Wivu ungekuwa ni ugonjwa…

wivu

SOMO: WIVU UNGEKUWA NI UGONJWA, MADAKTARI WENGI BINGWA WANGEANDALIWA MAANA WATU WENGI SANA WANAUMWA UGONJWA HUU. MAANDIKO: YOH: 11:45-53

1. UTANGULIZI
Mojawapo ya tatizo ambalo limeleta madhara katika jamii nyingi duniani, ni wivu; wivu ungekuwa na sura, ungemshangaa hata uliye jirani naye anayekuchekea kwa nje; Wivu ni ile hali ya kutofurahia mafanikio ya wengine, ni ile hali ya kukosa furaha na amani moyoni unapojilinganisha na wengi waliofanikiwa; ni ile hali ya kuwa na maumivu moyoni kwa nini Fulani ndiye kafanya hivi badala ya mimi; kwa nini Fulani ndiye aolewe/aowe Fulani badala ya mimi; ni ugonjwa unaokula furaha na amani ya watu wengi kimya kimya, umesababisha madhara mengi sana kwa watu wengi, na kwa sababu ni ugonjwa usiopimwa maabara watu wakajulikana kuwa wanaumwa ili watibiwe, umeendelea kuwa ugonjwa wenye kuleta madhara makubwa na hasa kwa wana wa Mungu tangu nyakati za Kaini. Mwaz. 4 : 1 -13

- Pamoja na sababu nyingine nyingi walizokuwa nazo Mafarisayo, Masadukayo pamoja na wakuu wa dini ya Kiyahudi wakati wa Yesu na mitume wake; sababu mojawapo kubwa ya kumsulubisha msalabani ni wivu; walijua anakuja kuchukua nafasi zao, watu watawaacha, heshima zao zitaisha na hivyo kwa kutaka kulinda heshima zao; wakaona bora kumwondoa anayetishia heshima zao kuondoka!! Wakamtenda, kama mhalifu na mnyanganyi mtu ambaye hakuwa na hatia.

2. Wivu limekuwa ni tatizo lililojificha sana hata kati ya ndugu na ndugu!! Mwanzo 30:1 ( Rahel ) anamwonea wivu dada yake kwa nini anazaa na mimi sizai!! Mwz 3 : 37 :4 ndugu zake Yusufu wanaona wivu/ wanachukia kwa nini Yusufu anapendwa sana na Baba yetu kuliko sisi!! Mwz: 37:20, Mdo 7:9

- Unafanya vyema kuliko bossi wako na kupata heshima kwa watu bossi wako hakuambii, lakini ndani yake kama wivu ungekuwa na sura ungeiona. 1Samwel 18 : 5 – 9.

- Sauli alijaribu kujikaza kwa kumchukua Daudi nyumbani kwake na kumfanya kuwa mchukua silaha zake waendapo vitani lakini ndani ugonjwa wa wivu unamla – anapanga namna ya kumwondoa tu!! 1 Samwel 18 : 10 – 29; INATISHA MTU AKIWA NA UGONJWA HUU WA WIVU!! Hana furaha hadi amwondoe mtu mwenye haki!!

- Watawala wengi sana duniani wameaagamiza watu wengi sana hodari kwa hofu ya kuchukua nafasi zao; na hata katikati ya wateule Mitume walipambana sana na roho ya wivu maana ingewamaliza!! Yak. 4:1 – 2, Yak. 3: 14

- Hii roho iliyowatesa sana Wayahudi enzi ya injili ya Mitume. Mdo 13: 42-52, 17:1-9!! Yaani wivu ni roho ya ajabu sana inamtafutia tu mtu sababu ili kumharibia sifa yake ili kumwangamiza pasipo sababu ya msingi!! Hii inanikumbusha kisa Fulani cha Askofu Mkuu wa dini Fulani aliyemwonea wivu makamo wake eti kwa nini mikutano yake ya injili watu wanakusanyika wengi kuliko mikutano yake!! akaamua kumsimamisha asihubiri mwaka mzima??

3. Kwa wakati huu nataka niwaambie wote walio na ugonjwa huu wa wivu kwamba kadri utakavyozidi kuwa na wivu kwa mafanikio ya wengine, ndivyo daima utakavyozidi kushushwa na Mungu chini zaidi na yule unayemwonea wivu na kupanga njama za kumwua atazidi kustawi zaidi. 2Smweli 3:1. Hii ndiyo kanuni ya Mungu.

- Kadri walivyomtesa Yesu na kumzomea na kumwaibisha ili watu wamwite mlaaniwa, ndivyo Yesu alivyopata umaarufu zaidi duniani baada ya kufufuka, na hakuna Mfalme yeyote leo hii duniani anayefikia umaarufu alio nao Yesu Kristo katika jamii.

- Kadri ndugu zake Yusufu walivyomwonea wivu na kumtesa na kumuuza, ndivyo kadri alivyopata umaarufu machoni pa Farao kuliko wataalamu wake wote aliokuwa nao na baadaye kuinuliwa zaidi na zaidi. Mwanzo 41 : 37 – 45; Haleluya.

4. Dawa ya wivu ni kuacha kujilinganisha na wengine, acha kuwahukumu wengine maana mojawapo ya dalili za wivu ndani ya mtu ni pale anapojikuta hafurahii mafanikio ya watu wengine zaidi ya kuona makosa yao!! Ni pale anapoanza kujiona kuwa wao wana neema na upendeleo kuliko yeye; nasema kweli kama vile mchwa wanavyokula nguo taratibu taratibu, ndivyo wivu unavyokula kiroho cha mtu na baraka zake. Mchwa ukishakula nguo za mtu anatengeneza tope Fulani juu yake; na wivu nao ukishamwingia mtu unakula na kutupilia mbali kabisa mafanikio yake. Wivu ndiyo njia ya mkato na fupi sana anayotumia ibilisi kuharibu mafanikio ya mtu hata kama ni kihuduma. Na hakuna jambo linalomrudisha mtu aliyeokoka nyuma kwa haraka sana kama kujaribu kujilinganisha na watu wengine katika viwango ambavyo wamevifikia kwa muda mrefu!!

- Kaini alimwonea wivu ndugu yake, akaishia kulaaniwa na Bwana Mwanzo 4 : 10 – 14

- Rahel akamwonea ndugu yake wivu, akafia njiani. Mwz 35 : 16 – 19 na akazikwa tu njiani mahala pasipo rasmi!!

- Sauli akamwonea wivu Daudi akaishia kujiua. 1Samwel 31: 3 – 6

- Absalomu akamwone wivu baba yake Daudi na kutaka yeye ndiye atawale; akaishia kuadhibiwa hata na miti kabla hajauawa!!
2 Samwel 18 : 6 – 15.

- Waliomwonea Yesu wivu waliishia kuliwa fedha zao na ukweli ukaendelea kuhubiriwa. Mt: 28: 11 – 15

Baraka tele juu ya kila mmoja wenu.

–Askofu Dr. L. Mwizarubi
20/4/2014

This is What Happens When We Worship the Lord

timm

by Pastor Tim Burt

One morning while I was praying and worshiping the Lord, the Lord spoke to me. It was very clear and what He said was a fresh word to my heart. By that I mean that I had never had the thought He was communicating to me. As I was worshiping Him He spoke to my heart and said, Tim, worship isn’t for my benefit. When the Lord speaks to me He usually doesn’t say a lot. He’ll make a statement and then as I think and pray about what He has said, His words—the thoughts He wants me to understand, just seem to follow. Sometimes scriptures or stories from the Word will instantly come to mind and I know the Lord is teaching me and revealing more of Himself to me.

As I began to think about what the Lord said, I heard more. I heard Him say, I am not ego deprived.That was all I heard. I just began to meditate further and think about what the Lord had spoken. Suddenly, it was as if the lights came on.

I am a worshiper of God and always have been since I gave my life to Jesus. I was so thankful for Him saving me that I always wanted to find ways to express my thanks and love to Him. Besides that, the Word of God instructs us to worship the Lord. The Lord alone is worthy of and deserves our worship and I’ve never questioned it. Yet now I could see worship in a new light. The Lord said, Tim, worship isn’t for my benefit.The Lord was showing me that worshiping Him was for my benefit, not His. It was so easy to see. And so true!

Sometimes life seems like more than a plateful. As a man, a husband, a father, a Pastor, a son, a brother, a friend, and a Christian, it can sometimes seem like there are so many responsibilities—so many things I should do and do well. I want to be good at every one of these things. I want to be diligent and do what’s right and show the proper respect and love and friendship while being responsible to each of these areas of my life. Because I do, it brings me to this simple truth; outside of God, I can’t do it. Jesus warned us of that in John 15:5 (NIV).  “He said, ‘I am the vine; you are the branches. If a man remains in me and I in him, he will bear much fruit; apart from me you can do nothing.’”

It’s only when I’ve ever thought I could do all this and attempted to do it in my own strength that I’ve fallen flat on my face feeling overwhelmed or like a failure. God never created us to live outside His grace, strength, and help. The grace of God is His supernatural help given to us to do all the things He has given us to do well. He knew we’d feel overwhelmed without Him. He wanted us to lean on and count on Him—on His grace. When we learn to really focus on the greatness of our God and upon the covenant of blessing He established with us and for our benefit, when we meditate on His love that surpasses human understanding that He has for us, when we truly believe He desires and is willing to help us, then and only then will we lean on Him, ask, and have faith in His grace to help us. We would gain the strength to look anything in the eye and know He’d help us handle it. When we did, then we’d feel like the writer of Psalm 46:1-3 (NIV) who wrote,  “God is our refuge and strength, and ever-present help in trouble. Therefore we will not fear, though the earth give way and the mountains fall into the heart of the sea, though its waters roar and foam and the mountains quake with their surging.”

You have to admit, if you were anywhere near mountains falling or caught in roaring seas, you’d be shaking in our boots. These are the kinds of things that cause instant panic. But the revelation being shared in these verses is that when God is worshiped and magnified for who He is and His love toward us, His presence grows within us. A revelation of His love grows within us. He becomes almighty God and our problems and feelings of being overwhelmed shrink in the light of His faithfulness, His promise and His love. Then we are strengthened to take on the day and the challenges before us a step at a time knowing His grace is there to help us!

That is why the Lord said to me, Tim, worship isn’t for my benefit. Worshiping the Lord is for us—for our benefit. Psalm 95:6-7 9 (NIV) says, “Come, let us bow down in worship, let us kneel before the LORD our Maker; for He is our God and we are the people of His pasture, the flock under His care.”Psalm 34:3 (NIV) says, “Oh, magnify the LORD with me, And let us exalt His name together.”

God is not egotistical. He does not tell us to worship Him for Himself. He tells us to worship Him so that when we look at the magnificence of the Heavens or of the creation around us—reflecting that He created it all, then we will also reflect that this great and magnificent God loves us and has adopted us as His children through Jesus Christ. Worshipping God strengthens us. That is why it is for us! Worship elevates the Lord in our hearts to His rightful place. When we worship the awesomeness of God, He is magnified in our spirit and the cares, worries and lies of the devil shrink. When we worship the Lord our faith grows in our heart and the supernatural help of God flows into our lives. When we worship the Lord, He becomes Almighty God and we become His children. Praise His Holy Name!

Psalms 89:15 (NLT) “Happy are those who hear the joyful call to worship, for they will walk in the light of your presence, Lord.” 

In His Love,
Pastor Tim Burt

How God See us!!

tim

Most of us look at ourselves in a mirror daily. We see what we see. You see yourself through your eyes and from perspective. Have you ever thought about how God sees you? Actually that thought scares too many people because they feel that in God’s eyes, they don’t measure up or they are in big trouble. They don’t want to think about how God sees them.

As a Christian, it’s important to learn not to look at yourself through your own eyes, but instead see yourself as God sees you. Do you know that this is the true key to supernatural change and what ignites the power to conquer your lame excuses for not obeying God in your life?

If you know the story of Moses, you know that the beginning years of his life were anything but normal. He was raised in the cross hairs of two cultures – Hebrew and Egyptian. They were two distinctly different religious and social cultures. It was easy for him to become confused over who he was in life and how he was supposed to walk his life out. He had to come to the place of discovery – deciding for himself what he believed and how he wanted to walk out his life.

At the time he finally mustered up the courage to choose the side of his Hebrew heritage and do something for God’s people, he failed in the worst way. He committed murder. Not on purpose. He was trying to protect a Hebrew slave from being beaten but through his efforts, he accidentally killed the Egyptian taskmaster. He panicked and fled giving up all his hopes and dreams for a great many years. That is until one day God called upon Moses to remind him of why He put him on this earth and to guide him toward his destiny. God asked Moses to step out in faith and do something for Him. Let’s read about it and as we do, begin to see the battle of excuses warring with the voice of God telling Moses who he was and who he could be with God working in and through him.

Exodus 3:9, “Come now, therefore, and I will send you to Pharaoh that you may bring My people, the children of Israel, out of Egypt.”

We see Moses’ first excuse – those words that the devil teaches us all to parrot and build into our thinking – “Who do you think you are?”

Verse 11 – “But Moses said to God, “Who am I that I should go to Pharaoh, and that I should bring the children of Israel out of Egypt?”

Moses struggled with his identity. He didn’t feel worthy or prepared and was sure there were others beside himself who were much more qualified. He was probably thinking – “God you’ve got to be kidding! I am absolutely incompetent to do this!” Moses was seeing himself through his own eyes and in his own ability rather than listening to God’s voice telling him that He would be with him to help him at every step. Moses, not unlike many of us, was afraid of failure. Most fears of failure in life are tied to the fear of the unknown, the scars of past failures, and of public opinion – What are others going to think? God answered Moses giving him a rod and the promise of signs and wonders to validate God was with him – the promise of a miraculous commissioning. Moses was still weak-kneed.

Look at God’s response. V12, “I will certainly be with you. And this shall be a sign to you that I have sent you: When you have brought the people out of Egypt, you shall serve God on this mountain.” What could inspire more confidence in anyone than a commission and promise from God that He will back you and be with you!”

Then Moses offered his second excuse. Verse 13 – “Then Moses said to God, “Indeed, when I come to the children of Israel and say to them, “The God of your fathers has sent me to you,’ and they say to me, “What is His name? What shall I say to them?” God told him what to say.

Then Moses had his third excuse. Exodus 4:1 – “Then Moses answered and said, But suppose they will not believe me or listen to my voice; suppose they say, “The LORD has not appeared to you.”‘

God was so patient with Moses. He listened to his excuses and worked through each one with him. If you’re a dad and your child is telling you his excuses for being afraid to step out and try something,  are you as patient to help him? Are you as willing to help him? Part of who he becomes is connected to your support and encouragement – you being his helper, his friend, and his supporter.

God desired to use Moses in spite of his extensive flaws and contradictions. God addressed his excuses and objections with great detail, assurance and power. What did Moses do? Offer more excuses.

Number Four Excuse: “I’ve never been eloquent – I’m just not a good speaker.” God helped him through that.

Then Excuse Five: “I just can’t do it” – the one most people pull out of the bag before they walk away from God. Exodus 4:13 “But Moses again pleaded, “Lord, please! Send someone else.”

All of the great leaders in the Bible outside of Jesus Christ were flawed, fearful of doing what God asked them to do, and tempted to decline with excuses. It’s easier to make excuses about our inadequacies than it is to take on a challenge at God’s request. We’re plagued by self-doubt. We say we don’t have the right skills for the job, and like Moses we may worry that people, even our families, won’t buy into our leadership – after all, Jesus’ own brothers and sisters didn’t!

God discerned the traits of leadership in Moses regardless of all shortcomings.  God ended up bringing Moses brother Aaron in to help with the job assignment. That was God’s second best. Time and again He supported and reassured Moses by addressing his fears and objections and by promising to be with him giving him the tools he needed to succeed. God choose to cultivate and develop leadership in Moses which would eventually inspire the future leaders of Israel. He would become one who modeled the leadership of trusting God more than himself. This is where excuses are defeated  – when one knows who He is in God, not in himself. This is where men become godly men and women become godly women. This is where families become a powerful light. This is where churches become centers of influence changing cities, states, and nations.

When God is leading you to do even small things that you are afraid to do, remember Moses being paralyzed with fear and how God helped him and taught him the answer to the question, “Who am I?” God is no respecter of persons and is waiting to help answer that question for you! The fulfillment of your destiny begins with one step of obedience to God at a time.

2 Timothy 1:7 (NKJV) “For God has not given us a spirit of fear, but of power and of love and of a sound mind.”

In His Love,
Pastor Tim Burt

UTISHO WA KUFUFUKA!!

msalaba
MAANDIKO: YOSH. 5: 1 (YOSH. 2: 1 – 24)

Mojawapo ya ahadi toka kwa Mungu wetu tunayemtumikia, ni pamoja na kutuma utisho wake mbele yetu (utisho wa Mungu wetu) huwa unatangulia daima mbele na kumfadhaisha adui yetu sana. Kutoka 23: 27 – 30

- Kwa kweli Yesu Kristo ni tishio, kwa wakuu wa dini ni tishio kwa Wafalme ni tishio, kwa mapepo na wachawi ni tishio, kwa wasomi ni tishio, kwa matajiri ni tishio, kwa askari ni tishio, kwa magonjwa na wafu ni tishio, nasi tunatakiwa kulijua hili na kulikiri daima hata tunapoona wengine wakiogopa na kukata tamaa kutokana na vitisho vya adui. Hes. 14: 6 – 9.

- Mpaka leo duniani kote, kufufuka kwa Bwana Yesu ni tishio kwa imani nyingine zote ambazo waanzilishi wake na umaarufu wao hatimaye waliishia kaburini na hawakutoka kamwe hadi sasa ilibaki mifupa tu makaburini na nyama zao zikawa chakula cha mchwa!!.

- Askari waliopewa kulilinda kaburi la Yesu, saa anafufuka walikipata cha moto!! Soma waliyoyakuta. Math. 28: 1 – 4, 11 – 15.

- Habari hii ya kufufuka kwa Yesu imeenea dunia nzima na adui hata anapojaribu kuifunika kamwe hataweza, Yesu amefufuka na huu ndiyo ukweli, ndiye aliye na mamlaka juu ya kifo na siyo nabii au mtume mwingine yeyote, na kwa kweli huu ndiyo ushindi mkubwa sana wa Wakristo wa kweli.

Ukitaka kujua kuwa Kristo ni tishio; soma
(a) Marko 5: 1 – 15
(b) Yohana 11: 43 – 53 n.k. 2

Kama ilivyokuwa katika nyakati za Joshua, ambapo watu wa Yeriko mioyo yao ilikuwa imeyeyuka na hofu ya Mungu kuiangukia Nchi ile; ndivyo ilivyo dunia hii ya sasa tunayoishi, pamoja na dini nyingi kujikakamua lakini viongozi wao wanajua kuwa Yesu Kristo ndiye nabii pekee aliye tishio, ambaye kaburi halikuweza kumshika, na habari zake zinaposhuhudiwa mahala popote kwa usahihi, zina uwezo wa kuwaondoa watu wa aina yoyote katika utumwa wao!!.

Hakuna imani katika nabii yeyote leo hii hapa duniani iliyo na uwezo wa kumweka mtu huru zaidi ya imani ya Yesu Kristo.

- Kama Joshua, hakuna sababu ya Kanisa kuishi kwa hofu hata kama dunia hii ingefanya vituko vyake; bado tutaishi, tutakula, tutavaa, tutajenga, watoto wetu watasoma, watafanya kazi na biashara nzuri; Bwana amekwisha ondoa uvuli wanaojivunia.

- Tunatamba kwa sababu mwanzilishi wa imani yetu hayumo kaburini, amefufuka, yu hai milele na milele, anajipigania, anasema, anatembea, anaishi, anazo funguo zote za mauti na za kuzimu, Wana wa Sayuni hatuna sababu ya kujikunyata!!

- Hakuna roho ya nguvu tena kwa shetani dhidi yetu. Ona alivyo tishio huyu Mwanaume!! Luka 11: 37 – 41

Joshua alipata ushindi sana sababu ya ufahamu huu, adui zangu Mungu ametuma utisho kwao, na mioyo yao tayari imeyeyuka!!
Bwana tusaidie

Na
REV. L.M. Mwizarubi

Finish What You’ve Started

joy2

Have you ever started a project and not finished it? Or put a dream on hold because other things got in the way? I think we’ve all experienced these frustrations at some point in our life. The truth is sometimes starting is the easy part. However, with God’s help we can finish whatever we start because the Bible says, “With God all things are possible” (Matthew 19:26 NKJV).

I believe when we feel a passion to do something, God has more than likely put that desire in us. For example, I am passionate about teaching people the Word of God. I’m so passionate about it that I’ve given my life to it for the last 38 years and will continue to do so. That’s because God spoke to me and put that desire in my heart. If I had gone and done something else instead, I probably would have spent the rest of my life feeling frustrated and unfulfilled.

That’s what happens when we are passionate about something and we don’t do something about it. But the good news is even when we’re tempted to think that it’s too late to start over, with God, it’s never too late. And God will give us what we need, especially in times of adversity.

It’s important to understand that when we step out to do the things God has planned for us, we need to be ready to stand our ground when opposition comes along. The apostle Paul said, “A wide door of opportunity for effectual [service] has opened to me…and [there are] many adversaries” (1 Corinthians 16:9 AMP).

Defeating Your Giants

These adversaries are like giants, and there are little ones and big ones. Sometimes they come in the form of a mental attack, or they could come through a person you’re close to. People actually laughed at me when I told them what I felt God was calling me to do. Or an adversary could be one of those little daily aggravations we all face.

The bottom line is that the devil sets us up to get us upset. Because he knows that as soon as we get upset and emotional, we stop hearing from God. All we’re hearing is our own frustration and thoughts, and we become aggravated at everybody else. But if you want to fulfill God’s call on your life, you have to learn how to face adversity—your giants—and overcome it.

First Samuel 17 gives us a formula for defeating the giants in our lives. All the soldiers of Israel were in a valley and a giant named Goliath was threatening them. No one wanted to fight Goliath so a shepherd boy named David decided that he would slay the giant. When King Saul heard what David wanted to do, he told him it was a ridiculous idea and that he was too young. David did eventually kill the giant, and we can learn a lot about defeating our own adversaries from his story.

Ignore Criticism

The first thing you have to do is ignore the criticism and the unbelief of others. In 1 Samuel 17:32-33 (AMP), David said to Saul, “Let no man’s heart fail because of this Philistine; your servant will go out and fight with him.’ And Saul said to David, ‘You are not able to go to fight against this Philistine. You are only an adolescent, and he has been a warrior from his youth.” David responded by telling King Saul all that God could do.

Remember Victories

The second thing you have to do if you want to defeat your giants is remember the past victories God has given you. When you get in a tight spot, look back at what God has already brought you through and delivered you from. Don’t look at how far you have to go; look at how far you’ve come.

Watch Your Words

It’s also important to speak the Word and not words of defeat. In 1 Samuel 17:46-47, David tells Goliath exactly how’s he’s going to defeat him. He says, “This day the Lord will deliver you into my hand, and I will smite you and cut off your head. And I will give the corpses of the army of the Philistines this day to the birds of the air and the wild beasts of the earth, that all the earth may know that there is a God in Israel. And all this assembly shall know that the Lord saves not with sword and spear; for the battle is the Lord’s, and He will give you into our hands.”

I love the fact that David knew what he had to do. He ran to the battle line, trusting God and confessing out loud what was going to happen to the giant. See, when we put our confidence in God, we can overcome any obstacle. You can speak the Word of God and say: “I know who I am, and I know who I belong to. I am a child of the living God. Nothing will defeat me. This is God’s promise to me in His Word, and I will not do without the very best that God says that I can have. I will not give up!”

Glorifying God

Ultimately, David was totally dependent on God and gave Him all the glory. He wasn’t really concerned with what he could do because he knew what God could do. We don’t need to look at ourselves; we need to look at God and know that with Him, all things are possible.

You don’t have to be defeated by Satan’s lies, and you don’t have to quit. You can defeat your giants and see the fulfillment of your dreams. God does not want you to give up—He wants you to get up. With His help and your determination, you can finish what you’ve started!

–Joyce Meyer

Kiwango cha Mungu – Double Agent

kanisa

UTANGULIZI.

Pamoja na mabadiliko makubwa ya nyakati zetu katika siasa, uchumi utamaduni (maadili) na kidini. Mungu anacho kiwango chake ambacho ndicho anakubaliana nacho katika maisha yetu. Ili tuweze kuishi na kufiti katika mipango na makusudi yake ni lazima tuangalie kukitunza kiwango cha Mungu katika maisha yetu.

“Kwa kuwa mimi Bwana si kigeugeu (sibadiliki)” Malaki 3:6 Biblia inaonyesha kuwa tumeitwa na tumfananie Mungu na kamwe si Mungu atufananie sisi. Kwa hali hiyo kama hali yetu haifanani na Mungu wito ni sisi kubadilika na wala si Mungu abadilike awe kama tunavyotaka sisi au rafiki zetu, mazingira yetu au jamii. Biblia huonyesha kuwa sisi tunabadilishwa toka UTUKUFU hadi UTUKUFU. Mungu anatunza kiwango chake na kiwango cha Mungu kinakwenda sawa sawa na Neno lake.

Biblia huonyesha mtu hufanana na mawazo yake. “Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo…”.Mithali 23:7 (Tafsiri ya King James hutumia kufikiri badala ya kuona katika nafsi.) Neno la Mungu ni mawazo ya Mungu; kwa hiyo linamfunua Mungu vile alivyo. Ili tumfananie Mungu inabidi tulitafakari Neno lake. Ndipo litaumba picha ya ki-Mungu katika mawazo yetu. Wala tusifanye kuifuatisha dunia na kuwaza ya dunia tu.“Wakuu wa Yuda ni kama watu waondoao alama ya mpaka; nitawamwagia ghadhabu yangu kama maji” Hosea 5:10

Wito wetu ni kutunza kiwango cha Mungu. Sisi ni vielelezo. Kiwango cha Mungu kinamtambulisha Mungu wetu katika jamii kama Jehova Nissi. Yaani yeye ni bendera yetu. Mfano mzuri ni jinsi Musa katika vita dhidi ya Amaleki alivyonyanyua kiwango cha Mungu (fimbo iliyowakilisha mamlaka ya Mungu) na hapo Joshua alishinda vita. Watumishi na viongozi wa kiroho wakinyanyua kiwango hiki ambacho ni neno la Mungu kina Joshua (kanisa) wanashinda vita. Kiwango kikiondolewa kanisa na taifa hupoteza mwelekeo. Kutoka 17: 11-15

DOUBLE AGENT

Kuna watu ambao katika ujasusi( upelelezi) hufanya kazi pande zote mbili huku kila upande ukiamini unafanyiwa kazi wenyewe. Double agent anakubalika pande zote na hulipwa mshahara na pande zote. Na katika ujasusi huyu ndiye mtu wa hatari ambaye akipatikana hawezi kusamehewa. Ndani ya kanisa pia wamo double agents. Kanisa la Laodikia walionywa kuacha tabia hii mbaya.

“Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala moto (wewe ni double agent);” Ufunuo 3:15 Haiwezekani kutunza kiwango cha Mungu kisha ukaonekana kote kote. Lazima uweke msimamo na dira itakayotambulisha matakwa na kiwango cha Mungu.

Ni lazima tufike mahali tunamtambulisha Mungu katika kila hatua ya maisha yetu kwa viwango vyaUPENDOwetu,UAMINIFU, USAFI, UVUMILIVU, UKARIMU, HURUMA, UNYENYEKEVU NA UTII.Sharti ifikie hatua maisha yetu yanaakisi hali ya Mungu wetu. Hapo tunaweza kuwa manabii( wasemaji wa Mungu) kwa kizazi chetu. Watu wanaotuona wapate ujumbe wa jinsi Mungu alivyo na anavyotaka katika maisha yao. Hatuwezi kuridhia maovu na kuchukuliana na udhaifu wa dunia hii na bado tutegemee kuwa nuru. Mungu atusaidie kuwa watu wanaosimamia kiwango cha Mungu katika siku zetu na hapo maisha yetu yatakuwa na faida katika ufalme wa Mungu.

Mungu akubariki.

–Rhema Tanzania

KUSHINDANIA IMANI

.mafunzo

Historia imejaa simulizi ya watu waliotetea na kushindania imani zao dhidi ya upinzani.

Wapenzi nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari za wokovu ambao ni wetu sisi sote, Naliona imenilazimu kuwaandikia, ili mwonyane kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu. Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu waliondikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo. Yuda 1:3

Yuda anawatia moyo watu wa Mungu kusimama kidete dhidi ya ukengeufu wa nyakati zake na kuitetea imani ya kweli. Watu wenye hila waliingiza mafundisho ya uongo katika kanisa ili kupotosha imani. Inashangaza leo jinsi watu wengi wanavyojitoa kufuata na kutetea imani kengeufu na mafundisho mapotofu kuishi. Haki za mashoga, imani za waganga wa kieneyeji, kujitoa mhanga kwa kujilipua ili kutimiza jihad, maafundisho ya dini mfu zisizo na msaada kwa roho za watu zinasisitiza taratibu za nje kama kubatizwa, kuzikwa na kiongozi wa dini na sherehe mbali mbali za dini bila mabadiliko ya kweli moyoni .

Yuda anatuhimiza kuweka nguvu zetu katika imani sahihi inayoleta wokovu toka kwa kwa Bwana Yesu. Wokovu ni maisha ya imani yanayoegemea kwa Bwana Yesu na kuongozwa naye. Ni maisha ambayo Yesu Kristo ndio mhimili, maana yake ni mwokozi. Hivyo jina Yesu linaisimamia kazi aliyokuja kufanya hapa duniani. Kama vile Mkulima ni jina la kazi afanyayo mtu anayefukua ardhi na kupanda mbengu na kuzitunza hadi kuvuna mazao, kama vile mwalimu kazi yake ni kufundisha basi mwokozi kazi yake ni kuokoa. Na kwa vile alikuja hapa ulimwenguni ina maana Mungu alipenda wokovu utufikie hapa duniani. Nikisema nimeokoka maana yake Mwokozi Yesu ametenda kazi katika maisha yangu. Yesu asipookoa basi hastahili kuitwa Yesu (Mwokozi)

IMANI KATIKA YESU KRISTO NI MUHIMU SANA.

Tunaweka msisitizo mkubwa katika imani ya wokovu kwa sababu kulingana na 1 Pet 1:6 imani ya wokovu ina thamani sana. Thamani yake inathibitishwa na vipimo vya ubora ambavyo ni majaribu. Imani ya wokovu inavuka majaribuni bila kumwaibisha mwokozi. Kama dhahabu inavyopimwa kwa moto, majaribu pia huipima imani ya wokovu na kuithibitisha.

• Hii ni imani takatifu Yuda 1:20 Imani ya wokovu imebeba upekee wa Mungu. Sifa ya uaminifu, ukweli na haki. Haichanganyi uongo au hila au ukatili katika kumwabudu na mkumfuata Yesu. Imebeba upendo na huruma, uaminfu na usafi. Imani ya wokovu haikubaliani na maisha ya uovu.

• Inatolewa mara moja Yuda 1:3 Biblia hudai Kristo baada ya toleo moja dhidi ya dhambi ameketi (amepumzika).

Waebrania 10:12,26, 33-34 Samson alitengeneza na kujirudi kabisa lakini alipoteza maisha yake pamoja na kisasi cha Wafilisti. Ni vigumu sana kurudi pale ulipokwishafikia na Bwana, gharama yake ni kubwa kurudi mahali uliokuwa kwanza.

Esau alitafuta sana nafasi ya kutubu hakuipata, Yakobo akachukua nafasi yake, naye Yuda Iskariote hakupata tana ile fursa aliyopoteza na usimamizi wake akautwaa mwingine.

LEO TUNAITWA KUSHINDANIA IMANI KWA SABABU:

1. NI NGAO YA MTU WA MUNGU. Usalama wa mtu Mungu umesimama hapo. Efeso 6:16 Shetani akitaka kudhuru mtu anawinda ngao yake ili kumwondolea ulinzi. Bila ulinzi huna kinga maana kila shambulio litakupata (UKOSEFU WA KINGA YA KIROHO)

2. NDIO MKONO WA KUPOKELEA MEMA NA BARAKA TOKA KWA BWANA Yakobo 1:6,7 Marko 11:24

3. NDIO NJIA (MAISHA YA MTU WA MUNGU) Hatuenedi kwa kuona 2 Wakolosai 5:7

4. NDIYO NJIA PEKEE YA KUMPENDEZA MUNGU. Waebrania 11:6 hapa inaelezwa mfano wa Maisha ya Henoko. Huu ni mfano mzuri wa mtu aliyeishi maisha ya kumpendeza Mungu. Bwana akaenda naye. Wako wapi watakaoenda na Bwana katika nyakati zetu. IKIWA UNATAKA KWENDA NA BWANA KATIKA MAISHA YAKO ITABIDI USHINDANIE IMANI YAKO. Jiunge na watumishi wa Mungu wa nyakati zote kuitetea imani yako.

KUNA ORODHA NDEFU YA MASHUJAA WA IMANI.

Naambiwa Mathayo alitetea imani yake na wokovu hadi akauwa kwa upanga kule Ethiopia.

Marko naye katika kuihubiri imani ya wokovu aliuawa pale Alexandria Misri baada ya kuvutwa na magari ya farasi katika njia za mji.

Luka yule tabibu naye alisimama kidete kwa imani yake hadi akatundikwa katika mti wa mtende pale Ugiriki.

Yohana naye baada ya kushindikana kumwua kwa kumtupa katika mafuta yanayochemka alifungwa katika kisiwa cha Patmos.

Petro alipotishiwa kusulubiwa asipoikana imani ya wokovu aliomba asisulubiwe kama Yesu badala yake yeye awekwe kichwa chini miguu juu. Akauwa kule Roma akiitetea imani yake kwa Yesu.

Yakobo alikatwa kichwa Yerusalem lakini hakuikana imani yake.

Bathlomayo alichunwa ngozi katika mateso ya kujaribu kumfanya aikane imani.

Andrea alikusulubiwa msalabani akiwahubiri waliomsulubu juu ya uzuri wa Bwana Yesu hadi akafa.

Thomas akihubiri imani ya wokovu kule India alichomwa mikuki kule India hadi akafa.

Yuda alipigwa mishale na kufa bila kuikana imani yake,

Mathia alipigwa kwa mawe kisha akakatwa kichwa bila kuikana imani yake.

Barnaba aliuawa kwa kupigwa mawe kule Salonike na,

Paulo akakatwa kichwa na Nero kule Roma, wote hawa wakabaki wakitetea imani yao kwa Yesu.

Mimi pia sikuwahi kupata upinzani kuhusiana na imani hadi nilipookoka.

Paulo vile vile ndipo akasema “wote wapendao maisha ya utauwa wataudhiwa” 2Tim 3:12

HATUWEZI KUIKIMBIA HISTORIA, WALA HATUWEZI KUMBADILI MUNGU AU SHETANI. TUNAWEZA KUBADILIKA SISI.

Ikiwa tutasimama kuitetea imani yetu, ndipo itakapodhihirika kuwa imani yetu ina thamani na ubora wake kufunuliwa.

Mungu akubariki

–UCF Bukoba

Ijue Vita yako – 1

vita

IJUE VITA YAKO

UTANGULIZI:

Biblia hutueleza kuwa mkristo anayo vita anayopaswa kupigana katika maisha haya. Ingawa vita si jambo linawafurahisha watu wengi, hata hivyo biblia inasema kwa mkristo haiepukiki. Hii ni kwa vile Mungu anawatafuta washindi. Ni lazima adhihirishe kuwa watu wake wana uwezo zaidi kama ikilinganishwa na watu wengine wowote. Katika kitabu cha mwisho cha biblia Ufunuo tunaona Bwana Yesu akifurahi kuwapokea washindi kukaa nao milele.

Hata hivyo biblia hutuasa kuwa vita hii si ya jinsi ya kibinadamu yaani ya mwilini.

Efeso 6: 12 Kwa maana kushindana kwetu si juu ya nyama na damu, bali dhidi ya falme, mamlaka, dhidi ya wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

2 Wakorintho 10: 3 Ingawa tunaishi duniani lakini hatupigani vita kama ulimwengu ufanyavyo. 4 Silaha za vita vyetu si za mwili, Bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome. 5 Tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo,

KUILEWA VITA YA KIROHO.

Kuilewa vita ni hatua muhimu kama utaweza kuishinda. Ndio maana katika dunia hii majeshi yote makini hutoa elimu ya vita. Unapojiandikisha tu kuingia jeshi unapimwa afya na kupekwa katika mafunzo ya awali. Hapo katika ukuruta (recruit) unafundishwa mambo ya msingi hasa nidhamu ya kijeshi na mbinu za vita. Baada ya kuhitimu hapo mafunzo zaidi ya kitaalamu ya jeshi hufuata. Katika elimu ya ufundi wa kivita (Military technology and equipment). Huko kuna elimu ya mawasiliano ya kivita, elimu ya ngome za kivita, roboti za kivita, zana za usafarishaji, mavazi ya kinga ya kivita n.k

Biblia inatufundisha kuwa aina ya vita ya kiroho ambayo ni tofauti na ile ya kimwili. Nayo vita ya kiroho ina shule yake ya kujifunzia vita.

Zaburi 18: 34 “Huifundisha mikono yangu kupigana vita, mikono yangu inaweza kupinda upinde wa shaba.”

Daudi alifundishwa na Mungu mwenyewe vita. Unaweza kuona alikuwa akiingia katika ulingo wa vita na maadui wa kidunia; lakini Daudi alikuwa juu yao wote. Mikono yake lipinda upinde wa shaba na akawafuatia maadui na kuwapata. Watu wengi walimwona Daudi kama mtu shujaa. Lakini Daudi alijua siri ya ushujaa wake ni Bwana.

Ukielewa vizuri nafasi yako katika vita ya kiroho, leo hii utatangaza vita juu ya vita ya shetani. Bado nakumbuka Nyerere alivyotangaza vita ya Kagera mwaka 1978. Nilikuwa nasikiliza redio akatoa hotuba akiwa Nachingwea “ …huyu mtu Amini, ameua watu wengi. Mtu huyu ni mshenzi, ameua watu wengi. Na sasa tutampiga. Uwezo wa kumpiga tunao, sababu ya kumpiga tunayo na nia ya kumpiga tunayo. Na sasa tutampiga!” Leo ufike mahali pa kumtangazia shetani sasa nitakushikisha adabu! Je utapambana vipi na maadui zako?

JE UNAWAJUA MAADUI UNAOPASWA KUWASHINDA?

Kama utafanikiwa vitani ni lazima umjue kwanza adui unayekabiliana naye na mbinu zake dhidi yako. Je unafahamu kuwa katika vita hii hupaswi kupambana na shetani? Hapo wengine mnagutuka, kama sikupambana na shetani nitapambana na nani!? Nami ndilo swali langu unamjua unayepaswa kupambana naye? Hatukuitwa kupambana na shetani. Yesu amepambana na shetani. Yesu alipokuja katika ulimwengu huu alisema huyu shetani ni saizi yangu. Aliwaacha kina Petro wakalala usingizi, alishughulikia tatizo hili yeye mwenyewe. Biblia yangu huniambia alichukua mwili ili afananishwe na hao aliotaka kuwatoa katika makucha ya shetani.

Waebrania 2:14 Basi kwa kuwa watoto wana nyama na damu, Yeye pia alishiriki katika ubinadamu wao, ili kwa kifo chake, apate kumwangamiza huyo mwenye nguvu za mauti, yaani, Shetani, 15 na kuwaweka huru wale waliokuwa utumwani maisha yao yote kwa sababu ya kuogopa mauti.

Tafsiri ya union version hutumia neno kumharibu badala ya lile la kumwangamiza. Je ina maana Yesu alikuja kumwua shetani? Tunajua hata mashetani alipomwona Yesu alishtuka na kung’aka; “umekuja kututesa kabla ya muhula wetu?” (Mathayo 8:29)hivyo neno kuharibu au kuangamiza hapa halina maana ya kuua. Tafsiri yake ya neno la kiyunani katargeo humaanisha:- isiyofaa (useless), zezeta (to be entirely idle),a kushindwa(fail), poteza (loose) fanya kuwa bure kabisa (bring to naught), ondosha (put away), tupu (void). Hivyo waweza kuona shetani amedhoofishwa mbele zako mithili ya simba mgonjwa aliye mahututi. Ingawa kwa wasiojua kilio cha maumivu ya simba mgonjwa huwafanya watimue mbio.

Angalia Wakolosai 2: 14 akiisha kuifuta ile hati yenye mashtaka yaliyokuwa yanatukabili pamoja na amri zake, aliiondoa isiwepo tena, akiigongomea kwenye msalaba Wake. 15 Mungu akiisha kuzivua enzi na mamlaka, alizifanya kuwa kitu cha fedheha hadharani kwa kuziburuta kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba wa Kristo.

Biblia hutuonyesha kuwa Bwana Yesu katika kifo chake aliteka mateka. Mstari wa 15 anaposema “akiisha kuzivua enzi na mamlaka…” hapa hamaanishi alikuwa amevaa enzi na mamlaka, kisha katika hatua fulani akazivua katika mauti yake msalabani. Tafsiri ya biblia ya Amplified husomeka hivi “ (Mungu) alizinyang’anya enzi na mamlaka…zana zote za kivita (kama mateka) na kuzifanyisha hizo enzi na mamlaka gwaride la aibu linalodhihirisha kushindwa …” Kwa hiyo katika kifo chake, Yesu alivunja uwezo wote wa shetani juu yako. Aliteka kama majenerali wafanyazo vitani, na kisha akamvua adui silaha zake zote na kumdhalilisha hadharani kwa gwaride. Je wewe unashangilia unapoona maandamano haya; Bwana Yesu ametangulia na shetani akiwa peku peku bila mkanda, amevuliwa vyeo vyote, ameweka mikono kichwani na akizomewa kila mtaa maandamo yanakopita. Je unaogopa kuwa labda shetani akikuona unashangilia anaweza akakata kamba azizofungwa na Bwana Yesu akakukimbiza? Baadhi ya wakristo hufikiri hivi, Hawataki shetani awaone wakimzomea hata kama Yesu ametagulia mbele ya maandamano!

Hivi nikuulize swali, unaamini kweli kuwa Yesu alimshinda shetani. Na kuwa shetani tayari ameshindwa. Na sasa kama ameshindwa tayari je una vita ya kupambana naye? Bado utasema nina pambana na shetani? Nafikiri wakristo wengi vita yao dhidi ya shetani inafunua ujinga wa neno la Mungu uliomo ndani yao. Vita hiyo ni vita isiyokuwa ya lazima. Shetani alikwisha shindwa na Bwana Yesu.

Vita yetu sisi ni vita ya imani.

2 Timotheo 4:7.

7 Nimevipiga vita vizuri, mashindano nimeyamaliza, imani nimelinda.

Mtume Paulo akimwandikia Timetheo aliweka wazi aina ya vita waamini waliyo nayo. Paulo hakusema nimepiga shetani, lakini alisema imani nimeilinda. Vita yetu ni ya kulinda imani. Shetani atajaribu kuishambulia imani yako ili akufikie. Kinga uliyo nayo ni imani yako. Mtume Paulo katika Waefeso 6 anasema imani ni ngao inayozima mishale yote ya moto ya yule mwovu. Kwa hiyo tunajua vita mtume Paulo aliyopigana ilikuwa ya kulinda imani yake.

1 Timetheo 6:12,

12 Pigana vile vita vizuri vya imani. Shika uzima wa milele ambao ndio ulioitiwa ulipokiri ule ukiri mzuri mbele ya mashahidi wengi.

Vita ya imani ndiyo vita uliyoitwa kupigana. Shetani hawezi kabisa kukugusa, wewe unalindwa mikononi mwa Mungu. Uhai wako umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. Wewe tayari ni mshindi na zaidi ya mshindi. Haya yote yamefanikishwa na Yesu. Shetani anachoweza kufanya kwako ni kukuondolea imani yako. Ngao uliyopewa na Mungu ni imani yako. Shetani hawezi kupenya kama kuna imani. Hivyo anachojaribu kufanya ni kukunyang’anya imani yako. Hapo imani yako ikiondolewa utakuwa dhaifu kama wanadamu wote. Utakuwa mhanga wa matukio ya kila siku, utakuwa mhanga upepo unaovuma duniani. Kama ni magonjwa ya mlipuko nawe hutakosa, kama ni msimu wa ugumu wa uchumi nawe utakuwemo. Wasi wasi wa kutopata kabisa mwenzi nawe utakuwa nao. Hali mbaya zinazowatisha watu wote nawe zitakutisha! Kisa? Imani yako imepokonywa!

1 Petro 5: 8 Mwe na kiasi na kukesha, maana adui yenu Ibilisi, kama simba angurumaye huzungukazunguka akitafuta mtu ili apate kummeza. 9 Mpingeni huyo mkiwa thabiti katika imani, siyo mpigeni bali mpingeni

Katika Petro neno linalosema mpingeni, humaanisha pia:- mkatalie, msikubaliane naye, msimfugulie njia, muwe na msimamo dhabiti dhidi yake. Vita unayopaswa kupigana ni ile ya kutunza imani kwa Mungu wako. Kuwa na uhakika kuwa kila alichosema ndivyo kitakavyo kuwa. Kujua kuwa Yesu anachosema juu yako kaatika biblia ndiyo kweli. Kulichukulia neno la Mungu kuwa ni sahihi.

Kwa mfano kama neno la Mungu linasema “ Ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka” Warumi 10:9 unakubaliana na hilo neno katika maisha yako. Unasema kwa vile nimemkiri Yesu kwa kinywa change, nikimaanisha kabisa toka moyoni kuwa ndiye Bwana wa maisha yangu. Nimeamini kabisa kuwa Yesu alifufuka katika wafu. Hivyo nimeokoka. Sihitaji ushahidi zaidi, tayari neno la Mungu linatangaza kuwa nimeokoka, na ndivyo nilivyo! Haleluya nimeokoka. Lakini ukianza kusema zamani nilikuwa najisikia vizuri moyoni ila siku hizi sijui bado nimeokoka au la! Mbona majaribu yangu na shida zangu zimekuwa nyingi. Hivi kweli nimeokoka. Hapo tayari utakuwa njiani kushindwa maana imani yako juu ya wokovu imechukuliwa.

Au unasoma 1 Petro 2:24

“Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa. Maneno haya haya yanatoka katika Isaya 53:5

“Bali alijeruhiwa kwa maskosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu, adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.

Na yamerudiwa Mathayo 8:17

“ ili litimie neno lililonenwa na nabii Isaya akisema. Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu. Na kuyachukua magonjwa yetu.”

Kutokana na maneno haya unaona Petro mwandishi wa mwisho katika mlolongo anatumia usemi wa wakati uliopita “na kwa kupigwa kwake mliponywa” sio mtaponywa au mnaponywa. Maana jambo lilikwishatendeka. Wakati mmoja nilipokuwa naomba juu ya jambo hili Roho mtakatifu alinionyesha kuwa mstari huu sio ahadi. Mstari huu wa 24 katika 1 Petro 2 ni ripoti ya tukio lililokwisha tendeka. Ni ukweli ulio katika kumbukumbu. Unaweza kukubaliana nao au ukaupinga lakini hautabadilika. Ni jambo lililokwisha tendeka. Faili limefungwa.

Unaweza kuanza kushindana na neno hili ukisema mbona sasa mimi bado sijapona? Unaweza kusema mambo haya yanasikika vizuri lakini ki matendo ni magumu. Lakini ukweli ni kuwa Yesu alipochapwa mijeledi na kujeruhiwa katika mwili wake akaumizwa, maumivu yale yalibeba maumivu yote ambayo yamekuwa yakiwatesa watu katika magonjwa. Tayari alikwisha yabeba. Na hapo kwa nini wewe uyabebe tena mara ya pili. Unaweza kufungua biblia yako na kusema hivi ndivyo nilivyo. Nimponywa pale Yesu alipopigwa katika kusulubiwa kwake. Magonjwa si sehemu ya maisha yangu. Nimeponywa kwa mapigo ya Bwana Yesu. Halleluya.

MAADUI WA IMANI YAKO.

Maadui unaopaswa kukabiliana nao ili kuilinda imani yako isipokonywe ni:-

1. MASHAKA JUU YA KILE MUNGU ANACHOSEMA JUU YAKO.

2. TARAJA

3. MAUNGAMO KINYUME NA UKWELI ANAOSIMAMA NAO KRISTO KAMA WAKILI

4. MATENDO YANAYOPINGANA NA IMANI YAKO

5. HOFU

Tutawaagalia maadui hawa mmoja mmoja na jinsi ya kukabiliana na kila mmoja wao kwa ushindi. Mtume Paulo alipambana nao wote akawashinda. Baada ya ushindi huu ndipo anasema “ 7 Nimevipiga vita vizuri, mashindano nimeyamaliza, imani nimelinda.”

–Unity Christian Fellowship – Bukoba

Kwa watu wa Mungu!

mwilii

Watu wa Mungu, ashukuriwe Mungu atupaye uzima na ya kwamba tu hai tena kwa neema yake.

Tunalo la kujivunia lakini si katika miili hii tuliyo nayo bali kwa kuwa tumeipata neema ya Jehova.

Ndugu wapendwa imetupasa kuwa na juhudi sana kuzidi sana katika kulijua Neno la Mungu ili tuwe na hakika na ushindi katika hatari nyingi za dunia.

Maana ”dunia” inasema inayo mazuri, lakini si mbele za Mungu, maana ifahamike hivi; yaliyo yote mazuri duniani ni yaliyo mabaya mbele za Mungu na yaliyo mabaya mbele za Mungu ni yaliyo mazuri kwa duniani, basi kila mtu na asema na akili yake mwenyewe.

Kwa hali hiyo basi; sisi tulio kwa Mungu sawa sawa twajua hivi, kheri uongo wa Mungu kuliko ukweli wa dunia, maana ikiwa kwa uongo huo wa Mungu sisi tu hai rohoni tukiiponya miili hii, basi una faida gani ukweli wa dunia ambao kwa huo tumehitirafiana sisi kwa sisi?

Nasema tena ikiwa kwa uongo huo wa Mungu hatukuwa wazinifu, naam hatujawa walawiti, hatujawa waasherati, hatujawa wafiraji, je si zaidi basi ya huo ukweli wa dunia ambao katika huo tu wanafiki?

Mwaonaje ninyi,
Maana si kwamba hatuoni ama hatusomi alama za kuenenda kwetu na kuishi kwetu maana kila mmoja wetu yu barozi na shahidi wa nyendo zake mwenyewe, jifunzeni katika hili.

Sikia yupo mmoja aweza sema amemaliza kwa sababu ya huu tuuitao wokovu lakini asijue ya kwamba yu apaswa kutambua wokovu ni mbegu iishiyo katika tunda bovu ambalo ni mwili wake mwenyewe.

Maana miili ni kikwazo sana katika maisha ya kuuishia haki, maana tumeokoka ndiyo lakini hatujaihama miili hii.

