Edward Lowasa, atabiriwa na TB Joshua?

Pichani Lowasa akiwa kanisani kwa TB Joshua kama anavyoonekana kwenye Emmanuel TV, 12 June 2011

MBINU za Edward Lowassa kutaka kurejea kileleni katika ulingo wa kisiasa zimemnasa mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shelukindo, imefahamika.

Beatrice ambaye alikuwa akijitambulisha kuwa mmoja wa “wapambanaji dhidi ya ufisadi,” waliopachikwa jina la “Mitume kumi na miwili,” sasa anatajwa kuhamia rasmi mtandao wa Lowassa.

Gazeti hili limepata ushahidi wa maandishi ya mkono wa Beatrice mwenyewe yanayoonyesha kuwa amekuwa mfuasi muhimu wa Lowassa kiasi cha kushawishi wengine kujiunga katika mtandao wake.

Akiandika kwa Pindi Chana, mbunge wa Viti Maalum (CCM), tarehe 14 Februari mwaka huu, Beatrice alieleza mambo matatu katika ujumbe wake kwa Chana.

Kwanza, kumshukuru Chana kwa kukubali kulinda kura zake. Pili,  kumshawishi kumuunga mkono Lowassa. Tatu, kumweleza juu ya ulokole wake na “mtumishi aliyepakwa mafuta” kutoka Nigeria.

Beatrice anamwambia Chana kuwa Lowassa ndiye kampeni meneja wake. Hii ilikuwa katika uchaguzi wa makamishina wa Bunge; nafasi aliyogombea na kushinda.

“Mungu ni wa ajabu, (Lowassa) ameniombea kura pasipo maelezo. Ameandaa lunch na dinner (vyakula vya mchana na usiku) ambako amekuwa akiniombea kura. Ana njia za ajabu za kufanya mambo. Ahsante kwa kukubali kuhesabu kura,” inasema sehemu ya ujumbe huo.

Chana, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, ndiye alihesabu kura za Beatrice kwenye uchaguzi wa kutafuta makamishina wa Bunge.

Ni kwenye ujumbe huo ambamo Beatrice anatoboa kuwa siri ya ushindi wake ni Lowassa aliyekuwa kampeni meneja wake.

Katika kusisitiza hoja yake, Beatrice anasema, “Nimezungumza na TB Joshua wa Emmanuel TV Nigeria aliyenipa unabii kuwa rais ajaye Tanzania ni Edward Lowassa, nikamuambia haiwezekani kwani amechafuka sana.”

Anasema Joshua alimjibu, “…alikuwa amechafuka sasa amesafishwa kwani katubu. Akaniambia his past is over (maisha yake ya nyuma si kitu). Akaongeza kwa kusema, wewe Beatrice ningeangalia your past (maisha yako ya nyuma) pengine nisingekuombea kabisa. Akasema my past is over (hajali maisha yangu ya nyuma),” inasema sehemu ya ujumbe huo wa Beatrice.

Hata hivyo, Beatrice hakueleza katika waraka wake kwa Chana maisha yake ya nyuma yalikuwa vipi. Wala hajaeleza alifanya nini, hadi kuamini kuwa kama Nabii Emmanuel angeyatazama, basi asingemuombea.

Kuvuja kwa taarifa hizi kumekuja wiki tatu baada ya Lowassa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Ulinzi, Usalama na Mambo ya Nje.

Mume wa Beatrice, William Shelukindo alikuwa mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambayo iliongoza harakati za kuundwa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mkataba tata wa Richmond.

Ni taarifa ya kamati hiyo iliyosababisha Lowassa kujiuzulu wadhifa wake wa waziri mkuu, Februari 2008.

Kwa mujibu wa watu waliokaribu na Beatrice na kwa ushuhuda wake mwenyewe, mwanasiasa huyo ameamua kujisalimisha kwa Lowassa kwa kile kinachoelezwa kuwa “Lowassa ndiye rais ajaye wa Tanzania.”

Aidha, kupatikana kwa taarifa hizi kumekuja huku kukiwa na juhudi kubwa zinazofanywa na Lowassa na kundi lake kutaka kujisafisha kwa lengo la kujitosa katika kinyang’anyiro cha urais mwaka 2015.

Miongoni mwa mikakati aliyojiwekea Lowassa na kundi lake ni kujitokeza katika maeneo yote muhimu na kutoa kauli ambazo zitafanya wananchi waanze kumkubali kuwa ni kiongozi anayefaa.

Katika kutekeleza mkakati huo, Januari mwaka huu, Lowassa alijitokeza kuzungumzia vurugu zilizotokea mkoani Arusha zilizotokana na mvutano katika uchaguzi wa meya wa jiji hilo kati ya CCM na CHADEMA.

Katika mnyukano huo, watu watatu walipigwa risasi na polisi na kufariki dunia baada ya polisi kutumia nguvu isiyo ya kawaida kuzima maandamano ya CHADEMA.

Kauli hiyo ya Lowassa ilikuwa tofauti na msimamo wa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba aliyemtaka kuwasilisha maoni yake katika vikao vya chama badala ya kutumia vyombo vya habari.

Kauli nyingine ya Lowassa ilihusu nyongeza ya viwango vya mishahara kwa wafanyakazi, kutokana na kile alichoita mfumuko wa bei kuwa mkubwa.

Bali wiki moja iliyopita, Naibu Katibu Mkuu wa vyama vya wafanyakazi nchini (TUCTA), Nicholas Mganya alimtuhumu Lowassa kwa kutoa kauli hiyo akisema ana ajenda ya siri nyuma yake.

Mgaya alisema TUCTA haihitaji msaada wa Lowassa katika kusimamia madai yao. Alisema “mbunge huyo wa Monduli inaonekana ana ajenda yake mgongoni.”

Hatua nyingine ya Lowassa katika kujikarabati kisiasa ni kugombea na kupata nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.

Lowassa amekuwa pia akihudhuria hafla nyingi, hasa za madhehebu ya Kikiristo (KKKT) ambao anaonekana akitoa maoni mbalimbali kama ilivyokuwa Jumapili iliyopita ukumbi wa Dimaond Jubilee kwenye uzinduzi wea albamu ya moja ya kwaya za injili.

Kwenye kusanyiko hilo, Beatrice naye alikuwepo. Lowassa alimtaka asome maoni ya gazeti la The Citizen juu ya ushirikina uliokithiri nchini; jambo ambalo Lowassa alizungumzia kwa urefu.

MwanaHALISI lilipowasiliana na Beatrice ili kupata maoni yake juu ya ushwahiba wake mpya na Lowassa, mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo:

Mwandishi: Tusaidie maelezo kidogo juu ya ujumbe uliomwandikia Mheshimiwa Pindi Chana kumjulisha kuwa uliambiwa Edward Lowassa atakuwa rais. Ni kweli?

Beatrice: Barua ameandika nani na umeipata wapi?

Mwandishi: Hii barua fupi – memo ndani ya Bunge, uliposema Mheshimiwa Lowassa ambaye amesimamia vizuri kura zako za ukamishna wa Bunge.

Beatrice: Sina taarifa hiyo. Wala siikumbuki. Unajua ndani ya Bunge tunaandikiana mambo mengi, tena mengine ya utani tu. Na mimi na Mheshimiwa Chana sote ni “walokole,” tunafanyiana utani sana.

Mwandishi: Kwani mheshimiwa Shelukindo, mkiwa ndani ya bunge kuna utani mwingi, kwamba huwa mnaandikiana utani sana?

Beatrice: Kabisa, unajua tunaandika mambo mengi. Na kama unaandika kwa utani kwa mwenzako inabaki hivyo ni utani tu. Sasa tatizo hao wanaowaletea mambo haya wanatumia mambo haya kutafuta mipango yao ya kufikia mwaka 2015.

