INJILI YA MILELE

 INJILI YA MILELE NI INJILI GANI?

“Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa, akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji’ (Ufunuo wa Yohana 14:6-7)

Kama ambayo maandiko yanasema hapo juu, tunaweza kuona kuwa INJILI YA MILELE ni Injili yenye ujumbe ambao ndani yake uko na maneno makuu matatu mbayo ni:

1.KUMCHA MUNGU

2.KUMTUKUZA MUNGU

3.KUMSUJUDIA MUNGU

“Ni nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako u Mtakatifu; kwa maana mataifa yote watakuja na kusujudu mbele zako; kwa kuwa matendo yako ya haki yamekwisha kufunuliwa. (Ufunuo wa Yohana 15:4).

Huu ndiyo ujumbe mkuu unaoletwa kwa kupitia Injili ya milele. Tofauti na hapo hiyo siyo Injili ya milele ambayo ilikusudiwa na Mungu ihubiriwe kwa wanadamu.

Kwa sabababu ya ukengeufu wa wanadamu, zimetokea aina nyingine za Injili ambazo ndani yake hazina ujumbe uliokusudiwa na Mungu.

 Mtume Paulo anaonya hapa  kuwa:

“Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe. Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe. (Wagalatia 1:8-9)

Maandiko hapo juu yanatuonyesha kuwa kuna baadhi ya Injili ambazo mtu anapokuwa anaihubiri tayari anakuwa ameshajipatia laana kwa sababu Injili hiyo siyo  ya Kristo, Siyo ya Milele! Aina hii ya Injili tunaweza kuiita ni injili ya Laana.

Aina nyingine ya Injili ni Injili ya Tumbo.

“Maana wengi huenenda, ambao nimewaambieni mara nyingi habari zao, na sasa nawaambia hata kwa machozi, kuwa ni adui za msalaba wa Kristo; mwisho wao ni uharibifu, mungu wao ni tumbo, utukufu wao u katika fedheha yao, waniao mambo ya duniani” (Wafilipi 3:18:19)

“Ndugu zangu, nawasihi, waangalieni wale wafanyao fitina na mambo ya kukwaza kinyume cha mafundisho mliyojifunza; mkajiepushe nao. Kwa sababu walio hivyo hawamtumikii Bwana wetu Kristo, bali matumbo yao wenyewe; na kwa maneno laini na ya kujipendekeza waidanganya mioyo ya watu wanyofu. (Warumi 16:17:18)

Aina nyingine ya Injili ni Injili ya Ushawishi.

“Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu,  ili imani yenu isiwe katika hekima ya wanadamu, bali katika nguvu za Mungu. (1Wakorintho 2:4-5)

Aina nyingine ya Injili ni Injili ya HUSUDA NA FITINA

“Wengine wanahubiri habari za Kristo kwa sababu ya husuda na fitina; na wengine kwa nia njema. Hawa wanamhubiri kwa pendo, wakijua ya kuwa nimewekwa ili niitetee Injili; bali wengine wanamhubiri Kristo kwa fitina, wala si kwa moyo mweupe, wakidhani kuongeza dhiki za kufungwa kwangu” (Wafilipi 1:15-17)

Kule mwanzo nilisema kila injili Inazaa wafuasi wake. Tunaweza kuyaona haya katika 1Wakorintho 4:15 isemayo:

“Kwa kuwa ijapokuwa mna waalimu kumi elfu katika Kristo, walakini hamna baba wengi. Maana mimi ndimi niliyewazaa katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili.

Wafuasi wanaozaliwa na Injili wa Milele, au Injili ya Kristo hao nao huendeleza Injili hiyo ya Kristo. Wale wanaozaliwa na Injili tofauti nao huendeleza kile ambacho walizaliwa nacho.

YESU KRISTO yeye alikusudia ihubiriwe Injili ya milele kuwa: Mwanadamu ni wa milele; Mbingu ni ya milele na Moto ni wa milele. Uchaguzi ni binadamu.

Ndiyo maana tunasoma maneno haya:

“Angalia, nimekuwekea leo mbele yako uzima na mema, na mauti na mabaya;  kwa hivi nikuagizavyo leo kumpenda Bwana, Mungu wako, kuenenda katika njia zake, na kushika maagizo yake, na amri zake, na hukumu zake, upate kuwa hai na kuongezeka; Bwana, Mungu wako, apate kukubarikia katika nchi uingiayo kuimiliki. (Kumbukumbu la Torati 30:15-16)

Bwana Yesu aliwaagiza wanafunzi wake wakawafanye mataifa kuwa WANAFUNZI.

Masharti ya mtu kuwa Mwanafunzi ni yapi?

Tunaona haya katika maandiko yafuatayo:

“Makutano mengi walipokuwa wakifuatana naye, aligeuka, akawaambia, Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu”. (Luka 14:25-27)

Wakristo wa kwanza walikuwa wanafunzi.

Wakristo wa kwanza walikuwa wanaitwa WANAFUNZI kwanza kabla ya kuitwa Wakristo.

