MILIMA, MITO, BAHARI na Uhusiano wa Kiroho

Je, Kuna uhusiano gani wa KIROHO na Milima, Mito na Bahari? Amri Kumi zilitolewa Mlimani – Kutoka 31:18. Yesu alisulubiwa Golgotha, Mlimani – Marko 15:22 Wale majini waliowaingia Nguruwe waliwapeleka Baharini – Mathayo 8:32 Kuna maneno mengi mitaani na shuhuda nyingi makanisani zinazohusisha Milima, Mito na Bahari na mambo ya Kiroho, ya kiMungu au ya … Continue reading

Nahitaji Maombi na Ushauri

Bwana Yesu asifiwe! Haja ya moyo wangu kwa Wakristo wenzangu hapa Strictly Gospel ni kuomba ushauri pamoja na kuhitaji muungane nami katika kuliombea suala hili. Mimi ni kijana nimeokoka  na ni mzaliwa wa kwanza kwenye familia yetu na mzaliwa wa kwanza kiroho kwa sababu Mungu alianza kuniokoa mimi ijapokuwa nina ndugu zangu wameokoka lakini bado … Continue reading

Matumizi ya VITU badala ya JINA LA YESU.

Kadri siku zinavyokwenda Matumizi ya vitu kama Vitambaa, Maji nk yanazidi kuongezeka ambapo watu wanaojulikana kama Watumishi wa Mungu HUVIOMBEA vitu hivyo kisha kuwagawia/Kuwauzia watu. Mtu akipatwa na tatizo anachotakiwa kufanya ni KUBANDIKA, KUPAKA, KUMIMINIA, KUNYWA au KUNUSA/KUVUTA kitu alicho alichonunua, kutegemeana na maelekezo ya matumizi ya kitu hicho. Je, Jambo hili ni Sahihi katika Ukristo?

Sala ya Bwana

  Bwana Yesu asifiwe! Napenda niwashirikishe kuhusu SALA YA BWANA ambayo watu wengi tunaijua. Tutakwenda  kuona ufafanuzi ambao unaweza kutusaidia ili kuweza kujua namna sahihi ya kutumia. Sala hii ya Bwana inapatikana katika kile kitabu cha Mathayo 6:9-13: 9: Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, 10:Mapenzi yako … Continue reading

TANGAZO

Bwana Yesu asifiwe! Tunapenda kukujulisha mpendwa msomaji kwamba Kama una MASOMO, USHUHUDA, MASWALI, MAHUBIRI nk ambayo ungependa kuwashirikisha wasomaji wengine hapa, utume kwenye email: “strictlygospel@yahoo.co.uk” Yakishatufikia tutayahakiki kabla ya kuyaweka hadharani. Kama itatokea ulichotuma hakijaonekana hadharani basi tutakujulisha sababu yake. Mungu akubariki sana kwa ushiriki wako hapa. SG

Kuyahoji Majini wakati wa Maombezi.

    Baadhi ya Watumishi wa Mungu wakati wa kufukuza Mapepo/Majini huwa wanahojiana nayo kwa muda mrefu. Anauliza; Anajibiwa na hata wengine huwaambia kusanyiko kuzingatia yanayozungumzwa na majini/mapepo hayo ili kama kuna la muhimu walichukue!! – Je, ni sahihi kuhojiana na majini wakati wa kuyafukuza? – Je, ni muhimu kuzingatia yale ambayo husemwa na majini/mapepo … Continue reading