Alisema, “Mimi najua hakuna anayenibeba ndugu yangu. Mimi ni very solid (ngangari), sibebeki. Nakwambia, mbona mimi nina nguvu nyingi mimi mwenyewe; sihitaji kubebwa. Najua wanajaribu kuonyesha tunabebwa, lakini huo ni ujinga wao wa kufikiri.

Mwandishi: Mheshimiwa Shelukindo, kwani nyie waheshimiwa huwa mnatafutana (kufitiniana)?

Beatrice: Hiyo inafanyika sana, watu wakishakuwa na mambo yao wanatumia wengine kutimiza dhamira zao. Lakini mimi ninafikiria wananchi. Nimeshaamua kwamba Beatrice nashughulikia shida za wananchi jimboni. Ninatafuta njia za kuwaondolea umasikini, njaa na mambo kama hayo. Sasa wengine wanatafuta tu pa kunishika.

Mwandishi: Kwa hiyo Mh. Lowassa ndiye alikuwa kampeni meneja wako katika kutafuta ukamishna pale bungeni, au siyo Mheshimiwa?

Beatrice: Lakini kama anafanya kazi ya kampeni vizuri; ni vizuri tu. Isipokuwa kila mtu anajichukulia mwenyewe alivyo. Mimi ni mtu wa kazi sihitaji kusimamiwa hivyo. Na hebu tujadili hili; unajua kaka nyinyi mnafanya kazi kubwa. Sasa hii kusikia, sijui MwanaHALISI hivi, sijui hivi, pengine kuna watu wanachomekea vitu vyao. Tunapenda kazi yenu.

Mwandishi: Mheshimiwa nakushukuru sana.

Beatrice: Karibu sana tutafanya kazi pamoja.

Akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, mume wa Beatrice, William Shellukindo, alikuwa na msimamo mkali dhidi ya watuhumiwa wakuu wa ufisadi nchini na hiyo ndiyo inayoelezwa kuwa sababu ya kushindwa kwake ubunge katika mchakato wa ndani ya CCM.

Shellukindo alikuwa mbunge wa jimbo la Bumbuli mkoani Tanga kwa zaidi ya miaka 20, alishindwa katika kura za maoni na January Makamba, mtoto wa katibu mkuu wa CCM anayetajwa kuwa mfuasi wa mtandao wa Lowassa.

S0urce by Mwanahalisi – 9 March 2011

52 thoughts on “Edward Lowasa, atabiriwa na TB Joshua?

  1. Julily Thomas,

    Ulichosema na kukifanya sikiamini. Si kila mtu anaweza akatamka laana na ikawa laana kweli. Hakuna laana ya hivyo kwa watu wa Kaskazini!
    Ni hilo tu!

  2. Naomba kuwafungua masikio Watanzania wenzangu kuhusu LAANA YA KANDA YA KASKAZINI ILIYOTOLEWA NA kiongozi mmoja wa Taifa letu kwamba WATU wa kaskazini hawafai kuingia Ikulu.jambo hili si la kufumbia macho hata kidogo .Kumbuka Yoshua 6:26 Yoshua aliulaana MJI WA YERIKO na matokeo yake tunayapata katika kitabu cha 2Wafalme 2:19…. ni kuwa ule mji uliendelea kuzaa mapooza. HATUNA BUDI KUIVUNJA LAANA HII.KWANI IMEATHIRI WATU WENGI WA KASKAZINI YA TZ SI KISIASA TU BALI HATA MAOFISINI AU KWENYE MAKAMPUNI .NDUGU ZANGU DAWA YA LAANA NI KUIVUNJA KAMA VILE ELISHA ALIVYOIVUNJA LAANA YA YERIKO HATUNA BUDI KUIVUNJA LAANA HII.NA KWA MAMLAKA NILIYOPEWA NA MUNGU NINATAMKA KUIVUNJA LAANA HII KWA JINA LA YESU .NAITUMA DAMU YA YESU IKUTANE USO KWA USO NA MANENO YA LAANA HII POPOTE YANAPOTENDEWA KAZI.DAMU YA YESU GARIKISHA MANENO YA LAANA HII KWA JINA LA YESU .ISAYA 59;19b…..maana yeye atakuja kama mkondo wa mto ufurikao uendeshwao kwa pumzi ya Bwana.nautuma mkondo wa mto wa damu ya YESU FUTA LAANA hii popote inapotekelezwa .NATAMKA UHURU KWA KILA MTANZANIA

  3. Sikia Lwembe,

    Ulichosema ni mawazo yako, na yatabaki kuwa mawazo yako!

    Lakini hata kama watu wa bodaboda wamepewa hela hizo elfu 30000/- unazosema (japo sijui kama una ushahidi wa hilo) sioni tatizo katika hilo. Kwani ubaya wake ni nini kulipia gharama za mafuta ikiwa ametaka bodaboda wawe kwenye msafara wake, ni dhambi kufanya hivyo? Wewe ulitaka walipwe na nani gharama za kufanyia hayo maandamano if at all kufanya maandamano hayo kuna gharama zinahitajika?

    Kwani biblia inaposema kuwa hakuna askari huenda vitani kwa gharama zake mwenyewe ilikuwa ina maanisha nini?

    Halafu nakushangaa, ni lini wewe umekuwa mwanasiasa mpaka ujue kuiongea siasa, dini yako si inakukataza kujishughulisha na mambo ya siasa!!!

    Inaonekana huyu jamaa ni tajiri hata kuliko Dangote, ikiwa ana hela za kuwalipa maelfu ya walioandamana Dar, na zingine tena akawalipa maelfu walioandamana Mbeya, akawalipa tena na maelfu walioandamana Arusha, tena akalipa zingine kwa maelfu walioandamana Mwanza, akamalizia kuwalipa tena maelfu walioandamana Zanzibar- ni tajiri sana huyu Lowasa!

    Nani kapandikiza chuki ndani ya waumini, kama si wewe ndo unapandikza chuki?

    Siasa ni maisha, tana yanayomhusu kila mmoja wetu, kuna ubaya gani ikisemwa katika mimbari if at all inasemwa katika ukweli wake? Au wewe unafurahia ujinga wa kuona kuwa siasa inawahusu wasio wacha Mungu, halafu wakisha kuwa madarakani hao wasiomcha Mungu, kazi yenu ninyi wacha Mungu inakuwa kuanza kuwaombea?

    Siasa inatuhusu, na tunatakiwa kushiriki.

    Sisi ni wa thamani kuliko mimbari!

  4. Lowassa hafai hata kidogo kuwa rais wa nchi hata kidogo kwa 7bu ulikula hela za richmond na kama ungelikua hujala usingejiuzulu ungesubi 2huma ili uwaumbue walio kula hzo hela lakn saiz unataka ku2mwangia mchaga machon

  5. Sungura,
    Jaribu unaposoma michango ya wenzako usikaze sana shingo!
    Alichokiandika James kiko wazi sana katika medani ya siasa na utawala kwa raia wa nchi yao, wanaojitambulisha na nchi yao; katika mabaya na mema.

    Unapotafuta Maandiko kuhusu ufisadi unaofanyika leo hii na wananchi wa Tanzania, kutoka madereva wa boda boda wanaopewa 30000/- za mafuta ili kuunga misafara, mpaka maaskofu wanaotegemea fadhila kwa viongozi wanaowapigia debe, mimbara zao wakizigeuza kuwa majukwaa ya kisiasa, na makusanyiko yao kuyapandikiza chuki; nilikutegemea uje na Maandiko yatakayowaonya hao wenye kuhusika na Maandiko kwamba, kwa kuipandikiza chuki ndani ya mioyo ya waumini wao, kwa pamoja wamejikatia tiketi za kwenda Jehanum kwani kwa chuki waliyonayo, wamekwisha kuhesabiwa pamoja na wauaji!!!

