu gani, ikiwezekana waige hadi kutembea kwao ili iwe ndio wamekuwa wafuasi kamili wa dini hizo. Natumaini wewe mwenyewe unaweza kupata mfano mmoja wapo wa dini hizo. Wanafanya hivyo kwa sababu hakuna uhai uliobakia wa kuweza ku-update mambo au mafundisho yao. Kwa hiyo wanajitahidi kutafuta nini walifanya waasisi wa dini ili nao wakopi. Lakini waliookolewa wao hujiweka chini ya Uongozi wa Roho ili awatumie na kuwaongoza apendavyo.

  Ukristo uko hai kwa kuwa Yesu yu Hai hata Leo!

  Ukristo ni tofauti. Hapa nazungumzia ukristo kama ukristo wa kuokoka na siyo ukristo wa dini. Yesu aliahidi kuja kwa Roho Mtakatifu ambaye ndiye angeendeleza mafundisho na Yesu na kuwawezesha wamwaminio kufanya hata makubwa zaidi ya yale aliyofanya Yesu. Kwa hiyo kilichoko kwenye Biblia ni msingi tu lakini maisha ya wokovu na namna ya kuenenda kunafanywa upya kutokana na uhuisho wa Roho wa Mungu. Isingekuwa hivyo basi leo ingebidi watu wakitaka kuombea wagonjwa ingelazimika kukopi akina Paulo walifanyaje; ingelazimika wagonjwa waguse sana pindo za mavazi ya wachunganji na maaskofu ili wapate uponyaji – kama kwa yule mama aliyekuwa na tatizo la kutoka damu; ingelazimika wenye matatizo ya macho wapakwe sana tope zilizofanywa kwa mate nk Lakini mambo hayako hivyo kwa sababu Roho wa Mungu huongoza utendaji wa mambo kutokana na wakati na sehemu. Lakini kila linalofanyika kwa uongozi wa Roho wa Mungu lazima liwe na msingi kwenye Biblia, kama ndugu yetu Alfred alivyotolea mfano.

  Jambo ninalotaka kushauri hapa ni kwammba siku hizi uko wokovu wa aina nyingi. Kuna wokovu wa kutengeneza ambapo watu hujiamulia wenyewe kufanya wanavyoona vema. Lakini ukiwauliza msingi wa jambo hilo wamelipata wapi wanakuwa na kugugumizi au wanakuwa bubu kabisa. Siku hizi lipo tatizo la ‘kuokoka halafu ubaki pale pale ulipo’ pasipo kujali imani ya hapo unapotakiwa kubaki ikoje. Hili pia limeongeza mkanganyiko wa mafundisho kwa sababu watu wengine wamejikuta wanasema wameokoka ukiangalia mafundisho yao ya mwenendo wao ni ya dini kabisa. Hali hii inawapotezea watu kuupata wokovu kamili kama unavyoelekezwa katika Biblia na hivyo kujikuta hawana furaha ya wokovu na hawawezi kusimama kushindana na shetani kwa sababu hawana silaha za rohoni;Efeso 6:10-18. Wakristo ambao hata kukemea pepo tu hadi waende kwa mtumishi!!!!

  Kama inafikia wakati mchungaji [sina uhakika kama ni mchungaji wako] anashindwa kupata maandiko kwenye Biblia yanayoongoza suala fulani basi ujue kuna tatizo. Na inawezekana kabisa kukawa na mambo zaidi ya hilo ambayo ukiuliza msingi wake kwenye Biblia unaweza usipate. Hali ya namna hii ni ya kujihadhari nayo sana.

  Kutokana na maelezo yako kwamba kila mtumishi uliyemuuliza kanisa husema siku za kufunga ni kama ulizooandika. Lakini umeona jinsi wapendwa walivyojibu hapa. Hii inatofautiana na watumishi kadhaa wa kanisani [kwako], ambao hadi sasa wanaendelea kutumika. Natamani kama wangesoma hapa nao ili kama wana msingi wa jambo hilo kwenye Biblia waseme. Lakini kwa ufupi ni kwamba inabidi uwe makini na mafundisho mengine hapo. Yaani uwe mtu unayesoma sana Biblia ili kuweza kubaini kati ya ukweli na uongo.

  Kwa hiyo mpendwa Msafiri kwa kuwa umeshaokoka inabidi umuombe Mungu sana ili akuongoze kukaa mahali ambapo utapata mafundisho ya kweli yote ya Neno la Mungu.

  Ninamalizia hapa kwa sasa. Kama mchango wangu umesababisha swali lolote unaweza kuuliza ili tuendelee kujifunza.

  Mungu azidi kukutunza.

 147. Shalom Asher,
  Bwana apewe sifa nimeuliza swali hili kwa sababu kuna mtu alifuga siku 4 na mchungaji akasema kuwa siku hizo ni za shetani, sijui kama alikuwa sahihi hapo akasema inatupasa kufunga 1,3,7,17,21,28,30 na 40 nilipoomba mafungu sikufanikiwa kuyapata. Nashukuru kwa ufafanuzi wako.

  Pia ndugu yangu Alfred Bwana akubariki kwa ufafanuzi wako ila swali langu lilitokana na maelezo yangu hapo juu na nimejaribu kuuliza watumishi kadhaa kanisani kila mtu anakuambia hakuna watu waliofunga siku zaidi ya nilizotaja hapo juu.

  Bwana awabariki na Roho mtakatifu awaongoze daima, Naombeni mniinue kwani nimeokoka karibuni ili kiwango changu cha kumtumikia Mungu kipande zaidi.

  Msafiri Thabit

 148. BWANA ASIFIWE!
  KUHUSU KUFUNGA NAPENDA KUCHANGIA KWA NAMNA HII,KAMA MTU NI MKRISTO ANAYEONGOZWA NA ROHO MT. SUALA LA KUFUNGA HALIWEZI KUMCHANGANYA MAANA ATAONGOZWA NA ROHO MWENYEWE MAANA KUNA KUFUNGA KWA AINA NYINGI NA WATU WENGI WANAFIKIRI KUFUNGA NI KUTOKULA TU LAKINI KUFUNGA NI ZAIDI YA KUTOKULA, KWASABABU HUYU NDUGU AMEULIZA ZAIDI JUU YA SIKU ZA KUFUNGA NAOMBA NISITOKE NJE YA MADA. NITOE MIFANO MIWILI AMBAYO IMEWAHI KUNITOKEA MIMI:

  NAKUMBUKA WAKATI FULANI NILIKUSUDIA KUFUNGA KWA MUDA WA SIKU 21 NA KATIKA KUKUSUDIA KWANGU NILIMWAHIDI MUNGU KUWA NITAKAA NDANI WIKI MBILI BILA KUTOKA NJE NA WIKI YA TATU NITATOKA NJE NIKIWA KATIKA HALI HIYO HIYO YA KUFUNGA. SASA NILIINGIA NA UTARATIBU WANGU KWAMBA NITAKUWA NINAFUNGA MASAA 12 YAANI KUFIKIA SAA 12 JIONI NITAKUWA NIKIFUNGUA KWA KUPATA CHAI AU UJI LAKINI SIKU ILE YA KWANZA TU YA KUANZA KWANGU KUFUNGA ILIPOFIKA JIONI NIKIWA NIMEMALIZA MAOMBI NA NINATAKA KUFUNGUA ROHO MT.AKASEMA NA MIMI KWAMBA NISILE CHOCHOTE BALI NIENDELEE NA MAOMBI ILIKUWA NGUMU LAKINI NILITII. NACHOTAKA UONE HAPO NI KWAMBA UNAWEZA UKAINGIA KUFUNGA KWA SIKU ULIZOPANGA WEWE NA MUDA ULIOPANGA WEWE LAKINI RATIBA YA KUFUNGA INATOKA KWA ROHO MWENYEWE KWA HIYO MTU ASIJE AKAKWAMBIA KUNA IDADI AU SIKU ZINAZOTAKIWA KATIKA KUFUNGA INATEGEMEA NA JINSI ULIVYOJIPANGA NA MUNGU WAKO MAANA KUFUNGA HAKUMBADILISHI MUNGU WALA SHETANI KUFUNGA KUNAKUBADILISHA WEWE MFUNGAJI NA NI SEHEMU YA UPANDE WAKO KATIKA KUMTAFUTA AU KUTAFUTA USO WA MUNGU.

  MFANO WA PILI NI HUU ULIONITOKEA TULIPOKUWA NA WENZANGU KATIKA MAOMBI YA MAPATANO. TULIKUWA TUMEPATANA KUFUNGA MASAA 24 NA USIKU ROHO MT. AKASEMA NA MIMI KWAMBA TUUNGANISHE MAOMBI TOFAUTI NA TULIVYOPATANA BADALA YA KUFUNGUA ASUBUHI TUUNGANISHE MPAKA JIONI MAANA TULIKUWA TUNAOMBEA MKUTANO WA INJILI. ILINIPA SHIDA NIKAANZA KUJIULIZA WENZANGU WATANIAMINI! AU WENZANGU WATAWEZA KUUNGANISHA MAOMBI HAYA MAANA WENGI WALIKUWA BADO NI WACHANGA KATIKA KUFUNGA, LAKINI ROHO MT.AKASEMA YEYE NDIYE ALIYESEMA NA NDIYE ATAKAYEWATIA NGUVU, KWA KWELI SIKUKUBALI KIRAHISI NIKASEMA MUNGU NITAJUAJE KAMA NI WEWE UNAYESEMA NAMI? PALEPALE AKAWEKA NDANI YANGU ANDIKO KUTOKA KATIKA KITABU CHA WAFALME SIKUMBUKI KWA SASA SURA NA MSTARI WA NGAPI MAANA SINA BIBLE HAPA LAKINI WASOMAJI WA BIBLIA WATAKUMBUKA, NI HABARI YA NABII ELISHA ALIPOKARIBIA KUFA ALIMWITA MFALME WA ISRAEL AKAMWAMBIA ACHUKUE UPINDE NA MSHALE AKAMWAMBIA PIGA NA ALIPOKUWA AKIPIGA ELISHA AKAWA ANATOA UNABII KUPITIA MSHALE ULIOKUWA UKIPIGWA, LAKINI UKIENDELEA KUSOMA UTAONA YULE MFALME ALIPIGA MARA TATU AKAACHA NA ELISHA AKAMKASIRIKIA MFALME AKAMWAMBIA ILIKUPASA KUPIGA MARA NYINGI NDIPO UNGEWAPIGA WASHAMI NA KUWAANGAMIZA KABISA… (Strictly Gospel: Habari hii inapatikana katika 2Wafalme 13:14-19)

  NILIPOTAFAKARI HIYO MISTARI ROHO MT.AKASEMA MKIENDELEA KATIKA KUFUNGA MPAKA KUFIKIA JIONI NITAFANYA MAMBO MAKUBWA LAKINI MKIISHIA ASUBUHI NITAFANYA LAKINI KIDOGO. NIKAWASHIRIKISHA WENZANGU TUKASOMA HIYO MISTARI NA UNAJUA WAKASEMA KAMA MUNGU AMESEMA SISI HATUWEZI KUPINGA; TOFAUTI NA MIMI NILIVYOKUWA NIKIFIKIRI.

  KITU NINACHOTAKA KUSEMA HAPO NI MUDA AU SIKU ZA KUFUNGA HAZINA SHERIA YOYOTE WALA IDADI NI KUJIPANGA KWAKO NA MUNGU WAKO.

 149. kuhusiana na suala la watu kunadi huduma zao ni kukosa kujiamini na kutafuta watu kinguvu ili wapate fedha ,tukiangalia Yesu alikuwa akifanya miujiza na watu walikuwa wanapashana habari na kumtafuta ila kwa kweli watumishi wamegeuka wenyewe kutafuta watu.neno la Mungu sisi ni nuru ya ulimwengu sidhani kama nuru itaitafuta giza ila nuru huondoa giza ,waache tabia hiyo kama wanasema wanamwanini Mungu wamwamini katika hilo ,Yesu siyo mganga au daktari aliyespecialize magonjwa anaweza yote katika yote ,inakuaje watu wanataja magonjwa ambayo wanajua watu wamekata tamaa wanaweza kwenda mbona hawasemi malaria ,tumbo la kuendesha au mafua kama wameamua kutangaza uweza wa Yesu watangaze yote wasimuwekee vipimo.hao ahao wanaosema ndoa zipone za watu za kwao zimevunjika siku nyingi na wameshindwa kuzirejesha waanze wao kwani Mungu ni Mungu wa kurejesha,Yesu alianzia nyumbani kwake Yerusalem ndipo akaenda Samaria.nawashauri watumishi waangalie kusudi la kristo ilikuwa kuokoa na kuwatoa watu kwenye maangamizi yao na siyo kufanyia deal la kupata mishiko.wamegeuza sehemu ya kuganga njaa zao

 150. Mpendwa MT,

  Bwana Yesu apewe sifa,

  Ninavyofahamu mimi, hakuna mahali katika biblia panapotoa idadi ya siku za kufunga, au panapoelekeza siku ambazo mtu anapaswa kufunga. Mara nyingi watu hufunga kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu na wakati mwingine hutemegemeana na jambo walilo nalo.

  Biblia imezungumza juu ya kufunga na kuomba, tangu zamani za agano la kale watu walikuwa wanafunga kwa muda ambao walikusudia kufanya hivyo. Mfano Esta alifunga na kuwaomba Israel wafunge muda wa siku tatu (Esta 4:16,17), Danieli alifunga siku 21 (Daniel 10:2,3), watu wa Ninawi walifunga baada ya kuambiwa kuwa mji wao utaangamizwa, lakini ukisoma Yona 3, biblia haijasema walifunga siku ngapi, lakini walifunga).

  Bwana wetu Yesu Kristo alifunga siku arobaini, mchana na usiku, (Mathayo 4:1,2) lakini hakuwahi kutoa maagizo kuwa watakatifu wafunge siku ngapi au kwa mlolongo upi wa siku. Alichokisema Yesu ni kuwa kuna wakati tutakuwa na mambo ambayo itatubidi kufunga (Mathayo 17:21) n.k.

  Kama nilivyosema hapo juu, sijawahi kukutana na andiko linaloelekeza mtiririko wa siku ambazo mtu anapaswa kufunga, nilichowahi kukiona ni mifano ya watu walivyofunga na matokeo ya kufunga kwao. Aidha, kuna maeneo mengi ambayo Biblia imeonyesha kuwa watu walifunga bila kusema walifunga siku ngapi.

  Inawezekana huyo aliyeanzisha huo mtiririko aliangalia maeneo ambayo biblia imetaja na siku ambazo watu walifunga. Hata hivyo ili jambo liwe fundisho ambalo linapaswa watakatifu walifuate, ni lazima kuwepo maelekezo kutoka kwenye neno la Mungu lenyewe. Kwa kuwa sijawahi kukutana na neno lenye kutoa mtiririko wa namna ya kufunga, kama kuna mtu ana ujuzi wa neno la Mungu katika hili, basi nitafurahi sana kujifunza kutoka kwake, lakini ninachokiona mimi ni kuwa mtu anaweza kufunga kutokana na kuongozwa na Roho Mtakatifu na atafunga kwa idadi ya siku alizoongozwa kufanya hivyo. Wakati mwingine mtu anakusudia kufunga na Mungu anamwezesha kufunga, lakini mtiririko wa siku, sijawahi kuona katika neno la Mungu, ila kama upo basi tunaweza kujifunza.

  Hivyo ndugu yangu MT kama unataka kufunga, wewe funga muda ule uliokusudia moyoni mwako bila kutafuta mtiririko maalum wa siku. Jambo la msingi ni uongozi wa neno la Mungu na Roho Mtakatifu.

  Shalomu

 151. Bwana apewe sifa,

  Wapendwa naomba kujua siku za kufunga ni ngapi? yaani kama kuna idadi fulani inayotakiwa kwani kuna mtu alifunga siku nne akaambiwa kuwa ni makosa alitakiwa kufunga 1,3,7,14,21,28,30 na arubaini ndo siku halali za kufunga je ni kweli na kama ni kweli naomba mafungu kutoka katika Biblia.

  Bwana awe nanyi.

  MT

 152. Dada vick.asante kututakia amani.ila hata mimi nataka kukujulisha kuwa YESU mpaka leo hii analeta manabii,wachungaji; na kadhalika sio kuwa wanajifanya kujiita MANABII , MITUME au WACHUNGAJI ni Bwana anayetenda hayo kweli wapo kabisa wanaopewa hivyo vyeo isipokuwa wote wanaomwamini BWANA ni watumishi wa YESU ila kuna tofauti ya huduma katika kirsto Yesu.
  Tunakupenda endelea na Bwana.

 153. hello its me again
  naomba tu, tuombeane na kujengana katika misingi ya kristo, haijalishi uko wapi, uwe na imani, lakini bado sioni haja ya mtu kujiita nabii i still dont get it and i dont really think we should have levels into huduma, if you are just a believer that’s who you are, uchungaji uaskofu na mengineyo ni vyeo vya kikanisa, my problem is when you start your name with high italics that you are the chosen one.. you are mighty… please… only one is.. we know who it is.. sisi wooote ni watumishi wake, na tubaki hivyo hivyo !!
  mbarikiwe mpaka mshangae !

 154. Bwana wetu Yesu asifiwe sana!
  Kwa kweli matangazo kama haya mimi nayaona kama ni utafutaji wa pesa tu, kwani wameona kuwa watu siku hizi wamekuwa na matatizo mengi sana ya kiafya na ya kiuchumi.
  Sasa wahubiri(feki) hebu niwaite hivyo kuwa wanatumia nafasi hiyo kutaja mahitaji ya watu kuwa wanaweza kutatuliwa kisha wanatozwa mali/pesa.

  Kwa kweli mimi naomba wale wote wanaofanya hivyo waache mara moja kwani ndio hao hao watakaosema siku ya mwisho kuwa tulitoa pepo kwa jina lako halafu Bwana Yesu hatawatambua kabisa.
  Na pia kwa wale wote waliowezeshwa kulifahamu hilo, wazidi kuliombea sana kwa kumaanisha ili hao hao wanaofanya GOSPEL DILI waache kabisa na badala yake wamfuate Yesu na waongozwe jinsi ya kuhudumia watu.
  Naomba niwaambie wahubiri na hao wanaoanzisha hizo MINISTRIES kuwa hebu jitahidini kwanza kwanza kumuweka Mungu mbele then hayo yote mengine kama Pesa , mali na mazuri mengine yatafuata kabisa kama ukifanya kwa uaminifu.

  Ni hayo tu kwa leo,
  Mungu apitaye fahamu zote na awabariki na kuwaongoza kufanya yale yote yanayompendaza yeye.
  Mubarikiwe sana.

  Ni wenu ndugu yenu,
  Lusekelo Richard Mwambyalo
  Wa Arusha-Tanzania
  +255 755 530 779

 155. kwanza kabisa tunalotakiwa kujua ni kwamba,madhehebu mengi yamekuwa ni biashara,ndiyo maana kumtafuta MUNGU aliye hai imekuwa ni ishu kwani ktk maandiko matakatifu YESU anasema njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo ya dhambi yeye atakutua,je niulize swali kila wakati wa mikutano ya kiroho kuna watu wanajitokeza kila wakati kwa kuombewa na kila mkutano watu km hao wamo si wanamjaribu Mungu kwani hawana imani,kwa sababu kila mkutani lazima atoke mbele kwa kuombewa yaani haponi hata kipindi kimoja,ndugu wasomaji lazima tuangalie vitu km hivyo havina uhakika ndani yake,na imani hawana.

 156. Dada Sabihi,
  Nafurahi kuwa msaada SG, pamoja na wana wengine wote wa Mungu tunaochangia hapa. Tuombeane ili siku moja tuonane mbinguni. Hilo ndilo lengo kuu la mijadala na mafundisho yote.
  Mungu atusaidie!

 157. Ndugu Lisa Wairimu,

  Si Bernad Mwenda peke yake ambaye anastahili pole, kama ni kweli, kutokana na utata wa ibada kwa Maria pamoja na sanamu vinavyofanyika katika kanisa la Katoliki.

  Kumbuka ni wewe ulianzisha mada hii ya Karismatiki katika Katoliki. Mada yako uliyoleta imeibua mswali mengi mazuri tu na watu wengi walikuwa wanafuatilia ili kusikia majibu ya maswali hayo kwa lengo kwamba LABDA YANGETOA MWANGA KUHUSU UHALALI WA IBADA HIZO AMBAZO ZINAMWINUA MARIA HADI KIWANGO CHA MUNGU NA USHIRIKI WA KARISMATIKI NDANI YA KATOLIKI

  Mtu aliyekuwa anatazamiwa ajibu maswali hayo ni wewe kwa sababu unaonekana kuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu Katoliki na Karismatiki. Lakini ninashangaa kwamba badala ya kujibu maswali yaliyoelekezwa kwako wewe unakuja kutoa pole kwa Bernad Mwenda. Sijajuwa ni kwa nini yeye peke yake kwa sababu ni wengi sana ambao tuna ufahamu wa namna hiyo kama wa Bernad. Hii ni kutokana na maandiko matakafitu yaani Biblia.

  Mimi ninakuomba ujibu maswali maana mjadala wa Karismatiki umekwama kwa sababu ya maswali kukosa majibu. Sasa kama wewe kwa kuwa UNA UFAHAMU WA KUTOSHA KUHUSU TAFSIRI NZIMA YA TENDO LA BIKIRA MARIA PAMOJA NA TAFSIRI YA KUABUDU inabidi utufafanulie hapa ili Bernad Mwenda pamoja na wengine tuondokane na na utata huo.

  Maswali yaliyoulizwa yanatokana na ukweli uliondikwa katika Biblia yenye vitabu 66 ambapo umeshapewa sababu za kwa nini vile vitabu vingine 6 si sehemu ya Biblia. Kwa hiyo wakati nawe unajibu maswali hayo inabidi ulete majibu kwa kutegemeana na Biblia yenye vitabu 66. Ukijibu kutokana na mfundisho ya Biblia yenye vitabu 72 utakuwa unaleta mambo ya dini. Na mara nyingi tulishaongea hapa kwamba dini hata kama ni nzuri au kubwa namna gani lakini kama haifundishi Kweli ya Mungu kutokana na mafundisho ya Yesu Kristo dini hiyo haiwezi kumsaidia mtu kufika mbinguni.

  Ninaongeza maswali mengine ambayo yametokana na mchango wako:
  Kama kanisa Katoliki ni takatifu kwa nini Karismatiki? Kama imani ya Kitatoliki ina utakatifu wa kutosha Karismatiki wanatafuta nini kuanzisha ibada ambazo zinapingana na utaratibu wa Kanisa hilo? Je, ina maana watu wanaojiunga na Karismatiki wanaukimbia au wanautafuta Utakatifu?

  Maswali tuliyouliza mimi pamoja na wengine kama yangejibiwa natumaini Bernad Mwenda angekuwa ameshapata uelewa. Sasa kwa kuwa maswali yameshaulizwa kinachosubiriwa ni majibu ili tuendelee kujifunza ili tuondokane na utata huu wa Karismatiki ndani ya Katoliki!

  Nasubiri kwa hamu kupata majibu ya maswali yaliyoulizwa!

 158. Shalom Bernad,
  Bwana atusaidie sana, nafikiri tafsiri ya neno kuabudu limekupiga chenga kidogo pole, na pia tafsiri ya tendo zima la Bikira Maria kwa kanisa takatifu katoliki hulijui, ningependa uulize kabla ya kutoa comment.

 159. Shalom watumishi wa Mungu.
  Mimi pengine ninamtazamo wa kuunga mkono hayo matangazo kutokana na mabadiliko tuliyonayo, kwa sababu sasahivi watu wanasukumwa mno na matatizo waliyonayo katika kutafuta ufumbuzi wa lazima sasa usipoandika maombi yatatatua shida za watu kwa kuzitaja moja kwa moja nani atageukia injili? kuhusu swala la utoaji ni lazima kutoa sadaka itakayosukuma maombi japo malipo ya maombi hayalingani na majibu Mungu Baba anayorudisha maana ni maradufu, tusishangae kwani hata waendao kwa waganga wanatoa pesa! Jamani inabidi tuwasupport tuwainue Watumishi wetu mnataka wawe omba omba? Lazima watumishi wawe Matajiri ndipo watu waamini kuwa kwa Mungu Baba kuna kila kitu na Pesa inawatumikia watumishi na si watumishi watumikie Pesa. Ahsanteni sana.

 160. Mimi nadhani kuna mambo mawili hapo, au kuingia mitini, au ukweli umeingia ndani yake sasa huenda anachukua hatua, atakapoibuka tena atakuja na shuhuda. Mimi binafsi ninawashukuru na kuwaombea wachangiaji wote, kupitia ninyi nimejifunza mambo mengi mno, mengine mmechangia kuyasahihisha kutoka nilivyoelewa mimi , kwenda kwenye uhalisia wa jambo lenyewe. MUNGU WANGU AWABARIKI/Tuendelee kuombeana, na kujifunza.

 161. Mimi nilikuwa nimefurahishwa sana na mjadala huu. Na nilipokuwa nafuatilia majibu ya Lisa nilikuwa nafikiri angeendelea zaidi na zaidi ili sisi wasomaji tuweze kujifunza na kama ikiwezekana kupata ukweli kuhusu uhalali au kutokuwa halali kwa Karismatiki [ambayo mimi naiona kama dini nyingine] kuota ndani ya dini ya Katoliki. Ndiyo maana tarehe 22/6/2009 nilimuomba dada Lisa awe mvumilivu kwa kuwa jinsi mada hii ilivyo inahitaji kwenda nayo pole pole maana ni ndefu. Lakini sasa sielewi kama Lisa amekata tamaa au anaandaa majibu mazuri zaidi. Natamani sana kama angeendelea ili kwa pamoja tuzidi kujifunza.

  Uzuri wa mjadala ni pale unapofikia suluhisho. Na suluhisho si lazima kukubaliana na upande mwingine, mimi nionavyo hata mtu akisema yeye habadilishi msimamo wake hilo nalo ni suluhisho. Kitakachomhukumu ni kwamba alishaelezwa ukweli. Mjadala huu ulivyokuwa unaendelea natumaini kuna maswali ambayo bado yalihitaji majibu kabla ya kufikia suluhisho lolote lile. Kuucha mjadala huu namna hii ni kuuacha hewani. Mimi nilitegemea nijifunze mengi sana kutokana na Katoliki na Karismatiki. Na nilitegemea Lisa angenisaidia kwa hilo. Lakini kama kuna mtu mwingine anayefuatilia mjada huu anaweza kuendelea na kujibu maswali kadahaa yaliyoulizwa na mimi na wachangiaji wengine, wakati tukisubiri labda Lisa anatakuja na majibu.

  Napenda sana uwanja huu wa mijadala kwa sababu watu hujadiliana kama vile tuko meza moja. Na hapa kuna uhuru wa kuuliza maswali hata ambayo pengine katika kanisa au dini fulani yasingeruhusiwa, si kwa sababu hayafai, bali kwa sababu majibu yake yatadhihirisha mapungufu au makosa ya kanisa/imani hiyo kwa kulinganisha na nenola Mungu. Lakini hapa tunaweza kujifunza mambo ambayo hata viongozi wetu wengine wa dini au makanisa hawayafahamu.

  Jambo jingine ninalopenda kuwashauri wasomaji na wachangiaji wenzangu ni kwamba mtu ukianzisha mjadala, ambao wewe ndio unafikiri unaweza kuwa msemaji mkuu, hakikisha una matirio za kutosha kuhusu jambo unalolizungumzia na pia kuhusu Biblia. Lakini hata kama hauna ujuzi sana wa kutosheleza hayo ni vizuri basi unapopewa ukweli kuhusu jambo hilo ulilolileta ukubali kujifunza, kwa kuwa hapa tunajifunza. Lakini hata kama hutaki kukubali ni vizuri ukatoa suluhu [conclusion] ili watu wafahamu kwamba mjadala huo umeuchukuliaje.

  Kuna watu kadhaa walianzisha mijadala huko nyuma lakini wakaingia mitini. Kukimbia maswali uliyoulizwa pasipokuyajibu [hata ‘ndiyo’; ‘hapana’; ‘sijuwi’; pia ni majibu] mimi naona haitusaidii kujifunza lolote. Ni kama vile kuchovya tonge kwenye mboga halafu lisifike kinywani!

  Tuendelee kujifunza

 162. Jamani mbona mafundisho hapa yamekwama? na hatujafika mwisho maswali hayajajibiwa tunasubiri majibu tuzidi kujifunza.Dada LISA njoo uendelee TUNAKUPENDA SANA.

 163. Lisa Wairimu pamoja na wengine wanaoamini dini ya Katoliki.

  Maandiko yanasema, Mungu ni Roho nao waniabuduo humwabuduu katika Roho na Kweli.

  Sasa inakuwaje mtu unayesema kuwa ni Mkristo tena anadai kuwa ameokoka aanze kumwabudu Mungu kwa kutumia nyenzo nyingine kama Bikira Maria na Sanamu n.k?

  Mungu Baba ni Roho, Mungu Mwana ni Roho, na Mungu Roho Mtakatifu ni Roho.
  Sifa za Mungu, ni kuwepo mahali popote wakati wowote muda wowote n.k. Tukimwomba Zanzibar yupo, akiombwa Marekani yupo, wakati huo huo akiombwa Uarabuni yupo pia, n.k,n.k. Hizo ndizo sifa za Mungu.

  Mungu hana mwanzo wala mwisho, yeye ni wa milele. Bikira Maria, yeye alikuwa mwanadamu aliyekuwa na mwanzo, aliyekuwa mtakatifu kama mimi niliyeokoka. Anachokuwa ananizidi ni kwamba yeye alipata neema ya kumzaa Yesu katika mwili, kama ambavyo pia Elizabeti alipata neema ya kumzaa Yohana mbatizaji aliyembatiza Yesu. Mimi nimepata neema ya kuzaliwa mara ya pili, yaani kuokoka katika Kristo Yesu ambapo hata Mariamu sifa hizo anazo.

  Mariamu anayo roho moja kama mimi, ninaamini pia kuwa kwa vile alikufa akiwa mtakatifu, amevaa mwili mpya kule mbinguni, hivi sasa yuko mbinguni kwa Mungu.

  Kwa msingi huo, kwa vile yeye ni mwanadamu kama mimi yanayofanyika hapa duniani hayaoni.

  Inakuwaje sasa mwanadamu uanze kuchukua hatua za kumwomba mwanadamu mwenzio ambaye hata hakusikii wala hana uwezo wa kukuona?

  Nanataka nikufahamishe kuwa, iwapo umeokoka na uko katika usafi na utakatifu wote, basi upo sawasawa na Mariamu aliyemzaa Yesu. Nawe pia huna uwezo wa kuyajua mambo yanayoendelea sehemu nyingine nje ya eneo ulilopo. Na pia utakapokufa na kuingia mbinguni, hutakuwa na uwezo wa kuyajua yanayoendelea huku duniani kama ambavyo nimeelezea juu ya Mariamu.

  Kwa vile hutakuwa na uwezo huo kwa sababu wewe ni mwanadamu, na Mariamu hana uwezo huo kabisa kwa sasabu yeye naye ni mwanadamu kama wewe wala si Mungu. Mwenye uwezo wa kusikia maombi ya watakatifu na kuyajibu apendavyo yeye ni Mungu pekee, na wala hakutoa uwezo huo kwa mwanadamu awaye yeyote. Yesu Kristo alituagiza mapema kabisa kuwa tunapoomba tuombe kwa jina lake kwa sababu yeye ni Mungu.

  Vivyo hivyo hata kwa wasujudu sanamu katika dini ya Katoliki na wengine wa namna hiyo, iwapo mtu anaenda kusujudia msalaba au vyovyote vinavyofanana na hivyo, hamwabudu Mungu katika Roho na kweli, bali anaabudu sanamu.
  Shalom!
  Tuendelee kujadiliana.

 164. Asante ndg Steve M kwa link zinahohusiana na Maria mama wa mwokozi wetu Yesu Kristo..

  Mimi nimefikiria kwamba inaweza isiwe rahisi kwa mtu mwingine kupata muda wa kufuatilia link zile kwa hiyo nimechukuwa machache ili niyaweke hapa kumrahishia msomaji aelewe ni kweli Katoliki humsheshimu tu au pia humwabudu Maria?. Katika niliyoyaweka hapa pia kuna habari ya Maria kama Mediatrix na Co-Redemtress, mambo ambayo Lisa katika majibu yake alisema siyo mafundisho ya Kikatoliki! [kama alivyonukuu ndugu Steve M]. Kwenye paragraph ya mwisho kuna maneno yanayosema kwamba Maria hushirikiana na Yesu Kristo katika mchakato wa mtu anapozaliwa mara ya pili, kiroho!

  Endelea kusoma yafuatayo…….

  ..Besides these recollections, moreover, as the sacred Mysteries pass by they cause our prayers to be transformed into impulses of entreaty that have an indescribable power over the heart of Mary. Yes, we fly to thee, we miserable children of Eve, O holy Mother of God. To thee we lift our prayers, for thou art the Mediatrix, powerful at once and pitiful, of our salvation. Oh, by the sweetness of the joys that came to thee from thy Son Jesus, by thy participation in His ineffable sorrows, by the splendours of His glory shining in thee, we instantly beseech thee, listen, be pitiful, hear us, unworthy though we be!

  ..celebrating and honouring the Mother of God, the mighty succourer of the Christian people, the most glorious Queen of Heaven. For Our own part, We confirm with all Our heart the favours and indulgences We have already awarded upon this point.

  ..Now may God, “Who in His most merciful Providence gave us this Mediatrix,” and “decreed that all good should come to us by the hands of Mary” (St. Bernard), receive propitiously our common prayers and fulfill our common hopes. May you receive a pledge thereof in the Apostolic Benediction which We give to you, to your clergy, and to your people, with all affection in Our Lord

  ..The recourse we have to Mary in prayer follows upon the office she continuously fills by the side of the throne of God as Mediatrix of Divine grace; being by worthiness and by merit most acceptable to Him, and, therefore, surpassing in power all the angels and saints in Heaven. Now, this merciful office of hers, perhaps, appears in no other form of prayer so manifestly as it does in the Rosary. For in the Rosary all the part that Mary took as our co-Redemptress comes to us, as it were, set forth, and in such wise as though the facts were even then taking place; and this with much profit to our piety, whether in the contemplation of the succeeding sacred mysteries, or in the prayers which we speak and repeat with the lips
  As we contemplate Him in the last and most piteous of those Mysteries, there stood by the Cross of Jesus His Mother, who, in a miracle of charity, so that she might receive us as her sons, offered generously to Divine Justice her own Son, and died in her heart with Him, stabbed with the sword of sorrow.

  ..Thence the Rosary takes us on to the Glorious Mysteries, wherein likewise is revealed the mediation of the great Virgin, still more abundant in fruitfulness. She rejoices in heart over the glory of her Son triumphant over death, and follows Him with a mother’s love in His Ascension to His eternal kingdom; but, though worthy of Heaven, she abides a while on earth, so that the infant Church may be directed and comforted by her “who penetrated, beyond all belief, into the deep secrets of Divine wisdom” (St. Bernard

  ..Therefore we behold her taken up from this valley of tears into the heavenly Jerusalem, amid choirs of Angels. And we honour her, glorified above all the Saints, crowned with stars by her Divine Son and seated at His side the sovereign Queen of the universe

  ..No man can meditate upon these without feeling a new awakening in his heart of confidence that he will certainly obtain through Mary the fulness of the mercies of God. And to this end vocal prayer chimes well with the Mysteries. First, as is meet and right, comes the Lord’s Prayer, addressed to Our Father in Heaven: and having, with the elect petitions dictated by Our Divine Master, called upon the Father, from the throne of His Majesty we turn our prayerful voices to Mary

  ..Thus is confirmed that law of merciful meditation of which We have spoken, and which St. Bernardine of Siena thus expresses: “Every grace granted to man has three degrees in order; for by God it is communicated to Christ, from Christ it passes to the Virgin, and from the Virgin it descends to us.” And we, by the very form of the Rosary, do linger longest, and, as it were, by preference upon the last and lowest of these steps, repeating by decades the Angelic Salutation, so that with greater confidence we may thence attain to the higher degrees-that is, may rise, by means of Christ, to the Divine Father. For if thus we again and again greet Mary, it is precisely that our failing and defective prayers may be strengthened with the necessary confidence; as though we pledged her to pray for us, and as it were in our name, to God.

  .. A soul that shall devoutly repeat these prayers, that shall ponder with faith these mysteries, will, without doubt, be filled with wonder at the Divine purposes in this great Virgin and in the work of the restoration of mankind. Doubtless, this soul, moved by the warmth of love for her and of confidence, will desire to take refuge upon her breast, as was the sweet feeling of St. Bernard: “Remember, O most pious Virgin Mary, that never was it heard that any who fled to thy protection, called upon thy help, and sought thy intercession, was left forsaken

  ..Moreover the conciliar text had already described the meaning of the title “Mediatrix” when it said that Mary “by her manifold intercession continues to bring us the gifts of eternal salvation” (Lumen gentium, n. 62).

  ..With regard to the objections made by some of the Council Fathers concerning the term “Mediatrix”, the Council itself provided an answer by saying that Mary is “a mother to us in the order of grace” (Lumen gentium, n. 61). We recall that Mary’s mediation is essentially defined by her divine motherhood. Recognition of her role as mediatrix is moreover implicit in the expression “our Mother”, which presents the doctrine of Marian mediation by putting the accent on her motherhood. Lastly, the title “Mother in the order of grace” explains that the Blessed Virgin co-operates with Christ in humanity’s spiritual rebirth

 165. MIMI nina mengi sana lakini naona kaka STEVE na kaka JOHN PAUL wanapitia maswali yangu. mimi sikubaliani na mengi maana baada ya mtu kuokoka hutakiwi tena kurudia mafundisho manyonge. ikiwa mnasali jumapili pamoja hii ni hatari maana mmeshakwepa mafundisho manyonge iweje tena mchanganyane na mhubiri awe padre wa siku zote ambaye mlikuwa mnafundishwa na yeye na mmeamua kujiunga na karismatiki. inakuwaje tena yeye awafundishe nyie ambao mmegundua mapungufu yao? Nakupenda dada LISA.

 166. Katika kusoma comment nimetambua kuwa mama MARIA alikufa jibu la bila kubisha hatuwezi kuomba atuombee.angekuwa hai sawa lakini kama amekufa haiwezekani kabisa.mbarikiwe wote.

 167. Dada Levana,

  Ninachofahamu mimi ni kwamba Mariamu, mama wa Yesu, alishakufa! Ndiyo maana nimemuuliza Lisa kama Katoliki wanafundisha kwamba mtu aliyekufa anaweza kuwaombea walio hai.

 168. Mch. Dk Malisa,
  Mimi binafsi nashukuru kwa maelezo ya msingi kuhusu imani ya Kikatoliki.

  Lisa,

  Nashukuru sana kwa majibu yako. Ninaendelea kujifunza kitu. Ninasubiri kwa hamu juu ya yale maswali ambayo unatafutia majibu. Lakini kwa sasa, wakati nasubiri majibu hayo, bado nitahitaji ufafanuzi juu ya masuala kadhaa yaliyojitokeza kutokana na majibu yako kwenye maswali niliyouliza mimi. Mahali pengine ninaweka ufafanuzi:

  1.Suala la kunywa pombe nilishaandika mengi sana na wengi walishachangia kuhusu hili katika mada ya “Je, ni halali kwa mkristo kutumia kileo?” Ukitafuta kwenye maswali utaipata mada hiyo.

  2. Kwa kuwa unakiri mwenyewe kwamba ni bora kumfundisha mtu madhara ya kitu ili aache mwenyewe kuliko kumlazimisha: Unakubaliana nami kwamba wanaokunywa pombe bado wanakunywa kwa sababu hawajuwi madhara yake? [Kama vile wewe ulivyokuwa unakula nyama za matambiko?]

  3. Suala la Mariamu kuwaombea watu niliuliza hivyo kwa sababu sidhani kama ni kwa bahati tu kwamba Katoliki wote dunia nzima wamtaje huyo huyo Mariamu kuwaombea kama si kwa agizo maalumu. Nilitegemea kama ni sawa na mtu kutaja kikundi fulani kimuombee basi Katoliki wengine pale kwenye sehemu ya Mariamu kuwaombea wangeweka jina jingine. Lakini suala hili litakamilika utakapoleta majibu ya swali 3&4 katika maswali yangu yaliyotangulia haya.

  4. Umeandika kwamba msingi wa Katoliki ni Kristo baada ya kumsimika Petro na ukaandika hata kama watu hawa walikuwepo [nadhani unamaanisha wakristo wa kwanza] hawakuwa na misingi ya Kikristu.

  Naomba tu kukuambia kwamba wakati wa mapambazuko ya Injili hakuna mtu aliyekuwa anajiita mkristu/mkristo kwa maneno tu pasipo kuwa na msimamo wa kweli. Siku hizi sisi ndio tunacheza na Neema hii ya wokovu. Watu walikatwa kwa msumeno; wengine walikaangwa kwenye rami inayochemka; wengine walichunwa ngozi wakiwa hai nk nk. Hawa wote wasingeweza kustahimili mateso ya namna hiyo kama hawakuwa na misingi ya Kikristo. Na ni kwa sababu ya kusimama kwao namna hiyo kwenye zamu zao ndiyo maana hata nasi tumeipata injili hii. Lakini inasikitisha sasa watu tunacheza na wokovu kama vile ni kitu cha mzaha!

  4. Nilikuuliza kwamba kama Katoliki msingi wake ni Wokovu ilikuwaje wakabadilika kiasi cha kuanza kuupinga wokovu uliokuwa unahubiriwa na waasisi wake? Katika kujibu hili umeandika pamoja na yafuatayo “KILA KIONGOZI ANAPOINGIA MADARAKANI ANAWEZA KUBADILISHA KABISA SYSTEM” Mimi ninavyofahamu [na hata wewe uliandika kwamba Katoliki halijameguka toka mwanzo wa sababu ya kuwa na uongozi mmoja] ni kwamba Katoliki ni moja ya dini ambazo zina misingi inayolindwa sana isije ikabadilika mwelekeo wake. Sasa tukichukulia maneno uliyoandika. Kutokana na hali hiyo,

  i) Je, tunaweza kusema Katoliki halina misingi imara kiasi ambacho kila kiongozi akiingia anaweza kubadilisha SYSTEM kabisa?
  ii). Kutokana na kila kiongozi kuwa na uwezo wa kubadilisha SYSTEM kama avyotaka, Je, tunaweza kusema kwamba Katoliki ya sasa yawezekana ikawa tofauti na ile ya mwanzo? [Ningefurahi sana kama tunaweza kupata ushahidi kutoka katika kumbukumbu za kanisa kama kuna wakati huko nyuma Katoliki ilikuwa inahubiri wokovu ule uliohubiriwa na mitume]

  5. Kuhusu kupingana kwa maandiko ya vitabu vile sita na maandiko mengine ya Biblia ile yenye vitabu 66:
  i).Je, Ulishawahi kufundishwa au kuuliza kwa nini Biblia ya Katoliki inatofautiana na Biblia ile inayotumiwa na Wakristo wengine?
  ii) . Je,Unafikiri Waprotestanti walivikataa tu vile vitabu 6 pasipo kuwa na sababu ya maana?
  iii). Je, Kama utafundishwa maneno ya kupotosha yaliyoko kwenye vitabu vile 6 uko tayari kuufuata ukweli?

  6. Umesema Karismatiki wanatumia Biblia takatifu, japo hujaandika ni ipi kati ya ile ya Katoliki au ya Waprotestanti. Sasa kama Karismatiki wanashiriki kikamilifu ibada ya Katoliki ikiwa ni pamoja na kuombea wafu, kumuomba Mariamu awaombee, kupiga magoti mbele ya sanamu [ingawa unatetea hili kwa nguvu zote pasipo kuonyesha maandiko yoyote] na mengine yote na kama yote hayo wanaridhika nayo;

  i) Je, ni nini kinawafanya wasitosheke na ibada hiyo hadi wafikie hatua ya kufanya ibada zingine pembeni?
  ii) Je, ibada ya Karismatiki ina tofauti au haina tofauti na ile ya Katoliki?
  iii) Kama ibada hizi zinatofauti Je, huoni kama hapo mkarismatiki ana IMANI MBILI MOYONI MWAKE? [Nini maslahi yake ya kusali ibada mbili zilizo tofauti?]
  iv) Kama ibada hizi hazina tofauti UAMSHO huu unaoletwa na Karismatiki utakujaje ikiwa wanachoshiriki Katoliki na Karismatiki ni kile kile?

 169. Dada Lisa,
  REJEA KIPENGELE CHAKO (3) KUHUSU PAPA. KWA UELEWA WANGU HAPAKUWAPO NA PAPA KABLA YA YESU NA WAKATI WA YESU,HUU UONGOZI ULIANZA IMMEDIATELY BAADA YA PETRO KUAMBIWA ‘WEWE NI MWAMBA……….’ KWA HIYO BAADA YA KIFO CHA PETRO NDIO WAKACHAGULIWA WENGINE. NA ANAPOKUFA BASI ATACHAGULIWA MWINGINE.
  —————————
  Ok, kama Yesu alimpa Petro Uongozi wa kanisa na kuwa wanafunzi wote walijua hilo je:
  1. Kwa nini wanafunzi walimwuliza Yesu ni nani mkuu kati yao. Je hawakujua kuwa Petro ndiye mkubwa?

  2. Je Petro alipokosea na Paulo kumkosoa, mbona hawakumwambia kuwa Petro hakosei?

  ————————————-

  POINT OF CORRECTION MIMI SIYO MKATOLIKI BUT ORIGINALLY KATHOLIK I CHANGED BECAUSE OF MARRIAGE

  Hakuna tatizo, maadamu unafahamu kuhusu ukatoliki tunaweza kujadiliana!
  ———————————————

  WAKATOLIKI WANAAMINI BIKIRA MARIA ALIKINGIWA DHAMBI YA ASILI ILA HILI SIJAFUATILIA SO SIWEZI KUTOLEA MAELEZO

  Hapa pia nina maswali pia:
  1. Hii imeandikwa wapi, maana Biblia inasema WOTE wametenda dhambi. Na kuwa tukisema hatuna dhambi tunamfanya Mungu kuwa mwongo? Ingawa hujafuatilia lakini ni kweli wanaamini hivyo taz.

  http://www.vatican.va/holy_father/benedict_xvi/speeches/2007/december/documents/hf_ben-xvi_spe_20071208_immacolata_en.html

  http://www.vatican.va/holy_father/john_paul_ii/homilies/1998/documents/hf_jp-ii_hom_08121998_en.html
  ————————————————–

  HUYO BIKIRA WAWEZA MWOMBA AKUOMBEE KWA JINA LA YESU KAMA VILE WEWE UNAVYOWEZA KUWAAMBIA KIKUNDI FULANI WAOMBE KWA AJILI YAKO. THE SAME WAY.

  Ok swali langu ni kuwa, wapi Biblia inaruhusu wafu wawaombee walio hai? Maria amekufa kama wanadamu wengine, je tunapata wapi ruhusa atuombee? Kumbuka vikundi ulivyotaja ni watu wako hai na Maria amekufa
  ——————————————————

  BIKIRA MARIA SIYO MWOKOZI MWENZA HUYO ALIKUWA NI MAMA WA MWOKOZI. ANAYESEMA KATHOLIKS WANAMWOMBEZI MWENZA AMBAYE NI MARIA HAYO SIYO MAFUNDISHO YA KIKATOLIKI NI UVUMI WA WATU WASIOELEWA MAMBO HAYA.

  Si mimi nimesema hivyo, ila kama unapingana na Vatican sawa. Soma hapa official documents za Vatican:

  http://www.vatican.va/holy_father/john_paul_ii/audiences/1997/documents/hf_jp-ii_aud_01101997_en.html

  http://www.vatican.va/holy_father/leo_xiii/encyclicals/documents/hf_l-xiii_enc_08091894_iucunda-semper-expectatione_en.html

  ————————————————–

  REJEA HOJA YA KWANZA; KATIKA BIBLIA TAKATIFU KUNA KITABU CHA WAMAKABAYO KINAELEZA AMBAVYO TUNATAKIWA KUOMBEA WATU WALIOKO TOHARANI

  Sawa, hicho kitabu si sehemu ya Biblia. Lazima ujue kuwa agano la kale na vitabu vyote vilikusanywa Israel na wayahudi na sio Vatican. Kwa hiyo unapoangalia Biblia usiangalie Vatican bali Israel. Katika Ukusanyaji wa vitabu hivi, hivyo havipo pamoja na Tobiti na vinginevyo. Vitabu hivi vina mafundisho ya ajabu na yasiyokubaliana. Lakini cha msingi ni kuwa Yesu, wala Mitume hawakunukuu kutoka kitabu chochote. Hata Wakatoliki wenyewe hawaviiti “Canon” bali deutracanon. Kwa hiyo siyo sehemu ya Biblia (The Canon)

  Kwa hiyo, Yesu hakufundisha Toharani, Mitume wake hawakufundisha toharani. Je Wakatoliki wamelipata wapi fundisho hilo?
  ————————————————-

  KUHUSU VITABU MIMI NITASOMA. LAKINI HII SIYO SABABU YA KUWALAUMU KWA MAUAJI LABDA ILIKUWA NI UPOFU TU. NDIYO MAANA HATA WACHAWI, MAJAMBAZI, WALEVI WANAOKOKA. NAAMINI HATA WAKATOLIKI WATAOKOKA WOTE HATA KAMA WAMELEWA DAMU YA WATAKATIFU. WATAITAKASA ARDHI KWA KUFUTA KUMBUKUMBU ZOTE KWA DAMU YA YESU KAMA VILE YESU ALIVYO FUTA DHAMBI YA YULE MWANAMKE MZINZI KWA KUANDIKA ANDIKA CHINI NA WOTE WALIOMSHTAKI WAKAINGIA MITINI(WAKAONDOKA MMOJA MMOJA)
  HILI NATAMANI LIWE KWA KATHOLIKS AND I BELIVE ONE DAY WILL HAPPEN.

  Asante kwa Imani yako yenye matumaini. Lakini hakuna kilichobadilika. Waweza kudhani watabadilika, lakini nay! Mafundisho yao ni yaleyale. Je umewahi kusikia Kanisa katoliki likiomba radhi kwa mauaji ya watakatifu liliyoyafanya? Je wametangaza kuwa waliouawa walikuwa na haki na wao (Rome/Vatican) ndio wenye makosa?

  Pia nina maswali yangu ambayo bado hayajajibiwa:

  1. Rejea 8:KUNA TOHARANI;WANAENDA WALE WENYE DHAMBI NYEPESI. Ni mstari upi katika Biblia unaonyesha kwamba kuna sehemu inaitwa Toharani? (Makabayo si kitabu cha Biblia)

  2. Ni lini hili fundisho lilianza kwa kanisa katoliki? Kabla ya hapo, watu wenye hizo “dhambi nyepesi” walikwenda wapi?

  3.Rejea 3:PAPA NI KIONGOZI WA JUU KABISA WA KANISA KATOLIKI NA NI MWENDELEZO WA PETRO. ‘WEWE NI MWAMBA NA JUU YA MWAMBA HUU NITALIJENGA KANISA LANGU.
  Swali: Fundisho hili lilianza lini? Baada ya kifo cha Petro na kabla ya fundisho hili, nani alikuwa Papa? (Ni wapi Yesu alitangaza mamlaka ya ki-Petro kama aliyo nayo papa leo?)

  4. Wewe Binafsi kama unaamini haya?:
  – Bikira Maria hakuwa na dhambi
  – Bikira maria ni Mwombezi mwenza (Co-mediatrix) na Yesu Kristo (Tumeona toka Vatican hapo juu)
  – Bikira maria ni Mwokozi mwenza (Co-redemptrix) na Yesu Kristo

  Mimi pia naomba uwe mvumilivu ili tujifunze!
  Mungu atusaidie

 170. Wapendwa naomba kuuliza ivi huyu mama wa mkombozi YESU mama MARIA yu hai au alikufa? nitafurahi kujibiwa sana.maana ikiwa tunaomba atuombee na kumbe na yeye alikufa anasubiri ufufuo basi tutakuwa tunajichanganya.kwa sababu mtu aliyekufa hawezi kutuombea.HUYU MAMA NI HAI AU AMEKUFA?????????????

 171. nimesoma kwa makini hoja mbalimbali kuhusu ukatoliki,nami nina machache ya kusema. Lakini kabla ya kufanya hivyo naomba ieleweke kuwa mimi sio mchungaji wa katoliki bali nimesoma theolojia yao, nahapa ninaelezea kwa kifupi misingi ya mafundisho yao ambayo yamejengwa katika sakramenti saba. Ukitaka kuuelewa ukatoliki nimuhimu ukaanzia hapa.
  Ubatizo (Baptism)
  ni sakramenti ya kwanza ya Ukristo. Unaitwa “mlango wa sakramenti”, kwa sababu ni lazima kuupokea kabla ya kupokea nyingine yoyote, hasa ekaristi.
  Sakramenti ya kwanza daima ni ubatizo, kwa kuwa ndio kupata uzima mpya kwa kushiriki kifo na ufufuko wa Yesu, inavyodokezwa wazi zaidi mtu akizamishwa na kutolewa majini. “Tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima” (Rom 6:4).
  Sakramenti nyingine zote ama zinastawisha ama zinafufua uzima huo wa Kimungu ambao ni sharti la kuingia mbinguni. “Amin, Amin, nakuambia: Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu” (Yoh 3:5).
  Jina linatokana na kitenzi cha Kigiriki βαπτίζω (baptizo, maana yake nazamisha majini, naosha, lakini pia nanawa).
  Maana ya kwanza inadokeza lengo la kumzika mtu ili afufuke pamoja na Yesu Kristo katika uzima mpya.
  Maana ya pili na ya tatu zinadokeza lengo la kumtakasa mtu kutoka dhambi zake
  Ibada zinazotumia maji zinapatikana katika dini nyingi, kutokana na kitu hicho kumaanisha wazi uzima na usafi.
  Ubatizo unatolewa pia kwa maji machache tangu mwanzo wa Kanisa. Kutokana na umuhimu wa sakramenti hiyo Yesu ametuagiza twende kubatiza watu duniani kote. Kitabu cha Matendo ya Mitume kinaonyesha waamini walivyotekeleza agizo hilo katika mazingira mbalimbali, sio tu yalipopatikana maji mengi. Hivyo Paulo alipokuwa ndani ya nyumba “akasimama akabatizwa” (Mdo 9:18). Kumbe Yohane Mbatizaji hakusogea mbali na mto Yordani, akisubiri watu wamuendee kutoka maeneo yote ya nchi ile kame. “Alikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na Salimu, kwa sababu huko kulikuwa na maji tele” (Yoh 3:23).
  Kadiri ya madhehebu mengi, watoto wachanga wanaweza kubatizwa kwa sababu hawakatai neema ya Mungu. Wanafunzi wa Yesu walipotaka kuwazuia wasiletwe kwake “alichukizwa sana, akawaambia, ‘Waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie; kwa maana watoto kama hawa ufalme wa Mungu ni wao. Amin, nawaambieni: Yeyote asiyeukubali ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hatauingia kabisa” (Mk 10:14-15). Yeremia aliambiwa, “Kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa” (Yer 1:5). Yohane Mbatizaji alitabiriwa “atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye” (Lk 1:15).
  Ingawa watoto wachanga hawawezi kuelewa kinachofanyika, Mungu anaweza kuwamiminia rohoni mwanga wa imani. “Vinywani mwa watoto wachanga na wanyonyao umeiweka misingi ya nguvu” (Zab 8:2). “Elisabeti aliposikia kule kuamkia kwake Mariamu, kitoto kichanga kikaruka ndani ya tumbo lake… kwa shangwe” (Lk 1:41,44). “Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako” (Math 11:25-26).

