Kuna watoto wa wachungaji wenye ushuhuda mzuri!

“Watoto wengi wa wahubiri hawana sifa nzuri kwa jamii” haya ni maneno yaliyo mitaani kwetu na hata kwenye makusanyiko tunapokutana. Lakini huu sio ukweli, kuna watoto wa wachungaji wanaoendelea vyema kiroho na kuwa ushuhuda mzuri kwa jamii iliyowazunguka. Napenda kuchukua nafasi hii kuwaomba watumishi wa Mungu, tuendelee kuombea na kuwakanya watoto wetu, watoto wa wachungaji. Tusihukumu wanaoonekana wanapotea. Hawatapotea, watarudi kwa baba yao.

10 thoughts on “Kuna watoto wa wachungaji wenye ushuhuda mzuri!

  1. Shalom wapendwa ni kweli
    kuwaombea ni lazima, na ni kweli kuwa ukiingia utumishi ni vita juu ya ufalme wa giza na kujitoa wewe na mali yako kwa Mungu, jiandae. Nadhani kila aliye Mkristo analijua hilo hivyo sio vizuri kuanza kulalamika kuwa maisha duni, shetani anatuwinda hapo unakiri kushindwa na hii vita je unaowaongoza inakuwaje kwao? Kuwapi kuyaweza yote ndani ya Yesu? Kuwapi kujua kudhiliwa? Je si kila silaha itakayoinuka juu yetu haitafanikiwa? Je watoto sio sehemu yetu pia? Je Mungu hakuahidi wamwaminio hawatapungukiwa chochoite kilicho chema? Je watoto wakipotea au kutookoka mwanzoni lakini wakaokoka wenyewe baadae kwa utashi wao ni vibaya, tumwache Mungu anajua analotuwazia sisi tutimize wajibu wetu kama watumishi bila kunungunika kisha Yeye atatenda kwa wakati wake. Bado siamini kuwa kwenye kila familia ya mtumishi kuna mtoto asiyefaa, wapo wachache ambayo ni idadi sawa tu na wa waumini wa kawaida. Mbona kuna watoto wa ma profesa au matajiri wengi hawana akili wala ujuzi wa biashara au kazi ila hawa hawanung’uniki waziwazi watabebana hadi kuwainua.
    Mtumishi omba pia kwa ajili ya wanao. waumini pia tuombe kwa ajili ya watumishi, watumishi wapate pia muda wa kuwa na familia zao, Timotheo kule inasema askofu, shemasi wawe ni watu na baba za familia njema hivyo ukitimiza wajibu wako kwa familia sidhani kuwa kutakuwa na watoto wa ajabu wasio mjua Mungu.
    Kila siku jioni omba pamoja na familia na asubuhi pia kabidhi mbele za Mungu, kila wiki kaa na watoto na mwenza na kuongea nao ujue nini kinawasumbua, kinawakera na kuwaeleza kwa upendo hali halisi ya kipato chako na malengo yako, maana ya kujitoa kwa Mungu, Yoshua…mimi na nyumba yangu tutamtumikia Mungu huyu…. kama mtumishi unakaa mbali na familia, huna muda nao, huombi wala kujadiliana nao ni amri tu, basi tegemea wasikuelewe maana huo utumishi unatumika peke yako sio na familia yote. Mtumishi pia kuwa kichwa na msimamo imara ktk familia maana kama mwenza hajasimama ni rahisi kunung’unika na kuharibu watoto, kutosimama kwa maombi ktk vita pamoja nk
    Lakini ktk yoooote mie bado naona tukiomba kwa imani hakuna lisilowezekana kwa Mungu Marko 11. Mbarikiwe

  2. Niwajibu wawaumini kwakweli kuombea nyumba za watumishi. Nakwawale washirika wanaosubiri tu maombi ya wachungaji kujuwa kuwa watumishi pia wanahitajikuchukuliwa kimaombi. Ubarikiwe Yusto

  3. Ni wazi kuwa wachungaji wana vita vikali sana.Ktk vita hivyo shetani anajaribu kuwapiga vita watoto ili kuharibu ushuhuda wa familia na kwa njia hiyo kurudisha nyuma kazi ya Mungu.Hatuna budi kuwaombea wachungaji wetu na familia zao

  4. Dada Rosemary nafikiri hujafanya uchunguzi wakutosha kuhusu familia hizi za watumishi.Tunaposema watoto hawa niwakorofi hatunamaana kuwa hawapo walio wazuri au wawaumini hawapo walio wakorofi wapo.Nataka ni kwambiye anza kufuatilia watumishi nakuongea nao kuhusu watoto wao watakwambia ukweli.Pili hatuzungumzii kuwafanya kuwa watumishi kama wazazi wao tunazungumzia kuwa na sifa nzuri ktk jamii (kuokoka na kumjuwa Yesu sawasawa) Swala la kazi ipi mtoto afanye ni matakwa ya mtoto ili mladi tu iwe ni kazi inayompendeza Mungu au inayolinda maadili ya wokovu. Mbarikiwe!!!!!!!