    Tukirudi ktk siasa, walichokifanya ukawa ni sawa na mtu aliyepofushwa macho kwa tamaa zake, na akaishia ktk kujidhalilisha! Lakini mara zote mwenye kujidhalilisha huwa ni mtu mwenye kuujali utu wake, asiye na utu huwa hajui hata kama anadhalilika; yaani mtu asiye na integrity hutafsirika kama “a mobile personality” yaani hana conviction; ndio hao ukawa!!!

    Najua ni vigumu kueleweka kwa upofu walionao, lakini ni jambo la kushangaza sana, hili kundi ambalo ukawa ime surrender kwao lina focus yenye msingi wa ccm, walichotofautiana ni nani apewe madaraka tu, na ukawa kwa kumkabidhi mgeni kuwaongoza maana yake ni kundi la wahuni wasio na sera yoyote zaidi ya kuishutumu ccm; ninaamini hapa ndipo walipokutania!!!

    Ama kweli ukishangaa ya Musa,….!!!

  6. James,

    Kumbuka hii ni strictly gospel, sjaona biblica stand yoyote kwenye makala yako, zaidi ya kuonyesha tu kwamba wewe una chuki na Lowasa.

    Tunatakiwa kufika mahali tukajua game ya siasa ikoje, kama ambvyo wengi tunajua game ya mpira wa mguu.

    Kwenye soka kuna kanuni moja kwamba adui yako akikupigilia mpira kwa makusudi kisha huo mpira ukatoka nje, wewe ndo unahesabika umeutoa, japo si wewe uliyeupiga.

    Si ajabu nikikutaka usema uthibitisho wa ufisadi na utajiri wa Lowasa ukachemka, au ukaleta ushahidi wa uliokuwa ukisemwa wanasiasa.

    Ivi huyu ndugu ni fisadi acording to scriptures au acording to sheria za Tz?
    Je sheria za nchi ndo zinazotupa std za utakatifu wa mtu?

    Ukiwauliza Ukawa waliosema sana kuwa Lowasa ni fisadi, watakwambia ni fisadi kulingana report ya Mwakyembe.
    Lskini hao hao ukiwaambia leo waseme usafi wa Lowasa juu ya Richmond watakwambia ni msafi kutokana na report hiyohiyo ambayo inasema kuwa yeye alipokea agizo toka ngazi ya juu kuwa mkataba usivunjwe.

    Hiyo ndiyo game ya siasa, inatumia sheria za nchi wala si sheria ya Mungu kwenye kuhukumu kama mtu ni fisadi au msafi.

    Shida ya watu wengi mlishashikilia tu ile sheria iliyomhukumu kuwa ni fisadi, lakini hamtaki kuitumia sasa sheria inayomthibitisha kwamba si fisadi.

    Alipokuwa ccm wengi tuliamini kuwa anatumia hela kuwapa watu ili wajitokeze kwenye misafara yake. Cha ajabu hata huku ambako tunaamini hawagawagi hela nyomi yake imekuwa kubwa kuliko akiwa ccm jana wakati anachukua form ya kugombea ofisi za NEC.

    Daudi alilala na mke wa mtu, akaja akàmuua mume wa huyo mwanamke, lakini aliendelea kuwa mfalme na Mungu kumnena kuw ni mtu aliyeupendeza sana moyo wake(Mungu).

    Usihukumu usije ukahukumiwa

    Kuna kila dalili kuwa jamaa anaweza akawa Rais mwaka huu.

    Let’s wait and see

  7. Well… Well unajua bongo ikotofauti sana na nchi zingine wabongo tunapenda kuonekana wajuaji sana na ndo moja ya kitu kinachotugarimu. Kifupi tupo kama bendera unako elekea upepo… Tusione kichaka unajua Lowassa alikuwa CCM kwa takribani miaka 40 lakini akiwa ndani ya ccm alisha wahi kumtaja fisadi yeyote? Kwa nini. Sawa ye sifisadi kama anavodai kwani ndani ya ccm mafisadi hawapo? Je aliwataja hata mara moja ndugu yangu amka watu kama hawa hawanajipya zaidi ya kutengeneza njia za mpasuko tanzania wapate mianya ya kuhujum hii nchi.

    Hakuna tajiri yeyote duniani mwenye nia ya kweli ya kumkomboa maskini zaidi ya kufikiria kumtumia kwa maendeleo yake .. Kifo cha nzige ni furaha ya kunguru. Ipo siku amani itakapo kata bongo nifuraha ya wanasiasa.

    Yalipo tokea machafuko Burundi hatuja sikia kifo hata cha mtoto moja wa mwana siasa. Ilipo ingia kwenye machafuko Libya hatuja ona mataifa ya magharibi kuwasaidia zaidi ya biashara za magendo ya silaha wao wapate nema ya madini na mafuta. Sijui utajisikiaje baba yako asipo kujali mtoto wa kambo bali aanze kukutafuta baada ya yule aliye mwona ni mwanae wa haki kufa ndo kukutafuta wa kambo sijui utamwelewaje.

    Well, kwa mtizamo wangu Lowasa ameutambua upinzani baada ya kumwagwa CCM ila upinzani nao kwa akili finyu wakawatoa wadau wao wa damu tena waanzilishi na kumpokea adui yao sidhani kama Lowasa hatashindwa kuwarudisha wakoloni in future ama kweli stahajabu ya musa yaone ya firauni. Imani potofu inawasumbua ukawa na uchu wa madaraka ndo maana wanahaha kama umbwa wenye kiu yote wachukue nchi wagawane dhidi yao kheri msomi uliye amua mapema kujitoa katika damu watakayo mwaga wa tz prof. Ibrahim Lipumba leo unaonekana msalit ila kivumbi kinakuja CHADEMA inashindwa kujikomboa yenyewe itawakomboaje wengine?.

    Kwa leo ni hayo tu yoyote anaweza kuiongoza nchi ila ahadi za uongo ndo kero yetu wa Tz kama ni njaa au uonekane na we ni prezda unasema tu … Lowasa sikuungi mkono una haha mno

  8. IKIWA LOWASA AMA MWINGINE YEYOTE BALI MTANZANIA MZALENDO AFAA KUWA RAISI WA TZ.TUSIWEMASHABIKI WASI-FAIDA.MITHALI 17:15.

  9. TUOMBEE NCHI YETU IWE NA AMANI NA UPENDO. UWEPO WA NENO LA MWENYEZI MUNGU MIONGONI MWETU NDIO UZIMA WETU WOTE. MIMI, WEWE NA YULE NDIO WENYE MAAMUZI NANI ATAWALE NCHI YETU.

  10. Nami pia ni mtazamaji mzuri sana wa Emmanuel TV, sijawahi kuona Nabii T.B. Joshua akitabiri masuala ya Mheshimiwa E. Lowasa. Nadhani wapendwa, tuvute subira, lisemwalo lipo kama halipo linakuja. Wakati wa uchaguzi yatupasa kuwa makini, mtu yeyote anafaa awe fisadi, masikini, tajiri, mcha Mungu, Je? anakubalika kwa wananchi?

  11. Mimi ni mtazamaji mzuri wa Emmanuel TV na sijawahi kumuona Nabii Joshua akitabiri chochote kuhusu Mweshimiwa Lowasa sasa sijui maneno haya mnayatoa wapi?

  12. Mimi niseme kitu kimoja tu Lowasa ni mtanzania anazo haki zote kama raia wa nchi hii kugombea nafasi yeyote,mimi na shangaa watu wanasema Lowasa ni fisadi,ameibia wa tanzania, mimi kama mtanzania nasema hivi hakuna mtanzania aliyesafi mbele za Mungu isipokuwa mbele ya nafsi yake mwenyewe ndiyo maana kuna neno TOBA .Tanzania inamhitaji Raisi kama Lowasa kwa kipindi hiki na hata chama cha CCM chenyewe, nikwamba ni Lowasa pekee anambavu za kukabiliana na makundi makubwa haya yanayo kitesa chama chetu kama akiungwa mkono la Rais wetu, nikiongozi bora sana sana,Msidanganyik jamii inampenda Lowasa kuliko wengi hachafuki kwa maneno ya majukwaani watu wana-reference ya utendaji wake.Naamini hata Raisi wetu anamwamini Lowasa kwa utendaji wake msiangalie mabaya tuu angalia mazuri pia.