  Kipaimara(Confirmation)
  Kadiri ya Kanisa Katoliki ubatizo hautoshi, bali unahitaji kukamilishwa na kipaimara na ekaristi, kama vile baada ya kuzaliwa tunahitaji kukomaa na kudumisha uhai wetu kwa chakula. Sakramenti hizo tatu kwa pamoja ni msingi wa maisha ya Wakristo wote, kumbe nyingine zinahitajika tu katika hali na nafasi maalumu. Mitume waliwaendea Wasamaria “wakawaombea wampokee Roho Mtakatifu; kwa maana bado hajawashukia hata mmoja wao, ila wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu. Ndipo wakaweka mikono yao juu yao, nao wakampokea Roho Mtakatifu” (Mdo 8:15-16). “Amin, amin, nawaambieni: Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu” (Yoh 6:53).
  Sakramenti inayohusiana zaidi na ubatizo ni kipaimara, kinachoendeleza kazi yake. “Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu. Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao” (Mdo 19:5-6). Sakramenti hizo ni kama pande mbili za pesa moja. Zinahusiana kama Pasaka na Pentekoste, ambayo ni utimilifu wake, kwa kuwa siku alipofufuka Yesu aliwapulizia Mitume Roho Mtakatifu, ambaye siku hamsini baadaye akawajia kama “upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote” (Mdo 2:2).
  Kwa Kanisa Katoliki, na wengineo Kipaimara ni sakramenti ya pili katika safari ya kuingizwa katika Ukristo ambayo inaanza kwa Ubatizo na kukamilishwa na Ekaristi..
  Ekaristi takatifu(Eucharist)
  Wakatoliki wanaamini kwamba katika karamu ya Bwana wanakula na kunywa Mwili na Damu ya Kristo. Katika sala kuu ya ekaristi padri anaporudia maneno ya Yesu juu ya mkate na divai, Roho Mtakatifu anavigeuza kwa dhati: mkate si tena mkate, wala divai si tena divai, ingawa maumbo yanabaki yaleyale kwa hisi zetu. “Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho. Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli” (Yoh 6:54-55). “Basi kila aulaye mkate huo, au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa amejipatia hatia ya mwili na damu ya Bwana” (1Kor 11:27).
  Baada ya mageuzo Yesu anabaki katika ekaristi moja kwa moja. Maumbo ya mkate na divai yanazidi kudokeza uwepo wake kama chakula na kinywaji chetu, hata kwa faida ya wagonjwa na wengineo wasiohudhuria. Ndiyo sababu tunazidi kumuabudu katika ekaristi, ingawa hatumuoni. “Tomaso alijibu, akamwambia, ‘Bwana wangu na Mungu wangu!’ Yesu akamwambia, ‘Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki” (Yoh 20:28-29).
  Vilevile Wakatoliki wanaamini ekaristi ni kafara ambayo Yesu alimtolea Baba msalabani na anaendelea kumtolea kwa wokovu wetu.
  Kitubio(Penance)
  Mungu aliwapa watu amri ya kusamehe dhambi kwa njia ya Mwanae. Yesu mfufuka aliwaonyesha Mitume alama ya mateso mwilini mwake, “akawavuvia, akawaambia, ‘Pokeeni Roho Mtakatifu. Wowote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wowote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa” (Yoh 20:22-23). Katika Kanisa tunafurahi kupewa msamaha wa dhambi kila tunapohitaji, mradi tutubu. Kwa njia ya mwandamizi wa Mitume, Yesu anatuambia, “Umesamehewa dhambi zako… Imani yako imekuokoa, enenda zako kwa amani” (Lk 7:48,50). Si dhana wala hisia tu, bali ni neno la hakika tunalolipokea kwa masikio yetu.
  Mungu aliwapa watu amri ya kusamehe dhambi zote, kwa sababu upendo mtiifu wa Mwanae aliyejitoa kuwa sadaka ya wokovu wetu unampendeza kuliko dhambi zote zinavyomchukiza. Ila hatuwezi kusamehewa dhambi ya kukataa neema ambayo Roho Mtakatifu anatusukuma tuamini na kutubu, kwa sababu pasipo imani na toba hapana msamaha. “Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa” (Math 12:31). “Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure” (2Kor 6:1).
  Hivyo, tumuendee padri ili kuondolewa dhambi tulizotenda baada ya ubatizo, kwa kuwa hatuwezi kupokea msamaha tukikataa masharti yake, na Mungu ametupangia watu ambao watuondolee kwa niaba yake.
  Mpako wa ugonjwa(Extreme unction)
  Kwa Kanisa Katoliki,na madhehebu mengine machache ni sakramenti iliyowekwa na Yesu Kristo, ingawa Injili haisemi.
  Pamoja na Kitubio ni kati ya sakramenti mbili za uponyaji, zinazolenga kumrudishia Mkristo afya ya roho na mwili, iliyoathiriwa na dhambi na ugonjwa.
  Kadiri ya imani hiyo, Mpako wa Wagonjwa ulianzishwa na Yesu, kama sakramenti zote. Maandiko yanasimulia huruma yake iliyomfanya awaponye wengi kwa namna mbalimbali na kuwapa Mitume uwezo wa kufanya vilevile kwa “kupoza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina” (Math 10:1). Nao “wakatoa pepo wengi, wakapaka mafuta watu wengi waliokuwa wagonjwa, wakawapoza” (Mk 6:13). “Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa, nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana. Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa” (Yak 5:14-15).
  Daraja takatifu(Holy Orders)
  Ni imani ya Kanisa Katoliki, ya makanisa ya Waorthodoksi na ya madhehebu mengine kadhaa kwamba daraja zinaweza kutolewa kwa wanaume tu, kwa sababu Yesu aliteua watu wa jinsia hiyo tu awape mamlaka yake ambayo inashirikishwa kwa daraja hizo, na kwa sababu ndiyo mapokeo ya Kanisa tangu mwanzo.
  Waprotestanti wanazidi kukubali wanawake katika nafasi zote za uongozi, wakisisitiza usawa wa wafuasi wa Yesu.
  Katika Kanisa Katoliki wanaopewa daraja wanaweza wakadaiwa pia hali na ahadi ya useja mtakatifu. Ni hivyo walau kuhusu uaskofu, lakini pengine hata kuhusu upadri. Sawa wa sakramenti za Ubatizo na Kipaimara, katika imani ya Wakatoliki daraja takatifu zinamtia mwamini alama isiyofutika ya kikuhani aweze kumtolea Mungu ibada katika liturujia na katika maisha yake yote. Kwa maana hiyo daraja inadumu ndani ya mtu hata akiacha kutoa huduma au kuasi kabisa.

  Ndoa(Matrimony)
  Ndoa kati ya wabatizwa wawili inahesabiwa na Kanisa Katoliki kama mojawapo kati ya sakramenti saba zilizowekwa na Yesu Kristo.Pamoja na Daraja takatifu ni kati ya sakramenti mbili za kuhudumia ushirika.
  Kadiri ya mpango wa Muumba, ndoa halisi ina sifa tatu: umoja, uimara na utayari wa kuzaa. “Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke, akasema, ‘Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe, na hao wawili watakuwa mwili mmoja?’ Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe” (Injili ya Mathayo 19:4-6). “Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, ‘Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha’” (Mwanzo 1:28). Mitara, uzinifu, talaka, ushoga na kukataa uzazi ni kinyume cha mpango huo. Muungano usiovunjika mpaka kufa kati ya mwanamume mmoja na mwanamke mmoja waliobatizwa, ambao unafanyika kwa makubaliano yao ya hiari ambayo yanathibitishwa na Mungu anayewatia neema zinazohitajika waweze kutimiza malengo ya ndoa, ni ishara ya muungano wa kiarusi wa Yesu na Kanisa. Yesu aliweka sakramenti ya ndoa kwa sababu ya umuhimu wa familia kwa ustawi wa mume na mke, watoto, jamii na ufalme wa Mungu, na kwa sababu ya uzito wa majukumu yanayohusika.

 172. BWANA YESU ASIFIWE SANA.
  JOHN
  1(I)SI WOTE WANAOKUNYWA POMBE NI WALEVI. WENGINE WANAKUNYWA KWA KUJIFURAHISHA NAFSI TU HII IKO KWENYE YOSHUA BIN SIRA. LAKINI INAPOKUZIDI UKASHINDWA KUFANYA YALIYO SAHIHI HUO NI ULEVI. NA SIKATAI MAPADRE WENGINE WANAKUNYWA HATA KULEWA NA HILI NI KOSA WAKATI TUMESHAURIWA KUNYWA KIASI. HATA KWENYE BIBLIA AGANO JIPYA IMEANDIKWA KWENYE MASUALA YA NDOA KWAMBA WANAWAKE WANYWE KWA KIASI. KWA HIYO KUNYWA NI RUHUSA LAKINI KWA KIASI.
  (II)KWA UPANDE WA KARISMATIK KUHUSU KUNYWA POMBE HAWA WANASHAURIWA KUACHA KUNYWA POMBE. LAKINI HAIMAANISHI KWAMBA UKISHAINGIA KWENYE HIYO KARISMATIK LAZIMA UACHE.
  NITOE MFANO MDOGO; LABDA MTU FULANI ANAGOMBANA NA MKE WAKE WAKATI ANAPOKUNYWA POMBE. HAPA INAONEKANA KABISA KWAMBA POMBE KWA HUYU MTU INALETA MAKWAZO NA KUFANYA YASIYO HAKI MBELE ZA MUNGU. HUYU MTU AACHE KABISA POMBE. KWA KARISMATIKI NDIVYO ILIVYO WANAFUNDISHA MADHARA YA POMBE MPAKA MTU ANAPOONA KWAMBA KILE KITU HAKIFAI.
  MFANO MWINGINE MDOGO. WAKATI KABLA SIJAOKOKA NILIKUWA NAKULA NYAMA ZA MATAMBIKO KULE KIJIJINI KWANI NIMEKULIA HUKO. BAADA YA KUOKOKA NIKIFIKA KIJIJINI KUSALIMIA KAMA WATACHINJA KWA SABABU YA KUTAMBIKIA NILIKUWA NAKULA. BAADA YA KUFUNDISHWA MADHARA YA MILO ILE NA QUOTATION KWENYE BIBLE KWA KWELI NILIJIHURUMIA SANA. NA NIKAACHA KABISA . HALI KADHALIKA KWENYE SWALA POMBE NI VYEMA KUMFUNDISHA MTU MADHARA KISHA AKAAMUA KUACHA MWENYEWE KAMA ATAONA NI MAKWAZO KWAKE.
  NA MADHEHEBU MENGINE KAMA HILI NILIOKO SASA NI WANAHUBIRIWA USINYWE POMBE LAKINI NI WANYWAJI WAZURI SANA. NI BORA KUMFUNDISHA MTU MADHARA KISHA AKAACHA KULIKO KULIKO KUMWAMBIA NA ASIKUELEWE.
  KUOKOKA SI KUACHA POMBE NASEMA HIVI KWA SABABU WENGI WANAPOTOKA KWA KUDHANI HIVYO. WAKISHAOKOKA NA KUIACHA POMBE BASI INAKUWA KUWATUKANA WALE WANYWAJI, HAPA INATAKIWA KUMWELEZA KWA TARATIBU MADHARA YA POMBE NA SI KUMSHUTUMU. HAYA MNAYAONA HUKO MITAANI.
  2)SI KUMTAJA MTU KAMA NI NIMEKUELEWA NI KUMWAMBIA MTU AKUOMBEE THE SAME WAY WE DO KWENYE MIKUSANYIKO YETU.
  SWALI LAKO LA 3,4 SINA UELEWA NALO. TUWEKE PAUSE KIDOGO
  5)KANISA HILI MSINGI WAKE NI KRISTO KAMA NILIVYOFUNDISHWA SO LILIKUJA BAADA YA YESU KUMSIMIKA PETRO KAMA KIONGOZI. HATA KAMA HAWA WATU WALIKUWEPO WALIKUWA HAWANA MISINGI YA KIKRISTU.
  6)NAVYOAMINI LABDA UONGOZI TOFAUTI KATIKA KANISA HILI UMESABABISHA HAYO. KILA KIONGOZI ANAPOINGIA MADARAKANI ANAWEZA KUBADILISHA KABISA SYSTEM. LABDA VIONGOZI WALISABABISA HILO,ILA SINA UFAHAMU NALO. ILA BAADA YA KUSHTUKIA HILO NDIYO KIKAJA KIKUNDI CHA UAMSHO NDANI YA KANISA.
  7)KWA UPANDE WANGU MIMI SIONI KAMA YANAPINGANA ILA TU NI KWA SABABU YAMEKATALIWA NA PROTESTANT. NA PROTESTANT WAKAJIWEKEA MISINGI YAO WALIYOONA INAWAFAA.
  SASA MIMI NAOMBA NIULIZE HIVYO VITABU SITA UTANIAMBIA NI MAANDIKO BINAFSI YA MTU AU NI VIPI HAPO SIELEWI.
  WAO WANAITUMIA BIBLIA TAKATIFU MIMI NIMEKUWA NAO KWA KIPINDI SIJAWAHI SIKIA MTU AKILALAMIKA KUHUSU IBADA YA KATHOLIK NA KAMA KUNA ANAYELALAMIKA HANA MSINGI MZURI WA KARISMATIKI.
  MARY.
  KUUBUSU MSALABA HAIMAANISHI KUUABUDU SANAMU NI ISHARA NA PICHA TU. ANAYEABUDIWA NI MUNGU PEKE YAKE. REJEA MAELEZO YANGU YA AWALI. KAMA KUWA NA MSALABA NI KOSA BASI MISALABA YOTE NDANI YA MAKANISA INGEONDOLEWA KWA SABABU VYOTE NI VYA KUCHONGWA. KWA UPANDE WANGU MIMI NINGESAMA MSALABA WENYE SANAMU NA USIO NA SANAMU ZOTE NO MBWEMBWE TU. KINACHOANGALIWA HAPA UNAMWABUDU NANI. HATA UNGECHUKUA VIJITI VIWILI UKAFANTYA NDIO MSALABA HILI SI KOSA. MKATOLIKI ATAKAYEKUAMBIA KWAMBA ANAUABUDU ULE MSALABA HUYO HAJUI ANACHOKIFANYA. HAMJAWAHI KUONA WATU WAKITOLEWA MAPEPO KWA JINA LA YESU PALE WANAPOSHIKA MSALABA MTAKATIFU? KWA NINI BASI USIANGUKE KWENYE HUU MSALABA UKAACHA UDHAIFU WAKO PALE ILI UZIKWE KABISA NA YESU NA UDHAIFU HUO KUOZEA MBALI. HIZI NI HATUA NZURI SANA ZA KIIMANI LAKINAI SASA KWA MKATOLIKI ASIYEELEWA ATAKWENDA PALE APIGE MAGOTI NA KUONDOKA KUMBE MUJIZA WAKE NI PALE PALE.
  KUSALI ROZARI: ROZARI NI MANENO YA KWENYE BIBLIA JAPO YAMEONGEZWA KIDOGO IKO KWENYE LUKA MOJA MANENO HAYA UTAYAPATA.
  MAJI YA BARAKA:
  KUHUSU MAJI YA BARAKA, TUMEBATIZWA KWA MAJI, KUNA MFALME ALIAMBIWA AKAOGE MTONI MARA SABA ATAPONA YALE NAYO NI MAJI, UBAVUNI PA YESU PALITOKA DAMU NA MAJI, WAPIGANAJI WALIAMBIWA WAKARAMBE MAJI MTONI KAMA MBWA ILI WAPATE SELECTION WATAKAOKWENDA KWENYE VITA, GIDEON MWAMUZI ALIMWOMBA MUNGU ATHIBITISHE KWAMBA YEYE NI MWAMUZI KWA KUTUMIA UMANDE NOA NI MAJI. MAJI YA BARAKA HUTIWA CHUMVI NA CHUMVI INA MAMLAKA. DAUDI ALIKABITHIWA UFALME KWA AGANO LA CHUMVI. KAMA SIJAKOSEA HUTIWA PIA MAFUTA YA MZEITUNI MAFUTA NI ISHARA YA ROHO MTAKATIFU’MPAKWA MAFUTA’. KUNA KILA SABABU YA HATA WEWE MWENYEWE KUYABARIKI MAJI NA UYAOMBEA KWA JINA LA YESU YAKAWE NDIYO DAWA YA MAGONJWA YANAYOKUSUMBU. HAMJAWAHI KUONA HAYA JAMANI?
  NIMEJITAHIDI KUZUNGUMZIA YALE NILIYO NA UELEWA NAYO KWA YALE AMBAYO SIJAGUSA NAHITAJI KUTULIA NA KUULIZA.

  SUALA LA BIKIRA MARIA WENGI WAAMINI HUYU ANAABUDIWA HUU NI UPOFU TU. NA BAADHI YA MAKANISA YA PENTEKOSTE UKIOKOKEA KWAO BASI LAZIMA UVULIWE ROHO ZA KUMWABUDU MARIA AMBAZO HAZIPO. YULE ANAHESHIMIWA TUUU.

  MBARIKIWE SANA NA BWANA
  TUNAJIFUNZA.

 173. Ni kweli dada Lisa hapo tunaomba utulie kweli ili tupate kuelewa,maana kuna mambo mengi ndani ya ukatoliki k.m. kusali rozali, na swala la sanamu siku ya ijumaa kuu kuna msalaba wenye sanamu huwa unabusiwa, kuna kitu kinaitwa maji ya baraka, hivyo vyote havipo kwenye Biblia.Na karismatiki haijamtenga Maria, bado wamempa kipau mbele. mpendwa unatuambiaje juu ya haya mambo 3 ?

  ubarikiwe.

 174. Nashukuru kwa majibu yako ndugu Lisa. Naendelea kujifunza. Lengo langu ni kutaka kuelewa vizuri imani ya Kikatoliki ili hatimaye niweze kulinganisha na Karismatiki kwa ajili ya kuona faida au hasara ya wao kukumbatia Ukatoliki.

  Katika mchango wako uliopita kuna maswali kadhaa yamejitokeza lakini ninauliza swali moja mengine yanatokana na maelezo yako ya mwanzo kabisa.

  1. Umesema suala la kunywa pombe ni hiari ya mtu kutokana na mafundisho ya Katoliki. Lakini wakati unakosoa utaratibu mbovu wa kupata mapadri uliandika kwamba wengine walikuja kuwa mapadri walevi. Hapa naomba ufafanuzi. i). Kama suala la mtu kulewa ni hiari yake kwa nini ulishutumu mapadri walevi? [Kama padri atalewa halafu akaenda kulala kuna tatizo gani?]
  ii). Je huu pia ndio msimamo wa Karismatiki kuhusu suala la pombe?

  2. Uliandika kwamba kumwambia Mariamu akuombee ni sawa na kuwaambia kikundi chochote wakuombee. Unamaanisha kwamba kuna wakati katika sala za Katoliki huwa wanataja mtu mwingine awaombee?

  3. Fundisho la Mariamu, aliyekufa, kuwaombea watu lilitoka kwa nani?

  4. Je, kutokana na mfundisho ya Katoliki mtu aliyekufa anaweza kuwaombea walio hai?

  5. Je, Kanisa Katoliki lilianza kabla au baada ya Yesu?

  6. Kama kweli Papa ni mtiririko wa mtume Petro, maana yake ni kwamba Katoliki litakuwa limejengwa juu yamsingi wa wokovu. Je, ilikuwaje tena Kanisa Katoliki likawa na mafundisho yenye kupingana na mafundisho ya mitume na hivyo kuwa kipingamizi kikubwa kwa Injili iletayo wokovu? [baadhi ya maelezo katika hili yameandikwa na ndg Steve M]

  7. Je, unafahamu kwamba katika vitabu vile 6 ambavyo havipo kwenye Biblia inayotumiwa na wakristo wengine kuna mafundisho ambayo yanapingana na mafundisho ya Yesu na hata maandiko mengine ya mitume na manabii? [kama vile mambo ya toharani, kuombea wafu, nk]

  8. Ninavyofahamu mimi ni kwamba kinachofanya Karismatiki wasiridhike na ibada ya Kikatoliki ni pamoja na kuwa ibada ya Kikatoliki ina mambo mengine kama kuombea Wafu, kumfanya Maria muombezi nk yaliyo tofauti na mafundisho ya Yesu Kristo. Sasa Je, nini maslahi ya wao kushiriki ibada ambayo taratibu zake ziko tofauti na Mafundisho ya Yesu, huku wao wakiwa wanalijua wazi suala hilo?

  Maswali haya yanatosha kwa sasa.

 175. YESU ASIFIWE SANA.
  JOHN PAUL
  I) THE SAME SAME KATHOLIKS WAKIONGOZWA NA PAPA YULE YULE WA KATHOLIKS
  II)HAWAPINGANI NALO KWA ASILIMIA MIA KWASABABU PAPA ALIVYORUHUSU PIA HAKULAZIMISHA WALIOKO CHINI YAKE WAPOKEE. PADRI, PAROKO,ASKOFU KARDINALI WAKIONA NI JEMA WALIPOKEE KWENYE PAROKIA AU JIMBO HATA TAIFA. LABDA WANAPOKATAA WAO WAUMINI HAWANYIMWI KUSHIRIKI KARISMATIKI. HII NI MTU KUPENDA MWENYEWE. KIONGOZI AKIKATAA WAUMINI WATAKUSANYIKA MAJUMBANI KWA WATU AU KWANYE VIWANJA N.K. KIONGOZI AKIKUBALI KARISMATIKI WATAPEWA KIBALI CHA KUKUTANIA KANISANI
  III)KWA WANOPINGA MAAGIZO YA PAPA KWA MFANO PADRI KARUGENDO WATACHUKULIWA HATUA JAPO NYINGI SIZIJUI.
  LABDA ANAWEZA KUPELEKWA ROMA KWENYE MAADILI
  ANAWEZA KUPUNZISHWA HUDUMA KWA MUDA FULANI
  ANAWEZA KUPELEKWA KWENYE HUDUMA TOFAUTI KAMA KUFUNDISHA N.K.
  2)I)MAPADRI WANAHUBIRI INJILI KAMA ILIVYO KUAMUA KUOKOKA NI HIARI YA MTU NA MISINGI NI ILE ILE YA ZAMANI ILA KAMA PADRI NI KARISMATIKI ANARUHUSIWA KUFANYA HIVYO HATA KWA YULE AMBAYE HAJAOKOKA VILE VILE.
  II)KUNYWA AU KUTOKUNYWA POMBE NDANI YA KANISA KATOLIKI NI HIARI YA MTU. KWA MTAZAMO WANGU REJEA ANDIKO’…MKONO WAKO UKIKUKOSA UKATE HALI KADHALIKA NA SIKIO. SO KWA NAYEKUNYWA POMBE AKAONA INASABABISHA DHAMBI KATIKA MAISHA YAKE BORA AACHE.
  III)ILI KUSEMA UMEOKOKA LAZIMA KUMPOKEA YESU KATIKA MAISHA YAKO. ILI UWE PADRI HUTAKIWI KUOA ILA KUNA MAHALI KWENYE INJILI IMEONYESHWA KAMA HUWEZI KUVUMILIA BORA UOE.KUTOKANA NA TARATIBU ZA KIZAMANI KUANGALIA MAMBO YA FAMILIA BADALA YA WITO HII IMELETA CASES ULIZOTJA NA KATHOLIKS WAMESTUKIA HILO NDIYO MAANA WAMEBADILISHA TARATIBU.
  IV)KUOA SI KUZINI ILA KATHOLIKS WALIPENDA IWE NO KWA MAPADRI KUOA ILA MISINGI YA KUMPATA PADRI WALIYOWEKA IKAWA MIBOVU.
  V)KWA UPANDE WANGU AACHE MAMBO YA KIDUNIA, NA ATII MAMLAKA YA ROMA IKIWA NI PAMOJA NA KUTOKUOA. KAMA HATAWEZA KUACHA KUOA ANAWEZA KUFANYA KAZI NYINGINE ZA KITUME LAKINI SI UPADRE.
  TUZIDI KUJIFUNZA JINA LA BWANA LIBARIKIWE

 176. Ndugu Lisa,

  Mimi naendelea kujifunza kutokana na yale unayoandika. Lakini katika kusoma michango yako mbali mbali kuna maswali ambayo yanajitokeza. Ninaomba tuende pole pole kwa sababu nina maswali mengi na lengo la maswali hayo ni kujifunza ili tuelewe vizuri kuhusu Katoliki na Karismatiki ili kuweza kujibu maswali niliyoyaweka kule mwanzoni pamoja na mengine yanayoweza kujitokeza. Naomba Mungu akupe uvumilivu kwa kuwa mada hii inaweza kuwa ndefu. Lakini nadhani kama kutakuwa na mwingine mwenye uelewa kuhusu KATOLIKI na KARISMATIKI akishiriki hapa inaweza kuwa ni baraka pia!

  Kwa sasa nitaanza na mchango wako kwenye mada ya Padri P. Kalugendo ambao mimi naomba tuuhamishie hapa ili tuweze kwenda vizuri.

  Umeandika maneno haya hapa chini wakati ukielezea mambo ambayo yamefanyiwa mabadiliko katika Kanisa Katoliki:

  1:KARISMATIKI YENYEWE IMETIPISHWA NA PAPA KWAMBA ‘WAACHENI WAKRISTO WAMWABUDU MUNGU KAMA WANAVYOHITAJI (KAMA WANAVYOPENDA)’ MATOKEO YA HILI NI KARISMATIKI.IMETOKA VATIKANI MOJA KWA MOJA.
  2:PILI NI KUHUSU MTU KUSOMEA UPADRI. ZAMANI VIJANA WALIOKWENDA KWENYE UPADRI NI WENYE SIFA ZIFUATAZO NITATAJA BAADHI.
  I) AWE AMETOKA KWENYE FAMILIA AMBAYO HAINA MAGONJWA YA KURITHI MFANO UKICHAA, KIFAFA, KUNYWA SUMU.
  II) FAMILIA AMBAYO HAWAJAWAHI KUUWA KWENYE KIZAZI CHAO. HAYA NI BAADHI.
  MATOKEO YA HAYA NI WATU KAMA KINA KARUGENDO AMBAO LABDA HAWANA WITO WA KIPADRI ILA TU WAMETOKA KWENYE FAMILIA SAFI AMBAZO HAZINA MATATIZO KAMA NILIYOYATAJA AU KWA MSUKUMO WA WAZAZI AU KUFUATA MKUMBO. WENGINE WAO WAKIWA NI WAZINZI WALEVI N.K
  N:B KWA SASA KILA MMOJA ANARUHUSIWA KUSOMEA UTAWA HATA KAMA UMETOKEA KWENYE FAMILIA YA WACHAWI AU YA NAMNA GANI. HII INAZALISHA MAPADRE WENYE WITO YAANI WAMEWEKWA NA MUNGU KAMA WAHUBRI INJLI WENGINE.MAPADRE WASIOKUWA NA MAPUNGUFU KAMA NILIYOTAJA NA WATAFANYA KAZI YAO KWA UAMINIFU.
  HII NI RUHUSA NA IMEPITISHWA NA PAPA NA IKO PRACTICALLY JIMBO LA ARUSHA FOR REAL EVIDENCE.

  Maswali niliyonayo kutokana na hayo ni haya yafuatayo:

  1. Kuna mahali umeandika kwamba hata kama Katoliki wataikataa Karismatiki lakini kwa maombi na kufunga wataikubali. Lakini hapa umeandika kwamba Karismatiki imeshapitishwa na Papa. [Ninavyofahamu Papa ndiyo maamuzi ya mwisho ya mwisho katika Katoliki]. Pia kuna mahali uliandika kuna Maparoko ambao bado wanazuia ibada za Karismatiki kanisani. Ninayopenda kujuwa ni haya:

  i)Hawa Katoliki wanaokataa Karismatiki ni wepi hawa?
  ii)Kwa kukataa huko ina maana wanapingana na agizo la Papa?
  iii)Kama wanapingana na agizo la Papa utii wao kwa mamlaka kutokana na mafundisho ya RC uko wapi?
  iv) Kanisa Katoliki lina utaratibu gani kwa watu wanaopingana na Mamlaka, ikiwa ni pamoja na kumpinga Papa?

  2.Kutokana na maelezo yako kuhusu mabadiliko ya vigezo vya kusomea upadre:

  i. Ina maana mapadri sasa wanafundishwa namna ya kuhubiri Injili yenye kufundisha Wokovu kwa kumpokea Yesu moyoni?
  ii). Ina sasa mapadri hawanywi tena pombe?
  iii). Kama sifa mbaya za mapadri ulizotoa ni kutokana na P. Karugendo, Je una maana KUOA kwa mtazamo wa Katoliki ni kuzini?
  iv). Msingi hasa wa fundisho hili la mapadri KULAZIMIKA kutokuoa ni wapi? [Nimeuliza hivyo kwa sababu cases za mapadri kuwa na watoto ni nyingi mno ndiyo maana mimi naona kama wanalazimishwa kutokuoa].
  v). Kwa ufahamu ulionao Padri asiyekuwa na mapungufu ni mwenye sifa gani?

  Hayo ndiyo mambo ambayo nahitaji ufafanuzi. Nitafurahi sana kama utajibu kutokana na mpangilio nilivyouliza.

  Tuendelee kujifunza.

 177. BWANA YESU ASIFIWE SANA.
  NIELEZE KIDOGO TU KUHUSU SANAMU NDANI YA MAKANISA YA ROMA.
  KUSEMA UKWELI VILE NI VIELELEZO TU NA PICHA NA SI VINGINEVYO.
  WENGI WALIOOKOKA WANASEMA KATHOLIKS WANAABUDU SANAMU HUO NI UONGO KABISA I M SURE 100%. AND BE CAREFUL USIJEHUKUMIWA KWA KUSEMA UONGO. ANAYEABUDIWA NI MUNGU PEKE YAKE HATA KWA KATHOLIKS.
  LADBA NISEME HIVI KWA KUWA WAKATI MWINGINE UELEWA WA MAMBO UNAHITAJI NEEMA YA MUNGU WATU WASISHUTUMU KATHOLIKS WANAABUDU SANAMU ILA WAWASHAURI KUZIONDOA MAANA HUENDA WAKAMFANYA MTU AABUDU SANAMU KAMA MTU YULE SI MWELEWA.
  NITOE MFANO RAHISI
  MIMI NAWEZA KUWEKA MSALABA, BIBLIA AU HATA NA MSHUMAA NDANI KWANGU NA KUTENGA KISEHEMU KWA AJILI YA MAOMBI. WAKATI NASALI NIKAPIGA MAGOTI PALE LAKINI SI KWAMBA NAVIABUDU. LADBA KATIKATI YA MAOMBI ROHO WA MUNGU AKANISHUHUDIA LABDA GUSA MSALABA. LABDA BAADA YA KUFANYA HIVYO NIKAPATA JIBU LA TATIZO LANGU LILILONITATIZA KWA MUDA MREFU.
  NEEMA YA MUNGU LAZIMA ITUMIKE HAPA KWAMBA SI MSALABA UMENIPATIA MAJIBU BALI YESU PEKE YAKE. TUKUBALI HAYA MAMBO YAPO.NA HATA MIMI NIMEONA. KAMA SI NEEMA YA MUNGU NAWEZA KUUAMINI MSALABA KUMBE ILIKUWA NI NAMNA TU YA KUFUNGULIWA.
  SO NIREJEE HOJA YANGU KWAMBA WAKATOLIKI HAWAABUDU SANAMU ILA HUENDA WAKAWAFANYA WAUMINI WENGINE WASIO NA UELEWA WAKAABUDU SANAMU.
  SO WASHAURINI WAZIONDOE KWA KUTOA REAL FACTS NA SI KUSEMA WAABUDU OTHER WISE HATA SISI TUTAHUKUMIWA KWA HILO KWANI TUNAWASHUTUMU KIVINGINE BADALA YA KUELEZA HALI HALISI.
  JINA LA BWANA LIBARIKIWE

 178. Ninafuatilia kwa karibu mjadala huu. Ninakupongeza ndugu Lisa kwa jinsi unavyoendelea kutoa ufafanuzi. Ninachokuomba ni kwamba ujitahidi kujibu maswali yote na ufafanuzi wowote unaoulizwa ili tuweze kujifunza kwa mtiririko mzuri.

 179. BWANAYESU ASIFIWE

  REJEA KIPENGELE CHAKO (3) KUHUSU PAPA. KWA UELEWA WANGU HAPAKUWAPO NA PAPA KABLA YA YESU NA WAKATI WA YESU,HUU UONGOZI ULIANZA IMMEDIATELY BAADA YA PETRO KUAMBIWA ‘WEWE NI MWAMBA……….’ KWA HIYO BAADA YA KIFO CHA PETRO NDIO WAKACHAGULIWA WENGINE. NA ANAPOKUFA BASI ATACHAGULIWA MWINGINE.

  POINT OF CORRECTION MIMI SIYO MKATOLIKI BUT ORIGINALLY KATHOLIK I CHANGED BECAUSE OF MARRIAGE

  WAKATOLIKI WANAAMINI BIKIRA MARIA ALIKINGIWA DHAMBI YA ASILI ILA HILI SIJAFUATILIA SO SIWEZI KUTOLEA MAELEZO

  HUYO BIKIRA WAWEZA MWOMBA AKUOMBEE KWA JINA LA YESU KAMA VILE WEWE UNAVYOWEZA KUWAAMBIA KIKUNDI FULANI WAOMBE KWA AJILI YAKO. THE SAME WAY.

  BIKIRA MARIA SIYO MWOKOZI MWENZA HUYO ALIKUWA NI MAMA WA MWOKOZI. ANAYESEMA KATHOLIKS WANAMWOMBEZI MWENZA AMBAYE NI MARIA HAYO SIYO MAFUNDISHO YA KIKATOLIKI NI UVUMI WA WATU WASIOELEWA MAMBO HAYA.

  REJEA HOJA YA KWANZA; KATIKA BIBLIA TAKATIFU KUNA KITABU CHA WAMAKABAYO KINAELEZA AMBAVYO TUNATAKIWA KUOMBEA WATU WALIOKO TOHARANI

  KUHUSU VITABU MIMI NITASOMA. LAKINI HII SIYO SABABU YA KUWALAUMU KWA MAUAJI LABDA ILIKUWA NI UPOFU TU. NDIYO MAANA HATA WACHAWI, MAJAMBAZI, WALEVI WANAOKOKA. NAAMINI HATA WAKATOLIKI WATAOKOKA WOTE HATA KAMA WAMELEWA DAMU YA WATAKATIFU. WATAITAKASA ARDHI KWA KUFUTA KUMBUKUMBU ZOTE KWA DAMU YA YESU KAMA VILE YESU ALIVYO FUTA DHAMBI YA YULE MWANAMKE MZINZI KWA KUANDIKA ANDIKA CHINI NA WOTE WALIOMSHTAKI WAKAINGIA MITINI(WAKAONDOKA MMOJA MMOJA)
  HILI NATAMANI LIWE KWA KATHOLIKS AND I BELIVE ONE DAY WILL HAPPEN.
  BWANA YESU NI MWEMA

 180. Asante Dada Lisa kwa ufafanuzi. Nitarudi baada ya kutafakari. Lakini nina maswali machache kwa sasa:
  1. Rejea 8:KUNA TOHARANI;WANAENDA WALE WENYE DHAMBI NYEPESI. Ni mstari upi katika Biblia unaonyesha kwamba kuna sehemu inaitwa Toharani?

  2. Ni lini hili fundisho lilianza kwa kanisa katoliki? Kabla ya hapo, watu wenye hizo “dhambi nyepesi” walikwenda wapi?

  3.Rejea 3:PAPA NI KIONGOZI WA JUU KABISA WA KANISA KATOLIKI NA NI MWENDELEZO WA PETRO. ‘WEWE NI MWAMBA NA JUU YA MWAMBA HUU NITALIJENGA KANISA LANGU.
  Swali: Fundisho hili lilianza lini? Baada ya kifo cha Petro na kabla ya fundisho hili, nani alikuwa Papa?

  4. Wewe Binafsi kama mkatoliki, unaamini haya?:
  – Bikira Maria hakuwa na dhambi
  – Bikira maria ni Mwombezi mwenza (Co-mediatrix) na Yesu Kristo
  – Bikira maria ni Mwokozi mwenza (Co-redemptrix) na Yesu Kristo

  Pia naomba usome vile vitabu ambavyo nilitoa Link. Nitarudi baadae, lakini naomba unijibu maswali yangu ili tuendelee kujifunza.
  Ubarikiwe!

 181. Shalomu,

  Nakushukuru sana Lisa kwa kutoa ufafanuzi juu ya Imani ya Kanisa la Romani. Ninaomba kupata ufafanuzi juu ya sanamu ndani ya kanisa la Romani.

  Mungu akubariki

 182. BWANA YESU ASIFIWE
  MAMBO YA MSINGI KATIKA IMANI KATOLIKI NINAYOYAFAHAMU MIMI NI KAMA:
  1:YOSEFU(YUSUFU) NI BABA MLISHI WA YESU
  2:BIKIRA MARIA NI MAMA WA YESU NA YESU ALIZALIWA KWA UWEZO WA ROHO MTAKATIFU. KATHOLIKI WANAMHESHIMU MARIA KUTOKANA NA MSTARI KWAMBA ‘TAZAMA VIZAZI VYOTE WATANIITA MBARIKIWA’
  3:PAPA NI KIONGOZO WA JUU KABISA WA KANISA KATOLIKI NA NI MWENDELEZO WA PETRO. ‘WEWE NI MWAMBA NA JUU YA MWAMBA HUU NITALIJENGA KANISA LANGU.’HILI PIA LIMEWEZESHA KATHOLIKS KUTOKUMEGUKA SANA TOFAUTI NA MADHEHEBU MENGINE.WAMEKUWA NA UTII NA UNYENYEKEVU NA HATA SASA WALOKOLE (KARISMATIKI) LAKINI HAWAJAMEGUKA.
  4:KATHOLIKS WANAAMINI UBATIZO WA MAJI KIDOGO (WINGI WA MAJI SI TATIZO ILA KIINGIACHO NDANI YAANI ROHO MATAKATIFU)
  5:YESU KRISTU ALISULUBIWA, AKAFA, AKAZIKWA, AKASHUKA KUZIMU, AKAFUFUKA KATIKA WAFU, AKAPAA MBINGUNI, ATARUDI KUCHUKUA WAZIMA NA WAFU.
  6:WANAAMINI ROHO MTAKATIFU NA USHIRIKA WA WATAKATIFU.
  7:KATHOLIKS WANAAMINI KUNA ONDOLEO LA DHAMBI NA UZIMA WA MILELE.
  8:KUNA TOHARANI;WANAENDA WALE WENYE DHAMBI NYEPESI,
  KUNA MOTONI; WANAKWENDA WALE WENYE DHAMBI YA MAUTI.
  MBINGUNI; WANAKWENDA WENYE USAFI WA MOYO.
  9:MISA; AMBAPO MKATE(KOMUNIO) HUGEUZWA KUWA MWILI WA YESU NA DIVAI KUWA DAMU YA YESU (KIIMANI). HIVI HUPOKEA MTU MWENYE MOYO SAFI.
  10: NIRUDI KWENYE MKATE KUGEUZWA KUWA MWILI WA YESU NI KWAMBA MWENYE UWEZO WA KUFANYA HAYO NI PADRI PEKE YAKE NA WANAZINGATIA MAANDIKO ‘HUU NDIYO MWILI WANGU NA HII NDIYO DAMU YANGU’ ‘FANYENI HIVI KWA KUNIKUMBUKA MIMI’.
  11: KATHOLIKS WANATUMIA BIBLIA TAKATIFU AMBAYO VITABU VYAKE NI VINGI 72 KAMA SIJAKOSEA. INASEMEKANA KWAMBA ‘BUT IM NOT SURE’ WAKATI PROTESTANT WANAMEGUKA TOKA KATHOLIK VITABU SITA VILIKUWA MEZANI VIKIFANYIWA KAZI KWA HIYO WAO WAKAONDOKA NA VILE VILIVYOKUWA TAYARI YAANI VITABU 66.MAANA MAANDIKO YANASEMA MAANDIKO MATAKATIFU NI MAREFU SANA SO HAYAKUANDIKWA YOTE. LAKIN HII HAIMAANISHI KWAMBA HAIRUHUSIWI KUSOMA BIBLIA NYINGINE LA HASHA KILA KITU KIKO SAWA ILA TU NI VITABI SITA VILIVYOKASORO.

  NIRUDI KWENYE MAMBO YA MSINGI KWENYE KARISMATIKI KATOLIKI
  1: NI KIKUNDI CHA UAMSHO NDANI YA KANISA KATOLIKI.NA UAMSHO UMETOKEA KATIKA KIPINDI HIKI AMBACHO WAKATOLIKI WAMEKIITA ‘UPYAISHO’ YAANI KAMA VILE TUNAINGIA KWENYE HATUA NYINGINE. AU KWA MANENO MENGINE NAWEZA KUSEMA KANISA KATOLIKI LIKO KWENYE KINDI CHA UPYAISHO.
  2:KARISMATIKI WANAAMINI UAMSHO NI KUMKUBALI YESU KUWA NI BWANA ( MWOKOZI,MTAWALA,MFALME,WA MAISHA YAKO)KWA MSAADA WA ROHO MTAKATIFU NA KWA UNYENYEKEVU NA UTULIVU UKIHESHIMU WAUMINI WENZAKO.
  3:WANAMKUBALI ROHO MTAKATIFU PAMOJA NA KUNENA KWA LUGHA.
  4:WANASALI KATKA MISA NA WAUMNI WENZAO NA KUSHIRIKI KILA KITU KWANI WAO NI WAKATOLIKI. LAKINI WAKATI WA KUKUSANYIKA KWAO WANAWEZA KUFANYA IBADA YAO YA KIKARISMATIKI. AU WAKATI MWINGINE KAMA PAROKO ANAKUBALI BASI IBADA YAWEZA KUFANYWA KIKARISMATIKI.
  5:UTII NDANI YA MAMLAKA YA KANISA NI SWAL LA MUHIMU KWA KARISMATIKI’ HATA BIBLIA INASEMA IMANI ITII MAMLAKA.
  6:KARISMATIKI WANAMPOKEA ROHO MTAKATIFU KWA NAMNA YA PEKEE KWAMBA SI SAWA NA VILE ULIVYOBATIZWA, ANAKUWA NDIYE KIONGOZI KATIKA MAISHA.
  7:KUSOMA NENO LA MUNGU KWA WINGI NA KUTEGEMEA ZAIDI NENO BADALA YA AKILI ZA KIBINADAMU POPOTE UENDAPO NA CHOCHOTE UFANYACHO.

 183. Ndugu lisa wairimu,

  Mimi naona mada ambayo umeipendekeza ni nzuri tu ili tujifunze wote kwa pamoja. Ninaloomba ni kwamba kwa kuwa wewe unaonekana kuwa na uelewa juu ya mambo yote matatu itakuwa vizuri uweke msingi wa mjadala huu. Naomba uweke msingi wa mjadala huu kwa kuandika yafuatayo:

  1. Mambo ya msingi katika Imani ya Kikatoliki

  2. Mambo ya msingi katika hiyo Karismatiki Katoliki

  3. Mambo ya msingi katika Imani ya Wokovu

  Hata kama unafahamu mambo ya msingi katika suala Imani mojawapo tu unaweza kuyaandika na msomaji mwingine anaweza kuandika juu ya Imani anayoifahamu vizuri. Tukishayajua mambo hayo ndipo tunaweza kufahamu mambo kama:

  1. Je, Ni kweli Imani ya Kikatoliki inafuata mafundisho ya Bwana Yesu?

  2. Je, Karismatiki bado inafuata mafundisho ya Kikatoliki?

  3. Kama Karismatiki haifuati mafundisho yote, au baadhi, ya Kikatoliki kuna sababu gani ya wao kuitwa tena kuwa ni sehemu ya Kanisa Katoliki?

  4. Kama Karismatiki wanafiti kote kote, yaani wanafuata misingi yote ya Katoliki pia wanafuata mafundisho yote ya Wokovu Je, maandiko yanasemaje kuhusu hali ya namna hiyo?

  ….na maswali mengine mengi yanayoweza kuwa yamo mioyoni mwa wasomaji.

  Tuendelee kujifunza

 184. CONCLUSION OF THE MATTER

  Now all has been heard;
  here is the conclusion of the matter:
  Fear God and keep his commandments,
  for this is the whole duty of man. For God will bring every deed into judgment,
  including every hidden thing,
  whether it is good or evil.

 185. BWANA YESU ASIFIWE SANA
  NAOMBENI TUJADILIANE KUHUSU WOKOVU NDANI YA KANISA KATOLIKI (KARISMATIKI KATOLIKI)

 186. Mitume na manabii wapo hata leo hii. Efeso 4 inaeleza hivyo. Waraka huu umeeleza vigezo ambavyo tukifikia hatutawahitaji tena, navyo hatujavifikia. Sasa kama mitume manabii n.k bado wapo, wana tofauti gani na wale wa mwanzo. Ukisoma Biblia vyema, inawagawa makundi matatu:

  1. Yesu – Ndiye jiwe la pembeni na mwanzilishi wa imani yetu. Yesu alikuwa ni mtume pekee ambaye alikuwa (Na milele atakuwa) Mungu. Hakuna mtume wa ngazi ya Yesu na mtume yeyote atakayekuja na mafunuo kinyume na Yesu, ni mtume wa shetani!

  2. Wanafunzi wa Yesu. Hawa ni mitume waliotembea na Yesu, na Paulo aliyekutana na Yesu njiani Dameski. Hawa walipewa mafunuo maalum ambayo yaliendelea hata kufungwa kwa Biblia (Kitabu cha ufunuo). Neno la Mungu kwa wanadamu limeakamilika na hakuna tena mitume wa ngazi hii. Mtume atakayekuja na mafunuo kinyume na ya mitume hawa, si ya Mungu, na alaaniwe!

  3. Mitume wa sasa – Hawa hupewa mafunuo ya kuifanya kazi ya Mungu kwa neno la Mungu yaani Biblia. Mungu huwapa ufunuo maalum wa neno fulani katika Biblia kwa wakati fulani. Hawana mafunuo nje ya Neno, na lolote watakalofanya, lazima liwe ndani ya neno la Mungu.

  Hili pia kwa manabii. Hakuna nabii wa ngazi ya Daudi, Yeremia, Ezekiel n.k hawa walipokea mafunuo toka kwa Mungu ambayo hayakuwapo bado. Pili Nabii aliye Mungu, Yesu Kristo, na mwisho manabii wa agano jipya (Mpaka Yesu arudi). Manabii wa agano jipya hawana mafunuo nje ya maandiko ya Mung. Kila aliye na mafunuo nje ya Biblia ni nabii wa ibilisi!

  Kifupi, kwa maneno yao, matendo yao na matunda yao tutawajua tu! Cha msingi si kuangalia huyu anajiita nani, cha maana ni kuwa ana qualify kwa nafasi hiyo? Hakuna mwenye akili timamu na ufahamu huru anayeweza kuhoji utume wa Yesu, Petro au Paulo. Vivyo hivyo unabii wa Yermia au Agabu! Sasa ukiona maswali mengi juu ya mitume wa leo, ni kutimia kwa unabii wa Yesu kuwa “watakuja manabii wa uongo na watadanganya wengi!”

  Sijaandika kwa utaratibu mzuri lakini natunai itasaidia. Tuwe makini Wapenzi!

 187. Dada VICK Mpaka sasa manabii wapo: mitume wapo,na wachungaji wapo, waamini pia wapo kwani watu mbona kuna ubishi? manabii na mitume wapo hata sasa na wanampenda Yesu sana na wanafundisha,Nabii ni wa muhimu,mhubiri ,mtume wote tunawahitaji na ashukuriwe Mungu ukikumbana na nabii yule mwenyewe aliyeitwa na Yesu utabarikiwa sana

 188. Si kila mtu alitajaye jina la Bwana ni wake, Yesu aliyasema haya na akionyesha wengine watakuwa wakifaya ishara na ajabu na hata kuponya watu! Inawezekana kabisa watu kama hao walianza na Bwana lakini tamaa ya dunia imewaweza sasa hawana tena Bwana wanafanya yaliyo yao! Ukisoma tu au kusikia matangazo yao unajua kabisa hawa watu wamemwacha Mungu au hawana Mungu kabisa nathubutu kusema hawa ni matapeli ni watu wa kuwaogopa sana, hawafai. Yesu hakuwahi kuita watu awaombee ili wajisikie vizuri humu duniani bali aliwaombea na kuwaponya kwa kusudi la uzima wa milele, watu hao wauone wema wa Mungu na wamrudie kwa kutubu na kuachana na dhambi. Aliita waliolemewa na mizigo awapumzishe Mathayo 11:28, aliwaambia aliowaponya msitende dhambi tena… sasa hawa watu waosema tutawombea mwende ulaya kufanya nini? kuna uzima gani ulaya? tutakuombea upate mtoto au pesa au gari mambo haya kweli yana kitu chochote cha kufanya na uzima wa milele? si hata mshetani yanatoa pesa? hao tunaowasikia ma-freemason si watu wenye pesa nyingi je wanauzima ndani yao? Na hili ndilo hitimisho langu kama mtu anatangaza maneno yeyote yasiyo na lengo la kuwapeleka watu katika toba, msamaha,utakatifu maneno hayo ni batili na ni ujumbe wa kishetani na yeyote anayefanya hivyo anamtumikia shetani kwa kujua au kwa kutokujua. Tukimrudia Mungu kwa toba yeye atatusamehe na kutupa mahitaji yetu yote kama watoto wake, hatuhitaji maombi ya mtu yatuletee mibaraka, Mungu anatoa mibaraka tukimtii na kumcha Isaya 1:18,19 Mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi. HHAO WATU NI MATAPELI NI WAHARIBIFU WA KWELI YA MUNGU!

  Mbarikiwe.

 189. habari za usiku ! maana ninachangia usiku usiku niko safarini..
  kuna mada ninaiona ya mitume na manabii, na wala sitaki kujiunga upande wowote wala kutoa neno kutoka kwenye kitabu kitakatifu, bali kwa ufahamu wangu nadhani tumuogope Mungu kabla hatujajiita manabii na mitume, ni nani ametupa hicho kibali ?? kwani lazima uwe mtume na nabii ndio utangaze injili? cant you live with it ?? mimi nadhani binadamu tunapenda sana kujikweza na kujinyanyua mara ooh nina upako mara mimi ni mtume mara nabii mimi nadhani tuishie kwenye utumishi, nadhani mtu awe ni mtumishi, ukiwa na mtume or nabii before your name i dont think it matters to me hey ? tumuogope Mungu tujinyeyekeze kwa kukubali utumishi kwake huo unabii na utume tuwaachie wale walioitwa na bwana enzi hizo …my thoughts

 190. Ndugu Kasegezya aliandika
  “li kuwavuta wanatumia mitego hiyo ila wakifika wanatoa neno linalowagusa mioyo yao nawengine wanapokea wokovu nakuziacha njia zao mbaya”

  Ni kweli lengo limekuwa ni kuvuta watu kwa makusudi mbalimbali likiwemo la biashara. Lakini kwa Mkristo, hapa kuna tatizo kubwa. Je Sauli hakukataliwa kuwa mfalme kwa kosa ambalo yeye aliona si kosa kwanza, na baadae akadhani ni kosa dogo? Soma ISamweli utaona.

  Tatizo tunajipa kazi ambazo Mungu hajatupa, Je mtumwa mwaminifu si yule anayetii kile tu alichoagizwa? Je hafanyi jinsi Bwana wake alivyomwagiza? Je huvumbua njia zake na kuziacha za Bwana wake?

  Ni vema tukafanya kazi ya Mungu kwa jinsi atakavyo Mungu mwenyewe badala ya kuja na mavumbuzi yetu. Tusimfundishe Mungu jinsi ya kufanya kazi yake na badala yake tujifunze kutoka kwa Mungu ni namna gani anataka tuifanye kazi yake

 191. Sidhani kama wanania mbaya sana,kwani watumishi wanahekima kubwa nakujua nini haja ya kizazi cha sasa.Ili kuwavuta wanatumia mitego hiyo ila wakifika wanatoa neno linalowagusa mioyo yao nawengine wanapokea wokovu nakuziacha njia zao mbaya.Nisawa na pale wamisionari walitumia sinema kuvuta watu

 192. Napenda kusema hivi, Kuna haja ya kutoa maana ya utajiri kwa mtizamo wa Yesu na utajiri kwa mtizamo wa dunia. Neno utajiri halina maana moja, inategemea umevaa miwani ya namna gani unapotazama “utajiri”

  Utajiri kwa maana inayofahamika kidunia ni dhambi, Yesu kasema mara nyingi na Neno la Mungu limezungunza mara nyingi.

  Kuimiza watu wawe matajiri bila kuwaelimisha namna ya kuupokea utajiri na pia namna ya kuishi kama tajiri katika ufalme wa Mungu ukitawala pamoja na Yesu ni jambo la msingi sana sana.

  Utajiri bila mafundisho sahihi ya kuishi kama tajiri ni maangamizi makubwa. Wanaoomba utajiri leo wengi wanajilinganisha tu na watu wa dunia, nakutamani kuishi maisha ya kitajiri kwa mtizamo wa dunia.

  Naomba ukumbuke habari ya mwana mpotevu, alitamani kumiliki mali yeye mwenyewe, mbele ya baba yake ule ulikuwa uasi, Mwana mkubwa aibaki nyumbani akitumika pamoja na baba yake, vile vyote vilivyobaki pale nyumbani vilikuwa vyake, shida hakuwa na mazoea ya kumwomba baba yake ndo maana mdogo wake aliporudi na kuchinjiwa ndama alilalamika. Hakujua haki yake, mimi na wewe tukiwa watoto wa Mungu, kelele za utajiri hazipaswi kutusumbua kwani alivyo navyo Baba yetu ni vyetu, ni suala tu la kuutambua upendo wa Baba yetu ni kumweleza mahitaji yetu, kila tunapohitaji. NA WALA SIO KUTAFUTA KUJILIMBIKIZIA MALI SISI WENYEWE NA KUISHI MAISHA YA ANASA, ILA TUMIA MALI ZA BABA YAKO ULIZOKABIDHIWA KUUJENGA UFALME WETU NA BABA YETU.

 193. Dada Alice mimi naomba nianzishe topic.

  Nilikuwa ninasoma Kitabu cha Mwanzo ni nilipofika Sura ya 4:7 ambapo imeandikwa pamoja na mengineyo “Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini inapasa uishinde.” Niliyatafakari maneno hayo na ninaamini Roho wa Mungu akaniangazia na kunifunulia.

  Usomapo utaona kuwa haya ni maneno ambayo Mungu alimwambia Kaini wakati alionekana kumwonea wivu mdogo wake Habili. Mungu anamwambia Kaini kuwa badala ya kumwonea wivu mdogo wako ambaye anatenda mema, kwa nini na wewe usitende mema kwa sababu fursa unayo ya kufanya hivyo? Halafu akampa somo kuwa usipotenda mema ujue unatenda dhambi. Na dhambi hiyo wala haiko mbali iko nje ya mlango wako inakusubiri (inakutamani wewe) kwa hiyo chukua hatua ya kuishinda.

  Maana ya maneno haya ni kuwa dhambi ni ya shetani na ni shetani ndiye anaeshawishi utende dhambi. Kwa hiyo wakati wote yuko karibu yako (mlangoni) anakuchochea uitende hiyo dhambi. Ndiyo maana ya “dhambi inakuotea mlangoni”. Dhambi kumtamani mtu ni kuwa shetani anakushawishi. Siku zote tamaa huwa haikai kimya huwa inatusemesha kwa kuturubuni na kutushawishi tuone uzuri wa kutenda dhambi.

  Pamoja na maelekezo ambayo Mungu alimpa Kaini bado Kaini alikaidi na akamrubuni ndugu yake akaenda kumuua. Aliamini kuwa kwa kumwondosha Habili duniani atakuwa ametatua tatizo la wivu. Kuwa Habili nimemuua kwa hiyo chanzo cha wivu ambacho huwa kilikuwa kero kwake hakipo tena. Basi akafikiri atakuwa na amani. Fundisho hapa ni kuwa hiyo amani hakuipata kwa sababu Mungu alimpa adhabu ya kutangatanga. Na sisi pia tufahamu tunaelekezwa tutende mema ili tusije tukaadhibiwa baadaye kutokana na maovu yetu. Tukiendelea kukaidi amani inatukimbia kwa sababu Mungu anatuacha. Na Mungu akikuacha amani nayo inaondoka. Kwa sababu God is PEACE.

  Jamani nimeanzisha naomba na wengine nao wachangie. Hii mada ni pana kweli kweli. Sisi katika maisha yetu ya kila siku wakati mwingine twatenda hii dhambi ya kuwaonea wivu wenzetu ambao wanaonekana kufanikiwa.

  Je twajifunza nini hapa?

  Changieni!

 194. Bwana Yesu asifiwe,ninapenda kuwashukuru na kuwaombea watenda kazi wote wa Mungu wale walioitwa naye na wanaotembea katika mapenzi yake watumishi wasio na hila wala kunyanzi popote pale walipo Tanzania.
  Ninataka kukutia moyo wewe uliyeokoka na kuyakabidhi maisha yako kwa Yesu, usichoke kutafuta na kufanya mapenzi ya Mungu siku zako zote za maisha yako, ulalapo, uamkapo, utembeapo, uwapo kazini, uwapo na marafiki zako, kwasababu Yesu anarudi na yu karibu sana kuliko watu wanavyofikiri, Yesu anasema, maneno yangu yakiwa ndani yenu basi mmekuwa wanafunzi wangu kwelikweli nanyi mtaifahamu kweli nayo kweli itawaweka huru nanyi mtakuwa huru kwelikweli. Ni maombi yangu Roho mtakatifu azidi kuwa juu yako au hata ndani yako na kila muda lazima taa yako iwe ina waka au kila muda lazima uwe umejaa Roho mtakatifu kwakuwa katika saa usiyodhani Yesu yu aja.

 195. Wapendwa Paul na Mwenda Mungu awabariki sana kwa maelekezo yenu yaliyojaa Roho wa Mungu.
  kwa kweli suala la kufunga ndoa kwa vijana wa kanisa la leo ni jaribu kubwa sana kwani wana mapungufu mengi katika hatua mbali mbali mpaka wanapofikia kuitwa hicho kinachoitwa ndoa. Ukweli ni kwamba ingawa ndoa ni taasisi muhimu sana kwa ustawi wa kanisa la Mungu lakini hakuna uthubutu wa kutosha uliowekwa kuhakikisha kuwa ndoa zinakombolewa kutoka mikononi mwa shetani hata inawezekana tukadhani kuwa ndoa nyingi zinazofungwa makanisani leo zinaonekana kuwa zina namna ya utakatifu lakini zimejaa matendo mengi maovu.
  Wakati fulani mimi na mke wangu tulijitolea kusaidia vijana ambao walikuwa wameamua kufunga ndoa kwa kufuata taratibu za kanisa. Kitu cha ajabu tulichokigundua ni kuwa kati ya ndoa tano tulizojitia nia kusaidia tatu katika hizo wachumba walishaanza kukutana kimwili muda mrefu kabla ya ndoa na walikuwa wanaonekana kuwa wameokoka katika makanisa yao. Hata ile ndoa moja ya mwalimu mmoja wa shule ya sekondari ambayo wachumba walikuwa wasafi kweeeli kwani wote hawakuwahi wala hawakuwa na ujuzi wowote wa tendo la ndoa (hapa niseme wazi kuwa walikuwa mabikira mpaka katika akili zao) hawakuwa na elimu yoyote juu ya hatua za uchumba wao na hata nini kitafuata mara watakapoanza maisha ya ndoa. Ukweli ni kuwa ilibidi wasimamizi wao wawaelekeze wanandoa ni nini cha kufanya.
  Kwa hiyo ninashauri sasa kupitia blogu hii hebu tufufue kazi ya Mungu katikati ya miaka katika kusaidia kuokoa taasisi ya ndoa ambayo ni nguzo muhimu katika ukuaji wa kanisa. Tukumbuke Paulo alipomwandikia waraka mzee FILEMONI alimsifu kwa habari za kanisa la nyumbani,Yohana alimtakia baraka mzee Gayo kwa habari za kanisa la nyumbani maana yake la familia yaani taasisi ya ndoa.
  Mungu awabariki sana

 196. Hii ndoa inao utata mkubwa sana. Mimi nami kwa upande wangu, naungana na mt. John Paul kuwa ndoa hii haikuwa na uhalali kabisa kibiblia.

  Hata hivyo maelezo ya Bw. Evarist yanaashiria kuwa huyu dada wa kipentekoste alikuwa hajaokoka bado. Au inawezekana alikuwa ameokoka siku za nyuma, lakini wakati wa pilikapilika zake za ndoa hiyo batili, alikuwa amesharudi nyuma kiimani.

