Tunakutakia Heri ya Mwaka Mpya 2023

Kwa muda wa kama miaka miwili hatukuweza kuwa hapa kutokana na sababu mbalimbali. Lakini kwa neema ya Mungu sasa tumerudi!

Tunakutakia heri kwa mwaka huu wa 2023. Wakaribishe ndugu na marafiki kutembelea blog hii kwa maana sasa iko hewani.

Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote” 2Kor 13:14

Tuendelee Kuombea UCHAGUZI

3

Bwana Yesu asifiwe!

Wakati kampeni zinaendelea na tarehe ya Uchaguzi inazidi kukaribia unakumbushwa kuendelea kuuombea Uchaguzi Mkuu unaofanyika siku ya Jumapili ya Tarehe 25/10/2015.

Yako mambo mengi ambayo yanahitaji msaada wa Mungu. Wakati unaombea uchaguzi huu unaweza pia kukumbuka kuombea hafuatayo:

– Mungu awape afya njema wagombea wote hadi uchaguzi ukamilike.

– Mungu aepushe ajali za misafara ya kampeni.

– Hila zozote mbaya kinyume na uchaguzi zikadhihirike na kuharibiwa

-Hekima, maarifa na Uzalendo vikatawale kampeni ili kuepusha vurugu na mifarakano isiyo ya lazima!

Mungu akubariki unapoendelea kuombea Uchaguzi huu.

TANGAZO

email-marketing-announcement

Bwana Yesu asifiwe!

Tunapenda kukujulisha mpendwa msomaji kwamba Kama una MASOMO, USHUHUDA, MASWALI, MAHUBIRI nk ambayo ungependa kuwashirikisha wasomaji wengine hapa, utume kwenye email:

“strictlygospel@yahoo.co.uk”

Yakishatufikia tutayahakiki kabla ya kuyaweka hadharani. Kama itatokea ulichotuma hakijaonekana hadharani basi tutakujulisha sababu yake.

Mungu akubariki sana kwa ushiriki wako hapa.

SG

Mtu na Utatu Uliofarakana

body-soul-spirit seowl

Binadamu/Mtu ameumbwa akiwa na muungano wa MWILI, NAFSI na ROHO. Vitu hivi vitatu ni picha au mfano wa Utatu Mtakatifu wa Mungu. Utatu Mtakatifu ni kitu Kimoja. Wameungana. Hufanya kazi pamoja!

Yohana 14:10 “Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake.”

Yohana 15:26 “Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia.”

Maandiko hayo mawili hapo juu yanaonyesha UMOJA wa UTATU huo.

Utatu wa Mtu, kama ilivyoandikwa pale mwanzoni, unatengenezwa na MWILI,NAFSI na ROHO. Tatizo lililopo hapa ni kwamba Utatu huu siyo mara zote unafanya kazi kwa pamoja! Siyo wakati wote vitu hivi vitatu huwa vinatembea pamoja. Kuna wakati Mwili unaweza kuwa sehemu moja lakini Nafsi iko sehemu nyingine! Ndiyo maana inawezekana mtu akawa, mfano, Kanisani lakini Mawazo/Nafsi iko mahali kwingine, akiwaza mengine tofauti kabisa na kile mwili unafanya pale kanisani! Bwana Yesu analijua hili ndiyo maana anasema, katika Mathayo 15:8, kwamba “Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami.”

Tena, wakati UTATU Mtakatifu hufanya kazi pamoja, lakini UTATU wa Mtu  HUSHINDANA:  Wagalatia 5:17 “Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.”

Yako maandiko mengi yanayoonyesha kwamba kuna Mgogoro ndani ya Mtu. Twaweza kumuona mtu anacheka, uso wake umejaa tabasamu lakini moyoni ana majonzi! Twaweza kumuona mtu anaimba na kucheza lakini kumbe mawazo yake yako mbali. Kwa wakati wako unaweza kusoma maandiko yafuatayo ili kuona jinsi kulivyo na mgogoro katika Utatu wa Mtu: Marko 9:47, Yeremia 17:9, Wagalatia 5:19-22)

Mtu Akimpokea Yesu na Kukubali kuishi maisha ya Kumcha Mungu, Mfarakano kati ya Mwili, Nafsi na Roho HUONDOLEWA. Huwa panatengenezwa Muungano unaoanzia Rohoni na kuishia Mwilini. Mtu aliyeokoka na Kujazwa na Roho Mtakatifu anao UWEZO wa Kuvitiisha Nafsi na Roho yake. Ndipo Neno la Mungu linasema, katika Wagalatia 5:16 “Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.” Huu ndio Uelekeo Sahihi wa Utawala ndani ya Mtu ili Utatu wake uwe na UMOJA. Haiwezekani kuwa na Umoja katika Utatu wa Mtu kwa Kuufanya MWILI NDIO UWE KIONGOZI “kwa maana kama mkiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi. (Warumi 8 :13). Na tena katika Wagalatia 5:19-22 yameorodheshwa mambo ambayo Mwili ukipewa Ungozi ndiyo yatapewa Msisitizo wa kwanza!

Mtu ambaye Utatu wake Umefarakana Ni rahisi tuu KUSEMA UONGO kwa kuwa ndani yake HAKUNA UMOJA. Twaweza kuona mfano mmoja ambao ni KUAPISHWA KWA WABUNGE NA VIONGOZI MBALIMBALI. Watu hawa Huapa wakiwa wameshikilia Vitabu Vya Dini, kwa kuamini kwamba wanayoyatamka hapo ni ya kweli. Lakini utashangaa mtu akiingia kazini na kupewa Ofisi Anayotenda ni tofauti kabisa na vie alivyoapa!! Hii ni kwa sababu aliapa kwa mdomo tuu lakini Moyo wake haukuambatana na Maneno aliyokuwa akiyatamka!

