NUKUU – Anthony Lusekelo

“Toa sadaka yako ili kuwezesha kipindi cha tutashinda tuma katika account halafu nitumie meseji kwa simu namba 0713725473 kwamba umetuma kiasi gani mimi nitakupigia halafu uniambie mambo yako kumi nitakuombea”

– Anthony Lusekelo (Mzee wa Upako), Channel 10, 25 June 2008

55 thoughts on “NUKUU – Anthony Lusekelo

  1. Alfa,
    Umenena ndugu.
    Katika mjadala huu kuna “VIPOFU” yaani wale wanaotetea UKAFIRI katika Ukristo na kuna wale WANAOONA yale Maandiko yanasema.
    Hata wakati Bwana Yesu alipokuwa Duniani,walikuwepo watu wengi waliokuwa wanawatetea MAFARISAYO,WAANDISHI na MASADUKAYO na Waliona kama Bwana Yesu alikuwa anawaonea/anakosea.
    MATHAYO 24:24,IMETIMIA.
    UNABII UMETIMIA.

  2. Naitwa EVANCE VENANCE MWANOSA naishi ifakara kilombero katika mkoa wa morogoro nahitaji maombi ya ufunguo niliopotea kwa kuachana na mke wangu bila ya maana ya msingi kwani mke wangu nampenda ila yeye amenikataa hanihitaji nami nipo pekeyangu sasa, na watumishi wanasema kila kilichounganishwa na mungu mwanadamu asikitenganishe

  3. BWANA YESU ANASEMA “Wala si hao tu ninaowaombea;lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao.Wote wawe na umoja;kama wewe,Baba,ulivyo ndani yangu,nami ndani yako;hao nao wawe ndani yetu;ili ulimwengu upate kusadiki kwamba wewe ndiwe uliyenituma. Yoh 17:20-22: Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao, ili wawe na umoja, kama sisi tulivyo UMOJA. Ili Ulimwengu upate kusadiki kuwa wewe ndiye uliyenituma. NI RAHISI SANA KUWAGUNDUA WATUMISHI WA SHETANI WANAOJIFANYA KUWA KAMA WATUMISHI WA KRISTO.(2Kor 11:13-15) WANAKWENDA KINYUME NA YALE ALIYOSEMA YESU.NA KWA SABABU HIYO WAO KWA WAO HAWAELEWANI ( Hawana UMOJA). KILA MTU ANA MAFUNUO YAKE KUTOKA KWA mungu WAKE. (Shetani mungu wa dunia) (2Kor 4:3-4) BWANA YESU ANAWAULIZA; Kwa nini mnaniita Bwana Bwana,walakini hamyatendi nisemayo? (Luka 6:46) BWANA YESU ANASEMA “Mmepata bure toeni bure” WAO WANATAKA PESA.(Mat 10:8). BWANA YESU ANASEMA; “Ombeni mtakalo lote nanyimtatendewa” WAO WANAWAOMBEA WATU.(Yoh 15:7). BWANA YESU ANASEMA; “Mkawafanye mataifa kuwa WANAFUNZI ” Wao wanawafanya mataifa kuwa WAKRISTO.(Mat 28:19-20). UKIFANYIKA KUWA MWANAFUNZI WA YESU,UTAFANYA KAMA BWANA YESU ALIVYOAMURU NA KUWA NA UMOJA. LAKINI UKIFANYWA MKRISTO, IMANI TOFAUTI, KUTENDA TOFAUTI, ASUBUHI KANISANI, JIONI KWENYE BAA NK.HAO NI WAFANYA BIASHARA KWA MTAJI WA JINA LA YESU WALA WASIKUSUMBUE. “IFAHAMU KWELI”.

  4. TATIZO LA WATZ NI KUSEMA SANA BILA KUSEMA KINACHOTAKIWA KIBIBLIA. KUSEMA NI TAALUMA KAMA SI KIPAJI. SEMA YALE YA KUWAJENGA WATU KIROHO. KILA USEMACHO KITOKANE NA MAANDIKO. BASI SEMA YAWAFANYAYO WATU WAVUTWE KWA YESU UTABARIKIWA.

  5. weiz ulichokisema ni sawa lakini kinachotuboa kwa huyo mzee wa upako anajifanya yeye ndo bora kuliko wengine anaponda watumishi wengine, yeye nalichotakiwa kufanya ni kuhubiri neno la mungu basi, sasananapoanza kuponda wahubiri wengine ndo hapo si tunamuona anakosea………

  6. Hakika hii ni biashara, kuna ulazima gani wa kutaja kiasi unachotoa ili upate kuombewa? Na kwa wale ambao ni masikini hatuna cha kutoa, hatustahili kuombewa?

  7. Kumbuka kitu hiki, maneno yoyote unayosikia hata kutoka kwa mpendwa mwenzako hata kama ameokoka yaneweza kuacha alama ndani ya Moyo wako, sasa inategema unakisika kitu gani, inawezakana kikawa kimekaa sawa au hakijakaa sawa, lakini angalia jinsi unavyokipokea kwasababu kina kuja ndani yake kikiwa na nguvu fulani ndani ya moyo wako ambapo unaweza ukakichukua na kukipokea kwasababu ni kitu ambacho hakilietwi na mtu wa kawaida tu, ni kitu kinacholetwa na mtu ambaye ameokoka kama wewe, ujue kina kuja ndani yake kikiwa na msukumo wa Nguvu fulani ndani yake, mpendwa mwenzako anaweza kabisa asilimia mia moja akatengeneza kitu ambacho kinawweza kikaweka alama ndani ya moyo wako, sasa hiyo alama inaweza ikawa sawa au siyo sawa, hata hili na watu waliokoka kuwasema vibaya watumishi wa Mungu, kuna kitu inazewekana kimewekwa ndani yao na wapendwa wenzao, hakijawekwa na watu wa kawaida ambao hawajaokoka, kama umeingia huko omba neema na rehema za Mungu ili uweze kutoka na kuachana na kitu cha namna hii