  Kuhusu uhalali wa ndoa hii, kwa vile walioana kama mataifa, yaani ambao hawapo katika Kristo, iwapo walichukua taratibu zote za kwawaida ya dunia, yaani kutoa taarifa kwa wazazi wa pande zote mbili na wakakubaliwa, na mume akatoa mahari au akatimiza masharti yaliyotolewa na wazazi wa mke na ikapokelewa/yakapokelewa nk. basi mimi kwa upande wangu naona ndoa hii ilikuwa ni halali kibinadamu.

  La msingi jingine, iwapo wote wawili walikuwa bado hawajawahi kuoa/kuolewa basi ndoa hii bado inazidi kuwa ni halali. Ninavyozungumzia uhalali, si halali katika Kristo bali kibinadamu.

  Wengi wa watu tunaookolewa nyakati hizi, tunaokolewa tukiwa na ndoa za namna hii, na haturuhusiwi ki- maandiko kuachana kwa kisingizio kuwa tulioana tukiwa mataifa! Bado maandiko yanatufundisha kuwa tuendelee na ndoa zetu za awali.

  Iwapo mazingira ya ndoa ya hawa watu yalikuwa hivi, basi kama nilivyosema hapo awali, ndoa yao kibinadamu ilikuwa halali, na yule dada kibiblia haruhusiwi kuolewa na mtu mwingine baada ya kuokoka. Bado atatakiwa kumwomba Mungu ili arudiane na mume wa ujana wake.

  Maandiko yanayoonesha kuwa kuna uwezekano wa kuoana kabla ya wokovu na baada ya wokovu ndoa ikawa halali ni [1Wakorinto 7:12…iwapo ndugu mmoja ana mke ASIYEAMINI na mke huyo anakubali kukaa naye asimwache ms.13 Na mwanamke ambaye anamume ASIYEAMINI, na mume huyo anakubali kukaa naye, asimwache mumewe.]

  Ni muhimu kufahamu pia kuwa, Mungu ametuitia katika amani, iwapo mke/mume wetu ambaye hajaokoka analeta ukorofi unaoweza kuhatarisha maisha yetu, kwa sababu tu ya wokovu wetu, tunaweza kujiepusha naye, iwapo ni kuondoka sisi katika nyumba au yeye tukubaliane na yote, huku tukiendelea kumwomba Mungu pasipo kutafuta wenza wengine. Huo ni mchango wango.

  S H A L O M !

 197. Ndugu Evarest, kisa hiki ulichokiweka hapa kwa njia ya maswali mimi nakiona kama ni kisa cha kweli ambacho kimetokea. Mimi ninajibu maswali yako kama ifuatavyo:

  1. Uhalali wa Ndoa

  Kitendo cha mwanamke kukaidi maonyo na mafundisho ya kanisa lake la pentekoste na kisha kufoji cheti ya ubatizo wa kanisa lingine ambalo si la kiroho ili tu afanikishe kufunga ndoa ni sababu tosha kabisa kufanya ndoa hiyo isiwe halali ki-imani.

  Mwanaume anayejali hali ya kiroho lazima angekuwa mstari wa mbele kumshawishi mchumba wake asifoji cheti cha ubatizo. Kutafuta cheti toka kanisa jingine ambako mtu hakubatiziwa ni uongo. Kwa hiyo ndoa ya namna hiyo tayari inakuwa imejengwa kwenye msingi wa uongo.

  Lakini hapa pia tunaweza kuona jinsi ambavyo viongozi wa makanisa yetu na pengine misingi ya madhehebu mengine isivyoweza kuwasaidia watu katika kweli. Kiongozi wa kanisa anayempa cheti cha ubatizo cha uongo mtu mwingine ambaye hamfahamu, mtu huyu hafai kuwa kiongozi wa kanisani. Hali kadhalika mtu anayemfungisha ndoa mtu mwingine ambaye cheti chake cha ubatizo ni feki, na pengine akiwa na taarifa kabisa kwamba huko alikotokea hakutoka kwa amani huyo naye hafai kuwa kiongozi wa kanisa. Lakini hawa ndio viongozi tulionao kwenye madhehebu yetu ambayo mengine yana majina makubwa sana na kuheshimika. Hii inasikitisha sana. Kipofu kumuongoza kipofu wote hutumbukia shimoni. [Mathayo 15:14]

  Si ajabu kusikia watu hawa walitengana lakini inasikitisha. Lakini haishangazi kwamba ndoa hiyo ilivunjika. Nimeandika kwamba ndoa hii ilijengwa kwenye msingi wa UONGO kwa hiyo kusimama kwake ingekuwa vigumu sana. Bila kujali nani alikuwa chanzo cha kuvunjika ndoa hiyo lakini ni wazi kwamba wote, mke na mume, walihusika 50/50.

  2. Sehemu ya pili ya swali lako sijaielewa vizuri na ni nadhani haieleweki wazi.

  i). Mwanaume alioa mke mwingine. Je, ni yupi alidaiwa kuwa ni mke wa kwanza? Ni yule aliyeolewa kwa ndoa ya bomani au ya kanisani?
  ii). Mwanamke ambaye hatimaye akawa ameokoka Je, ni yule aliyeolewa bomani au yule wa kanisa la pentecoste?
  iii). Je,Mwanamke ambaye unauliza kama anaweza kuruhusiwa na kanisa kufunga ndoa ni yule wa bomani au yule wa kanisani?

  Kanisa ambalo linaweza kuwafungisha ndoa watu wenye vyeti vya kugushi sidhani kama lina mipaka gani mingine ya kutokumfungisha mtu ndoa. Lakini kama mtu alikuwa dhambini na hatimaye akaokoka hakuna kipingamizi chochote cha kibiblia cha kumzuwia mtu wa namna hivyo asiruhusiwe kufungiwa ndoa. Wako watu wengi ambao walikuwa ni makahaba wa kike na wa kiume ambao wanapookoka wanakuwa ni washirika kamili wa familia ya watakatifu. Hakuna kumbu kumbu tena ya mambo waliyokuwa wakiyafanya walipokuwa dhambini.

  ISEMAVYO BIBLIA

  KUHUSU NDOA – Biblia inasema kwamba SI vema kufungiwa nira pamoja na watu wasioamini kwa jinsi isivyo sawa sawa. Kufungiwa huku ni pamoja na kuoa au kuolewa na mtu ambaye hamwamini Bwana Yesu! [2Korintho 6:14-18]

  KUHUSU MTU ALIYEOKOKA KUOLEWA – Biblia inasema kwamba Mtu akiwa ndani ya Kristo mambo yanakuwa mapya, ya kale yanakuwa yamepita naye anaanza maisha mapya ndani ya Kristo. [2Korintho 5:17]

  Mtu anapokuwa dhambini yuko dhambini kwa hiyo yote anayoyafanya hayana rekodi katika maisha ya utakatifu. Mtu anapokuwa ametubu mambo ya kale yanasamehewa na kusahauliwa kainsa na Mungu na dhambi zinawekwa mbali sana naye.

  Mambo ambayo mtu aliyedhambini hufanya si masuala ya uzinzi na uasherati peke yake. Kuna wizi, uchawi, uongo, uchonganishi na mengine mengi. Mtu akiokoka matendo haya maovu hayawi kwenye kumbu kumbu tena kwamba huyu alikuwa mwizi kwa hiyo haruhusiwi kufanya jambo fulani au huyu alikuwa mchawi kwa hiyo naye haruhusiwi. Kama hali iko hivi katika matendo maovu mengine , hali inatakiwa kuwa hivyo hivyo hata katika suala la kuoa na kuolewa.

  Hivi ndivyo nilivyoweza kujibu kwa sasa.

  Mjadala huu uko wazi na mtu yuko huru kuchangia anavyoamini au anavyojuwa yeye lakini kwa kulingana na neno la Mungu!

 198. nauliza watu wawili walikifunga ndoa,huku mwanaume ni kanisa la Roman Catholic na mwanamke kanisa la pentecoste, lakini huyu wa pentecoste akatafuta cheti cha ubatizo wa kanisa lingine ambalo siyo la kiroho ili afunge hiyo ndoa, baada ya kanisa lake kutokumruhusu na kumnyima cheti cha ubatizo,hii ndoa ni halali? wakatengana na kupeana talaka na mme akaamua kuoa mwanamke mwingine bomani na huku akisema ni mke wa kwanza, na yule mwanamke akawa ameokoka anaweza kuruhusiwa na kanisa kufunga ndoa tena na mtu mwingine? bibilia inasemaje kuhusu hilo,naomba mnisaidie katika hilo.
  Mungu awabariki

 199. Wapendwa wana wa Mungu waenda mbinguni,

  Ninasikitishwa kidogo na baadhi ya ndugu wanaodiriki kusema kwa njia wanayoijua wao wakisingizia ni Yesu wanapata utajiri na kisha wataenda mbinguni. Ninatamani kutokuwa mkali katika hili, lakini pengine niseme yafuatayo:

  Ninashangazwa na (watumishi wa Mungu?)ktk mabano kwa sababu siamini kama ni watumishi kweli wanaoweka matangazo ya jinsi hiyo. Kazi ya mtumishi wa Mungu yeyote yule ni kuhubiri Injili ili watu waokoke na kumjua Mungu aliyewaumba (Mathayo 28:18-19). Miujiza na baraka ni kazi ya Mungu naye hutoa kwa wakati wake na kwa aliyekusudia kumpa, mwanadamu yeyote hana uwezo wa kulazimisha Mungu afanye miujiza hiyo, ama sivyo tutatia shaka na nguvu iliyo ndani yake.Sina maana nakataa miujiza hapana, ninaamini ipo Mungu anatenda na mimi ni shahidi wa mambo makuu amabayo amenitendea, lakini si kwa njia hii.

  Pili, utajiri na starehe za ulimwengu ni mambo ya dunia tu ambyo mtumishi wa Mungu Yakobo anayasema tusiyapende (Yakobo 4:4)na tena anayeyapenda hayo ni adui wa Mungu. Sasa itashangaza kama mtu anajiita mtumishi wa mungu na huku anaipenda dunia hali Biblia inasema mtu wa jinsi hiyo ni adui wa Mungu. Mimi nadhani inatubidi kufikiri kidogo kabla ya kutenda, maana kuna watu wengi sana sasa wanaojiita watumishi wa Mungu lakini ukweli ni kwamba sio. Injili wanazohubiri haziwaelekezi watu kwa Mungu bali kwa vitu vya dunia hii.

  Kumbukeni sisi tuliookoka sio wa dunia hii “sisi ni wapitaji tu” kwetu ni mbinguni. Wapendwa napenda niweke wazi hapa, simaanishi kwamba kuwa tajiri ni dhambi, wala kutafuta mali ni dhambi: bali ninashida na jinsi gani tunaipata mali. Shetani ni tajiri kuliko tunavyodhani, naye hugawa kwa wingi kwa wale wanaokubaliana naye. Si ajabu kaingia makanisani kwa sababu watu wengi wamegeuka hawajali kile ambacho Mungu anasema, bali husikiliza hali ya maisha waliyonayo na hufuata na kuamini wanakopata msaada KWA HARAKA.

  WAPENDWA UKWELI NI KWAMBA UKIKAA KIKAMILIFU KWA MUNGU NA KUMTEGEMEA YEYE UTAFANIKIWA BILA KUUTMIA SHORCUT YOYOTE. MUNGU MWENYEWE ANASEMA UKIKIRI NA KUTUBU UTAKULA MEMA YA NCHI. USIDANGANYIKE KWANI YAFAA NINI UPATE MALI NYINGI DUNIANI KISHA UKOSE FURAHA YA MILELE MBINGUNI NA MUNGU?

  Niishie hapa kwa leo, kisha nitaendelea wakati mwingine baada ya kusikia kutoka kwenu. Neema ya Bwana ikae mioyoni mwenu.

 200. Mpendwa Ev. Seni,

  Umesema umetupatia utangulizi wa majibu yako, ni vema. Lakini mimi naona ingekuwa vizuri tukamaliza kuwekana sawa kwanza juu mitume.

  Weka wazi kwamba sifa za mtume ulizozitaja una uthibitisho wa kibiblia au ulizipata toka mahali pengine. Uwe wazi tu! Itasaidia kumaliza dukuduku nililonalo mimi halafu tusonge mbele

  Napenda kufahamu kama sifa hizi za mtume ni za Kibiblia au vinginevyo:

  1. Awe aliyeishi katika karne ya kwanza
  2. Awe ametoka ndani ya Palestina.

 201. Wapendwa katika Bwana haleluya!!!…..napenda tu kuwapa utangulizi wa majibu yangu juu ya mitume na manabii wa siku hizi. TUSOME Luka 16:16…nadhani inaeleweka sana hata kwa wewe unayejiita nabii, kwamba mwisho wa manabii ni YOHANA MBATIZAJI kilichobaki ni kupigania ufalme wa Mungu tu.

 202. Leo nataka kuleta hoja hii kwenu, nataka kujua kama kweli maandiko yanalithibitisha jambo hili; KUNA TETESI KWAMBA YUDA ISKARIOTE alitubu wakati wa mahubiri ya YESU huko kuzimu,(yaani wakati Yesu alipokufa msalabani aliziendea roho zilizoasi tangu wakati wa Nuhu) je usemi huu ni kweli au vipi? Na pia inawezekana kwamba alianza kutubu hata wakati Yesu akiwa hai, kwani alivirudisha vipande vya fedha—-na hii toba ilikuwa toba kweli ya kurudisha ulivyochukua (MT 27:1ff je na huu usemi vipi wapendwa. Tusaidianeni katika hili kwani watu wengi wanadanganywa na madhehebu ya UNIVERSALISM (UNIVERSAL SALVATION) yaani mkazo wao hawa ni kwamba HAKUNA MTU WA KUPOTEA NI LAZIMA WOTE WAOKOKE!!!! JE ni kweli???

 203. BWANA apewe sifa sana ndugu John! kulingana na jinsi ambavyo unazidi kuchimba (exegeses)neno la Mungu kwa undani zaidi, nahitaji kupata muda mzuri kwa ajili ya kufafanua kwa upana hoja hii nzito…lakini pia bwana John naona unazidi hata mimi kunifunulia mambo ambayo yamefichika sana! labda pengine kwa ufahamu wangu haiwezekani kujua Mungu peke yake ndiye anayeweza kunifunulia!kwa kweli mpaka nisikie sauti ya Mungu juu ya jambo hili.
  Nitajiandaa vizuri zaidi kuelezea full katika somo hili wiki ijayo! kwa sasa acha niseme wikiend njema!

 204. Mwinjilisti Seni,

  Naomba univumilie ilituendelee kuchambuwa maandiko kwa faida yetu sote.

  Maandiko uliyosimamia wewe ni haya hapa. Katika kiingereza (KJV) yanasema hivi:

  Wherefore of these men which have companied with us all the time that the Lord Jesus went in and out among us.Beginning from the baptism of John, unto that same day that he was taken up from us, must one be ordained to be a witness with us of his resurrection.

  Na katika kiswahili yanasema:

  Basi katika watu waliofuatana nasi, wakati wote Bwana Yesu alipouwa akiingia na kutoka kwetu, kuanza tangu ubatizo wa Yohana , hata siku ile alipochukuliwa kwetu kwenda juu inapasa mmoja wao awe shahidi wa kufufuka kwake pamoja nasi.

  Mwinjilisti Seni maandiko haya yaonyesha jinsi walivyokuwa wanachaguwa mtu wa KUWA SHAHIDI wa kufufuka kwa Yesu. Sijuwi, labda siwezi kusoma vizuri: inapasa mmoja wao awe shahidi wa kufufuka kwake pamoja nasi- haisomeki inapasa mmoja wao awe mtume! Baada ya shahidi huyo, wa kufufuka kwa Yesu, kupatikana ndipo akashika mahali katika huduma hiyo ya utume naye akahesabiwa kuwa pamoja na mitume.
  Au nakosea?

  Lakini hata kama utaratibu huo ndio waliotumia kuchaguwa mtume wakati wa kanisa la Kwanza mimi naona huo ungekuwa ni mwongozo wetu katika kuchagua [kama ni lazima kufanya hivi] au kuwatambuwa mitume wa nyakati za siku zetu.

  Na kwa kuwa sasa tunaenenda kwa imani na si kuona; Tunaweza kuziweka sifa hizo kama ifuatavyo:

  i). Awe ni mtu aliyemwamini Yesu na anaishi maisha matakatifu ndani ya wokovu, [kufuatana na Yesu ikilinganishwa na wakati ule Yesu akiwepo hapa duniani]

  ii). Awe amekaa katika wokovu kwa kipindi cha kutosha na hivyo kuwa na uzoefu katika utumishi na mwenendo wa maisha katika wokovu [ mfano wa Kipidi kutoka ubatizo wa Yohana mbatizaji hadi unyakuo wa Bwana Yesu]. Siyo mtu kaokoka jana na leo ni mtume.

  iii). Awe ni mtu anayeamini kwamba Yesu kristo alikufa, akafufuka na akapaa mbinguni. Kwa kifupi awe ameokoka [Kwa kuwa kwa siku zetu shahidi wa kufufuka kwa Yesu ni kila mtu anayeamini kwamba Yesu Kristo alikufa, akafufuka na akapaa mbinguni].

  Kwa hiyo mtu mwenye sifa hizo ambaye Mungu anaweza kumchagua anaweza kuwa mtume!

  Au unafundisha sasa hivi tufanye mambo ya kwenye biblia kwa kuiga kimwili kila kilichofanyika wakati huo? [nimeshasikia kuna kanisa wao wakifika kwenye ibada mchungaji wao anaanza kuwanawisha miguu washirika wote]

  Hata hivyo katika sifa za mtume ulizozitaja naona ni moja tu ndiyo umetafuta maandiko yake na kuyatafsiri ili yaendane na hoja yako.

  Naomba kukukumbusha sifa ulizozitaja na zikaleta maswali yote haya ni hizi hapa:

  1. Awe aliyeishi katika karne ya kwanza
  2. Awe ametoka ndani ya Palestina
  3. Awe aliyewahi kuwa na Yesu

  Kama maandiko uliyoyaandika yameonyesha sifa zote hizi ulizotaja naomba kufahamishwa. Lakini kama sivyo basi endelea kuleta maandiko!

  Lengo la kuandika haya ni kusababisha tupate wakati wa kujifunza na kulielewa vema neno la Mungu ilitusije danganywa na elimu za siku za mwisho.

  KUHUSU MANABII

  Manabii wa uongo walikuwepo tangu agano la kale. [Luka 6:26 – Ole wenu ninyi wakati watu watapapowasifu, kwa kuwa baba zao waliwatenda manabii wa uongo mambo kama hayo]. Kwa hiyo wakati wa agano la kale manabii wa uongo walikuwepo pia.

  Katika Mathayo 24:11 imeandikwa ‘Na manabii wengi wa uongo watatokea na kuwadanganya wengi’.
  Hii haina maana kwamba manabii wote wa siku za mwisho watakuwa wa uongo.

  Kwa habari ya manabii wa uongo Yohana anaandika katika 1Yoh 4:1-3 kwamba:
  “Wapenzi msiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani. Katika hili mwajuwa roho wa Mungu, kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu. Na kila roho isiyo mkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambaye mmesikia kwamba yaja na kwamba imekuwako duniani.

  Ishara kubwa kabisa ya wazi tunayoipata hapa ni kwamba nabii wa uongo hupotosha watu kwenye kweli ya Mungu na hata kumkana Yesu mwenyewe. Hili limeshatokea tayari. Wengi wameshadangayika na hili kwa kuamini mafundisho yanayosema Yesu si mwokozi, wala hakufa na wala hakufufuka. Watu wanaokwenda kukaa milimani hadi miili yao inadhoofika wakimsubiri Yesu awachukuwe hawa pia ni wahanga wa manabii wa uongo. Mifano iko mingi lakini naishia hii miwili.

  Katika Mathayo 7:15-16 imeandikwa:

  “Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaovaa maazi ya kondoo lakini ndani ni mbwa mwitu wakali. Mtawatambuwa kwa maunda yao.”

  Katika mistari inayofuata hapo anaelezea matunda ya hao manabii wa uongo. Mtu anayesema kuwa ni nabii au mtumishi wa Mungu wakati maisha yake mwenyewe anaishi tofauti na Neno la Mungu huyo ni muongo. Kwa hiyo kwa matunda ya twaweza kuwatambuwa manabii wa kweli na wa uongo.

  Mathato 24:24 imeandikwa “Kwa kuwa watatokea maktisto wa uongo na manabii wa uongo nao watatoa ishara kubwa na maajabu, wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata na wateule.

  Ni kweli manabii na makristo wa uongo watatokea [na tayari wameshatokea] wenye kufanya ishara nyingi na maajabu. Lakini katika hawa wafanyao ishara nyingi na maajabu utambulisho wao ni MATUNDA YAO ambayo tunayapata katika Mathayo 7:15-23.

  Kuponya wagonjwa na kufukuza pepo si pekee ndizo ishara za nabii wa uongo; maana haya pia ni maagizo ya Bwana Yesu. Nabii wa uongo kazi yake kuu ni kuwapotosha watu kutoka kwenye ukweli wa neno la Mungu na kuwapoteza. Na kama hawafundishi upotovu matunda ya matendo yake yataonyesha. Hakutakuwa na tunda la Roho Mtakatifu ndani yake.

  Naona kinachosumbuwa hapa labda ni kule kusikia habari mbaya za watumishi wengi, siyo manabii peke yao. Kuna habari mbaya za watumishi wa Mungu katika kila huduma! Iwe ni wainjilisti, walimu, wachungaji, maaskofu nk. Lakini kusikika kwa habari hizi mbaya haimaanishi basi watumishi wote ni waovu. Hapana. Kuna watumishi ambao ni waaminifu katika utumishi wao, ni wasafi kabisa. Hivyo kuchafuka kwa baadhi ya watumishi katika huduma mbali mbali katika mwili wa Kristo haimaanishi kwamba aina hiyo ya utumishi haipo.

  Lakini maandiko yanaeleza pia kwa habari ya watu kufukuzwa mbinguni pamoja na kusema walitoa pepo na kuponya wagonjwa kwa jina la Yesu. Hii haimaanishi KUTOA PEPO NA KUPONYA WAGONJWA ndiyo kosa. Hapana. Kosa ni kushindwa kuishi maisha matakatifu. Ni kushindwa kuonyesha maisha yenye matunda mema.

  Ndugu Mwinjilisti Seni naona umekaa upande mmoja tu wa wa kupima manabii wa uongo kwamba kutoa pepo na kutenda miujiza wanfanya usanii tu. Ni kweli hatuwezi kupima kwa namna hiyo kwamba mtu akitenda hivyo basi ni nabii wa uongo. Tukumbuke pia kwamba kutenda miujiza na kuponya wagonjwa si pia kipimo peke yake cha kusema huyu ni nabii wa kweli.

  Ni kweli shetani anaweza kufanya ishara kubwa pia LAKINI hii haina maana si kila ishara kubwa ifanyikayo ni ya shetani na Mungu ndiye hufanya ishara kubwa zaidi kuliko za shetani.

 205. SHALOM! bwana John nashukuru kwa maswali yako mazuri na ya kutia changamoto kwa watumishi wa MUNGU ili wazidi sana kusoma neno la Mungu.

  Nijibu swali la kwanza hivi; BIBLIA ni kitabu pekee ambacho kiko (inspired by the Holy Ghost)kimevuviwa na R.M! Kwa hiyo kwenda kinyume na hapo nitakuwa nimevuka mipaka ya Mungu! Pia Biblia ni inajitoshereza kabisa kwa mafundisho yake….mimi ninaposema kwamba tuangalie historia, nataka tuone kanisa la kwanza walifanya nini katika kuchagua mtume! na utata mkubwa hata kipindi kile cha mwanzo wa kanisa ilikuwa ni swali kwamba “nani ni mtume na nani sio mtume” na ndiyo maana usishangae Paulo walitaka kukataa kwamba sio mtume na ikabidi ajieleze ameupataje huo utume, na hata kwa leo inabidi tuwe tunawauliza watu hawa wanaojibandika vyeo vya kuwa mitume na manabii!!!! TUONE KITABU CHA HISTORIA YA KANISA CHA MATENDO YA MITUME 1:21-22. Katika fungu hili kuna sifa za mtu kuchaguliwa kuwa mtume nazo ni;
  1. Mtu aliyefuatana na YESU wakati wote kama wale Thenashara.
  2. Tangu ubatizo wa Yohana hadi Yesu alipochukuliwa toka kwa wanafunzi wake
  3. Awe shahidi wa kufufuka kwa YESU
  Hapa tunaona kwamba Mathiasi aliteuliwa kushika huduma hii ya utume v.25
  Pengine labda unaweza kujiuliza kwamba kwa nini Paulo anajiita mtume wa BWANA YESU? Jibu lipo katika Biblia MDO 9:27-28. Hapa tunaona kwamba;
  1. Barnaba alimpeleka Paulo kwa mitume baada ya kuwaona wanafunzi wa YESU bado wana wasiwasi naye kuhusu kuokoka kwake. v26
  2. Alikaa pamoja nao na akaendelea kumtumikia Mungu kwa ujasiri v 28….hii ina maana kwamba kama ni mafundisho ya kitume alikuwa amepokea toka kwa mitume 12
  Hebu jiulize mpendwa kwamba ni kwa nini katika lile kundi la wanafunzi hakuibuka mtu yeyote kusema “mimi ni mtume”?
  Kiongozi wa wakristo ni BIBLIA ambapo katika Biblia kuna historia! na kama tunakubaliana kwamba kiongozi ni Biblia, basi tuifate inasema nini na kwa vipi kanisa la kwanza liliweza kutenda kazi zake! BIBLIA HAIPINGANI YENYEWE(BIBLE CAN NOT CONTRADICT ITSELF) Lakini watu tunapingana wenyewe!

  Kusema kweli hakuna mtu ambaye sasa hivi anaweza akasema yeye ni NABII AU NI MTUME!!!!! huo ni uongo kabisa, na pia kwa kipindi kama hiki mtu akisema yeye ni nabii—yule ni mwongo kwani Biblia inasema kwamba nyakati za mwisho kutakuwako manabii wa uongo! Mtu asikutishe kutenda miujiza na kuponya wagonjwa na kutoa mapepo na kufufua wafu..huo ni usanii tu hakuna lolote kabisa!!!…hatuwezi kupima kwa namna hiyo…maana hata shetani anaweza kufanya ishara kubwa sana tu! kipimo ni BIBLIA TU….amina!!!!!

 206. Mwijilisti Seni nashukuru kwa ufafanuzi wako.

  Naomba kuendelea hivi.

  Umeandika maneno haya ulipokuwa uanaandika kujibu maswali yangu ‘yote’.

  “Kuhusu sifa za mitume ni kwamba; wakati mwingine inabidi turejee katika historia ya kanisa sio kuangalia biblia kwa kila jambo! Ukisoma historia ya kanisa inatoa hizo sifa kwamba kanisa la kwanza ilibidi waweke sifa za mtu kuwa mtume kwa maana kila mtu alikuwa akijiita mtume, na hivyo mitume wa uongo waliweza kujitokeza wengi sana kama vile kwa sasa mnavyoona wapendwa! kwa hiyo hata wakati huu inabidi tukumbuke historia ya kanisa maana ndiyo inayotuongoza kukumbuka yaliyotukia kabla yetu!”

  Lakini katika maelezo yako hayo naona kuna kitu muhimu sana kimejitokeza. Ninaomba kukuliza tena maswali machache.

  1. Je, una maanisha Biblia HAIJITOSHELEZI kutoa majibu na mafundisho sahihi kwa ajili ya kuwafikisha watu mbinguni?

  2. Je, Kiongozi wa UKRISTO/WAKRISTO ni Historia ya Kanisa au ni Biblia?

  3. Nitafurahi kufahamishwa hizo sifa za Mtume zinapatikana katika historia gani ya kanisa.

 207. Shalom wapendwa

  Mpendwa Daniel Seni,
  Hii mada ya unabii na utume, ni nzito sana kwa kweli. Ilifaa waulizwe hao wanaojiita Mitume na Manabii, labda wangetupa jibu nzuri. Mambo haya ni mambo ya rohoni, tusije tukawa tunapingana na kitu ambacho hatujakijua.

  Mpendwa daniel umetaka kujua iwapo ninao ujasiri wa kujiita Nabii “Bernard Mwenda”. Wow! kwa kweli mimi binafsi sina ujasiri huo kabisa, kwa sababu sina lolote. Lakini kama nilivyochangia hapo juu, ni kwamba iwapo tunasema kuwa kuna manabii wa uwongo, lazima manabii wa kweli watakuwepo. Hauwezi kuwepo uwongo bila kuwepo ukweli.

  “1Yohana 4:1-3 Wapenzi msiiamini kila roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uwongo wengi wametokea duniani. Katika hili mwamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu amekuja katika mwili yatokana na Mungu. Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani”. Haya ni maneno ambayo aliyaandika Yohana, yule aliyeandika kitabu cha Ufunuo.

  Sura hii aliiandika baadaye sana, baada ya Yesu kuwa ameondoka duniani. Maneno haya ukiyasoma katika roho, yanaonesha wazi kuwa manabii wa kweli kwa kipindi hicho walikuwepo, japo sisi tunaona kama waliisha baada ya Yesu Kristo kuja duniani. Maandiko yanasema “Wapenzi msiiamini kila roho kwamba zimetokana na Mungu” Roho zinazozungumzwa hapa ni roho za manabii, ambao ni wa uwongo na wa kweli. “Kwa sababu manabii wa uwongo wengi wametokea duniani”. Yohana hapa alikuwa anawafundisha wanafunzi wake, kuwa watasikia mafundisho kutoka kwa manabii mbalimbali, lakini wasiwaamini wote kwa sababu miongoni mwao watakuwepo wa uwongo! Mimi hapa ninajifunza kuwa, kumbe hata leo tunafundishwa na Manabii, lakini tunatahadharishwa kuwa, tujihadhari na manabii wa uwongo ambao wapo hata sasa.

  Mimi pia nadhani kama kuna ofisi za kitume na kinabii, anayekuwepo hapo lazima aweze kufanya hiyo kazi inayohusika na hizo ofisi. Mtu hawezi kuwepo katika ofisi ambayo hawezi kuzifanya kazi zinazohusiana na ofisi hiyo. Huwezi kukalia kiti cha mhasibu, ukasema upo hapo kwa kazi ya umakenika. Watu watakaokuja hapo watashangazwa sana na majibu hayo.

  Hii ni changamoto, mimi binafsi bado sijawaamini hao manabii wanaojitangaza. Lakini katika maandiko naona inapaswa kuwepo manabii nyakati hizi.

  Tuzidi kuitafuta kweli!

  S H A L O M !

 208. Bwana apewe sifa sana! Bwana Mwenda kwa kweli umenigusa sana kwa kujaribu kuelezea kuhusu huduma hizi za manabii! kweli umesema kwamba watu wote waliookoka ni manabii….kama vile jana mimi nilivyoelezea juu ya jambo hilo…lakini nina swali moja kwako bwana Mwenda, JE wewe unaweza kukubali kuitwa NABII BERNARD MWENDA? na kama ukikubali ni kwa misingi ipi? au hata kama ukikataa ni kwa misingi ipi? Na kama ndio hivyo tu mtu anaweza kuitwa nabii…..basi mimi kuanzia leo niitwe NABII DANIEL SENI tena sio hivyo tu ni MHESHIMIWA NABII NA MTUME DANIEL SENI!!!!!!!!!! je inaleta sense?

  Bwana Mwenda tujaribu kusaidiana katika maneno kama haya! mtu hawezi kwa leo kujiita nabii….vinginevyo wachungaji wote ni MANABII, maana wana neno la Kristo! kwa leo HAKUNA NABII WALA MTUME KUNA HUDUMA TU ZA HIZO OFISI na anayeshika ofisi hiyo ni MCHUNGAJI na wala sio mtume au nabii! Acheni kudanganywa wapendwa na watu wanaojitangaza katika huduma. AMINA….mimi EV DANIEL SENI

 209. Mimi nadhani nyakati hizi, wote tuliookolewa tunayo Roho ya unabii, kwa sababu unabii ni Neno la Mungu lenye uzima lenye kuwafanya watu wengine ambao hawajalipokea wapokee na kuwa na uzima wa milele. Unaposema tubu dhambi zako uokoke vinginevyo utaangamia na kwenda zako jehanam ya moto! je, huo si unabii? Yule mtu akikataa hatakwenda kweli jehana ya moto?

  Nyakati za zamani Neno la Mungu lilikuwa linawajilia watu wachache tu kama akina Musa, Ibrahim, Daudi n.k. Hao manabii ndio walioweza kuongea na Mungu kwa niaba ya wengine. Lakini nyakati hizi kila mtu anaweza kuongea na Mungu, anaweza kuambiwa lolote na Mungu, anaweza kusikia sauti ya Mungu n.k. Kinachotakiwa ni kwamba amejikabidhi kwa huyo Mungu kiasi gani. Jinsi anavyokuwa amejizatiti kwa Mungu sana, ndivyo na Mungu anatenda kazi ndani yake. Ndiyo maana kwa sisi watu wa Mungu, ukiomba masafa marefu na ukatoa hoja zenye nguvu katika maombi yako, utaona kuna kitu cha ziada sana kwako katika uwepo wa Mungu, ujasiri na imani vinaongezeka.

  [Yohana 3:33 Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu……]. Hivi aliyetumwa na Mungu ni nani? Kama nilivyojaribu kuelezea hapo juu, kila anayekuwa ameokoka na anayelihubiri Neno la Mungu ili wengine waokoke, ametumwa na Mungu. Kwa sababu anayenena maneno ya Mungu, anatoa unabii ambao mtu anayeambiwa asipotenda ataangamia hakika.

  Nyakati za kabla ya Kristo, Roho wa Mungu alikuwa hashuki kwa kila mtu, lakini nyakati hizi kila anayemwamini Kristo na kuokolewa anakuwa na Roho wa Mungu kama alivyokuwa kwa, Ibrahim, Mussa, Daudi, Eliya, Haruni na wengineo. Tatizo lililopo nyakati hizi ni kwamba, bado watu hawajajizatiti kumtafuta Mungu kwa bidii. Hii imefanya hata shetani naye amepata nafasi ya kuwaingilia na kuwafanya wafanye mambo ya ajabu ajabu.

  Tunachotakiwa kuamini ni kwamba manabii wapo, japo katika hali ya udhaifu, na pia roho wa Mungu anatenda kazi ndani yao japo katika hali ya udhaifu. Ndiyo maana tunaiona miujiza kama ilivyokuwa nyakati za manabii wa agano la kale. Pia ni muhimu kufahamu kuwa, manabii wa uwongo wapo kwa sababu maandiko ndivyo yanavyosema, kwamba nyakati za mwisho watatokea manabii wa uwongo. Kama nyakati hizi hakuna manabii wa kweli, basi hata manabii hao wa uwongo hawapo, watakuja kuleta uwongo wa nini wakati kweli haipo? Kama kweli ya Neno la Munhu ipo na inahubiriwa, basi na upande wa pili upo. Hivyo tusing`ang`anie kwa kusema kuwa manabii wote nyakati hizi ni wa uwongo, je wa kweli wapo wapi?

  Haya ni maoni tu.
  Ni changamoto ninayoileta kwenu watakatifu wa Mungu, tuzidi kuchangia mawazo katika Roho Mtakatifu.

  S H A L O M !

 210. Bwana apewe sifa sana! Amen! pole bwana John maana mpaka sasa hujanielewa kwa jinsi ambavyo najaribu kuelezea kwa undani suala hili la mitume na manabii wa leo! lakini kwa sasa nitajaribu kurejea maswali yako ili yote niyajibu….okey karibu tuendelee!
  KUHUSU SWALI LA KWANZA: maana yangu ni kwamba, si kila mtu ambaye anamtumkia Mungu ni nabii na mtume.
  Ili kutambua zaidi ni kwamba kama tukisema leo kuna manabii maana yake ni kwamba sisi sote ni manabii. Kwa maana sisi sote tunashiriki siri za Mungu kupitia Roho Mtakatifu. Pia katika agano jipya tangu Yohana hakuna mtu yeyote aliyejaribu kujiita yeye ni nabii…japokuwa Yesu alimjua kuwa Yohana ni nabii lakini Yohana mwenyewe hakuwa tayari kupokea cheo hicho kikubwa (Mt 11:9 na Yoh 1:21)…Yohana alikataa kuitwa nabii kwa sababu kazi yake kubwa hakuja kutabiri
  Hata sasa Wakristo wote ulimwenguni tumeagizwa kwenda ulimwenguni kote “KUHUBIRI” MT 28:19-20 na MDO 1:8. Labda naomba msaada popote pale palipoandikwa kwamba “enendeni ulimwenguni kote MKATABIRI NA KUWA MANABII”
  Nataka pia nieleweshe sentensi yangu kwamba “Manabii wa siku hizi wanategemea biblia”—maana yake ni kwamba manabii wa agano la kale walipewa ufunuo na Mungu moja kwa moja! hakuna nabii ambaye kwa sasa anaweza kuongea na Mungu moja kwa moja (Ebr 1:1-2) sasa cha ajabu ni kwamba kuna watu ambao mpaka sasa bado wanategemea kuletewa maneno na manabii–watu kama hao wana mapungufu makubwa sana ya kiroho lazima wafundishwe! kwa upande wangu mimi mtu hawezi kuja na kuniambia Mungu kasema hivi au hivi..no! why? kwa sababu Mungu kwa sasa haneni nasi kupitia manabii…bali kama nikisoma Biblia na kuufungua moyo wangu kwake yeye atajifunua kwa njia ya neno lake..sio kwa mawazo ya watu wanaochemka madhabahuni tu.
  Mfano mzuri kabisa ni UFUNUO WA YOHANA…mtume huyu hakuwahi kuitwa “Mtume na nabii” japo Mungu alimfunulia mambo mengi sana ya wakati wa mwisho…je umewahi kujiuliza kwa nini hakuitwa nabii? Ni kwa sababu Mungu haneni na watu kwa njia ya manabii siku hizi!
  Kuhusu roho ya unabii ni kwamba “inafanya kazi pale ambapo ni pagumu sana na panahitajika msaada wa haraka kwa ajili ya kutia moyo au kuonya watu! lakini anayetoa kamwe hatuwezi kumwita nabii hata siku moja na kamwe kwa leo hatuna mtu anayeitwa nabii katika kanisa maana hicho ni cheo tu na wengine wanataka kujinufaisha nacho kwa kutaka kuheshimiwa hata kuliko na mitume wenyewe na manabii wa agano la kale.
  Ukisoma Waefeso 2:20inasema “mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye kristo mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni”…je unafikiri ni nani anayeambiwa hapa? kama sio sisi wenyewe kwa leo pamoja na ndugu wanaojiita manabii??
  Kuhusu sifa za mitume ni kwamba; wakati mwingine inabidi turejee katika historia ya kanisa sio kuangalia biblia kwa kila jambo! Ukisoma historia ya kanisa inatoa hizo sifa kwamba kanisa la kwanza ilibidi waweke sifa za mtu kuwa mtume kwa maana kila mtu alikuwa akijiita mtume, na hivyo mitume wa uongo waliweza kujitokeza wengi sana kama vile kwa sasa mnavyoona wapendwa! kwa hiyo hata wakati huu inabidi tukumbuke historia ya kanisa maana ndiyo inayotuongoza kukumbuka yaliyotukia kabla yetu!
  Tukumbuke kwamba Mungu anatumia watu kufikisha ujumbe wake mahali alipokusudia, na ndiyo maana hata kanisa la kwanza liliamua kuweka sifa hizo! Angalieni kwa sasa jinsi watu wanavyotumia vibaya huduma hii, mara mwingine “mzee wa mafunuo” au “mzee wa……………….? jamani hawa ndio mitume wetu na manabii wetu ambao tunawategemea watupe maneno toka kwa Mungu? kujibandika jina ni sifa? lazima tuwe makini huu ni ukweli usiopingika? Najua ninyi ni watu wa hekima, je mnafikiri hawa watu wanaishi kama manabii kweli?kwa leo nikomee hapa, Mungu awabariki sana wapendwa katika Bwana! amina

 211. shalom wapendwa.
  nashukuru kwa fundisho,hakika ;najifunza vingi na nitaendelea kujifunza kutoka kwenu.

 212. Ndugu Mwinjilist Seni,

  Asante kwa majibu yako kwa baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wachangiaji wenzangu.

  Kwangu mimi kila unapojibu ninapata maswali mengine kutokana na maelezo yako. Maswali haya ninayopata ni YA KIBIBLIA KABISA. Lakini kwa sasa (mimi) sitakuuliza kwa kuwa bado kuna maswali mengi ambayo hujayajibu.

  Natumaini unaendelea kujibu maswali mengine yaliyobakia!

  Tuko pamoja!

 213. Bwana apewe sifa sana!! wapendwa katika Bwana kwanza nawapa pole kazi ya Mungu! nataka nitumie wakati huu kujibu maswali mliyoniuliza wapendwa, naomba niyaainishe maswali nami nitajibu moja moja.
  Kuhusu fungu la Waefeso 4:11 nataka kusema hivi: Paulo alikuwa akielezea kwamba kanisani kazi ziko nyingi sana. Paulo anaelezea huduma tano; Mitume, Manabii, Wainjilisti, Wachungaji na Waalimu. Kwa hapa ninachotaka kusema ni kwamba hao wote ni kwa kusudi la kulijenga kanisa.
  Mtu anayelea kanisa ni MCHUNGAJI, huyu ndiye aliye na kazi ya kulea kanisa. Mchungaji huyo huyo anaweza kufanya kazi ya unabii-lakini yeye hatuwezi kumwita nabii, pia Mchungaji anaweza kufanya kazi ya utume-lakini hatuwezi kumwita mtume. NASEMA SANA JUU YA HUDUMA HIZI MBILI kwa sababu zinasumbua kidogo!
  Paulo kila waraka aliouandika ilibidi aseme “Paulo mtume wa Yesu Kristo” {hebu soma Wagalitia 1:1) “Paulo anasema “si mtume wa wanadamu, wala kutumwa na mwanadamu”…..kwa hiyo lazima tutambue kwamba ilikuwa kazi ngumu kupokea utume wake lakini ilibidi aelezee kwa undani ni kivipi alikutana na Yesu,kwa sababu kipindi kile mtume alitakiwa yule aliyepata mafundisho ya Yesu moja kwa moja! Ila kwa sasa sijui hawa mitume kama wamepata mafundisho moja kwa moja…Ila Paulo namkubali kuwa ni mtume..maana alikutana na Yesu huko njia ya kwenda Dameski. kuhusu Timotheo watu wa kanisa la kwanza walimwita mtume….niseme pia kwamba SISI SOTE KWA SASA TUNAITWA……SOMA MATENDO 11:26.
  Kwa maana ya wazi ni kwamba MCHUNGAJI ANAWEZA KUFANYA HUDUMA ZOTE lakini title yake anabaki kuwa ni MCHUNGAJI TU.
  Kuhusu utumishi kwa Mungu ni kwamba MUNGU ANATUTAKA TUMTUMIKIE lakini sisi nasi ni lazima TUTAKE KUMTUMIKIA soma 1TIMOTHEO 3:1 “mtu akitaka kazi ya asikofu atamani kazi njema”…..”AKITAKA” maana yake yeye mwenyewe ametaka awe mtumishi wa Mungu–naomba uelewe pale bwana John.
  Kuhusu theology ni kwamba YESU alikuwa na chuo cha theologia cha miaka mitatu, maana ya theology ni Elimu ya Mungu “theo-God” logy-study or theory…hivyo theologia ni kujifunza zaidi juu ya Mungu wetu…na NENO linatuambia kwamba tunaweza kujisifu kwa sababu tunamjua Mungu. Na pia kutaka kumtumikia Mungu ni jambo jema, tunashuhudia watu wanaokoka wakiwa katika vyuo vya theologia na wanakuwa watumishi wa Mungu wazuri mno.Nadhani mpaka hapo nimeeleweka, Mungu awabariki sana —-SISI SOTE NI WANAFUNZI KATIKA ELIMU YA Mungu—–amen

 214. Ndg Seni,

  Nashukuru kwa majibu yako. Lakini sijaelewa kwa sababu HUJAJIBU baadhi ya maswali yangu wala kuyagusia kwenye mchango wako. Niliuliza kutokana na maelezo uliyokuwa umeyatoa wewe. Hivyo naomba tena maajibu ya maswali yangu namba 1 & 2 katika mchango wangu uliopita.

  Pia niko gizani bado unaposema NABII WA LEO ANATEGEMEA BIBLIA TU sasa napata tabu kwamba KWA NINI TUSISEME MANABII WAPO LAKINI WANATEGEMEA BIBLIA? [hiyo ni kutokana na maelezo yako]

  Hata hivyo bado unazidi kunichanganya hasa pale ulipoandika hivi “Aliyepewa vingi kwake huyo vitatakwa vingi” na wewe unayesema ni nabii…basi ujue kwako vitatakwa vingi sana/sio kwamba ninakwepa wajibu–lazima tutumike kwa sana tu mpaka Yesu aje!”….Hapa pia nimekosa jibu la swali hili kwamba HUYO ANAYEJISEMA NI NABII VITATAKWAJE VINGI SANA KWAKE WAKATI YEYE SI NABII?

  Lakini ndugu Seni Biblia imesema wazi katika Efeso 4:11 kwa habari ya kuwepo kwa MITUME na MANABII katika Nyakati hizi za Uongozi wa Roho Mtakatifu. Ndugu Steve amekuuliza maandika haya yana maana gani? Hili pia hujalijibu.

  Kuna suala la kwamba HUDUMA YA KINABII INAFANYAJE KAZI PASIPOKUTUMIA WATU? Kama ilivyo huduma ya Uinjilisti kufanya kazi ndani ya Muinjilisti ndivyo ilivyo huduma ya UNABII kufanya kazi ndani ya Nabii.
  Hili pia hujalifafanua.

  Hata hivyo naona ndugu Mwinjilisti Seni kuna maswali mengi ambayo hujayajibu. Kuna suala la SIFA ZA MTUME mbazo ulizitoa wewe tarehe 18/2/2009. Baada ya SIFA hizo ulizitaja wengi wameuliza maswali. Ndugu Bernad Mwenda ameuliza maswali kama sita [6] hivi. Pia ndugu Raphael akauliza na kuhitaji ufafanuzi. Ndugu Steve pia aliuliza kwamba anahitaji kupatiwa uthibitisho kwenye Neno la Mungu. Na kisha ndugu Abigail na mimi [John Paul] tutaungana wenzetu nami nikaongeza mengine kutokana na mchango wako.

  KINACHONITATIZA NI KWAMBA KATIKA MAJIBU YAKO UMEKWEPA KUJIBU MASWALI KAMA YALIVYOULIZWA. MIMI NAOMBA UZINGATIE KWAMBA MADA HII NI NZURI NA KUBWA NA KUNA MENGI YA KUTUFAA WATU TULIO KATIKA IMANI YA WOKOVU. SASA HEBU CHUKUWA MUDA,[kama alivyokuomba ndugu Abigail] JIPANGE VIZURI, UJIBU MASWALI KAMA YALIVYOULIZWA. KUKWEPA KUJIBU MASWALI HAKUTATUSAIDIA KUJIFUNZA.

  TAFADHALI MWINJILISTI, CHUKUWA MUDA, FAFANUA MASWALI ULIYOULIZWA ILI ULETE MAJIBU. TAMBUWA KWAMBA KWA KUFANYA HIVYO TAYARI UNAMTUMIKIA MUNGU.

 215. Asante sana bwana Steven, John na dada Abigaili–kwa kweli maswali mliyoniuliza ni ya maana na yana msingi katika Biblia!
  Kuhusu nyazifa za kitume na kinabii nataka niseme hivi, MANABII wa leo wanategemea Biblia tu (Bible centered)na kama akienda tofauti na Biblia basi hata nyie ndugu zangu ni lazima mtamkataa tu!
  Manabii wa zamani walipokea neno la Mungu moja kwa moja toka kwa Mungu na maneno yao yamevuviwa (inspired by the Holy Ghost) kwa maana hiyo basi hakuna kwa sasa mtu anayeitwa nabii! kwa kweli nashangaa kwa sasa unakuta mtu anajiita “mheshimiwa NABII” hata haoni aibu!!! kwa nini hapo nyuma watu kama hawa hawakuwepo? tuangalie tusije tukadanganywa na usanii wa watu wanaotaka maslahi yao binafsi tu na mungu wao ni tumbo!
  bwana John usiogope kuniita mwinjilist maana hiyo ni endelevu! kweli watu wote wanaomwamini Yesu ni watumishi wa Mungu katika nafasi zao!
  Kuhusu Theology najua kweli kwamba Mungu anatumia ujuzi wetu kwa ajili ya kutangaza sifa zake! Roho Mtakatifu anatumia elimu ya mtu kwa ajili ya huduma ya Mungu, lakini naamini pia kwamba bila kwenda Theology mtu anaweza kumtumikia Mungu kwa special gifts from God!
  Kwa kumalizia tu ni kwamba HATA UWE NABII uwe mtume au pastor,hiyo siyo identity ya kwenda Mbinguni(Mt 7:21)–na mbele za Mungu sisi sote tuko sawa! “Aliyepewa vingi kwake huyo vitatakwa vingi” na wewe unayesema ni nabii…basi ujue kwako vitatakwa vingi sana/sio kwamba ninakwepa wajibu–lazima tutumike kwa sana tu mpaka Yesu aje!
  Asante sana bwana STEVEN na bwana John na dada Abigail kwa chalenge nzuri ya kutaka kujua kwa undani neno la Mungu Mungu awabariki sana! hili ni darasa zuri la kujifunza! tujifunze!

 216. Nami pia nimepata maswali baada ya kusoma alivyoandika ndugu Seni. Ni vema ndugu Seni ukatumia muda mwingi kidogo kutufafanulia maswali waliyokuuliza walionitangulia.

  Bwana ni amani.

 217. Ndugu Seni [sijataka kukuita Mwinjilisti kama ulivyojiita naogopa usijeniambia kwamba siku hizi hakuna Wainjilisti bali kuna HUDUMA tu ya Uinjilisti],

  Nami naungana na ndugu Steve M kwenye maswali aliyokuuliza. Lakini wakati unapojibu maswali yake nami naomba uchanganye na majibu ya maswali yangu machache kutoka katika maelezo yako.

  1.Umeandika hivi- “Kama tukisema kwamba kuna mitume kwa sasa maana yake ni kwamba kila mtu anayefanya kazi ya Mungu ni mtume maana ametumwa na Yesu! Yesu hakuita kila mtu kwamba ni mtume–lazima tuwe makini sana hapo”

  Swali: Je, kwa kuandika hivyo unamaanisha kwamba kila mtu anayefanya kai ya Mungu ni mtume kwa sababu ametumwa na Yesu? AU unamaanisha kwamba kwa kuwa Yesu hakuita kila mtu mtume kwa hiyo si kila mtumishi wa Mungu ni mtume?

  2.Umeandika pia hivi: “Ukisoma vizuri Galatia 2 utagundua jinsi Paulo anavyojaribu kutetea utume wake na kudai kwamba mitume waliotembea na Yesu wamemkubali. Pia Paulo naye aliwahi kusema kwamba Yeye amemwona Yesu wakati wa kwenda Damaska.”

  Swali:
  i).Je, kwa kuandika hivyo unamaanisha kwamba Paul hakuwa mtume?
  ii).Je, unaweza weka wazi imani yako kwamba UNAAMINI au HUAMINI kwamba Mtume Paul, wakati huo akiwa anaitwa Sauli, alikutana na Yesu wakati akipeleka nyaraka za kuwatesa Wafuasi wa Yesu Kristo kule Dameski?

  Ninaomba sana ujibu maswali haya pia ili watu ambao hatujakuelewa tuweze kukuelewa. Nafikiri ni bora tukakuelewa sasa lakini kusema tutakuelewa baadaye labda inaweza kuwa too late!

  Kwa habari ya kwenda kusoma Theology ndipo mtu awe mtumishi wa Mungu mchango wangu, kwa kifupi, ni huu:

  Mtu ANAYETAKA kuwa mtumishi wa Mungu ndiye hutafuta kusoma kwanza ili apate mambo ya kuwaeleza watu kutokana na alivyojifunza chuoni. LAKINI mtu ambaye Mungu ANAMTAKA AMTUMIKIE huyo hufundishwa na Mungu mwenyewe mambo ya kuwaambia watu kutokana na huduma ambayo Mungu anamuitia. [soma habari za Isaya, Yeremia, Daudi nk utaona jinsi Mungu alivyowaita katika utumishi wakati wao wakiwa hawana ujuzi wowote wa utumishi lakini akawafundisha mwenyewe. pia waweza soma habari za Bwana Yesu alivyowachaguwa wale wanafunzi 12. Hakuhitaji CV zao kwanza ndipo awachaguwe]. Mtu aliyeitwa na kufundishwa na Mungu mwenyewe huduma yake hufanyika kwa MWONGOZO wa Roho wa Mungu lakini mtu ALIYETAKA kuwa mtumishi na hivyo kwenda kujifunza chuoni KWANZA huduma yake huongozwa na THEOLOGY, ambayo ni mafundisho ya wanaadamu. Hata kama mtu huyo hajaokoka na yuko kinyume kabisa na Neno la Mungu lakini akiwa ni ‘fundi wa kuongea’ watu wanaweza fikiri ana Neno la Mungu moyoni mwake kumbe Neno hilo liko kwenye akili tu, Theology!

  Mtu anayetaka kumtumikia Mungu katika eneo fulani maalumu ni LAZIMA AUTHIBITISHE wito wake kwa Mungu Aliye Hai ili kuona kw\ama ni KWELI AMEITWA au ni MSISIMKO tu. Wako wengi WANAOTAKA kumtumikia Mungu, wanakwenda vyuoni kusoma hiyo theology lakini wakiingia katika UTUMISHI wanaishia kuleta AIBU na kusababisha Jina La Yesu litukanwe! Kwa nini?…..kwa sababu ni wao WALIOTAKA kumtumikia Mungu na wala SI MUNGU ALIYEWAHITAJI WAO KATIKA UTUMISHI huo.

  Lakini hata hivyo kila mtu ANAYEMWAMINI NA KUMFUATA YESU tayari ni mtumishi wa Mungu. Kushuhudia watu habari za Yesu tayari huo nao ni utumishi. Hii haihitaji mtu kwenda chuoni kusomea theology. LILE BADILIKO ALILONALO MTU MOYONI MWAKE BAADA YA KUMWAMINI YESU ni UJUZI TOSHA kwa ajili ya kuwashudia wengine habari hizo za Yesu! Kuchangia kwa pesa na mali ili KUWEZESHA INJILI kuhuburiwa huo nao ni utumishi tosha. Lakini kama ni utumishi katika eneo fulani maalumu kama vile uchungaji, uinjilisti, ualimu hakikisha Mungu amekuita kweli. Hii itaepusha KUWADANGANYA WATU kwa kuwafundisha mafundisho makavu ya theology yasiyoweza kuwafanya watu wakutane na Mungu alye Hai!

  Nitaishia hapa kwa sasa.

  Nasubiri majibu ya maswali yangu kutoka kwa ndugu Seni.

  Tuendelee kujifunza!

 218. Ndugu Seni,
  Ningependa kufahamu hizo sifa zinapatikana katika sura gani katika Biblia! Nafikiri ni vema kama tukisikia mambo uliyojifunza/kufundishwa toka katika Biblia.

  Ndugu Seni, ningefurahi kama ungetueleza sura ya 4 ya waefeso kuanzia mstari wa 11 una maana gani? Je tumefikia viwango ambavyo vimeandikwa? Je tumefikia umoja wa imani na vingine ambavyo vimeelezwa hapo chini? Maelezo yako ni ya muhimu. Pia unaposema kuna utume hakuna mtume, nashindwa kukuelewa. Ni vipi kuwe na huduma ya uinjilisti lakini hakuna mwinjilisti?

  Pia suala la mtu mpaka apitie Bible college, siliafiki. Wakati nakubaliana na wewe kuwa kila ambaye Mungu atampa neema ya kwenda Bible college lazima aende, lakini Mungu hahitaji mtu aende Bible college ili amtumie. Mungu mwenyewe atamfundisha ili amtumie. Kama atatumia Bible college au home college au life college, hilo sio la msingi. Ni Mungu ndiye anayemuita mtu katika huduma, na ni Mungu ndiye anamwandaa mtu huyo!

  kwa sasa ningefurahi kupata maelezo ya maswali yangu hapo juu! Ubarikiwe

  Ephesians 4
  11And he gave some, apostles; and some, prophets; and some, evangelists; and some, pastors and teachers;

  12For the perfecting of the saints, for the work of the ministry, for the edifying of the body of Christ:

  13Till we all come in the unity of the faith, and of the knowledge of the Son of God, unto a perfect man, unto the measure of the stature of the fulness of Christ:

  14That we henceforth be no more children, tossed to and fro, and carried about with every wind of doctrine, by the sleight of men, and cunning craftiness, whereby they lie in wait to deceive;

 219. DADA MILIAM JOSEPH! nashukuru maana unataka kujua kwamba mtumishi wa Mungu lazima aende chuo au la! Unaonekana una wito wa kumtumikia Mungu sana! Mungu akubariki sana
  kuhusu jibu lako dada yangu ni kwamba-sio kwamba wale ambao hawajaenda chuoni sio watumishi wa Mungu, hao ni watumishi kabisa ila ni katika kiwango cha chini sana maana hawana maarifa ya kutosha kwa ajili ya utumishi. Kuna baadhi ya watumishi ambao hawajawahi kwenda chuo chochote cha Biblia lakini wanafanya kazi ya Mungu vizuri sana! hii inakuwa ni special gift from God–not for all” sio kwa wote wanaweza kuwa hivyo! hata hao waliona na special gift wanajiendeleza kusoma kwa namna mbalimbali!
  Katika agano la kale SAMWELI alikuwa na chuo cha MANABII–hata Elisha ukisoma vizuri agano la kale katika Wafalme ya kwanza utagundua kwamba walikuwa na wana wa manabii ambao walikuwa wakiwafundisha(train)–na pia Paulo mtume alisoma sana chini ya Gamaliel, alisoma torati na hata akawa FARISAYO mkubwa! kama ni kwa sasa Paulo angekuwa na Degree ya Theologia!hivyo kwa namna hiyo ni lazima mtumishi wa Mungu apate knowledge ya neno la Mungu!
  Siku hizi dada yangu kuna vyuo vingi mno na kwa bei nafuu sana unaweza kuvuna elimu ya Mungu na ukawa mtumishi safi wa Mungu!
  Kila mtu aliye na Elimu ya Mungu kwa kupitia Theology mara nyingi utendaji kazi wake utakuwa makini maana wakati huo Roho Mtakatifu atataka kuitumia sana elimu yake katika kanisa!
  Dada nataka kukushauri kwamba kama unataka kumtumikia Mungu sana–kasome Theology–ila uangalie ni chuo gani unaenda maana kuna zingine zinafundisha LIBERAL lakini naamini Mungu atakusaidia– kama kweli unataka kuwa mtumishi wa Mungu nitaomba kwa ajili yako sasa ili Mungu akutie Nguvu–AMINA!

