Wachungaji Msitangazie washirika dhambi ya mtu mwingine!

“Mchungaji unapotangaza dhambi/makosa ya mtu kwa washirika/waumini kinachotokea ni kwamba yule mtu hata kama ameshatubu kwa Mungu wale washirika watabakia wakimhukumu “fulani alitenda dhambi hii”. Kwa kufanya hivyo watu hao wanabakia na dhambi hiyo hadi siku yao ya kufa. Maana mtu akitubu Mungu humsamehe lakini watu ni vigumu sana kusahau.

Na wewe mtu uliyeokoka, mtu akitenda dhambi achana naye, usiweke dhambi yake moyoni mwako bali songa mbele katika kumwangalia Yesu”

Mwinjilisti Obadia alipokuwa akihubiri katika mkutano wa Injili mjini Arusha tarehe 22, June, 2011.

3 thoughts on “Wachungaji Msitangazie washirika dhambi ya mtu mwingine!

  1. Inabidi watumishi waombe hekimu ya R/Mtakatifu maana watumishi wetu wengi hawana, Mfano mimi ninapokwenda kwa mtumishi wa Mungu na kumweleza shida yangu iwe ya kiroho au kimwili halafu akaniombea ile inapaswa iwe siri kati yangu na yeye, lakini watumishi wengi akishakuhudumia kesho utasikia ndio mahubiri ya siku hiyo ,hapo mtumishi wa Mungu anashindwa kuweka siri, sijasikia hata siku moja Daktari akitoa siri ya mgonjwa wala Mganga wa kienyeji akitoa siri ya mteja wake, kwa walokole kuna shida gani? .Tuwaombeee watushi wetu Mungu awape hekima

  2. Naona mwinjilisti Obadia amekosea maana Biblia haisemi kwamba wachungaji wasitangaze dhambi za watu wengine hadharani. Kuna watu wanafanya dhambi hadharani hivyo wanapaswa kuonywa hadharani maana hiyo itasaidia kondoo wengine kujua kwamba yale maovu yanapingwa na wachungaji. Sasa kama sisi tunaenda kuwahukumu malaika walioasi , si zaidi sana kuwaonya watu ili wawe na hofu ya Mungu na wapone hukumu ijayo?

    Tusipende longolongo ambazo sio Neno la Mungu. Hata kama mtu angekuwa na cheo gani kama hasemi Neno hizo asemazo ni porojo tu na kamwe hatutamsikiliza maana yeye hajatufia msalabani, cheo chake ni cha kidunia tu, BALI NENO LA MUNGU LITASIMAMA MILELE!

  3. Kuna mwingine aliwahi kusema, msinifuate mimi tabia zangu ila fuateni yale ninayoyahubiri. Inabidi kuonya kama mtu haendi vyema ili akatubu baadae aurithi uzima wa milele. Tusipoonyana watu watatawaliwa na viburi vya uzima.

Andika maoni yako