Mtume na Nabii Josephat Mwingira asaidia maendeleo mkoa wa Rukwa

Mwingira

Rais Jakaya Kikwete akipokea mchango wa shilingi milioni 10 kutoka kwa kiongozi wa kanisa la Efatha nchini, Mtume na Nabii, Josephat Mwingira katika harambee ya kuchangia Mfuko wa Maendeleo wa Mkoa wa Rukwa iliyoongozwa na Rais kwenye hoteli ya Kilimanjaro- Kempinski jijini Dar May 27, 2009. Zaidi ya shilingi bilioni 1.4 zilichangwa,Katikati ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

22 thoughts on “Mtume na Nabii Josephat Mwingira asaidia maendeleo mkoa wa Rukwa

  1. Pingback: Mwingira wa EFATHA awaita viongozi ya serikali ni washenzi - Page 3

  2. TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD
    MPONDA TAG CHURCH
    +255 (0) 784 341971 – 715 341971 – 767 341971

    C/O ASSEMBLIES OF GOD KONGOWE CHURCH P O BOX 100163 DAR ES SALAAM
    Our ref;ag/mpd/012/2013

    FROM PASTOR THOBIASI MOSHA

    TO BRETHRENS

    REV/PROF/DR/ENG/BRETHRN…………………………………

    Greeting you in the name of Jesus Christ our survivor
    It is great honor to submit our request for the church working tools to you these tools are for the fercitilitation of day to day operations at Mponda village;Mianzini ward ;Temeke district; Dar es salaam

    The village situated along the Indian Ocean strip it has a population of 7316 (in 1463.2 households) people of which 92% are Muslims, 2% pagan and 6% Christians denomination (from 6% Christian who been born again is 1.5% our church members)

    The church in subject is under supervision of Mather church Kongowe Assemblies of God church which ministered by Rev Charles Luoga (his contact mobile +255 784 423077 & +255 753 234448) the ministerial work at Mponda village beginning on 13 September 2009 until 31 December 2012 through in partnership with several good Samaritans we have been able to achieve the following

    1. Purchasing of a piece of land
    2. Construct a Sunday school house which we are currently using for worship service
    3. Buying some equipments such as spiritual song books and few plastic chairs

    We want to share our plan and vision with you for construction of permanent building and we believe that you will cooperate with us in one way or another to the effort of achievement under consideration of the blessing set before us in return to our spiritual calls to spread the Gospel to the society. It’s our hope that you and all will understand our needs and feel free to play part in our attempt to realize our goal
    Philemon 1-12 and 11 Corinthians 9-10-14
    Yours in the service of Jesus Christ
    THOBIASI NICHOLAUSI
    Pastor
    MPONDA ASSEMBLIES OF GOD CHURCH

    ________________________________________

  3. Hongera sana mtume na nabii kazi yako ni njema kwakuchangia maendeleo ya nchi,wewe ni mfano wa kuigwa na watumishi wengine wa mungu na wote ubarikiwe.

  4. MUNGU AZIDI KUKUPA MOYO WA UPENDO WA DHATI KWA KUWATETEA WANYONGE KATIKA MAUBIRI YAKO MALA NYINGI UNAKEMEA UFISADI NA HATA KUOMBA KWA BWANA AWAONDOE MAFISADI KTK HII NCHI MUNGU AKUBARIKI NABII

  5. Mtume na Nabii Josephat Mwingira anastahili kupongezwa kwa moyo wake wa upendo na ukarimu kwa watanzania wenzake.Mimi naamini kwamba hizo pesa za mchango wa Rukwa ni za kwake na wala hazitokani na sadaka.Nahamasika kusema hivyo kwa sababu ya kauli zake anazozitoa mara kwa mara kwamba yeye hagusi hata shilingi za sadaka…jamani huyu mtu amebarikiwa na Mwenyezi Mungu!! Ni wangapi Tanzania hii wana pesa lakini hawana msaada kwa jamii?