  8. Jamani wapendwa, sio kitu kizuri kunyosha vidole kwa watumishi wa Mungu, kumbuka neno moja, huyo mtumishi ambaye wewe unaona hakuhusu kuna mwingine huyo mtumishi amefanyika baraka katika maisha yake kwa kumuhubiria na kumpa mafundisho ya neno la Kristo ambayo yamemsogeza kutoka katika hali moja na kuingia hali nyingine, na akaona jinsi Mungu alimvyosaidia katika jambo lolote, labda ni hali yake ya kiuchumi au hali yake ya kiroho, amemuona Mungu katika maeneo mengi ya maisha yake, Hata kama unajiona umeokoka kiasi gani, una Roho ndani yako, lakini kiburi cha uzima huwa kinaanza katika kuwawonyeshea watumishi wa Mungu vidole, kama wewe ni mtumishi unaona kabisa kuna utumishi ndani yako kwasababu kila aliyeokoka ni mtumishi wa Bwana ingawa wengine hawalijui ili na kuishi mfumo mwingine wa maisha lakini huyo pia ni Mtumishi, mimi si mshirika wa Lusekelo lakini nina wiwa kusema haya, kuna siku moja niliwasikia akina mama wawili ambao walikuwa wanamsema vibaya na kumtukana mchungaji mama Rwakatare live , na mimi nikiwa karibu yao, sikutilia maanani sana, nikasema tumezoea watumishi wa Mungu wakisemwa vbaya, lakini baadaye niliporudi nyumbani nikasikia kukosa raha, amani na uchungu ukiwa ndani ya Moyo wangu, uwepo wa Mungu ukaondoka ghafla, nikawa katika hali hiyo mpaka saa nne usiku, nikatoka nje, nikawa naanza kutubu kwa akili ya dhambi zangu, ninazozikumbuka na nisizozikumbuka, baada ya toba hali hiyo haikuondoka, ndipo niliponza kumlilia na kumwuliza Mungu tatizo liko wapi, nimekorofisha eneo gani? ghafla Roho mtakatifu akanisemesha ndani yangu na kunikumbusha akaniambia maneno yale uliyoyasikia yakirushwa kwa mtumishi mama Rwakatare unabidi uyashughulikie, akanipa muongozo, ndipo nikaanza kufanya toba nikianza na wale akina mama waliokuwa wanarusha yale maneno, harafu nikija kwa mchungaji ambaye yale maneno yaliyokuwa yanaelekezwa kwake, baada ya kuomba na kufanya toba jinsi Roho mtakatifu alivyoniongoza ghafla hali hiyo ikaondoka, uwepo wa Mungu ukarudi, Raha na amani vikarejea. Sasa unaweza ukaona hali hiyo, sikushiriki katika kunena maneno dhidi ya mtumishi huyo, ila nilisikia, na kitendo cha kukaa kimya ni kama nilikuwa nimekubaliana nayo, kitendo cha kusema moyoni mwangu ni kawaida watumishi wa Mungu kusemwa vibaya, ndicho ambacho hakikuwa sawa mbele za Mungu, inawezakana watu wengi waliokoka hata wewe pia umewahi kufanya hivi au kusema ni kawaida ya watumishi wa Mungu kusemwa vibaya, na hiko kitu kikakaa ndani yako, na kuzoeleka, lakini nataka kukuambia hiyo ni roho nyingine umebeba, Mimi sio mshirika wa mama Rwakatare nina mchungaji wangu lakini Mungu hakujali hiko kitu, nilibebeshwa mzigo wa kufanya toba na kuomba, wapendwa ningependa sana tujifunze katika haya,

  9. Mungu wetu ni Mkuu sana, hapangiwi nini afanye, huwa anafanya atakavyo yeye.
    Ni imani yetu kumwambia na kuutukuza ukuu wake ili awe sehemu ya utendaji katika maisha yetu ya kila siku.

  10. Kuhusu kesi ya Mzee wa upako. Sina mengi yakusema. Isipokua kuunga mkono Bernard Mwenda na wengine walio comment kama yeye.

    Kwa kweli, angefundisha watu neno peke yake. Watu wakiguswa na Roho wa Bwana, watatowa pesa kwa mchango wa huduma na watatowa na upendo, na sadaka hiyo itamfurahisha Mungu kweli. Na kazi ya Mungu itazidi kuendeleya na maumini wataokoka kwa wingi.

    Kuambiya watu wajitambulishe watakapo toa na watume maitaji ya shida zao kwa maombezi, itachangiya kuonyesha kama huduma inakuwa business. Acha wataoguswa na miujiza ao neema ya Mungu, watoe kwa initiative yao wenyewe and not giving in exchange of a miracle as this type of teaching would be heretical and very dangerous for the Body of Christ.

    Kingine: kuepuka haya maneno yote ya kwamba kanisa za walokole ni business, watumishi wa Mungu na makanisa wafikiriye njia zingine za kuingiza pesa zitakazo saidiya kwa huduma (income generating projects or ventures); hapa tunaweza kuiga mfano wa kanisa katolika. Wanafanya kazi kweli na inasaidiya sana kwa huduma. Pesa hizi zitajiongeza kwa zile waumini wanajitoleya kwa upendo na itasaidiya kweli. Yote nikuzungumza na kusharikiyana. Kanisa zitakuwa managed katika financial indipendence badala ya kuwa mzigo kwa waumini. Sijui wengine wanafikiriyaje?

  11. Bwana asifiwe sana.

    Nimesoma comments zote na nimefurahi sana. Inaonyesha wazi kama watu tofauti kutoka pande zote (walokole na wale bado kuokoka) wanafatiliya swala hili. Na kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake.

    1. Shida ya watu wamoja hapa (=walokole kuzidi wengine), wanataka kuogopesha wenzao eti watapata ukoma sijui nini na kadhalika. Badala ya kuwaogopesha wale mnaowaita kama hawajui ukweli na hawajaona mwanga, kwa nini nyie mnao ujuzi huo msiwafundishe na wenyewe wapate kufahamu neema na fadhili za Mungu?

    2. Kuna mabo yanayo pitikana ndani ya kanisa tukufu la Bwana leo hii, mengi mazuri na yangine yanasikitisha sana. Ukweli ni kwamba kuna denja inayoletwa na enjili inayoitwa “Prosperity Gospel”. Kuna baadhi ya wanaoitwa “watumishi wa Mungu” wanachangiya sana kwa kupeperusha enjili hii, na waumini wengi wanafundishwa kwamba watapo toa sadaka zao (tithe, seed etc…), watamfanya Mungu kufunguwa milango ya mbingu na kuwamwgiya mvuwa ya baraka zake ktk maisha yao. Denja ni kwamba, wengi ya watumishi hawa wanatumiya lugha ya ki saikoloji wakiisapoti na mistari kadha ya bibliya, wangine wanatumiya hypnosis na kuwaitikisha watu kuwa wamepona ao wamepata miujiza mbali mbali hata wangine wanajidai kuwa wanauwezo wakuwapa watu nguvu za Roho Mtakatifu, wengine wanatabiri maneno ya uongo mtupu na kuchonganisha na kutenganisha watu na vinginevyo. Mambo yakusikitisha ni chungu nzima. Hapa naomba radhi, sijataja jina la mtu; kusitokee mtu atakayesema eti nimemtukana ao nimetunga kidole mtumishi fulani. La. Nasema kiujumla mambo yasiowezekana yanayotendwa ndani ya kanisa kwa kutumiya neno la Bwana.

    Wakristo wengine wanakaa kanisani utafikiri ni mashabiki; wengi hawafundishwi neno ki halali. Wanasomewa mistari fulani, alafu matafsiri yanakuwa ya kugusa shida za kimwili (sijui ugonjwa, uponyaji, kupata kazi, kupewa promosheni, kutajirika kwa miujiza, kupewa viza za ulaya na marekani, kuowa na kuolewa, etc…) Sikatai kuwa Mungu hawezi kuyatimiza haya yote; anweza na zaidi.

    Misheni ya kanisa (kama mwanzoni pale Bwana Yesu alipowatuma mitume wake) ni kuipasha habari njema ya uokovu, tukifundisha watu kuacha njia ya dhambi na maovu yote na kuirudiliya njia sawa ya Mungu. Kwake njo kuna amani, furaha na baraka zote.

