Category Archives: MITAZAMO
Nini maana ya Ndoto hii?
Shalom wana Blog!
Naombeni kuambiwa maana ya ndoto hii kwani sio mara moja nimeota.
Kuota unapanda sehemu yenye mteremko sana(kilima) tukiwa na wenzetu lakini mimi hufanikiwa kupita, kisha kufanyiwa uchawi na watu nisowajua, na kuzungukwa na mapepo lakini huwa nayakemea sana kisha kutoweka.
Maana yake ni nini?
Mimi Sia
Shalom!
Adui King’ang’anizi
Mhhh!
Maadui wengine kwenye maisha wako kama
Farao!
Unakutana na mtu kazini, kwenye biashara au
katika uwanja mwingine wowote wa maisha.
Inatokea tuu anakuwa adui yako pengine kwa
kusikiliza maneno ya uongo ya kuwachonganisha,
anayakazia kamba, anakuwa adui na kujiapia
kwamba atakula na wewe sahani moja! Au tuu
inatokea ulitaka kumshauri jambo, anageuza post,
inakuwa wewe ndiyo unajifanya unajua kila kitu,
anaanza kupambana na wewe ili udhaifu wako
auweke hadharani!
Kwa yule inayewezekana kujitenga naye
unajitenga, unahakikisha huingii katika “18” zake,
ukijua yatakwisha! Lakini wapi. Utashangaa
anaanza kupeleleza shughuli unayoifanya na
kutaka kukusanya data kwa kila mtu
anayekufahamu ili tuu apate pa kukutafutia
sababu akufuate huko huko uliko, pamoja na
kuwa ulishampisha kabisa katika uelekeo wake
wa maisha!
Anaanza kutafuta ulipopita ili na yeye akufuate!
Hapati raha kama hajapata nafasi
yakukukarahisha na anaweza akazua jambo
kubwa la kukusingizia ili tuu uadui uendelee
kuimarika na watu wakuone kumbe hufai!
Sasa unaanza kuwaza: Mbona huyu
nilishamuachia mambo ya maisha yake? Mbona
kama ni ofisi tulitengana kila mtu akabakia na ya
kwake?? Mbona nilishahama kabisa toka kwenye
kampuni anayofanyia yeye kazii?? Sasa kwa nini
bado ananifuatilia??
Ndipo linakuja jibu hiviiii: Kuna watu wana “roho”
ya Farao!
Wana wa Israel wameshakwenda zao lakini bado
jamaa aliwafuatilia hadi ndani ya baharii!!
Huyo mtu anayelazimisha vita na mtu asiye na
hatia mwisho wake ni lazima uwe kama jeshi la
Farao: Kumezwa na bahari!!
Solution: Ukiona mtu wa namna hii yuko nyuma
yako, kila ukibadilisha gia, na yeye anabadilisha.
Ukiingia garini na yeye anaingia; ukisema ngoja
nimuachie ntasafiri kwa trekta na yeye anashuka
anapanda trekta: Ukibadili namba ya simu
unashangaa kishaipata na anaendelea
kukuandikia sms za maudhi na vitisho-bubu….
Ukimuona mtu wa Hivyo Kaza Kumtazama
Mungu! Tafuta uso wa Mungu aliye Mtetezi wa
wenye haki! Kwa Hakika Mungu atakuelekeza
kwenye Bahari…siyo lazima iwe ya Shamu!
Itafika tuu mahali Mungu atamshughulikiaa na
atapotelea humo na ndiyo unakuwa mwisho wa
kumuona tena akisumbua sumbua maisha yako!
(Na ole wako wewe ambaye itamlazimu Mungu
akushughulikie ili mtu wake, mcha Mungu wake,
apate Amani maishani mwake!!!)
Wanadamu tupendaneni!
John Paul
KAZI na FAMILIA
Haina maana yoyote kusifiwa kuwa wewe ni kiongozi mzuri, manager mzuri, Mchungaji mzuri, halafu wakati huo huo familia yako ikawa katika mapungufu makali kwa sababu baba au mama hana muda na familia yake kwa kisingizio cha majukumu mengi!! Kwa kisingizio cha kutafuta pesa, shame!
Eti kwa sababu baba ni mbunge, ni waziri, ni CEO wa kampuni, ni mfanyabiashara au vyovyote eti hana muda na familia yake! Hii ni uzembe wa hali ya juu tena juu sana! Kuwa na kazi nyingi haikuhalalishii wewe, baba au mama kuisahau familia yako!
Ni kweli umefanya vizuri sana, biashara yako imeendelea sana ni sawa, ni kweli unaongoza kampuni vizuri sana ni sawa, ni kweli ni Mchungaji mzuri sana Kanisa limesimama imara kwa sababu yako. Lakini familia yako umeisahau, sisi wanafamilia tunahitaji muda na wewe, tunahitaji malezi yako, tunahitaji upendo wako, tunahitaji uwepo wako nyumbani katika wakati sahihi, tunahitaji connection na wewe, tunahitaji uongozi wako!
Eti unawadanganya watoto kwa kuwapa kila kitu wanachohitaji na wasivyohitaji (physical things). Simu kali, usafiri kwenda shule wanapelekwa, I-pads, Computer games, vyakula vya kila aina, vingi vikiwa processed viwandani matokeo yake unawaharibu afya. Ni kweli umefanya vizuri, lakini hii ndo inaitwa being SUCCESSFUL IN A WRONG THING! Unadhani maisha ni vitu? Jamii inabaki kukushangaa tu, mbona yuko vizuri sana lakini watoto wake mmoja tu ndo amesoma, wengine wamekataa shule, wanavuta bangi, ni wezi, ni wakorofi, wamezalishwa zalishwa tu! Wakati mwingine unaiga mambo ya wazungu, sasa wewe ni mzungu? Acha kuigaiga, unapotea!
