Utata kuhusu Mafuta ya Upako!

Bwana Yesu Asifiwe, samahani naombeni mnisaidie kuhusu mafuta ya upako. Sijajua kama mimi ni mchanga kiroho au vipi? nashindwa kuelewa kuna wachungaji wanayaombea hayo mafuta halafu wanayagawa na wengine wanayauza sh 10,000 yanakuwa kwenye kichupa kidogo sana.

Wanasema kama umepata strock unajipaka na unapona na wengine wanasema kama unaumwa pia unatumia na unapona na wengine wanasema kama una kesi unaweza kujipaka siku unaenda kwenye kesi na ukashinda kesi. Ninacho ongea nina uhakika nacho. Lakini mimi mbona siamini hiki kitu?

Ninachoamini mimi ni maombi. Lakini kuhusu mafuta yaani siyaamini kabisa na siku hizi makanisa mengi wanatumia sana hayo mafuta. Kama ukienda unahitaji maombi wanakuombea halafu wanakwambia ununue na mafuta ya upako. naomba mnieleweshe.

Amina

Advertisements

18 thoughts on “Utata kuhusu Mafuta ya Upako!

 1. Mwenye haki ataishi kwa imani, kama huamini acha wale wanaoamini na wameona matokeo waendelee ipo siku nawe utakuwa katika hali ambayo itakusogeza kupata imani na yamkini ukawa shuhuda mzuri wa hili, USILAZIMISHE WATU WOTE KUISHI KATIKA KIWANGO CHAKO CHA IMANI WE YAPE MAMBO MUDA WA KUTOSHA……

 2. BAADHI YA MAJIBU KUTOKANA NA HOJA YA MILINGA KUHUSU MAFUNDISHO “POTOFU” https://strictlygospel.wordpress.com/2013/07/08/je-mafundisho-haya-ni-potofu/

  JIBU LA SELELI KIPENGELE CHA MAFUTA YA UPAKO:

  ——————————–

  KUPAKA WATU MAFUTA NDIO UPAKO!

  Hello! Everybody,

  Ninaendelea kutoa mchango kwa hoja za Mr. Milinga J.V, nawatia moyo/hamasa karibuni na wengine kwa michango/ uchambuzi na hata feedback( maswali, challenges nyongeza, maboresho, masahihisho,maandiko, shuhuda, criticism na comment yoyote utakayopenda Wandugu.Leo nashughulika na hoja ya Saba nayo ni kama ifutatavyo alivyoisema Milinga.

  HOJA no.7 =Mafundisho ya Kupaka watu MAFUTA eti ndio UPAKO hadi wengine huitwa wazee wa UPAKO!

  Kabla sijaenda mbali, nikumbushe kua Milinga ameleta hoja 11 na kutoa statement izi 2: MOJA: ‘’Mafundisho hayo ni potofu ukubali au ukate na MBILI: ‘’Yote hayo mimi nayaweka kuwa ni mafundisho yenye utata sana na bila kujizungusha naomba niseme kwamba ni POTOFU’. Ivyo katika michango yetu tunayoendelea kutoa, bila shaka systematically itapendeza na kujenga kweli aidha KUKANUSHA KUA HAKUNA UPOTOFU KWA USHAHIDI WA KIBIBLIA/NEO LA MUNGU AU HATA UTHIBTISHO WA KIMAISHA, AKILI, UZOEFU WA HUDUMA NA KUTEMBEA KWAKO NA MUNGU as long as vyote havitakizana na Neno AU KUKUBALI KUA NI POTOFU PIA KWA USHAHIDI TOKA BIBLE AU SOURCES NYINGINE IN ALIGNMENT WITH THE WORD. Kwa kuelewa ilo, mimi so far nimechangia/nimejadili Hoja no. 1, 2,3,9 na 10 na kutamka yafutayo kwa ushahidi( Rejea majadiliano yangu ktk hoja izo kwa maelezo zaidi)

  HOJA no.1 Nyota zilizoibiwa= NILISEMA NA KUTHIBITISHA KUA NI FUNDISHO POTOFU KWELI NA UHUNI KUFUNDISHA/KUSUMBUA WANA WA MUNGU NA MADUDE KAMA HAYO KWA KUWALAGHAI KISHA KUWAVUNA