  6. SHALOM,
    Naomba namba ya simu pamoja na email address za Mtume na Nabii Josephat Mwingira.

  7. Shalom!

    kwa mujibu wa Neno la Mungu ki msingi na haki ni kila mtumishi anastahili apate na kutumia sehemu ya kumi ya zaka za washirika wa kusanyiko analolihudumia ila yeye anawajibika kutoa sehemu ya kumi ya pato hilo katika uongozi wa juu na sehemu ya kui ya mapato mengineyo nje ya madhabahu hii kwake ndio maongeo na kama pato litakuwa kubwa zaidi ya kiwango cha kima cha kati cha mshahara wa mtumishi wa serekali hapo inabidi pawepo schedule itakayotumika ili asifanye kanisa ndio mtambo wa kumzalishia mali asijefikia kuona kuwa utumishi ni njia sahihi ya kutajirika pia kama uchumi wa kanisa hauendani sambamba na idadi ya watu hapo kuna takiwa alama ya ulizo kwani lengo ni kuwafikia watu na wala sio kuridhika na mapato

    Sijui kwa wale ambao walijipachika vyeo vya uaskofu nafikiri hawana maongozi yanayoweza kuwauliza jambo lolote ndio maana kuna huduma huwa zinakufa na mwenye maono au kubadilika kuwa shirika au kampuni hapa kwetu tanzania hayo ndio mengi
    lamsing watu warudi katika neno la mungu
    asante kwa leo
    mini

    THOBIASI NICHOLAUSI MOSHA
    MCHUNGAJI
    KANISA LA TAG MPONDA

  8. Asante sana KIJANA WA KRISTO. Nilipouliza kama kuna mtu anayempa hilo Jina Mtume ama Nabii nilimaanisha kuwa inakuwaje ama huyo Mtume na Nabii anafikiaje hatua ya kuitwa hivyo? Ni tofauti na tunavyoona waKatoliki wanawataja WENYE HERI NA WATAKATIFU? Ni nani ama inakuwaje mtu anapata “cheo” hicho? Kuna mambo anayostahili kufanya ili ahakikiwe kuwa yeye ni Mtume na Nabii?
    Napata shida kujua (kwa mfano) huyu Mtume na Nabii Joseph Mwingira ametambulika lini kuwa Mtume na Nabii na ilikuwaje mpaka akakubalika mpaka kuitwa hivi?
    Nakuombea KIJANA WA KRISTO ili uweze kunielimisha katika hili. Naelekeza maombi haya hata kwa wengine wenye uwezo wa kuwa msaada kwangu katika hili
    Baraka kwenu

  9. Kaka Mubelwa, Nimelisoma swali lako karibu mara tatu na kiukweli unahitaji msaada kwa vile Biblia inasema kitu kikirudiwa mara kwa mara, tafsiri yake kitu kile kina umuhimu na cha kutiliwa mkazo!

    Nitakujibu kwa ufafanuzi zaidi nitakapokuwa nimeipata nafasi nzuri ya kufanya hivyo. Kwa sasa ninaijibu kwa ufupi kutokana na ukweli kwamba muda wangu wa kutumia “internet” unaniacha na nimeisoma “post” yako mwishoni.