    Tuwafundishe walio inje na ndani ya kanisa enjili ya uokovu na kusamehewa zambi, enjili itakayo fasiriya watu kufika msalabani, enjili ya ufalme wa Mungu. Tunawajibika kufundisha watu na kuwakuza katika mambo ya kiroho. Ndipo watapenda maneno ya Mungu na watamfurahisha kweli. Watajazwa na Roho wa Bwana. atawasaidiya kugeuza mwenendo wao na kuzaa matunda ya kiroho. Kwa kifupi, maisha yao yatabadilika natashudiya ipaswavo kwa ukweli na kiroho. Watahubiriya ndugu, jamaa, marafiki na wengieo kwa enjili walioijua na matunda safi ya kiroho.

    Ila shida ni kwamba, hii “Prosperity Gospel” inayofundishwa leo, imewafanya wengi kuwa vilema kwa neno la Mungu na yangine mabo ya kiroho. Wengi wanakuja kanisani wakitafuta miujiza na majibu ya shida zao za kimwili badala ya kutafuta uponyaji wa roho zao na kusamehewa zambi. Kuna wengine kweli wanataka kuokoka, ila wanakutaka na enjili ya kutajirika, wanakwama apo apo.

    Tujuwe ya kwamba shetani ameingiza watumishi wake ndani ya kanisa, na hawa wanachanganya watu kweli.

    Nitarudi.

    Guillaume

  12. jamani hvi wapendwa tutaacha lini kuwasema vbaya watumishi wa mungu we kama unaamini mungu yuko toa kwa moyo we mtumishi akila pesa mungu atamuangamiza kumbuka uongo hau last forever, ila mi binafsi siamini kama mzee wa angekuwa tapeli angendumu kwa miaka 25 kwenye huduma na miaka 5 yenye upako wa nguvu ambao unafanya leo tuwe hapa kumtetea na wengine kumsema vibaya pasipo kumjua au atakumshuhudia akihubiri ila sishangai maana hata yesu mwana wa mungu alizikiwa sembuse mzee wa upako.mungu ambariki asante kama mtanielewa ?

  13. Mchungaji Anthony Lusekelo anatufundisha jinsi ya kukaa karibu na Mungu Tatizo wengi wetu hatufahamu umuhimu wa kumtolea Mungui Sadaka na hivyo kujiwekea hazina Mbinguni na vilevile ili kazi ya injili iweze kuendelezwa hapa duniani na watu wengi kupata ufunuo wa injili sadaka ni muhimu sana

    Kanisa linahitaji kulipiwa umeme,wachungaji na watenda kazi wapate mshahara,usafiri na kulipia matangazo ya Television ili injili iwafikie watu wengi zaidi.

    Hii haina maana ya kununua injili. Unapotoa sadaka basi unamtolea Mungu Mbona Kristo alisubiliwa ili tuokelewe!! Wote mliotoa maoni mna majina ya kikristo ni aibu kubwa kwa mkristo kutokufahamu maana ya sadaka Hebu someni Biblia zenu vizuri mfahamu maana ya kumtolea Mungu. Hakuna Kanisa lolote ambalo hakuna sadaka. Kuombewa na wachungaji ni jambo la kawaida Makanisa yote KKKT, Katoliki baada ya sadaka kutolewa mchungaji au Padri anaziombea kabla ya kufunga ibada. Kuna sadaka mbalimbali za viwango kuhusu ujenzi wa kanisa na mahitaji mengineyo ya kiroho Ndugu zangui Makanisa yote tunayoyaona hapa Duniani yamejengwa kwa sadaka za waumini.Ulaya na Marekani wanaendelea kuwa matajiri na kubarikiwa na mungu kwa ajili ya kutupa misaada huku Africa Sisi waafrika au watanzania tuko tayari kuchangia harusi za kifahari, kunywa pombe, kufanya zinaa kuliko kutoa sadaka Hata ndugu zetu na marafiki zetu wanapokuwa na shida za kupeleka watoto shule tunashindwa kuwasaidia na kuendekeza anasa zaidi kuliko kutoa.

    Acheni upumbavu wa kutukana watumishi wa Mungu, kasomeni Biblia zenu vizuri mfahamu neno la Mungu na umuhimu wa kutoa sadaka Hali kadhalika mnatakiwa kusoma mara kwa mara kuhudhuria makongamano mbalimbali au kujiunga na Bible Schools za online ili mfahamu vizuri injili

  14. Hakuna apingae kumtolea Mungu. Ila watu wanapotumia tumia neno kwa maslahi zao hili ni tatizo. Huwezi kununua huduma yeyote toka kwa Mungu, maana Mungu hana dhiki kiasi cha kukuuzia huduma. Utoaji ukifanyika kwa moyo wakupenda hii ni sawa lkn si vingnevyo.

  15. Hakuna apingae kumtolea Mungu. Ila watu wanapotumia tumia neno kwa maslahi zao hili ni tatizo. Huwezi kununua huduma yeyote toka kwa Mungu, maana Mungu hana dhiki kiasi cha kukuuzia huduma. Utoaji ukifanyika kwa moyo wakupenda hii ni sawa lkn vingnevyo.

  16. msidanganyike apandacho mtu ndicho atakachovuna,kama mtu hawezi kumtumikia mungu kwa njia ya utoaji ni bora akae kimya kuliko kumtolea matamshi mtumishi mtumishi wa mungu,na ni kwa vile watu hawaujui ulimwengu wa roho ulivyo.kama kwa yeyote kutoa ni ngumu kuna watu wamepakwa mafuta kwa ajili ya kazi ya mungu.so acheni kumjadili mtumishi wa mungu.tafuteni mada nyingine

  17. need to know the account number for deposit, kwasababu kweli nimeguswa na maombezi anayofanya mtumishi, kwahiyo namimi nahitaji

  18. natamani wasonge mbele huku anayejaliwa kupata chochote awawezeshe kwani injili nayo ni gharama.biblia tu huuzwa kwa gharama kubwa n.k
    mungu awabariki wote wanaomtangaza kwa gharama yoyote.
    HAKIKA TUSIKATE TAMAA TUTASHINDA.

  19. Mungu Akusaidie Mtumishe ,nimepitia maoni mengi Mungu aendelee kuwatunza na kuwa linda manaowapa moyo watumishi,hata Mwakasege alitufundisha usikubali kabisa mtu akukataze utoaji kwa ajili ya huduma ya Mungu na ndiyo maana kuna michango kwa ajili ya kuendesha vipindi vyake katika Star TV na radio station nyingine,huduma ya vitabu tunanunua siyo bure kwasababu kuna gharama,na ikiwezekana unaweza hata kununua zaidi ukagawa ni sadaka yako,perception za watu kutokana na tangazo mtumishi hajasema nitawaombea au kuwahudumia watakaotuma hela pekee yake.tusiwe na tafsiri sisisi,ambayo inaleta upotoshaji,huku upande wa pili hata wakiambiwa milioni moja ili kitu fulani kiendelee wala hawabishi,ni dakika lakini shetani ameweka mioyo migumu,na zaidi kutafsiri vibaya pale inapobidi ili kuua Roho ya utoaji ili huduma ya Mungu isisonge mbele “WATAENDAJE WASIPOPELEKWA”gharama za tv ni kubwa na mwenye kuguswa na kuona kuwa huduma ya Mtumishi inawabariki wengi kwa Utukufu wa Mungu basi wasaidie,wachangie.
    Hizi ni mbinu za Ibilisi tu na zitashindwa na Injili Itasonga mbele,hatutaabika kuomabomba kwa ajili ya huduma bali kila mtu ataguswa na kutoa kwa Ajili Ya Bwana
    Amen.