–Mwamfupe Anyisile

Hatua kwa Hatua na Bwana

hatua

Amani ya Bwana iwe nanyi enyi nyote,   Baraka nyingi za Kiroho na Kimwili tayari tunazo na zinajidhirisha ktk macho ya nyama na rohoni lakini pia zile zinazofahamika kama kubwa-kubwa tunazotakaga sana,  ni zetu ila kama hazijajidhihirisha, usipate shida ya kunyong’onyea moyo maana Mungu wetu huenda nasi hatua kwa hatua ktk kutupatia mema   Kumbukumbu la Torati. 7:1,6,7,8,20,22,23…1Bwana, Mungu wako, atakapokutia katika nchi uendayo kuimiliki, atakapoyang’oa mataifa mengi watoke mbele yako, Mhiti, na Mgirgashi, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, mataifa saba makubwa yenye nguvu kukupita wewe; 6  Kwa maana wewe u taifa takatifu kwa Bwana, Mungu wako; Bwana Mungu wako, amekuchagua kuwa watu wake hasa, zaidi ya mataifa yote walioko juu ya uso wa nchi. 7Bwana hakuwapenda ninyi, wala hakuwachagua ninyi, kwa sababu mlikuwa wengi kuliko mataifa yote, maana mlikuwa wachache kuliko watu wote; 8  bali kwa sababu Bwana anawapenda, na kwa sababu alitaka kuutimiza uapo wake aliowaapia baba zenu, ndiyo sababu Bwana akawatoa kwa mkono wa nguvu, akawakomboa katika nyumba ya utumwa, katika mkono wa Farao, mfalme wa Misri. 20  Tena Bwana, Mungu wakoatampeleka mavu kati yao, hata hao watakaosalia, hao wajifichao, waangamie mbele zako. 22  Naye Bwana, Mungu wako, atayatupia nje mataifa yale mbele yako kidogo kidogohaikupasi kuwaangamiza kwa mara mojawasije wakaongezeka kwako wanyama wa mwitu..   Kutoka.23:29-3029.Sitawafukuza mbele yako katika mwaka mmojanchi isiwe ukiwa, na wanyama wa bara wakaongezeka kukusumbua. 30Nitawafukuza kidogo kidogo mbele yako, hata utakapoongezeka wewe, na kuirithi hiyo nchi.   Mistari ya 22 na 30(Kumbu na Kutoka) kuna neno KIDOGO-KIDOGO, in English Biblia nyingi zimetumia adverb - little by little maana yake ‘a little bit at a time, ‘by small degrees or increments’, ‘gradually, ‘by small degrees or amounts,  ‘piece by piece, ‘progressively, ‘slowly. Kwaiyo ni sawa sawa na kusema kwa hakika kua Mungu alisema  kua atayatoa mataifa nje kidogo-kidogo au kidogo kidogo kwa muda fulani halafu tena kidogo-kidogo kwa muda tena mwingine au pole-pole au hatua kwa hatua au kipande kwa kipande au kwa kiasi kichache-chache  ili hatimaye Israeli kurithi nchi yote wakati wakiwa nao wana Israel wanaongezeka  Kinyume cha neno Kidogo-kidogo(little by little) ni kikubwa-kikubwa-kwa Kiswahili kisichofasaha au maana  ghafla, kushitukiza, haraka-haraka,  ya kasi nk. kwa ivyo tunaweza sema kwa hakika kua Mungu alisema  kua HATAyatoa/fukuza mataifa yale haraka-haraka,Ki-ghafla, kwa mshitukizo,kwa kasi nk. Kwa nini Hatayatoa haraka-haraka katika mwaka mmoja bali kidogo-kidogo- little by little? AU… SWALI KUU: Unadhani Kibiblia na kiuzoefu wako na Bwana ktk kutembea na kumtumikia, kwa nini Mungu ameonekana kua ni Mungu wa hatua kwa hatua, hana presha na time? Kuna mambo gani katikati hapo tunapata/Mungu anakusudia tupate before His full visible manifestations on us?. Maandiko ya Msingi kwa soma hili yamesema sababu 2 nazo ni:  

 • · Nchi itakuwa ukiwa,wasije wakaongezeka kwako wanyama wa mwitu/bara wakakusumbua. Yaani NCHI/BARAKA NILISHAWAPA SIKU NYINGI NILIPOKUJA KUWAOKOA- Kutoka.3:8,16-17 na kwa kua Mungu   hutangaza mwisho tokea mwanzo-Isaya 46:10, ivyo baraka alishaindaa na kuitamka kua ni yao ila KUIDHIHIRISHA/KABITHI ni kidogo-kidogo/hatua kwa hatua, maana atakua anawatimua Mataifa upande mmoja wa Nchi kisha watamalaki LAKINI upande wa mwingine wa Nchi, Mataifa mengine yanakuwepo yakingoja kufukuzwa ila yanasaidia kutuza Nchi, uwepo wao huko usababishe wasizaliwe wanyama mwitu ikawapa tabu Wana wa Mungu  ktk kutamalaki , ivyo hapa anawatimua, wanatwaa, kule wanabaki kwa faida yao 

 • Wao Wana wa Israel pia Waongezeke ktk Nchi…Kutwaa baraka kunaambatana na kuongezeka = KUKUA( Imani, utakatifu, maombi, utumishi, kicho, Utii, Unyenyekevu, mahusiano,Uvumilivu, Heshima kwa Mungu, Kujua kuisikia Sauti yake,Tabia kubadilika…jumla ya yote ni KUUKULIA WOKOVU

Kwa hiyo, Baraka zile kubwa-kubwa tunazotakaga sana, ziwe za Kiroho or Kimwili, zipo, ni zetu ila ni hatua kwa hatua na Bwana, kidogo-kidogo na Bwana, tuvumilie kwa furaha tuki- Kumbe kuna baraka nyingine zinakua delayed but not denied…zinatimia polepole(kutowatoa Mataifa yale kwa mwaka mmoja) uku jaribu lile lile (mataifa yale) yanayoonekana kuleta tishio kwa baraka yenyewe(nchi kurithiwa), linafanyika baraka tena yaani Mataifa yale kuachwa ili kuzuia wanyama wasiongezeke wasijekuwasumbua kwa kua nchi itakua ukiwa/tupu. Kwa hiyo uwepo wa jaribu/tatizo ni udhirisho dhahiri wa kuja/kuwepo kwa baraka Dondoo za Kukazia kuhusu Hatua kwa Hatua na Mungu yaani ‘’kidogo-kidogo’’ na si ‘’Kikubwa-Kikubwa’’/’’Kiharaka-haraka’’   Unakumbuka ilimchukua MUSA miaka mingapi toka kukua ndani ya jumba la kifalme kuja kua mchunga mifugo kisha kua Mkombozi wa Wana-Israel? Remember, Step by step na Bwana, twende naye tu  taratibu   Unakumbuka ilimchukua Mungu siku ngapi kuumba uilimwengu? Kwani si ana nguvu zote, si nikusema/kutamka tu mara moja na vyote kwa sekunde au chini ya sekunde vinatokea kwa ukamilifu wote kwa kua ana uweza WOTE kabisa, kwanini siku 6? Remember, Step by step na Bwana, twende naye tu  taratibu na kwa utaratibu wake   Unakumbuka ilimchukua Mungu mapigo mangapi ili hatimaye Pharao kuachilia wapendwa? Si angemtandika tu ‘’kik moja’’ maridadi kabisa ikawa movie THE END?Remember, Step by step na Bwana, twende naye tu  taratibu   Unakumbuka ilimchukua Daudi muda gani toka machungani kuja kumiminiwa mafuta mpaka kukalia kiti kwa hakika? Remember, Step by step na Bwana, twende naye tu taratibu   Unakumbuka Daudi  alivyo muombea maombi ya aina gani mwanae Selemani wakati anakua mfalme na kua alihitaji kupata  uzoefu kwanza ,so he needed people close to him for guidance? Remember, Step by step na Bwana, twende naye tu  taratibu   Unakumbuka ilichukua muda gani toka kua Petro wa leo kiroho kesho kukana mpaka kua Petro kiongozi na mtumishi imara? Remember, Step by step na Bwana, twende naye tu  taratibu   Unakumbuka ilimchukua Yesu miaka mingapi kabla hajajitokeza rasmi kuanza kazi wazi wazi? Why would He have to live 30 yrs ndipo atokeze kikwelii? Remember, Step by step na Bwana, twende naye tu  taratibu.

Press on,

Edwin Seleli

Vuka Historia Yako

conieee
Bwana YESU Asifiwe, kwanza nataka ujue kuna watu HISTORIA ya Maisha yao imesimama hapo hapo haiendi mbele wala hairudi Nyuma,Wakati Mwingine hali hii imesababisha hata watu wako wa karibu waone hiyo ni historia yako siku zote..Lakini nataka nikuambie HISTORIA HIYO leo inakwenda kubadilika,Watu wa karibu walimuona yule RAHABU kama ni kahaba aliyeshindikana na hata ndugu walikuwa wanamtegemea yeye na kazi ile ya Ukahaba,Ni kweli Rahabu alikuwa na msaada mkubwa sana kwa ndugu zake,lakini msaada ule ulikuwa na dosari (Shetani ndiye alikuwa anahusika) Rahabu alipochukua hatua ya kumsogelea MUNGU,MUNGU akambadilisha (Yoshua 6:25) “Lakini Yoshua akamhifadhi Rahabu,yule kahaba,na watu wa nyumba ya baba yake,na vitu vyote alivyokuwa navyo naye akakaa kati ya Israel hata leo;kwa sababu aliwaficha wale wajumbe aliowatuma Yoshua ili kuupeleleza mji wa Yeriko”..

Ukiusoma huu mstari kwa umakini utaona Kupitia Rahabu nyumba nzima waliokoka, Biblia inatuambia akakaa kati ya Israel hata leo (Maana yake akahesabiwa ni kizazi cha Israel) Hujanielewa? Ebu soma hapa (Waebrani 11:31) “Kwa imani Rahabu,yule kahaba,hakuangamia pamoja na hao walioasi;kwa kuwa aliwakaribisha wale wapelelezi kwa amani” Unaweza ukaona Rahabu alifanya kitu kidogo sana lakini kwa MUNGU ni kikubwa sana…MUNGU akaona vema Amuweke Rahabu katika kundi la wazee wa IMANI (Waebrania 11:39) “Na watu wote hao wakiisha kushuudiwa kwa sababu ya imani yao”

Ebu leo Vuka historia yako “Bwana yu pamoja nawe Ee shujaa (Waamuzi 6:12b) Vuka Historia yako leo,yawezekana una ugonjwa ambao waliumwa Babu/Bibi zako au Baba/Mama zako,yawezekana unahistoria ya kujikaata kuwa wewe haufahi au kuna dhambi umetenda unaona ni vigumu kurudi kwa MUNGU….Sikia nikwambie MUNGU anasamehe..Rudi leo….Rahabu aliporudi kwa MUNGU Historia MPYA ilifunguka katika maisha yake.

–Conrad

Yesu asema na John Mulinde!

mulindejohn

Bwana asifiwe wapendwa

Nawasalimu nyote kwa Jina la Yesu Kristu.

Naombeni mkipata nafasi msikilize huyu mtumishi wa Mungu kutoka Uganda anaitwa John Mulinde

“After working in the power of the Holy Ghost and seeing signs, wonders and miracles, JOHN MULINDE was an Evangelist fully sure of his Salvation. But when JESUS revealed himself to him, he was shocked of what he was told.”

Mungu alimonyesha maisha yake ya ndani na kwa uhakika alimwambia kuwa kama angerudi wakati ule anauhakika angebaki.

Sikiliza mtu wa Mungu na Bwana atusaidie. tumuombe atupatie Roho ya Toba na tumuangalie yeye katika maisha yetu. tumuombe atufunulie siri za Neno lake ili tumjue yeye aliyetupenda hata akamtoa Mwanae Yesu ili aturudishe kwake

Kama Daudi alisema ‘funua macho yangu nione uzuri wa maneno yako’ 

Utakatifu ndo tunatakiwa kukimbizana nao maana bila huo hatutaweza kumuona Bwana. na hatutaweza kwa nguvu zetu wenyewe ndo maana Yesu akatuahidi Roho wa Mungu ili akae ndani yetu na atuongoze. 

Naomba nisiseme sana, niwaache msikilize halafu basi mtaleta maoni yenu tuweze kujengana.

Kama ukishindwa kufungua hiyo link basi nenda youtube na u-type 

 

shocking message from Jesus to John Mulinde. imepandikwa na Yves YN Nahishakiye

Mubarikiwe wapendwa.

-CM

Ukombozi sio tukio ni safari!!

Pastor Carlos Kirimbai.

Kuna wimbi kubwa sana la huduma za ukombozi ambalo limeibuka katika siku za hivi karibuni. Zingine ni halisi lakini nyingi sio hata kidogo. Sasa sio nia ya post hii kuhukumu huduma ya mtu maana sina mamlaka hiyo ila ni nia ya post hii kusaidia japo kwa sehemu kuwa na msingi wa kimaandiko kwa ajili ya huduma ya ukombozi. Nisingependa kuingia katika unaga ubaga wa kama ukombozi ni sahihi kwa walio okoka au la ila ningependa kuweka chini msingi wa kimaandiko wa huduma ya ukombozi. 

Ninaposoma maandiko, kwanza kukombolewa ni jambo ambalo limewekwa ndani ya package ya wokovu.

Pia huu ukombozi sio jambo ambalo linatokea tu mara moja bali ni jambo ambalo linajidhihirisha katika maisha ya mtu kwa kadiri anavyokua katika kuijua kweli na kutembea katika hiyo.

Yesu alisema maneno haya:

Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru. (YN. 8:31, 32 SUV).

Yesu alikuwa anasema na watu waliyomwamini. Ukisoma alichowaambia ni wazi kuwa Yesu alikuwa anadhihirisha kuwa kumwamini ni mwanzo tu wa safari. Yale uyafanyayo baada ya kumwamini ndo yanaamua ubora wa maisha katika Yeye utakayofurahia. Ukimwamini alafu huendelei katika neno Lake kuna kiwango cha uhuru katika Yeye hutafurahia. Na ni wazi huu uhuru anaouzungumzia hapa hauji kwa njia ya kumwamini tu bali unakuja kwa njia ya kuijua kweli Yake na kuiishi pia.

Sasa wengi wetu katika huduma ya ukombozi tunawafunza tu watu kufunguliwa na vifungo vya adui, kuvunjiwa laana nk bila ya kuweka msisitizo wa kuishi maisha ya kulisoma neno na kuliishi neno. Yesu aliweka wazi TUTAIJUA KWELI NA HIYO KWELI ITATUWEKA HURU. Uhuru wowote unaokuja katika maisha ya mwamini unatunzwa na kweli aijuaye na kuiishi. Sasa sijajua katika huduma za ukombozi kama msisitizo huo unawekwa. Maana watu wanaenda tu kuombewa ambayo sio mbaya lakini hawawajibiki binafsi na maisha yao na matokeo yake huduma ya ukombozi badala ya kuwasaidia ndo inawaharibu.

Kwanini nasema hivyo.

Soma haya maneno ya Yesu hapa:

Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate. Halafu husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa. Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya. (MT. 12:43-45 SUV).

Sio mimi nimesema maneno haya. Ni Yesu ndo kayasema. Pepo likishatolewa kwa mtu kwa njia ya huduma ya ukombozi, litaenda alafu kuna siku litarudi. Kama huyu mtu aliyetolewa mapepo hajajua jinsi ya kujipanga anaweza akawa amejiweka katika hali ya hatari sana. Kinachomfanya pepo arudi alipotoka ni pale ajapo na kukuta nyumba imefagiwa na kupambwa lakini tupu. Ni ule utupu wa maisha ya mtu ndo unamweka katika hali ya hatari sana. Kinachoweza kujaza maisha ya mtu sio maombi endelevu na huduma endelevu ya ukombozi ni neno la Mungu na neno la Mungu peke yake.

Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. (KOL. 3:16 SUV).

Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi. (ZAB. 119:11 SUV).

Hatuwezi kukwepa wajibu wa kulijaza neno la Mungu ndani ya maisha yetu.

Na halijai kwa kulisoma tu linajaa kwa kulisoma na kuliishi.

Sijui kama tunaona jinsi ilivyo hatari kufunguliwa kwa njia ya maombi peke yake bila msisitizo kuwekwa katika maisha ya usomaji na kuliishi neno.

Hali ya mwisho ya huyu muathirika au mhanga ni mara saba mbaya kuliko ya kwanza.

Katika agano la kale ambalo ni kivuli cha agano jipya, Mungu aliwaambia wana wa Israel maneno haya:

Nami nitapeleka mavu mbele yako, watakaomfukuza Mhivi, na Mkanaani, na Mhiti, watoke mbele yako. Sitawafukuza mbele yako katika mwaka mmoja; nchi isiwe ukiwa, na wanyama wa bara wakaongezeka kukusumbua. Nitawafukuza kidogo kidogo mbele yako, hata utakapoongezeka wewe, na kuirithi hiyo nchi. (KUT. 23:28-30 SUV).

Cjui tunaona hayo maneno. Mungu anasema hatawaondoa wote mara moja. Ukweli ni huu japo unauma. Huwezi tu kwenda mahali na matatizo yako yoooooote yakaondoka mara moja. Ondoa dhana ya kuwa nitaenda mahali kuombewa, kutolewa mapepo, sijui kufanyiwa ukombozi na matatizo yangu yataisha. Mungu mwenyewe anasema hatayaondoa mara moja maana akifanya hivyo wanyama wa bara wataongezeka kukusumbua. Yaani ni kama kuyaondoa matatizo yote mara moja ni kufungulia matatizo makubwa zaidi. Yeye anaahidi kuyaondoa kidogo kidogo kwa kadiri sisi tunavyoongezeka na kuirithi nchi aliyotupa au ahadi alizotupa. Kuongezeka katika kimo ni muhimu mno.

Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu; (1 PET. 2:2 SUV).

Kuongezeka au kuukulia wokovu ni matokeo ya neno na neno peke yake linaloingia maishani mwako kwa njia ya kulisoma, kufundishwa na hatimaye kuliishi. Ndipo unaanza kukua kiroho. Na matokeo ya kukua kiroho ni:

Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu rohoni, akakaa majangwani hata siku ya kutokea kwake kwa Israeli. (LK. 1:80 SUV).

Kwa kadiri unavyokua ndivyo unavyoongezeka nguvu rohoni.

Angalia maneno ya Paulo kwa wazee wa kanisa la Efeso:

Basi, sasa nawaweka katika mikono ya Mungu, na kwa neno la neema yake, ambalo laweza kuwajenga na kuwapa urithi pamoja nao wote waliotakaswa. (MDO 20:32 SUV).

Neno la Mungu unapolisoma, kufundishwa na kuliishi ndilo linalokujenga na ndilo linalokupa urithinpamoja na wengine waliyotakasea kama wewe.

Tumeweka msisitizo mkubwa kuliko kwenye huduma ya ukombozi, kuvunja laana na kutoa mapepo bila ya kuweka mkazo wa kutosha katika kuwajibika binafsi katika kulisoma neno, kupata mafundisho sahihi na kuishi kila kinachofunuliwa kwetu tusimapo na tufundishwapo. Iko kama tunainua kizazi cha watu waliyookoka ambao hawapo tayari kulipa gharama ya kulijua na kuliishi neno ili kutembea katika ukamilifu wa uhuru ambao Yesu alienda msalabani kuununua kwa ajili yao.

Kila aliyeokoka ni mrithi pamoja na Yesu wa ahadi zote za Mungu. Lakini kama Paulo asemavyo:

Lakini nasema ya kuwa mrithi, wakati wote awapo mtoto, hana tofauti na mtumwa, angawa ni bwana wa yote; (GAL. 4:1 SUV).

Mrithi anapoendelea kuwa mtoto, hata afanyiwa huduma ya kufunguliwa kiasi gani, hata avunjiwe laana kiasi gani, hata atolewe mapepo kiasi gani, ataendelea tu kuwa kama mtumwa ingawa ni Bwana wa yote. Tumeitiwa kuwa bwana wa yote lakini adui mkubwa wa kutuzuia tusiyaone hayo sio mapepo, sio laana sio vifungo. Ni utoto. Na utoto ni matokeo ya kutoijua na kuiishi kweli.

Kama tunataka kuona ubora wa uzima ambao Kristo aliulipia pale msalabani ukiwa halisi maishani mwetu, tuache kukimbizana na huduma hii na ile na ile tukidhani kuna moja itaweka majibu yote mikononi mwetu tena kwa kuombewa tu na maombezi. Tulia mahali ambapo unajua Mungu amekuweka, tia mizizi yako chini hapo na kua katika kumjua Yeye na utaona uhru wako ukiachiliwa katika maisha yako hatua kwa hatua.

Nimalize kwa maneno haya ya Yesu:

Basi wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki. Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. Kwa kuwa po pote ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai. (MT. 24:26-28 SUV).

Yesu hapa anatuonya kuhusu kichaa kitakachoibuka siku za mwisho za watu kuambiana yupo huku, au kule au pale. Yesu keshasema tusiwasadiki. Alafu akasema maneno magumu sana ambayo sijui kama huwa tunayaelewa, akasema palipo na mzoga, tai hukusanyika. Kiswahili chetu hakikutenda haki hapa. Maana isemapo tai unaweza haraka ukafikiri ni yule ndege kwa kiingereza tunamwita eagle lakini ndege anayetajwa hapa ni vulture ambaye ni ndege ambaye anasekiaga harufu ya mizoga au kuna namna anajua mnyama anapokaribia kufa alafu wanasogea. Hawa ndege hawali vilivyo hai. Wanakula tu vulivyokufa. Ni mbaya sana mzoga unapokusanya na bahati mbaya mzogo haukusanyi ila ndege na wanyama waliyo maarufu kwa kula mizoga. Huko kukimbia kimbia kwako usije ukawa msaka mizoga.

Sasa kusema hivyo haimaanishi kuwa kila palipo na uwingi wa watu kilichowakusanya ni mzoga. Hapana. Kuna huduma nyingi kubwa nazijua ambazo zimekusanya watu kwa sababu ya kitu cha kipekee cha kiMungu kilichopo hapo na watu wanakifuata. Ila pia zipo nyingi zinazojiita “huduma” ambazo zinakusanya kwa sababu ni mzoga unaovutia tai.

Mzoga ni mrahisi sana kuujua. Unatoa harufu mbaya.

Asomaye na afahamu.

Pastor Carlos Kirimbai

……………………………………………………………..

Mafundisho mengine yanayokubali Kufunguliwa yaliwahi kujadiliwa bila kupata majibu sahihi

http://strictlygospel.wordpress.com/2011/09/08/kufunguliwa-kutoka-katika-ndoa-ya-mapepo-au-majini-mahaba/

http://strictlygospel.wordpress.com/2013/07/22/balaa-laana-na-mikosi-ya-kifamilia/

Wanawake Katika Huduma

joy

Kwa kuwa ni kitu kinachojulikana kwamba wanawake ni zaidi ya nusu katika kanisa la Bwana Yesu Kristo, ni muhimu kuelewa nafasi yao waliyopewa na Mungu katika mwili wa kristo. Katika makanisa mengi na huduma, wanawake huonekana kama watenda kazi wa maana sana, kama ambavyo ni kawaida hata katika huduma ya jumla.

Lakini, si wote wanaokubaliana kuhusu nafasi zao. Wanawake mara nyingi wanazuiwa kufanya maeneo fulani ya huduma kanisani, yenye kuhusiana na kusema na uongozi. Makanisa mengine yanaruhusu wanawake wachungaji; mengi hayaruhusu. Mengine yanaruhusu wanawake kufundisha, na mengine hayaruhusu. Wengine wanawazuia wanawake wasiseme kabisa wakati wa ibada za kanisa.

Kutofautiana huko kwa sehemu kubwa kumejengwa kwenye tafsiri mbalimbali za maneno ya Paulo kuhusu nafasi za wanawake katika 1Wakor. 14:34-35 na 1Timo. 2:11 hadi 3:7. Maandiko hayo tutayatazama zaidi katika sura hii, hasa pale mwishoni.

Kuanza Mwanzo

Tunapoanza, hebu tutazame Maandiko yanadhihirisha nini kuhusu wanawake, tangu mwanzo kabisa. Sawa na wanaume, wanawake wameumbwa katika mfano wa Mungu.

Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba (Mwanzo 1:27).

Bila shaka tunajua kwamba Mungu alimwumba Adamu kabla ya kumwumba Hawa, na hilo ni jambo lenye umuhimu wa kiroho kulingana na Paulo (ona 1Timo. 2:3). Baadaye tutatazama umuhimu wa mpango huo katika uumbaji kama unavyoelezwa na Paulo, lakini inatosha tu kwa sasa kusema kwamba hiyo haithibitishi ubora wa wanamume juu ya wanawake. Wote tunajua kwamba Mungu aliwaumba wanyama kabla ya binadamu (ona Mwanzo 1:24-28)[1]

Mwanamke aliumbwa awe msaidizi wa mumewe (ona Mwanzo 2:18). Hapa tena, huo si uthibitisho wa udogo wake bali huonyesha tu nafasi yake katika ndoa. Roho Mtakatifu ametolewa kuwa msaidizi wetu, lakini si wa hali ya chini kuliko sisi. Roho Mtakatifu yuko juu yetu! Na ni sahihi kabisa kusema kwamba Mungu alipomwumba mwanamke awe msaidizi wa mumewe inathibitisha kwamba wanaume wanahitaji msaada!Mungu ndiye aliyesema kwamba haikuwa vema kwa manamume kuwa peke yake (ona Mwanzo 2:18). Ukweli huo umethibitishwa mara nyingi sana katika historia, wakati wanaume wanapoachwa wenyewe bila wake wa kuwasaidia.

Mwisho – tunaona tangu kurasa za kwanza kabisa za Mwanzo kwamba mwanamke wa kwanza aliumbwa kutoka nyama ya mwanamume wa kwanza. Alichukuliwa kutoka kwake, kuonyesha kwamba kuna anachokosa pasipo yeye, na kwamba hao wawili walikuwa mmoja hapo kwanza. Zaidi ni kwamba, kile ambacho Mungu alikitenga kilikusudiwa kuunganika tena kwa njia ya mahusiano ya kushirikiana kimwili, jambo ambalo si la kuzaana na kuongezeka tu, bali la kuonyesha upendo na kufurahiana wote wawili, ambapo kila mmoja anamtegemea mwingine.

Kila kitu juu ya masomo haya kutoka uumbaji kinapingana na wazo la jinsia moja kuwa juu au bora kuliko nyingine, au moja kuwa na haki ya kutawala nyingine. Na kwa kuwa Mungu ameweka wajibu tofauti kwa wanawake au huduma haihusiani na usawa wao na wanaume ndani ya Kristo, ambako “hakuna mtu mume wala mtu mke” (Wagalatia 3:28, TLR).

Wanawake Katika Huduma – Agano La Kale

Baada ya kuweka msingi huo, hebu sasa tutazame baadhi ya wanawake ambao Mungu aliwatumia kutimiza makusudi Yake katika Agano la Kale. Ni dhahiri kwamba Mungu aliwaita wanaume kuingia katika huduma kama kazi katika kipindi cha Agano la Kale, kama alivyofanya katika kipindi cha Agano Jipya. Habari za wanaume kama vile Musa, haruni, Yoshua, Yusufu, Samweli na Daudi zimejaa katika kurasa za Agano la Kale.

Ila, kuna wanawake wengi tu wanaotokezea hapo kama ushahidi kwamba Mungu anaweza kumwita na kumtumia yeyote atakaye, na wanawake waliowezeshwa na Mungu wanatosha kufanya kazi yoyote atakayowaitia.

Kabla ya kutazama mwanamke mmoja, ni vizuri ijulikane kwamba kila mtu maarufu wa Mungu katika Agano la Kale alizaliwa na kulelewa na mwanamke. Asingekuwepo Musa bila ya mwanamke aliyeitwa Yokebedi (ona Kutoka 6:20). Wala wasingekuwepo watu wengine maarufu na wakuu wa Mungu kama si akina mama wa hao watu. Wanawake wamepewa na Mungu wajibu mzito na huduma yenye sifa kubwa ya kuwakuza watoto katika Bwana (ona 2Timo. 1:5).

Yokebedi hakuwa mama wa wanaume wawili walioitwa na Mungu tu – Mus ana Haruni – bali pia alimzaa mwanamke aliyeitwa na Mungu. Huyo ni Miriamu dada yao, nabii wa kike na kiongozi wa kuabudu (ona Kutoka 15:20). Katika Mika 6:4, Mungu anamweka Miriamu pamoja na Musa na Haruni, kama viongozi wa Israeli.