    Mtume ni mtu aliyetumwa/ kuagizwa kufanya kitu. Sii kwa ridhaa yake anafanya, isipokuwa ipo mamlaka juu yake inayomwelekeza au kumwamuru kwenda. Mtume imetokana na neno “aliyetumwa” (uone uhusiano huu “mtume” na “tumwa”). Mtumwa hupeleka ujumbe na ni juu ya aliyepelekewa ama kuupokea au kuukataa. Mitume tunao wengi kwenye Biblia mfano Paulo, Petro na wale tenashara wa Yesu. Utakumbuka Yesu alipowatuma wanafunzi wake kuwaendea ndugu zao Israeli? Ndio, aliwatuma/ aliwaagiza kwenda. Mwisho alipokuwa akiwatuma alisema kwamba mtakapoingia katika nyumba isalimuni! Ikastahimili salamu yenu na kuwakubali, amani yenu na iwe juu yao.
    Laa wamewakataa, kung’uteni mavumbi ya viatu vyenu…. kwamba, walipeleke neno kama alivyowaagiza na hawakupewa ruhusa ya kuwalazimishia watu kwa habari ya ujumbe waliopewa na Yesu kuhusu Ufalme wa Mungu. Biblia inasema mtumwa ni mtumwa tuu mbele za Bwana wake na ndio maana Yesu mwenyewe alituambia tukiisha kuyatimiza tuliyoagizwa na Mungu turejee na kusema “Sisi ni watumwa tusiofaa kitu”.
    Kwanini nimefafanua hili?
    Ni ili kuyafafanua maneno niliyoyaweka kwanza kwamba “Mtume” ni mtu ambaye “hutumwa/aliyetumwa”, na kama ametumwa anapaswa kutekeleza alichoagizwa na Bwana wake tuu na sii kinyume.

    Nabii hatofautiani sana na Mtume isipokuwa Nabii yeye ni mtu asemaye kitu kabla ya kutokea na baadae kitu kile hutokea. Lakini pia Biblia inamsema nabii kama mtu asimamaye mbele ya Mungu. Ipo mifano mingi hai kwenye Biblia inayoonyesha jinsi Nabii alivyo mbele za Mungu. Kwamba, hata Malaika anaweza akawa Nabii kutokana na maelezo niliyoyatoa hapo juu, habari zihusuzo Nabii. Mfano Malaika Gabrieli amekuwa akiziwasilisha jumbe nyingi za Mungu.
    Ndiye aliyeleta ujumbe kwa Mariamu kabla ya Yesu kuzaliwa, Ndiye aliyepeleka ujumbe kwa baba yake Yohana kwamba Yohana angezaliwa kwanza,
    Lakini yupo pia Nabii Samweli aliye mtabiria Sauli habari za kuwa mfalme na jinsi angetakiwa kuondoka na kukutana na kundi la Manabii wakitabiri na yeye angeanza kutabiri. Kwa hiyo utagundua kwamba Nabii amepewa uwezo wa kuliona tukio mapema au kuliona kwenye ulimwengu wa Roho kabla ya tukio hilo kuvalishwa mwili au kuwa dhahiri.

    Hakuna mtu ampaye ama Mtume au Nabii Jina isipokuwa Mungu pekee anayewatumia watu hao kwa hivyo sidhani kama mtu anaweza kuyaondoa majina hayo kwao. Sema inapotokea watu wanakataa kuwapokea, ndipo wanapojiamulia wao wenyewe (yaani hawa watu wasiowataka)kusema huyu sii Mtume, huyu sii Nabii!
    Ndio maana Yesu aliwaambia wanafunzi aliowatuma “wakiwafukuza mjii huu, kimbilieni/ nendeni mji mwingine” maana nyingine ya neno kufukuzwa ni kukataliwa! Na unapokataliwa na watu haina maana watu watakuondolea nafasi uliyopewa na Mungu. Ndio maana ya Yesu kusema pia, Nabii hakosi heshima isipokuwa katika nchi yake mwenyewe. Kwamba, Wayahudi wasipouona umuhimu wa Nabii, Galilaya wanamuhitaji Nabii.

    Mengine mema kuhusu haya, ni hata wewe Mungu angependa sana ukipokee kile anachowaagiza watumishi wake kwako, kusudi akuzidishe na kukubariki katika kila utendalo. Kati ya hao watumishi wapo Manabii na Mitume ambao Kanisa hujengwa juu ya misingi hiyo Jiwe Kuu akiwa Yesu.

