Msimamo wa Tanzania Kuhusu ndoa ya jinsia moja

Katika kikao cha Bunge la Bajeti kinachoendelea hivi sasa mjini Dodoma, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe alilazimika kusimama na kutoa majibu kwa swali lililoulizwa na Mbunge wa Konde, Khatibu Said Haji (CUF) aliyetaka kujua msimamo wa Tanzania kuhusu suala la kuridhia ndoa za watu wa jinsia moja hasa baada ya shinikizo la nchi wahisani kuwa awtasitisha misaada kwa nchi zitakazoweka vikwazo kwa watu wa kundi hilo.

Akijibu swali hilo Membe ameelezea msimamo wa Tanzania, Membe amesema sheria ya ndoa ya mwaka 1971 inatafsiri ndoa kuwa ni muungano wa hiari kati ya mwanamume na mwanamke wenye lengo la kudumu katika maisha ya wawili hao.

Akasema suala la msingi ni kuwa, kulingana na matakwa ya sheria ya Tanzania ili kuwepo na ndoa inayotambulika kisheria ni lazima kuwepo na pande mbili za jinsia tofauti, yaani mwanamume na mwanamke.

“Dini zetu zote za hapa nchini hazikubaliani na uwepo wa ndoa za jinsia moja na viongozi wake wapo kwenye mstari wa mbele kukemea jambo hili,” alisema Membe.

Akasema utamaduni wetu na sheria zetu hazitambui ndoa ya jinsia moja. Akasema muungano kati ya watu wa jinsia moja, yaani mwanamume na mwanamume mwingine au mwanamke na mwanamke mwingine hautambuliki kama ndoa kisheria nchini Tanzania.

Katika swali la nyongeza, Haji pia alitaka kujua ni mikakati gani Tanzania imejiwekea endapo nchi hizo wahisani zitasitisha misaada yao kwa nchi hii, kutokana na msimamo wake ambapo Membe alisema fursa za kiuchumi ambazo zimeendelea kuibuliwa nchini ni moja ya mikakati ya Serikali kuhakikisha kuwa inajitegemea kiuchumi badala ya kuzitegemea nchi wahisani.

Alitoa mfano wa gesi iliyovumbuliwa katika mikoa ya Kusini kuwa ni moja ya nguzo ya uchumi ambayo Tanzania itaitumia ili iweze kujiendesha kiuchumi mara nchi wahisani waking’ang’ania sharti hilo la kuruhusu ushoga. Membe akasema rasilimali hizo na nyingine zikitumiwa vizuri hakuna taifa ambalo litaichezea Tanzania ovyo ovyo kwa kuwapa masharti ya ajabu.

Membe amesema itakapotokea wahisani wanasitisha misaada kwa sababu ya msimamo wa Tanzania wa kupinga ndoa za jinsia moja, Watanzania wako tayari kujifunga mikanda na kujibeba wenyewe badala ya kukubali kudhalilishwa utu na utamaduni wao.

Membe ameliambia Bunge kuwa Tanzania itaendelea kupokea misaada ile tu ambayo haina masharti ya kubadili sera, utamaduni na sheria za nchi kuhusu ndoa za jinsia moja.

“Nchi marafiki duniani zikiwemo zile za Magharibi, zimeendelea kutuheshimu kutokana na msimamo wetu huo thabiti na usiotetereka kwa kuendelea kutoa misaada ya ushirikiano wa kiuchumi kwa Serikali ya Tanzania,” alisema Membe.

–Wavuti

17 thoughts on “Msimamo wa Tanzania Kuhusu ndoa ya jinsia moja

  1. NDOA YA JINSIA MOJA NI UDHALILISHAJI ULIOPITILIZA , HIVYO HATUNA BUDI KUIPINGA VIKALI.

  2. kiukweli mungu atabaki kuwa mungu tu na jina lake lihimidiwe milele na milele.mwenye macho na ayaone mwenye masikio na asikie.tufunge na kuomba kikombe hicho cha freemasons kituepuke