  HOJA no. 2: Kutoa Zaka kila mwezi au upatapo kipato= NILISEMA SI POTOFU HATA KIDOGO KWA KUA KUTOA NI MOJA WAPO YA TABIA ZA MUNGU, KWAMBA WATU WA KALE WAKUU WA MUNGU WALITOA NA KWAMBA KWAKUA TUNAIONA ZAKA INAANZA KUTOLEWA KABLA YA SHERIA YAANI MOYO WA MTU TU KUMUHESHIMU NA KUMPENDA MUNGU BASI NA SISI LEO, MTU ANAPOMPENDA MUNGU NA HIARI/MOYO WA KUTOA UPO NA HATA WANAOFUNDISHA, WAKIFANYA IVYO KWA NIA IYO IYO YA UPENDO NA MZINGO WA MAMBO YA MUNGU YAWE SAWA KWA WATU WAKE NA KAZI YAKE, NI NJEMA SANA NA IVYO UHIARI NA MOYO WA KUTOA IN THIS CASE, HAUFUNGAMANI KAMWE NA AGANO KALE WALA JIPYA AU MWISHO WA MWEZI AU KATI, HENCE WAKATI WOWOTE MTU ATAMFANYIA BABA YAKE JAMBO KWA JINSI WANAVYOPENDANA NA KUHUSIANA NA PIA KWA KUA YEYE MTOTO WA BABA NI MWENYE AKILI TIMAMU INAYOMPA UFAHAMU KUTHAMINI MAMBO YAO/YA BABA YAKE/YA NYUMBANI KWAO/KWA BABA YAKE NA PIA UELEWA KWAMBA YOTE ALIYONAYO/AYAPATAYO/AMILIKIYO,KAMA SI NEEMA/ PUMZI TOKA KWA MWENYEWE NA UWEZESHWAJI MWINGINE,ASINGEKUA NAVYO WALA KUWEPO KTK USO WA NCHI.

  HOJA no. 3,9,10: MAKATAZO MBALIMBALI KWA WANAWAKE= Nilisema yanakua potofu na actually the good term in this case ingekua ‘Upotoshaji’ pale yanapo hamishiwa kama yalivyo kwetu leo, kizazi cha leo , ktk tamaduni za leo, sehenu ya Duniani ya leo nk. Nikasema kua kwa wao hasa pale makatazo haya yalipotolewa, yalikua sawa kwa ajili ya mahali husika, kwa Kanisa na kundi la Watu husika na maono/mzingo/maongozi ya kiroho na namna ya utendaji wa kazi ya Bwana wa mhusika pale alipokuwepo na kule alikoitiwa kwa huduma na Mungu. Nikasema ukweli kua hata katika ulimwengu wao kipindi kile si kila kanisa nilikua linatekeleza haya( maana hakuandika hayo kwa makanisa yote na ukweli mwingine pia kwamba kabla ya makatazo hayo kuwekwa kwa makanisa ya wakati huu( wa Paulo), uko nyuma walikuwepo Watumishi wengine wa Mungu- Mitume waliokua na makanisa na hawakuwahi kuweka makatazo ya aina hii kwa KILA kanisa, na ukweli tena mwingine kua ktk Biblia kumerekodiwa pia maneno na matendo ya Mtu kama mtu na si Mungu, IVYO BASI makatazo dhidi ya Wanawake kipindi kile yalikua ni sawa lakini kuyahamisha yote kama yalivyo leo hii ni UPOTOSHAJI MKUBWA. PIA NIKUSUMBUA WATU WA MUNGU KWA KUWABANA KWA MIZIGO AMBAYO YESU ALIYE KIELELEZO CHETU NO. 1 KUZIDI KILA KIUMBE, KTK MAISHA YAKE YOYE YA UTUMISHI HAKUWAHI KUWEKA MAKATAZO KWA MAMBO HAYO NA KWAMBA KAMA KWELI INGEKUA WANADAMU WANAWAKE WASIPOJUA HAYO WANAKWENDA JEHANUM STRAIGHT WAKIFA, BASI KWA HAKIKA HUYU BWANA WETU, ASINGEFANYA KOSA KAMA ILO LA KUTOSISITIZA MAMBO HAYO.