Kwa maana nalikupandisha kutoka nchi ya Misri, na kukukomboa utoke katika nyumba ya utumwa, nami naliwapeleka Musa, na Haruni, na Miriamu, watangulie mbele yako (maneno mepesi kutilia mkazo).

Ni kweli kwamba nafasi ya Miriamu ya uongozi katika Israeli haikuwa kubwa sana kama Musa. Lakini, kama nabii wa kike, Miriamu alinena kwa niaba ya Mungu, nami nadhani kwamba ni salama kusema kwamba jumbe za Mungu kupitia kwake zililengwa kwa wanaume wa Israeli, si wanawake tu.

Mwamuzi Mwanamke Juu Ya Israeli

Mwanamke mwingine ambaye Mungu alimwinua kuwa kiongozi katika Israeli ni Debora, aliyeishi wakati wa kipindi cha waamuzi wa Israeli. Yeye naye alikuwa nabii wa kike, na alikuwa mwamuzi juu ya Israeli sawa na akina Gidioni, Yefta na Samsoni wakati wao. Tunaambiwa kwamba “wana wa Israeli walimwendea awaamue” (Waamuzi 4:5, TLR). Basi, akatoa maamuzi kwa ajili ya wanaume, si wanawake tu. Angalia usikose hili: Mwanamke aliwaambia wanaume kitu cha kufanya, na Mungu alimtia mafuta afanye hivyo.

Kama wanawake wengi ambao Mungu huwaita katika uongozi, Debora alikabiliwa na mwanamume mmoja ambaye aliona taabu kupokea neno la Mungu kupitia chombo cha kike. Jina lake aliitwa Baraki, na kwa sababu alikuwa na mashaka kuhusu maagizo ya Dobora ya kinabii kwake kwamba akapigane vita na jemadari Mkanani aliyeitwa Sisera, Debora alimwambia kwamba heshima ya kumwua huyo Sisera ingemwendea mwanamke. Ndivyo ilvyokuwa, na mwanamke aitwaye Yaeli anakumbukwa katika Maandiko kwamba ndiye aliyemtoboa kichwa Sisera akiwa amelala, kwa kigingi cha hema (ona Waamuzi 4). Kisa hiki kinamalizika kwa Baraki akiimba wimbo wa kupokezana, na Debora! Baadhi ya mafungu yamejaa sifa kwa ajili ya Debora na Yaeli (ona Waamuzi 5), kwa hiyo, pengine Baraki alikuja kuamini “huduma ya wanawake” mwishowe!

Nabii Wa Tatu Mwanamke

Mwanamke wa tatu anayetajwa katika Agano la Kale kwamba ni nabii wa kuheshimika ni Hulda. Mungu alimtumia kutoa mtazamo unaoaminika wa kinabii na maagizo kwa mwanamume, mfalme aliyekuwa na wasiwasi sana, wa Yuda (ona 2Wafalme 22). Hapa tena tunaona mfano wa Mungu akimtumia mwanamke kumfundisha mwanamume. Bila shaka Hulda alitumiwa na Mungu kwa huduma kama hiyo mara kwa mara, vinginevyo Yosia asingekuwa na imani kubwa katika aliyomwambia.

Kwa nini Mungu alimwita Miriamu, Debora na Hulda kufanya kazi kama manabii wanawake? Mbona asiwaite wanaume?

Hakika Mungu angeweza kuwaita wanaume kufanya hayo hayo yaliyofanywa na wanawake watatu. Lakini hakuwaita. Na hakuna ajuaye sababu. Tunachotakiwa kujifunza kutokana na hili ni kwamba ni vizuri tujihadhari juu ya kumweka Mungu kwenye sanduku kwa habari ya anamwita nani kwenye huduma. Ingawa Mungu kawa kawaida alichagua wananume kufanya kazi wa uongozi katika Agano la Kale, wakati mwingine alichagua wanawake.

Mwisho – ijulikane kwamba hiyo mifano yote mitatu ya watumishi wanawake katika Agano la Kale walikuwa manabii. Zipo huduma zingine za Agano la Kale ambazo wanawake hawakuitwa kuzifanya. Kwa mfano: Hakuna wanawake walioitwa kuwa makuhani. Hivyo, yawezekana Mungu ametenga huduma fulani kwa ajili ya wanaume tu.

Wanawake Katika Huduma – Agano Jipya

Cha kushangaza ni kwamba tunamkuta mwanamke aliyeita na Mungu kuwa nabii mwanamke katika Agano Jipya. Yesu alipokuwa na umri wa siku chache tu, Ana alimtambua na kuanza kutangaza kwamba ndiye Masiya.

Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi. Alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake. Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba. Huyu alitokea saa ile ile akamshukuru Mungu, na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu akawatolea habari zake (Luka 2:36-38. Maneno mepesi kutilia mkazo).

Ona kwamba Ana aliwaambia wote waliokuwa “wanautarajia wokovu wa Yerusalemu” habari za Yesu. Bila shaka walikuwemo na wanaume. Kwa hiyo, tunaweza kusema kwamba Ana alikuwa anawafundisha wanaume habari za Kristo.

Kuna wanawake wengine katika Agano Jipya ambao Mungu aliwatumia kwa karama ya unabii. Mama yake Yesu – Mariamu – yuko katika fungu hilo (ona Luka 1:46-55). Kila mara maneno ya kinabii ya Mariamu yanaposomwa katika ibada ya kanisa, ni sawa kusema kwamba mwanamke analifundisha kanisa. (Na Mungu aliwaheshimu wanawake bila swali kwa kumtuma Mwana Wake duniani kwa njia ya mwanamke. Angeweza kufanya kwa njia zingine nyingi!)

Orodha hii inaendelea. Mungu alitabiri kwa kinywa cha nabii Yoeli kwamba wakati atakapomwaga Roho Wake, wana wa kiume na wa kike katika Israeli wangetabiri (ona Yoeli 2:28). Petro alithibitisha kwamba unabii wa Yoeli ulikuwa unafanya kazi katika kipindi cha agano jipya (ona Matendo 2:17).

Tunaambiwa katika Matendo 21:8-9 kwamba mwinjilisti Filipo alikuwa na binti wanne waliokuwa manabii.

Paulo aliandika kuhusu wanawake wakitoa unabii katika ibada za kanisa (ona 1Wakor. 11:5). Ni dhahiri kutokana na mantiki kwamba, wanaume walikuwepo.

Kwa mifano yote hiyo ya Maandiko kuhusu wanawake kutumiwa na Mungu kama manabii na kutoa unabii, kweli hatuna sababu nzuri ya kukataa wazo kwamba Mungu anaweza kuwatumia wanawake katika huduma hizo! Tena, hakuna kitu chochote kinachoweza kutupelekea sisi kufikiri kwamba wanawake hawawezi kuwatabiria wanaume kwa niaba ya Mungu.

Wanawake Kama Wachungaji?

Vipi kuhusu wanawake kutumika kama wachungaji? Inaonekana dhahiri kwamba nafasi ya mchungaji au mzee au mwangalizi imekusudiwa na Mungu ishikiliwe na wanaume.

Ni neno la kuaminiwa: Mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema. Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja (1Timo. 3:1-2. Maneno mepesi kutilia mkazo).

Kwa sababu hii nalikuacha Krete, ili uyatengeneze yaliyopunguka, na kuweka wazee katika kila mji kama vile nilivyokuamuru; ikiwa mtu hakushtakiwa neno, naye ni mume wa mke mmoja (Tito 1:5,6. Maneno mepesi kutilia mkazo).

Paulo hasemi moja kwa moja kwamba wanawake wamekatazwa kushika wadhifa huo, kwa hiyo, tuwe makini tusitoe uamuzi wa mwisho. Inaonekana kwamba kuna wachungaji wengi wa kike, na wazee na waangalizi duniani kote siku hizi – hasa katika nchi zinazoendelea – ambao wanafanya vizuri sana. Ila, bado ndiyo wachache. Pengine Mungu mara moja moja anawaita wanawake kufanya kazi hiyo wakati ambapo katika hekima Yake, makusudi ya ufalme Wake yatatimizwa vizuri zaidi, au wakati kuanpokuwepo upungufu wa uongozi wa kiume wenye sifa zinazotakiwa. Pia yawezekana kwamba wachungaji wengi wa kike walio katika mwili wa kristo leo wana wito wa kushika nafasi zingine za huduma ambazo zinafaa KiBiblia kwao, kama vile nafasi ya nabii, ila, mfumo uliopo wa kanisa unawarhusu kufanya kazi kama wachungaji tu.

Kwa nini nafasi ya mchungaji au mzee au mwangalizi imetengwa kwa ajili ya wanaume tu? Kuelewa utendaji wa nafasi hiyo kutatusaidia. Sharti moja la Maandiko kuhusu mchungaji au mzee au mwangalizi ni kwamba,

[Awe] Mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu; (yaani, mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje Kanisa la Mungu?) (1Timo. 3:4-5).

Sharti hili linaleta maana kabisa tunapotambua kwamba mzee wa Agano Jipya alisimamia kanisa dogo la nyumbani. Wajibu wake ulikuwa ni sawa na baba kusimamia familia yake. Hili linatusaidia kuelewa ni kwa nini nafasi ya mchungaji ishikwe na mwanamume – kwa sababu inafanana sana na mfumo wa familia, ambayo, kama inalingana na mpango wa Mungu, inatakiwa kuongozwa na mume, si mke. Tutasema zaidi juu ya hilo baadaye.

Wanawake Kama Mitume?

Tumegundua kwamba wanawake wanaweza kufanya kazi katika nafasi ya nabii (wakiitwa na Mungu). Vipi kuhusu aina zingine za huduma? Inasaidia kusoma salamu za Paulo katika Warumi 16, ambapo anawasifu baadhi ya wanawake waliofanya huduma kwa ajili ya ufalme wa Mungu. Yawezekana hata mmoja akawa amepangwa kama mtume. Katika mafungu matatu yanayofuata, nimeandika majina ya wanawake wote kwa herufi nyepesi kama hizi.

Namkabidhi kwenu Fibi, ndugu yetu, aliye mhudumu wa kanisa lililoko Kenkrea; kwamba mmpokee katika Bwana, kama iwapasavyo watakatifu; mkamasaidie katika neno lolote atakalohitaji kwenu; kwa sababu yeye naye amekuwa mssaidizi wa watu wengi, akanisaidia mimi pia (Warumi 16:1, 2. Maneno mepesi kutilia mkazo).

Amesifiwa kweli kweli! Hatujui Fibi alikuwa anafanya huduma gani, lakini Paulo anamwita “mtumishi wa kanisa la Kenkrea” na “msaidizi wa wengi” pamoja na yeye (TLR). Chochote alichokuwa anafanya kwa ajili ya Bwana kinaonekana kilikuwa kikubwa sana mpaka Paulo anamsifu kwa kanisa lote la Rumi.

Kisha tutasoma habari za Priska (au Priskila), ambaye, pamoja na Akila mume wake, walikuwa na huduma muhimu sana kiasi cha kwamba makanisa yote ya Mataifa yaliwafurahia.

Nisalimieni Priska na Akila, watenda kazi pamoja nami katika Kristo Yesu, waliokuwa tayari hata kukatwa kichwa kwa ajili ya maisha yangu; ambao ninawashukuru, wala si mimi tu, ila na makanisa ya Mataifa yote pia. Nisalimieni na kanisa lililomo katika nyumba yao. Nisalimieni Epaineto, mpenzi wangu, aliye malimbuko ya Asia kwa Kristo. Nisalimieni Mariamu,aliyejitaabisha sana kwa ajili yenu. Nisalimieni Androniko na Yunia, jamaa zangu, waliofungwa pamoja nami, ambao ni maarufu miongoni mwa mitume; nao walikuwa katika Kristo kabla yangu (Warumi 16:3-7. Maneno mepesi kutilia mkazo).

Kwa habari ya Yunia – inaonekana kwamba mtu ambaye ni “maarufu miongoni mwa mitume” bila shaka naye ni mtume tu. Kwa mahesabu hayo, Yunia alikuwa mtume wa kike. Priska na Mariamu walikuwa watenda kazi kwa ajili ya Bwana.

Nisalimieni Ampliato, mpenzi wangu katika Bwana. Nisalimieni Urbano, mtenda kazi pamoja nami katika Kristo, na Stakisi, mpenzi wangu. Nisalimieni Apele, mwenye kukubaliwa katika Kristo. Nisalimieni watu wa nyumbani mwa Aristobulo. Nisalimieni Herodioni, jamaa yangu. Nisalimieni watu wa nyumbani mwa Narkiso, walio katika Bwana. Msalimieni Trifaina na Trifosa,wenye bidii katika Bwana. Nisalimieni Persisi, mpenzi aliyejitahidi sana katika Bwana. Nisalimieni Rufo, mteule katika Bwana, na mamaye, aliyae mama yangu pia. Nisalimieni Asinkrito, Flegoni, Herme, Patroba, Herman a ndugu walio pamoja nao. Nisalimieni Filologo naYulia, Nerea na dada yake, na Olimpa, na watakatifu wote walio pamoja nao (Warumi 16:8-15. Maneno mepesi kutilia mkazo).

Basi ni dhahiri kwamba wanawake wanaweza kuwa “watenda kazi” katika huduma.

Wanawake Kama Waalimu?

Vipi kuhusu waalimu wa kike? Agano Jipya halitaji hata mmoja. Wala Biblia haitaji wanaume wowote walioitwa kuwa waalimu. Priska (aliyetajwa hapo juu) mke wa Akila, alihusika katika kufundisha kwa sehemu ndogo. Kwa mfano: Wakati yeye na Akila walipomsikia Apolo akihubiri Injili yenye upungufu mwingi sana huko Efeso, “walimchukua na kumwelezea njia ya Mungu kwa usahihi zaidi” (Matendo 18:26, TLR). Hakuna awezaye kupinga kwamba Priska alimsaidia mume wake kumfundisha Apolo, aliyekuwa mwanamume. Tena, Paulo anawataja Priska na Akila mara mbili katika Maandiko, wakati anaposema juu ya “kanisa lililoko nyumbani mwao” (ona Warumi 16:3-5; 1Wakor. 16:19), na anawaita wote wawili “watenda kazi wenzangu katika Kristo” katika Warumi 16:3. Hapana shaka kwamba Priska alikuwa na nafasi tendaji katika huduma pamoja na mume wake.

Wakati Yesu Alipowaamuru Wanawake Wawafundishe Wanaume

Kabla hatujashughulikia maneno ya Paulo kuhusu wanawake kunyamaza kimya kanisani nay eye kuwakataza wanawake kufundisha wanaume, hebu tutazame andiko moja litakalotusaidia kulinganisha vizuri hayo.

Yesu alipofufuka, malaika aliwaagiza wanawake watatu kwenda kuwafundisha wanafunzi wa kiume wa Yesu. Hao wanawake waliamriwa kuwaambia wanafunzi kwamba Yesu amefufuka, na kwamba angewatokea huko Galilaya. Si hayo tu. Muda mfupi baadaye, Yesu Mwenyewe aliwatokea wanawake hao na kuwaamuru wakawaambie wanafunzi waende Galilaya (ona Mat hayo 28:1-10; Marko 16:1-7).

Kwanza, mimi nadhani ni kitu muhimu sana kwamba Yesu alichagua kuwatokea wanawake kwanza, kisha wanaume. Pili, kama kungekuwepo na kitu chochote kibaya kimsingi au kiadili, kuhusu wanawake kuwafundisha wanaume, ungetarajia kwamba Yesu asingewaambia wanawake wawafundishe wanaume kuhusu kufufuka Kwake – jambo ambalo si dogo – na ambalo Yeye Mwenyewe angeweza kuwafikishia (kama alivyofanya baadaye). Hakuna mtu awezaye kupinga hoja hii: Bwana Yesu aliwaagiza wanawake wafundishe kweli muhimu sana na kutoa maagizo fulani ya kiroho, kwa wanaume.

Maandiko Yenye Utata

Sasa kwa kuwa tunafahamu kidogo yale ambao Biblia inatuambia kuhusu nafasi za wanawake katika huduma, tutaweza kutafsiri vizuri yale “Maandiko yenye utata” katika nyaraka za Paulo. Hebu kwanza tutazame maneno yake kuhusu wanawake kunyamaza makanisani.

Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo. Nao wakitaka kujifunza neno lolote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa (1Wakor. 14:34-35).

Kwanza – Kuna wenye swali kutokana na sababu nyingi, ikiwa hayo ni maagizo ya Paulo au anarudia kusema yale ambayo Wakorintho walikuwa wamemwandikia. Ni dhahiri kwamba katika sehemu yapili ya barua yake hiyo, Paulo alikuwa anajibu maswali ambayo Wakorintho walikuwa wamemwuliza kwa barua (ona 1Wakor. 7:1, 25; 8:1; 12:1; 16:1, 12).

Pili – katika mstari unaofuata, Paulo anaandika kitu kinachoweza kuhesabiwa kuwa ni itikio lake kwa desturi ya Wakorintho ya jumla ya kuwanyamazisha wanawake makanisani. Anaandika hivi:

Au je! Neno la Mungu lilitoka kwenu? Au kuwafikia ninyi peke yenu? (1Wakor. 14:36).

Vyovyote vile, Paulo ni kama anayeuliza maswali mawili ambayo majibu yake ni dhahiri. Jibu kwa yote niHapana. Si Wakorintho waliotoa Neno la Mungu, wala Neno la Mungu halikutolewa kwao tu. Maswali ya Paulo basi ni kama makemeo, yanayoelekezwa kwenye viburi vyao. Kama ndiyo itikio lake kwa mistari hiyo miwili inayotangulia, inaonekana ni kama ifuatavyo: “Hivi, ninyi mnafikiri ni nani? Tangu lini mnatoa amri kuhusu Mungu amtumie nani kulisema Neno Lake? Mungu anaweza kuwatumia wanawake akitaka, nanyi ni wapumbavu kuwanyamazisha.”

Tafsiri hii inafaa kama tutafikiria kwamba Paulo – katika barua hii hii – tayari amekwisha andika juu ya njia inayofaa kwa wanawake kutoa unabii makanisani (ona 1Wakor. 11:5), kitu ambacho kinawataka wasinyamaze. Tena, mistari michaceh baada yah ii tunayochunguza, Paulo anawahimiza Wakorintho wote[2], ikiwa ni pamoja na wanawake, “watamani sana kutabiri” (1Wakor. 14:39, TLR). Basi itakuwa anajipinga mwenyewe kama kweli alikuwa anatoa amri ya jumla kwa wanawake kunyamaza katika ibada makanisani katika maandiko ya 14:34-35.

Mawazo Mengine

Lakini – hebu tuseme tu kwamba pengine hayo maneno ya 1Wakor. 14:34-35 ni maneno ya Paulo mwenyewe, naye anawaagiza wanawake wanyamaze. Tutafsirije maneno hayo?

Hapa tena, tutalazimika kushangaa ni kwa nini Paulo anatoa amri ya jumla namna hiyo kwa wanawake kunyamaza kabisa katika mikutano ya kanisa, wakati aliposema katika barua hiyo hiyo kwamba wanaweza kuomba hadharani na kutabiri – bila shaka katika mikutano ya kanisa.

Tena – Bila shaka Paulo aliijua mifano ile yote ambayo tumeitoa hapo mwanzoni kuhusu Mungu kuwatumia wanawake kulisema Neno Lake hadharani, hata kwa wanaume. Sasa – kwa nini awanyamazishe kabisa wale ambao Mungu amewahi kuwatia mafuta mara kwa mara ili waseme?

Kweli mawazo ya kawaida tu yanadai tukubali kwamba Paulo hakumaanisha kwamba wanawake wanyamaze kimya kabisa wakati wa ibada za kanisa. Kumbuka kwamba kanisa la kwanza walikutanikia majumbani na kula chakula pamoja. Kweli tufikiri kwamba wanawake hawakusema chochote tangu walipoingia nyumbani humo mpaka walipotoka? Kwamba hawakuzungumza chochote wakati wa kuandaa au kula chakula cha pamoja? Kwamba hawakusema chochote kwa watoto wao muda wote? Kufikiri hivyo ni ujinga.

Ikiwa mahali ambapo “wawili au watatu wamekusanyika” kwa jina la Yesu Yeye yuko katikati yao (ona Mathayo 18:20), na kama hiyo ni idadi halali ya mkutano wa kanisa, inakuwaje basi wakati wanawake wawili wanapokutanika pamoja katika jina la Yesu? Je, wasisemezane?

Hapana! Kama 1Wakorintho 14:34-35 kweli ni maagizo ya Paulo, basi alikuwa anashughulikia tatizo dogo la utaratibu katika makanisa. Kuna wanawake waliokuwa hawafuati utaratibu kwa namna fulani, kwa habari ya kuuliza maswali. Paulo hakumaanisha wanawake wanyamaze kimya kabisa kwa kipindi chote cha mkutano. Hata alipotoa maagizo yanayofanana na hayo mistari michache kabla ya hapo, yanayowahusu manabii, hakuwa na maana hiyo.

Lakini [nabii] mwingine aliyeketi akifunuliwa neno, yule wa kwanza na anyamaze (1Wakor. 14:30, Maneno mepesi kutilia mkazo).

Hapa, maneno “anyamaze” maana yake “aache kusema kwa muda.”

Paulo pia aliwaagiza wale wanaonena kwa lugha kunyamaza kama hakuna mtafsiri kwenye kusanyiko.

Lakini asipokuwepo mwenye kufasiri, na anyamaze katika kanisa; aseme na nafsi yake tena na Mungu (1Wakor. 14:28, Maneno mepesi kutilia mkazo).

Je, Paulo alikuwa anawaagiza watu kama hao kunyamaza kabisa wakati wote wa mkutano? Hapana! Alikuwa anawaambia wanyamaze kwa habari ya kunena kwao kwa lugha wakati hakuna mfasiri. Ona kwamba Paulo anawaambia “wanyamaze katika kanisa,” ambayo ndiyo maagizo anayotoa kwa wanawake katika 1Wakor. 14:34-35. Basi, kwa nini tutafsiri maneno ya Paulo kwa wanawake kwamba wanyamaze kanisani kuwa maana yake ni “wanyamaze kwa kipindi chote cha ibada”, kisha tutafsiri maneno yake kwa wanaonena kwa lugha bila utaratibu kuwa maana yake ni “wasiseme katika kipindi fulani cha ibada”?

Mwisho ni vizuri tuone kwamba Paulo hakuwa anazungumzana wanawake wote katika fungu hilo. Maneno yake yanawahusu wanawake walio na ndoa tu, kwa sababu wanaagizwa “wakawaulize waume zao nyumbani” kama wana maswali.[3] Pengine sehemu ya tatizo au tatizo zima kwa ujumla ni kwamba wanawake wenye ndoa walikuwa wanawauliza wanaume wengine maswali, zaidi ya waume zao. Kama ni hivyo, hali hiyo si halali, na ingedhihirisha aina fulani ya kutokuheshimu na kutokutii waume zao wenyewe. Kama hilo ndilo tatizo analoshughulikia Paulo, ndiyo sababu anajenga hoja yake kwenye ukweli kwamba wanawake wanapaswa kuwa watiifu (kwa waume zao bila shaka!) kama Torati ilivyodhihirisha kwa namna nyingi katika kurasa za kwanza kabisa za kitabu cha Mwanzo (ona 1Wakor. 14:34).

Kwa kuhitimisha, ni hivi: Kama Paulo kweli anatoa maagizo kuhusu wanawake kunyamaza kimya katika 1Wakor. 14:34-35, basi anawaambia wanawake walio-olewa tu wanyamaze kwa habari ya kuuliza maswali kwa wakati usiofaa, au kwa namna ambayo ilionyesha kutowaheshimu waume zao. Vinginevyo, wanaweza kutabiri, kuomba na kusema.

Andiko Lingine Lenye Utata

Mwisho, tunafikia fungu la pili “lenye utata” linalopatikana katika barua ya kwanza ya Paulo kwa Timotheo.

Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna. Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu. Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye. Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa (1Timo. 2:11-14).

Hakika Paulo alijua kuhusu Miriamu, Debora, Hulda na Ana – manabii wanne wanawake waliosema kwa niaba ya Mungu na kuwaambia wanawake na wanaume maneno ya Mungu na kuwafundisha mapenzi ya Mungu. Hakika alifahamu kwamba Debora, mwamuzi wa Israeli, alikuwa na mamlaka kiasi fulani juu ya wanaume na wanawake. Hakika alijua kwamba Mungu alimimina Roho Wake siku ile ya Pentekoste, akitimiza kwa sehemu unabiiw a Yoeli kuhusu siku za mwisho wakati ambapo Mungu angemimina Roho Wake juu ya wote wenye mwili, ili wana na binti watabiri na kutangaza Neno la Mungu. Hakika alijua kwamba Yesu aliwaagiza wanawake fulani wapeleke ujumbe kutoka Kwake kwa mitume Wake wanaume. Bila shaka alijua maneno yake mwenyewe, ya kuunga mkono wanawake kuomba na kutoa unabii katika mikutano ya kanisa, aliyowaandikia Wakristo wa Korintho. Bila shaka alikumbuka kwamba aliwaambia Wakorintho kwamba yeyote kati yao anaweza kupokea fundisho la kuwaambia wengine kutoka kwa Roho Mtakatifu (ona 1Wakor. 14:26). Sasa, alitaka watu wapate nini alipoandika maneno haya kwa Timotheo?

Ona kwamba Paulo anajenga hoja yake kwenye kweli mbili zinazokubaliana kutoka Mwanzo, kwa ajili ya kufundisha: (1) Adamu aliumbwa kabla ya Hawa, na (2) Hawa ndiye alidanganywa, si Adamu, naye akaangukia katika kosa. Kweli ya kwanza inathibitisha mahusiano sahihi kati ya mume na mke. Kama uumbaji unavyofundisha, mume anatakiwa kuwa kichwa – jambo ambalo Paulo analifundisha mahali pengine (ona 1Wakor. 11:3; Waefeso 5:23-24).

Kweli ya pili anayotaja Paulo haikusudii kuonyesha kwamba wanawake ni rahisi zaidi kudanganywa kuliko wanaume. Si hivyo. Ukweli ni kwamba, kwa kuwa wanawake ni wengi kuliko wanaume katika mwili wa Kristo, hoja inaweza kutolewa kwamba wanaume ndiyo rahisi kudanganyika kuliko wanawake. Hata hivyo – kweli yapili inaonyeah kwamba wakati mpango uliokusudiwa wa Mungu katika familia unapopuuzwa, Shetani anaweza kuingia. Tatizo la binadamu lilianza bustanini, wakati mahusiano kati ya mume na mke wake yalipotoka kwenye utaratibu – mke wa Adamu hakumtii. Adamu lazima alimwambia mke wake agizo la Mungu kuhusu tunda lililokatazwa (ona Mwanzo 2:16-17; 3:2-3). Shida ni kwamba yeye hakufuata alichoambiwa na mumewe. Kuna jinsi alivyotumia mamlaka juu yake wakati alipompa tunda hilo ale (ona Mwanzo 3:6). Hapo, si Adamu aliyemwongoza Hawa, ni Hawa alimwongoza Adamu. Matokeo yakawa balaa.