    TUHUMA ZAKE HAZILINGANI NA UBORA WAKE

    TUMWOMBEE UZIMA TUU.

    Sosy

  13. haya bhaaaana hayo yote yaliyosemwa let us weit mpaka hiyo2015 TUTAJUA MBIVU NA MBICHI BWANA.

  14. Kusema ukweli kuhusu uraisi wa 2015 ni kigugumizi ambacho ata mimi kimenichanganya akili nashindwa kuwaelewa watanzania! Wengine wanasema Mcha Mungu ndiye atakuwa raisi wa nchi ya Tz mwaka 2015 na tunaona Lowasa saizi kampokea Mungu kuwa ndiye mkombozi wa maisha yake ,lakini pia tunajua kuwa Lowasa ni wa CCM na kwa saizi watanzania wengi wameichukia CCM na hatimaye kuipa majina mengi mfano: Chama Cha Mafisadi, Chukua Chako Mapema, Chama Cha Majambazi, n.k na majina yote haya aliyesababisha sana ni Mh. Lowasa, Asa Mh.Lowasa atatumia nguvu gani kuwafanya watanzania wamuamini na wakati watanzania wengi wamekikimbia Chama Cha Mapinduzi kwa sababu ya ufisadi ambapo anayetajwa sana ni Mh. Lowasa? Pia upande wa pili kuhusu CHADEMA kama watu walivyosema kuwa raisi wa 2015 ni lazima awe Mcha Mungu na saizi watanzania wanaamini kuwa CHADEMA ndiyo itakayochukua nchi , je kwenye chama cha CHADEMA kuna Mcha Mungu au Dr. Willbroad Slaa ni Mcha Mungu? Mi ninachoamini ni kwamba swala la uongozi hasa uraisi anayepanga ni Mungu, ijapokuwa tutafurahi sana endapo atakaye kuwa raisi wa 2015 ni Mcha Mungu kwa sababu atajitahidi kuilekebisha nchi kimwili na kiroho, Maana mbali na serikali yetu kuchafuka sana lakini pia saizi ata makanisa ya siku izi ni makanisa jina lakini ndani yake ni uchafu mtupu mbele za Mungu, Watumishi wa Mungu wanatumia nguvu za giza makanisani nia na madhumuni kujipatia fedha na sio kumtumikia Mungu, ata huyo Mcha Mungu sijui atatokea dhehebu lipi? Saizi Lowasa aliiba fedha serikalini na anaenda kuchezea alambee makanisani na anaambiwa amebarikiwa! Fedha ambazo zilitakiwa kwa ajili ya umeme wa Tz, mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, mafao ya wafanyakazi, kulekebishia miundo mbinu ya Tanzania n.k , fedha zote hizo kachukua mtu 1 na wenzie wachache alafu anaenda kucheza alambee makanisani anaambiwa amebarikiwa! Ivi kweli watanzania tuna akili timamu?

  15. MIMI namuunga mkono Lowassa kwani anarejesha alichokuwa amekichukua kwa Watanzania na asiporejesha tunajua haendi nazo mbinguni ataziacha hapa hapa kwakuwa hakuna ajuaye nani atafika mbinguni na nani hafiki huko ila naweza sema kuwa anawajibika kwa alichokifanya alipopewa majukumu makubwa katika nchi.
    Alichokifanya alipopewa nafasi ya kuwa waziri mkuu hakutosheka anataka apewe na urais ili auze nchi ya TANZANIA KABISA, mimi nilimsikia alipofika nchini toka nje hivi karibuni akiongea mbele ya runinga kwa kujiamini kuwa NIMEKUJA NIKO MZIMA WA AFYA, NIKO TAYARI KUPAMBANA akimaanisha uchaguzi wa Arumeru kwa mkwewe lakini matokeo yake chama chake kikapoteza jimbo kwa sababu ya DHAMBI aliyowatendea Watanzania miaka minne iliyopita.
    TUSIKUBALI KUONGOZWA TENA NA ANAYEUTAKA URAIS KAMA ANATAKA KUWA WA KWANZA DARASANI.

  16. Utabiri wowote ambai TB Joshua huwa anatoa, huwa upo kwenye mitandao yake miwili. Kama huu haupo basi ni feki. Maana imeshatokea watu wakatumia upako wa TB Joshua kuzua jambo, ila TB Joshua anasisitiza kuwa yote anayotoa kama unabii yapo katika tovuti zake. Kwahiyo siwezi sema kama unabii huu wa kweli ama la, maana sijapata muda wa kwenda kuangalia tovuti hizo. http://www.SCOAN.org na http://www.emmanuel.tv

    Mbarikiwe nyote….

  17. Naona kuna watu wana roho ya Yohana,kwan Mungu alipomtuma Ninawi hakwenda sababu yake aliona hawawezi kutubu,na ndivyo watu tunavyomuona Lowassa,lakini tunatakiwa kufahamu bora alikimbilia kwenye nyumba ya Mungu iwe kwa unafiki au kweli,sisi tukipata matatizo tunakimbilia wapi?tukumbuke njia za Mungu si njia zetu,PAULO MTUME hapo awali aliitwa Sauli alikuwa muuaji aliyeliudhi la kanisa la Mungu lakini maisha yake yalibadilika alipokutana na Yesu,naomba nieleweke kuwa siongelei urais wa Lowasa bali kidole anachonyooshewa kwa kwenda kwake kanisani,KAMA WATOTO WA MUNGU TUENDELEE KUMUOMBA MUNGU ATUPE MATAIFA KUWA URITHI SAWA SAWA NA NENO LAKE (ZABURI 2:8)

  18. SHIKA NENO/ TENDA NENO UKIFANIKIWA HAPA UTA WIN MUNGU AMEMLETA NABII NDANI YA TAIFA HILI LA TANZANIA LAKINI BADO HAMJAJUA KWASABABU MNATAKA ISHARA NA MIUJIZA HIZO ZITAFANYIKA LAKINI KWA UTARATIBU WA KIUNGU NA SI RAHISI KAMA MTAKAVYO NYINYI NI LAZIMA UPITE KWENYE KIKAANGO CHA MUNGU MWNYEWE NYIE MNATAKA MTEREMKO, MNANDELEA KUZULUMU, ZINAA, UFISADI, UBAYA WOTE MNAO NYIE. MUNGU HAWEZI KUKUPA UNAYOYATAKA BILA KUJITAKASA NA KUTENGNEZA NJIA ZAKO, NA NINATAKA MJUE KUWA NABII TUNA NDANI YA TAIFA HILI SASA HIVI NA HII NCHI HAITAONGOZWA NA LOWASSA, ITAONGOZWA NA NABII WA BWANA AMBAE ATANENA YA BWANA NA SI YA KWAKE NA ILI UWE CHINI YA NABII LAZIMA UOKOKE WOKOVU WA KWELI NA SIO ULOKOLE, SO WATCH OUT. KINYUME NA HAPO UTAKUFA BASI.