Nelson Mandela ni kiongozi aliyepita ambaye kwa Afrika nzima na hata dunia yote wengi au wote walimkubali kuwa HE WAS A GREAT MAN in leadership and humility. Lakini tunaweza kusema, he was SUCCESSFUL IN A WRONG THING! Maana Hakupata muda na familia yake, matokeo yake watoto wake 4 wamekufa na HIV/AIDS. Jambo la kusikitisha sana!
Wako wachungaji wanakuwa committed kweli kweli kwenye kulea Kanisa, familia inamkosa baba. Yupo nyumbani kila siku kumbe hayupo, kwa macho yupo na sisi kumbe hayupo! Matokeo yake watoto mpaka wanaichukia kazi ya uchungaji!
Ukweli ni kwamba, kama huna muda juu ya jambo fulani, fahamu kuwa jambo hilo si MUHIMU KWAKO, halina MAANA KWAKO. Je, familia yako (mke au mume, watoto) ni wa muhimu kwako?? Au ATM CARD yako ni muhimu kuliko mtoto wako wala mke au mume wako! Tatizo umeweka fedha mbele sana kuliko utu, tena uliingia kwenye ndoa kwa kufuata MAZOEA, hujui kulea familia, hujafundishwa wala hutaki kujifunza. Ndo maana unaacha familia Arusha wewe unaishi Dar, familia Mwanza wewe Morogoro! Hayo siyo maisha bali ni utumwa wa maisha. Jifunze nini maana ya familia, malezi yake, nini wanahitaji toka kwako ili uwe BABA au MAMA mzuri. Familia kwanza ndiyo utakuwa kiongozi mzuri, anayejitambua. Huwezi angalia kutafuta fedha tu halafu familia inaharibika, fedha hizo hazina maana kama familia yako imeparanganyika.
Jamii yetu ina watu wasiojitambua, wezi, hawajiamini, waongo, wachakachuaji, wasiojituma, wavivu, wazembe, wala rushwa na mafisadi wengi maana wazazi wao hawajafundishwa namna ya kulea familia, hakuna malezi kwa watoto maana wanazaliwa na kuachwa watafute wenyewe nini maana ya maisha, nini maana ya kuwa mtu katika jamii, matokeo wanajifunza kwa wezi, mafisadi, wavivu nk. Ee Mungu tusaidie kuifahamu kweli!
Connect na watoto tangu uchanga wao hadi unapowaozesha, ili uwaonyeshe nini maana ya maisha, nini maana ya kuwa mtu katika jamii. Wafundishe ili wajitambue, endelea kuwa-mentor katika ubaba au umama wao pia. Ukiwaacha wawe wakubwa ndiyo uwe karibu nao tayari watakuwa wamejitengenezea mifumo ya maisha yao, na wewe wanakuona STRANGER kwenye mifumo waliyotengeneza. Kuwa baba au mama acha kujifanya uko busy, kwa nini ulianzisha familia kama uko busy???
Mungu utusaidie kuiona kweli, tukafanye kama inavyopaswa kuwa ili kukuza familia zenye michango katika jamii. Amina.
NOTHING CHANGES UNTIL YOUR MIND CHANGES!
Theophil
Sala ya Bwana
Utasimama Wapi?
Hezekia alipougua ugonjwa ambao aliambiwa utamsababishia Kifo alilia mbele za Mungu, akamkumbusha jinsi alivyokwenda mbele zake kwa UKAMILIFU na Unyoofu wa Moyo na Mungu akamponya. (2Wafalme 20:1-7).
Mtu huyu wa Mungu alikuwa amejitengenezea Hazina na Ushahidi wa kumfanya akumbukwe na Mungu. Mungu alikubaliana kabisa na maisha ya Hezekia kwamba yalikuwa ni Mema!
Katika Kitabu cha Hosea 6:1 kuna maneno haya:
Njoni, tumrudie Bwana; maana yeye amerarua, na yeye atatuponya; yeye amepiga, na yeye atatufunga jeraha zetu.
Hapo tunaona jinsi watu wa Mungu walivyojikuta katika matatizo kwa kuwa Mungu mwenyewe ndiye aliyekuwa Amewararua. Hawa wakawa wanahimizana Kumrudia Mungu kwa kuwa ni mwenye Rehema. Hawakuwa na ujasiri wa kusema wamwambie Mungu angalau jema fulani walilofanya kwake.
Maandiko hayo mawili yanaonyesha namna mbili za kwenda mbele za Mungu. Aliyotumia Hezekia na hii inayoelekezwa katika Hosea.
Ni changamoto kwetu leo kwamba Ikitokea umepatwa na tatizo, utatumia njia gani wakati wa kumuomba Mungu akutoe katika shida hiyo?
Utamkumbusha mema uliyotenda au Utaomba rehema zake tuu ndiyo zikubebe? Je, tuna ujasiri wa kumwambia Mungu kwamba kuna mema kadhaa ambayo basi hata Mungu ayaangalie hayo ili aiondoe shida iliyopo mbele?
Ni jambo la kutafakari kwetu sote!
JP