  20. Mungu akukumbuke mtumishi wa Mungu Antony kwa maombi yako hakika wengi tumepona kupitia huduma yako ya tutashida hivyo nakutia moyo endelea ujira wako uu kwa baba aliye mbinguni.

  21. Mi nawaomba wapendwa tusibishane kuhusu huyu mtumishi wa Mungu. ni bora kukaa kimya kama unaona wewe unaibiwa basi usichangie hiyo pesa yako, maana unamshtumu bure wakati hakuna anayeijua kweli. Ni Mungu pekee ndo anajua. Cha kufanya ni kupiga magoti muombe Mungu wako akusaidie ili uweze kufahamu kweli. Kuliko kupoteza muda wako kuandika kuwa mtumishi wa Mungu anafanya biashara/anatapeli..! mwenyenzi Mungu atusaidie

  22. Mungu akutie nguvu mtumishi wa Mungu Anthony Lusekelo.Hata kwenye maharusi kuna viwango vya kutoa.Na Bwana Yesu anasema hata asiye na kitu kido atanyang’anywa apewe mwenye vingi.Tuwaache wanaokumbatia umaskini.Kipindi hela,unamuona mzee wa upako kwenye t.v kwasababu kipindi kimelipiwa.Watu wanachanga kichen party,send off,harusi lakini kwa Mungu kila mtu anajiona najua neno.It’s not true,kama ilivyo ukiumwa unaenda hospital,ndivyo ilivyo kwa maswala ya rohono kwa watumishi wa Mungu.Cha ajabu hata mlevi anakwambia anajua neno.Mungu akutie nguvu mtumishi wa Mungu Baba yangu Anthony Lusekelo.Kazi yako ni njema.Ipo siku Mungu atakuvalisha taji,an pia utafuta machozi,atakwambia karibu mwanangu.Niko Marekani lakini siwezi kukusahau babayangu.

  23. Edmund John Oguda,

    Shalom!

    Pole sana ndugu yangu Oguda, nakuona una uchungu sana na unasikitishwa na kauli za watu mbalimbali katika blog hii, wanavyomwandika mtumishi wa Mungu mchungaji Antony Lusekelo.

    Mimi kwa maoni yangu, naona hiyo iwe ni changamoto kwa kila mtumishi wa Mungu kuelewa kuwa, kumbe kuna mambo mengine tunaweza tukayafanya kwa kudhani kuwa ni sahihi mbele za wale tunaowalenga, kumbe kwa upande wa pili ikawa sivyo.

    Kuhusu kuchangia huduma, kwa mtazamo wa mhubiri, tangazo hili ataliona kuwa ni sahihi kwa sababu macho yake yanakuwa yanamtazama mlengwa, ambaye ni mwenye shida na pia anakuwa anamtazama mshirika wake ambaye pia tayari anaikubali huduma yake. Pia macho ya mhubiri yanakuwa yanatazama uhalali wa mtu kujitoa kwa ajili ya kazi ya Mungu, bila kutazama pia kuwa tangazo lake linatazamwa na na watu wa aina ipi na ipi! Mhubiri kosa analokuwa analifanya hapa ni kwamba haangalii upande wa pili, kwamba wale wasio na shida kama ile anayoiona yeye, na pia wale ambao hawajamkubali kama ni mtumishi mwenye kuweza kutoa msaada huo watamwonaje, hili ndilo kosa analokuwa analifanya mhubiri, wakati mwingi pasipo kujua. Tangazo kama hili litakuwa limewapata wale walio upande wake, na wale ambao hawapo upande wake litakuwa limewatupa mbali zaidi, badala ya kuwasogeza.

    Mimi kwa sasa naishi Zanzibar, nakumbuka siku moja nikiwa katika luninga nyumani kwangu, niliona mahubiri ya mtumishi wa Mungu Askofu Kakobe, ambayo yalikuwa yanahusu mavazi. Katika kipindi hicho alisimulia pia kuwa, yeye kabla hajaweza kujua sana juu ya umuhimi wa mavazi ya mtu aliyeokoka, siku moja mke wake alikuwa anashuhudia mitaani. Katika kushuhudia kwake, alikutana na dada moja dukani, kama kawaida kwa kazi aliyotumwa na Kristo mama huyo alimshuhudia yule dada wa dukani juu ya Yesu anayeokoa. Kakobe anasema, yule dada wa dukani alimwambia mke wake maneno haya, “Mimi nikiokoka nitaokoka kweli kweli; sitaokoka kinafikinafiki kama hivi” Yule dada aliyasema maneno hayo huku akimwangalia mke wa Askofu Kakobe kwa dharau.

    Mama wa watu aliondoka pale akiwa amehuzunishwa sana, asijue ni kwa nini aliambiwa hasa maneno hayo. Alimsimulia mumewe yaani Askofu Kakobe, naye Kakobe alihuzunika na kumwambia mkewe kuwa asijali; hao ni watu wasiojua maana ya wokovu kwa sababu wao hudhani kuwa wokovu uko katika mavazi! Lakini Kakobe anasema katika mahubiri yake niliyofuatilia kuwa, siku moja alipata ufunuo juu ya mavazi yanayostahili kwa watu wanaokuwa wameokolewa, wanawake na wanaume. Anasema mke wake alikuwa ni mtu wa kujipamba sana, mawigi, eleni bangili n.k. Aligundua kuwa, kumbe watakatifu wa Mungu katika maisha yetu ya wokovu tunatakiwa tusiwe na lolote ambalo litawafanya wale ambao hawajaokoka kukwazwa. Alifundisha siku hiyo kuwa, lolote tunaloambiwa na watu ambao hawajaokoka kuwa halifai, tujue kuwa ndivyo ilivyo; kwa sababu nao wana roho anayewashuhudia, akiwashitaki au kuwatetea. Nikilinganisha mafundisho hayo ya Mch. Kakobe na huzuni anayoipata ndg. yangu Oguda kwa mch. Lusekelo, nagundua kuwa kuna kitu kinachofanana na yale yaliyompata Kakobe juu ya mavazi aliyokuwa amevaa mke wake akiwa katika kushuhudia mitaani.

    Narudi kwa kwako ndg. Oguda. Lengo la Injili ni kuwafanya watu wengi wamjue Kristo, na katika kufanya hivyo, tunatakiwa kuhakikisha kuwa, Injili yetu inahubiriwa pasipo lawama zisizo za lazima. Kila kanisa linahitaji fedha kwa ajili ya kuendeshea huduma ya kanisa, tunatakiwa kufahamu kuwa huduma ya Injili kwa njia ya luninga inaporushwa, kila anayefungua station hiyo anakuwa anakiona kipindi hicho. Aliyeokoka, asiyeokoka, aliye kinyume na mtumishi anayekuwa hewani, wote wanakuwa wakiangalia kipindi hicho, na hapo ndipo tatizo linapoanzia. Lengo kama nilivyosema hapo juu ni kuhubiri Injili kwa watu ambao hawajamjua Kristo, watu hawa wanatakiwa kuipata injili hii bure, pale tunapokuwa tunachanganya Injili hii [ambayo Mungu anatuagiza kuwa tuitoe bure] na matangazo ya michango, watu ambao hawajamjua Kristo tunakuwa tunawachanganya; watatuona kuwa tunafanya biashara, na badala ya kuwafanya waokoke tutakuwa tunazidi kuwapeleka mbali zaidi.