  3. AMA KWELI SHETANI HANA AIBU,LILE USILODHANIA YEYE NDO ANAFANYA. KUBWA ALILOFANIKIWA NI KUDUMAZA AKILI ZA WANADAMU MAMBO YALIYOKUWA HAYAZUNGUMZIKI KWA SABABU YA UCHAFU WAKE SASA YAMEPATA NAFAS YA KUJADILIWA TENA KWA HOT DISCUSION NA WATU BILA HAYA WANADAMU TUNAYATETEA.TUKUMBUKENI WAKATI WA GARIKA,SODOMA NA GOMORA NA HABAR YA NINAWI, NUHU ,RUTH NA YONA NI WAJUMBE AMBAO MUNGU ALIWATUMIA KUYARUDISHA MATAIFA HAYA YALIPO KENGEUL WALIOPUUZA NA KUENDELEZA MATAKWA YAO MUNGU ALIWACHAPA KWA FIMBO YAKE..!DHAMBI YA TAIFA NI JANGA LA KITAIFA “MUNGU ATATUCHAPA” ENYI VIONGOZI WA JUU MNAOSHIKILIA HIZO KALAM ZA KUTILIA SAIN MAKUBALIANO HAYO EPUKENI KUHALALISHA LAANA KWA MIKONO YENU .MWENYEZI MUNGU AWALINDE NA TAIFA LOTE KWA UJUMLA. ZINGATI HAKUNA AJUAE SIKU YA HUKUM .UFUNUO 16:15.AMEN.

  4. waziri kaza uzi mataifa makubwa yanambinu ya mbali ya kutaka kupunguza idadi ya watu kupitia mipango mbalimbali ikiwemo ndoa ya watu wawili wa wa jinsia moja(mwanamumw kwa mwanamume)magonjwa kama vile UKIMWI iepushe tz na maovu hayo. Na jua kila mmoja wetu ana dini basi someni hivyo vitabu vya ndini ukurasa baada ukurasa kifungu baada ya kifungu

  5. Mungu ni mwenye huruma,uvumilivu na upendo kwa watu wake.Kumkosea kwa makusudi anafikia kipindi anaamua kuturudisha kwa fimbo yake.Hiyo fimbo yaweza kutuumiza maana ni kwa ajili ya kuturudisha zizini.Tusisubir fimbo ituchape…

  6. MYAONAPO HAYO,BASI CHANGAMKENI MKAVIINUE VICHWA VYENU…SASA NI WAKATI WA KUSIMAMA NA KUUCHUNGUZA UKWELI.NIHATAR KUPOKEA MAPOKEO BILA YA KUYACHUNGUZA,TUTAPOTEA. UNABII UNATIMIA,NA KILA MTU ANAHUSIKA,SWALI NI KWAMBA UNATIMIZA UNABII KWA UPANDE UPI?

  7. AHSANTE MH MBUNGE KWA KUHOJI MSIMAMO WA SERIKALI USICHOKE TUKO PAMOJA NAWE MUNGU AKUBARIKI SANA

  8. Hatuwezi tukaishia hapo tu, kufurahia kuwa serkali imekataa misada ya aina hiyo, ndiyo hiyo ni sehemu, lakini tuende zaidi ya hapo. Je ni ushoga tu na usagaji ndio dhambi? Nimeshukuru kwa Mh. Membe kutamka kuwa dini zetu hazikubaliani ni hayo. Ebu niendelee kuorodhesha dhambi zingine. 1kor 6.8,9,10,11. Nianzie mst.9. AU HAMJUI YA KUWA WADHALIMU HAWATAURITHI UFALME WA MUNGU? MSIDANGANYIKE. WAASHERATI HAWATAURITHI UFALME WA MUNGU, WALA WAABUDU SANAMU. WALA WAZINZI, WALA WAFIRAJI, WALAWITI, WEVI.WATAMANIO, WALA WALEVI, WATUKANAJI,WANYANG’ANYI, Anamalizia kuwa baadhi yenu mlikuwa watu wa aina hiyo, akiwa na maana kuwa ukiokoka hayo unayaacha, WAFIRAJI, WALAWITI wameoreshwa pamoja na dhambi zingine. Niongeze zingine kidogo. Gal 5.19.20 na 21. UASHERATI, UCHAFU,UFISADI. IBADA YA SANAMU, UCHAWI, UADUI, UGOMVI, WIVU, HASIRA, FITINA, FARAKA, UZUSHI, HUSUDA, ULEVI, ULAFI, na yanayofanana na hayo, anasema watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi UFALME WA MUNGU. Pamoja na kuwa tumekataa misaada ya Magaribi ambao wemehalalisha ndoa za jinsia moja, nimesema tusibweteke tukadhani hata mbele za Mungu tuko salama tumlilie Mungu awageuze mashoga, wasagaji, na dhambi zingine. Thanks..

