SADAKA YA UKOMBOZI

Mimi natoka Kenya na nimeingia kwa blog hii kusoma na kujifahamisha mengi kuhusiana na wokovu. Nimependezwa sana na somo hili na hata mimi naomba kuuliza swali:


1. Nimesikia wengi wa wachungaji na watumishi wa Mungu wakiitisha Sadaka ya Ukombozi kwa wanaotaka kufanyiwa.

(a).Je! ni halali kutoa sadaka ya ukombozi?


(b).Ni maandiko yapi yanayodhibitisha hayo?

Nitafurahi sana kupata majibu ya maswali yangu.

Elvis Nyale

Je, Ni sawa Kupiga picha ukiwa katika Maombi kisha unaituma kwenye mtandao?

wp-1476940721194.jpg

Bwana Yesu alisema:

“Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. (Mathayo 6 : 6).

Siku hizi mtu anakuwa kwenye maombi, anapigwa picha kisha anairusha kwenye mtandao na kutangaza kwamba alikuwa mbele za Mungu, au anaandika alikuwa anabubujika!!

Mwingine anaamua kufanya maombi ya Kufunga, anakwenda Mlimani, halafu anakuwa anapiga picha kila siku, akiwa huko mlimani na kuzituma katika mtandao.

Nini maoni yako kuhusu suala hili??

 

Kuokoka vs Kutenda Dhambi

wp-1470656303150.jpg

 

Biblia katika 1Yohana 5:18 inasema hivi:

“Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hamgusi”

Swali lililopo hapa ni kwamba:

a). Hivii, Mtu AKIOKOKA huendelea tena KUJIZUIA kutenda dhambi au HUWA HAJISIKII kufanya dhambi kwa kuwa msukumo wa kutenda dhambi haumo ndani yake?? ( Yaani HAIHITAJI KUJITAHIDI asitende dhambi bali huwa HAWEZI kutenda dhambi kwa kuwa Nguvu ya dhambi haimo ndani yake??)

b) Kama anatakiwa aendelee KUJIZUIA ASITENDE DHAMBI hata baada ya kuwa amempokea Yesu, Je! Nini tofauti na mtu ambaye HUJITAHIDI KUTENDA MEMA hata kama hajampokea Yesu (Yaani anajitahidi kutimiza Sheria zile 10)?

 

Kuonyeshwa Mbinguni

heaven.jpg

Hebu Tujadili jambo hili.

Yawezekana umeshasikia ushuhuda wa mtu ambaye alisimulia jinsi ALIVYOPELEKWA MBINGUNI kisha akarudi tena hapa Duniani. Au pengine ni mmoja wao wa watu waliopata ujuzi wa namna hiyo.

Jambo linalosababisha mjadala huu ni kwamba katika Shuhuda hizi kila anayesimulia husimulia mambo tofauti na mwingine! Yaani mmoja akisimulia jinsi alivyoingia na Mambo aliyoyaona huko Mbinguni huwa TOFAUTI na asimuliavyo mwingine.

Mfano: Ā Mmoja anaweza kusema aliowaona kule Sura zao zinafanana, mwingine akasema sura hazifanani. Mmoja anaweza kusema walifika mahali wakala vitu fulani, Mwingine akasema kule hakuna wala kunywa; na mambo mengine mfano wa hayo!!

Mambo ya kujadili ni pamoja na yafuatayo:

Je, Suala hili la watu kuchukuliwa katika Roho kisha akapelekwa Mbinguni lipo kweli? Na usahihi wake ni upi? Twaweza kulipata katika Biblia?

Kama kweli Mbingu ni moja ni kwa nini kila anayeshuhudia kwamba alifikishwa Mbinguni masimulizi yake hutofautiana na mwingine, ambaye naye husimulia habari za huko huko Mbinguni?

Je, Inawezekana mtu kwenda akaonana na Mungu kisha akarudi tena hapa Duniani kuishi?