    Mungu akinipa nafasi tena, nitakuletea maeneo muhimu ya wewe kuendelea kujifunza kuhusu Mitume na Manabii na kwahiyo omba kwa ajili yangu niipate nafasi hiyo. nA KIPIMO KWAMBA UTANIOMBEA, NI KWA JINSI NITAKAVYOREJEA KWENYE KIPENGELE HIKI.
    Ubarikiwe Kaka.

  10. Ningependa kujua kuhusu Utume na Unabii kwa mujibu wa Biblia. Naomba mwenye kufahamu vema anisaidie.
    Mfano.
    Ni nani na kwanini aitwe nabii na mtume
    Ni nani apaswaye kumpa hadhi hiyo
    Na inakuwepo kwa muda gani ama inaweza kutenguliwa na nini
    Na mengine mema kuhusu haya
    Natanguliza shukrani

  11. Jamani mi naomba kuuliza, mafungu ya kumi ya wachungaji walioanzisha huduma kubwa wanapata kutoka makanisa yao yote? nimesikia kuna mchungaji mmoja kafungua huduma yake kutoka kanisa fulani, anasema mafungu ya kumi ya wachungaji wa mikoani lazima yaende kwa kiongozi wa dhehebu hilo, kwahiyo mchungaji husika hapati fungu la kumi ila posho ya kazi amefanya. Kama ni kweli hii si sahihi jamani, watu wanatajirika tu!

  12. Mengi ya mashirika yanayojitokeza kusaidia maendeleo ya ukristo,yamekuwa yakipata changamoto ya watu wachache kufanya kitega uchumi kwa mashirika hayo.Ni matumaini yangu kuwa mtajitahidi kutunza vision and mission yenu ili msipoe kiroho.
    Pia ombi langu jitahidini kusaidia watumishi walioko vijijini,hali yao inatisha.Ila wale wa mijini wako vizuri hawahitaji sana misaada yenu hii.Pia tunaweza kuona namna waislamu wanavyofanya inapofika wakati wa kutetea dini yao,wako radhi wabebe mapanga,wapige viongozi wao makofi na kuomba misaada ya marais toka Afrika hii kujenga misikiti.Wapendwa tujue kuwa kazi yetu itapimwa,Pia haki yenu isipozidi hiyo ya mafarisayo na waandishi hamtauona kamwe ule ufalme wa MUNGU.

  13. Mungu awabariki watumishi wa Mungu kwa maono hayo, Kati ya wengi ni wachache wanafikiria hivyo! Nitawaombea.

  14. kuna watumishi ambao Mungu amewapa maono ya kuwa saidia watakatifu. soma na ombe huduma hii:
    SHIRIKA LA KUWA HUDUMIA WATAKATIFU
    (SHILAKWA)
    UTANGULIZI
    VISION/MISSION

    Hili ni shirika ambalo misingi ya kuanzishwa kwake inapatikana katika 2 Kor. 8:4, 9:1.
    Lengo lake ni kuwahudumia watakatifu, yaani wale wote wanaomkiri Yesu Kristo kama Bwana na mwokozi wa maisha yao. Watakatifu hawa ni wale ambao kimaisha wana hali ngumu ya mapato, haswa wajane, yatima, wazee wasio na msaada, walemavu, nk.
    Hii haimaanshi kuwa wale wasio na sifa hizo hawatahudumiwa, bali nafasi ya kwanza watapewa wao. Msimamo wetu ni kutobagua mtu ye yote anaehitaji msaada.
    HUDUMA ZETU

    1. Kazi za kujitolea:
    Watakatifu walio katika fani mbali mbali kama, madaktari, wauuguzi, wanasheria, wajenzi, waalimu, wafanya biashara, nk; watahitajika kutoa huduma zao kwa wahitaji kwa njia ya kujitolea. Hili lina weza kufanyika kwa vipindi tofauti kutegemea na hitaji lenyewe.