    ESTA H. ELIYA

  19. NI MPANGO WA MUNGU KWELI KLA TAIFA LIWE NA KIONGOZI ANAYEMPNDA MUNGU JAPO JAPO NI WATU WACHACHE WANAO JUA HILO,HIVYO BASI KAMA WATANZANIA YATUPASA KUWAUNGA MKONO VIONGOZI KAMA HAO AMBAO WAMEONA WAZI KUWA MUNGU NI KIMBILIO LAO,BIG UP SANA EDU LOWASA

  20. HAKUNA MAMLAKA,MADARAKA AU FALME ISIYOTOKA KWA MUNGU,HATA ALIYEMHUKUMU YESU,ALIJULISHWA KUWA U-BOSS WAKE ALIOKUWANAO WAKATI HUO,ALIUPATA KWA MUNGU! MUNGU, huchagua kiongozi kwa sababu zake si kwa sababu yako na yangu,jifunze kwa ISLAELI na SAULI-Mfalme wao wa kwanza…ilikuwaje jiulize,kwanini akawa mfalme wa Islaeli,soma kwa makini maandiko.Jiulize kama mamlaka ya kiutawala huletwa kwa ajili ya kanisa au la, jiulize! KAMA IPO IPO TU, LOWASA GOMBEA UKIJISIKIA KUFANYA HIVYO,UNAHAKI ZOTE KAMA RAIA KAKA! Ndiyo maana ukafanywa Mtu na kukubaliwa kumiliki yale yote uliyonayo,zaidi ya yote uliumbwa utawale- achana na waoga wasiojitambua kuwa waliumbwa watawale! Nani anajua pengine utawala wako ni kutawala Taifa hili ili kanisa “linyooke”?! UKIONA VIPI GOMBEA TU,KURA ZIPO tu ili mladi umekusudiwa na mtoa UTAWALA-Waliopo madarakani Duniani kote Wanausafi kukuzidi kwa lipi?! .

  21. Ni sawa tu Kama ametabiriwa kuwa rais.Tatizo ni kwamba sina imani na utabiri wake.Hii ni kwa sababu alitabiri kwa kuwa Lowasa alienda kanisani kwake kuombewa.Nabii hutabiri mambo yajayo bila ushawishi wowote,aitha kwa kutembelewa au kwa kuhitajika maombi yake.HATA SIASA HIZI ZA UOVU NI ZA SHETANI WALA MUNGU HABARIKIWI NAZO.Tangu kanisa la kweli la Bwana Yesu lizaliwe,siasa ilikuwa adui wa kanisa.Hivyo mtazamo wangu ni kuwa awe LOWASA au KIKWETE au SITTA au Dr.SLAA au yeyote yule, hakuna mwenye siasa ya kumpendeza MUNGU.Tunatarajia ufalme wetu wa haki hivi karibuni wenye siasa ya kweli ambayo haki hukaa ndani yake.

  22. Kutoka korogwe kwenye kijiwe cha kahawa kwa mzee Ally. Wazee kwa vijana wameonyesha kumpenda sana Mh. Edward Lowasa. Vijan wanaamini imefika wakati tunamhitaji raisi mwenye utashi na ubabe kama E. Lowasa. Hakuna ushahidi wowote kama edward LOWASA ni fisadi, ni maneno ya kisiasa sasa tunasema basi, Lowasa chukua fomu na ugombee Uraisi. Tulikuona utendaji wako kama waziri mkuu, nakumbuka hapa Korogwe Kuna shule ya Sekondari Chief Kimweri ilijengwa Usiku kwa usiku wakiofia ujio wa Mh. Lowasa. Tunakuombea lowasa uchukue nchi hii, na mambo yawe safi.

  23. Lazaro,

    Naomaba niwajulishe tu kuwa anaye wafahamu binadamu vizuri ni Mungu. Mahusiaano ya mtu na Mungu wake yasiingiliwe. biblia inasema hivi, hukana hata mmoja aliye safi isipokuwa yeye Mungu tu. katika wale wanaojidai ni makamanda wa vita dhidi ya ufisida wafikirie matendo yao pale ambapo mtu hawaoni, watuambie usafi wao, na unafiki wao. Mungu, kama ameamua jambo, amepanga lazima liwe hata shetani apinge litakuwa tuu.

  24. USIHUKUMU USIJE UKAHUKUMIWA….
    Yesu alisema ” Asiye na dhambi awe wa kwanza kumtupia jiwe…..”
    “Ondoa kwanza boriti kwenye jicho lako……”
    Paulo akasema ” Ajidhaniae amesimama na aangalie asianguke…”
    umeshawai kujiuliza kama wewe si fisadi? Je unalipa kodi sahihi bila kuchakachua?
    Je unafika kazini kwa muda unaotakiwa na kufanya kazi kwa masaa yanayotakiwa?
    mfugaji unayeuza maziwa ni kweli watuuzia maziwa bila kuongeza maji?
    asali mnayotuuzia haijachakachuliwa? Mbona hata nyie mwawaibia wananchi? au kwavile waona ni kidogo sana?
    wewe unayeiibia serikali nusu saa, au shilingi chache za kodi, wewe unayewaibia wananchi kwa kuwauzia bidhaa zilizochakachuliwa n.k na wewe pia ni Fisadi unahitaji rehema za Mungu tu Mwizi ni mwizi tu hakuna wizi mkubwa wala Mdogo.
    Hakuna aliye mkamilifu katika dunia hii, sote twahitaji rehema za Mungu na neema yake kutuwezesha.
    Naungana na wewe kakangu Osiah Mwasulama…
    Lowasa Kagombee 2015

  25. Lowasa akiamukugombea urais 2015 ni vizuri tu kwani ni atakuwa ametumia demokrasia ya kweli.
    Nadhani watanzania si jambo zuri kuzungumzia mapungufu ya mtu la msingi ni kuona uwezekano wa huyu mtu kusimamia maamuzi nina mifano hai ya maamuzi aliyotoa mheshimiwa Lowasa na kuyasimamia mfano madawati mashuleni nk hapakuwa na uzembe katika hilo. Kama Yesu alikufa msalabai kwa ajili ya wote na Lowasa alijiuzulu kwa ajili ya makosa ya wengi kwa masilahi ya umma. Dhambi hiyo imekwisa samehewa jamani tuwe wakristo tazama imani ya mapendo.

    Lowasa nenda kagombee 2015

  26. Nadhani iko haja ya kuruhusu hukumu ya Mungu ipite kwa kila aliefanya ufisadi dhidi ya nchi yetu,tena kwa manyangumi kama akina Lowasa,Rostam,Chenge pamoja na rais anaepaka watu mafuta kwa mgongo wa chupa watoweshwe madarakani hata ikiwezekana kwa kushinikizwa.Hivi tujifunze kwa Misri walioamua na wamefanikisha adhma yao natena tutambue NO WINNER WITHOUT FIGHT,wananchi tuamke jamani.

  27. Namalizia kwa kusema watumishi wa Mungu imetosha kuishi mijini kwani 80% ya watanzania wanaishi vijijini wakiishi kiukulima usiolipa wanahitaji faraja ya neno la Mungu,inazipongeza huduma zilizopenya hadi vijijini nikizitaja chache Full Gospel,Efatha,Siloam na huduma mpya iliyoanza kwa kasi ya kwenda vijijini huduma ya VHM Pastor Mitimingi

  28. Mimi naomba kuwarudia wapakwa mafuta wetu Mitume ,Waalimu mpaka viongozi wa dini,Yesu wakati anachagua mitume wake na hao mitume walikuwa na kazi zao kama akina petro walikuwa wavuvi wazuri lakini Yesu aliwaambia mitume wateule wamfuate yeye kumsaidia kaitika kuwasaidia watu kuokaka na kuwa waamini na mtume paulo katika 1kor 14;1 anawasihii sana waumini watake sana kuhutubu Je Mitume,Manabii,Maaskofu,wainjilisti,wachungaji na waalimu ndivyo mnavyo hubiri ,ukisoma injili yote ya Yesu tunayemwamini kama Bwana na Mokozi wa maisha yetu ametusihi sana tubebe misalaba yetu na kumfuata Yeye na tuishi kwa jinsi anavyotaka yeye tuishi hasa kuhutubu na sio kufurahia kuwa na ndege,meli,Hammer,visiwa,maghorofa,utitiri wa suti ndio maana matajiri wanapokuja makanisani viongozi wa dini wengi wanakenua meno wakizitamani pochi za watu hao badala ya kuwakaribisha na kuwaelekeza jinsi gani wanavyoweza kutumia mali zao kutangaza kazi ya Mungu ambayo ina thamani kulika hata urais wa nchi hata ufalme.Mungu aturehemu Amen