  Sasa naanza Hoja no. 7 karibu. Ifahamike kwamba, wanadamu wote tu wenye dini na imani, wanamjua au hawanjui Mungu, inapokuja maswala ya imani na kuabudu, hua wanaiga/chukua toka kwa Mungu. Wapo wanaokosea kabisa namna ya kumfanyia Mungu mambo ya imani na ibada kwa kuingiza na ya Kibinadamu kibaya( maana kipo kizuri ofcoz, cannot be all devilish!), wengine wanapatia vema sana mambo hayo na wengine to the extreme, wanayachukua ya Mungu na changanya na ya shetani pamoja!!!!!!!! Embu tujiulize, Wapi mambo haya ya Mafuta au kupakwa Mafuta/upako kumetokea? JIBU- Ni kwa Mungu tu na ushahidi ni kama ifuatavyo: Kutoka 25:6, 29:7, 29:2, 29:29,30:3,22-26,40:9, 40:15, Walawi.8:10,8:12, 4:3,5,16, 6:20,Zaburi.132:10,1Sam.16:13,2Sam.24:4,1Nyakati.16:22;Zab.105:15,1Wafalme-19:16,1Nyakati.16:22, Zab.105:15, Isa. 21:5,Luke 7:38-40, Kumb. 28:40, Ruth 3:3,2Samuel 14:2, Zab.104:15, 109:18, Isaiah 1:6,Mark 6:13, Yakobo. 5:14, Mark 14:8,Luka. 23:56, Zab. 2:2; Dan. 9:25, 26,Isa. 61:1, Zab. 45:7; Heb. 1:9, John 1:41; Mdo. 9:22; 17:2, 3; 18:5, 28, 1 Yoh. 2:20, Matt. 25:1-13)

  Kutokana na maandiko hayo juu, Utaona kwamba mafuta ya marashi na Mmea e.g. olives yanatumika kupaka/miminwa kwa Mtu/Viti Kuweka Wakfu kuchukua/kufanya majukumu ya KiMungu au Jamii pia Wakati wa kuombea wagonjwa, tena Kutunza ngozi( kama vile vaseline au lotion ya ngozi kwa leo), pia Kutunzia Maiti, vilevile kama dawa ya kimwili, na kwa akili ya toba za dhambi, ishara ya Roho Mtakatifu juu/ndani ya Mtu na mwisho kuonyesha ukarimu( Yesu ndani ya nyumba ile).

  Attention! Take heed that Mtu asiwatishetishe hata kidogo, tuelewane mapema kabisaaa kua neno ‘Upako’ ni la kawaida tu sana, nothing special in it kwa kua ni unyumbulishaji wa maneno mfano: ‘Kupaka’, ‘Kupakwa’ ‘Kupakaa’, ‘Upako’, ‘Upakwaji’, ‘Upakaaji’’ yaani mengine ni Nomino na mengine Kitenzi Kikuu na Kiilezi.Hence, Upako si nguvu kama ambavyo tunadhani au kuchukulia. Tunaposema ‘Mpakwa Mafuta wa Bwana’’-The anointed Man of God simply means ‘MTU ALIYERASIMISHWA KUFANYA KAZI YA BWANA’’ basi ivyo tu. Kwahiyo yale maneno yetu kua da! ‘jamaa si mchezo, ana upako kweli’, au ‘ana shusha upako ile mbaya kwa maana na nguvu nyingi/sana’’ au ‘’ana shusha upako yaani uwepo wa Mungu’’, ni kuandaa seminar tu hapo kanisani kwenu kisha hatimaye, yatoweshwe milele mambo hayo yasiwepo tena makao yake ktkt ya Wanadamu.

  Zingatia strictly and correctly kua hayo ni mafuta tu na yanatumika kwa Watu na vitu kwa makusudi mbambali hapo juu ivyo yatumikapo,hayahusiana na kuingiza kitu mfano nguvu, muujiza, uwepo wa Mungu, mamlaka,kuleta malaika au Roho Mtakatifu. Si tu hayaleta ivyo vitu bali HAYANA KABISA. Ni sawasawa na mafuta ya nazi, beby care au lotion kutumika ktk shughuli izo baada ya kuombea. MAANA HALISI YA VITU IVYO NI ILE INAYO WAKILISHWA AU KWANINI KWAVYO TUNAVITUMIA KUFANYA HAYO TUYAFANYAYO.