    Cha kufanya:-
    Ili kupata fedha au nyenzo yoyote kwa kwa ajili ya kazi ya Mungu, fedha hizo au nyenzo hizo tuchangishane kanisani mwetu, bila kushirikisha watu wengine ambao hawajamjua Kristo. Kazi hii ya kutafuta fedha, luninga au magazeti yasitumike kama chombo cha kutangazia. Walioko katika makanisa yetu, wanaopata huduma za kiroho kwetu, wanakuwa tayari wanaelewa maana ya kujitoa na wanaelewa pia umuhimu wa kufanya hivyo, kwa sababu tayari tunakuwa tumewafundisha. Pia kama tutakuwa na uhusiano mzuri na makanisa mengine, tunaweza kuwaomba hao eidha kwa kuwaandikia au physically, tukielezea nia yetu ya kuhitaji kupata msaada kwao. Hapo tutakuwa tumefunga kinywa cha ibilisi. Tusimwage mambo yetu kwa watu wasiojua hata maana ya wokovu, na tunapoona re-action kama hizi, tujue kuwa ndivyo inavyochukuliwa na watu wengi kwamba, huduma za walokole ni za kibiashara tu.

    Haya ni maoni yangu tu.

    Shalom!

  24. Ndg zangu,ktk Bwn Yesu,nawasalimu ktk hlo jina kubwa? Ndg zangu,haswa Leornad na John Paul na wengineo,lzm kutambua kuwa kila mtu anaitwa kwa wito wake,hatuitwi wote kuwa wa aina moja ktk utumishi huu, Mungu ni mpana sana,na utumishi wake umepanuka saana. Hivyo,ni makosa makubwa kumfananisha hata Nabii huyu na Nabii yule ktk wito na utendaji wao ingawa wote ni Manabii,Wainjilisti,Waalimu,Mitume ama Wachungaji. Kuweni makini sana mnapojadili kwa kumlinganisha Mch. Lusekelo na Mwakasege, Kakobe au Fernandes wa Atn,labda kwanza tulielewe andiko hili,na Roho mtakatifu awasaidie kung’amua siri yake; ktk kitabu cha 1KOR.12:6-7,”Kisha pana TOFAUTI za KUTENDA KAZI,bali Mungu ni yy yule azitendaye kazi zote ktk wote. Lkn KILA MMOJA HUPEWA UFUNUO wa Roho kufaidiana”. Mmeelewa hpo? Ss,kuanza kuuliza kuwa,kwa nini Lusekelo atangulize kuomba kuchangiwa,kisha ktk hy michango ueleze shida zako,hapo mnakwenda mbali,ninyi ni wachokozi pasina sababu,yaani, ‘very provocative men of God’,kwani,hao watumishi wengine nao wanasemaje? Hawanaga lugha mbadala,wao,huwa wanahubiri,kisha wakimaliza wanakwambia kuwa, ‘km umebarikiwa na kipindi hiki,hebu tuma mchango wako na Mungu atakubariki’,baadhi yao husema kuwa, ‘nitaomba nawe ktk shida yako’. Nambieni,hz statement zina tofauti gani? Mtambue,km ilivyoandikwa ktk,1KOR.12:28,”Na Mungu AMEWEKA wengine ktk Kanisa,wa kwanza Mitume,wa pili Manabii,wa tatu Waalimu,kisha MIUJIZA,kisha karama za KUPONYA WAGONJWA,…….”. Mungu amempa Mch. Lusekelo ktk vipawa hivyo sehemu,yaani,miujiza na uponjaji,sasa,na hili ndo tatizo kubwa la mwanaadamu,zaidi asiye na Mungu,wako watu waliofungwa,wako mikoani ht nje ya nchi,siyo kila mtu ana uwezo wa kufika Dsm,ama pl Ubungo Kibangu. Ss kwa mtu wa masafa afanyeje mnadhani ili apate huduma ya kuombewa? Na wale wasiojiweza wenye nauli tu pengine ya kufika Ubungo pasipo hy michango ya tv na wakapata uponyaji,unabii au miujiza ya papo kwa papo na kisha baadaye wakaja kumshukuru Mungu wa Upako kwa matendo makuu. Maana,hao ndio mnaodai kana kwamba mnawasemea ati,lkn si kweli,nililisikia na kulisoma lile tangazo,halina nia mbaya km mnavyozungumza kwa dharau hvyo, kwani kumtolea mnaelewa maana yke? Kristo aliyatoa maisha yake kwanza,ili atununue kwa damu,naam,alipokuwa akiuelekea msalaba,thamani ya ukombozi ilikuwa ni damu yake,sikiliza,nisemacho ni hki,zipo kanuni za utoaji wa sadaka mbalimbali,sadaka yoyote siyo zawadi,alipomtoa Kristo,kwa ile damu,alitarajia mimi,nanyi na yeyote atakayekubali kuyatoa maisha yatu kwake, ‘xchange program’,nothing goes free,ndg zangu, hakuna sadaka isiyosemewa neno,alichofanya Mzee wa Upako ni kuwafundisha hao wachangiaji hizo fikra za kuisemea sadaka yao watakayochangia wakiwa long ‘distances’,where is the problem wana wa Mungu? Msimchukie mtu kwa kiwango hicho nyie watumishi,the guy(MCH.LUSEKELO) means,business ,anataka kusaidia kila mtu,siyo kweli kuwa anaangalia wenye nazo tu,hapana,walio mbali na kuwa na shauku ya kuchangia wafanyeje? In return,ni lzm waorodheshe shida zao. Kwani,mmesahau,apandacho mtu, wana wa Mungu? Mubarikiwe.

  25. Jamani casiana tambua ya kuwa mungu anatambua maskani wanapatia nini lakin ukiwa maskin waweza tuma maombi yako ili mungu aweze mgusa aliye nayo awezeshe huduma yake na pia usi2mie advantage ya kusema maskini kwa mungu hakuna maskini fanya kaz kwa jitihada na bwana atabariki kaz ya mikono yako kama umeokoka kutoa ni lazima na kuendeleza kazi ya mungu niwajibu wakila aminie mnanikera mnaopinga huduma ya watumish kwanini mzidiscus bila sababu omben kuhuishwa nafsi zenu ndo mtaelewa kuwa mnasema nini

  26. Mimi nadhani tunapochangia hoja hizi za kiroho tusigubikwe naa upenzi na ushabiki ni vizuri turuhusu fikra na mitazamo yote kwa upole upendo na stahi nadhani hapo mjadala wa hoja utakuwa na maana.

    Pamoja na mambo mengine lakini bado Mungu ameongeza kwa kutupa akili na hekima katika kupima mabo yote yakiwemo ya kiroho. nadhani kwa kila mchagiaji ajitaidi kuzui jazba na hukumu za moja kwa moja kwani unaweza ukadhani huko sahii kumbe sio pengine ni kwa kukosa kuelewa au upungungufu wa maelezo na habari zihusuzo jambo husika.