  29. Mheshimiwa Mbunge Lowasa amejikuta akiwa kafara ya onyo iliyokuwa ikitolewa na Muasisi wa Taifa ili Nyerere.Rais wa kwanza Nyerere alipiga vita ubepari,ukabaila na ubwanyenye kwa zama zile alikuwa sahihi kwa kuwa Taifa lilihitaji kuwa na umoja na kuvunja ukabila na kuwa sawa kijamii yaani maisha ya ujamaa,bahati mbaya waafrika kiasilia tunatofautiana utu,uchapakazi kwa hiyo ujamaa ulishindikana kutokana na wengi kutokuwa na utu na uvivu na kilichopatikana kwa nguvu za ujamaa kililiwa zaidi na viongozi wananchi wengi wakakata tamaa. Ubepari ni nguvu ya mtaji binafsi kwa faida binafsi. Maisha ya sasa ubepari haukwepeki kinachotakiwa ni kutafuta njia dhahiri za kuchunguza vyanzo vya mitaji ya watu. Haipingiki Lowasa ni bepari kinachotakiwa ni kuchunguza mtaji wake aliupata wapi? Inasadikika Nyerere aliwahi kumuuliza Lowasa kuhusu utajiri wake na inasemekana alishindwa jinsi ya kumshughulikia zaidi ya kulikata jina lake kugombea uraisi mwaka 1995. Sasa Nyerere hayupo na Lowasa bado anautaka Urais nani wa kumzuia? Watu wa Mungu tuombe sana kuhusu uhalisia wa maisha ya sasa tunatoka kwenye ujamaa na tunaingia kwenye ubepari je ubepari sio ndio makanisa yanahubiri sana kuhusu mibaraka. Ndio maana Lowasa ameenda mpaka kwa Joshua, kwa hiyo makanisa yanahubiri ubepari inavyoonyesha serikali bado inataka ujamaa.

  30. Wanablog,

    Labda kama muendelezo wa kila ambacho nimepost hapo juu, Wakristo wengi tumepiga kelele kuhusu ufisadi katika taifa letu, kwa kifupi kama raia wa taifa hili tuna haki kabisa ya kufanya hivyo, lakini naona tunasahau kabisa kuwa inawezakana ufisadi huu unaweza kutoa picha hata kama si ya hakika kuhusu kanisa la Mungu Tanzania.

    Hao tunaowatuhumu kwa ufisadi ndi hao hao tunawaoita kuzindua album na matamasha ya muziki wa Injili na kutufungulia majengo ya makanisa, Kiu ya kutafuta mali na uwezo wa madaraka na kuonekana katika jamii kunakowasukuma mafisadi ndio pia imekuwa ni injini inayowasukuma watu wa Mungu!

    Yesu alisema wazi toa kwanza kibanzi katika jicho lako ndio utaweza kutoa boriti kwenye jicho la mwenzio! Nadhani umefika wakati wa Kanisa kukemea maovu yaliyomo ndani ya kanisa KWANZA! Waumini wengi wanakufa ganzi kuonyesha maovu yanayofanyika katika nyumba ya Mungu! ila tumekuwa wepesi kuonyesha vidole kwa kwa Akina Lowassa, Rostam na akina Chenge…..lakini inapofika kwetu tunapata kigugumizi!

    Mbona tunajua wazi wachungaji na wanaojiita watumishi miongoni mwetu ambao wamejilimbizia mali na utajiri kana Kwamba Biblia zao hazina neno KIASI! au hata kutambua hapa Ulimwenguni tunapita tu!

    Tumeona watu kwa kivuli cha kusaidia yatima na wenye shida wakitumia kama daraja au mtaji wa kuchuma mali! Tumeona watu wa Mungu wakiwa mimbarini kwa kutumia tafsiri potofu ya kuwa Paulo alikiwa ni mtengeneza mahema wakitumia Pesa ya mimbarini kufungua biashara mbali mbali! lengo ni kuzungusha pesha ili kupata “faida” na kutumia kueneza Injili! Mungu hadhihakiwi! Pesa chafu haziwezi kueneza Injili! Kanisa la Kwanza lilieneza Injli kwa uweza wa Roho Mtakatifu na wala sio fedha! hUWEZI KABISA UKAZUNGUSHA FEDHA ZILIZOTOLEWA KWA KAZI YA MUNGU…..KATIKA BIASHARA UKATEGEMEA BWANA ATABARIKI FEDHA HIZO……HII NI KUTAFUTA LAANA NA HUKUMU YA BWANA!

    Hivyo kabla ya kuanza kunyoosha vidole nje ya kusanyiko la Mungu……hebu tukumbuke kuwa hukumu itaanza kwanza katika nyumba ya Mungu…..! Na Mungu hadhihakiwi…….na tunachokipanda ndio tutakachovuna……..! Kama tunataka uamsho wa Uwepo wa Mungu katika taifa letu ambalo ndilo litakaloondoa ufisadi……..basi inabidi tujitakase kwanza sisi wenyewe……..ili NURU YETU IPATE KUANGAZA KATIKA JAMII!

  31. JMW,

    Naungana nawe kwa hoja yako, ila kumbuka tu Ufisadi Tanzania ni dhambi iliyolilemea taifa lote! Hayo tunayayona kwa wanasiasa ni picha halisi ya jamii yote katika Tanzania ndani ya ulingo wa siasa na nje hata mimbari! Ili kila jiwe lazima lipanguliwe kuuondoa ufisadi ina maana kila eneo katika taifa hili!

    Na kwangu mimi ufisadi kwa kutumia Biblia ndio ufisadi mkubwa kupindukia! Wachungaji wameingiza magari kukwepa misamaha ya kodi kwa shughuli zao binafsi! Pesa za waumini zinatumika kununua magari ya thamani na ni wengi mno Watumishi wanajitarisha kwa kusema wanasaidia yatima na masikini kumbe ni janja tu kupata misaada toka nje na kuizungusha na kufanyia biashara na na kujitajirisha! Kwangu mimi ufisadi huu ni mkubwa kuliko anaotuhumiwa Lowassa na kundi lake!

    Ufisadi wa Tanzania unataka uamsho wa Kiroho na Toba ya kweli ili taifa limgeukie Mungu

  32. Wapendwa, Lowassa kaenda kw aTB Joshua kama mtu mwingine yeyote anavyoweza kufanya. Kwamba kaenda kwa sababu za kujisafisha kisiasa au la, muda pengine utathibitisha kuwa hoja hiyo ni ya kweli au la. Na kama kaenda kwa nia ya kusogea karibu na Mungu, Mungu mwenyewe na amwongoze katika harakati hizo.

    Tukimzungumzia Lowassa kwa mtazamo wa kisiasa, hii nchi ina mambo mengi sana ambayo wengi wetu hawayafahamu.

    Mmeshawahi kujiuliza ujasiri ambao Lowassa anaripotiwa kuwa nao, kuwa hayuko tayari kung’oka kwenye uongozi wa CCM kwa sababu ya tuhuma za Richmond, anaupata wapi? Mimi nikifikiri kwa haraka haraka, naamini sababu ni kwamba hayo aliyoyafanya kwenye sakata ya Richmond hakuyafanya mwenyewe – wapo vigogo wengine ambao wengine wao bado wako serikalini na wana nafasi kubwa sana tu hata leo, ambao walihusika.

    Point yangu kusema hivi si kumtetea, lakini ni kusema kuwa kama nia kweli ni kupambana na ufisadi, basi kusiachwe mawe mengine yasalie juu ya mawe — every stone should be turned upside down.