  Mfano- Tunapomsimika Mfalme na kumpaka/miminia mafuta, ni ishara ya nje tu sawa na kusema..’’Sasa umeithinishwa kuanza kazi rasmi lakini hayo mafuta kama mafuta ni mafuta tu basi-nothing important or special at all in it-hakuna magic or Holy power humo. Yesu alivyosema, Roho wa Mungu yu juu yangu,amenipaka mafuta kuhubiri Injili kwa maskini nk, He was simply saying ‘Sasa niko tayari/rasmi na nina uwezo nimepewa kuanza lile lililonifanya niache mbingu-muhimu hapo si ‘anointing’ ya kuonekana( ambayo the interesting thing about Jesus, hakutumia chochote na wala wakati anasema ivyo kua nimepakwa , hakuwepo mtu anammiminia-which tells/means a lot kua what matters in kile cha ndani alichokua nacho si ya nje. That invisible anointing yaani Roho Mtakatifu aliyekua ana/alimrasimisha Bwana kuanza mission yake) is the deal, nothing more or less-(ni kama vile kuapisha Rais,Waziri,MP na Biblia,Mkuki,Nyundo na Jembe, Katiba- ivyo ni vifaa/vitu vya ishara tu ya nje vya kurasimisha Mtu kuanza kitu/kazi/jukumu.Tunapoombea mgonjwa kwa kumpaka mafuta(anointing oil), that visible mafuta is NOTHING BY ITSELF BALI ILE IMANI KTK JINA LA YESU KWETU SISI WAOMBEAJI NA YULE AOMBEWAYE, NDIO MUHIMU NA BIBLICAL!

  KWA SABABU IZO JUU, NAPENDA KUHITIMISHA hoja no. 7 ya Milinga KWA POINTS IZI.

  • Kutumia ‘Mafuta ya Upako’ au ‘Kupakaa Mafuta’ wakati wa maombezi au shughuli nyingine kama nilivyosema, KWA JINA LA BWANA, SI UPOTOFU HATA KIDOGO, NI BIBLICAL.

  • Ifahamike kwa udhabiti imara kabisa (and am very, very, very, very serious on this) kua tunaposema ‘mafuta ya upako’ si mali fulani au bidhaa ya mtu fulani, shirika au kikundi cha dini/imani, milki binafsi au hati milki wala si utambulisho/identity strictly and privately owned by kundi fulani la imani. ‘’Mafuta ya Upako’’ simply means ‘’Mafuta kwa ajili ya kupakaa!(An Anointing oil-simple/easy/ clear..period!!!!!!) Hakuna jipya hapo wala creativity out of special IQ/big thinking, mountainous beyond reach logic of a special human or an ever seen revelation! Yakiwepo Mafuta ya kupakaa na yanatumika na kufahamika/kuchukuliwa kua ni ya mtu au mwanzilishi fulani tu, ya kikundi cha imani fulani tu, hiyo si tu ni UPOTOFU BALI PIA INAKASIRISHA KWELIKWELI KUJUA WATU WANAOMJUA MUNGU KUFANYA IVYO/HAYO CONFIDENTLY,PROUDLY, PUBLICALLY and so LOUDLY.

  • ‘’Mafuta ya upako/ya kupakaa’’ si lazima yawe ya kutoka mizabibu na mitini ya Israel bali hata ya alizeti za Sumbawanga, pamba ya Mwanza, nazi za Chalinze, cha msingi yanachukulia na kuombewa kwa jina la Bwana kisha kutumika kwa kusudi lilipo (notice: Jina la Bwana hapo ndio muhimu nasi hayo mafuta yaombewayo-LET NO ONE ON EARTH CHEAT YOU TO LOOSE THAT FOCUS/PRINCIPLE),Kuchukulia kua lazima ‘mafuta ya kupakaa kua yatoke Nchi fulani, kwa mtu fulani, ni UPOTOFU MKUBWA NA UTAPELI WA KUSAKA ELA ZA WATU WA MUNGU BURE KWA NJIA YA kiroho-roho vile.( I like using this.. ‘’ya kupakaa’’ ili kukwangua kabisa uspesheli na maana fulani baadhi ya watu walioweka wanapotumia phrase ‘’Mafuta ya Upako’’-wakati maana yake ni iyo iyo tu very common namely ‘Mafuta ya kupakaa’’)

  • Vitu vyote tuvitumiavyo ktk mambo ya ibada na imani(maombi) mfano Mafuta, vitambaa, nguo, tope ( Yesu), funguo,sabuni, tochi,maji,mbegu, fedha, fimbo, kijiti, nk ,ARE NOTHING SPECIAL AND GOT NOTHING IN THEM BY THEMSELVES! Kudhani/kuchukulia kua vina uwepo, nguvu, malaika, Roho si tu ni UPOTOFU BALI PIA NI UJINGA! Kwa kua always kuna nguvu halisi juu yake isiyo onekena, iyo ndio muhimu kuishika, in our case, the name of Jesus.