    Mchango wangu ni kwamba ziko njia nyingi za kupata kipato kama kanisa na si michango tu.

  27. we abishai jamani sio kama tunamsema pastor vibaya hapana ila hata wewe mweyewe uangalie maisha yanatofautina sana,shida yangu ni kuwa kwa wale masikini watachangia nini na baraka wanazitaka,yeye angesema tu atakayeguswa kuchangia,bila kusema ataje na maombi anayoyataka.

  28. jamani mambo makubwa kwelikweli,navyojua mimi uponyaji wa yesu ni bure kabisaaaaaaaaa,sasa hizo hela tena ni za nini?kwa hiyo kama si hela na nina shida nitakufa na shida yangu kisa tu sina hela,most of wach.wakikuombea wanataka pesa,sio vema,vipi kwa yule masikini hamuwezi kumfanyia huduma?yesu ni bwana wa wote masikini na matajiri mungu ni yule jana leo na milele.

  29. Shalom mchungaji huduma yako ipo juu na na nyie mnaotafsiri ujumbe huu vibaya mkome. kuchangia vikao vya harusi wa kwanza lakin kuwezesha kipindi mnaona ishu na wewe unayekandia ujue utalipa gharama ya kumsema mtumishi na mtubu wote mnaotoa kashfa

  30. Shalom,
    samahani kama mnaona tunatukana hapana, mie naona iko haja kama anavyosema Leonard ujumbe wake kubadilishwa. Mtumishi huyu kila kona wanamfanya ni kituko kutokana na hicho kipindi kwa nini? hilo tangazo la kuomba hela, kwani askof Kakobe hahitaji hela/ halipii vipindi? wanaotumia redio kama Mwl Mwakasege hawalipii? amwombe Mungu amwonyeshe jinsi gani hela ipatikane kwa ajili ya huduma hiyo. Ni lazima tuseme ukweli kuwa lugha hii inawafanya watu waone kama watumishi wa Mungu ni wachumi au wasanii fulani hivi. Kwanini asitumie muda mwingine kabisa kufanya tangazo maalumu la kuomba kuchangia huduma na sio kuliweka pamoja na anayetuma maombi hapa imesomeka ni biashara zaidi. Mtumishi au mtu yeyote unapotoa huduma ukiishatanguliza lugha ya hela unaelewekaje? hata iwe ni ofisini? Tunajifunza.

  31. AMEN AMEN MTUMISHI WA MUNGU JOHN, NIMEKUELEWA VIZURI SANA ,HAPA NAFIKIRI SASA KUNA HAJA YA WATUMISHI WA MUNGU KABLA YA KUTOA TANGAZO LOLOTE NI MUHIMU KUWASHIRIKISHA VIONGOZI WA HUDUMA PIA, KUANGALIA NAMNA YA KUFIKISHA UJUMBE KWA WATU WENGINE, ASANTE SANA JOHN, TUNAJIFUNZA

  32. Ndugu Leonard,

    Mimi nakubaliana nawe kabisa kwamba hakuna mtu anayelazimishwa kuchangia kuhusu huduma hiyo ambayo kwa kweli inahitaji pesa nyingi kwa ajili ya kulipia muda wa hewani kwenye TV pamoja na mahitaji mengine.

    Pia ninakubaliana nawe kabisa kwamba watu ambao hawajaokoka hawajajua laana ya kunyooshea vidole watumishi wa Mungu. Lakini kwa kiasi hicho ambacho hawajajua laana ya kunyooshea mikono watumishi wa Mungu vile vile hawawezi kuelewa ni kwa nini hadi mtu utume pesa ndipo utaje mahitaji yako.

    Mimi nafikiria hivi;

    i. Si lazima anayetuma pesa awe na mahitaji ya kuombewa: kwa hiyo kama kila ukituma pesa ni lazima utaje mahitaji yako 10, asiye na mahitaji ya kutaja anaweza akashawishika kutokutuma kwa sababu hana mahitaji ya kutaja atakapoulizwa kufanya hivyo. Ataona kwamba wanaotakiwa kuchangia ni wale wenye mahitaji peke yao.

    ii. Siyo kila mwenye mahitaji atakuwa na pesa za kutuma. Hivyo yule mwenye uhitaji wa maombezi na hana pesa za kuchangia atakosa maombezi hayo maana hadi utume pesa ndipo upigiwe simu utaje mahitaji yako.

    Ndiyo maana kwenye mchango wangu wa tarehe 4, Sept, 2008 niliandika kwamba una kumuhimu wa kutafuta lugha nzuri ili kuliweka suala hili vizuri kwamba uponyaji hauuzwi. Hii itamuwezesha hata asiye na pesa kupiga simu yake na kutaja mahitaji yake hata kama hajachangia. Vile vile mtu ambaye hahitaji maombezii ataweza kuchangia kwa ajili ya kusapoti kazi ya Mungu.

    Ninafikiri ni sahihi nikisema hivi: Kuchangia pesa kwa ajili ya huduma si kwa watu wenye mahitaji tu na pia maombezi si kwa ajili ya watu wenye pesa tu!

    Mungu wa mbinguni atusaidie kuwa hekima na maarifa na azidi kuwapa nguvu watumishi wake wote kwa ujumla.

  33. Mimi ninachoona hapa ni namna ya jinsi ujumbe ulivyotumwa na jinsi ya tafsiri ya ujumbe wenyewe, mtumishi hajamlazimisha mtu,watu wengi huwa wanachangia sana mambo ya kidunia hata bila kuombwa , kama michango ya harusi labda ni kwa sababu tu kuwa watakula na kunywa, hii inaonyesha ni jinsi gani watu hawana hofu ya mungu,mimi nilivyo muelewa mtumishi Anthony ametoa kama kipau mbele kua badala ya kwenda kanisani kwake labda uko busy, basi baada ya kumjulisha kuwa umechangia basi umtumie mahitaji yako nae atakuombea, watu wasiookoka hawajajua laana inayotokana na kuwanyooshea vidole watumishi wa Mungu, jamani tafadhari sana chungeni vinywa vyenu. Hajasema lazima kuchangia,
    karibu tunajifunza.

  34. Mtumishi huyu alichoomba ni kuchangiwa ili kuwezesha kipindi! hapewi bure na Channel 10 wala DTV, analipia, na yeye si mfanyakazi wala mfanyabiashara, sioni tatizo kwa wanaoweza kumchangia, ili awasaidie wasioweza wapate neno la uzima na maombi. Sidhani kwamba analazimisha kila mtu, unatoa kwa hiari na kwa imani.

  35. kwakweli Mungu anasema umepewa bure towa bure sasa unasema mpaka upewe hela ndipo utowe huduma ya maombezi haipendezi mbele za Mungu kwanini asikwambie wewe nilipe kwanza ndipo nikupe nguvu za kuwaombea wagonjwa msifanye dini kama nisehemu yakujipatia hela hicho nikinyume cha biblia muogopeni mungu aliyejuu sio vizuri.

