Kundi La Strictly Gospel Lajipanga!

Pichani Mchungaji Abel Orgenes Akiombea Viongozi Wa Kundi

Kundi La Strictly Gospel limejipanga kuanza kufanya kazi ya Mungu kwa vitendo. Akiongea kwenye mkutano wa wana SG uliofanyika tarehe 18/9/2010, kiongozi wa kikundi Bi. Mary Damian alisema: “Tunahitaji tuwafikie wengine, tunahitaji kutatua matatizo yaliyopo kwenye jamii yetu, Tuwaambie watu Waache Kufanya Maovu Wamgeukie Mungu. Tuwafikie wafungwa, wagonjwa wa hospitalini, yatima na kuwahubiri masikini habari njema za Bwana Yesu pia kuwategemeza wachungaji wanaofanya kazi kwenye mazingira magumu”

Bi Mary Aliendelea Kusema “Tunahitaji watu wenye huduma na wito wa kumtumikia Mungu, japokuwa watu wako busy na majukumu mbalimbali inawezekana kuutoa muda wao hata kwa siku moja na kufanya kazi ya Mungu hali ambayo tasaidia kusimama imara na kuwa karibu  na Mungu”

Dada Rose Lusinde Kwenye Maombezi

Mkutano Huo Ulifanyika Jijini Dar es salaam Na Kuhudhuriwa na wajumbe wa kikundi cha Strictly Gospel na kupanga mikakati ya kuanza kazi mara moja Oktoba mwaka huu.  Akiongea kwenye mkutano huo, mgeni mualikwa Mchungaji Abel Orgenes Alisema “Huu ni wakati mzuri wa kumtumikia Mungu, watu wanapata fursa kupitia kundi hili pasipo kujali madhehebu yao”

Kundi la Strictly Gospel Group linataraji kuanza huduma hizo kuanzia October mwaka huu na kuanzia January 2011 Watakuwa wakifanya semina na matamasha mbalimbali ya Injili. kwa maelezo jinsi ya kujiunga na kundi hili wasiliana nasi kwa simu. +255 715 730 813, +255 752 730 813.

Waweza pia kututumia email kupitia: strictlygospel@yahoo.co.uk

16 thoughts on “Kundi La Strictly Gospel Lajipanga!

  1. Upendo wa kristo hauishii madhabahuni pekee,huwafuata watu wenye mahitaji mbalimbali na kuwaganga kwa utukufu wa MUNGU.MUNGU awabariki sana watumishi.

  2. Shaloom watumishi.Nafurahi kuona kristo akifunuliwa kwa watu katika matendo na sio kwa maneno pekee.Mbarikiwe sana wana strictly gospel,napenda kuwaambiwa kua kazi yenu sio bure mtalipwa kwa wakati wake msipozimia Roho.NOTHING BUT THE GOSPEL

  3. Shalom kaka,
    Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo atukuzwe ktk hili, tunaendelea kukuombea nawe usikate tamaa.
    Endelea kuomba kwa bidii. Mtwike Mungu fadhaa zako zote yeye alisema ktk Isaya kwa kupigwa kwake sisi tumepona, ameyachukua masikitiko yetu yote…
    Ubarikiwe

  4. Bwana Yesu asifiwe,kwa kweli kundi la strictly gospel mna staili pongezi MUNGU azidi kuwapa nguvu na jitihada katika utumishi wake.
    ONGERENI SANA STRICTLY GOSPEL TEAM!!!

  5. Bwana Yesu asifiwe, nawashukuru wote walioshirikiana nami katika maombi ya kurudishiwa kiwanja changu kwani Mungu ni mwema jana Jumapili nilikwenda kwenye kikao na mwenyekiti wa kijiji akathibitisha kweli kiwanja ni changu na itabidi kirudi mikononi mwangu, hivyo sina budi kumshukuru mungu kwa vile ndie aliniwezesha yote haya. Na ninawaomba tena tushirikiane wote katika maombi ili mwenyekiti wa kijiji aweze kupata kibali cha kubomoa pale kwenye kiwanja changu kwani alieuza alijenga hapo haraka haraka ili nisikipate hivyo Mungu aweke mikono yake tuweze kushinda hili la pili, naamini mungu ni mwenye kutetea wenye haki zao. Mungu awabariki wote walioniombea. Asanteni sana na tuzidi kuombeana.

  6. Mbarikiwe watumishi wa Mungu kwa maoni mazuri. Tunawaombea mafanikio!

    Nimefurahi kumwona Pasta Abel Ng’eni na Elia Kisigila kwenye picha uliyoweka. Bila shaka huu utakuwa mwanzo mpya kwa vijana wa Kitanzania!

  7. Hongereni Strictly Gospel, ni mpango mzuri. Mungu awaongoze vyema ktk utendaji wenu. Mzidi kuwa chachu ya mshikamano na maelewano miongoni mwa walimwengu ili mwisho wa siku, sote kwa pamoja tuweze kushangilia na malaika wa mbinguni, mahali palipo pema pa Mungu aliye hai, Alfa na Omega.

  8. Damu ya Yesu iwafungulie milango yoote ya Baraka mkavishinde vita vyote; nawatakia Mafanikio mema, kuishi kwetu ni kupambana tu na huyu anayejiita mkuu wa ulimwengu. Mbarikiwe.

  9. Amina kaka Mubelwa, sifa na utukufu kwa Mungu, asante kwa maombi yenu watakatifu yaliyoifikisha SG hapa ilipo. barikiweni

  10. Watumishi Mungu awabariki kwa kazi yenu njema, mtalipwa msipozimia moyo. Huduma yenu ni nzuri sana na mipango yenu ni mizuri pia.
    Mungu awafanikishe kwa jina la Yesu.
    Bwana wa majeshi awatie nguvu zaidi.
    Amen.

Andika maoni yako