Kanisa – Mfano Wa Familia

Utaratibu ambao Mungu amekusudia kwa ajili ya familia unapaswa kuonyeshwa na kanisa. Kama nilivyosema mapema, ni muhimu kukumbuka kwamba kwa miaka mia tatu ya kwanza ya historia ya kanisa, vikundi vya kanisa vilikuwa vidogo. Walikutania majumbani. Wachungaji na wazee na waangalizi walikuwa kama baba wa familia. Huo mpango wa kanisa wa KiMungu ulifanana sana na familia, na kwa kweli ulikuwa ni familia ya kiroho, kiasi cha kwamba uongozi wa kike juu yake ungepeleka ujumbe usio sahihi kwa familia za nje na hata ndani ya kanisa. Hebu fikiri mchungaji au mzee au mwangalizi wa kike akifundisha kila wakati katika kanisa la nyumbani, na mume wake ameketi kwa utii pale, akimsikiliza akifundisha na kutii mamlaka yake. Hiyo ingekwenda kinyume na utaratibu wa Mungu katika familia, na kuweka mfano usio sahihi.

Hicho ndicho Paulo anashughulikia. Ona kwamba maneno hayo yako karibu tu na maelezo kuhusu masharti ya mtu kuwa mzee (ona 1Timo. 3:1-7). Shartri moja ni kwamba awe mwanamume. Pia ijulikane kwamba wazee walipaswa kufundisha mara kwa mara kanisani (ona 1Timo. 5:17). Maneno ya Paulo kuhusu wanawake kupokea mafundisho kwa utulivu na kutoruhusiwa kufundisha au kutawala wanaume bila shaka yanahusiana na utaratibu sahihi wa kanisa. Anachosema kwamba si sahihi ni mwanamke – kwa sehemu au kikamilifu kabisa – kutimiza kazi ya mzee au mchungaji au mwangalizi.

Hii si kusema kwamba mwanamke au mke hawezi kuomba, kutabiri, kupokea fundisho fupi la kuwaambia washirika, au kusema kwa ujumla katika mkutano wa kanisa – akiwa chini ya mamlaka ya mume wake. Hayo yote anaweza kufanya kanisani bila ya kuharibu utaratibu wa Mungu, kama ambavyo anaweza kufanya hayo yote nyumbani bila kuwa amekiuka mpango wa Mungu. Alichokatazwa kufanya kanisani ni sawa na alichokatazwa kufanya nyumbani – kumtawala mume wake, au kuwa na mamlaka juu ya mume wake.

Kutokana na mistari ya baadaye tunaona kwamba wanawake wangeweza kufanya kazi kama shemasi, sawa na wanaume (ona 1Timo. 3:12). Kuhudumu kanisani kama shemasi au mtumishi (ambayo ndiyo maana ya neno lenyewe) hakudai kuvunjwa kwa utaratibu wa Mungu kati ya mume na mke.

Hii ndiyo njia pekee ya kulinganisha maneno ya Paulo katika 1Timo. 2:11-14 na mengine yote yanayofundishwa na Maandiko. Katika kila mfano wa Maandiko tuliotazama wa Mungu kuwatumia wanawake, hakuna uliokuwa mfano wa familia kama kanisa lilivyo, na kwa hali hiyo, hakuna unaovunja utaratibu wa Mungu. Hatupati popote mfano wa wanawake wakiwa na mamlaka juu ya waume zao katika familia. Kumbuka tena kusanyiko dogo la familia kadhaa katika nyumba, na mke ndiye anasimamia kundi hilo: akifundisha na kulisimamia wakati mume wake ameketi tu na kutii uongozi wake. Mungu hataki hayo, maana ni kinyume na utaratibu Wake kwa ajili ya familia.

Ila – kwa Debora kuwa mwamuzi wa Israeli, Ana kuwaambia wanaume habari za kristo, na Mariamu na rafiki zake kuwaambia mitume kuhusu ufufuo wa Kristo – hakuna ujumbe wowote mbaya unaopelekwa au kwa njia yoyote ile kuonyesha isivyostahili utaratibu wa Mungu katika familia. Kusanyiko la kila mara la kanisa ni nyeti, ambapo ipo hatari kwa ujumbe usiostahili kutumwa ikiwa wanawake au wake watakuwa na mamlaka na kuwafundisha wanaume au waume kila mara.

Kumalizia

Kama tukijiuliza tu hivi: “Ni kitu gani kinachoweza kuwa kosa kimsingi kwa wanawake kufanya huduma, wakiwatumikia wengine kwa moyo wa huruma na kutumia vipawa vyao walivyopewa na Mungu? Kuna kanuni gani ya kiadili inayovunjwa?” Ndipo baadaye tunatambua kwamba kuvunjwa kwa kanuni ni kama huduma ya mwanamke kwa namna moja au nyingine ingehalifu utaratibu wa Mungu kwa habari ya mahusiano kati ya wanaume na wanawake, kati ya waume na wake zao. Katika mafungu yote mawili “yenye utata” tuliyotazama, Paulo anataja utaratibu wa Mungu katika ndoa kama sababu yake ya kusema anachosema.

Basi, tunatambua kwamba wanawake wamezuiliwa kufanya huduma kwa sehemu ndogo sana. Kwa njia zingine nyingi tena kubwa, Mungu anataka kuwatumia wanawake kwa ajili ya utukufu Wake, Naye amekuwa akifanya hivyo kwa maelfu ya miaka. Maandiko yanazungumza kuhusu michango mingi inayofaa ambayo wanawake wameitoa kwa ufalme wa Mungu – na tumekwisha tazama baadhi yake. Tusije kusahau kwamba baadhi ya marafiki wa Yesu wa karibu sana walikuwa wanawake (ona Yohana 11:5), na kwamba wanawake walisaidia huduma Yake kifedha (ona Luka 8:1-3). Hakuna mwanamume anayetajwa kuwa alifanya hivyo. Yule mwanamke kisimani Samaria aliwaambia wanaume habari za Kristo kijijini kwake, na wengi walimwamini Yesu (ona Yohana 4:28-30, 39). Mwanafunzi mwanamke aitwaye Tabitha anasemekana kuwa “alizidi katika matendo ya wema na fadhili aliyofanya daima” (Matendo 9:36, TLR). Mwanamke ndiye alimtia Yesu mafuta kwa ajili ya maziko Yake, na alimsifu kwa hilo wakati wanaume wengine wlaipolalamika (ona Marko 14:3-9). Mwisho, Biblia inaandika kwamba wanawake ndiyo waliomwombolezea Yesu alipobeba msalaba Wake katika mitaa ya Yerusalemu. Hakuna mwanamume anayetajwa katika hilo. Hii mifano na mingi kama hiyo inapaswa kuwatia moyo wanawake kuinuka na kutimiza huduma zao walizopewa na Mungu. Tunawahitaji wote!

———————————–

- Ijulikane kwamba kila mwanamume mwingine tangu Adamu ameumbwa na Mungu baada ya Mungu kuwaumba wanawake ambao walimzaa. Kila mwanamume baada ya Adamu ametoka kwa mwanamke, kama Paulo anavyotukumbusha katika 1Wakor. 11:11-12. Sidhani kama kuna yeyote ambaye atatoa hoja kwamba huo utaratibu wa KiMungu unathibitisha kwamba wanaume ni wadogo ukilinganisha na mama zao.

- Ushauri wa Paulo ni kwa “ndugu” – neno analotumia mara 27 katika barua hii, na ambalo linawahusu Wakristo wote katika Korintho, si wanaume tu.

-Ni vizuri kujua kwamba katika lugha ya asili ya Kiyunani, hakuna maneno tofauti kwa wanawake na mke,au mwanamume na mume. Hivyo inabidi kutambua kutoka mantiki ikiwa mwandishi anazungumza juu ya wanaume na wanawake, au waume na wake. Katika fungu tunalotazama, Paulo anazungumza na wake, kwa sababu wao ndiyo wangeweza kuwauliza waume zao chochote wakiwa nyumbani.

—David Servant

Hadithi ya Daudi na Goliathi!

david

 MAMBO YA MSINGI 20 YA KUJIFUNZA KUTOKA KWA HABARI YA DAUDI NA GOLIATHI.

1SAMWELI 16:1-55, NA 18: 1-5.

 1. JINA LA YESU lina uwezo mkubwa kuliko majina yote. Daudi akasema nakujia kwa Jina la BWANA. Tumia jina hilo unapotaka maombi yako yawe na ushindi.

 2. Mawe matano yanawakilisha huduma tano, uchungaji, utume, unabii, ualimu na uinjilisti. Hawa wote wanatakiwa kuwepo katika kanisa na kulelewa na mchungaji ndio maana ya Daudi kuweka mawe hayo ndani ya mkoba wa kichungaji.

 3. Daudi alichukua mawe matano pia kwa sababu alipeleleza na kujua Goliathi ana ndugu wengine wanne wenye mwonekano kama wake (THEOLOGY). Katika hili tunajifunza kujipanga kwa changamoto za baadaye hata kama bado hazijafika. Kama leo ni shwari basi jipange kwa ajili ya Kesho. Kwa lugha ya uchumi tunasema jifunze kuweka akiba.

 4. Upako wa Kwanza ulimpa Daudi nguvu ya kujihesabia mshindi hata kabla ya watu kujua kuwa yeye ni mshindi. Alitafuta kutumia nguvu yake. Usikae kimya wakati kuna jambo linaharibika na unajua kabisa unao uwezo wa kuweka mambo kwenye mstari.

 5. Ajionavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo. Sauli na majeshi ya Israeli walijiona wanyonge na dhaifu kwa Goliathi.(walifadhaika na kuogopa sana)  lakini Daudi alijiona kuwa mshindi na kweli akamshinda Goliathi.

 6. Daudi alitumia silaha dhaifu (kombea na jiwe) lakini alishinda, maana yake hata kama unahisi huna nguvu nyingi, huna pesa nyingi, huna jina kubwa, huna elimu kubwa, unadharaulika kama Goliathi alivyomdharau Daudi, Mungu akikutia nguvu, kile kidogo ulichonacho kinaweza fanya mambo makubwa saana! Efeso 3:20 Mungu hufanya zaidi hata tuwazayo na tuombayo.

 7. Daudi hakutafuta umaarufu, kwa sababu kama angependa umaarufu basi baada ya kuua dubu na simba angejitangaza lakini alitulia mpaka alipokutana na Goliathi. Tena hata baada ya kumuua Goliathi ni wana wa Israel walioanza kumwimbia nyimbo nzuri zaidi ya zile za mfalme. Si yeye aliyejitangaza. Nia yake haikuwa kujulikana bali kufanya mapenzi ya Mungu. Usihubiri au kuimba ili tukujue bali fanya kwa ajili ya ujenzi wa ufalme wa Mungu. Mungu akikuinua hutapata shida ya kujitangaza.

 8. Mungu huwainua watu kutoka kiwango kimoja kwenda kingine. Upako mmoja hadi mwingine. Daudi alipomuua simba na dubu ndipo alipoweza kumuua Goliathi. Unapotulia na kunyenyekea chini ya Mkono ulio hodari wa Mungu,basi Yeye atakuinua kwa wakati wake(1Petro 5:6). Muda mwingine Mungu anaonekana kama anachelewa kwa sababu tunataka kuruka hatua, katika maisha yako, Mungu anajua hatua unazotakiwa kupita, ukiisha kuua simba na Dubu Mungu atakuwezesha kumuua Goliathi. Mungu anapotaka kukuinua lazima aruhusu tatizo ambalo wewe peke yako ndo utakuwa na jibu lake.

 9. Tunajifunza pia kwamba matatizo siku zote yapo tu haijalishi unafanya kazi gani. Usifikirie kwamba ukiwa mtumishi basi majaribu yanapungua.ooh, mengi tu. Popote  ulipo jifunze kuwa mwaminifu na Bwana atakuinua. Daudi alikuwa mwaminifu kwa kuhakikisha usalama wa wanyama malishoni ndipo Mungu akamwamini na kumpa Taifa zima la Israel. Umeshindwa kuongoza familia yako, utawezaje kuendesha kanisa la watu mia? Umeshindwa kuongoza idara ya watu 6 unataka kuwa mkurugenzi wa kampuni ili iweje? Usije sema labda nikioa ndo nitaacha uzinzi, labda nikipata milioni mia ndio nitaacha wizi, au labda nikibadilishiwa kazi ndo nitaacha rushwa. HAPANA, tenda kwa uaminifu hapohapo ulipo na Bwana atakuona.

 10. Katika kila jambo, hata kama dunia nzima watasema hili haliwezekani wewe soma LUKA 1:37. “hakuna la kumshinda Mungu” Ndio maana kaka zake  walipomkebehi Daudi, yeye hakujali akamfuata Goliathi na kumuua. Vikwazo vya mafanikio yako vinaweza kutokea hata ndani ya familia yako au kwa watu wako wa karibu sana, tena wanaoonekana wenye uwezo kuliko wewe, hakuna sababu ya kukata tamaa ni mwanzo mwisho tunasonga mbele. Umetengwa baada ya kumpokea Yesu? Kaza buti songa mbele mpaka Goliathi atie amri chini.

 11. Daudi hakufurahia watu wa Mungu wanapotukanwa. Kama mtu wa Mungu kamwe usifurahie watu wanapomsema mtumishi wa Mungu vibaya, hata kama ni kweli katenda uovu, endapo ni mpakwa mafuta wa Bwana kuna utaratibu wa kuyasema na si kuropoka tu. Kumbuka watu wa karibu ya Musa waliadhibiwa na Mungu kwa sababu walimsema vibaya Musa japokuwa ni kweli alikosea.

 12. Vita kati ya wana wa Israeli na wafilisti vinawakilisha vita vya watu wa Mungu dhidi ya Shetani na jeshi lake na imetupasa kulishinda kwa kukaa ndani ya Neno(ujumla wa huduma tano kanisani) na kulitumia Jina la Bwana.

 13. Shetani ana mikwara mingi sana. Anatumia ufahamu wetu kutufanya tuhisi kwamba yeye anaweza zaidi yetu. Goliathi alitumia muda mwingi kuwatisha majeshi ya wana wa Israeli, kama ilivyo leo shetani anavyokutisha kwamba hutapona, hutafanikiwa, utakufa, utachekwa ukiokoka nk. Daudi hakutishwa kamwe. Unapoiruhusu roho ya hofu ndani yako basi unafanyika mateka wa Shetani. Tunatakiwa kuangusha ngome za fikra zetu zipate kutii uwezo wa Jina la Bwana badala ya kuogopeshwa na matatizo. Tatizo lako ni la muda mfupi tu amini sasa na Bwana atakutokea na kukushindia.

 14. Usijadiliane na adui. Wana wa Israeli walitakiwa kujipanga kuvamia, kwa mfano wangeamua watu sita wamvamie Goliathi na wengine wavamie jeshi la wafilisti wangemaliza kelele zote za Goliathi. Kitendo cha kujadiliana na Goliathi kilimpa Goliathi nafasi ya kuingiza hofu mioyoni mwao, don’t compromise with devil’s deceptions /techniques.

 15. Daudi alivaa nguo za kijeshi lakini akavua baada ya kuona hazimfai. Maana yake unaweza kujaribu suluhisho/njia za mtu mwingine lakini haishauriwi kwa sababu Mungu alikuumba wewe original, unapocopy na kupaste maana yake uwezo wako na wajibu wako unauweka kuwa kipolo na ufanisi wako unaweza kuwa na matunda kidogo. Japokuwa unaweza usijue kama matunda yako ni madogo. Usiseme kwa sababu wengi wanasoma sheria au udaktari basi na mimi lazima nisome, usiseme kwa kuwa wengi wanapinga Injili basi na mi naogopa kuwa wa tofauti. Mungu alikuumba ukiwa tofauti kabisa na watu wengine, Mungu huwa hafanyi duplications. Anaumba vitu vipya. Hata mapacha wa kufanana nao wanatofauti kubwa sana. Mungu ana kusudi na maisha yako, tafuta kujua na utende vema.

 16. Kuwa na umri mdogo si kigezo cha kukuzuia kufanya mambo makubwa ya ufalme wa Mungu. Daudi alikuwa na miaka 17 wakati anamuua  Goliathi. Alikuwa mtoto wa mwisho na aliyedharaulika  (katika sura ya 16 mzee Yese hakumuhesabu kati ya watoto wake lakini Samweli alisisitiza kama yuko mwingine ndipo Yese alipoagiza Daudi aitwe kutoka malishoni) lakini alitoa suluhisho la nchi nzima. Jitambue na kuelewa ni hazina gani Mungu ameweka ndani yako! Leo kuna milionea wengi tu ulaya ambao wana umri wa miaka ishirini, hata wewe unaweza kuwa miongoni mwao. Hii ndio sababu sioni ugumu kufundisha na kuandika masomo ya mahusiano, kwa sababu Mungu amenifundisha hata kabla sijaoa.

 17. Mtu asiyetahiriwa (asiye na agano la Mungu, yaani mganga wa kienyeji, mchawi, mshirikina, kibaka, mwuaji, na wafananao na hao) hana uwezo wa kuyatisha maisha yako ukimtegemea Kristo.

 18. Daudi akasema asizimie moyo mtu yeyote kwa ajili ya huyu, mimi mtumishi wako nitakwenda kupigana na mfilisti huyu. Nami nakuambia leo usizimie moyo kwa ajili ya jambo hilo (Ukosefu wa ajira, ugonjwa, fitina, umasikini nk) maana katika yote tunaye atushindiaye, Kristo atayamulika mapito yako na kukushika kwa mkono wake wa kuume pale tu utakapoamua kumwamini kwa moyo wako wote.

 19. Daudi alimkata kichwa Goliathi kwa upanga (Neno la Mungu ni kama upanga). Kwa hiyo hakikisha unapoingia vitani una neno la Mungu la kutosha na unaliweka katika matendo, hata Yesu alipojaribiwa alitumia Neno la Mungu kwa ufasaha na akamshinda shetani.

 20. Mfalme Sauli hakumwacha Daudi arudi nyumbani kwake. Unapokuwa mshindi, yaani umeleta suluhisho au kufanya jambo la kipekee sehemu fulan(kanisani, ofisini, idarani, wizarani, ndani ya taasisi nk) lazima heshima yako itapanda tu, bosi atatamani uwe assistant wake, Daudi kutoka malishoni mpaka kuishi ikulu si mchezo. Fanya vizuri sehemu uliyopo ndipo Mungu atakupeleka hatua ya juu zaidi, kuwa mnyenyekevu, mwenye bidii na mcha Mungu.

Ubarikiwe sana msomaji wangu, yapo Mengi ya kujifunza lakini kwa sasa tuishie hapa, mweleze na ndugu yako na rafiki yako habari hizi njema na za kuleta tumaini jipya kwa kizazi hiki. Haleluuuya!!

–Mussa Kisoma

Roho ya Kukataliwa

kukataliiwa

Roho ya kukataliwa inawasumbua watu wengi. Wengi wanaosumbuka na kukataliwa inawezekana walikuwa na wazazi wasiojali, wazazi walitengana, wamelelewa na mzazi wa kambo, hawakuwa vizuri darasani, n.k. Kukataliwa kunaumiza sana na kunaua kabisa hali ya kujiamini na shetani huitumia sana kuharibu maisha ya watu. Shetani anawafanya watu wasahau kabisa juu ya upendo wa Mungu na kuendelea kuumia na kuteseka.

EFE. 3:19 “na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu.”

Kukataliwa kunaleta vidonda kwenye hisia na visipotibiwa hukua na kuwa vidonda vya kiroho kama kutokusamehe, wivu, chuki, uchungu na kumlaumu Mungu. Vidonda hivi hufungua milango kwa roho chafu kukuingilia kupitia milango hiyo. Shetani anafurahia moyo wako ukijaa mawazo mabaya juu ya watu wengine unaowaona kwamba hawajakutendea mema.

Kukataliwa kunamfanya mtu kuwa na tabia zifuatazo:
1. Uasi
2. Unafiki (ukiwa mbele za watu fulani unabadilika ili ukubalike)
3. Kukataa wengine
4. Kila wakati kujihisi kuwa unakataliwa
5. Kuhitaji sana kukubaliwa na kila mtu
6. Kujihurumia
7. Kutokuwa tayari kukosolewa au kusahihishwa
8. Kutokuweza kupokea wala kuonyesha upendo.
9. Kumlaumu Mungu kwa hali uliyonayo
10. Kiburi
11. Ukiwa hata ukizungukwa na watu.
12. Kujiona huna thamani, wala tumaini
13. Wivu, chuki na husuda.

Wengine wanahisi kukataliwa wakati si kweli. Roho hii ya kukataliwa inakufanya uone kama kila ambaye hajafanya jambo fulani kukusaidia au kukufurahia basi anakukataa. Biblia inasema aonavyo nafsini mwake ndivyo alivyo. Pia kuna wanaojikataa wenyewe na kupelekea kujichukia. Hali hii hutokana na kushindwa kujisamee kwa kosa fulani ukilotenda siku za nyuma na likakuletea madhara makubwa.

Unapoweka thamani yako kwa wanadamu ni lazima utaona kukataliwa na kujikuta unaruhisu roho za kukataliwa kuingia kwako. Lazima utambue kuwa thamani yako inatoka kwa Mungu na si wanadamu wanakuonaje. Haijalishi nani anasema nini bali tafuta Mungu anasema nini. Acha kumlaumu Mungu na kujilaumu unayopitia, biblia imasema mapito ya mwenye haki ni mengi lakini Bwana humlinda na hayo yote.

Usiruhusu chuki, uchungu, hasira na wivu vipate nafasi ndani ya moyo wako. Soma neno la Mungu lijae ndani yako na maombi kwa wingi. Kataa roho ya kukataliwa isipate kibali ndani yako kwa kuondoa milango ambayo ni kutokusamehe, chuki, wivu, uchungu na kumlaumu Mungu. Usiangalie yule aliyekutendea mabaya na kukukataa kama vile yeye ndiye mwenye hatima ya maisha yako bali muangalie Mungu aliyeahidi kuwa nawe siku zote.

EBR. 13:5b-6
“kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa. Hata twathubutu kusema, Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?”

Mambo ya kufanya kushinda kukataliwa
1. Mruhusu Roho mtakatifu akuonyeshe umeumizwa wapi na kwa kiasi gani kwa kukataliwa.
2. Samehe wale waliokuumiza
3. Tupilia mbali matunda ya kukataliwa: chuki, hasira, uasi, uchungu n.k.
4. Kubali kuwa Mungu amekukubali kupitia Yesu Kristo.
5. Jikubali

ZAB. 71:5-7, 13 
“Maana ndiwe taraja langu, Ee Bwana MUNGU, Tumaini langu tokea ujana wangu.    Nimekutegemea Wewe tangu kuzaliwa, Ndiwe uliyenitoa tumboni mwa mama yangu, Ninakusifu Wewe daima.    Nimekuwa kitu cha ajabu kwa watu wengi, Na Wewe ndiwe kimbilio langu la nguvu.    Waaibishwe, watoweshwe, adui za nafsi yangu. Wavikwe laumu na aibu wanaonitakia mabaya.”

Soma pia Ebrania 4:16 Zaburi 23 1 Samwel 53:4

–WomenofChrist Blog

Ubatizo Wa Roho Mtakatifu

rm

Mtu anaposoma kitabu cha Matendo ya Mitume, utendaji wa Roho Mtakatifu katika kanisa la kwanza ni dhahiri kwenye kila ukurasa. Ukiondoa kazi ya Roho Mtakatifu katika kitabu cha Matendo, huna kitu kilichobaki. Kweli, aliwatia nguvu wanafunzi wa kwanza ili “kuupindua ulimwengu” (tazama Matendo 17:6).

Siku hizi katika dunia yetu, mahali ambapo kanisa linakua kwa haraka ni pale ambapo wafuasi wa Yesu wamejitoa kwa Roho Mtakatifu kabisa na kuwezeshwa Naye. Hili lisitushangaze. Roho Mtakatifu anaweza kufanikisha mambo mengi kwa muda wa nukta kumi kuliko tunayoweza kufanikisha sisi kwa muda wa miaka elfu kumi, kwa juhudi zetu. Kwa hiyo, ni kitu muhimu sana kwamba mtumishi anayefanya watu kuwa wanafunzi aelewe Maandiko yanafundisha nini juu ya kazi ya Roho Mtakatifu katika maisha na huduma za waamini.

Mara kwa mara katika kitabu cha Matendo ya Mitume tunapata mifano ya waamini wakibatizwa kwa Roho Mtakatifu na kuwezeshwa kufanya huduma. Tuwe na busara kujifunza somo hili ili ikiwezekana, hata sisi tupate walichopata na kufurahia msaada wa kimuujiza waliopata wao kutoka kwa Roho Mtakatifu. Ingawa kuna wanaodai kwamba matendo hayo ya miujiza ya Roho Mtakatifu ilikuwa ni kwa ajili ya wakati wa mitume wenyewe tu, mimi sipati hoja ya kiMaandiko, kihistoria wala ya kiakili, yenye kuunga mkono maoni hayo. Wale wanaoamini kinachoahidiwa katika Neno la Mungu watapata baraka zilizotajwa. Sawa na Waisraeli ambao hawakuamini, walioshindwa kuingia katika Nchi ya Ahadi, wale wasioamini ahadi za Mungu kwa leo watashindwa kuingia katika yote ambayo Mungu amewaandalia. Je, wewe uko kundi gani? Mimi niko miongoni mwa wenye kuamini!

Kazi Mbili Za Roho Mtakatifu

Kila mtu aliyemwamini Bwana Yesu Kristo kabisa amefanyiwa kazi na Roho Mtakatifu maishani mwake. Utu wake wa ndani – au roho – umezaliwa upya kwa Roho Mtakat ifu (ona Tito 3:5), na Roho Mtakatifu anakaa ndani yake (ona Warumi 8:9; 1Wakor. 6:19). Yeye “amezaliwa kwa Roho” (Yohana 3:5).

Kwa kutoelea hili, Wakristo wengi wa Pentekoste na Karizmatiki wamekosea kwa kuwaambia waamini fulani kwamba hawakuwa na Roho Mtakatifu kama hawakuwa wamebatizwa kwa Roho Mtakat ifu na kunena kwa lugha. Hili ni kosa kutokana na Maandiko na hata ujuzi halisi wa maisha. Waamini wengi wasiokuwa WaPentekoste au WaKarizmatiki wana ushuhuda zaidi kwamba Roho anakaa ndani yao kuliko baadhi ya waamini wa KiPentekoste au KiKarizmatiki! Wanaonyesha matunda ya Roho yaliyotajwa na Paulo katika Wagalatia 5:22-23 kwa kiwango kikubwa sana, kitu ambacho kisingewezekana bila kuwa na Roho Mtakatifu ndani.