 220. Kaka Benard Mwenda! asante kwa maswali yako mazuri ambayo yanahitaji ufafanuzi zaidi juu ya sifa za mitume.
  Kwa kweli kwa sasa ninavyojua mimi ni kwamba kwa LEO hakuna mtu anayeitwa MTUME bali kuna huduma ya UTUME. Kama tukisema kwamba kuna mitume kwa sasa maana yake ni kwamba kila mtu anayefanya kazi ya Mungu ni mtume maana ametumwa na Yesu! Yesu hakuita kila mtu kwamba ni mtume–lazima tuwe makini sana hapo
  Najua kwa sasa watu wanataka kuitwa majina makubwa makubwa kama vile mitume na manabii.
  Ukisoma vizuri Galatia 2 utagundua jinsi Paulo anavyojaribu kutetea utume wake na kudai kwamba mitume waliotembea na Yesu wamemkubali. Pia Paulo naye aliwahi kusema kwamba Yeye amemwona Yesu wakati wa kwenda Damaska.
  Kwa upande wa Timothy yeye aliishi katika karne ya kwanza kabisa wakati Injili inaenea ulimwenguni na kwa sababu alikuwa ni mchungaji wa kanisa la huko Efeso yeye hakudiriki hata siku moja kujiita mtume lakini watu wa kanisa la kwanza baadaye walimweka kwenye kundi la mitume!
  Labda tu kwa kueleza kwa ufupi ni kwamba ndugu yangu Mwenda kwa sasa hatuna watu wanaoitwa mitume lakini kuna HUDUMA ya UTUME na pia hatuna mtu anayeitwa NABII ila tuna HUDUMA ya UNABII– hii ni kwa sababu kwa sasa hakuna mtu anayeweza kuleta unabii upya tofauti na ulio katika Biblia! kila unabii ni lazima uwe na msingi katika Biblia ndo ujulikane kuwa ni unabii–na mtu nayetoa unabii kwa sasa hatuwezi kumwita nabii– kama ni mchungaji tutamwitwa mchungaji tu ila ana huduma ya unabii!
  Asante ndugu yangu kama umenielewa lakini hata usiponielewa-baadaye najua utanielewa tu–usibabaishwe na watu wanaotaka sifa tu! Amina

 221. Elimu ya Mungu ni ipi kaka mwinjilisti? kwani mpaka usome chuo cha Biblia? ina maana waliosomea chuo cha Biblia ni wa maana au ndio kweli watumishi wa Mungu kuliko ambao hawajasoma chuo? Kwani Theology ndio mwisho wa elimu ya Mungu?. Tafadhali mi sijaelewa haka kakipengele! kama vipi nami niende chuo.

 222. Ukikuta mtumishi wa Mungu anatangaza kanisa lake kama biashara ujue kwamba yule ni nabii wa uongo! jamani hii ni saa ya kuamka katika usingizi (Rum 13:11) maana watu wanadanganywa wazi wazi kabisa! yapo matangazo kama haya “NJOO UPONE! UKUTANE NA MTUMISHI WA MUNGU oooooo ATAKUOMBEA NAWE UTAPONA KABISA! JE UNASUMBULIWA NA KIFUA KIKUU? UKIMWI? KIFAFA? KANSA? NJOO HARAKA UKUTANE NA MTUMISHI WA MUNGU ALIJAA UPAKO WA MUNGU NAYE ATAKUOMBEA KIBINAFSI!” Matangazo kama haya tunayasikia redioni kila kukicha–utafikiri wanatangaza biashara! au wanapiga debe ili kupata watu wengi makanisani na kupokea sadaka nyingi! mimi binafsi sipendi hii tabia na kama yupo mtu anayeifanya kazi kama hii aiache mara moja kwani Mungu sio mdori wako! Kuna watumishi wa Mungu wanaouza upako——hao usihangaike nao—-HAO MUNGU WAO NI MATUMBO YAO!nao watalia siku moja Mt 7:21! be careful my friend!
  Hawa watu wanaofanya mambo kama haya hawana elimu ya Mungu–maana hawajawahi hata kwenda Bible school yoyote, ukiwaambia waende kusoma theology wanadai Roho Mtakatifu ndiye darasa tosha! jamani msipotoshe watu!

 223. Kaka Muinjilist Seni hizo sifa ni kwa Roho Mtakatifu au Theology? na kama ni kwa Roho Mtakatifu nachelea kuamini labda mpaka unithibitishie kwa NENO LA MUNGU,vinginevyo kama ni theology nadhani Roho Mtakatifu ni zaidi ya theology.Asante

 224. Kwako, Ev.SENI wa Calvin Theological College-DSM

  Mimi binafsi nashukuru kwa maelezo yako ya hapo juu,
  hata hivyo kutokana na maelezo yako, ninaomba
  ufafanuzi wa maswali hafuatayo!

  -Hizi sifa za mitume ulizozitaja, ndizo zinazotakiwa hivi sasa, au ndizo zilizotakiwa nyakati za kanisa la kwanza tu?

  -Kama hizo ndizo sifa zinazotakiwa hivi sasa,
  hao walioishi karne ya kwanza tutawapata wapi!

  -Kwa maelezo yako hayo, je nyakati hizi tunao mitume
  na manabii?

  -Manabii wanatoka Palestina tuu?

  -Je Mtume Paulo, Timotheo na wengineo ambao hawakuwepo nyakati za Yesu tuwaweke kundi gani?

  -Manabii na Mitume ni watu wa namna gani? Asante!

  S H A L O M !

 225. Nataka wapendwa nitoe somo ufupi jinsi ya kuwatambua mitume wa kweli au namna kanisa la kwanza lilivyopata kuwatambua mitume
  SIFA ZAO ZA NJE.
  1. Awe aliyeishi katika karne ya kwanza
  2. Awe ametoka ndani ya Palestina
  3. Awe aliyewahi kuwa na Yesu
  sifa hizi zilitumika hata wakati wa ku-replace badala ya Yuda Iskariote-wakamchagua Mathias.
  SIFA ZA NDANI
  1. Awe tayari kwa wito kuhubiri Injili kwa watu wote
  2. Aishi kwa utukufu wa Mungu na kwa kumtegemea Mungu
  3. Awe na ushuhuda mzuri kwa watu-ushuhuda wa ndani.
  Sasa swali ni kwako wewe unayesema ni”MTUME” je unazo hizo qualifications za utume wako? kama huna wewe sio mtume hata kidogo! asante kama mmenielewa!

 226. ni kweli matangazo hayo huwa hata mimi yananikera sana yaani utadhani ya waganga wa kienyeji na wahubiri siku hizi wanawadanga watu kwa kuwaonyesha vitu vizuri tu hakuna tena ANAYESEMA TUBUNI NA KUAMINI KWENYE MATANGAZO, kwa kufuata matangazo hayo mtu ataenda kanisani akiamini huko ni raha tu so akijaribiwa kidogo lazima aanguke sababu alitegemea raha tu, ngoja niwape mfano mmoja unajua kwanini Petro alimkana Yesu ni kwa sababu Petro tangu aitwe kumfuata Yesu alikuwa anaona vitu vizuri tu kutoka kwa Yesu watu kupona ,watu kulishwa maelfu kwa mikate 2, watu kutawanya kule hekaluni ktk biashara so Petro alimjua Yesu katika ushindi tuu so kibinadamu aliipoona anakamatwa anapelekwa huku na huko anatemewa mate na mengine mengi akamkana akasema mimi simjui mtu huyu sababu akaona tofauti na alivyozoea so wahubiri msiite watu kwa kunadi huduma nzuri nzuri kazi ya MUNGU sio biashara
  MUngu awabariki wahubiri wote

 227. Brethren in Christ, in 1988 I was in Congo for a month and I crossed to Uganda, 2001 again I Crossed to Kenya and right in septemer 9th 2008 in Toronto- Canada.

  I have not seen a peaceful,smooth and simple like.
  Yesu alisema,”Duniani munayo dhiki lakini jipeni moyo”
  Mungu awabariki.
  Bama Yosse.

 228. Hallejah

  kuna maswali mengine ukiangalia kwa hali ya kwaida unaweza ukaona kama hayana msingi wowote au yanalenga kumdhalilisha Mungu au kudhalilisha ukuu wake lakini kuna haja ya kwenda zaidi ya hapo ili kuyafahamu mambo kwa kina.

  Tabu Zonga ameuliza, nukuu, Nauliza jee yawezekana Mungu akaumba jiwe kubwa ambalo yeye hawezi kuliinua?

  majibu toka kwa John Paul, nukuu.
  Ni kweli kwamba Mungu anauwezo wa kufanya jambo lolote. Ni kweli pia Mungu ana uwezo wa kuumba chochote. Lakini kusema jiwe kubwa ambalo ‘yeye hawezi kuliinua’ inapingana na ukweli wa uwezo mkuu wa Mungu Mwenye Enzi.

  Vyovyote tunavyoweza kuelezea hatuwezi kuelezea kwa utimilifu jinsi ukuu na uweza wa Mungu ulivyo.
  TUNAWEZA KUELEZEA YALE TU TULIYOFUNULIWA NA YAKO KWENYE UWEZO WETU WAKU YAELEZEA KAMA WANADAMU.

  Kibinadamu tuna sema kinga ni bora kuliko tiba.

  MUNGU ANATOA TAHADHALI KABLA YA HATARI 1.

  mwanzo 2;16
  Bwana Mungu akamuagiza huyo mtu akisema matunda ya kila mti wa bustani waweza kula 17, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mbaya usile, maana siku utakapo kula matunda ya mti huo UTAKUFA HAKIKA.

  TAHADHALI 2.

  mwanzo 3:22
  Bwana Mungu akasema , basi huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu kwakujua mema na mabaya nasasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima akala akishi milele.
  Tahadhali namba 2 inaonyesha kwamba baada ya mwanadamu kutenda dhambi kama angefanikiwa kula tunda la uzima angeweza kuishi milele bila kufa akiwa mwenye dhambi, ndio maana Mungu akawafukuza bustanini na kuweka ulinzi mkali wa malaika wenye panga zinazo kata kuwili.

  Yaani kama unaona jambo furani linaweza kuleta madhara baadaye ni bora ukachukua tahadhali mapema kuliko usubiri madhala harafu uanze kuhangaika nalo. kimungu sijui inakuaje ila Mungu huwa anafahamu mwisho wa jambo kabla ya mwanzo. lakini pia kwasababu kuna hukumu ya Mungu tuna tahadhalishwa kuiepuka kwa kumpokea Yesu kama bwana na mwokozi wa maisha yetu na hukumu hii imeanza baada ya dhambi kuingia ulimwenguni kupitia Adamu na Hawa.

  kwanini shetani? na ingekuwaje kama Mungu angemuhukumu tu baada ya kuasi kwake mbinguni pamoja na malaika walio asi pamoja naye ili duniani kusiwe na kitu kina itwa shetani au mapepo?
  inamaana kama shetani asingekuwepo duniani au kwenye bustani ya edeni inawezekana hata tunda la kujua mema na mabaya lisingekuwepo. na kama tunda la kujua mema na mabaya lisingekuwepo kuanguka kusingekuwepo.

  na kama dhambi na uovu wote visingekuwepo duniani inamaana ingekuwa haina haja ya Yesu kuja wala neema kuja duniani ili kuokoa wenye dhambi maana wasinge kuwepo.

  Hivyo hata historia ya dunia ingekuwa tofauti na ile tuliyo nayo leo.

  MUNGU YUKO JUU YA VYOTE NA ANATAWALA VYOTE NA ANAWEZA KUFANYA CHOCHOTE WAKATI WOWOTE POPOTE.

  Jambo la muhimu ni kutii nini Mungu anatuagiza katika Neno lake, na peke yetu hatuwezi isipokuwa kwa msaada wa Roho wake.

  MUNGU NI MKUBWA SANA KIASI AMBACHO HATOSHI KWENYE UBONGO WA WANADAMU WOTE DUNIANI JAPOKUWA ANAWEZA KUKAA NDANI YA MWANADAMU MMOJA.

  NAKUABUDU MUNGU WA KWELI.

 229. Ndugu Tabu Zonga,

  Kwa kuwa umeweka swali hili hapa, natumaini ni letu sote, kwa hiyo nami nina haki ya kujibu.

  Jibu la swali lako ni hili:

  Kama unakubali Mungu ana uwezo wa kufanya lolote, Hakuna Jiwe kubwa ambalo hawezi kuliinua.

  Ufafanuzi:

  Ni kweli kwamba Mungu anauwezo wa kufanya jambo lolote. Ni kweli pia Mungu ana uwezo wa kuumba chochote. Lakini kusema jiwe kubwa ambalo ‘yeye hawezi kuliinua’ inapingana na ukweli wa uwezo mkuu wa Mungu Mwenye Enzi.

 230. Amin Nguluma

  Nakushukuru kwa maelezo yako.

  Umendika nakunukuu ”

  MUNGU ANAWEZA KUFANYA YOTE KAMA AMBAVYO ALIVAA MWILI AKAJA KWETU AKAKAA KWETU NASI TUKAUONA UTUKUFU WAKE [YOHANA1:14] ”
  mwisho wa kunukuu.

  Mimi nakuuliza unakubali kuwa Mungu anaweza kufanya lolote? Nauliza jee yawezekana Mungu akaumba jiwe kubwa ambalo yeye hawezi kuliinua?

  Natumai mara hii sitotupwa jaani.

 231. NINAKUSHUKURU SANA NDUGU YANGU MGUMBA KWA UFAFANUZI WAKO MZURI KUHUSIANA NA SWALI LANGU AMBALO NINAAMINI KABISA NDILO JIBU JEPESI KWA WOTE WANAOFIKIA UKOMO WA UELEWA KUHUSIANA NA UTATU WA MUNGU. SIKUWEZA KUENDELEA NA MJADALA KWA MUDA SASA KUTOKANA NA MAJUKUMU YA KIKAZI AMBAYO YALINILAZIMU KUWA KATIKA MAENEO AMBAYO HAYANA MTANDAO.

  HATA HIVYO NAOMBA NISHUGHULIKE KWANZA NA MGUMBA AMBAYE AMEJITOKEZA KUTOA JIBU ANALODHANI KUWA NDILO JIBU LA SWALI LANGU KUHUSIANA NA URAISI ,UENYEKITI NA UAMIRI JESHI MKUU WA JAKAYA MRISHO KIKWETE.
  NINASHUKURU KUWA MGUMBA UNAELEWA KUWA URAISI,UENYEKITI NA UAMIRI JESHI MKUU SI MAJINA ILA NI HADHI YAANI CHEO,UMEFANYA VEMA KUELEWA HIVI NA NINADHANI SASA CHUKUA HATUA NYINGINE YA KUONA KAMA MANENO HAYA YAFUATAYO NI MAJINA AMA NI VYEO.
  BABA,MWANA NA ROHO MTAKATIFU. NAOMBA AKILI YAKO IPATE MATUNDA ILI UUJUE UKWELI NA SI KUENDELEZA UBISHI USIO WA LAZIMA KWA JAMBO AMBALO HUJAKAA CHINI UKATAFAKARI KWA KINA. ELEWA KUWA MAJIBU YOTE YA MASUALA YALIYO NA UTATA KUHUSU MUNGU YANA MAJIBU RAHISI SANA KATIKA MAZINGIRA TUNAYOISHI BILA KUSUMBUA MISIMAMO YA VITABU VYA DINI KWANI MUNGU NI HAI NA MANENO YAKE NI HAI YALIYO POPOTE NAYO HUYATAMBUA MAWAZO NA MAKUSUDI YA MOYO.
  ENDAPO UTAPATA JIBU LA SWALI HILI LA NYONGEZA BASI TUTAENDELEA KATIKA ENEO JINGINE LA MASHAKA YAKO KUHUSIANA NA UTATU WA MUNGU WA WAKRISTO.

  PENGINE NILIPOKUWA NINAPITIA MICHANGO YA WATU KADHAA NILIONA MTU ALIYEULIZA ENDAPO MUNGU ALIACHA MBINGU NA KUWA KITOTO KICHANGA ALIMUACHIA NANI MBINGU. NINAAMINI KUWA MTOA SWALI AMA HOJA HIYO ANALO JIBU ZURI TU ASOME BIBLIA NA KAMA ATAONA KUWA BADO LINAMSUMBUA TUTAMSAIDIA ILI AMJUE MUNGU WA KWELI WA WAKRISTO ALIYEJIFUNUA KWA JINSI YA MWILI NASI TUKAUONA UTUKUFU WAKE KAMA WA MWANA WA MUNGU ATOKAYE KWA BABA AMEJAA NEEMA NA KWELI.

  HATA HIVYO NAOMBA UELEWE KUWA HAKUNA MAHALI WAKRISTO WANAPOTAJA UTATU WA MUNGU WANAPOSEMA MUNGU BABA, MUNGU YESU NA MUNGU ROHO MTAKATIFU BALI TUNASEMA MUNGU BABA,MUNGU MWANA NA MUNGU ROHO MTAKATIFU NA HAYA SI MAJINA BALI NI CHEO CHA MUNGU WETU WAKRISTO ALIYEUMBA MBINGU NA NCHI. TENA MUNGU WETU ALIJITAMBULISHA KWA WATU KATIKA NYAKATI KADHAA KULINGANA NA UHITAJI AMA ULAZIMA WA WAKATI NA TUKIO HUSIKA NA KILA ALIPOJIFUNUA KWA WATU ALIJIFUNUA AIDHA KWA KULITAJA JINA LAKE YAANI JAHWEH (NIKO AMBAYE NIKO) AMA WATU WALITOA JINA KULINGANA NA NAMNA MUNGU ALIVYOJIFUNUA MFANO JEHOVA NISHI,JEHOVA RAFA,ELOIM N.K.

  KWA HIYO USIJARIBU KUCHANGANYA WATU KWA KUBADILISHA KILE AMBACHO WAKRISTO WANACHOKIELEWA NA KUKIAMINI.
  HALAFU UMELETA SWALI RAHISI SANA KUWA BWANA YESU ALIPOKUFA KWA SIKU TATU MBINGU ILIKUWA INAONGOZWA NA NANI. HII INADHIHIRISHA JINSI AMBAVYO MAWAZO YA MUNGU WA KIKRISTO YALIVYO MBALI SANA NA MAWAZO YAKO NA NJIA ZA MUNGU MKUU WA WAKRISTO ZILIVYO MBALI SANA NA NJIA ZAKO NDUGU YANGU. UNAHITAJI KUKUBALI KUKAA CHINI NA KUELEKEZWA NA SI KUJISOMEA TU BIBLIA KWA KUTUMIA MAFUNUO MCHANGANYO YA DINI YAKO AMBAYO KAMA TUKITHUBUTU KUIGUSA TU UTATANGAZA FATWA.

  NI HIVI NDUGU YANGU. KWA VILE UMEKUWA UKISOMA BIBLIA KWA UBISHI UBISHI SASA NAKUOMBA ISOME KWA NIA YA DHATI YA KUELEWA MAUDHUI YAKE,HISTORIA YAKE NA VUNJA MPAKA WA UBISHI KUWA KILA UNACHOKISOMA KATIKA BIBLIA NI MAKOSA TU. MIMI BINAFSI NILIFANYA HIVYO ILI KUIHAKIKISHA IMANI YANGU KWA KUITAZAMA QURANI YAKO NDIPO NILIPOPATA UJASIRI WA KUSIMAMA POPOTE NA KUSEMA KUWA YESU NI MUNGU MKUU BILA WOGA HATA KAMA WATU WOTE WATABISHA NAMI NIKAPUNGUKIWA NA MANENO YA KUWAFAFANULIA.
  NILICHUKULIA KAMA MUHAMADI NI NABII WA KWELI NA ALLAH NI MUNGU WA KWELI NA QURANI NI KITABU CHAKE KITUKUFU NA KUAMUA KUFUATILIA HATUA BAADA YA HATUA KISHA NIKAUJUA UKWELI NA UONGO WA IMANI HIYO.

  HIVYO NAOMBA KWA WAKATI WAKO ACHA MASWALI HAYO MADOGO AMBAYO YANAFAFANULIWA VIZURI SANA NA BIBLIA KWA KUSOMA MAELEZO KADHAA KATIKA BIBLIA. BIBLIA INATAMKA KWA WAZI KABISA KUWA MUNGU YUPO MAHALI POTE KWA WAKATI WOTE NA KATIKA HALI ZOTE. MUNGU ANAWEZA KUFANYA YOTE KAMA AMBAVYO ALIVAA MWILI AKAJA KWETU AKAKAA KWETU NASI TUKAUONA UTUKUFU WAKE [YOHANA1:14] NDIYO MAANA YESU KATIKA SURA ZA MWANZO KABISA KATIKA INJILI YA YOHANA ANASEMA KUWA YEYE ANAUTOA UHAI WAKE NAYE ANAO UWEZO WA KUUTWAA TENA. MUNGU NI KILA KITU NDIYE ALIYEUMBA KILE SISI TUNAONA KUWA NI MASWALI MAGUMU KAMA KUZALIWA, KUFA, KUFUFUKA, NGUVU, UTUKUFU N.K KWA HIYO SI TATIZO KWAKE KUFANYA LOLOTE HUKU AKIENDELEA NA UUNGU WAKE.
  KWA HIYO KAMA KICHWA CHAKO KIMEGOMA KUELEWA HILI TAFADHARI WAULIZE KWA UTARATIBU WAKRISTO WAKUSAIDIE NA KAMA HAMU YAKO NI KUUBOMOA UKRISTO KWA KUTAFUTA UNACHODHANI KUWA NI UPOTOVU BASI NISEME UMECHELEWA KWANI WALIKUWAPO WENGI MNO AMBAO LEO HOJA NA FALSAFA ZAO ZINATUMIKA SANA KATIKA MAMBO KADHAA YA KIIMANI, KISIASA, KISAYANSI N.K AMBAO WALIFANYA HIVYO NA WALISHINDWA NA KUUACHA UKRISTO UKISONGA MBELE KWANI WAKRISTO HUSEMA MANENO HAYA “KITU GANI KITATUTENGA NA UPENDO WA MUNGU WETU, JE NI KIFO, MATESO, DHIKI N.K

  KARIBU KWENYE MAISHA YA UPENDO NA AMANI NDANI YA YESU UMPENDAYE SANA MUNGU AKUBARIKI.

  [Ujumbe kutoka Strictly Gospel: Mjadala huu ulikuwa umesogea mbele sana kutoka hapo ambapo ndugu Mgumba alijibu maelezo ya Amin Nguluma. Mjadala wa UTATU/UUNGU wa Yesu Kristo uliishia mahali ambapo Waislamu walitakiwa kujibu maswali kadhaa yaliyotokana na michango yao katika mada hii. Tumeruhusu maelezo haya kwa kuwa ndugu Amin alikuwa hajajibu. Kwa hiyo kama ndugu Mgumba hajaelewa mahali fulani katika melezo haya anaweza kuuliza. Lakini swali lazima liwe ni kutokana na maelezo haya na si vinginevyo. Nia yetu ni ile ile njema ya kuweza kumsaidia mtu anayefuatilia aweze kupata maana nzuri kutokana na mtiririko wa mjadala huu. Tunajuwa ndugu Waislamu wana Maswali mengi ambayo wangehitaji kupata ufafanuzi wake kutoka kwa wakristo. Lakini ili maswali haya yaweze kujibiwa kwa utaratibu na kumsaidia msomaji kufuatilia ndiyo maana Strictly Gospel tukasema inabidi mijadala ifuate mtiririko. Hata hivyo mijadala yote inayohusu masuala ya Ukristo na Uislamu ina ukurasa wake maalumu.

  Katika ukurasa wa UISLAM/UKRISTO mada inayoendelea ni kuhusu KUBADILISHWA/KUCHAFULIWA KWA BIBLIA. Hapa napo Waislamu wameulizwa maswali kadhaa ambayo wanatakiwa wajibu. Mada hiyo itakapofikia mwisho tutaruhusu MADA nyingine iendelee kujadiliwa.]

 232. Mimi kwa ufupi nasema hivi! kwa mda uliobaki hapa duniani wewe usipomjua MUNGU aliye hai aliyekufa msalabani kwa ajili yangu mimi na wewe, ukakiri ya kuwa ni BWANA na MWOKOZI wako na kumtumikia kwa asilimia mia moja UMEKWISHA HABARI YAKO! huna ujanja kabisa (yaani kwa maana nyingine wewe sio mjanja)

  Ritha.

 233. Ndugu Achipete,

  Asante sana kwa ufafanuzi mzuri kutoka kwako kutokana na jambo ambalo tumekuwa tukilijadili hapa. Nashukuru kwa kuwa umeweka nia yako ya kutaka kuandika kile ambacho ulikikusudia. Mungu akubariki wa kazi nzuri unayoifanya!.Lakini pia napenda kuelezea pale nilipotumia mfano wa Paradiso kwamba tunaamini japo hatujaiona. Ule ulikuwa ni mfano tu wa mambo mengi ambayo TUNAAMINI pasipo kuyaona. Sikuchukuwa mfano huo kwa sababu Paradiso imeandikwa mara nyingi kwenye Bible. Ningeweza kuchukuwa mfano wowote, hata jambo ambalo limeandikwa mara moja tu kwenye Biblia lakini bora tu liwe ni jambo ambalo hakijawahi kuonekana kwa macho. Lengo la mfano huo lilikuwa tu ni KUTOA MFANO WA MAMBO MENGI TUNAYOYAAMINI PASIPO KUYAONA KWA MACHO.
  Nashukuru kwa changamoto yako….TUKO PAMOJA!

  Kwa ndugu Mlindo Tabu,

  Naomba kukusaidia tu kwamba Suala la KUNYOFOLEWA au KUTOLEWA Kabisa kwa baadhi ya maswali nalo lina baraka zote za Biblia. Mimi naamini barua zinazozuiliwa kuonekana hapa ni zile ambazo HAZIENDANI NA MJADALA, au ZINAKIUKA MAADILI, au ZINALETA MALUMBANO YASIYO NA MAANA, nk. Ninaamini pia maswali yanayowekwa hapa ni yale yanayoleta mtiririko mzuri kwa mtu anayefuatilia ili aweze kupata maana na kitu cha kuweza kumsaidia katika maisha yake.
  Nilishaandika huko juu jinsi blog zisizo na moderation kulivyo na vurugu tupu na kwamba mimi mwenyewe siko tayari kuchangia katika blog isiyo na udhibiti wa mambo yanayoingia!

  Umenukuu vizuri sana katika 1Pet 3:13-16. Lakini nafikiri umesahau au hufahamu yaliyoandika katika 2Tim 2:16- ‘But shun profane and vain babblings: for they will increase unto more ungodliness’. Kuna maswali ambayo badala ya kuleta msaada huwa yanaleta upotevu zaidi. Vile vile kuna maswali ambayo hata kama likijibiwa, jibu hilo haliwezi kuwa na faida yoyote kwa aliyeuliza. Kwa hiyo kuzuia baadhi ya barua au mswali yasionekane hapa ni jambo la Kikristo pia.

  Bado nasisitiza juu ya maswali niliyomuuliza ndugu Mjema Kaaya naye akasema yanajibika kwa urahisi lakini ni zaidi ya siku 20 sasa hajajibu. Najuwa lengo si kushindanana bali ni kwenda pamoja hadi tufikie mahali pa kukubaliana juu ya UKWELI ni upi na UONGO ni upi! Lakini sasa ninaomba mtu atakayejibu maswali hayo ajibie kwenye UKRISTO/UISLAMU ili tuende kweye ukurasa wetu rasmi.

  Kwa dada Happiness,

  Asante kwa ushauri wako. Lakini mimi napenda kusema kwamba Waislamu au mtu yeyote ambaye HAMWAMINI YESU, [pamoja na wengine waliojipa majina ya dini za Kristo lakini wao wenyewe wakiwa hawafuati aliyosema Yesu] ni ndugu zetu. WENGI TULIKUWA HUKO!. Lengo la kuandika mambo mengi hapa ni kuplay part katika kuwasaidia ili waweze kutoka katika TABIA YA SILI, ya mwili, kwa kutumainia akili zao, ili kwa Neema ya Mungu waweze kuingia katika roho na hatimaye waweze kuyatambuwa MAMBO YA ROHO ambayo sasa yanaonekana kwao kama ni upuuzi! Kwa kuwa YESU AMEKUJA KUOKOA KILICHOPOTEA [Math 18:11]. Na waislamu wakiokoka huwa wanakuwa Mabalozi wazuri sana wa Yesu Kristo!

  Naamini unatambuwa andiko lisemalo Mwenye dhambi mmoja akimpokea Yesu huwa ni furaha mbinguni. Kwa hiyo kama kwa haya tunayoandika hapa muislamu mmoja atampokea Yesu tutakuwa tumefanya kazi njema!

  Naomba Samahani kwa kuwa tuliingilia ukurasa usio wa kwake.

  ….Amani!

 234. Ndugu wapendwa.

  Imekuwa ni kawaida kunyofolewa au kutolewa kabisa masuali.
  Huku ni kwenda kinyume na mafundisho ya biblia. Hii inadhihirisha ni namna gani kanisa lenu linavyo kiuka maamrisho ya biblia .

  Kumbukeni Biblia inasema

  Muwe tayari sikuzote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu, lakini kwa upole na kwa hofu. (1 Pet 3 :13-16)

 235. Ndg Steve na J Paul, nwashukuru sana kwa majibu yenu mazuri. Hurudia mara tatu hata zaidi kusoma maoni yenu yenye ushauri wa maana sana. Ukweli hufuatilia kwa makini ushauri wenu nikielewa wazi kuwa mnania ya kunisaidia.

  Pengine ningeweka wazi pale Ndg Steve alipoandika kuwa mimi nini matatizo. Hakika Ndg Steve hakukosea kabisa, kwani ningekuwa sina matatizo nisingetembelea tovuti hii. Kama mjuavyo kuna tovuti(blog) zaidi ya milioni, zenye jumbe tofauti toka muziki mpaka siasa. Lakini nikaziacha zote hizo na kutua hapa! Ukweli ni kwamba mimi nimesimama katika point D kizani, na nikasikia sauti au maneno kuwa point C(strictlygospel) kuna mwanga, na ndio niko mbioni kufika point C. Nafikiri umenielewa, kwani hata Mungu huwaita wote wenye matatizo waende kwake.

  Nikirudi kwenye suala la IMANI, hilo tumeenda vizuri sana na Ndg Paul na kwa hilo tuko pamoja. Ila pengine kwa kurudia mfano aliotoa Ndg Paul ule wa kuamini kuwepo kwa Paradise japo hatujaiona akilinganisha na utatu. Paradise imetajwa katika vitabu vyote vilivyotangulia (agano jipya na la zamani) kwa ufasaha zaidi. Laiti kama katika agano jipya ingeandikwa kuwa sasa hakuna tena Paradise, nafikiri imani ya watu kuhusu paradise ingegawanyika kwa mbili. Na kwa kurudia neno hilo hilo kwa nyakati zote na katika vitabu vyote ndiko kunako imarisha imani bila mgawanyiko. Na ndio maana binafsi pamoja na waumini wengine tunawaelewa wasomi wanapojiuliza kwanini UTATU haukutajwa katika vitabu 39 vilivyotangulia kama nilivyoeleza hapo juu.

  Nia kubwa ya kunukuu baadhi ya vitabu vilivyoandikwa na wasomi wanaofahamika zaidi na baadhi yao ni waumini kama makardinal na Pope, ni kuonye jinsi maandiko hayo yanavyoweza kuadhiri waliowengi. Kwa mfano Denmark ni nchi iliyokuwa ya kikristo (kwa maana ya kutotenganishwa kanisa na serikali kama Saudi Arabia) kwa miaka mingi sana. Ni kiasi ya miaka 15 iliyopita ndio serikali imetenganishwa na kanisa. Chuo kikuu cha Uppsala Sweden kilifanya utafiti mwaka 2005 na kuwauliza wadenish laki 3. Swali lilikuwa hivi “JE UNAAMINI KUWA YESU NI MUNGU”. Jibu moja kati ya majibu matatu
  a) Ndio
  b) Hapana
  c) Sijui
  25% walijibu ndio, 46% walijibu hapana, 29% walijibu hawajui.

  Swali hilo hilo liliulizwa mwaka 1990 na majibu yalikuwa kama ifuatavyo.

  36% walijibu ndio 20% walijibu hapana 24% walijibu hawajui

  Kwa maana hiyo binafsi niliconclude kuwa wanazuoni wamechangia sana katika namba zinavyojionyesha hapo juu. Hivyo ni muhimu kwa wahubiri kutopuuzia hayo maoni ya wanawazuoni. Isitoshe teknolojia imepanuka na ni rahisi kuufikia mtazamo mwingine.

  Nilimalizia kwa kuoba kueleza UTATU katika uislamu. Ndg Paul aliandika ” hata kama ukiandika dini nyingine zinavyofahamu kuhusu UTATU haina maana yeyote. Maana dini hizo zina mitazamo tofauti na IMANI KATIKA YESU”. Aidha umeandika Yesu aliyemuokozi wa ulimmwengu na baadaye ukaandika Yohana 12: 47 kuokoa ulimwengu.

  Nilipotoa wazo hili nia yangu ilikuwa ni kuwasaidia waislamu wamjue yesu vile ambavyo Biblia inahitaji au vile ambavyo YESU mwenyewe alitaka afahamike. Na nilionelea kuwa hapa ni pahala pazuri kwa waislamu kupata mahubiri mema. Lakini nilifikiri ni muhimu kwanza kutoa dondoo juu ya waislamu wanavyomueleza YESU na suala la UTATU, ILI IWE RAHISI KWENU KUJUA MUANZIE WAPI.

  Kama ulivyoeleza hapo juu kuwa YESU kaja kwa ajili ya walimwengu wote ikiwa pamoja na wamasai, wahindu, wabudha na waislamu. Lakini kwa yeyote atayeelezwa neno ni lazima atatoa mtazamo wake, na hapa ndipo nilifikiri ni muhimu kutoa machache juu ya dini nyingine. 1 Wakorintho 9.19-22 ” Maana ingawa nimekuwa huru kwa watu wote, nalijifanya mtumwa wa wote, ili nipate watu wengi zaidi, nilikuwa kama myahudi kwa wayahudi ili niwapate wayahudi; kwa wale waliokuwa chini ya sheria nilikuwa kama chini ya sheria, ili niwapate waliochini ya sheria, kwa wale wasiokuwa na sheria nilkuwa kama sina sheria ili niwapate hao wsiokuwa na sheria, kwa wanyonge nilikuwa mnyonge ili niwapate wanyonge. Nimekuwa hali zote kwa watu wote, ili kwa njia zote”.

  Nilifikiri ili kuwapata waislamu basi tungeyapata mawazo yao, kwani tunaweza kwenda hata umasaini na kuwasikiliza dini zao za asili basi isingekuwa vigumu kwa waisalam.

  Yote ni amani, kwanu mungu ni mkubwa na pale apendapo yote huwezekana. Ila kwa kipindi hiki sitoandika mpaka muda ukifika na moderator akawa na mawazo kama yangu kwa ruksa yake ndio nitaandika kwani materials ninazomkononi tayari.

  AMANI, AMANI, AMANI!!!!

 236. Preach the Good news of Escaping from Hell and all penalty of sin, paid by shed blood of Jesus. Then teach them to do the thing Jesus told us to do, obedience to God will result into blessings (of course in work of your hands) plus persecution
  see here serially

  “Go ye therefore, and teach all nations, baptizing them in the name of the Father, and of the Son, and of the Holy Ghost: Teaching them to observe all things whatsoever I have commanded you: and, lo, I am with you alway, even unto the end of the world. Amen” (Mat 28:19 – 20)

  “And it shall come to pass, if thou shalt hearken diligently unto the voice of the LORD thy God, to observe and to do all his commandments which I command thee this day, that the LORD thy God will set thee on high above all nations of the earth: And all these blessings shall come on thee, and overtake thee, if thou shalt hearken unto the voice of the LORD thy God. Blessed shalt thou be in the city, and blessed shalt thou be in the field. Blessed shall be the fruit of thy body, and the fruit of thy ground, and the fruit of thy cattle, the increase of thy kine, and the flocks of thy sheep. Blessed shall be thy basket and thy store. Blessed shalt thou be when thou comest in, and blessed shalt thou be when thou goest out. ” (Deu 28:1 – 6)

  ” But it shall come to pass, if thou wilt not hearken unto the voice of the LORD thy God, to observe to do all his commandments and his statutes which I command thee this day; that all these curses shall come upon thee, and overtake thee: Cursed shalt thou be in the city, and cursed shalt thou be in the field. Cursed shall be thy basket and thy store. Cursed shall be the fruit of thy body, and the fruit of thy land, the increase of thy kine, and the flocks of thy sheep. Cursed shalt thou be when thou comest in, and cursed shalt thou be when thou goest out. The LORD shall send upon thee cursing, vexation, and rebuke, in all that thou settest thine hand unto for to do, until thou be destroyed, and until thou perish quickly; because of the wickedness of thy doings, whereby thou hast forsaken me. The LORD shall make the pestilence cleave unto thee, until he have consumed thee from off the land, whither thou goest to possess it. The LORD shall smite thee with a consumption, and with a fever, and with an inflammation, and with an extreme burning, and with the sword, and with blasting, and with mildew; and they shall pursue thee until thou perish. And thy heaven that is over thy head shall be brass, and the earth that is under thee shall be iron. The LORD shall make the rain of thy land powder and dust: from heaven shall it come down upon thee, until thou be destroyed. The LORD shall cause thee to be smitten before thine enemies: thou shalt go out one way against them, and flee seven ways before them: and shalt be removed into all the kingdoms of the earth” (Deu 28:15 – 25)

  Note: we have been grasped into Abrahamic covenants Through Isaac and Israel, so this applies to us Christians!

 237. nasikitika kuona kwamba watu wengi humu (mbali na wale ambao wanapinga kabisa)wanachukulia injili ya mafanikio kama ka-namna fulani hivi ka kuwavuta watu kwa Yesu tu halafu wakifika ndo wapate injili ya kweli(ambayo kwa mtazamo wa wengi ni ile ya parapanda italia siku chache zijazo hivo uwe safi!).sina matatizo na injili ya UTAKATIFU sababu ndio MAMA WA KILA KITU KATIKA IMANI HII.
  Ninachopinga hapa ni kuelezea mafanikio kama staili tu ya kuvutia watu makanisani(same as wengine wanavyotumia uimbaji kuwavutia watu mikutanoni). mafanikio ni halisi jameni!! kuna mifano mingi ya kibiblia ya watu waliofanikiwa sana na wakaendelea kuwa wacha Mungu sana pia. talk of David,Solomon,Job etc. afterall biblia inasema fedha na dhahabu ni mali ya Mungu so ni haki ya watoto wa Mungu. kinachofundishwa ni kanuni za kubarikiwa ki MUNGU na hapa ndipo pagumu hasa kwa wakristo wengi.
  Watumishi wengi pia hukosea sana kwa kufundisha upande mmoja tu wa misingi na kanuni za mafanikio wakisahau upande muhimu sana ambao ni mama wa kila kitu, UTAKATIFU! hapo ndo watu kama mimi hukimbia haraka sana kutoka kwa sababu hatuwezi kufundishana mafanikio january-december bila kufundishana na kufunguana katika msingi-mama wa kila sekunde moja ya maisha ya mkristo.
  Kuhusu matangazo ya makanisa napata utata kidogo. Kwa waliosema yako kibiashara huwa mnaona pia yanayotangaza uponyaji, kufunguliwa mapepo, laana, na vitu kama hivyo? Sijasikia mtu analalamikia hivi. Sababu kama hizi zilikuwa huduma za Yesu mniambie kwamba ujio wake ulikuwa maalum tu kwa sisi kwenda mbinguni pekee. (sijui mara mia alioambiwa Petro tutaipata lini na wapi!). kwa upande mmoja sioni shida sana coz hivi pia ni miongoni mwa vitu ambavyo Mungu anatumia hao watumishi kuwafanyia watu lakini kwa upande mwingine TUUTAFUTE KWANZA UFALME WA MUNGU NA HAKI YAKE NA MENGINE YOTE TUTAZIDISHIWA!
  Kuhusu wanaotoza pesa nionavyo mimi si ki-Mungu kabisa wala sina maneno ndefu hapa,IT’S NOT RIGHT!

  niko tayari kujifunza wapendwa, nirekebisheni nilipokosea.

  blesses

 238. Wahubiri kuhubiri utujiri au mafanikio ya mwilini ni la kibiblia kabisa,tukifahamu kuwa Yesu alimwaga damu yake mara 7 kwa sababu 7 ndipo tutajua kuwa kuhubiri utajiri siyo makosa
  YESU ALIMWAGA DAMU YAKE MARA 7 KWA
  SABABU 7

  TUKIO
  1.ALIPOTAIRWA

  2.WAKATI ANAOMBA
  JASHO LA DAMU LILITOKA

  3.ALIPOPIGWA MIJEREDI

  4.ALIPOCHOMWA MIKUKI
  UBAVUNI
  5.ALIPOVIKWA TAJI YA MIIBA
  KICHWANI DAMU ILITOKA
  6.ALIPOPIGILIWA MISUMARI
  MIKONONI
  7.ALIPOPIGILIWA MISUMARI
  MIGUUNI

 239. Shalom wapendwa!
  Ndugu Steve na ndugu John:
  1korintho 2:14;Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya roho wa Mungu maana kwake huyo ni upuuzi,wala hawezi kuyafahamu maana yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.
  Nadhani mnalielewa vizuri hili andiko,kwa maelezo yote mliyoyatoa kama bado yanaleta ugumu kwa mtu kuelewa,basi huo mstari unaweza kuconclude.Mungu awasaidie ktk kuweka muafaka juu ya hilo ili tuendelee na main topic tuliyopewa.Wote mbarikiwe na articles mlizotoa, tumejifunza mengi.
  Ni vizuri kuwekana sawa panapo onekana kuwa na tofauti,lkn tufike conlusion ya hizi subtopic na kuendeleza zaidi main topic ili tupate vitu vingi zaidi.
  Mungu awabariki.

 240. Asante ndugu Steve kwa kumfafanulia tena kile nilichomaanisha. Tatizo lao ni lile lile kwamba wanakata mistari na kuchukuwa sentesi moja ambayo kwa namna moja au nyingine yaweza kupotosha maana ya kilichokukusudiwa. Hata katika maelezo yake kwamba CONTEXT za kwenye Biblia hukamilishwa na mistari inayozunguka. Hii ndivyo uhalisia ulivyo. Hakuna HOTUBA AMBAYO HUKAMILISHWA KWA SENTESI MOJA tu. Hakuna somo lolote ambalo laweza kukamilika kwa sentesi moja tu. Lazima kuwe na mfululizo wa maelezo kwa ajili ya msomaji kuelewa kinachozungumziwa. Hii ndiyo sababu Biblia inaeleweka kwa urahisi. Mtu anayepinga mafundisho ya biblia kwa kusema ni kwa sababu hayaeleweki ni muongo!

  Lakini ninaomba yale maswali niliyomuuliza ndugu aliyetumia jina la Mjema Kaaya yajibiwe. Si lazima Mjema ajibu, yeyote aliye upande wake anaruhusiwa kujibu maana mjadala uko wazi. Mjema alisema ni maswali yaliyowazi kabisa kujibika. Lakini nashangaa ni muda mrefu sasa umepita hajafanya hivyo. Natumaini maswali hayo yakijibiwa, majibu mengine yanaweza kutupatia mwelekeo wa namna ya kujadili suala hili au kuliacha kabisa.

 241. Ndugu Achipete,
  katika kuhubiri, sisi tumetumwa kumhubiri Yesu, ila kwa habari ya fundisho la msingi LA IMANI YA KIKRISTO, utatu NI fundisho la msingi na MTU ANAYEPINGA UTATU SI MKRISTO. nadhani J. Paul alimaanisha kuwa sisi hatuhubiri utatu ila Yesu kwa kuwa dunia inamhitaji kama mwokozi wao. Hivyo hatuwezi kuwahubiria utatu wakati wao wanamwitaji Yesu. wakiisha kuja kwa Yesu, watajua mafundisho yake, si utatu pekee!

  Pia nashangaa unapenda ku-judge ukristo kwa jinsi WATU KAMA WEWE, wenye fahamu kama watu wengine na kutumia kama kinga yako. Hivi inaingia akilini kabisa mtu unamshitaki mahakamani kuwa amesema uongo, ilhali hujasikia na unajaribu kutafuta watu ambao watakusaidia, na wakati huo huo mtu anakuletea sauti iliyorekodiwa kipindi anaongea, wewe unaikataa na kung’ang’ania hao mashahidi wako? Lazima una matatizo. Nasema hivyo kwa sababu umejaribu kutumia dini mbalimbali na hujatumia Biblia. Ndugu unapoteza Muda wako, na as matter of fact uko close minded! Tuendelee…

  Nashangaa sana watu kuona imani ni kitu kigeni!! Unakaa ktk kiti kwa sababu unaamini hakitavunjika. Unapanda magari, meli na ndege sababu unaamini kuwa utafika, na unakuwa na sababu concrete za kuamini hivyo. Sasa kipi cha ajabu mtu kuamini imani inayoweza kuwa proved? Waislamu hawaruhusiwi Ku-Question Koran, Mormons lazima wakubaliane na Usemi wa “nabii toka Utah”, Mashahidi wa Yehova– Watch tower, wakatoliki — Pope nk…. lakini wakristo wana hiyari ya kutilia shaka chochote na kukichunguza na kama siyo kukiacha, sasa kuna imani gani ipo open minded zaidi ya ukristo?

  Ndugu, kwa sababu unasoma sana maandiko ya watu walioshindwa kujua utatu, ndio maana hautapata jibu milele, kama usipobadili mwenendo wako wa kutafuta supportive opinions. Mungu hajaleta hiyo confusion, na wewe na hao jamaa zako ndio mnaji-confuse wenyewe. Biblia iko crystal clear juu ya hilo na kama unataka jibu, tafuta ktk Biblia. Huwezi tafuta Jibu la DNA inavyofanya kazi kwa mwalimu wa kiswahili!

  Pia uliandika: Protestant publication yaelrza “The word Trinity is not fgound in the Bible… it did not find a place formally in the theology of the church till the 4th century”

  Huo ni upungufu wa uelewa na mbinu dhaifu! Ni sawa na kusema “There is no where in the christian scriptures written the world bible, so bible doesn’t exist”, au kusema, katika Biblia, hakuna sehemu iliyoandikwa Mungu aliumba Mamba, kwa hiyo Mungu hakuumba Mamba!
  Nakushauri uache kukopi na kupaste, maana sitapoteza muda wangu ku-prove kitu ambacho kiko plain clear, huu ni ubishi usio na faida. Aidha, fungua biblia, ambayo ina muda zaidi ya Karne ya nne, kama ukikosa fundisho la Mungu na nafsi zake tatu; ndipo uulize

  Hapa tena ukaandika:
  “The new Catholic Encyclopedia inatoa proof text hizo lakini vile vile inakubali “The doctorine of the Holy Trinity is not taught in the Old Testment.”

  Inaonekana wewe na huyo aliyeandika hayo hamsomi Biblia zenu, maana nashindwa kuelewa ni vipi hamuelewi! Kama mtu anaweza kuwa mwanazuoni ambaye anaandika encyclopedia, anshindwaje kuona hilo katika kitabu cha kwanza cha agano la kale?(rejea comment yangu juu)

  Kuhusu mfano wako mfu, wa Ibrahim Isaka na Yakobo, hivi ni wapi mmoja wao alisema yeye ni umoja na mwingine? Sioni sehemu Ibrahimu akisema: mimi na Isaka ni umoja, au wengine wote uliowataja, fikiria hilo!!

  Ukaandika:
  “Na hii ni kweli imejionyesha pahala pengi kama tunavyowezakuthibitisha kati ya ndugu Paul na Othodox”
  Inaonesha wewe ni mjanja wa kupanga maneno! Siajaona sehemu yoyote J. Paul (Na yeye atasema kama alimaanisha hivyo) akisema utatu si fundisho la msingi la IMANI YA KIKRISTO. Alichosema na kufafanua hapo juu ni kuwa alimaanisha sisi hatuhubiri utatu. Na kwa mkristo yeyote hilo li dhahiri. Yesu alitutuma tukahubiri injili yake: yaani msamaha wa dhambi kupitia kifo chake. Lakini kama biblia inasema Mungu ni utatu, utajiitaje mkristo na ilhali unapingana na Katiba ya Mkristo?

  Ndugu msomaji, huyu jamaa anaweza kueleza uongo! Isis Horus na Osiris si Miungu sawa! Isis ni mungu mke, Horus ni kuzuka kwa Osiris. Hii inahusiana vipi na utatu? Je hawa si miungu wawili– Horus akiwa ni kurudi kwa marehemu Osiris? Katika utatu kuna mungu mke? John Paul amepatia kusema kuwa huyu jamaa ni muislam, kwa kuwa waislamu waliamini wakristo wanaabudu miungu watatu: Baba, Yesu na Maria heeehe, kwa mkristo hicho ni kichekesho! Ndugu soma biblia ujipatie ukweli badala ya KUKOPY NA KUPASTE MAMBO HATA USIYOYAJUA. Usiokote chochote, ilmradi kinasema ukristo sio sahihi!

  SWALI KWAKO: MTUME GANI ALIYESEMA YEYE NA MUNGU NI UMOJA?

  Ukaandika: “Nikihitimisha makala hii napenda nieleweke kuwa pamoja na maelezo mengi niliyoyatoa na kunukuu wasomi mbali mbali, imani yangu si lazima ikubaliane na yale waliyoandika”

  KICHEKESHO KINGINE HIKI. Unapeleka mashahidi mahakamani ambao hata wewe huna imani nao? Hebu unataka kumaanisha nini hapa??

  Huhitaji kusema mitazamo ya dini zingine. Watoto wa arian wanafahamika. Mashahidi wa yehova, Watakatifu wa siku za mwisho, waislamu, unitarian na ndugu zao wote wanaamini Yesu si Mungu! Kwa nini, kwa sababu mwanzilishi wao ni mmoja na baba yao ni yuleyule

  Hii ni zawadi yako Ndugu Mziray, whhoooh sorry Achipete!
  ni maandiko miaka yapata 300 kabla ya Nicea:
  Matthew 28:19 Go ye therefore, and teach all nations, baptizing them in the name of the Father, and of the Son, and of the Holy Ghost:

  Na hii ni zawadi nyingine ya swali:
  Proverbs 30:4 Who hath ascended up into heaven, or descended? who hath gathered the wind in his fists? who hath bound the waters in a garment? who hath established all the ends of the earth? what is his name, and WHAT IS HIS SON’S NAME, if thou canst tell?

  Zawadi hii ni kwa ajili yako na wanazuoni wenzako wasiojua utatu uko ktk agano la kale: בראשית ברא אלהים את השמים ואת הארץ

 242. Ndg Achipete,

  Nafurahi kwamba tunakwenda pamoja. Lakini napenda nami niendelee kuchangia kuhusu mjadala huu. Ninajuwa wewe unachangia kutokana na imani yako ya Uislam na jinsi unavyoelewa wewe binafsi nami nachangia kutokana na imani yangu ya Kikristo, yaani kumwamini Yesu na ninayofahamu kutokana na Biblia. Natumaini lengo letu ni moja kwamba tufike mahali tupate muafaka kwamba upande upi uko sahihi kutokana na yale yaliyoandikwa katika Biblia, ambacho ndicho Kitabu kinachotumika kama Maandiko Matakatifu. Kwa hiyo kuelezea suala hili kutokana na imani tofauti na Ukristo lazima itakuwa ni tofauti na Ilivyoandikwa katika Biblia. Na mimi nafikiri lengo langu/letu ni KULIANGALIA SUALA HILI KUTOKANA NA MTAZAMO WA BIBLIA kwa sababu Biblia ina maeelezo ya kutosha pasipo kutegemea MAWAZO YA WANATHEOLOGIA na WANAZUONI ambao wengi wao HAWAMWAMINI YESU!

  Tuendelee………….

  Kuhusu suala la IMANI umeandika: HIVYO KUDHANI KWAMBA MLANGO WA FAHAMU WA IMANI NI MLANGO USIOFIKIKA MPAKA UOKOKE, HILO MIMI SILIAMINI NA WALA SIKUBALIANI NALO.

  Naona hapa ndugu hukusoma vizuri au hukuelewa nilivyoandika. Angalia nilivyoandika mahali fulani: MAMBO HAYA YAKIHUBIRIWA KWA PAMOJA , NA UDHIHIRISHO WA NGUVU ZA MUNGU KWA JINA LA YESU VINATOSHA KUMFANYA MTU AMWAMINI YESU. …Hivyo hapa inaonyesha wazi kwamba SIYO MAANA YAKE kwamba hadi mtu aokoke ndipo AUFIKIE MLANGO WA FAHAMU WA IMANI. Mtu ambaye hajaokoka anayo IMANI mbayo akiitumia inamwezesha AMWAMINI YESU.

  Umeonyesha kufurahia jinsi nilivyomalizia kwenye kipengere cha mwisho pale nilipoandika: ”Mafundisho ya habari ya UTATU siyo mafundisho ya msingi katika kuhubiri injili” Lakini ili kupata ujumbe ninaotaka kuufikisha kwa msomaji ni vema tukatambuwa MAFUNDISHO YA MSINGI NI YAPI. Niliendelea nikaandikwa kwamba: FUNDISHO LA MSINGI NI MTU KUMWAMINI NA KUMPOKEA YESU MOYONI. Huu ndio ujumbe ninaotaka msomaji aupate! Kuna mahali pegine niliandika kwamba MTU AKIISHA MPOKEA YESU MOYONI SUALA LA UTATU SIYO AJENDA kabisa.

  Baadaye hapo katikati ya maelezo yako umeandika mambo mengi uliyonukuu kutoka kwa wanazuoni na wanatheolojia. Mimi naamini BIBLIA INAJITOSHELEZA kama nilivyosema huko juu. Kwa hiyo sitegemei kupata uthibitisho wa imani yangu kutoka kwa mawazo ya watu hao. Nawe pia pale mwishoni umeandika vizuri kwamba pamoja na kunukuu kutoka kwao lakini imani yako si lazima ikubaliane na yale waliyoyaandika, bali uwezo wako wa kutumia akili na IMANI uliyonayo ndio vinajenga muhilimi wa uelewa wa mafundisho haya. Ni vizuri kwa kuwa unatambuwa IMANI uliyonayo inajenga muhimili wa uelewa juu ya jambo hili. Lakini naomba kukupa tahadhari kwamba KAMA IMANI YAKO IKO KINYUME NA KRISTO YESU, MUHIMILI UTAKAOJENGWA NA IMANI HIYO UTAKUWA PIA NI KINYUME NA MAFUNDISHO YA YESU. Na hivyo suala hili huwezi kulielewa kama ambavyo Yesu anataka lieleweke kwako kwa kuwa tayari una IMANI PINGAMIZI. Narudia tena kwamba KWA MTU MWENYE IMANI KATIKA KRISTO YESU suala hili wala si ajenda kwake, maana liko wazi kabisa. Hivyo ndugu unaweza kuona kwamba tatizo hapa ni MIHIMILI ILIYOJENGWA MIOYONI MWA WATU KUTOKANA NA IMANI ZAO ambazo ziko kinyume na imani katika Bwana Yesu! Lakini suala la UTATU lilivyo si tatizo! Kwa hiyo kinachosababisha suala la UTATU kuwa bado ni kitendawili, pamoja na kwako, ni kwa sababu ya IMANI ambazo watu wameweka katika mambo mengine na wala SI KATIKA YESU aliye mwokozi wa ULIMWENGU.

  Mahali fulani kwenye maelezo yako umenukuu toka kwa mtu uliyesema anaamini katika UTATU. Huyu pia namuweka katika wale ambao umewanukuu. Lakini Biblia inamajibu yote. Umesema tusome hadi Yohana 10:31-36. Lakini tusome hadi 38 na 39: Lakini nikizitenda, ijapokuwa hamniamini mimi, ziaminini zile kazi, mpate kujuwa ya kuwa Baba yu ndani yangu , nami ni ndani ya Baba; Wakatafuta tena kumkamata, lakini akatoka mikononi mwao. Hapa pia maandiko yanaeleza WAZI KWAMBA YESU YU NDANI YA MUNGU BABA na MUNGU BABA YU NDANI YA YESU! Hili halijabadilika!

  Umenukuu pia Yohana 5:18. Hapa umesema walitaka kumuua kwa sababu anajifanya Mungu. Baadaye ukatoa ufafanuzi wa waumini wenzako kwamba ”aliyesema anajifanya Mungu si Yesu”……. Mkanganyiko tupu! Sasa kama si Yesu kusema hivyo kwa nini walitaka kumuua? Yesu ndiye aliyesema Yeye na Mungu Baba ni kitu kimoja. Hili ndilo liliwakasirisha!
  Baadaye ukanukuu mstari kutoka Yohana 5:19 ambao naamini umeukata, hukuumalizia. The complete verse reads: Then answered Jesus and said unto them, Verily, verily, I say unto you, The Son can do nothing of himself, but what he seeth the
  Father do: for what things soever he doeth, these also doeth the Son likewise. Tukiumalizia tunaona jinsi Yesu alivyo na mamlaka ya kufanya yeye mwenyewe!