Mtu aliyezaliwa mara ya pili ni Mkweli. Hawezi kusema Uongo maana akitaka kudanganya Roho yake hukataa. Mtu akifika katika kiwango hicho ” Ndiyo” yake inakuwa ni “Ndiyo” na “Hapana” inakuwa ni “Hapana”. (Mathayo 5:37 “Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.”)

Hasara za UTATU ULIOFARAKANA

Mtu ambaye Hana Umoja katika Nafsi yake:

-Ni Muoga,

-Hana amani,

-Hana Furaha ya kweli,

-Hana ujasiri wa kwenda mbele za Mungu kwa maana Anapopiga magoti kumuomba Mungu mashitaka ya maovu huanza kutangulia ndipo maombi yake yanafuata nyuma! (1Yohn 3:21).

-Hawezi kuwa na Uhakika kama kweli Mungu kasikia maombi yake.

-Ni mtu wa kujihukumu mbele za Mungu.

-Hana Ujasiri wa Kumkiri Yesu mbele za Watu!

-Hawezi kukubali kosa hata kama anajua kabisa ametenda bali hutafuta sababu za uongo ili kutetea uongo wake.

Hakuna Amani kubwa kwa mtu zaidi ya ile Ipatikanayo kwa Kufanywa Upya kwa Kuzaliwa Mara ya pili na Roho ndiyo ikachukua Usukani wa Uongozi. Mtu anakuwa ni mkweli. Yuko huru mbele za Mungu na Watu. Hata akiitwa Kufa hana wasiwasi kwa kuwa Roho yake hushuhudia kwamba ni mtenda mema; ni mcha Mungu wa kweli.

Jichunguze mwenyewe kwa maana Shahidi wa mambo ya mtu ni mtu mwenyewe!

Kuelekea Uchaguzi mkuu, Kanisa tusiyumbishwe!!

mwigulu

Huu ni wakati ambao nchi yetu iko kwenye mchakato wa kuchuja wagombea uraisi kutoka vyama mbali mbali vya kisiasa, ambapo mpaka sasa zaidi ya wanasiasa ishirini wametangaza nia ya kugombea kiti cha Uraisi. Katika harakati zote hizi baadhi ya wanasiasa wataonekana sehemu mbali mbali wakijihusisha na Injili au kushiriki Ibada na kuongea na washirika kwa njia kuwashawishi kwa namna moja au nyingine.

Ndugu zangu, tusiyumbishwe na maneno ya wanasiasa, tusiyumbishwe na ahadi kwenye makanisa yetu. Madhehebu yote ni muda wa kuongea na Mungu juu ya viongozi sahihi wenye kumcha yeye, wenye hofu ya Mungu. Kama tukiridhika na hali inavyoonekana ni rahisi uovu na mwaribifu kuivamia nchi.

Wachungaji, Manabii huu ni wakati wa kusikia sauti ya Mungu juu ya nchi yetu, tukinyamaza wanajimu na waganga wa kienyeji watasema badala yenu.

Mungu awabariki.

Mungu awabariki!

ej

Mtumishi wa Mungu EJ Oguda kushoto wakati wa maandalizi ya mkesha wa Strictly Gospel

Bwana Yesu asifiwe wapenzi Familia ya SG, naamini mnaendela vyema katika BWANA, ninawashukuru wote ambao bado mnaendelea kuchangia mada mbali mbali, kutuma email na kuomba ushauri na maombezi. Ninatambua mchango wa kila mmoja hata watembeleaji wa blog hii. Kutokana na matatizo yaliyo nje ya uwezo wetu group email yetu haifanyi kazi kwa sasa, tunatazamia kufungua group jipya, ikiwa ungependa kujumuika nasi tafadhali tujulishe na utaungana na wenzako kupata habari na mafundisho mbali mbali kuhusu ufalme wa Mungu. Kama umejaza form ya kushirikiana na Strictly Gospel unaweza kuacha tu hii na kwa wale ambao ni wageni au ambao wangependa kuwa kwenye group hilo na kufahamu zaidi kuhusu sisi. Tujulishe kwa kutuma email strictlygospel@yaho.co.uk

Kwa Tanzania tumekua kimya kwa muda kwa sababu tunashughulikia masuala muhimu kuhusu huduma na kuanza kazi ni pamoja na kuwafikia watu wengi kiurahisi. Wana maombi tuendelee kuomba hasa kwa viongozi wa huduma hii ili maono Mungu aliyoweka ndani yao yakatimie na Utukufu ukawe kwa Mungu, Tuendelee kufarijiana kuhusu Upendo Mkuu wa Bwana wetu Yesu Kristo na pia kuwaombea wenye mahitaji mbali mbali yanayoletwa kwenye blog hii.

Kwa USA na Canada huduma yetu na maombezi itaanza mwezi August ikiwa na watumishi kutoka sehemu mbali mbali watakaohudumu ukipenda kupata updates kwa njia ya simu au email tafadhali wasiliana nasi kwa email strictlygospel@yaho.co.uk

Na mwisho kabisa Ndugu yetu EJ Oguda amefiwa na mkewe na wameshazika wiki iliyopita, unaweza kuwasiliana naye moja kwa moja na kumfariji kwa simu no 0762-925-577. Mtumishi wa Mungu Oguda amekuwa nasi kwa shughuli mbali mbali za huduma. Itapendeza akipata simu kutoka kwako

Mungu awabariki wote, ninawapenda!

–MD