  5. Shalom mie naona sio kweli sababu:
    1. Ingekuwa takwimu zinaonyesha ktk kila mtu / mtoto mwenye maadili mabaya nk asilimia kubwa ni mtoto wa mchungaji au mwinjilisti hapo tungesema sawa lakini, kuanzia na watoto wa watumishi wachache na kuamua kuwa wote wako hivi sio sawa
    2. Kama ilivyo kwa mzazi yoyote wajibu ni kuwalea wakiwa wadogo lakini wakiishakuwa na utashi wao ni wajibu wao wenyewe kuendelea kuukulia wokovu au kugeukia upande wa pili, wazazi tunawaombea ndio lakini Mungu tu ndiye anayejua kilicho moyoni kwa mtu. Hivyo tuendelee kuwaongoza ktk njia njema na tuendelee kuwaombea hata wakipotea. Mfano Ayubu alikuwa akifanya toba kwa wanawe akihofia wanaweza kuwa wanamkosea Mungu. Yesu alikuwa anajaribu kurudi kwa nduguze na kuwahubiria ila walikuwa hawamuamini, ktk mitume wa mwanzo alikuwa na undugu nadhani na Yohana ila sio kutoka familia yake. Watu walitegemea kila mtoto au ndugu wa mtumishi awe mnyoofu au mtumishi pia ila tujue kila mmoja anao wito na huduma yake kulingana na kusudi la Mungu utumishi haugaiwi kama vyeo vya kifalme au siasa. Mungu aliliona hili na kuamua kuuachana na mambo ya ukoo wa na kumchagua Samuel badala ya watoto wa nabii Eli. Alimuacha Essau na kumchagua Yakobo, Isaka badala ya Ishmael ambao ktk jamii walistahili kwa kuwa wazaliwa wa kwanza. Hata Yuda alikotokea mfalme Daudi na kisha Yesu alikuwa ni mtoto wa ktkt tu na Rahabu mama wa Boazi alikuwa kahaba. Mungu hupenda kuvitumia vinyonge na kuviinua kwani ktk hivyo utukufu wake hudhihirika.
    Nadhani hili liwe ni fundisho kwa watu wa Mungu tusiwalazimishe watoto waingie utumishi bila ya kuitwa, pili tusiwakwaze na kuwakataa watoto wa kiroho tulionao ktk kuwarithisha huduma au maono kwa wivu kwamaba si damu yetu ndio kuishia kuwa kama Eli. Wote tuombe kwa ajili ya Roho mt awe na kanisa ili tuenende kiroho na si kimwili.
    3. Watumishi tuache kunung’unikia kipato na utumishi kuwa tuna hali duni hadi kupelekea watoto kuona kuwa kumtumikia Mungu hakuna faida Malaki 3: 14-15 Mmesema, Kumtumikia Mungu hakuna faida; na, Tumepata faida gani kwa kuyashika maagizo yake, na kwa kwenda kwa huzuni mbele za Bwana wa majeshi? Na sasa twasema ya kwamba wenye kiburi ndio walio heri; naam, watendao uovu ndio wajengwao; naam, wamjaribuo Mungu ndio waponywao…. tukijenga dhana hasi kama hii ktk familia zetu ni lazima wote watauchukia wokovu na si utumishi tu. Tuwe na shukurani kwa Mungu, tuwe na Imani na saburi kwa Mungu pia tumtumaini Mungu kuwa anatuwazia mema tu siku zote. Mbarikiwe

  6. Namuunga mkono Eliya Lukindo. Jambo hili ni kweli. Utakapo simama na kujitoa kwa BWANA, shetani anaanza kuingia kwa familia yako. La muhimu hapo ni kuzidi kuombeana. Barikiwa

  7. KUONDOA MAWAZO HAYO NI VIGUMU KWAKUWA NI MAMBO YANAYO ONEKANA KWA WATOTO WENGI WA WACHUNGAJI.SHETANI ANAFUATILIA SANA FAMILIA ZA WACHUNGAJI ILIKUWAVUNJA MOYO WATUMISHI

  8. Ni kweli watu wamekuwa wakinena maneno mabaya juu ya watoto wa watumishi wa Mungu. na utafiti unaonesha kwamba 85%ya watoto wa watumishi hawana ushuhuda mzuri kwa sababu zifuatazo: 1. kujiona wao ni watoto wa watumishi hivyo hamna sababu ya kuokoka kwelikweli 2. wachungaji kukosa muda wa kuwakanya mara kwa mara kama alivyoshindwa Kuhani Eli 3. watoto hawa wanaona maisha ya baba zao au mama zao yapo katika shida hivyo wanaona ni bora tu waache kuishi maisha kama ya wazazi wao. 4. Watoto wa wachungaji wanaangaliwa na kila mtu==wewe fikiri mbona watoto wa watu wengine wanafanya mabaya makubwa tu lakini leo afanye wa kwa pastor Daniel eeeeeee—— utaona mtaa mzima wanaongelea jambo hilo tu

    hivyo basi ni jukumu letu kuondoa mawazo kama hayo na kupanda mawazo ya kwamba watoto wa wachungaji ni kama watoto wengine tu hakuna tofauti

  9. amen this is a good idea not all I know a few who are God fearing people

Andika maoni yako