  Kisha umeandika kwamba mimi, John Paul, nimendika kama yale aliyoyafanya Yesu ALIYAFANYA KWA NGUVU ZAKE MWENYEWE. Kiisha ukawaonya watu kuachana na mafundisho ambayo yanataka kumpa Yesu uwezo ambao yeye hana na ameshaeleza. Lakini tukisoma Biblia tunapata ukweli wa hayo niliyoandika. Tukisoma Yohana 5:21 inasema; Maana kama Baba awafufuavyo wafu na kuwahuisha, vivyo hivyo na Mwana awahuisha wale awatakao. Ona maneno haya MWANA AWAHUISHA WALE AWATAKAO na wala si WALE BABA AWATAKAO. Bado hapa hujaona MAMLAKA YA YESU KRISTO?
  …Yohana 5:22 , Tena Baba hamhukumu mtu yeyote; bali amampa Mwana hukumu yote. ….Haya nayo ni maneno ya Yesu!

  Labda kwa uchache tuangalie maandiko ya Biblia yanayoeleza mamlaka aliyonayo Yesu Kristo:
  1. Kusamehe dhambi – Marko 2:10
  2. Kufufua watu siku ya kiama – Yohana 6:39-40
  3. Kuukoa Ulimwengu – Yohana 12:47.

  Mwisho
  Hata kama moderator atakuruhusu, kuandika juu ya Dini nyingine zinavyofahamu kuhusu UTATU haina maana yoyote. Maana Dini hizo zina mitazamo tofauti na IMANI KATIKA YESU. Na wala katika Dini hizo hakuna UZIMA. Bali UZIMA UKO KWA YESU KRISTO!

  ….Amani!

 243. Kwanza kabisa ningependa kutoa shukurani zangu za dhati kwa wote waliochangia mada hii na hasa kwa ndugu John Paul. Majibu ya ndugu J. Paul ya tarehe 22/12 juu ya UTATU yametoa ufafanuzi wa kina sana, na nimeonelea nichangie kwa jinsi nilivyomuelewa.

  Katika maelezo yake yote nimefurahishwa sana na kipengele cha mwisho pale alipoandika “Mafundisho ya habari za UTATU siyo mafundisho ya msingi katika kuhubiri injili”. Kwa sababu wakatoliki katika -The catholic Encyclopedia wameandika “The Trinity is the term employed to signify the central doctine of the Christian religion”. Wa- Othodox wameenda mbali zaidi katika kitabu Our Othodox Christian faith wameandika ” The fundamental doctrine of christianity,” hata wakaeleza ” CHRISTIANS ARE THOSE WHO ACCEPT CHRIST AS GOD”. Na kusisitiza kuwa ” God is triune… The Father is TOTALLY God. The Son is TOTALLY God. The Holy Spirit is TOTALLY God. Hivyo habari za ndugu Paul zinaniweka katika matumaini maoya.

  Kabla sijaendelea mbele ningependa kulizungumzia hili suala la IMANI. Hata kama muumini wa kikristo haamini katika UTATU, bado imani ni msingi mkubwa wa kuilewa Biblia. Ni sawa wasemao DINI NI IMANI. Na ili kuufikia huo mlango wa fahamu wa imani ni lazima upitie katika baadhi ya milango mikuu ya fahamu uliyoieleza, yaani ama umesikia, umesoma n.k. Hivyo kudhani kwamba mlango wa fahamu wa IMANI ni mlango usiofikika mpaka uokoke, hilo mimi siliamini na sikubaliani nalo.

  Tukirudi katika somo kuu la UTATU, The Encyclopedia America The doctrine of Trinity is considered to be “beyond the grasp of human reason”. Kardinali John O’Connor anaeleza “We know that it is a very profound mystery, which we don’t bigin to understand” zingatia ni miaka zaidi ya 2000 toka Yesu atoe mahubiri hayo. Na Pope John Paul II alieleza “the inscrutable mystery of God. Na katika kamusi ya elimu ya dini imeandikwa ” Precisely what that doctrine is, or rather precisely how it is to be explained, Trinitarians era agree among themselves”. Na hii ni kweli imejionyesha pahala pengi kama tunavyowezakuthibitisha kati ya ndugu Paul na Othodox.

  Mungu si wa kujichanganya, sasa mafundisho haya ya kujichanganya yametoka wapi? 1 corithians 14:33 “God is not a God of confusion”. Hivi Mungu angeweza kutoa mafundisho yanayochanganya juu ya yeye mwenyewe ambayo hata wasomi wa kihebrew, wakigiriki na walatino wakashindwa kumueleza katika mada hii? Hapana! hapa kuna walakini. Na zaidi ya hayo yahitajiwa waumini wawe wanathiolojia ili “to know the only true God and Jesus Christ who he sent” John 17:3. Isitoshe wasomi wa kidini wa kiyahudi walimtambua Yesu kama messiah.

  Protestant publication yaelrza “The word Trinity is not fgound in the Bible… it did not find a place formally in the theology of the church till the 4th century” na mamlaka ya kikatoliki inaeleza Trinity “is not .. directly and immediately (the) word of God.” Katika The Encyclopedia of religion inakubali “Theologians today are in agreement that the hebrew Bible does not contain adoctrine of the Trinity” hali kathalika katika New catholic Encyclopedia, New International Dictionary of new Testment theology,Origin of and evolution of religion. Kwa hiyo hakuna uwazi wa moja kwa moja wa mafundisho ya UTATU katika vitabu vyote 39 vya Biblia ambavyo vinafanya true cannon of inspired Hebrew Skriptures.

  Karne nyingi kabla ya kuja kristo, kulikuwa na imani ya UTATU wa miungu wa zamani katika Babylon na Assyria. Encyclopedia ya kifaransa ” Larousse Encyclopedia of Mythology” inaelezea UTATU katika Mesopotamia. ” The universe was divided into three regions each each of which became the domain of a god. Anu’s share was the sky. The earth was given to Enlil. Ea became the ruler of the waters. Together they constituted the triad of the Great Gods.” Angalia kwamfano Matendo 20:29, 30, JB. 2Peter 2:1; John 4:1-3, jude 3, 4. Mwana historia Will Durant aliandika ” Christianity did not destroy paganism; it adopted it… From Egypt came the idear of a divine Trinity.” Edward Gibbon’s history ameandika “if paganism was conguered by Christianity, it is equally true that Christianity was corrupted by Paganism”. Maelezo hayo hupatikana kayika vitabu vingi vingie kama Encyclopedia of religion and ethics, The paganism in our Christianity, Adolf Hannack katika Outlines of History of Dogma. n.k. Hebu tuangalie UTATU ulivyokuwepo kabla na baada ya Yesu. Egypt- Triad of Horus, OSIRIS, ISIS, 2nd mellenium B.C.E (kabla ya kuja Yesu), Babylon- Triad of Ishtar, Sin, Shamash, 2nd mellsnium B.C.E. Palmyra- Triad of moon god, Lord of heavens. Sun god c. 1st century C.E. iNDIA Triune Hindu, godhead, c 7TH CENTURY c.e. fRANCE Trinity, c 14th century C.E. Norway- Trinity (Father, Son, holy spirit, c. 13th century C.E. Hapa unaweza kupata fununu juu ya UTATU ulivyojipenyeza katika ukristo.

  BULET PROOF TEXTS kwa wanaoamini UTATU, hueleza kuwa Biblia imeeleza wazi juu ya UTATU na kutumia baadhi ya mistari katika biblia. Lakini hata hiyo mistari ukiisoma mistari hiyo utakuta kwamba si Biblia wala wanahistoria waunga mkono UTATU. kILA MSTARI ULIOTOLEWA KAMA BULET PROOF KATIKA utatu ni lazima ueleweke katika CONTEXT yake. Mara nyingi ukweli au CONTEXT ya maelezo hayo hukamilishwa na mistari iliyoizunguka, hivyo ni muhimu kusoma mistari kabla na baada yake.

  The new Catholic Encyclopedia inatoa proof text hizo lakini vile vile inakubali “The doctorine of the Holy Trinity is not taught in the Old Testment. Katika agano jipya kuna 2 cor13:13 ( mstari wa 14 kwa baadhi ya biblia) na 1cor 12.4-6, Mt 28.19. Katika Cor 13.13(14) ” the grace of the Lord Jesus Christ, the love of God and and the fellowship of the Holy Spirit be with you all” 1Cor 12:4-6 ” There many different gifts, but it is always the same spirit; there are different ways of saving, but it is always the same Lord. There are many different forms of activities, but in everybody it is the same God who is at work in them all. Mt 28:19 “Go therefore, make disciples of nations; baptise them in the name of the Father and of the Son and of the Holy Spirit”. Hivi hiyo mistari inaeleza kuwa Mungu, Kristo na ROHO MTAKATIFU wanafanya UTATU wa Godhead. Kuwa hawa watatu ni sawa katika maumbile, nguvu na umilele? Hapana hazionyeshi hivyo, bali yametajwa majina matatu kama vile Achipete, Paul na Ashery. Kama ilivyoandikwa katika MaClintock and strong’s Cycxlopedia of biblical, theological and Ecclesiastical literature “ptroves only that there are the three subjects named,.. but it does not prove, by itself that all the three belong necessarily to the divine nature and possess equal divine honor”

  Abraham, Isaak, na Jacob wametajwa pamoja mara nyingi tu lakini hii haiwafanyi wao kuwa mmoja. Halikadhalika Peter, James, na John wametajwa pamoja naye haiwafanyi wao kuwa mmoja. Sehemu nyingine iliyotajwa ni 1 John 5:7. Wasomi wameielezea sehemu hii kuwa iliongezwa baadaye. Hata baadhi ya Biblia nyingine za sasa hivi hukiondoa kipengele hicho. Proof text nyingine zaelezea kati ya Mungu na Yesu. John 10:30 ” I and the Father are one” Hapa hakuna mtu wa tatu aliyetajwa, hivyo hauwezi kuwa UTATU pengine UWILI. John 17:21, 22, “may all be one, just as you, Father, are in union with me and i am in union with you, that they also may be in union with us,… that they may be one just as we are one” Yesu alimaanisha kuwa yeye ni mwili mmoja na Mungu? Hapana hapa yaonyesha wazi kuwa alimaanisha kuwa wamoja katika mawazo, lengo kama ambavyoi yeye na Mungu walivokuwa. Angalia vile vile 1 Cor 3:6, 8 Paulo anasema” “I planted , Apollos watered,… He that plants and he that waters are one” Paul hamaanishi kuwa yeye na Apollo ni watu wawili katika mmoja. Anamaanisha kuwa waliungana kwa malengo.

  John Calvin ambaye ni muumini wa UTATU anaandika katika kitabu Commentary on the gospel According to John “The ancients made a wrong use of this passage to prove that Christ is .. of the same essence with the Father. For Christ does not argue about the unity of substance, but about the agreement which he has with the Father”. Katika cotext ya John 10:30 Yesu alikuwa akiwajibu wayahudi kuwa maneno yake hayakumaanisha kuwa yeye ni Mungu. Endelea John 10:31-36 ” Why do you charge me with blasphemy because i, consecrated and sent into the world by the Father, said, ‘i am God’s Son?” No Jesus claim that he was, not God the Son, but the Son of God.

  John 5:18 Wayahudi walitaka kumuuwa Yesu kwa sababu ” he was also calling God his own Fateher, making himself equal to God”. Waumini wenzangu hapa lazima tuwe waangalifu na kujiuliza hivi ni nani aliyesema kuwa Yesu anajifanya Mungu. Sio YESU. Hapa alikuwa anajidefend kutokana na false charge kama inavyojieleza katika mstari wa 19″To this accusition Jesus replied… ‘the Son can do nothing by himself; he can do only what he sees the Father doing.'”-JB. Na hivi ndivyo ilivyokuwa kwa mitume yote, Mungu hutoa amri nao wanatekeleza au wanaufikisha ujumbe huo kwa wanakondoo. Wala hakuna cha kushangaza katika maelezo haya.

  Aidha nisiwachoshe wasomaji, kwani kuna sehemu muhimu inayoeleza juu ya Mfalme Constantine wa Nicaea alivyowakusanya maaskofu 300 na kufikiwa makubaliano juu ya mafundisho ya UTATU katika 325 C.E. Hatua hii ilichukuliwa kutokana na ubishani mkali kati ya wale wasioamini UTATU na wale wanaoamini utatu. Hii ilidhoofisha utawala wake. Wengine waliotumia vyeo vyao kukuza UTATU ni Plato miaka yapata 400 kabla ya kristo.

  Ndugu Paul ameandika au kuuliza kuwa ni mtume gani aliyefanya kama alivyofanya Yesu. Maelezo haya hayana mantiki kwa sababu sote tunaamini kuwa Mungu ana uwezo wa kufanya lolote lile. Na yesu alishaeleza kuwa yote anenaye yanatoka kwa Mungu na yeye hawezi kufanya lolote ila yale Mungu amtumayo. Hivyo maneno ya Ndugu Paul yanataka kuonyesjha kama yale aliyoyafanya Yesu ALIYAFANYA KWA NGUVU ZAKE MWENYEWE. Mafundisho haya ni lazima tuachane naye kwani yanamakusudi ya kumpa yesu uwezo ambao hana na yeye mwenyewe kashaeleza.

  Nikihitimisha makala hii napenda nieleweke kuwa pamoja na maelezo mengi niliyoyatoa na kunukuu wasomi mbali mbali, imani yangu si lazima ikubaliane na yale waliyoandika, bali uwezo wangu wa kutumia akili na imani niliyonayo ndio vinavyojenga muhimili wa ueleo wa mafundisho haya. Hivyo elimu ya utatu bado ni kitendawili.

  Ikiwa moderator ataniruhusu, safari ijayo nilipenda kuandika juu ya Dini nyingine zinavyoufahamu UTATU. Mimi niko open minded na husoma mtazamo toka pande tofauti, na mara hii kwa ruhusa ya moderator nilipenda kuandika mtazamo wa UTATU katika uislam.

  Asanteni

 244. Ndugu Mjema,

  Suala la MODERATION liko kwa waendesha blog hii. Na ninaamini ni haki yao. Kutokana kutembelea blog mbali mbali, blog isiyo na MODERATION huwa ni vurugu tupu. Ni vigumu kwa watu kujifunza maana mijadala huwa haina mtiriko na watu hurukia mada zingine badala ya kwenda mada moja baada ya nyingine. Sauala la nanmna hii likiruhusiwa hapa HATA MIMI SIKO TAYARI KUINGIA KWENYE MJADALA AMBAO HAUNA MTIRIRIKO. Napenda kujifunza na ninaamini NJIA SAHIHI YA KUFANYA HIVYO NI KAMA TULIVYOPEWA MWONGOZO KWAMBA NI AJENDA BAADA YA AJENDA.

  Nakumbuka katika mjadala wa Biblia kuchafuliwa au Kutokuchafuliwa Strictly Gospel walitoa mwongozo kwamba ili kuwa na mtiririko wenye kuleta maana ni vema tukawa tunajadili ajenda moja baaya nyingine. Yawezekana ni kwa sababu hii barua zingine zinaondolewa; kwa sababu zinakuwa haziko kwenye mwendelezo wa mjadala ulioko.

  Mimi naamini mjadala huu uko wazi kwa watu wote. Lakini pia nafikiri ni vema mtu anayechangia achangie kwenye mada inayoendelea. Mimi natumaini hilo ndilo litatupatia kujifunza kikamilifu.

  Mungu ndiye shahidi wa yote haya na ndiye atakayetulipa!

 245. Bwana Yesu Asifiwe ndugu Mjema! Mijadala hii lazima awepo moderator! ili kuwaepuka wale wenye lengo la kupachafua mahala hapa, kwa maneno yao ambayo hayaujengi mwili wa Kristo!

  NI kweli tunanyofoa na kufuta kabisa baadhi ya comments kutoka kwenu hii ni baada ya kugundua mko kundi au ni mtu mmoja anatumia majina tofauti ya kikristo kwa lengo la kuuchafua Ukristo.

  Wakristo ni watu wa amani hatupendi MAJIBIZANO yasiyokuwa na mwisho ambayo yatachochea UGOMVI au MASHINDANO. Badilisheni majina mtakavyo lakini kuweni ni watu wa kuheshimu amani na mwendelezo wa mahala hapa! pia kuweni na ustaarabu kwa baadhi ya lugha mnazotumia! Tungependa kufundishana kwa upendo na wala sio kwa kulazimishana!

  Mungu wetu Yesu Kristo awabariki!

 246. John Paul na wakristo wengine.

  John Paul umeleta masuala mengi ambayo yako wazi kabisa kujibika. Ningalipenda mjadala huu ukawa uko wazi bila kuwepo moderation kwani ikiwa nyinyi ni wakweli majibu yangu yaingie moja kwa moja bila unyofoaji au kufutwa kabisa. Huu ndio uadilifu.
  Mimi hapa sishindani bali nataka kuwaonyesha kweli ya Mungu katika biblia. Malipo yangu yako kwa mwenyewe Mungu.
  Hata mahakamani unapopeleka mashitaka yako . Hakimu anakuwa anasikiliza pande zote. Mimi pia ningalipenda watu wengine wachangie ili sote tupate faida na sio kuzinyofoa barua au kuzitia kapuni barua nyengine.

  JEE MUKO TAYARI KUWACHA MODERATION BARUA ZIINGIE????

  MUNGU NDIYE SHAHIDI WA YOTE HAYA NA NDIYE ATAYETULIPA:

 247. Ndugu Mjema, karibu sana katika mjadala huu ambao unafanyika kwa uhuru na amani. Ninakupa pole tu kwa sababu hata wewe pia umeingia kwenye mkumbo wa KUKOPI na kuja KUPESTI hapa. Lakini nakushauri kwamba ungekaa chini ukaruhusu AKILI YAKO ifikirie kidogo maana tunayoyaandika hapa ni mambo ya msingi kabisa ambayo kila mtu aliyeweka AKILI YAKE katika mazingira ya kuufahamu UKWELI anaweza kuelewa kwa urahisi kabisa. Lakini sielewi una uhuru kiasi gani wa kutumia akili yako.

  Tuendelee….

  Inavyoonekana ni KAMA UNAIAMINI BIBLIA lakini nashangaa kwamba inakuwaje mtu anayeamini Biblia achukuwe kifungu kimoja halafu kingine akipinge. Tutakwenda pole pole tukipitia mistari michache uliyoinukuu. LAKINI NAOMBA KUKUULIZA SWALI AMBALO KAMA UKILIJIBU ITAKUWA VIZURI. Swali liko hivi: JE, NI KWELI UNAIAMINI BIBLIA? Kama jibu lako ni NDIO, basi niliyoandika hapa yatakuwa na msaada kwako lakini kama jibu ni HAPANA yote niliyoandika hapa yataishia machoni tu pasipokufika kwenye AKILI kwa ajili ya kuyachambuwa na kuyaelewa kwa ajili ya KUONGOKA.
  Nimeandika kwa kirefu kidogo, hii inatokana na hoja yako. Lakini natumaini utaisoma taratibu ili uweze kupata kile nilichokusudia.
  Naomba Mungu NEEMA YAKE iwe juu yako unaposoma yafuatayo:

  1. Naanza kwa kunukuu jinsi ulivyoanza:

  ”Katika Injili ya Yohana tunasoma:

  Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma. Mimi nimekutukuza duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye.
  Yohana 17.3-4

  Kwa unyenyekevu wa safi ya niya Yesu anamkhatibu Mola wake, “Mungu wa pekee wa kweli”, siye mungu wa uwongo miongoni wa miungu ya uwongo uwongo iliyokuwa ikiabudiwa na makafiri.” ……Mwisho wa kunukuu!

  Kwa hiyo ndugu Mjema, kwa kunukuu kutoka katiika kitabu cha Injili kama Ilivyoandikwa na Yohana, maana yake UNAKUBALIANA NA KILA KILICHOANDIKWA KATIKA KITABU HIKI.

  Wewe umenukuu Yohana 17: 3-4. Lakini kwa upendo kabisa, hebu tuendelee hadi mstari wa 5. Mstari huu wa tano unasema hivi:

  ”Na sasa Baba, unitukukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya Ulimwengu kuwako”

  Ndugu Mjema, natumaini akili yako inaweza kufahamu wazi wazi yaliyoandikwa katika mstari huu. Lakini pia yawezekana KOSA LAKO ni KUKOPI pasipo hata kuisoma Biblia yenyewe. Mstari huu wa 5 unasema KABLA YA ULIMWENGU KUWAKO YESU ALIKUWA NA UTUKUFU TAYARI. Yaani kabla Mungu hajaziumba Mbingu na nchi! Sasa hebu ruhusu akili yako ifikirie majibu ya maswali haya hapa, halafu utaleta majibu hapa:

  a. Kuna mtume gani aliyekuwa na utukufu kabla ulimwengu haujakuwako? Je, huyu atakuwa ni binaadamu wa kawaida?
  b. Ni binaadamu gani aliyekuwa na utukufu kabla ya ulimwengu kuwako? Je, huyu atakuwa ni binaadamu wa kawaida?
  c. Ni nabii gani aliyekuwa na utukufu kabla ya ulimwengu kuwako? Je, huyu atakuwa ni binaadamu wa kawaida?
  d. Je, yawezekana binaadamu wa kawaida kuwa na kumbukumbu ya mambo aliyokuwa nayo kabla hajazaliwa katika ulimwengu huu?

  2. Matendo 3:26 Mungu, akiisha kumfufua mtumishi wake Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza, ili kuwabarikia kwa kumwepusha kila mmoja wenu na maovu yake.
  Swali kutokana na mstari huu:
  Je, kwa kuwa umetumia mstari huu UNAAMINI SASA KWAMBA YESU ALIFUFUKA KUTOKA KWA WAFU KAMA YANVYOSEMA MAANDIKO? [Nahitaji jibu tafadhali]

  3. Umetuumia pia maandiko kutoka Matendo 3:13. Lakini hebu mara hii tena tuendelee na mstari wa 14-16;
  14: Bali ninyi mlimkana yule Mtakatifu, yule Mwenye haki, mkataka mpewe mwuaji;
  15: Mkamwua yule Mkuu wa uzima, ambaye Mungu amemfufua katika wafu, na sisi tu mashahidi wake.
  16: Na kwa imani katika jina lake, jina lake limemtia nguvu mtu huyu mnayemwona na kumjua, na imani ile iliyo kwake yeye imempatia huyu uzima huu mkamilifu mbele yenu yote;

  Maswali:
  a. Nabii aliye binaadamu aweza kuwa Mkuu wa uzima?
  c. Kwa kuwa Petro na Yohana ni mashahidi wa kufufuka kwa Yesu, Je, sasa unaamini kwamba kweli Yesu alifufuka?
  d. Kwa kuwa imeandikwa ‘jina lake limemtia nguvu mtu huyu mnayemwona…’ unaamini sasa kwamba jina la Yesu lina Uweza?
  e. Umeandika hivi; ”Jina la Yesu huenda likatumiwa, lakini ni kama chombo tu, wasila, mwombezi,. . . .” Homework: Kama anayeponya ni Mungu na jina la Yesu ‘huenda’ likatumiwa tu HEBU JARIBU KUTOA MAPEPO/MAJINI KWA JINA LA YESU, hivyo hivyo ulivyo, [maana unasema wewe ni mcha Mungu] halafu KITAKACHOTOKEA uje utueleze hapa!

  f. Katika Matendo 4:13 imeandikwa: Basi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kuwajua ya kuwa ni watu wasio na elimu, wasio na maarifa, wakastaajabu, wakawatambuwa ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu; Je, Unaamini sasa kwamba KATIKA MAMBO YA ROHONI AKILI HII YA KAWAIDA HAINA NAFASI? [ Hebu angalia jinsi wenzako walivyokosa neno la kusema baada ya muujiza huu katika Matendo 4:14: Na wakimwona yule aliyeponywa akisimama pamoja nao hawakuwa na neno la kujibu]
  ……lakini pamoja na KUKOSA NENO la kusema BADO WALITAKA KUWANYAMAZISHA PETRO NA YOHANA WASIFUNDISHE TENA KWA JINA LA YESU.
  ……Hawa walikuwa wameona moja ya matendo makuu yanayotendeka kwa jina la Yesu, lakini bado walifanya fitina. Sasa ndugu Mjema, sina uhakika kama umeshawahi kuhudhuria hata mara moja tu kwenye Mkutano wa Injili wenye uwepo wa Mungu [au kwenye kanisa ambalo linahubiri wokovu] ili ukaone mambo ambayo Yesu anayafanya hata sasa!. Hebu jaribu hata mara moja tu kuhudhuria kwenye mkutano wa Injili/Kanisani. Ninaamini wewe utakapoona imani inaweza kujengeka ndani yako na kukufanya ujiponye nafsi yako kwa kumwamini huyu Yesu Kristo!

  USHAHIDI HUU WA KUFUFUKA KWA YESU UNABATILISHA MAFUNDISHO YOTE ULIYONAYO YANAYOKANA KUFUFUKA KWA YESU!

  Katika mstari wa 17: Basi sasa ndugu,[Mjema] najuwa ya kuwa mliyatenda haya kwa kutokujua kwenu, [kukopi na kupesti] kama na wakuu wenu walivyotenda [kuandika mafundisho hayo ya uongo]. 18: Lakini mambo yale aliyoyahubiri Mungu tangu zamani kwa kinywa cha manabii wake wote ya kwamba Kristo wake atateswa, ametimiza hivyo.
  19: Tubuni [tubu] basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana.

  Unaona hapa maandiko yasemavyo kwamba MTU AKIMWAMINI YESU NA KUTUBU DHAMBI ZAKE HUFUTWA na nyakati za kuburudishwa huja. Lakini hebu kumbuka jinsi ambavyo mnadanganyana kwamba DHAMBI ITAPIMWA KAMA KWA MIZANI.

  Swali: Je, unaweza kuamini sasa kwamba DHAMBI ZITAPIMWA KWA MIZANI ni mafundisho ya UONGO?

  4. Umetumia Matendo 4: 29-30. Hebu tuendelee na ule msatri wa 31:

  Hata walipokwisha kumwomba Mungu mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena Neno la Mungu kwa ujasiri.

  Swali: Je unakubali sasa kwamba Roho Mtakatifu SIYO Muhammad kama Mnavyofundishwa? [Kwa sababu wakati huu Muhammad alikuwa hata hajadhaniwa angekuwepo]

  5. Umetumia Yohana 7:28-29. Lakini tukisoma katika Yohana 6:53-54 inasema:

  Basi Yesu akawaambia, Amin, amini, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake hamna uzima ndani yenu. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.

  Maswali:
  a. Unaamini sasa kwamba DAMU YA YESU ndiyo iletayo WOKOVU kwa ajili ya uzima wa milele?
  b. Ni nabii gani mwenye uwezo wa KUFUFUA MTU yeyote siku ya mwisho?
  c. Kama Yesu hakufufuka anawezaje kufufua watu siku ya mwisho, kama naye anasubiri kufufuka siku hiyo?

  6. Umetumia Marko 9:37
  Mtu akimpokea mtoto mmoja wa namna hii kwa jina langu, anipokea mimi: na mtu akinipokea mimi, humpokea, si mimi, bali yeye aliyenituma.

  Hebu pata tafsiri hii rahisi na halisi…..

  Mtu akimpokea Yesu anampokea si yeye, bali aliyemtuma. Maana yake Mtu akimpokea Yesu anakuwa amempokea Mungu. Yaani mtu akimwamini Yesu huyo anamwamini Mungu. Kwa hiyo KUMWAMINI YESU NDIKO KUMWAMINI MUNGU!….tuko pamoja?

  7. Umetumia Yohana 4:34 Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake.

  Swali: Unayajuwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu kumtuma Yesu ulimwenguni? Kama unayafahamu yaorodheshe hapa.

  …hebu tuone katika Yohana 4:42
  Wakamwambia Yule mwanamke, Sasa tunaamini, wala si kwa sababu ya maneno yako tu, maana sisi tumesikia wenyewe, tena twajuwa ya kuwa hakika huyu ndiye Mwokozi wa Ulimwengu.

  Swali: Je, nawe pia waamini kwamba Yesu Kristo ndiye Mwokozi wa Ulimwengu?

  8. Umetumia Yohana 7:16-18 isemayo ”Mafunzo yangu si yangu mimi, ila ni yake yeye aliyenipeleka. Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo, kwamba yatoka kwa Mungu, au kwamba mimi nanena kwa nafsi yangu tu. Yeye anenaye kwa nafsi yake tu hutafuta utukufu wake mwenyewe; bali anayetafuta utukufu wake aliyempeleka, huyo ni wa kweli, wala ndani yake hamna udhalimu”

  Swali: Kama unaamini Yesu ndiye wa kweli , kwa nini usiamini kila Neno lililonenwa Juu Yake na yote aliyoyasema?

  9. Umetumia Yohana 6:14; Basi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya, walisema, Hakika huyu ni nabii yule ajaye ulimwenguni.
  …lakini tukiendelea hadi mstari wa 15 inasema Kisha Yesu, hali akitambuwa ya kuwa walitaka kuja kumshika ili wamfanye mfalme, akajitenga, akaenda zake mlimami yeye peke yake.

  Swali: Ni nabii gani, kwa manabii unaowafahamu, ambaye watu WALITAKA KUMFANYA MFALME KWA KUMLAZIMISHA?

  …..hebu tusome pia katika Yohana 6:39-40
  Na mapenzi yake aliyenipeleka ni haya, ya kwamba katika wote alionipa nisimpoteze hata mmoja, bali nimfufue siku ya mwisho. Kwa kuwa mapenzi ya Baba yangu ni haya, ya kwamba kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, awe na uzima wa milele, nami nitamfufua siku ya mwisho.

  Ndugu Mjema, hebu tazama JINSI ULIVYOPOTOKA SANA ULIPOTAFSIRI MAANA YA UISLAMU kwa kutaka kutafsiri Yohana 4:34. Wewe uliandika hivi:
  ”Haya khasa ndio maana ya neno Uislamu. Uislamu ni kujisalimisha nafsi yako kwenye mapenzi ya Mwenyezi Mungu, kutenda apendavyo Mola wako Mlezi”

  …lakini TUMEONA WAZI JINSI YESU ALIVYOSEMA KUHUSU MAPENZI YA MUNGU: Kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, yaani Yesu, awe na uzima wa milele, na Yesu mwenyewe atamfufua siku ya mwisho.?

  Swali:
  a.Je, Uislamu unafundisha kwamba Mapenzi ya Mwenyezi Mungu ni kumwamini na kumtazama Yesu?
  b. Je, Uislam unafundisha kwamba Yesu ndiye atakayewafufufua watu siku ya mwisho?
  c. Kama ana uwezo mkubwa MAMLAKA KUBWA HIVI, bado tulazimishe akili zetu kwamba YESU NI NABII tu, basi?
  d. KAMA UISLAMU HAUFUNDISHI HIVI JUU YA YESU KWA NINI TUSIKUBALIANE KWAMBA MUNGU ANAYEFUNDISHWA NA UISLAMU SI MUNGU WA YESU KRISTO?

  10. Umetumia Mathayo 21:46 Nao walipotafuta kumkamata, waliwaogopa makutano, kwa maana wao walimwona kuwa nabii.
  …Hapa hakuna cha kukusaidia maana kama vile WALIVOKUWA WANAMWONA KUWA NI NABII, ndivyo hivyo nawe pia, pamoja na maandiko yote yahayohusu Ukuu na Uungu wa Yesu, BADO UNAMWONA KUWA NI NABII tu.

  11. Umetumia Mathayo 21:10-11.
  Mstari wa 9 unasema ” Na makuhani waliotangulia , na wale waliofuata, wakapaza sauti wakisema Hosana, Mwana wa Daudi, ndiye Mbarikiwa, yeye ajaye kwa jina la Bwana; Hosana juu mbinguni.”

  Swali: Je, unaamini kwamba Yesu ni Mwana wa Daudi?

  12. Kwa kuwa una amini maneno aliyoyasema Yesu katika Marko 10:18; Yesu akamwambia, Kwa nini kuniita mwema? hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu.. . .

  Swali: Je, Unayaamini maneno ambayo pia ni Yesu aliyasema katika Marko 10:11-12 Akawaambia Kila mtu amwachaye mkewe na muoa mwingine azine juu yake na mke akimwacha mumewe na kuolewa na mtu mwingine, azini?

  Mukhtasari wa yote tuliyokwisha yazungumza, ni kuwa tumepata uthibitisho wa kutosha kutokana na Biblia kuwa Yesu wa Nazareti ni mwanaadamu, Nabii wa Mungu, na Mtume wake. Hapo ndipo ulipoishia wewe. Sasa hebu tuongeze mengine ambayo tumepata uthibitisho kutoka Biblia. . . .Yesu ni Mwokozi wa Ulimwengu, Aliyekuja kutimiza Mapenzi ya Mungu, ambayo ni Kila amwaniniye Yesu yuna uzima wa Milele, Mwenye mamlaka ya Kuwafufua watu siku ya mwisho, Kristo nk.

  Je, ni nabii au mtuma gani mwenye CV ya namna hii?

  HITIMISHO

  Yesu Kristo ana vyeo vyote vya kitakatifu, vyovyote ambavyo vinaweza kutumika kwa mtu aliyetoka Mbinguni kuja Kuokoa wanaadamu… ALIPITIA UTUMISHI WOTE HUO NA HATIMAYE AKARUDI MBINGUNI ALIKOTOKA BAADA YA KUKAMILISHA KAZI NA MWISHO ATARUDI KUWAHUKUMU WANAADAMU KUTOKANA NA IMANI YAO KWAKE KAMA WALIMWAMINI AU LA! Kwa hiyo mtu huyu LAZIMA, LAZIMA AWE NI ZAIDI YA NABII. Ukimwita Nabii ni sawa. Lakini si hilo tu…., ukimwita ni Mtume ni sawa, lakini si mwisho, Ukimwita ni mwanandamu sawa, lakini kuna zaidi, ukimwita ni Mwana wa Adamu ni sawa…lakini kuna zaidi, ukimwita ni mwana wa Mungu, ni sawa tu…lakini kuna zaidi, na tena na tena na tena!

  NAHITAJI MAJIBU YA MASWALI YOTE NILIYOYAANDIKA HAPA. NAAMINI KWAMBA KOMENTI YAKO INAYOFUATA ITAKUWA NI KWA AJILI YA KUJIBU MASWALI HAYA, NA WALA SI KULETA HOJA TOFAUTI, ILI TUWEZE KWENDA PAMOJA, KWA MTIRIRIKO UNAOWEZA KUTUSAIDIA KADRI TUNAVYOENDELEA NA MJADALA HUU.

  …..Amani!

 248. Katika Injili ya Yohana tunasoma:

  Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma. Mimi nimekutukuza duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye.
  Yohana 17.3-4

  Kwa unyenyekevu wa safi ya niya Yesu anamkhatibu Mola wake, “Mungu wa pekee wa kweli”, siye mungu wa uwongo miongoni wa miungu ya uwongo uwongo iliyokuwa ikiabudiwa na makafiri. Ajuulikane Mwenyezi Mungu na kadhaalika ajuulikane yeye Yesu Kristo, Mtume na mtumishi wa Mwenyezi Mungu. Katika kitabu cha Matendo ya Mitume kiliomo katika Agano Jipya la Biblia tunasoma:

  Mungu, akiisha kumfufua mtumishi wake Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza, ili kuwabarikia kwa kumwepusha kila mmoja wenu na maovu yake.
  Matendo 3.26

  Mungu wa Ibrahimu na wa Isaka na wa Yakobo, Mungu wa baba zetu, amemtukuza mtumishi wake Yesu, ambaye ninyi mlimsaliti na kumkana mbele ya Pilato, alipokuwa ametoa hukumu yake afunguliwe.
  Matendo 3.13

  Basi sasa, Bwana, yaangalie matisho yao; ukawajalie watumwa wako kunena neno lako kwa ujasiri wote, ukinyosha mkono wako kuponya; ishara na maajabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako mtakatifu Yesu.
  Matendo 4.29-30

  Wagonjwa wanaponyeshwa, ishara zinaonyeshwa, na maajabu yanatendeka. Nani afanyae yote haya? Ni kudra na uwezo wa Mwenyezi Mungu. Jina la Yesu huenda likatumiwa, lakini ni kama chombo tu, wasila, mwombezi, kwani kama atavyokuwa yeye ni “mtumishi mtakatifu wa Mungu.” Katika Matendo 3.26 na 3.13 hapo juu Paulo aliwaandikia Mayahudi ambao walimkataa mtumishi wa Mungu, Yesu Kristo, alipowajia na utumishi kutoka kwa Mungu wa babu zao Mayahudi, Mungu wa Ibrahimu na wa Isaka na Yakobo. Mwenyezi Mungu ni yule yule mmoja, Mitume ni mbali mbali, lakini utumishi wao ni mmoja. Mayahudi wakawakubali wote waliotangulia wakamkataa Yesu. Mwenyewe Yesu anawasimanga Mayahudi kama inavyotueleza Injili ya Yohana:

  Mimi mnanijua, na huko nitokako mnakujua; wala sikuja kwa nafsi yangu; ila yeye aliyenipeleka ni wa kweli, msiyemjua ninyi. Mimi namjua, kwa kuwa nimetoka kwake, naye ndiye aliyenituma.
  Yohana 7.28-29

  Katika Injili ya Marko Yesu anasimuliwa alimchukua mtoto akasema:

  Mtu akimpokea mtoto mmoja wa namna hii kwa jina langu, anipokea mimi: na mtu akinipokea mimi, humpokea, si mimi, bali yeye aliyenituma.
  Marko 9.37

  Kama hayo aliambiwa Mtume Muhammad s.a.w. na Mwenyezi Mungu katika Qur’ani:

  Sema: Ikiwa ninyi mnampenda Mwenyezi Mungu, basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakusameheni madhambi yenu, kwani Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
  (Qur’ani) Al Imran 3.31

  Yesu amesema:

  Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake.
  Yohana 4.34

  Haya khasa ndio maana ya neno Uislamu. Uislamu ni kujisalimisha nafsi yako kwenye mapenzi ya Mwenyezi Mungu, kutenda apendavyo Mola wako Mlezi. Na hicho ndicho chakula chake Yesu, kama asemavyo, yaani kama anavyohitaji kula kila siku ili aishi, kama wanavyohitaji wanaadamu wote, basi hali kadhaalika kuwa daima anajisalimu mbele ya matakwa ya Mwenyezi Mungu aliyemtuma duniani kuwa ni Mtume. Tena Yesu amesema:

  Mafunzo yangu si yangu mimi, ila ni yake yeye aliyenipeleka. Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo, kwamba yatoka kwa Mungu, au kwamba mimi nanena kwa nafsi yangu tu. Yeye anenaye kwa nafsi yake tu hutafuta utukufu wake mwenyewe; bali anayetafuta utukufu wake aliyempeleka, huyo ni wa kweli, wala ndani yake hamna udhalimu.
  Yohana 7.16-18

  Tunaona basi kwa ushahidi wake mwenyewe Yesu kuwa fakhari yake ni kunyenyekea kwa Mwenyezi Mungu wake aliyemuumba na akamtuma kwa Wana wa Israili waliopotea kama kondoo. Kwa uthibitisho wake mwenyewe yeye ni mtumishi wa haki aliyepewa Unabii na kufanywa Mtume. Hataki utukufu wake yeye, bali utukufu wa Mungu wake aliyemtuma na kumpeleka awaongoe watu wafwate njia iliyo nyooka. Katika Injili ya Mathayo anazidi kufafanua nini wadhifa wake na nini cheo chake mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya wanaadamu wenziwe. Alipowateua wanafunzi wake kumi na mbili kuwapeleka kuwahubiria Mayahudi alisema:

  Awapokeaye ninyi, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi, ampokea yeye aliyenituma. Ampokeaye nabii kwa kuwa ni nabii, atapata thawabu ya nabii; naye ampokeaye mwenye haki kwa kuwa ni mwenye haki, atapata thawabu ya mwenye haki.
  Mathayo 10.40-41

  Yeye mwenyewe Yesu amesema kuwa yeye ni Mtume, yeye ni Mtumishi, yeye ni Nabii. Je, nini mawazo ya wale wafwasi wake waliomuamini na wakamwona na wakaishi naye? Injili zinatwambia:

  Basi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya, walisema, Hakika huyu ni nabii yule ajaye ulimwenguni.
  Yohana 6.14

  Nao walipotafuta kumkamata, waliwaogopa makutano, kwa maana wao walimwona kuwa nabii.
  Mathayo 21.46

  Hata alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakisema, Ni nani huyu? Makutano wakasema, Huyu ni yule nabii, Yesu, wa Nazareti ya Galilaya.
  Mathayo 21.10-11

  Na tazama, siku ile ile watu wawili miongoni mwao walikuwa wakienda kijiji kimoja, jina lake Emau, kilichokuwa mbali na Yerusalemu kama mwendo wa saa mbili. Nao walikuwa wakizungumza wao kwa wao habari za mambo hayo yote yaliyotukia. Ikawa katika kuzungumza na kuulizana kwao, Yesu mwenyewe alikaribia, akaandamana nao. Macho yao yakafumbwa wasimtambue. Akawaambia, ni Maneno gani haya mnayosemezana hivi mnapotembea? Wakasimama wamekunja nyuso zao. Akajibu mmoja wao, jina lake Kleopa, akamwambia, Je! wewe peke yako u mgeni katika Yerusalemu, hata huyajui yaliyotukia humo siku hizi? Akawauliza, Mambo gani? Wakamwambia, Mambo ya Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii, mwenye uwezo katika kutenda mbele za Mungu na watu wote.
  Luka 24.13-19

  Injili kwa umoja wao zinathibitisha kuwa watu wake Yesu waliokuwa naye na kumuamini na wakaona miujiza yake tangu kuzaliwa kwake mpaka mwisho wake walimjua kuwa ni Nabii wa haki, naye ni mtu, mwanaadamu.
  “Hakika huyu ni nabii”, anasema Yohana.
  “waliwona kuwa nabii”, anasema Mathayo.
  “Huyu ni yule nabii, Yesu”, anasema tena Mathayo.
  “Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii”, anasema Luka.
  Jinsi ya hadhari zake asisingiziwe kuwa anazo au anadai sifa za ungu, Yesu alikataa hata kuitwa “Mwalimu mwema”. Sikiliza masimulizi ya Injili ya Marko:

  Hata alipokuwa akitoka kwenda njiani, mtu mmoja akaja mbio, akampigia magoti, akmwuuliza, Mwalimu mwema, nifanye nini nipate kuurithi uzima wa milele? Yesu akamwambia, Kwa nini kuniita mwema? hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu.
  Marko 10.17-18

  Tafsiri kubwa kabisa ya Biblia iitwayo The Interpreter’s Bible inasema kuwa kauli hiyo ya Yesu, yaani: “Kwa nini kuniiita mwema? hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu”, imewatatiza wataalamu wa thiolojia (ilimu ya Ungu) ya Kikristo wa baadaye. Wameona taabu kuambatisha maneno haya yalio wazi na imani yao kuwa Yesu ni mungu, na hali hapo dhaahiri yake ni kuwa anakataa ungu. Kwa hivyo basi kujitoa kimasomaso ikaandikwa katika Injili ya Mathayo (ambayo iliandikwa baada ya Marko) kwa njia nyengine. Ilivyoandikwa katika Mathayo ni hivi:

  Na tazama, mtu mmoja akamwendea akamwambia, Mwalimu, nitende jambo gani jema, ili nipate uzima wa milele? Akamwambia, Kwani kuniuliza habari ya wema? Aliye mwema ni mmoja.
  Mathayo 19.16-17

  Kila imani ilipozidi kugeuka maandiko mapya yaliandikwa na kunasibishiwa Yesu. Kitabu hicho The Interpreter’s Bible kinaikataa tafsiri ya kusema kuwa makusudio ya Yesu yalikuwa ni kusema: Kama unanita mwema, basi unakusudia kuwa mimi ni Mungu. Hayo siyo. Aliyokusudia Yesu kusema ni kuwa :Sifai kupewa sifa za Mungu.
  Mtaalamu wa Biblia wa Kitaliana, Marcello Craveri, ameandika katika kitabu chake The Life of Jesus (Maisha ya Yesu):

  “Yesu kwa mara moja alimpa somo zuri kabisa la unyenyekevu, ambalo juu ya mengineyo, ni ushahidi ulio wazi ya kwamba hakupata kabisa kujiona mwenyewe ni sawa na Mungu: Kwa nini kuniita mwema? Hakuna mwema ila mmoja, ndiye Mungu.”

  Mukhtasari wa yote tuliyokwisha yazungumza, ni kuwa tumepata uthibitisho wa kutosha kutokana na Biblia kuwa Yesu wa Nazareti ni mwanaadamu, Nabii wa Mungu, na Mtume wake.
  Jee, Mtume huyo katumwa kwa nani?

 249. Asherialiandika:
  Kitu kingine ndugu Mgumba umesema Mungu ambaye ni Yehova huitwa pia Allah. Naomba niseme hivi, kama anamaanisha Allah ambaye ni Mungu wa waislamu, basi huyo siyo YEHOVA.

  Hellow, Allah siyo Mungu wa Biblia wala sio cheo
  Kwa Kiarabu Mungu ni Illah. Kwa hiyo Illah wa wakristo ni Yehova na Illah wa waislamu ni Allah

 250. Shalomu!!

  Nimeangalia hoja nyingi zinazotolewa na hawa ndugu zetu ambao ni wapinzani wa neno la Mungu na kuona kuwa nami nitoe mchango wangu mdogo:-

  Kama mtu anaisoma Biblia kwa nia ya kuipotosha, ataendelea kufanya hivyo mpaka pale atakapopata neema na kuamua kuacha kufanya hivyo. Hawa ndugu wanaleta hoja nyingi ambazo kimsingi si hoja za kibiblia ila ni mawazo yao ya kumpinga Mungu wakiyatafutia maandiko. Nasema wanampinga Mungu kwa sababu wanamkataa Yesu ambaye ni Mungu.

  Utashangaa mtu anachukua kipande cha mstari wakati katika sura hiyo hiyo aliyochukua hicho kipande kuna majibu yote aliyoyauliza. Wakati mwingine ndani ya sura hiyo hiyo kuna mambo mengine mengi tu ambayo hayakubali na anayapinga. Hivyo ndivyo ilivyo kazi ya shetani, yaani mpinga Kristo. Huwezi kusema juu ya Biblia kama wewe unampinga Yesu Kristo, maana Biblia imemjaa Mungu Baba, imemjaa Yesu ikielezea juu ya Uungu wake, imejaa Roho Mtakatifu ikielezea na Uungu wake.

  Nitatoa mifano wa mistari michache aliyoitaja ndugu Mgumba.

  Matendo 4: (amechukua msitari wa 27). Ndani ya sura hii kuna mambo mengi sana ambayo yeye kama muislamu hayaamini mfano kufa na kufufuka kwakwe Yesu Kristo, Roho Mtakatifu, Mungu Baba, Jina la Yesu kuwa ndilo Jina la pekee walilopewa wanadamu lisapalo kuokolewa kwalo. Je haya wanayaamini? maana huwezi kuchukua mstari wa 27 ndani ya sura hii ukauamini kama mengine ndani ya sura hii ya 4 huyaamini. Nawauliza hayo mengine wanayaamini? Wakiamini hayo mengine, basi utaona sura ya 4 ina majibu yote.

  Matendo 3: (amechukua mstari wa 13), ndani ya sura hiyo kuna maelezo ya kina juu ya Yesu Kristo (Kufa na Kufufuka kwke), swali ni je haya mengine anayaamini? Anaamini na kukubali kuwa Yesu Kristo alikufa na kufufuka kwa ajili ya dhambi za wanadamu ikiwemo dhambi zake? Yuko tayari kutubu dhambi zake ili apate ondoleo la dhambi?

  Ufunuo 1: (amechukua mstari wa 1-2), ndani ya sura hiyo kuna habari za Roho Mtakatifu, Yesu ni wa Milele, kufa na kufufuka kwa Yesu, Kuja kwa YESU mara ya pili, Yesu ni wa kwanza na wa mwisho na mengine mengi tu ya ajabu. Je hayo mengine yota anayakubali?

  Yohana 17 (amechukua mstari wa 3), ndani ya sura ya 17 ya kitabu cha Yohana kuna mambo ya ajabu sana ambayo Yesu Kristo aliyasema. Mstari wa 5 Yesu anasema hivi, (Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako), sijui kama huu mstari aliuona na sijui kama ameuelewa? naomba ajaribu kuusoma tena na autafakari kuona ni nini Yesu anakisema katika mstari huu. Mstari wa 21 Yesu anasema (kama wewe Baba ulivyo ndani yangu nami ndani yako) na mstari wa 22 anasema (nami utukufu ule ulionipa nimewapa ili wawe na umoja kama sisi tulivyo UMOJA). Hapa Yesu anasema kama sisi (yaani Yeye Yesu na Baba walivyo UMOJA), angalia hajasema kama walivyo na umoja, anasema wao ni umoja. Hivi ndugu yangu Mgumba na wengine wote, HAYA MNAYAAMINI? ama hamuyaelewi?

  Luka 24: (amechukua mstari wa 19), ndani ya sura hii ya 24 kumezungumzwa mengi kuhusu Yesu kuteswa, kufa na kufufuka (mstari wa 26), kupaa kwakwe na mengine mengi sana, JE HAYA MENGINE WANAYAKUBALI NA KUYAAMINI?

  Marko 13: (amechukua msitari wa 31) lakini katika sura hiyo Yesu alisema juu ya kuja kwake mara ya pili katika mawingu, jee hilo wanalikubali?

  Kama nilivyosema hapo awali, Biblia haijawahi kujipinga na wala haina kitu chochote ambacho kina makosa. Biblia ni neno la Mungu na ina uwezo wa kuyabadili maisha ya mwanadamu, kutoka kuwa mwenye dhambi hadi kuwa mtakatifu, mtu anayeenda mbinguni. Lingekuwa jambo la maana sana kama wangekubali tuwafundishe sisi tunaoijua Biblia. Lakini kwa kuwa nia zao ni kupinga, ndiyo maana utaona wanachukua kipande huku sura nzima ina majibu ya yote wanayoyasema. (PAMOJA NA UPINZANI WAO, NAWAHAKIKISHIA KUWA MUNGU ANAWAPENDA NA AANAWATAKA WATUBU NA KUMWAMINI YESU, LAKINI WASIPOTUBU BASI IPO SIKU WATAKUTANA NA YESU AKIWA KWENYE KITI CHA ENZI NA NDIPO WATAHUKUMIWA KWENDA JEHANAMU YA MILELE, HILI HAWATAKWEPA WASIKUBALI KUTUBU LEO)

  Kitu kingine ndugu Mgumba umesema Mungu ambaye ni Yehova huitwa pia Allah. Naomba niseme hivi, kama anamaanisha Allah ambaye ni Mungu wa waislamu, basi huyo siyo YEHOVA.

  Mungu (YEHOVA) ambaye yupo ndani ya Biblia hawezi kuwa ndiye yule wa waislamu. Nasema hivyo kwasababu huyu YEHOVA alimtuma mwanae Yesu Kristo kuja kuokoa ulimwengu, ambapo Yesu akiwa Mungu alikufa Msalabani na siku ya tatu akafufuka na baadae akapaa kwenda mbinguni. Baada ya hapo akamtoa Mungu Roho Mtakatifu, aje ulimwenguni ili awe na watakatifu hata ukamilifu wa nyakati.

  huyo wa waislamu hana sifa hizi nilizozitaja hapo juu.

  Mungu wetu ni mwenye rehema, si mwingi wa hasira na ni mwenye upendo. Anawapenda hata wale wanaompinga kama hawa ndugu ndiyo maana pamoja na kusema vibaya bado anawahurumia. Angekuwa yule mwingine, ni upanga, marungu, mabomu, kujitoa mhanga n.k.

  NAWASIHI NDUGU ZANGU KWA HURUMA ZAKE YESU KUWA MKUBALI KUWA YESU NI BWANA, MWOKOZI WA ULIMWENGU NA KUWA BIBLIA NI NENO TAKATIFU LA MUNGU. KUBALINI KUYATOA MAISHA YENU KWA YESU KRISTO ILI MUOKOLEWE. HAKIKA MTAKUWA VIUMBE VIPYA, NANYI MTAUONA MWEMA WA MUNGU NA UTUKUFU WAKE, AIDHA MTAIKIMBIA HUKUMU YA MILELE

  ONJENI MUONE YA KUWA BWANA YU MWEMA.

  Shalomu

 251. Mjema,
  Yesu haimaanishi Mungu alikuwa mtu, kabisa hilo haliwezekani, Mungu hawezi kuwa mtu na mtu hawezi kuwa Mungu. Mungu aliongeza utu (alivaa mwili) katika uungu wake. Si kuwa Mungu alijishusha akawa Binadamu la hasha, bali Katika uungu wake aliongeza ubinadamu

  Ubarikiwe

 252. Ndugu adamu, Ni vema umesema kwa sehemu, kuwa Yesu alitumwa na Baba, na kuwa alivaa Ubinadamu. Excellent! Lakini Yesu huyo huyo alisema Yeyeni Mungu. Kwa maelezo yako inawezekana kabisa ukawa au Msabato au Shahidi wa yehova. Ok anyway, kwa jinsi utakavyokuwa majibu haya yanatoka katika Biblia, karibu!!

  MWANZO NA MWISHO?
  “Who hath wrought and done it, calling the generations from the beginning? I the LORD, the first, and with the last; I am he” Isaiah 41:4
  Nani anasema hapa kuwa ni Mwanzo na Mwisho? ni Yehova, Mungu wa agano la kale! Sasa angalia mistari hii kutoka ufunuo 1 :

  ” 5And from Jesus Christ, who is the faithful witness, and the first begotten of the dead, and the prince of the kings of the earth. Unto him that loved us, and washed us from our sins in his own blood,

  6And hath made us kings and priests unto God and his Father; to him be glory and dominion for ever and ever. Amen.

  7Behold, he cometh with clouds; and every eye shall see him, and they also which pierced him: and all kindreds of the earth shall wail because of him. Even so, Amen.

  8I am Alpha and Omega, the beginning and the ending, saith the Lord, which is, and which was, and which is to come, the Almighty”

  Nani hapa mwanzo na mwisho? Yesu Kristo! Wow Yesu Kristo ni Mwanzo na Mwisho!

  MUNGU?

  ” And of the angels he saith, Who maketh his angels spirits, and his ministers a flame of fire. But unto the Son he saith, Thy throne, O God, is for ever and ever: a sceptre of righteousness is the sceptre of thy kingdom” Hebrewa 1:7-8

  Simple Mungu Baba anamwita Yesu hapa Mungu, kwa sababu Yesu ni Mungu. Maadamu Mungu hajipingi na yeye amesema Utukufu wake hatampa mwingine, kwa hiyo amemwita Yesu ni Mungu maana Alikuwa kwa Mungu naye alikuwa ni Mungu

  Mbarikiwe

 253. Ndugu Adamu Mgumba,

  Umesema kweli kabisa Jambo ambalo Bwana Yesu hakulilteta lazima litakuwa silo. Kwani Mwenyezi Mungu si mwenye kuwaletea binaadamu Matatizo. Ni sawa kabisa.

  Je, ikiwa suala hili tunalozungumzia hapa lililetwa na Yesu Mwenyewe utakuwa tayari kulikubali? Na ninafurahi kwa sababu unaiamini Biblia.

  Kwa ufupi ni hivi: Suala ya Uungu wa Yesu lililetwa na Yesu mweyewe. Hata alipolileta kwa Wayahudi, wao pia hawakuwa tayari kukubali. Na walitaka hata kumpiga mawe. Lakini ni heri kwako kwa sababu unatambuwa kwamba Yesu lichokileta ndicho sahihi.

  …Tusome maneno haya:

  John 10:27-33 My sheep hear my voice, and I know them, and they follow me: And I give unto them eternal life; and they shall never perish, neither shall any man pluck them out of my hand. My Father, which gave them me, is greater than all; and no man is able to pluck them out of my Father’s hand. I and my Father are one. Then the Jews took up stones again to stone him. Jesus answered them, Many good works have I shewed you from my Father; for which of those works do ye stone me? The Jews answered him, saying, For a good work we stone thee not; but for blasphemy; and because that thou, being a man, makest thyself God.

  Natumaaini umesoma vizuri hapo juu na kuelewa. Angali mstari wa mwisho hapo juu kwamba WAYAHUDI WALITAKA KUMPIGA MAWE BWANA YESU KWA SABABU WALISEMA YEYE ALIYE BINAADAMU ANAJIFANYA NI MUNGU.

  Kwa hiyo tunaona wazi kwamba tatizo hili liko tangu wakati wa Uhai wa Yesu. Kwa hiyo zaidi ya miaka 2000 baadaye haishangazi kuwepo watu ambao wana mawazo sawa na Wayahudi wa wakati wa Uhai wa Yesu. Maana Yesu ni Yeye Yule Jana, Leo na hata milele! Yesu hajabadilika, na upinzani uliopo kwake haujabadilika. Na kazi yake ya kuokoa watu haijabadilika. Watu waliokoka wakati wake na hata sasa wanaendelea kuokoka. Watu walimpinga wakati wa uwepo wake na hata sasa wanaendelea kumpinga. Na kumkataa Yesu maana yake ni kupotea!

  Kwa kuwa tumeona kuwa suala la Uungu wa Yesu lililetwa na Yesu mwenyewe uko tayari kukubali kwamba jambo hilo ndilo?

 254. Mimi nauliza jee ikiwa Yesu alikuja kama mtoto wa kawaida hadi katoto kakawa mtu mzima. Wakati wote akila chakula na kuishi maisha ya kawaida kama binaadamu wengine.
  Mimi kwa ninavyoona Mungu atakuwa na sifa zake za kiungu na Binaadamu atakuwa na sifa zake za kibinaadamu . Kwa akili ya binaadamu Mungu kuwa mtu kitu hicho hakiwezekani.

 255. Mpendwa Amin Nguluma

  Sijui kama maelezo yangu haya hayatonyofolewa ili kulinda ugali.

  Lakini kinachonishangaza ni kipi kinachoogopwa hata barua yangu ikawa haikuwekwa. Mimi nafikiri ni hofu ya watu kuujua ukweli. Mwenyezi Mungu haogopewi. Watu wanafikiri kwa kunyofoa barua za wengine ndio ukweli hautojulikana lakini huwezi kushindana na nguvu ya Mwenyezi Mungu.

  Ndugu uraisi ni cheo , si jina . Amiri jeshi Mkuu ni cheo si jina . Mwenyekiti wa CCM ni cheo si jina. Kikwete ni jina la mtu.