“hata alipokwisha kumwona akamleta Antiokia. Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hapo Antiokia” (Matendo ya Mitume 11:26)

Walikuwa wanaitwa Wanafunzi Hapo Antiokia wakaamua waitwe ndipo wakaitwa Wakristo. Hakuna Zaidi ya hapo. Katika Ukristo hatuna:

-Mkristo-Mwizi

Mkristo-Mzinzi

Mkristo-Wa dini

Mkristo-Asiyebatizwa

 Mkristo- Asiyemtakatifu

Katika Ufunuo 13:11 tunasoma:

“Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka’

Hapa tunaona mfano wa mwana kondoo, pembe zilikuwa zinaonyesha ni mwana-kondoo, lakini akiongea ni Joka!

Hii inatuonyesha kuwa mtu anaweza kuonekana kama muhubiri wa Injili kwa kuwa anafanana na wahubiri anavyovaa na anavyojiweka muonekano wake. Lakini akiongea anaongea mambo mengine, siyo Injili ya milele!

Tuchukue tahadhari!

Askofu Samuel Imori

VITABU VYA MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU

Askofu Samuel Imori aliyeleta hapa mfululizo wa somo la MSTARI UNAONILIZA KULIKO YOTE KATIKA BIBLIA, kwa msaada wa Mungu, alifanikiwa kukusanya mfululizo huo wa mafundisho na kuyaweka katika Kitabu ambacho kina jina VIKWAZO VYA KUURITHI UZIMA WA MILELE, 1 & 2. Pamoja na kitabu hicho hadi sasa ana vitabu vingine Tisa (9) ambavyo majina yake ni:

1.Kanisa Ni nini?

2.Huduma Tano ndani ya Kanisa

3.Kiongozi Bora

4.Yesu ni Nani?

5. Mtu

6.Silaha anazotumia Shetani kuwaangamiza watu wa Mungu

7. Injili ya Milele

8.Roho Mtakatifu na Kazi zake

9. Tofauti kati ya Agano Jipya na la Agano la Kale.

Kwa sasa vitabu hivi vinapatikana katika duka la vitabu la KIMAHAMA lililoko jijini Arusha kwa bei ya Shilingi 10,000. Pia unaweza kupata vitabu hivi popote ulipo kwa kuwasiliana na Askofu Samuel Imori kwa simu namba +255 765 446611 ambapo mtakubaliana namna ya kukutumia hadi mahali ambapo unaweza kuvichukua kwa urahisi.

Kusoma vitabu kunaongeza maaarifa!

SADAKA YA UKOMBOZI

Mimi natoka Kenya na nimeingia kwa blog hii kusoma na kujifahamisha mengi kuhusiana na wokovu. Nimependezwa sana na somo hili na hata mimi naomba kuuliza swali:


1. Nimesikia wengi wa wachungaji na watumishi wa Mungu wakiitisha Sadaka ya Ukombozi kwa wanaotaka kufanyiwa.

(a).Je! ni halali kutoa sadaka ya ukombozi?


(b).Ni maandiko yapi yanayodhibitisha hayo?

Nitafurahi sana kupata majibu ya maswali yangu.

Elvis Nyale

Tunakutakia Heri ya Mwaka Mpya 2023

Kwa muda wa kama miaka miwili hatukuweza kuwa hapa kutokana na sababu mbalimbali. Lakini kwa neema ya Mungu sasa tumerudi!

Tunakutakia heri kwa mwaka huu wa 2023. Wakaribishe ndugu na marafiki kutembelea blog hii kwa maana sasa iko hewani.

Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote” 2Kor 13:14

Injili Ruksa kuhubiriwa vilabu vya pombe

3137de4f-218b-4125-8a76-506085aaa093

Mkuu wa Mkoa Wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda tarehe 8 mwezi Wa tisa ametoa kibali kwa Watumishi wa Mungu wa Dini zote kuhubiri na kutangaza neno la Mungu kwenye Sehemu za Club, Disko na Kumbi za Starehe ili neno la Mungu lizidi kuenea na kuwafikia watu wote jambo litakalosaidia kujenga jamii inayomjua Mungu.
_
RC Makonda amesema Mtumishi wa Mungu atakapohitaji kuhubiri mziki utazimwa kwa muda wa Nusu saa na baada ya hapo watu wataendelea na starehe zao wakiwa tayari wamepokea Neno la Mungu na kuahidi kuwa Mmiliki wa Club atakaemkatalia Mtumishi Kuhubiri RC Makonda atamwombea Mtumishi huyo na ikibidi atamsindikiza.
_
Hatua hiyo ya RC Makonda imekuja baada ya kubaini uwepo wa Idadi kubwa ya watu kwenye sehemu za starehe na pindi watu hao wakienda Makanisani na Misikitini wanaishia kusinzia na wengine wanakuwa wamechoka kiasi cha kushindwa kulisikiliza kwa ufasaha neno la Mungu.
_
Hayo yote yalijiri wakati akizungumza na Waumini wa Kanisa la Arise and Shine linaloongozwa na Mtumishi wa Mungu Apostle Boniface Mwamposa.