  • Kutumia vitu ivyo Wakati wote-an order of day/life mfano wakati a kulala, kusafiri ndani ya gari, shambani,mfukoni NI UPOTOFU, DINI, UTOTO KIROHO, KUTOJUA NENO NA HIRIZI KATIKA umbo la kiroho-roho!

  • Mtu kudhani kua yeye ndiye spesheli mwenye mafuta ya upako( Mafuta ya kupakaa) wakati hata kariokoo tu tunaweza nunua mafuta ya mimea, tukaombea kisha kuyatumia, ni UPOTOFU ,MBWEMBWE NA LONGOLONGO ZA MADHABAHUNI ZA BAADHI YA WATUMISHI WA TUMBO WA KILEO AMBAO WAKO KWA AJILI YA MAMBO YA KIMWILI NA SI YA UFALME WA MUNGU,hence there is no mzee, mtoto,kijana, bibi, babu mume,mke, mchumba wa upako!!!!!!!!!

  Conclusively, Ukiishi ktk mambo yako ya Imani na Ibada BILA HATA SIKU MOJA KUTUMIA VITU IVYO JUU BALI JINA LA YESU LIPITALO KILA JINA, AMBALO KWA HILO KILA GOTI LITAPIGWA NA KILA ULIMI UTAKILI NA KWAMBA HAPANA JINA JINGINE CHINI YA MBINGU TULILOPEWA ZAIDI YA HILO JINA LA BWANA NA MWOKOZI WETU MPENZI SANA(I LOVE U SO MUCH JESUS MY LORD), LINATOSHA SANA PAST,PRESENT AND FURUTE ETERNALLY-Mdo.4:12 na Wafilipi.2:9-11.

  Press on,

  Edwin Seleli

 3. JAMANI NI SWALA LA UELEWA TUUU, MAFUTA YA MZEITUNI HAYATOLEWI BURE YANAUZWA MADUKANI, SO NI LAZIMA UNUNUE NA KWENDA NAYO KATIKA MADHABAHU SAHIHI, ILI KUHANI ALIYEPO KATIKA MADHABAHU SAHIHI AYAOMBEE NA UNAONDOKE NA MAFUTA YAKO YAKIWA NA NGUVU TELE, NA TAYARI KWA MATUMIZI. KWA UPONYAJI, N.K.

 4. Hayo mafuta mimi nayajuwa, sio lazima kuombewa na kiumbe chochote kile hapa duniani, mwenye nayo hayo mafuta basi na apake kidogo mkononi na amshike mtu mwenye mapepo, basi yule mtu ataanguka mpaka chini kwa kupandisha mapepo

 5. SUALA LA KUELEWA HAPA NI IMANI , NDIO SUALA KUBWA SANA , HAYO MAFUTA NI LAZIMA YATOKE KATIKA MADHABAHU AMBAYO NI SAHIHI, AMBAYO YAMEOMBEWA NA MTUMISHI WA MUNGU,NA TAMBUA KUWA SIO KWAMBA KILA MTU NI MTUMISHI WA MUNGU NALO NI JAMBO LA KUANGALIA SANA

 6. mafuta yana fanya kazi kubwa, tena yawe ya mzeituni. Roho wa Mungu kupitia Mafuta haya anakuhuisha na unapata kibali maalum. lakini ni lazima upate mafuta haya toka katika madhabahu sahihi, na mtumishi ambaye ana agizo ili yaweze kufanya kazi. si kila mtumishi anaweza akayatumia yakafanya kazi.
  lakini anayeyauza baada ya kuyaombea, hapo huyo ana walakini. ila unaweza ukayapata kwa kuyanunua kwa kawaida tu, then yakaombewa ili nguvu za Mungu ziyatakase na kuyatenga na maagano yote yaliyotangulia.

  SHIKA NENO ,TENDA NENO ULIYEPEWA NEEMA KUBWA SANA.