Kwa kuwa tu mtu amezaliwa na Roho si uhakikisho kwamba amebatizwa pia kwa Roho Mtakatifu. Kulingana na Biblia, kuzaliwa na Roho Mtakatifu na kubatizwa kwa Roho Mtakatifu ni vitu viwili tofauti.

Tunapoanza kuchambua mada hii, hebu kwanza tutazame yale ambayo Yesu aliyasema wakati fulani kuhusu Roho Mtakatifu, kwa mwanamke asiyeokoka, huko kisimani Samaria.

Kama ungeliijua karama ya Mungu naye ni nani akuambiaye, ‘Nipe maji ninywe’, ungalimwomba yeye naye angelikupa maji yaliyo hai. … Kila anywaye maji haya [kutoka kisimani] ataona kiu tena; walakini yeyote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele (Yohana 4:10, 13-14).

Ni halali kufikiri kwamba yale maji yanayokaa ndani ya mtu ambayo Yesu alizungumzia ni Roho Mtakatifu, anayekaa ndani ya wale wanaoamini. Baadaye katika Injili ya Yohana, Yesu alitumia tena maneno “maji yaliyo hai”, na hapo hakuna shaka kwamba alikuwa anazungumza juu ya Roho Mtakatifu.

Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama na kupaza sauti yake, akasema hivi: ‘Mtu akiona kiu na aje kwangu anywe. Aniaminiye mimi kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.’ Na neno hilo alilisema kwa habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa (Yohana 7:37-39, TLR. Maneno mepesi kukazia).

Hapa, Yesu hakuzungumza juu ya maji yaliyo hai kuwa “chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele”. Badala yake, hayo maji yaliyo hai yanafanyika mito ibubujikayo kutoka ndani ya mwenye kupokea.

Mafungu haya mawili ya Maandiko kutoka Injili ya Yohana huonyesha vizuri sana tofauti kati ya kuzaliwa kwa Roho na kubatizwa kwa Roho Mtakatifu. Kuzaliwa kwa Roho ni kwa faida ya yule aliyezaliwa upya, ili aweze kufurahia uzima wa milele. Mtu anapozaliwa tena kwa Roho, anapata hifadhi ya Roho ndani yake yenye kumpa uzima wa milele.

Lakini kubatizwa kwa Roho Mtakatifu ni kwa faida ya wengine, maana inawawezesha waamini kuwahudumia watu wengine kwa nguvu za Roho. “Mito ya maji yaliyo hai” itabubujika kutoka ndani yao, ikileta baraka za Mungu kwa wengine kwa nguvu za Roho Mtakatifu.

Ubatizo Wa Roho Mtakatifu Unahitajika Kwa Nini?

Tunahitaji sana msaada wa Roho Mtakatifu ili tuweze kuwahudumia wengine! Bila msaada Wake, hatuwezi kutumaini kuwafanya watu wote kuwa wanafunzi. Hiyo ndiyo sababu hasa iliyomfanya Yesu kuahidi kuwabatiza waamini kwa Roho Mtakatifu – ili dunia ipate kusikia Injili. Aliwaambia hivi wanafunzi Wake:

Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu, lakini kaeni humu mjini hata mvikwe uwezo utokao juu (Luka 24:49 – Maneno mepesi kutilia mkazo).

Luka tena anaandika maneno mengine ya Yesu, kwamba:

Si kazi yenu kujua nyakati wala majira, Baba aliyoyaweka katika mamlaka yake mwenyewe. Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi (Matendo 1:7-8. Maneno mepesi kutilia mkazo).

Yesu aliwaambia wanafunzi Wake hata wasiondoke Yerusalemu mpaka “wavikwe uwezo kutoka juu.” Alijua wasingekuwa na uwezo kama si hivyo, na wangeshindwa kabisa kutekeleza kazi aliyokuwa amewapa. Tunaona kwamba mara baada ya kubatizwa kwa Roho Mtakatifu, Mungu alianza kuwatumia wao kwa njia ya ajabu sana kueneza Injili.

Wakristo milioni nyingi duniani, baada ya kubatizwa na Roho Mtakatifu, wamefahamu na kutambua kiwango kipya cha nguvu, hasa wakati wa kuwashuhudia watu ambao hawajaokoka. Waligundua kwamba maneno yao yalikuwa na maana zaidi, na kwamba wakati mwingine walitaja maandiko ambayo hawakujua waliyafahamu. Baadhi yao walijikuta wenyewe wakiwa wameitwa na kupewa karama kwa ajili ya huduma fulani, kama vile uinjilisti. Wengine waligundua kwamba Mungu aliwatumia kama alivyopenda katika karama mbalimbali za Roho Mtakatifu. Ujuzi wao ni wa KiBiblia kabisa. Wale wanaopinga ujuzi wao hawana msingi wowote KiBiblia kwa ajili ya kuwapinga. Ukweli ni kwamba wanapingana na Mungu.

Isitushangaze sisi ambao tumeitwa kumwiga Kristo kwamba tumeitwa kuiga ujuzi Wake na ROho Mtakatifu. Yeye alitungwa mimba tumboni mwa Mariamu kwa Roho Mtakatifu (ona Mathayo 1:20). Yeye aliyezaliwa kwa Roho alikuja kubatizwa na Roho kabla ya kuanza huduma Yake (ona Mathayo 3:16). Kama Yesu alihitaji kubatizwa na Roho Mtakatifu ili kumwezesha katika huduma, sisi je?

Ushahidi Wa Kwanza Kwamba Mtu Amebatizwa Katika Roho Mtakatifu

Mwamini anapobatizwa katika Roho Mtakatifu, ushahidi wa kwanza wa ujuzi wake ni kwamba ananena kwa lugha mpya, au kama Maandiko yanavyosema wakati mwingine, “lugha nyingine.” Kuna maandiko mengi sana yanayothibitisha jambo hilo. Hebu tuyatazame.

Kwanza – Muda mfupi tu kabla ya kupaa Kwake, yesu alisema kwamba mojawapo ya ishara zitakazofuatana na waamini ni kwamba wangesema kwa lugha mpya.

Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka, asiyeamini atahukumiwa. Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio: kwa jina langu watatoa pepo, watasema kwa lugha mpya (Marko 16:15-17. Maneno mepesi kutilia mkazo).

Kuna waandishi wa vitabu vya mafafanuzi vya Biblia wanaodai kwamba maandiko hayo hayapaswi kuwa katika Biblia zetu kwa sababu baadhi ya magombo fulani ya zamani ya Agano Jipya hayana fungu hilo. Lakini, mengi katika magombo ya kale yana fungu hilo, na hakuna tafsiri nyingi za Kiswahili za Biblia ambazo hazina fungu hilo. Tena, yale ambayo Yesu alisema katika maandiko haya yanalingana vizuri tuna ujuzi wa kanisa la kwanza kama tunavyopata habari zake katika kitabu cha Matendo ya Mitume.

Kuna mifano mitano katika kitabu cha Matendo, yenye kuonyesha waamini wakibatizwa kwa mara ya kwanza na Roho Mtakatifu. Hebu tuitazame yote, na tutakapokuwa tunafanya hivyo, tutajiuliza maswali mawili yafuatayo: (1) Je, Ubatizo kwa Roho Mtakatifu ulikuwa ni kitu baada ya wokovu? Na (2) Je, waliopokea walinena kwa lugha mpya? Hii itatusaidia kuelewa mapenzi ya Mungu kwa ajili ya waamini siku za leo.

Yerusalemu

Mfano wa kwanza unapatikana katika Matendo sura ya 2, wakati wale wanafunzi mia na ishirini walipobatizwa kwa Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste.

Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja. Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka (Matendo 2:1-4. Maneno mepesi kutilia mkazo).

Hakuna shaka yoyote kwamba wale waamini mia na ishirini walikuwa wamekwisha okoka na kuzaliwa mara ya pili kabla ya wakati huo. Basi, walipokea ubatizo wa Roho Mtakatifu baada ya wokovu. Hata hivyo isingewezekana kwao kubatizwa katika Roho Mtakatifu kabla ya wakati huo kwa sababu Roho Mtakatifu hakuwa ametolewa kwa kanisa kabla ya siku hiyo.

Ni dhahiri basi kwamba ishara iliyoambatana na tendo hilo ilikuwa kunena kwa lugha nyingine.

Samaria

Mfano wa pili wa waamini kubatizwa kwa Roho Mtakatifu unapatikana katika Matendo sura ya 8, wakati Filipo alipokwenda jijini Samaria na kuhubiri Injili huko.

Lakini [WaSamaria] walipomwamini Filipo, akizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake. … Na mitume waliokuwako Yerusalemu waliposikia ya kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu, wakawapelekea Petro na Yohana, ambao waliposhuka, wakawaombea wampokee Roho Mtakatifu, kwa maana bado hajawashukia hata mmoja wao, ila wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu (Matendo 8:12-16).

Ni wazi kwamba Wakristo WaSamaria walipokea ubatizo wa Roho Mtakatifu kama kitu cha zaidi baada ya wokovu wao. Biblia inasema wazi kabisa kwamba kabla Petro na Yohana hawajafika, WaSamaria tayari walikuwa “wamelipokea neno la Mungu,” wameiamini Injili na kubatizwa katika maji. Lakini, wakati Petro na Yohana walipokuja kuwaombea, Maandiko yanasema ni ili wampokee Roho Mtakatifu.” Iwekwe wazi zaidi kuliko hapo jamani?

Je, waamini wa Samaria walinena kwa lugha mpya walipobatizwa kwa Roho Mtakatifu? Biblia haisemi, lakini inasema kwamba kitu cha kushangaza kilitokea kwao. Wakati mtu aitwaye Simoni alipoona yaliyotokea baada ya Petro na Yohana kuweka mikono yao juu ya Wakristo wa Samaria, alijaribu kununua kutoka kwao uwezo huo huo wa kumtoa Roho Mtakatifu.

Ndipo wakaweka mikono yao juu yao, nao wakampokea Roho Mtakatifu. Hata Simoni alipoona ya kuwa watu wanapewa Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono ya mitume, akataka kuwapa fedha akisema, ‘Nipeni na mimi uwezo huu, ili kila mtu nitakayemweka mikono yangu apokee Roho Mtakatifu’ (Matendo 8:17-19).

Je, Simoni aliona nini kilichomshika hivyo? Tayari alikwisha ona miujiza mingi tu mingine, kama vile watu wakitolewa mapepo na waliolemaa na viwete wakiponywa (ona Matendo 8:6-7). Yeye mwenyewe alikuwa amehusika katika uchawi hapo kwanza, akiwashangaza watu wote wa Samaria (ona Matendo 8:9-10). Kama ni hivyo, alichokiona wakati Petro na Yohana walipoomba lazima kingekuwa kitu cha ajabu sana. Ingawa hatuwezi kusema kwa uhakika kabisa, inaonekana ni sawa kufikiri kwamba aliona kitu cha kushangaza kile kile kilichokuwa kinatokea kila mara ambapo Wakristo walipokea Roho Mtakatifu katika kitabu cha Matendo ya Mitume – aliona na kuwasikia watu wa Samaria wakinena kwa lugha nyingine.

Sauli Huko Dameski

Mara ya tatu katika kitabu cha Matendo kunapotajwa mtu akimpokea Roho Mtakatifu ni kwa habari ya Sauli wa Tarso, ambaye baadaye alijulikana kama mtume Paulo. Aliokolewa akiwa njiani kwenda Dameski, na alikuwa amepofuka kwa muda. Siku tatu baada ya kuokoka kwake, mtu aitwaye Anania alitumwa kwake na Mungu.

Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani, akamwekea mikono akisema, ‘Ndugu Sauli! Bwana amenituma, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu.’ Mara vikaanguka machoni pake vitu kama magamba, akapata kuona, akasimama, akabatizwa (Matendo 9:17, 18).

Hapana shaka kwamba Sauli aliokoka kabla ya Anania kufika kumwombea. Alimwamini Bwana Yesu alipokuwa yungali njiani kwenda Dameski, na mara moja akatii maagizo ya Bwana wake mpya. Tena, wakati Anania alipokutana na Sauli mara ya kwanza alimwita “Ndugu Sauli.” Ona kwamba Anania alimwambia Sauli kwamba amekuja ili apate kuona na kujazwa na Roho Mtakatifu. Basi kwa Sauli, kujazwa na Roho Mtakatifu – au kubatizwa basi – kulitokea siku tatu tu baada ya kuokoka kwake.

Maandiko hayasemi tukio hilo la Sauli kubatizwa na Roho Mtakatifu, lakini bila shaka lilifanyika muda mfupi tu baada ya Anania kufika mahali Sauli alipokuwa. Hakuna shaka kwamba Sauli alinena kwa lugha kwa sababu, baadaye anasema katika 1Wakor. 14:18 hivi: “Namshukuru Mungu kwamba mimi nanena kwa lugha kuliko ninyi wote” (TLR).

Kaisaria

Mara ya nne ambapo waamini wanatajwa kwamba wamebatizwa kwa Roho Mtakatifu ni katika Matendo 10. Mtume Petro alikuwa ameagizwa na Mungu kwenda kuhubiri Injili huko Kaisaria, nyumbani kwa Kornelio. Mara tu baada ya Petro kudhihirisha kwamba wokovu hupokelewa kwa imani katika Yesu, wasikilizaji wake wote waliokuwa si Wayahudi (yaani, WaMataifa) waliitikia kwa imani, na Roho Mtakatifu akawashukia.

Petro alipokuwa akisema maneno hayo Roho Mtakatifu akawashukia wote waliolisikia lile neno. Na wale waliotahiriwa, walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu Mataifa nao wamemwagiwa kipawa cha Roho Mtakatifu. Kwa maana waliwasikia wakisema kwa lugha na kumwadhimisha Mungu. Ndipo Petro akajibu, ‘Ni nani awezaye kuzuia maji, hawa wasibatizwe, watu waliopokea Roho Mtakatifu vile vile kama sisi?’ Akaamuru wabatizwe kwa Jina lake Yesu Kristo (Matendo 10:44-48a).

Hapa, inaonekana kwamba watu wote wa nyumbani mwa Kornelio, waliokuwa wasiokuwa Wayahudi wa kwanza kumwamini Yesu, walizaliwa mara ya pili na kubatizwa hapo hapo.

Tukijifunza maandiko yanayoambatana na hayo pamoja na mantiki kihistoria, kuna sababu iliyo dhahiri kabisa iliyomfanya Mungu asingojee Petro na waamini wenzake wawawekee mikono waamini wale wasiokuwa Wayahudi, ili wapokee Roho Mtakatifu. Petro na waamini wanzake wa Kiyahudi walikuwa na shida sana kuamini kwamba wasiokuwa Wayahudi wanaweza kuokoka – achilia mbali kumpokea Roho Mtakatifu! Yawezekana wasingewaombea familia ya Kornelio wapokee ubatizo wa Roho Mtakatifu. Basi Mungu akafanya kwa enzi Yake. Mungua likuwa anamfundisha Petro na wenzake kitu kuhusu neema Yake ya ajabu kwa wasiokuwa Wayahudi.

Kilichomshawishi Petro na wale waamini wengine Wayahudi kwamba familia ya Kornelio walipokea Roho Mtakatifu kweli ni nini? Luka anaandika hivi: “Kwa maana waliwasikia wakisema kwa lugha” (Luka 10:46). Petro akatamka kwamba wasiokuwa Wayahudi wamempokea Roho Mtakatifu kama wale mia na ishirini walivyofanya siku ya Pentekoste (ona 10:47).

Efeso

Mara ya tano ambapo waamini wanatajwa kubatizwa katika Roho Mtakatifu ni katika Matendo sura ya 19. Alipokuwa anasafiri na kupitia Efeso, mtume Paulo alikutana na wanafunzi fulani, akawauliza hivi: “Je, mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini?” (Matendo 19:2, TLR).

Paulo, mtu aliyeandika sehemu kubwa ya nyaraka za Agano Jipya aliamini dhahiri kabisa kwamba inawezekana kumpokea Yesu na usiwe umempokea Roho Mtakatifu.Vinginevyo, asingeuliza swali alilouliza.

Wale ndugu wakajibu kwamba hawakuwa hata wamesikia kuhusu Roho Mtakatifu. Ni kwamba walikuwa wamesikia kuhusu Masiye anayekuja tu kupitia Yohana Mbatizaji, ambaye alikuwa amewabatiza. Paulo mara moja akawabatiza tena kwa maji, na wakati huu wakawa wamebatizwa Kikristo. Hatimaye, Paulo akawawekea mikono ili wapokee Roho Mtakatifu.

Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu. Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao, wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri. Na jumla yao walipata wanaume kumi na wawili (Matendo 19:5-7).

Hapa tena ni kitu wazi kwamba ubatizo wa Roho Mtakatifu ulikuwa baada ya wokovu, bila kujali kama hao watu kumi na mbili walikuwa wameokoka kabla ya kukutana na Paulo. Tena, ishara iliyoambatana na wao kubatizwa kwa Roho Mtakatifu ilikuwa kunena kwa lugha (na hapa, kutabiri pia).

Sawa – Hebu tuitazame tena ile mifano mitano. Katika mifano minne, ubatizo kwa Roho Mtakatifu ulikuwa kitu kilichotokea baada ya wokovu.

Katika mifano mitatu, Maandiko yanasema wazi kabisa kwamba wahusika walinena kwa lugha nyingine. Tena, Paulo alipokutana na Anania, yeye kubatizwa kwa Roho Mtakatifu hakuelezwi, lakini tunajua kwamba hatimaye alikuja kunena kwa lugha. Huo ni mfano wa nne.

Katika mfano uliosalia, kitu kisicho cha kawaida kilitokea wakati waamini huko Samaria walipompokea Roho Mtakatifu kwa sababu, Simoni alijaribu kununua nguvu za kumtoa Roho Mtakatifu.

Basi, ushahidi uko wazi kabisa. Katika kanisa la kwanza, waamini waliozaliwa mara ya pili walipata kitu kingine na Roho Mtakatifu, na walipofanya hivyo, walinena kwa lugha nyingine. Hii isitushangaze kwa sababu Yesu alisema wale wanaomwamini watanena kwa lugha nyingine.

Tunao ushahidi thabiti kabisa kwamba kila mtu aliyezaliwa mara ya pili anatakiwa pia kupokea kazi nyingine ya Roho Mtakatifu – kubatizwa katika Roho Mtakatifu. Tena, kila mwamini anapaswa kutazamia kunena kwa lugha nyingine wakati anapobatizwa kwa Roho Mtakatifu.

Jinsi Ya Kupokea Ubatizo Wa Roho Mtakatifu

Roho Mtakatifu hupokelewa kwa imani (Wagal. 3:5), sawa tu na zawadi nyingine zote za Mungu. Ili kuwa na imani ya kupokea, mwamini anatakiwa kwanza ashawishike kwamba ni mapenzi ya Mungu kwake kubatizwa kwa Roho Mtakatifu. Kama ana mashaka au wasiwasi, hatapokea (ona Yakobo 1:6-7).

Hakuna mwamini yeyote mwenye sababu nzuri ya kuamini kwamba si mapenzi ya Mungu kwake kupokea Roho Mtakatifu, kwa sababu Yesu alieleza waziwazi mapenzi ya Mungu kuhusu swala hilo.

Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao? (Luka 11:13).

Ahadi hiyo kutoka kwa Yesu inapaswa kumwaminisha kila mtoto wa Mungu kwamba ni mapenzi ya Mungu yeye apokee Roho Mtakatifu.

Mstari huo huo pia unathibitisha ukweli kwamba kubatizwa kwa Roho Mtakatifu hutokea baada ya wokovu, kwa sababu hapa Yesu aliwaahidi watoto wa Mungu (watu pekee ambao Mungu ndiye “Baba yao wa mbinguni”) kwamba angewapa Roho Mtakatifu, wakiomba. Bila shaka ni kwamba, kama ujuzi pekee na Roho Mtakatifu ambao mtu angepata ni kuzaliwa mara ya pili wakati wa wokovu tu, basi ahadi ya Yesu isingekuwa na maana. Kinyume na kikundi cha wanatheolojia wachache wa kisasa ambacho kinaelekea kutoweka, Yesu aliamini kwamba ni sawa kabisa kwa watu waliokwisha zaliwa mara ya pili kumwomba Mungu awape Roho Mtakatifu.

Kwa maneno ya Yesu, kuna masharti mawili tu ambayo lazima mtu atimize ikiwa anataka kupokea Roho Mtakatifu. Kwanza – Mungu lazima awe Baba, na ndivyo ilivyo kama umezaliwa mara ya pili. Pili – umwombe Roho Mtakatifu.

Pamoja na kwamba kumpokea Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono ni kitu kinachoungwa mkono na Maandiko (ona Matendo 8:17; 19:6), si lazima. Mkristo yeyote anaweza kumpokea Roho Mtakatifu akiwa peke yake katika faragha yake ya maombi. Anachohitaji kufanya ni kuomba tu, kupokea kwa imani, na kuanza kunena kwa lugha kama Roho atakavyomwezesha kutamka.

Hofu Za Wengi

Kuna watu wenye kuogopa kwamba wakiomba Roho Mtakatifu, wanaweza kujiweka wazi kuingiwa na pepo. Hakuna msingi wowote wa hofu kama hiyo. Yesu aliahidi hivi:

Maana ni yupi kwenu aliye baba, ambaye mwanamwe akimwomba mkate atampa jiwe, au samaki, badala ya samaki atampa nyoka? Au akiomba yai, atampa nge? Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba yenu wa mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao? (Luka 11:11-13).

Tukiomba Roho Mtakatifu, Mungu atatupa Roho Mtakatifu. Tusiwe na hofu kwamba tutapokea kitu kingine chochote!

Kuna wengine wenye kuogopa kwamba, wakinena kwa lugha, ni kitu chao watakachokuwa wametunga badala ya lugha ya kimuujiza itolewayo na Roho Mtakatifu. Sawa – ila, kama utajaribu kutunga lugha ya hakika kabla ya kubatizwa na Roho Mtakatifu utagundua kwamba ni kitu kigumu sana, kisichowezekana. Ila, ni lazima uelewe kwamba kama utanena kwa lugha nyingine, itakubidi utumie midomo yako, ulimi, na ngano za sauti. Roho Mtakatifu hakusemei – anakupa lugha. Yeye ni msaidizi wetu, si anayetenda. Inakupasa weweuseme. Ni kama Biblia inavyofundisha, kwamba:

Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka (Matendo 2:4 – Maneno mepesi kutilia mkazo).

Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanzakunena kwa lugha (Matendo 19:6 – Maneno mepesi kutilia mkazo).

Baada ya mwamini kuomba zawadi ya Roho Mtakatifu, anatakiwa kuamini na kutazamia kunena kwa lugha nyingine. Kwa kuwa Roho Mtakatifu anapokelewa kwa imani, mwenye kupokea asitazamie hisia za namna fulani au msisimko kimwili. Anatakiwa kufungua kinywa chake tu na kuanza kutamka zile sauti mpya na silabi zitakazosababisha ile lugha mpya ambayo Roho Mtakatifu anampa. Mwamini asipoanza kusema kwa imani,hakuna maneno yatakayotokea kinywani mwake. Ni lazima yeye aseme, ndipo Roho Mtakatifu atakapomjalia kutamka.

Mahali Lugha Inapotoka

Kulingana na Paulo – aaminiye anapoomba kwa lugha – si akili yake iombayo bali ni roho yake.

Maana nikiomba kwa lugha,roho yangu huomba, lakini akili zangu hazina matunda. Imekuwaje, basi? Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia, nitaimba kwa roho, tena nitaimba kwa akili pia (1Wakor. 14:14-15).

Paulo alisema kwamba alipoomba kwa lugha, akili yake haikuwa na matunda. Maana yake ni kwamba akili yake ilikuwa haihusiki, wala hakuelewa alichokuwa anaomba kwa lugha. Basi, anachosema ni kwamba, badala ya kuomba kwa lugha wakati wote na huku haelewi anachosema, alikuwa pia anaomba kwa akili, kwa lugha yake mwenyewe. Alitumia muda mwingi kuimba kwa lugha na kuimba kwa akili yake pia. Ipo nafasi kwa maombi ya aina zote hizo mbili pamoja na kuimba kwa aina zote hizo mbili, nasi tuwe na busara kufuata mfano wa Paulo.

Ona pia kwamba, kwa Paulo, kunena kwa lugha kulikuwa chini ya mamlaka ya mapenzi yake, sawa na jinsi kuzungumza lugha yake kulivyokuwa. Alisema hivi: “Nitaomba kwa roho na nitaomba kwa akili pia” (TLR). Mara nyingi wakosoaji hudai kwamba kama kunena kwa lugha siku hizi ni zawadi kweli kutoka kwa Mungu, hakuna mtu ambaye angeweza kuitawala, maana kufanya hivyo ni sawa na kumtawala Mungu. Wazo kama hilo halina msingi wowote. Kunena kwa lugha zamani na siku hizi kuko chini ya mamlaka ya mtu binafsi, na ndivyo Mungu alivyopanga. Wakosoaji hao ni vizuri waendelee na kusema kwamba watu wenye mikono ambayo imeumbwa na Mungu kweli hawana mamlaka na utawala juu ya mikono yao, na watu wenye kufanya maamuzi ya kutumia mikono yao wanamtawala Mungu.

Ukisha batizwa kwa Roho Mtakatifu, ni rahisi sana kuthibitisha kwamba kunena kwa lugha kwako kunatoka rohoni na si akilini mwako. Kwanza – Hebu jaribu kuzungumza na mtu huku unasoma mahala hapa. Utaona kwamba huwezi kufanya yote mawili kwa wakati mmoja. Lakini, utagundua kwamba unaweza kuendelea kunena kwa lugha unapoendelea kusoma hiki kitabu. Sababu ni hii: hutumii akili yako kunena kwa lugha – tendo la kunena hutoka rohoni mwako. Basi, unapotumia roho yako kuomba, waweza pia kutumia akili yako kusoma na kuelewa.