Kuna watu wamekuwa wakizinduka akielezea ushuhuda wake anasema Amepewa ujumbe aje awaambie watu, mfano, juu ya kutubu na kuacha dhambi au ujumbe mwingine. Je, Hii haipingani na maneno ambayo aliambiwa Tajiri kwamba Watu yawapasa kusikiliza maneno ya watumishi wa Mungu walioko Duniani, maana hata akitumwa mtu kutoka kwa wafu haiwezi kusaidia kitu? (Kisa cha Tajiri na Lazaro masikini)

Karibu katika mjadala kuhusiana na hayo, pamoja na mengine yatakayojitokeza!

 

Usikate Tamaa!

wp-1468997924869.jpg

ELIYA ALIKATAA KUKATISHWA TAMAA

OMBI: Mwenyezi Mungu na Baba yetu mwema wa mbinguni, tunakushukuru sana kwa ajili ya ukuu na upendo Wako kwetu! Asante kwa kutupenda na kutusamehe dhambi zetu. Tunaalika uwepo Wako katika tafakari hii. Tusaidie kulifahamu Neno Lako, tubadilishe ili tufanane Nawe, na pia tupatie uwezo wa kuyatenda mapenzi Yako. Tunaomba na kuamini katika Jina la Yesu Kristo. Amina!

Tuendelee na kutafakari bahari za Eliya:

“Ikawa mara ya saba akasema, Tazama, wingu linatoka katika bahari, nalo ni dogo kama mkono wa mtu. Akanena, Enenda, umwambie Ahabu, Tandika, ushuke, mvua isikuzuieā€ (1 Wafalme 18:44 ).

Hapa tunapata mafundisho muhimu kutokana na uzoefu wa Eliya. Alipokuwa pale Mlimani Karmeli aliomba mvua inyeshe, imani yake ikajaribiwa, lakini “alidumu katika kufanya maombi yake yajulikane kwa Mungu.”

Aliomba kwa dhati mara sita na bado hapakuwa na ishara iliyoonesha kwamba ombi lake lilikuwa limekubalika, lakini huku imani yake ikiwa na nguvu, alisisitiza ombi lake kuelekea kwenye Kiti cha Enzi cha neema. “Kama angechoka na kukata tamaa mara ya sita ombi lake lisingejibiwa.”

Tunaye Mungu ambaye sikio Lake halijafungwa ili asisikie maombi yetu, na “ikiwa tutalijaribu Neno Lake, ataheshimu imani yetu”. Yeye anataka shauku zetu zote ziwe zinefungamanishwa pamoja na mapenzi Yake na hapo ndipo atatubariki kwa uhakika kabisa, kwani hapo ndipo hatutajitwalia utukufu wakati baraka zitakapokuwa zetu, bali “tutaelekeza sifa zote kwa Mungu.”

Siyo mara zote ambapo Mungu hujibu maombi yetu papo kwa papo tunapomwita kwa mara ya kwanza, kwani akifanya hivi, “tunaweza kukichukulia kirahisi tu kwamba tulikuwa na haki kupata baraka na fadhili zote ambazo alitupatia”.

Mtumishi wa Eliya alikuwa akimtazama Eliya alipokuwa akiomba. Alipokuwa akichunguza moyo wake, alionekana kupungua zaidi na zaidi, kulingana na alivyojitazama mwenyewe na jinsi alivyojiona machoni pa Mungu. llionekana kwake kwamba alikuwa sio kitu na kwamba Mungu ndiye aliyekuwa kila kitu, “na pale alipofikia hatua ya kuikana nafsi, huku akimng’ang’ania Mwokozi kama nguvu na haki yake pekee, jibu lilikuja.”

Hata mtu awe jasiri na mwenye mafanikio kiasi gani afanyapo kazi maalum, “asipodumu kumtazama Mungu” wakati mambo yanapotokea kujaribu imani yake, “atapoteza ujasiri wake”. Hata baada ya Mungu kumpatia vielelezo dhahiri vya uwezo Wake, hata baada ya kuimarishwa kufanya kazi ya Mungu, atashindwa asipomtegemea kikamilifu Yeye aliye na uwezo wote!

Unapokuwa umekwenda mbele za Mungu kwa ajili ya hitaji lako kamwe Usikate tamaa!!

Mchungaji Samuel Imori