 7. Wisdom, divai na mkate hatuvigeuzi kuwa mwili na damu kawa Imani,divai na mkate ni element tu,

 8. Context ya kutumika kwa mafuta ambayo tunaiyo kwa kanisa la kwanza (mitume) ilikuwa ni kwaajili ya wagonjwa tu.lakini matumizi ya leo kuna errors na extreme nyingi,kila kitu mafuta,sasa ni kama uganga wa kienyeji kwa jina la mafuta ya upako.matumizi yoyote ya mafuta nje ya ugonjwa sio kibiblia,ndoa ina matatizo mafuta,una kesi mafuta,unataka kufaulu mtihani mafuta…

 9. Wapendwa
  Mafuta ya upako, matumizi yake tunayaona kwanza katika Agano la Kale. Kwa siku hii ya leo, kulingana na hali iliyopo na mfumuko wa mafundisho yenye msukumo wa kumfanya mwaminio kuwa tegemezi zaidi, basi ni muhimu kwetu waumini kujifunza kumtegemea Mungu zaidi kuliko kuwategemea hawa viongozi ambao hawataki kutupeleka kwa Yesu na wao kuishia, badala yake wanatung’ang’ania na kutugeuza ng’ombe wa maziwa tena asiyelishwa!

  Agano la Kale lilikuwa ni la mwilini, kwa hiyo mambo mengi tunayoyaona yalitendeka kimwili kama ilivyo tohara na mambo hayo ya Mafuta ya Upako. 

  Mafuta hayo tunaendelea kuyaona katika Agano Jipya kutokana na wahusika katika kipindi hicho kuwa ni Wayahudi ambao ni wale wa mwilini ambao sasa wanaingizwa katika mambo ya Rohoni. Ndio maana tunaona mitume wakiagizwa kuwawekea mikono wagonjwa, na pia tunaona matumizi ya vitambaa na hayo mafuta ya upako. 

  Lakini unapoyaangalia Maandiko vizuri pale unapoitafuta nafasi yako humo, basi utaona kuwa mambo hayo ya mwilini si yako wewe unapoipokea Imani hii ya Kristo. Hebu mtazame yule askari wa Kirumi aliyeuguliwa na bintiye, alipomuendea Kristo kwa shida yake, Kristo alimwambia atakwenda nyumbani kwake akamtimzie shida yake, yaani akamwekee mikono; lakini yule askari akamweleza kuwa kwa Mamlaka aliyonayo akisema tu itakuwa! Kristo anasema hajaona imani kama hiyo, hiyo ndio imani tuliyonayo watu wa mataifa. Sisi tunaliamini Neno lisemacho. Usilitilie shaka Neno la Mungu. Angalia kile Mungu anachosema na ukiamini hicho. Hawa wahubiri wanaokuja na mambo hayo ya Upako, hawatokani na Huduma ya Kristo, watakuwa ni wale waliojiingiza katika kazi hiyo wakiwa chini ya Upako Mwingine yaani Principalities and Powers, jilindeni kwa kuweka Imani zenu katika Neno la Mungu kwa kujitoa wakati wenu ili muyachunguze mafundisho mnayopewa iwapo ni Neno la Mungu au la, vinginevyo mtaingizw utumwani na kufia huko kusiko na ufufuo!

 10. Kaka Alfred,
  kama ulisoma vizuri comment yangu sikusema mafuta yapo toka enzi za agano la kale kwa kuuzwa ila nilikuwa nazungumzia matumizi yake tu.
  Kuhusu matumizi ya mafuta, namshukuru Mungu amenipa uelewa mahali na wakati wa kuyatumia ila kwa suala la watumishi kuuza hayo mafuta hata mimi sikubaliani nao kwa sababu hutakiwi kuuziwa na watumishi.
  Kama vile ilivyo meza ya Bwana tunabadili kwa imani divai na mkate na vinakuwa ni mwili na damu ya Yesu na mafuta vivyo hivyo tunayanunua dukani na kuyaombea kisha yanakuwa mafuta ya upako.
  Amani ya Yesu iendelee kuwa nanyi.