Sasa – Kwa Kuwa Umebatizwa Kwa Roho Mtakatifu

Usisahau sababu kuu ya Mungu kukupa ubatizo wa Roho Mtakatifu – ni ili kukutia nguvu kwa ajili ya kuwa shaiidi Wake, kwa madhihirisho ya tunda na karama (au zawadi) za Roho Mtakatifu (ona 1Wakor. 12:4-11; Wagal. 5:22-23). Unapoishi maisha yanayofanana na Kristo na kujonyesha upendo Wake, furaha na amani Yake kwa dunia pamoja na kudhihirisha karama zisizo za kawaida za Roho, Mungu atakutumia kuwavuta wengine Kwake. Uwezo wa kunena kwa lugha ni sehemu moja tu ya “mito ya maji yaliyo hai” inayotakiwa kububujika kutoka ndani mwako.

Pia kumbuka kwamba Mungu alitupa Roho Mtakatifu atuwezeshe kuwafikishia Injili watu wote duniani (ona Matendo 1:8). Tunaponena kwa lugha zingine, tunapaswa pia kutambua kwamba lugha tunayosema inaweza kuwa lugha ya kabila fulani au nchi fulani ya kigeni. Kila mara tunapoomba kwa lugha, tukumbuke kwamba Mungu anataka watu wa kila lugha wasikie habari za Yesu. Tunapaswa kumwomba Bwana kuhusu jinsi anavyotaka sisi tuhusike kutimiza Agizo Kuu la Yesu Kristo.

Kunena kwa lugha ni kitu tunachopaswa kufanya mara nyingi iwezekanavyo. Paulo – mtu wa hali ya juu sana kiroho – aliandika hivi: “Ninamshukuru Mungu kwamba mimi nanena kw alugha zaidi yenu wote” (1Wakor. 14:18, TLR). Aliandika maneno hayo kwa kanisa lililokuwa linanena sana kwa lugha (japo kwa nyakati zisizofaa). Basi, Paulo bila shaka alinena kwa lugha mara nyingi sana mpaka akawazidi. Kuomba kwa lugha hutusaidia kumtambua Roho Mtakatifu anayeishi ndani yetu, na itatusaidia “kuomba bila kukoma” kama Paulo alivyofundisha katika 1Wathes. 5:17.

Vile vile Paulo alifundisha kwamba kunena kwa lugha zingine humjenga mwamini (ona 1Wakor. 14:4). Maana yake ni kwamba inatujenga kiroho. Kwa kuomba kwa lugha, tunatia nguvu utu wetu wa ndani kwa njia tusizoelewa kabisa. Kunena kwa lugha kunatakiwa kuleta utajiri mpya kila siku katika maisha ya kiroho ya kila aaminiye, wala si tukio la wakati mmoja tu tunapojazwa na Roho Mtakatifu mara ya kwanza.

Ukiisha batizwa kwa Roho Mtakatifu, ninakutia moyo utumie muda mwingi kila siku kumwomba Mungu kwa lugha yako mpya. Itakusaidia sana katika maisha yako ya kiroho na kukua kwako kiroho.

Majibu Kwa Maswali Kadhaa Ya Kawaida

Je, tunaweza kuwa na uhakika kabisa kwamba wote ambao hawajawahi kunena kwa lugha hawajabatizwa na Roho Mtakatifu? Mimi nadhani sivyo.

Sikuzote nimewatia watu moyo watazamie kunena kwa lugha wakati nilipowaombea kubatizwa kwa Roho Mtakatifu, nami nadhani asilimia 95 ya hao walifanya hivyo baada ya kuwaombea kwa nukta chache. Ni maelfu ya watu kwa kipindi cha miaka mingi sana.

Lakini siwezi kusema kwamba Mkristo aliyeomba kubatizwa kwa Roho na ambaye hajanena kwa lugha hajabatizwa na Roho Mtakatifu. Hii ni kwa sababu ubatizo wa Roho hupokelewa kwa imani, na kunena kwa lugha ni kitu cha hiari. Ila, nipatapo nafasi ya kuzungumza na mwamini ambaye ameomba kubatizwa na Roho Mtakatifu lakini hajawahi kunena kwa lugha, ninachoanza nacho ni kumwonyesha mtu huyo maandiko yote katika kitabu cha Matendo kuhusu swala lenyewe. Isha, ninamwonyesha huyo mwamini jinsi ambavyo Paulo aliandika, kwamba yeye husimamia wakati wa kunena na wakati wa kutonena kwa lugha. Kama Paulo, mimi mwenyewe naweza kunena kwa lugha wakati wowote ninaotaka, na hivyo naweza kuamua, nikitaka, kutonena tena kwa lugha. Kama ni hivyo, inawezekana nikawa nimebatizwa kwa Roho Mtakatifu na kutonena kwa lugha kwa kutoshirikiana na tamko analoleta Roho Mtakatifu.

Basi – ninapokuwa na nafasi ya kuzungumza na Mkristo ambaye ameomba kwa imani apokee ubatizo wa Roho Mtakatifu lakini hajawahi kunena kwa lugha, simwambii jinsi ambavyo kunena kwa lugha si kitu Roho anachofanya bila sisi. Ninajaribu kumweleza kwamba Roho Mtakatifu ndiye ajaliaye kutamka, lakini sisi lazima tuseme – au tunene – sawa tu na jinsi ambavyo inakuwa mtu anaposema lugha ya kawaida. Kisha ninamtia moyo mtu huyo kushirikiana na Roho Mtakatifu na kuanza kunena kwa lugha. Mara nyingi baada ya hayo, watu hao hunena baadaye.

Je, Paulo Hakuandika Kwamba Si Wote Wanenao Kwa Lugha?

Swali la Paulo – “Kwani ni wote wanenao kwa lugha?” (1Wakor. 12:30) – ambalo jibu lake dhahiri ni “Hapana” lazima litazamwe kwa kuangalia Agano Jipya kwa jumla. Swali lake linapatikana katika mantiki ya mafundisho aliyotoa juu ya karama za kiroho, ambazo zinadhihirishwa kadiri Roho apendavyo tu (1Wakor. 12:11). Paulo alikuwa anaandika kuhusu karama ile ya “aina za lugha” (1Wakor. 12:10), ambayo, kulingana na Paulo, lazima kila mara iambatane na karama ya kiroho ya tafsiri za lugha. Hii karama isingeweza kuwa ile ambayo Wakorintho waliitumia mara kwa mara kanisani mwao, kwa sababu wao walikuwa wananena kwa lugha hadharani pasipo kuwepo na mtu wa kutafsiri. Tunatakiwa kujiuliza hivi: Kwa nini Roho Mtakatifu atoe karama ya lugha kwa mtu katika ibada ya hadhara, bila ya kumpa mtu mwingine karama ya kutafsiri?Jibu ni kwamba hawezi kufanya hivyo, maana akifanya, hawi anaendeleza mapenzi ya Mungu.

Bila shaka Wakorinto walikuwa wanaomba kwa lugha kwa sauti wakati wa ibada zao kanisani bila ya kuwepo na tafsiri aina yoyote. Basi, tunajifunza kwamba kunena kwa lugha kuna matumizi mawili tofauti. Moja ni kuomba katika lugha, ambako Paulo anasema kufanywe kibinafsi. Matumizi hayo hayaambatani na tafsiri, kama Paulo alivyoandika, kwamba, “Roho yangu huomba, lakini akili yangu haina matunda” (1Wakor. 14:14). Ni kwamba Paulo hakujua kila wakati alikuwa anasema nini aliponena kwa lugha. Hakuelewa, wala haikuwepo tafsiri.

Ila pia kuna matumizi ya kunena kwa lugha ambayo ni kwa ajili ya kusanyiko, na hayo huambatana na karama ya tafsiri ya lugha. Hiyo hutokea wakati Roho Mtakatifu anapomjia mtu fulani kama apendavyo, akimpa karama hiyo. Mtu huyo atanena waziwazi, kisha inakuwepo tafsiri. Ila, Mungu hamtumii kila mtu hivyo. Ndiyo sababu Paulo aliandika kwamba si wote wanenao kwa lugha. Si wote wanaotumiwana Mungu katika kile kipawa kitolewacho mara moja cha lugha, kama ambavyo Mungu hamtumii kila mtu katika karama ya tafsiri za lugha. Hiyo tu ndiyo njia rahisi ya kufafanua swali la Paulo – “Kwani ni wote wanenao kwa lugha?” – na yanayofundishwa na Maandiko kwa ujumla.

Mimi naweza kunena kwa lugha wakati wowote nitakao, kama na Paulo pia. Basi, hatuwezi kusema kwamba kila tunaponena kwa lugha, ni “kama Roho apendavyo tu.” Hapana – ni kama sisi tupendavyo. Kwa hiyo, tunachofanya kila tunapotamani si karama ya kunena kwa lugha itokeayo “kama Roho apendavyo tu.” Tena, Paulo – kama mimi – alinena kwa lugha kibinafsi pasipo kuelewa alichokuwa anasema. Basi, hiyo si karama ya lugha ambayo aliandika habari zake katika 1Wakorintho, aliyosema kwamba lazima kila mara iambatane na karama ya tafsiri ya lugha.

Ni mara chache sana nimenena kwa lugha katika kusanyiko. Ni wakati nilipojisikia kwamba Roho Mtakatifu amenishukia ili nifanye hivyo, japo ningeweza (kama Wakorintho walivyokuwa wanafanya) kuomba kwa lugha kwa sauti wakati wowote niliotaka nikiwa kanisani bila ya kuwepo tafsiri. Ninapohisi Roho Mtakatifu akinijilia kwa nguvu na karama hiyo, kila mara imekuwepo tafsiri ambayo ilileta kujengwa kwa mwili wa Kristo wakati huo.

Tunapohitimisha sehemu hii, ni vizuri kutafsiri Biblia kwa umoja. Wale wanaosema kwamba si waamini wote wanaopaswa kunena kwa lugha kwa sababu ya swali la Paulo katika 1Wakorinto 12:30, wanapuuza maandiko mengine mengi sana yasiyokubaliana na tafsiri yao. Kwa sababu ya kosa lao, wanakosa baraka kubwa sana kutoka kwa Mungu

–David

Sifa na kuabudu

praise1

Yule mwanamke akamwambia [Yesu], ‘Bwana, naona ya kuwa u nabii. Baba zetu waliabudu katika mlima huu, nanyi husema ya kwamba huko Yerusalemu ni mahali patupasapo kuabudia.’ Yesu akamwambia, ‘Mama, unisadiki. Saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu wala kule Yerusalemu. … Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana, Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli’ (Yohana 4:19-24).

Maneno hayo kutoka kinywa cha Yesu yanaweka msingi wa sisi kuelewa juu ya mambo muhimu sana katika kuabudu. Yeye alizungumzia juu ya “waabuduo halisi” na kueleza sifa zao. Hii huonyeha kwamba wapo watu wanaoabudu, lakini si waabuduji wa kweli. Wanaweza kudhani kwamba wanamwabudu Mungu lakini ukweli si hivyo maana hawatimizi masharti Yake.

Yesu alitangaza alama za waabuduji wa kweli – wao huabudu “katika roho na kweli.” Basi, kinyume chake ni kwamba, waabuduji wasio wa kweli ni wale wenye kuabudu “katika mwili na uongo. Kimwili, waabuduji wasio wa kweli wanawea kufanya matendo yote ya kuabudu, lakini ni maonyesho tu maana hayatoki katika moyo unaompenda Mungu.

Ibada ya kweli kwa Mungu inatoka katika moyo unaompenda Mungu tu. Basi, kuabudu si kitu tunachofanya wakati tunapokutanika kanisani, bali ni kitu tunachofanya kila dakika ya maisha yetu, tunapotii amri za Kristo. Inashangaza kwamba yule mwanamke aliyekuwa anazungumza na Yesu alikuwa ameolewa mara tano, na wakati huo alikuwa anaishi na mwanamume, na bado alitaka kuhojiana na Yesu kuhusu mahali panapofaa kumwabudu Mungu! Yeye ni mfano wa watu wengi sana wenye dini, wanaohudhuria ibada huku wakiishi maisha yao kila siku katika kumwasi Mungu. Hao si waabuduji wa kweli.

Wakati fulani Yesu aliwakemea Mafarisayo na waandishi kwa sababu ya ibada yao ya uongo, isiyotoka moyoni.

Enyi wanafiki! Ni vema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu, akisema, ‘Watu hawa huniheshimu kwa midomo; ila mioyo yao iko mbali nami. Nao waniabudu bure, wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu’ (Mathayo 15:7-9. Maneno mepesi kukazia).

Ingawa Wayahudi na Wasamaria katika siku za Yesu walitilia mkazo sana kuhusu mahali pa watu kuabudia, Yesu alisema kwamba mahali hapakuwa na maana sana. Cha muhimu ni hali ya moyo wa kila mtu, na jinsi anavyomheshimu Mungu. Hayo ndiyo yanaamua jinsi ibada yake ilivyo.

“Ibada” nyingi katika makanisa siku hizi ni taratibu tu zilizokufa, zinazotendwa na waabuduji waliokufa pia. Watu wanarudia maneno ya mtu mwingine kuhusu Mungu, bila hata kuyafikiri, wanapoimba “nyimbo za kuabudu.” Kuabudu kwao ni bure, maana maisha yao yanaonyesha kilicho halisi katika mioyo yao.

Mungu angetamani hata kuambiwa “Nakupenda” rahisi tu itokayo moyoni kutoka kwa mtoto wake mmoja mtiifu, kuliko kuvumilia kelele zisizotoka moyoni za maelfu ya Wakristo wa Jumapili asubuhi, wakiimba “Jinsi Wewe Ulivyo Mkuu.”

Kuabudu Katika Roho

Kuna wanaosema kwamba kuabudu “katika Roho” ni kuomba na kuimba kwa lugha zingine. Hiyo ni tafsiri ngumu kukubali, ukitazama maneno ya Yesu. Yeye alsiema kwamba “saa inakuja, na sasa ipo, ambayo waabuduji wa kweli watamwabudu Baba katika roho na kweli,” kuonyesha kwamba tayari walikuwepo watu waliotimiza masharti ya kuabudu “katika Roho” alipotoa tamko hilo. Ni kweli kwamba hakuna yeyote aliyenena kwa lugha mpaka Siku ya Pentekoste. Basi, aaminiye yeyote, awe ananena kwa lugha au hapana, anaweza kumwabudu Mungu katika roho na kweli. Kuomba na kuimba kwa lugha zingine hakika huwa ni msaada kwa mwabuduji katika kuabudu kwake, lakini hata kunena kwa lugha kunaweza kuwa utaratibu usiotoka moyoni.

Picha ya kusisimua kuhusu ibada ya kanisa la kwanza inapatikmana katika Matendo 13:1, 2.

Na huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, nao ni Barnaba, na Simeoni aitwaye Nigeri, na Lukio Mkirene, na Manaeni aliyekuwa ndugu wa kunyonya wa mfalme Herode, na Sauli. Basi hawa walipokuwa wakimfanya Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, ‘Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia’ (Maneno mepesi kukazia).

Ona fungu hili linavyosema: “walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada.” Basi tunajifunza hapo kwamba ibada ya kweli humhudumia Bwana. Ila, ni hivyo wakati Bwana anapokuwa ndiyo lengo la upendo wetu.

Njia Za Kuabudu

Kitabu cha Zaburi ambacho tunaweza kusema ni kitabu cha nyimbo cha Israeli, kinatushauri kumwabudu Mungu katika njia nyingi tofauti tofauti. Kwa mfano: Katika Zaburi ya 32 tunasoma hivi:

Pigeni vigelegele vya furaha; ninyi nyote mlio wanyofu wa moyo (Zaburi 32:11b. Maneno mepesikukazia).

Japo kuabudu kimya, kwa utaratibu na heshima kuna nafasi yake, pia kuna nafasi ya kupiga kelele za shangwe.

Mpigieni Bwana vigelegele, enyi wenye haki, kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo. Mshukuruni BWANA kwa kinubi, kwa kinanda cha nyuzi kumi mwimbieni sifa. Mwimbieni wimbo mpya, pigeni kwa ustadi kwa sauti ya shangwe (Zaburi 33:1-3. Maneno mepesi kukazia).

Tunapaswa kumwimbia Bwana katika kuabudu, lakini kuimba kwetu kuwa kwa furaha, ambalo ni onyesho lingine la nje kuhusu undani wa moyo wa mtu. Pia tunaweza kuimba kwa furaha tukitumia vyombo mbalimbali vya muziki. Ila, katika mikutano mingi ya kanisa, vyombo vya muziki vinakuwa na sauti ya juu kiasi cha kwamba vinafunika kabisa sauti ya uumbaji. Ni vizuri vipunguzwe sauti au vizimwe. Ukisoma zaburi, tatizo hilo halikuwepo!

Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai. Kwa jina Lako nitaiinua mikono yangu (Zaburi 63:4. Maneno mepesi kukazia).

Tunaweza kuinua mikono yetu juu kwa Mungu kama ishara ya kujitolea Kwake na kumheshimu.

Mpigie Mungu kelele za shangwe nchi yote; imbeni utukufu wa jina lake; tukuzeni sifa zake.Mwambieni Mungu, ‘Matendo Yako yatisha kama nini! Kwa ajili ya wingi wa nguvu zako, adui zako watakuja kunyenyekea mbele zako. Nchi yote itakusujudia na kukuimbia, naam, italiimbia jina lako’ (Zaburi 66:1-4. Maneno mepesi kukazia).

Tunatakiwa kumwambia Bwana jinsi alivyo mkuu na kumsifu kwa jinsi alivyo wa ajabu. Zaburi ni mahali pazuri sana pa kupa ta maneno yafaayo ya kumsifu Mungu. Tunahitaji kwenda zaidi ya kurudia rudia maneno haya: “Nakusifu, Bwana!” Kuna mengi sana ya kumwambia.

Njooni tuabudu, tusujudu, tupige magoti mbele za BWANA aliyetuumba (Zaburi 95:6).

Hata jinsi tulivyo ni onyesho la ibada: iwe ni kusimama, kupiga magoti au kusujudu.

Watauwa na waushangilie utukufu, waimbe kwa sauti kuu vitandani mwao (Zaburi 149:5. Maneno mepesi kukazia).

Si lazima tuwe tumesimama au kupiga magoti ili kuabudu – tunaweza hata kuwa tumelala kitandani.

Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru, nyuani mwake kwa kusifu. Mshukuruni, lihimidini jina lake (Zaburi 100:4. Maneno mepesi kukazia).

Hakika, kushukuru kuwe sehemu ya kuabudu kwetu.

Na walisifu jina lake kwa kucheza (Zaburi 149:3. Maneno mepesi kukazia).

Tunaweza hata kumsifu Bwana kwa kucheza. Lakini kucheza kwenyewe kusiwe kwa kimwili, kwenye kuamsha ashiki, au kwa ajili ya kustarehesha watu.

Msifuni kwa mvumo wa baragumu; msifuni kwa kinanda na kinubi. Msifuni kwa matari na kucheza; msifuni kwa zeze na filimbi. Msifuni kwa matoazi yaliayo; msifuni kwa matoazi yavumayo sana. Kila mwenye pumzi na amsifu BWANA. Haleluya (Zaburi 150:3-6).

Mungu ashukuriwe kwa walio na vipawa vya muziki. Vipawa vyao vinaweza kutumika kumtukuza Mungu kama watavipiga kwa moyo wa upendo.

Nyimbo Za Kiroho

Mwimbieni BWANA wimbo mpya, kwa maana ametenda mambo ya ajabu (Zaburi 98:1a. Maneno mepesi kukazia).

Hakuna kosa lolote kuimba wimbo wa zamani, mpaka inapokuwa mazoea. Hapo ndipo tunahitaji wimbo mpya utokao mioyoni mwetu. Katika Agano Jipya, tunajifunza kwamba Roho Mtakatifu atatusaidia kutunga nyimbo mpya. Tunaambiwa hivi:

Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu (Wakolosai 3:16).

Tena msilewe kwa mvinyo ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho; mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; na kumshukuru Mungu Baba siku zote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo (Waefeso 5:18-20).

Paulo aliandika kwamba tunapaswa kuwa tunaimbiana “zaburi, na tenzi na nyimbo za rohoni”. Basi, hizo tatu zina tofauti. Uchunguzi wa lugha ya Kiyunani hautoi msaada wowote, ila pengine “zaburi” maana yake ni kuimba zaburi kama zilivyo katika Biblia, pamoja na vyombo. Pengine “tenzi” ni nyimbo mbalimbali za shukrani zilizokuwa zimetungwa na waamini katika makanisa. “Nyimbo za rohoni” labda zilikuwa nyimbo za papo kwa papo kutoka kwa Roho Mtakatifu, ambazo ni sawa na ile karama ya unabii, ila, zenyewe ziliimbwa.

Kusifu na kuabudu vinapaswa kuwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku – si kitu fulani tunachofanya wakati wa kukutanika kanisani. Mchana kutwa tunaweza kumhudumia Bwana na kufanikiwa kujisikia ushirika wa karibu na Yeye.

Sifa Ni Imani Ikitenda Kazi

Kusifu na kuabudu ni madhihirisho ya kawaida kabisa ya imani yetu kwa Mungu. Kama kweli tunaamini ahadi za Neno la Mungu, basi tutakuwa watu wenye furaha, waliojaa sifa kwa Mungu. Yoshua na Waisraeli walitakiwa kupiga kelele kwanza, ndipo kuta zikaanguka. Biblia inatushauri hivi: “Furahini katika Bwana sikuzote” (Wafilipi 4:4), na “Shukuruni kwa kila jambo” (1Wathes. 5:18a).

Mfano mmoja wa hali ya juu sana kuhusu nguvu za sifa unapatikana katika 2Nyakati sura ya 20, wakati taifa la Yuda lilipovamiwa na majeshi ya Moabu na Amoni. Akijibu maombi ya Mfalme Yehoshafati, Mungu aliwaagiza Israeli hivi:

Msiogope wala msifadhaike kwa ajili ya jeshi kubwa hili kwani vita si yenu bali ni ya Mungu. Kesho shukeni juu yao … Hamtahitaji kupigana vita, jipangeni, simameni, mkauone wokovu wa BWANA ulio pamoja nanyi, enyi Yuda na Yerusalemu (2Nyakati 20:15b – 17).

Kisa kinaendelea, hivi:

Wakaamka asubuhi na mapema, wakaenda nje katika jangwa la Tekoa; nao walipokuwa wakitoka, Yehoshafati akasimama akasema, ‘Nisikieni enyi Yuda nanyi wenyeji wa Yerusalemu; mwaminini BWANA Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waaminini manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa.’ Naye alipokwisha kufanya shauri na watu, akawaweka wale watakaomwimbia BWANA, na kumsifu katika uzuri wa utakatifu, wakitoka mbele ya jeshi, na kusema, Mshukuruni BWANA; kwa maana fadhili zake ni za milele. Nao walipoanza kuimba na kusifu, BWANA akaweka waviziao juu ya wana wa Amoni, na Moabu, na wa mlima Seiri, waliokuja juu ya Yuda; nao wakapigwa. Kwani wana wa Amoni na wa Moabu waliwaondokea wenyeji wa mlima Seiri kuwaulia mbali na kuwaharibu; nao walipokwisha kuwakomesha hao wakaao Seiri, wakajitia kuharibu kila mtu mwenziwe. Hata Yuda walipofika mnara wa kulindia wa jangwani, wakalitazama hilo jeshi; nao angalia, walikuwa maiti walioanguka nchi, wala hapana aliyeokoka. Nao Yehoshafati na watu wake walipokuja kuchukua nyara zao, wakaona kati yao wingi wa mali, na mavazi, na johari za thamani, walivyojivulia, zaidi kuliko wawezavyo kuchukua; wakawa siku tatu katika kuteka nyara, maana zilikuwa nyingi sana (2Nyakati 20:20-25. Manenomepesi kukazia).

Sifa iliyojaa imani huleta kulindwa na husababisha utoaji wa Mungu!

Kwa maelezo zaidi kuhusu mada hiyo ya nguvu za sifa, ona Wafilipi 4:6-7 (sifa huleta amani), 2Nyakati 5:1-14 (sifa huleta uwepo wa Mungu), Matendo 13:1, 2 (sifa hudhihirisha makusudi na mipango ya Mungu), na Matendo 16:22-26 (sifa huleta kuhifadhiwa na Mungu, na kufunguliwa kutoka gerezani).

––David Servant

KUTOA ZAKA kila mwezi au kila upatapo kipato.

sadaka+zaka

Wana SG, mafundisho ya kutoa zaka kila upatapo kipato ni SAHIHI, sio mafundisho potofu hata kidogo. Naomba ninukuu maandiko ambayo tunayafahamu sote kisha nitayafafanua. “Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae; nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo Bwana atakuwa Mungu wangu. Na jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi“. - Mwanzo 28:22. Hebu ongezea na andiko hili “Lakini, ole wenu, Mafarisayo, kwa kuwa mwatoa zaka za mnanaa na mchicha na kila mboga, na huku mwaacha mambo ya adili, na upendo wa Mungu; iliwapasa kuyafanya hayo ya kwanza, bila kuyaacha hayo ya pili”. - LUKA 11:42 (SUV msisitizo added).

Utoaji wa Zaka/Fungu la kumi/Sehemu ya kumi ni jambo lilikuwepo hata kabla na baada ya sheria. Yakobo anasemakatika kila utakalonipa hakika ………. Bwana Yesu anawaambia mafarisayo wasiache kutoa zaka za mnanaa na mchicha na kila mboga. Swali ni kwamba ni wakati gani mboga mboga hizi zinapatikana? Je si wakati wa kuzivuna? Lakini jambo la kuzingatia ni kuwa kila atoae zaka yampasa kuleta ZAKA KAMILI ( Malaki 3:10). Logical thinking rahisi ni zipi, kuleta zaka kamili kwa mtu wa kawaida ambaye uwekaji wa kumbu kumbu sio kivile? Hivi Mungu huagiza wanawe na kisha kuweka ugumu wa kuyatekeleza. ukikaa na zka muda mrefu hakuna uwezekano wa kusahau, na ukisahau itakuwa umetoa zaka kamili? Kwa nini mambo yasiwe rahisi kwa kutoa kila unapopata? Hebu chukulia mfanyakazi akae na zaka kisha baada ya mwaka ndipo atoe, Je, ataweza kutoa mapato ya 120% (yaani 10% mara miezi 12)?

Ninajua tunakubaliana kuwa kutoa Zaka ni wajibu wa kila mwamini. Sasa frequency (mara ngapi kwa kipindi gani) isiwe issue. Huenda mpendwa Milinga unatatizwa na andiko lifuatalo; nanukuu “Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka”.  - KUMB 14:22. Kama ndiyo andiko hili, basi naomba uangalie tafasiri zingine zinasema nini kuhusu maongeo. Hebu angalia ya KJV – neno maongeo limetafsiri ni “increase”, yaani ongezeko. Hawa ndugu zetu walikuwa na aina mbali mbali za Zaka katika kitu kimoja. Wote tunajua kuwa zaka zinatolewa nyumbani mwa Bwana lakini hebu ona hii “Kila mwaka wa tatu, mwisho wake, toa fungu la kumi lote la maongeo yako ya mwaka huo, uliweke ndani ya malango yako;”. - KUMB 14:28(SUV – msisitizo added). Agizo hapa ni kuiweka zaka ndani ya malango yako sio nyumbani mwa Bwana!!!