    2. Michango:
    Tutakuwa tunakusanya michango mbali mbali kwa ajili ya kuwasaidia watakatifu wenye mahitaji. Michago hii itatoka kwa watakatifu ambao wanasukumwa kuwasaidia wengine katika moyo wa ukristo. Michango hii ni, fedha, nguo, vifaa vya nyumbani, usafiri, vyakula, ushauri, kuwatembelea wahitaji, n.k.

    3. Kujitoa kwa Bwana:
    Hii ina maana, moja ya mikazo ya huduma hii ni kuwawezesha wale wanaotaka kujitolea kuwasaidia wengine, wajitoe wao wenyewe kwanza kwa Kristo. Hili litafanyika kwa kuendesha vipindi vya kujifunza Biblia na maombi.

    MSINGI NA MOYO WA HUDUMA HII
    Tunasoma katika 2 Kor. 9:7, “Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.”
    Wote watakaojiunga na huduma hii watapaswa kuzingatia msimamo huo wa neno la Mungu.

    WATUMISHI WA HUDUMA HII
    Katika Matendo 6:3, tunaona sifa za wale watakao kuwa viongozi katika kuwahudumia watakatifu. Nasi tutazingatia sifa hizo kwani huduma hii ni ya Kristo mwenyewe na sisi ni watumishi tu.

    ENEO LA HUDUMA
    Lengo ni kuanzia katika baadhi ya maeno machache nchini, na hatimae kupanua huduma kwa mikoa yote ya Tanzania.

    USHIRIKIANO NA MAKANISA
    Vifungu vyote vya Biblia vilivyotumika kama msingi na nguzo ya huduma hii vinaonyesha kuwa huduma kwa watakatifu ilifanyika kanisani. Hii ina maana tutafanya kazi kwa ushirikiano na makanisa yote katika kuwa hudumia watakatifu.

    MSIMAMO NA MTAZAMO WETU
    Mtume Paulo akielezea moyo wa Wamakedonia katika kuwahudumia watakatifu, alisema: “Tena ndugu zetu, twawaarifu habari ya neema ya Mungu, waliyopewa makanisa ya Makedonia; maana walipokuwa wakijaribiwa kwa dhiki nyingi, wingi wa furaha yao na umasikini wao uliokuwa mwingi uliwaongezea utajiri wa ukarimu wao.” 2 Kor 8:1-2.
    Wamakedonia walitoa sana japo walikuwa na umasikini mwingi, na huduma hii inawategemea wale wenye moyo wakutoa na sio matajiri au wafadhili toka Ulaya tu.
    Kwa maneno mengine, huduma hii itafanywa na watakatifu watanzania wenye moyo wa kuwasaidia watanzania wenzao kwa jinsi watakavyo wezeshwa na Krsito bila kutegemea misaada toka nje ya nchi. Tunaamini hii ndio njia sahihi ya watakatifu wa Mungu hapa Tanzania kupokea kwa wingi Baraka za Mungu, kwa kuwa watoaji na kuwahudumia watakatifu katika kanisa la Kristo.
    Pamoja na kutoa huduma, lengo jingine kubwa litakuwa kuwawezesha watakatifu hawa kufikia wakati wakaweza kujitegemea na kuondoa roho ya umasikini na utegemezi kila wakati.

    UTEKELEZAJI
    1.Kwa kushirikiana na makanisa, kupata orodha ya wajane, yatima, wazee wasio na msaada, walemavu wasio na usaidizi, nk. Orodha hii itatusaidia kupata picha ya jinsi kuwahudumia wahitaji hawa.
    2. Kuwasiliana na watakatifu wanaotoa huduma zinazohitajika na kupanga ratiba ya jinsi na wapi huduma hizi zitakuwa zikifanyika.
    3.Kuanzisha mfuko utakao toa misaada/ mikopo isiyo na riba au riba iliyo chini ya viwango vya taasisi za fedha kwa watakatifu wenye uhitaji. Lengo kubwa la mfuko huu ni kuwawezesha watakatifu kujitegemea kimaisha ili na wao wawe Baraka kwa wengine wenye mahitaji.
    4. Kutakuwa na vipindi vya kujifunza neno la Mungu na maombi. Ratiba kamili itapangwa kutokana na mahitaji ya watakatifu.