 11. nilicomment kwenye facebook kwamba huyo anayesema kwamba mafuta ya upako yalikuwepo hata agano la kale atuonyeshe mahali ambapo watu waliuziwa hayo mafuta. kitu kingine watu wa Mungu tusome alama za nyakati hapa bado hayajazungumziwa maji ya upako kuna sabuni za upako vitambaa vya upako. bado kidogo wengine watakuja na ufunuo wa matope ya upako kisa yesu alimpaka kipofu matope machoni akaona.tena nilisahau kuna chumvi za upako pia. lakini ukisoma kwenye Bible vitu kama mafuta kama alivyoeleza mchangiaji mmoja kwa kutoa mfano wa samweli alivyompaka daudi mafuta vilitumika kwa makusudi maalum na kwa wakati maalum kwa watumishi kuwapaka wahusika au kuwamiminia vichwani kama ishara ya Mungu kuwa juu ya muhusika kwa ajili ya utumishi. lakini kwa sasa haya mafuta ya “upako” yako kama hirizi kwamba unaweza ukawa nayo wewe mwenyewe bila ya muongozo wa Mtumishi na ukayatumia wewe mwenyewe kitu ambacho hakipo maana hapo kwenye agano la kale watumishi (manabii) ndio walitumwa na Mungu kuwapaka wahusika mafuta kwa maelekezo ya MUngu mwenyewe na siyo wahusika kupewa au kuuziwa hayo mafuta na kuwa nayo nyumbani kama ilivyo sasa. kwenye agano jipya mojawapo ya mistari inayozungumzia habari ya mafuta inasema kama mtu hawezi(anaumwa) awaite WAZEE WA KANISA nao wamwombee na KUMPAKA MAFUTA kwa JINA la BWANA………………(yakobo 5:14).Mimi ninaona hii ni biashara tu kama ambavyo mtumishi mmoja anavyofanya anaombea watu wanapona wakitoa ushuhuda watu wanaanza kutuza huyo mtumishi! dada Mary hebu hii ya watumishi kutuzwa kwa sababu eti wameombea wagonjwa wakapona naomba uitafutie nafasi wapendwa waijadili maana mimi inanipa shida kwakweli..UTUKUFU NI WA MUNGU hata naamani alipoponywa ukoma alitaka kumtuza Elisha lakini elisha hakukubali na tena mtumishi wa elisha alipoamua kumfuata Naamani akachukua zile zawadi Elisha alimwambia,”Je huu ndio WAKATI wa kupokea fedha,na kupokea mavazi na mashamba ya mizeituni na mizabibu na kondoo na ng’ombe na watumwa na wajakazi?Basi ukoma wa naamani utakushika wewe na wazao wako hata milele.watumishi wa sasa hawangalii wakati wa kupokea na wakati wa kutopokea kwa sababu wengi wako kibiashara zaidi na siyo kihuduma.Yesu alipomponya yule mgerasi,mgerasi alimwambia yesu kwamba nitakufuata popote utakakokwenda lakini Yesu alimwambia nenda kwa ndugu zako kawahubiria au kawashuhudie mambo ambayo Mungu amekutendea! kwa nini? kwa sababu UTUKUFU NI WA MUNGU PEKEE!!! ndo maana mfalme herode alipolewa sifa za watu na kukubali kupokea utukufu wa Mungu alipigwa na malaika akaliwa na chango akafa!(matendo 12:21 – 23). mbarikiwe! samahani kama nitakuwa nimetoka nje ya mada!

 12. Swala la kuuza mafuta ya upako hii ni ajabu sana. Kazi ya Mungu haiuzwi, Bwana alisema mmepewa bure toeni bure. Sasa kuuza tena karama ya Mungu? kama yangekuwa mafuta ya kula kama korie au sunflower oil, , unanunua unakwenda kupikia… hapo sawa. Au mafuta kama Vaseline au aina yake kwa manufaa ya matumizi ya ngozi tu …hakuna shida, unaweza kununu. Kwa swala la kutumika kwa matumizi ya kiimani, inakuwa kama uganga tu wa kienyeji kama mchangiaji wa kwanza alivyoosema. Wakristo tulielewe vizuri neno la Mungu. Watu wengi wanaangamia kwa kukosa maarifa ya Neno la Mungu.

 13. Mimi napata shida kidogo juu ya mambo ambayo yapo katika ulimwengu wa sasa na yanayoendelea kufanyika.
  Naamini kuwa mafuta ya upako hayana tatizo kama mafuta, ila yanawezekana yana shida kwa kutokana na dhamira ya mhusika kwenye hayo mafuta.
  mfano suala la nani ameyaandaa mafuta hayo?
  je dhamira yake kuyaandaa mafuta hayo ni nini?
  je mafuta hayo yametolewa kwa dhamira ya kueneza ufalme gani?