  33. Nam,

    Nadhani si jambo zuri kuzungumzia mapungufu ya mtu la msingi ni kuona uwezekano wa huyu mtu kusimamia maamuzi, kama Lowasa akiamukugombea urais 2015 ni vizuri tu. nani ana ukweli kwamba hayo anayosemwa vibaya yote ni ya ukweli? Yesu alikufa kwa ajili ya wote na Lowasa alijiuzulu kwa ajili ya makosa ya wengi wakiwamo viongozi wenzake kwa masilahi ya umma. sasa dhambi imesamehewa kuna haja gani ya kukumbuka hayo?

    Lowasa nenda kagombee 2015 ,

    kibona 0754800337

  34. Napenda kuungana na wale wanaosema kuwa kama ndugu Lowasa kafanya toba ya kumrudia Muumba wake hilo ni jambo la furaha mno na hata mbinguni hufurahia jambo hilo na kila kitu ndani ya Kristo hufanyika upya…….ya kale yamepita na tazama yamekuwa mapya!

    Lakini inapokuja utabiri wa kuwa yeye ndio Raisi wa nchi yetu hapo baadaye hapo napata kigugumizi…..maana mimbarini Tanzania kumetoa matamko mengi sana…….mara huyu ni chaguo la Mungu…….mara Bwana amesema CCM si chaguo lake……na hata kama utabiri unasema kiongozi wa taifa hili mwaka 2015 ni LAZIMA awe mcha Mungu…….je ni huyu Bwana Lowasa? Hakuna wacha Mungu wengine katika taifa letu?

    Mimi naamini mwelekeo wa taifa letu huko mbeleni hautegemei kuwa na viongozi wacha Mungu madarakani tu! Ni zaidi ya hapo! Uvuguvugu na ukengeufu ndani ya makanisa leo pamoja na mafundisho potofu unaweza kuondolewa na Kiongozi mcha Mungu aliyeko kileleni katika faifa?

    Hebu tufunguke macho ya rohoni ili kutambua ni kwa vipi tunaweza kuirudisha hofu ya Mungu katika nyumba ya Mungu (Kanisa) Tanzania ili kuweza kurudisha hofu ya Mungu katika taifa letu!

    Uwepo wa Mungu katika taifa haurudishwi tu na kuwa na Kiongozi mcha Mungu……..hurudishwa na toba ya kweli na kanisa linaposimama katika nafasi yake kama Nuru ya Ulimwengu……..au Taa iliyowekwa Kilimani…….!

    Mungu na aturehemu!

  35. Ndg john,

    Mimi Nimevutiwa na maoni yako hasa ulipoandika yale ambayo UTABIRI unaonyesha kuhusu kiongozi wa Tz wa 2015.

    Samahani, kwa kuwa hapa ni mahali pa kujifunza Naomba kufahamu HUO UTABIRI KUHUSU KIONGOZI WA TZ WA 2015 ni utabiri UPI na kutoka WAPI?

    Natanguliza shukurani zangu.

  36. Nafikiri walitaka kusikia Lowasa kaenda kwa toboa tobo ili waweze kumsakama zaidi. Utabiri unaonyesha kiongozi wa 2015 atakuwa mcha Mungu ambaye ametosheka na mali alizokuwa nazo. maandiko yanasema ukisamehewa dhambi zako hata zile ulizozitenda jana pia zimesamehewa!!!!!!!!!! Sioni la ajabu kwa Lowasa kutubu kumrudia Mungu wake na kupewa uongozi wa njiiiiiiiii. Endeleza harakati zako za kutaka uongozi wa nchi tupo nawe na Bwana akutangulie. Ufanisi wako ulipokuwa Waziri Mkuu kwa muda mfupi umeonekana

  37. hivi dhambi ya ufisadi haisameheki? Imeandikwa kwa chuma? Mbona watu tunajifanya sisi wasafi sana? Badala ya kupongeza kuwa lowasa amechagua njia sahihi ya kumrudia Mungu mnamsema tena mlitaka aende kwa waganga kwanza kabla ya hapo lowasa anaonyesha ni mnyenyekevu alikubali kujiuzuru mimi si mwanasiasa wala sipendi siasa ila kinachoniudhi ni vile watu kuingilia kazi za Mungu mara nyingi nasoma humu akiokoka mtu maarufu tu angalia comments za watu yaani hawaamini sijui ya Mungu aachiwe Mungu kama mtu anafanya mzaha muda utafika kila kitu kitawekwa peupe

  38. Jamani msipende kufatilia mahisha ya nyuma ya mtu, Siku moja yesu aliwaambia wanafunzi wake kuaSIKUHIYO MTA WAONA MAKAHABA WA KIWA TANGULIA sasa mnapo jaji mahisha yamtu alieamua kumkimbilia MFALME YESU mnakua Mme sahahu alio ya sema MWNAUME YESU?je, angekua ka wakimbilia wa ganga wa kienyeji mge semaje ?
    hiwe ni mbinu ya ki siasa au nikweli mimi sijuhi najua mungu nikweli nakila amkimbiliae hauache uwovu
    asante

  39. Hivi hiyo mitambo inayosemekana aliileta nchini ikiwa mibovu, si hiyohiyo mitambo imenunuliwa na kampuni ya wamarekani SYMBION? Wana wa MUNGU tuwe makini tutakuja kuhukumiwa kwa maneno yetu. Nchi hii kuna mengi yanayoendelea, kumbuka pia kuna zile ajenda za Abuja za mwaka 1987 ambazo kuna watu wamekusudia kuzitekeleza kwa juhudi zao zote na ktk ajenda hizo mojawapo ni nafasi za juu serikalini kushikwa na waishimael tuu. Yawezekana wakati mwingine mtu akazushiwa jambo ili aonekane hafai kwa leo la kutimiza zile ajenda. wana wa MUNGU tuwe macho tusichukuliwe na mikumbo. Tuombee taifa letu.

  40. napenda kutoa onyo kwa wale wooote ambao tunapenda kuingilia kazi za Myenyezi Mungu. nani anayemnyooshea kidole Lowasa? Je una uhakika na mahusiano yako na Mungu au unajaribu kufurahisha nafsi yako.
    natumaini Ni wakati wa kila mmoja kujihoji uhusiano wake na mungu na kufanya marekebisho na sio wakati wa kumnyooshea kidole mwingine.
    Kumbuka Yesu Kristo alikuja ulimwengu huu kwa Dhumuni la kuokoa kile kilicho KINYONGE NA SIO KILICHO IMARA.
    TATIZO KANISA LA LEO HUWA LINAPENDA KUJIKWEZA NA KUJIONA NI SAFI, SHIME WAPENDWA NA WANA SG TUEPUKE HIYO DHANA MAANA KUNA HATARI YA KUKOSA MBINGU KWA KUHANGAIKIA MAMBO YASIYO NA MAANA HASA KWA KUHUKUMU WENGINE.
    LOWASA AMEENDA KUMTAFUTA MUNGU KWA TOBA YA KWELI AU UONGO NI LAKE NA MUNGU WAKE MIMI NA WEWE HATUNA MAMLAKA YA KULITAFITI MAANA HATUNA UWEZO WA KUTAMBUA ZAIDI KAMA TUNATAKA KULIFANYA HILO BASI TUTAKUWA WASHIRIKINA WA KUPIGA RAMLI.
    MWACHENI LOWASA NA MUNGU WAKE TAFUTENI KUJISAFISHA KWANZA NYIE WENYEWE.

  41. Jamani mbona Lowasa akionekana Azania front hamsemi? leo kaonekana Kwa tb Joshua Imekuwa gumzo? Mie nadhani huu ni uvivu wa kufikiri.
    ALikwenda rais wa Ghana, mbona hatukusia watu waki-comment? Mungu niwa wote wenye mwili. Mimi, wewe na yule!