  Tuje kwa Yesu , hili ni jina si cheo. Hata watu hii leo wako wengi wanaitwa Yesu kwa vile ni jina. Mungu ana jina lake kama alivyokuwa akiitwa na Wayahudi naye ni Ellah au kama wanavyomwita Jehovah witness Jehovah. Waarabu humwita Allah.
  Hakuna binadamu anayejiita jina la Mungu au Jehovah au Elohim au Allah

  Jee unataka kutwambia Bwana Yesu ikiwa alikufa msalabani kwa siku tatu ulimwengu ulikuwa ukiendeshwa na nani. Kwani Kikwete akifariki hii leo basi vyeo vyake vitachukuliwa na mtu mwengine kwa haraka kabla uchaguzi.
  Tafuta mfano mwengine kwanini Bwana Yesu Mwenyewe ashindwe kujieleza unakuja kutueleza wewe au kupewa mifano na binadamu wengine. Ndugu Jambo ambao Bwana Yesu hakulileta lazima litakuwa silo. Kwani Mwenyezi Mungu si mwenye kuwaletea binadamu Matatizo

 256. Kwa wote ambao wana mashaka na UTATU wa Mungu wa wakristo naomba watafakari maelezo haya na watafute majibu yatawasaidia kwani yale yaliyo ndani ya Biblia yameshindwa kuwafaidia na kuwaelea.
  RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA AMIRI JESHI MKUU WA MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA NA MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI NDUGU JAKAYA MRISHO KIKWETE. Hawa ni watu wangapi,inakuwaje na je ikitokea wakatakiwa wote mahali pamoja wataenda wangapi?. Je hili haliwezekani.
  Mtakapopata majibu enyi msioelewa na maandiko basi jueni kuwa hamtaweza kujua UUNGU WA BABA NA MWANA NA ROHO MTAKATIFU.
  Mimi nadhani Mungu awabariki sana

 257. UTATU MTAKATIFU

  Ndugu Achipete

  1.Matamshi ya Yesu mwenyewe kuhusu Uungu wake. Anasemaje?

  2.Wanafunzi wa kwanza wa Bwana Yesu walimfahamu kwamba ni Mungu au vipi?

  3.Maaskofu waliofuata baada ya wanafunzi wa kwanza tangu Karne ya kwanza hadi karne ya tatu je? Walifundisha vipi kuhusu Yesu.

  4.Imani ya utatu ilivyoanza hadi kuwa fundisho kamili na kanuni ya Wakristo Duniani pote.

  Yesu anasemaje?:
  Yohana 17:3 imeandikwa hivi – …uzima wa milele ndiyo huu wakujue Mungu wa pekee na Yesu uliyemtuma.
  Katika Aya hii Yesu anasema kwamba ili kupata uzima lazima tumjue kwanza Mungu wa pekee na umjue Yesu Kristo aliyetumwa na Mungu, hapa Yesu hasemi lolote kuhusu yeye kuwa nafasi ya pili ya Mungu ila anakiri wazi yeye ametumwa na Mungu mmoja wa pekee.

  Luka 2:40 imeandikwa hivi: – …Yule mtoto akakua akaongezeka nguvu amejaa hekima na neema ya Mungu ilikua juu yake.

  Katika Aya hii tunaambiwa kwamba Yesu alijaa hekima na neema ya Mungu. Tahadhari ufikirie vizuri kwa makini sababu hapa inayonyesha kwamba bila ya Mungu kumpa neema Yesu asingelikuwa na hekima hii inaonyesha wazi Yesu ni kiumbe aliyeteuliwa na Mungu na hii ni kawaida yake Mwenyezi Mungu kwa Mitume na Manabii wake kuwapa neema na hekima.

  Yohana 13:13 imeandikwa hivi: – Nanyi mwaniita Mwalimu na Bwana nanyi mwasema vema maana ndivyo nilivyo. Maneno hayo yatueleza wazi kwamba alikuwa anajua wazi kwamba yeye ni Mwalimu na Bwana ndiyo maana anawasifu wanafunzi wake, NANYI MWASEMA VEMA.

  Mathayo 23:9 imeandikwa: – Wala msimwite mtu Baba maana Baba yenu ni mmoja wa Mbinguni wala msiitwe Kiongozi maana Kiongozi wenu ni mmoja naye ndiye Yesu Kristo. Hapa Yesu anaendelea kutuonyesha jinsi alivyo tofauti na Mungu, na yeye hayuko sawa na Mungu daima Mungu ni Baba lakini Yesu ni Kiongozi tu.

  Ufunuo: 1:1-2 imeandikwa hivi: – Ufunuo wa Yesu Kristo aliopewa na Mungu awaonyeshe watu wake…Naye akatuma Malaika akamuonyeshe Mtumwa wake Yohana…
  Wakati ufunuo unatolewa na Mungu na kupewa Yesu wakati huo Yesu ameshatoka Duniani yuko Mbinguni, lakini bado inaonyesha Mungu ndiye mkubwa Yesu bado ni wakutumwa ili awaonyeshe watumwa kuhusu mambo yao yatakayokuja kama tulivyosoma. Zipo Aya nyingi sana zinazoonyesha wazi kuwa Yesu alikuwa halijui kabisa fundisho la tatu.

  Wanafunzi wa kwanza walimuelewaje Yesu?
  Matendo ya Mitume 3:13 imeandikwa hivi… Mungu wa Ibrahimu na wa Isaka na wa Yakobo, Mungu wa Baba zetu amemtukuza Mtumishi wake Yesu ambaye nyinyi mlimsaliti na kumkana mbele ya Pilato, alipokuwa ametoa hukumu yake ili afunguliwe.

  Maneno ya wanafunzi yalikuwa wazi kuwa Yesu ni Mtumishi wa Mungu tu yaani Mtume pia ni Nabii.

  Matendo ya Mitume 4:27 imeandikwa hivi… maana ni kweli Herode na Pontio Pilato pamoja na Mataifa na watu wa Israel walikusanyika katika mji huu juu ya Mtumishi wako Mtakatifu Yesu uliyemtia mafuta.

  Wanafunzi wanaendelea na msimamo wao kwamba Yesu ni Mtumishi wa Mungu aliyetumwa (Mtume) tu.

  Luka 24:19 imeandikwa: – …Akawauliza mambo gani? Wakamwambia mambo ya Yesu Wanazareti aliyekuwa mtu nabii mwenye uwezo wa kutenda na kusema mbele za Mungu na Wanadamu.

  Marko 6:2 imeandikwa: – Na ilipokuwa Sabato aliingia katika Sinagogi, wengi waliposikia walishangaa wakasema huyu ameyapata wapi haya! Hekima gani hii? Aliyopewa huyu? Nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake? Huyu si ni yule Selemala mwana wa Mariamu na nduguyao Yakobo na Yosef na Yuda na Simoni na Maumbu wake hawapo hapa? (Maana ya Maumbu ni Madada)

  Maneno haya yanathibitisha kwamba watu waliomfahamu Yesu walishangaa matendo makubwa anayoyatenda hata hivyo walijua kwamba yeye ni Selemala wa Mwana wa Mariamu tu. Na ni kiumbe mwenye ndugu zake na dada zake, kama watu wengine.

  Marko 13:31 tunasoma hivi – Mbingu na Nchi zitapita lakini maneno yangu hayatapita kamwe. Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna anaye ijua hata malaika wala Mwana (Yesu) ila Baba tu Mungu… hapa Yesu alikua anazungumza habari ya siku ya mwisho alikiri wazi kwamba yeye siku haijui hata Malaika hawajui ila Mungu peke yake.

  Uungu wa Yesu ulianza hivi: –
  Justin Martyr: Alimtaja Yesu kwamba hakuwa Binadamu alikua Malaika aliyeumba… Yesu alikua na cheo kidogo kuliko Mungu… Justin aliuwawa mjini Rome mwaka 165 A.D. kwa kukatwa kichwa.

  Irenayo. Alifundisha kwamba Mungu ni mmoja wa pekee hakuna tena mwingine wa kulingana naye…Yesu aliumbwa kama Malaika hayuko sawa na Mungu. Ilikuwa mwaka 200 A.D.

  Naye Clement, wa Alexandaria. Alifundisha kwamba Mungu ni mmoja tu wa kweli asiyeumbwa na hawezi kuangamia Yesu ni wa pili lakini hayuko sawa na Mungu. Clement alikufa mwaka 215 AD.

  Askofu Mkuu Tertuliano: Alifundisha kwamba Mungu ni mkubwa kuliko vyote. anayetumwa ni mdogo kwa yule anayemtuma. Yesu alitumwa na Mungu alifundisha hivyo mwaka 230 AD.

  Askofu Hippolytus. Alifundisha kwamba Mungu ni mmoja wa pekee, Muumba wa vyote hakuna tena kilichomtangulia. Na Yesu aliumbwa na Mungu. Askofu Hippolytus inasemakana alikufa mwaka 235 AD. Kwa kuvutwa huku na huku na kuchanika vipande viwili. Wauwaji walitumia farasi kumfuta muanga huyu.

  Naye Askofu Origen. Alifundisha kwamba Baba Mwana ni asili mbili tofauti ukilinganisha na Baba Mwana Yesu anayo nuru ndogo sana mbele za Baba aliishi kati ya mwaka 185-254 AD.

  Ndugu msomaji baada ya kumsikiliza Yesu katika Injili yake katika Aya nilizotoa hatukuona Neno linalosema yeye ni Mungu hata kidokezo kidogo hakuna.

  Baadaye tumewasikia wanafunzi wake wa kwanza waliotembea na Yesu pia hawakutuambia kwamba Yesu ni Mungu tumeona wakitaja kwamba. Yesu ni Mtume, Mwalimu, Nabii, mtiwa mafuta, Bwana, mtu, Selemala, na Mwana wa Mariamu tu.

  Kama tulivyoona Maaskofu wa kwanza nao hawakutuambia wazi kwamba Yesu ni Mungu au Roho Mtakatifu ni Mungu kufika hapa ndugu msomaji unaweza kuuliza sasa fundisho hili kubwa na ndiyo kanuni ya Wakristo lilianza vipi? Hadi kuwa ndiyo imani kuu namna hiyo? Je? Ni mpango wa Mungu kweli? Naomba uendelee kusoma.

 258. hello Ndugu zangu, naomba nichangie japo kidogo juu ya hili suala. Kwanza lazima tukubali kuwa Mungu yu juu sana ya ufahamu wetu. Yeyote atakayetumia njia zake na kumjua Mungu 100%, huyo nastahili kuwa Mungu pia. Hivyo basi, tunamfahamu Mungu kadri ambavyo amejifunua kwetu.

  Mungu ni Utatu, maana yake ni Nafsi Tatu tofauti, lakini Mungu yule yule. Kwa tafsiri rahisi ni hivi: Yesu(Neno) ni Mungu, Baba ni Mungu, Roho Mtakatifu ni Mungu, na wote hawa ni Umoja. Yesu sio Baba, wala Baba sio Roho, wala Roho sio Yesu, lakini wote hawa ni Umoja. Nimelenga kutoa jibu fupi lakini la kueleweka. Ukitaka kuelewa zaidi, biblia ipo kwa ajili yako!

  Utatu katika Uumbaji:
  בראשית ברא אלהים את השמים ואת הארץ (Bereshith bara Elohim eth hashshamayim veeth haarets )—> God in the beginning created the heavens and the earth. (Genesis1:1)
  Neno Elohim ni Wingi wa Eloah au El ambalo maana yake ni Mungu (Umoja) na Elohim maana yake ni wingi (Miungu).
  Tunaona umoja katika neno aliziumba, kuonyesha wingi katika umoja (utatu). Hivyo ukiendelea mbele utaona Roho Alitulia juu ya uso wa maji na Baba aliumba kwa Neno.

  Katika maandiko hili liko wazi, Yesu ni mungu, Baba ni Mungu na Roho ni Mungu na hawa wote ni Umoja. Ukijifunza biblia, huu ni ukweli ambao hauepukiki. Mashahidi wa Yehova wanakana hili, ila Biblia yao wenyewe inkubaliana na utatu!

  Maswali kwa mahali sijaeleweka yanakaribishwa.
  Mtume wa Yesu

 259. Ndugu Achipete,

  Nashukuru kwamba tunakwenda pamoja. Kwa pamoja tunaendelea kuutafuta ukweli ambao tukiufahamu utatuweka huru. [John 8:32 And ye shall know the truth, and the truth shall make you free.]

  Nitaanza na jinsi ambavyo umeanza kujibu jinsi ulivyonielewa kutokana na niliyosema mahali fulani juu ya KUAMINI na KUELEWA. Umeandika kwamba mtu akiamini tu mambo yote yanakuwa marahisi. Lakini naona umeacha sehemu muhimu [yawezekana umeielewa lakini ulitaka kufupisha] kwamba MTU AKIAMINI ILE IMANI HULETA MATOKEO YANAYOELEWEKA KWA AKILI NA HIVYO ATAFAHAMU KWAMBA ALICHOKIAMINI NI KWELI. Imani hii inayoleta matokeo ndiyo hufanya mtu aelewe kwamba alichoamini ni kweli. Kwa mfano: Mtu anapomwamini Yesu kama Bwana na mwokozi na kumpokea moyoni mwake, mtu huyu hujisikia ule MGUSO WA ROHONI ambao HAKUWA ANAJISIKIA KABLA HAJAMPOKEA YESU. Badiliko hili ndilo humfanya atambuwe KUMBE KWELI MTU AKIMWAMINI YESU anakuwa ameamini kitu halisi! Lakini kwa upande wa pili Mtu ambaye anakataa kumwamini Yesu HUWA HANA BADILIKO LOLOTE AMBALO LINAMTOFAUTISHA NA ALIVYOKUWA KABLA HAJAKATAA KUMPOKEA YESU. [Yaani kwa ufafanuzi zaidi ni kwa mfano leo tarehe 22/12/2008 kama kuna mtu mmoja ambaye hajamwamini Yesu, kesho tarehe 23/12/2008 akahubiriwa habari njema za Yesu halafu akakataa, siku inayofuata, tarehe 24/12/2008 mtu huyu atakuwa katika hali ile ile kama aliyokuwa nayo tarehe 22/12/2008 kwa sababu hajaamini habari za Yesu]

  Leo tutasogea mbele kidogo hadi kwenye Suala la IMANI, kwa maana ya KUAMINI. IMANI, kwa tafsiri ya Biblia, NI KUWA NA HAKIKA YA MAMBO YATARAJIWAYO, NI BAYANA YA YAMBO YASIYOONEKANA [ Hebrews 11:1]. Na PASIPO IMANI HAIWEZEKANI KUMPENDEZA MUNGU [Hebrews 11:6]. Nilieleza kwamba katika mambo ya Rohoni AKILI YA BINAADAMU HAINA UFAHAMU WA KUTOSHA na baada ya akili kufikia ukomo wa kuelewa NDIPO IMANI HUCHUKUWA MKONDO WAKE. Imani ni mlango wa fahamu katika ulimwengu wa Roho. Watakatifu wa Mungu hushi kwa IMANI, na si kwa kuona [2Cor 5:7 (For we walk by faith, not by sight]. IMANI huja kwa kusikia, na kusikia huja kwa Neno la Mungu [Romans 10:17 So then faith cometh by hearing, and hearing by the word of God].

  Akili hutumia milango mitano ya FAHAMU kuelewa jambo. Kuona, Kugusa, Kusikia, Kuonja na Kunusa. Ili kitu kitambulike kwenye akili ni LAZIMA KIWE KIMEPITIA KATI YA MILANGO HII YA FAHAMU. Kitu chochote ambacho hakionekani, hakiwezi kuguswa, hakisiki sauti yake masikioni, wala ladha yake haiwezi kutambulikana kwa ulimi na wala hakina harufu, KITU HICHO HAKIWEZI KUTAMBULIKA KWA AKILI KWAMBA KINA-EXIST. MAMBO YALIYO KATIKA ULIMWENGU WA ROHO HAYANA TABIA HIZI ZA KUWEZA KUTAMBULIKA NA MILANGO YA FAHAMU. Mfano MALAIKA: Hatuwaoni kwa macho, hatuwasikii wakipita, hatuwezi kuwagusa kwa mikono, wala hauwezi kunusa harusu yao, KWA UJUMLA MWILI HAUNA UTHIBITISHO KWAMBA KUNA MALAIKA na NDIVYO ILIVYO AKILI, kwa kuwa tumeona akili inategemea milango yake mitano ya Fahamu. Lakini kutoweza kuwahisi Malaika kwa namna yoyote ile HAIMAANISHA MALAIKA HAWAPO. Na WALA KWA NAMNA YOYOTE ILE WANASAYASI HAWAWEZI KUTHIBITISHA KWENYE MAABARA KWAMBA MALAIKA WAPO. Watu wengi wamekuwa wakienda Hospitali kupima kwenye darubini za kitaalamu hawaonekani kuwa na ugonjwa wowote lakini mtu mwenyewe ni mgonjwa na mwenye kuteseka. Darubini zisipoona Ugonjwa Madaktari husema hakuna Ugonjwa. Lakini ukisema Hakuna ugonjwa wakati mtu anajisikia maumivu anashindwa kutambuwa kwamba msaada wa Daktari uko wapi. Lakini cha kufurahisha mtu akienda KUOMBEWA KWA JINA LA YESU ugonjwa ule unatoka na mtu anakuwa mzima!

  Wazo nililokuwa nalijenga hapa ni kwamba Akili ya binaadamu ina mpaka wa kuelewa mambo. Na mpaka wake unaishia kwenye milango yake mitano ya fahamu. Na mambo ya rohoni yako nje ya milango hiyo ya fahamu. Kwa hiyo ili kuweza kuelewa mambo ya Rohoni tunahitaji mlango mwingine wa fahamu. Mlango huu wa fahamu katika mambo ya Rohoni ni IMANI. Suala la UTATU NI SUALA LA KIROHO, si suala la KIMWILI. Ni suala linalohusu Mungu. Mungu ni Roho nao wamwabuduo imewapasa Kumwabudu katika Roho na Kweli [John 4:24 God is a Spirit: and they that worship him must worship him in spirit and in truth]. Haisemi kwamba Mungu aabudiwe katika AKILI NA KWELI. BINADAMU NAYE NI ROHO INAYOISHI KATIKA MWILI. Akili ya mwilini inatufaa katika mambo yahusuyo maisha katika Ulimwengu wa Mwili. Lakini kwenye sehemu ya roho tunahitaji IMANI ili kuweza kuyaelewa mambo ya rohoni. Narudia tena kwamba UTATU NI JAMBO LA KIROHO na si la kimwili! KWA HIYO INATAKIWA IMANI, KWA JILI YA UFAHAMU WA KIROHO, KATIKA KULIELEWA SWALA HILI.

  Ndugu Achipete, mimi bado naamini kuna mambo mengi ambayo binaadamu tunayakubali kwa KUYAAMINI TU na wala SI KWA KUYAELEWA. Natumaini nawe unakubali pia kwamba KUNA PARADISO [Wengine wanaita MAHALI PEMA PEPONI ingawa yawezekana hii isiwe tafsiri sahihi]. Labda tujiulize: Kuna mtu yeyote ambaye ALISHAPAONA hapo mahali pema PEPONI? NI WAPI HUKO? Mtu akisema hawezi kukubali hadi apatiwe picha [photo] ndipo akubali atakuwa na kosa? Lakini pamoja na kukosekana Majibu na Uthibitisho wa akili ya Binaadamu bado TUNAKUBALI PASI NA SHAKA KWAMBA KUNA PARADISO. Je, kukubali huku ni kwa sababu TUNAELEWA [kama ilivyo 1+1 = 2] au ni kwa sababu TUNAAMINI. Kuna ndugu mmoja kwenye Blog hii hii katika kutetea kwamba lazima akili ielewe kila kitu Aliuliza KUZIMU NI WAPI?, NI ANGA ZIPI?, DARUBINI GANI INAWEZA KUONA KUZIMU?, MILANGO YA KUINGIA HUKO IKO WAPI? Kwa hiyo akasema hizo ni propaganda tu kwa kuwa kitu hicho hakiwezi kuwa-proved Scientifically! UNAONA JINSI AKILI ILIVYO NA UFAHAMU FINYU KWA MAMBO YA ROHONI. Kwa hiyo tuseme kwa kuwa KUZIMU hakuonekani kwa darubini basi hakuna kitu kama hicho?

  Natumaini tunakwenda pamoja ndugu Achipete. Sasa nanukuu kutoka paragrafu yako ya pili halafu nitaendelea:

  ”Kama ulivyoeleza katika utangulizi kuwa UKIAMINI basi yote yatakuwa marahisi. Aidha umeeleza kuwa katika hali ya KIBINAADAM, ni vigumu kuelewa baadhi ya mambo mengi katika Biblia. Hapa ndio penye utata kwani Bwana Mungu si aliileta Biblia kwa ajili ya wanadam? Kama hatuwezi kupata majibu ya maswala mengi katika biblia hiyo sasa kwanini tuisome? Ama kwa maneno mengine Bwana PAUL unataka kusema kuwa mimi niamini tu bila kujiuliza.”

  …….tuendelee!

  Unaona maswali kama hayo. ..Mfano DARUBINI GANI INAYOWEZA KUONA KUZIMU? Hili pia nalo ni swali la binaadamu, tena msomi sana, ambalo NINA UHAKIKA JIBU LAKE HALIWEZI KUPATIKANA KUTOKA KWENYE BIBLIA! Unaona?…..Hatuwezi kupata Aina ya Darubini inayoweza kuona kuzimu kutoka katika Biblia. Je kwa sababu hatupati jibu hilo toka kwenye Biblia TUACHE KUSOMA BIBLIA? La hasha! Biblia INA MAJIBU YA KUTOSHA juu ya MASWALI YOTE YANAYOHUSU MAMBO YA MAISHA YA BINAADAMU NA HATIMA YAKE pamoja na MPANGO WA WOKOVU KWA WANAADAMU. Maswali yote ambayo majibu yake yana manufaa kwa Binaadamu majibu yake yako kwenye Biblia. Lakini maswali ya Ubishi na utafiti na mengine ambayo yako Beyond Human reasoning hatuwezi kupata majibu yake. Haya ndiyo nilimaanisha niliposema MASWALI MENGI MAJIBU YAKE HAYAKO KWENYE BIBLIA. Na nikaongeza kwamba NI BAHATI MBAYA MAANA NI MACHACHE AMBAYO MAJIBU YAKE YANAELEWEKA KWA AKILI ZA KIBINAADAMU. Maana yake YALE YANAYOHUSU HABARI ZA ROHONI YANAELEWEKA KWA IMANI!

  Ngudu Achipete, YAKO MASWALI MENGI SANA AMBAYO NIKIKUULIZA NATA HUWEZI PATA MAJIBU TOKA MAHALI POPOTE PALE bali utaniambia tu NIAMINI!!!!! Lakini ukikosa majibu mimi halinisumbuwi kwa kuwa najuwa Ufahamu wa Binaadamu uko Limited katika yale tu yanayomfaa kwa ajili kuweza KUMWABUDU MUNGU na kumfanya aweze kukabili maisha katika siku hizi chache za kuishi hapa.

  Hata Biblia imeelezea kuhusu mambo hayo ambayo yako beyond human reasoning: Deutronomy 29:29 The secret things belong unto the LORD our God: but those things which are revealed belong unto us and to our children for ever, that we may do all the words of this law.

  …..Tuendelee na mada yetu ya UTATU.

  Nanukuu: ”The doctrine of the trinity wasn’t even established until the fourth century. So for all of the purists who believe that nonbelievers of the trinity are doomed to hell, well, that’s four hundred years of damned souls. Sorry. Don’t get me wrong here – I know what the trinity is, but I’ve always had a hard time swallowing it. The whole notion of the trinity is that The Father, the Son, and the Holy Spirit are not the same entity, and yet at the same time they are the same entity, namely, God”.

  ….Mtu yeyote anayetaka kuelewa UTATU kwa kutumia AKILI YA KIMWILI lazima ataishia na utata huu. Mambo katika ulimwengu wa Roho hayako kama tunavyoona mambo yaliyo katika Ulimwengu wa Mwili. [Soma mfano huu: Nilishasikia Mchawi mmoja akitoa ushuhuda baada ya Kukutana na Yesu na kuacha Uchawi wake kwamba WALIKUWA WAKIRUKA ANGANI KWA KUTUMIA UNGO na ungo mmoja (kama futi mbili kwa diameter) una uwezo wa Kubeba watu 17!…ndiyo! Sasa fikiria kwa akili yako kwamba Ungo mmoja utabebaje watu 17 halafu jibu kaa nalo mwenyewe] Ili kulielewa suala hili la UTATU inahitajika IMANI. Tatizo lililopo watu wanataka KUUELEWA UTATU PASIPO KUWA NA IMANI. IMANI IKIINGIA MOYONI MWA MTU, SUALA LA UTATU LINAELEWEKA WAZI KABISA!

  …Umesema kwamba watu kama ndugu Gapid wako wengi, na wewe ni mmoja wao ndiyo maana mnatafuta huku na kule kutafuta Ukweli. Ni jambo jema sana. Kama KIU YAKO NI KUUJUWA UKWELI, Mungu ameona kiu yako. Na Yesu alisema HERI WENYE NJAA NA KIU YA HAKI MAANA HAO WATASHIBISHWA [Mathew 5:6]. Nami ninamuomba Mungu, kwa Jina la Yesu!, kwamba hapa upate kitu ambacho hujawahi kukisoma popote pale na ambacho kitakupa mwanga mpya katika kuifahamu kweli na hivyo kukuongezea angalau hatua moja zaidi!
  .. Amina!

  Gapid anasema; The there’s the really confusing John 8:58. Mstari huu unasomeka hivi: ”Jesus said unto them, Verily, verily, I say unto you, Before Abraham was, I am”
  Sasa mimi sielewe kwa nini anasema ni ‘really confusing’. Watu wengi wameshafundisha kwamba Yesu alikuwa mbinguni kabla ya kuja duniani kukamilisha mpango ukombozi kwa wanadamu. Yesu alikuwa ni Mungu pamoja na wanadamu. Kwa hiyo Kabla Abraham hajazaliwa Yesu alikuweko tayari, lakini wakati huo akiwa Mbinguni. [Halafu waweza linganisha I AM ya kwenye John 8:58 ile ya kwenye maneno aliyoambiwa Musa alipomuuliza Mungu katika kile kijijti kilichokuwa kikiwaka moto wakati akitumwa kuwaongoza wana wa Israel kutoka Misri. Musa alipouliza atawaambia ni nani aliyemtokea na kumtuma Kwao? Jibu lilikuwa Exodus 3:14 And God said unto Moses, I AM THAT I AM: and he said, Thus shalt thou say unto the children of Israel, I AM hath sent me unto you.]

  Kama ndugu Gapid angekuwa anaamini kwamba Yesu alikuwako mbinguni kabla ya kuja duniani, mstari huo wala hausumbuwi. Lakini kwa wale wasioamini hivyo basi mstari huu ni ‘really confusing’. Unaweza kusoma John 8:59 ambapo wale Wayahudi walipokuwa ‘rearlly confused’ na neno hili waliokota mawe wakataka kumpiga Yesu. Hata sasa wapo watu ambao wanapohubiriwa habari za Yesu wakishindwa kuelewa kwa sababu wanataka ku-equate kama mahesabu wanaishia kuwa-confused na kwa sababu hiyo wanawatupia mawe watu wanaohubri habari hizo njema! Inasikitisha sana.

  ………Mistari uliyosema niipitie naomba tuipitie tena kwa pamoja

  a. 1Timothy 2:5 For there is one God, and one mediator between God and men, the
  man Christ Jesus;
  Najuwa kinachochanganya hapa ni pale inaposema ‘the man Christ Jesus’. Lakini maelezo yake hapa ni kwamba Yesu alipokuja duniani alikuja akaingia katika mwili na akawa ni Mungu pamoja na Wanadamu. Na katika kukaa kwake duniani alikuwa sawa na Mtu mwingine Ye yote. Alikuwa ni kama binaadamu wa kawaida. Tofauti ilikuwa ni kwamba hakutenda Dhambi. Kwa hiyo hapa mtume Paul alipoandika alikuwa ana-refer ile HUMAN STATE aliyokuwa nayo Yesu kabla ya kufufuka na kupaa mbinguni. Kwa kuwa hadi Yesu alipofufuka ndipo akadhihirika kwamba hakuwa binaadamu wa kawaida.

  b. John 14:28 Ye have heard how I said unto you, I go away, and come again unto you. If ye loved me, ye would rejoice, because I said, I go unto the Father: for my Father is greater than I.
  Tatizo lililopo hapa ni mwendelezo wa tatizo lililokuwepo tangu wakati wa enzi za Uwepo wa Yesu katika mwili duniani hapa. Wakati huo Wayahudi walitaka kumpiga kwa sababu alikuwa anajiita ni Mwana wa Mungu. Hapa tatizo lililopo ni kwa sababu Yesu anasema Baba ni mkuu kuliko yeye Yesu. Kwa hali ya kawaida baba huwa kwenye higher ranking kuliko mtoto. Inaposemwa Mungu Baba, na Mungu mwana ni wazi kwamba Mungu Baba atakuwa kwenye higher ranking. Lakini mahali pengine anasema Yesu yuko ndani ya Baba na Baba yuko ndani yake [John 17:21]

  c. John 17:3 And this is life eternal, that they might know thee the only true God, and Jesus Christ, whom thou hast sent.
  Nimeeleza hapo juu Yesu anaposema Yeye na Baba, ambaye hapa anamwita the Only true God, ni kitu kimoja kwa kuwa Baba yu ndani ya Mwana na Mwana yu ndani ya Baba. Na tena hawa ni Umoja. John 17:22 And the glory which thou gavest me I have given them; that they may be one, even as we are one:

  d. John 5:19 Then answered Jesus and said unto them, Verily, verily, I say unto
  you, The Son can do nothing of himself, but what he seeth the Father do: for what things soever he doeth, these also doeth the Son likewise.
  Hapa inaonyesha umoja huu uanvyofanya kazi kwa pamoja.

  e. John 17:20-23 Neither pray I for these alone, but for them also which shall believe
  on me through their word; That they all may be one; as thou, Father, art in me, and I in thee, that they also may be one in us: that the world may believe that thou hast sent me. And the glory which thou gavest me I have given them; that they
  may be one, even as we are one; I in them, and thou in me, that they may be made perfect in one; and that the world may know that thou hast sent me, and hast loved
  them, as thou hast loved me.
  ..Hapa sijajuwa tatizo liko wapi maana maelezo yako wazi.

  f. Mathew 27:46 And about the ninth hour Jesus cried with a loud voice, saying, Eli,
  Eli, lama sabachthani? that is to say, My God, my God, why hast thou forsaken me?
  ..Hapa pia sijajuwa tatizo lilipo. Lakini nayafananisha maneno haya na yale aliyoyasema Yesu wakati wa kumfufua Lazaro [John 11:41-42]na pale alipokuwa akiomba kule Gethemane [Mark 14:36]. Ni maneno ambayo ni kama anayeitwa au kuombwa yuko mbali naye. Lakini naamini katika Ulimwengu wa Roho distance haina magnitude. Ndiyo maana hata Biblia inasema Mungu yu karibu na waliovunjika moyo [34:18 The LORD is nigh unto them that are of a broken heart; and saveth
  such as be of a contrite spirit.]

  Umemalizia kwa kuandika kwamba mpaka sasa suala la UTATU HALIJAWAINGIA WANAADAMU. Naopenda hapa turekebishe iwe SUALA LA UTATU HALIJAWAINGIA WALE AMBAO HAWAJAMWAMINI YESU. Watu wote waliomwamini Yesu na kumpokea kama mwokozi, kama Biblia isemavyo, suala hili la UTATU wala siyo ajenda kwao. Si tatizo kabisa. Hata hivyo kwa watu waiomwamini Yesu TATIZO siyo suala la UTATU tu, yako mengi ambayo yanaonekana kuwa ni kikwazo.

  Umeeleza pia juu ya Madhehebu yasiyoamini UTATU kwamba wanaweza kuwa na maelezo sahihi zaidi. Uko sahihi kabisa kwa sababu KUUKATAA UTATU HAKUHITAJI IMANI. Kunahitaji akili tu ya binaadamu, akipiga mahesabu kwamba itakuwaje kama Yesu na Mungu ni Umoja, mara Yesu yuko ndani ya Mungu Baba na Mungu Baba yuko ndani ya Yesu, hii inachanganya…..! au Hii haiwezekani….!. Na watu wakakubali kwamba kwa akili ya kawaida inakataa. Ni rahisi kuwaelewa hawa kwa sababu WANAWAELEZA WATU AMBAO NAO HAWATAKI KUAMINI…. Mitaani wanasema NI SAWA NA KUMSUKUMA MLEVI!

  Kusema kwamba nadharia ya UTATU iliingizwa katika karne ya 20 ni utani tu kwa sababu UTATU ni maandiko ya Biblia. Na Biblia iko kwa muda mrefu sana uliopita ikiwa na maandiko hayo hayo.

  SUALA LA MSINGI KULIJUWA

  Mafundisho ya habari za UTATU siyo mafundisho ya MSINGI katika kuhubiri Injili. Fundisho la Msingi ni MTU KUMWAMINI NA KUMPOKEA YESU MOYONI. Kwa maana Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanaye wa pekee ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele [John3:16]. Mtu akiishakumwamini Yesu, IMANI huingia ndani yake, kama mlango wa Ufahamu kwa mambo yahusuyo ulimwengu wa Roho. [Tulishaona kule mwanzo kwamba Imani huja kwa kusikia, na kusikia kwa neno la Mungu]. Wala kwenye mikutano ya Injili wahubiri/hawafundishi watu habari za UTATU ndipo watu wamwamini Yesu. Kinachohubiriwa zaidi ni Anguko la binaadamu, Upendo wa Mungu, na Mpango wa Ukombozi aliouleta kupitia Yesu kwa kuzaliwa, kufa na kufufuka. Mambo haya yakihubiriwa pamoja na udhihirisho wa Nguvu za Mungu kwa Jina la Yesu vinatosha kumfanya mtu AMWAMINI YESU. Mtu akishampokea Yesu, wakati anaendelea na maisha mapya katika wokovu, ndipo hupata mafundisho hayo ya UTATU na kwa wakati huo ndipo mtu hutambuwa kwamba kumbe mambo yanaeleweka kabisa.

  Watu wachache ambao ni watafiti, watu ambao wameshapita katika imani tofauti tofauti na kusoma vitabu vingi, na pengine walishawahi kuwa katika imani PINZANI KWA KAZI YA WOKOVU ALIOLETA YESU, hawa waweza kusema kwamba ili amwamini Yesu ni lazima aelewe kwanza kwa ukamilifu habari za UTATU kwa kutumia akili [nimeshaandika sana jinsi IMANI ndiyo mlango wa fahamu katika mambo yahusuyo ulimwengu wa roho]. Kwa hiyo wanapoambiwa WASIKILIZE NENO LA MUNGU NA KULIAMINI, WAKISHALIAMINI LITALETA IMANI ITAKAYOWASAIDIA KUELEWA MAMBO YA ROHONI, wanang’angania LAZIMA KIELEWEKE KWANZA AKILINI. Hivyo mzunguko huu huendelea pasipo kufika mwisho. Na hapa inanikumbusha swali la KUKU NA YAI KIPI KILITANGULIA? Mwaisho wake mtu anakufa kabla ya kumpokea Yesu.

  Kusema kweli IMANI NI KITU CHA LAZIMA KWA MAMBO YA ROHONI
  Hebrews 4:2 For unto us was the gospel preached, as well as unto them: but the word preached did not profit them, not being mixed with faith in them that heard it.

  HATA HIVYO SIJAELEWA KAMA KUNA WATU AMBAO HAWAAMINI kwamba Kuna Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu, HALAFU WANAMWAMINI YESU, yaani WAMEOKOKA na Ishara zote alizosema Yesu zinatendeka kwao kama kwa wale wanaomwamini Yesu kwa kila Nyanja!

  Tuendelee kijifunza..

 260. Ndugu ACHIPETE

  Shalomu!!!

  Nimeyasoma maswali yako pamoja na majibu ya kina yaliyotolewa na Ndugu John Paul. Aidha, nimeusoma mchango wako wa nyongeza baada ya majibu ya ndugu John.

  Ndugu John amejaribu kwa kiwango kikubwa sana kufafanua mambo ambayo ni vigumu kuyafafanua kwa watu ambao hawajamwamini Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wao, yaani watu ambao hawajaokoka, (Mungu amubariki sana Ndugu John Paul).

  Katika maelezo yake, Ndugu John ametoa utangulizi ambao ni msingi sana alipoweka tofauti ya ulimwengu wa mwili na ulimwengu wa roho. Nadhani ungetafakari juu ya tofauti hiyo, ungeweza kuelewa zaidi juu ya kile alichokisema. Kutokana na hali hiyo, nimeona nami nijaribu kutoa ufafanuzi kidogo.

  Mambo ya Rohoni yanatambulikana kwa jinsi ya rohoni na watu wa mwilini hawawezi kuyatambua. Tunaposema juu ya Roho Mtakatifu, Biblia inaeleza wazi kuwa ulimwengu hauwezi kumpokea wala kumtambua, lakini huyo Roho anakaa ndani ya watakatifu (Yohana 14:17).

  Bila kuwa na Roho Mtakatifu, huwezi kuyatambua mambo ya rohoni, na moja ya mambo ya rohoni ni suala la Mungu Baba, Mungu mwana na Mungu Roho Mtakatifu. Sisemi hivi ili kujitetea, bali nasema hivi kulingana na maandiko niliyoyaonyesha hapo juu, maana unapozungumzia utatu unazungumzia Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, na Biblia imesema wazi kuwa ulimwengu hauwezi kumtambua Roho Mtakatifu. (Anaposema ulimwengu ana maanisha wanadamu ambao hawajamkubali Yesu Kristo kuwa ni Bwana na Mwokozi)

  Kwa habari ya Yesu Kristo, kuna watu wengi tu duniani, bila kujali dini zao hawamkubali kama ni Bwana na Mwokozi wa maisha yao, wengine wanamkataa kuwa si mwana wa Mungu na wengine wanasema kuwa hakufa msalabani. Hapa napo utaona jinsi Yesu asivyojulikana kwa wanadamu (mfano ni kuwa wapo watu wengi wanaosema ni wakristo lakini hawakubali kuokoka).

  Kutokana na maelezo niliyoyatoa hapo juu, ninakurudisha kwenye maelezo ya ndugu John kuwa MAMBO YA ROHONI huanza kwa mtu kuamini.

  Ndugu Achipete, naomba nikuhakikishie kuwa, siku utakapompa Yesu maisha yako, utaona jinsi alivyo mwokozi wa ulimwengu kwani atayabadilisha maisha yako na utakuwa kiumbe kipya, hili nalo linaanza kwa kuamini (Matendo 8:37, Matendo 18:31, Warumi 3:21-26, Waebrania 11:6). Imani ndiyo msingi wa kwanza utakaokupatanisha wewe na Mungu kwa njia ya Yesu Kristo ambapo utaokoka na maisha yako yatabadilika kabisa.

  Baada ya kuokoka, Mungu atakupa neema ya kuyajua mambo ya Rohoni kwani atakupa Roho Mtakatifu na kwa huyo Roho utaanza kuzijua siri za rohoni kwani atakuketisha katika ulimwengu wa roho, (Waefeso 2:6).

  Ninapenda sana niendelee kuchangia, lakini kama nilivyosema inakuwa vigumu kwangu kukueleza kwa lugha ya kibinadamu kile kilicho ndani yangu, ila tu ninachoweza kusema ni kuwa YESU aliyabadilisha maisha yangu baada ya kuamini.

  Tunaposema kuamini ni tunamaanisha ni ile hali ya kujitambua kuwa wewe ni mwenye dhambi (maana ndugu yangu unajifahamu mwenyewe kuwa u mwenye dhambi na biblia inasema kuwa wenye dhambi hawawezi kuurithi uzima wa milele (tafadhari sana soma Wagalatia 5:19-21). Ukisha jitambua kuwa wewe ni mwenye dhambi, unapaswa kujua kuwa huwezi kujiokoa toka kwenye hizo dhambi ndiyo maana unatenda kile ambacho hukipendi. Biblia inasema kuwa atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi (Yohana 8:31-36). Ukisha fahamu kuwa huwezi kujiokoa (maana mtumwa hawezi kujiokoa mpaka apatikane mwokozi) basi tambua kuwa unamhitaji mwokozi na mwokozi ni YESU KRISTO (Matendo 4:12) pekee.

  Nadhani mpaka hapo tumeelewana, sasa kinachofuata ni kumkubali huyo mwokozi kuwa alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zako na kuwa Mungu alimfufua katika wafu (Warumi 10:9) basi utapata wokovu. Katika siku hizi za neema, Mungu anaagiza watu wote watubu (Matendo 17:30), na moja ya dhambi ambayo wengi itawapeleka katika moto wa milele ni kutokuamini (Yohana 3:17-19).

  Kama nilivyosema, baada ya kuokoka, utauona uhalisi wa UTATU maana Mungu atajifunua kwako na kuwa dhahiri kabisa, ndipo utakapomjua Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu, maana wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu (Yohana 1:12), nawe pia utapewa uwezo huo, (soma pia 1Yohana 3:1-2).

  Imani ndiyo msingi, hakuna msaada mwingine zaidi ya kuamini. NI KUAMINI TU. UNAAMINI KWANZA NDIPO UNAPATA FAIDA ZA KUAMINI na matokeo yake (EFFECTS kama alivyosema ndugu John) yataonekana na kutambulikana kwa jinsi ya mwili).

  Ni maombi yangu kuwa Mungu wa rehema akupe neema yake ili uweze kuamini na kuokoka.

  Mungu awabariki wote.

  Shalomu

 261. Ndugu John Paul, nashukuru kwa majibu yako ambayo nafikiri wengi watafaidika. Pengine maswali yalikuwa mengi au yenye mtazamo mrefu, hivyo ningependa sana kuzungumzia hili la UTATU tu.

  Kama ulivyoeleza katika utangulizi kuwa UKIAMINI basi yote yatakuwa marahisi. Aidha umeeleza kuwa katika hali ya KIBINAADAM, ni vigumu kuelewa baadhi ya mambo mengi katika Biblia. Hapa ndio penye utata kwani Bwana Mungu si aliileta Biblia kwa ajili ya wanadam? Kama hatuwezi kupata majibu ya maswala mengi katika biblia hiyo sasa kwanini tuisome? Ama kwa maneno mengine Bwana PAUL unataka kusema kuwa mimi niamini tu bila kujiuliza.

  Samahani kwa jinsi ninavyofahamu mimi Bwana Mungu kamuumba binadamu katika umbo bora zaidi na kumpa akili ambayo itatafakari na kupata majibu ya maswali ajiulizayo. Aidha Bwana Mungu akampa muongozo(Biblia) mwanadamu kupitia Mitume au manabii wake. Kwa hiyo muongozo alioutoa lazima alipima uwezo wa binadamu kuelewa. Na katika mantiki hii ni lazima kilichoandikwa binaadamu akielewe.

  Aidha unaandika “BAHATI MBAYA binaadam katika maswali aulizayo ni machache tu ambayo majibu yake yanaweza kuelewa kwa akili yake ya kibinaadam” Ni kweli hiyo ni BAHATI MBAYA, na hata walio wengi hawaoni kama bahati mbaya ila ni kujichanganya. Nimetembelea katika blog nyingi sana, nitajaribu kunukuu baadhi ya watoa maoni katika blog za GAPID SMACK, gapid.blogspot.com na katika answering-islam.org.

  Jonathan katika answerin-islam.org aliueleza UTATU kama ifuatavyo “God’s tri-unity is quite complicated; in fact, it’s probably the most complicated revelation in the entire Bible. I like to compare it to nuclear physics: you have to study it for a long time before you understand it, and most people never get that far unless they really want to spend the rest of their lives deeply involved”.In any case, please don’t follow the temptation to say, “It’s too confusing, so it must be wrong.” Maelezo haya hayatofautiani na yale ya kwako, kwani anachosisitiza ni kwamba, mtu aamini tu kwa vile inachanganya. Hii inanipa wasi wasi kama hata yeye mwenyewe anaelewa kinachozungumziwa katika UTATU.

  Katika gapid.blogspot.com Gapid aandika “The doctrine of the trinity wasn’t even established until the fourth century. So for all of the purists who believe that nonbelievers of the trinity are doomed to hell, well, that’s four hundred years of damned souls. Sorry. Don’t get me wrong here – I know what the trinity is, but I’ve always had a hard time swallowing it. The whole notion of the trinity is that The Father, the Son, and the Holy Spirit are not the same entity, and yet at the same time they are the same entity, namely, God”. Gapid anajaribu kwa nguvu zake zote, roho yake yote na kwa akili yake yote toaka udogo kupata maana iingiayo akilini ya UTATU, LAKINI HAJAFANIKIWA. Watu kama yeye na mimi ni wengi, na ndio maana tunajaribu kuangalia huku na kule kutafuta ukweli.

  Katika kutafuta ukweli Gapid aendelea kuandika “There are several more verses that seem to somewhat contradict the whole notion of the trinity. But on the other hand, there are several verses that directly support the notion of the trinity. The most popular, of course, is Matthew 28:19. Then there’s the really confusing John 8:58. And Colossians 2:9 confirms the divine nature of Jesus”. Ni kweli kuna sehemu za biblia zinazokubaliana na sehemu nyingi tu ambazo zinapingana. Jaribu kuzipitia Timothy 2:5, John 14:28, 17:3, 5:19, 17:20-23, Mathew 27:46.

  Mpaka bado suala la UTATU halijawaingia wanaadam, pengine hata waumini wazuri walioamua kumeza kauli hiyo bila kuielewa, kuna mwanya mkubwa wa mathehebu yasiyoamini UTATU kuwa na maelezo sahihi zaidi. Ama hii itathibitisha zaidi kuwa yasemwayo na wale wasioamini UTATU, kuwa nadharia hiyo iliingizwa katika karne ya 20 kuwa ndio sahihi.

  Asanteni.

 262. Ndugu Achipete Chipaga

  Ni kweli kabisa kama ulivyosema kwamba Kumjua Bwana Yesu ni ushindi wa Amani na Upendo duniani.

  Napenda kuungana nawe kwamba Mwanadamu ni mdadisi na haachi kujiuliza kwa yale aonayo, ayasikiayo nk. Bahati mbaya binaadamu katika maswali mengi aulizayo ni machache tu ambayo majibu yake yanaweza kuelewa kwa akili yake kibinaadamu. Hii inatokana na ukweli kwamba binaadamu anaishi katika ulimwengu wa aina mbili. Ulimwengu wa roho ambao ni wa milele na ulimwengu wa mwili ambao huisha baada ya kifo cha mwili huu. Kwa hiyo maswali anayokabiliana nayo huwa yamegawanyika katika sehemu hizi kuu mbili. Maswali yanayohusu ulimwengu wa mwili huu hueleweka kwa akili ya mwili huu hali kadhalika maswali yanayohusu ulimwengu wa roho hueleweka na ufahamu wa kiroho. Mfano ni rahisi kuelewa kwa akili kwamba 2+2 = 4 lakini ni vigumu sana kuelewa kwa akili (na haiwezekani kabisa) kwamba Mungu Mwenyezi hana Mwanzo wala Mwisho! Akili inaposhindwa kutambuwa mambo yanayohusu ulimwengu wa roho, ndipo IMANI huchukuwa mkondo wake na binaadamu hukubali kwa KUAMINI TU na SI KUELEWA! Lakini jambo la kushukuru Mungu ni kwamba Binaadamu anapokuwa AMEAMINI juu ya jambo fulani ATHARI (effects) za KUAMINI HUKO huonekana na kutambulika na akili ya mwili. Na inapofikia katika hali hii ndipo mtu huyo hutambuwa kwamba KUMBE ALICHOAMINI NI CHA KWELI. KUAMINI AMBAKO HAKULETI ATHARI ZOZOTE ZINAZOONEKANA AU AMBAZO HAZILETI TOFAUTI KATI YA ANAYEMAINI NA ASIYE AMINI KITU HICHO BASI KUAMINI HUKO NI BURE. Ndiyo maana Yesu akasema juu ya ISHARA/DALILI ambazo zitaambatana na wale WATAKAOMWAMINI kama vile KUNENA KWA LUGHA NYINGINE, KUTOKA MAPEPO/MAJINI KWA JINA LAKE, KUOMBEA WAGONJWA NAO WANAPATA AFYA KWA JINA LAKE nk. KWA HIYO MTU ANAYEMWAMINI YESU AKIONA DALILI HIZO ZINATIMIA KWAKE ndiyo uthibitisho kwamba ni kweli amemwamini Yesu. Kwa maana nyingine mtu akisema anamwamini Yesu halafu kwake hakuna dalili/ ishara hizo basi mtu huyo hana uthibitisho wowote kwamba anamwamini Yesu na huyu anaweza kuitwa tu ni muongo. Katika kundi hili wapo watu ambao wana dini nzuri ambazo zinajitangaza kwamba wanamwamini Yesu lakini wakikataa yale ambayo Yesu alisema kuwa ndiyo UTHIBITISHO wa watakaomwamini. Jibu tumeshalipata kwamba watu hawa ni SIMPLY HAWAMWAMINI YESU, bali wanaamini kitu kingine!

  Natumani tuko pamoja mpaka hapo!

  Sasa twende kwenye maswali yako. Nitajibu kwa ufupi na majibu yangu siyo ndiyo majibu pekee, naamini wengine wataendelea kujibu maswali hayo au kuweka sawa mahali ambapo nitakuwa nimekosea kujibu inavyopasa. Maana hapa naamini ni darasani:

  1.UTATU
  a. Uungu una nafsi tatu yaani Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho. Moja ya kielelezo cha jambo hili ni katika Mathew 3:16-17 And (Jesus), when he was baptized, went up straightway out of the water: and, lo, the heavens were opened unto him, and he saw the (Spirit of God) descending like a dove, and lighting upon him: And lo a (voice from heaven), saying, This is my beloved Son, in whom I am well pleased.
  ANGALIA MANENO NILIYOWEKEA MABANO: Jesus, Spirit of God na Voice from Heaven – Kutoka kwa Mungu Baba. Hapa inaonyesha habari ya utatu huu. Utatu huu hufanya kazi kwa pamoja na umoja. Mchanganuo wake ni vigumu sana kueleweka kwa akili ya kibinaadamu na hivyo suala hili ni moja ya mambo ambayo yanatakiwa yakubalike kwa KUAMINI. Na mtu anapoamini HUWEZA KUSHUHUDIA YEYE MWENYEWE NAFSINI MWAKE KWAMBA ALIVYOAMINI NI SAHIHI. KUAMINI UTATU HUENDA SAMBAMBA NA KUMWAMINI YESU. John 14:1 Let not your heart be troubled: ye believe in God, believe also in me. (maneno ya Yesu)
  Kuna maandiko mengi kwenye Biblia na maelezo mengi sana ambayo yanaelezea kuhusu jambo hili lakini kwa ufupi kabisa (mimi) nitaishia hapa.

  b. Madhehebu mengine kutokuamini UTATU ni tatizo la kibinaadamu. Na ukifuatilia kwa undani si UTATU tu ambao huwa hauaminiwi na dini kama Jehova Witness. Wao HAWAAMINI KUNA KUOKOKA, HAWAAMINI KWAMBA MUNGU ATAWAANGAMIZA WAOVU KATIKA JEHANUM YA MILELE, HAWAAMINI KWAMBA DUNIA HII ITAANGAMIZWA KWA KUCHOMWA MOTO na tena HAWAAMINI KWAMBA BINAADAMU ANATAKIWA AFANYE LOLOTE KWA AJILI YA UTAKATIFU UTAKAOMWEZESHA KUINGIA MBINGUNI na mambo mengi mengi ambayo ni tofauti kabisa na ilivyoandikwa katika Biblia. Kwa hiyo watu hawa husihi maisha jinsi wanavyotaka kwa kuelewa kwamba MUNGU NI WA HURUMA SANA HAWEZI KUWACHOMA WANADAMU KATIKA MOTO. Wanasema ni Baba mwenye REHEMA NYINGI.

  Sasa ndugu yangu, watu ambao IMANI yao imekaa kama nilivyoelezea hapo juu (na kuzidi) ambapo mambo yao ni tofauti kabisa na yale aliyoyasema Yesu mwenyewe TUSISHANGAE WASIPOAMINI KATIKA UTATU HUU. Mimi naweza kuhitimisha kwa kusema kwamba hawa HAWAMWAMINI YESU bali wanaamini DINI YAO. KWA HIYO KUTOKOUAMINI KATIKA UTATU NI MISINGI YA DINI YAO na MSINGI WA BIBLIA NA UKRISTO.

  2. UWEZO WA MUNGU KATIKA KUIFAHAMU BIBLIA
  a. Biblia ni kitabu kinachosomeka kwa LUGHA za BINAADAMU. Kwa sababu hii haihitaji uwezo wa Mungu ili kuifahamu. Kinachotakiwa hapa ni kupata tafsiri sahihi za yale yaliyoandikwa kwenye Biblia. Kuna mambo mengi sana ambayo ni ya Kihistoria kama vile Kutabiriwa kwa Yesu, Kuzaliwa kwake, Mafundisho yake, Kufa na Kufufuka kwake na mengine mengi ambayo maana yake iko kama hivyo yalivyoandikwa. Lakini pia kuna mambo mengi pia ambayo namna ya kutafsiri kwake kunahitaji NGUVU ITOKAYO KATIKA ULIMWENGU WA ROHO. Ni kama vile MANENO YA UNABII YA VITABU MBALI MBALI KATIKA BIBLIA, au Daniel na Yusufu walivyotafsiri NDOTO kwa msaada wa MUNGU. MAMBO HAYA HUWA NI ZIADA YA WALE WALIO KATIKA IMAMI YA KUMWAMINI MUNGU na kwa wakati wetu WANAOMWAMINI MUNGU KUPITIA YESU KRISTO. {Watu wasiomwamini Mungu kupitia Yesu nao pia hupewa nguvu za kiroho kutoka katika ulimwengu wa giza ambao mambo yake ni kinyume na ilivyo kwa wale wanapota nguvu kutoka katika ufalme wa Mungu}. MAMBO HAYO YAKO KATIKA MAFUMBO NA MIFANO AMBAYO KUPATA MAANA YAKE HALISI KUNAHITAJI MSAADA TOKA KWA ALIYEWEKA MAFUMBO HAYO. Ni kama vile wakati Yesu alipokuwa na wanafunzi wake aliwafundisha kwa mafumbo na baadaye kuwatafsiria maana ya mafumbo hayo.
  KWA HIYO KWA MAMBO YA MSINGI YA BIBLIA (ambayo ni kwa ajili ya watu kuwafanya waamini habari za Yesu na Wokovu wake) HAPAHITAJIKI UWEZO WA MUNGU KATIKA KUYAFAHAMU.

  b. Neno la Mungu tayari lilishafunuliwa, Nalo ni hili:
  Titus 2:11-14 For the grace of God that bringeth salvation hath APPEARED TO ALL MEN,Teaching us that, denying ungodliness and worldly lusts, we should live soberly, righteously, and godly, in this present world; Looking for that blessed hope, and the glorious appearing of the great God and our Savior Jesus Christ; Who gave himself for us, that he might redeem us from all iniquity, and purify unto himself a peculiar people, zealous of good works.

  Neno la Mungu kwa wanaadamu ni kwamba Watu Wamwamini Yesu na kumfuata. Na hii ni kwa kila mtu anayetaka. ”Yohana 3:16 – Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanaye wa Pekee ili KILA MTU AMWAMINIYE asipotee, bali awe na Uzima wa Milele.” Hili ndilo NENO la Mungu kwa Wanaadamu. Binaadamu ana hiari ya KUAMINI au KUTOKUAMINI.

  c. WEWE KUWA MMOJA WAO
  Kama nilivyojibu hapo juu kwamba Neno la Mungu na Neema yake vimeshafunuliwa KWA WATU WOTE. WATU ‘WOTE’ NI PAMOJA NA ACHIPETE CHIPAGA! Kwa hiyo ndugu yangu nawe ni mmoja wa wale ambao NENO LA MUNGU LIMESHAFUNULIWA na unasubiriwa ULIAMINI TU!

  d. YESU na NENO la Mungu si kwa ajili ya WAKRISTO. MTU HUFANYIKA MKRISTO BAAYA KUMWAMINI YESU. Mtu hawi Mkristo kwa kuitwa Petero au John bali ni kwa kuishi kwa kumfuata YESU ambaye ndiye KRISTO. MKRISTO MAANA YAKE NI MTU ANAYEISHI KWA KUMFUATA KRISTO. NDIYO maana Yesu akasema SI KILA MTU ANIAMBIAYE BWANA, BWANA, ATAKAYEINGIA KATIKA UFALME WA MBINGUNI; BALI YEYE AFANYAYE MAPENZI YA BABA YANGU WA MBINGUNI – Mathayo 7:21.
  Kufanya mapenzi ya Baba wa Mbinguni ni KUMWAMINI NA KUMFUATA YESU.

  Yesu hakuja kwa ajili ya Wakristo kwa sababu Ukristo haukuwepo kabla ya Yesu. Vivyo hivyo Mtu hawezi kuwa Mkristo pasipo kumwamini Yesu! Kilichokuwepo kabla ya Yesu Kristo ni watu waliishi kwa kufuata TORATI au kwa maneno Mengine sheria ya Musa. Mungu aliyetoa Torati ndiye Mungu aliyemleta Yesu duniani. ”John 1:17 For the law was given by Moses, but grace and truth came by Jesus Christ”. Wakati wa Torati/Sheria ulikwisha sasa ni wakati wa NEEMA mbayo hupatikana kwa kupitia Imani katika Yesu. Mtu akimwamini Yesu huwa juu ya sheria maana nguvu ya kutenda MEMA huwa ndani yake. Hahitaji kutishiwa kwa Sheria ili atende mema. Kwa maneno mengine mtu asiyemwamini Yesu nguvu ya kutenda Maovu iko ndani yake. SHERIA haiwezi kumuondolea mtu nguvu hiyo ya kutenda uovu bali SHERIA KAZI YAKE NI KUHUKUMU.

  Kwa hiyo ndugu Achipete UNASTAHILI KABISA. (Sijajuwa ni kwanini umeuliza hivyo kwamba …..KWA NINI HUSTAHILI?. Kama kuna mtu alikuambia hivyo basi alikudanganya).