  Kuwa na hadhari kuhusu mafuta hayo ni vyema maana unaweza ukabebeshwa roho ambazo kimsingi si za kumtukuza KRISTO bali ni kwa ajili ya Utukufu wa Nguvu za Giza

 14. Kweli itasimama daima. Mimi sipingani na matumizi ya mafuta. Ila suala la kwamba mafuta yanauzwa hilo siyo sahihi na siyo la kibiblia.Maana yake hawa watu wanafanya biashara ya mafuta kwa kisingizio cha imani. Wajinga kiimani ndiyo waliwao.Ushauri wangu: usinunue mafuta hayo. Omba Mungu akuongeze IMANI nawe utaishi. Na pia mwombe Mungu akupe uimara usiyumbishwe na mikate na majina ya watumishi. Soma neno mwenyewe kwa utayari wa kumwona Mungu katika maisha yako, usiwe mshabiki wa watumishi na uwe makini na wimbi la mafundisho.Kumbuka kutendeka kwa miujiza siyo ushahidi wa uhalali wa miujiza hiyo.Tumekwisha onywa kwamba kama siku hizo zisingalifupishwa basi hata wateule wangalipotea. Usiende kwa kuona bali kwa imani yenye matendo. Ubarikiwe kwa hekima na mafunuo katika kipindi hiki cha mpito. Njoo Bwana Yesu, njoo!

 15. Amani ya Yesu Kristo iwe nanyi,
  Kuhusu suala la mafuta ni kwamba halijaanza leo lipo toka enzi za agano la kale, ukisoma kitabu cha kutoka 29:7 “Then shalt thou take the anointing oil, and pour it upon his head, and anoint him” hapa Aaron alikuwa akipewa ukuhani.
  kutoka 30:1-38 Biblia inatuelezea habari za namna ya Mafuta ya upako Mungu alivyoagiza yatengenezwe.
  Pia kumbuka katika Agano la kale hakuna aliyewahi kuwa mfalme bila kuwa anointed soma vizuri habari za wafamle waliowahi kuongoza enzi za agano la kale.
  Ukisoma 1Samuel 16:13 “Then Samuel took the horn of oil, and anointed him in the midst of his brethren: and the spirit of the LORD came upon David from that day forward. So Samuel rose up, and went to Ramah” Hapa biblia inatuambia kuwa Samuel alichukua pembe iliyokuwa na mafuta akampaka Samuel mafuta lakini kilichokuja juu ya David ni Roho Mtakatifu, ndipo sasa tunaelewa na kuamini kuwa ni njia mojawapo ya kuingiziwa (Impartation) Roho Mtakatifu.
  Pia katika agano jipya mafuta haya yalitumika na Yesu mwenyewe ndiye aliyeagiza mafuta haya yatumike. Ukisoma Mark 6 kuanzia mstari wa 7 utaona Yesu anawatuma wanafunzi wake na katika kuwatuma aliwaambia wasibebe chochote hata koti la ziada wasibebe lakini ukifika mstari wa 13 tunaambiwa “And they cast out many devils, and anointed with oil many that were sick, and healed them” waliwapaka mafuta wagonjwa nao wakapona sasa hii inamaana kuwa Yesu aliwaruhusu kubeba mafuta ya upako na kuyatumia na waliporudi walishuhudia kuwa haya mambo.
  Ni sehemu nyingi sana mafuta ya upako katika Biblia kwa matumizi tofauti na ukiangalia James 5:14 “Is any sick among you? let him call for the elders of the church; and let them pray over him, anointing him with oil in the name of the Lord” Hii inamaana hata wagonjwa wanapona kwa kuombewa na kupakwa mafuta ya upako.

  ANGALIZO:
  Mafuta ya upako ukiyatumia bila uelewa na usipochanganya na imani unakuwa huna tofauti na mganga wa kienyeji. (Samahani kama nimetumia maneno makali) kwa kuwa Biblia inatuambia katika Rom 1:17 “For therein is the righteousness of God revealed from faith to faith: as it is written, The just shall live by faith” neno hilohilo likarudiwa tena Gal 3:11 “But that no man is justified by the law in the sight of God, it is evident: for, The just shall live by faith” na Heb 10:38 “Now the just shall live by faith: but if any man draw back, my soul shall have no pleasure in him”
  MIMI, Wisdom, NAAMINI KUWA KATIKA UKRISTO NI LAZIMA UELEWE UNACHOKIFANYA NA UKIFANYE KWA IMANI.

  AMANI YA YESU KRISTO IWE NANYI

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s