Huwezi kuwa Huru usipotafuta Uhuru!!!

shangazimtoto

Picha kwa hisan ya gumzolajiji

Mtu hawezi kuwa huru asipoutafuta uhuru; katika harakati kutaka kuwa huru ni pamoja kutafuta kujiweka huru; Lakini itawezekana vipi mtu kuwa huru asipotaka kuwa huru?

Maana ili utoke katika usioyapenda ni lazima uyape nafasi kubwa unayo yapenda ikiwa ni pamoja na kukata mahusiano na yale yote usio yapenda!

Kwa maana hii Unapotaka kwenda mbele lazima uzikatae hatua za kurudi nyuma ukipiga hatua za kwenda mbele

Ili kuutambua usahihi wa mahali ulipo sasa lazima upatazame kwa kuutambua ubaya wa ulipokuwapo jana;

Hivyo usijihukumu kwa kuondokewa na moja; kwa kuwa ili bidi moja iondoke ili uipate thamani ya mbili kwa maana moja huwa ni ngazi tu ili mbili ije juu yake. Ubaya wa lililokukuta usikukatishe tamaa maana hilo ni kama kikapu cha ukuu na thamani ya lijalo ujaposugua goti!

Wapenzi kila jambo lina kusudi lake; hima liwe baya ama liwe Jema! Maana kwa baya twajifunza habari za jema; Kadharika katika jema ndimo kulimo na jicho la lile baya ili lipate kudhihirika machoni petu nasi tujihami kwalo!

Sasa Je ni nani katika sisi aso na historia mbaya nyuma yake kwa ajili wema wake wa leo? Hapa kila mtu analo jibu lake mwenyewe. Lakini u kheri anao yeye ajipaye jibu sawa sawa ili azidi kujithaminisha utu wake kwa msaada wa roho Mtakatifu.

Mimi nisingeliitambua heshima ya hapa nilipo leo kama sikuwahi kuwa kinyume na hivyo nilivyo maana kuishi kwangu mwenyewe ni ushuhuda wangù mwenyewe

Sifa kwa Mungu wapendwa!

Hivyo basi ilinibidi niyapende mabaya yangu mwenyewe ili nisipate kujilaumu na kujihumu nisijeshindwa kuyafurahia maisha; maana katika hayo ndimo nilimokutana na Mungu katika Yesu Kristo

Hapa mwingine hustuka na kusema huyu anaongea nini! Iko hivi kama nilihukumu nafsi yangu kwa ajili ya Kristo ili yale mema ya Mungu yapate kuishi moyoni mwangu pasi mimi kujuta

Kwa kuwa nikapata nguvu ya kusonga mbele pamoja na Kristo utu wangu wa zamani ukirudi nyuma na kufa ili mimi wa leo nipate kuishi!

Kwa uhuru nikaujua utumwa; ili kuupata ule uhuru ulio uhuru wa roho kuudhibiti utumwa mwili kwa bwana wake dhalimu; nikawa na nguvu niliye imara maana adha ya utumwa sikuipenda abadani

Ndugu mtu asiye huru hawezi kuyaelewa haya maana; ni kama vile kwa yeye mwenye shibe asivyoijua adha ya mwenye njaa ama mwenye uhitaji wa kipande cha mkate asivyoijua raha ya aliyeshiba

Basi kwangu mimi iko hivi naliwapenda na kuwasamehe walioyatenda ya hiana maisha yangu maana wamenipa kuwathamini ninyi mketio pamoja nami tukipeana maarifa kwa kupenda naam; tukiheshimiana na kujaaliana naam; wenye kuhurumiana na kuadabina!

Zaidi wale haswaa waliofanywa kuwa namna mpya kabisa katika mimi lakini nisiye na nafasi ya kuwahumu wa jana kwa sababu yao wale wa leo bali mwenye kuwathamini wa leo zaidi kwa kuwa katika wao nalioona faraja mpya ya Mungu nikitua juu yangu na kuyafunika yooooooooote ya kale ili nipate kuishi maisha ya furaha!

Nawapenda!

–Mwamfupe Anyisile

Andika maoni yako