Pia kuhusu ile zaka ya kila mwaka inawezekana walikuwa wanavuna mara moja kwa mwaka. Ona tafasiri hii  “You shall tithe all the yield of your seed, which comes forth from the field year by year”. - Deut 14: 22 – RSV. Hivyo mavuno ya shamba ni tofauti na mambo ya msharaha au faida katika biashara ambayo mpendwa anapata mapato kila mwezi, wiki n.k. Nimalizie kwa kusema, Zaka ya kila mwaka iliyoonyeshwa hapo juu, ilikuwa inatolewa nyumbani mwa Bwana lakini inaliwa na mtoaji pamoja na mlawi. Swali ni hili Je, Zaka unazotoa huwa unakula mwenyewe? Zaka ya kila baada ya miaka mitatu ilikuwa inatolewa na kuwekwa malangoni ili mlawi, mjane, watima na mgeni wakiiona waweze kuchangamkia (Soma mwenyewe KUMB 14:22-29 uthibitishe).

Ninaona kuwa nimejibu hoja hii na kuthibitisha kuwa kutoa zaka kila unapopata mapato ni mafundisho sahihi na inawezekana pia nimekuongezea na aina nyingine ya Zaka.

Keep on digging.

Mathew.

Kuota unakimbizwa na nyoka

gm

Ni ujumbe kwako kwamba roho ya uongo inakunyemelea maana nyoka katika ulimwengu wa roho ni roho ya uongo na kumbuka shetani alivaa umbo la nyoka na kuwadanganya hata akina Adamu na Hawa katika bustani ya Edeni wakatenda dhambi (Mwanzo 3:4) na katika Ufunuo 20:2 shetani anaitwa nyoka wa zamani yaani aliyewadanganya akina Adamu na Hawa. Hivyo ni kuwa makini sana na kuvunja roho hiyo kwa jina la YESU KRISTO na mpango huo wa kuzimu hautafanikiwa.

Na mfano mzuri ni mimi siku moja nikiwa kanisani tunaomba nilimwona nyoka anazunguka na kwa sababu nilikua sijajua kwamba hiyo ni roho ya uongo unanyemelea watu wa MUNGU hakika kesho yake ulizuka uongo mkubwa na kusababisha hadi baadhi ya viongozi wa kanisa kukosana na ndio ikawa mwanzo wa mimi kujua kwamba nyoka anamaanisha nini katika ulimwengu wa roho.

MUNGU akubariki sana ndugu na kumbuka kuwa suluhisho pekee la yote haya na yote yanayowasumbua wanadamu ni YESU KRISTO na yeye mwenyewe katika Mathayo 11:28

–Gasper Madumla

Happy Father’s Day!!

happy-fathers-day

Fathers, don’t exasperate your children by coming down hard on them. Take them by the hand and lead them in the way of the Master.—Ephesians 6:4 (MSG)

Happy Father’s Day to every one you…who are fathers!

Being a father is the most important responsibility we have, and one of the hardest jobs we will ever do. To truly be effective as a Godly father, we must submit ourselves to God first and lead our children in His Way and His Word; this way we will leave a greater legacy that any trust fund! Place your trust in God to help you to do it well!

Have a blessed day!

A Father’s Love

A father is respected because
He gives his children leadership…
Appreciated because
He gives his children care…
Valued because
He gives his children time…
Loved because
He gives his children the one thing
they treasure most – himself.

–James

Malezi ya Mtoto – Mithali 22:6

 watoto

“Mlee mtoto katika njia impasayo, naye hataiacha hata atakapokuwa mzee.”

Kumlea mtoto maana yake ni nini ?

Ni kumtunza na kumfundisha/kumuelimisha mpaka afikie mahali pa kujitegemea mwenyewe.

Ni kumtunza na kumfundisha kwa vitendo na maneno mpaka awe mzima, kiakili na kiutu kiasi cha kuweza kuendelea mwenyewe bila ya kukutegemea.

Njia ipasayo kumlea mtoto ni ipi?

Ni njia ile nzuri yenye maadili mema yanayokubaliwa na Neno la Mungu pamoja na jamii unayoishi katikati yake.

 

Mwenendo wenu ni fundisho kubwa kabisa mbele ya mtoto wenu. Njia ipasayo kumlea mtoto ni kuketi na mtoto na kumshauri maadili mema ya maisha (Kumb 6:7). Ni kumwelekeza kwenye mambo matakatifu, kabla hajaharibiwa na walimwengu.

Kwa mfano:-

Pale Nyumbani: Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hataatakapokuwa mzee.

- Ibada za nyumbani kwa wazazi pamoja na mtoto/watoto ni kitu muhimu sana.

- Mazungumzo yenu yanayohusu watu wengine, majirani, watumishi wenzako nk.

- Mnavyojibizana na mkeo/mumeo mbele ya watoto na hata sura yako ya kila siku mbele za watoto.

- Unavyowaelekeza watoto wako kuhusu maadili mazuri kwa waliomzidi umri.

- Adabu na heshima mezani mkiwa peke yenu na watoto au mbele ya wageni.

- Ikiwa wewe ni omba omba kila wakati hata watoto wako watakua hivyo.

Mahudhurio ya ibada: Mlee mtoto katika njia ipasayo naye hataiacha hata atakapokuwa mzee.

- Unatarajia mtoto atachukua fundisho gani ukibaki nyumbani wakati wa ibada?

- Unatarajia mtoto atajifunza nini kama kila siku unachelewa ibada na kuwahi kutoka au kukaa nje ya kanisa saa ya mahubiri?

- Unatarajia mtoto atajifunza nini kama huchukui Biblia wala kitabu cha nyimbo unapoenda ibadani?

- Unatarajia kuelewekaje unapowaacha watoto nyuma wakati unapokwenda kuhudhuria vipindi mbali mbali vya ibada?

Tunapokuwa ibadani: Mlee mtoto katika njia ipasayo, naye hataiacha hata akiwa mzee.

- Usimwache mtoto acheze cheze na kutembea hovyo wakati wa ibada huku akipiga makelele.

- Sio vema wakati wa utoaji wa sadaka kumpa mtoto senti 20 au 50 wakati unazo pesa zaidi ya hizo. Au kukaa tu bila kutoa sadaka wakati unapofika wa kutoa sadaka.

- Sio vizuri kupiga usingizi wakati ibada inaendelea. Au kutafuna pipi au “gum“ na kuchafua kanisa.

Kumbuka unayomfundisha mwanao kwa vitendo, yaweza kuwa picha nzuri au mbaya ambayo kwake itakuwa vigumu sana kuisahau au kuiacha hata atakapokuwa mzee!!!

Kwa nini?

Mzazi ni mwalimu wa kwanza kabisa kwa mtoto. Hivyo kila utakalomfundisha mwanao:-

- Atalizingatia na kulishika siku zote za maisha yake. Mfano: kama unapenda nyimbo za “dance“ au za kidunia yeye naye atazipenda hizo.

- Yale anayoyaona kwako anajifunza na kuyatendea kazi. Kwa mfano, kusema uongo, kuahidi bila kutimiza ahadi, kutukana nk

- Ukifanya kazi au kuishi katika hali ya uvivu usishangae mtoto wako akiwa mvivu.

- Ukiwa na bidii au ulegevu katika mambo ya Mungu, mtoto wako atakuwa hivyo.

- Ukiwa na hali ya usengenyaji na kuwadharau wengine mtoto wako atayaiga hayo.

- Kama una kiburi na majivuno au hali ya kutokumtii mumeo au kumpenda mkeo mtoto atajifunza hali hiyo.

- Kama una hali ya kutokuwa na ibada za nyumbani na uvivu wa kushiriki vipindi kanisani, mtoto atayaiga hayo.

- Kama unashabikia ya dunia na kuweka kando mambo ya kiroho mtoto atakuwa hivyo.

Hivyo mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hata atakapokuwa mzee.

TUWE VIELELELEZO VIZURI KWA WATOTO WETU NAO WATAKUA HIVYO.

Mchungaji Marandu

UTOAJI: ANGALIA MADHUMUNI (MOTIVE) YAKO

bukobawadau
Wapendwa wana SG,

Ninamshukuru Mungu kwa kunijalia kuwashirikisha somo hili japo kwa ufupi.

Katika nyakati tunazoishi, swala la utoaji limekuwa ni mada kubwa katika makanisa mengi na kupitia mahubiri yanayorushwa kupitia vyombo vya habari vya Kikristo au vinavyofahamika hivyo. Watu wanahamasishwa kutoa kupitia mafundisho na maneno mengine yenye kutia hamasa. Katika mazingira hayo, kwa muda mrefu sana nimekuwa nikitafakari kama tunapotoa huwa tunafanya hivyo kwa nia iliyo safi, inayompendeza Mungu tunayesema tunamtolea. Hii ndiyo inayopelekea tafakuri hii. Endelea kusoma!

Ninapozungumzia nia (motive) ya kutoa ninamaanisha lile jambo hasa ambalo linamfanya au KUMSUKUMA mtu kumtolea Mungu (au kutoa kwa imani kuwa anamfanyia Mungu), ambalo kama likiondolewa huyo mtu hatatoa.

Mungu ndiye kielelezo chetu katika swala zima la utoaji. Adamu na mkewe Hawa walipotenda dhambi pale katika bustani ya Edeni, Mungu alimtoa mnyama, akamchinja na kuwapatia ngozi ya kujisitiri (Mwanzo 3:21). Wakati tungali wenye dhambi, Mungu alimtoa Mwana wake wa pekee, Yesu Kristo, ili amwage damu yake kwa ajili ya ondoleo la dhambi zetu (Yohana 3:16). Hii ni mifano michache kati ya mingi ambayo inatuonyesha jinsi Mungu alivyo mtoaji. Yesu pia alipata kusema Mungu anawapatia jua na mvua watu wema na wabaya (Mathayo 5:45). Katika kutoa huko, Mungu anakufanya kwa sababu ya upendo, kwa lugha nyingine, ni upendo ndio unaomsukuma kutoa. Ndiyo maana Maandiko yako wazi kabisa kuwa, Mungu alifanya ule utoaji ulio mkuu kabisa (wa kumtoa Yesu Kristo Mwanae) kwa sababu ya upendo:

Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. (Yohana 3:16, msisitizo wangu)

Je, Mungu Baba alipomtoa Mwanae, tunaweza kusema kulikuwa na faida fulani aliyokuwa akiiwaza hata ikamsukuma kumtoa mwanae? Hapana. Sana sana waliokuwa wakifaidika na utoaji huo ni sisi wanadamu. Faida hiyo ni sisi kufanyika wana wake (Yohana 1:12-13) pamoja na ahadi zote zinazoambatana na hali ya kuwa wana wa Mungu (kwa mfano, soma 2 Petro 1:2-4).

Hebu tumwangalie na Yesu Kristo. Aliutoa uhai wake kwa sababu ya kutupenda tu na sio kutarajia faida fulani (Yohana 10:17-18). Na hata alipowapa watu mikate hakuna faida yoyote aliyoitarajia baadaye.

Yesu akatoka, akaona mkutano mkuu, akawahurumia, akawaponya wagonjwa wao.  Hata kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea, wakasema, Mahali hapa ni nyika tupu, na saa imekwisha pita; uwaage makutano, waende zao vijijini, wakajinunulie vyakula.  Yesu akawaambia, Hawana haja kwenda zao, wapeni ninyi vyakula.Wakamwambia, Hamna kitu hapa ila mikate mitano na samaki wawili. Akasema, Nileteeni hapa. Akawaagiza makutano waketi katika majani; akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akabariki, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi, wanafunzi wakawapa makutano. Wakala wote wakashiba; wakayaokota masazo ya vipande vya mikate, vikapu kumi na viwili, vimejaa. (Mathayo 14:14-20, msisitizo wangu)

Yesu angeweza kuruhusu umati ule wa watu uondoke kila mtu akajitafutie chakula, lakini kwa sababu ya upendo wake kwao, akaamua kuwapa chakula.

Si tu kwamba Mungu amekuwa akitoa kwa kusukumwa na upendo na si kwa sababu ya matarajio ya faida fulani, bali pia ndivyo ambavyo amekuwa akiagiza wanaomcha Yeye kufanya hivyo kwa kusukumwa na upendo. Upendo ndiyo iwe nia (motive) sahihi ya kutufanya tumtolee.

Tunasoma:

Bwana akanena na Musa, akamwambia,  Waambie wana wa Israeli kwamba wanitwalie sadaka; kila mtu ambaye moyo wake wampa kupenda mtatwaa kwake sadaka yangu. (Kutoka 25:1-2, msisitizo wangu)

Ni kweli kwamba Mungu ameahidi kuwabariki wale wanaotoa sawa sawa na mapenzi yake, lakini baraka hizo kamwe ZISIWE ndio sababu ya sisi kutoa. Tukumbuke kuwa Mungu anaichunguza mioyo yetu kuona nia zetu katika kila tulifanyalo:

Nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye viuno na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake.(Ufunuo 2:23, msisitizo wangu)

Nia ya kufanya huduma na mambo mengine kwa ajili ya Mungu ni moja ya vigezo ambavyo vitatumika katika kupima kazi zetu siku ya kutolewa thawabu, na kazi zetu zikionekana hazifai zitateketea (soma 1 Wakorintho 3:9-15, hata hivyo hilo ni somo lililoko nje ya mada tuliyo nayo sasa).

Mambo yote tuyafanyayo, ikiwemo utoaji, hatuna budi kuyafanya kwa kusukumwa na upendo, vinginevyo ni kazi bure.

Mambo yenu yote na yatendeke katika upendo. (1 Wakorintho 16:14, msisitizo wangu)

Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao. Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi. Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu. (1 Wakorintho 13:1-3, msisitizo wangu)

Utajuaje kwamba unatoa kwa sababu ya kutaka baraka? Jibu ni rahisi! Jiulize, je kama ukiambiwa hakuna baraka za kimwili utakazozipata kwa sababu umetoa, je uko tayari kutoa fedha na mali zako kwa ajili ya kazi ya injili au kusaidia wapendwa wengine? Jibu unalo!

Hebu tuangalie Wakristo wa kanisa la kwanza walifanyaje katika swala la utoaji.

Na jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho mojawala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu cho chote alicho nacho ni mali yake mwenyewe; bali walikuwa na vitu vyote shirika.   Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi, na neema nyingi ikawa juu yao wote.  Wala hapakuwa na mtu mmoja miongoni mwao mwenye mahitaji; kwa sababu watu wote waliokuwa na viwanja au nyumba waliviuza, wakaileta thamani ya vitu vile vilivyouzwa,  wakaiweka miguuni pa mitume; kila mtu akagawiwa kwa kadiri ya alivyohitaji.  Na Yusufu, aliyeitwa na mitume Barnaba, (maana yake, Mwana wa faraja), Mlawi, asili yake ni mtu wa Kipro,  alikuwa na shamba akaliuza, akaileta fedha, akaiweka miguuni pa mitume. (Matendo ya Mitume 4:32-37, msisitizo wangu)

Bila shaka Wakristo hawa walishirikiana kile walichokuwa nacho kuwasaidia wengine miongoni mwao waliokuwa na uhitaji kwa sababu walisukumwa na upendo, wakikumbuka maneno ya Bwana wetu Yesu Kristo aliposema:

Amri mpya nawapa, MpendaneKama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.  Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu,mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi(Yohana 13:34-35, msisitizo wangu)

Upendo huu miongoni mwa jamii ya waaminio hauonekani kwa kauli tupu za “Nawapenda wote”, “Mungu awabariki”, na nyingine za jinsi hiyo. Unaonekana kwa vitendo. Tunasoma:

Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu.  Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitajiakamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo?  Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli. (1 Yohana 3:16-18, msisitizo wangu)

Wakristo wa kule Filipi walitoa vitu vyao kumsaidia mtume Paulo alipokuwa na uhitaji katika safari zake za uinjilisti:

Nalifurahi sana katika Bwana, kwa kuwa sasa mwisho mmehuisha tena fikira zenu kwa ajili yangu, kama vile mlivyokuwa mkinifikiri hali yangu lakini hamkupata nafasi.  Si kwamba nasema haya kwa kuwa nina mahitaji; maana nimejifunza kuwa radhi na hali yo yote niliyo nayo.  Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yo yote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa.  Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.  Lakini mlifanya vema,mliposhiriki nami katika dhiki yangu.  Nanyi pia, ninyi wenyewe mnajua, enyi Wafilipi, ya kuwa katika mwanzo wa Injili, nilipotoka Makedonia, hakuna kanisa lingine lililoshirikiana nami katika habari hii ya kutoa na kupokea, ila ninyi peke yenu.  Kwa kuwa hata huko Thesalonike mliniletea msaada kwa mahitaji yangu, wala si mara moja.  Si kwamba nakitamani kile kipawa, bali nayatamani mazao yanayozidi kuwa mengi, katika hesabu yenu.  Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi, tena nimejaa tele; nimepokea kwa mkono wa Epafrodito vitu vile vilivyotoka kwenu, harufu ya manukato, sadaka yenye kibali, impendezayo Mungu.  Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu. (Wafilipi 4:10-19, msisitizo wangu)

Kuna mambo ya msingi ya kujifunza hapa:

1. Wakristo wa kule Filipi walimpenda na kumjali mtume Paulo na hivyo kufikiri jinsi ya kumsaidia. Katika Biblia ya Kiingereza, tafsiri ya King James, inasema:
But I rejoiced in the Lord greatly, that now at the last your care of me hath flourished again; wherein ye were also careful, but ye lacked opportunity. (Phillipians 4:10).

2. Upendo ule waliokuwa nao wapendwa wa kule Filipi uliwasukuma kushiriki na mtume Paulo katika dhiki aliyokuwa akiipitia ya uhitaji. Walishiriki dhiki hiyo kwa kutoa vitu na kumtumia, na sio maneno matupu ya ‘Mungu akubariki mpakwa mafuta wa Bwana’! Walifanya hivyo mara kadhaa na si mara moja tu na kumsahau.

3. Utoaji huu wa Wakristo wa kule Filipi ulimpendeza Mungu, na hilo ndilo ambalo lilimfanya Mungu awe tayari kuwabariki na kuwapa thawabu kwa matendo yao mema. Neno la Mungu linatuagiza tusichoke kutenda mema, hasa kwa jamii ya waaminio (Wagalatia 6:10). Baraka na thawabu hizi hazikuwa vitu vilivyowasukuma kutoa, bali matokeo ya utoaji wao uliosukumwa na upendo, jambo ambalo lilimpendeza Mungu.

Mtume Paulo alipokuwa akiwaandikia Wakristo wa kule Korintho (2 Wakorintho 8 – 9), alisimulia jinsi makanisa ya Makedonia walivyotoa kwa ukarimu mkubwa licha ya umaskini waliokuwa nao (2 Wakorintho 8:1-5), na kuwahimiza Wakristo wa Korintho wafanye vivyo hivyo (2 Wakorintho 8:7; 9:5).

Katika nyakati zetu kuna wahubiri wengi wanaowahimiza watu kumtolea Mungu kama watu wanaowekeza (invest) kwenye biashara. Mafundisho ya jinsi hiyo, ambayo sijaweza kuyapata katika Maandiko Matakatifu (kama nilivyojaribu kufafanua hapo juu), yanawafanya wale wanaoyapokea kumtolea Mungu kwa lengo la kutajirika. Kauli kama “Mtolee Mungu atazidisha mara mia moja (wakinukuu Mathayo 19:29), ukitoa shilingi elfu moja utapata laki moja, ukitoa shilingi laki moja utapata sh 100,000 x 100 = shilingi 10,000,000, ukitoa shilingi milioni moja utapata shilingi milioni 100″ kamwe haziwaelekezi watu kumtolea Mungu kwa sababu ya upendo wao kwake, kazi yake na watu wake bali zinawahimiza kutoa kwa ajili ya kupata faida. Na mara nyingi wahubiri wanaotoa kauli za jinsi hiyo huwaelekeza wanaowasikiliza kutoa kwenye huduma zao! Na kama utachukua hatua za ziada za kufuatilia maisha yao, aghalabu utakuta wengi wa wahubiri hao wanaishi maisha ya anasa mno kwa kiwango ambacho hata wasioamini wanabaki midomo wazi kwa mshangao!

Ni kwa nini tumefikia hapo?

Maandiko yanasema wazi wazi kuwa, katika siku za mwisho watu wengi watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha na kupenda anasa kuliko kumpenda Mungu (2 Timotheo 3:1-5). Hali hii imewavaa hata wahubiri wengi wa kizazi hiki, ambao wamegeuza injili kuwa mradi wa kujinufaisha. Wanachokifanya wahubiri wa jinsi hii – Mungu awabariki wale wachache ambao bado wanamcha Yeye – ni kuhubiri mafundisho potofu yanayowapendeza watu walio wengi (2 Timotheo 4:1-4) na kuwaghilibu ili watoe pesa kwenye huduma zao, ili wahubiri hawa waweze kutajirika.

Kwamba watu tofauti huweza kuhubiri injili kwa nia na malengo tofauti ni jambo ambalo mtume Paulo aliliandika:

Wengine wanahubiri habari za Kristo kwa sababu ya husuda na fitina; na wengine kwa nia njema.  Hawa wanamhubiri kwa pendo, wakijua ya kuwa nimewekwa ili niitetee Injili;  bali wengine wanamhubiri Kristo kwa fitina, wala si kwa moyo mweupe, wakidhani kuongeza dhiki za kufungwa kwangu.  Yadhuru nini? Lakini kwa njia zote, ikiwa ni kwa hila, au ikiwa ni kwa kweli, Kristo anahubiriwa; na kwa hiyo nafurahi, naam, nami nitafurahi. (Wafilipi 1:15-18, msisitizo wangu)

Kama watoto wa Mungu tunaotafuta kuishi sawa sawa na mapenzi ya Mungu, hatuna budi kumtolea kwa nia iliyo sahihi, nayo ni upendo wetu kwake, kazi yake na kwa jamii ya waaminio wenye uhitaji. Upendo ndio utusukume kufanya hivyo na si jambo jingine liwalo lote.

Mungu awabariki; asante kwa kusoma hadi mwisho!

–Joel

Maskini tunao sikuzote, lakini Yesu….

chukuahatua

Shalom Wapendwa,

Maskini tunao siku zote, lakini Yesu …..

Napenda kushirikiana nanyi katika ujumbe huu niliou-copy na kuu-edit kutoka kwenye kitabu kiitwacho KUTAWALA FEDHA NA MATUMIZI.

Biblia inasema “maana sikuzote mnao maskini pamoja nanyi, na kila mpendapo mwaweza kuwatendea mema; lakini mimi hamnami sikuzote.” – MARK 14:7. Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake maneno hayo baada ya mwanamke mmoja kumimina marhamu kwenye kichwa chake na wao wakaanza kunung’unikia tendo hilo. Ni kweli masikini tunao siku zote; Hivyo wasiwe ndiyo sababu, kikwazo au kisingizio cha kushindwa kumtendea jambo jema Bwana Yesu. Masikini hao wapo kwenye matumizi yako ya fedha, kwenye muda wako na maamuzi mbali mbali.

Ninaposema maskini kwenye FEDHA zako ninamaanisha matumizi ya kila siku ya maisha; Kwenye MUDA wako ninamaanisha mambo ya kawaida ambayo unayafanya siku zote; Kwenye MAAMUZI yako ninamaanisha uchanguzi uliouzoelea siku zote; Hao ndiyo maskini ambao kila mtu anao na wapo siku zote. Je, maskini hawa wanakufanya ushindwe kufanya kitu cha tofauti katika maisha yako? Kunapotokea na maelekezo tofauti na ulivyozoea kufanya/kutumia fedha, umekuwa ukinung’unika (kama wanafunzi wa Yesu walivyomnung’unikia yule mwanamke)?

Nimesema kuwa matumizi kwa ajili ya maisha yapo siku zote hao ni MASKINI, ukiwaendekeza huwezi kufanya kitu cha tofauti katika maisha yako. Huwezi kuweka hata akiba, huwezi kuwekeza fedha nga kidogo ili ikuletee fedha zaidi. Wakati mwingine umekuwa ukisema na kuona kuwa maisha ni magumu sana na hivyo huwezi kufanya cho chote. Elewa kuwa ugumu wa maisha ni MASKINI wapo siku zote. Hivyo ugumu wa maisha usikufanye ushindwe kufanya kitu.

Yako mambo ambayo ni ya siku zote na ziko fursa ambazo hutokea kwa nadra sana. Mwanamke yule (Mariamu) aliiona fursa hiyo, akachukua marhamu akampaka Bwana kichwa chake. Bwana Yesu ali-conclude kwa kusema kuwa, “Kila ihubiriwapo Injili katika ulimwengu wote, na hili alilotenda huyu litatajwa kwa kumbukumbu lake. “ – MARK 14:9 (na leo nimelitaja). Lakini jambo la kujiuliza hapa ni kuwa huyu mwanamke alipata wapi fedha za kununulia marhamu ya bei kubwa namna hii. Jibu ni kuwa aliamua kuacha baadhi ya mambo na kuweka akiba hadi akafanikiwa kupata fedha hizo. Ukiwaendekeza hao maskini wako hutaweza kuweka kumbukumbu kwa ajili yako na uzao wako. Achia baadhi ya mambo, baadhi ya matumizi ya kila siku, baadhi ya maamuzi uliyoyazoea na chukua hatua mpya ya kubadilisha hali uliyonayo.

Hivyo katika fedha ulizo nazo na muda ulionao na uamuzi unaochukuwa unaweza kuubadilisha nga kidogo. Katika fedha hizo hizo unazopata ukaweka akiba nga kidogo; Katika muda huo huo unaobaki nao ukafanya jambo la tofauti nga kidogo; Na katika maamuzi hayo hayo, ukaamua maamuzi yanaweza kuufanya usijisikie comfortable nga kidogo. Kinachotakiwa ni kukubali kubadilika kwa kubadilisha mtazamo wako. Je utaendelea kuruhusu maskini ndio wawe sababu ya kukubakisha hapo ulipo? Uamuzi ni wako wa kuuza marhamu ili fedha zitakazopatikana uwape maskini au kuifungua marhamu hiyo na kuimimina juu ya kichwa cha Bwana Yesu!!!!

(Copied and Edited from the Book – Kutawala Fedha na Matumizi, Uk. 117-118; by Mathew D. Maduhu)