  3. CHRISTMASS
  a. Mimi nimendika CHRISTMASS kwa sababu ni Makusanyiko kwa ajili ya CHRIST, Kristo ambaye ni Yesu. X-MASS inaweza kuwa chochote kama vile Y-MASS, Z-MASS!
  -Sikukuu hii husherehekewa kwa Nyakati tofauti kutokana na kutokuwepo kwa kumbukumbu HALISI ya tarehe aliyozaliwa Yesu. Kwa hiyo watu mbali mbali, hasa makundi ya dini, kwa kutumia utaalamu wa kibinaadamu wamejaribu kupanga na kukubaliana kuweka tarehe moja ambayo itakuwa ni siku ya kukumbuka tukio hili la kuzaliwa kwa Yesu. Swala la muhimu hapa ni KUZALIWA KWA YESU na wala SI TAREHE ALIYOZALIWA. HII NI KWA FAIDA YA WANAADAMU WASIJE WAKAABUDU SIKU!

  b. Mimi sifahamu tarehe aliyozaliwa Yesu. Lakini kwenye Biblia inasema katika Luka 1:26 -27 : Mwezi wa Sita Malaika Gabriel alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti. Kwa Mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na Yusufu, wa Mbari ya Daudi, na jina lake bikira huyo ni Mariamu” Habari inayopatikana katika mistari hii na inayofuata baada ya hapo inaelezea jinsi Mariamu alivyoambiwa na Malaika Gabriel jinsi atakavyochukuwa mimba kwa Uwezo wa Roho Mtakatifu.
  Kwa hiyo kwa kawaida ya binaadamu kubeba ujauzito kwa miezi 9, mwezi wa SITA TUKIJUMLISHA MIEZI TISA tunapata kwamba iliangukia mwezi wa TATU.
  KUSHEREHEKEA CHRISTMASS 25/12 ni KUKUMBUKA TUKIO LA KUZALIWA YESU na WALA SI KUKUMBUKA SIKU YA KUZALIWA YESU!

  Hivi ndivyo nilivyoweza kujibu kwa sasa.

  Tuendelee kujifunza.

 263. Bwana Yesu asifiwe!
  Kwanza napenda kuwashukuru sana waanzilishi wa tovuti hii, kwa kutoa nafasi ya kumjua Bwana YESU kwa aliye popote duniani. Huu ni ushindi wa amani na upendo ambao unatafutwa sana duniani, kila kukicha.

  Mwanadamu ni mdadisi, na haachi kujiuliza maswali kwa yale ayasikiayo, ayasomayo, ayaonayo n.k. Mimi nikiwa mmoja ninayo maswali napenda kujua. Majibu mengi yananitoa nje ya imani yangu. Haya ni majaribu makubwa kwangu, na ninafikiri mimi si peke yangu ninayetaka kufahamu.

  Maswali yangu ni .
  1) Nini maana ya UTATU MTAKATIFU? madhehebu mengine kama Mashahidi wa YEHOVA hawaamini katika UTATU. Naomba mnifundishe vema juu ya hili.

  2) Je ni lazima uwe na uwezo wa Mungu ili uifahamu Biblia? Mungu huwafunulia baadhi ya watu kulijua Neno lake? Je mimi si mmoja wapo maana mimi sio Mkristo. Kama si mmoja wapo kwa nini sistahili?

  3) Kwanini X-MASS husherehekewa katika nyakati tofauti? Kwa mfano Katoliki husherekea 25/12 wakati OTHODOX hushrekea 7/1.
  Hivi ni tarehe ipi aliyozaliwa YESU?.

  Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa majibu yenu.

 264. Mpendwa Isara;

  Kwa kuendelea na mjadala; katika kutafakari maneno yako nimeibuka na mambo yafuatayo:

  1. Kusudi la Kristo kufa msalabani ni ili watu WAOKOKE
  2. Wahubiri wa injili wanatumia matangazo yenye msisimko ili kuwaita watu
  3. Watu wa kizazi hiki wanapenda kusikia mambo ya kimwili zaidi
  4. Wahubiri wa injili wa siku hizi wana ajenda za kimwili zaidi kuliko za kiroho
  5. Wahubiri wanalazimika kufuata matakwa ya watu
  6. Watu wenye shida mbali mbali ni WATEJA (ingawa hujasema ni wateja wa nani).
  7. Kwa mtu aliyeokoka kweli kweli matangazo hayo si tatizo.

  Kisha nikapata maswali yafuatayo, ambayo kama utayajibu nitajifunza kitu.

  1. Je, ni sahihi kwa watumishi wa Mungu kufuata watu wanavyotaka badala ya kufuata kweli yenyewe?
  2. Kama kweli wahubiri wa siku hizi wana ajenda za kimwili zaidi kuliko za kiroho, Je, hakuna namna ya kuwasaidia na kuwarejeza kwenye mstari ili wawe na ajenda za kiroho zaidi kuliko kimwili?

  Lakini pia nikatafakari yafuatayo:

  Katika Mathayo 11:20 -24 tunapata habari za Yesu alivyoikemea miji ambayo ndani yake kulifanyika miujiza mingi, miji kama Korazini, Bethsaida na Kapernaumu, lakini watu hawakutubu. Na kuwaambia itakuwa rahisi kwa Tiro, Sidoni na Sodoma kuliko miji hiyo.

  Hivyo kazi moja MUHIMU ya miujiza ni kuwafanya watu waamini uweza wa Jina la Yesu na kwamba ndilo jina tulilopewa wanadamu wa siku zetu ambalo linatupasa kuokolewa kwalo. Na wakishaamini hivi waokoke. Kwa hiyo miujiza kwa jina la Yesu ni uthibitisho kwamba kweli Yesu ndiye Bwana.

  Ni kweli wengi sana wanaokoka kutokana na miujiza hiyo, maana HAKUNA JINA JINGINE AMBALO LAWEZA TAMKWA NA MUUJIZA UKAFANYIKA. Kwa kuwa wengi wanafunguliwa kutoka katika NGUVU ZA GIZA ambazo hawakuweza kupata msaada mahali popote pamoja na dini zao nzuri! Na wanapookoka inakuwa baraka kwao! Lakini wakati wengine wanapokea baraka hiyo wako wengine wanapokea OLE kubwa , kwa maana pamoja na kuona mambo yanayofanyika kwa Jina pekee la Yesu, Bado wanafanya mioyo yao migumu. Hawataki kuamini! Wanaziba Macho, Masikio, Pua ili kukaidi kwa makusudi uthibitisho wa ukweli wa Jina la Yesu. Na hili ni jambo la kusikitisha. Maana Yesu kwa hasira anasema MIUJIZA HII INAYOFANYIKA SASA INGEFANYIKA WAKATI FULANI HUKO NYUMA au sehemu zingine ambako Injili imezuiliwa kabisa, WENGI WANGETUBU NA KUAMINI. Ole wetu tusipoamini!

  Lakini pia si wote wasikiao habari za YESU wanaamini. Kwa wengine ni ushuhuda tu. Ni kufanya watu wakose cha kujitetea mbele za Mungu. Maana kama watu wengine wanaosikia na kuona Yesu anayofanya wanaamini, kwa nini wewe usiamini?

  Kwa hiyo MIUJIZA KWA JINA LA YESU itaendelea! na mapungufu ya kibinaadamu katika kutekeleza hili nayo yataendelea maana ni vita ipo kati ya giza na nuru. Lazima tuvipige vita hivi. Washindao ndio watakaolipwa na Mungu. Ni kwa sababu hii ili HUKUMU YA HAKI ya Mungu iweze kufanyika.

  Amani!

 265. Shalom,
  Mimi naona matangazo ya namna hii kwa nyakati tuishizo ni sahihi KABISA kwa maana akili za watu wa zama hizi ndivyo zinavyotaka kusikia!Sidhani kama utapata watu kwenye mkutano wenye tangazo litakalosema:JE WATAKA KUOKOKA? kwa maana hata watumishi wenyewe wanajua kuwa kimsingi hili ndilo kusudi la Kristo kufa msalabani lakini kwa kuwa wao nao ni watu wa kizazi hiki, wenye ajenda za kimwili kulikoza kiroho, ndo maana wawavutia wateja kwa maneno ya msisimko!!

  Lakini mtu akiwa na mafanikio ya kiroho, matangazo haya si lolote wala chochote kwa maana mtu huyo atakuwa anayajua mawazo ya matangazo hayo….na mwazo ya watangazaji kabla ya kuwaendea!
  Ni vizuri kuokoka kweli kweli……
  Mbarikiwe

 266. MIMI NINACHOJUA NA KILA MTU AJUE HILO; MUNGU WETU NI MWEMA, NI MWAMINIFU, NI MKWELI, NI MZURI, ANA UPENDO, ANA HURUMA, ANA SAMEHE, ANAJALI, ANATULINDA ,ANATUJUA VEMA, ANATUTUNZA, ANATULISHA, ANATUBARIKI ANATUVISHA NAMENGINE MENGI LAKINI NA SISI WENYEWE TUJITAHIDI KUFANYA MAPENZI YAKE I LI NA YEYE AZIDISHE MAPENZI KWETU NA AHADI ZAKE ZITIMIE KWETU AMEN

 267. Wapendwa;

  Hakuna hata wakati mmoja katika historia ya binaadamu ambapo Mungu alituma ujumbe kwa watu na watu wote wakaupokea kwa mikono miwili. Shida hii ilianza tangu mwanzo kabisa katika maisha ya Adamu na Hawa. Mungu alikuwa amewaagiza utaratibu wa kufuata wakiwa katika Bustani ya Edeni lakini walikwenda kinyume nao Mwanzo 3:1-24. Tangu wakati huo hakuna wakati ambao wanadamu waliungana wote kwa pamoja katika kumfuata Mungu. Manabii karibu wote walioandikwa kwenye Biblia kabla ya kuzaliwa Yesu na mitume wa Yesu hawakuwahi kupigiwa makofi na watu wote kwamba wanayosema ni kweli yametoka kwa Mungu. Hata Kristo Yesu mwenyewe wakati wa uhai wake hakuwa akikubaliwa na watu wote. Sasa kama alikataliwa na wengi wakati akiwa hai hakuna la kushangaza kwa sasa, miaka zaidi ya 2000 baadaye, akikataliwa na wengi pia. Sitaweka hapa leo vipingamizi na mateso ambayo kila Nabii alipata wakati akiwa katika kazi ya kuwafikishia watu ujumbe wa Mungu lakini waweza fuatilia katika Biblia na kuona ambavyo watumishi hawa wa Mungu wamekuwa wakipingwa vikali na umati mkubwa wa watu. Wapo wachache sana kama Nabii Yona ambaye alikuwa ametumwa mahsusi kwa ajili ya mji mmoja- Ninawi, ambapo mtawala wa mji ule aliupokea ujumbe huo na kuufanyia kazi na matunda yakaonekana. Soma kitabu chote cha Yona. Narudia tena ni wachache sana wa namna hii na hawa walikuwa wanapewa ujumbe kwa jamii ndogo katika eneo fulani.

  MWENDELEZO WA WACHA MUNGU

  Jambo ambalo liko wazi ni kwamba Watu waliokuwa wacha Mungu walipokezana kutoka kizazi hadi kizazi katika aina hiyo hiyo ya kumcha Mungu huku wakitambuwana kutoka kizazi hadi kizazi. Kizazi kilichokuwa kinafuatia kilikuwa kikirithi au kukumbwa na vipingamizi hivyo hivyo kama ambavyo waliokuwa wametangulia walivyokumbana navyo. Na WATU AMBAO WAMEKUWA WAKITESWA NI WALE WACHA MUNGU WA KWELI. Watu wote walio kinyume na Mungu wa kweli wamekuwa wakiungana kuwatesa na kuwashurutisha Wacha Mungu ili waiache Imani yao. Hakuna wakati ambao wacha Mungu waliungana na kuwatesa wasiomwamini Mungu. Jambo hili la kusikitisha limekuwa likifanyika tangu enzi za kale, kabla kabisa ya Uislamu, na hadi sasa bado linaendelea duniani kote.

  Kwa mfano tu; Tangu enzi za Manabii: Musa, Eliya Mtishbi, Elisha, Isaya, Yeremia na wengine wengi hadi Yohana Mbatizaji, walikutana na vipingamizi vikubwa na mateso mengi na hata kifo katika kufanya kazi ya Mungu. Akaja Yesu mwenyewe naye akakataliwa na kuteswa. Wafuasi wake Yesu, Mitume na watakatifu wengine, wote walikutana na vikwazo vingi na mateso makali na wengi kuuawa. Hadi nyakati zetu hizi wengi wanateswa kwa sababu ya kumwamini Yesu Kristo. Wengi wanafukuzwa nyumbani kwao; wengine wanakataliwa katika ukoo; wengi wanafukuzwa kazini kwa kuwa tu wamempokea Yesu. Na kibaya zaidi wengi wanauawa duniani kote kwa sababu ya kumkubali Yesu. Ndiyo maana ikaandikwa katika Zaburi 34:19 kwamba MATESO YA MWENYE NI HAKI NI MENGI LAKINI BWANA HUMPONYA NAYO YOTE! Kupona kwa mteso haya wakati mwingine ni kuwahishwa kwenda Mbinguni kama ilivyokuwa kwa Stephano aliyepigwa mawe hadi kufa wakati akiwahubiria watu habari Njema za Injili ya Yesu Kristo kwa kuwapa mtiririko wa mpango wa Mungu kuwaokoa wanaadamu kuanzia Abraham akiwa Iraq hadi kuja kwa Yesu. Matendo ya Mitume 7:1-60.

  Yesu Kristo alipokuja duniani alikuja kufunua wazi habari za Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo; Mungu wa Isaya, Jeremia, Daniel nk; ambaye ndiye Mungu Mwenyezi, Muumba wa Mbingu na nchi. Kwa hiyo watu wanaompinga Yesu Kristo WANAFANYA SAWA SAWA NA WATU WALIOWAPINGA MANABII wote wa Mungu. Mtu anayempinga Yesu Kristo ni sawa na kuwa anapingana na manabii wote waliotangulia na wengi kutabiri habari za Yesu. Na kwa kufanya hivyo mtu huyu yuko kinyume na Mungu Mwenyezi! Kwa mfano mtu hawezi sema anamtambuwa Nabii Isaya, aliyetabiri HABARI ZA KUJA KWA YESU NA UMILELE WA UFALME WAKE katika Isaya 7:14 & 9:6-8; akatabiri pia HABARI ZA KUTESWA NA KUFA KWA YESU katika Isaya 53:1-12 na pia Yesu mwenyewe akatumia maandiko kutoka Isaya 61:1-3 alipoyatumia katika Luka 4:18-19, halafu mtu huyo aseme Yesu si mwokozi wa Ulimwengu! Haingii akilini!

  MTUME WA MWISHO?

  Waislamu kila mara nawasikia wakisema Muhammad ndiyo mtume wa mwisho wa Mwenyezi Mungu. Lakini kwa bahati mbaya huwa Sijuwi imeandikwa wapi! Lakini kama nilivyoeleza huko juu kwamba Watakatifu wa Mungu walipokezana aina hiyo hiyo ya Ucha Mungu na Yesu mwenyewe alitambuwa utakatifu wa Ibrahim na mashujaa wengine wa Imani; mfano ktk Luka 16:24-31. Lakini mafundisho ya Quran huwa hayatambuwi mtiririko huo wa watakatifu. Kama ndivyo basi mafundisho hayo yangekubaliana pia na Mpango wa ukombozi kwa ulimwengu ambao Mungu aliuweka ndani ya Yesu Kristo maana Agano lote la Kale limekamilika katika Ujio wa Yesu Kristo. Mafundisho ya Quran ni kitu kipya kinachojitegemea. Rejea zilizoko kwa habari ya Manabii waliotangulia zipo zile za juu juu zisizohusianisha wazi wazi Mtiririko wa Ukombozi kwa wanaadamu. Maneno ambayo yanasikika kwa Waislamu kwamba Yesu si Mwokozi wa Ulimwengu, mara Yesu hakuzikwa, mara wengine waseme hakufa; yanaibua zana mpya ambayo iko kinyume kabisa na Unabii mbali mbali wa Manabii wa Mungu ambao baadhi yao hutambuliwa na Waislamu wenyewe.

  Suala la kuwa Yesu ni Mwokozi wa Ulimwengu halipingiki, Isaya 53:10; Mathayo 1:21. Pia suala kwamba baada ya Yesu hakuna mkombozi mwingine halipingiki, Isaya 9:7; Mathayo 24:35; Matendo 1:11. Kwa hiyo kwamba kuna Mtume mwingine wa mwisho, yaani baada ya Yesu, (ingawa Yesu si mtume bali ndiye njia ya kwenda kwa Mungu) ni kinyume kabisa na Biblia na wala siyo mwendelezo wa habari za Manabii wa Mungu walionenwa katika Biblia.

  VITA YA UISLAMU KWA UKRISTO

  Chuki ya Uislam kwa Ukristo imechochewa na chuki ya Waarabu kwa Wayahudi. Vita ya Waislamu kwa Wakristo si vita kwa ajili ya dhambi. Ni vita ya Ukabila. Hata mafundisho mengi yatolewayo misikitini hutolewa mifano mingi mibaya, kama si yote, kwa Wayahudi. Niliambiwa na Muislam fulani kwamba Wayahudi wana wivu kwa Waarabu sababu Mtume wa mwisho katokea kwa Waarabu ndiyo maana wanaupiga vita Uislamu. Lakini ukifuatilia utakuta hakuna mtu aliyeteswa/kuuawa kwa sababu kaukataa Ukristo lakini hebu fikiria maelfu wanaouawa kwa sababu wameukataa Uislamu. Kwa hiyo kwa hali halisi ni Uislamu ndiyo unaupiga vita Ukristo! Ni vita juu ya wacha Mungu wa kweli! (Nimeeleza huko juu).

  Sasa nataka twende pamoja kwenye Ugomvi kati ya Waarabu na Wayahudi (au Israel). Suala hili ni la Ki-Biblia. Katika Mwanzo 16:12 tunapata habari za Ishmaeli (Baba wa Waarabu ambaye alizaa Maseyidi 12) alizotabiriwa kwamba :And (Ishmael) he will be a wild man; his hand will be against every man, and every man’s hand against him; and he shall dwell in the presence of all his brethren. Wakati wana wa Israel wanarudi kuja kuchukuwa nchi ya ahadi waliambiwa na Mungu kuwaangamiza wenyeji wote wa Kaanani, maeneo ya Yordani, Jeriko na kuzunguka sehemu hizo, bali wasipowaondoa WATAKUWA KAMA SINDANO MACHONI NA KAMA MIIBA UBAVUNI; Hesabu 33:55. Wana wa Israel hawakuweza kuwaondoa wenyeji wote wa miji ile. Wenyeji waliokuwa katika nchi hiyo ni kizazi cha Ishmaeli, Waarabu. Hivyo Ukorofi wa Waarabu kwa Israel ulitabiriwa ni maandiko yanatimia.

  Kwa hiyo Waarabu wanapoupiga vita Ukristo kwa hali halisi wao huwapiga vita Wayahudi. Na kwa Kristo alizaliwa Israel, Waarabu wanapowapiga Wayahudi hufikiri wanaupiga vita Ukristo. Na kwa bahati mbaya pia Waislamu ambao si waarabu wanapoupiga vita Ukristo hufikiri wanawasaidia Waarabu kuwashambulia Wayahudi kwa sababu Kristo alizaliwa Uyahudi. Lakini Mtu ambaye ni mpagani, asiye na dini, hana ugomvi wowote na Uislamu na ndivyo ilivyo kwa mtu wa dini yoyote isiyo ya Kikristo. Tatizo huja tu mtu anaposema yeye anamwamini Yesu Kristo. Hali hii pia imeingiliana sana na Imani ya Kiislamu kiasi cha kuona kwamba mtu mwenye ugonvi na mwarabu au nchi yoyote yenye ugomvi na nchi yoyote ya kiarabu basi ugonvi huo hutafsiriwa kama vita juu ya uislamu.

  KWA TAARIFA: Adui wa Ukristo si Uislamu bali ni DHAMBI na DHAMBI ni adui wa wanaadamu wote. Kristo Yesu alikuja duniani ili kuwaokoa watu kutoka dhambini, si kutoka katika Uislamu. Yesu alikuja kwa watu wa mataifa yote, kabila zote, lugha zote na jamaa zote. Jambo la kutia moyo hapa ni kwamba WAARABU WENGI WANAMPOKEA YESU SASA japo wana mateso mengi. Kila amwaniye Yesu hatapotea bali ana uzima wa Milele, Yohana 3:16. Na kwa kuwa Mungu ni mwaminifu Waarabu hawa wanaomwamini Yesu wanajihakikishia kuishi milele na Yesu mbinguni.

  Yesu ni mwokozi wa Ulimwengu!

 268. NAMIMI NAGONGOMELEA VIGONGO VYANGU HAPO HAPO JAPO SIJA SOMA MJADALA WOTE ILA NAWEZA KUELEWA NINI KINACHO. KATIKA HALI YA KAWAIDA TU YAKUFIKIRIKA HEBU WACHUKUE MITUME NA MANABII WOTE DUNIANI HARAFU PIMA MAISHA YAO PAMOJA NAKAZI WALIZO ZIFANYA HARAFU PIMA NANI ZAIDI. ANZIA KUZALIWA KWAO NANI KATI YA MITUME NA MANABII ALITABILIWA KUJA KUWAKOMBOA WANADAMU? AU NANI ALIZALIWA KWA UWEZA WA MAAJABU? YAANI MTOTO KUZALIWA NA MWANAMKE TU BILA MWANAUME?MTOTO GANI ALIKUWA NA UWEZO WA KUWAULIZA WAKUFUNZI WAKE MASWALI MAGUMU MPAKA WAKA KUNA VICHWA? NANI ALITEMBEA JUU YA MAJI? NANI ALIWEZA KULISHA MAELFU YA WATU SAMAKI WATANO NA MIKATE MIWILI WATU WAKALA MAPAKA WAKA SAZA?NANI ALIWAHI KUFUFUA MTU? NANI ALIWAHI KUWASAMEHE MAADUI ZAKE?NANI ALIWAHI KUJIITA YEYE NI NJIA KWELI NA UZIMA NA AKAISHI
  AKISEMA UKWELI? NANI ALIWAHI KULIA MPAKA MACHOZI YAKAWA DAMU?NANI HAKUWAHI KUWANYANYAPAA MAKAHABA AU WENYE DHAMBI NANI ALIKUFA AKAZIKWA HARAFU AKAFUFUKA?NANI UKIMTAJA JINA LAKE TU SHETANI NA MAPEPO WANAKANYAGANA?NANI HAKUTENDA DHAMBI HATA KIDOGO?
  SASA WAWEKE WOTE MITUME NA MANABII UNAO WAFAHAMU,WAWE
  WAKRISTO, WAISLAMU,BUDHA,BAHAI,DINI ZA ASILI,HINDU, YAAANI WOTE HARAFU PIMA NANI ZAIDI? NAJUA UMESHAMJUA SIRI YAKO HATA MIMI USINIAMBIE MKUBALI KIMOYO MOYO

 269. Ndugu Dominick,
  Nimesoma kwa haraka sana ulichoandika na nitasoma tena kwa undani nikipata muda. Hivi ni vitu vichache ambavyo nimevipata kwa sasa (Kama sivyo ulivyosema unaweza kunisahihisha)

  Nukuu:
  “Kama tulivyoona itikadi ya utatu mtakatifu haina uhusiano kabisa na Mwenyezi Mungu, Mitume wake wala wafuasi wa Mitume.”

  Hilo si kweli! Nafahamu watu wengi hasa waislamu hujaribu kusema kwamba Constantine alianzisha utaratibu wa Yesu ni mungu na kwamba imani ya Mungu na nafsi zake tatu ilitokea Nikea, kitu ambacho ni Uongo halisi, usio na chembe ya ukweli!

  Katika hili la utatu, nitathibitisha kwamba, vyanzo vyote vya kihistoria, vya karne ya kwanza, vinaonyesha walimwabudu Mungu aliye na nafsi tatu, Yaani Mungu Baba, Yesu Kristo(Mungu Mwana), na Mungu Roho Mtakatifu. Katika Agano la kale na jipya, Mungu ametajwa na nafsi zake tatu na kwa sababu ya Muda mfupi nili nao hapa, nitathibitisha kwamba Quran, document ya Karne ya Saba, haiwezi kamwe kuwa kithibitisho cha kuishushua Biblia, iliyojaa mashahidi walioshuhudia kwa macho yote yaliyotokea. Kwa sababu hiyo basi,sitatumia biblia (Ambayo wapinga Ukristo husema imebadilishwa), bali document za kihistoria, na kuthibitisha nani Mwongo kati ya Mungu wa biblia na mungu wa koran

  Shuhuda wa kwanza ni mwanahistoria wa kiyahudi aliyekuwa si mfuasi wa Yesu; Josephus Flavius. Kama hujawahi kumsikia hapa ni maelezo kwa kifupi:

  Josephus (AD 37 – c. 100),[1] also known as Yosef Ben Matityahu (Joseph, son of Matthias) and, after he became a Roman citizen, as Titus Flavius Josephus,[2] was a first century Jewish historian and apologist of priestly and royal ancestry who survived and recorded the destruction of Jerusalem in AD 70. His works give an important insight into first-century Judaism.
  Josephus’s two most important works are The Jewish War (c. 75) and Antiquities of the Jews (c. 94).[3] The Jewish War recounts the Jewish revolt against Rome (66-70). Antiquities of the Jews recounts the history of the world from a Jewish perspective. These works provide valuable insight into the background of first century Judaism and early Christianity.[3]

  Now there was about this time Jesus, a wise man, if it be lawful to call him a man; for he was a doer of wonderful works, a teacher of such men as receive the truth with pleasure. He drew over to him both many of the Jews and many of the Gentiles. He was [the] Christ. And when Pilate, at the suggestion of the principal men amongst us, had condemned him to the cross, (9) those that loved him at the first did not forsake him; for he appeared to them alive again the third day; (10) as the divine prophets had foretold these and ten thousand other wonderful things concerning him. And the tribe of Christians, so named from him, are not extinct at this day. (The Antiquities of Jews: Book XVIII Chapter 3:3 From The Works of Flavius Josephus Translated by William Whiston )

  Hapa Tunaona Document iliyoandikwa na Josephus aliyekuwa si mfuasi wa Yesu, akikiri kufa na kufufuka kwa Yesu. Kufufuka kwa Yesu, ndio uthibitisho mkuu zaidi ya kuwa hakuwa mwanadamu bali Mungu pamoja nasi! Hii document inaonesha Uongo wa mungu wa koran, kwa kuwa angalikuwa ni Mungu wa kweli asingesema Yesu hakufa ilhali walioshuhudia wanasema alikufa na kufufuka!

  Tacitus, ni mwanahistoria na shahidi namba mbili wa kesi hii: Kama hujui juu ya mwana historia huyu, haya ni maelezo:

  Publius (or Gaius) Cornelius Tacitus (ca. 56 – ca. 117) was a senator and a historian of the Roman Empire. The surviving portions of his two major works—the Annals and the Histories—examine the reigns of the Roman Emperors Tiberius, Claudius, Nero and those that reigned in the Year of the Four Emperors. These two works span the history of the Roman Empire from the death of Augustus in AD 14 to (presumably) the death of emperor Domitian in AD 96. There are significant lacunae in the surviving texts.

  Other works by Tacitus discuss oratory (in dialogue format, see Dialogus de oratoribus), Germania (in De origine et situ Germanorum), and biographical notes about his father-in-law Agricola, primarily during his campaign in Britannia (see De vita et moribus Iulii Agricolae).

  An author writing in the latter part of the Silver Age of Latin literature, his work is distinguished by a boldness and sharpness of wit, and a compact and sometimes unconventional use of Latin.

  Tusikie sasa Tacitus anasema nini juu ya hili:
  Consequently, to get rid of the report, Nero fastened the guilt and inflicted the most exquisite tortures on a class hated for their abominations, called Christians by the populace. Christus, from whom the name had its origin, suffered the extreme penalty during the reign of Tiberius at the hands of one of our procurators, Pontius Pilatus, and a most mischievous superstition, thus checked for the moment, again broke out not only in Judaea, the first source of the evil, but even in Rome, where all things hideous and shameful from every part of the world find their centre and become popular. Accordingly, an arrest was first made of all who pleaded guilty; then, upon their information, an immense multitude was convicted, not so much of the crime of firing the city, as of hatred against mankind. Mockery of every sort was added to their deaths. Covered with the skins of beasts, they were torn by dogs and perished, or were nailed to crosses, or were doomed to the flames and burnt, to serve as a nightly illumination, when daylight had expired. (Tacitus, Annals 15.44, translated by Church and Brodribb.)

  Hapa tena ushahidi Juu ya kifo cha Yesu, kutoka kwa mtu ambaye si mkristo na hakuwa anaelezea specific juu ya kifo cha Yesu. Hapa tena korani inapingana na historia na mashahidi walioona.

  Wa mwisho, kwa sasa, atakuwa Pliny the Younger:
  Kama ulikuwa humjui haya ni maelezo kwa ufupi:

  Gaius Plinius Caecilius Secundus, born Gaius Caecilius or Gaius Caecilius Cilo (61/63 – ca. 113), better known as Pliny the Younger, was a lawyer, author, and natural philosopher of Ancient Rome. Pliny’s uncle, Pliny the Elder, helped raise and educate him and they were both witnesses to the eruption of Vesuvius on August 24th, 79 AD.

  Hii ni Barua aliyomwandikia mfalme Trajan, alivyochanganyikiwa na jinsi gani awahukumu wakristo. Hii ilikuwa yapata kama mwaka 112 AD.

  Sir,

  It is my constant method to apply myself to you for the resolution of all my doubts; for who can better govern my dilatory way of proceeding or instruct my ignorance? I have never been present at the examination of the Christians [by others], on which account I am unacquainted with what uses to be inquired into, and what, and how far they used to be punished; nor are my doubts small, whether there be not a distinction to be made between the ages [of the accused]? and whether tender youth ought to have the same punishment with strong men? Whether there be not room for pardon upon repentance?” or whether it may not be an advantage to one that had been a Christian, that he has forsaken Christianity? Whether the bare name, without any crimes besides, or the crimes adhering to that name, be to be punished? In the meantime, I have taken this course about those who have been brought before me as Christians. I asked them whether they were Christians or not? If they confessed that they were Christians, I asked them again, and a third time, intermixing threatenings with the questions. If they persevered in their confession, I ordered them to be executed; for I did not doubt but, let their confession be of any sort whatsoever, this positiveness and inflexible obstinacy deserved to be punished. There have been some of this mad sect whom I took notice of in particular as Roman citizens, that they might be sent to that city. After some time, as is usual in such examinations, the crime spread itself and many more cases came before me. A libel was sent to me, though without an author, containing many names [of persons accused]. These denied that they were Christians now, or ever had been. They called upon the gods, and supplicated to your image, which I caused to be brought to me for that purpose, with frankincense and wine; they also cursed Christ; none of which things, it is said, can any of those that are ready Christians be compelled to do; so I thought fit to let them go. Others of them that were named in the libel, said they were Christians, but presently denied it again; that indeed they had been Christians, but had ceased to be so, some three years, some many more; and one there was that said he had not been so these twenty years. All these worshipped your image, and the images of our gods; these also cursed Christ. However, they assured me that the main of their fault, or of their mistake was this:-That they were wont, on a stated day, to meet together before it was light, and to sing a hymn to Christ, as to a god, alternately; and to oblige themselves by a sacrament [or oath], not to do anything that was ill: but that they would commit no theft, or pilfering, or adultery; that they would not break their promises, or deny what was deposited with them, when it was required back again; after which it was their custom to depart, and to meet again at a common but innocent meal, which they had left off upon that edict which I published at your command, and wherein I had forbidden any such conventicles. These examinations made me think it necessary to inquire by torments what the truth was; which I did of two servant maids, who were called Deaconesses: but still I discovered no more than that they were addicted to a bad and to an extravagant superstition. Hereupon I have put off any further examinations, and have recourse to you, for the affair seems to be well worth consultation, especially on account of the number of those that are in danger; for there are many of every age, of every rank, and of both sexes, who are now and hereafter likely to be called to account, and to be in danger; for this superstition is spread like a contagion, not only into cities and towns, but into country villages also, which yet there is reason to hope may be stopped and corrected. To be sure, the temples, which were almost forsaken, begin already to be frequented; and the holy solemnities, which were long intermitted, begin to be revived. The sacrifices begin to sell well everywhere, of which very few purchasers had of late appeared; whereby it is easy to suppose how great a multitude of men may be amended, if place for repentance be admitted.

  Kama umesoma vyema, utaona kuna sehemu bwana Pliny anasema hivi:
  “on a stated day, to meet together before it was light, and to sing a hymn to Christ, as to a god”

  Kwa hiyo Wakristo wa Mwanzo, mamia ya Miaka kabla ya Nikea walimwabudu Yesu kama Mungu. Hapa Korani imekosea na mtu rational hawezi kuamini Mungu anakosea. Haya yote Yako 100% katika makubaliano na Biblia.

  Yesu ni Mungu sawa na ilivyo kwa Baba na Roho. Nikea ilikutana ili kupambana na mafundisho ya Arian ambayo corrupted version yake ni Uislam. Mashahidi wametoa ushahidi wao, nami naamini kila mtu ananhitaji kuamua mwenyewe kama afuate biblia au Koran.

  Mbarikiwe na Yesu!
  Mtume wa Yesu

 270. SHALOM, WAPENDWA KATIKA KRISTO YESU!.

  Mpendwa Dominik Mzirai,
  Nimefuatilia makala yako, inayoelezea juu ya miujiza inayofanywa na baadhi ya Watumishi wa Mungu wa nyakati hizi. Umejitahidi kuelezea kwa mapana na marefu ili kila mmoja aweze kukuelewa, na umehitimisha kwa kusema kuwa, japo miujiza hiyo inawasaidia baadhi ya watu waache madhambi ya kimwili, lakini inawang`ang`aniza wafanye dhambi kubwa sana ya kiroho yaani dhambi potofu juu ya mwenyezi Mungu na kumkataa Roho Mtakatifu.

  Kutokana na hilo, nami nimeona nitoe mchango wangu kadiri ninavyofahamu juu ya jambo hili kama ifuatavyo:-

  Juu ya miujiza, mimi ninavyofahamu ni kwamba miujiza ni mpango wa Mungu kabisa, na Mungu ameuweka mpango huo ili kuwavuta watu waje kwake. Yesu Kristo kwa nyakati zake, kusingekuwa na miujiza ni wachache ambao wangemwendea Yesu na kumwamini. Lakini kwa sababu ya miujiza, watu wengi walimwendea ili kupata uponyaji, na Yesu aliwaponya na kuwahubiria Neno lake na hatimaye wakaokolewa. Ndiyo maana alisema, “…..mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele (Yoh.10:10). Uzima anaouzungumzia mwanzo ni uzima wa mwili na uzima anaozungumzia mara ya pili, yaani uzima tele, ni uzima wa mbinguni ambao ni wa milele. Hivyo alikuja ili tuwe wazima wa mwili na uzima wa milele mbinguni iwapo tutampokea. Kwa mantiki hiyo, tukiokolewa na tukikaa ndani yake, hata magonjwa kwetu yatakuwa mbali nasi kwa sababu ni mpango wake na ndivyo alivyosema.

  Kuhusu uponyaji, kabla ya kuondoka hapa duniani, Yesu Kristo aliacha maagizo kupitia watumishi wake wa Mungu wa nyakati hizo katika kitabu cha, (Marko 16:18…..wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya). Pia Yesu Kristo alisema kuwa ishara hizo za kuponya wagonjwa zitafuatana na hao watakaokuwa wanamwamini, kwa jina lake (Yesu) watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya. (Marko 16:17).

  Hivyo, miujiza kwa watu wa Mungu kwa mujibu wa maandiko tunaona ni mpango wa Mungu kabisa. Ndiyo maana hata nyakati hizo za biblia wanafunzi sabini waliotumwa kutenda kazi ya Bwana walirudi kwa furaha wakisema Bwana hata pepo wanatutii kwa jina lako, (Luka 10:17). Hivyo, Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele, (Waebrania 13:8).

  Hivyo hata nyakati hizi tulizonazo, kama hakutakuwa na miujiza, wengi watakwenda motoni kwa sababu hawataokolewa kwa misingi ya kushikwa na dini, kama ilivyokuwa nyakati za mafarisayo. Mimi mwenyewe bila miujiza nisingeujua wokovu, nilikwenda kwa walokole baada ya kuzidiwa na magonjwa yaliyokaribia kunimaliza. Sikwenda kwa ajili ya kuokoka, kwa sababu nilisema ninayo dini yangu ambayo niliamini kuwa ndiyo ya kweli kuliko dini zote. Baada ya kufika kule, nilielezwa juu ya dhambi na nikajikuta sifai kabisa japo nilikuwa na dini, hii ilinipelekea kuokoka!

  Kuna andiko, ambalo wengi hulitumia wakimaanisha kuwa, miujiza siyo mpango wa Mungu, wanatumia andiko katika Mathayo 7:22 linalosema ,…Bwana, Bwaba, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu ninyi mtendao maovu).

  Ni muhimu kufahamu kuwa nyakati hizi tulizonazo maandiko yalishasema kuwa watatokea manabii wa uwongo, (Mtathayo 24:24-25 Kwa maana watatokea makristo wa uwongo, na manabii wa uwongo nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini hata waliowateule. Tazama nimekwisha kuwaonya mbele).

  Sasa, manabii au hao makristo wa uwongo tutawatambuaje? Luka 6:44 kwa kuwa kila mti hutambulikana kwa matunda yake; maana katika miiba hawavuni tini, wala katika michongoma hawachumi mizabibu. Mathayo 12:33 Ufanyeni mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri;au ufanyeni mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, KWA MAANA KWA MATUNDA YAKE MTI HUTAMBULIKA!.

  Mtumishi wa Mungu, anapohubiri, matunda tunayotakiwa kuyatazama ni watu anaowahubiria, kwamba je wanaacha dhambi na kuishi maisha ya utakatifu? Wanaacha uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugimvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevu, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo kama ilivyo katika Wagalatia 5:19-21? Je wanaelewa maana ya Roho Mtakatifu na kujazwa nguvu zake, kama maandiko yasemavyo katika (Matendo 2:4, 8:17?). Katika “Yoh. 4:24 maandiko yanasema “Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli, “.

  Hivyo, ili kuweza kuthibitisha kuwa huyu ni mtumishi wa Mungu, mtumishi huyo bila shaka lazima tumwangalie matunda anayozalisha, ambayo ni watu anaowahubiria kwamba wakoje. Kama ni miujiza tu, hata Farao naye anayo miujiza, Musa na haruni waligeuza maji kuwa damu kumkomesha Farao, na waganga wa Farao wakafanya mambo KWA MFANO WA HAYO, (Kutoka 7:19-22). Kimsingi miujiza ya watu wanaodhaniwa kuwa ni watumishi wa Mungu, mingine ni ya kweli, kwa sababu Mungu analithibitisha Neno lake; Mtu akisema “Kwa jina la Yesu Kristo pepo toka” Kwa vile Yesu Kristo mwenyewe alishasema, kwa Jina lake tutatoa pepo, basi hana budi kutimiza andiko, hata kama anayesema maneno hayo si mtu wake. Kuna miujiza mingine, haihusiani kabisa na Bwana Yesu, inafanyika tu kwa sababu ya roho za upotevu, na watu wanaiamini na kudhani kuwa inatoka kwa Mungu, lakini siyo. (2Wathesolanike 2:9-11 …kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uwongo;10 – na katika madanyanyo yote ya udhalimu, kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa. ….Mungu aliwaletea nguvu ya upotevu, WAUAMINI UWONGO).

  Msingi mkubwa wa kufika mbinguni, ni kutubu dhambi zetu kwa Jina la Yesu Kristo kwa kumaanisha kuziacha, na kupata wokovu. Yesu Kristo alikuja KUTAFUTA na KUOKOA KILE KILICHOPOTEA AMBACHO NI MIMI NA WEWE! LK. 19:10

  Shalom watu wa Mungu!

 271. Miujiza mbali mbali huwafanya watu wengi warukeruke mara kwa mara toka dini moja kwenda nyingine au dhehebu moja kwenda lingine. Baadhi ya wahubiri wamekuwa wakitumia mazingaombwe ya uponyaji kama chambo cha kuwania waumini kwa wingi bila jasho. Lakini je “miujiza” ndio inathibitisha ukweli na usahihi wa dini au dhehebu?

  Ili kujibu kwa ufasaha swali hilo, inabidi tuangalie vitu vitatu vifuatavyo: (i) Miujiza ni nini, na kwa nini ipo? (2) Usahihi wa dini au dhehebu ni nini (3) Uhalali wa miujiza inayofanywa na baadhi ya Wakristo. Hapa tuzingatie kuwa, tutazungumzia miujiza ya Wakristo, sio ya Mtume Yesu (a.s.) wala wafuasi wake wa mwanzo. Miujiza ya Mtume Yesu (a.s.) na wafuasi wake wa awali ni halali moja kwa moja na hauna utata wowote.

  Miujiza ni nini?

  Miujiza ni kitendo au tukio lisilo la kawaida kwa mujibu wa maumbile ya kawaida. Zipo sababu mbili tofauti za Mwenyezi Mungu (s.w.) kuruhusu miujiza. Ya kwanza ni kuonyesha nguvu na uwezo wake mkuu ili watu wameuamini yeye pamoja na Mitume, Manabii au watu wake aliowateua kwa makusudi maalum. Tazama kutoka 20:18-20, Yohana 14:1-11 n.k. Sababu ya pili iliyotofauti kabisa na hiyo ya mwanzo ni hii ifuatayo: “Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu, ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, “Na tuifuate miungu mingine USIOIJUA, tuitumikie hiyo; wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto; kwa kuwa Bwana Mungu wenu, YU AWAJARIBU, apate kujua kwamba mwampenda Bwana Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote. Tembeeni kwa kumfuata Bwana Mungu wenu, mcheni na kushika maagizo yake, na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye. Na yule nabii, au yule mwotaji wa ndoto, na auawe, kwa kuwa amesema yaliyopotoka juu ya Bwana Mungu wenu, aliyewatoa katika nchi ya Misri, akakukomboa katika nyumba ya utumwa, apate yule mtu kukupotoa katika njia aliyokuamuru Bwana Mungu wako, uiendee. Ndivyo utakavyouondoa uovu utoke katikati yako. “(Kumbukumbu la Torati 13:1-5). Hivyo sababu ya pili ni mtihani toka kwa Mwenyezi Mungu ili tuthibitishe utii wetu na kutoyumbayumba tukiona vitu visivyo vya kawaida vikifanywa na watu wanaojiita “watumishi wa Mungu” wakati wanaenda kinyume na Mwenyezi Mungu.

  Usahihi wa Dini

  Usahihi au uhalali wa mhubiri wa Mwenyezi Mungu, unafafanuliwa vizuri na Wanatheolojia. Wanasema, “18:21 Wayahudi walihangaika kubaini Manabii wa kweli na wa uongo (Taz.1 Fal 22; Yer.28). Alama ni hizi, Nabii wa kweli hufuata kiaminifu mafundisho ya Bwana (s.13), tena ukurasa 159). Wakifafanua zaidi wanasema “Alama ya mwalimu wa kweli ni kwamba afundisha yale yaliyopokewa na Mitume. Yohana awaonya wasisadiki hadithi za walimu wa uongo (1 Yoh 2:18 n.k. Tit 3:9; Tim 2:16)” Biblia Takatifu Tabora Uk. 1119. Ili kuwasaidia wale wasomaji wasiotaka kusikia neno “Wanatheolojia” maneno hayo ya wanatheologia ni ufafanuzi wa maneno ya Biblia yafuatayo:” “kila apitaye cheo, wala asidumu katika mafundisho ya Kristo, yeye hana Mungu. Yeye adumuye katika mafundisho hayo, huyo ana Baba na Mwana pia. Mtu akija kwenu naye haleti mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani mwenu, wala msimpe salamu. Yeye ampaye salamu azishiriki kazi zake mbovu”. (1 Yohana aya 9-11).

  Hapo tumeona kuwa, mhubiri wa kweli ni yule anayefuata mafundisho sahihi toka kwa Mwenyezi Mungu na Mitume au Manabii wake, kisha akafundisha mafundisho yatokayo kwa Mwenyezi Mungu na Mitume wake. Mafundisho ya Mwenyezi Mungu ni mengi. Yapo makubwa na madogo. Makubwa hayabadiliki kabisa tangu zamani. Mafundisho makuu ni tafsiri ya uungu wa Mwenyezi Mungu (s.w.), kuamini Mitume na Manabii wake, kuamini Malaika zake, kuamini Maandishi yake (vitabu, vyaraka n.k.), kuamini siku ya mwisho (kiyama) na kuamini kuwa, uendeshaji wa dunia, mbingu na vilivyomo (Qadari), uko mikononi mwa Mwenyezi Mungu (S.W.). Mafundisho madogo yanayobadilika kulingana na mazingira ni kama utekelezaji wa ibada (rituals), sheria ndogondogo, hukumu za makosa n.k.

  Fundisho lililo kuu kuliko yote ni tafsiri ya Mwenyezi Mungu Mwenyewe. Hili ndilo fundisho kuu la kwanza kabisa kuandikwa katika kitabu rasmi cha Mwenyezi Mungu (Torati). “Mungu akanena maneno haya yote akasema.Mimi ni Bwana, Mungu wako; niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. USIWE NA MIUNGU MINGINE ILA MIMI” (kutoka 20:1-2). Kutokana na uzito wa fundisho hili, kinaitwa kwa Kiebrania “Shema” ((Tazama Kumb. 6:4, na Marko 12:28-20), na wanafundishwa watoto wa Kiebrania waweze kulitamka kabla ya kusema “Baba” na “Mama”. “Shema” inaanza na “sikia eeh Israel……”. Mitume na Manabii wote kabla ya kufundisha lolote, walihimiza na kusisitiza hilo (Taz. Isaya 45:21-23 n.k. Mtume Yesu (a.s.) naye anasema “Na uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma (Mtume)”. (Yohana 17:3). Paulo naye akisisitiza upweke wa Mwenyezi Mungu anasema: “Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanaadamu ni mmoja, mwanaadamu Kristo Yesu” (1 Timotheo 2:5). Hivyo mhubiri yeyote, ajiite vyovyote atakavyojiita, akifundisha tafsiri ya Mwenyezi Mungu kinyume na hiyo ya Mitume, Manabii na wafuasi wa Manabii (Paulo), atakuwa anafundisha na kufuata miungu migeni. “Kukizuka kati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu, ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia, akisema, Na tuifuate miungu mingine usioijua, tuitumikie hiyo; wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au mwotaji wa ndoto; kwa kuwa Bwana Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda Bwana Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zetu zote.” (Kumb. 13:1-3).

  Uhalali wa miujiza ya Wakristo

  Kama tulivyokwisha ona, ili miujiza iwe halali yenye kuthibitisha utukufu wa Mwenyezi Mungu (s.w.), lazima mfanya miujiza (Mhubiri) awe mfuasi wa dini yenye mafundisho sahihi ya Mwenyezi Mungu hasa upweke wa Mwenyezi Mungu, na afundishe mafundisho sahihi yanayotokana na vyanzo halali (Mwenyezi Mungu na Mitume wake).

  Ili tujue kama miujiza ya uponyaji inayofanywa na baadhi ya wahubiri wa Kikristo ni halali au la itabidi tuangalie kwa ufupi historia ya fundisho kuu sana la Mwenyezi Mungu, kwa mujibu wa tafsiri ya dini ya Kikristo. Yaani Mungu moja mwenye nafasi tatu, za Mungu Baba (Mwenyezi Mungu), Mungu Mwana (Yesu) na Mungu Roho Mtakatifu. Kabla ya kuona historia hiyo, tuangalie kwanza Mtume Yesu (a.s.) anasemaje kuhusu wafanya miujiza wanaofuata na kufundisha mafundisho potofu Anasema “kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule”. (Mathayo 24:24). Na kwa wale wahubiri watakaofanya miujiza kwa jina la Yesu ili kuwapotosha watu, anasema “Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali. Mtawatambua kwa matunda yao (mafundisho). Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? Vivyo hivyo kila mti (Mhubiri) mwema huzaa (hufundisha) matunda (mafundisho) mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya. Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. Ndipo sasa kwa matunda (mafundisho) yao mtawatambua. Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana atakayeingia katika ufalme wa mbinguni. Wengi wataniambia siku ile (kiyama), Bwana, Bwana hatukufanya unabii kwa jina lako, na jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawambia dhahiri, sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendapo maovu (kupotosha watu)” (Mathayo 7:15-23).

  Kwa kuwa Mchungaji A.T. Manoni ameshaeleza kwa ufasaha sana historia ya itikadi ya utatu (Tazama AN-NUUR Na. 158 Uk. 11), mimi nitaeleza kwa ufupi sana. Mara baada ya Mtume Yesu (a.s.) kuondoka, Wapagani waliokubali Ukristo walizusha itikadi za Wanikolai (Taz. ufunuo 2:6) ambao waliukubali Ukristo lakini waliendelea na matambiko yao waliyoyapa sura ya Ukristo. Na walikuwepo Wagnostik walioamini kuwa Mwenyezi Mungu (Yahwe) ni Mungu Muumba aitwaye “Demiurgos” (mtenda kazi). Lakini yupo Mungu mwingine mkubwa zaidi yake. Hatimaye waliibuka Waamontanist wafuasi wa Montano aliyekuwa kuhani wa Mungu wa Kipagani “Cybele”. Hatimaye aliibuka Manes Mmedi na wafuasi wake waitwao Wamanikayo. Yeye alisema ndiye paracretos aliyetabiriwa na Yesu (Yohana 16:7-16). Hayo ni baadhi ya madhehebu ya Wakristo toka Upagani. Lakini pia kulikuwepo na madhehebu ya Wakristo wa Kiyahudi ya Ebionites (maskini) na Essene Ebionites (Watawa – Mamonaki) yaliyokuwa yameshika sana torati.

  Ili nifupishe makala hii, naona niachane na hayo madhehebu mengine yaliyokuwa na itikadi ambazo hivi sasa hazipo, niingilie itikadi hii ya utatu iliyodumu hadi sasa. Itikadi ya Mungu Mwenye nafsi tatu haikuanza ghafla kama watu wengi wanavyofikiria. Itikadi hii ilianza kipengele kwa kipengele. Alianzisha rasmi mtakatifu Yustino ajulikanaye sana kwa jina Yustino Shahidi (Justine Martx) aliyeuwawa mwaka 165 B.K. Yeye aliposoma Mithali 8:1-36 hasa aya ya 2-31 alipoyachanganya maneno ya Yohana 1:1-14, akafasiri kuwa, “hekima” ndiye “Neno” na ni sehemu (nafsi) ya Mwenyezi Mungu mmoja. Na kuwa nafasi hiyo ni Yesu. Hivyo neno la Kigiriki “Homo-ousios” yaani Baba ni sawa na Mwana, akimaanisha kuwa Yesu ni Mungu sawa na Mwenyezi Mungu likaanza kufundishwa rasmi.

  Fundisho hilo lilipoanza kukolea, Askofu Paulo wa Samosata wa Antiokia tangu 260-2709 BK, alilipinga vikali. Hatimaye neno “Homo-ousios” lilipigwa marufuku katika mkutano wa kanisa uliofanyika antiokia mwaka 270 BK, japo askofu Paulo alifukuzwa Uaskofu. Hata hivyo liliendelea kufundishwa na likaimarika zaidi na zaidi. Hatimaye kasisi (Padre) Ario (Areus) wa Mtaa wa Boucalis katika jimbo la Alexandria (Misri), (aliyezaliwa mwaka 250 BK na kufa 336 BK), alipinga vikali sana neno hilo na akaanzisha dhehebu la Waario. Mzozo ulikuwa mkubwa sana hadi ikabidi kaisari (mfalme) Constantino aitishe mkutano mkuu wa kanisa uitwao “first aecumenical council of Nicea” mwaka 325 BK. Katika mkutano huo uliokuwa chini ya mpagani kaisari (Constantino), Shemasi Athanasio (Athanasius) wa Alexandri “alithibitisha” uhalali wa neno. “Homo-ousios”. Hivyo Padre Ario alifukuzwa kazi na neno hilo likaingizwa rasmi katika imani ya kanisa uitwayo “kredo ya Nikea”. Alipokufa kaisari Constantino, alitawala mwanaye aitwaye Constantio. Yeye alikuwa mwario, hivyo mwaka 343 BK katika mkutano uliofanyika Philopopulis baada ya kutokea mzozo Sardica, imani ya Nikea ikakataliwa rasmi. Hapo ikaidhinishwa rasmi imani ya nne ya mkutano wa Antiokia wa mwaka 341 BK ambayo neno “Homo-ousios” liliondolewa. Lakini alipokufa kaisari Valenis mwaka 378 BK, itikadi ya Uungu wa Yesu ilirudishwa kwa nguvu sana na kaisari Theodosio aliyetawala mwaka 378-395 BK. Mwaka 381 BK katika mkutano wa Constantinopol imani ya Nikea ikarudishwa rasmi na kuongezewa Uungu wa Roho Mtakatifu ili kukanusha imani ya Wamekedoniano waliokataa Uungu wa Roho Mtakatifu. Baada ya hapo zilitumika nguvu kubwa za dola ili kufuta. Kisiasa imani nyingine.Kwa ufafanuzi zaidi rejea makala ya uchanguaji A.T. Manoni “Ni mwaka gani Yesu alianza kuitwa Mungu” katika AN-NUUR No. 158 Uk. 11.

  Kama tulivyoona itikadi ya utatu mtakatifu haina uhusiano kabisa na Mwenyezi Mungu, Mitume wake wala wafuasi wa Mitume. Hata maneno katika Mithali 8:22-31, Yohana 1:1-14, Yohanda 20:28), Rumi 89:5, Tito 2:13 n.k., hayathibitishi Uungu wa Yesu bali yanatafsiri yake sahihi ya Kitheologia. Wanatheologia wanajua vizuri sana tafsiri sahihi ya manenmo hayo. Wameamua akujikausha makusudi ili waendelee kuwakaamua Waumini wao, na wanaishi maisha bora bila jasho. Kwa hiyo miujiza inayofanywa na Wakristo kwa jina la Yesu, sio miujiza halali kwani imesemea kwenye mafundisho potofu juu ya Mwenyezi Mungu rejea tena kusoma kumbukumbu la Torati 13:1-5.

  Hivyo japo miujiza hiyo inawasaidia baadhi ya watu kuacha madhambi ya kimwili (kuiba, kuzini, kuua n.k.) na kuwa waongofu (walokole), lakini inawang’ang’aniza watu wafanye dhambi kubwa sana ya kiroho. Yaani dhana potofu juu ya Mwenyezi Mungu (s.w.) na kumkataa “Roho Mtakatifu: (Mathayo 12:31-32). Kwa hiyo waongofu hao wanakuwa kama waongofu wa Kiyahudi walioacha madhambi ya kimwili bila kumkubali Mtume Yesu (a.s.). Hivyo wakawa watu wa motoni kuliko hata hao “waliowaokoa”. “Ole wenu waandishi na mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnazunguka katika bahari na nchi kavu ili kumfanya mtu mmoja kuwa mwongofu (mlokole), na akiisha kufanyika, mnamfanya kuwa mwana wa jehanam mara mbili zaidi kuliko ninyi wenyewe.” (Mathayo 23:15).

  From MAOMBI, 2008/11/17 at 11:02 AM
  2008

 272. Niwashukuru wapendwa kwa mafundisho yenu mazuri mno juu ya kongwa hili ambalo wakristo wamejivika kuhusiana na kushika ama kutoshika sabato. Ninadhani ni mtu mwenye matatizo ya uelewa wa maandiko ama yule tu aliyezoea kusikia tu kutoka dhehebuni kwake ndiye anayeweza kushupaza shingo kupinga kile mlichokichangia kwa moyo wa upendo wa Kristo ndani yenu.

  Tatizo ninaloliona mimi ni kuwa watu tumestick kwenye kile tulichosikia kutoka midomoni mwa waalimu wetu na hatupendi kujishughulisha kujua zaidi ndio maana leo mtu anaweza kung’ang’ania fundisho hata kama lina ufunuo wa Roho Mtakatifu ataona kama ni kumkufuru Mungu. Wakristo tutambue kuwa kanisa la Mungu limepewa ufunguo wa kuzijua siri za ufalme wa Mungu kwa Neno la Kristo linalofunuliwa na Roho Mtakatifu.

  Tumuombe sana Mungu alisaidie kanisa lipate AKILI KUTOKA KWA MUNGU yaani UFAHAMU NA HEKIMA YA KUJUA NI NINI YALIYO MAPENZI YA MUNGU KATIKA KRISTO YESU.
  Mbarikiwe nyote.

 273. Shalom Watakatifu wa Bwana,
  Nashukuru Mungu kwa kuwa ametutunza na saa hii tumekutana tena.
  Karibu Ndugu Elinaza na hongera kwa mada nzuri.

  Wapenzi, Kumekuwa na mkanganyiko juu ya wapi sheria ya Mungu inaanza na inaishia wapi na Neema pia. Hivyo kabla sijaendelea, ningeomba nitoe mwanga kidogo. Hili ni somo refu na linahitaji Neema ya Mungu kulijua na utii kulifuata.

  Kifupi sheria ya Bwana haijabadilika na haitabadilika kamwe. Kama Mungu alisema kuna sabato lazima tuifuate na kama alisema usiue vivyo hivyo. Mpaka hapa najua wengi watanyoosha vidole lakini ndivyo ilivyo kwa sheria ya Mungu, haibadiliki (Immutable).

  Hapo tunakuja sehemu ya pili. Je nini Mungu anasema. Unajua Binadamu walitafsiri sheria namna ambayo Mungu hatafsiri. Nafikiri ni kwa sababu ya ufahamu finyu wa sheria ya Mungu kwetu sisi. Mfano, Mungu aliposema usiue, alimaanisha hata kumkasirikia ndugu yako bila sababu umeua! Sasa kwa tafsiri ya Mungu wengi ni wauaji, kinyume na tafsiri ya wanadamu. Vivyo hivyo kwa uznzi na dhambi nyingine. Je Mnakumbuka Yesu aliposema hakuja kuitangua sheria? Hivyo ndivyo alivyomaanisha, alikuja kutufundisha ujinga wetu juu ya sheria ya Mungu na kutimiliza yaliyonenwa kwa vinywa vya manabii.