  36. Wapendwa wakristo wa kanisa ka Tanzania tuache umbea.Si hekima sana kudiscuss watumishi wa Mungu.Tuwaombee,wngine mnaongea wakati hata hamjaokoka.Kama ilivyo ukiumwa unaenda hospital kumuona doctor ndivyo ilivyo kwa watumishi wa Mungu.Biblia imeweka wazi kwamba tusiwaguse manabii zake,hata kwa maneno.Mchungaji Lusekelo hajamlazimisha mtu kutoa.Ni ihiari yako.I don’t see the reason of making it a big issue.Hizi the so blog tunazofungua za kikristo ni nzuri tukitumia kwa utukufu wa Mungu.Hata kama Daudi alianguka bado Mungu alimwita kipenzi chake.Hata leo Yesu anaitwa mwana wa Daudi.Si mbaya tukaiga nchi zingine wanavyowaheshimu na kuwaeenzi watumishi wa Mungu.Hata tusiende mbali,hapo Kenya tu.Kumbukeni watumishi wa Mungu ni kitovu cha nchi.Tanzania iko mikononi mwao.
    Blessings!!!

  37. BWNA YESU ASIFIWE!!!
    TUSIMLAUMU SANA HUYU MTUMISHI. BINAFSI NASEMA LABDA NDIVYO MUNGU ALIVYOTAKA IWE. LABDA ATAKAYECHANGIA KIPINDI HICHO ATAPATA BARAKA ZA KIPEKEE KUPITIA MAHITAJI HAYO KUMI.
    TUSIMZOMEE TUKAPATA UKOMA BURE NAYE NI MTUMISHI WA MUNGU. SIKU HIZI KUNA MAFUNUO MENGI SANA LABDA NA HILO NI MOJAWAPO.SISHANGAI!!!!
    TUNAJIFUNZA

  38. Aibu!… huyu anayeitwa Mtumishi anashindwa kujua kuwa hawa wenye matatizo wana shida na yeye akiwahudumia kwa moyo wote, Mungu atamlipa. Kumlipa huko si kuwakamua wagonjwa au wenye vifungo wengi wao yatima na wajane, bali wale walio nazo ambao watavutwa na Roho Mtakatifu kuchangia ktk huduma yake kama kina Dorcas, Yufuf wa Arimathaya, Mariam wa Magdalena na dadaye walivyofanya ktk Biblia. Mtume Paulo aliwaelekeza kufanya kazi wasiwaelemee watu, sasa huyu anawaelemea wagonjwa! Aibu, ndo maana injili haipokelewi kwa sababu ya watu wa aina yake. Mungu aturehemu na inatupasa tukemee na kuombea sana Roho hizi za ubinafsi na tamaa mbaya.
    Mbarikiwe

  39. mimi nadhani tafsiri ya uombaji michango ya kueneza ndio inawachanganya watu. Mzee wa upako ni mtumishi wa kweli wa Bwana hafanyi biashara kanisani.anahitaji sapoti kuendeleza kazi ya Mungu.tv ni sehemu ndogo sana inahitajika misaada zaidi kwa kazi aliyoitiwa.mimi ni sikuwa napesa lakini kupitia huduma yake nina maisha ya amani na furaha familia yangu ina afya tele na uwezo wa kuhimili mikimikiki ya maisha.songa mbele mzee wa upako NGULUVI NGHWE MWENE ILIKUKUHONGESIA PA KIGHONO KILA SIO VANAMUNU AMEN

    MY PHONE NO 0755333409/0715200262/0786333409

  40. Mimi ni m bantu wa tz east africa.Naamini antony ni mtumishi imara huko

  41. nimacho sema ni kwamba simama kwenye utakatifu na endelea kufanya kazi bwana aliyokuita mkono wa bwana uje juu ya maisha yako,napenda sana Mungu akutumiavyo ila usirudi nyuma wewe ni jeshi la bwana na bwana anakutumia sana wacha wanene mabaya ila kyala akutule pakafu, bwana kaniambia nisene nawe leo na nikupe moyo nitakuja Tanzania baada ya mwaka mmoja na ministy yangu itakuwa iringa
    asante

  42. Wakati Bwana Yesu alipokuwa akiitoa injili bure, Biblia inasema kulikuwa na wanawake kadha wa kadha waliokuwa wakimuhudumia kwa mali zao Lk 8:2-3,. Kumbe kulikuwa na watu waliokuwa wakimsaidia aweze kuitoa bure. Sasa basi Mtumishi wa Mungu anapotuomba tuchangie gharama za injili maana yake anatuomba sisi tunaomjua Mungu tumsaidie aweze kuitoa injili bure kwa wasiomjua Mungu bado. Ninaamini kama channel ten wangempa kipindi bure mzee wa upako naye angeitoa injili bure. TUMUUNGE MKONO MTUMISHI WA MUNGU

    Pastor John Said
    Dar es Salaam

  43. Church business?!

    Naishangaa sana hekima ya Mungu hata akatamka kupitia kinywa cha Bwana Yesu Kristo kuwa ‘mmepewa bure, toeni bure’. Kuhusisha pesa/utoaji na maombi kwa shida za mtu sikubaliani nako hata kidogo. Bwana Yesu alisema ‘mtawatambua kwa matunda yao’. Matunda ni jumla ya maneno na vitendo ambavyo mtumishi wa Mungu (na yeyote anayedai anamwamini Kristo Yesu) anasema na kufanya, siyo ya madhabahuni tu; siyo miujiza ya kwenye nyumba ya ibada tu.

    Katika kipindi tunachoishi, Wakristo HATUNA BUDI kujifunza kuangalia kwa karibu matunda ya watumishi wanaotuhubiria. Kipimo ni Neno la Mungu.

    Swali: Je angekuwa ni Bwana Yesu, angeagiza kama mtumishi huyo alivyosema, kwamba ‘ukishaingiza pesa katika akaunti yangu, nitumie meseji na uandike mahitaji yako kumi nikuombee’?

  44. Hello my name is Fredrick Abraham
    God called me into the ministry almost 3 years ago I thank God for confirming that I’m not crazy. I don’t believe that you should preach the gospel for money either. If God touches someones heart to give me a gift, that’s fine, but I never ask for,or demand anything. The Lord told his disciples, freely you have received freely give. The is no monetary cost for being anointed and appointed of God. You cant put a price on Gods love. It should be enough of a reward for anyone to know that you have been chosen by God to preach his word. Money hungry preachers that corrupt God’s word will eventually have to pay the ultimate cost. The scripture says what does it profit a man to gain the whole world and lose his soul.

  45. Hii ndo shida ya wakristo wa majina, kupata uponyaji ni kwa kila aaminiye maana Yesu alisema kila atakayeliamini jina lake atafanya mambo makubwa kuliko hata yale aliyofanya Yesu miaka 2000 iliyopita.Leo watu wanaambiwa waingize hela kwenye acc ya mtumishi ndo waombewe!!. Mkristo wa kweli hujiombea yeye mwenyewe na uponyaji upo palepale. Tutachumwa pesa bila kujua umeomnbewa au laa, nawaombeni wenye hela za kutoa namna hii wawape wajane na yatima wanahitaji sana hela hizo kwa ajili ya ada na matumizi mengine kuliko kuwapa hawa watumishi wenye kutia mashaka

  46. Yaani maisha siku hizi kila kitu ni pesa! ukitaka uponyaji pia unaununua! sasa IMETOSHA. Biblia gani mnaisoma? Yesu alishalipa kila kitu msalabani! au hilo andiko hamjakutana nalo? Sasa wasio na pesa waende wapi? nyie ndio mnawakosesha mbingu watu wengine wanaweka imani zao kwenu matokea yake huwafanya mungu. UJUMBE HII NI KWA WALE WANAOLIPISHA PESA ILI KUWAOMBEA!