  15. kwako mpendwa Steve Bicco je hiyo pesa anayochangia ameitafuta mwenyewe?, ameifanyia kazi au biashara?, au ni zile za sadaka za sisi waumini ambazo hatuambiwi mapato na matumizi?. kama ni katika fungu la kwake ambalo si sadaka za waumini. Mungu amwongezee na ampe baraka tele.

  16. Martin, naungana nawe mia kwa mia. Nafikiri ipo haja ya kuiundia “discussion thread” issue uliyoigusia. Mmh, let me see, pengine nitajaribu kui-frame vizuri na kuileta hapa SG!

  17. Mbona hawa watumishi wa Mungu hapa Tanzania hawasaidii watumishi wenzao wa madhehebu mengine hapa hapa Tanzania?Mbona sijaona watumishi wa makanisa mfano ya Kipentekoste(ambao wengi wao wanaukubali wokovu) wakisaidiana wao kwa wao?wanapokuwa wote wameokoka lakini wakiwa kwenye madhebu tofauti hawasaidiani.TUSIKUBALI KURIDHIKA KWA MAMBO HAYA.MWILI WA KRISTO HAPA TANZANIA BADO UNA SHIDA KUBWA YA UBINAFSI NA UCHOYO NA KUPENDA SIFA ZA KUJIONYESHA KWA WANADAMU. TUOMBEE WATUMISHI WAACHE UBINAFSI NA KUPENDA KUJIONYESHA KWA WATU.SISI WATEULE TUNATAKIWA TUWASAIDIE WATEULE WENZETU WENYE SHIDA. LEO HII NENDA MAKANISANI WATEULE WENYE SHIDA NI WENGI SANA.HAKUNA MTU ANAYEWAJALI. HATA WACHUNGAJI WENGI HAJALI WATU WAO WANAISHIJE. SASA INABIDI TUOMBE MUNGU ATUSAIDIE TUWEZE KUFIKIA WAPENDWA WENZETU NDANI YA KANISA KWANZA. KUMBUKA, KANISA SIO DHEHEBU WALA SIO MINISTY(HUDUMA). KANISA NI KILA ALIYEMKUBALI KRISTO NA KUAMUA KUMFUATA BILA KUJALI ANASALI KWENYE DHEHEBU GANI.

    ” As we have therefore opportunity, let us do good unto all men, especially unto them who are of the household of faith.-Wagalatia 6:10″

    PAULO ALISISITIZA TUTENDE MEMA HASA KWA WALIOAMINI ILI NAO WAWEZE KUMTUMIKIA MUNGU KATIKA MOYO WA FURAHA!

  18. Ningependa kujua kuhusu Utume na Unabii kwa mujibu wa Biblia. Naomba mwenye kufahamu vema anisaidie.
    Mfano.
    Ni nani na kwanini aitwe nabii na mtume
    Ni nani apaswaye kumpa hadhi hiyo
    Na inakuwepo kwa muda gani ama inaweza kutenguliwa na nini
    Na mengine mema kuhusu haya
    Natanguliza shukrani

  19. Praise God
    kwakweli nimeguswa na mchango wa Mtume Mwingira kwani jinsi siku zinavyokwenda maandiko yanatimia kwamba utajiri wa mataifa utakuja kwa watakatifu zamani utasikia masikini kama panya wa kanisani usemi huu umebadilika sasa. Juzi juzi katoka kuweka mafuta kwenye ndege ya Bishop Oyedepo leo tena kachangia maendeleo ya Rukwa Bwana ambariki mtumishi wake.

Andika maoni yako