  9. Mbingu na Nchi zitapita, lakini Neno la Mungu halitapita, Biblia iliyaona hayo, ikayasema, ni juu ya mtu kuamua, ama kutii, au kutokutii. Ni sawa kwamba Serkali yetu imetoa tamko kuhusu swala hilo, ndiyo, lakini swala ni hili MASHOGA WAPO? Jibu ni ndio wapo, napenda kuwasaidia kuwa ni dhambi, pia niwaambie imeandikwa wapi katika Biblia. RUMI 1.24-32. KWA AJILI YA HAYO MUNGU ALIWAACHA KATIKA TAMAA ZA MIOYO YAO, WAUFUATE UCHAFU, HATA WAKAVUNJIANA HESHIMA MÍLI YAO, KWA MAANA WALIIBADILI KWELI YA MUNGU KUWA UONGO, WAKAKISUJUDIA KIUMBE NA KUKIABUDU BADALA YA MUUMBA ANAYEHIMIDIWA MILELE, HIVYO MUNGU ALIWAACHA WAFUATE TAMAA ZAO ZA AIBU, HATA WANAWAKE WAKABADILI MATUMIZI YA ASILI KWA MATUMIZI YASIYO YA ASILI, WANAUME NAO VIVYO HIVYO WALIYAACHA MATUMIZI YA MKE, YA ASILI, WAKAWAKIANA TAMAA, WANAUME WAKIYATENDA YASIYOWAPASA, WAKAPATA NAFSINI MWAO MALIPO. Swala si Serkali kukataa misaada, swala ni MASHOGA Tunao nchini, wasagaji tunao, ni akina nani hawa,? Ni kaka zetu, ni baba zetu, wadogo zetu, watoto wetu, TUFANYEJE!?.

  10. Kwa hivi sasa Tanzania wanasema kwamba ndoa za jinsia moja si utamaduni wetu. Naogopa iko siku huu utajakuwa utamaduni wetu. Watawala wetu wangesimama imara na kusema ya kwamba jambo hili ni dhambi na Mungu amekataza jambo hili kwa wanadamu wote badala ya kujitetea ya kwamba huu si utamaduni wetu

  11. YESU UTUSAIDIE, MAANA HIZI NI SIKU ZA MWISHO SHETANI ANATUMIA MBINU ZOZOTE APATE KUWAMEZA WATU. NI WAKATI KILA MMOJA ASIMAME KWA BIDII KATIKA ZAMU YAKE. HABAKUKI 2:1,
    MBARIKIWE. (YESU-JANA/LEO/MILELE)

  12. YESU UTUSAIDIE, MAANA HIZI NI SIKU ZA MWISHO SHETANI ANATUMIA MBINU ZOZOTE APATE KUWAMEZA WATU. NI WAKATI KILA MMOJA ASIMAME KWA BIDII KATIKA ZAMU YAKE. HABAKUKI 2:1249299

  13. Wanaoafiki ushoga ni miongoni mwa Mashoga akili zao zimekoma kufikiri,hakika watalaniwa,tuwaepuke hata kuwasikiliza daima.mungu atusaidie daima.

  14. bora Tanzania isibadili msimamo kama mpango wa msaada na masharti ya madhambi kama hayo waacheni na misaada yao.

  15. tuko siku za mwisho ndoa gani ya jinsia mbili jamani tutubu nakuiamini injili tuaje maovu hayo, jamani inasikitisha

  16. jamani samahanini ukitaka kuwa member wa strictly gospel wordpess unajiunga vipi anayefahamu anijuze. hatua hizo

  17. Watanzania tuzidi kumuomba Mungu atasaidie taifa letu lisimame imara lisiyumbishe kwa kuchukulia kigezo cha misaada hatutaki ndoa za jinsia moja kwa jina la yesu maana hiyo ni laana kwa taifa Mungu atusaidie sana.

Andika maoni yako