  47. HII BIASHARA ANGEKUWEPO MWENYEWE KWA NAMNA YA MWILI NADHANI ANGEWASHUSHUA WENGI LEO NA KUPINDUA MEZA NYINGI ZA BIASHARA KWENYE MAKANISA YA LEO. KWASABABU YEYE ALISULUBIWA,ALICHUBULIWA,ALITEMEWA MATE,ALICHOMWA MKUKI UBAVUNI NA KUTUNDIKWA MSALABANI YAANI MAUMIVU YOTE ALIPATA AKIWA PEKE YAKE. HARAFU AKATOA ZAWADI KWA KILA MTU AMWAMINIE APONE BULE ,ABARIKIWE BURE,AWAFANYE WENGINE WAPONE BURE,WATOE MAPEPO BURE, WAFUFUE WAFU BURE, WASAMEHE WENGINE BURE,WAWAFANYE WENGINE WAMKUBALI YESU BURE,NA HATA WAENDE MBINGUNI BURE. NA ALISEMA KABISA MMEPATA BURE TOENI BURE LAKINI LEO WATU WAMEJIFANYIA MILADI DAMU YA KALVARI,MUNGU ANAWAPA MAONO YA HUDUMA BURE BILA GHARAMA WAO WANAWEKA NI KITEGA UCHUMI NA WANA RITHISHA WAZAO WAO HARAFU NI MAJASIRI KAMA SIMBA.HII INATISHA WACHA NIENDELEE KUIMBA HIP HOP NYIMBO ZA UKOMBOZI SIKILIZA UKITAKA http://www.myspace.com/ponagospelart

  48. Ndg Mtumishi,

    Mimi nashauri kuwe na namna fulani ya kuwajulisha watu ambao meseji zao zimepokelewa ili wawe na amani. Nafikiri ndiyo ushirika wenyewe! Mungu mwenyewe tukimuomba hutujibu nadhani sisi wanaadamu hatuna sababu yoyote ya kutokufanya hivyo.

    Ila tatizo moja ninaloliona hapa ni kwamba mtu asipopata majibu ya maombi yake atadai pesa zake zirudi. Ndiyo maana Yesu huponya na kufunguwa watu bure ili asidaiwe na kuonekana ni tapeli. Kupokea msaada toka kwa Mungu wakati mwingine hukwamishwa na mtu mwenyewe anayehitaji msaada huo kwa kutokujitoa kikamilifu kwa Mungu. Lakini mtu wa namna hiyo ni vigumu kumfanya atambuwe kwamba naye anasehemu katika muujiza wake.

    Ni kweli watumishi wanahitaji pesa ili kuendesha huduma zao na maisha yao pia lakini ni vyema wakatafuta lugha nzuri ya kuwahamasisha watu kuchangia kuliko kuwabana kwenye matatizo yao. Ni sawa na kumtegea mtu aliye karibu na kukata roho ndipo apewe sala ya toba. Ni lazima ataisema tu lakini Je, ni kweli kaisema kwa sababu anamwamini Yesu au kwa sababu ameona anakaribia kufa?

    Kumwambia mtu atowe pesa kisha aorodheshe mahitaji yake humfanya mtu aone matatizo yake ni muhimu kuliko kuchangia huduma na hivyo hutowa pesa kwa sababu anahitaji msaada toka kwa Mungu si kwa sababu anataka kuchangia huduma. Pesa ya namna hii ndiyo inayofanya Mungu asitukuzwe kupitia huduma zetu na pia tunajizuwia wenyewe kupokea zaidi toka kwa Mungu. Na mbaya zaidi tunalifanya jina la Mungu wetu litukanwe! Je, Mungu akiamuwa kuuondoa upako itakuwaje?

    Watumishi inabidi mliweke wazi suala hili kwamba hamuuzi uponyaji. Mkikaa kimya namna hii inaleta mkanganyiko!

    Wafikishie ujumbe huu wahudumu wa mtumishi Lusekelo.

  49. Hivi wapendwa, kuombewa siku hizi na `Watumishi wa Mungu` mpaka uwe na pesa? Kwa nini asitangaze tu kuwa mwenye moyo wa kuchangia, achangie kwa ajili ya kuendesha huduma yake? Kusema kuwa eti atoe pesa kisha aombewe! Kwa kweli ninapata mashaka, kwa sababu imeandikwa mmepewa bure toeni bure!.

    Watu wasioamini ndiyo maana wanasema ulokole ni biashara tu.

  50. kwa mujibu wa wahudumu wa mzee wa upakoni kwamba namba yake amei-set kwa namna ambayo inapokea msg tu na sio calls ndio mana ukituma message zinaenda lakini ukipiga inagoma

  51. Mimi niliguswa na kipindi cha TUTASHIDA kilichoendeshwa na Mzee wa upako channel 10 ya tarehe 25-06-008, nikatuma msg kuahidi kuwa ningechngia laki moja mara nirudipo Dsm kwani nilikuwa nje ya Dsm kwa wakati huo,

    Leo Mungu amenijalia nimechangia laki moja na kuweka Corporate bank makao makuu ya NBC yaani leo 08-07-008

    Ninatuma msg kwenye no tuliyopatiwa siku ya kipindi ina kwenda lakini nikipiga haiende sina uhakika kama maombi yangu niliyokusudia kumweleza Mchungaji wangu kama kweli utamfikia

    No Zangu ni 0714-900128 na 0764-021229, ninaomba kuapatiwa no sahihi ili nitume shida zangu kwa mchunagi kwani huaenda nilinukuu vibaya no ya simu siku ya kipindi

    Ahsante

    Dr Kingu Said Mtemi

  52. SASA HUYU MTUMISHI TENA ANAKOSEA HAPO .UKIOKOKA HATA WEWE HAYO MAMBO KUMI UNAWEZA KUOMBA BILA KUNYIMWA MAADAM UWE NA YESU NDANI YAKO NA SADAKA UNAWEZA KUTOA PALE AMBAPO YESU ANAKUONGOZA KUTOA SI LAZIMA KWAKE.WOTE WALIOMPOKEA ALIWAPA UWEZO WA KUFANYWA WATOTO WA MUNGU.SISI NI WATOTO WA MUNGU TUNAWEZA TU KUMUOMBA BABA BILA KUNYIMWA TUKIOMBA SAWA NA MAPENZI YAKE.AMINA

  53. mi naona sio lazima ukitoa useme,tena useme na kiasi!si dhani km inapendeza!kwasababu km unatoa kwaajili ya Bwana haina haja mwanadamu ajue,wengi ambao wamebarikiwa huwa ni watoaji na mara nyingi hawasemi km wametoa!!!toa kwa ajili ya Bwana,km ni kazi ya Bwana nae atashughulika na mambo yako!

Andika maoni yako