  42. Ushauri wangu kwa wana wa Mungu ni kusimama kwenye nafasi zetu sawasawa na kuhakikisha kwa maombi yetu tunakuwa sababisho la amani na utulivu katika taifa letu.
    Kumekuwa na hali ya watu kushabikia baadhi ya mambo yanayoibuliwa na wanasiasa bila hata kutafiti undani wake na chanzo cha kuibuka kwa hoja hiyo, akibuka mwanasiasa akamtaja mtu fulani ni fisadi watu wanabaki kushabikia bila kufanya utafiti,utashangaa unapita mtaani watu wanazungumza kiongozi fulani fisadi mwizi ukiuliza kwa kigezo gani anamwita fisadi au mwizi hajengi hoja akaeleweka.
    Yawezekana kweli lowassa anataka urais 2015 lakini kama yeye hajatangaza kugombea sioni haja ya mtu mwingine kumsemea kwa sababu hatapewa uraisi kwa siri kama ndivyo itafika wakati ataomba kugombea na watanzania watampima kama anakidhi viwango vya kiongozi wanayemtaka kwa wakati huo.

  43. Shalom jamani,
    hivi mtu kama alitenda ubaya kisha ameamua kutubu na kuupokea wokovu au kumtafuta Mungu bado mnamnyooshea kidole tu… mie naona tumuombee ili aweze kukutana kweli na mkono wa Mungu. Simoni mchawi alipoke wokovu na ndani yake alitaka apate ile karama aliyokuwa nayo Petro imfaidie kimwili (auze) lakini alikuta nia yake imejulikana aliogopa na kutubu kiukweli. Kwanini msimfurahie huyu kondoo anaeingia zizini na kumuombea? Mbarikiwe

  44. Jana Ameonekana live akiwa SCOAN Nigeria, lakini sijafanikiwa kusikia kama alipata kuombewa au kuzungumziwz/kutabiriwa lolote na watumishi wa pale. Kama kuna mwenye taarifa atujuze tafadhali.

  45. Wapendwa.
    Sina sababu yoyote ya kumtetea Edward Lowasa ingawa napenda kusaidia kanisa kujiepusha na shutuma za kisiasa zinazoendelea.
    Kwa wale wenye maarifa na hekima hawawezi kumnyooshea kidole Lowasa ama Chenge ama Rostam kutokana na kile kinachoonekana kuwa magwiji wa ufisadi kwani hakuna chombo chochote cha dola ama kiongozi yeyote wa kitaifa amethubutu kuchukua hatua kujenga hoja ya kisheria ili hatua za ziada zichukuliwe kwa hawa tunaowaita mafisadi.
    Pia hakuna hakika yoyote kuwa Lowasa anauhitaji uraisi kama ambavyo wengi tumekuwa tukituhumu.
    Na kama kweli Lowasa,Chenge na Rostam ni mafisaji na wamekuwa wakiifisidi nchi hii basi fisadi mkubwa anapaswa kuwa Raisi kwani kwa muda mrefu wananchi kupitia sauti mbali mbali yaani vyombo vya habari,vyama vya siasa,Kamati maalumu za bunge na hata wanaharakati wamepiga kelele sana kuhusiana na matukio ya ufisadi kwa kipindi kirefu sana lakini viongozi wa serikali wakiwemo marais Mkapa na Kikwete mara zote wamekanusha. Mawaziri wakuu,mawaziri wa wizara mbali mbali,taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa pamoja na tume kadha wa kadha zimeshiriki kusafisha,kufumbia macho ama kufunika uozo huu. Mfano mwepesi ni kesi ya mtu anayeitwa Mahalu ambayo bado ipo mahakamani kwa sasa. Utaona waziri muhusika alishatoa majibu bungeni kuonyesha kuwa hakukuwa na ufisadi katika ununuzi wa nyumba kule Italia lakini miaka michache baadaye Mahalu na wenzake wamefunguliwa kesi ya uhujuma uchumi. Kuna hili sakata la Richmond,nakumbuka mwezi wa kumi mwaka 2006 gazeti la mwananchi lilichapisha habari kufunua ufeki wa Richmond na kuwa si kampuni inayotoka Marekani kama ilivyojitambulisha. Mwandishi alienda mbali zaidi kuufahamisha uma kuwa alipata nafasi ya kumuhoji hata Meya wa jiji la Texas na akamhakikishia kuwa hakuna kampuni jimboni mwake yenye jina hilo inayojishughulisha na biashara ya umeme. Gazeti hili lilitoka muda mchache tu tangu Rais kikwete atoke Marekani ambapo pia alimtembelea Rais wa Marekani wakati huo George Bush aliyekuwa mapumziko kwenye shamba lake la farasi lililopo Texas. Kwa maana kuwa raisi wetu akiwa na wasaidizi wake angeweza kufahamu lolote kuhusiana na mkombozi wa tatizo la umeme kwa wakati huo aitwawye Richmond ambaye anatoka Texas Marekani.
    Sote pia tunafahamu kwa hakika kuhusiana na sakata la rada,ndege ya raisi na mengine kuwa yalipigiwa kelele tangu yalipokuwa kwenye hatua za mapema tena mengine yalikuwa hayajaanza. Matokeo yake nchi imeingia kwenye matatizo makubwa ya upotevu wa rasilimali na uhuru wetu ndipo watu wanapoona umuhimu wa kujivua gamba.
    Kama chama tawala kingepata asilimia 80% ya kura za urais na kama vyama vya upinzani vingepoteza viti vingi suala zima la kujivua gamba lisingekuwepo na Lowasa,Chenge na Rostam wangeendelea kuonekana kuwa makamanda wa chama. Kumbukeni jinsi walivyonadiwa na mtukufu Raisi wakati wa kampeni.
    Wapendwa tueni rohoni ili tupate hekima ya kuisaidia nchi yetu kwa maombi na neno la hekima litokalo kwa Mungu muumba wa mbingu na nchi tuache ushabiki wa kisiasa kwani tunaenda pabaya.
    Sote tunaona kwa macho yetu na kusikia kwa masikio yetu mgawanyiko wa kidini na kidhehebu unaopandwa na viongozi wetu ili kutimiza matakwa yao ya kutawala wao na vizazi vyao na hatuoni hatua za dhati za kupambana na roho hii chafu ya ubaguzi.Leo hii viongozi wanapendwa kwa dini zao,wanashutumiwa kwa sababu wako dini nyingine,wanapata nguvu kwa sababu ya dini zao n.k
    Kwangu mimi Lowasa,Chenge wala Rostam si tatizo bali tatizo ni la kimfumo na ufahamu wetu kuhusiana na hali tuliyofikia hivi sasa. Kama tunahitaji kweli chama tawala kijisafishe kwangu naona wa kwanza kujivua gamba yaani UONGOZI anapaswa kuwa mheshimiwa raisi Kikwete,kisha wengine kama raisi mstaafu,mawaziri wa awamu zote,wabunge wa awamu zote,maafisa usalama na viongozi wa dini wanapaswa kuwajibika kwa kuwaomba radhi watanzania tena kukiri kuwa walitukosea kwa kuacha nchi ielekee huku kubaya na ndipo tuone mabadiliko ya kweli.
    Haya hayatawezekana kama sisi tulioitwa na Mungu kwa kusudi maalumu tutaendelea kushikilia falsafa za wanasiasa ambao wanataka kuendelea kupata heshima zao kwa kuwatosa wenzi wao ambao walifanya kazi kubwa kuwafikisha hapo walipo
    Mungu awabariki sana.

  46. Makala hii ni ya siku nyingi sana, mbinu ambazo watuhumiwa wa ufisadi wamekuwa wakiitumia kujisafisha kwa watanzania katika azma yao kufikia ndoto zao kuusaka urais 2015. Nasi tusitekwe katika website hii kuanza kuchangia, imepitwa na wakati.Lakini hadi hii leo huwa najiuliza huyo Lowasa anahaha kuutafuta urais haja sema ni kwa nini anataka kuwa rais wa Tanzania? hata huyu rafiki yake rais wa sasa sikupata kusikia akisema ni kwa nini alitaka kuwa/amekuwa rais wa Tanzania?

    Ahsante
    Mwalongo, T.M.

Andika maoni yako