Tunatakiwa kutazama kwa macho ya rohoni! – Kamugisha

Tunatakiwa kutazama kwa macho ya rohoni! – Kamugisha

Wapendwa katika BWANA YESU KRISTO. Ni neema kubwa kutoa sadaka yangu katika blog ya INJILI HALISI.Binafsi sikujua kama kuna siku nitatoa hii sadaka kwa wale wote wenye DHAMIRA YA KUISHI NDANI YA UNYENYEKEVU HALISI yaani unyeyekevu wa YESU (Wafilipi 2:3-4). Lakini Mungu aliye hai anayetangaza mwisho kabla ya mwanzo alijua ya kwamba UJUMBE WAKE  UTATUFANYA TUANZE KUISHI … Continue reading

ZAKA Malipo ya Kabla!

ZAKA Malipo ya Kabla!

  Wapenda kwa jina la Yesu naomba msaada katika kuuliza, nimepewa bahasha kanisani nawatumia picha, Je, Zaka inatolewa kabla ya kupokea mapato au ukishapokea mapato? Mungu awabariki –Paul  

Si dhambi kuoa wake wawili – Magreth

Si dhambi kuoa wake wawili – Magreth

Japo wengi watanishangaa lakini hakuna aliyepigwa na mawe kwa kuoa wake wawili katika biblia. Lakini ukificha na kufanya kimada walikupiga mawe hadi kufa. Biblia haisemi kuwa ni dhambi ukioa wake wawili, lakini kimada ni dhambi kwa kuwa unazini. Mapokeo ya kanisa yanaambia watu ni dhambi kuoa wake wawili na sio kweli. –Magreth

Unamwabudu Mungu kwa ajili ya nani?

Unamwabudu Mungu kwa ajili ya nani?

Mama mchungaji Victoria Osteen ameibua mjadala kwa Wakristo wengi baada ya kuongea maneno yafuatayo hivi karibuni “Unapoabudu (na kumtii) Mungu, hatufanyi hivyo kwa ajili ya Mungu, tunafanya hivyo kwa ajili yetu, kwasababu hicho ndicho kinachomfurahisha Mungu” Kutokana na mtazamo huu, Kwa maoni yako, Unamwabudu Mungu kwa ajili ya nani? Je ni kwa furaha yako? Unapoenda kanisani … Continue reading