  Neema kwa upande mwingine ni kuhesabiwa haki kwa kazi ya Msalaba na kupewa bure Uweza utokao Juu kwa ajili ya kazi ya injili. Roho Mtakatifu, ambaye ndiye Bwana wa Kanisa, na Kiongozi wake (aliyetumwa na Bwana Harusi), amekuja kwa kusudi la kutuwezesha kumtukuza Yesu. Ndio maana huwezi sema umejazwa na Roho wa Mungu, ilhali unamuaibisha Yesu kwa maneno, mavazi na mengine utendayo. Roho huweka utaratibu mpya wa maisha (culture) ambao ni tofauti na wa dunia. Kwa hiyo Neema ni kupewa mabo ambayo hatukustahili bure, kwa sababu ya Kazi ya Kristo Yesu pale Msalabani

  Sasa juu ya sabato. (Nitanukuu kwa Kiingereza maana hakuna Biblia ya kiswahili mtandaoni)
  Wakolosai 2 ikielezea wokovu wetu (Neema) inasema
  16Let no man therefore judge you in meat, or in drink, or in respect of an holyday, or of the new moon, or of the sabbath days:

  Hapa kuna swali! Kama sheria ya Mungu haibadiliki, vipi mtu asinihukumu kwa ajili ya sabato?? Hapa sheria imebadilika?? Jibu ni hapana na tatizo ni ule ujinga wetu juu ya sheria ya Mungu. Kwanza katika Biblia hakuna sehemu inayosema Jumamosi ndio sabato! “Siku sita fanya kazi….lakini siku ya saba…” Kwa hiyo cha msingi ni kufanya kazi siku sita na ya saba ni sabato. Kwa utaratibu walioamua wayahudi, siku ya saba ikaangukia siku hiyo ambayo wao huiita sabato (Wengi husema ni Jmosi lakini frankly, sijaifuatilia kujua ni ipi). Hepu tupate pich ya Mungu mwenyewe juu ya sabato:

  Lazima tukubali kukubaliana na Neno la Mungu. Linaposema moja na sisi LAZIMA tuseme moja! Hebu tazama mstari baada ya Kol 2:16

  17 Which are a shadow of things to come; but the body is of Christ.

  Kwa hiyo, sabato ilikuwa kivuli, pamoja na sikukuu zote lakini Kristo ni yote katika yote. Kwa wale ambao wangependa kufuatilia zaidi someni Sura yote ya 4 ya Waraka kwa Waebrania hapa ni baadhi ya mistari:

  “For he spake in a certain place of the seventh day on this wise, And God did rest the seventh day from all his works. And in this place again, If they shall enter into my rest. Seeing therefore it remaineth that some must enter therein, and they to whom it was first preached entered not in because of unbelief: ” (Heb 4:4-6)

  kisha anasema: “For if Jesus had given them rest, then would he not afterward have spoken of another day. There remaineth therefore a rest to the people of God. ” (Heb 4:8-9)

  Kwa hiyo sabato Mungu aliyosema si hii tunayolazimishwa na wanaojiita “wasabato”. Sikieni wapendwa, sabato yetu ni Mbingu ambayo tutapumzika! Kama ni sabato ya siku ya saba
  mstari wa nane na wa tisa hautakiwi kuwapo ktk Biblia! Kwa sababu Upo katika Biblia, ina maana wanadamu wamepoteza mwelekeo wa maana halisi ya sabato. Kama kanisa lingekuwa la wasabato, tungehubiri juu ya hii sabato kwa ulimwengu badala ya kuwahubiria utajiri uliwao na kutu na nondo.

  Kuna siku kwenye gazeti ndugu mmoja alisema hatuendi mbinguni mpaka tuwe wasabato, lakini bahati mbaya ni kwamba sabato aliyoizungumzia ilikuwa ni sabato nyingine! Anyway, ukitaka kupumzika Jmosi, sio tatizo, ukitaka kutunza sabato sio shida lakini tunza sabato halisi ya Bwana.

  Tutengeneze jamii ya wakristo Badala ya kufanya jaamii ya dini. Watu wameamua kuufanya Ukristo kuwa dini tata, lakini ni Imani rahisi kuliko ulivyowahi kudhani. Yaani unampokea Yesu kama Mwokozi na Bwana wa Maisha yako

  Ni Mwokozi kwa sababu yey ndiye aliyekuokoa na mauti ya milele na akakupatanisha na Yeye. Ni Bwana kwa Sababu Yeye ndiye ana HAKI ya kuongoza maisha yako. Yeye ndiye Mungu wako. Roho wa Neema, ndiye alishika uongozi huu. Yeye ni Mungu na Bwana wa Kanisa. Tatizo la Kanisa kudharaulika ni kwa sababu limeamua kumkataa Roho wa Mungu kama Mungu wao na Bwana wa kanisa. Kanisa limeishia kuutukuza upako na kumwaibisha Yesu. Moja kati ya makanisa haya ni yanayojiita ya kisabato (Lazima niwe wazi ili nao wapone!)

  Wamemwaibisha Yesu kivipi? Kama kushika sabato (na sheria kedekede za vyakula) ni sehemu ya mambo ya kufanya ili ufike mbinguni, hakukuwa na haja ya Yesu kuja. kama Yesu alikuja ilhali hakukuwa na haja ya yeye kuja, je afaa hata kuitwa Mungu? Mungu gani anayefanya mambo yasiyohitajika na hata kujiumiza kwayo? Huu ndio ujumbe wanaopeleka kwa Yesu wanapojaribu kupata wokovu kwa kufuata sheria za wayahudi. Na ndio maana sasa Paulo akasema:

  “For I testify again to every man that is circumcised, that he is a debtor to do the whole law. Christ is become of no effect unto you, whosoever of you are justified by the law; ye are fallen from grace” (Gal 5:3-4)

  Mbarikiwe na Bwana,
  Mtume wa Yesu!

 274. Leo Tujadiliane sabato

  SABATO

  Ndugu yangu kuna watu leo wanafundisha kuishika SABATO kama ilivyokuwa nyakati za mtumishi wa Mungu Mussa, na watu wengi wamechukuliwa na mafundisho ya sabato. Lakini je ni kweli kwamba yatupasa kufanya hivyo?

  Muda na nafasi haingetosha kuelezea kwa kirefu somo hili, lakini ili kupata maarifa ya kutusaidia ktk hili nitakueleza kwa kifupi tu hapa kama ifuatavyo.

  Biblia inatusisitizia sisi tunaoishi zamani za agano jipya kumfuata YESU KRISTO ktk mwenendo wetu wote kwani yeye ndiye mwanzilishi na mtimilizaji wa IMANI yetu(Ebr 12; 2). Na kipimo cha kujua kama kweli tu wanafunzi wa YESU ni pale tunapoenenda kama yeye(YESU) alivyoenenda(1Yoh 2; 6). NB kama mtu haenendi kama Yesu Kristo huyo ni kinyume chake.

  YESU KRISTO aliivunja sabato tena kwa makusudi, na kwa sababu hii wakataka kumuua(Yoh 5;10-18) pia ktk mistari hii Yesu anasisitiza kuwa “Mungu Baba anafanya kazi hata sasa” yaani siku ya sabato. Kwa msingi huu wewe pia kama unasema unamfuata Yesu hunabudi kuivunja sabato ama sivyo uko kinyume cha Yesu Kristo yaani mpingakristo.

  Mtu mmoja alimuuliza Yesu kuwa “Nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?” katika majibu na maelekezo ya Yesu kwa mtu huyo kamwe hakumueleza kuishika sabato, bali yalitolewa maelekezo mengine, hii ni kuonyesha kuwa sabato si chochote wala lolote tena baada ya Yesu kuja. (Math 19; 16-20).

  Maandiko mengine yanayotupa kielelezo cha Yesu Kristo na sabato ni Lk 13; 10-17. pamoja na Marko 2; 23-24, 27-28.

  Ndugu zangu leo hii tunatawaliwa na sheria za YESU KRISTO(Wagalatia 6; 2), hatuko chini ya sheria za Mussa. Ni muhimu pia kufahamu kuwa MUNGU amekuwa akibadilisha sheria zake wakati kwa wakati, mfano, wakati wa Adam hadi Ibrahim, hakukuwa na amri kumi, wala sabato, wala kula baadhi ya wanyama, na baada ya Mussa tunaambiwa kuleni vyote(1Kor 10; 25-27). Sasa kwa kujua hilo lazima tujifunze kwa makini wakati wetu MUNGU anataka tuishi vipi.

  Kwa msingi huu wote wanaoishika sabato leo wako kinyume kabisa cha Yesu Kristo na sijui siku ya mwisho watajitetea vipi kwake, maana YESU KRISTO mwenyewe ndiye hakimu siku ya mwisho, bila shaka atasema hivi kwao siku hiyo Lk 19; 27.

  Asante sana kwa kufuatilia somo hili ingawa limekujia kwa kifupi sana , bila shaka hadi hapo utakuwa umepata maarifa ya msingi sana yatakayo kujenga ktk kufanya mapenzi ya Mungu kwa usahihi maana YESU alisema(Math 22; 29).

  Mungu wangu akubariki sana .

  Na Mpwagi AP.

 275. Mpendwa John ninashukuru kwa mchango wako kuhusiana na mada ya dada yetu katika Kristo Allice. Ninakupongeza kwa mchango wako mzuri wa kujenga.
  Nikirejea katika swali lako juu ya hoja yangu inayotanabahisha utofauti wa malezi ya kiroho nikuombe tu unipe muda niandae majibu mazuri ambayo yatazingatia kweli ya kristo kwani nikijaribu kujibu sasa ambapo nina majukumu yanayonikabili sitatoa kile ambacho moyo wangu umejaa kwa ajili ya utukufu wa Mungu wetu mpendwa.
  Mungu akubariki.

 276. Mpendwa Alice,
  Naungana nawe kuhusu tatizo la watu kupangwa kwa madaraja katika utoaji wa sadaka na michango mbali mbali makanisani. Tatizo lililopo ni kwamba watumishi wengi wa siku hizi zetu wanaangalia kibinaadamu. Hawatazami kwa macho ya Rohoni. Na hata maandiko wanachaguwa yanayosapoti misimamo yao ndiyo wanayashikilia. Kwa mfano suala la kupima utoaji wa mtu kwa kuangalia kiasi cha pesa alichotoa ni kinyume kabisa na jinsi Mungu anavyotazama. . . .

  Katika Marko 12:41-44 tunapata habari kuhusu Yesu alivyokaa karibu na chombo cha kukusanyia sadaka na kuangalia jinsi watu walivyokuwa wakitoa sadaka zao. Matajiri walitoa zaidi. Ndipo akaja mjane mmoja masikini akaweka sarafu 2, ambacho kikawa ndio kiwango cha chini kabisa kulinganisha na walivyotoa wengine. Cha ajabu Yesu alishindwa kujizuia kutoa siri jinsi mambo haya yanavyoonekana katika Roho na kuwaambia wanafunzi wake kwamba yule mjane masikini ndiye alikuwa ametoa kuliko wote! kwa kuwa alitoa vyote alivyokuwa navyo. Hili ni kinyume kabisa na hali ilivyo sasa katika sehemu nyingi ambapo watumishi husisitiza tu wingi wa sadaka, na kwamba anayetoa nyingi ndiye huonekana katoa sana. Kumbe kwa Mungu si hivyo…..

  Kuna maandiko mengine yasemayo ”Wapeni watu vitu kipimo cha kujaa na kushindiliwa maana kipimo mpimacho ndicho mtapimiwa ninyi….(Luka 6:38). Hii nayo inatumika vibaya siku hizi maana imegeuzwa na kuwa kwamba mtu akikupatia fungu kubwa nawe unamrudishia fungu kubwa, na hata watu sasa wanachaguwa watu wa kuwapa huku akifikiria kwamba nikimpa fulani, kwa kuwa anazo, naye siku ninashida atanisaidia tu kwa kiwango hicho hicho hata na kuzidi. Kwa hiyo utoaji unageuka kuwa mtaji…..! Lakini tukisoma katika Luka 6:34 Yesu alisema “Kama mkiwapa watu ambao mnategemea kupokea tena kutoka kwao ni thawabu gani mnapata? Hata wenye dhambi huwapa wenye dhambi wenzao ili wapokee tena kutoka kwao! Hili nalo limekuwa tatizo sana maana waumini makanisani nao wanatowa mafungu makubwa kwenye matoleo ili wapate upendeleo toka kwa wachungaji. Na utashangaa kwamba wengi wa wanaotoa mafungu makubwa ya pesa ndio wanaopewa vyeo makanisani pamoja na uzee wa kanisa! Kanisa linakwenda wapi? Mbona tunamzimisha Roho wa Mungu kwa kuchaguwa kutokana na vigezo vya kibinaadamu. Na hata nje ya kanisa utakuta matajiri wanapeana wao kwa wao na hivyo utakuta hadi manisani eti kuna makundi ya wenye nacho na wasio nacho!

  Ni kweli kabisa tunatakiwa kumtolea Mungu kitu kizuri. Ni kweli kabisa kipimo tutoacho ndicho tutapimiwa. Ni kweli kabisa tutanashauriwa kuwatendea wengine vile tunavyotaka tutendewe sisi..LAKINI HAISHII HAPO..! Kama ni suala la ukubwa tu wa matoleo Yesu asingemsifu yule mjane masikini. Lakini aliona moyo wake na akiba yake aliiona pia.Kwa hiyo hapa kuna mambo matatu ya kujifunza katika utoaji:
  1). Moyo wako uko namna gani wakati unatoa;
  2). Ulichotoa ni asilimia ngapi ya hazina yako; na
  3). Nini kimekusukuma kutoa kiashi hicho.

  Mungu haangalii kama watu waangaliavyo. Mungu na atujalie kuwa na macho ya kiroho ili tuweze kuyafahamu yaliyo mapenzi ya Mungu kweli na kuyatenda!

  Kwa mpendwa Amin:
  Kuna jambo ambalo umeliandika kwamba “SOTE TUNA MALEZI TOFAUTI YA KIROHO”. Nimekuwa nikijiuliza KAMA KWELI Mwili wa Kristo ni mmoja; Roho ni mmoja; Tumaini ni moja; Bwana ni mmoja; Imani ni moja; Ubatizo mmoja na Mungu ni mmoja ambaye ni Baba wa wote aliye juu ya wote na katika wote na ndani ya wote, (Efeso 4:5-6). Je, NINI NINI AMBACHO KINASABABISHA MALEZI YA KIROHO YAWE TOFAUTI???? Je, Tofauti hizi za malezi ulizozitaja siyo kinyume na UMOJA huu wa Roho katika kifungo cha Amani?
  Ikiwa tu mzazi huhakikikisha anawalea watoto wake wawe katika maadili ya familia yake Iweje Mungu, Baba yetu aliye mbinguni atowe malezi tofauti tofauti kwa sisi watoto wake? (ambayo mengi wa hayo huleta migongano na mitafaruku kwa waaminio?

  Wapendwa mimi nahitaji kufundishwa katika hili!

 277. Wapendwa tusihesabu mabaya kwani hicho ndicho kipimo cha upendo. Tuwe pia wavumilivu kabla ya kuamua kuwa hatutendewi vyema na watumishi ambao wamejitolea kutuhudumia kiroho. Zaidi sana turejezane kwa upole tukionyana na kuombeana kwani sote tuna malezi tofauti ya kiroho.
  Hata hivyo napenda tujue kuwa chanzo kikubwa cha mabaya ni kupenda pesa hivyo watumishi wanaowabagua watu kwa misingi ya kiwango cha matoleo ni tatizo na wanahitaji msaada wa kushauriwa na akiwa mkaidi aambiwe kwa ukali ili ajue kuwa kanisa la kristo si mali yake bali ni la Mungu mwenyewe na hakuna aliye na haki kupita wenzake.
  Ndio maana niliamua kuandika makala juu ya UHALALI WA WAKRISTO KUTOA ZAKA unaweza kuliona katika blog hii. Soma na utapata kitu cha kukusaidia kwenye maisha yako ya utoaji kwa Mungu.
  Mungu akubariki sana

 278. Bwana Asifiwe wapendwa!!!
  Nimeguswa pia na mada hii na huwa nakwazika sana!!Pia kuna makanisa mengine ikifika muda wa kutoa sadaka waumini wanapangwa kulingana na kiasi cha fedha…utasikia mchungaji anatangaza hivi… haya wenye elfu kumi kumi wasimame..waje na sadaka zao…niwaombee….akimaliza anasema haya wenye elfu tano tano…. then wenye elfu mbili mbili…….mwisho wenye hela nyingine (wanakuwa wa mwisho)……Kwa kweli jambo hili sio zuri mbele ya macho ya Mungu na Binadamu. na yangu mimi Alice!
  WADAU MNASEMAJE???

 279. NINA WAPONGEZA WOTE MLIOCHANGIA MADA HII KWA UELEWA MKUBWA MMENIJENGA KWA KIASI KIKUBWA MNO
  MUNGU AWABARIKI NYOTE

 280. Wapendwa katika Kristo Yesu, mbarikiwe sana na Bwana wetu; Yesu Kristo, aliyetupa ukombozi, kwa Damu Yake ya Thamani!.

  Unajua, matatizo ya Kanisa la nyakati hizi, miongoni mwa Watumishi wake hawajaweza kushika kuwa, Mungu anawaleta watu wake kwake, kupitia matatizo mbalimbali wanayoyapata ili waokolewe. Mimi mwenyewe, bila matatizo nisingeweza kuokoka kabisa, lakini kwa sababu ya matatizo na magonjwa niliyokuwa nayo, nilikuja kwa watumishi wa Mungu ili niombewe (siyo kuokoka). Lakini pamoja na kuombewa, nilikutana na Neno la Mungu likanibadilisha, na nikaokolewa kwalo.

  Kwa sababu ya kutokushika hilo, Watumishi wengi wa Mungu, wamekuwa wakijishughulisha sana na ibada za maombezi na baraka mbalimbali, kila siku ya ibada, kama wanaokuja kuombewa walivyokusudia. Watumishi wamekuwa hawana maono yaliyo tofauti na wenye matatizo, wamekuwa kama waganga. Waganga wanapowapokea wagonjwa wao, huwauliza shida na magonjwa yanayowasumbua watu wao, na kisha huanza kushughulika nayo kwa kuwapa dawa husika. Watumishi wa Mungu nao, wamefanya maombezi kuwa ni kama hospitali; hawajapata maono kuwa huo ni mpango wa Mungu wa kuwaleta watu kwake (Mungu) ili waelezwe makosa yao. Hilo limesababisha watu wengi kutokufunguka katika matatizo yao, kwa sababu ya kuwekewa imani kuwa wakiwa na matatizo, mtumishi wa Mungu ndiye anayepaswa kuwaombea.

  Magonjwa yaliyo mengi kwa watu wa Mungu, kimsingi yanatokana na kutokukaa katika usafi na utakatifu. Hii inatokana na kukosa mafundisho ambayo wangepaswa mtu afundishwe, mara tu baada ya kuokoka. Pia mafundisho ya usafi na utakatifu iwe ni sehemu ya maisha ya huyo mkristo, ili aimarike zaidi na zaidi.

  Watumishi kama watakuwa na maombezi tu bila Neno lenye nguvu la kuwabadilisha wanaowaombea, hakika Kanisa litabaki kuwa vuguvugu, na walio vuguvugu Mungu anasema atawatapika watoke katika kinywa chake!(Ufunuo 3:16). Mpango wa Mungu kuwaokoa watu, siyo tu waokoke na kuwepo kanisani, bali pamoja na kuwepo kanisani waishi maisha ya usafi na utakatifu.

  Kuendelea kumwombea mtu siku zote ni kumrudisha nyuma kiimani. Mtu akifundishwa kweli ataweza yeye mwenyewe kuomba pale anapokuwa na matatizo, na Mungu akamsikia na kumjibu, kwa sababu wote tunafanywa kuwa makuhani wa Bwana, (1Petro 2:9 Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa Kifalme….). Pia, mtu huyu atakuwa ni msaada kwa wengine wanaookolewa, kwa sababu tumeokolewa ili tumtumikie Mungu.

  Kufundisha kwamba kila mhitaji anapokuwa na matatizo amkimbilie mtumishi wa Mungu muda wote, mimi naona si kweli. Watumishi wa Mungu wamewekwa kwetu ili kutufundisha yapasayo kufanya si kutuombea tuuuu siku zote, hapana.

  Hata hivyo, si kwamba watu wa siku nyingi katika imani hatuhitaji kabisa maombezi, la hasha, maombezi yanahitajika sana, ndiyo maana hata watumishi wa Mungu wanahitaji maombi yetu. Tuombewe, lakini isiwe ndiyo ibada yenyewe kila inapokuwa ibada!

  Kutokana na hayo, mimi ningeshauri watumishi wa Mungu, wawe wanachukua muda mwingi sana, kuwafundisha watu namna ya kukaa katika kweli yote, na muda unaosalia utumike kwa ajili ya kuwaombea wageni au watoto wachanga kiroho, ambao hawajajua hata namna ya kusema na Mungu! Au maombezi yanaweza kuwekewa muda maalum.

  Ibada za maombezi za kila J`pili, hata kwa wale ambao hawana shida (japo shida haziishi) kwa kweli si makusudi ya Mungu, makusudi ya Mungu ametuokoa au kututoa Misri ili tukamtumikie, (Kutoka 9:1).

  Asante sana wapendwa katika Kristo Yesu.

 281. Shida nyingine nionayo mimi juu ya matangazo ya namna hii yanatokana na kutokujua makusudi ya Kanisa.
  why does the church exist?
  what are we to be as a Church?
  what are we to do as a Church?
  and how are we to do it?
  wachungaji wengi hatupend kuchukua mda na kutafakari maswali haya matokeo yake tunachanganya mambo ya kwanza yaani primary issues na mambo ya pili yaani secondary ones!
  The primary issues of the church is
  who is our master? what was his message? that should be ours!
  what is it driving us to do what we do?the way we do church,
  nasikitika kusema tumekuwa na walimu wengi, matokeo wakristo wengi wanachanganyikiwa na matokeo badala ya kutafakari njia iliyoleta matokeo .People confuse the means with the end,in onother word as christians we should not allow the end justfy the means.watu hawajali kufuat maandiko yanasemaje maadamu pepo linatoka inatosha, au watu wanaanguka,mafundisho yote ni mafanikio tu na kupona lakini hatusiki mafundisho ya kujikana na kubeba msalaba Yesu alisema wengi watasema Bwana tulitoa pepo kwa jina lako ,atasema ondokeni siwajui.
  Mungu anataka tumpende yeye kwanza ,tujifunze kwake mpole na mnyenyekevu wa moyo.maoni yangu KANISA LA TANZANIA LINAHITAJI MATENGENEZO WALA SIO UAMSHO KAMA WENGI WANAVYODHANI,

  BAADHI YA WAHUBIRI WA TV NA RADION WANATUMIA MDA MWINGI KULUMBANA NA NA KILA MOJA ANAVUTIA KWAKE HII NADHANI TUNAUUMIZA MWILI WA KRISTO KULIKO KUUJENGA. NAAMINI WANAMISSUSE PLATFORM

  MADHABAHUNI NI MAHALI PAKULETA BARAKA SIO MAHARI PA KUJERUHIANA

  PLEASE STOP THIS!WHO SI FOOLING WHO?

 282. Mpendwa katika Bwana Kingston ED ninashukuru sana kwa mchango wako ambao ni kweli tupu katika Mungu tumuabuduye lakini tatizo si juu ya mafanikio hapa tatizo ni advertizement wanazotoa watumishi katika luninga. Ingawa sikataia hata Bwana Yesu alitangaza kuwafahamisha watu wasumbukao na kulemewa na mizigo waje kwake na mahali pengine akawaita wote wenye kiu waje kwake n.k. lakini utaona wito wa Bwana Yesu ulifunua upendo wake wa dhahiri wa rohoni kwa kutoa matangazo ambayo kwa yakini yaliwafanya watu watamani vya rohoni zaidi kuliko vya mwilini. Tena utaona hata katika injili ya Yohana sura ile ya sita Bwana Yesu alithubutu kuwakaripia makutano ambao walimfuata yeye kwa ajili ya mkate. katika fundisho hili utaona njaa na kiu ya Yesu ilikuwa ni kumpatia baba wa Mbinguni matunda ambayo ni watu walio tayari kumuishia Mungu na si haya matangazo ya wahubiri wetu wa sasa ambayo ni sawa tu na yale ambayo waganga wa kienyeji wanajitangaza. Ninakushukuru sana ndugu yangu kwa mchango wako mzuri.

  Napenda kusema kwa ufupi tu kuwa kanisa linahitaji sana kurudi katika wito wake mkuu ambao ni kutangaza habari njema za Yesu kristo kwa kila kiumbe na kila kabila.
  Haya matangazo yanayohusu mafanikio si sehemu ya Injili kama injili ila ni matamanisho kwa watu ili waone kuwa watumishi hawa wana ukaribu sana na Mungu.
  Lakini fahamuni neno hili kuwa awaye yote aliyeitwa na Bwana Yesu hawezi kuhangaika na kutafuta mtumishi wa kumuombea apate fedha wala kazi kwani atajua yakini wito wake kuwa UTAFUTENI KWANZA UFALME WAKE NA HAKI YAKE NA YOTE MTAZIDISHIWA. Pia ninapinga dhana kuwa kuna watumishi wakubwa na wadogo katika kazi ya Mungu makundi hayo yanatengenezwa na watu wasiotambua nafasi zao katika kanisa la Mungu aliye hai. kwa faida yao tafadharini someni kwa makini 1korintho12:4-27
  Mungu awabariki sana

 283. HAPO TUOMBE TU MUNGU ATUFUNULIE KWELI YAKE ITUWEKE HURU. USIJE UKAJIDANGANYA KWAMBA KUPATA HAYO YANAYOTAJWA- MALI, AFYA, NA VINGINEVYO VITAKUSAIDIA KUUTEKA UFALME WA MBINGUNI. OKOKA UWE NA YESU KRISTO NDANI YAKO ILI UFANIKIWE KATIKA MAMBO YOTE. UKIMPENDA KWA KUZISHIKA AMRI ZAKE NA KULITENDEA KAZI NENO LAKE BILA KWENDA KUSHOTO WALA KULIA YATAKUWA KWELI KWAKO KAMA ANAVYOSEMA KATIKA WARUMI 8:28, 3YOH 1:2 NA KUMB 28:1-14
  MUNGU AWABARIKI SANA,, TAJI YA UZIMA USIKUBALI KUIKOSA KAMWE HATA KWA GHARAMA YA KUKOSA JICHO, MKONO, NA MALI NA MARAFIKI WA DUNIA NA MAMBO YA DUNIA.

 284. Kwa kweli matangazo ya namna hii yanaliaibisha kanisa yani mwili wa kristo, na hii inatokana na uelewa mdogo wa the so called wapakwa mafuta. Inasemekana kuwa kina cha neno la Mungu kwa wakristo wengi ni kifupi sana lakini ndio wako mstari wa mbele kutaka kufundisha, makanisa yamegeuzwa kama waganga wakienyeji, na wengi wanaiga matangazo ya kimarekani wakidhani kila wanachokiona kwenye Tv ni cha ki Mungu, THE BIG QUESTION IS: WHY WE DO WHAT WE DO THE WAY WE DO?
  HUKO NI KUWAIBIA WATU BILA KUTUMIA NGUVU.

  MAY GOD HELP US KUELEWA HII

 285. Mbali na matangazo jamani hata mahubiri ya most of the churches siku hizi yananishangaza, i think most of the pastors preach what people wants to hear thats why utajiri, biashara yako ifanikiwe, uende ulaya, upande cheo au upate kazi nk, Mi nadhani yote ni katika kuwavutia watu waje kanisani na at the same time believe me wanasaidia sana maana people are confused out there, watu wana matatizo jamani and at times they dont know what to do, who to talk to, but in the church wanapata faraja na kuona mwanga mpya ndani ya matatizo waliyomo otherwise watu wangekuwa wanaiua sana ama kufa na pressure. Thats why i love the bible and the word of God it really console people. Cha msingi mapastors wajitahidi kuwapa watu injili ya kweli maana after all these kuna hukumu, tu-focus mbali zaidi.

 286. i support your point barnabas. hata mtume paul alisema wengine watahubiri injili kwa unafiki, lakini vyovyote iwavyo iwe katika roho au unafiki, itahubiriwa tu. ni kweli mafanikio ya kiungu ni mpango kamili wa Mungu kwa watoto wake, ila ni jukumu lako kama mkristo kutambua mambo kwa jinsi ya rohoni. watangaze tu wanavyoweza na kuita watu, na Yesu wa huruma atawatendea hao watu kwa imani iliyowapeleka huko, wala si lazima iwe kadri ya nia za waliowakusanya. one thing i love about the Lord is His ability to catch the devil unawares, He always capitalizes on negative intents to bring about good for His people, take the case of Haman against Mordecai and the Israelites. stay blessed in His love, assured that even if we don’t know what 2moro holds, He holds 2moro

 287. injili nyingi za siku hizi zimekuwa ni kama usanii. kikubwa Wapendwa tunamuhitaji Roho Mtakatifu kila mtu binafsi kutufungua macho ya roho kupambanua yote haya!
  ni ngumu sana kwa hali ya kawaida kusema nani yuko sahihi na nani hayuko sahihi, nuru daima hujitenga na giza….ni vema ”Amani ya Kristo iaumue mioyono Mwetu”.

 288. Shalom! kwakweli hata mimi hiyo hali imekua ikinikera sana wengine wanaomba wachangiwe pesa na kutangaza akaunt namba hivi yesu alivokua akiombea watu alihiitaji pesa hata manabii na mitume zamani hawakufanya ivo watu bado tutoe sadaka bado tuombwe michango ndio tuombewe inasikisikitisha sana minadhani tuombee kwa jili ya hii hali iishe kwani inashusha utukufu wa Mungu manabii wa uongo wanazidi kuongezeka.
  mbarikiwe sana

 289. HATA MIMI SIKO MBALI SANA NA KAKA STEVE KWANI MATANGAZO YA SIKU HIZI HAYANA UTUKUFU WA MUNGU.
  KWANI TUSIMTEGEMEE TU MUNGU KWANI TUONE KAMA HATA TUFUNGULIA NJIA?NAWAPENDENI SANA.

 290. JP,

  You are right kwenye last paragraph, ata mimi huwa mara nyingi huwa najiuliza kwanini mtu anataka kumsaidia mtu kiroho then aweke charges?? Utakuta kuna mkutano mzuri wa kiroho na yale ambayo yatazungumzwa mle ndani utakuta mtu pia wayahitaji lakini utakuja sikia kuna kiingilio cha Tshs 15,000 per head sasa sijui hapo wanamsaidiaje mtu. Ninachoamini kazi ya kutangaza neno na la mungu ni wito na wala si biashara. Nashukuru kwa somo ulilotuwekea nawe Mungu akubariki

 291. Ndugu wapendwa,

  Kwa mtazamo wangu Mafanikio ya Kimwili ni suala la ki-Biblia kabisa, sina shaka na hilo! Lakini si mafanikio haya ya magari, pesa, nyumba na aina zingine za utajiri wa mwilini vinavyomfanya mtu awe mwana wa Mungu. Katika vitu hivi hakuna uzima. Ndiyo maana Yesu aliliona hili akasema “Uzima wa mtu hauko katika wingi wa vitu (mali) alivyonavyo” (Luke 12 :15)”. Kwa mkristo wa ROHONI utajiri na mambo yake yote si kitu. Hivi tunaviacha kesho! Wala si vitu vya kumfanya mkristo ajisifu kwamba kafanikiwa. Iko sababu moja tu ya kumfanya binaadamu ajisifu nayo ni hii:
  Jeremia 9:24 But let him that glorieth glory in this, that he understandeth and knoweth me, that I am the LORD which exercise lovingkindness, judgment, and righteousness, in the earth: for in these things I delight, saith the LORD. ( Maandiko yoye kutoka KJV Bilble)

  Kuupima wokovu kwa kiwango cha mafanikio ya kiuchumi (utajiri au umasikini) ni sawa na kujaribu kupima UMBALI kwa kutumia MZANI!…..(kwa mfano mtu anataka kupima umbali kutoka Dar kwenda Chalinze kwamba patakuwa na umbali wa kilo ngapi)! Kipimo cha mafanikio ya Mkristo ni kwa kiasi gani analeta athari katika ulimwengu wa roho juu ya ufalme wa giza (Phil. 6:12). Utajiri au mafanikio ya kimwili yalikuwepo kabla Yesu hajaja Ulimwenguni na ndiyo maana Yeye hakusisitiza kwenye hili. Yeye alisisitiza kwenye UZIMA WA MILELE kama ilivyo katika John 3:16 For God so loved the world, that he gave his only begotten Son, that whosoever believeth in him should not perish, but have everlasting life. Lakini anatambuwa kwamba tunahitaji pia mafanikio ya mwilini ndiyo maana akasema tuutafute kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake ( Huu ndiyo Uzima wa Milele. Hakuna kinachozidi Uzima wa Milele!) …na mengine (utajiri, amani katika ndoa na familia, usingizi kama wa mtoto nk) ni ‘marupurupu’ tu! Sasa ‘tunapompigia debe’ Yesu kwa kutanguliza marupurupu badala ya ‘package’ yenyewe tunamshusha hadhi! Kuna kitu kingine zaidi katika Ufalme wa Mungu kabla hujashuka hadi kwenye Mafanikio ya Kimwili: Paulo aliwaonya Warumi katika Rom 14:17 For the kingdom of God is not meat and drink; but righteousness, and peace, and joy in the Holy Ghost! Na pesa haiwezi kumpatia mtu hata kimoja wapo wa hivi vitatu!

  Hatari inayosababishwa na Matangazo kama ya biashara kwa Yesu ni kwamba watu wengi wanafikiri ni watu wenye shida tu ndiyo wanamuhitaji Yesu. Lakini kuna watu wengi wana maisha ya raha mustarehe. Hawa pia wanamuhitaji Yesu. Na hii inaongeza ugumu wa matajiri kuingia mbinguni kutokana na jinsi Neema ya wokovu inavyoelekezwa zaidi kwa watu wenye matatizo. Lakini ukweli ni kwamba: Uwe masikini au uwe Tajiri, Uwe mgonjwa au mzima, nk Wote tunahitaji wokovu wake Yesu Kristo! ili tuweze kuwa na Uzima wa Milele.

  Kuhusu watu wanaotoza pesa ili wawaombee watu kuna mambo mawili tu hapa: Ama Ni Manabii wa Uongo Au ni kati ya wale ambao Yesu alisema siku hiyo watasema ‘Tulitowa pepo kwa jina lako….’. Maana siamini kwamba Kifo cha Yesu hakikutosha hadi uongezee na pesa ndiyo upokee uponyaji kutoka kwake Yesu. Na uponyaji wa namna hii hautoki kwa Yesu Kristo Mwana Wa Mungu Aliye hai. Yeye alitowa uzima Bure na kila atakaye atapata Bure. Ila kama kweli unatoka kwa Yesu basi atakuwa amewaweka ili waje watimize maneno aliyoyasema!

  Nawatakia Baraka za Mungu mafanikio katika kila mnalolitenda!

 292. WAGANGA NI WACHAWI ,UKIENDA KWAO WANAKULOGA ZAIDI.KAA NA YESU TU HILO TATIZO LAKO LIMESHAONDOLEWA UKIWA NA YESU UKIONA HOFU KIRI KWA KUPIGWA KWA YESU HOFU HUNA NAFASI.UTASHANGAA SANA HOFU INAHAMA, WAGANGA NI WACHAWI USIWASOGELEE KABISA.NJOO HUKU KWA YESU.

 293. HAWA WAGONJWA BADO WAMEFUNGWA KITAMBAA CHEUSI USONI ,NI LAZIMA TUOMBE WAFUNGURIWE WAJUE KUWA KUNA YESU MWANA WA MUNGU ANAPONYA BURE .MAANA WENGI TANGU AZALIWE ,BABA NA MAMA NI KWA WAGANGA TU NAHUKU WANAENDA KANISANI YAANI WANACHANGANYA WAKITAKA MUUJIZA WANAENDA KANISANI ALAFU WANAAMINI DAWA ZA WAGANGA HILO NDIO TATIZO BADO HAWAJAAMINI YESU BILA WAGANGA . WANADHANI MAOMBI BILA WAGANGA SIO SAWA.HAWA WATU HATUWEZI BILA YESU LAZIMA TUFUNGE NA TUOMBE TENA KWA BIDII MPAKA WAACHE KUAMINI UONGO HUO WA WAGANGA NA KUMKIRI YESU WAPONYWE KITAMBA CHEUSI KIWATOKE USONI.MIMI MWENYWE NILIKUWA NIMEFUNGWA LAKINI HUYU YESU ALINIFUNGUA NIPO HURU HAKUNA WAKUNIDANGANYA TENA.,

 294. Niseme kwa kifupi kuwa kama watu wanaweza kutangaza biashara zao ili wapate wateja basi kwa habari za Yesu ni zaidi ya hapo. Najua kinachotuathiri zaidi ni namna tulivyokuzwa na dini tulizotoka. Sioni tatizo kuwaeleza faida ya kumjua Mungu na kuwapa watu tumaini. Ingekuwa ni mbaya sana kama watu hawa wa Mungu wangekuwa sasa wanawakatisha watu tamaa.Iko haja ya kuwaambia watu ukuu wa Mungu. Mambo ambayo yameorodheshwa hapo si kwamba ni ya uongo ni mambo yamekuwa yakitendeka kila siku kwenye kanisa la Mungu. Hatuwezi kumpima mtu kwa vigezo hivo kwamba anafanya biashara au la.

 295. KWA NJIA HIYO WENGI WAMEMJUA YESU HAYO MATANGAZO NI KWA WALE WENZETU AMBAO HAWAJUI WAPI WANAWEZA KWENDA KUPOKEA UPONYAJI MAANA KUNA WENGINE HAWAJAJUA KAMA YESU YUPO NA NILAZIMA ATANGAZIWE ILI AACHE KWENDA KWA WAGANGA ATAFUTE PALE ALIPOAMBIWA YESU ANAPATIKANA KWA HIYO NI MUHIMU SANA KWA DUNIA YA SASA KUTANGAZA ILI WOTE WAJUE KUWA YESU NI BWANA MATANGAZO NI MUHIM SANA KWA WALE AMBAO HAWAAMINI HATA HIVYO HAWATANGAZI UONGO HIYO MIUJIZA YESU ANAFANYA.JAMANI WATUMISHI WA MUNGU WANAITWA NI WATUMISHI WA MUNGU ALIE JUU SANA. MMOJA TU.

 296. fedha na dhahabu vyote ni mali ya BWANA na sisi ni watoto wake ndio maana katuumba tutawale……..kuwa maskini si mpango wa MUNGU……….
  KARIBUNI KTK MAFANIKIO!!!!!!!!!!!!!!

 297. acheni mambo ya kizamani wapendwa………..maovu yote yanayotendeka sababu kubwa ni umaskini……….kwani mtu ukiwa tajiri ni dhambi???????????kalaghabaho wenzenu tunafanikiwa na YESU tunaye na mbinguni tunaenda.

 298. Nami naomba kuchangia mada hii kama ifuatavyo:

  Tatizo tulilonali sisi watu wa kizazi cha sasa ni kwamba tunataka kupima wokovu na utakatifu kutokana na kiasi gani cha utajiri ulionao. Imefikia mahali sasa kwamba wewe kama ni mhitaji (sikupenda kutumia neno ‘masikini) unaonekana kama si mtakatifu. Na kwa sababu hiyo pita makanisani utakuta matajiri wengi ambao ushuhuda wa mienendo ya maisha yao siyo mzuri lakini wamepewa vyeo vya uzee wa kanisa nk. Na hii inasababisha jina la Yesu litukanwe! Hapa ndipo tunapokosea!

  Pesa ni kitu kizuri sana. Mambo yote ya duniani yanahitaji pesa ili yaweze kuendelea. Lakini pia shina la mabaya yote ni kupenda pesa. Pesa ikitangulia mbele halafu Yesu ndiyo atajwe baadaye hilo tayari ni tatizo. Maana yake mtu asipopata pesa alizoitiwa hana haja tena ya Yesu maana yeye aliitika wito kwa haraka maana anahitaji pesa. Pesa isipopatikana anajuwa kumbe Yesu hayupo. Lakini Yesu hakufa msalabani ili watu wapate pesa kwanza. Yesu alikufa msalabani ili watu waokoke, waache matendo yao maovu ili wakifa waende mbinguni. Mambo ya pesa, magari, biashara kubwa siyo msingi wa wokovu. Pesa ni kwa ajili ya mavazi na chakula na mambo mengine ambayo ni ya muda mfupi sana. Lakini wokovu wa Yesu ni wa milele. Ndiyo maana akasema tuutafute kwanza ufalme wa Mungu na haki yake mengine ni marupurupu tu!

  Napenda kuweka jambo moja wazi kwamba kamwe pesa hailetwi na utakatifu. Kama pesa inaletwa na utakatifu basi wasiomwamini Yesu wote wangekuwa omba -omba! Pesa inaletwa kwa kufanya kazi kwa bidii. Ndiyo maana Katika Kumbukumbu la Torati 28 Mungu aliwaambia wana wa Israel kwamba watakapoitii sauti yake (sawa na kuokoka, kwanza) watabarikiwa mijini – (WAKIFANYA KAZI) na tena watabarikiwa mashambani – (WAKIFANYA KAZI). Ukiwa mjini ukajishughulisha pesa itakuja tu. Ukiwa shambani ukajituma kulima kwa bidii pesa itakuja tu. Ni rahisi sana kupata pesa kuliko kuokoka. Ndiyo maana Yesu akasema hivyo vitakuwa ni nyongeza tu maana mtu akiokoka anakuwa na akili kamili, anaweza kudhibiti matumizi ya pesa zake, anaacha kuwa mzembe na kwa hivyo pesa automatically inaongezeka.

  Kuthibitisha hoja yangu hii ni kwamba watu ambao wameshafika Japan (au nchi yoyote ya waabudu miungu) wataelewa ninachosema. Wale watu ni wapagani asilimia 100. Wanaabudu sanamu tu. Lakini nani asiyejuwa utajiri wa Japan. Je, ni kwa sababu wana Yesu? Hapana. Wale watu wanafanya kazi kama mchwa. Wanajuwa siri ya kupata pesa ni bidii. Sasa sisi tunadanganyana. Watu hawataki kufanya kazi kwa bidii, wanataka waende madhabahuni wawekewe mikono halafu tayari wawe matajiri. Hiyo siyo kanuni ya pesa.

  Ningefurahi sana siku moja kusikia mchungaji yoyote akiwahimiza watu waliokoka wafanye kazi kwa bidii. Waamke mapema wawahi makazini halafu wachelewe kurudi nyumbani. Watanzania tunapenda sana starehe. Utakuta mtu kajiajiri lakini saa 10 anafunga kazi. Wapi na wapi?

  Tukishaokoka kwanza, tunapata akili njema, tunaifahamu kweli nayo kweli inatuweka huru kutokana na vifungo vyote vya shetani pamoja na umaskini. Maana hakuna uvivu tena. Uaminifu kazini unaongezeka na hivyo promosheni zinafuatana nk…nk

  Ndoa nyingi zinawaka moto kwa sababu watu walikwenda makanisani ili wapate wake/waume. Na kwa sababu hiyo wakakuta wanaoa/kuolewa na mtu asiyeokoka kabisa. Wokovu wake ulikuwa wokovu wa kupata mwenza si wa kwenda mbinguni! Baada ya Honey moon tayari biblia anaweka chini maana ameshapata alichokuwa anataka. Naamini kila mmoja wetu anao mfano kuhusu hili.

  Ni vema sana kwamba watu wamwamini Yesu kwa sababu ,kwanza,
  ya kuokoa roho zao. Wakisha okoka ndipo mafundiso mengine yafuate. Lakini tukigeuza wokovu nje-ndani, Ole wetu!

  Mbabrikiwe!

 299. praise god,
  kwakweli haya matangazo yamepitiliza ayajakaa kimungu bali kidunia si kimungu kabisa na hii inaonyesha watu wamejituma wenyewe awajatumwa na mungu ndio mana wanaendesha kibiashara kabisa

 300. Mungu awabariki kwa huduma hii njema. Nimebarikiwa kuona Mungu wetu anatukuzwa kwa njia hii ya kisasa. Tunapaswa kumtukuza Mungu wetu katika Yesu Kristo kwa bidii zote. Waulimwengu wamekuwa katika mwendo wa kasi sana. Namshukuru Mungu kwa kutupatia teknolojia ambayo inatuungaisha watanzania wote katika kulisifu na kuliinua jina la Yesu Kristo.

  Mara baada ya kusema hayo, ninapenda kusema kidogo juu ya watumishi wanaoigeuza Madhabahu Takatifu kama chombo cha “biashara” zisizo za utukufu. Ninadhani kutumia jina la Yesu na kuwapa watoto wa Mungu mafundisho potofu ni dhambi KUBWA! Jambo hili halipendezi mbele za Mungu. Nadhani “viongozi” hao wamesahau KUSUDI KUU la Mungu kwa watoto wake, yaani wanadamu.

  Mungu hupenda kutoa baraka zake kwetu. Vionozi wa dini wameitwa, wamewekwa wakfu kutoa huduma ya Mungu kwa watoto wa Mungu. Inasikitisha kuona, baadhi ya viongozi ETI wa dini wanaitumia MADHABAHU ya KRISTO kwa biashara za kifisadi. Hiyo ni dhambi KUBWA.

  Vilevile, ninapenda kuwashauri waumini wenzangu kuwa na masikio ya kiroho. Masikio yatakayotusaidia kusikia na kuchambua UJUMBE unaoletwa mbele yetu. Sisemi kuwa kila ujumbe una mapungufu, ila ninawaalika WATOTO wa Mungu kupambanua UJUMBE unaoletwa mbele yetu. Yesu Kristo anatuonya kuwa kuna watu watakuja kwetu na kujiita watumishi wa KRISTO. Yesu anawaita hao ni makristo na manabii wa uwongo. Wapendwa na tunakumbushwa na Hosea kuwa WATOTO wa MUNGU wanaangamia kwa kukosa maarifa.

  Naomba niwaache na ujumbe huu….”Kesheni Msije Mkaingia Majaribuni.” Yesu Kristo mwingi wa huruma anatupa ujumbe huu. Mungu atubariki sisi sote.

 301. Nimependa point yako mpendwa Mbilinyi kuhusu suala la “malisho”. Umesimamia pazuri sana kwenye andiko lisemalo “tafuteni ufalme wa Mungu na haki yake, na mengine mtazidishiwa…” Unajua hata wakati ule wa Yesu wengi walijichanganya katika point ya upi, utakuja lini au uko wapi ufalme wa Mungu. Tunaona hapa huu ufalme unakwenda pamoja na haki, ukivipata hivi pamoja basi mengine bwana anasema utazidishiwa.

  Suala la Malisho nionavyo mimi ni mafundisho sahihi kama ilivyokusudiwa na bwana kwa watoto wa Mungu. Ufalme nionavyo ni tendo la kuwa na bwana Yesu moyoni/maishani na sio mdomoni au kichwani tu. Hapa unaweza ukagundua wapo wengi wanaojiita wakristo lakini Yesu hajafanya makao katika mioyo (roho/nafsi) yao. Na suala la haki nionavyo ni kuijua kweli ya Mungu (Neno lake) katika mazingira yote ya maisha ya mhusika.

  Somo la mafanikio kifedha n.k. ni sehemu ya neno la Mungu ambalo muamini imempasa kujua au kujifunza mara anapomkaribisha bwana Yesu kufanya makao katika moyo wake. Neno la Mungu linasema mtaifahamu kweli na hiyo kweli itawaweka huru. Kuna uwezekano mkubwa wa kuishi kifungoni kwa kutokuifahamu kweli. Kielelezo kizuri cha mojawapo ya kweli ni somo la kubarikiwa kwa njia ya matoleo.

  Ngoja nimalizie kwa kukumbusha kuwa, kanisa la kwanza la bwana Yesu Kristo chini ya mitume wake ni kielelezo kizuri kwetu kwa namna ya kufanyia kazi maneno ya Mungu. Kama ni msomaji mzuri wa biblia utaona waziwazi namna Mitume wa Yesu walivyokuwa wakiwafundisha waumini. Waliwafundisha hata namna ya kumtolea Mungu kwa uaminifu wa hali ya juu. Story ya Ananias na Safira namna bwana alivyowahukumu ni sehemu moja ya mafundisho ya utoaji ninayoogelea. Wenzetu walifikia mpaka kuuza viwanja vyao na kuleta matoleo kujenga ufalme wa Mungu. Tunapofanya hivyo leo watu wanapiga makelele kuwa tunageuza makanisa sehemu za biashara.

  Wapendwa katika Kristo Yesu, nakumbusha kuwa, kazi ya Mungu ina gharama na Yesu pale msalabani alivunja laana ya ufukara. Ni jukumu la kila muamini kuifahamu kweli na kufunguliwa vifungo na kimojawapo ni mawazo ya kifukara. Kuna watu wanafikiri kutokuwa na pesa ndio utakatifu. Mimi nimepitia maisha ya kuwanazo na kutokuwa nazo na nilijifunza hata wasionazo wamejawa na wivu na dhambi nyingine tele. Suala hapa sio kuwa nazo kwasababu binafsi. Hata wana wa Izrael Mungu aliwakomboa toka Misri wakiwa na mali zao waende kumwabudu na kuachana na sanamu.

 302. Kwa kweli watangaza utajiri au mafanikio kupitia makanisa au dini zao nafikiri si vyema hata mioyoni haikubali katika uwepo wa kumtangaza Kristo,maana yeye Yesu alikuja kuwatoa na kuwakomboa watu dhambini na kuwapa uweza watu watakaompokea wa kushinda dhambi,hivyo ni vyema tumtangaze kristo kupitia neno la Mungu (Biblia),uponyaji,utajiri,uchumba,masomo nk hizo ni kati ya karama au vitu vidogo sana katika uweza wa ki Mungu hivyo tusifurahie sana kupata sadaka, kuponya au kuwaombea watu wakafanikiwa kulioko kuwa katika safari na matendo ya kiungu(mbinguni),watu wa Mungu natujirekebishe Wapendwa!

 303. Naona tupo kwenye information society (generation) kiasi kwamba watu sasa wapo makini sana kwenye masuala ya habari yoyote, Sasa watumishi nao wanajaribu kutumia lugha ile ambayo generation tuliyo nayo inapenda kusikia.
  Kitu cha msingi ni je baada ya kuwapata watu wanalishwa nini kwani kwa Yesu Kristo tunashiriki baraka zote za mafanikio katika afya, roho, utajiri kama baba Yetu Ibrahimu.
  Naamini kitu cha msingi ni kuwalisha watu baraka za rohoni kwanza then mafanikio kiafya, pesa nk Yesu atafanya.

 304. Waongozwao na Roho wa Mungu, ndio wana wa Mungu. Palipo na mwongozo wa Roho wa Mungu pana udhihirisho wa nguvu za Mungu hivyo hakuna haja ya ushawishi wa kibinadamu kwa watu kumtolea Mungu. Upo usemi kwa kiswahili debe tupu, halikosi kelele. Ukipindua maana ya usemi huo kikristo ni sawa na kusema, ujazwapo Roho na kutembea katika udhihirisho wa Nguvu za Roho Mtakatifu, huna haja kuwashurutisha watu kutoa, wataongozwa kumtolea yeye anayewahudumia.

  Kwa maoni yangu mimi sioni tatizo katika kumtolea Mungu kwa moyo safi. Thamani ya kifo cha Yesu msalabani haiwezi kulinganishwa na chochote katika dunia hii. Tunamtolea Mungu kuthibitisha utii wetu kwake na kutimiza kanuni ya kupokea baraka kupitia matoleo. Biblia iko wazi kabisa juu ya kanuni za kumtolea Mungu. Mimi binafsi sijivuni, ila ninathibitisha kuwa nimemuona Mungu akinibariki kupitia uaminifu kwa njia ya matoleo.

  Ninajua wapo waliojitumbukiza katika ufalme wa Mungu kama mbwa mwitu waliovaa ngozi ya kondoo. Mimi alinisumbui hili kwani biblia imeshaeleza kuwa bwana ndio anayeshughulika na magugu yanayoota pamoja na ngano. Ebu tuwe na mtazamo-positive katika kuliangalia suala hili kwani Mungu anangalia uaminifu wetu ili atubariki sawa sawa na ahadi zake. Ninaishi nje ya africa, nimejifunza wenzetu wana mtazamo tofauti katika kumtolea Mungu, na matokeo yanaonekana jinsi wanavyobarikiwa. Roho ya ufukara katika bara letu itazidiwa nguvu tukiwa watu wa vitendo na sio maneno matupu. Andiko la ngamia kwenye tundu ya sindano, watu wengi wanajengea hoja ya kudumaa katika kumtolea Mungu wakati biblia ina maandiko mengi yenye kuonyesha kuwa, bwana ndiye atowaye uwezo kwa watu wake kufanikiwa/kubarikiwa. Wapo watu wa Mungu kwenye biblia walio matajiri na hata wakati wa Yesu matajiri wakristo walikuwepo.

 305. pesa na kila kitu mimi naona ni muhimu kwa mwanadamu kwa kupigwa kwa yesu sisi hatutakiwi tena kuishi chini ya magonjwa umasikini wala kitu chochote kinacholeta huzuni maana yesu amechukua kila huzuni ila tu tusiabudu pesa ,tumuabudu yesu na kitu cha muhim ni kujua kuwa amelaaniwa mtu amtegemeaye mwanadam watumishi wa mungu hawana kosa kabisa wanahubiri utajiri kwa maana watu wengi wanafikiri yesu aliponya tu.kumbe kama watoto wa mungu hata utajili ni wetu,ikiwa Baba yetu ni tajiri ni lazima hata watoto wake tufanane nae tuonekane ni watoto wa Muumba mbingu na nchi hawa watumishi wanatufundisha kuwa umasikini ni wa shetani.na utajiri ni wa watoto wa mungu.mbarikiwe na Bwana amina

 306. Sidhani kama kuna mtu hapendi kuwa tajiri nadhani wote tunapenda! Yesu alivyosema ni vigumu tajiri kuingia katika ufalme wa mbingu alijua kwamba shina la uovu wote ni kupenda pesa, wengi wameacha imani, wakamsahau Mungu. Yaani unaweza kukuta mtu alikuwa mtumishi mzuri au mtu mzuri ana upendo kwa watu, hakosi kanisani lakini akishapata pesa tu! humuoni anaanza kiburi na majivuno, anaona hakuna kama yeye au bila yeye hakifanyiki kitu. Anaweza kufanya lolote kwa sababu ya PESA na huwezi kumshauri lolote. Hao wenye utajiri wa namna hiyo ni vigumu kuuona ufalme wa mbingu.

  Hawa watumishi wanaohubiri kuhusu utajiri ni sawa, watapataje watu? watu wengi wanawaza utajiri/pesa kuliko kitu chochote kile. Wasiojiweza ni wengi, Wanaweza kufanya lolote lile wanaposikia suala la utajiri! Tatizo linakuja ni namna gani wahubiri wanavyowavua watu, kwa style gani na wanawalisha nini (mafundisho). Kuna watumishi walioitwa na Mungu na waliojiita wenyewe. Hapo ndio magugu na ngano vitakapo onekana.

 307. Mungu alipoumba mbingu na nchi nakumtuma yesu kristo wakati wa huduma yake hakuwahi kuwaita watu kuwaombea wapate utajiri isipokuwa kaulimbiu yake ilikuwa ni vigumu tajiri kuingia ktk ufalme wa mbinguni sasa,watumishi wanao tumia mbiu hii wanaongozwa na andikogani ? Sipingi utajiri lakini ninahofu na watumishi hawa!

 308. This is a nice blog can you please provide us na mafundisho and mahubiri mbalimbali so that na sisi tulio mbali na nyumbani tuweze kubarikiwa. Asanteni kwa kuanzisha hii blog page.

 309. siku ya hukumu kila mtu atatoa hesabu ndomaana yesu akawaambia viache ngano na magugu vikue pamoja wakati wa mavuno mwenye shamba atachagua ngano na magugu kuyachoma motoni.

 310. Lakini pia imewasaidia kwa kiasi kikubwa wale waliokuwa wanakimbilia kwa waganga wa kienyeji siku hizi wanakimbilia kwa Yesu hata kama wanalipa lakini wanaponywa na miujiza inatendeka kwao. Hao watumishi watapambana na Mungu, kwani biblia inasema sio wote wamwitao Bwana Bwana watakaoingia mbinguni, na wale waliotoa pepo na kuponya magonjwa kwa jina la Yesu, Yesu aliwaambia ondokeni kwangu siwajui. Injili itahubiriwa kwa vyovyote vile, wenye ufahamu wataelewa na wasiolewa watatekwa katika ufahamu wao. Ufalme wa Mungu unatekwa na wenye nguvu. Ni vizuri kama tukizitambua roho zidanganyazo na kuomba kwa ajili ya wale wanaojifanya wanakondoo lakini ndani yao ni mbwa mwitu wasifanikiwe katika malengo yao.

 311. Ni kweli kabisa sasa hivi watu wengi wanamuomba Mungu kwa kufanya biashara zisizo halali kwa kuwavutia watu kwenye makanisa na kuwapa maneno ambayo ni kinyume na Biblia inavyosema. Mungu anasema hivi njooni kwangu nyinyi nyote msumbukao na kuelemewa na mizigo nami nitawatua. Lakini watu hawafanyi kama Mungu alivyoagiza wao wanafanya dini kama biashara ya kujipatia kipato ole wao wamchukizao Mungu siku ya mwisho watalia na kusaga meno. Mbarikiwe sana StrictlyGospel kwa blogu yenu mliyoifungua kwani itatutia moyo.

 312. wananitia mashaka hawa sababu naona wanawavutia watu zaidi kwa mambo ya kidunia hasa pesa,mambo ya waenza sijui nini kusudio lao lakini wanatia wasiwasi,wanahitajika wajirekebishe kama kweli wao ni wa bwana,maana “Vya kaisari wampe kaisari navya Mungu wampe Mungu.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s